Chombezo : Usiku Wa Balaa
Sehemu Ya Tano (5)
ILIPOISHIA
“Nisamehe sana Rose. Haikuwa kusudi langu kukukimbia”. Nilijaribu kumpooza Rose.
“Haikuwa kusudi lako? Tena Ima ulinidanganya kwamba wanipenda. Baadaye unakuja fumaniwa na Nancy. Hivi ukoje wewe mwanaume?”. Rose aliongea kwa uchungu huku machozi yakimtiririka.
SASA ENDELEA
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nisamehe sana Rose”. Niliendelea kusisitiza msamaha.
“Yaani nikusamehe kirahisirahisi tu! Hebu tazama hali yangu nilivyo. Maisha magumu mpaka nakosa hela ya chakula cha mtoto wakati wewe baba yake upon a umenawiri sana!”.
Maneno ya Rose yalinichoma sana moyo. Rose alikuwa katika hali mbaya sana. Miguuni alikuwa amevaa ndala huku mavazi yake yakiwa hayatamaniki hata kidogo.
Niliingiza mkono mfukoni na kutoa kitita cha noti karibu milioni moja na laki saba ambazo nilipewa na Meselina kwa ajili ya kununulia samani za chumbani kwangu.
Nilimkabidhi pesa zote Rose na nikizidi kumwomba radhi kwa yale yote mabaya ambayo nilikuwa nimemtendea.
“Chukua pesa hizi Rose. Zitakusaidia wewe pamoja na mtoto. Mtunze vizuri mtoto. Nitakutafuta Rose”. Niliongea huku nikimfuta Rose machozi yaliyokuwa yakimtiririka.
Rose alishangaa sana kwa kupewa pesa nyingi kiasi kile. Hakuwahi kuziona katika maisha yake yote. Alinitazama usoni.
“Ahsante Ima. Nakuomba uje tulee mtoto wetu pamoja. Nakuhitaji Ima”. Rose aliongea.
“Usijali Rose. Nitakutafuta. Ngoja nikakamilishe kwanza maswala fulani”. Niliongea huku nikimpa business card yangu yenye nambari ya simu.
Baada ya hapo nikaondoka mitaa ile haraka sana. Niliona kumpa pesa Rose ndiyo namna nzuri ya kumsaidia kuliko kumchukua na kumleta nyumbani kwangu kwani angeliharibu mipango yangu mingi ya kupata warembo wa kustarehe nao.
**************
Leo ni siku nyingine ya Jumaipili ambapo majira haya ya saa nne usiku nimejifungia chumbani kwangu mimi na Meselina tukila raha za dunia. Mumewe Meselina alikuwa amesafiri sasa siku ya tatu na safari yake ingemchukua takribani siku saba.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mimi na Meselina tuliona huu ndio wasaa mzuri wa kuzitumbua raha za dunia pasipo kupata bughudha ya aina yoyote.
“Nakupenda sana Ima. Nataka uwe wangu pekee milele”. Meselina aliongea.
“Usijali Meselina. Mimi ni wako peke yako. Hakuna mwingine zaidi”. Nilimwambia Meselina.
“Lakini Ima mimi najua unaniongopea kwani nimesikia una wanawake wengi sana mtaani. Hata mimi mwenyewe nilizisikia sifa zako mtaani kwamba unayaweza sana mahaba ndiyo maana nikakutafuta”. Meselina aliongea.
“Hiyo ilikuwa ni zamani sana lakini tangu nikupate wewe mahabuba wangu nimeamua kutulia tuli kama maji ya mtungi”. Nilimwongopea Meselina kwani kiuhalisia mimi nilikuwa ni zaidi ya kiwembe.
Ghafla mlango uligongwa. Sikufahamu ni nani ambaye alikuwa akigonga mlango kwa wakati ule. Nikajaribu kukumbuka ratiba yangu kwa siku ile nikagundua kwamba sikuwa na miadi na mwanamke yeyote. Sasa ni nani ambaye alikuwa amefanya ziara ya kushtukiza kwa wakati ule? Sikupata jibu. Nikaona kabisa harufu ya hatari ilikuwa ikinukia.
“Ni nani huyo mpenzi?”. Meselina alihoji.
“Hata mimi sifahamu. Pengine anaweza kuwa ni jirani”. Nilimjibu huku hofu sasa ikiwa imetanda moyoni mwangu.
Niliamka na kwenda kuufungua mlango ili nijue ni nani ambaye alikuwa akigonga mlango kwa wakati ule.
“Hallow my sweet darling! Nilikumiss ndo maana nikaamua nije usiku huu nispend nawe”. Ilikuwa ni sauti ya Mariam mmoja ya wasichana ambao nilikuwa na mahusiano nao ambaye alikuwa amejaa pima katika mlango wa chumba changu.
****************
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mbona hukunipigia Mariam?”. Niliongea nikijaribu kumzuia kuingia ndani.
“Kwani kuna tatizo gani Ima mimi kuja sasa hivi kwako. Mbona siku zote huwa nafanya hivi na huwa hulalamiki”. Mariam aliongea hayo huku akiwa amenichoriopoka na kuingia ndani.
Salaaaale! Mariam hakuamini kile ambacho alikuwa akikiona ndani ya chumba changu kwa wakati ule. Macho yake yalimshuhudia Meselina akiwa amejilaza juu ya kitanda akiwa mtupu kama alivyozaliwa.
“Ni nani huyu mbwa Ima?”. Mariam alihoji kwa ghadhabu kubwa.
“Tulia Mariam. Nitakueleza kila kitu”.
“Nani mbwa wewe mwanamke? Nitakupasua pasua”. Meselina naye alipagawa huku akishuka chini kutoka kitandani.
“Shika adabu yako wewe Malaya mkubwa usiye na haya!”. Mariam alifoka.
“Tulia Mariam”. Nilijaribu kumtuliza Mariam kwani nilimfahamu fika tabia yake kwamba ni hatari sana.
“Leo lazima nikuonyeshe kwamba mimi ni nani”. Meselina aliongea akiwa ameshuka kitandani na kumvaa Mariam.
Pale sebuleni sasa pakawa ni kindumbwendumbwe. Ukawa ni USIKU WA BALAA. Sikujua nitatua vipi ugomvi wa wanawake hawa wenye jazba.
Sasa nikamkumbuka Rose. Nikaona ni vema ningetulia na Rose na tulee mtoto wetu. Sasa ona hawa wanawake wanavyodhalilishana na kuniletea matatizo mimi.
Ugomvi ukaendelea huku hawa wanawake wakipigana na kutoleana maneno makali sana. Nilijaribu kuwaamulia lakini sikuweza kwani walinizidi ubavu.
Ghafla Mariam alikiona kisu ambacho kilikuwa juu ya meza ya kioo ambayo ilikuwa pale sebuleni. Kisu kile nilikuwa namenyea machungwa mchana na sikupata wasaa wa kukitoa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nikiwa bado nimeduwaa nilishtuka pale nilipoisikia sauti ya uchungu ya Meselina huku macho akiwa ameyatoa pima. Kisu chote kile kilikuwa kimezama tumboni kwa Meselina na kubaki mpini tu.
Meselina aliendelea kupiga kelele na kuanguka chini huku akiwa amekishikilia kile kisu. Aligalagala pale chini na hatimaye akakata roho kwa uchungu.
“Nimeuaaaaa! Ima nimeuaaaa!”. Ilikuwa ni sauti ya makelele ya Mariam ambaye alianza kulia mara baada ya kugundua madhara aliyoyasabibsiha kwa Meselina. Alikuwa ameutoa uhai wa mtu.
Mariam alijaribu kukimbia lakini aliteleza na kichwa chake kikajigonga katika ile meza ya kioo na kusababisha jeraha kubwa sana kichwani ambalo lilipelekea mauti yake.
Moyo wangu ulishtuka sana. Sikufahamu nifanye nini kwa wakati ule. Ndani ya chumba changu kulikuwa na miili miwili ya watu ambao walikuwa wafu tayari. Nilichanganyikiwa sana na kujuta sana.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Niliijutia tabia yangu ya kupenda wasichana ambayo leo hii ilikuwa imeniachia balaa kubwa la kesi ya mauaji. Niliamini ya kwamba majuto ni mjukuu na sikuwa na namna yoyote ya kufanya katika kuninusuru na balaa lile. Hakika ule ulikuwa ni USIKU WA BALAA ambao sitakuja kuusahau katika maisha yangu.
************* MWISHO **************
0 comments:
Post a Comment