Chombezo : Na Mimi Nataka
Sehemu Ya Tano (5)
“Kama wewe umeweza kuweka uangalizi kwangu kwa umakini mimi nitashindwa vipi kulikariri jina lako tena rahisi hivyo? Tena herufi ya kwanza J inaendana na mdogo wangu anayeitwa Junior. Hivyo si mbaya ili wakati nikihitaji msaada wako nisikuite WEWE bali nikuite kwa jina lako kama nidhamu” Kwa maneno yangu nesi Joan akaonekana kuchangamka na kuongeza ucheshi zaidi. Akainuka na kuanza kutembea kuja kitandani kwangu lakini kabla hajanifikia, mlango ukafunguliwa. Akaingia dokta akiwa na vipimo shingoni mwake.
"Joan, unahitajika mapokezi mara moja."
"Sawa dokta" Joan akaondoka na kutuacha wawili wodini. Dokta akaanza kunifanyia vipimo bila kupoteza muda. Alipomaliza akavuta kiti na kukaa karibu na kitanda nilicholazwa.
"Naomba unisikilize kwa makini katika yale nitakayokueleza kwakuwa ni muhimu na yanahitaji utulivu pindi ukiyasikiliza."
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
" Mimi nipo tayari wala hakuna shaka dokta katika hilo."
"Vizuri kijana sasa nisikilize." akakohoa mara mbili na kuanza kuniweka roho juu maana akili yangu hapo ilihama na kuwaza kwamba tayari nimeshakwaa ugonjwa. Haikupita muda akaanza kuongea.
"Una mke na watoto au mtoto?"
"Sina" Nilijibu kwa kifupi.
"Unaweza niambia ni kwanini hadi umri huo huna mke wala mtoto!"
"Sidhani kama kuna kubwa zaidi ya kujiweka sawa kimaisha ili kama nikimleta asiweze kupatwa na tamaa ndogondogo kwakuwa wanawake wengi hukumbwa na tamaa kwa kukosa baadhi ya mahitaji katika familia hata kama ni madogomadogo lakini yawe ya muhimu na yanayohitajika kwa wakati muafaka. Hivyo sihitaji litokee hilo kwakuwa huwa linateteresha moyo."
"Vizuri. Lakini unaye mchumba maana umri wako unaruhusu kabisa kumiliki mwanamke wa kukuondolea hisia pindi zikikukaba."
"Ni kweli dokta lakini kauli ambayo huwa naishikilia kauli yangu kwamba ni vyema kuzitawala hisia kuliko mimi kutawaliwa na hisia kwakuwa ukiruhusu kutawaliwa na hisia, ukubali na kitakachotokea. Kiwe cha hasara ama cha faida. Lakini mara nyingi hasara nd'o huwa kubwa kuliko faida"
"Una maneno mazuri sana lakini huyafuati kama unavyoyatamka. Na laiti ungeyafuata, usingekuwa kama hivi ulivyo."
"Kwani nikoje dokta hebu nipeleke katika lile lililokufanya unambie nikusikilize kwa umakini."
"Huwa inahitaji kupokea taarifa mbaya lakini endapo ukijivika ujasiri, basi kila kitu utakiona ni cha kawaida hata kama kimebeba ugumu kiasi gani. Utajisikiaje ukiambiwa wewe kwa sasa hutaweza kumpatia ujauzito mwanamke?" Maneno yake yalinishtua mno na kunifanya niinuke na kukaa kitako maana wazi kulikuwa na tatizo kubwa ila tu alikuwa anashindwa kuniweka wazi kwa kuogopa mshtuko.
"Nitachukulia kawaida japo itaniuma kwakuwa hakuna anayefurahia jambo baya kama hilo."
"Ni kweli hakuna anayefurahia jambo baya lakini kwa mujibu wa vipimo, inaonyesha umeukwaa ugonjwa wa GONO. Ni ugonjwa mbaya sana na unahatarisha mirija ya mbegu za uzazi. Ugonjwa huu nakushauri uutibu kwa dawa za kienyeji. Natafuta fedha lakini mdogo wangu lakini katika hali yako siwezi kupendezewa kukuona ukimkosa mtoto. Usipokuwa makini katika dawa, via vyako vya uzazi vinaharibiwa na gono. Yupo mzee mmoja atakusaidia katika hilo."
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mpaka kufikia hapo nilikuwa nikitokwa na jasho katika kwapa zangu. Moja kwa moja nikarudisha fikra katika yale niliyokuwa nikiyafanya na wanawake. Ilikuwa ni burudani pindi nawapanua mapaja, lakini sasa nimepatwa na janga lakini hakuna hata mmoja aliyekuja kunitembelea angalau kuijua hali ya mtu aliyekuwa akimpa utamu kitandani. Nikazidi kujiona mpuuzi wa mwisho kati ya wapuuzi.
"Huu si wakati wa kufikiria yale uliyoyatenda hapo awali. Cha muhimu ni kuitafuta tiba maadam ipo na vilevile kulipa deni lililosalia hapa shilingi laki moja na elfu kumi." Inamaana yupo mtu aliyenilipia fedha nyingine. Ni nani huyo?
"Nashukuru sana dokta kwa ufafanuzi wako lakini naomba kumtambua mtu aliyenileta hapa hospitali pamoja na aliyelipa hiyo fedha nyingine."
"Ni kijana mmoja mrefu mweusi na alichoweza kuniambia ni kwamba wewe ni mpangaji mwenzake ila kaamua kukusaidia baada ya kuona hakuna anayekujali ukiwa katika hali ya kutojitambua kwa masaa kadhaa" Maelezo yake yakanishangaza kidogo kwasababu pale nilipopanga hapakuwepo na kijana yoyote na kwa kumbukumbu zangu nilizimia nikiwa chumbani kwangu usiku pamoja na mama Zabron. Ikawaje huyo kijana akajua mimi nimezimia?"
"Nililetwa usiku au asubuhi?"
"Ilikuwa saa kumi na mbili asubuhi na huyo kijana alionekana kuwa na haraka sana . Alichoacha hapa ni kiasi cha shilingi elfu thelathini kisha akaondoka na kusema angerejea baada ya muda mfupi lakini hadi leo hii sijamuona." Alizidi kunichanganya kiasi fulani lakini kwa kuhisi tu nikajua ni Sam yule kijana wangu wa kazi.Japo sikuwa na uhakika sana."
"Nsikucheleweshe kwa maswali, cha mwisho naomba msaada wa simu ili niweze kumpigia mtu aniletee fedha kwa ajili ya malipo."
"Usijali, nitampa Joan akuletee maana ipo ofisini kwakuwa sipendi kuwa nayo karibu nikiwa na mgonjwa ili kuepukana na usumbufu."
"Asante dokta kwa mara nyingine."
"Usijali ni wajibu wangu." Akaondoka na kuniacha katika lindi zito la mawazo. Sikuwahi kuwa hata na wazo kwamba ipo siku nitaukwaa ugonjwa wa namna ile japo alinambia dawa ipo. Baada ya muda kama wa nusu saa akaingia Joan na kunikabidhi simu kama nilivyoahidiwa na dokta.
Sikupoteza wakati, nikaandika namba za Sam na kupiga lakini cha ajabu nikaambiwa huduma za mteja ninayempigia zimesitishwa. Nikadhani ni utani nikajaribu tena lakini hakuna kilichobadilika. Nikaingiwa na hofu kubwa na mwili ukahisi baridi. Nikajikuta natamka kwa sauti. "Nimekwisha."
"Umekwisha kivipi?" Alikuwa ni Joan baada ya kunisikia nikijiuliza swali kwa sauti ya juu. Nimfiche kwa ajili gani? Nikamueleza nini tatizo.
"Huyu ninayempigia ndiye msaada mkubwa kwangu katika suala la kupata fedha za kulipa deni ninalodaiwa hapa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Kumbe ni hilo tu hadi unaghafirika kiasi hicho! Kwani dokta amekwambia ni kiasi gani unatakiwa kulipa?"
"Amenambia bado laki moja na elfu kumi ikiwa ni baada ya kulipiwa shilingi elfu thelathini na mtu aliyenileta."
"Nilijua tu lazima utajiwe kiasi kikubwa na ndiyo maana akanitoa humu ndani kijanja ili aweze kupata cha juu." Pamoja na maneno ya Joan, kuwa na ukweli kiasi fulani maaana kwa mtizamo kiasi nilichotajiwa ni kikubwa lakini bado kutolewa kwake mle ndani ilikuwa ni msaada wa kuificha Gono kwake maana ni aibu.
"Siyo mbaya lakini hapa mawazo yote ni jinsi gani nitapata hiyo fedha niweze kuepukana na deni."
"Hilo usijali endapo patakucha kabla hujapata ufumbuzi katika hilo nitajua cha ufanya ili niweze kukusaidia halafu ukishatoka hapa na wewe ufanye uungwana unirejeshee kama mimi nitakavyokuwa nimefanya uungwana kwako." Wakati akiniambia hivyo, akasogeza kiti na kukaa karibu kama ilivyokuwa kwa upande wa dokta wakati akinieleza suala la ugonjwa wangu.
"Asante Joan kwa kulitambua tatizo langu na kulichukulia kama la kwako."
"Tumeumbwa wengi ili tusaidiane katika nyakati zote. Za raha na hata za shida japo wengi wetu huwa hatuyachukulii kwa uzito matatizo ya wengine."
"Asante." Nilimjibu Joan.
"Naomba nikuulize swali la kizushi."
"Uliza tu Joan."
"Eti ni kwanini mwanamke akimfikishia wa kwanza mwanaume huonekana hajiheshimu na wengine hufikia hatua ya kumuita hata majina machafu kama kahaba na mengineyo?"
"Huo ndiyo utamaduni wa mwafrika. Mwanaume humuanza mwanamke na si mwanamke kuwa wa kwanza. Lakini wapo wachache wameshaaanza kuliona kama jambo la kawaida."
" Vipi kwa upande wako utamchukulije mwanamke wa hivyo?"
"Nami kama hao wachache ambao tayari wanaliona kama la kawaida, basi na mimi ni mmoja wao. Kama mwanaume unapofikishiwa hisia na mwanamke halafu ukachukulia vibaya na hata kumjibu maneno ya kashfa, ni wazi unamnyima haki yake. Na kibaya zaidi ambacho wengi bado hawajakitambua ni kwamba upo uwezekano mkubwa sana wa kumpenda mtu uliyekuwa ukimchukia siku zilizopita. Na bado wakaenda mbali na kusahau kwamba moyo wa mtu ukichanua kwa mtu fulani halafu mtu huyo akaupuuzia mpaka ukasinyaa, basi uwezekano wa kuurudisha na uchanue kama mwanzo ni mgumu sana. Hivyo ni vyema zikatumika busara katika hilo."
"Hivi wewe mwanaume mchumba wako yupoje japo sijamuona akija kukujulia hali."
"Sina mchumba na wala sihitaji kuwa naye hata wa kusingiziwa." Wakati tuizungumza, kwa kuyaangalia macho ya Joan, alikuwa tayari ameshajenga hisia juu yangu. Kitendo cha kumwambia kwamba sina na vilevile sihitaji mchumba, nikayaona mabadiliko ya wazi usoni mwake na midomo ikaanza kumtetemka.
"Huyu vipi?" Nikajiuliza kimoyomoyo juu ya hilo. Nikiwa sina hili wala lile, macho ya Joan yakaanza kuteremsha machozi kuashiria maneno yangu yamemuumiza.
"Mbona unalia?"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Kwani kila wanaolia wanayo majonzi mioyoni mwao?"
"Sina uhakika katika hilo."
"Siwezi kuumia ilihali anayesababisha maumivu hayo yupo na sioni sababu ya kumzuia asiyaponye maumivu yangu. Siko tayari kukukosa. Nakupenda na nipo tayari kwa lolote hata kama ni ndoa sasahivi."
Duh! Balaa lingine hilo tena mbele yangu huku mwenzake namiliki Gono mwilini mwangu.
"Unadhani kwa maneno yako naweza kukujibu nini Joan?"
"Siyo kunijibu nini bali useme unanipenda na upo tayari kuishi na mimi hata kuanzia muda huu."
"Siwezi kutoa kauli ya namna hiyo harakaharaka na ukizingatia hapa nilipo ninayo maswahibu kibao na yananichanganya akili kuliko unavyofikiria."
"Hiyo si shida kwakuwa kinachoridhia jambo hili ni moyo na si vinginevyo."
"Mimi nipo lakini hebu naomba unipatie muda na nikishaondokana na tatizo hili ndipo tujue nini kitafuata nakuahidi kuwa na subira."
"Nimekuelewa lakini kumbuka nitakuwa katika wakati mgumu mno katika kuingoja kauli yako ya mwisho."
"Usijali naamini yatakuwa si maamuzi ya kuiumiza nafsi yako."
"Itakuwa moja ya furaha kubwa kuwahi kutokea maishani mwangu. Naomba nikuache kidogo ili niweze kushughulikia suala la deni lako pamoja na chakula" Baada ya maongezi yale, Joan akaondoka na kuniacha katika dimbwi la kuiwaza GONO. Ni ugonjwa niliokuwa nikiusikia katika vinywa vya watu hapo awali lakini sasa upo mwilini mwangu. Hadi napitiwa na usingizi bado fikra zilikuwa ni zilezile hasa ni kwanini niliendekeza tamaa kwa wanawake na kusahau kama yapo magonjwa.
"Amka tule" Sauti ya Joan ilinishtua toka usingizini. Nikaamka na kuketi kitako. Akakaa kitandani na kufungua hotpot yenye chakula. Viazi na nyama. Mh! Kwa mbwembwe ili kunipagawisha zaidi, Joan akaanza kunilisha kwa mkono wake. Raha iliyoje? Nikafaidi kulishwa naye huku pia naye akijilisha kwa pozi hadi pale tuliposhiba.
"Umejisikia vibaya au vizuri kulishwa na mimi?" Joan aliniuliza.
"Nimefarijika mno kwa tendo hili lakini pia limenisisimua na kutamani litokee kila siku"
"Oohps! Vizuri. Nimelipenda jibu lako."
"Nami nimependa ulivyokuwa ukinilisha" alijibu Joan.
"Usijali! Ipo siku utafaidi zaidi ya leo."
"Nitafurahi sana." Nilipomjibu akaniaga na kuondoka huku akiniahidi kuwahi asubuhi kunijulia hali.
***
"Kama nilivyokwambia, usipuuzie dawa ili usijejutia baadaye na kuonekana si chochote kwa mwanamke. Namba nd'o hizo utaongea naye na umueleweshe kwa urefu zaidi tofauti na mimi nilivyomueleza. Naamini atakusaidia kwa asilimia miamoja na hamsini" alikuwa ni dokta wakati akiniruhusu kurejea nyumbani baada ya deni langu kulipwa na Joan."
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Sawa dokta na nitakuwa makini katika yale yote nitakayoelezwa na dokta mwenzako wa kienyeji."
"Nakutakia kila la kheri lakini mdogo wangu kuwa makini katika mienendo yako"
"Asante dokta nitarekebika." Tukaagana na dokta na hapo nikatoka nje ambako nilimkuta Joan akinisubiri. Tukaondoka kwa pamoja na kukodi bodaboda zilizotupeleka moja kwa moja hadi mahali nilipokuwa nimepanga. ukimya ulitawala pale nyumbani kama kawaida. Nikamuongoza Joan hadi katika mlango wa chumba changu lakini ajabu nikasikia sauti za watu ndani tena wakiwa wanafanya mapenzi. Hii ni baada ya kusikia miguno ya kimahaba. Nikashangaa sana lakini sikusita kufungua mlango. Nikanyonga kitasa nacho kikaitikia pasi na ubishi. Hamali! Nikakatisha starehe za watu lakini macho yangu yakashangazwa na mabadiliko ya chumba changu. Kila kitu kilikuwa cha tofauti kuashiria mabadiliko katika chumba kile.
"una kichaa au? Wapuuzi wengine buana?" Ilikuwa sauti ya hasira kutoka kwa mwanaume yule wakati huo akivaa suruali huku mimi nikiwa katika bubuwazi isiyo na mfano. Kutahamaki nikakwidwa na kuanza kushushia ngumi mfululizo toka kwa mwanaume yule. Afya yangu wala haikuwa sawa hivyo ngumi sikuweza kuzikwepa.
Mpaka mama mwenye nyumba pamoja na mume wake wanatoka baada ya kelele za Joan kuomba msaada, tayari nilishalowa damu. Walipofika, wakatuachanisha na kusababisha nipumue lakini macho yangu yakiona maluweluwe.
"Wewe ulikuwa mpangaji wangu lakini ujinga wako nd'o chanzo cha yote yaliyokukuta. na kwa taarifa yako mama Zabron amekomba vitu vyako pamoja na vyake akahama hapa na hatujui ni wapi alikoelekea." taarifa ile toka katika kinywa cha baba mwenye nyumba ilinishtua sana na kuzidi kunitia presha. Sikuamini kile nilichokuwa nikikisikia lakini haikuwa na jinsi nikakubali matokeo. Nikamuomba radhi jamaa niliyemvurugia starehe naye akaniomba radhi kwa kunipiga. Sikuwa na changu pale, nikaondoka mikono mitupu huku nikiwa na maumivu makali sana katika baadhi ya sehemu za mwili wangu kutokana na kichapo. Akili yangu haikunituma kingine kwa wakati huo zaidi ya kuelekea moja kwa moja ofisini kwangu lakini nako huko balaa lilikuwa ni lilelile. Sam alikuwa kafagia kila kitu na kutokomea kusikojulikana. Nikabaki yatima wa maisha. Nilijikuta nikilia sana tena kwa sauti ya juu nje ya mlango wa iliyokuwa ofisi yangu ya kuniingizia riziki. Joan akajitahidi kunibembeleza hadi nilipotulia. Tukapanda tena bodaboda na kulekea nyumbani kwake.
"Jikaze Emma. Kumbuka maisha ni katika mapito mengi tena ambayo hutajua yanakuja kwa wakatti gani." Joan alikuwa akinibembeleza na kujaribu kuniweka sawa. Nilimsikiliza lakini yalipita upande wa sikio lingine. Akili yangu haikuwa hapo. Pesa sina na ninahitaji dawa kwa hali na mali. Nitafanya nini? Nimueleze ukweli Joan? Hapana! Nilihisi aibu kubwa endapo nitathubutu kumwambia hali yangu kiafya. Lakini nitapata vipi pesa na Mirerani sina hata ndugu wa kusingizia ambaye naweza kumueleza shida yangu akanielewa na kunisaidia?
"Mbona unaonekana kama kuna linalokuchanganya akili zaidi ya hili la kuibiwa vitu vyako?"
"Hapana Joan, hakuna la ziada."
Nikamficha lakini moyoni nikiwa na jilaumu sana kwa kushindwa kumueleza ukweli. Lakini upande mwingine nikiona nimeepukana na aibu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Siku tatu baadaye nikiwa naishi kwa Joan, nilipata nguvu kabisa na kuwa na uwezo wa kufanya kazi. Lakini tatizo likaja kwenye kukojoa. MUNGU wangu! Naanzia wapi mimi Emma? Hali hiyo ilinitokea mchana Joan akiwa kazini na jioni alipotoka kazini, akanitaka tukaoge wote. Mshtuko ukanikumba!!!!!
Siku tatu baadaye nikiwa naishi kwa Joan, nilipata nguvu kabisa na kuwa na uwezo wa kufanya kazi. Lakini tatizo likaja kwenye kukojoa. MUNGU wangu! Naanzia wapi mimi Emma? Hali hiyo ilinitokea mchana Joan akiwa kazini na jioni alipotoka kazini, akanitaka tukaoge wote. Mshtuko ukanikumba!!!!! Ile ilikuwa ni aibu kubwa endapo ningemwelezea Joan lakini nisipomueleza fedha nitapata wapi? Nikajipa moyo na kuona asiponielewa atakuwa hanipendi kwakuwa lile ni tatizo linalotibika. Nikapanga jioni akirejea kutoka kazini nimueleze. Saa kumi na mbili iliwadia naye Joan akarejea akiwa ametawaliwa na tabasamu mwanana usoni mwake. Furaha ya wazi meno yake yenye weupe safi yakionekana na kukipendezesha kinywa chake. Akanikumbatia na kuninong’oneza sikioni. “Nataka.” Ujue nini msomaji! Niliingiwa na baridi kali na vinyweleo vikanisisimka. Anataka? Basi hii ndiyo nafasi ya pekee ya kumuelewesha.
“Joan” niliita kiunyonge macho yangu yakiwa usoni mwake.
“Abee” aliitika na kutulia ili kunipa nafasi ya kumueleza sababu ya kumuita.
“Nakupenda sana na nakuhitaji katika maisha yangu yajayo.”
“Huna tofauti na mimi Emma. Mimi pia nakuhitaji lakini naomba unipe kwanza nd’o tuweze kupanga mipango yetu ya baadaye” laiti angejua ananitesa moyoni kwa maneno yake, asingeendelea na maongezi yale.
“Joan.” Niliita tena lakini safari hii machozi ya hisia yalianza kunibubujika. Nikaamini kumbe upo wakati ukifika hata kama roho yako ilikuwa na ugumu kiasi gani, utajikuta ukiymwaga machozi bila kutarajia. Mapenzi ni kitu cha ajabu mno. Ikuwahi kulifikiria hilo hata siku moja wala sikuwahi kulipa nafasi katika maisha yangu. Moyo wangu ulikuwa umegubikwa na tamaa ya ngono tu na si upendo. Mwanamke kwangu nilimchukulia kama wa kunistarehesha tu na si vinginevyo. Kumvua mwanamke nguo yake ya ndani nilichukulia kama usupastaa na nilitamani nikilala kabla ya kupitiwa na usingizi, nikiwaza wanawake niliowapitia katika nyeti zao, nishindwe kuwahesabu. Mawazo hasi kwa kipindi hicho na haswaa niliyachukulia kama jambo la kawaida mno lakini sasa yananipeleka pabaya.
“Nakusikiliza Emma wangu” alijibu Joana huku akijiondoa kifuani mwangu. Na kukaa pembeni yangu huku mkono wake wa kulia akiuzungusha shingoni mwangu kisha uso wake akauinua na kufanya tutizamane.
“Utajisikiaje pindi likitokea jambo ambalo laweza kuliteteresha hili lililopo mioyoni mwetu?” nikafungua kinywa changu na kumuuliza Joan swali la msingi.
“Haswa likijitokeza jambo gumu, unaiweka pupa pembeni na sidhani kama utapata utatuzi usiokuwa na manufaa kwa pande zote mbili.” Alijibu bila kupoteza muda.
“Mwanzo wa mapenzi ya wengi, hutawaliwa na furaha na hata likitokea lisiloeleweka, huwekana sawa tena wao wenyewe bila kuhitaji msaada wa yeyote yule. Lakini kadri siku zisogeapo, watu hao hubadilika na mioyo yao hutawaliwa na fikra tofauti na yote hii ni, ni kwasababu ya dharau.” Bado sikutaka kumuweka wazi haraka namna ambayo wengi huwa tunaitumia katika jambo rahisi.
“Kwani kuna tatizo gani??” aligusa penyewe Joan. Alihitaji majibu name sikuzunguka tena, nikaamua kulenga point ya jambo husika.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Joan, katika mwili wangu kuna tatizo ambalo linahitaji msaada wa haraka” nilipofika hapo nilisita kidogo maana mapigo ya moyo yalianza kunienda kasi hadi mimi mwenyewe nikajishangaa. Nikabaki kutumbua macho huku nikiwa kimya.
“Lipi tena hilo Emma hadi upatwe na shaka katika kunieleza?”
Nikafumba macho na kumwambia Joan, “N’na GONO.” Nikategemea kumuona Joan akishtuka na hata kunitimua nyumbani kwake lakini haikuwa hivyo. Alichoonyesha ni kutafakari kisha akaniambia, “itabidi utumie dawa haraka ili ukishapona tulifurahie penzi letu.” Katika hili nilihisi nipo ndotoni nap engine muda wowote ningeshtuka na kuketi kitako huku nikihema kwa nguvu lakini haikuwa ndoto bali kitu cha kweli. Furaha yangu sikuidhihirisha kivingine zaidi ya kumkumbatia. Naye akanipokea kwa furaha. Basi ikawa furaha na siyo huzuni tena moyoni mwangu.
“Nashukuru sana Joan wangu.” Hapo sikutaka kutumia neno asante hii yote niitafsi ASANTE kama haina nguvu zaidi ya NASHUKURU.
“Usijali wewe ni wangu name ni wako. Cha muhimu ni kuutunza upendo wetu. Tusikubali kutetereshwa na walimwengu katika penzi letu ili siku zote tuwe ni wenye kuishi kwa Amani.” Maneno ya Joan yalikuwa mazuri na ama kwa hakika nikashukuru kumpata mwanamke wa aina yake. Tukayaanza maisha yetu nikiwa naishi pale kwake ambapo hata siku moja Joan hakuwahi kunionyeshea dharau. Kwanini nisimpende? Kwanini nisimuheshimu? Anastahili kuheshimika name sikuona cha kunifanya nisimpe heshima yake.
Siku huwa zinajongea tu wala hazina kurudi nyuma. Baada ya kutumia dawa, nikapona kabisa na siku ya kwanza nakutana na Joan, nikampa ujauzito. Furaha iliyoje. Hakika MUNGU alinijibu kwa vitendo kumaanisha mimi ni mzima kabisa. Tulitawaliwa na amani wakati wa kuilea mimba. Lakini bahati mbaya siku ya kujifungua nikakipoteza kilicho chema. Joan kipenzi changu akapoteza maisha. Hatukuwa tumejipanga kwa kiasi kikubwa hivyo baada ya msiba, sikuona sababu ya kuendelea kubaki Mirerani. Nikaifunga safari kurudi Tanga nyumbani kwetu. Haikujalisha niliondoka katika mazingira gani. Nikapokelewa mimi na kichanga changu. Shangazi yangu akabeba jukumu la kukilea. Alikuwa ni mtoto wa kike nikaamua kumpatia jina la mama yake ili isiwe rahisi kwa mimi kumsahau Joan. Nikajiingiza katika shughuli ya kilimo ili niweze kumpatia huduma nzuri mwanangu. Kila siku sikuchoka kumuomba Mungu amlinde mwanangu na kumuepusha na magonjwa na kweli aliyasikia maombi yangu hadi Joan wangu akatimiza miaka mitano akiwa na afya tele japo maisha yangu hayakuwa mazuri kifedha. Nilishajitenga na masuala ya wanawake na nikaamini unapendwa na kutamaniwa ukiwa unang’aa na si katika hali ya uchovu. Wakati wangu wa kujihusisha na kilimo hakuna aliyeonyesha matamanio kwangu nami nikahisi kufarijika kwasababu ningeweza hata kumkata mwanamke kwa panga. Kilichokuwa kimenitokea Mirerani, ni kikubwa mno.
“Habari yako?” Ni takribani miaka saba ilikuwa imepita lakini kamwe nisingeweza kuisahau sauti ile. Sauti ya mtu aliyeniachia elfu thelathini hospitali na kisha kutokomea kusikojulikana baada ya kuondoka na vifaa vyangu vya kuniingizia chochote mfukoni nikiwa nimekaa napulizwa na kiyoyozi. Alikuwa ni Sam. Nikageuza macho upande wa kushoto ilikotokea sauti ile. Kilichokuwa kimenipeleka mjini siku hiyo ni kuuza mazao yangu ndipo nikabahatika kukutana na mtu huyo. Nikiwa nimechoka kwelikweli na baiskeli yangu ya kichovu. “Sam!” nijikuta nikilitamka jina lake kwa sauti uliochanganyikana na mshangao mkubwa. Si mshangao wa kwamba ni mtu aliyeniibia na leo yuko mbele ya macho yangu hivyo ni mimi tu kujua
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
nimfanyeje, lah! Alikuwa amebadilika. Akiwa na gari na akionekana mwenye fedha. Kweli maisha ni mzunguko mrefu na huwezi tambua ni wapi ulipo mlango wako wa kutokea. Yawezekana wewe ni mponda kokoto lakini kumbe si ufunguo sahihi wa maisha yako. Cha msingi ni kujaribu huku na kule pasipo kukata tamaa. Kumbuka adui mkubwa aliyekaribu na maisha ya mwanadamu, ni kukata tamaa. Ukishakata tamaa unapoteza mengi hasa ya muhimu.
“Naam kaka!” aliitika huku akisogea karibu yangu na kunipa mkono. Tukasalimiana kisha akanipatia namba yake ya simu katika karatasi. Akaondoka huku akiniachia kiasi kikubwa cha fedha ambacho mara ya mwisho kukimiliki ilikuwa ni Mirerani nilipopata madini. Ujue nilibaki nimeduwaa kwa muda kabla ya kuipanda baiskeli yangu na kurejea nyumbani nikiwa na shauku ya kukutana tena na Sam.
“Baba mbona leo furaha hivyo?” mwanangu aliniuliza name sikumficha kwakuwa uongo hujiumbua pale usipopataraji. Tukafurahi wote na mwanangu na jioni nikatafuta simu kwa jirani nikampigia Sam. Akanielekeza mahali pa kukutana. Ilikuwa ni nyumbani kwake. Haki ya MUNGU pata fedha uijue dunia. Maisha ya kifahari wapo watu wanaoyaishi wakiwa hapa hapa Tanzania na pengine wapo waishio ulaya lakini maisha yao si mazuri kama watanzani tunaosadikika kuwa maskini. Mke wake pia alikuwa sawa na mng’aro wa nyumba yake. Tuliongea mengi na kufurahi kwa pamoja karibia muda wa masaa mawili na ahadi kibao aliweza kuniahidi lakini kubwa zaidi ambalo si mbaya nawe msomaji ukalitambua. Aliweza kuniambia kwamba ishi na watu leo vizuri haijalishi upo katika nafasi fulani ili kesho uweze kupokea mema kwa wachache kwani si wote wakumbukao mema waliyotendewa. Ni maneno ya hekima sana na ni vyema wengi tukayaweka akilini kwakuwa hakuna aijuaye kesho yake. Siku hiyo wakati wa kurejea nyumbani alinirudisha kwa gari lake na kunitaka tukutane kesho tena ili aanze kutekeleza alichoniahidi.
Wapo wanaoahidi na ahadi zao kuishia hewani lakini kwa upande wa Sam aliuchukulia wema wangu wa nyuma kwa uzito. Cha kwanza alinikabidhi duka kubwa la vifaa vya umeme pamoja na ujenzi lililokuwa Muheza mjini. Hakuishia hapo, mwanangu akahamishiwa Dar katika International school liyokuwa akisoma mtoto wake. Nipewe nini tena? Umaskini nikauaga. Hadi hapo sikuwa na mwanamke lakini nikaamua kuoa mwanamke ambaye sikutaraji kama ningemuona tena. Huyu alikuwa ni Nasra. Nilikutana naye tena Dar katika mizunguko yangu ya biashara ambapo hadi wakati nakutana naye, nilikuwa nikimiliki biashara zaidi ya tatu zote zikiwa za halali. Tukaona na akafanikiwa kunizalia watoto watatu kabla sijamfumania na kijana wangu aliyekuwa akiniendesha. Nikamfukuza na habari ya kuoa sikuhihitaji tena. Nikaamua kutulia na maisha yangu huku wanangu wote waisoma shule nzuri zenye kutoa elimu bora lakini katika wote kipenzi cha moyo wangu kuliko wote ni Joan. Kila alichokihitaji nilimtimizia bila kufikiria ikiwa ni njia ya kumuenzi mama yake kwani wakati wa uhai wake aliponiambia nataka sikuchelewa mradi tupo ndani. Nilimpa bila kumchelewesha. Kwa sasa ni msichana mkubwa na nipo tayari kupokea mahari ila siyo kwa muhunimuhuni kama mimi enzi hizo.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwa sasa umri wangu umeenda na pindi nikiwaona vijana wakikukuruka na wanawake mimi huishia kuwaonea huruma kisha naelekea kwenye kahawa kupiga stori na wazee wenzangu. Ndiyo maana kama unakumbukumbu nzuri mwanzo wa kisa hiki, nilikuwa nikipita katika uchochoro wa nyumba ya kulala wageni na masikio yangu yakanasa sauti za mahaba katika chumba. Na baadaye nikawashudia vijana wawili ambao bado damu zinawacheka wakitoka kwa mwendo wa madaha. Nikawasikitikia na ndiyo kikawa chanzo cha kuwasimulia kisa hiki. Asanteni kwa wote mliochukua muda wenu kusoma maandishi haya tangu mwanzo. Yapo makosa madogomadogo yaliyojitokeza nap engine kuwakwaza baadhi yenu lakini hebu niwieni radhi ili wakati mwingine nijitahidi kurekebisha pindi nikiamua kuwaletea kisa kingine kitamu kama hiki cha na mimi nataka. Wengi walitaka nikawapa lakini nikapata kupitia magumu mengi.
Mwisho!!!!!!
0 comments:
Post a Comment