IMEANDIKWA NA : FRANK MASAI
*********************************************************************************
Chombezo : Haa! Kumbe Tamu
Sehemu Ya Kwanza (1)
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hali fulani ya ubaridi ilikuwa inaendelea kuchukua nafasi kubwa kwenye Jiji lile la Mbeya,kwenye Wilaya moja inaitwa Chunya. Hali hiyo ya ubaridi ilisababisha kila mtu ajifungie chumbani kwake na kujivisha masweta mazito ya sufi.
Wale wageni waliotoka maeneo ya joto kama Dar es Salaam,walikuwa ndani ya sufi hilo na pia wakaongeza na blanket zito ambalo lilisababisha faraja iliyoletwa na joto mwilini mwao.
Wakati hayo yakiendelea humo ndani mida ya saa mbili za usiku, huku nje kulikuwa na kijana mmoja mwenye mwili kiasi, na mrefu kwenda juu huku akitanuka kifua chake kama wanyanyua vyuma au wacheza mpira wa kikapu.
Licha ya mikono yake kuvaa grovu za sufi, lakini bado alikuwa akiifikicha kwa pamoja kama mtu àpakaye mafuta au anatengeneza moto kwa kutumia Ulimbombo na Urindi.
Hakuishia hapo kwenye kuifikicha ili kupata joto litakalompa ahueni katika baridi ile kali, mara nyingine alikuwa ànaipuliza mikono na kuipumulia kwa mdomo wake ili kuipa joto na saa nyingine kuiingiza makwapani ili kuitafutia joto lililopo huko.
Macho yake hayakutulia. Kila mara yaliangalia upande wa kulia inapotokea njia ya mtaa wa pili,njia àmbayo ilikuwa haionekani vizuri kwa sababu ya ukungu uliotanda usiku ule.
Anaitwa Longino Mshama. Kipa hodari wa timu ya Chunya. Lakini usiku ule alikuwa na nia moja tu! Ya kukutana na mrembo aliyeutesa moyo wake kwa muda mrefu, mrembo ambaye anamfanya apigwe na baridi kila usiku wa mida kama ile.
Mrembo anayekwenda kwa jina la Subira Msafiri, mtoto wa tatu kati ya watoto watano wa Mzee Msafiri. Mzee ambaye anasifika kwa utajiri ng'ombe pale Chunya.
Mzee Msafiri alibahatika kupata watoto watano katika maisha yake ya ndoa. Mtoto wa kwanza ambaye alikuwa ni wa kiume,alishafariki miaka kumi iliyopita.
Mtoto wa pili ni wa kiume pia. Yeye ni mlanguaji wa bidhaa ambazo anazitoa Dar na Zanzibar na kuzileta pale Mbeya hasa Wilaya ile ya Chunya.
Wa tatu ndio huyu Subira ànayesubiriwa na Longino katika baridi kali la Mbeya. Wa nne na wa tano,hawa ni pacha. Kulwa akiwa mme na Doto akiwa mke,wote walikuwa wanamiaka mitano.
***CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya Longino kusubiri sana,hatimaye alipata ahueni pale alipomuona fahari wa macho yake anatokea kwenye ukungu ambao ulikuwa unaendelea kutanda kwa wingi usiku ule.
"Nashukuru umekuja Subira."Longino aliongea kwa sauti nzito na ya chini huku akimwangalia kimwana yule mwenye rangi nadhifu ya chokleti,huku usoni akiwa kabeba uso mwembamba na macho ya duara pamoja na pua ndefu kiasi kama ya Kihindi.
"Nakusikiliza. Time inaenda si unajua home geti kali."Subira aliongea huku akionesha kweli hana muda mrefu wa kuendelea kuwa pale.
"Subira sina jipya zaidi ya kukuomba uwe mpenzi wangu. Embu nitazame jinsi navyoumia kwa baridi kwa ajili yako. Kwa nini hutaki kunielewa Subira?. Nifanye nini ili ukubali moyo wangu kuwa unakuhitaji? Naomba unielewe Subira,unanitesa mwenzako." Longino maneno yalimtoka huku uso wake kauweka katika masikitiko yasiyo na kifani.
"Umemaliza?."Ni swali la maudhi kwa kila mwanaume ambaye angeulizwa na mwanamke wakati anamtongoza, lakini kwa Longino lilikuwa kama pipi. Sijui kwa nini, labda kwa sababu mapenzi ni upofu ndio maana swali lile kwake halikumkera.
"Nakuomba uelewe hayo machache niliyoyaongea, nakupenda Subira."Longino alizidi kuonesha uhitaji wake mbele ya mwanadada yule gwiji la urembo pale Chunya licha ya kuwa ndio kwanza yupo kidato cha tano.
"Tayari umemaliza au unaendelea."Sauti ya kijasiri ilimtoka Subira huku mdomoni mwake akiwa anasindikizwa na bazoka na wakati huo mikono ilikuwa kiunoni na mguu mmoja aliutikisa kama anayesubiri mwanamke mwenzake amalize ili aanze yeye kumchamba.
"Ndio nimemaliza Suby."Sauti ya upole ilimtoka Longino lakini haikumfanya Subira asiseme alichokusudia.
“So, its my turn.” Subira aliongea Kiingereza huku bado yale manjonjo ya kutafuna jojo yakiendelea mdomoni kwake kama kocha mstaafu wa Manchester United, Sir Alex Ferguson.
“Nadhani sina la nyongeza hadi hapo Suby. Waweza nipa msimamo wako.” Nafasi ya kuongea iliwekwa wazi na Longino na sasa mwanadada alikuwa tayari kumwaga vumbi la shombo.
"Nisikilize we kinyago cha mpapure.”Longino alilegea ghafla na kuwa kama samaki aliyechina baada ya kuitwa jina lile, lakini ulegevu ule haukufanya shombo zitokazo mdomoni mwa Subira kukwamia kooni.
“ Haya matawi anayaweza twiga, we sungura huyawezi. Tafuta saizi yako, hii saizi ni large huiwezi we small,itakupwaya bure. Na hata ukijaribu kunibana ili nikutoshe, utaambulia patupu kwani sitakuwa tayari kuharibiwa na wewe mfuga panzi." Subira alimtolea shombo Longino, kisha akageukia kule alipotokea kwa ajili ya kuondoka. Lakini kabla hajaondoka, alimgeukia Longino.
"By the way. Sivaagi mabati kama haya. Hizi levo za dhahabu au silva. Hayo mabati kawavishe darasa la tano, nikutakie baridi njema."Maneno yalimwendea Longino yakifuatiwa na kutupiwa cheni, hereni na bangiri alizozinunua juzi kabla ya siku hiyo.
Longino baada ya kutupiwa urembo ule wa kike kwenye uso wake,aliinama taratibu na kuokota vile vito vya shaba ambavyo Subira aliviita mabati.
Kuna vingine vidogo kama hereni, ilimpasa awashe kurunzi ya simu yake ili avione na kuviokota.
Hakika àlikuwa katika fadhaha kubwa hasa pale aliponyanyua macho yake na kumuona Subira akitokomea gizani huku ukungu ukiongeza ladha ya kutoonekana kwa mwanadada yule mwenye manjonjo mengi kama pishi la sikukuu.
Longino alikuwa karibu atokwe na chozi la mfadhahiko, lakini alivumilia huku akijiahidi moyoni mwake kutokata tamaa hata kama itachukua miaka mia kumpata kisura yule.
Aliviangalia tena vile vito alivyotupiwa na Subira,kisha alikumbuka jana yake baada ya kuvinunua siku moja liyopita.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hela aliyotumia kununulia vito vile aliipata baada ya kutoka kambini ambapo timu yao ya mpira ilijichimbia. Siku ile ya Ijumaa, walipewa ruhusa ya kwenda kusalimia nyumbani kwao.
Kwa kutumia fedha kidogo ambazo alipewa na mfadhili wa timu ile ya Chunya, aliweza kununua vito vile kwa ajili ya mwanamke anayeutesa moyo wake, mwanamke ambaye badala ya kuuthamini upendo huo, anamwachia aibu ya moyo mwanaume.
Baada ya kupumzika Ijumaa ile yote, Jumamosi yake ndipo alimtafuta Mercy, rafiki wa karibu kabisa wa Subira.
Mercy hakuwa mbovu kisura wala hakuwa na nyodo kama za Subira. Mara nyingi alimsikitikia sana Longino kwa kumfatilia mtu ambaye alikuwa hana muda kabisa na yeye.
Uzuri wa Mercy, Longino hakuuona japo binti yule msomi wa kidato cha tano pia, alijitahidi kila kukicha ajipendezeshe mbele ya macho ya Longino.
Hakika Mercy alimchagua Longino, lakini angefanya nini na wakati dume lenyewe limekula yamini ya kuwa na Subira tu!?.
Swali hilo ndilo likawa kikwazo cha Mercy kumpata Longino.
*****
Mercy kusikia anaitwa na Longino, alifurahi sana hasa ukizingatia ni wiki mbili hajamuona mwanaume yule kutokana na kambi waliyokuwa wamewekewa.
Furaha ya Mercy ilihitimishwa na kuingia kisusunu pale alipopewa zawadi za kumpelekea rafiki yake kipenzi, Subira. Uso wa Mercy ulipoteza tabasamu lake halisi na kubaki tabasamu la kuchonga lililokaa ili lisipoteze maana katika kichwa cha Longino.
Alijua wazi Subira hatokuwa na shukrani kwa vile vichache ambavyo Longino aliacha kumnunulia mdogo wake kipenzi, Jesca.
Mdogo ambaye alipata ajali mbaya enzi za utoto wake, na àjali hiyo ikaaribu miguu ya mtoto yule hivyo kumfanya àwe anatembelea kiti tangu anaumri wa miaka mitano hadi sasa hivi anatimiza miaka kumi na moja.
Mercy alitimiza wajibu wake kwa kumpelekea vito vile vya shaba Subira. Na kama àlivyotegemea kuona na kusikia, Mercy wala hakuumiza kichwa juu ya tabia ya rafikiye.
Na hata pale msonyo wa kifedhuri ulipomtoka Subira baada ya kuambiwa Longino anamuhitaji kesho yake, Mercy hakuutilia maanani kwa kuwa tayari mjumbe alishafikisha ujumbe kwa muhusika.
****
Longino hata baridi hakuihisi baada ya maneno yale ya kashfa kutoka kwa Subira.
Alipohakikisha hajaacha kitu kati ya vile alivyotupiwa na Subira,alianza kujikongoja taratibu huku akili yake ikiwa kama imeganda kwa sababu ya maneno aliyoyasikia muda mchache uliopita.
Alipofika nyumbani alimkuta Jesca,mdogo wake akiwa anajisomea kitabu chenye hadithi ya My Rose, lakini lengo la Jesca kufanya hivyo, ilikuwa ni katika kuvuta muda ili kaka yake aje maana hakujisikia kulala bila kumuona kaka yake ambaye alitoka usiku ule.
"Huyoo karudi."Jesca alimkaribisha kaka yake kwa shangwe huku akinyoosha mikono ya kutaka kumbate dogo la kaka yake kipenzi.
"Oooh! Katoto kangu,mmwah."Kaka naye alijibu mapigo akiwa na furaha.
"Naona unasoma peke yako. Mama tayari àmelala?." Longino alimuuliza mdogo wake juu ya mzazi mmoja wanayeishi naye kutokana na ajali îliyomvunja miguu Jesca, kumpeleka kaburini baba yao.
"Mama kalala. Nataka na mimi unisomee hadi nilale."Jesca àlideka mbele ya kaka yake huku anampa kitabu alichokuwa akikisoma.
"Haya. Ila kabla sijasoma nataka kukupa zawadi,"
"Zawadi gani?."
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Fumba macho."Longino alimtaka mdogo wake afumbe macho naye akafanya hivyo,na hapo ndipo alipomvisha cheni ile ya shaba lakini yenye mvuto kwa kuiangalia.
Dogo alipofumbua macho,alijawa na furaha na kumkumbatia kwa nguvu kaka yake huku akitamka kwa hisia maneno "nakupenda kaka".
Longino alikabwa na donge la uchungu alipokumbuka alichofanyiwa na Subira na sasa mdogo wake anamuonesha thamani ya vile vito vilivyoitwa mabati na mshenzi mmoja.
Mshenzi ambaye hata ungekuwa wewe ungemuita mshenzi,lakini kwa Longino, aliona kawaida tu. Siku zote alijua hakuna marefu yasiyo ncha, hivyo muda wake ukifika, atampata tu yule mwanamke. Hakutaka kufikiria marefu hayo yasiyo na ncha yanaweza kutokea kwake pia, na ndicho ambacho alitakiwa kukifanya. Alitakiwa kuachana na mapenzi ya kujimbeleza na badala yake aangalie mwenye nia naye.
"Yaani huyu Subira wakunitupia hivi vitu na kuviita mabati?. Vitu ambavyo mdogo wangu anaviona kama dhahabu.
Huyu anajua nimevitoa wapi hivi? Anajua nimetoa shilingi ngapi ya kununulia hivi vitu? Anajua nimeacha kununua vingapi kwa ajili ya familia yangu?. Anajua kweli huyu?
Naonesha kiasi gani namuhitaji na kumjali lakini malipo yake kwangu ni kunifadhahisha. Subira kanipa fadhaha ya moyo, Subira kaufadhahisha moyo wangu kwa sababu nampenda.
Mdogo wangu kaitoa fadhaha hii. Huyu Subira anauzuri gani kuliko familia yangu? How beautiful she is than my family?."
"Kaka mbona umepoa hivyo? Au hutaki asante yangu?" Sauti ya Jesca, mdogo wake kipenzi ndio ilimtoa katika mawazo yake ambayo alikuwa ànamfikiria kwa kina Subira. Mwanadada ambaye alimfanyia mbovu muda mchache uliopita kabla ya mdogo wake kumfanyia mazuri kwa kile ambacho kilioneka siyo kwa Subira.
"Hamna dada, ujue umenishangaza kuipenda hiyo cheni." Longino alimjibu mdogo wake huku akijaribu kuchongesha tabasamu dogo la kufariji.
"Hii nzuri kaka. Inang'aa kama dhahabu." Jesca naye alimjibu huku akiweka uso wa furaha kuonesha kakubali zawadi ya kaka yake.
"Haya chukua na hivi. Hizo bangiri utavaa ukiwa mkubwa. Walikataa kunibadilishia wanipe ndogo kwa àjili yako." Longino alimpa na vile vito vingine huku akijitetea kuhusu bangiri ambazo zilikuwa kubwa wa Jesca.
"Asante kaka,"Jesca alishukuru tena na kuzidi kumkumbatia kaka yake.
"Haya twende kitandani sasa ukalale."Longino alimnyanyua mdogo wake kutoka pale kwenye kiti cha walemavu wa miguu na kumpeleka chumbani anapolala na wakati huo mdogo mtu alikuwa kakamatia kitabu chenye hadithi ya kusisimua.
Hadithi iliyowatoa machozi wengi. Hadithi ya kweli kabisa iliyomuhusu Generose na Frank Masai.
Ndiyo hiyo My Rose ambayo Longino alimkuta dada yake anaisoma usiku ùle.
"Kaka nisomee kitabu ndio uondoke humu."Jesca alitoa ombi baada ya kaka yake kumfunika blanketi.
"Sawa. Ehee,uliishia wapi?."Longino alimuuliza Jesca baada ya kushika kitabu kile. Jesca àlimuonesha na kaka yake alianza kumsomea hadi pale alipomuona kalala kabisa.
Alimbusu shavuni na kumfunika vizuri kisha àkatoka chumba kile cha mdogo wake na kuelekea chumbani kwake ambapo kilikuwa ni chumba cha nje na kilichojitenga na cha mdogo wake na mama yake.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alijitupa kitandani kisha mawazo juu ya Subira yakaupamba ubongo wake. Mawazo yalikuwa mengi sana, lakini hakuna hata jibu sahihi juu ya fikra àmbazo ndizo zilikuwa chanzo cha mawazo yale.
"Mercy."Jina hilo lilikuja na kuufanya uso wa Longino upambike kwa tabasamu na faraja nzito kurudi moyoni mwake.
"Hivi kwa nini sikuona uzuri wa Mercy mchana hadi sasa hivi usiku ndio nauona?."Longino alijikuta akijiuliza peke yake na kuzidi kutabasamu.
"Hivi Suby kamzidi nini Mercy? Au yale macho ya duara ndio yamenidatisha mimi nini?. Lakini mbona Mercy mkali sana tu. Embu angalia yale meno yake yalivyopangana kinywani. Sura na umbo lake, mbona vipo poa sana tu. Anajua kumuhendo mwanaume na anajali muda. Huyu mwingine mbona hayupo kama mwenzake?
Kuna haja gani ya kuwa Subira na wakati Mercy yupo?. Ila "Mawazo yalikuwa mengi kichwani mwa Longino, lakini mwisho wake aliamua jambo moja tu! Ambalo ndilo aliliona sahihi kwake. Aliamua kumtafuta Mercy kesho yake kabla hajarudi kambini.
“Kesho nitamtafuta huyu Mercy na kumpa ukweli juu yake. Japo nampenda sana Subira,ila haiwezekani kuwa naye, ataniumiza huko niendako hata kama atanikubali niwe naye. Mwache aende zake.”Longino alikubali kushindwa mbio za moyo wake na kuamua kugeuza upande mwingine wa shilingi ambapo kulikuwa na sura ya Mercy.
Haileweki ni mawazo gani yalikuwa ya mwisho kwake, lakini alijikuta ameshapitiwa na usingizi baada ya fikra nyingi za matukio ya siku nzima kupita kichwani kwake.
******
Asubuhi ya Jumatatu,Longino aliwahi kuamka na kuweka vizuri mazingira yanayoizunguka nyumba yao na za majirani. Pia aliteka maji kwa ajili ya matumizi ya pale kwao na kazi nyingine za nyumbani. Hadi mida ya saa nne alishamaliza kazi nyingi ikiwemo kumpeleka mdogo wake shule.
Pale nyumbani alibaki peke yake kwa kuwa mama yake alienda kwenye shughuli zake zinazoendesha familia ile.
Longino aliona huo ndio muda muafaka wa kumuiita Mercy ili waongee kiutu uzima. Waongee kuhusu yale aliyoyafikiria jana.
Alikamata simu yake na kutafuta namba ya Mercy. Alipoipata akabofya kitufe cha kupigia simu na bila kinyongo nayo simu ikaita kwa sekunde kadhaa na baadae ilipokelewa na sauti tamu ya kimwana yule ilianza kupenyeza kwenye sikio la Longino. Kwa kuwa siku hiyo Mercy hakwenda shule, basi alikubali ombi la Longino haraka baada ya kuombwa aende anapoishi mwanaume yule.
Bila kujiuliza mara mbili, binti yule alijivuta hadi anapoishi Longino.
Longino alimkaribisha chumbani kwake kimwana yule ambaye naye mashalah hakuwa skrepa, japo yeye uzuri wake haukumfikia Subira.
"Ehe,nipe stori player." Mercy alianzisha maongezi baada ya kukaa katika kitanda cha Longino.
Mercy alishapazoea mule ndani hivyo hakuwa na wasiwasi hata kidogo kwa maamuzi yake ya kuingia na kuwa huru na chumba kile.
"Dah! Rafiki yako kanizingua tena jana." Longino aliyasema hayo huku ùso wake ukiwa unatabasamu kana kwamba haikumuuma.
"Lazima ingekuwa hivyo. Ila endelea kufight." Mercy alimpa moyo Longino.
"Aah,yaani niendelee kufight pasipo na wazo juu yangu? Kwa nini nisifight kwa àmbaye anaelewa umuhimu wangu." Maneno yalimtoka Longino.
Wakati huo alikuwa àmesimama karibu na mlango wa chumba chake.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Kama umeamua hivyo,hamna tatizo pia, sababu ni moyo ndiyo umekutuma, basi sidhani kama kuna tatizo." Mercy aliongea huku akiachia midomo yake kutanuka kwa tabasamu.
"Nimeishaamua na ndio maana upo hapa." Longino hakuwa nyuma kuyapamba maongezi yale.
"Kwa hiyo wataka niwe kuwadi tena?" Mercy aliuliza huku akionesha wazi kutokuwa tayari na suala la kutumwa kwa mwanamke mwingine.
"Nataka uwe kuwadi wa kichwa chako pmoja na moyo wako." Longino alifunguka lakini alitoa pambo la tabasamu na kuweka sura ya umaanishaji katika maongezi yale.
"Unamaana gani?" Swali lilimfata Longino.
"Hapa namaana kwamba." Longino akasogea karibu na kitanda chake na kukaa sambamba na kimwana yule japo hawakugusana.
"Namaana kwamba,ipe nafasi akili yako ili inifikirie na kunipa nafasi ya kuwa na wewe. Ufungue moyo wako na uweze kuingiza upendo wangu kwako." Longino alitoa maneno machache ambayo yaliingia vyema katika masikio ya Mercy.
Kimya kikatanda kidogo huku Mercy akiwa kichwa chini kama anatafakari maneno yale ya Longino.
Nimesema "Kama ànatafakari", kwa kuwa alikuwa hayatafakari maneno yale bali alijawa na furaha moyoni baada ya kutamkiwa maneno yale na kijana ambaye alikuwa anamuota kila ndoto kuwa mpenzi wake.
Mercy alitamani kunyanyua kichwa chake na kumgeukia Longino kisha kumkumbatia kwa nguvu, lakini alishindwa kutokana na aibu iliyochukua nafasi katika kila kichwa cha mwanamke wa Kitanzania aliyelelewa katika maadili halisi ya wazazi wake.
"Mercy." Sauti nzito kiasi ilimtoka Longino kumuita Mercy.
"Abee." Naye kwa sauti ya chini aliitika lakini akishindwa kumwangalia Longino usoni. Uso ambao ulikuwa si dhambi kama ukiuita ni mzuri au wa kitanashati.
"Nifikirie mwenzako. Usinifanyie vibaya. Najua nilikuwa namtaka rafiki yako na ninampenda kweli, lakini naomba upendo huo uhamie kwako. Nakuahidi nitakupenda sana kama ukinipa nafasi ya kuwa na wewe." Longino alisisitizia ombi lake huku akijaribu kuweka sauti yake iwe katika mbembelezo.
Mercy alizidi kukaa kimya huku uso wake akiudondosha chini tena kwa sababu ya àibu.
"Mercy."Safari hîi jina liliitwa huku Longino akiunyanyua uso wa binti yule kwa kushika kidevu chake na kumgeuzia upande alipo yeye.
Mercy alipomuangalia Longino machoni,yalikuwa mekundu kama mtu anayetaka kulia au analia kabisa. Moyo wake ukashindwa kuhimili macho yale ya Longino japo uso ulijikaza na kuendelea kuangalia. Mercy alimuonea huruma sana Longino, huruma ambao ndio unawaponza wanawake wengi katika dunia hii.
"Nakupenda." Neno moja lililomtoka Longino na kuufanya moyo wa Mercy kulia PAA.
Haukulia kwa kuwa ni mara ya kwanza kutamkiwa neno hilo na mtu baki. La! Hasha, alishasikia neno hilo kwenye vinywa vingi sana vya wanaume wa pale mtaani kwao na anaposoma. Ila ulishtuka kwa kuwa aliambiwa na mwanaume ambaye hakuwahi kufikiria kama ipo siku atayasema hayo.
Neno hilo la Longino,lilisindikizwa na busu dogo kwenda kwenye midomo ya Mercy.
Binti hakuwa na upinzani juu ya hilo. Na Longino alikuwa kamà mwenye kujaribu bahati yake aone kama atapata ukinzani.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kitendo hicho cha Mercy kutulia,kilimpa nafasi Longino ya kujivuta hadi karibu na ubavu wa Mercy ambapo alizungusha mikono yake kwenye shingo ya binti yule, kisha taratibu akapeleka midomo yake katika midomo ya Mercy. Kufika hapo midomo yao ikafunguka na ndimi zao zikatoka na kuanza kusabahiana huku mikono yao ikiwa inaoneana aibu kushikana hapa na pale.
Ni Longino ndiye alianza kumpeleka taratibu Mercy kwenye utamu wa raha, utamu ambao kama hujawahi kuuonja, basi utataka kila siku uuonje.
Longino alitoa mikono yake kwenye shingo ndefu kiasi kama ya twiga,aliyokuwa kabeba Mercy. Mikono hiyo ikahamia kwenye kifua cha mwanadada yule na kukutana na matiti madogo kiaina kama embe sindano lakini magumu kama rimao. Matiti yaliyotia mshawasha hata kwa kuyaangalia yakiwa yamevishwa nguo.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment