Search This Blog

Monday, October 24, 2022

MWAJUMA UTAMU - 2

 







    Chombezo : Mwajuma Utamu

    Sehemu Ya Pili (2)



    Kiukweli sikuweza kumkubalia kirahisi, nilihofia mambo mengi mabaya ambayo angeweza kunifanyia lakini baada ya kunohakikishia kuwa ningekuwa salama na kuniondoa hofu ilibidi nimkubalie. Akanichukua na kunipeleka mpaka kwake.

    Kilikuwa ni chumba kimoja, nilipofika nilifikiria ni jinsi gani ambavyo ningeweza kulala humo lakini hilo halikuwa tatizo. Yule mwanaume aliniambia kuwa nilitakiwa kulala kitandani na yeye angelala chini na maisha yangeendelea hivyo.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ngoja nikuambie kitu msichana mwenzangu, kijana mwenzangu unayeisoma simulizi hii. Unajua kwenye haya maisha unaweza ukakutana na vikwazo vingi lakini baadhi ya watu wanaokutazama wakakuchukulia kuwa hayo yote unayopitia ni haki yako, wengine wanaweza kwenda mbali zaidi na kukutukana na kukulaumu kwa ujinga uliyoufanya.

    Yote haya yanaweza yakatokea katika maisha na kitu unachotakiwa kukifanya ni kujua ni jinsi gani ambavyo unatakiwa kupambana nayo na si muda wa kujilaumu na kuona kama wewe ni mkosani mbele za Mungu na hutakiwi kusamehewa.

    Kwanini nakwambia haya ni kwasababu ya makosa niliyoyafanya katika maisha yangu, ujinga niliyoufanya, sitaki urudie makosa yangu sitaki urudie kufanya ujinga wangu, nataka ujifunze kitu kupitia simulizi hii ya maisha yangu.

    Angalia kwa muda ambao niliweza kukutana na mwanaume ambaye hata sikuwa nikilifahamu jina lake tayari nilimuamini, niliukubali msaada aliyohitaji kunipa, bila kufuata taratibu zozote nikajikuta nikiingia ndani kwake na maisha yakaanzia hapo.

    Mwanzoni alionyesha moyo wa kunisaidia kweli, aliguswa na simulizi yangu ya kufukuzwa, hakujua nini kilisababiaha ila moja kwa moja aliamini nilionewa hivyo alihitaji kunisaidia.

    Maisha yalianzia hapo huku kila siku mwanaume huyo akiniaga kwenda kwenye mihangaiko yake. Aligeuka kuwa msaada mkubwa sana kwangu, alinihudumia kwa kila kitu nilichokuwa nikikihitaji, maisha yalikuwa rahisi kwangu.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ama kwa hakika penzi ni kikohozi kama wasemavyo wahenga, baada ya kupita siku kadhaa nikajikuta nikiwa katika mahusiano na mwanaume huyo ambaye nilifanikiwa kulifahamu jina lake tayari. Nakumbuka alijitambusha kwa jina la Oscar, ni katika penzi hili ambalo lilienda kunipa funzo lingine jipya la maisha yangu.



    Nilijikuta nikizama kwenye dimbwi la kimapenzi na Oscar, huyu alikuwa ni mpiga picha, alikuwa akimiliki studio yake ya picha iliyokuwepo Sinza Palestina.

    Kimuonekano alikuwa ni kijana mtanashati, kiukweli nilitokea kumpenda kwa moyo wangu wote. Kipindi nipo katika mahusiano naye nilisahau shida na matatizo yote niliyokutana nayo katika maisha yangu, sikutaka kukumbuka kitu chochote kilichotokea nyuma.

    Oscar alinipenda sana, ahadi zake za kunioa ndizo zilizonifanya nikazidi kumuamini mara dufu, bila kujali nikamkabidhi mwili wangu ambao aliutumia autakavyo.

    Maisha yalibadilika kwa kiasi fulani, nilikuwa nikiishi maisha yenye furaha, Oscar aliendelea kunijali, alinipa matunzo pamoja na mapenzi moto moto.

    Kiukweli wazo la kurudi nyumbani kichwani mwangu halikuwepo kabisa kwa wakati huo, niliona ni jambo gumu mno kurudi katika maisha ya kimasikini niliyozaliwa katika familia yetu.

    Nilikuwa nikiishi maisha ya furaha yaliyogubikwa na amani tele, sasa kwanini nikumbuke maisha ya kimasikini ya nyumbani kwetu?

    Hilo lilikuwa ni jambo gumu mno kutokea.

    Siku ziliendelea kukatika huku penzi likizidi kupamba moto, Oscar aliendelea na kazi yake ya upiga picha, muda mwingi aliutumia katika kazi yake hiyo, mwanzoni sikuwa na wasiwasi wowote, niliamini katika mapenzi ya dhati pamoja kazi yake, sikutaka kumuwazia vibaya.

    Baada ya kupitia mwezi mmoja nilianza kusikia maneno ya chinichini kutoka kwa majirani ambao tayari nilianza kuwazoea. Waliniambia kuwa Oscar alikuwa ni mume wa mtu na kipindi hicho mke wake alikuwa amesafiri.

    Nilipoyasikia maneno hayo sikutaka kuamini hata kidogo, nilihisi walipanga kutugombanisha hivyo sikutaka kuyapa uzito maneno yao.

    Maisha yaliendelea huku kila siku maneno yakiwa ni yaleyale. Mwanzoni nilionekana kuyapuuzia lakini nilipoona yamezidi ilibidi nimuulize Oscar.

    "Nani kakuambia maneno hayo?" aliniuliza huku akionekana kukubwa na mshangao.

    "Kuna watu wameniambia," nilimjibu.

    "Nilikwambia usipende kuamini kila unachoambiwa," aliniambia.

    Kiukweli ilikuwa ni vigumu kuamini kama Oscar alikuwa akinidanganya, alionekana kumaanisha kila kitu alichokuwa akikizungumza, hakutaka kuona nikiendelea kuyasikiliza maneno ya watu ambayo yangeweza kuvuruga amani ya mapenzi yetu.

    Hilo lilizidi kunifanya nimuamini sana Oscar kupita maelezo hata pale nilipokuwa nikitahadharishwa na watu sikutaka kuwasikiliza, niliwaona ni binadamu wenye nia mbaya kwangu, hawakupenda mafanikio yangu.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Binti utajiingiza katika matatizo huyo unayeishi naye ni mume wa mtu," aliniambia Mama mmoja niliyemfahamu kwa jina la Mama Musa.

    "Si kweli," nilimwambia huku nikiamini hakukuwa na ukweli wowote.

    "Shauri yako binti unachokitafuta utakipata tu," aliniambia huku akionekana kunihurumia.

    Bado sikutaka kuyaamini maneno yao, niliendelea kuwa katika mahusiano na Oscar. Miezi iliendelea kukatika hatimaye mwaka huo ukapita, ulipoingia mwaka 2011 mwezi wa kwanza ndipo nilipofanikiwa kubeba ujauzito wa Oscar.

    Nilifurahi sana baada ya kuubeba ujauzito huo, niliamini huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa kuyaanza maisha mapya ya familia lakini ilikuwa ni tofauti kabisa na mawazo yangu.

    Oscar alibadilika ghafla! baada ya kumpa taarifa hizo za ujazito, hakuwa Oscar yule niliyekuwa nikimfahamu, hakutaka kuamini kama nilikuwa nimebeba ujauzito wake, hilo lilizidi kumchanganya sana.

    Nilishindwa kuelewa ni nini kilichokuwa kikiendelea, nilishangazwa na mabadiliko yake na hata nilipomuuliza nilishangaa akinigombeza na kunitolea maneno makali.

    Nilihisi kuchanganyikiwa, sikutaka kuamini kama Oscar aliukataa ujauzito wake, hilo lilizidi kuniumiza sana, nilishindwa kuvumilia machozi yakaanza kunidondoka mfululizo.

    Wakati nilipokuwa katika maumivu ya kukataliwa ujauzito ndipo hapohapo ambapo nilipokea maumivu mengine nisiyoyatarajia katika moyo wangu, Oscar aliamua kunieleza ukweli wa maisha yake.

    Aliniambia alikuwa ni mume wa mtu na kipindi hicho mke wake ndiyo alikuwa akikaribia kurudi kutoka safarini.

    Nilihisi kuchanganyikiwa baada ya kusikia maneno hayo, niliyakumbuka yale maneno niliyowahi kuambiwa na baadhi ya majirani lakini kutokana na kiburi changu sikutaka kuwasikiliza.

    Mapenzi hatimaye yakaniingiza katika dunia ya maumivu na machozi, sikujua nilitakiwa kulia na nani kwani kama kuonywa nilionywa sana lakini sikutaka kusikia la mwadhini wala la mnadi swala.

    “Kwahiyo unaamuaje?” nilimuuliza.

    “Kuhusu nini?” aliniuliza.

    “Huu ujauzito wako?”

    “Mwajuma wewe ni chizi, mpumbavu, mshenzi, fala, hujielewi kabisa hivi unahisi ninaweza kuwa baba wa huo ujauzito wako? nenda katafute Baba halali lakini siyo mimi,” aliniambia Oscar maneno yaliyonifanya nitokwe na machozi. Nilishindwa kuzungumza, niliendelea kulia.

    Kama ni makosa tayari nilikuwa nimeshayafanya. Kitendo cha kuishi na mwanaume bila ndoa, nikamuamini pasipokutegemea kama mwisho wa siku ningeweza kuvuna maumivu, hakika lilikuwa ni kosa kubwa mno nililolifanya.

    Hatimaye Oscar aliweza kunifukuza, nikaanza kuishi maisha ya kutangatanga mitaani. Sikuwa na ndugu wala rafiki kusema labda ningeenda kumuomba hifadhi kwa muda, nilikuwa ni mimi na ujauzito wangu pekee.

    Maisha yangu yalikuwa ni ya kutangatanga mitaani huku nikiomba msaada wa pesa na wakati mwingine nilikuwa nikienda kwa Mama Ntilie kuomba chakula, usiku ulipoingia nilikuwa nikilala nje, kiufupi hayo ndiyo yalikuwa maisha yangu tangu nilipoweza kufukuzwa na Oscar.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mwanzoni niliona ugumu kuishi maisha hayo lakini kadri siku zilivyokuwa zikizidi kusonga mbele, nilijikuta nikizoea na kuona ni maisha ambayo ni ya kawaida kuishi.

    Siku moja nilikutana na msichana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Savela, aliponiona alihitaji kunisaidia. Nilipojitambulisha Savela alianza kunisifia, nikashangazwa na sifa zake yaani iliwezekana vipi msichana mwenzangu kama yeye akaanza kunisifia kama mwanaume?

    Hilo lilinifanya nianze kuogopa, nilihisi Savela hakuwa mtu mwema kwangu, nilipokuwa nikimuangalia nikatamani anipe pesa kisha niondoke zangu.

    Baada ya Savela kunihoji na kugundua mengi yaliyokuwa yamenitokea, alihitaji kunisaidia.

    Nilisita kuchukua maamuzi ya haraka lakini baada ya kujifikiria maisha ambayo tayari nilikuwa nikiishi nilijikuta nikikubali tena bila kipingamizi chochote.

    Alinichukua na kunipeleka mpaka nyumbani kwake alipokuwa akiishi maeneo ya Tegeta. Kwa muonekano wa nyumba yake jinsi ilivyokuwa ikionekana ilikuwa ni vigumu kuamini kwamba Savela ndiye ambaye alikuwa mmiliki wa nyumba hiyo, hakufanania kabisa.

    "Hapa ni kwako?" nilijikuta nikiropoka na kumuuliza.

    "Ndiyo hii ni nyumba yangu," alinijibu huku akionekana kuwa kawaida, hakujali lolote.

    "Hongera ni nyumba nzuri sana," nilimwambia huku macho yangu yakiendelea kutazama sehemu za nyumba hiyo.

    "Unaishi na nani?" nilimuuliza.

    "Peke yangu," alinijibu.

    Ilionekana kuwa ni nyumba kubwa iliyokuwa na vyumba vingi sana, kitendo cha Savela kuniambia kuwa aliishi peke yake kilinishangaza sana, sikutaka kuamini lakini huo ndiyo iliyokuwa ukweli.

    Siku hiyo ikapita huku nikiwa nimeshapata bahati ya kufadhiliwa na Savela ambaye alionekana kuwa na moyo wa kipekee sana.

    Hapa ngoja nikwambie kitu, nilikuwa mchafu sana, sikuwa na nguo zaidi ya niliyokuwa nimeivaa. Siku iliyofuata Savela aliamua kunipeleka kwenye duka la nguo maeneo ya Kinondoni, tulipofika huko alininunilia nguo, alinipeleka saluni ambapo huko nikazidi kupendezeshwa, ndani ya masaa kadhaa nilikuwa nimebadilika, sikuwa Mwajuma yule mchafu ambaye nilishindia nguo moja.

    "Kwanini unayafanya yote haya?" nilimuuliza.

    "Usijali Mwajuma nafanya haya kama masaada wangu kwako, najua umepitia magumu mangapi, sitaki kuona ukirudi kule wakati wewe bado ni msichana mrembo, unavutia, wasichana wenzako kama wewe mjini hawafi njaa, wanafanikiwa kiulaini," aliniambia maneno ambayo aliniacha nayo njia panda.

    "Unamaanisha nini?"

    "Usijali muda ukifika utajua namaanisha nini au wewe hupendi kuona ukiwa na maisha mazuri, ukamiliki nyumba ya kifahari, ukamiliki gari la gharama, ukawa mfanyabiashara mkubwa sana hapa mjini yaani kila mtu akawa anakuzungumzia wewe tu?"

    "Napenda ila..."

    "Basi kila kitu kinawezekana, mimi binafsi nimewahi kuishi kama yako, niliteseka mno, hakukuwa na mtu wa kunisaidia yaani kama sio mimi mwenyewe kujitambua sijui leo hii ningekuwa wapi?" alisema Savela kisha akaendelea kuzunguza.

    "Umeiona ile nyumba yangu ya Tegeta nimeinunua juzi tu, nafanya biashara inayoniingizia pesa nyingi mno, sijasoma lakini nimeweza kufanya vitu vikubwa ambavyo wasomi wameshindwa kuvifanya," aliniambia Savela.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa muda ambao Savela aliutumia kuzungumza na mimi tayari alikuwa ameipandikiza mbegu ya tamaa ya mafanikio ndani yangu, alijua kunishawishi, alijua kuzungumza yaani maneno yake yalitosha kunifanya nitamani kujua ni biashara gani hiyo ambayo alikuwa akiifanya.

    Siku ziliendelea kukatika huku ujauzito nao ukiendelea kukua, mwanzoni nilimficha Savela hali niliyokuwa nayo lakini kama unavyojua mimba haiwezi kufichika mwisho wa siku alifahamu kila kitu.

    Hakuonekana kuchukia baada ya kufahamu ukweli ambao nilimficha hapo awali, alinikumbusha kuhusu msaada ambao aliamua kunipa ulikuwa ni wa lengo la kufanya biashara. Ilibidi nimuulize ni biashara gani hiyo ambayo kila siku alikuwa akinidokeza na ndipo hapo ambapo aliniambia ukweli, aliniambia biashara hiyo ilikuwa ni ya uchangudoa yaani ilitakiwa nijiuze ili niweze kupata pesa, alienda mbali zaidi na kuniambia kuwa mafanikio yake yote yalisababishwa na biashara hiyo uchangudoa.

    Nilihisi mwili wote ukipigwa na ganzi baada ya kuyasikia hayo, sikutaka kuamini hata kidogo, kuna muda nilidhani labda alinitania lakini hakukuwa na utani kati yangu na yake.

    “Baba wa huo ujauzito ni nani?”

    “Ni Oscar.”

    “Anajua?”

    “Ndiyo ila anifukuza, aliukataa.”

    “Sawa, sasa kwenye kazi hii ya uchangudoa ujauzito hautakiwi, utakupotezea wateja," aliniambia Savela.

    Licha ya kuwa nilitokea katika maisha ya kimasikini pamoja na kukutana na changamoto zote mpaka kufikia hatua ya kukutana na Savela bado nilikuwa mwenye tamaa.

    Tamaa ya utajiri ilishakwishaniingia, kila nilipokuwa nikimuangalia Savela pamoja na mafanikio aliyokuwa nao katika maisha yake sikutaka kuamini kama biashara hiyo ya uchangudoa ndiyo iliyomletea mafanikio yote hayo, kuna muda nilikataa lakini mwisho wa siku nilijikuta nikiamini.

    Kwa kuwa nilikuwa tayari kufanya lolote Savela alinishauri niende hospitali nikautoe ujauzito niliyokuwa nao kwa madai kuwa ingeniharibia soko la biashara yangu ya uchangudoa.

    Hilo halikuwa tatizo hata kidogo, mipango ikaandaliwa kisha nikaenda kwenye hospitali moja ya kibinafsi maarufu sana hapa mjini, sitaweza kuitaja kwasababu za kibiashara.

    Nilifanikiwa kuutoa ujauzito wa miezi mitatu, hilo lilimfurahisha Savela mno, aliniambia huo ndiyo ulikuwa mwanzo wangu wa kutengeneza pesa na kuwa mwenye mafanikio kama aliyokuwa nayo yeye.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Kichwa changu kilikuwa kikifikiria utajiri ambao ningeweza kuupata kutokana na biashara hiyo ya uchangudoa.

    Hakukuwa kuna kitu nilichokuwa nikikitamani kama kuwa na maisha mazuri. Niliutamani sana utajiri, nilipokuwa nikimsikia mtu akipiga stori za pesa nilihisi kusisimka mwili.

    Kipindi hicho biashara niliyoambiwa kuwa ingeweza kunipa utajiri wa haraka ilikuwa ni ya uchangudoa, nilitakiwa kujiuza kwa wanaume ambao wangenilipa na mwisho wa siku maisha yangu yangeweza kubadilika.

    Mwanzoni biashara hiyo ya uchangudoa haikuniingia akilini, niliogopa kuifanya lakini Savela aliendelea kunishawishi.

    Siku moja majira ya usiku alinipeleka Sinza kwenye klabu moja maarufu sana, Ambiance. Ilikuwa ni sehemu maarufu kwa wasichana kufanya biashara hiyo ya uchangudoa.

    Macho yangu hayakutulia sehemu moja, nilikuwa nikiyashangaa mazingira niliyokutana nayo mahali hapo, wakati huo tulikuwa tumekaa nje ya baa hiyo upande ambao niliweza kuiona barabara ya Shekilango.

    "Unashangaa nini?" aliniuliza Savela, wakati huo alikuwa ameagiza pombe kwa muhudumu aliyekuja kutusikiliza.

    "Hakuna kitu," nilimjibu huku nikijiweka sawa.

    Muhudumu huyo akanigeukia na kuniuliza kuwa nilihitaji nini kwa muda huo, sikuwa ni mtumiaji wa kilevi chochote, nilimuagiza soda.

    Jibu hilo likamshangaza sana Savela, akazidi kuniona nilikuwa mshamba sana.

    "Hutumii pombe?" aliniuliza, muda huo yule muhudumu alikuwa tayari ameenda kuleta vinywaji.

    "Ndiyo situmii," nilimjibu.

    "Kwanini?"

    "Sijazoea."

    "Mmh!"

    Baada ya dakika kama tatu hivi yule muhudumu aliweza kurudi na vinywaji, alipomaliza kutuhudumia nikashangaa akimsogelea Savela, akamnong'oneza kitu, nikamuona Savela akitabasamu. Sikufahamu kwa muda huo ni nini kilichokuwa kikiendelea.

    Nilianza kuinywa soda yangu taratibu huku nikiendelea kuyashangaa mazingira ya sehemu hiyo. Kwa mbali niliwaona wasichana watatu waliyokuwa wamevalia mavazi yaliyowaacha sehemu kubwa za mwili wao kuwa wazi, walikuwa wakiikimbilia gari iliyokuja na kupaki eneo hilo la baa, walikuwa wakigombaniana, kila mmoja alihitaji kuwa karibu na kioo ambacho kilifungiliwa na dereva wa gari hilo.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya sekunde chache wasichana wawili wakaondoka na kubaki msichana mmoja, mazingira niliyoyaona yalitafsiri wazi kulikuwa kuna biashara ya uchangudoa iliyokuwa inafanyika, kuna muda yule msichana nilimuona akiwa anajigeuza sehemu za nyuma ya maumbile yake. Haikuchukua muda, msichana yule akaingia ndani ya gari kisha likawashwa na kuondoka.

    "Mwajuma," aliniita Savela baada ya yule muhudumu kuondoka.

    "Abee," nilimuitikia.

    "Umemuona huyu muhudumu?"

    "Ndiyo nimemuona kwani amefanya nini?"

    "Kuna mtu amemuagiza aje kuniambia kuwa ananiita."

    "Mtu gani?"

    "Ni mwanaume."

    "Mmh!"

    "Subiri nikaongee naye," aliniambia kisha akainuka na kwenda kwenye meza iliyokuwa jirani kidogo na sisi.

    Katika meza hiyo alikuwa amekaa mwanaume mmoja ambaye alionekana kuwa na mwili wa miraba minne, pembeni yake alikuwa amekaa msichana mmoja ambaye alionekana kuwa katika mavazi yaliyomuweka nusu uchi.

    Savela alipofika katika meza hiyo nikamuona akikumbatiana na yule mwanaume, walionekana kama ni watu wanaofahamiana muda mrefu hivyo sikutaka kujaji sana, niliendelea kunywa soda yangu huku nikiwa sina wasiwasi wowote.

    Bado niliendelea kuwashuhudia wasichana wakifanya biashara ya uchangudoa, biashara ilikuwa ikifanyika waziwazi wala hakukuwa na mtu aliyeonekana kuogopa au kushangaa, ilionekana kuwa ni biashara ya kawaida ambayo watu walizoea kuiona.

    Nilibaki peke yangu katika meza hiyo mpaka pale ambapo Savela alirudi, aliniambia kuwa nilitakiwa kwenda kukaa naye meza moja na yule mwanaume aliyekuwa akizungumza naye, nilimkubalia kisha nikaenda kukaa naye katika meza ya mwanaume huyo, tulihamisha na vinywaji vyetu.

    Yule msichana niliyemuona mwanzo akiwa amekaa na mwanaume huyo akainuka na kutupisha halafu nikamuona akimpa ishara fulani Savela ambayo nilishindwa kuielewa maana yake.

    "Mwajuma huyu anaitwa Ibra, the big boss. Ibra huyu anaitwa Mwajuma ni msichana wangu na yeye ndiyo anainza hii kazi," alinitambulisha kwa mwanaume huyo ambaye nilishikana naye mikono.

    "Okay..anaonekana kuwa mrembo sana aisee nahisi hata yale mambo yetu yatakuwa mazuri," alisema Ibra huku akitabasamu.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Ndiyo hapo ni wewe tu sema kingine," alisema Savela kisha Ibra akanitazama, Savela akaniambia nisimame, nikafanya kama alivyoniambia.

    Unajua huwa sipendi kujisifia sana lakini kwenye ukweli acha niwaambie, nilikuwa nina chura, nadhani ninaposema nilikuwa nina chura mmeshanielewa nini ninachokimaanisha, nilikuwa nina kila sifa zinazoweza kumteka mwanaume rijali.

    Ibra aliponiona alizidi kupagawa, alikosa neno la kuzungumza kwa wakati huo, muda wote huo macho yake yalikuwa yakiangalia chura yangu.

    "Mimi nilikwambia chombo si cha nchi hii," alisema Savela huku akitabasamu, aliimimina pombe kwenye glas kisha akanywa.

    "Duh! Hiki chombo si mchezo ni balaa," alisema Ibra, wakati huo tayari nilirudi kukaa.







    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog