Search This Blog

Monday, October 24, 2022

MWAGIA HUMO HUMO - 1

 





    IMEANDIKWA NA : MARIAM SAID AMOUR





    *********************************************************************************





    Chombezo : Mwagia humo humo

    Chombezo : Kumbe Vikiungwa Vitamu

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    Toka nimezaliwa nimekuwa mwanamke mwenye mkosi kila mpenzi wangu mwanzo wa mapenzi yalikuwa motomoto. Lakini baada ya muda fulani mwanaume alinimwaga bila sababu za msingi. Kila siku ya Mungu nilishindwa kuelewa nina matizo gani mtoto wa kike miye. Kibaya zaidi ndoa niliyofunga miezi minne iliyopita ilivunjika huku mpenzi wangu akipagawa na penzi la nje. Jamani mbona makubwa, huyo mwanamke aliyenivunjia ndoa yangu hata mkonioni hajai, hanizidi kwa lolote si kwa sura wala umbile. Niliamini maneno ya watu huenda yule mwanamke ni mchawi. Kitendo cha ndoa yangu kuvunjika na historia yangu ya nyuma ya kuachwa kwenye mataa na wanaume kiasi cha kugeuzwa jina ubao wa shabaha kila mwanaume kujifunza kulenga kwangu na akichoka hiondoka bila kwaheri. Bahati niliyokuwa nayo mwanaume yeyote aliyenitaka, yupo radhi kunihonga hata milioni ili mradi anipate, Mungu alijilalia umbile na sura lakini niliamini kuna kitu

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kikubwa kimepungua kwangu kinachofanya wanaume wanikimbie. Kwani moto anaoanza nao mwanaume kama maji ya moto lakini baada ya muda hupoa. Lakini hachelewi kupoa, wapo niliokaa nao mwezi mwili, mitatu , wiki na wengine wakionja hawarudi tena. Kuna watu walionifuata na kunieleza labda niende kwa waganga wa kienyeji ili nisafishwe nyota yangu. Ushauri ule niliufuata baada ya kutumia dawa zile sikuchelewa kupata bwana aliyetangaza ndoa kabisa. Lakini baada ya miezi minne ndoa yangu ilivunjika, kitendo kile kilinitia aibu, yote ya kuchezewa na wanaume na kuachwa ilikuwa tisa, kumi ilikuwa kuachwa bila sababu huku mume wangu akizama kwenye penzi ya kinyago msela mwanamke asiye na mbele wala nyuma. Kitendo kile kilinidhalilisha sana, sikuweza kuvumilia bila kujieleza siku ya pili nilipanda gari mpaka Dar na kufikia kwa rafiki yangu niliyekuwa nasomanaye shule moja ambaye baada ya kumaliza shule alikwenda Dar kutafuta maisha na baadaye alinieleza amepata chumba tena anafanya kazi kwenye kampuni ya mtu binafsi. Kwa vile nilikuwa na siku yake nilipomjulisha nakwenda Dar hakunikatalia Nilipanda basi hadi Dar. Baada ya kufika nilikaa mwa muda wa mwezi mmoja na kunitafutia kibarua katika kiwanda kimoja, ajabu msimamizi alinizimikia na kuanzisha mahusiano na mimi. Kwa vile kila mmoja alikuwa na ujiko kuwa na uhusiano na bosi basin a mimi nilimkubalia. Kama kawaida haikuchukua hata mwezi akanimwaga na kashfa nyingi kwamba heri atembee na mwanaume mwenzake kuliko kulala na mimi. Kwa kweli kitendo kile kilizidi kunidhalilisha na kuniweka kwenye wakati mgumu, kibaya kila mwanaume niliyekuwa nakutana naye na kuniacha hakunieleza tatizo langu. Kwa kweli niliumia sana na kuamua kuacha kazi, niliapa sitakuwa tayari kufanya kazi wala kuanzisha uhusiano na mwanaume yeyote. Baada ya shoga yangu kupata bwana ilinibidi nihame kwa kutafutiwa chumba sehemu za uswahili kwa bibi mmoja maarufu pale mtaani Bi Shuu, ni bibi wa miaka 55 lakini mambo yake temea chini. Bibi yule alinilea kama mwanaye wa kuzaa hata kodi yangu hakuitaka. Kuhamia kwa Bi Shuu nilijikuta nikiingia dunia nyingine kabisa, kweli nimekubali tembea uone mambo, ningekaa Arusha ningeyajua haya. Nazidi kukubali kweli vikiungwa vitamu, tena mtu ataomba aongezwe na akimaliza kula lazima ajilambe vidole. Najua una hamu kuvijua hivyo vitamu vilivyo ungwa mpaka watu wakajilamba, Naomba twende pamoja tuipate wote faida ya kuwa karibu na makungwi kama Bi Shuu. ******** Katika mambo niliyokuwa siyapendi katika maisha yangu ni pamoja na kusumbuliwa na mwanaume wakati wa kilimo cha mhogo. Ooh! Inama, mara jipinde hivi, mara geuka hivi. Siku zote nilijiuliza kwani bila kukusumbua hivyo mwanaume hawezi kufikisha mzigo wake. Kitendo cha kijana huyu ambaye alinipata kupitia kwa Bi Shuu kutaka kunisumbua kilinikera sana. “Manka mbona hivyo sasa raha ya mapenzi ipo wapi?” “Nimesema sifanyi unavyotaka, sipo kwenye mazoezi ya yoga hapa kama huwezi hivi, vaa nguo zako ondoka, ” nilisema kwa ukali bila kumuangalia nyuma yangu alipokuwa amekaa. “Lakini Man…,” “Ee..ee..eeh, nasema hivi kwani tatizo nini bila hivyo unavyotaka hufiki safari yako?” Nilimkata kauli Edward. “Manka raha ya chakula ubadili mapishi mchele mmoja lakini una mapishi zaidi ya kumi.” “Kwani huo mchele ukipika bila kubadili mapishi hauivi?” “Lakini Manka kuna tatizo gani kufanya ninavyotaka, sema niongeze kiasi gani ukubaliane na mimi ili nami nifaidi raha ya mapenzi?” “Kaka eeh! Mimi sio chombo cha mazoezi, mlango huoo, unaweza kuondoka hukuitwa na mtu chumba changu mwili wangu eeh.” Yule kijana alipandwa na hasira, alinyanyuka na kupitia suruali yake na kutoka bila kuaga, nilifyonza na kujilaza huku nikinyanyuka na kupitia upande wa kanga na kujifunga kisha nilirudi kujilaza kitandani. Nilijikuta nikipandwa na ghadhabu kitendo cha Bi Shuu kunitafutia wanaume na kugawana kitakacho patikana. Nilijikuta nikijiona nimekataa nini na ninafanya nini. Sikuwa na tofauti na wale wanawake wanaojiuza kwenye vyumba vyao kwa wanaume kupanga foleni. Japo kwangu haikuwa hivyo, mimi ilikuwa naitwa na Bi Shuu na kuelezwa juu ya kijana kunipenda na kuwa mtu wangu wa karibu wakati mambo yangu hayajawa mazuri. Lakini kila mvulana aliyekuja baada ya kunionja hakurudi tena, lakini wa leo yeye alikuwa tofauti na waliotangulia, alikuwa mwanaume msumbufu ambaye sikukubaliana naye. Baada ya kuondoka nikiwa bado nimejilaza katika vazi la kanga moja Bi Shuu aliingia chumbani kwangu kama askari aliyevamia chumba cha jambazi. Sikushtuka niligeuza shingo na kumtizama, mama mtu mzima asiye na haya wala kujua vibaya kunigeuza kitega uchumi chake. Japo alinisaidia vitu vingi kama chakula na matumizi madogo madogo ninapokwama kipindi kila nilipoacha kazi bila kujua hatima ya maisha yangu. Akiwa amenisimamia pembeni ya kitanda changu kama jini la kutumwa huku akinikata jicho kali ambalo hakuwahi kulionesha kwangu. Nilijikuta nikishtuka na kujiuliza kulikoni kuniijia kama shetani wa kutumwa. “Manka,” aliniita jina langu. “Abee.” “Unataka msaada gani kwangu?” “Upi huo?” nilimuuliza huku nikaa kitako. “Kila kijana ninayemleta kwako anaondoka bila kuaga tatizo nini?” “Kwani wao wamekueleza nini?” “Hakuna hata mtu wa kuelezea kitu zaidi ya kuondoka bila kuaga, kwani kuna tatizo gani?” “Kwangu sina, labda wao.” “Kwa mtindo huu, hali itakuwa ngumu si muda utageuka mzigo wa moto usioshikika wala kubebeka.” Mmh! Nilijua nimenyea kambi, nilijiuliza kama Bi Shuu kama ataniona mzigo sikujua nitakwenda wapi. Kurudi Arusha sikuwa tayari, kuendelea kulipiwa chumba na shoga yangu niliona aibu baada ya kujitoa kwake, lakini ningefanya nini katika mji wa watu. “Kwa mtindo huo kuanzia mwezi ujao utalipa kodi,” Bi Shuu aliniambia kwa sauti kavu. “Bi Shuu, nitatoa wapi pesa za kodi nami kazi sina.” “Kazi huna au hutaki kazi.” “Kazi za kudhalilishana hata siwezi.” “Kipi cha ajabu dunia ya leo, Mungu amekupa vitumie.” “Navitumia lakini sina bahati.” “Basi habari ndiyo hiyo, mwezi ujao utalipa kodi, la huna rudisha chumba changu.” “Bi Shuu, lakini si wewe ndiye uliyemkataza shoga yangu kuwa aache kulipia kodi nitaishi nawe kama mwanao?” “Mwanangu gani asiye na msaada, mimi na mzee wangu ninatulia na mwanaume akionja lazima arudie na akimaliza sharti ajilambe.” “Sasa mimi nimekataa mwanaume gani, wenyewe ndiyo wananikataa.” “Basi utakuwa na kasoro ambayo unaificha, lakini nitaijua muda si mrefu.” Bi Shuu alisema huku akitoka nje, nilibakia nimejilaza kitandani nikiwa na mawazo mengi juu ya mapungufu yangu kwa wanaume, kufikia hatua kila mwanaume akionja harudii tena. Kingine kilichonichanganya ni kulipa kodi na kazi sina, nilishangaa Bi Shuu kunigeuka kama kinyonga.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nikiwa katikati ya mawazo nilisikia hodi ikigongwa chumbani kwangu. “Pita mlango u wazi,” nilipaza sauti kumruhusu anayegonga aingie. Mlango ulifunguliwa na mtu aliingia, ha! Kumbe alikuwa shoga yangu Mage. “Aah, Mage umenikumbuka leo.” “Ni kweli Manka, vipi mbona ka.a.maaa?” Nilijua kuna hali ilimfanya aingie wasiwasi, nilishukuru Mage hakumkuta yule mwanaume alikwisha nionya nisikubali kuugeuza mwili wangu kitega uchumi na kunieleza ninapozidiwa kimaisha nikimbilie kwake. Lakini niliona aibu motto wa kime niliye kamilika kuomba kwa mtu kila siku. “Hamna kitu, nilikuwa nataka kwenda kuoga,” nilidanganya. “Ni hivi shoga yangu, shemeji yako amekupatia kazi kwenye kampuni moja kama secretary, si bado unakumbuka kutaipu kwa computer?” “Mmh muda, lakini sijasahau, labda wepesi.” “La muhimu uipate hiyo kazi, mengine yatajulikana humo humo.” “Nitashukuru shoga yangu.” “Na kazi yenyewe ni kesho asubuhi jiandae shemeji yako atakupitia, kesho asubuhi na kukupeleka kwenye hiyo kazi kisha atakwenda kazini kwake.” “Nashukuru shoga yangu kweli wewe ni ndugu wa damu” Nilimkumbatia Mage huku nikimuomba Mungu asitokee mwanaume atakaye nitaka kimapenzi. Niliamini hata kama nitamkataa huo utakuwa mwanzo wa kuchukiwa na mwisho wa siku kufukuzwa kazi. Lakini nilimuomba Mungu kabla ya kuianza hiyo kazi, aniepushe ni matamanio ya wanaume japo kila vazi nililovaa liliwaweka katika wakatii mgumu wanaume. Lakini nilimuomba Mungu usiku na mchana ili aniepushe na mataanio ya wanaume. &&&& Japo nilikuwa na furaha ya kupata kazi kwenye ofisi, lakini bado moyo wangu ulikosa raha kutokana na kuwa na bahati ya kupendwa lakini mkosi wa kuachwa. Lakini nilijipiza moyoni kuwa na msimamo wa kutojirahisi kwa wanaume yoyote.



    Baada ya taarifa zile shoga yangu aliondoka na kuniacha nikijipanga kwa ajili ya siku ya pili. Niliapa tena kutomkubalia mwanaume yoyote kimapenzi kutokana na kujijua nina kasoro ambayo sikuifahamu. Mwanzo nilikuwa nikisimama mbele ya kioo na kujiangalia niliona mwanamke mzuri kuliko wote. Hata nilipotipa mbele za watu, watu waliumia shingo kunitazama, wenye pesa waligongana. Nilimchagua niliyempenda lakini mwisho wa siku walinitema kama ganda la mua. Lakini sasa hivi hata kusimama mbele ya kioo naona udhia sikuwa na kipya, sikujua sababu ya mimi kugeuzwa mpira wa kona kila mmoja anataka kufunga na akifunga hana hamu tena na mimi. Nikiwa katika lindi la mawazo mara aliingia Bi Shuu bila hodi kama kawaida yake. Alipofika alisimama mbele yangu kama jini wa kutumwa, kwa sauti ya nyodo alisema. “Hivi Manka utaendelea kuwa tegemezi mpaka lini?” “Mbona sikuelewi Bi Shuu, mbona leo umenishupalia hivyo mtoto wa mwenzio?” Nilijikuta namtolea uvivu maana toka asubuhi amekuwa na mimi huku akizidi kunikosesha raha bila kosa. “Hujui?” Aliniuliza kwa jicho la kukata.

    ”Kujua nini Bi Shuu?” “Baada ya kukueleza ujitume katika maisha yako unaona nakuonea, badala yake unampigia simu shoga yake. Hujisikii aibu mwenzio ana maisha yake utaendelea kuomba mpaka lini?” Mmh, makubwa nilijikuta nikimshangaa Bi Shuu kwa kunishupalia kwa maneno bila sababu, hata bila kujua Mage alikuja kufanya nini yeye ananibwatukia. Au sababu nipo kwake kanigeuza mtoto wake. “Bi Shuu leo naona umeniamkia.” “Sijakuamkia bali nakupa makavu, chungu lakini dawa.” “Unajua shoga yangu kaniletea nini?” Nilimuuliza huku nikumtazama jicho kali. “Kuna kingine zaidi ya kukuletea ya pesa za kodi, hivi hujiulizi mwenzako anaishi vipi na mumewe muda wote na wewe kwa nini umekuwa kama ubao wa shabaha kila mwanaume akionja arudi una tatizo gani mtoto wewe wa kike?” “Lakini Bi Shuu, shoga yangu hakuleta pesa alikuja na mengine kabisa.” “Mankaaaa weweee, unataka kunidanganya mtu mzima mimi niliyeona jua kabla yako.” “Bi Shuu unanionea, shoga yangu hakuniletea hela.” “Haya nieleze amekuletea nini?” “Taarifa ya kazi.” “Kazi! Wapi?” “Kwenye kampuni ya rafiki ya mumewe.” “Mmh, kazi gani?” “Ya secretary wa bosi.” “Mmh, kama nakuona vile, kama kweli chumba utaendelea kukaa bure sitaki hata senti tano yako. Shida yangu kubwa ujishughulishe si kingine ndiyo maana hata hao wanaume niliwatafuta ili upate chochote na ikiwezekana upate mume miongoni mwao.” “Nashukuru Bi Shuuu, niombee niipate hiyo kazi.” “Si umesema kila kitu tayari?” “Eeh, pamoja na dua zako ni muhimu wewe ni mama yangu.” “Dua zangu zote kwako wala usiihofu utaipata.” Tulijikuta nimekuwa kitu kimoja tena kwa kuondoa tofauti za mwanzo, Bi Shuu alikenua mpaka gego la mwisho lilionekana baada ya taarifa zangu za kupata kazi. “Manka kaoge basi tuje tupate kifungua kinywa.” Nilikwenda kuoga na kuungana na Bi Shuu kupata kifungua kinywa, moyoni nilijiuliza bila kupata taarifa za kazi Bi Shuu angenifanya nini. Lakini nilimshukuru Mungu kwa muujiza alionifanyia wakati nilikuwa nimeisha kata tamaa. ******* Usiku kabla ya kulala nilitafuta nguo nzuri yenye heshima itakayofaa mbele ya macho ya watu. Kuhusu umbile na sura Mungu alinipendelea lakini sijui alininyima nini mwilini kiasi cha kuonekana Big G za Kichina ukitafuna kidogo utamu umekwisha. Baada ya kuchagua suti rangi ya bluu, niliinyoosha vizuri na viatu vyangu ambavyo nilivipiga kiwi tangu mchana niliviweka vizuri na kupanda kitandani. Saa kumi na mbili nilikuwa tayari nipo bafuni naoga, baada ya kuoga wakati najipamba mlango uligongwa. Nilijua shemeji amefika, kumbe alikuwa Bi Shuu nilipomuona nilitabasamu na kumkaribisha. “Bi Shuu karibu, mbona asubuhi?” “Hakuna cha ajabu, umeamkaje?” “Mmh, salama shikamoo.” “Marahaba, umeisha jipamba?” “Ndiyo Bi Shuu.” “Njoo mara moja.” Nilitoka hadi chumbani kwake, nilipofika nilikutana na kitezo kilichokuwa kikifuka moshi uliokuwa na harufu nzuri. Nilijiuliza vitu vile alivifanya wakati gani na alimfanyia nani au mimi. Nikiwa nimesimama nisijue alichoniitia aliniambia. “Manka chutama kwenye kitezo hicho,” mmh, makubwa madogo yana nafuu, nilifanya kama alivyoniagiza. Baada ya kuchutaka alitoa udi kwenye karatasi na kuuongeza kwenye makaa ya moto, baada ya kuuweka ulianza kutoa moshi wenye manukato mazuri. Alinipa shuka nijifushe, niliuinamia ule moshi ulionifanya ninukie kila kona ya mwili. Baada ya kujifusha alinieleza niufunike ule moshi na sketi kwa kuchutama moshi wote uliingia chini. Mtoto wa kike nilinukia kama malkia wa Kihindi, baada ya kuhakikisha nanukia kila kona alinipa pafyumu ambayo sikuwahi kuiona na kunipulizuia kidogo na mwisho alinipa wanjaa mwembamba kwa kunisaidia kunipaka. Kwa kweli nilipendeza mtoto wa kike. “Manka leo mwanangu umependeza,” Bi Shuu alinisifia. “Asante.” Wakati huo

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    shemeji alikuwa amefika kwa kupiga hoi, kabla ya kuondoka Bi Shuu alinipa usia. “Manka Mungu kakujalia kila kitu alichotakiwa kuwa nacho mtoto wa kike, kama ningekuwa mtoto wa kiume ningekupata kwa gharama yoyote. Sasa usiwe macho juu. Hii inaweza kuwa nafasi ya pekee kupata bwana aliye bora ambaye atakuwa mumeo. Itumie nafasi yako vizuri, kazi njema.” “Asante, pia nimekusikia Bi Shuu yote nitayafanyia kazi.” “Basi kazi njema mmmwa.” Kwa mara ya kwanza Bi shuu alinibusu kuonesha furaha ya ajabu moyoni mwake. Baada ya kuachana na Bi Shuu alikwenda chumbani kwangu kupitia mkoba wangu kisha niliifuata gari aliyokuja nayo shemeji. Shemeji aliponiona tu alitanguliza sifa. “Hakika mke wangu umependeza.” “Asante mume wangu.” “Kwa mtindo huu nisije ibiwa tu.” “Ni wewe tu mume wangu, haya ni mapambo lakini upendo wangu kwako upo moyoni.” Nilijibu shemeji huku nikiingia ndani ya gari. Gari liliondoka huku utuli niliojinyunyizia ukitalawa ndani ya gari, baada ya kujuliana hali na shemeji aliniuliza maswali mawili matatu. “Mmh, shemu ulikuwa unaishije bila kazi maana mwenzio aliniambia siku hizi huchukui huduma?” “Bi Shuu kwa kweli alinilea kama mtoto wake.” “Sasa ungekaa kumtegemea mpaka lini?” “Ndiyo hivyo kazi zenyewe kila mtu anakutaka kimapenzi ukiwanyima inakuwa kero, nitawakubali wangapi?” “Ooh, pole.” “Sasa ni hivi kampuni ni ya rafiki yangu kipenzi hivyo nakuomba ujiheshimu ili kunilindia heshima yangu.” “Nakuahidi shemeji kujiheshimu.” “Itakuwa vizuri.” Tulipofika kwenye kampuni ya rafiki ya shemu tulitelemka na kuingia ndani, tulipofika tulipokelewa. Muda ule Mkurugenzi alikuwa hajafika tulikaribishwa kwenye makochi. Baada ya dakika kumi aliingia alipomuona shemeji walisalimiana kwa kukumbatiana. “Ooh, Aloys karibu sana.” “Asante Mr Shaka .” “Samahanini kwa kuchelewa.” “Bila samahani hatujafika muda mrefu.” “Basi karibuni ofisini.” Tuliongozana naye hadi ofisini kwake, mmh lilikuwa bonge la ofisi ambalo sikuwahi kuwaza kuingia katika ofisi kama ile. Nilibakia nang’aa macho mtoto wa kike kwa ushamba. Lakini niliuficha ushamba wangu, baada ya kutulia tuli kitini mwenyeji wetu ambaye nilimfahamu jina kwa kumsikia akiitwa na shemu Mr Shaka alikuwa akipitia vitu muhimu mezani kabla ya kutugeukia. “Mhu, Mista lete habari?” “Habari nzuri, huyu ndiye shemeji yangu,” alisema huku akinigeukia. “Ooh, mrembo kwanza nilisahau kukusalinia, za asubuhi?” “Nzuri tu.” “Pia hongera umependeza” ‘Asante.” “Basi kama ulivyoelezwa kazi ipo na unatakiwa kuianza mara moja, wala usihofu ugeni ila nitakuwa nawe pamoja muda wote.” “Nitashukuru kwa hilo.” Baada ya kupokelewa kazini shemeji aliaga na kuniacha kwenye kazi yangu mpya, baada ya kuondoka nilibaki nimeinama chini kama mwanamwali. Pamoja na ukali wa Bi Shuu bado alinipa mafunzo kwa mtoto wa kike kuinamisha macho mbele ya mwanaume. “samahani mrembo unaitwa nani” “Manka” “Manka nani Kileo” “Jina zuri” “Asante.” Mr Mateja alinyanyuka na kunishika mkono huku akisema. “Hebu njoo uanze kazi mama.” Alinipeleka katika computer iliyokuwa nje ya ofisi yake ilikuwa imekaa vizuri sana. “Basi hapa kuanzia leo ndio ofisi kwako.” “Nashukuru sana” Alinionesha kazi za kufanya siku ile, kabla ya kuanza nilijitetea. “Lakini bosi ni muda mrefu sijafanya kazi hivyo lazima nitakuwa mzito.” “Usihofu kwa hilo fanya kwa uwezo wako,” pia alinielekeza kutumia simu nikiwa nana shida ame nimelaliza kazi bila kumfuata ofisini kwake. “Asante bosi,” nilishukuru kwa upole na ukarimu wa bosi “Niite Mr Mateja” “Sawa Mr Mateja” “Nakutakia kazi njema.” “Nawewe pia” Baada ya kuondoka niiliingia kwenye kazi ya kuchapa kazi zilizokuwa wenye meza yangu. Hazikuwa kazi ngumu sana nilizifanya kwa muda mfupi sikuwa nimepoteza kasi ya mikono kihivyoo. Baada ya kuchapa kazi niliyopewa, niliziprinti kwenye karatasi na kuzipiga pini kisha nilimpelekea ofini. Nilimkuta bosi macho yapo kwenye monitor ya computer, nilimuona alinyanyua macho kunitazama. Aliponiona aliachia tabasamu pana, nakiri kuwa bosi wangu Mr Shaka alikuwa mwanaume mtanashati tena mwenye umbile la mvuto kwa mwanamke yoyote. Kule kutabasamu kwake kuliniweka katika wakati mgumu sana kwa kumuomba Mungu aniepushe na shetani wa upendo. Niliamini kama akinitaka kimapenzi jibu la sitaki litakosekana mdomoni mwangu, lakini nilipiga moyo konde kufuata kilichonipeleka ofisini kwa bosi. “Manka karibu.” “Asante bosi, kazi iliyokuwa na haraka nayo tayari.” “Ooh, vizuri sana sikutegemea ungeifanya kwa muda mfupi hivi.” “Najitahidi japo nilikuwa na muda mrefu sijagusa computer,” nilimjibu huku nikimkabidhi kalatasi, nami nikiachia tabasamu pana ambayo huogopa kuitoa kwa wanaume ili kuepusha ungongano wa mawazo. Ilikuwa ugonjwa wa wanaume kila ninapotabasamu mashavu huweka visima ‘dimples’ wanaume wengi ulikuwa uchawi mkubwa kwao. Kila mwanaume niliyekutana naye alipenda kunifurahisha ili aone madhari mantashau ya mashavu yangu.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA



0 comments:

Post a Comment

Blog