Chombezo : Kahaba
Sehemu Ya Nne (4)
“Mke wangu mimi sielewi kabisa ni nini ambacho unakizungumza”. Niliongea huku nikiendelea kusikilizia maumivu pale juu ya sakafu.
SASA ENDELEA
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ninarudia tena kwa mara nyingine, ninataka kujua vito na baadhi ya nguo zangu vimeenda wapi? Haiwezekani vitu vyangu vikatoweka kiajabuajabu!”. Mama Careen aliendelea kuongea huku akiendelea kunishushia kipigo kitakatifu.
“Mimi sielewi mama Careen. Mbona wewe umekazania kwamba mimi ndiye ambaye nimechukua vitu vyako?”, Niliongea kwa kujitetea katika sauti ya maumivu.
“Sasa humu ndani tunaishi wangapi”. Aliuliza mama Careen baada ya kuwa amenitandika upawa katika makalio yangu.
“Humu tunaishi wengi na wewe mwenyewe unajua kabisa”. Niliendelea kujitetea.
“Kwa hiyo una maana huyu mtoto mdogo Careen ndiye ambaye amechukua?”. Mama Careen alihoji kwa ghadhabu sana.
“Huwezi jua mke wangu”. Nilijibu hivyo kwa lengo la kumshawishi akubaliane nami.
Ukweli wa dhahma ile yote mimi ndiye ambaye nilikuwa naufahamu. Mimi ndiye ambaye nilikuwa nimechukua baadhi ya vifaa vya urembo vya mke wangu kama vile; bangili, herein, pete n.k na kwenda kumpa Jasmine kama zawadi.
Nakumbuka nilimpa Jasmine nikimdanganya kwamba nilikuwa nimemnunulia. Jasmine alifurahi sana na kuamini kwamba kweli mimi nilikuwa ninamaanisha penzi la dhati kwake. Aliahidi kulidumisha penzi letu hili changa na kunipenda milele.
“Nasema hivi baba Careen, mimi sihitaji maelezo yako ya kitoto na yasiyo na kichwa wala miguu. Ninachokihitaji ni vitu vyangu virejee hapa. Hii ni tabia mbaya kabisa”. Mama Careen aliendelea kufoka huku sasa akibubujikwa na machozi na kuondoka kutoka eneo lile ambalo alikuwa akinisulubu.
Nami kwa aibu na fedheha kubwa nikajizoazoa kutoka pale chini huku mwili wangu ukiwa umelemewa mzigo mzito sana wa maumivu yasiyomithilika. Nikaamua kwenda chumbani ili nikayapunguze mawazo yangu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
***********
Penzi langu na Jasmine lilizidi kukua kwa kasi mithili ya moto mkali ulao nyika. Jasmine sasa alikuwa ameiacha ile kazi yake ya ukahaba na nilikuwa ninajaribu kuiweka sawa mipango ya kumfungulia mradi ambao utayaendesha maisha yake.
Nilikuwa nimeamua kabisa kuimarisha koloni langu kwa Jasmine baada ya kuona mke wangu mama Careen ananiletea mambo ambayo siyaelewi kabisa.
“Baby nina jambo moja nyeti ambalo ninapenda nikushirikishe”. Jasmine aliongea siku moja tukiwa nyumbani kwake tukiyafurahia mapenzi yetu.
“Jambo gani tena mpenzi wangu?”. Nilimwuliza Jasmine.
“Ni jambo la kawaida tu”. Jasmine aliongea huku akiniachia busu mwanana.
“Umeanza kunitisha sasa mpenzi wangu”. Nilimwambia.
“Usihofu mpenzi, ni kawaida”. Jasmine aliongea.
“Ok, ni jambo gani hilo?”. Nilimwuliza.
“Katika siku za hivi karibuni nilikuwa najihisi tofauti katika mwili wangu. Nimekuwa nikijisikia uchovu wa mara kwa mara, kichefuchefu na miguu kuniuma”. Jasmine aliongea.
“Aaaaah! Hayo yatakuwa ni malaria”. Nilimjibu kwa kujiamini sana utadhani mimi ni daktari.
“Kwa nini wasema hivyo mpenzi?”. Jasmine aliuliza huku akinitazama usoni.
“Unajua malaria mimi naifahamu sana. Dalili zake ni kama hizohizo ambazo umezitaja. Itakubidi uende hospitali ukapime ili uanze dozi mapema?”. Nilongea huku nikimfariji Jasmine.
“Basi jana niliamua kwenda hospitali kwa lengo la kupima. Baada ya vipimo, niligundulika kwamba nina ujauzito wa mwezi mmoja”.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Unasemaje weweeeee?”. Niliuliza kwa taharuki utadhani ya kwamba nilikuwa sijakisikia kile ambacho Jasmine alikuwa amekiongea.
“Nina ujauzito wa mwezi mmoja mpenzi”. Jasmine alirudia kuongea tena kwa mkazo.
“Hapana haiwezekani!”. Niliongea huku ubongo wangu ukiwa kama umeacha kufanya kwa sekunde kadhaa.
“Sasa haiwezekani nini?”. Jasmine alihoji kwa mshangao.
“Sasa wewe unafikiri tutafanyaje?”. Nami nilimjibu kwa kumkandika swali.
“Tutafanyaje kivipi?”. Naye alinijibu kwa kunirushia swali lilelile.
“Hivi wewe huoni kama hili ni tatizo kubwa?”. Nilimwambia.
“Sasa kuna tatizo gani hapo wakati wewe ulisema wanipenda na wataka kuanza maisha na mimi”. Jasmine aliongea.
“Sawa, lakini vipi mama Careen akiligundua hili? Huoni kwamba patachimbika?”. Nilijaribu kutoa tahadhari.
“Hilo utajua wewe maana tangu mwanzo mimi nilikwambia kuhusu hili. Je, wewe ulinijibuje? Si ulisema nikuachie wewe ya kwamba utajua namna ya kufanya!”. Jasmine aliongea huku sasa akionekana kukasirika kidogo usoni.
“Sawa la … la … lakini ….”. Kigugumizi cha ghafla kilinijia.
“Lakini nini?”. Jasminie aliuliza.
“Tena ulisema wewe ndiye mwanaume wa nyumba na unaamua nini ukifanye na nini usikifanye. Hebu acha kunichanganya bwana”. Moto wa Jasmine sasa ulizidi kupanda.
“Ok, mama wala usijali. Mimi nitajua namna ya kufanya. Nakupenda sana Jasmine”. Niliamua kumuweka sana ili kuisafisha hali ya hewa ambayo niliona inaanza kuchafuka taratibu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hayo ndiyo maneno. Siyo unakuwa unaleta ngonjera zako hapa ambazo hazieleweki kama siyo mwanaume bwana!”. Jasmine aliongea huku akionesha wazi kwamba alikuwa na furaha kutokana na maneno yangu.
*********
Ujauzito wa Jasmine ukazidi kuyaimarisha mapenzi yetu. Mimi nikampenda sana Jasmine na yeye pia akanipenda sana. Tulithaminiana na kuheshimiana. Tuliweka ahadi na mipango mingi na kabambe katika kuliimarisha penzi letu.
Ujauzito wake ukazidi kukua kwa kasi. Miezi ikazidi kukatika. Kichwa changu kikawa na mawazo mengi sana ambayo yalikuwa yakizidi kuongezeka kila uchao.
Nilikuwa nikiwaza ni namna gani nitaweza kukabiliana na varangati la mama Careen pindi ambapo atakuja kuyagundua mahusiano yangu ya kimapenzi na Jasmine.
Hilo lilikuwa ni dogo kati ya yale ambayo nilikuwa nikiyawaza. Jambo kubwa ambalo ndilo liliniumiza kichwa hasa ni suala la ujauzito wa Jasmine. Suala la mimi kutembea na Jasmine niliona ningeweza kulizima endapo moto wa mama Careen ungewaka lakini suala la ujauzito mh!
Hili lilikuwa kubwa na nilishindwa kulibeba kabisa. Nilikuwa nikiliona kabisa jahazi likienda mrama na mimi kama nahodha nilikuwa sina uwezo wa kulinusuru jahazi hili katika gharika hili kubwa.
“Lakini haya yote ameyataka yeye mwenyewe mama Careen. Mwanamke ni mshari balaa. Hajui hata kuibembeleza na kuitunza ndoa. Kila siku ni ugomvi tu ambao hauna hata sababu ya msingi”. Niliwaza siku moja nikiwa chumbani wakati mama Careen akiwa nje uwanjani akicheza na Careen.
“Furaha ya ndoa yetu ilipotea miaka mingi nyuma. Siku za mwanzo za ndoa yetu ndipo nilipolifurahia penzi langu na mama Careen lakini baada ya hapo, ndoa yetu ilibadilika na kuwa chungu kabisa”. Niliendelea kuumizwa na mawazo kichwani mwangu.
“Na kila nikijaribu kumsogeza jirani mke wangu ili tuitengeneze ndoa yetu, yeye alikuwa mbali nami zaidi ya kuzidisha ushari wake. Hajali kabisa ustawi wa ndoa yake”. Nilizidi kutiririkwa na mawazo lukuki mengine yakiwa ni maswali ambayo yalikosa majibu.
Hatimaye taratibu machozi ya uchungu yakaanza kuniporomoka. Niliumia kwa sababu mimi na mke wangu tulikuwa tumeshindwa kuitengeneza ndoa yetu na hatimaye ilikuwa ikielekea katika misukosuko.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baadaye usingizi ukanipitia na kunisahaulisha yale yote ambayo yalikuwa yakiniliza. Nilianza kuota ndoto nzuri na tamutamu juu yangu na Jasmine. Niliota tukiyafurahia maisha pamoja.
***********
Siku moja mama Careen akawa amepata mgeni. Mgeni huyu alikuwa ni mwanamke. Mwanamke huyu alikuwa ni mzuri na mrembo sana.
“Mh! Mdogo wangu wewe una mambo makubwa sana”. Mama Careen aliongea pindi walipokuwa wamekaa sebuleni.
“Kwa nini waongea hivyo dada?”. Mgeni aliuliza.
“Yaani tumepoteana miaka mingi sana hatuonani. Halafu jambo la kushangaza eti sote twaishi katika jiji hilihili la Kano”. Mama Careen aliongea.
“Nisamehe dada yangu. Ni maisha tu ndiyo yamesababisha yote haya”. Mgeni aliongea.
“Wala hata usiyasingizie maisha. Maisha ndiyo yakufanye ushindwe hata kunijulia hali nduguyo?”. Mama Careen aliendelea kuongea kwa kutoa lawama kwa mgeni ambaye alikuwa ni mdogo wake.
“Halafu naona mambo yako si mabaya. Yaani safari hii umeamua kabisa kutundikwa mpaka mimba. Mbona siyaamini macho yangu!”. Mama Careen aliongea kwa mshangao huku akilitazama tumbo la mdogo wake ambalo kwa sasa lilikuwa kubwa.
“Dada yangu. Mimi safari hii ninataka kuolewa. Nimepata mchumba ambaye ananijali na yuko tayari kabisa kunioa”. Mgeni aliongea.
“Ha ha ha ha haaaaaaaa! Yaani Jasmine wewe leo hii unataka kuolewa?. Mh! Haya bwana. Je, na biashara yako ya ukahaba unamwachia nani?”. Mama Careen aliuliza.
“Ile biashara nilikwishaiacha dada. Huyu mchumba wangu ndiye ambaye amenibadilisha na kunifanya niiache biashara hii kabisa. Nimeamua kubadilika kabisa na kuanza maisha mapya dada yangu”. Mgeni aliongea huku machozi yakimlengalenga.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Yaani leo ndiyo unatambua kwamba biashara uliyokuwa ukiifanya ilikuwa ni mbaya. Je, wakati mimi nakukanya juu ya biashara ile mbona hata ulikuwa hunisikilizi?”. Mama Careen aliongea.
“Nisamehe dada yangu. Na ndiyo maana leo hii waniona niko hapa mbele yako nikiwa nimebadilika kabisa. Mimi si yule Jasmine wa zamani, kahaba. Mimi ni Jasmine mpya. Naomba unisamehe kwa yote ambayo nilikukosea dada yangu mpenzi”. Jasmine aliongea huku akiporomokwa na machozi.
“Haya nimekusamehe mdogo wangu”. Mama Careen aliongea huku akimkumbatia Jasmine.
Ghafla simu ya Jasmine iliita.
“Hallo! Baby”. Jasmine aliongea mara baada ya kubonya kitufe cha kupokelea simu.
“Uko wapi? Mbona nimefika hapa kwako sijakuona?”. Upande wa pili wa simu uliongea.
“Nisamehe mpenzi wangu. Leo nimeenda kumtembelea dada yangu yule ambaye nilikwambia”. Jasmine aliongea.
“Sasa mbona hukunitaarifu?”. Upande wa pili wa simu uliongea.
“Naomba unisamehe mume wangu. Mimi nilifikiri kwamba hutakuja nyumbani kwa wakati huu ndiyo maana sikukutaarifu. Nisamehe sana mpenzi wangu”. Jasmine aliongea.
“Ok, nimekusamehe”. Upande wa pili wa simu uliongea.
“Halafu mpenzi, nilipenda jioni ya leo twende pamoja huku kwa dada yangu ili nikutambulishe kwani dada ana hamu kubwa sana ya kukuona”.
“Ooooh! Hilo wala usijali. Nitajaribu kuziweka sawa ratiba zangu ili kusiwe na usumbufu wowote”. Upande wa pili wa simu uliongea.
“Ahsante sana mpenzi”. Jasmine alishukuru.
“Ok, usijali”. Upande wa pili wa simu uliongea.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya Jasmine kuongea na ile simu, basi maongezi yake na mama Careen yakaendelea. Wakaendelea kupeana michapo ya hapa na pale ambayo iliwaletea furaha tele katika nyoyo zao.
“Ndiyo hivyo dada. Hakika utampenda kwani ni mwanaume mzuri, mtanashati, anayejali na ambaye anajua nini maana ya pendo la dhati”. Jasmine aliongea.
“Mh! Haya bwana. Waswahili walisema mtu chake. Tutaona hiyo jioni kama hizo sifa unazompamba kweli anazo?”. Mama Careen aliongea huku akicheka.
************
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment