Search This Blog

Monday, October 24, 2022

CHACHANDU ZA BEKA WA TANGA - 2

 





    Chombezo : Chachandu Za Beka Wa Tanga

    Sehemu Ya Pili (2)





    Mzee Kibandiko alipoingia ndani, Rhoda alimwambia Beka alikuwa akimuogopa tu baba yake kumbe alikuwa mchangamfu vile . Beka alimfahamisha msichana huyo kwamba baba yake hakuwa na noma ni mtu aliyependa utani wa hapa na pale. “ Basi mimi nilivyokuwa naumuona nilifikiri ni mkali, hata nilipomuona anakuja moyo ulipiga pa nikajua angetufurumsha, ” Rhoda alimwambia Beka , wakacheka . CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “ Sasa atufurumshe kwa kosa gani ?” Beka alimwuliza . Kufuatia swali hilo, msichana huyo alisema si baada ya kuwakuta wanazungumza angefikiria walikuwa wakiongea mambo ya mapenzi ! Kutokana na kauli hiyo , Beka alicheka na kumweleza baba yake asingeweza kufikiria hivyo kwa sababu yeye Beka hakuwa na tabia mbaya zaidi ya kupenda kujisomea. Rhoda ambaye alikuwa akivutiwa sana na ‘ uhandsome’ na utulivu wa Beka , alimfagilia kwa tabia hiyo na kumwambia jambo hilo lilimfanya ampende ila basi tu ! “ Basi nini?” Beka alimwuliza . “ Si wewe upo bize na masomo na kukaa hapa nyumbani kwenu utafikiria mwari ?” Rhoda aliyekuwa na lake la moyoni alimwambia Beka . “ Mimi siwezi kutembea huku na huko utafikiri daladala, mimi nataka hapo baadaye niwe rubani au daktari bingwa wa magonjwa ya akina mama, ” Beka alimwambia demu huyo, wakacheka . Wakati wakicheka , mama Beka aliyekuwa ndani alimwita kijana wake ndipo baba yake aliyekuwa sebuleni akifuatilia maongezi ya kijana wake na Rhoda kupitia dirishani alimuuliza mkewe alikuwa akimuitia nini. Mama huyo alisema alitaka amletee jagi la umeme ili achemshe maji ya kunywa , ili mwanaye azidi kuzungumza na Rhoda, mzee huyo aliinuka akachukuwa jagi na kumpelekea mkewe. “ Ee ! Makubwa !” Mama huyo aliguna . “ Makubwa nini?” Mzee Kibandiko alimwuliza mkewe. “ Kwani wewe ndiye Beka ?” Mkewe alimwuliza . “ Wewe unamtaka Beka au ulikuwa unataka jagi?” Naye alimwuliza . “ Haya bwana yameisha, asante kwa kuwa baba mwema , ” mama Beka alimtania mumewe , wakacheka . Baada ya mama huyo kutoa kauli hiyo , aliendelea na shughuli zake za jikoni na mzee huyo alikwenda sebuleni akatega masikio yake kusikia maongezi ya Beka na Rhoda. “ Huyu binti kampenda sana Beka lakini mwanangu sijui karogwa , anaacha kuchomekea mambo ya kueleweka yeye anasema anataka kuwa sijui rubani sijui dokta bingwa, ” mzee huyo aliwaza . Hakuishia hapo , alijisemea moyoni kwamba enzi zake binti kama Rhoda angetafunwa fasta kwani alikuwa kajileta tunduni mwenyewe . Beka ambaye hakusikia alipokuwa akiitwa na mama yake , aliendelea kupiga stori za kawaida na Rhoda ambazo silimfanya mzazi wake aliyekuwa sebuleni kutakamani kumwambia achomekee ishu ya yale mambo yetu lakini alishindwa . Baada ya vijana hao kuzungumza kwa muda CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ mrefu , Rhoda alimuomba Beka amsindikize lakini kijana huyo alikataa na kumweleza muda ule alitaka kumsaidia mama yake kuchota maji. “ Hayo maji utachota, nisindikize mpaka pale kwenye mchungwa halafu unarudi, ” Rhoda binti ambaye pale mtaani kwao alikuwa tishio kwa uzuri alimwambia Beka lakini kijana huyo alikataa . Kitendo hicho kilimkera sana baba yake Beka ambaye kuna wakati alikuwa akisimama dirishani na kuwachungulia. “ Hili toto ni majanga tupu, binti mzuri kama huyu kamfuata nyumbani mtoto kajirahisi hadi mwisho lakini halielewi eti linataka kumsaidia kuchota maji mama yake , kweli hili ni ----- la mabwege !” Baba Beka alipandwa na hasira . sehemu iliyopita niliishia pale mzee Kibandiko aliyekuwa akifuatilia mazungumzo kati ya kijana wake na Rhoda binti aliyeonesha kumpenda Beka lakini Beka hakuwa na habari naye jambo lililomkera sana mzazi wake na kumwita ----- . Je , kilifuatia nini? Songa mbele na uhondo huu. . . ale kibarazani , Beka alimuaga Rhoda lakini msichana huyo aliyekuwa na shepu tata na kila alipotabasamu vishimo vilitokea kila upande wa mashavu yake , aliendelea kumbembeleza amsindikize japo kidogo . “ Rhoda kama nilivyokuambia nataka kumsaidia mama kuchota maji wewe nenda tu ila nashukuru kwa kunitembelea maana haijawahi kutokea , ” Beka alimwambia Rhoda. “ Haijawahi tokea nini?” Rhoda alimuuliza. “ Si kupiga stori na msichana kwa muda wote huo, tena kama mama ametusikia tukiongea lazima ataniuliza , ” Beka alimwambia Rhoda . “ Atakuuliza nini, kwani yeye hapendi wakamwana?” Rhoda alimuuliza Beka . Kufuatia msichana huyo kumuuliza hivyo Beka , mzee Kibandiko aliyekuwa akisikiliza kila walichoongea alitabasamu na kumfagilia sana Rhoda . “ Huyu binti ana akili na kampenda sana mwanangu , sema Beka mwenyewe haelewi chochote , waliosema penye miti hapana wajenzi hawakukosea , ” mzee huyo aliwaza . “ Rhoda, suala la mama kuhitaji wakamwana halipo na kwa upande wangu sihitaji kuwa na msichana , mimi ni mwendo wa kujisomea tu mpaka kieleweke, ” Beka alimwambia . Kwa kuwa muda ulikuwa umekwenda na msichana huyo kuhitajika kwenda kupika kwao , akiwa mnyonge alimuaga Beka na kuahidi wangekutana siku nyingine, akaondoka. Njiani Rhoda alijisemea kwamba kwa jinsi vijana wenye rika la Beka walivyokuwa wakimsumbua kumtaka kimapenzi na licha ya kumuonesha dalili za kumpenda Beka na kijana huyo kuwa na domo zege, alikuwa na tatizo tu ! “ Si bure, yaani nimemfuata mpaka kwao na CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ kumuonesha hisia zangu lakini kashindwa kunitokea , yule atakuwa mgonjwa ila nitafanya kila njia kujua kama yupo fiti au la, ” Rhoda alijisemea moyoni . Huku nyuma baada ya msichana huyo kuondoka, Beka aliingia ndani na kukutana koridoni na baba yake ambaye alimkata jicho na kwenda kukaa sebuleni. Beka aliyemjua vizuri mzazi wake anavyokuwa akikerwa na jambo akawa anajiuliza alikuwa kaharibu wapi bila mafanikio. “ Mbona sikumbuki kama kuna kazi alinipatia sijaifanya, nitakuwa nimekosea wapi ?” Beka aliyekuwa ameketi chumbani kwake alijiuliza . Akiwa anatafakari hivyo , aliona mlango wa chumba chake ukifunguliwa kisha baba yake aliingia na kusimama katikati ya kitanda na mlango . Kwa jinsi mzee huyo alivyokuwa, moyo wa Beka ukapiga paa kwani alijua alikuwa kaharibu tu mahala na kwa akili ya fasta alijua baba yake hakupendezwa na ujio wa Rhoda pale nyumbani kwao . “ Baba nahisi nimekukosea naomba unisamehe , ” Beka alimuwahi mzazi wake . “ Umenikosea nini?” mzazi wake alimuuliza. Beka alimwambia kitendo cha kumkuta akizungumza na Rhoda pale kibarazani , mzazi wake akamwambia hakuwa na tatizo na Rhoda isipokuwa alikuwa anataka kujua kwa nini alikuwa hasafishi banda la mbwa . Kufuatia kuulizwa hivyo , Beka aligundua ni kweli alipitisha siku moja bila kusafisha banda hilo lakini kabla hajajitetea mzazi wake alimdaka na kwenda naye sebuleni. Alipofika sebule alichukuwa fimbo aliyoificha chini ya kiti na kuanza kumtandika Beka , Beka akaanza kulia . “ Leo utanitambua, sipendi kijana mzembemzembe hata kidogo, ” mzee Kibandiko aliendelea kumtandika Beka bila kijana wake kujua kama sababu haikuwa kutofagia banda la mbwa isipokuwa kushindwa kumtokea Rhoda aliyejileta nyumbani kwao bila kuitwa. Huku akimtandika moyoni alikuwa akisema : “ Wewe mtoto mjinga sana , binti mzuri kama Rhoda kajileta mwenyewe wewe unashindwa kumpa maneno matamu unamwambia unataka kumsaidia mama yako kuchota maji, si upuuzi huo?” Mpenzi msomaji ,sehemu iliyopita niliishia pale mzee Kibandiko alipomsifia mkewe kwamba alikuwa mwanamke mrembo asiyechuja . Je , mama huyo aliposifiwa alisemaje ? Songa nayo “ Asante , hata wewe ni mwaume wa shoka , unajua kunitunza na kunifikisha pale ninapopataka, ” mama Beka alimwambia mumewe . “ Nashukuru mke wangu kama umeligundua hilo, hata hivyo nisipokupa raha mimi akupe nani?” Mzee Kibandiko CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ alimwambia mkewe na kuweka kikombe cha tangawizi mezani . “ Umeona eh ?” mkewe alimsapoti , wakacheka . Mzee Kibandiko aliyekuwa kamaliza tangawizi iliyokuwa kwenye kikombe, alinyanyua miguu na kulala chali kitandani , wakaendelea kupiga stori. “ Mama Beka nikuulize kitu ?” mzee huyo alimwambia mkewe. “ Uliza hata maswali mia yakiwa ndani ya uwezo wangu nitakujibu , ” alimwambia . Mzee Kibandiko alipoambiwa hivyo , alicheka na kumweleza mkewe atupie macho dirishani kulikuwa na mtu alikuwa akiwachungulia. Mkewe alipofanya hivyo hakumuona mtu na alipogeuza macho kumtazama mumewe alishangaa alipomuona kafungua taulo na kubaki mweupe pee ! Mama Beka alicheka na kumfuata mumewe akampiga kibao chepesi kwenye paja na kwa sauti nyororo alimuuliza ndilo swali alilotaka kumuuliza! “ Kwani wewe ni dada yangu, upo hapa kwa ajili ya kunifurahisha nami nikufurahishe ,” mzee huyo mpenda mahabati alimwambia mkewe kisha alimvutia kifuani kwake . Mama huyo akiwa kajaa tele kifuani kwa mzee huyo wa mjini, mumewe akaanza kuuterezesha mkono wake wa kulia maeneo mbalimbali yenye shoti ya umeme. Wanandoa hao waliendelea kuleteana fujo hadi kila mmoja akaiva , mama Beka alipotupia macho mlangoni alibaini hawakuufunga, akaamka kichovu kwenda kuufunga. Wakati akifanya hivyo alikuwa kabaki na skeni taiti nyeupe , mumewe alipoangalia hipsi na bambataa la mkewe lilivyokuwa limenona , akawa anameza mafunda ya mate mfululizo . Mama huyo alipofunga mlango alimalizia kiwalo chake cha mwisho , akajongea kwa mumewe aliyempokea kwa mikono miwili kama wakuu wa mikoa wanavyokabidhiana Mwenge wa Uhuru mpakani mwa mkoa fulani unapomaliza mbio zake . Kwa kuwa hakuna kitu alichokipenda kabla ya kulicheza segere kama kula mua a. k . a denda , alimpa mumewe nyama ya ulimi naye bila noma akaipokea. Wawili hao ambao wakati huo hawakuwa na habari kabisa na kijana wao Beka zaidi ya kazi iliyokuwa mbele yao, walipagawishana si kidogo na mwishowe walizama kwenye kisiwa cha wapendao na kupeana raha ya dunia . “ Ila wewe baba Beka wewe!” Mama Beka ambaye muda huo alikuwa hoi alimwambia mumewe . “ Mimi nini?” Baba Beka alimuuliza. “ Si hivi unavyonifanyia !” alimwambia . “ Nakufanyia nini?” mkewe alimuuliza. Kufuatia kuulizwa hivyo alimwambia kuhusu tabia yake ya kupenda kunaniliu mchana hata kama kijana wao yupo. “ Tatizo liko wapi , kwani tunakutana hadharani halafu elewa kwamba wewe ni CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ mke wangu hakuna mtu yeyote hapa duniani atakayenipangia muda wa mimi kuwa na wewe, ” mzee huyo alimwambia mkewe. “ Ni kweli unachosema lakini kumbuka Beka amekua kitendo cha sisi kujifungia ndani mapema yote hii atajua kinachoendelea , siyo vizuri bwana!” mkewe alimwambia . “ Tena akijua ndiyo safi, itamsaidia kuchangamka , toto gani wenzake wote wapo shapu yeye ni kukaa tu hapa nyumbani utafikiri padri , ” baba Beka alimwambia mkewe. “ Baba Beka maneno gani hayo , unaacha kumshukuru Mungu mwananetu katulia wewe unataka afanye mambo ya kipuuzi ?” mama huyo alimwambia mkewe. “ Kuwa na demu ndiyo upuuzi, kwa taarifa yako mtoto wa kiume kama yeye kukaa nyumbani na kuchotachota maji ndiyo upuuzi mkubwa, mtoto wa kiume hatakiwi kuwa kama Beka , ” baba Beka alimwambia mkewe. “ Haya bwana wewe muombee mtoto mambo yasiyofaa, siku akianza kukuletea kesi za kuwapa mimba watoto wa watu ndiyo akili itakaa sawa , ” mama huyo alimweleza mumewe . “ Hicho ndicho ninachokitaka , mimi nataka wajukuu hata wakwe zangu wakifika mia moja mhusika akiwa Beka nitawalea , ” mzee huyo alimwambia mkewe. Kufuatia kauli hiyo , mama Beka aliishia kucheka kisha alimwambia mumewe kwamba alishinda waachane na maongezi hayo . Je , baada ya mama huyo kutoa kauli hiyo mumewe alijibuje ? Mpenzi msomaji , sehemu iliyopita niliishia pale aliposisitizia mkewe kwamba anahitaji kijana wake Beka achangamke kisha alimuuliza ‘ wife ’ wake huyo kama alimwambia asante kwa raha aliyompa. Je , baada ya kumuuliza hivyo mkewe alisemaje? Twende mdodomdogo Kufuatia mama huyo kuulizwa hivyo alicheka na kusema : “ Si tayari umemaliza shida yako kwani asante ina umuhimu?” Kufuatia dongo alilorushiwa na mkewe, mzee huyo alimvutia mkewe maungoni mwake akambusu na kumwambia asante kwa kumpa raha. “ Nami nakushukuru mume wangu kwani unanipatia sana na kuniacha hoi kwa hilo jiandae kupokea zawadi yangu, ” mama Beka alimwambia mumewe , wakacheka . “ Zawadi gani mama?” Baba Beka akamuuliza mkewe. “ Wewe subiri utaiona siku hiyo , usiwe na haraka besti , ” mkewe alimwambia mumewe , wakacheka . Baada ya utani wa hapa na pale, mama Beka aliingia bafuni akaoga kisha akatoka na kumuacha mumewe akiwa kajipumzisha . Jioni wakiwa wamemaliza kula wakiwa CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ wameketi sebuleni, mzee huyo alimuita Beka aliyekuwa anajisomea na kumwambia kwamba huwa hapendi kumchapa ila aache uzembe . Beka ambaye hakufahamu kama alichapwa kwa sababu alishindwa kumtokea Rhoda aliahidi kuwa makini na atahakikisha anafanya usafi kwenye banda la mbwa kila siku. Kufuatia kauli hiyo , baba yake alicheka kwani alipomsisitiza aache uzembe , moyoni alimaanisha kuwatokea mademu lakini kijana wake hakujua hilo. “ Hivyo ndivyo inatakiwa kufanya , mtoto akikosea mwelekeze kwa kumuambia lakini siyo unamchapa, ” mama Beka alimwambia mumewe . “ Kama hasikii viboko ndiyo dawa yake , ” mzee huyo alimuambia mkewe. Muda wa kulala ulipowadia, Beka alikwenda chumbani kwake na wazazi wake walikwenda chumbani kwao . Kulipokucha Beka alikwenda shuleni, baba yake kazini na mama yake ambaye hafanyi kazi alibaki nyumbani . Siku hiyo Beka alichelewa kurudi nyumbani jambo ambalo halikuwa kawaida , na aliporejea mama yake alimuuliza alikochelewa . “ Kuna mwalimu mgeni kaanzisha darasa la tuisheni , hivyo mimi , Jacob , Jully , Sara na wanafunzi wengine tulibaki kwa ajili ya kujifunza, ” Beka alimwambia mama yake . “ Hapo mwanangu ndipo unaponifurahisha, soma ipo siku utakuja kuwa mtu mwenye madaraka makubwa hapa nchini, ” mama huyo alimwambia mwanaye . Kwa kuwa Beka alipenda sana kumsaidia mama yake kazi za nyumbani , alipomaliza kula alimuuliza mama yake kama kulikuwa na kazi ya kufanya akamwambia apumzike tu . Beka aliyependa kukaa kibarazani kwao , alipoambiwa hivyo alizunguka nyuma na kukaa juu ya ukuta wa kibaraza . Haukupita muda mrefu , alimuona Rhoda akiwa amekaribia alipokuwa , akamkaribisha , ingawa hakuwa mtu wa mademu alijikuta akivutiwa na mavazi aliyovaa msichana huyo. “ Karibu Rhoda , halafu hizo nguo ulizovaa zimekupendeza sana, ” kwa mara ya kwanza Beka akamsifia msichana huyo japo hakuwa na lengo la kumtaka kimapenzi. “ Jamani asante Beka , hata hivyo nimevaa kawaida mbona !” Rhoda alimwambia . Beka alimwambia Rhoda kwamba hata kama alivaa kawaida lakini alipendeza , msichana huyo akasema asante . Wakati Rhoda na Beka wakipiga stori, mzee Kibandiko aliyekuwa kazini aliwasili na kuwakuta pale kibarazani kama ilivyokuwa siku ya kwanza kumuona Rhoda pale nyumbani kwake . “ Shikamoo baba na pole kwa kazi , ” Beka CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ alimwamkia baba yake . Kabla yam zee huyo hajaitikia salamu ya kijana wake , Rhoda naye alimwamkia ndipo mzee huyo aliitikia salamu zao kwa pamoja . “ Naona Beka umepata mgeni , safi sana mnapotembeleana na kubadilishana mawazo, ” mzee huyo alimwambia kijana wake . “ Nashukuru baba , kwani tunataka kujisomea pamoja kwani mitihani imekaribia , ” Bela alimwambia mzazi wake . “ Hilo ndiyo tatizo la mwanangu , yeye kila wakati anawaza kujisomea badala ya kuuangasha mbuyu , hebu kaangalie kabinti kalivyo kazuri , hii ni sheedaaa kweli, ” mzee huyo alijisemea moyoni. Akiwa amesimama mlangoni , alimtania Rhoda kwamba anafaa sana kuwa mkwewe kwa jinsi walivyopendezana na Beka , Rhoda aliishia kucheka huku akiangalia chini kwa aibu. Mzee Kibandiko alipoingia ndani, Rhoda aliachia tabasamu pana ndipo Beka akamuuliza alifurahishwa na nini. Je , baada ya Rhoda kuulizwa hivyo alijibu alijibuje? Mpenzi msomaji , sehemu iliyopita niliishia pale Mzee Kibandiko alipoingia ndani baada ya kumtania Rhoda kwamba anafaa kuwa mkwewe kwa jinsi walivyopendezana na Beka ambapo msichana huyo alitoa tabasamu pana ndipo Beka akamuuliza alifurahishwa na nini? Songa mbele . .. Rhoda aliuliza "baba yako , kumbe anapenda utani eh ? Beka : kama nilivyokuambia siku ya kwanza kwamba baba yangu anapenda sana mizaha na pia ni mcheshi . Rhoda :“ Leo nimeamini , si ulimsikia alivyosema nafaa kuwa mkwewe kwa vile tunapendezana ?” beka: “ Wewe utamuweza baba yangu kwa utani , tena ilibakia kidogo angekwambia nguo ulizovaa zimekupendeza sana ,” wote wakacheka . Kufuatia kauli hiyo ya Beka , Rhoda alimweleza asingeweza kutoa kauli hiyo kwa sababu kidesturi mimi naweza kuwa mkwewe . beka: “Mkwewe kwa nani ?” Rhoda: “ Si kwako, kwani wewe huwezi kunioa mimi ?” Rhoda alimtupia swali Beka bila kujua kama mzee Kibandiko alikuwa akiwasikiliza kupitia dirishani. beka: “ Mimi mambo hayo sitaki kuyasikia kwa kwa sasa , nataka kusoma kwa kwenda mbele ,” Beka alimwambia Rhoda ambaye alikosa raha ghafla. Kule ndani mzee kibandiko aliposikia kauli hiyo ya mwanaye alikunja sura na kujisemea moyoni “ Huyu anataka bakora tena, tena leo nitamtandika na kumweleza kwa nini nimemtandika , siwezi kuvumilia upuuzi wake . ” Rhoda aliamua kufunguka :Kwani Beka watu wakisoma ndiyo hawaoi au kuwa na wapenzi , mbona ukiamua tunaweza CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ kuwa pamoja huku tukiendelea kusoma?” Kauli ya Rhoda ilimpa raha sana mzee Kibandiko na kujisema moyoni kwamba atafanya kila awezalo amtafutie Rhoda zawadi yoyote . Beka : “ Mimi mambo hayo hapana tena mama akikusikia anaweza kukufukuza kabisa hapa nyumbani , ukitaka afurahi atukute tunajisomea, ” Wakati wanaendelea kupiga stori, baba Beka aliyekuwa amekasirika aliinuka na kwenda stoo ambako kulikuwa na fimbo za mifagio ya nje akachukua moja . Wakati akitafuta fimbo hiyo mkewe aliyekuwa jikoni ambaye hakujua kama mumewe alirejea , alisikia kama kuna mtu alikuwa akitafuta kitu stoo akafikiria ni Beka . Kutokana na kumpenda sana mwanaye aliamua kumfuata ili kujua alikuwa akitafuta nini ili amsaidie , ile anafungua mlango wa kwenye korido akamuona mumewe kashika fimbo. “ Mwenzangu, umerudi saa ngapi na hiyo fimbo ya ufagio ya nini?” alimwuliza . ingawa mzee huyo alikuwa na hasira , alimdanganya mkewe kwamba alipoingia chumbani alimuona panya hivyo alitaka kumsaka na kumuua . “ Halafu na wewe baba Beka kwa ubishi ndiyo mwenyewe , kila siku nakuambia ziba hilo tundu kwenye mlango hunielewi , yaani chumba kimegeuka uwanja wa panya!” Aliongea mama huyo bila kujua kama mwanaye Beka asingemaliza siku hiyo bila kula bakora . mzee kibandiko : “ Itabidi kesho nimuite fundi alizibe , ” mzee huyo alimwambia mkewe. Baada ya kumaliza mazungumzo kuhusiana na panya , mkewe alimpa pole ya kazi akashangaa baada ya kujibiwa ilikuwa nzuri kiasi “ Kwa nini kiasi ?” alimwuliza . “ Siku hazifanani tu , hivi mwanao kafagia banda la mbwa ?” mzee huyo badala ya kumweleza mkewe kilichojiri kazini akamchomekea swali . “ Nafikiri atakuwa kasafisha, ngoja nitamuuliza akimaliza kujisomea, ” mama huyo alimwambia mumewe . Kwa kuwa alimdanganya mkewe kwamba chumbani kwao kulikuwa na panya, aliingia na kujifanya anamsaka lakini moyoni alisema lazima Beka atamtambua hata kama atakuwa kasafisha banda la mbwa atamtafutia sababu ya kumcharaza bakora tena. Mama Beka alimshauri mumewe wakati akimsaka panya huyo azibe lile tundu ili asitoke kisha alikwenda jikoni kuandaa tangawizi ambayo baba Beka alikuwa akipenda kunywa aliporejea kutoka kazini . Hata hivyo , hakukaa muda mrefu mle chumbani alitoka na kwenda kuketi sebuleni kusikiliza maongezi ya kijana wake na Rhoda. “ Vipi umeshindwa kumpata ?” mama Beka alimwuliza mumewe baada ya kumkuta CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ ameketi sebuleni. Kufuatia sauti ya mama huyo kuwafikia akina Beka , vijana hao walipunguza sauti ambapo Rhoda alimwuliza Beka kama mama yake hakuwa na noma . Beka: Kwa kuwa tupo hapa kwa ajili ya kujisomea hana shida, yeye hapendi mambo ya kipuuzi tu ! î Mambo ya kipuuzi ndiyo mambo gani ? Rhoda alimwuliza . Kama ya wanawake na kuwa na marafiki wasiozingatia maadili , î Beka alimwambia . ìWewe Beka na huyo mama yako mh ! Hivi hujui kama hivi sasa umekua unafaa kuwa na rafiki wa kike kama mimi ?î Rhoda alifunguka . Sehemu iliyopita ;Mambo ya kipuuzi ndiyo mambo gani ?” Rhoda alimuuliza. “ Kama ya wanawake na kuwa na marafiki wasiozingatia maadili , ” Beka alimuambia. “ Wewe Beka na huyo mama yako mh! Hivi hujui kama hivi sasa umekua unafaa kuwa na rafiki wa kike kama mimi ?” Rhoda alifunguka . songa nayo sasa... Licha ya Rhoda kujitahidi kumshawishi Beka lakini kijana huyo hakuonesha dalili kama alikuwa na hisia za mapenzi na msichana huyo, akamuambia wakati ukifika ataoa kabisa siyo kurukaruka kama chura na kila msichana . Kufuatia kauli hiyo , Rhoda alicheka na kumuambia Beka kwamba dunia ya sasa imebadilika siyo kama ya wazazi wetu ambao waliogopa kujaribu baadhi ya mambo . beka :“ Kujaribu mambo gani?” Rhoda aliangua kicheko na kusema : “ Mfano unapoambiwa usijihusishe na masuala ya mapenzi sasa utayafahamu vipi bila kujihusisha nayo?” Msichana huyo huku akiwa hajui kama kulikuwa na mtu alikuwa akiwasikia , alimuambia Beka kwamba hakuona kikwazo cha wao kuwa wapenzi kikubwa ni kuwa makini. beka: “ Kuwa makini kivipi, yaani Rhoda hujatulia kabisa wewe !” Wakati wakiendelea na stori hizo , mzee Kibandiko aliyekuwa amekaa kwenye sofa lililokuwa dirishani kwa ndani, alimfagilia sana Rhoda . “ Huyu binti ana akili sana, anakoelekea atamuweka sawa tu huyu ----- wangu, kijana gani anashindwa kumuelewa mwenzake mpaka amuambie kabisa kwamba wakananiliu ndiyo atamuelewa?” mzee huyo aliwaza. “ Beka nimevumilia muda mrefu nikifikiri utanielewa na kucheza na hisia zangu lakini mwenzangu huoneshi dalili zozote za kunihitaji, ngoja nikuambie la moyoni ,” Rhoda aliendelea kufunguka, Kule ndani mzee Kibandiko kidogo aruke juu kwa furaha kwani alielewa Rhoda alitaka kumueleza moja kwa moja Beka kwamba CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ alimpenda . “ Huyu binti leo lazima nimpe hela ya matumizi, ngoja nisikilize anachotaka kumuambia huyu domo zege wangu, ” mzee huyo aliyekuwa akimuita majina ya ajabu mwanaye aliwaza . “ Sikiliza Beka , hivi tangu unifahamu umeshawahi kuniona nahangaika na wavulana hapa mtaani?” Rhoda alimuuliza . beka: “ Sijawahi!” Rhoda aliendelea kuchombeza:“ Unajua kwa nini sina taimu nao ?” beka:“ Mimi sijui bwana!” Kufuatia kuambiwa hivyo , Rhoda alimueleza Beka kwamba chaguo lake alikuwa yeye na kwamba alikuwa akimpenda sana kwa sababu nyingi . Rhoda hakutaka kumpa beka nafasi ya kuzungumza kabla ya kumaliza, alimuambia kwanza alikuwa handsome boy, mpole , mtanashati , alipenda kujisomea. Aliendelea kummwagia sifa kwamba ukiacha sifa hizo , hakuwa bize na mambo ya wasichana kama wenzake , alipenda kumsaidia mama yake kazi za nyumbani na alikuwa na macho mazuri . Kule ndani kila Rhoda alipommwagia sifa Beka , mzee kibandikoa alitikisa kichwa kwani aliamini asingeweza kuchomoa na kujisemea moyoni kwamba kama angemjibu tofauti msichana huyo siku hiyo angemtimua pale nyumbani . “ Kwa hatua aliyofikia huyu binti Beka asipomuelewa, kwanza atakula bakora zakutosha kisha namtimua hapa nyumbani , sitaki ujinga mimi ,” mzee huyo aliwaza . “ Beka , ” Rhoda alimwita Beka aliyekuwa ameduwaa kwa muda baada ya kumwagiwa misifa kibao. Je, beka ataingia line baada ya sifa hizo?? Mpenzi msomaji, sehemu iliyopita niliishia pale Rhoda alipomuita Beka ambapo kijana huyo aliduwaa kwa muda kwa kumwagiwa sifa kibao. Je , kilifuatia nini? Songa nayo mdau wangu. . . Nakusikiliza Rhoda , ” Beka alijibu huku akiwa na hisia fulani kwa msichana huyo ambazo hakuwahi kuwa nazo tangu alipoingia katika umri wa kikubwa a. k . a kubalehe . “ Hayo ndiyo yalikuwa yakinisibu moyoni mwangu kwa muda mrefu , kwa kifupi nakupenda , rafiki zako akina Saidi, Jafari, Dan na wengine wamekuwa wakinisumbua lakini nawakataa kwa sababu moyo wangu umekupenda wewe , nipe nafasi moyoni mwako Beka ,” mtoto wa kike alijieleza kwa hisia kali... Kama unavyofahamu katika dunia hii hakuna mtu asiyependa kusifiwa , Beka aliyemwagiwa sifa kibao alifurahi sana na kujitambua kwamba alikuwa handsome boy. Beka : Nashukuru kwa kuniambia hisia zako ila naomba kwenye saa moja au mbili kasoro tuonane pale uwanjani kwenye goli la kusini , hata kama nitachelewa nisubiri na kama nitawahi kufika nitakusubiri,” CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Msichana huyo alitamani kumrukia kwa furaha lakini mazingira hayakuwaruhusu akaishia kuporomosha bonge la tabasamu , akamshukuru Beka kwa kumkubalia ombi lake . Kule ndani , mzee Kibandiko aliyekuwa kafurahi kupita maelezo , aliinuka na kwenda chumbani ambako alifungua waleti yake iliyokuwa juu ya meza akatoa wekundu mmoja wa msimbazi na kusema "lazima awapatie Rhoda na Beka ili wagawane elfu tano tano." Akiwa na fedha hiyo , alipitia mlango wa uani na kujifanya hakufahamu chochote kilichojiri kati ya Rhoda na Beka . Vijana hao walipomuona , walijifanya wanajisomea, mzee huyo alitamani kucheka lakini akapotezea na kusogea pale kibarazani. “ Naona mnajisomea !” aliwaambia. Kama vile waliambiana wajibu kwa pamoja , wakasema ndiyo,, ndipo mzee Kibandiko akasema walimfurahisha sana, akatoa ile noti ya shilingi 10,000 na kumpatia Beka na kumwambia wagawane hiyo ilikuwa ofa yake kwao . Beka ambaye ilikuwa nadra kupewa fedha kubwa kiasi kile alipigwa butwaa na kumshukuru mzazi wake akifuatiwa na Rhoda aliyepiga magoti na kumshukuru mzee huyo. “ Msijali wanangu , leo mmenifurahisha mno , mimi huwa napenda sana watoto wakielewana na kujisomea pamoja kama mnavyofanya,” Beka na Rhoda ambao hawakujua mzee huyo alimaanisha nini walifurahi, lakini kabla mzee Kibandiko hajaondoa alimtania Rhoda "aangaliaBeka asimpunje hela yako" Rhoda alicheka na kusema : "Beka hawezi kufanya hivyo kwani ni kijana mzuri" Mzee kibandiko : "aaahh nakutania mwanangu" Kitendo cha Rhoda aliyekuwa na akili za ziada kutoa kauli hiyo , Beka hakujua alichomaanisha Rhoda badala yake alifurahi mno kufagiliwa kwa mzazi wake kwamba mzee Kibandiko aliwaacha Beka na Rhoda wakiendelea kupiga stori akaingia ndani huku akiimba wimbo wa Lucy Bandawe uliopigwa na Ottu Jazz Band ambao moja ya shairi lake linasema Lucy Bandawe. . . Lucy wangu nampenda ! Mkewe aliyemfahamu vizuri mumewe alipofurahi alikuwa na kawaida ya kuimba hasa wimbo huo, Mama beka : "eeehh bab umefurahishwa na nin..!??" Mzee huyo alicheka na kumwambia kuna jambo lilimfurahisha sana muda ule angemwambi baadaye . Kwa kuwa mkewe alikuwa bize na mapishi na shughuli zingine za jikoni , aliishia kutabasamu kisha alimwita Beka ili amtume dukani. Beka alipoitika na kutaka kwenda kumsikiliza mama yake , mzee Kibandiko alimuuliza mkewe alimuitia nini mtoto aliyekuwa akijisomea na mwenzake? “ Nataka nimtume hapo dukani mara moja , ” mama huyo alimwambia mumewe . CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Kufuatia mkewe kutoa kauli hiyo , mzee huyo alimwambia Beka aendelee kujisomea kisha alimuuliza mkewe alitaka kumtuma nini ili aende yeye kwa sababu hakuwa na kazi yoyote. Mkewe alicheka na kumwambia mumewe kwamba kweli siku hiyo alifurahi mpaka kuamua kwenda dukani kununua chumvi na dawa ya meno ! “ Wewe lete hiyo hela niende, kwanza ni moja ya mazoezi si unaona kitambi kinaninyemelea?” alimwambia mkewe. Alipotoa kauli hiyo mkewe aliendelea kucheka na kumwambia atumie hela aliyokuwanayo mfukoni mwake, baba Beka akamwambia anataka ampe hela ya bajeti aliyomuachia , huku mkewe akicheka alimpatia shingili elfu mbili ndipo mzee huyo akaelekea dukani. “ Mh! Hii furaha siyo bure, huenda atakuwa kapandishwa cheo kazini au kuna dili lao limekwenda vizuri, na ninavyomfahamu anavyopenda kufinyana anapokuwa kafurahi , leo usiku mbona shughuli ninayo mie!” mkewe aliwaza na kuachia tabasamu. Kule nje Rhoda alimwambia Beka kwamba hakutegemea kama baba yake alikuwa mtu poa namna ile ; “ Yaani katupatia ten moja kwa sababu ya kujisomea tu , hivi akisikia umefaulu si atakufanyia mambo makubwa zaidi ?” “ Si nilikuambia siku ile , ila akichukia ni balaa , juzi kanilamba bakora sina hamu naye ,” Beka alimwambia Rhoda. “ Eh ? Ulifanya kosa gani ? Kwanza siamini kama unachosema kina ukweli mbona mshua wako mpole , mcheshi na mpenda utani ?” Rhoda alimwambia Beka . “ Tukikutana baadaye nitakuambia sababu ila elewa akichukia kaa naye mbali , ” Beka alimwambia Rhoda, wakacheka . Rhoda aliyekuwa amemuweka sawa Beka ambaye awali hakuwa kabisa na hisia za mapenzi juu yake , alimuaga kijana huyo na kumwambia kwamba anakwenda kupika hivyo wangeonana uwanjani kama walivyokubaliana. Mpenzi msomaji, sehemu iliyopita niliishia pale Rhoda na Beka walipokubaliana kukutana kwenye uwanja wa mpira kuanzia saa kumi na mbili na nusu hadi saa moja jioni . Je, wakatapokutana eneo hilo kijana huyo atafunguka ? Endelea na utamu huu . Kwa mara ya kwanza, Beka alimsindikiza Rhoda umbali wa mita kama thelathini huku maongezi baina yao yakiwa yamepamba moto. Walipofika kwenye duka moja , Beka alichenji ile hela na kumpatia Rhoda shilingi elfu tano, kisha wakaagana huku akiwa na hamu ya kuendelea kupiga stori na msichana huyo ambaye wakati huo alimuona mrembo CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ sana. “ Hivi Rhoda kumbe ni mrembo namna ile , nimefurahi kaniambia hisia zake kwamba ananipenda, acha niwe naye karibu lakini si kimapenzi urafiki tu !” Beka aliwaza wakati akirudi nyumbani . Alipoingia sebuleni alimkuta baba yake akiwa anaangalia muziki uliopigwa na bendi ya Ottu ambayo aliisifia kwamba ilikuwa ikipiga nyimbo zilizokwenda shule kwa ujumbe wake . Ingawa ilikuwa kawaida yake kujisomea, alishangaa kumsikia mzazi wake akimsifia kwamba alimfurahisha sana siku hiyo . “ Nami nafurahi kama mzazi wangu unafurahishwa na jinsi ninavyojisomea, ipo siku nitawanunulia gari kwani najua nitakuwa bosi , ” Beka alimwambia baba yake , wakacheka . “Kujisomea sawa lakini sijakuambia nimefurahishwa na unavyojisomea, leo umejitahidi kuonyesha wewe ni mtoto wa kiume hivyo ndivyo ninavyotaka , ” mzee huyo alijisemea moyoni . “ Ukiwa bosi itakuwa vizuri tena bosi mwenye mke mzuri na watoto, ” baba yake alimwambia kimafumbo . Baada ya mazungumzo mafupi, Beka alitaka kuelekea chumbani kwake kuweka madaftari , akiwa ametembea hatua mbili mzazi wake akamwita . “ Naam !” aliitika wito wa baba yake . Mzee huyo aliyekuwa na lake jambo , alimwambia kwamba jioni alihitaji kumtuma aende akamsalimie shangazi yake Mwajuma anayeishi Barabara ya Tatu. Beka alifurahi sana kutumwa huko kwani alikuwa anafikiria njia ambayo angeitumia kutoka pale nyumbani wakati wa kwenda kuonana na Rhoda kwani wazazi wake walikuwa wakimkataza kutoka usiku . “ Hakuna shida baba , tena nitaondoka mapema kidogo ,” Alifurahi bila kujua kama mzazi wake alitunga safari hiyo makusudi ili apate chansi ya kuonana na Rhoda kwani alitamani sana Beka aanze kujilia vitamu vya binti huyo. “ Kwa akili yake anaona zari la mentali limemuangukia kumbe nimemurahisishia ili akaonane na mwenzake, mimi ndiyo mzee Kibandiko niliyebobea katika fani ya mahaba!” mzee huyo alijifagilia . Kwa jinsi mzee huyo alivyokuwa mahiri kwenye tasnia ya mahaba, alijua Rhoda na kijana wake watakapokutana lazima msichana huyo atamfanyia vituko vya kumlainisha. Ilipofika saa 12 kasoro jioni , mzee Kibandiko alimuhimiza kijana wake awahi kwenda alikomtuma, Beka akiwa mwenye furaha akaondoka. “Ngoja niende fasta kwa shangazi kisha nikakutane na Rhoda , jambo la muhimu nitakalomuambia ni kwamba nami nampenda lakini siyo kufanya mambo ya kijinga...... , ” Beka CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ aliwaza. Kwa kuwa Barabara ya Tatu hapakuwa mbali, hakuchukua muda mrefu akafika kwa shangazi yake aliyemkuta ameketi nje akisukwa. Beka aliwasalimia kisha akaenda moja kwa moja kwenye suala lililomleta "unaendeleaje shangazi??" Shangazi:" naendelea vizuri jana homa ilinikamata haswa, ila namshukuru mungu nimepata ahueni" “ Nafurahi kusikia hivyo maana baba alinituma nije nikujulie hali, ” Beka alimwambia shangazi yake . Baada ya mazungumzo mafupi na shangazi yake, Beka hakutaka kupoteza muda , alimuaga na kuelekea Barabara ya 5 kwa rafiki yake aitwaye Hemed, lengo lake alitaka akapige stori kusubiri muda aliopanga kukutana na Rhoda ufike . Alipofika hakuweza kumkuta rafiki yake huyo ambapo dada zake walimwambia alitumwa kwa bibi yake . Kwa kuwa dada zake Hemed walipenda sana kupiga stori walianza kuzungumza mambo mbalimbali na Beka yakiwemo yaliyohusu shule. “ Hivi bado tu unaendelea kushikilia namba moja mnapofanya mitihani?” Khadija dada wa Hemed alimwuliza Beka . “ Hiyo simuachii mtu, nitaing ’ang ’ ania hadi nitakapomaliza shule, ” Beka alimwambia . Kufuatia kusema hivyo , dada zake Hemed walimpongeza Beka na kumfahamisha kwamba rafiki yake Hemed kichwani alikuwa ziro sababu ya michezo . Akina dada hao walimuomba Beka ajitahidi kumsaidia mwenzake ili aweze kufanya vizuri katika masomo , Beka akawaambia hakukuwa na tatizo angezungumza naye . Kwa kuwa ilikaribia saa moja , Beka aliwaaga wenyeji wake akashika njia kuelekea uwanjani alikopanga kukutana na Rhoda . Baada ya kutembea kama dakika nane hivi alifika uwanjani ambapo muda huo walikuwepo watoto kadhaa wakicheza mpira pembeni ya uwanja. Alishukuru kuona kwenye goli walilokubaliana kukutana na Rhoda ambalo mita kama kumi palikuwa na miembe iliyokuwa na matawi yaliyoanguka mpaka chini hakukuwa na watu. Beka alijongea mpaka kwenye mwembe huo na kukaa kwenye gogo la mnazi akakaa na kuanza kumsubiri Rhoda . Haukupita muda mrefu alimuona Rhoda akija , kwa mara yake ya kwanza moyo wake ulipiga paa hakujielewa kwa nini alipatwa na hali hiyo .



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog