IMEANDIKWA NA : ELIADO TARIMO
*********************************************************************************
Chombezo : Mama Vanessa
Sehemu Ya Kwanza (1)
Muda ulikuwa umeenda sana macho ya Lucas Manyama yalianza kujifumba yenyewe ishara kuwa mwili wake ulikuwa umechoka na ulihitaji kupumzika. Saa yake ya ukutani ilionenesha kuwa ilikuwa ni saa 8 usiku na alikuwa anasoma story pendwa inayoitwaSECRET OF LOVE iliyotungwa na mtunzi maarufu kwa jina Eliado. Nia ya kusoma story hii usiku ni kupunguza mlundikano wa mawazo aliyokuwa nayo na kutafuta faraja kupitia matatizo ya wengine..Siku hiyo pia ni siku ambayo alikuwa na sress nyingi sana ambazo kwa yeye alihisi kuwa zilikuwa zinamzidi umri. Kwanza ni siku ya 6 tangu asimamishwe kazi kutokana na tuhuma za uwongo ambazo boss wake alijaribu kumbambikizia. Si kusimamishwa kazi tu bali pia mke wake kuondoka nyumbani kwa madai kuwa amemchoka. Ilikuwa haimuingii akilini kuwa eti mke wake amechoka na kuamua kumuacha katika kipindi hiki kigumu.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kwa nini hakunichoka kipindi nikiwa nina kazi? kwa nini hakuondoka kipindi hicho? nini kimemfanya aondoke?”Aliwaza Lucas bila kupata majibu. Usingizi kwake ulikuwa ni mgumu sana na alitamani hata asilale. Mziki wa taratibu ulitosha kabisa kuelezea ni jinsi gani alivyokuwa anakijisikia. Machozi yalitosha kabisa kulowanisha karatasi za kitabu cha story alichokuwa anasoma. Badala ya kufuatilia kitabu hicho ambacho kilikuwa ni kizuri alikuwa amekishika kama pambo na wala alikuwa haelewi kilichoandikwa. Alikuwa na huzuni iliyopitiliza. Alitamani hata kama asubuhi ingefika alione jua alihisi labda kuliona jua kungefanya roho yake kutulia. Alijawa na hisia kuwa giza la usiku huo lingeweza kumuathiri kwa kiwango kikubwa. Mvinyo wa kizungu aliokuwa anakunywa hakuweza hata kuusikia, alikunywa kama maji.
Alikunywa hakulewa.Kila alipokuwa anavuta kumbukumbu ya yaliyomtokea alilia kilio kisicho na machozi.
“Nilimpa kila kitu nilimpenda kupita vitu vyote lakini leo ananiacha?” aliwaza bila kupata majibu.
Huyu mwanamke alikuwa ni kila kitu kwake, huyo mwanamke alimtoa mbali, huyo mwanamke alikuwa na umuhimu sana maana kwake alikuwa kama mama na hii ni baada ya kumpoteza mama yake mzazi ambaye aliitwa na Mungu.Apumzike kwa amani mama yake mpendwa.
“Huyu mwanamke nilimsomesha kwa gharama zangu huyu mwanamke nilimwinua kutoka familia masikini mpaka akafikia hapo alipo. Hiyo kazi anayoringia ni sawa tu mimi ndio niliyomuwezesha kwa maana bila elimu niliyomsadia kuipata hasingekuwa hapo.Lakini kwa nini sasa hataki kuyatambua hayo. Kwa nini athamini mchango wake kwangu?”.
Manyama aliongea kwa nguvu utafikiri labda huyo mwanamke wake alikuwa hapo. Alinyanyua glass ya kinywaji kikali alichokuwa akinywa na kukidigida utadhani sio kilevi. Mara simu yake iliita na aliangalia kwa haraka maana sio kawaida yake kupigiwa simu usiku. Aliichukua simu ambayo ilikuwa kwenye chaji na kuipokea.
“Helow mambo Lucas” ilisiskika sauti nyororro sauti ya kike iliyojaa bashasha na furaha.
“Mambo poa, sijui naongea na nani?”.
“Jamani mbona unaharaka hivyo, mimi najua hunijui lakini utanijua maana ni zaidi ya malaika niliyetumwa na Mungu nije kukukomboa na kukuondoa kwenye upweke uliokuwa nao”.
“Makubwa kumbe kuna binadamu malaika..Utanisamehe kama huwezi kujitambulisha sitoweza kuongea na wewe.” Lucas alijibu kwa hasira na kukata simu.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kama hiyo haitoshi aliamua kuizima kabisa, alivurugwa akavurugika.Alihisi kabisa walikuwa ni vibaraka wa mkewe Misheli walitumwa kumkejeli.Pamoja kuwa alichukua maamuzi hayo bado roho ilimsuta kwa jinsi sauti hiyo ya kike ilivyokuwa tamu masikioni mwake. Alitamani sana kumjua mwanamke huyo lakini hakutaka kuwasha simu. Alijitupa kitandani na kuanza kuutafuta usingizi ambao takribani wiki nzima alikuwa akiupata kwa shida sana. Aliendelea kuwaza vitu vingi sana ikiwa ni pamoja atapata wapi pesa ya kodi kwa sababu mwezi huo ndo ulikuwa wa kulipa kodi hili hali amesimamishwa kazi kwa sababu ambazo ni za kusingiziwa.
“Yaani Boss Yule mwanamke ni mchepuko wake tu je ingekuwa ni mke wake si angenifunga jela kabisa.Mwanamke mwenyewe hamtaki anataka vijana wezniye yeye kazi kuonga tu. Faidha ametamka kwa kinywa chake kuwa hampendi boss bali mimi sasa mimi ningefanyaje. Yaani mwanamke mzuri kama Faidha amejilengesha mwenyewe mimi nimwache kisa eti ni mchepuko wa boss ambaye hajawahi kulala naye?”.Manyama aliendelea kuwaza na kuwazua.
“Akafu mke wangu alijuaje yote haya yanayoendelea kazini?. Na kwa nini hakuniuliza akaamua kuondoka kimya kimya bila hata kuniambia sababu. Nimepiga simu mpaka nyumbani kwao hawapokei tatizo ni nini hasa?”.
Maswali yote hayo hayakuwa na majibu kwa kijana huyu. Alifikiria jinsi kupata kazi ilivyokuwa ngumu. Alifikiria kuwa hata kazi hiyo aliipata kwa msaada wa mjomba wake. Ni kweli elimu yake ilikuwa nzuri kuliko wafanyakazi wengine na hata utendaji wake wa kazi ulikuwa na ufanisi mkumbwa kuliko wengine. Tatizo kumbwa ni mfanyakazi mpya wa mambo ya masoko aliyeletwa hapo kazini kwao. Msichana huyu alikuwa mrembo kupita kiasi. Urembo wa Faidha ndo huo ulileta kizaazaa katika taasisi yao. Lucas Manyama ni mfanyakazi wa benki moja ya kibiashara mkoani Mara. Ni miezi 3 tu tangia apate kazi hiyo na katika muda huu mfupi ndo analetwa Faidha binti ambaye alimvutia kila mwanaume hapo benki. Boss naye alikuwa mtu aliyevutiwa na mfanyakzi huyo na yeye alitumia cheo chake kumshawishi na kutaka kuwa naye. Lakini Faidha alikuwa ni mwanamke mjanja sana bado aliangalia future yake. Ni msichana ambaye hakupenda kujihusisha kimauhusino na wazee.
Lakini moyo wake ulivutiwa na kijana Lucas ambaye alikuwa ni kipenzi cha wafanyaakzi wengi na wateja kutokana na ufanisi wake wa kazi kuwa uliotukuka. Hali hii ilijenga ukaribu sana na kupeleka kujikuta wakizama kwenye uhusiano bila kutajaria. Faidha alijua kabisa kuwa Lucas alikuwa na mke ambaye naye ni mfanyakazi wa taasisi nyingine hapo hapo Musoma. Wote waliingiwa na upofu ambao kwa kweli ulileta majanga makumbwa kwa upande wa Lucas. Lucas alijiuliza kama walifanya siri yeye na Faidha imekuwaje mkwe akajua na kuamua kuondoka. Mkewe aliondoka ghafla bila kutoa sababu yoyote na kipindi hiko tayari alishasimamishwa kwa kazi kwakile kilichoitwa ubadhilifu wa fedaha. Kitu kingine kilichokuwa kikumuuama ni kuwa Boss na mkewe walikuwa wakijuana maana walitoka mkoa mmoja na walikuwa karibu.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Lucas Manyama alihisi labda Boss ameamua kumwaga sumu kwa mkewe na ndio maana ameondoka. Alichokifanya alilala na asubuhi na mapema aliamka na kuelekea ukweni ambapo ni Bukoba. Aliamua kwenda ili kujua kama mke wake alirudi huko au la kuna sehemu ambayo alienda bila yeye kujua. Ila ile simu alivyoiwasha asubuhi hiyo alikutana na meseji nyingi za yule mwanamke aliyempigia simu usiku huku akijichkesha chekesha.
“Lucas najua upo katika kipindi kigumu sana, kipindi cha mawazo lakini mini mimi ndo naweza kukufumbua macho na kujibu maswali yako yote magumu yanayokutatanisha. Hata mimi nina maumivu sana ila naomba tushirikiane nitakufuta machozi na pia nitakufanya ujue ukweli kuhusu mkeo na boss wako..Ukiwa tayari tafadhali nitafute naitwa mama Vanessa.” Meseji ilisomeka hivyo na kumfanya Lucas hazidi kuchangnyikiwa. Alitamani kushuka kwenye gari lakini aliamua kuendelea na safari ya ukweni maana ingetoa mwanga pia kwa nini mkewe aliamua kuondoka tena kimya kimya…
Meseji hiyo ilimfanya atamani kushuka lakini tayari alikuwa kwenye gari. Huyo alifika Mwanza na kupanda gari la kuelekea Bukoba. Alifika ukweni na alipokelewa na baba mkwe. Alipokelewa vizuri tofauti na alivyotarajia hapo awali. Na baadaye alikuja mama mkwe.
“Karibu sana mwanangu naona umefanya ziara ya kushtukiza kama muheshimiwa Rais afanyavyo.
“Ni kweli mama angu sijui mnaendeleaje maana nimekuwa nikipiga simu kwa muda mrefu mmekuwa hampokei”.
“Tusamehe tu baba si unajua huku shughuli za shamba zinatubana hatuna hata habari na hizo simu” alidakia baba mkwe.
Kimya kilitawala kidogo kabla ya Lucas kuvuta ukimya.
“Wazee wangu mimi nimekuja kuwasalimu lakini pia mwenzangu aliondoka wiki sasa imepita bila kuaga sijui alifika huku kwenu?”
“Hapana mwanangu Mishel hajafika hajafika huku ila mara ya mwisho kuongea naye alisema kuwa umebadilika. Umekuwa Malaya na unaangaika na mapenzi nje ya ndoa. Pia kuna mwanamke kazini kwako anakuchanganya na umeapa kumuoa. Mwanetu amesema kuwa hayupo tayari wewe umletee magonjwa hivyo amejeitoa kwako. Ameamua kuanza maisha yake na sisi utaratibu wetu ni kuwa mwanamke akishaolewa basi akae huko kwa mme wake na wakaichana hasirudi nyumbani atafute mwanaume mwingone wa kumuoa.” Aliongea maana mkwe wake kwa hisia na kukaa kimya.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mama yangu na baba yangu naweheshimu sana lakini kwa kitendo hiki cha Mishel kuondoka kimya kimya bila hata kuoga na kutoa sababu za kufanya hivyo ni kukosa heshima kwa mume. Kama kulikuwa na tuhuma ilimpasa kuniuliza ili nimwelezee.Hapa nilipo nimesimamishwa kazi kwa sababu ya Boss.
“Umefukuzwa kazi?, kisa nini?”alihoji mama mkwe kwa mshangao.
“Nasingiziwa tu vitu vya ajabu ambavyo sijavifanya. Na kilichotokea ni kwamba kuna mwanamke alikuja na huyo mwanamke mpo ofisi moja sasa na uhusiano na boss na uhusino huo umemfanya hasifanye kazi na mimi kuwa nafanya kazi sana. Mimi kuhoji kwa nini ananiachia kazi zote ndo shida ilipoanzia.”
“Pole sana baba ingawa maelezo yako na ya mwenzio yanatofautiana. Sisi hatutaki kumtafuta mkorofi cha msingi mtafute mke wako kisha mje tuyazungumze. Nikushauri pia mwanangu ndoa yenu bado changa sana na mmetoka mbali sana jaribu kukumbuka na usikubali kumpoteza mke wako kiurahisi. Usikubali kuachana na mkeo maana umewekeza sana kwake. Umemsomesha mpaka amepata kazi. Lakini usitumie wema huo kumnyanyasa. Yeye tulishaongea naye na tutaendelea kumsahauri.”Aliongea Baba mkwe.
“Nimewaelewa wazazi wangu naomba mnisaidie kumpigia simu na kumweleza kuwa alichokifanya sio kitendo cha uungwana kabisa.”
“Sawa baba tunashukuru kwa ujio wako pia tumegundua mengi..Tutafikisha ujumbe wako.
Lucas Manyama aliaga na kuondoka zake. Tofauati na siku zingine ambazo huwa anamwachia pesa ya matumizi siku hiyo alikaa kimya hakutoa hata elfu 1. Hiyo ilikuwa ni ishara kuwa amechacha na hana pesa. Aliamua kuondoka na kurudi zake Musoma. Akiwa njiani aliendelea kutafakari juu ya mahali ambapo mke wake angekuwepo.Kwa kuwa muda ulikuwa umeenda sana ilimlazimu kwenda kulala Mwanza ili kesho ndo aende Musoma. Alivyofika Mwanza aliamau kumtafuta rafiki yake kwa jina Kimaro. Huyu alikuwa ni rafiki yake wa kufa na kuzikana tangia wakiwa chuo. Walipendana sana na waliishi kama ndugu. Kimaro alipokea simu lakini ilionekana kama kulikuwa na tatizo kidogo alionekana kuwa sehemu yenye kelele nyingi.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kimaro alimwandikia sms na kumueleza kuwa yupo sehemu moja hivi wanakula bata. Lucas akamweleza kuwa na yeye yupo Mwanza stend. Kwa kuwa sehemu yenyewe haikuwa mbali sana alimwelekeza afike hapo. Manyama hakutaka kubisha na alienda moja kwa moja mpaka sehemu hiyo ambapo music wa bendi ulikuwa ukipigwa. Aliingia huku akiwa na hofu kwa sababu mfuko wake haukuwa vizuri. Watu walikuwa ni wengi sana na wenye furaha. Alipewa kiti wakaketi na alimkuta rafikiye Kimaro akiwa tayari ameshapendeza. Aliongea lugha za kuashiria alianza kulewa. Hakuwa peke yake bali na mwanamke pembeni yake ambapo Lucas hakumtambua. Lucas kwa haraka haraka alijua kuwa huo ulikuwa ni mchepuko wake tu. Na yeye alikwa akinywa bia tena zile za bei ghali.
Lucas alivyoambiwa aagize aliagiza maji jambo ambalo lilimfanya Kimaro kuwa mkali na kusema apewe kinywaji anachotumia kwa sababu pesa sio tatizo. Baada ya kulazimishwa aliamua kunywa ili kupunguza mawazo. Alikunywa pombe kali kabisa na stori ziliendelea. Lucas alimweleza rafiki yake jinsi anavyoumia kwa sababu mke wake ameondoka katika mazingira tatanishi. Alimweleza kuwa hapo ametoka ukweni nab ado mke wake hayupo. Anaumia sana maana hajui mkewe mahali yupo.
“Huna haja ya kuumia toa taarifa polisi tu kuwa amepotea.Ahhhhhh kwa dunia ya sasa mtu hawezi kupotea atakuwa yupo mahali amewekwa. Wanawake si viumbe vya kuwaamini zaidi ni kuwaogopa sana maana wanaweza kufanya kitu kibaya na ukajuta kumfahamu”.
“Ebu tuyaache hayo maana yanaumiza naamini wapo wasichana wenye roho nzuri kama huyo uliyekaa naye.
“Bora hata umeliona hilo maana nilianza kuboreka” alisema mrembo huyo.
Waliendelea kunywa na kula na sasa Lucas alianza kulewa. Watu kwenye ukumbi huo walikuwa na raha na wengi walionekana ni watu wenye uwezo kifedha. Watu na vitambi vyao walikuwa wakicheza mziki na kuomba nyimbo walizokuwa wakizipenda. Ilikuwa ni burudani iliyoleta raha kwa kila ambaye alikuwa eneo hilo.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Eeeeeeeh!!!!!!! yule si shemeji… yule au naona kwa makengeza ebu angalia”,Kimaro alisema huku akionesha mkono kule mbele.
Lucas ilibidi aangalie kule mbele. Hakuamini macho yake alipomuona boss wake akiwa anacheza mziki na mkewe. Macho yalimtoka kama mjusi aliyebanwa na mlango. Alianza kupiga hatua kuelekea mbele lakini rafiki yake alimshika mkono na kumwambia.
“Haikupasi kuwa na papara kwenye mambo haya. Tulia tuone mwisho wa mchezo huo”
“No no I say no I cant tolerant any more(hapana, hapana nasema hapana siwezi vumilia tena)..” Lucas alinyanyuka kwa nguvu na kuanza kuelekea kule mbele ambapo boss na mkewe walikuwa wanacheza.
Kimaro ambaye na yeye alionekana kuwa tayari ameshalewa alinyanyuka kwa nguvu na kumshika Lucas. Alitumia nguvu zake zilizochagizwa na pombe kumzuia na kumsogeza kwa pembenni.
“Ndugu yangu nakuomba unisikilize kwa umakini sana kwa sababu ulimwengu huu sio wa kutumia nguvu bali akili. Huyo ni mke wako sawa najua anauma kuliko kitu kingine chochote ila sasa yupo na boss wako na wewe umesimamishwa kazi tu. Kitu cha kujua ni kwamba hujafukuzwa kazi bali umesimamishwa kazi hivyo lazima uwe mjanja ili kurudishwa kazini ikibidi huyo boss yeye ndo afukuze..
“Nifanyaje sasa”, Lucas alihoji kwa kuvuta pumzi..Hasira zilimshuka kidogo.
“Unatakiwa kutumia akili . Kwa kuwa Boss wako yupo na mkeo hapa tupate ushahidi wa picha. Tukishapata ushahidi huo ni rahisi sana kuieleza jamiii kuwa boss amekunyanyasa na anatoka na mkewe na pia anatumia fursa hiyo kukufukuza kazi.”.
“Wazo zuri sana sasa utawezaje kuwapiga picha bila wao kujijua na bila kuleta madhara maana yule boss ni mkorofi sana”
“Hilo niachie mimi wewe rudi kakae.Vaa roho ya ushujaa na uwe na amani kwa sababu huu mchezo sisi ndo tutashinda.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Lucas Manyama alionesha kuelewa na alirudi kukaa kwenye kiti na alishangaa kukuta kuna msichana mwingine amekaa kwenye kiti chake. Macho hayana pazia kwa sababu msichana huyo alikuwa akifanana kabisa na msichana wa mwanzo. Kwa haraka haraka aliwaza na kugundua kuwa anaweza kuwa ni pacha wake. Manyama alivuta kiti na kukaa.Alielekeza macho yake mbele na kuangalia kwa makini kama kweli rafiki yake Kimaro anaweza kufanikisha kuwapiga picha. Hakumwona hata huyo Kimaro jambo ambalo lilizidi kumchanganya.
“Shemeji usiwe na wasiwasi wala usiwaze sana wanawake bado hawajaisha huku duniani na kama kweli yule ndo mkeo na anayafanya yale huku wewe ukiangaika kumtafuta ili kujua alipo basi huna chako.”
Yalikuwa ni maneno ambayo yalizidi kumuuma Lucas na kutamani kama angefanya kitu. Bila kutarajia alinyanyuka na kusimama. Aliwaza kutoweka eneo hilo na kwenda sehemu nyingine kabisa mbali na upeo wa vitu vya kuumiza vilivyokuwa vikiendelea. Kimaro alimshika begani na kumwambia arudi kukaa.
“Vipi umekamilisha huo mpango?”.
“Nimekamilisha kwa kiwango kikumbwa”.Kimaro alijibu huku akimpa simu yake ili aweze kuangalia. Aliziona picha na jinsi mkewe alivyokuwa amekumbatiwa na boss wake. Alishindwa kujizuia machozi yalimtoka.
“Jamani Lucas usiwe na roho ndogo hivyo wewe ni mwanaume usilie jipe moyo”alisema Yule msichana aliyekuja mara ya pili.Msichana huyo aliongea kwa upole huku akitoa kitambaa chake na kumpa afute machozi. Lucas alisista kukichukua lakini mwanamke huyo kwa ujasiri alijisogeza zaidi na kumfuta machozi. Ilikuwa ni faraja kwa Lucas kwani alichukua glass akaminiia kinywaji chake na kunywa. Alikunywa kwa nguvu kisha kushusha chini. Aligonga meza kwa nguvu kuwa aongezewe kinywaji. Muhudumu alikuja na kumuongezea. Sasa ilikuwa ni kunywa kwa nguvu ili kutafuta stimu za kupunguza mawazo. Kila mtu alikunywa kadri alivyoweza na nikama boss na mke wa Lucas walishtuka na kutoweka ghafla eneo hilo. Wao wakabaki wanaendelea kula raha na kujaribu usahau shida ambazo walikuwa nazo.
“Sasa ni saa ya utambulisho, kila mtu akae kimya” aliropoka Kimaro.
Watu wote walicheka maana kumbe wengine hapo mezani walikuwa hata hawafahamiani. Kimaro akanza kujitambulisha yeye.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mimi naitwa Godfrey Kimaro kijana mdogo mwenye mafanikio hapa mjini”.Wote kwa pamoja walitabasamau.
“Mimi naitwa Lucas Manyama mwanaume ambaye namiliki mke mzuri mjini lakni Boss akanipokonya”..Hapo kila mtu akaangua kicheko huku Lucas akitingisha kichwa kuonesha masikitiko yake juu ya jambo hilo.
“Mimi naitwa Julieth mpenzi wa kijana mwenye mafaniko hapa mjini”
“Mimi naita Juliana pacha wa Julieth”.
“Safi sana sasa timu imekamilika na hatuwezi kukubali mziki uishie chini. Kila mtu amshike mtu wake tunaenda mbele kucheza.” Kimaro aliongea huku akimnyanyua Julieth. Pombe ilikuwa imekolea na hao taratibu walisogea mbele kwenda kucheza mziki na kuwaacha Lucas na Juliana wakiwa wanaangaliana.Juliana hakuwa na aibu maana na yeye pombe ilikuwa imekolea. Alisimama akajitingisha tingisha kidogo kwa madaha nakuonesha ni jinsi gani alivyoumbwa akaumbika. Macho kodoo macho ya Lucas yalimkodolea huku akimkagua kuanzia kifuani kushuka chini. Juliana akanyanyua mkono mmoja kisha akampatia ishara kuwa wanyanyuke. Lucas alikuwa ni mtu mwenye aibu sana hivyo alikuwa akijifikiria kwenda mbele kucheza muziki. Lakini mikono laini ya Julaina ilitosha kumsisimua na kumuinua kutoka pale kwenye kiti.
Hao walisogea mbele na kuanza kucheza. Mbele kulikuwa na watu wengi hivyo ilikuwa ni swala la kubambia kwa kwenda mbele. Sasa ilikuwa ni fursa ya Lucas kuona ulimbwende wa binti huyo. Kwa kweli alichanganyikiwa na alitamani hata kumtongoza usiku huo huo. Alijizuia lakini kitendoa cha Juliana kuzungusha nyonga na kumtingishia makalio kilimfanya kumtamani mlimbwende huyo. Juliana naye alimwonea sana huruma na aliamua kumfanyia vitu ambavyo vingempa faraja usiku huo. Alikuwa akicheza na binti huyo huku mawazo yake yakiwa kwa mtu aliyejitambulisha kuwa anaitwa Mama Vanesaa. Aliifikiria ile sauti ambayo ilionekana ya binti mdogo kabisa na jinsi mwanamke huyo alivyoamua kujitambulisha kwa jina mama Vanesa. Baadaye walirudi kukaa na sasa walikuwa wameagiza nyama choma. Walikula na wakati wakiendelea kula simu ya Lucas iliita na kuangalia alikuwa ni mama Vanesa. Alikata na kumuomba amtumie sms kwa kuwa yupo kwenye kelele.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nimepata dharura ambayo itanifanya kesho kutwa nisafiri hivyo nilikuwa naomba kama hutojali tukutane kesho nikueleze matataizo yangu kisha tupange mikakati ya kusaidiana kwa sababu matatizo yako tayari nayajua.” Meseji kutoka kwa mama Vanesa ilisomeka hivyo.
“Kula brother nataka nikupe huyu mtoto Juliana ukalale naye upunguze hata mawazo.”Iliingia meseji ingine kutoka kwa Kimaro.
Alitabasamau kimoyomoyo na kujisemea kama litataokea hilo basi itakuwa bahati ya mkenge. “Mtoto mzuri hivyo nitamla mpaka aimbe zeze”aliendelea kuwaza huku akiweka finyango ya nyama mdomoni.Mara Juliana na yeye alichukua nyama na kumlisha jambo lililozidi kumsisimua na kujikuta akitamani hata kumrukia muda huo. Viungo vingine vya mwili navyo vilishasimama kwa hisia za mahaba…
Waliendelea na sasa Kimaro alikuwa akitumia jina lake na uwezo wake wa kushawishi kumtaka mpenzi wake Julieth aweze kumkubali Lucas na ikibidi ampe faraja usiku huo. Kwa hiyo kulikuwa na mawasilaino na watu walikuwa wakichati hapo. Julieth alikuwa akichati na Juliana na kumshawishi atumie uwezo wake wa kike kuwa na Lucas maana ni mwanaume mwenye mafanikio na hueda akawa mpenzi mzuri. Juliana hili swala kwake lilikuwa gumu kwa sababu tayari alikuwa na mpenzi mpya mara baada ya mchumba wake wa muda mrefu kuzinguana. Huyu mpenzi mpya alikuwa hafahamiki na mtu yeyote na ndio maana pacha wake alikuwa akimpigia chapuo ili kuona kama anaweza kuwa naye. Juliana hakuwa mjanja kama Julieth hivyo aliweza kumshawishi ingawa Juliana alikuwa akisingizia kuwa siku hiyo hakuwa poa labda siku ingine.
Muda ulizidi kwenda na baadaye Kimaro aliamua kutumia nguvu kwa maana alilipa vitu vyote walivyokuwa wanadaiwa kisha waliiingia kwenye gari na safari ya kueleka pasipojulikana ilianza. Kimaro alipakia gari kwenye moja ya lodge ambayo ilikuwa inamilikiwa na baba yake. Julieth na yeye alishangaa maana hakujua kama ilikuwa ni ya kwao.Walishuka na kuwa tayari alishaongea na wahudumu wa hapo kuwa anakuja na wageni tayari alishawekewa.Alipewa funguo za room zilizofuatana. Wakati Julieth na Julaina waliabaki wameduwaaa tu wasijue nini kilikuwa kinaendelea. Julieth alikuwa akijiuliza maswali mengi kwa nini siku hiyo huyo mwanaume hakutaka kumpeleka kwake kama alivyozoea na kwa nini ameamua kuingia gharama hizo. Mwanzo alidhani kuwa walikuja hapo kuwaleta Julaina na Lucas lakini aligundua sivyo mara baaada ya kuona Kimaro akikabidhiwa funguo mbili. Kimaro yeye baada ya kupewa zile funguo alimkabidhi moja Lucas na kumwambia kazi kwako. Alimshika Julieth mkono na kuwaaga kwa kuwambia usiku mwema. Hao kwa mwendo wa madaha waliingia kwenye chumba chao.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Juliana na Lucas walibaki wamesimama na kuduwaha tu wasijue nini cha kufanya kwa wakati huo.Waliangaliana na kila mmoja alionesha kuwa alikuwa akimwogopa mwenzake. Waliogopana kwa sabbau mwaznoni hawakuwa na makubaliano ya aina yoyote kuwa watalala pamoja. Lucas baada ya kuona mrembo yupo njia panda na hana njia ingine ya kuondoka hapo alimkabidhi funguo. Juliana alisita kuzipokea na kubaki amesimama akimshangaa tu. Lucas sasa iliamua kutumia njia za kiume mara baada ya kugundua kuwa msichana huyo hawezi kuondoka. Alimnyanyua juu juu na kwenda naye moja kwa moja mpaka kwenye chumba ambacho walitakiwa kuingia. Hata Juliana alishangaaa mwanaume huyo amepata wapi nguvu za kumbeba juuju. Alivyofika alifungua mlango kisha kuingia naye ndani.Alimbwaga kitandani huku akihema kwa nguvu utadhani punda aliyeutua mzigo mzito. Kweli wanaume wanakuwa na nguvu linapokuja swala la mapenzi. Unaweza kukuta mwanaume ana kilo pungufu na mwanamke lakini akambeba bila matatizo yoyote.
Juliana alijilaza hapo kitandani huku akilaala na tumbo na kuacha kijungu mbinuo kikiwa juu. Kinguo kifupi alichokuwa amevaa kilipanda kwa juu na kufanya weupe wa majapa yake yaliyojazia kama godoro la Dodoma kuonekana. Lucas alipiga magoti kisha kwa utaratibu alimvua viatu na kuvishusha chini. Juliana alijigeuza na kupandisha miguuu juu ya kitanda kabisa.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment