IMEANDIKWA NA : HUSSEIN O. MOLITO
*********************************************************************************
Sehemu Ya Kwanza (1)
Ni miale ya jua la asubuhi ikijitokeza kwa kasi kubwa. Watu wengi waishio katika jiji lenye pilika nyingi Tanzania kuliko majiji yote wakionekana wakienda kwenye majukumu ya kila siku.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wanafunzi wakielekea shuleni kutokana na kuwa ilikua ni siku ya kufungua shule baada ya likizo kubwa ya mwezi wa kumi na mbili. Wanafunzi wengi walionekana kuwa na nyuso za furaha kwa kuwa walikuwa wamawakumbuka sana marafiki zao waliopoteana mwezi mzima na siku kadhaa. Pia walikua na furaha ya kupanda kidato.
FRANK ni mmoja kati ya wanafunzi wa chuo kikuu huko Dodoma. Yeye alikuja Dar mara moja kwa ajili kuwasalimia wazazi wake kutokana na kuwakumbuka sana.
Siku hiyo ndio siku aliyokua anaisubiri kwa hamu ili aondoke na kurudi zake chuo kuendelea na masomo.
Akiwa nje akipaki mabegi yake tayari kwa safari, alikuja msichana mmoja akiwa na ua mkononi na kumpa Frank.
“nakutakia masomo mema.” Aliongea yule msichana huku akiwa ameendelea kulishika lile ua bila kupokewa na Frank.
“hivi Lulu ni mara ngapi nimekukataza tabia za kunishobokea?” aliongea Frank kwa hasira na kulichukua lile ua na kumpiga nalo yule dada usoni.
Kwa huzuni yule dada aliguza njia na kuondoka huku machozi yakimlenga lenga.
Lile tukio zima lilishuhudiwa na mama yake Frank, hakukubaliana nalo. Alimfata Frank kwenye gari na kumpa makavu yake.
“sijaipenda tabia uliyoinyesha kwa mwenzio. Hata kama amekukoosea, hupaswi kufanya yale uliyomfanyia.” Aliongea mama yake Frank na kuingia ndani kwa hasira. Frank hakujali, aliendelea kuingiza mizigo yake kwenye gari. Alipomaliza , baba yake alitoka na kungia kwenye gari tayari kwa kumpeleka Frank ubungo.
Waliagana baba na mtotoo, na basi lililokuwa linasubiri abiria wachache tu kutokana na muda wa kuondoka kufika, lilianza taratibu kutoka kwenye kituo kikubwa cha mabasi ya mikoni ubongo. Safari ilianza salama na kila abiria alionekana kuridhishwa na mwendo wa basi hilo. Zawadi mbali mbali zilitolewa kila mara huku movie tamu zikiendelea luwa kiburudisho kikuu ndani ya basi lile lenye hadhi ya kuitwa luxury.
Baada ya masaa saba, tayari basi lilikua limeshafika Dodoma. Abiria wote walishuka wakiwa na uchovu kiasi lakini wakimpongeza dereva kwa kuwa makini. Pia walimshukuru sana mungu kwa kuwafikisha salama.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Frank alikodi Taksi iliyomfikisha mpaka chuoni anaposoma. Huko alikutana na marafiki zake kibao walikuja kumlaki kutokana na kuwa kipenzi chao ambae walikua wanampenda sana.
Utanashati wa Frank pamoja na uzuri wa sura na mwili aliokuwa nao, uliwavutia wasichana wengi waliosoma chouni hapo. Ucheshi na uongeaji wake pia uliwatuia wanaume wenzake ambao hakuwaletea pozi.
Uwezo wake wa kujibu maswali na kujiamini kuliwafanya watu wengi kumtegemea kwenye group discutions nyingi ambazo alikua mfafanuaji mzuri wa maswali yaliyowasumbua.
Umuhimu wake huo ulimfanya ajulikane si kwa rika lake tu, bali hata wazee waliokuwa wanasoma hapo walimjua na kumfata awasaidie.
Kipaji chake cha kusakata kabumbu ndio kilichomfanya awe Super star chuo kizima. Hata walipoenda kushindana na taasisi mbali mbali, basi timu ya chuo chao iliibuka kidedea kutokana na uwezo wa kukaba na kufumania nyavu wa Frank.
Wasichana wengi walimgombania, lakini Frank aliwajibu majibu ya Dharau kama hakuna msichana wa pale chuoni mwenye hadhi ya kuwa naye.
Nyodo zake juu ya wasichana hakukumfanya achukiwa na wasichana wote, bali wengi walijiangalia na kukiri kuwa hawana hadhi ya kuwa na mvulana mzuri kama yule.
Kila nguo aliyovaa ilinata na mwili na kuwa mpya kila siku. Alibadilisha style za nywele kila msimu na kuwa na muonekano mwingine wa kuvutia zaodi ya mwanzo.
Taarifa za kuingia msichana mpya na kisu chuoni hapo zilipenya vizuri kwenye ngoma za masikio ya Frank na kumfanya atamani kumuona.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Siku ya pili yake akiwa darasani, kwa mbaali alimuona msichana ambaye alikua mgeni machoni mwake akiingia kwa pozi na kwenda kukaa kwenye kiti ambacho kipo mbali nay eye. Alipata muda wa kumuangalia na kuutathmini uzuri wa yule dada mweupe wa asili na wenye kuvutia. Macho yake yaliongezwa muonekano mzuri na kope za kubandika pia style ya nywele ndio ilikua ya kipekee na kumfanya kuwa tofauti na wasichana wote aliowahi kuwaona pale chuoni.
Frank alitabasamu na kujisemea kimoyo moyo.
“bila shaka huyu ndio chaguo nililolikua nalisubiria muda mrefu”
Moyo wa Frank ukajikuta kwenye zone ya mateso kwa kipindi kile. Hakikia yule dada hakubisha hodi, alipenya moyoni mwa Frank moja kwa moja.
Uvumilivu ulimshinda na kumfata yule msichana pale alipokaa.
“mambo.” Alisalimia Frank na kuinyoosha kola yake vizuri ambayo ilidondoka kwa kuwa yeye alipenda kuisimamisha kola yake kama style ya uvaaji aliyichagua.
“safi tu.” Aliongea yule dada na kumtazama Frank. Kitu kama upinde kiligota moyoni mwake na kuondoka bila kuacha maumivu wala damu kwa jinsi alivyokuwa anajisikia Frank baada ya kusikia lafudhi nzuri ikitoka kinywani mwa yule binti.
Alizidi kuchanganyikiwa baada ya kumuona alivyo vaa. Alikua kavaa ngou laini yenye rangi nyekundu iliyomshika mwili wake mwembamba kiasi. Chini alivaa sketi fupi nyeusi iliyomfanya sehemu kubwa ya miguu yake mpaka kwenye mapaja kuwa wazi. Mvuto wa ngozi ya yule msichana uliongezeka zaidi kwenye mapaja yake ambayo yalikuwa meupe kumshinda yeye mwenyewe.
Ukaguzi mfupi wa macho ya Frank ulimpa majibu mengi na ukiyachukua majibu yote na kuyapatia jina moja tu utasema kwa herufi kubwa kuwa yule dada ni MZURI.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“heheheee.. we ni mgeni bila shaka.” Aliongea Frank na kuanza kujichekesha chekesha.
“yap,.. nina siku mbili tu toka nimeanza chuoni hapa.” Aliongea yule dada kwa swaga ambazo Frank hajawahi kuziona kwa msichana yeyote toka anazaliwa.
“naomba niwe mwenyeji wako” alijikuta Frank akiongea maneno yale baada ya kuweka kambi karibu na yule dada.
“mbona nimeshakuwa mwenyeji!, nimejuana na watu wengi na nimeyafurahia mazingira yote ya hapa chuo.” Aliongea yule dada na kutabasamu. Hakika alibonyea sehemu zipatazo mbili kwenye uso wake. Alibonyea kwenye mashavu kama watu wangi ambao tumewaona. Lakini yeye alibarikiwa kubonyea tena pembeni ya midomo yake. Hilo nalo lilizidi kuwa chachu ya uzuri wa yule dada aliyeumaliza kabisa moyo wa majivuno na kumuweka moyo wa kutapa tapa Frank ambaye alizidi kujipendekeza kwa yule dada.
“basi tujuane hata kwa majina. Kuitana kaka na dada wakati tuna majina yetu naona kama sio poa?” aliongea Frank na kumuangalia yule dada usoni.
“naitwa NEILA” aliongea yule dada na kumuangalia Frank usoni kwa mapozi ya hali ya juu na kuyanyanyua macho yake kivivu na kuwa kama ameyarembua Fulani hivi na kuzidi kumuweka mwenzake kwenye hali mbaya.
“waooooooh!... jina zuri sana. Mimi naitwa Frank.” Alijitambulisha Frank na kuendelea kumuangalia Neila ambaye alikua na vitu vingi vinavyovutia kwenye macho yake.
“Frank Patrick.” Aliongea Neila na kulitaja jina kamili la Frank.
“wewe, umelijuaje jina langu kamili?” aliongea Frank kwa mshangao mkuu.
“cha ajabu ni nini?.. kwani kuna mtu asiyekufahamu hapa chuo. Hata mtu akija leo taarifa za kwanza ataambiwa kuhusu wewe.”
Alifafanua yule dada na kumfanya Frank acheke.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Usiku wa siku ile haukupita usingizi kabisa. Usiku kucha sura na umbo la Neila lilizidi kumjia Frank na kumfanya wakati mwingine kutabasamu pake yake.
Asubuhi aliingia darasani kama kawaida na kumfata yule dada na kumsalimia. Siku hiyo alivaa nguo ndefu na kujipigilia ushungi juu. Style ya kujifunga kitambaa na kujiviringita ushungi na kuonekana kama ana nywele nyingi ndio kulimfanya kubadilika kabisa. Hakutofautiana na waarabu kwa jinsi alivyokuwa mweupe na kope za bandia zilivyomtoa. Hata Frank na yeye akaamua kubadilisha salamu tofauti na salamu aliyompa jana yake.
“assalaam-aleykum.”
Alijikuta Frank anasalimia hiyo salamu wakati yeye alikua haitumii kabisa akiamini hiyo salamu wanapeana waislamu wakutanapo tu. Na si yeye mkiristo kuitamka. Lakini kwa muonekano wa yule dada ilimbidi ajikakamue na kuitoa japo matamshi yake yalikuwa ya kubahatisha.
“waaleykum salaam, kayfal-khaly” aliitika yule dada na kutabasamu.
“hapo umeniacha kidogo” Aliongea Frank na kumfanya yule dada kuangua kicheko. Mpangilio mzuri wa meno meupe ya Neila ulionekana wazi kwa mara ya kwanza kwa Frank.
“kayfal-khaly maana yake vipi hali yako au wajionaje na hali.” Alifafanua Neila.
“ sasa unatakiwa ujibu vipi ukiulizwa hivyo?” aliongea Frank na kuonyesha wazi kuwa yupo tayari kujifunza salamu hiyo ya kiarabu japokuwa alikua mkiristo.
“twayib au bikhayri walilahil-hamdu.” Alijibu Neyla na kumuonyesha Frank kuwa kapita pita kidogo madrassa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“haya,..maana yake?” aliuliza Frank na kukaa vizuri.
“twayib maana yake ni nzuri. Na bikhayri walilahil-hamdu maana yake ni njema na mungu anasaidia.” Alijibu Neila na kutabasamu.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment