Search This Blog

Monday, October 24, 2022

MAPIGO YA MOYO - 2

 







    Chombezo : Mapigo Ya Moyo

    Sehemu Ya Pili (2)





    Baada ya maongezi machache, Frank akaenda kukaa kwenye kiti chake na kuendelea kujisomea akisubiri kipindi kianze.



    Muda wa mapumziko ulipofika, wote walitoka na kwenda kupata chakula. Frank alienda canteen kununua chakula na kuanza kumtafuta Neila alipo. Alimtafuta vya kutosha na baadae akamuona akiwa amekaa peke yake kwenye bustani iliyokuwa na upepo tulivu kwa ajili ya kujisomea. Neila alikua anapata kinywaji chake na kufunua baadhi ya vitabu vyake na kuanza kujisomea.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Frank aliamua kumfuata pale alipokaa na kumuuliza ni kitu gani amletee.



    “nikuambie kitu Frank, kuanzia leo hii sihitaji mazoea na wewe. Tena kaa mbali na mimi.”

    Aliongea maneno yale yule dada na kumfanya Frank atoe macho kwa mshangao. Hakuamini alichokisikia kutoka kwa yule dada.

    Kwanini jamani?” aliuliza Frank huku akiwa na hofu juu ya kubadilika ghafla kwa Neila. Maana masaa matatu yaliyopita walikua wanaongea vizuri mpaka kufundishana salamu ya kiarabu.



    “kaa wewe kama unaona nafaidi…. Stupid.” Aliongea Neila kwa hasira na kukusanya vitu vyake na kuondoka huku anasonya.



    “Neila, Neilaaaa”

    Aliita Frank, lakini sauti yake haikuwa na uwezo wa kumbakisha Neila pale walipokua. Zaidi aliongeza spidi bila kumuangalia Frank na kumfanya ajione ameonewa kwa kitendo alichofanyiwa.

    Alitamani kulia kwa kile kilichotokea. Frank alitaka kujenga mazoea ili amuweke wazi juu ya upendo wake juu yake. Leo anajikuta anakataliwa hata urafiki wa kawaida. Roho ilimuuma kiasi cha kubakia chembe tu kupasuka. Bila ridhaa yake, machozi yalianza kujenga mifereji kwenye mashavu yake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mawazo juu ya Neila yalichukua nafasi kwenye kichwa chake. Hata hivyo alipiga moyo konde baada ya kujiangalia na kujiona yupo safi. Alikua na umbo la kumvutia msichana yeyote anayependa wavulana wazuri. Hakua na kasoro yoyote. Alijiuliza labda ni kipi alichomtendea labda ndio sababu mpaka Neila ameamua kumtamkia maneno kama yale.



    Kwa dakika kadhaa alijirundikia maswali kichwani mwake bila kupata majibu sahihi. Alitamani kwenda kumuuliza kama kuna kosa lolote alilomtendea labda ili amuombe msamaha. Lakini roho ya kiume ilimjia na kuona kumuuliza huyo msichana ni udhaifu wa wazi na inaweza ikawa sababu ya huyo msichana kumdharau.



    Toka anaanza mapenzi, hakuwahi kumtongoza msichana ingawaje wasichana aliokutana nao kimwili hawakua na idadi.

    Wengine walijisikia raha kutembea na staa kama yeye toka alipokuwa shule ya msingi.

    Sio wanafunzi tu, alipokua sekondari mpaka walimu wadogo wadogo waliokuwa wanafanya field kwenye shule yao walimtamani na wengine kudiriki kumvulia nguo ya ndani Frank ambaye alikua na umbo kubwa na lenye mvuto toka alipobalehe.



    Kumbukumbu hizo zilitaka kuwa story baada ya wazazi kadhaa wa majirani zao kuleta kesi kwa wazazi wake juu ya tabia mbaya ya mtoto wao.



    “yaani huyu ndio ananitoa machozi. Ana nini cha ajabu?..mbona nishatembea na wasichana wazuri zaidi yake na wote walikua wananililia na kuniachia malighafi zao bila ya kuwatongoza? Ana nini huyu??”

    Maswali ya kishujaa yalimfuta machozi na kuamua kujipa majibu chanya juu ya kuangalia ni nini kitatokea mwisho wa safari.



    Pia idadi kubwa ya wasichana wanaojigonga kwake kila siku ilimpa moyo labda yule dada alikua anajikosha ili abembelezwe.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Roho ya kijasiri ikajijenga kwa Frank na yeye akaamua kuuchuna na wote wakawa kila mtu na zake bila kujua sababu ya kuwa vile.



    Mitihani ya kumaliza semester ilifika na kila mmoja akawa bize zaidi katika kusongoka ili apate matokeo mazuri.



    Kipindi chote hicho cha miezi minne, Frank na Neila walikua hawana hata salamu. Kila mmoja aliangallia yake.

    Neila nae alipata marafiki wengi wa kike na wakiume kwa uzuri wake na uwezo pia wa darasani.

    Alikua kichwa na kuwasaidia baadhi ya wanafunzi waliotaka msaada wake. Kitu hicho ndicho kilichomfanya Frank aongeze bidii katika kusoma ili asije kupitwa na Neila kwenye mitihani.



    Muda uliosuburiwa ulifika na wote wakaingia kwenye chumba cha mtihani na kufanya hiyo mitihani huku kila mmoja akihofia kupitwa na mwenzake.



    Baada ya kumaliza mitihani, kuliandaliwa mechi kubwa kati ya chuo chao na timu ya mkoa wa Dodoma.



    Ilikua ni mechi kali na kubwa iliyochezeka kwenye uwanja wa mkoa na iliyojaza mashabiki wengi kutokana na viongozi kadhaa kuahidi kuhudhuria mchezo huo. Iliandaliwa harambee ya kuchangia watoto watima na bunge kupitia mchezo huo. Hivyo kiingilio cha elfu moja kilitumika na V.I.P walichangia elfu ishirini.



    Kipyenga kililia kuashiria mchezo unaanza. Wachezaji wa Tiger Fc ambayo ndio jina la timu ya chuo, walionekana kushangiliwa zaidi kuliko timu ya Dodoma heroes F.c ya mkoa wa Dodoma kutokana na ufundi wa wachezaji kadhaa akiwemo kapteni wao Frank

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Daudi anapiga chenga mbili tatu na kumpenyezea nani pale jezi namba saba mgongoni, ni Frank pale anachukua mpira na umati wote hapa unapiga kelele. Anamfinya wa kwanza hapa..anapiga shuti kaliiiii….ni ni hapa.. ni.. gooooooooooooool”



    Ilikua sauti ya mtangazaji iliyowanyanyua watu karibia wote waliokua kwenye uwanja ule. Mashabiki wengine walivua jezi na kubaki na T-shirt na wasichana kubaki na vitopu vilivyoandikwa FRANK THE AMAZING PLAYER.



    Frank aligeuka na kuwaangalia wasichana waliokuwa wakiogoza kwa kushangilia na kuona walivyopendeza kwa kuvaa vitopu hivyo vilivyofanana.



    Alipotupa macho yake vizuri, alipigwa na butwaa baada ya kumuona Neila akiwa amevaa kitopu hicho huku akiwa anashangilia kama amepagawa huku akipuliza vuvuzela.



    Ghafla akajikuta moyo wake umefarijika. Hakutegemea kutokea kitu kama kile. Kuanzia hapo sasa alianza kucheza kwa sifa.



    Mpaka mapumziko timu ya Tiger F.c ilikua inaongoza kwa magoli matatu ambayo yote yalifungwa na kiungo mshambuliaji hatari Frank.



    Kipindi cha pili kilianza kwa kasi. Ujuzi mkubwa wa kumiliki mpira uliwafanya Tiger F.c kuwachezesha wenzao nusu uwanja.



    Wakati Frank anawapangua mabeki ili akashinde, ndani ya kumi na nane akachezewa rafu mbaya na mabeki wa timu pinzani.

    Uwanja wote ulitulia baada ya kumuona Frank akigalagala kwa uchungu. Machela ilikuja na kumchukua haraka na kumtoa nje ya uwanja.



    Kutokana na maumivu makali ailiyokuwa anayasikia, Frank alimuonyeshea kocha wake ishara ya kufanya mabadiliko kwakua hatakuwa na uwezo wa kuendelea na mechi. Ambulance ilifika na kumchukua Frank na kumpeleka hospitali.



    Baada ya masaa kadhaa Frank alirejewa na fahamu baada ya kupigwa sindano ya ganzi. Alipoangalia mguu wake, alikuta amefungwa ogo kuashiria ulikua umeteguka.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya kuangaza huku na huko. Alikuta wanafunzi wenzake wengi wamekuja kumuangalia.

    “pole sana Frank.”



    Ilikua kama kengele aliyoizoea kuisikia baada ya kusikia lafudhi iliyompa afueni ya maumivu kwa muda huo. Haraka aligueza shingo yake kuangalia upande wa pili ambao ulikua na wanafunzi wachache na kukutana na tabasamu murua la mtoto mzuri aliyeukosha moyo wake. Si mwingine bali ni NEILA.



    Frank alipokea pole nyingi kutoka mashabiki wake walioendelea kumiminikia kama mvua pale hospitali.



    Baada ya chuo kufungwa, Frank alirud Dar akiwa na ogo mguuni. Alipokelewa na wazazi wake ambao hawakumshangaa kwakua mechi hiyo walikua wakiishuhudia live kwenye tv.



    Taarifa za kurudi kwa Frank zilimfikia Lulu na kuamua bila kupoteza muda kumfuata Frank nyumbani kwao.

    “shikamoo mama.” Alisalimia Lulu kwa heshima zote.

    “marahaba mwanangu, karibu.” Aliitikia mama yake Frank na kutabasamu. Baada ya kuhakikisha Lulu amekaa katika moja ya masofa yaliyojaa pale sebuleni, alienda chumbani kwa Frank na kugonga mlango. Frank alifungua mlango na kumkaribisha mama yake ndani.

    “kuna mgeni wako amekuja.” Aliongea mama yake Frank.

    “nani tena huyo mama.” Aliongea Frank na kumuangalia mama yake.

    “we toka nje utamuona” aliongea mama Frank na kutoka nje.



    Baada ya kujishauri kama dakika moja hivi, Frank alitoka ndani kwake na kwenda sebuleni na kumkuta Lulu amekaa pale sebuleni. Alimuangalia kwa muda kisha akaenda kukaa umbali mdogo kiasi na Lulu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “mambo Frank” alisalimia lulu hukua akiwa na uoga kiasi kutokana na macho makali aliyokuwa akiangaliwa na Frank.

    “safi,” alijibu kifupi Frank na kufanya kimya kitawale kwa dakika kadhaa.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog