Search This Blog

Monday, October 24, 2022

SEX MACHINE - 5

 







    Chombezo : Sex Machine

    Sehemu Ya Tano (5)



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Huku Nairobi kwa siku iliyofuata, asubuhi, Catherine aliamka mapema sana. Aliamka saa kumi alfajiri, aliingia kwenye uwanja wa mazoezi na kuanza kupasha mwili taratibu. Kwa muda huo huo, kwa upande mwingine wale vijana wanne walikuwa pembezoni mwa barabara wakikimbia kutafuta pumzi na kuyaweka mapafu yao vizuri. Ilipofika mida ya saa kumi na nusu, alionekana father D.A akiwa ndani ya chumba chake maalumu akiwa anachukuwa mazoezi yake ya Kishaolin, alikuwa akifanya mazoezi ya nguvu sana tena yakiwa ni ya hisia kali. mivumo ya kurusha mikono ilikuwa ikisikika hadi kwenye korido ndefu ya kutokea nje ambako ndiko Catherine alipokuwa akipasha mwili. Chriss muda huo ndiyo alikuwa anaamka ikiwa tayari imetimu saa kumi na moja kamili. Huu ndiyo ulikuwa muda wa kijana huyo kufanya mazoezi. Alinawa maji ya uso kidogo kisha akapita hapo koridoni akiwa anaelekea mahali pa kuchukulia mazoezi. Hapo akasikia mvumo wa nguvu sana uliokuwa unatokea kwenye chumba kimoja, akasimama ili kusikiliza mvumo huo unapotokea. Akasikia kuwa mvumo huo ulikuwa ukitokea kwenye chumba kimoja, ikabidi kusogea mahali hapo na kuchungulia ili kujua ni kitu gani kinachotoa mvumo wa namna hiyo. Alishangaa sana baada ya kumuona father akiwa anarusha makonde ya nguvu hewani tena huku akitumia mitindo ambayo hakuwahi kuiyona. Chriss alivutiwa sana baada ya kuona mtindo mmoja wa komfuu style ambayo ilikuwa ni style ya kuvutia sana. Hakutaka kupoteza muda mahali hapo, aliondoka mbio kwa mwendo wa kasi hadi kwenye uwanja wa mazoezi. Alitafuta sehemu nzuri na kianza mazoezi taratibu hadi pale mwili ulipokuwa umepata moto ndipo mazoezi yakawa yanazidi kupamba moto. Alichukua mazoezi kwa muda mrefu kidogo tena alikuwa akijituma na alionekana akiwa na hisia za hali ya juu mno kwa kile alichokuwa akikifanya mahali hapo. Wakati yeye akiwa anachukua mazoezi hayo, hakuwa akijua kabisa kuwa wenzake wote walikuwa wamemaliza mazoezi yao na walikuwa hapo wakimtazama yeye kwa jinsi alivyokuwa akijiumiza. Ilikuwa ni timu nzima ya Father D.A ambayo ilikuwa ikimtazama yeye mahali hapo.

    "kikosi kimekamilika sasa" alijisema father D.A alipokuwa hapo na vijana wake wakiwa wanatazama jinsi ndugu yao anavyo jifua.

    "sikujua kama unaweza kutumia mitindo ya kishaolin kijana wangu?" aliongea D.A kwa sauti ya juu na kumfanya Chriss abaki kuganda kama anayetaka kupigwa picha. Alijishangaa sana kutumia mtindo ambao hakuwahi kujifunza hata siku moja. Ulikuwa ni mtindo ambao aliuona asubuhi wakati huyo father alipokuwa akijifua kwenye chumba chake cha siri.

    "kwani ulishawahi kupitia mafunzo yoyote ya tempo kijana?" aliuliza D.A huku akiwa anasogea taratibu na vijana wake mikono yake akiwa ameikunjia kwa nyuma.

    "hapana fadher sikuwahi kupitia tempo lolote mimi nimejifunza mapigano kwenye vyuo vya kawaida tu" alijibu Chriss akiwa amesimama sawasawa na kugeuka nyuma ambapo alipatwa na mshangao kidogo baada ya kuiona timu nzima ikiwa ipo mahali hapo. Catherine alikuwa akikitazama kifua cha kijana huyo na jinsi kilivyokuwa kinachuruzika jasho na kukifanya kimeremete, kifua kilichopasuka katikati. Alijikuta akimeza mate ya tamaa bila hata kujijua.

    "mbona unaitumi hii mitindo ya ki Tempo kama vile uliwahi kujifunza hapo nyuma?" alizidi kumchimba kijana huyo D.A.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "nisamehe father, nilipokuwa natoka ndani kuja hapa, nilisikia sauti za mvumo kwenye chumba chako cha siri, ndipo nikachungulia ili kujua ni nini. Nikaona ukichukua mazoezi kwa mitindo hii, ndipo na mimi nikawa najaribu kama nitaweza, nisamehe sana kwa kufanya hiki kitu pasipo ridhaa yako" aliomba radhi Chriss. Fadha akamtazama huyo kijana kwa undani sana kisha akaachia tabasamu pana usoni mwake baada ya kujua kuwa kweli alichokisema kijana huyo mahali hapo, hakuwa akidanganya. Catherine na wale vijana wengine, wakabaki wakiwa na mshangao mkubwa baada ya kusikia eti, hiyo mitindo aliyokuwa akiionesha Chriss mahali hapo, haikuwa ni miongoni mwa mitindo ambayo alikuwa nayo bali amejifunzia hapo hapo tena ikiwa ni kwa muda mfupi tu na kwa kumuangalia fadher pekee. Lilikuwa ni jambo la ajabu sana kwao kwa mtu kujua mitindo ya mapigano pasipo kufundishwa.

    "unauwezo wa pekee sana, tulikuwa tumekaa pale kwa muda kidogo tukikufuatilia, nimependa unavyojifua na unaonekana ni mwepesi mno na unaweledi wa hali ya juu sana. Hauna muda mrefu sana na kesho unatakiwa uwe Tanzania hivyo muda huu ni vizuri tukautumia ili kuujua uwezo wako zaidi, hebu kuja hapa." aliongea father huku akiwa bado mikono ameitupia nyuma kama kawaida yake. Alisogea hadi sehemu ambayo ilikuwa imekaa vizuri kisha akamwambia kijana huyo, anahitaji kufanya naye mazoezi ili kumjua zaidi. Chriss akajawa na hofu ya kimtindo lakini hakuwa na jinsi zaidi ya kukubali kupambana na mzee huyo aliyeonekana mpole sana na mwerevu mno. Aliikunjua mikono kwa mtindo wa karate, father yeye alikuwa bado mikono yake ameitundika nyuma kama kawaida akimtazama kijana huyo. Alikuwa akizunguuka huku akiwa makini sana kwa mzee huyo Chriss, kwani alijua kabisa kuwa father si daraja lake hata kidogo. Alipeleka mashambulizi kama manne hivi lakini yote yalikuwa patupu, father aliyatoka yote na kumfanya kijana huyo arudi nyuma ili kujipanga upya. Chrissa alisogea tena, safari hii akiwa anakuja kwa kasi kubwa sana. Alikuwa akipeleka mashambulizi ya nguvu tena akiwa kwenye kasi ya aina yake. Kasi ambayo D.A ilikuwa ikimchanganya na kumpa.wakati mgumu sana wa kuweza kukwepa mapigo hayo. Alitumia uzoefu. Aliyumba D.A, kwenda kushoto, kulia na kuweza kuyatoka mapigo hayo kwa utaalamu wa hali ya juu. Chriss hakupunguza kasi na kila alipokuwa akishambulia, ndivyo alivyokuwa akizidi kumsogelea mzee huyo karibu zaidi hadi akawa anampa wakati mgumu wa kuweza kuyatoka mapigo hayo. Hakutaka kutoa nafasi ya father kuweza kupumua. Father aliikosa nafasi hata ya kurudisha mashambulizi. Alikwepa hadi sasa akaiona ile mikono ikiwa inakuja kama nane au tisa kama siyo kumi. Uwezo wake wote wa kukwepa ukawa umefika mwisho, pumzi ilikuwa imekata na kijana huyo alikuwa hapunguzi kasi ya kuleta mashambulizi. Father alijikuta akipokea pigo moja la nguvu sana lililomrudisha nyuma kwa hatua kadhaa. Hapo ndipo father alipoitoa mikono yake nyuma na kujifuta kifuani pale ambapo pigo hilo lilitua, aliunguruma kidogo kama Mbwa dume na kuizunguusha mikono yake kama feni kisha akakaa kwa mtindo wa taichi. Chriss alimtazama father kwa udadisi mkubwa kabla ya kutafuta mtindo mwingine wa kuweza kupambana na mtindo aliouweka mzee huyo. Father hakusubiri, aliamua kushambulia kwa kasi kubwa sana, wakakutana katikati. mpambano ukawa wa aina yake, si Chriss wala father aliyekubali kurudi nyuma, wote walikuwa katika nguvu ya juu mno. Walisimama sawa. Father akigusa, Chriss analipiza. Chriss akigusa, father anarudisha. Hadi wanakuja kusimama, hakuna aliyepigwa. Father alikuwa anahema si utani. Chriss akakaa mkao wa aina yake, mkao ambao aliuiga kutoka kwa fadha asubuhi, wakati yeye anaiga, father alitabasamu na kumuonesha kuwa yeye ni mwalimu na anamitindo mingi isiyopungua ishirini na kitu. Alianza kulegea father na kuyumbayumba huku akiwa ameweka mikono yake kama nyoka anayeshambulia lakini haikuwa style ile ya nyoka ambayo watu wengi wamezoea kuitumia au kuiona. Hii ilikuwa tofauti, mikono ilijikunja kuanzia kwenye kifuti halafu hapa juu kwenye kiwiko ikawa imelala kidogo. Hakuacha kuyumba yumba kama kimbaumbau anayesukumwa na upepo au mlevi kisha akatamka neno moja tu.

    "D.A." Chriss akadhani labda ule ulikuwa ni mchezo wa kuigiza ambao father alikuwa akiuonesha mahali hapo, kumbe alikuwa akimtaja nyoka hatari sana mahali hapo. Chriss yeye hakulijua hilo. Akaenda mbele kwa kasi ya kushambulia. Alikosea. Alikutana na pigo moja kubwa na baya sana kisha mzee huyo kubaki akiwa anatetemeka mikono, hiyo ilionesha kuwa pigo hilo lilitumia hisia kali. Alikuwa amefumba macho kama siyo yeye mahali hapo. Chriss kwa wakati huo alikuwa akigalagala chini kwa maumivu makali sana. Catherine na wenzake wote pale wakakumbwa na taharuki ya nguvu sana, hawakutegemea kumuona mzee huyo akiwa katika hisia za namna hiyo. Chriss alikuwa akihangaika bila kutoa sauti yoyote, ila alionesha hali ya kuitafuta sauti lakini haikutoka hata mara moja.

    "father?" Catherine alijikuta akiita kwa sauti ya kuuliza. Father hakuinyanyua hata sura yake kumtazama muitaji na badala yake, alimsogelea huyo kijana aliyekuwa akitapatapa hapo chini na kufumba macho tena. Akanyanyua mkono wake wa kushoto juu na kuushusha kifuani kwa Chriss kwa nguvu sana. Chriss alikurupuka ma kukohoa sana, damu zikawa zinamtoka mdomoni kila alipokuwa akitema mate. Alikohoa kwa muda hadi pale alipokuja kutulia na kuhema juu juu.

    "nimefanikiwa sasa, umekuwa kijana hodari na makini zaidi. Nimekupa mafunzo ya hisia kwani huko utakapokwenda ninaimani kuwa huwenda yule mshenzi atakuwa ameandaa vijana wanaotumia Star Poison (SP)." maneno hayo aliyoyaongea father yalisikiwa na kila mmoja lakini hakuna aliyeelewa hata mmoja. Father D.A alinyanyuka na kumuambia Catherine amchukue huyo mtu hapo na ampeleke kwenye chumba cha mapumziko kisha aanze kumwambia yeye ni nani, kwanza wote tuelekeeni kwenye meza ya chakula."

    "meza ya chakula?" walijikuta wakisema kwa pamoja na kuangaliana. ndipo walipogundua kuwa miongoni mwao, mmoja hakuwepo, Amiri hakuwepo na walipomuangalia fadha alikuwa akiondoka eneo hilo na kuelekea ndani huku mikono yake ikiwa nyuma kama kawaida. Walipofika huko ndani kila mmoja aliingia kwenye chumba chake huku Catherine akiwa anamdemeza kijana Chriss. Alimpeleka hadi kwenye chumba chake na kumuingiza bafuni ambako alimuacha huko. Baada ya muda wote walikutana kwenye meza ya chakula cha asubuhi ambacho kiliandaliwa na kijana Amiri.

    "vipi Chriss unajisikiaje sasa?" aliuliza father mezani hapo.

    "niko vizuri father, najisikia vizuri sana sasa." alijibu kijana huyo.

    "ulikuwa ni lazima uingie kwenye uchovu ule, kupokea mapigo ya kihisia tena kwa muda mfupi ni ngumu sana, tena wewe uko vizuri sana, kwa mtu mwingine angelala siku nzima......



    alisema father. Wakanyamaza hapo na kuipa nafasi midomo yao kuendelea kupata chakula hicho cha asubuhi.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Chriss muda wote alikuwa na mawazo sana ya kujua kuwa kuna nini ambalo lipo mbele yake na anatakiwa kulijua? Aliwaza sana lakini hakukuwa na jibu ambalo liliulainisha moyo wake. walipo maliza kupata hicho kifungua kinywa, Catherine aliondoka na Chriss hadi kwenye chumba alichotakiwa kumpeleka. Kilikuwa ni chumba kitupu kisicho hata na kitu kimoja. Catherine alikuja na picha moja mkononi lakini hakuwa amemuonesha hadi walipofika ndani hapo. Kimya kikatanda kwa muda. Kimya ambacho hakikudumu sana baada ya kijana huyo kukivunja.

    "madame Cathe........!"

    "Chriss, wewe ni mtu mkubwa sana kwetu sote humu ndani, sisi ndiyo tunapaswa kukupa heshima wewe na siyo wewe kunipa heshima mimi" aliongea Catherine akiwa amemkatisha kauli Chriss.

    "mimi ni nani kwani Cat?"

    "wewe ni ROI na siyo Chriss tena, jina la Chriss tunaliuwa leo kama ambavyo tumeliuwa la Sex Machine" aliongea Catherine na kumfanya kijana huyo kukumbwa na mshangao mkubwa na hali ya sinto fahamu ikimtawala. Mbona anakuwa ni mtu wa danadana sana? Mbona hana ukamilifu sasa? Kwanini kila siku yeye ndiyo awe mtu wa kupokea mambo mapya yanayomhusu yeye? Yeye ni kiumbe wa aina gani kwani? Hayo yalikuwa ni maswali yaliyokuwa yakipita kichwani mwake pengine, maana alimtazama Cat na kusema.

    "nashindwa kujielewa vizuri mimi, na nashindwa kujielewa vizuri kwa sababu ninyi mnaonielewa hamtaki kunieleza mimi ni nani na kwanini kila siku sikamiliki" alikuwa hatanii kijana huyo ndani ya hayo maneno yake hata kidogo.

    "na ndiyo maana umeletwa hapa Roi, na ndiyo maana hautaruhusiwa uondoke hapa kwenda Tanzania hadi ujifahamu"

    "haya nifahamishe sasa?" aliongea Chriss ambaye kwa muda huu alikuwa akifahamika kwa jina la Roi. Nadhani wale waliowahi kuifuatilia riwaya ya Dereva Tax, watakuwa wanamkumbuka huyu kijana. Sasa huku ndiko historia ya kijana huyo ilipotokea. Cat alibaki kimya muda huo, aikuwa akikumbuka mbali sana dada huyo. Aliyakumbuka maisha yaliyowahi kutokea miaka ishirini iliyopita, alikumbuka hata jinsi mtu aliyekuwa akimpenda na kumjali, alipouwawa kwa kupigwa risasi kisha na mkewe kuuwawa pia kwa kifo hicho hicho..........!

    Kumbukumbu zake zilikuja kukatishwa na swali kutoka kwa kijana huyo.

    "vipi, hauko tayari mimi nijijue ni nani? Mbona umebaki kimya na hutaki kusema chochote?" ndivyo alivyouliza Chriss/Roi.

    "napambana na uchungu mzito sana Roi, ni kumbukumbu ambayo nikiikumbuka, inanifanya nijione bado ninadeni kubwa sana kwa baba yako." aliongea Cat. Kisha akajikohoza na kusema tena.

    "inabidi ujue kila kitu leo Roi."



    "ni kama miaka ishirini iliyopita, nakumbuka ilikuwa ni mwaka 1997. kipindi cha uwepo wa Raisi wa awamu ya tatu Mh. John Pomela. Sikuwa mdogo wa hivyo kipindi hicho na hata wewe ulikuwa nafikiri umetimiza takribani miezi kadhaa lakini umbo lako lilikuwa si dogo sana na kukufanya kuonekana mkubwa kwa macho ya kila aliyekuwa akikutazama. Baba yako alikuwa ni mfanya biashara mkubwa sana na alikuwa ana utajiri kiasi, alifahamika kila kona kutokana na tabia ya kuwa mtu wa kusaidia watu. Alikuwa akipendwa na kila mtu baba yako, alikuwa akifahamika sana sehemu kubwa ya mji wa Morogoro. Ni nani utamuuliza jina la Isihaq asilifahamu. Baba yako alikuwa na rafiki yake mmoja, huyu aliseama kuwa ni rafiki yake wa siku nyingi sana na ni kweli muda wote walikuwa pamoja na walionekana wakiwa wanajadili mambo mengi sana wakiwa pamoja. Siku moja, nafikiri ilikuwa ni siku ya juma tano, Baba alichelewa sana kurudi nyumbani siku hiyo hadi mama, ambaye ni mama yako, akapatwa na wasiwasi. Usishangae mimi kumuita baba yako baba, Roi na pia usishangae kumuita mama yako mama. Mimi hapa hadi nakuwa na kujitambua nilijikuta mikononi mwao na wao ndiyo walionipa jina hili la Catherine. Nilipopata makamo kidogo ndipo wakaniambia kuwa mama yangu alikufa kwenye mikono ya mama yako akiwa hospitali wakati mama yangu amekwenda huko kujifungua. Sijui walikutana vipi lakini niliambiwa hivyo. Wakati wa kujifingua ulipofika, mama alikumbwa na ugonjwa mbaya sana wa kupoteza fahamu kiasi cha kushindwa kufanya jitihada za kuweza kusukuma mtoto. Fahamu zake zilikuwa zinapotea na kurudi, hali hii ikaleta hofu kubwa kwa madaktari. Hawakujua huo ulikuwa ni ugonjwa gani na dokta mkuu alipofika hapo hospitali, alielezwa hali ya taharuki hiyo ambayo hata yeye ilimchanganya. Daktari akasema kuwa hawata subiri kuona mama huyo atakaa tayari muda gani aweze kujifungua wakati mtoto alikuwa tayari kutoka kwa hiyo kama wakizidi kupoteza muda hapo, kuna hatari ya kumpoteza mama ama kuwapoteza wote wawili. Akatoa amri kuwa liwalo na liwe lakini lazima mama huyo ajifungue. Kwani aliamini ugonjwa huo unaweza kuwa ni kifafa cha mimba ambacho kimemkuta mama huyo ghafla. Na waliamini hivyo, kutonakana na ugonjwa huo kufanana kila kitu na kifafa mimba. Amri ya dokta ikawa ni mama kujifungua kwa njia ya upasuaji, mama akaingizwa kwenye chumba cha upasuaji na kutaka kuchomwa sindano ya nusu kaputi, kabla ya kuchomwa hiyo sindano, akarudiwa na fahamu. Akauliza hapo alipo yuko wapi na aliuliza akiwa katika uchungu mkali sana. Madaktari wakamwambia kuwa yupo kwenye chumba cha upasuaji na anatakiwa kufanyiwa upasuaji ili kuweza kujifungua. Mama akaomba kuitiwa yule dada aliyemleta hapo hospitali na kujitolea kumsaidi. Mama huyo alikuwa ni mama yako. Mama yako akaitwa kipindi hicho yeye pia alikuwa amekwenda hapo hospitali kwa tiba maalumu. Mama yako akaingia huko kwenye chumba cha upasuaji na kusogea hadi kwenye kitanda alichokuwa amelazwa mama yangu. Ndipo mama yangu alipompa mama yako wosia. Kwa nilivyoelezwa niliambiwa kuwa mama yangu alisema hivi.



    "dada, najua kuwa umenikuta njiani nikiwa katika hali mbaya sana ya uchungu. Walinipita wengi na magari yao, wanawake kwa wanaume lakini wewe ukaonesha moyo wa kunisaidia. Naomba usiwe na moyo wa kunisaidia mimi tu bali msaidie na huyu mwanangu ambaye hata kuwa na ndugu, ndugu yake ni mimi ambaye nitakufa leo kwa huu upasuaji na kumuacha mikononi mwako. Naomba uwe ndugu yake na mwangu awe ndugu yako, najua atakuwa na ndugu mwanangu mimi baada ya kufa na kunifanya mimi ninayemtelekeza leo, nikaishi kwa amani huko niendako." alikomea hapo mama yule mwenye uchungu mkubwa wa kutaka kujifungua na mama yako akataka kusema jambo lakini alikuwa amesha chelewa kwani tayari mama yule ugonjwa wa kupoteza fahamu ukawa umemrudia tena, akapoteza fahamu na madaktari wakamchoma na dawa ya usingizi juu. Walifanikisha zoezi lao la kunitoa duniani nikiwa salama lakini mama hakwenda kinyume na kauli yake. Kweli aliniacha mikononi mwa mama yako. Mama yako akarudi nyumbani na mimi, akamueleza baba yako kilichotukia, bila malalamiko wala

    nung'uniko, akakubali niwe miongoni mwa familia yake. Lakini hakwenda kinyume na mama alivyotaka, mama alitaka niitwe Catherine ili historia yake ibaki duniani." aliweka kituo kwanza hapo Cat. Roi alishusha pumzi nzito sana na kabla hajaongea chochote, Cat akamuwahi.

    "samahani sana kwa kukuchanganyia historia mbili kwa wakati mmoja Roi, lakini nilikuwa nataka usiwe na swali jingine kuhusu mimi nataka utege sikio ili uweze kusikia kwa umakini." akazidi kuendelea.



    "wasiwasi ulikuwa mkubwa kweli lakini ilipofika saa tano za usiku ndipo aliporudi nyumbani. Mama akamuuliza ni kwa nini amechelewa hivyo. Akasema kuwa alipitia kwa rafiki yake aliyemtaja kwa jina moja la Joesan. Akasema kuwa walikuwa na maongezi mengi sana na kubwa likiwa ni kutaka kumpa kiasi kikubwa cha pesa bwana huyo ili naye aingie kwenye uwanja wa kibiashara. Mama akamuuliza amkopeshe au ampe? Baba akasema kuwa ni kweli bwana huyo alitaka kukopeshwa kiasi kidogo cha pesa ili kuimarisha biashara yake lakini akaonelea si vema kumkopesha wakati aliishi naye kama ndugu pia wakiwa ni marafiki wa siku nyingi sana. Siku takribani nne zikapita lakini huyo bwana aliyejiita Joesan hakuacha kuja nyumbani kila wakati, muda mwingine alikuwa akija hata kama baba hayupo na muda mwingine alikuja watu wote wakiwa hawapo, alipokuwa akija hakuwa na jambo jingine ambalo alikuwa akilizungimza zaidi ya kuizuunguka nyumba na kutembea tembea bila jambo la muhimu kisha huondoka. Siku ya tano, ambayo ndiyo ilikuwa siku ya ahadi ya baba na huyo Joesan, ya kutaka kukutana na kuelekezana jinsi ya kukabidhiana hiyo pesa pia na kuelekezwa jinsi ya kuitumia pesa hiyo. Pia siku hiyo ilikuwa ni siku ambayo baba alisema kuna safari ya kwenda Arusha kwenda kuangalia biashara zake na alipanga kwenda na familia nzima. Baba akasema kuwa limekuwa ni jambo zuri sana kwani Safari yake ya kwenda Arusha, imeingiliana na safari ya kukutana na rafiki yake ili kwenda kupanga mbinu za kibiashara na jinsi ya makabidhiano na Joesan, alipanga kukutana na baba Mombo.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku iliyofuata, tuliingia kwenye gari na kuanza safari ya kuelekea Mombo kisha Arusha. Tulifika Mombo mapema sana baba akatafuta nyumba nzuri ya kulala wageni. Tukashuka hapo na kuingia ndani ya Lodge hiyo. Ilipofika jioni ndipo baba akasema kuwa muda wa kwenda kukutana na rafiki yake ulikuwa ukiwadia. Akasema atakwenda peke yake na hato chelewa kurudi kwani hayatakuwa maongezi marefu sana. Tukakubali lakini cha ajabu, ilipofika saa mbili usiku, ambao ndiyo ulikuwa muda wa miadi, baba akabadili maamuzi. Akasema ni lazima twende wote ili pia tuujue mji wa Mombo vizuri, mama hakuwa mtu wa kupinga................



    ila mimi nilipata mashaka na moyo wangu ulikuwa hautaki kabisa kuamini hilo jambo. Sikuwa na jinsi ya kuzuia hata kidogo. Tukatoka mimi nikiwa nimekubeba wewe, tukaingia kwenye gari na safari ya kwenda huko anapopajua yeye ikaanza. Haikuwa safari ndefu lakini kila tulipokuwa tukisonga mbele, ndivyo hofu yangu ilivyojuwa ikizidi maradufu. Nakumbuka baba alisema hivi.

    "huku mbona hakuna nyumba wala mitaa? huyu Joesan siku hizi anaelekea kuchanganyikiwa au? Huku si porini kabisa Mungu wangu!" alisema hivyo baba nakumbuka lakini alichukulia ni mzaha tu wa rafiki yake na alikuwa akisema kuwa anamjua sana rafiki yake huyo kwa mzaha. Tukafika sehemu moja iliyokuwa nyeupe kiasi na vichaka vya kuhesabu, hapa tukaona pikipiki kubwa likiwa limepaki. Walikuwa watu wawili, baba akasema tumsubiri garini, tukafanya hivyo na yeye akashuka. hatukujua kilichoendelea huko nje hadi pale tulipomuona huyo Joesan akiinua bastola na kumuelekezea baba kwenye paji la uso. Mama alivyoona vile akashtuka na kukurupuka. Akasema.

    "Catherine na mimi nikifa usimuache mdogo wako hakikisha unakuwa naye bega kwa bega, inabidi usirudi nyuma nenda Arusha mwanangu" alipomaliza kusema hivyo Mama akashuka garini na kukimbia kule ambako baba alikuwa amenyooshewa bastola huku akipiga kelele za kuomba msaada. Lilikuwa kosa sana. Kitendo cha mama kupiga kelele ndiyo ilikuwa tiketi yake ya kwenda kuzimu. Taa ya gari ilikuwa inamulika kule ambako walikuwa wamekaa hivyo nilishudia mama akipokea risasi kadhaa zilizo tua kifuani mwake na kumdondosha chini. Baba hakukubali kuona mkewe anakufa mbele ya macho yake, akapambana lakini masikini ya Mungu baba hakuwa na uwezo hata wa kujua ngumi inakunjwaje, hakuwa mpambanaji baba. Joesan alimpiga kama anapiga kibaka, alipiga sana Joesan hadi nikajiukiza, hivi kweli yule alikuwa ni rafiki yake. Maana nilishuhudia ngumi zikitua mdomoni na kusababisha damu nyingi kuruka na kutoka na meno. Kila akipigwa, damu zilikuwa zikiruka mithili ya mtu anayesukutua maji na kuyatema. Kipigo kilikuwa kikali mno. Baba akaona kuwa hapo hawezi kufua dafu kwa huyo bwana hata afanye nini na tayari alishajiona hata yeye ni wa kufa tu hivyo aliona ni bora akafe akiwa karibu na mkewe pale alipoangukia, baada ya kupigwa risasi. Alikuwa akikimbia huku akilitaja jina langu na kuniambia, Catherine kimbia, kimbia mwanangu, kimbia na mdogo wako, Joesan ameamua kuingiwa na tamaa ya kuutaka kabisa utajiri wangu. Nakufa Cath...............!!!" hakumalizia, ukelele ukamtoka wa uchungu, wakati huo mimi nikiwa tayari nipo chini ya gari, sikuwa na jinsi ya kufanya Roi, ningefanyaje wakati nilikuwa binti mdogo sana. Nami nilikuwa na hofu ya kufa. Baba kila alipokuwa akipigwa hizo risasi hakukubali kuanguka, alizidi kukimbia akiwa na lengo la kufa akiwa na mama. Joesan akazidi kumimina mvua ya risasi, alipiga risasi nyingi zilizozama mgongoni na kutoboa tumbo, damu zilikuwa zikiruka kama machinjioni. Joesan alipoona baba haanguki, aliamua kumaliza mchezo kwa kupiga risasi ya kichwa. Hiyo ndiyo iliyompeleka baba chini lakini akiwa ametimiza kile alichokikusudia kwani alianguka pembeni kidogo ya mama akiwa tayari ni marehemu, hakuweza hata kulishika paji la uso la mkewe lakini alikufa akiwa karibu naye kabisa. Nilipoona hali imekuwa ngumu, sikuweza kukaa mahali hapo tena, nilikimbia bila kuonekana na kuvipita vichaka kadhaa usiku huo na kutulia mahali ili kuweza kujua kama kunakitu watafanya kwako kwani sikuweza kukimbia na wewe usiku ule. Mombo kulikuwa na baridi sana, nikakuhurumia hivyo nikamuomba Mungu akujaalie tu wasikufanye kitu. Kweli walipokukuta mahali hapo hawakukufanya chochote bali nilimsikia Joesan akiahidi kuwa kwa kitendo cha kumuuwa rafiki yake alichokifanya, hivyo eti, atalipa fadhila kwa kukulea wewe. Baada ya hapo waliichukua ile miili ya wazazi wako kisha wakaaingiza garini na kulitia moto gari hilo. Baba na mama walikufa kwa risad

    si pia miili yao kuteketezwa kwa moto. Hakuna kaburi la baba na mama Roi, hakuna. Joesan akaita kwa jina moja tu baada ya kuona amekamilisha yale aliyoyakusudia.

    "Babuu, twende zetu bwana hapa pasije pakajaa askari ikawa tabu bure." alisema hivyo akiwa amekuweka kifuani kwake. Huyo mwenzake akapanda pikipiki na kuliwasha, Joesan akadandia na kutokomea kizani. Nililia sana, nililia sana Roi. Haswa nikikumbuka jinsi ambavyo nngeweza kuishi mwenyewe. Nililia pasi na kifani. Ilinibidi kuwa na moyo wa kijasiri wa kurudi pale kwenye ile Lodge. Tulikuwa tumelipia kulala kwa siku moja kisha asubuhi yake ndiyo tuelekee Arusha. Akili za kitoto zikanifanya niwe nalia kila wakati na kila sekunde. Wakati naingia ndani, kuna babu mmoja alikuwa amekaa kwenye kiti kirefu akiwa na birauli yake ya kinywaji, akaona jinsi nilivyokuwa napita huku nalia. Kama akashtuka yule babu kisha akaniita. Nikaenda, nikamsalimia akaitika na kuniuliza.

    "vipi mbona unalia?" Sikuweza kumjibu kwa kweli ni kama alikizidisha kilio changu lakini sikuwa nikitoa kwa sauti, nilikuwa nikilia kilio cha kwikwi. Yule babu ambaye hakuwa mzee wa hivyo sana, alikuwa ni mtu wa makamo tu. Akanitupia swali jingine baada ya kuona la kwanza nimeshindwa kulijibu. Aliniuliza, mbona uko mwenyewe na nilikuona ukitoka na wazazi wako pamoja na mdogo wako ukiwa umembeba, wako wapi wote? hapo nili nyamaza na kuanza kuangaza kila kona kabla ya hata sijafikiria kulitoa hilo jibu. Yule babu akajua hapo si salama na akajua kuna kitu cha ziada, hata nilipotaka kuanza kusema, akaniziba mdomo na kuniambia.

    "oooh! Hapa si salama kwa usalama wako, twende, utakwenda kuniambia vizuri ndani". Akanishika mkono na kunipeleka hadi ndani ya chumba chake kisha nikakaa kitandani na kumueleza kila kitu tangu mwanzo wa safari hadi hapo aliponiona. Alichofanya ni kuniuliza swali moja tu.

    "umeshuhudia kila kitu?" nikamwambia ndiyo. Kisha akaniuliza tena.

    "umekula?" nikamjibu kwa kutikisa kichwa kwa ishara ya kukataa l

    alipotaka kuniagizia chakula pia nilikataa. Sikuwa na hamu ya kula kabisa. Hakusema kitu kingine huyo mzee, alinichukua na kunilaza kwenye chumba kingine hadi asubuhi alipokuja na kunichukua. Akaniambia, Catherine utaishi na mimi na siku ukija kurudi Morogoro, unakuja kwa kazi moja tu ya kumtafuta ndugu yako na kulipiza kisasi. Alisema hayo maneno tukiwa ndani ya gari tukiwa tunaelekea Arusha. Huo ndiyo ukawa mwanzo wa maisha yangu mapya.



    Niliishi kwa furaha sana Roi, lakini bado nilikuwa na uchungu mkubwa juu ya walezi wangu. Pamoja na umri wangu kuwa mdogo lakini lile tukio la baba yako na mama yako kupigwa risasi kisha kutiwa moto baada ya kufungiwa ndani ya gari, hiyo ikawa ndiyo ndoto yangu ya kila siku na muda mwingine baba yako alikuwa akija na kuniuliza kama nilikukumbuka siku ile. Nilikuwa sina jibu la kumpa zaidi ya kulia, Nilijiona kama nimekupelrka kwenye kifo, basi akawa anaondoka akiwa amenyong'onyea sana. Nikamuahidi ipo siku nitakuwa nawe pamoja. Siku moja huyo mzee ambaye nilikuwa nikiishi naye huko Arusha, alinikuta nikiwa nalia sana. Hakunisemesha, aliniacha hadi kilio changu kilipokoma chenyewe ndipo akanifuata na kuniambia inabidi tutoke kwani amenitafutia shule nzuri nchini Marekani. Nilishangaa sana lakini sikuwa na uwezo wa kumpinga pia nilikuwa na ndoto pia za kusoma. Tukaondoka hadi nchini Marekani. Huko akaamua kunipeleka kwenye kituo kimoja. Akanikabidhisha kwa rafiki yake mmoja kisha yeye akaondoka. Alikuwa kama kanitelekeza hivi. Haikuwa shule niliyoizoea mimi au zile shule ambazo niliona watoto wenzangu wakiwa wanasoma, hiyo ilikuwa ni shule ya mafunzo maalumu. Niliteseka sana, yalikuwa ni mafunzo ya kufa kabisa. Muda mwingi tuliutumia kufanya mazoezi magumu na makali kupita maelezo na muda mchache tulijifuza vitu vya ki teknolojia. Baada ya miezi mitatu ya mafunzo ndipo nilipojua ni kwa nini yule babu alinipeleka pale. Kipindi chote hicho, hakuwahi kuniambia jina lake hata mara moja, mimi nilimfahamu kwa jina la babu tu. Mwezi wa nne ulipofika ndipo akapiga simu kwa yule rafiki yake ambaye ndiye alikuwa mwalimu wangu mkubwa aliyekuwa akinifundisha kwa nguvu sana na muda mwingine nilikuwa nikipata mafunzo ya ziada nikiwa nyumbanu kwa sababu nilikuwa nikiishi naye. Babu alifurahi sana kuisikia sauti yangu ya furaha. Akasema niliondoka bila kukuaga ili tu usinikumbuke, nilitaka ujue kama vile nimekutelekeza ili uwe na uchungu wa kujifunza. Sasa akaniambia kuwa natakiwa kujifua kwa juhudi na bidii kubwa kwani nikitoka hapo ndiyo natakiwa kumtafuta ndugu yangu na kulipa kile nilichokiahidi. Hueezi amini, aliponiambia maneno hayo, nilijikuta nikiongeza bidii kweli na kuwa mtu wa pekee sana hadi walimu wangu wakawa wananishangaa. Miaka mitatu ya mafunzo nilikuwa nimefuzu kwa daraja la kati. Akaniambia daraja lililobakia ambalo ni la juu, atanifundisha mwenyewe. Nikarudi Arusha na kuendelea na n'gwe ya mwisho. Nikafuzu daraja la tatu nikiwa na umri wa kuwa binti mkubwa. Siku moja babu alinifuta na kuniambia kuwa hawezi tena kuishi Arusha kwani Mtoto wake wa kiume aliyekuwa akiishi Morogoro, ameuwawa na kisha mjukuu wake kutekwa. Ilikuwa ni kama utani lakini ilippfika mida ya saa tano usiku, tuliondoka Arusha kwa siri sana na kurudi Marekani. Huko ndiko alipotengeneza vikosi imara vya kazi. Alinitambulisha kwa wale vijana. Zomba na wenzake pamoja na kunionesha lile handaki ambalo sisi tulipaita shimoni. tukaianza mikakati ya kuhakikisha tunakurudisha nyumbani wewe pamoja na Mery kisha tuimalize kazi hii tukiwa pamoja"



    ndivyo alivyotoa historia hiyo Catherine. Roi akajikuta anadondoka chini na kukaa bila hata kutarajia, alichoka vibaya sana.

    "Joesan kumbe umeniulia wazazi wangu?" aliwaza Roi. Wakati akiwa anazidi kuwaza hapo, Cat alimwambia anyanyuke na amfuate. Alijinyanyua mahali hapo akiwa na uchungu mkubwa sana. Wakaingia kwenye chumba kimoja ambacho kilikuwa kina scrine moja kubwa ukutani. Cat akachukua rimoti na kusimama karibu na Roi kisha akasema.

    "Joesan alikulea kweli akakubadilisha jina kabisa pamoja na ubini wako, ukawa mtu usiyeelewa nini historia yako. Alikupa historia ya uwongo na akafanikiwa. Alikuita Christiano Robin Isaya. Na mara nyingi alikuwa akilitaja jina lako, alikuwa akipenda kusema kuwa jina la pili linaweza kuwa la kwanza, nadhani unakumbuka kama ulishawahi kumsikia?"

    "ndiyo, nakumbuka Cat" alijibu Roi, Cat akaendelea.

    "basi alikuwa na maana kubwa sana, alikuwa hataki kukuweka mbali na maisha yako ya asili............................





     Alikuita hivyo ili kuendana kidogo na jina lako la asili kwani jina lako ambalo wazazi walikupa ni Rajab Ishaq Omair. Sasa alipokuwa akisema kuwa jina la pili linaweza kuwa la kwanza, alikuwa anamaana ya kwamba herufi R ndiyo iliyotakiwa kutangulia na kuleta jina la Rajab na siyo Robin, ambalo kwake lilisimama kama ubini wako. Herufi ya jina la mwisho alilokupa ambalo ni Isaya ilikuwa ndiyo iwe katikati na kusimama kama Isihaq ambalo ndilo jina la baba yako mzazi. Baba yako alikuita Roi kwa sababu azijuazo yeye, lakini kubwa alisema kuwa ameunganisha majina matatu kuwa pamoja na kuleta jina hilo Roi. La kwanza likiwa ni jina lako, pili, akiwa amechukua jina la babu yako na kuliweka katikati na la baba kuliweka mwisho. Father naye akatafuta maana yake ikiwa ni kunisaidia mimi pia akiwa na mpango wa kulipa kisasi cha kijana wake ambaye wauwaji ni hao hao ambao walikuwa na maana moja tu ya kutekeleza mauwaji hayo. Yeye alikuita hivyohivyo Roi lakini akiwa na maana ya Rivange Of Isihaq (ROI). Upo hapa kwa ajili ya kulipiza kifo cha baba yako Roi" alisimama Cat na kumgeukia kijana huyo na kumuangalia usoni. Roi hakummaliza binti huyo hata kidogo. Kumbe alikuwa anamzigo mzito aliubeba kifuani mwake na leo ndiyo alikuwa akimtemea.

    "sasa umewezaje kugundua kuwa Joesan alinigeuza kuwa mashine ya ngono kwa mitambo maalumu?" aliuliza Roi.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "ilikuwa ni ngumu kujua japo nilikuwa katika harakati za kukutafuta ili urudi nyumbani, lakini nilikuwa sijui kama Joesan amekufanya vile. Ni siku moja nilipokuwa kwenye Casino moja huko Brazil. (hapo Catherine alivuta kumbukumbu nyuma na kumpa picha halisi kijana huyo na jinsi alivyoanza kufuatilia nyendo zake.). Walivyo taja jina J, from Tanzania, nikalitilia mashaka. Sasa Cheap niliyoitega kwenye simu ya BC, yule mmarekani mwenye kikosi kilichotuvamia kule baharini, ndiyo ikanipa mwanga na hapo ndipo nilipojua kuwa tayari amesha kuathiri. Nikampa taarifa Father, father akaniambia ipo mashine ya kazi ambayo imeundwa na mtu mmoja hatari sana. Charls. Ambayo itakurudisha kwenye uwezo wako halisi. Nikaanza kukufuatilia kwa safari yako ya kwanza kabisa ya kwenda kutekeleza ngono nchini Uingereza ndani ya jiji la London. Nikakutafuta hadi nikagundua hoteli uliyofikia na kupanga mipango ya kukamilisha kazi ile. Ulipokuwa unatafuta mbinu za kuingia mule ndni yalile jingo, nami pia nilikuwa nazitafuta vivo hivyo. Tulikutana wote ndani ya jumba la yule mama. Na wote tuliingia kwa tiketi za watu wengine. Hapo nikafanikiwa kukuweka cheap memory iliyokuwa na uwezo wa kunasa kila kilichokuwa kikirekodiwa na lile vazi ulilopewa. Kazi hiyo niliifanya wakati nikiwa nyuma yako. Hebu angalia hapo kwenye hicho kioo mambo uliyokuwa ukiyafanya ndani ya lile jingo." aliposema hivyo Cat, akawasha kile kioo pale mbele. Kila kitu alichokuwa akikifanya kijana huyo kilionekana. Roho ilimuuma sana, hakuamini kama yale ndiyo yalikuwa maisha yake ndani ya kipindi cha mwaka mmoja na nusu. Catherine akamwambia kijana huyo kuwa kila picha iliyokuwa inarushwa hapo baada kunyoywa na kile kifaa alichomuwekea, walizitengeneza kwa mfumo wa video kwa kutengeneza Santuri. Walifanya hivyo ili kubakiwa na ushahidi. Historia ikaendelea, akaambiwa kuwa yeye ndiye aliyekuwa ametekeleza mauwaji ya kifo cha waziri wa zamani wa awamu ya tatu, waziri Musolin pamoja na mlinzi wake mmoja pia akauwa kiongozi mwingine wa Kenya Don Kemoi. Alifanya matukio mengi sana na yote akiwa ameyashuhudia hapo. Nilikuwa nikikanyaga kila ulipopita. Ulipita sehemu nyingi sana hadi nikajua unaweza kufa lakini mungu alisimama upande wetu.

    "walipofikia kwenye hatua ya kutaka uwaingilie kimwili mashoga, hapo ndipo walipoanza kuujua huu moto. Kwanza nilivamia kwenye kampuni yao na kutega kamera zangu za siri ambazo nyingi bado zipo ila moja tu ndiyo iligindulika na aliyegundua hiyo kamera ni mzee Rafael, huyu naye nadhani unamjua. Nilipotoka ndani ya hiyo kampuni yao ya uwongo wanayosema inajihusisha na masuala ya utalii kumbe ni maabara mbaya inayo haribu maisha ya watu. Na ikiwa ni baada ya kuiba siri zao baadhi. Niliondoka na kwenda nyumbani kwa Joesan na kumuuwa mkewe kisha nikaondoka na Mery. Hapo ndipo walipochanganyikiwa na huku Joesan akipata maumivu makali sana kwa kumuondolea mkewe duniani. Sikufichi Roi, niliuwa mashoga wote ambao walipangwa kushiriki ngono na wewe, niliuwa na kukuacha wewe katika taharuki kubwa pamoja na mabosi waliokuwa wakikutumia. Sikuishia hapo" Alipofika hapo Cat akatulia na kumeza mate kisha akampa picha amabazo alikuwa akipigwa na vijana wake wa kazi pindi alipokuwa akitekeleza hayo mauwaji ya mashoga. Mwisho kabisa akamalizia jinsi ambavyo alicheza mchezo wa kumtia mikononi yeye mwenyewe, huko nchini Marekani ndani ya jiji la Miami. Roi alikuwa hoi. Aliumia sana, akaapa kumpa Joesan kifo kile alichowaulia wazazi wake ikiwa ni kama kuwafurahisha wazazi wake huko waliko. Alikuwa amekaa kimya chini sakafuni. Kimya kikatanda mule ndani ni mihemo tu ya wastani ndiyo iliyokuwa ikisikika. Cat akampa Roi picha moja kubwa kiasi yenye ukubwa wa A3. Roi akaitazama ile picha na kujikuta akishtuka na kumtazama mrembo huyo kabla ya kumuuliza.

    "hii picha ilikuwa chumbani kwangu nilipokuwa nikiishi na huyo mshenzi Joesan, wewe umeipataje hii au uliichukua siku uliyokwenda kumchukua Mery?"

    "hapana hizo picha zilikuwa mbili na hata sijui kwa nini zilikuwa mbili, lakini nakumbuka hivyo, baba yako ndiye aliyenipa picha hizo nikae nazo. Moja ikatengenezewa fremu na kuwekwa ukutani pale sebuleni kwetu nakumbuka. Na moja nikawa natembea nayo kama nguo zangu za mwilini, sikutaka kuiacha hata kidogo. Siku nilipokuwa nakwenda kumchukua Mery, nilishtuka sana kuikuta picha ile chumbani kwako. Nikaamini kuwa Joesan alikuwa anakuangamiza huku familia yako ikiwa inakutazama. Sikuichukua ile picha ipo na kila siku nikiangalia kupitia kamera zangu nilizotega kwenye kile chumba naona jinsi Joesan alivyo na ghadhabu na ile familia yaani utadhani labda imemkosea. Jamani nyie wanadamu hawana shukurani aaaah! Sijapata kuona." aliongea Cat. Roi akatulia na kusema ni lazima akaichukue picha ya familia yake hawezi kuicha kwa yule mshenzi hata siku moja. Lakini muda huo huo akabadili maamuzi, akasema kuwa, acha akamilishe kazi kwanza na ile picha itakuwa ya mwisho.



    walipomaliza kupeana historia hiyo, Roi aliamka kutoka hapo sakafuni akiwa mpya kabisa. Alimshukuru sana Catherine kwa kuwa na moyo wa upendo. Akamsogelea na kumkumbati kwa nguvu sana. Pumzi za Roi zilipokuwa zikishuka, Cat alikuwa akihisi kitu moyoni mwake. Alikitega kifua chake kizuri kilichowauwa wanaume wengi wakora. Chuchu msumari zikawa zikakita katika kifua cha mwanaume huyo. Roi alitoka kifuani hapo taratibu huku akiwa anamtazama huyo binti kifuani. Aliporudisha macho usoni alikutana na tabasamu la ndani kabisa hadi kijana huyo akaangalia pembeni. Cat alijitoa haraka na kumwambia Roi amfuate. Wakatoka humo ndani hadi kwenye chumba kingine ambacho kilikuwa na mazagazaga mengi sana. Father D.A. Alikuwa ameketi kwenye kiti kilicho na meza kubwa ya duara mbele yake huku kukiwa na kiti kimoja ambacho kilikuwa hakijakaliwa na mtu. Cat akamwambia Roi akae huku yeye akiwa amesimama.



    "nadhani hakuna wasiwasi tena kichwani mwako Roi?" lilikuwa ni swali la kwanza la D.A baada ya Roi kuketi.

    "ndiyo, father hakuna" alijibu Roi.

    "hivyo ndivyo nilivyokuwa nataka kusikia kisha tuingie kwenye hatua ya mwisho na ngumu ya kuhakikisha unalipa yale waliyotendewa wazazi wako. unakwenda kupambana na watu

    wenye uweledi mkubwa kijana wangu, watu makatili lakini pia wakiwa ni watu wanaotumia zaidi silaha za kuuwa tofauti na mikono" alipofika hapo akanyamaza na kutulia kitini hapo kama si yeye aliyekuwa akiongea muda huo mfupi. Akavuta gilasi ya maji na kupiga funda moja kisha akasema.

    "unakwenda kupambana na mtu anayetumia zaidi sumu. Huyu mzee anafahamika kwa jina la Lee Kim. Mzee aliyekuwa akikutumia kwa kazi ya kulipa visasi vyake vya kishenzi huku akikutumia kama kifaa cha kumuingizia pesa kwa kukosa utu. Ni mtu wa siku nyingi sana na alikuwa hanipendi kwa tamaa zake za kipumbavu. Aliapa kuniuwa kwa kipindi kirefu sana. Aliponikosa na, ndipo akamuua baba wa Mery ambaye alikuwa ni mwanangu wa pekee. Aliniumiza sana lakini sikutaka kufanya papara kutokana na yeye alikuwa ameshajenga mizizi imara ndani ya nchi ya Tanzania. Huyu mzee hana utu hata kidogo na anatakiwa afe na siyo kuingia kwenye mikono ya sheria. Lee anatumia sumu ya Star Poison (SP) Sumu hiyo aanaitumia kuipakaa kwenye risasi zake amabazo zinaumbo la nyota, anazoziita Star Bullet (SB). Ni sumu ambayo kama utafanikiwa kupigwa na hiyo risasi kwa kupapuza eidha ikakuchubua au kuingia kwenye nyama ambayo si ya kukusababishia madhara makubwa zaidi ya jeraha, basi utakuwa ukiishi kwa maumivu makali sana na ni kwa muda mfupi tu kama wa masaa 27 hadi 36 kisha unapoteza maisha. Huwa risasi hizo hazilifanyi jeraha la muhanga kutoa damu, ni sumu inayokausha damu kwa haraka sana. Ukiwahiwa na kupewa dawa ambayo tunayo, utakuwa umepona lakini kama hautowahiwa jua wewe ni buriani." aliongea father.

    "sasa mimi nitaweza kupambana na huyo mtu kweli?" akauliza Roi.

    "ndiyo, utaweza. Kwanini usiweze. wahenga walisema kuwa dawa ya moto ni moto wenyewe. Hivyo kama wao wanatumia sumu na sisi tunatumia sumu na pia tutakupa mavazi maalumu ambayo utavaa wewe tu kwa sababu wewe ndiye utakayekuwa kipaumbele kwa kila jambo, hivyo mavazi hayo yatakufanya hizo risasi zao zisifue dafu hata kidogo."

    "ohoo hapa sawa." alijibu Roi kwa furaha sana kisha mzee huyo akasogeza begi dogo la kuvaa mgongoni na kulifungua, akasema.

    "humu kuna dhana mbalimbali kama visu, Cheni za kukata na bastola tatu. Hizi bastola ndizo zinazohitaji maelezo zaidi. Ukizitazama hazijafungwa kiwambo cha kuzuia sauti lakini hizi huwa hazipigi kelele pindi zinapofanya kazi yake. Zinatumia risasi nyembamba sana na zina sumu mbaya kuliko, usicheze mchezo mchafu na hizi silaha hata kidogo. Risasi zake zimetengenezwa kwa mfano wa meno ya nyoka hatari anayepatikana kwenye misitu ya huko Australia. Nyoka hao wanaitwa Death Adder (D.A). Na risasi hizo zinaitwa Bullet pin (BP) au Snake Teeth Bullet (STB). Sumu iliyotumika kuundia hizi risasi ni hatari ...................

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    sana kijana wangu na imechanganywa na sumu ya kiumbe nyika huyo niliyekutajia na kemikali nyingine. Hii inauwa papo hapo kwa sababu inashambuli mara tatu, kwanza inashambulia mfumo wa upuaji, pili inashamulia neva zote na hapo hapo inasimamisha mapigo ya moyo kwa haraka sana. Sumu hii haichagu sehemu ya kuleta madhara kama ya kwake, hii inapokutana na damu tu, hapo hapo inaanza kazi." lilikuwa ni somo kubwa na linalohitaji utulivu na usikivu mkuwa endapo utakuwa si muelewa unaweza kusababisha madhara makubwa sana. Somo likawa limekwisha ikabakia tu mzee huyo kuhitimisha ili Roi kesho aelekee nchini Tanzania.

    "hakikisha utakapofika Tanzania Roi, unakutana na mzee mmoja anayeitwa Rafael, huyu atakupa mengi na ninaimani atakusaidia." alisema father na Roi akauliza.

    "lakini Rafael si miongoni mwa watu wa huyo Mr. Kim?"

    "ndiyo najua lakini wewe ukifika mwambie uko hapo kwa ajili ya D.A, halafu tulia"

    "ok, sawa father nimekuelewa" alijibu Roi kisha D.A akamgeukia Cat ambaye alikuwa ametulia kimya akifuatilia hayo maongezi, akasema.

    "niliwahi kukuambia kuwa nataka ukirudi Tanzania ni kwa ajili ya kwenda kulipa kisasi na kumpata ndugu yako. Roi ameshapatikana, sasa pati iliyobaki na ya mwisho ni kummaliza huyo mkorea kisha sisi turudi nyumbani tukalijenge Taifa letu. Utaongozana na Roi kwenda Morogoro na mtamchukua kijana mmoja kwa ajili ya kuwapa msaada zaidi." alihitimisha na kisha yeye akaondoka hapo akiwaacha wenyewe wawili. Walitazamana kwa kina sana bila kusemezana. Cat akamsogele huyo kijana na kijana huyo akasimama. Cat akasema.

    "sasa nimeamini kuwa wewe pekee ndiyo mwenye uwezo wa kumuangusha Lee Kim. Father nakimbuka alinipa hizo silaha mara moja tu tena kwa masharti makali pindi nilipokwenda kuwapa salamu wale wapuuzi kwa kumuuwa Martha. Lakini wewe hata hakupi kwa mashart hayo tena amekukabidhi nyingi tu"

    "hata kama ni mimi Cat, lakini tambua kama pembeni yangu haupo wewe, hakuna kinachofanyika. Umekuwa ni mtu muhimu na wa pekee sana kwenye maisha yangu. Sina cha kukulipa zaidi Cat, ni Mungu ndiye anayeweza kukulipa wewe, wewe ni wa pekee sana" aliongea Roi na kumfanya Cat akose namna yoyote ya kuongea wakabaki wanatazamana tu. Cat akavuta picha ya mbali sana kwa kijana huyo, akiuwangalia mwili wake alijikuta akivutika zaidi. Alishamuona kila kitu kijana huyo, alichobakisha ni kuvifanyia kazi vile alivyoviona tu basi. Catherine akawa anazidi kumsogelea Roi hadi akawa anaipata pumzi ya kijana huyo iliyokuwa ikipumuliwa kwa jinsi ambavyo walikaribiana. Alikuwa anaufuata mdomo wa Roi ili tu kutimiza ahadi ambayo alimuahidi kijana huyo kuwa akishajitambua yeye ni nani na kumtambua yeye ni nani kwenye maisha yake, na ndiyo siku atakayomkabidhi moyo wake. Hakuna kitu ambacho kingemzuia Cat kutokuwa kimapenzi na Roi. Hawakuwa ndugu wa kuzaliwa japo waliishi kama familia moja kipindi hicho cha utoto lakini hiyo si sababu ya kumfanya Cat asiutoe moyo wake na kumkabidhi kijana huyo. Sasa walikuwa wamesogeleana kabisa. Wote wakiwa na lengo la kupokeana. Wakati wanakaribia kugusana, wakiwa wamebakiza zero distance, Wakashtuliwa na sauti ya Mery iliyoingia ndani ya chumba hicho.

    "dada nimekutafuta kote huko sikukuona, kumbe uko huku na kaka Chriss, mmenikimbia si ndiyo?" alilalamika Mery.

    "hapana hatuja kukimbia, tulikuwa tuna maongezi kidogo huku na babu" alisema Cat huku akimbeba.

    "oohoo! Kama ni hivyo sawa"

    "lakini kuanzia leo huyu usimuite kala Chriss sawa?"

    "nimuite nani?"

    "utakua unamuita kaka Roi"

    "oo jamani ni jina zuri sana, hata mimi nitabadilisha jina nikisha kuwa umchezaji mkubwa wa Tenes" alisema Mery. Wote hapo wakacheka lakini ghafla Mery akanuna hadi wakapatwa na wasiwasi na kumuuliza kwa nini amenuna na alikuwa na furaha. Akajibu kuwa, walikuwa wanamcheka, inamana hawezi kuwa mcheza Tenes mkubwa kama yule dada wa Uingereza sijui ndiyo nani yule.

    "jamani siyo hivyo Mery tulikuwa tunafurahi sana kwa kuchagua mchezo huo ukiwa bado na umri mdogo, hivyo kama utakuwa na nia na kuongea juhudi, utakuwa maarufu kweli." Mery aliposikia maneno hayo alijikuta akifurahi na kuona kumbe watu wote mule ndani walikuwa wanapenda kipaji chake. Cat alimuangalia Roi muda wote huku akiona kama Mery alikuwa ameharibu. Roi akamsogelea na kumng'ata sikio na kumwambia kuwa yeye yupo kwa ajili yake hivyo aache papara kwani hata yeye anamtamani sana. Siku ikaisha kinamna hiyo.



    ******************************************************************************



    Siku iliyofuata, Roi, Cat pamoja na Jay, walikuwa ndani ya gari wakiwa wanaelekea uwanja wa ndege. Dakika chache baadae, walikuwa ndani ya uwanja huo wa Jomo Kenyata wakiwa wanasubiria ndege ianze safari kuelekea kilimanjaro kisha wachukue tena ndege hadi Morogoro. Siku hii ndiyo siku ambayo wana kampuni walikuwa wakimsubiria SM wao kwa ajili ya kumpa pole na kumpongeza kwa kuweza kupambana hadi kufanikiwa kumtoka yule mwanamke aliyejifanya mteja kumbe ndiye muuwaji na mkwamishaji wa mipango yao. Walisha wasiliana na Suzane kuwa atakapofika uwanja mdogo wa hapo morogoro, yeye ndiye atakayemfuata kwani amemmisi sana. Katika siku ambazo hakuwepo. Ndege ndogo ya shirika la Emirates, ilitua na kutoa matairi yake, katika uwanja wa hapo Morogoro. Wakashuka watu hao na kupitia kwenye ukaguzi wa hapo uwanjani kisha kutoka ili kuelekea mahali zilipo gari.



    "SM!, SM!" sauti ya kike iliita. Roi akageuka kutazama sauti inapotokea. Alikuwa ni mwanamke mrembo sana mwenye umbo la kuvutia ambaye alikuwa anakuja mahali alipo. Wakati akiwa anashangaa Catherine akampita na kumwambia kuwa huyo ni mwanamke ambaye alikuwa anauhusiano naye wa kimapenzi na ndiye aliyekuwa ameihifadhi namba yake kwa jina la Honey. Chriss akajua kazi ipo. Akazuga na kujifanya hajamuona, alijua fika Catherine alimwambia yale kwa kumtega, alijichanganya na watu akapotea na kutokea mahali ambapo Suzane alikuwa amepaki gari. Tayari kwa muda huo walikuwa wameshaachana na akina Jay, hakupata tabu kumjua Suzane, kwa sababu ni mwanamke aliyekuwa akimfahamu kitambo tu pia alikumbuka kuwa alishawahi kushiriki naye kitanda. Walikumbatiana na mwanamke huyo kwa furaha kubwa, Roi alikuwa akifanya vile vile vitendo alivyokuwa akivifanya wakati ni Sex Machine. Hakuonesha mabadiliko yoyote mahali hapo. Muda huo Cat na Jay, walikuwa wanaingia kwenye Tax na kuondoka taratibu maeneo hayo. Suzy akaondoa gari hiyo kwa kasi kubwa sana huku akiwa na furaha kubwa pasi na kujua kuwa humo ndani ya gari hakukuwa na SM bali kulikuwa na Roi mwenye hasira ya kuuwawa kwa wazazi wake. Walifika kwenye kampuni yao, wakaegesha gari maegeshoni, wakashuka. Moja kwa moja ilikuwa ni ndani ya kampuni hiyo. Humo ndani walikuta tafrija fupi iliyokuwa imeandaliwa kwa ajili ya kumpongeza. Walimmwagia Pombe ikiwa ni furaha kubwa kwake. Muda ukafika wa kuelezea yale yote yaliyotokea huko, hapo wakiwepo wafanyakazi wote wa kitengo hicho cha kishenzi. Alieleza kila kitu lakini hakugusia habari za kuvamiwa na maadui kule Brazil kwa sababu ile ilikuwa ni oda ya nje ya kampuni. Muda wote huo wakati wakiwa wanasikiliza yale yaliyomtokea kijana huyo huko nje, Rafael alikuwa hana amani hata kidogo kwani muda wote jicho la kijana huyo lilikuwa likimtazama yeye. Amani aliikosa hadi kijana huyo alipoondoka hapo na keulekea ofisini kwake baada ya kulikabidhi lile vazi kwa Tai ambalo lilikuwa limeharibika vibaya. Alitulia ofisini hapo akiwa na tabasamu la aina yake kwa kutokujulikana.

    "mmekwisha sasa." alijisemea Roi huku akiwa hapo kwenye kiti amekaa. Alikaa kwa muda kidogo akifanya hiki na kile mwishoe akaondoka na kuwaaga wafanyakazi baadhi kuwa anaelekea nyumbani kupumzika kwani amechoka sana.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "nimekumiss sana SM, leo usiku nitakuja kwako kwa ajili ya kukupongeza" aliongea Suzane. Roi akamtazama na kumuonea huruma sana, laiti angejua kuwa hapo anaongea na mtu anayejitambua, asingethubutu kabisa kumkaribia.

    "ooh no, Suzane, leo niko na uchovu sana wa safari hivyo sidhani kama nitamudu kukupa vitu vizuri" alijibu Kijana huyo.

    "jamani kidogo tu si unajua nimemisi kifaa chako cha kazi na nataka unikandamize nacho chote leo"

    "najua lakini nadhani ni vizuri zaidi kama tutafanya kesho kwani leo sitakuwa vizuri" alisema hivyo Roi. Suzane ikabidi amuelewe kijana huyo kwa shingo upande. Hakuwa na jinsi ya kufanya japo alikuwa kweli akimuhitaji kijana huyo kwa dhati kubwa. Roi alikumbuka maneno ya Cat kuwa kwa muda huo haruhusiwi kufanya mapenzi na mtu yeyote ndani ya hiyo kampuni kwani kufanya hivyo ni kuwapa nafasi ya kumjua. Roi kwa wakati huo alikuwa ana kila kitu cha asili kwenye mwili wake. Alitoka hapo na kupita kwenye korido kubwa, wakati akiwa anachuku uelekeo wa kutoka nje, alimuona Mzee Rafael akiwa anatokea upande wa nje. Roi aliachia tabasamu pana alipokuwa amegongana macho na mzee huyo. Hali hiyo ikampa maswali mengi sana mzee wa watu. Hakuwa na raha hata kidogo, haikuwahi kutokea hata siku moja kuliona tabasamu la huyo kijana, iweje siku hiyo. Mzee Rafa aligeuka na kumtazama huyo kijana kisha hakuonesha kitu chochote hapo, aliyageuza macho yake na kuzitazama kamera za koridoni hapo na kuondoka akaingia ofisini kwake.

    "lipo jipya hapa siyo bure?" aliwaza mzee huyo mara tu alipojikalisha kitini mwake.



    "ni wapi mmefikia Cat?" aliuliza Roi mara baada ya kuwa garini mwake.

    "Kilakala juu utatukuta, njoo hadi kiwanja cha mpira cha kilakala kilicho nyuma ya shule ya chekechea.................



    A to Z kisha tutakupa maelelekezo mengine." alitoa maelekezo ya awali Cat. Roi akawasha gari na kutokomea. Alifika kwenye huo uwanja, haikumpa tabu kwani uwanja huo wa mpira wa miguu, uko barabarani kabisa. Hapo akapewa maelekezo mengine na kuambiwa aifuate barabara inayopanda juu upande wake wa kushoto. Akafanya hivyo. Dakika chache akawa ndani ya jumba kubwa lenye fensi ya maana kabisa. Jumba lenye kupendeza kimtazamo wa nje tu. Roi akapaki gari mahali pa maegesho na kushuka. Catherine na Jay wakatoka nje na kumlaki.

    "hapa mlipaandaa kabla nini, maana ni pazuri sana eti, pako kifalme sana Cat?" alisema Roi.

    "kwahiyo panavutia sana eeh!" aliuliza Cat akiwa na alama ya mshangao kidogo. Inamaana hata hapo Roi alikuwa hapakumbuki. Alitingisha kichwa kusikitika kisha akamwambia.

    "hii ni nyumba yako Roi, uliinunua ukiwa ni Sex machine na si hii tu bali ulinunua nyumba mbili, hii ya huku na nyingine iko mjini"

    "mbona kama najiona kichaa Cat, unaongea nini sasa?"

    "hata mimi nilikuwa sijui hilo ila father ndiyo alinipa hizi ripoti kabla hatujaondoka Nairobi na aliniambia kuwa wakati wewe ukiwa unaelekea Kwenye kampuni yenu, mimi na Jay tutafikia hapa. Roi usishangae, hii nyumba uliifanya ni moja ya nyumba zako za siri sana. Hukutaka mtu yoyote ajue kuwa kama unanyumba huku. ila hiyo moja ndiyo inajulikana" alisema Cat kwa utulivu sana.

    "ipi hiyo inayojulikana?" akauliza kwa haraka mno.

    "unakumbuka kuwa kuna binti alikuita tukiwa uwanja wa ndege?"

    "ndiyo nakumbuka."

    "huyo binti ndiye uliye kuwa ukishiriki nae kila kitu na ndiye alikusaidia kuzipata hizi nyumba." alitulia kwa takriban dakika moja nzima kisha akaondoka hapo na kuingia ndani, alijawa na ghadhabu sana kijana huyo. Wenzake wote wakamfuata huko ndani. Roi aliingia kwenye chumba kimoja akavua nguo kisha kuingia bafuni. akaoga na kumaliza haja zake za msingi kisha kurudi ndani. Alipofika chumbani akamkuta Cat akiwa na nguo laini akiwa amejilaza kitandani. Akashangaa.

    "vipi Cat, nataka kubadili nguo" alisema Roi.

    "huu nimeuona ni muda muafaka wa kufanya hili jambo Roi." aliongea Cat huku akijinyanyua pale kitandani. Akasema tena.

    "kinachofuata ni kazi na hakuna muda mwingine kama huu. Nahitaji ushughulikie huu mwili Roi. Huu ndiyo muda wa kuitengeneza historia nyingine ya maisha yetu. Nakupenda sana na siwezi kuzificha hisia zangu tena. Sitaki kuwa mtuhumiwa wa moyo wangu mwenyewe." alizidi kuongea dada huyo kisha nguo zikaanguka sakafuni, Roi akakumbwa na mshtuko hatimae taulo likamdondoka, wakakumbatiana, wakapeana midomo na kuiruhusu miili yao ihisi joto la asili. Wakatupana kitandani na kuiruhusu miguno adimu ya mahaba ikimeze hiko chumba. Wakafaidi kile kilichopadwa kufaidiwa na wawili hao.



    MAZIMBU



    Usiku wa saa tatu, mzee Rafael alikuwa ametulia ndani kwake akijipatia chakula cha usiku taratibu. Muda mwingi alikuwa akifikiria jambo fulani, aliendelea kula kwa upole sana hadi akamaliza kisha akarudisha vyombo mahali vinapokaa baada ya kuvifanyia usafi. Akawa anapata sharubati kusukumizia chakula alichokula. Aliipeleka birauli kinywani, alipoirudisha chini, alisikia mchakacho kwenye kitasa cha mlango. Akageuka na kutazama mlango huo. Akaona kitasa kinanyongwa na mlango kufunguka akajua kuwa mtu huyo anayetaka kuingia, hakuwa na dhamira nzuri na yeye. Aliruka na kujificha mahali akatulia kimya. Mtu huyo ambaye alikuwa akiingia hapo hakuwa mwingine, alikuwa ni Roi. Alifungua mlango taratibu hadi akapata uwazi wa kuweza kuona ndani. Akaona birauli ikiwa imetulia pale juu ya meza ambayo aliamini kuwa si muda mrefu palikuwa na mtu mahali hapo. Akapiga hatua na kuingia ndani humo kwa uangalifu mkubwa sana. Wakati akiwa anazidi kuingia ndani humo, mzee Rafael alifyatuka mahali alipo na kumvamia kijana huyo kwakushtukiza lakini kijana huyo alijua zamani jambo hilo. Alihama zamani sana na kumuacha mwenyewe mahali hapo.

    "tulia mzee wangu ni kitu kidogo sana nimekifuata mahali hapa ila naona kama unataka kuharibu urafiki" alizungumza Roi kwa sauti ya upole. Rafael hakugeuka lakini sauti ya mtu huyo aliyevamia hapo nyumbani kwake aliitambua vema tu.

    "nilijua tu utakuja mahali hapa ila sijajua nini hasa kimekuleta kijana wangu?"

    "kwani umeshanifahamu?"

    "ni vigumu sana kukusahau SM, unaweza kuniambia kilichokuleta hapa nyumbani kwangu?"

    "labda ni roho yako mzee wangu maana ni ngumu sana kumuacha mtu ambaye unajua fika amekutendea mabaya" maneno hayo yalimfanya Rafael kushtuka sana. Kumbe alichokuwa akikiwaza ni kweli tupu. Alijua kuwa ingetokea siku kama hiyo ya kutokea kijana huyo. Alikuwa tayari kufa mzee huyo, aliona ni bora sana kufa lakini ajue kuwa Taifa lake linakuwa katika hali ya usalama. Akifa yeye na watu waliomuajiri na kumfanya atumikie mambo hayo yasiyofaa, ni sawa kabisa na yuko radhi kwa jambo hilo.

    "ha ha haaa! Nilijua kuwa kuna siku ningekufa na ningeuliwa na watu wanaoisaka haki ya Taifa lao na wananchi wao kwa ujumla, wewe unayetaka kuniuwa ni kipi hasa unachotaka kulifanyia Taifa lako?" aliongea mzee huyo huku akiwa na kicheko kikubwa sana kisha akageuka kumtazama kijana huyo aliyepo hapo. kisha akaendelea kusema.

    "najua kuwa kwa sasa siyo Sex machine tena wewe ni Chriss si ndiyo, wewe ni Chriss, umerudi kwenye jina lako la awali ama?"

    "ndiyo nimerudi kwenye jina langu la awali na si awali tu bali ni asili kabisa, kwa sasa mimi ni Rajab Isihaq Omair au waweza kuniita Roi. Ni mtoto wa marehemu Isihaq, baba yangu ni Isihaq Omair. Baba yangu ndiye aliyedhurumiwa uhai na huyu mnaemuita Boss" aliongea kwa hisia za juu sana kijana huyo huku akisogea kari na mzee huyo.

    "wewe ni mtoto wa Isihaka?"

    "ndiyo." alijibu Roi.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "nini kimekuleta hapa sasa ni kuja kuniuwa pekee ama kuna jingine?"

    "hilo silo lililonileta Rafael," aliweka koma Roi na kumuangalia mzee huyo na kufanikiwa kuuona mshtuko mkubwa kwenye sura ya mzee huyo. Rafael alishtuka sana na kukumbwa na taharuki kubwa, alisema kuwa yuko hapo kwa ajili ya kutaka roho yake pengine, mbona amebadilisha na kusema kuwa hayupo hapo kwa ajili ya jambo hilo? Ni lipi sasa? Kichwa cha Rafa kilijaa maswali lukuki dhahiri ya shahiri alikuwa na mkanganyiko mkubwa wa mambo. Alipotaka kuinua mdomo kuuliza, akawahiwa.

    "nimekuja kwa kazi moja tu kama jina langu la zamani lilivyonituma, nimekuja kwa ajili ya RIVANGE OF ISIHAQ (ROI) lakini siwezi kufanya malipizi hayo ikiwa sijapata mwanga na kile unachokijua kutoka kwenye kampuni ya SC." aliweka tuo hapo Roi.

    "hakuna kitu chochote ninachokijua kijana wangu, mimi ni mtu mdogo sana ndani ya ile kampuni" alijitetea mzee Rafa.

    "nilikuwa na uwezo mkubwa wa kukulazimisha ili useme lakini wewe si wa kulazimishwa na ulikuwa ukionekana muda tu kuwa uko kinyume na wale wapuuzi. Sema ulibanwa na sheria kali za kampuni ile. Labda nikuweke wazi kuwa anayetaka unisaidie kazi hiyo ni

    father D.A." Mzee Rafael alishtuka nusura alambe sakafu au kusujudu kwenye hiyo nafasi kwa kutaka kuanguka. Macho yalimtoka pima. Kitendo cha kuambiwa kuwa aliyehitaji msaada ni father D.A, alishtuka sana. Alinyong'onyea mithili ya kamba ya mkonge inayonyong'onyea pindi ikiwa imefungwa juu na kuning'inia. Alipiga hatua za taratibu na kwenda kukaa pale kwenye kiti alipokuwa amekaa awali wakati akijipatia chakula cha usiku. Kijana Roi naye akajivuta na kwenda kukaa mahali hapo na kuzidi kumtazama mzee huyo kwa jinsi alivyokumbwa na unyong'onyevu wa namna yake. Rafael alikinyanyua kichwa chake juu na kulitazama dari la hapo sebule akafumba macho yake akiwa anaziruhuhusu fikra zake zikumbuke mengi yaliyotukia nyuma.



    "hakikisheni anakufa ndipo tutakapoondoka hapa tukiwa tumeridhika kujitoa kwake kwenye kundi la kimafia" sauti nzito ilisikika ikiongea mahali hapo huku muongeaji akiwa amekamata jambia kuukuu mikononi mwake. Kikosi cha watu zaidi ya kumi na watano kikamvamia mtu mmoja anayekimbilia kuwa kwenye umri wa makamo. kipigo kikatembea mahali hapo. kila jamaa hao walivyojaribu kumzidi mtu huyo katika mapigano walifeli. Mtu huyo alikuwa mahili sana katika nyanja za mapigano. Walitembezewa kichapo na wingi wao. Walikuja wengi kumvamia k

    mtu huyo aliyeonekana mpole kabisa lakini akiwa ni moto wa kuotea mbali. Aliwachangua wote mahali hapo kila mmoja akaangukia kwake kisha mtu huyo akasimama kwa tambo kubwa na kusema.

    "nimeamua kujitoa kwenye kundi la mafia na kwenda kuishi maisha yangu mwenyewe. Tumefanya unyama sana na kupokonya watu roho zao zisizo na hatia. Mimi ni mtanzania safi sitaki tena kuuwa jamani naombeni mniachie niondoke na sitawatafuta wala kuwachomea popo......!!" hakumaliza bwana huyo, ukwenzi wa uchungu ukamtoka mtu huyo. Lile jambia lililokuwa mikononi mwa mtu yule mweusi ambaye ndiye aliyetoa amri vijana wale wampige mtu huyo, alikuwa amelipitisha lile jambia kwenye mgongo wa yule mtu, lilimkata sana. Alijipinda kwa nyuma yule mtu kwa maumivu makali hapo hapo yule bwana mweusi akasema.

    "tunaongozwa na sheria pia taratibu, hakuna sheria kwenye kundi letu inayosema kuwa mtu anaweza kujitoa atakavyo kama mwanamke asiyefunga ndoa aondokavyo kwa mumewe. Ulikubali kujiunga na huwezi kujitoa, umeshakuwa mtu muhimu sana kwenye kundi hili la mafia" ndivyo alivyokuwa akibwata mtu huyo. Wale vijana waliopigwa, walikuwa tayari wameshasimama wakisubiri amri nyingine. Amri ilivyotolewa ya kuvamia, wakachezea tena kichapo na kudondoka chini tena. Lakini hapo hapo, yule mtu mweusi .................



    , yule mtu mweusi alimshtukiza tena. Alipitishiwa panga jingine la mgongoni, mkononi na mkononi tena kijana yule akawa hana nguvu. Hapo sasa wale vijana wakapewa amri ya kushambulia. Walimpiga sana, walimpiga bila kujali kuwa wanaweza kuuwa. Lakini ghafla bin vuu, yule mtu ashtukia kundi lile la vijana lililokuwa likimuadhibu, likirushwa mbali na kila mmoja akiwa anahisi maumivu makali. bwana mmoja amabaye hakuwa amzee wala kijana, alitua mbele ya mtu yule aliyekuwa akiadhibiwa. yule mtu hakuamini hata kidogo kuona ameibukiwa na msaada lakini pamoja na msaada huo kuibuka, alijua fika hapo hauwezi kufua dafu kwa kundi hilo la mafia. wale watu wakaja tena. walikosea tena walikosea sana. Walikula mkong'oto wa nguvu sana. Ndani ya sekunde kumi na tano wote wale walikuwa marehemu. Yule mtu mweusi akajisogeza naye na jambia lake, wapi! Hakufanya kitu pia naye akasafirishwa kuzimu.



    Mzee Rafael alishusha pumzi nzito sana baada ya kukumbuka kumbukumbu hiyo na kumuangalia yule kijana ambaye alikuwa hapo mbele yake akiwa bado anahamu ya kujua hiyo kumbukumbu imeishia wapi. Rafael alijiweka vizuri kitini na kusema.

    "baada ya kunipa ule msaada yule bwana, alinichukua na kunipeleka mahali alipokuwa akiishi. Alinipa matibabu hadi nikatengemaa kabisa kiafya. Hapo ndipo alipojitambulisha kwangu kwa jina hilo la Father D.A na kunipa kazi ambayo alitaka nimsaidie na yeye akaahidi kinisaidi siku moja. Aliniambia kuwa kuna kampuni inajihusisha na masuala ya utalii iko Morogoro maana kwa kipindi hicho tulikuwa mjini Arusha. Akaesema kuwa kampuni hiyo si kwamba inajihusisha na masuala ya utalii tu laa hasha. Ilikuwa inafanya mambo ya kijasusi na utalii ni kama mwamvuli tu. Akaniambia kuwa anataka nikaombe ajira kwenye kampuni hiyo. Nikamwambia kuwa siko tayari kufanya ujasusi kwa sababu si kazi nzuri na hata pale aliponiokoa na kifo, nilikuwa najitoa kwenye kikosi cha mafia. Akaniambi anajua hilo na anafanya hivyo ili kuleta amani ya nchi. Basi mimi nikakubali kumsaidia lakini nilimwambia kuwa afanye haraka maana sitopenda kuuwa kila wakati. Akaniambia si muda mrefu. Basi akanipa njia za kuja kwenye kampuni hiyo kutoka Arusha. Nilipofika hapa nikakutana na mwenzangu ambaye kwa sasa ni marehemu, tukaingia hapa kwa njia nilizopewa nikampa na mwenzangu, tukapewa majaribio na tuliposhinda, tukaajiriwa rasmi." alimaliza kutoa historia hiyo mzee Rafa. Roi akawa ameelewa sasa kwa nini Father amemtuma mahali hapo.

    "amechelewa sana kuja hadi nilikata tamaa na kutaka kufanya njia za kujitoa mwenyewe kwa kujua labda amenitelekeza" aliongea tena Mzee huyo. Roi akamwambia kuwa kila kitu kina chanzo, huwezi kukurupuka halafu utegemee kushinda.

    "ni kweli kabisa kijana. Haya niambie ni nini unahitaji nikusaidie?" alisema Rafa kisha Roi akatulia kidogo na kusema.

    "umeishi miaka mingi sana kwenye ile kampuni toka kijana hadi sasa ni mzee, kuna vingi vya siri na vya muhimu unavijua"

    "ni kweli kijana, ni kweli kabisa." alidakia Rafa.

    "nataka vichache lakini vyenye umuhimu" aliongea Roi na mzee Rafael kuanza kumpa vitu vya msingi. alimwambia kuwa kila kitu kinachoendelea mule ndani ni unyama mtupu, alimchambulia vingi hadi nyumba sita za siri za mr. Kim.

    "vijana wengi wa hapa morogoro na nje ya morogoro, wameharibiwa na huyu mzee. Ni bora hata wewe uligeuzwa kuwa mashine ya ngono lakini mamia ya vijana wamebadilishwa na kuwa mashoga. kuna mitambo iliyotengenezwa na kijana anayefahamila kwa jina la Tai, mtambo huo unakazi ya kuwapadikiza vija homoni za kike kwa wingi na hatimaye kuwa mashoga. Wengi anaishi nao kwenye jumba lake miongoni mwa majumba hayo sita ya siri kama wake zake. Kila siku anatafuta wa kulala naye na akiwachoka anakwenda kuwaweka kwenye jumba namba 03. Jumba ambalo ukilitazama kwa nje huwezi kujua kama ndani kuna ushetani. Hili ni Happy Club"

    "mzee wangu unaizungumzia ile Happy Club pale masika?" alidakia Roi na kumkatisha mzee huyo. Mzee akajibu ndiyo. kisha akaendelea.

    "kuna mashoga wengi mule ndani na wengine walitawnywa mitaani ili wazidi kujaa huko kwenye mitaa" alipomaliza hivyo, Roi alimshukuru mzee huyo na kumwambia kuwa muda si mrefu anakwenda kuibadilisha hali hiyo na kuifanya Morogoro iwe ni ya amani pamoja na Tanzania kwa ujumla. Roi aliondoka hapo kwa siri sana huku akiwa na wingi wa tabasamu usoni mwake. Hakutaka kwenda Kilakala, alipitia kwenye nyumba yake aliyopewa na Kampuni baada ya kuelekezwa na Cat.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ############@#@###@##@@@@@@##@@#@@@@@@@@####



    "ooh, my umekuwa kijana mzuri utadhani hukuwa kwenye matatizo huko nje ya nchi?" ilikuwa ni sauti ya Merina ikimwbia Roi ambao bado wao walikuwa wakimfahamu kwa jina la SM.

    "Merina naomba uwe mbali na mimi bwana si unajua wewe ni mali ya bosi" alijibu Roi/Chriss.

    "unadhani nakolea basi hata akipanda, anakuwa hoi mapema sana, wewe ndiyo unajua kunikuna pande zote kila nitakapo kupa unapatendea haki"

    hata sasa huta kolea ukikunwa na mimi, siyo kama zamani Merina" alisema Roi na kumfanya Merina kushtuka kidogo.

    "kivipi, kwanini unasema hivyo?" likawa swali.

    "sitakuwa huru kukushindilia, nitakuwa na hofu we si unajua bosi ninavyomuogopa" alisema.

    "tena huyu anatakiwa akae mbali kabisa na wewe, hii ni muzigo ya bosi" aliongea Suzane akiwa anaingia humo ndani ya ofisi. Tena akiongea kwa kuweka utani.

    "muzigo ya bosi nini, mzigo wa bosi unaujua wewe, mzigo anatembea nao kwenye suruali hapa ni kama mwanzo, kwanza nimeukumbuka sana ule mchezo tuliocheza sikuile tukiwa watatu. Leo tuko wawili lazima ukome maana unajifanya hutaki kutiwa madole ya huko nyuma, leo lazima nikutie na utaliwa huko nyuma na SM leo nasimamia mwenyewe hiyo kazi." alisema Merina na kumfanya Suzane kuganda kama kapigwa picha ya mnato. Alijua kweli kwa muda huo sasa bikira ya nyuma inamtoka maana mbele ya huyo jambazi wa kike si mchezo.

    "SM mtoto mnato huyu hajawahi kuguswa nyuma leo rinda unazichangua mwenyewe wa kwanza raha iliyoje hiyo" alizidi kuropoka kahaba huyo wa kike. Muda wote huo Roi alikuwa akiwachora tu kama anayewaambia yaani nyie hakuna kitu mnachokiwaza hapo zaidi ya huo uchafu. Wao hawakujua mahesabu ya huyo kidume hapo. Muda wote huo alikuwa anafikiria mbinu ya kuwatoka hapo bila kumtilia mashaka.

    "mbona huoneshi hamasa yoyote SM?" aliuliza Merina baada ya kumuona kijana huyo kaganda mahali hapo akiwashangaa tu.

    "kwanza namtazama Suzy kwa jinsi alivyoduwaa baada ya kusikia kuwa leo ananipa utamu wa nyama ya bata hadi anatia huruma. Unadhani nakuacha mama, leo utaita jina langu la zamani, kitu kipya hicho kipira, nakifungua mwenyewe"

    "bwana usiseme hivyo SM mwenzako hapa karoho kananidunda sijui kama hata nitaweza." alilalamika Suzy, Merina akacheka kwa nguvu sana. lakini Roi akamalizia.

    "pili nawaza kumtungua mamaa bosi, itawezekana kweli"

    "enhee, kwenza bibi wewe ondoka" alisema Suzy. Merina akaweka ngumu kuwa hatoki ni lazima aliwe leo hapo hata kwa kufunga mlango. Roi akaona kazi anayo. Ghafla mlango wa hiyo ofisi ukafunguliwa na Joesan akaingia.

    "na nyinyi hamchoki kuwa na huyu mtu, hebu nipisheni kidogo nina maongezi nae." aliongea Joe. Wale mabinti wakatoka humo wakiwa wamechukia kabisa. Roi alitabasamu na kuona kuwa sasa kazi imekuwa nzuri. Maongezi yakafuata. Hakuna kikubwa walichokiongea mahali hapo hata moja la msingi, kubwa lilikuwa ni kuhusu habari za Urusi na Marekani. Joesan alimwambia kijana huyo kuwa Chalcovich hakukubali hata kidogo alipozipata habari kuwa amedhulumiwa, akahiidi kumuuwa kila mtu aliyeshiriki. Alikwenda ufaransa yeye na kikosi chake na kwenda kumuangamiza bwana yule wa kule Ufaransa kisha akageukia Marekani na kwenda kukutana na BC. Huko ndiko kulikokuwa na mapigano makali, vijana wote wa BC waliangamizwa lakini pia vijana wote wa Chalco, waliangamizwa nao. Wakabaki wababe hao wawili BC na Chalco. Chalco akamwambia BC kuwa anauwa yeye kisha anakuja kunimalizia na mimi huku. Nilipozipata taarifa hizo nilicheka sana, nani anaweza kunigusa mimi wakati nikiwa nalindwa na mtu mithili ya jini. Nani anaweza kukuuwa wewe Sex machine. Roi akajibu hakuna huku akiwa anamlamba kisogo.

    "Sasa mabwana wale walipigana sana hadi mwisho wa siku wakauwana wenyewe kwa risasi. Roi aliposikia kuwa makundi yote matatu yameangania sambamba na viongozi wao, alitabasamu na kujua kuwa mpango wao umefanikiwa. Joesan akasema.

    "kesho kuna kazi moja tu ambayo anatakiwa kuifanya ya kuitafuta harufu ya mtu anayejiita D.A. Hapo sasa ukiuwa huyo mtu, hata wewe ukifa haina shida." alisema Joe. Roi alimtazama Joe kwa uchungu mkubwa sana, Joesan. Hakuamini kama huyo jamaa hapo mbele yake ndiye yule aliyekuwa akijifanya kuonesha upendo mkubwa kwake.

    "nilipambana kwa ajili yako mbwa wewe, nilihakikisha hupati maumivu na wakati mwingine nilidiriki kuyabeba mimi maumivu ili tu uwe na amani kwa kudhani umeonesha wema kwangu na kunipa msaada mkubwa kwa kudhani umenilea baada ya wazazi wangu kufa. Niliamini wewe unaundugu na mama kama ulivyowahi kuniambi, kumbe ulikuwa unaning'ong'a, kumbe ulikuwa ukinilamba kisogo kwa ulimi wako wa kifirauni, kumbe wewe ni muuwaji Joesan. Hata kufa Father D.A Joesan, bali utakufa wewe na utakufa kifo walichokufa wazazi wangu kunguni wa miaka arobaini wewe" aliwaza Roi, moyoni alikuwa akilia na moyo wake ukimwaga machozi ya moto yaliyokuwa yakimuunguza lakini usoni alikuwa akitabasamu, tabasamu ambalo Joesan aliliona kama linamtukuza na kumpa sifa ya umungu.

    "kwangu mimi huyo D.A hatachukua hata masaa sabini na mbili, atakuwa mikononi ...................

    mwangu akiwa tayari ni mfu" alisema Roi akiwa na ujumbe moyoni mwake uliokuwa ukisema 'msumeno safari hii unarudi nyuma na kuitenda haki' kisha akatabasamu tena. Joesan akamwambia huyo kijana kuwa kesho asubuhi awahi ili apewe mwanga wa kuweza kujua angalau chimbo za huyo D.A. Roi akaitikia na kuomba ruhusa ya kwenda kupumzika. Akaruhusiwa na kunyanyuka mahali hapo. Alikuwa na hasira, na laiti kama moyo wake ungekuwa ni mfuko wa nailoni, kwa muda huo ungekuwa umeshatoboka kwa jinsi hasira dhiri ya Joesan zilivyowamba moyoni mwake. Akatoka humo ndani na kuelekea kwenye korido ya kumtoa nje. Akiwa katikati ya ile korido, akasikia sauti zikisema nyuma yake, alipogeuka, alikuta ni Suzy na Dokta Emmy. Akampa hai dokta kisha akataka kuondoka.

    "kwani Sex machine anajua?" akasikia swali hilo kutoka kwa Emmy likiwa limemlenga Suzy. Suzy akajibu kuwa SM hajui kitu kwani hata Boss mwenyewe pia hajui. Suzy alipojibu hivyo, Emmy akamsogelea kijana huyo na kumwambia kuwa mzee Rafael amepoteza maisha asubuhi ya kuamkia siku hiyo. Roi habari hizo zilimshtua sana, alishtuka kupita kawaida.

    "jana usiku nilikuwa nae leo niambiwe amefariki?" alijiuliza na kuamua kuuliza kabisa.

    "jana si tulikuwa tunacheka nae vipi leo.....na nini sababu ya kifo chake?"

    "Mkuu ndiyo amemuangamiza kwa sababu alikuwa hamuelewi nyendo zake muda kidogo, alikuwa mkimya na hata mazoezi ya kuwafundisha vijana alipunguza, alikuwa ni mtu wa mawazo mengi kila wakati sasa hali hiyo ilikuwa ikimpa maswali mengi sana mkuu" aliongea Emmy. Roi akang'ata meno kwa siri sana kisha akageuka na kutaka kuondoka Suzy akamwambia kuwa atamfuata nyumbani kwa ajili ya kufanya mapenzi na yuko tayari kwa mambo yote hata kama atakuwa peke yake. Kabla hajajibu chochote, Merina aliwapita hapo bila kuongea neno na kwenda mahali zilipo ngazi za kupanda juu ya flow nyingine. Roi akamtazama kwa macho ya muda kidogo, akajua Merina hakuwa binadamu wa kawaida tena kama siyo mnyama ni roboti. Hakuwa akicheka hata mara moja. Akaondoka hapo bila kuonngea kitu hadi kwenye maegesho ya magari.



    KIFO CHA MZEE RAFAEL.



    Asubuhi ya siku hiyo, Rafa kama kawaida yake alikuwa akitoka kutanya mazoezi ikiwa ni kama dozi kwenye maisha yake, alipoingia ndani, aliekea moja kwa moja jikoninkwa ajili ya kujiandalia kifungua kinywa. Aliandaa kwa utulivu na utaratibu mkubwa kisha akarudi mezani kwa ajili ya kuujaza mwili kwa kifungua kinywa hicho. Akiwa anazidi kujiburudisha kwa chai ya rangi na supu ya kuku, mlango ukafunguliwa bila ya yeye mwenyewe kujua. Akashukia kitu cha baridi kikiwa kisogoni kwake.

    "msaliti wa kampuni" yalikuwa ni maneno machache tu aliyoambiwa kwa majira hayo. Rafa hakugeuka wala kutetereka, alikuwa ametulia kimya huku akikirudisha kikombe mezani kutokea kinywani mwake. Akashusha pumzi nzito na kusema.

    "kwa mnavyodhani nyinyi ni sawa."

    "ni nani basi uliyekuwa ukimmwagia siri za kampuni labda unaweza kuokoka na kifo"

    "mmeshaamua kuniuwa, sidhani kama mtu mzima kama mimi nitakuwa namwaga siri kipumbavu" alisema fadha kisha kimya akapiga.

    "ulipunguza mazoezi kwa vijana wa kazi, ulikuwa ukijitenga sana na wafanyakazi wenzako na pia ulikuwa ni mtu wa mawazo kila wakati. Bado utanidanganya tu kuwa wewe si msaliti?" alisema mvamizi huyo.

    "hahaha hahaha, aahahaha haaa! Merina, wewe ni jasusi na kibaraka wa Lee najua"

    "sheet! Yote hayo unayajua? Haki nimegundua kuwa wewe ni spy sasa. Kufa na uende kwa amani" aliongea Metina na kuitoa usalama silaha yake.

    "mnasema nimetoa siri, kifo changu ndiyo kitafanya siri nilizozitoa zirudi mikononi mwenu au zitazigeuza kuwa uongo?"

    "haijalishi lakini ninaimani ukifa hakuna siri itakayokuwa uchi tena na tutafanya yetu kwa uhuru zaidi." aliongea tena Merina, hapo hapo akairuhusu risasi ipige kwenye mfupa wa shingo ulioungana na uti wa mgongo. Rafael akadondoka chini na kupoteza maisha huku akiwa anaamani moyoni mwake kwani alijua muda wowote Tanzania inakuwa salama.



    "ahadi ya father haikutimia kwa mzee Rafael, amekufa akiwa anakaribia kuwa huru na maisha yake." alikuwa akiwaza Roi kisha akapandisha vioo vya gari yake kisha akageuka kiaina kutazama juu ya jingo la kampuni ile. akamuona Merina akiwa amesimama juu ya lile jingo akiwa anaongea na simu.

    " huyu binti ameanza kunifuatilia, tayari ameanza kunitilia mashaka, pumbavu zake." aliongea kwa sauti ndogo kijana huyo na kutoa simu yake mfukoni huku gari ikiingia barabarani.

    "Cat wasiliana na Father mwambie Mzee Rafa ameuwawa baada ya kuwa wakimtilia mashaka muda mrefu na pia kwa sasa kuna dalili za kuwa wamenza kunitilia mashaka na mimi pia. Tukutane Kilakala muda huu" alimaliza kuongea na kuiweka simu kwenye mfuko wa shati. Akiburuza gari kwa kasi kubwa sana.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    DAKIKA TANO NYUMA



    "nadhani huyu mzee ndiye aliyekuwa akifanya hali ya hewa kutoilewa ndani ya kampuni yangu. Kifo chake kinaweza kubadilisha hii hali. Asante sana Shetani wa kike kwa kuweza kufanya hayo mauwaji." alikuwa ni mr. Kim akiwa pembeni ya Merina huku mzee huyo akiwa haonekani sura. Aamma! Inamaana kumbe Merina anamjua huyo mzee kwa sura kabisa. Tena Merina akiwa anajulikana kwa jina la Shetani wa kike? Mpya hii. Kama uliukuwa hujui basi, hiki ndicho kifaa cha kazi kilichoandaliwa na mr. Kim. mzee wa kikorea asiyeeleweka yeye na mipango yake. Hakuwa ni mzee wa mchezo mchezo kabisa. Merina ni moto wa kuotea mbali huo na usiombe ukakuwakia, ni moto ambao Kim alitoa ufundi wake wote katika kumfundisha yaani huyo ndiye aliyekuwa jicho pekee la babu huyo.

    "hata nyendo za SM sizielewi kabisa kwa sasa. Nilikuwa namchombeza ili nifanye naye ngono lakini alinikatalia kwa kigezo cha kuogopa kuwa eti, mimi ni mali ya boss. Huyu hajui kuwa sisi tunamjua na hakuwa mtu wa hivyo, alitengenezwa ili afanye ngono hata na mama yake mzazi au baba yake, lakini cha ajabu eti, anakataa mali ya bosi?" aliongea Shetani wa kike Merina. Mkuu akahema kwa nguvu na kumwambia kuwa s

    aanze kumchunguza taratibu. Merina akaondoka. Kwahiyo hata pale juu alipokuwa anamtazama, ulikuwa ndiyo mwanzo wa kuanza kumchunguza.



    KILAKALA



    "kiongozi, D.A amehuzunika sana na si kuhuzunika pekee, father amelia kabisa kiongozi. Amesema kazi ianze leo usiku anataka lifikapo jua la kesho kutwa kuwe hakuna kiumbe kilichobakia." Alisema Jay. Mara muda huo huo Catherine akaingia na kumpiga busu Roi na kukaa.

    "nadhani sasa hakuna cha kuchelewa tunawaumiza kwanza...!" alisema Roi lakini alipokuwa aksema hayo, simu ya Catherine ikaita. Wote wakakaa kimya kuisikiliza simu hiyo.

    "niambia Amiri nini kimejiri kwenye watoto wangu niliowatotoa kwenye kampuni yao?" aliongea Cat baada ya kuipa uhai simu hiyo.

    "wameita kikao cha wafanya kazi wote lakini Sex machine hayupo, hiyo inamaana kuwa tayari kazi imeanza" aliongea Amiri na sauti yake ikasikika na kila mtu mahali hapo kupitka spika ya nje ya simu hiyo.

    "kilikuwa kinahusu nini hicho kikao?"

    "Tai kijana mshenzi wa kiingereza, ametoa mtambo fulani mdogo sana, mtambo huo unatoa mionzi hatari na mionzi hiyo inasafiri kwa nguvu ya umeme yaaani system yake imeundwa kitaalamu sana, inatembea na umeme hivyo inamaana kuwa mtambo huo ukiwashwa na kuruhusiwa mionzi hiyo isambaye kwa kutumia nyaya za umeme zilizosambazwa tanzania nzima, niwazi watanzania wengi wanakwenda kuathirika. Hebu fikirieni ni sehemu gani ya Tanzania kwa sasa haijapitiwa na umeme. Na mionzi hiyo inaathiri ubongo moja kwa moja na kuleta mtindio wa ubongo. Mionzi hiyo itakoporuhusiwa inamaana kuwa wote wanaotumia umeme majumbani mwao, ndiyo watakaokuwa waathirika wa kwanza kisha sumu hiyo kuzagaa mitaani. Tanzania inakwenda kuangamia kupita huo mtambo." alikomea hapo Amiri. Watu wakapumua kwa nguvu sana. Hakuna aliyeamini kitu kama hicho kingefanywa na mgeni lakini huku watanzania wakiwemo ndani yake. Joesan amekuwa mjinga kiasi gani.

    "tupe information inzima Amiri" aliongea Cat.

    "hakuna binaadamu mwingine anayeweza kuuendesha huo mtambo zaidi ya huyo Tai. Kwa maana hiyo Tai akifa hakuna mwingine atakayeweza kuunyanyua na kuupa uhai. Mnatakiwa kumuuwa Tai leo kwani hawtabiriki kuanzia sasa. wameshaandaa ndege za kuwaondoa hapo nchini. Kumbukeni tu kuwa mtambo huo ukiwashwa hakuna atakayeweza kuu contral tena." alimaliza Amiri na kukata mawasiliano. wakachoka. Roi akasimama kama kiongozi na kuwapangia majukumu mapya ya usiku huo.

    "Tai atakufa kwa mikono yangu isiku wa leo ila Jay hakikisha Dokta Emmy anakufa kwani hawa ndiyo kikwazo kikubwa kwetu, wakiondoka hao hata kazi itakuwa nyepesi" alimaliza kuongea huku akimwambia Cat kuwa yeye atakuwa hapo kwa ajili ya lolote litakalotokea. Wakakubaliana.



    Saa 22:30. Usiku. Roi anazama ndani ya nyumba ndogo tulivu kabisa ambayo inapatikana ..

     inapatikana maeneo ya hapo mjini, mtaa wa Boma Road. Alizama taratibu ndani kwa uangalivu mkubwa. Nyumba ilikuwa kimya kiasi cha kudhani labda hakukuwa na kiumbe anayeishi humo ndani. Akaona taa zinawaka sebuleni, akasogea hadi kwenye kona ya kuingia kwenye sebule hiyo. Alipotokea hapo, alimuona mzungu huyo ambaye alikuwa ameinamia Kompyuta kubwa sana, akiwa anabonyeza kitufe hiki na kuacha kile. Akamrushia sindano kwenye meza ambayo ilitoa kelele ndogo ya kushtua baada ya sindano hiyo kuangukia kwenye meza hiyo. Alishtuka huyo mzungu na kuangalia mbele ambako alikumbwa na mshtuko mkubwa baada ya kumuona kijana huyo akiwa amekaa kwenye kochi bila hata presha yoyote ile.

    "Sex mac......!"

    "my name is Roi, don't call me Chriss or Sex machine" alionge kwa utulivu mkubwa bila hata kumtazama mzungu huyo.

    "ooooh! Mungu wangu kumbe ni kweli umekuwa mtu, sasa kwanini umekuja huku kwangu jamani si uonevu huo" alipiga kelele mzungu huyo. Alikuwa ni muoga sana.

    "kwani watu si ndiyo wanatembeleana, nimeona tu nikutembelee my friend au hupendi?" aliuliza Roi.

    "ndiyo usiku hivi? hapa....nna...wewe hukuja kirafiki, si kweli hukuja kirafiki eeeenh!?" mzungu huyo aliuliza vitu vya kijinga sana, alikuwa amechanganyikiwa waziwazi. Alikuwa akiujua mziki wa kijana huyo, sasa unafikiri angekuwa na amani mahali hapo?

    "usipige kelele utawafanya watu wajenge wasiwasi tulia tu" alisema Roi.

    "haaa! angalia sasa ulivyo muongeaji mzuri hivyo, Sex machine niliyemtengeneza mimi wala hakuwa muongeaji alikuwa akifuata tu kila atakachoelekezwa" alizidi kujichanganya mzungu huyo.

    "kumbe wewe ndiyo ulinitengeza na kuniharibu akili?" aliuliza Roi huku akisimama taratibu. Mzungu huyo akaogopa na kuanza kujipapasa. Kosa alilolifanya hapo huyo mzungu ni kusogeza kitu kama simu. Alichelewa. Roi aliruka na kumvamia kwa mateke mawili ya nguvu yaliyomtoa huyo mzungu mahali hapo na kupigizwa ukutani. Alikema kwa mayowe ya maumivu kisha mzungu huyo, alisimama ghafla na kutaka kukimbilia swichi moja iliyopo ukutani hapo ili azime taa aweze kutoweka, Kosa. Kisu kilirushwa kwa nguvu na kwa ustadi mkubwa na kumchoma kwenye kitanga chake cha mkono ukelele wa uchungu ukamtoka.

    "huwezi kunikimbia hata kidogo na najua kuwa nyumba yako kila kona ina vitu vya kujihami kwa sababu ya woga ulionao. Kwanini unafanya kazi na maharamia halafu unakuwa mwoga?" aiuliza Roi huku akiwa amesimama pale pale alipokuwa mwanzo. Kijana huyo alikuwa akilia kwa maumivu na uchungu mkubwa. Lakini hakutaka kufa kizembe bila kutoa taarifa kwa wakubwa wake au kukimbia mahali hapo. Alikamata stuli moja iliyopo hapo ndani, akamrushia Roi. Roi akaisukumia pembeni ile stuli halafu akabaki anamtazama huyo jamaa kwa dharau na udadisi wa hali ya juu. Akainama akiwa na lengo la kubonyeza kifaa kimoja kilichopo chini ya kochi. Nalo likawa kosa. Teke zito lilipiga kwenye paji la uso na kwa vile alikuwa ameinama, alibinuliwa huku akipaa hewani hadi anafika chini baada ya kutoka huko juu alikokuwa amerushwa, alikuwa na akili sio zake, pigo lile lilimvuruga kabisa akili. Roi akachomoa bastola na kumpiga nayo ya kifua bila bastola hiyo kutoa sauti yoyote. Muda mfupi tu Tai alijitupa chini akiwa marehemu. Na muda huo huo, Roi akapokea simu kutoka kwa Catherine. alipopokea simu hiyo. Akaambiwa kuwa haraka sana iwezekanavyo awahi nyumbani kwa Dokta kwani Jay yupo katika hali mbaya baada ya kuvamiawa na mtu mwingiene aliyevaa kinyago usoni. Roi hakupoteza muda, alikurupuka na kuparamia pikipiki na kuelekea mahali nyumba ya Dokta Emmy ilipo. HATARI.



    *******CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Jay hakuwa mwenyeji wa mji wa Morogoro hivyo alipokuwa anakwenda kwa kwa dokta Emmy kwa kuelekezwa njia za kupita hadi kufika mahali ambapo dokta Emmy anaishi. Alipofika mahali hapo, alikuta mlango umefungwa. Mmiliki wa nyumba hiyo alikuwa amelala tayari. Jay alichokifanya ni kupita njia za kitaalamu azijuazo yeye mwenyewe hadi akafanikiwa kupita sebuleni ambako alipokelewa na giza kali. Akaanza kuingia kila chumba kumtafuta mmiliki wa nyumba hiyo ambaye ndiyo kwanza alikuwa akibingilia kitandani kwa muda huo. Chumba ambachi dokta huyo alikuwa wmelala, taa ilikuwa bado inawaka japo ilikuwa ni kwa mwanga mdogo sana. Jay alifika kwenye mlango wa chumba hicho na kukamata kitasa cha mlango huo. Alipokinyonga, mlango huo ukaitikia lalini ndani Emmy alikuwa tayari ameshaona jinsi kitasa chake cha mlango, kinavyo tikisika. Emmy alikuwa ni mwoga sana hivyo mara nyingi huwa kuna vitu anaviweka ili kuwa kama ulinzi kwake. Mlango ule ulipokuwa unanyongwa kitasa chake, Emmy alishtuka sana baada ya kushtuliwa huko na mitego yake midogo aliyoitega. Alichokifanya dokta Emmy ni kutoa taarifa haraka sana kwa kubonyeza kifaa fulani kidogo sana mfano wa simu ya Nokia torch kisha akawa ametulia pale pale kitandani akisubiri kumuona huyo mvamizi. Jay alizama ndani na alipoingia tu ndani humo, hakuwa na muda wa kupoteza. Alimnyooshea bastola binti huyo ili kutaka kumuua. Ghafla Emmy akakurupuka na kujifanya ndiyo anaamka kutoka usingizini. Kitendo hicho kikamfanya Jay kushtuka kidogo na kupoteza dhamira yake. Teke moja kutoka kwa Emmy, lililopigwa kwa ufundi mkubwa sana baada ya dokta huyo kujifyatu kiubavu ubavu, iliirusha mbali bastola ya Jay. Jay hakutaka tena kuchelewa, alimvamia dada huyo na kumpa makonde ya nguvu hadi akamdondosha chini. Wakati Jay akiwa anamfuata mtu huyo ili kumuadabisha, ndipo mlango ulipofunguliwa kwa nguvu nyingi kisha Jay kujikuta akipokea kichapo mfululizo kutoka kwa mtu aliyevamia hapo ambaye hakumfahamu kutokana na mtu huyo kuvaa kinyago usoni. Jay alisimama kwa shida sana ili kujaribu tena bahati yake mbele ya mtu huyo. Mvua ya kichapo ikamnyeshea tena. alipigwa kwa ufundi mkubwa na kila mahali ambapo pigo lilitua kwenye mwili wa kijana huyo, lilikuwa likiacha madhara makubwa mno. Jay alivunjwa vunjwa vibaya sana. Hapo ndipo Cat aliona kupitia vifaa maalumu waliokuwa wamefungiwa watu hao. Kifaa hicho kilikuwa mfano wa camera ndogo lakini hii huwa haipigi picha wala kutuma picha bali hurusha taarifa tu, mara baada ya muhusika kukumbwa na matatizo. Amiri pekee aliyeko Uganda ndiye aliyeona jinsi Jay alivyokuwa akipigana na mtu asiye daraja lake na alikuwa tayari amepata madhara makubwa kwenye mwili wake. Amiri aliliona hilo kwa kuvamia kamera za ulinzi ambazo zikitegwa kwenye chumba cha dokta Emmy. Hapo ndipo alipotoa taarifa kwa Catherine kisha Catherine kuzirusha taarifa hizo moja kwa moja kwa Roi.

    "hutafanikiwa ulilolipanga mwanaume, utakufa wewe kisha mtakufa wote kwa pamoja. Utamwambia bwana wako aliyekutuma kuwa umekutana na Shetani wa kike" alibwata mwanamke huyo kwa kiburi kizito. Kumbe hakuwa mwingine mwanamke huyo alikuwa ni Merina. Aliposema hivyo binti huyo, alimsogelea Jay na kumpiga pigo baya sana la kifuani lililopelekea kijana huyo kutapika damu. Jay akadondoka chini akiwa marehemu tayari. Merina kabla haja mgeukiukia Emmy pale chini, uvamizi mwingine wa nguvu ukaibuka mule ndani na mlago kubaki wazi. Roi alikuwa amechelewa sana, alikuta tayari Jay ameshapoteza maisha. Kitendo cha yeye kuvamia mahali hapo kilimpa hofu Merina kwa kiasi kikubwa sana ni kweli alikuwa mpambanaji mzuri na hatari lakini bado alikuwa akimjengea hofu sana Roi ambaye yeye alimfahamu kama SM.

    "ooh! SM umebadilishwa akili kumbe tayari?" aliuliza binti huyo akiwa kama anayejiweka mkao mzuri wa kimapambano lakini si hivyo, hapo alikuwa yupo katika mahesabu makali.

    "jina hilo la SM kamuite baba yako kuanzia sasa silo jina langu hilo. Call me Roi." alijibu Roi na kujiandaa kwa ajili ya kumuadabisha huyo mrembo lakini kumbe mrembo huyo alikuwa tayari ameshapiga mahesabu makubwa sana ya kuweza kutoroka mahali hapo. Hakuona haja ya kupambana na mtu huyo kwa wakati huo. Merina alikuja kwa mtindo wa kama anadansi kisha akaruka, akadanda ukutani na kjizunguu akiulenga mlango uliokuwa wazi. Roi aligundua kuwa binti huyo analenga kukimbia, Merina akiwa tayari ameshajaa kwenye ule mlango. Alimsindikiza na pigo zito la kwenye mbavu hadi binti huyo akatoa mguno wa maumivu. Alidondokea kwenye korido akaamka kwa kasi kubwa kisha akachoropokea nje huku akiwa anakimbia kwa kuinamia upande mmoja kutokana na pigo alilopigwa mbavuni, akatoweka. Roi alichokifanya ni kummalizia Emmy japo mwanamke huyo aliomba msamaha kwa kijana huyo lakini haikufaa kitu, aliuwawa. Roi alimsogelea kijana wake na alitoa chozi la uchungu sana. Ni kwa muda mfupi wameishi pamoja lakini walikuwa wakishilikiana kwa nguvu moja na upendo wa hali ya juu mno.

    "Mungu aihifadhi roho yako mahali pema peponi Jay, tulikupenda sana na mungu amekuhitaji, umekufa ukiwa na nia ya kuliokoa Taifa na pia kunisaidia mimi kulipa kisasi. Damu yako italipwa hata kama si hivi karibuni." aliongea Roi sambamba na kufuta machozi kisha akaokota bastola na kutoweka maeneo yale kwa tahadhari sana.



    Ilikuwa ni siku ya huzuni, siku ambayo pande zote mbili ziliumia. Mr. Lee Kim, aliondokewa na viungo muhimu sana kwenye kazi yake huku D.A akipoteza kifaa kimoja cha kazi. Amiri, Chars na Zomba, walilia kupita kawaida. Hawakuamini kama kijana mwenzao angekufa mapema kiasi hicho. Zomba ndiyo alilia zaidi, kijana ambaye walikuwa wakicheza karata tatu pamoja huku wenyewe wakisema kuwa wanacheza kamari, walikuwa wanatengeza na kubuni vifaa mbalimbali pamoja wakiwa wote. Anakuwa mwenyewe sasa. Kilio kilikuwa ni kikubwa mno.

    "father tunaomba ruhusa yako tukatie nguvu huko Tanzania ili hadi kesho tuwe tumewasambaratisha." alisema Zomba ambaye alikuwa tayari amevaa nguo za kazi kwa ajili ya safari hiyo muda wowote. Vijana wenzake wote nao wakatoka vyumbani mwao na kusimama mbele wakiwa wanamuunga mkono Zomba. D.A aliwatazama kisha akasema.

    "najua ni jinsi gani mlivyokumbwa na ghadhabu juu ya kifo cha ndugu yenu. Lakini mkumbuke kuwa huko wapo watu ambao tunawaamini sana. Wasaidieni mkiwa hapa. Kwani wamesha sema kuwa kesho ndiyo kilele na ndipo itakapojulikana mbivu ma mbichi. ....................



    "father tunaomba ruhusa yako tukatie nguvu huko Tanzania ili hadi kesho tuwe tumewasambaratisha." alisema Zomba ambaye alikuwa tayari amevaa nguo za kazi kwa ajili ya safari hiyo muda wowote. Vijana wenzake wote nao wakatoka vyumbani mwao na kusimama mbele wakiwa wanamuunga mkono Zomba. D.A aliwatazama kisha akasema.

    "najua ni jinsi gani mlivyokumbwa na ghadhabu juu ya kifo cha ndugu yenu. Lakini mkumbuke kuwa huko wapo watu ambao tunawaamini sana. Wasaidieni mkiwa hapa. Kwani wamesha sema kuwa kesho ndiyo kilele na ndipo itakapojulikana mbivu ma mbichi. Lakini kwa hiki kilichotokea hapa Roi anaweza hata kuwavamia usiku wa leo" aliongea father. Vijana hao hawakuwa watu wa kumpinga father tangu anakuwa nao wakiwa bado ni vijana wadogo. Pia waliyaamini maneno yake kwa kiasi kikubwa sana. Wakaonelea ni bora kufanya kama father alivyosema. Japo walikuwa na ghadhabu sana. Walirudi vyumbani mwao na kubadili nguo kisha wakarudi kwenye nafasi zao za kazi huku wakiahidiwa kuwa kesho jioni ni lazima mambo yatakuwa shwari na wanaweza kurudi Tanzani.

    "father kazi inatisha fadher, hawa jamaa wako kikaoni kwa sasa ndani ya kampuni na wanampango mbaya sana" aliongea Amiri akiwa anashangaa sana baada ya kukaa kwenye kompyuta yake kubwa ya kazi.

    "wasiliana na Cat na umwambie kila unachokiona" aliongea father huku akinyanyuka na kuingia chumbani kwake kwenda kufuatilia hayo yaliyokuwa yakiongelewa hapo na wote walikuwa wanashuhudia hayo kupitia kamera ndogo za siri ambazo aliwahi kuzitega Cat siku moja usiku alipoivamia kampuni ile. Kila mmoja hapo akawa na harakati zake.



    "Wanajaribu kutuchanganya zaidi sasa basi cha kufanya ni kuwaonesha kuwa sisi siyo watu wa mchezo hata kidogo." iliunguruma sauti ya mkuu, alikuwa bado hataki kuonekana hata kidogo lakini wakati anaongea hayo, alikuwa hapo hapo ndani ya kampuni.

    "mimi" akendelea.

    "kesho nitauwasha huo mtambo hata kama sijui ni jinsi gani unawashwa lakini nitauwasha tu ili nchi hii waone kile kitawatokea. Nitahakikisha nauwa watanzania wote kiakili pumbavu zao. Joesan, hakikisha muda huu nitakapomaliza kuongea haya, ita vijana na waingie mtaani, wakabidhi silaha na wahakikishe wanafanya mauwaji kwa kila watakeyekutana naye njiani. Hii itafanya polisi kujaa mitaani lakini pia kuwavuta maadui zetu karibu. Wao wanazuia sisi tunaharibu hivyo ni lazima waende mtaani kuzuia hili huku sisi tunafanya kitu kitakachokwenda kuiharibu Tanzania kwa ujumla." alimaliza kuongea Kim lakini Joesan alikuwa ni kama amepigwa na butwaa, alikuwa akishangaa na kujiuliza, yaani vijana niwaamrishe wakauwe kila watakauekutana naye mtaani! alikuwa akijiuliza namna hiyo Joesan. Moyo wake ulikuwa kama unasita kufanya kitu hicho, nguvu ya kufanya aliona kama inamsaliti huku moyo ukimwambia 'yaani uko tayari kuteketeza ndugu zako kwa amri ya huyo mkorea ambaye anauwezo wa kukimbilia kwao? Kumbuka hata kama utaweza kukimbia ndani ya nchi hii na kwenda kujificha kwenye nchi nyingine, bado utakuwa mtumwa si huru tena. Uhuru mzuri ni ule wa nyum.....!!"

    "unashangaa nini wewe, hujui nimekuagiza nini. Hawa watanzania wamesha kusaliti na hata kama utatoka na kwenda kanisanani kuungama dhambi zako hadi kanisa litakuhama wewe na utabaki peke yako ukichomwa na jua." sauti hiyo aliyokuwa akiisikia Joesan, ilikatishwa, tena alikuwa akifoka Kim mahali hapo. Joesan akashtuka na kujikuta akijitafuna. Kim akazidi kubwata.

    "huna unachopoteza kwa sasa utauwa watanzania wote na wewe utakwenda nchi yoyote duniani kula raha" Joesana akajua kweli ni bora auwe ili akaishi mbali kwa furaha. Akatoka hapo na kwenda kwenye kempu la vijana wa kazi kwenda kuwapa amri kisha kuwakabidhi silaha. Huku nyuma Kim alizidi kutoa maelekezo.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "house no. 05, ina silaha za maangamizi hizi ni siha zenye sumu kali sana hivyo mimi nitakapo maliza kuuwasha huu mtambo hapo kesho, nitaelekea 05 kwenda kuilipua ile nyumba na kisha tunaondoka hapa nchini kabla sumu ile haijasambaa. Sumu hiyo ni hatari sana, ni zaidi ya dilaha za Nyuklia na itaharibu kabisa watu wote wa hapa morogoro. Haitanuacha mtu hai hata kidogo. Moshi wake ukisambaa tu hewani basi hakuna mtu atakayebaki maana kila atakayeivuta hiyo hewa ni kifo, ni zaidi ya Carbon monoksaid hiyo hewa." alizidi kuongea mzee huyo. Alishindwa kuipa jina zuri sumu hiyo ambayo haikuerza kushindanishwa na vitu vyote vya hatari avijuavyo yeye. Muda huo akamwambia Merina kuwa asiwe mbali na yeye kwani ndiye anayemtegemea zaidi. Suzane na wafanya kazi wengine wao wakawa na kazi ya kuhakikisha ulinzi wa hiyo kampuni. Wakati wakiwa hapo. Huko mtaani hali ilishaanza kuwa tete. Vijana walikuwa wanauwa kweli, kuanzia masika kuja mjini huku wengine wakichukua uelekeo wa kwemda kituo kikuu cha magari Msamu, wengine wakiwa wanaelekea maeneo mbalimbali ya mji huo. Zilikuwa ni risasi za sumu pekee ndizo zilizokuwa zikitumika hapo. watu walichanganyikiwa kweli. Raia walikufa kwa wingi sana huku waliobahatika kupona wakiukimbia mji huo. Roi na Cat, walikuwa wameshapewa habari zote na kila mpango uliokuwa ukipangwa ndani ya kampuni ile. Roi alifikiri kwa muda na kumwambia Cat akimbilie Kilakala kwa ajili ya kupanga nini cha kufanya kwani tukio hilo lilikuwa ghafla sana na lilikuwa ni mtego. Baada ya kumpa maelezo hayo, Cat alipanda gari na kuelekea kilakala kisha yeye akakimbilia kule ambako alikuwa akiishi wakati akiwa ni Sex machine, kwenye ule mjego ambao alikuwa amepewa na kampuni. Hapo alikuwa na zana za kutisha na alifanya hivyo kwa makusudi kwani alijua fika kuwa nyumba ile itakuwa imewekwa kamera za siri ambazo zilikuwa zikimfuatilia. Aliamini akiwa kule ni lazima watamuona kuwa anakimbilia kule. Hapo alijua ni lazima wale vijana wanaouwa mtaani watapunguzwa kwa wingi na wengine kuletwa kule alikokimbilia yeye kwa ajili ya kumuuwa. Wakati Roi anatoka hapo kwenye nyumba yake ya mjini ambayo alikuwa ameinunua pamoja na Sauda, akiwa anapanda Pikipiki tu, Sauda kumbe naye alikuwa akija maeneo hayo baada ya kumkosa mpenzi wake huyo kwa muda mrefu. Hivyo wakati huo anapanda pikipiki na kuondoka, Sauda aliita sana lakini Roi hakusikia kutokana na kuchanganyikiwa. Hali ile ya taharuki iliyolivamia jiji ilikikuwa bado haijafika maeneo hayo. Hivyo Sauda akaona kama kijana huyo anamkimbia, hivyo akapanga kumfuatilia. Alikuwa yupo ndani ya gari yake Noah. Akaiongeza kasi gari yake hiyo na kuanza kumfukuzia kwa nyuma. Roi alikimbiza pikipiki lake kwa kasi kubwa hadi anafika mahali nyumba ilipo na kuzama ndani.



    Wakati Roi anafika ndani ya nyumba ile huku kwenye kampuni walimuona kweli kupitia kamera za siri ambazo zilitegwa mule ndani. Kundi kubwa la vijana wauwaji waliomwagwa mtaani wakaambiwa waache kuuwa na waelekee kwenye nyumba aliyokuwa akiishi Sex machine na wakaiteketeze nyumba ile Sex machine akiwa ndani. Kundi hilo likaingia kwenye mitaa hii na ile hadi wakatoke kwenye nyumba hiyo ambayo walikuwa wanaiona kwa mbali. Wakati wanazidi kuja, Sauda akawaona watu wale jinsi wanavyotisha huku wakiwa wamebeba silaha za hatari. Walikuwa wengi sana kiasi cha kutokutazamika.

    "lile ni jeshi?.....ah!, ah!, lile siyo jeshi.....Jeshi gani halina sare maalumu. Hebu nnifikirie kama niliwahi kuona jeshi ambalo linafanyaga mazoezi au maandamano likiwa vifua wazi?.....Mbona sijawahi kuona na hata sikumbuki......labda jeshi la mazombi?" alikuwa akijiuliza sijui kujiswalika maswali sijui nini, maana alikuwa hata haeleweki Sauda. Akaona ngoja atulie hapo hapo aone kuna nini kinajiri kwa kunfi lile kubwa la viumbe wale wa kutisha ambao alishindwa kuwalinganisha na binadamu. Mdada huyo akaona hapo usalama hakuna. Tena watu wale walikuwa wanazidi kusonga mbele bila kusimama. Akaigeuza gari yake na kupita njia nyingine na kutokea kwenye barabara kubwa. Akaendesha gari kwa kasi huku akipiga simu polisi na kuwaelekeza watu hao walipokuwa wanaelekea. Alilia sana Sauda baada ya kuona kundi la viumbe wale likielekea keenye nyumba ambayo alikuwa ameingia mpenzi wake. Hakutaka kwenda mbali sana, aliegesha gari yake kando ya barabara, sehemu ambayo inautulivu ili kupata kusikia kitakachotokea huko nyuma. Kama siyo milio ya risasi basi ulikuwa ni mlipuko mkubwa sana. Kwani kwa zile silaha alizoziona, alijuwa fika ule ndiyo ulikuwa mwisho wa penzi lake.



    Polisi walikuwa tayari wamemwagwa mtaani wakipambana na watu hao, shughuli ilikiwa pevu mno, hakuna askari polisi hata mmoja aliyelitegemea tukio hilo kwanza lilikuwa ni tukio la ghafla sana kutokea. Wakaamua kugawana, wengine wakaelekea mahali ambako simu hiyo imepigwa na wengine wakibaki mitaani. Polisi walijaribu kuzuia hali hiyo lakini wapi. Watu wale hawakurudi nyuma walizidi kusonga mbele na kuzidi kusababisha mauwaji makubwa ya askari polisi pamoja na raia wao. Wale jamaa walikuwa ni kama wameharibiwa akili. Walikuwa wanalengo la kuuwa tu na si jambo jingine. Miliyo ya risasi ilizidi kurindima ndani ya mji wa Morogoro. mr. Kim alikuwa akicheka kwa furaha kubwa na kujua sasa amefanikiwa.



    "D.A, onesha uwezo wako sasa, zuia ninachokifanya kama unaweza, zuia sasa nione, zuia." alijitapa Kim. Watu walikufa mitaani, walikufa kama uchafu na huku kwenye nyumba tayari askari walikuwa wameshashindwa kuwazuia hao mabwana na walikuwa wameizunguuka nyumba hiyo tayari kuivamia. Askari wengi hapo walikuwa wamepoteza maisha sasa wakawa hadi wanaogopa kushambulia tena wakawa wamebaki kuona nini lengo la watu hao kuizunguuka hiyo nyumba.

    "Catherine unanipata?" aliuliza Roi akiwa amekaa sehemu moja upande wa juu wa ile nyumba akiwa anaangaliana na jingo moja lienye usawa na hiyo nyumba.

    "ndiyo, nakusikia kiongozi, watu wanakufa sana mtaani na polisi wameelemewa tunafanyaje sasa?" alihoji Cat.

    "hatuna jinsi Catherine, hata kama serikali ikitukamata poa lakini huu ndiyo muda wa kutumia zana zetu za kazi, hakuna njia nyingine. Hawa walionizunguuka hapa wote ni marehemu watarajiwa kwani kuna mzinga mkubwa wa bomu huko ndani una fukuta, wakianza kupiga rusasi zao tu wamejiuwa wenyewe. Chukua pisto Bomba three na two, zama nayo mtaani tutakutana huko" alimaliza kuongea Roi kwa kutumia kisafirisha sauti alichokuwa amekibana kwenye fulana yake iliyombana vizuri huku kipokea sauti kikiwa sikioni kisha hapo hapo akakimbia kwa kasi kubwa kule juu kisha akarukia kwenye nyumba ya jirani na kukimbia tena na kurukia upande mwingine. Askari walibaki ................



    Chukua pisto Bomba three na two, zama nayo mtaani tutakutana huko" alimaliza kuongea Roi kwa kutumia kisafirisha sauti alichokuwa amekibana kwenye fulana yake iliyombana vizuri huku kipokea sauti kikiwa sikioni kisha hapo hapo akakimbia kwa kasi kubwa kule juu kisha akarukia kwenye nyumba ya jirani na kukimbia tena na kurukia upande mwingine. Askari walibaki wakishangaa uwezo wa yule mtu kule juu. Hapo wakajua kuwa kundi la watu wale wadioeleweka walikuwa wakimtaka mtu yule. Walitaka kumlenga kwa risasi kwa kudhani ndiye chanzo lakini walichelewa. Wale jamaa waliotumwa kuuwa waliwahi kupiga risasi kwenda mule ndani. Muda huo huo askari wale walishuhudia mlipuko mkubwa sana ambao hata kwenye muvi za kivita hawajawahi kuuona. Walishuhudia wale jamaa wakifa kifo kibaya sana kwa kurushwa hewani na kudondoka chini wakiwa maiti. Wote waliangamia na kubaki wawili tu wakiwa wanachechemea, askari polisi wakawamalizia kwa hasira. Mlipuko ule ukaleta ushindi kiasi fulani kwa polisi lakini ukazalisha kilio kizito kwa Sauda ambaye alikuwa ameigamia usukani wake wa gari. Kwa mlipuko ule mazima aliamini SM wake si hai tena. Alilia pasipo kunyamaza, penzi lilimliza Sau. Mwanaume kama SM alijua hawezi kutokea tena katika maisha yake. Hakutaka hata kidogo kuacha kulia mahali hapo.



    Mtaani nako kulikuwa kumechafuka mwanadada Cat alikuwa kachafukwa na roho. Alikuwa akiwakausha wale wauwaji kama kachanganyikiwa. Pistol Bomba 3 na 2 zilikuwa zikiteuka risasi za Snake Teeth Bullet (STB) kama uchafu. Kila risasi ilikuwa ikiondoka na mtu na nyingine zilikuwa zikiondoka na kundi la watu. Mtoto huyo mzuri alikuwa juu ya pikipiki kubwa kabisa akiwa analiendesha kwa weledi mkubwa huku akizitema hizo sindano za sumu. Roi naye alikuwa mtaani na pikipiki lake akifanya yake. Ndani ya masaa mawili tayari mji ulishaanza kupoa kabisa. Kim alibadilika ghafla badala ya kucheka akawa analia kwa uchungu. Vijana wake walikuwa wakipukutika mtaani kama uwele kwenye jua kali.

    "jamani Roi SM amekufa na sasa tunapambana na mzimu wake. Huyu mtoto kumbe ni laana hivi. Yaani hata sijui amewatokaje wale mashetani wangu na kuwauwa wote kisha eti, arudi na mtaani!" alichanganyikiwa Kim, tena alidata vibaya sana.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "nadhani unayajua majengo ya siri ya huyu Kim my love, hakikisha yote unayatekeza kwa kuyalipua lakini uhakikishe watu wasiokuwa na hatia wanakuwa hai. Bakisha jingo moja tu ambalo ni Happy Club, hilo litabaki kama ushahidi kwetu." aliongea Catherine walipokuwa wamekutana yeye na Roi mara baada ya kuwapukutisha wengi.

    "nimekupata mke wangu, kuwa makini hawajaisha bado na sijui ni nini wanafikiria.......,Nini plani yako baada ya kuwamaliza kabisa hawa?" aliuliza Roi.

    "nikiwafyeka hawa wote hakuna budi kulivamia kampuni ninaimani kwa hali hii Kim hatangoja kesho leo leo anaweza kuwasha huo mtambo"

    "ok, kuwa makini my love nategemea kupata mtoto wa kwanza nawe baada ya kumaliza huu mchezo" alisema Roi kisha Catherine akatabasamu kisha kulipa utani huo.

    "sina mpango wa kuzaa na malaya kama wewe ila ninahamu sana ya kukufaidi baada ya hili gemu kuisha" Roi akacheka kisha akaiondo pikipiki yake kwa kasi kubwa. Roi alihakikisha anaanza Nanenane ambako huko kuna majumba si chini ya matatu ya Mzee huyo na kuyamalizia mengine. Alipofika huko alifanya yake kwa kuuwa kila aliyekuwa mlinzi wa majumba hayo, kisha wale wote ambao walikuwa wafanyakazi wa kawaida, huku wengi wakiwa ni wanawake watoa huduma, wakitolewa nje. Majengo yote yalitiwa moto na kulipuliwa kabisa. watu walishangilia huku wengine wakilia kabisa kwa furaha.

    "mkombozi huyu ametoka wapi jamani" walisikika watu wakisema hivyo. Wale ambao walikuwa ni kama kiburudisho kwa wateja. Mashoga wengi waliotolewa. Lilikuwa ni kundi kubwa la vijana ambao waliharibiwa. Wote hao walikabidhiwa mikononi mwa polisi huku aliyetenda hayo akiwa haonekani.



    Joesan aliona sasa hali ni tete na muda wowote jumba bovu linamuangukia, alichokifanya ni kuchukua gari na kukimbilia kwenye jingo lake la siri lililoko Mazimbu road. Huko kwenye hilo jumba, kumbe hakuwa akifanya mambo yake ya kimawasiliano tu bali alikuwa na chumba kidogo alichokuwa akiifadhi pesa. Kila pesa alizokuwa akiziingiza kwa biashara zake haramu, chache alikuwa akizipeleka benki lakini nyingi, akizihifafhi ndani ya nyumba hiyo. Alikuwa na pesa nyingi kupindukia.



    Sasa wakati akiwa anatoka ndani ya ile kampuni kwa mtindo wa kutoroka, baada ya kumuona hata mkuu wake wa kazi, mtu aliyekuwa akimtegemea, akiwa kachanganyikiwa, na asijue la kufanya, alijua hapo hali si hali. Aliona bora ni kuziwahi pesa zake na kukimbia nchi. Kwa mabaya aliyoyafanya laiti kama serikali itamtia mikononi, hakuna msalie mtume hapo ni kunyongwa hata kama sheria ya kunyongwa imefutwa. Sasa ni heri akutane na mkono wa serikali kuliko kukutana na kijana aliyemnyanyasa na kumuulia wazazi wake. Aliona ni bora kifo cha kunyongwa kina afadhali kuliko hukumu atakayopewa na kijana huyo. Kila wkikifikiria kifo chake kitakavyokuwa alikosa kabisa amani moyoni mwake. Alifika Mazimbu road lakini huku nyuma tayari jicho kali la Amiri mwenye uchungu wa kuuliwa ndugu yake, lilishamuona.

    "kiongozi umeshamaliza kazi ya kuteteketeza hizo nyumba za huyo hayawani?" aliuliza swali Amiri kwa Roi. Jibu likaja kuwa si yote, amebakisha mawili moja akiwa halijui hilo likiwa ni jingo no. 05. Jingine hakuwa na mpango wa kuliteketeza hivyo aliliacha kama ushahidi ambalo ni 03 au Happy Club. Hilo walikubaliana waliache ili liwe ni ushahidi wakati wa kujisalimisha serikalini kwa kufanya uharibifu wa mali nyingi pamoja na rasilimali watu.

    "faster Mazimbu road, nakupa location sasa hivi, Joesan amekimbilia huko nafikiri anampango wa kutoroka." alisema Amiri. Hapo Roi akawa kama anawazimu. Alipopewa tu mueekeo, alikimbiza pikipiki lake kwa kasi ya hatari sana hadi mahali alipoelekezwa. Alipaki pikipiki nje na kuzama ndani kwa makini sana kwani alijua kuwa lolote lingeweza kutokea. Milango yote ilikuwa wazi. Alinyata taratibu hadi alipofika mahali ambako alimkuta Joesan akikusanya pesa na kisha kuzijaza kwenye mabegi.



    *********



    Huku nako Catherine baada ya kuteketeza kundi lote la wale jamaa, hakutaka kujua Roi ameelekea wapi pia hakutaka hata kuwadiliana nae. Moja kwa moja aliondoka hapo alipokueepo akichukua uelekeo wa lilipo jumba la kampuni la SC company. Huko ndani ya kampuni kulikuwa kumeharibika tayari. Kim hakuwa mtu wa kujificha tena aliamua kujitokeza mwenyewe bila kupenda, kila mtu aliyekuwa akimuona akabaki kumshangaa. Huyo ndiye alikuwa mkuu wa hiyo kampuni yenye kuharibu future za watu na kuwaendesha vile wanavyotaka wao wakisha waharibu. Lee Kim alikuwa ni mfupi mwenye mwili usioeleweka kama ni mnene au umevimba, alifanana kabisa na nyoka jamii ya Kifutu au Moma. Alikuwa na weupe uliofifia, nywele fupi zilizoweka uwaraza katikati, sura pana sambamba na macho madogo yaliyojifinya kwa ndani huku yakiwa yamehifadhiwa kwa mawani ya macho. Kim alikuwa na kazi moja tu nayo ni kuhakikisha anawasha ule mtambo ambao ulikuwa na kazi mbaya ya kumwaga mionzi yenye kudhoofisha afya kwa kuziharibu neva pamoja na kushambulia ubongo wa kati. Ni dhahiri kabisa mtambo huo ukiwashwa unakwenda kuharibu watanzania na kuwageuza kuwa mazuz kama siyo wenda wazimu kabisa. Kim alisogea hapo mtamboni na kuutazama lakini muda huo huo akapewa taarifa aliyoichukia na kumchanganya. Ni juu ya kulipuliwa majengo yake yote anayoyategemea.

    "Wanataka kuniangusha chini hawa aaaaghr!!"

    "unadhani labda utafanikiwa D.A. Nakwenda kuuwa akili zenu wajinga nyinyi na mtakufa nawaambia. Mtakufaaaaaa!!" Alifoka Kim na kuanza kubonyeza batani za ule mtambo hovyo hovyo bila kufikiri. Alikuwa akifanya hivyo huku akijivuta nywele zake kwa hasira sambamba na kupiga kelele. Wakati yeye akizidi kufanya hivyo, tayari Cat alikuwa amelivania jingo hilo akiwa anafanya mauwaji ya kimya kimya kwa kila mlinzi anayemsogelea. Kim pamoja na walinzi wa ndani walishamuona dada huyo jinsi anavyokuja na tayari alishawafyeka walinzi wote wa nje hapo alikuwa akipiga hatua za kujiamini kabisa kwa kuzama upande ule walipokuwa wakina Kim.



    Joesan huko ndani nako alikokuwa akikusanya kila kilicho chake kutimka, alihisi hali ya hatari imesha mkaribia. Alijizunguusha haraka sana akiwa na bastola mkononi mwake.

    "na wewe unataka kufa kama walivyokufa wazazi wako?" aliuliza Joesan lakini hakujibiwa kitu. Kila alivyokuwa akiuliza jibu halikuja. Akajua kuwa hapo hakuwa na mtu bali mzimu. Akaitoa usalama bastola yake kisha kuachia risasi iliyompiga Roi tumboni na kumrusha ukutani. Akasema bwana huyo kwa kujiamini.

    "umesau kuwa nilikuahidi kuwa utakufa tena utakufa kwa kifo kitakachosababishwa na mikono yangu? Baba yako na mama yako niliwauwa mimi na kuuteka utajiri wao wote kisha kukulea wewe uje kuwa mateka wangu kama siyo mtumwa utakayenitumikia hadi kifo chako, hawajakwambia hao waliokubadilisha kutoka kwenye kuwa mashine ya ngono hadi ubinadamu tena? Hawakukuambia?" aliongea Joesan huku akiwa anesimama hatua chache kutuka kwa kijana huyo ambaye alikuwa akihisi maumivu makali ya tumbo kwa kupigwa na ile risasi ye nguvu sana. Roi alikuwa akihema kwa tabu sana na kila alipokuwa akijitahidi kusimama, alikutana na pigo zito lililomrudisha hapo chini.

    "mimi ndiye Joesan ambaye sijawa kushindw katika swala la uhitaji wa pesa. Ngoja ufe bila kelele yani unakufa kama Ng'ombe aliyekumbwa na ugonjwa wa kimeta." alizidi kujitapa Joesan. Aliongea maneno ambayo yalimtia hasira na uchungu mkubwa kijana huyo. Alirudishiwa machungu yale aliyoyapata wakati anapewa historia ya vifo vya familia yake. Vazi alilopewa na D.A ambalo lilikuwa na uwezo wa kuzuia risasi zenye nguvu kubwa ambazo ndizo zilikuwa zikitumiwa na Lee Kim, liliweza kuzuia ile risasi japo alihisi maumivu makali sana kutokana na uzito wa msukumo wa risasi ile. Joesan akamwambia ................





    Aliongea maneno ambayo yalimtia hasira na uchungu mkubwa kijana huyo. Alirudishiwa machungu yale aliyoyapata wakati anapewa historia ya vifo vya familia yake. Vazi alilopewa na D.A ambalo lilikuwa na uwezo wa kuzuia risasi zenye nguvu kubwa ambazo ndizo zilikuwa zikitumiwa na Lee Kim, liliweza kuzuia ile risasi japo alihisi maumivu makali sana kutokana na uzito wa msukumo wa risasi ile. Joesan akamwambia kijana huyo ambaye sasa alikuwa anataka kufanya kitu kitakachomuacha hoi bwana huyo, kuwa sasa ndiyo anampiga risasi itakayokwenda kufuta historia yake. Hapo akajishangaa tena alijishangaa kuliko hata mshangao wa kawaida ulivyo. Alishangaa kuona bastola ikimtoka mikononi kama mtoto aliyeponyokwa na Panzi aliyemkamata kwa kumuwinda kwa muda mrefu. Joesan alipiga yowe la uchungu, uchungu wa kutokwa na silaha yake mikononi mwake. Alibaki kushangaa huku akitega mikono kuisubiria ikitoka huko juu ilikoligonga dari, irudi mikononi mwake. Roi akamdaka na kumtupia sebuleni yeye na begi lake la hela ambalo alikuwa amelikamata mkononi.

    "uliweza kuuwa Joesan lakini huwezi kumuuwa mtu aliyekuja kwa kulipa kisasi. Naona kama unakufa wewe sasa Joe." aliongea Roi huku akiwa anapiga hatua za taratibu kumfuata bwana huyo. Joesa n alipapatika pale alipoangukia na kusimama kutaka kukimbia, alichelewa. Alichezea mateke kama manne hivi mfululizo na kujikuta akibwagika tena chini.

    "ulikuwa unataka kukimbia wakati bado hujakamilisha kazi yako." alisema Roi.

    "nimesha maliza kila kitu na ndiyo maana nataka kuondoka hii nchi." alijibu kwa kiburi bwana huyo.

    "bado"CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "bado nini?"

    "bado hujakufa Joesan, lazima ufe kwanza ndiyo uondoke" alisema Roi na kuzidi kumfanya huyo mtu achanganyikiwe. Akamsogelea na kumpa kipigo cha dakika tano, hicho kilikuwa ni kipigo cha kumnyong'onyeza. Joesan alikuwa hoi kwa kipigo hicho mbaya zaidi alikuwa akipigwa mbele ya hela zake mwenye. Mbona hizo hela hazimsaidii sasa. Mbona anapigwa zikiwa zinamuangalia. Roi baada ya kutoa kichapo kile, alimuweka chini na kuanza kumkumbusha yote mabaya aliyoyatenda, alimkumbusha kila kitu kilichopita.

    "wewe ni mtanzania kweli wewe? Wewe ni mtanzania gani uliyekuwa tayari kuwauwa watanzania wenzako. Tazama, ni vijana wangapi leo hii wamekuwa mashoga kwa kuendekeza ujinga. Joesan unakufa leo kama kalenda ya leo inavyo soma. Hivi utakwenda kujibu nini sasa mbele ya mungu. Pesa kwako imekuwa ndiyo ibada, umekuwa humsikilizi mtu wa aina yoyote mbele ya pesa. Umethubutu kunigeuza mashine ya mgono kwa sababu ya tamaa zako. Nimefanya dhambi kubwa sana kwa kuwaingilia watu kinyume na maumbile, nimetenda dhambi ambayo Mungu anazichukia kupita dhambi zote naweza kusena hivyo. Unakumbuka Mungu alichowafanyia wana wa Nuhu wewe? Unakumbuka Mungu alichowafanyia wana wa Sodoma na Gomola nakuuliza. Tena narudia tena kukuuliza kwa mara ya mwisho, hivi unakumbuka Mungu alivyoifanya ile nchi juu ya dhambi ya mapenzi ya kuingiliana kinyume na maumbile? Mbona wewe ulikuwa chanzo cha matendo hayo ukiongozwa na yule mkorea kisa tu pesa. Haya sasa pesa hiyo hapo na nyingine ipo huko ndani, sema nayo basi ikusaidie." alikuwa na uchungu mkubwa sana Roi. Ametendewa mabaya mno, ameumizwa sana, amejikuta anafanya vitu ambavyo vinamchukiza Mungu sababu ya mtu huyo aliyeamini ni ndugu yake, mtu aliyeishi naye kama mjomba wake. Alipiga kelele kubwa sana na kuanza kumpiga Joesan kama anapiga mpira ama ngoma. Alipiga mateke, alipochoka alipiga ngumi kisha akamburuza hadi kwenye mlango wa kutokea nje akiwa na ile bastola ya Joesan ambayo ilimpiga risasi ya tumbo mkononi mwake. Alimbwaga kizingitini kama mzigo. Joesan alikuwa akivuja damu kila kona ya mwili wake hata kama hakuwa na uwezo wa kusema lakini moyoni alikiri kuwa amepigika. Yuko wapi Sembugi? Wako wapi vijana wake aliokuwa akiwatumia kuuwa. Hawakuwepo. Alipigwa peke yake, wale vijana wake wa kazi hawakuwepo na hata kuwakumbuka kuwa alikuwa na vijana wa kazi, alishindwa na hata kama angewakumbuka wangefika hapo kufanya nini. Vijana waliozoea uuwaji wa kawaida wa kimtaani kwa huyo Jasusi wa kimataifa Roi wangethubutu hata kishika viatu vyake. ni wazi hakuwa na msaada. Joesa alikurupuka na kuliangalia begi lake la pesa, hakuliona. Yaani alikuwa ni kama anayetoka usingizini, alipoangalia kule ndani aliliona akaona hata, haweza kufa wakati alikuwa na uwezo wa kutoroka pengine kwa uwezo wa Mungu na zile pesa zikamfikisha mbali. Eti, bado alikuwa na imani ya kutoroka tu hapo alipo. Alisimama ghafla na kuanza kukimbia kuelekea mahali begi lilipo kule ndani. Alikuwa akikimbia huku akichechemea kwa kuuburuza mguu moja kutokana na kipigo alichokula. Mguu ambao ulikuwa umevunjika vibaya sana. Roi hapo ndipo alipoikumbuka historia aliyowahi kupewa na Catherine. Picha ya baba yake alipokuwa akikimbia hivyo kumuwahi mkewe, ilimjia. Ilikuwa ni hivyo hivyo sema utofauti ni kwamba Baba yake alikuwa akimkimbilia mkewe na Joesan alikuwa akizikimbilia pesa zake.



    "acha nilivae koti lako la miaka kadhaa nyuma" alisema kwa sauti ndogo Roi kisha akanyanyua mkono ule uliobeba silaha yake mwenyewe. Silaha ambayo ilitaka kumtoa uhai baada ya kupigwa tumboni kama asingekuwa amezawadiwa lile vazi la kumkinginga na risasi za aina ile na father D.A. Risasi ya kwanza ikamtoaka na kupiga katikati ya uti wa mgongo wa bwana Joesan. Risasi iliyotengua pingili mbili za uti wa mgongo wa bwana yule. Ikiwa ni risasi ambayo pia iliuwa mawasiliano ya baina ya upande wa miguu na kichwani.

    "aaaaaaahhghrr!" alipiga kelele za maumivu makali Joesan huku akiwa ameganda katikati kama Zombi aliyeshushiwa shoka la kichwani. Begi la pesa alikuwa akiliona lile pale lakini kulifikia ndiyo ikawa mtihani. Akajaribu kupiga hatua, hakuweza. Miguu ilikuwa mizito. Risasi ya Star ilikuwa imevunja pingili ya uti wa mgongo kisha kuharibu mawasiliano maxima. Nguvu zote zilimkimbia kitu kilichomsbabishia yeye kushindwa kutembea kwani risasi ile ilikata mawasiliano baina ya vingo vya chini na juu kwa asilimia mia moja na zaidi. Akabaki kugeuka ili kutaka kumuomba kijana huyo msamaha. Ujinga kiasi gani. Unaomba msamaha ukiwa tayati si wa kuishi. Alijidanganya pia kwani sauti haikutoka. Sumu ya Star bullet ilishasambaa mwilini mwake. Risasi tatu za kifua nyingine zikammaliza kabisa mara baada ya kugeuka na kumpeleka chini. Roi alikuwa bado hajaridhika alimsogelea na kumburuza hadi garini na kumtumbukiza humo ndani ya gari yake kisha akalisogeza gari karibu kabisa na nyumba yake kwa lengo la kuiteketeza maiti ya mtu huyo sambamba na hiyo nyumba yake ya mafichoni lakini kabla hajatia moto mara simu ikaita. Hakutaka kuipokea kwanza hadi alipowasha moto. Joesan akafutika katika historia ya dunia yeye na pesa zake.



    Catherin wakati anazidi kuingia mule ndani, vijana wa kumuadabisha walikuwa wameshaandaliwa. walikuwa ni wanaume watatu walioshiba mazoezi na wenye misuli minene. Kim hakuwa na habari na mwadada huyo kwani aliamini hapo yuko na wanawake wawili ambao wako vizuri. Alikuwepo Suzane huku akikuwepo Merina ambaye macho yake yote yalikuwa kwa Kim akiwa anazidi kupambana na mtambo ule ili kuuwasha. Cat alipokanyaga tu hapo, hao jamaa wakaruhusiwa. Kabla hawajamsogelea jamaa wale akacheka kwa sauti kubwa na kusema.

    "kila mlichokuwa mkikifanya humu ndani, kilikuwa kinarushwa kwetu kwa camera hizi ndogo nilizoziweka humu zikiwa kwenye kila kona ya jumba hili." alimaliza kusema hayo huku akitoa kamera moja kwenye picha moja ya kizamani iliyopo ukutani kisha kumpiga nayo ya kichwani Kim pale alipokuwa akikazana kuwasha mtambo.

    "mpuuzi wewe tena mwanaharamu mkubwa, uliwezaje kuingia humu kwenye ulinzi mkali kila kona?" aliuliza Kim kwa hasira baada ya kupigwa na ile kamera kichwani.

    "siku mliodhani umeme umekat......?!"

    "aaaaah!" aling'aka Kim kisha akasema.

    "maliza huyo kahaba nyinyi, mbona mnamuangalia sasa amenitukana sana, mimi ngoja nimalizie kuuwasha huu mtambo niwaangamize." alitoa amri Lee Kim. Mkono ukachezwa baada ya wale jamaa kupokea amri ile kwa mara ya pili. Catherine hakuwa mama wa mchezo, alijua kucheza na mwili wake pia alijua kuwa hakutakiwa kuchukua muda mrefu mahali hapo, kwa jamaa hao kwani wapo wanawake wenzake hao ndiyo aliokuwa akiwahitaji zaidi. Jamaa wale walikuwa wakirusha ngumi huku wakiwa wanapiga kelele za nguvu. Ngumi zote walizokuwa wakirusha zilikuwa zinapiga hewa. Hakutaka kuchelewa Catherine, aliwageuzia kibao watu hao kwa muda mfupi tu. Walipigika jamaa hao kwa muda mfupi sana kisha Catherine akasonga mbele kuzidi kuwafuata wale wadada kabla ya kumstopisha Kim asiendelee na ushenzi wake. Suzane akasogea mbele kwa ajili ya kazi ya kupambana na Cat lakini Merina akamstopisha na kumwambia Suzy kuwa ni muda wa kuuwa na kupotea kwenye hii ardhi ya Tanzania hivyo huyo kinyago atamuadabisha yeye.



    Wakati Shetani wa kike anamsogelea Cat taratibu, ndipo huko Nairobi father akaona lile tukio. Akamwambia Amiri haraka iwezekanavyo, Roi anatakiwa awepo hapo. Ndipo kijana huyo akapigiwa simu na wakati huo yeye akiwa anamaliza kazi ya kumpoteza kabisa Joesan yeye na pesa zake. Merina alizidi kusogea taratibu huku ule mtambo ukianza kuunguruma na kuwasha taa. Merina alifyatuka na kupeleka mapigo ya karate ya kushtukiza kwa Cat lakini dada huyo akayaona na kuyapisha. Mikono myepesi ya Merina ikaanza kufanya yake. Kwa jinsi ilivyokuwa ikichezeshwa mahali hapo ni kama ilikuwa imevunjika. Cat alishangaa sana huo uwezo, ulikuwa ni uwezo mkubwa ambao abadani yeye hakuwa nao. Kitendo chake cha kushangaa, kilikuwa kosa kubwa sana. Alikula mapigo mengi yaliyotua kifuani hadi akakohoa damu. Merina alikuwa na lengo la kuuwa hapo kabisa kabisa. Alimrukia Cat kwa double kick, Cat akajitahidi na kuzikwepa lakini Shetani wa kike aligeuka hapo hapo juu na kimtandika Cat ngumi maridadi ya pua. Cat aliyumba huku akivuja damu na maumivu makali yakimtambaa mwili mzima. Shetani wa kike Merina alikuja kwa kasi kwa lengo la kuchangua kabisa kifua cha Cat, Catherine akajua anakufa. Alimsubiri dada yule aje na alivyokuja kweli kwa kasi ile ile, akampisha, Merina alipita mazima. Merina akageuka tena lakini ghfla, kelele za kumshtua kila mtu pale ndani zikasikika. Merina aligeuka ili kujua ni nani huyo aliyekuwa akija kwa fujo .............



    Shetani wa kike aligeuka hapo hapo juu na kimtandika Cat ngumi maridadi ya pua. Cat aliyumba huku akivuja damu na maumivu makali yakimtambaa mwili mzima. Shetani wa kike Merina alikuja kwa kasi kwa lengo la kuchangua kabisa kifua cha Cat, Catherine akajua anakufa. Alimsubiri dada yule aje na alivyokuja kweli kwa kasi ile ile, akampisha, Merina alipita mazima. Merina akageuka tena lakini ghfla, kelele za kumshtua kila mtu pale ndani zikasikika. Merina aligeuka ili kujua ni nani huyo aliyekuwa akija kwa fujo namna hiyo. Alikuwa ni Roi. Kile kitendo cha yeye kugeuka, ikawa ni nafasi kwa Cat. Pigo baya sana likamtoka Cat ambalo lilitua kwenye titi la kushoto la Merina pamoja na teke lililopiga magotini. Merina alipinduliwa vibaya na kutupwa mbali huku maumivu yakilivamia titi lake sambamba na kifua kwa ujumla. Roi alijua uhatari wa Merina hivyo akataka abaki naye lakini Suzy akamuwahi kwa mateke mepesi akimwambia.

    "njoo upambane na mimi mpenzi.?" Ni bora basi Suzy asingemuita huyo bwana mpenzi maana hilo neno ni kama lilikwenda kuzinyanyua juu chuki zake dhidi ya mwanamke yule. Kichapo alichokipokea hapo hadi Kim akajikuta anaacha kazi yake na kuangali jinsi Suzy anavyokufa kwa maumivu. Suzy alipigwa hadi akapoteza kabisa nguvu. Alipoona juwa kitakachomuamsha ni mapenzi ya Mungu, ndipo alipomuacha na kumgeukia Merina, huko alimuona Cat akiwa amechoka sana kusimama baara ya kupokea kichapo kutoka kwa mtoto wa kike anayejiita Shetani wa kike. kwake Cat ilikuwa ni shida sana kupambana na Merina. Shetani wa kike alikuwa anakwenda kwa pigo la kumalizia. Japo Cat alichoka na kupigika sana lakini pia Merina alikuwa taabani alikuwa akijikaza tu mahali hapo. Pigo lile la kifua lilimuumiza sana. Alivyokuwa anajindaa kushusha pigo, alishutukia akichezea mapigo ya kushtukiza yaliyokuwa yakitokea nyuma. Merina akadondoka kwa Cat. Cat akala kichapo cha haraka haraka kabla ya kudondoka chini akiwa hoi. Merina akageuka kumtazama Roi. Roi akamsogelea. Hapo ndipo palipojulikana kweli huyo ni Shetani wa kike. Ule uchovu aliokuwa akiuonesha hapo ukawa umekwisha. kule kwenye mtambo, mambo yalikuwa yanatisha. Kim alishindwa kuuwasha ule mtambo na badala yake ukawa umeandika Fire. Hapo Kim akakumbuka maneni ya Tai kuwa.

    "ukikosea tu kuingiza namba za kuukontro mtambo huo basi unakuwa umetega bomu baya sana la masaa ambalo litakwenda kulipuka bila kumwaga sumu ya mionzi iliyokusudiwa. Mionzi hiyo itakwenda kugeuka moto ambao si mdogo. Kweli kwenye kioo hapo juu kitakuandikia Fire. Sasa lilipokuja tu hilo neno fire, Kim akajua si heri tena. Siri akabaki nayo mwenyewe. Akaamua amsaidie Merina kumuangusha huyo kiumbe asiyepigika. Roi. kichapo kilikuwa kikali sana, watu walipigana na ilikuwa ni piga nikupige. Roi akaona hapo anaweza akazidiwa endapo wote wawili wakiamua kutumia nguvu za kishaolin. Akaamua kudili kwanza na Kim. Alimchezesha kwa mapigo ya kiaina aina ambayo alijifunza kutoka kwa D.A hadi akampiganisha ukutani. Roi aliruka juu na kuukamata mkono mmoja wa Kim kisha akaufunga juu kwenye mbao ngumu kwa kutumia visu vyake vyenye cheni zinazo kata. Kim alipiga kelele sana lakini hakuweza kujinasua. Roi akamrudia Merina, zilipigwa, zilipigwa hadi Merina akapigwa tena chini. Kijana huyo akaruka tena na mkono wa pili wa Kim, baada ya ngumi nyingi za tumbo za kumlegeza kisha akaufunga kama wa awali. Mzee huyo akabaki kusimamia ncha ya vidole huku maumivu ya kukatwa na zile cheni yakimchonyota kwenye chemba ya moyo wake. Hapo sasa ndipo Kim alipopiga kelele kama mtoto.

    "nifungue wewe unataka nife humu?" alifoka sana. Kila akijivuta alishindwa, damu zilikuwa zikimwagika sana kwa jinsi cheni zile zilivyokuwa zikimkata. Sauti kali ikasikika mule ndani, ilikuwa ni sauti kutoka kwenye ule mtambo. ulikuwa ukitahadharisha kuwa kwa muda huo zilikuwa zimesalia dakika mbili tu na moto uweze kutokea. Kim alijua kuwa sasa anakufa kifo kibaya sana tena vitu vilivyokuwa vikitengenezwa kwa amri yake ndiyo vilikuwa vina muuwa. Merina alikuwa chini baada ya kupigwa pale mwanzo kabla Kim hajafungwa mkono wa pili. Alijinyanyua kwa kasi na kutaka kumrukia kijana huyo asiyewezekana. Suzy yeye alikuwa siyo wa kuamka tena hapo alipolala labda kama atawekewa roho iliyo hai. Kipigo kile alichopigwa awali pekee, kilitosha kumuondoa duniani. Merina kabla hajafanya alichokitaka. Roi aliikunja mikono yake kwa hisia kali na kupiga kelele.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "D.AAAAA!!!" kelele hizo zilipaa angani kisha zikazunguuka mule ndani na kujenga mwangwi mzito uliojirudirudia. Kelele zilizomfanya Kim kuchanganyikiwa na kujikuta na yeye akipiga kelele za haja.

    "Merina Kimbiaaaaaa, kimbia haraka Merina!!" Kim alipiga kelele kwa kumtaka akimbie, alishaelewa maana ya jina hilo. Huyo kijana alikuwa anataka kumpiga Merina kwa kuuwa kabisa. Pigo hilo lilikuwa ni pigo la hisia kali za mabuda. Merina aka jump kwenye kioo kimoja kisha kimya kikatanda. Roi alimtazama Kim kisha akautazama mtambo, zilikuwa zimebaki sekunde arobaini na tano tu. Akajua kifo cha mtu huyo ni huo mtambo. Alimkamata Cat kisha akarudi naye nyuma kidogo na kuchukua kadi kisha kujirusha kwenye kioo cha dirishani. walipofika chini walinyanyuana na kujikokota kwa taabu sana lakini kwa haraka mno ili kukaa mbali na jumba lile. Hawakufika mbali. Mlipuko mkali ukasikika huku nyuma ambao uliwasukuma kidogo kisha moto mkali kuibuka. Roi akampakiza Catherine kwenye gari na kumuelekeza njia ya kupita na kumwambia aondoke haraka sana kwani anahitaji kujua ni wapi Merina alipo. Alitaka kuhakikisha hakuna kiumbe anayetakiwa kubaki mahali hapo. Catherine hakupoteza muda aliwasha gari na kutoweka japo alikuwa akiendesha kwa shida lakini ilibidi, hakutakiwa kubaki mahali hapo ambapo muda wowote pangejaa askari polisi. Baada ya kama dakika nne au tano za kuwepo mahali pale Roi akitafuta kwa nacho ili kujua ni uelekeo gani ambao labda Merina atakuwa amechukua, kwani aliamini kwa ule mlipuko ni lazima Kim angepoteza maisha. Lakini ghafla bin vuu!, alishuhudia kwa macho yake mwenyewe. Helkopta ikipaa angani kwa kasi kubwa sana likitokea upande wa pili wa jingo hilo linaloteketea. Kilichomshtua na kumchanganya zaidi ni ndani ya helkopta ile, alimuona Merina akiwa ndiye muongozaji wa ile Helkopta huku nyuma alimuona Kim akiwa ameungua vibaya sana na pia alikuwa yuko katiaka hali mbaya kwa mtazamo.



    "shit! Huyu Merina kweli ni shetani na inavyoonekana amekula kiapo cha kuwa karibu na Kim" aling'aka Roi akiwa na ghadhabu nyingi kisha akasema.

    "hamuendi popote wanaharamu nyinyi" aliongea hivyo akiwa tayari amechomoa bastola kubwa yenye uwezo mkubwa na kutaka kuilipua ile Helkopta. Wakati anainyooshea ilr Helkopta kule juu, Vyuma vya bundiki zikitolewa usalama vilisikika ikiambatana na sauti kali nyuma yake.

    "shusha silaha yako chini kwa usalama wako. Ukikaidi nisawa na kukiruhusu kifo chako." Roi aliitazama ile helkopta kwa hasira jinsi inavyo chana mawimbi kisha akageuka kutazama sauti za amri zilizomsimamisha. Walikuwa ni askari maalumu wa jeshi la polisi wakiwa katika gwanda zao na mitutu ikiwa hewani kumuelekea yeye. Aliishusha ile silaha na kuiangusha chini kisha pingu zikafuatia. Wakati anataka kukokotwa kupelekwa garini akasema.



    "wameona kuwa nimewekwa chini ya ulinzi nanyi, hivyo wanaweza kukamilisha maangamizi yao waliyoyapanga wale. Naombeni mukaiweke chini ya ulinzi mkali Club ya Happy na muifanyie uchunguzi mkali kwa msaada wa jeshi maalumu linalohusika na ugunduzi na utambuzi wa silaha za kivita. Hapo nitakuwa tayari kufungwa maisha au kinyongwa, maana watanzani wataishi kwa amani ya milele." aliongea hivyo kijana Roi kisha kuwa tayari kutembea kulifuata gari la polisi. Kiongozi ambaye alikuwa anaongoza kile kikosi maalumu kitoka Dar es salaam, alimtazama yule kijana kwa muda sana kisha akalikumbuka sekeseke la masaa matano nyuma, akajua huwenda lisemwalo lipo na kama halipo unaweza kulitengeneza kwa upuuzi wa kutokuyatilia maanani maneno ama ushauri wa msingi kama huo. Kiongozi huyo akanyanyua simu ya upepo na kuiweka sikioni.

    "ndiyo afande, kitumwe kikosi maalumu kwa ajili ya kwenda kuiweka chini ya ulinzi mkali Happy Club haraka sana Over!"

    "umesomeaka kiongozi over?"

    "copy and out" ndivyo walivyo kuwa wakipeana taarifa maafande hao. Roi alitabasamu sana baada ya kumaliza kivumbi kile. Japo mahasimu wake wakuu hawakufa wote lakini aliamini palipo na nia siku zote hapakosi njia na mwenye hulka ni vigumu kuiacha. Aliingia kwenye gari hiyo ya polisi bila ubishi wowote, na safari ya kituo kikubwa cha polisi Morogoro, ikaanza.



    Father alishusha pumzi nzito sana baada ya kuona kijana wake ameingia mokononi mwa polisi. Alifikiri kwa muda na kuona kuwa hakuna kitakacho haribika kwani ushahidi mkubwa upo wa kuithibitishia serikali na aliamini kwa kazi ile kubwa ya kushukuriwa aliyoifanya, hakuna baya litakalo mkuta kijana wake.

    "Amiri kusanya kila kilicho cha muhinu turudi nyumbani. Roi watanzania wanakwenda kujua sifa zake kama serikali itaamua kumuanika hadharani lakini kama haitamuanika, ha ha haaa!" akacheka D.A bila kumalizia ni nini kitatokea kama hawata muanika. Chars na Zomba wakapewa taarifa hiyo kuwa sasa wanarudi nyumbani tanzania, wala hata hawakutaka kumwambia father D.A amalizie alichotaka kukisema. Ilikuwa ni furaha tu ya kurudi nyumbani baada ya miaka kibao kutokomea wakiwa ughaibuni.

    "vipi tunaweza kusafiri na mashine zetu za kazi mkuu?" Chars akauliza.

    "ndiyo nyingine zinasafirishika lakini mtambo wako ni mkubwa sana Chars hivyo ndege haitaweza kuubeba huo" alijibu D.A. Chars kama alinyongea hivi na kujiona hana bahati lakini Zomba akasema.

    "ndege hii ikotofauti sana. na ile tulioiteketeza kule Brazil. Hii inaweza kufunguka kwa nyuma bila shida halafu ipo nafasi ya kubeba hata gari ndogo mbili. Chars my brother usiwe na shaka, safari hii hatutaiteketeza bali tunaondoka nayo mitambo yote kwenda nayo nyumbani tena ngoja nikusaidie kuufungua." Maneno hayo ya Zomba, yalimfanya Chars kuwa na furaha sana. Wakakusanya kila kitu na kupaki ndegeni humo kisha wakaingia na wao. Mery akiwa wa kwanza baada ya kuambiwa anarudi nyumbani Tanzania. Zomba alikava nafasi ya urubani kisha kukiwasha chombo hicho ambacho amekifanyia mutundu mwenyewe akiwa pamoja na ndugu yake Jay, ambao waliishi kwa fadha kama familia moja tangia wakiwa wadogo kabisa. Na ndiyo maana wakapenda kumuita mtu huyo father. Ndege hiyo ilichomoka kwa kasi ya ajabu sana. Bila kusomeka kwenye rada ya aina yoyote ile. Waliiacha nyumba hiyo kubwa bila kuiharibu wala nini.



    Baada ya siku tatu za uchunguzi mkali uliofanywa na askari polisi maalumu wakishirikiana na wanajeshi wa kikosi cha uundaji wa silaha, Mzinga, ndani ya Happy Club, Hapo ndipo walipogundua kuwa hilo ndilo lililokuwa jingo namba 03 na 05. Yaani jingo la silaha kali za sumu na huku ikiwa ni Club. Walikwenda hadi chini kabisa ya ardhi, huko wakakuta mashehena ya silaha za kutisha baadhi wakizifahamu kwa majina lakini nyingi wakiwa hawazifahamu. waliogopa hata kuzitoa silaha nyingine, wakaamua kutoa chache zile wanazozifahamu na nyingine kuziacha humo hadi watakapopata wataalamu wa kuzijua silaha hizo. pia walitoa mashoga wengi sana humo ndani pamoja na watoto wa kike huku wengene wakiwa ni wadogo kabisa. Walipohojiwa wakasema kuwa walikuwa wakiishi humo kwa amri mwanzoni wakati wanaingia lakini kadiri walivyokuwa wakiishi, ndivyo walivyokuwa wakiyazoea mazingira. Vijana wote kutoka kwenye majumba yote ya siri ambao walikuwa wamehifadhiwa baada ya majumba yale kulipuliwa. Walikuwa ni vijana wengi mno wavulana kwa wasichana. Wasichana walikuwa ni zaidi ya mia moja na Hamsini huku wavulana wakiwa ni zaidi ya themanini. Hebu fikiria ndugu msomaji, wavulana wote hao wameharibiwa maisha. Ni ukatili kiasi gani uliokuwa ukifanyika mahali hapo. Ulikuwa ni unyama na ushetani mkubwa sana. Serikali ilijaa hapo kwa muda. Kitendo cha kugundua jingo hilo ndipo wakayahusisha na baadhi ya matukio ya mauwaji yaliyopita. Hakukua na mtaalamu mwingine wa kuzitambua zile silaha bali Father D.A ilibidi ajitokeze na kutoa historia nzima kuanzia mwanzo hadi meisho ilivyokuwa hadi kuamua kuvaa jukumu kama yeye ikiwa ni kama kulipa kisasi laikini pia kumzuia asiendelee kuwaharibu vijana wa Tanzania mzee huyo. Ilikuwa ni ngumu kueleweka lakini alipoamua kuileta timu ya vijana wake hatari wa kazi mahali hapo, maafisa wakubwa kabisa wa majeshi mbalimbali nchini, wakiwemo na viongozi wakubwa wa serikali. Hawakuwa na budi kuwaelewa na kuamini kuwa hao walikuwa ni watu muhimu sana kwani kwa mziki ule ni wazi majeshi ya nchi yangesumbuka sana kuzuia. Father akajitolea kuwafahamisha juu ya silaha zile.



    Siku tatu nyingine mbele, Viongozi wakuu wa nchi walikuwa wameizunguuka meza wakijadili jambo. kilikuwa ni kikao cha siri kweli ambacho kilikuwa kikimjadili kijana Roi pamoja na watu wake. Kila mtu alimuona kijana huyo anamoyo na imani ya pekee kabisa na laiti asingelikuwa yeye basi Tanzania ingekuwa pabaya na wangekumbuka shuka ni asubuhi tayari.

    "kuna kila sababu ya kumuweka mahali huyu kijana" alisema mtu mmoja mweusi na mnene kiasi aliyepiga suti nzito ya gharama, lakini wakati wanaendele kujadili mahali hapo, bwana mmoja mwenye suti nyeusi akapokea simu na alipo maliza kuongea na simu hiyo, akatulia na kuwaambia watu wale waliokuwa kama wakifuata muongozo wake.

    "jamani mkuu wa nchi amesema kuwa kijana huyo ahifadhiwe mahali pa siri sana akiwa huru huku ngazi za juu zikifikiria ni nini afanyiwe kwa ajili ya nchi yake. Na wale wenzake wataishi huko waliko fikia ambako wao wamekuchagua wenyewe. Serikali inawathamini sana watu kama hawa. Hivyo basi kikao hiki kinavunjwa na maamuzi yatakayotolewa mutajulishwa." Roi alitoka ndani akiwa kwenye ulinzi mkali sana kisha watu wale wenye silaha waliokuwa wakimlinda kama mifugo na mchunga wakazuiwa na kuambiwa kuwa huo ndiyo mwisho wa kumlinda kijana huyo na badala yake watapangiwa kazi nyingine. Roi alikumbatiana na watu wake kisha akavutwa pembeni na mtu yule mwenye suti nzito ya gharama kwa ajili ya kuteta jambo.

    "wiki moja ya mapumziko unapewa ukiwa na familia yako kisha mkuu wa nchi anakuitaji White House Dar es salaam" aliongea mtu huyo. Roi akatikisa kichwa kukubali kisha akaifuata gari yenye vioo vya giza tupu, akavunguliwa mlango na Cat huku dada huyo akiwa kwenye tabasamu pana.

    "karibu nyumbani mtukutu" alionge Catherine. Roi akaushika ule mlango na kugoma kuingia.

    "nipe sharubati mtoto" alisema Roi kisha kumkumbatia na kuanza kunyonyana. Walinyonyana sana hadi D.A uzalendo wa kukaa ndani kwa muda mrefu ukamshinda, akaamua kushusha kioo na kuchungulia.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "nyie watoto twendeni nyumbani jamani."

    "father anazingua" alisema Roi akimuangalia Cat usoni kwa jicho la mahaba.

    "twende nyumbani ukapumzike kifuani mpenzi wangu" alisema Catherine kisha wakaingia garini, Zomba akaliondoa gari hilo ambalo ni zawadi ya pekee kutoka serikalini.



    MWISHO



0 comments:

Post a Comment

Blog