Search This Blog

Monday, October 24, 2022

CHACHANDU ZA BEKA WA TANGA - 1

 





    IMEANDIKWA NA : GLOBAL PUBLISHERS



    *********************************************************************************



    Chombezo : Chachandu Za Beka Wa Tanga

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    Akiwa amefikisha umri wa kubalehe, Beka anayetokea Tanga mjini hakuwa bize na masuala ya mabinti kama vijana wa umri wake ambao walikuwa wanakwenda puta kuvifukuzia vidosho.



    Mbaya zaidi vijana hao watukutu walikuwa wakiwatokea mpaka dada zao, walichokihitaji ni kumaliza tamaa za miili yao. " Mama Beka , kuna jambo linanitatiza ni vizuri tulizungumze," baba Beka almaarufu kwa jina la Mzee Kibandiko alimwambia mkewe. " Na wewe umeanza , yaani kitendo cha siku mbili hizi kukwambia mgongo unanisumbua unaona shida!" mama Beka alimwambia mumewe . " Hahahaha!" baba Beka alicheka. " Sasa unacheka nini?" mama huyo alihoji.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kufuatia mkewe kuuliza sababu ya kucheka, Mzee Kibandiko aliyepewa jina hilo kutokana na kupenda kuvaa kibalaghashia kwa staili ya kukiegesha kichwani alimwambia hakuwa na maana aliyoitafsiri. " Sasa unamaanisha nini kama siyo kugeuza maneno baada ya kuona nimekubana ?" mkewe alimwuliza . Mzee Kibandiko alicheka na kumweleza kwamba jambo alilotaka kumuuliza ni kuhusiana na kijana wao Beka . " Umeanza, mtoto kafanyaje ?" mama huyo alihoji . " Siyo kafanyaje , we unamuona yupo sawa na wenzake ?" Mzee Kibandiko alimwuliza mkewe. " Kwani ana tofauti gani, hajafanyiwa suna au hasomi shule nzuri ?" mama huyo alimkomalia mumewe kwa maswali.



    Mumewe ambaye kicheko chake kilikuwa karibu , alicheka na kumwambia mkewe kwamba alichotaka kumwambia siyo suala la Beka kufanyiwa suna au kusoma shule nzuri isipokuwa ni zaidi ya hayo . " Eh ! Makubwa ! Madogo yana nafuu!" mama huyo alimwambia mumewe . " Tena tusipokuwa makini yatakuwa makubwa haswa !" Mzee Kibandiko alimwambia mkewe.



    Mama huyo alipoona mumewe hafunguki kuhusu alichotaka kumweleza alimwambia hakuwa na lolote zaidi ya kulilia chakula cha usiku ambacho zilipita siku tatu bila kukitafuna. Mzee Kibandiko alicheka lakini kabla hajamwambia hisia alizokuwanazo juu ya kijana wao , mlango wa sebuleni ulifunguliwa Beka aliyetoka shuleni akaingia. " Shikamoo baba, shikamoo mama?" aliwaamkia wazazi wake . " Marhaba mwanangu za shule?" mama mtu alimwuliza mwanaye. " Nzuri mama, " Beka aliitikia. " Vipi we mswahili za huko shuleni kwenu ?" baba yake alimsabahi . " Nzuri tu , pole kwa kazi !" Beka aliyekuwa kidato cha kwanza alimpa pole baba yake kisha akaelekea chumbani kubadili nguo.



    Beka aliyekuwa handsome boy alipobadili nguo alitoka na kwenda sebuleni na kunyoosha sehemu ya chakula . Kabla hajafanya chochote, mama yake alimwambia kwenye poti kulikuwa na wali isipokuwa mboga, akamwambia asuburi akaipashe moto . Mama huyo aliinuka akaenda jikoni akawasha jiko la Mchina akawa anapasha moto mboga, wakati huo Beka alikuwa akisoma kipande cha Gazeti la Ijumaa Wikienda ambacho mama yake alifungiwa bidhaa alipotoka sokoni.



    Huyu Kulwa Mwaibale na hizi stori zake za mapenzi sijui huwa anazitoa wapi ? Mfano hii ya Chikoko wa Mtwara inafurahisha sana ! Beka alijisemea moyoni wakati akisoma kipande hicho cha gazeti kilichokuwa na chombezo la Chikoko wa Mtwara lilomuhusu kijana aliyekuwa akipenda sana masuala ya mademu badala ya masomo . Wakati akiendelea kusoma , mama yake alirejea akiwa na mboga aliyoipasha moto na kumuwekea kisha mama huyo alikwenda kuketi alipokuwa mumewe. " Sasa mama Beka mimi naona nilichotaka kukueleza tutakiongea baadaye muda huu ngoja niende kwa baba Tunu kuna jambo nataka kuongea naye, " mzee huyo alimwambia mkewe. Mimi nilijua huna lolote zaidi ya kutaka naiii , lakini ngoja nisubiri utakaporudi nisikie unachotaka kuniambia, " mama huyo alimwambia mumewe.



    Mzee Kibandiko ambaye kucheka ilikuwa kawaida yake alicheka na kumwambia amsubiri kisha aliomba ampikie tambi. " Na wewe na hizo tambi , hazipiti siku tatu lazima ule tambi, hamia basi huko Unguja ukazile mpaka uchoke!" mkewe alimtania.



    Mzee huyo alipoondoka mkewe huku nyuma akajaribu kuchekecha akili kujua mwanaye alikuwa na tatizo gani lakini hakugundua . " Sijui atakuwa kafanyaje lakini kama anamtuhumu kwa mambo mabaya nitamtetea Beka wangu, kwanza hana makundi yeye muda wote ni kujisomea na kunisaidia kazi za nyumbani , akitoka ni kwenda kucheza mpira tu !" mama huyo aliwaza..



    MPENZI msomaji , sehemu iliyopita niliishia pale mama yake Beka alipokuwa akijiuliza jambo ambalo mumewe alitaka kumwambia kuhusiana na kijana wao Beka lakini hakupata jibu kwa sababu kijana huyo alikuwa mtulivu sana. Je , nini kiliendelea? Songa Nayo Wakati Mzee Kibandiko akielekea nyumbani kwa rafiki yake baba Tunu , akawa anajisemea moyoni kwamba alihisi Beka alikuwa na matatizo kwa sababu hakuwahi kumuona akipiga stori na wasichana kama walivyofanya wenzake . “ Huyu mtoto ananishangaza sana mbona tangu akiwa mdogo anaonekana hana tatizo, asubuhi akiamka jogoo wake huchangamka kama kawaida , inakuwaje hajishughulishi na mabinti kama akina Hussein na Rajabu?” Mzee huyo alijiuliza . CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/-- Mzee Kibandiko ambaye enzi za ujana wake alikuwa moto wa kuotea mbali kwa mademu kwani akiwa kidato cha pili tu tayari aliwapiga mimba wasichana wawili, aliapa kumchunguza kwa kina Beka ili kujua kama alikuwa na tatizo amtafutie tiba . “ Beka ndicho kidume changu pekee cha mbegu , nikizembea hatutawaona watoto wake , lazima nipigane , mtoto gani hana habari kabisa na wasichana wazuri kama akina Salma na Prisca ?” mzee huyo aliwaza . Kufuatia kutumia muda mwingi kutafakari tabia ya mwanaye , alishtukia amefika nyumbani kwa baba Tunu rafiki yake wa siku nyingi . Bahati nzuri alimkuta baba Tunu na mkewe wakiwa wameketi chini ya mti wa muarobaini wanapiga stori, wakamkaribisha kwa bashasha. “ Na nyie mnavyopenda kuwa pamoja utafikiri mumeoana juzi ?” Mzee Kibandiko aliwatania wenyeji wake baada ya kukaribishwa . “ Kwa taarifa yako , jinsi tunavyozeeka penzi letu ndivyo linavyonoga, mama Tunu asiponiona anakosa raha nami nisipomuona nammisi sana!” Baba Tunu alimwambia rafiki yake huyo, wakacheka . Baada ya baba Beka kukaa kwenye kiti , alimuuliza rafiki yake kuhusu maendeleo yake kazini akamwambia kwamba hakukuwa kuzuri. “ Kuna tatizo gani?” Alimwuliza. Rafiki yake huyo alimfahamisha kwamba bosi wao alifumwa akifanya mapenzi na mke wa mtu ofisini kwake na kwamba alikong’ otwa hadi kuvunjwa mkono. “ Sasa hilo ni tatizo? Hiyo ndiyo dawa ya mabosi wapenda michepuko na wake za watu mimi nimeipenda sana hiyo !” Mzee Kibandiko aliwaambia, wakacheka . Baba Tunu alimwambia kwamba kitendo cha bosi wao ambaye alikuwa akiendekeza sana michepuko kufumaniwa kiliwafurahisha wengi lakini tatizo ni kwamba tangu alipobambwa hakufika ofisi hivyo hawakupata mshahara . “ Kwani yeye kufumaniwa inahusiana nini na masuala ya mishahara yenu ?” Mzee Kibandiko alihoji . Baba Tunu alimwambia kutokana na mfumo wa kampuni yao, hakuna mtu mwingine anayesaini cheki ya mishahara zaidi ya bosi wao . “ Kama ni hivyo hilo ni tatizo , pole sana ndugu yangu, ” mzee Kibandiko alimpa pole rafiki yake kisha alifungua waleti akachomoa wekundu watatu wa msimbazi na kumpatia. “ Kaka yaani ujio wako ni kama Mungu kakuleta, hapa tulikuwa tunaumiza vichwa leo hadi kesho tutaishije na watoto maana sikuwa na kitu kabisa na ndani hatuna hata punje ya mchele ,” baba Tunu alimwambia rafiki yake . CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “ Hakuna tatizo ndugu yangu, mambo yako yakiwa safi utanirudishia shilingi ishirini inayobaki ikaushie ,” Mzee Kibandiko alimwambia baba Tunu . Mke wa baba Tunu alimshukuru sana shemeji yake , kwa vile alipata fedha aliwaaga akaelekea sokoni kununua chakula . “ Kaka siyo siri, umeokoa jahazi lisizame nilikuwa nachekecha akili nikamkope nani, yaani asante sana ndugu yangu, ” baba Tunu alimwambia rafikiye . Rafiki yake huyo alipomshukuru , Mzee Kibandiko alimweleza alikuwa amemfuata ili amsaidie jambo lililokuwa likimtatiza . “ Eh ! Nini tena?” Baba Tunu alimwuliza . “ Si mwanao Beka ?” alimwambia. Baba Tunu aliyekuwa akimuona kijana wake Said aliyekuwa katika kipindi cha balehe alivyokuwa akihaha kuwafukuzia mademu akajua Beka ambaye naye alikuwa katika kipindi hicho kishamdungua mtu mimba . “ Vipi kisha mtundika mtu mimba nini? Maana Said naye anavyohaha kuwafukuzia mabinti kama fisi aliyeona mzoga wa swala, ” mzee huyo alimwambia rafiki yake , wakacheka . “ Si afadhali Said anayehaha , kidume cha mbegu kinatakiwa kuwa hivyo , ” Mzee Kibandiko alimwambia rafikiye . “ Sasa mtoto kafanyaje , kaanza udokozi nini?” Baba Tunu aliyekuwa na shauku ya kujua kilichomsibu rafiki yake akamuuliza . itaendelea hapa hapa.... Mpenzi msomaji, sehemu iliyopita niliishia pale Mzee Kibandiko baba wa Beka alipomweleza rafiki yake baba Tunu kuhusiana na tatizo la kijana wake ambalo alikuwa bado hajaliweka wazi, rafiki yake huyo alimwuliza alikuwa kaanza udokozi? Je, baada ya kumwuliza hivyo alijibiwa nini? Tuwe pamoja ufuatia kuulizwa hivyo, alimfahamisha kwamba hakuwa mdokozi isipokuwa alihisi alikuwa na tatizo kubwa mwilini mwake. “Kaambukizwa virusi vya ukimwi nini?” Baba Tunu alimwuliza. Baada ya rafiki yake kumuuliza hivyo, Mzee Kibandiko alimwambia hakuwa na virusi isipokuwa alihisi hakuwa kidume cha mbegu.“Unaposema siyo kidume cha mbegu unamaanisha jogoo wake hawiki?” Baba Tunu alimwuliza. “Haswa, tatizo hilo linanikosesha raha sana!” Mzee Kibandiko alimwambia rafiki yake. “Wewe umejuaje kama jogoo wake hawiki?” Baba Tunu aliendelea kumwuliza. Alipoulizwa hivyo, alimwambia alijaribu kumchunguza kwa muda mrefu kama alikuwa na rafiki wa kike lakini hakuambulia kitu. Kauli hiyo ilimfanya rafiki yake kuangua kicheko na kumweleza katika jamii wapo vijana ambao hawana matatizo kiafya ila hawana habari na mambo ya wasichana. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Napingana na kauli yako, kwa vijana wa kizazi hiki cha doticom labda katika kumi atakuwepo mmoja na akichunguzwa atakuwa na tatizo flani lakini katika hali ya kawaida haiwezekani,” Mzee Kibandiko alimwambia rafiki yake ambaye alicheka. Kutokana na kauli hiyo, baba Tunu alimfahamisha rafiki yake huyo kwamba asiwe na mashaka na afya ya kijana wake kwani hakuwa na tatizo na vijana waliotulia wapo. “Kaka siku zote maji hufuata mkondo, sasa inakuwaje kwa umri alionao Beka asiwe na pilika za mabinti? Nashindwa kumuelewa huyu kijana,” Mzee Kibandiko alimwambia rafiki yake. “Kwa hiyo ungekuwa na furaha kama ungemuona anawashughulikia mabinti wa wenzako si ndiyo?” Baba Tunu alimwuliza. “Tena sana, mimi nilipokuwa kama yeye nilikuwa balaa ndicho kipindi nilichowadunga mimba mama wa mwanangu Jamila na mama wa Renatha, si unaona wanavyonisaidia hivi sasa?” Mzee Kibandiko alimwambia rafiki yake, wakacheka. Rafiki yake huyo alisisitiza kwamba Beka hakuwa na tatizo na amshukuru Mungu kumpa kijana mpole, aliyetulia, aliyezingatia masomo na kuwasaidia kazi za nyumbani.“Kaka unachonieleza ni sawa lakini pamoja na kuzingatia masomo na kutusaidia kazi za nyumbani, inafurahisha kama unamuona mwanao anapiga stori na vijana wenzake wa kike tena inafurahisha zaidi akiwa anazungumza nao hata chumbani kwake,” Mzee Kibandiko alimwambia rafiki yake. “Kaka wewe shukuru kuwa na kijana aliyetulia, mwenzako Said anatusumbua sana na masuala ya wanawake jana tu kapigana na wenzake, kisa kugombea msichana,” baba Tunu alimwambia. “Huyo sasa ndiye mwanaume, kijana wa kiume lazima awe na mpenzi lakini siyo Beka yeye akishamaliza kazi zake ni ndani tu kama mwari,” Mzee Kibandiko aliendelea kulalamika. Mwishoni alimuomba ushauri rafiki yake huyo kama alikuwa akimfahamu mtaalam yeyote wa tiba za jadi amwelekeze ili ampeleke kijana wake aliyeamini alikuwa na tatizo. “Kaka naomba uelewe Beka hana tatizo, ukitaka kubaini hilo kesho alfajiri mgongee chumbani kwake, akifungua mlango tupia macho eneo la jogoo wake ukiona amefura ujue hana tatizo,” baba Tunu alimwambia rafikiye, wakacheka. “Hilo nalo neno kaka, nitafanya hivyo,” Mzee Kibandiko alimwambia rafikiye, wakacheka. Wakati marafiki hao wakiendelea kuzungumza, mke wa baba Tunu alirejea CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ kutoka sokoni, aliwasalimia na kupita mbele yao akawa anaelekea ndani. Kwa kuwa mzee Kibandiko na mke wa baba Tunu kiasili ni watani, baba Beka alimuita ambapo mama huyo aligeuka kumsikiliza. “Shemeji, hongera na mshukuru mkubwa wangu kwa kukulisha vizuri maana umefungashia si kidogo, ukitembea ni tentemente hadi mzee anajisikia raha!”Mzee Kibandiko alimtania shemeji yake. “Na wewe baba Beka hukui tu, yaani mambo yako ni yaleyale ya mwaka arobaini na saba,” mama Tunu alimwambia Mzee Kibandiko, wote wakacheka. ILIPOISHIA :Mpenzi msomaji sehemu iliyopita niliishia pale baba Tunu alipomeza funda la mate baada ya kulitazama wowowo la mkewe lililokuwa likitikisika kulia na kushoto wakati mama huyo alipokuwa akienda ndani na kujisemea moyoni kwamba , kufuatia kummisi sana lazima usiku wangenaniliuu . Je , kilijiri nini? Songa mbele Baada ya mama Tunu kuingia ndani , marafiki hao waliendelea na maongezi kubwa baba Tunu alimsisitiza rafiki yake huyo kufanya kama alivyomshauri ili kubaini kama jogoo wa Beka alikuwa anawika au la!“Kaka kazi hiyo nitaifanya alfajiri ya kesho , lazima nijue kama mwanangu yupo salama au mtoto si riziki , wewe mtoto gani nyumba zote zilizotuzunguka kuna mabinti wazuri wana maziwa ya kuchoma , yeye hana habari nao, ” Mzee Kibandiko alimwambia rafiki yake . Kufuatia kauli hiyo , baba Tunu alicheka na kumwambia rafiki yake huyo hakutulia kabisa kwani badala ya kufurahi mwanaye alitulia yeye alikuwa anataka awe kiwembe kwa mademu. “ Kaka we cheka lakini ukweli ndiyo huo, mtoto wa kiume lazima aoneshe urijali wake mapema ndiyo furaha ya wazazi, ” baba Beka alizidi kutetea hoja yake . Baada ya kumaliza kuzungumza ishu ya Beka iliyowachukuwa muda mrefu , mama Tunu aliyemaliza kupika aliwakaribisha ndani kwa ajili ya kupata mlo. Marafiki hao wakiwa wamejumuika mezani kwa ajili ya mlo , baba Beka alimwita mama Tunu aliyekuwa anakula jikoni . “ Ila wewe mwanamke unajua kupika , hivi nani alikufundisha kukaangiza namna hii ? maana chakula ni kitamu zaidi ya vitamu !” Baba Beka alimwuliza . “ Yaani wewe baba Beka wewe , kuniita kote huko nilifikiri unataka kuniambia jambo la maana kumbe utani tu , hivi wewe mwanaume utakua lini ?” Mama huyo alimwuliza . “ Sasa mama nimekosea nini? Kukufagilia kwa kujua kukaangiza ndiyo tatizo ? Kweli nimejua sababu ya kaka yangu kuwa na kitambi , ” baba Beka alimwambia shemeji , wakacheka . “ Kama umependa chakula changu CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ nashukuru , mlete mkeo nimfundishe namna ya kukupikia , ” mama huyo alimweleza baba Beka na kuelekea jikoni huku akicheka. Walipomaliza kula , Baba Beka aliwaaga wenyeji wake ambapo rafiki yake alimsindikiza hadi nje wakaagana akarejea kwake. Alipofika nyumbani kwake, mkewe alimkaribisha chakula lakini alimwambia alikuwa ameshiba alikotoka . “ Yaani baba Beka hapo ndipo unaponikwaza mwenzako, nimekupikia wali wa nazi unaoupenda na samaki ili ufurahie kuwa nyumbani unaniambia umeshiba , ” mkewe alilalamika. Hata hivyo , baada ya mumewe kumuomba msamaha na kumfahamisha kwamba alikula kwa rafiki yake baba Tunu , mkewe akawa mpole . Wakiwa wameketi sebuleni huku Beka akiwa ametoka, mkewe aliyekuwa na hamu ya kujua jambo ambalo mumewe alitaka kumweleza alimuomba afunguke. Kufuatia kuambiwa hivyo , alimuomba kama hatajali amweleze usiku lakini mama huyo alimsihi amwambie kwani moyo wake ulikuwa juujuu. “ Kwani mwanao katoka ?” Baba Beka alimwuliza mkewe. Mkewe alimwambia hakuwepo na kuhoji kama angekuwepo angezuia nini, mumewe alimwambia hakuhitaji asikie aliyotaka kumweleza kuhusu yeye . “ Kwani mtoto kafanyaje mbona hutaki kuniambia?” Mama Beka alimwuliza mumewe . “ Hebu twende chumbani nafikiri tutakuwa huru zaidi , ” Baba Beka alimwambia mkewe kisha aliinuka na kuelekea chumbani. Mkewe aliyeacha mlango wa jikoni wazi , aliinuka na kwenda kuufunga kuhofia paka mmoja msumbufu angekula samaki aliowaandaa. Baba Beka licha ya umri kusogea alikuwa mtundu sana, alipoingia chumbani alivua nguo zote na kubaki kama alivyokuja duniani akalala chali. Mkewe akiwa hana hili wala lile alipofungua mlango na kumuona mumewe alivyokuwa, akaanza kucheka na kumwambia: Mpenzi msomaji, sehemu iliyopita niliishia pale Mzee Kibandiko ambaye alikuwa mtundu sana alipoingia chumbani kwake na kuvua nguo zote na kubaki kama alivyokuja duniani. Mkewe alipoingia aliishia kucheka na kumwuliza : “ Hivi wewe baba Beka utakua lini ? Kwa mfano mwanao akiingia ghafla na kukukuta hivyo utajisikiaje?” Je, baba Beka alijibu nini? Songa mdogomdogoufuatia swali aliloulizwa na mkewe, mzee huyo alicheka na kumjibu: “ Ndiyo atakoma kuingia chumbani kwa wazazi wake bila kubisha hodi. ” “ Ila siyo vizuri unavyofanya ipo siku CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ utaumbuka!” mkewe alimwambia mumewe na kuketi kitandani . Kutokana na mumewe ‘ mkuu wake wa kaya ’ kuchachamaa, mkewe alipokiona chombo kilivyokuwa , akapata hisia za yale mambo yetu . Mama huyo alimwambia mumewe kwamba alivyofanya haikuwa vizuri, ambapo mumewe alimwuliza kosa lake lilikuwa nini?“Si hayo mambo yako , wewe ukishinda nyumbani huwezi kutulia na kusubiri usiku , ” mkewe alimwambia. “ Wewe ukishikwa na njaa na chakula kipo , utasubiri mpaka usiku ?” Baba Beka alimwuliza mkewe. Kutokana na swali hilo, mama Beka alicheka na kumwambia alikuwa akijiendekeza na kumwambia muda ule haukuwa muafaka kwa chakula cha usiku kwa sababu kijana wao angeweza kufika muda wowote. “ Akifika na kugundua tupo huku chumbani atajua tunacheza kombolela ya kikubwa, ” mzee huyo alimjibu mkewe. Mama huyo ambaye tayari akili yake iliachana na mambo mengine kutokana na hisia alizokuwanazo , aliinuka na kwenda kufunga mlango kwa funguo. Alipofanya hivyo , alijongea karibu na kitanda chao akaanza kuvua nguo na alipobakiza ya mwisho , mumewe akamwambia ‘ stop ’ . “ Sasa nistop nini, umegahiri ?” mkewe akamwuliza . “ Simaanishi hivyo bwana, hebu sogea huku, ” mzee huyo alimwambia mkewe. Mkewe ambaye naye alikuwa kaumbika na kujaaliwa kuwa na nido zilizosimama wima utafikiri hakuwahi kunyonyesha , alijongea ile anataka kulala mumewe alimdaka na kumvutia kifuani kwake . Licha ya mshua huyo umri kwenda flani hivi mambo aliyaweza , baada ya kumtuliza mkewe kifuani alimletea mautundu ya kufa mtu, mama Beka akaishiwa nguvu . Mzee huyo ambaye zilipita siku kadhaa bila kula tunda la mti wa katikati , hakufanya ajizi alimalizia kukitoa kile kiwalo cha mwisho na kujilia tende kwa raha zake . “ Ila wewe baba Beka wewe mh !” mkewe ambaye alifikishwa Kigoma mwisho wa reli alimwambia. “ Nimefanyaje?” Baba Beka alimwuliza mamsapu wake . “ Yaani kadiri unavyozeeka ndiyo unakuwa naniii” mkewe alishindwa kumalizia sentesi yake akawa anacheka . “ Umeona eh , sasa ungenibania ungefurahi namna hiyo ?” mzee huyo alimwambia mkewe. Wanandoa hao waliendelea kupiga stori za hapa na pale ndipo mama Beka akamwomba mumewe amwambie jambo alilotaka kumwambia. “ Oke mke wangu uliyeumbwa ukaumbika , CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ unayejua kunitoa uchovu ninapokuwa nimechoka , unayenipikia chakula kitamu ninapokuwa na njaa na unayenipa chakula cha usiku hata mchana, ” mzee huyo alimwambia mkewe, wakacheka . “ Umeanza utani wako , ningejua ningekubania , ” mama huyo alimwambia mkewe. “ Hahahahaa, usingeweza kwani nakujua sana unavyokuwa unapomuona mkuu wa kaya akiwa amekasirika ,” Mzee Kibandiko alimwambia mkewe wakacheka . “ Haya niambie sasa hilo jambo la mtoto !” mama Beka alimwambia mumewe . Kufuatia kubanwa, mzee huyo alimwuliza mkewe kama aliwahi kumuona Beka akiwa bize na mabinti. “ Kivipi?” mkewe alimwuliza . “ Wewe nijibu kwanza swali langu!” Kufuatia mama huyo kuulizwa hivyo , alimfahamisha mumewe kwamba mbona alikuwa akizungumza nao na hata asubuhi ya siku hiyo alimuona amesimama na Sofia mtoto wa jirani yao. “ Na wewe mama Beka , mimi nachotaka kujua ni zaidi ya kuzungumza nao, ” mzee huyo alimwambia mkewe. “ Sasa hapo ndiyo sikuelewi , zaidi ya kuzungumza nao ndiyo kufanyaje ?” mama huyo alimwuliza . Kutokana na swali hilo, mumewe alimwambia si alikuwa amekua , je aliwahi kumuona na mkamwana wake ! Kutokana na kauli hiyo mkewe alimuelewa akamjia juu kwamba hakutegemea kama angemweleza upuuzi wa namna ile . “ Mama Beka , mimi nakuambia jambo la maana kuhusu kijana wetu unasema ni upuuzi, mimi ningekuwa mzembemzembe kama yeye unafikiri ningekuoa na kumzaa yeye ?” Baba Beka alihoji kwa hasira . Mpenzi msomaji , sehemu iliyopita niliishia pale baba Beka alipomjia juu mkewe aliyemuita mpuuzi kufuatia mzee huyo kumuuliza kama aliwahi kumuona kijana wao akiwa na mkamwana wao yaani mpenzi . Je , kilifuatia nini? Ungana nami Mama Beka , nakuambia jambo la maana kuhusu kijana wetu unasema ni upuuzi, mimi ningekuwa mzembemzembe kama yeye unafikiri ningekuoa na kumzaa yeye ?” Baba Beka alihoji kwa hasira . Licha ya mama huyo kugundua mumewe alikuwa amekasirishwa na kauli yake , hakujishusha badala yake alisisitiza kwamba alikosea kumuuliza kama aliwahi kumuona Beka akiwa na mpenzi . “ Mimi sijakosea , nipo sahihi mke wangu kwani sitaki aje awe mtoto si riziki !” Baba Beka alimwambia mkewe. “ Awe mtoto si riziki kwa sababu gani ? Hivi mbona unamchulia mtoto mambo mabaya ?” Mama Beka alihoji . CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Kufuatia mkewe kutoa kauli hiyo , mzee Kibandiko alimweleza kuwa vijana wote wanaojihusisha na vitendo vya kishoga dalili zilionekana tangu mapema. “ Unajua sikuelewi mume wangu, sasa Beka ana dalili gani za mambo hayo?” mkewe alimwuliza . “ Sasa kama mtoto hajishughulishi na masuala ya wanawake kama wanavyofanya wenzake hapo kuna nini kama siyo majanga ?” Mzee Kibandiko alimwuliza mkewe. Mama huyo alimwambia mumewe amshukuru Mungu kumjaalia utulivu Beka kwani kuna vijana wamekuwa wasumbufu kwenye familia zao mpaka wazazi wao wamewachoka. “ Kama ni usumbufu wa kutoka na wenzao wa kike huo hauna tatizo, napenda kumuona kijana wangu anachangamka kama enzi zangu si unakumbuka mapigo yangu mama Beka ?” mzee huyo alimwambia mkewe. Ingawa mkewe awali hakupendezwa na maneno ya mumewe , kufuatia kuulizwa kama alikumbuka mapigo ya mumewe enzi zao alijikuta akicheka peke yake . “ Ila baba Beka una maneno mengi sana, hapa tunamzungumzia Beka siyo mambo yetu ya zamani, ” mama huyo alimwambia mumewe . Wanandoa hao walizungumza mengi lakini kubwa mama Beka alimsihi mumewe aachane na mawazo mabaya kuhusu kijana wao na amshukuru Mungu kuwajalia kijana aliyetulia. “ Huo ni mtazamo wako , mimi nitafuatilia kujua kama ni mzima au ana tatizo kwani Beka ndiyo jembe ninalolitegemea hivyo lazima lijue kulima na kung ’oa visiki ,” mzee huyo alimwambia mkewe, wakacheka . Kwa kuwa mama huyo alikuwa na majukumu mengine ya nyumbani , alimuacha mumewe akiwa amelala akaelekea bafuni kuoga. “ Hawa wanawake hawajui tu , mtoto wa kiume aliyepevuka lazima awachangamkie wenzake wa kike , ” baba Beka alijisemea moyoni baada ya mkewe kuondoka. Baada ya saa moja mbele , mkewe aliingia chumbani na kumwambia mumewe kwamba maji ya kuoga yalikuwa tayari pamoja na chai ya tangawizi aliyokuwa akipenda kunywa jioni . Mzee huyo ambaye hadi muda ule alikuwa bado hana nguo mwilini aliinuka , mkewe alipotupia macho sehemu ‘muhimu’ na kumuona mkuu wa kaya alivyokuwa amelala doro akaanza kucheka. “ Sasa unacheka nini? Huo ndiyo uchokozi!” mzee huyo alimwambia mkewe aliyekuwa anaendelea kucheka. Alimpofikia alimkumbatia kwa kuzungusha mikono katika kiuno chake na kumbusu shavuni mmwaaa , hakuishia hapo akawa anaziminya hipsi zake zilizokwenda shule. Mpenzi msomaji, miongoni mwa wanawake CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ ambao hukosa ustahimilivu wanapobusiwa na kushikwa sehemu za mapaja ni mama Beka , alipofanyiwa hivyo alipagawa kabisa . Mumewe aliyemfanyia vile kwa makusudi hakuishia kumshika tu maeneo hayo, aliingiza mkono wake kwenye blauzi aliyovaa na kushika nido zake zenye ukubwa wa wastani , sijui akawa anayafanyaje, mama wa watu akawa anahema. Wakati akimfanyia vimbwanga hivyo vya mahabati, naye damu ilimchemka si kidogo akajisemea moyoni kwamba : “ Mama Beka huna ujanja lazima tulicheze segere tena. ” Alichokifanya, alimvutia mkewe kwenye uwanja wa fundi seremala na kumketisha akaenda kufunga mlango na kurejea tena kwa ‘ wife’ wake . Wawili hao wakiwa tayari kwa kipute cha pili walikatishwa na Beka aliyeingia ndani na kuanza kumwita mama yake , kabla mama yake hajaitika mumewe alimuwahi. “ Beka unasemaje ?” baba yake alimwuliza . Beka alimwuliza baba yake ni wapi alikokuwa mama yake ndipo mzee huyo ambaye alifahamu kama angemwambia walikuwa wote chumbani angewaharibia dili lao la kupeana tende tamu za Uarabuni, akamdanganya kwamba alitoka. Kumuondoa kabisa pale nyumbani , alimtuma aende kwa shangazi yake Pili akamwambie kesho akirudi kutoka kazini alihitaji kuzungumza naye hivyo afike pale nyumbani . Kwa kuwa Beka alikuwa akipenda sana kuendesha baiskeli, alimwuliza baba yake kama atumie usafiri huo au angempa nauli ili apande gari . ìNenda na baiskeli yako ila uwe muangarifu barabarani kwani magari ni mengi , î mzee huyo alimwambia kijana wake . Mzee huyo alimruhusu atumie usafiri huo kwa vile alijua angechelewa kurudi kwani watoto wa dada yake walikuwa wakipenda sana kuendesha baiskeli hivyo baada ya Beka kufika kule wangeanza kuendesha. Beka alipoondoka , mzee huyo alimkabili mkewe kwa kumpagawisha mpaka mama wa watu akawa hoi , hakumchelewesha akampa mkomboti wa haja utafikiri muda mfupi uliopita hawakuwa pamoja . Kwa kuwa Beka alikuwa akipenda sana kuendesha baiskeli, alimwuliza baba yake kama atumie usafiri huo au angempa nauli ili apande gari.“Nenda na baiskeli yako ila uwe muangarifu barabarani kwani magari ni mengi,” mzee huyo alimwambia kijana wake. Mzee huyo alimruhusu atumie usafiri huo kwa vile alijua angechelewa kurudi kwani watoto wa dada yake walikuwa wakipenda sana kuendesha baiskeli hivyo baada ya Beka kufika kule wangeanza kuendesha. Beka alipoondoka, mzee huyo alimkabili CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ mkewe kwa kumpagawisha mpaka mama wa watu akawa hoi, hakumchelewesha akampa mkomboti wa haja utafikiri muda mfupi uliopita hawakuwa pamoja. Kutokana na kipute alichopewa na mumewe, mama wa watu akawa hoi, mumewe alipomwambia waende wakaoge akamsihi atangulie. “Twende bwana tukaoge!” baba Beka alimwambia mkewe. “Kwa nilivyochoka wewe nenda ngoja nipumzike kidogo, maana umeniweza kweli,” mama huyo alimwambia mumewe.Baba Beka aliyekuwa anamuelewa vizuri mkewe anavyokuwa mara baada ya kumchezesha kwata ipasavyo, kabla ya kuelekea bafuni aliishia kucheka. “Kwahiyo hapo roho yako nyeupeee!” mkewe alimwuliza. “Tena nyeupe kama theruji, kwa ujumla nimelifurahia penzi lako mke wangu, wewe ni mwanamke wa ukweli! “ baba Beka alimfagilia mkewe. Baada ya mzee huyo kumsifia mkewe, akajishika kiunoni na kuanza kufanya mazoezi ya kurukaruka huku akiwa kama alivyotia timu duniani, mkewe akaishia kucheka kwa vituko vyake. “Hivi baba Beka utakua lini, sasa kufanya hivyo ndiyo nini?” mkewe alimwuliza. “Si nafanya mazoezi mama?” alimjibu mkewe. Kituko kilichomuacha hoi mkewe ni pale alipolala chali sakafuni akawa anainua miguu juu na kuishusha chini huku akihesabu moja mpaka kumi.Baada ya mzee huyo kufanya mazoezi yaliyokuwa na lengo la kumfurahisha mkewe, aliingia bafuni ambapo alioga akarejea chumbani, akavaa bukta. Alipomaliza, alitoka na kuelekea sehemu ya kulia chakula akafungua chupa na kumimina chai ya tangawizi kwenye kikombe. Hakuishia hapo, alifungua chupa iliyokuwa na asali akachota kijiko kimoja kikubwa na kuchanganya kwenye tangawizi, akakoroga.Kabla hajaelekea chumbani alikomuacha mkewe, alipiga mafunda mawili ya tangawizi, akajilamba na kujisemea moyoni ‘safi sana.’ Mzee huyo alikuwa akipenda sana kupata kinywaji hicho kwa sababu kilimchangamsha na kilimuongezea nguvu za simba alipohitaji kumkabili mkewe.Alipoingia chumbani alimkuta mkewe kapitiwa na usingizi, akajisemea moyoni; “chezea mzee Kibandiko wewe?” Kwa kuwa alibaki peke yake, alikwenda kukaa sebuleni na kuendelea kunywa tangawizi huku akitafakari jinsi walivyopeana raha na mkewe.Kufuatia kupenda sana vichekesho vya Mzee King Majuto, aliweka DVD ya vichekesho vya CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Majuto akawa anaangalia huku akicheka peke yake. Wakati anaendelea kutazama vichekesho hivyo, mkewe akiwa kajifunga kanga nyepesi maungoni mwake alitoka chumbani na kwenda sebuleni.Alipomuona mkewe akiangalia vituko vya Kingí Majuto, akacheka na kumtania kwamba kumbe ndiye alikuwa akimuiga mambo yake. “Mambo gani?” alimwuliza. “Si unayofanyaga, wewe si muda mfupi baada ya kunanii ulianza kurukaruka huku ukiwa huna nguo?” mkewe akamwuliza. Mpenzi msomaji, wiki iliyopita niliishia pale mke wa mzee Kibandiko alipomfuata mumewe sebuleni na kumkuta akiangalia DVD ya vichekesho vya Mzee Majuto akacheka na kumtania kwamba kumbe ndiye alikuwa akimuiga mambo yake . Je , baada ya mkewe kutoa kauli hiyo mumewe alisemaje? Songa mbele . . . ufuatia mkewe kumweleza hivyo , mzee Kibandiko licha ya kujua mambo aliyokuwa akiyafanya, alimwuliza ni mambo gani aliyomuiga Mzee Majuto ? “ Si unayofanyaga, wewe si muda mfupi baada ya kunanii ulianza kurukaruka ukiwa huna nguo mwilini ?” mkewe akamwuliza . “ Sasa kurukaruka ndiyo nimemuiga Mzee Majuto?” alimwuliza mkewe. “ Kuna tofauti gani?” mkewe alimwambia , wakacheka . Mama huyo ambaye siyo siri siku hiyo alifurahi sana kupewa raha na mumewe , alikwenda kuoga kisha akaingia jikoni kupika . Akiwa anaendelea na zoezi hilo huku mumewe akiwa sebuleni , alisikia kengele ya baiskeli ya mwanaye Beka aliyerejea kutoka kwa shangazi yake . Beka alipoingia ndani alimsalimia mzazi wake na kumfahamisha kwamba alimkuta shangazi na kwamba angefika siku iliyofuata . Beka alipompa taarifa hiyo mama yake , mama huyo alimweleza aende akamfahamishe baba yake kilichojiri kwa anti yake . Kijana huyo aliyemkosesha raha baba yake kufuatia tabia ya kutokuwa bize na mademu kama rafiki zake , aliingia na kumwambia mshua wake kwamba anti yake angefika kesho yake kama alivyomtuma. Beka alipompa taarifa hiyo baba yake , aliinuka kwenye kochi alilokalia akataka kuondoka lakini mzazi wake huyo akaomba asubiri kidogo. Alichokifanya alimwambia aangalie juu ya kabati la tv palikuwa na shilingi elfu moja achukue kwa ajili ya matumizi ya shuleni siku iliyofuata. Beka alimshukuru baba yake , akaenda kabatini akachukua fedha hiyo na kuelekea chumbani kwake . “ Kijana handsome boy lakini sijui kwa nini hana habari na wenzake wa kike , huyu CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ atakuwa na tatizo lakini kesho alfajiri ndiyo nitajua kama yupo fiti au la!” mzee Kibandiko aliwaza. Baada ya kula chakula cha usiku , kama kawaida yake , Beka alichukua madaftari yake na kuwaambia wazazi wake kwamba anakwenda kujisomea chumbani huku baba na mama yake wakiwa wanaangalia tamthiliya. “ Haya mwanetu sisi tunaburudika na tamthiliya, uwe na usiku mwema , ” mama Beka alimwambia kijana wake . Wakati wanandoa hao wakiendelea kuangalia tamthiliya, mama Beka aliyekuwa akimuwazia mambo mazuri mwanaye alimwambia mumewe : “ Baba Beka , huyu mtoto kama ataendelea na juhudi ya kujisomea, atakuja kututoa kimasomaso hapo baadaye . ” “ Ni sawa , hata aje awe msomi na kuwa na fedha nyingi lakini haitakuwa na maana kama atashindwa kuoa, ” baba Beka aliyekuwa na wasiwasi sana na mwanaye kwamba jogoo wake hawiki alimwambia mkewe. “ Sasa mtoto asioe kwa nini? Tena kwa taarifa yako ataoa msomi mwenzake na familia yao itaishi maisha mazuri , yaani sipati picha hao wajukuu zetu watakavyoishi kwa raha, ” mama huyo alimwambia mumewe . “ Hivi una uhakika kama mwanao yupo salama, wewe unafikiri wajukuu wanaokotwa huko mabondeni ee?” mzee Kibandiko alimwambia mkewe. “ Hivi kwa nini unasema hivyo baba Beka ?” mkewe alimwuliza . Kufuatia swali hilo, mzee Kibandiko alimwambia mkewe kwamba tatizo kila anapomweleza kuhusu Beka kutokuwa mjanja kama wenzake hamuelewi . “ Sikuelewi kivipi, mbona mtoto hana tatizo lolote , anapenda kujisomea, kutusaidia kazi na hana mambo ya ajabu kama wenzake , akitoka shule muda mwingi hupenda kuwa nyumbani !” mama huyo alimfagilia kijana wake . “ Sasa wewe unaona kukaa nyumbani au kuwa goigoi ndiyo tabia nzuri? Mtoto angekuwa na msichana wake hapo ingekuwa sawa , ” mzee Kibandiko alimweleza mkewe. Kufuatia kauli hiyo , mkewe alichukia na kumjia juu mumewe kwa mambo yake ya kijinga akainuka na kwenda chumbani. Mumewe hakuwa na habari naye akabaki akijisemea moyoni kwamba majibu kama mwanaye alikuwa kidume cha mbegu au la angeyapata alfajiri, akazima runinga na kwenda kulala . Alipofika chumbani alimkuta mkewe kalala na kaangalia ukutani huku wowowo lake pana likiwa limemwagika pande zote za CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ dunia. ìBahati yako nimechoka vinginevyo ningekubilingisha mpaka asubuhi , î mzee huyo alijisemea moyoni . Alichokifanya alipanda kitandani akalala bila kumbughudhi mkewe, kutokana na uchovu wa sebene la nguvu walilolicheza siku hiyo , hakuchukuwa muda mrefu akapitiwa na usingizi. Mpenzi msomaji sehemu iliyopita niliishia pale mzee Kibandiko aliyebaki sebuleni alipozima runinga kisha kwenda chumbani na kumkuta mkewe akiwa amelala. Je, kilifuatia nini? Songa mbele... Alipofika chumbani alimkuta mkewe kalala na kaangalia ukutani huku wowowo lake pana likiwa limemwagika pande zote za dunia. “Bahati yako nimechoka vinginevyo ningekubilingisha mpaka asubuhi,” mzee huyo alijisemea moyoni. Alichokifanya alipanda kitandani akalala bila kumbughudhi mkewe. Kutokana na uchovu wa sebene la nguvu walilolicheza siku hiyo, hakuchukuwa muda mrefu akapitiwa na usingizi. Kwa kuwa alipanga kumchunguza kijana wake Beka kujua kama jogoo wake alikuwa na hitilafu au la, alfajiri na mapema aliamka na kwenda chumbani kwake. Akiwa ndani alimuamsha Beka ambaye aliamka fasta na kutaka kujua mzazi wake alitaka kumweleza nini alfajiri ile.Beka alimuamkia baba yake huku mbele ya bukta yake pakiwa pamefura, mzazi wake aliitikia salamu huku akitabasamu na kumuuliza kwa nini hakujifunika shuka! Beka bila kujua kama mzazi wake alikuwa akimchunguza alimjibu kwamba alihisi joto ndiyo maana hakujifunika shuka. Wakati kijana huyo akimweleza hivyo mzazi wake, bado jogoo wake alikuwa kachangamka jambo lililomfurahisha sana baba yake.“Oke, Beka endelea kulala ngoja nijiandae ili niende kazini,” mzee huyo alimwambia kijana wake ambaye alibaki kujiuliza sababu ya baba yake kuingia chumbani kwake asubuhi ile wakati hakuwa na mazoea hayo. “Huyu kijana hana tatizo kwani damu inamchemka kama kawaida, nafikiri kinachomtatiza ni aibu,” mzee Kibandiko alijisemea moyoni huku akiangalia marudio ya taarifa ya habari kupitia runinga ya TBC. Mkewe alipoamka alimkuta mumewe akiangalia runinga, walisalimiana kisha mzee huyo alimwita na kumwambia aketi ili amwambie jambo flani. “Hapana baba Beka, wewe huoni kama kumekucha halafu mwanao akitukuta hapo unafikiri itakuwaje?” mama Beka aliyejua mumewe alitaka mambo flani pale sofani alifunguka. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Baba Beka aliyekuwa akipenda kumpa mkewe vionjo sehemu yoyote hata sebuleni Beka alipopitiwa na usingizi, alimwambia asihofu alitaka kumwambia jambo zuri kuhusu kijana wao. Mama Beka ambaye wakati huo alikuwa kajitanda kanga pekee aliketi ndipo mumewe alimwambia kwamba asubuhi ile alikuwa na furaha mno. “Furaha ya nini?” mkewe alimwuliza. “Mwanao kanifurahisha sana tena sana!” mzee huyo alimwambia mkewe. “Kwani kafanyaje?” Kufuatia kuulizwa hivyo, alimweleza kuhusu wasiwasi aliokuwanao kwa mwanaye na kwamba alifanya uchunguzi na kugundua hakuwa na tatizo, isipokuwa uwoga ndiyo ulimtatiza. “Huo uchunguzi umeufanyaje?” mkewe alimwuliza.Baba Beka alimweleza kila kitu mkewe ambaye aliishia kucheka na kumuuliza atakua lini maana mambo aliyoyafanya hayakupaswa kufanywa na mtu mzima kama yeye. “Mimi kama mzazi napaswa kujua afya ya mwanangu kiundani, kujua kama anaweza kuoa na kupata watoto siyo kukaa tu kumbe mtoto ana Joka la Kibisa,” mzee Kibandiko alimwambia mkewe, wakacheka. Wakati wanandoa hao wakipiga stori walisikia mlango wa sebuleni ukifunguliwa wakajua Beka, wakasitisha maongezi yao.Beka alipofungua mlango aliwasalimia kisha alikwenda kuoga, huku nyuma baba yake alimwambia mkewe kwamba walikuwa na kijana wa ukweli, mama akacheka. Baada ya mzee huyo kuangalia taarifa ya habari na Kipindi cha Jambo, alikwenda kuoga na kunywa chai kisha akaelekea kazini. Jioni aliporejea kutoka kazini, kwa mara ya kwanza alimkuta Beka akipiga stori na binti mmoja aliitwaye Rhoda wakiwa wamesimama kibarazani.Kitendo hicho kilimfurahisha sana na kumshukuru Mungu wake kusikia kilio chake kwani awali alijua kijana wake hakuwa kidume cha mbegu. “Hayo ndiyo mambo ninayoyataka, mtoto wa kiume unatakiwa uwe shapu siyo unawaogopa mademu ambao wameletwa duniani kwa ajili ya wanaume,” baba Beka alijisemea moyoni wakati akikaribia kuingia geti la nyumba yake. “Shikamoo baba na pole kwa kazi,” Beka CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ alimwamkia baba yake. Baada ya Beka kumpa heshima yake mzazi wake, Rhoda naye alimwamkia ambapo mzee huyo aliitikia salamu yake kwa uchangamfu wa hali ya juu.



    ITAENDELEA

    0 comments:

    Post a Comment

    Blog