Search This Blog

Monday, October 24, 2022

USIKU WA KIGODORO - 2

 





    Chombezo : Usiku Wa Kigodoro

    Sehemu Ya Pili (2)





    ILIPOISHIA: Wakati mazungumzo yakiendelea, mume wa Lina alifunga breki nje ya nyumba ya Eg na kupiga honi ana shida na mke wake huyo…

    “Pii pii piii!”

    JIRUSHE MWENYEWE SASA…

    Eg ndiye aliyechungulia nje baada uya kusikia honi ya gari, akashtuka sana na kusema…

    “Ha! Lina, shemeji Semi…”

    “Kweli?”

    “Mungu tena, amesimamisha gari hapo nje.”

    “Mungu wangu, sasa?”

    “Hata sijui! Kwani amefuata nini huku? Au ametonywa ishu nzima?”

    “Hapana, atakuwa ana shida na mimi. Lakini sasa nimeshavaa itakuaje? Si ataniona nimekuwa rasmi sana kuliko huyo niliyemsingizia?”

    “Na kweli.”

    Semi alipiga tena honi, Eg akatoka. Lina alivua gauni la kitchen party na kuvaa alilokwenda nalo kisha naye akatoka. Ndugu na marafiki wa Eg nao wakafuata hadi kwenye gari…

    “Shem mambo?” alisalimia Eg…

    “Poa, mzima wewe?”

    “Mimi mzima. Karibu sana.”

    “Asante sana.”

    “Huyu ndiye shemeji kwa Lina?” ndugu mmoja wa Eg aliuliza akiamini Semi ndiye bwana harusi mtarajiwa…

    “Eee, ndiyo huyu.”

    “Oo! Karibu sana shemeji…sisi leo mambo yatakwenda vizuri kabisa ukumbini…bibiye atapendeza kupita kawaida,” aliropoka yule ndugu bila kujua kwamba anakaribia kulipua bomu.

    Kilichosaidia ni kwamba, maneno yake yalifunga ufahamu wa Semi kwani kule kusema sisi leo mambo yatakwenda vizuri, Semi alijua ni sherehe ambayo mkewe alishamwambia ipo.

    Kule kusema bibiye atapendeza kupita kawaida hakukumfanya Semi ahisi kitu kwani ni kweli mke wake alitoka nyumbani na gauni zuri la kitenge ambalo alisema atalivaa kwenye kitchen party ya rafiki yake, ubaya uko wapi sasa!CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Sawa jamani, nawatakia sherehe njema, nimekuja kumpa maagizo huyu, mimi nakwenda Morogoro nikichelewa nitarudi kesho.”

    “Sawa mume wangu,” alisema Lina. Mwanamke mmoja akadakia…

    “We, bado hajawa mume wako, atakuwa mumeo ukishafunga naye ndoa.”

    Lina na Eg walishtuka sana kwa kauli hiyo, walijua sasa mambo hadharani lakini katika hali isiyotarajiwa, Semi akajibu…

    “Tufunge ndoa mara ngapi? Shemeji Eg hujawaambia nini?” akawasha gari na kuondoka huku akicheka.

    Mambo yalikuwa mambo, mkorogano ulitawala kila aliyesema, aliyesikia alitafsiri vingine kabisa.

    Hata yule mwanamke aliyejibiwa kwamba ‘tufunge ndoa mara ngapi?’

    alijua ameambiwa kwa kutaniwa kwani alijua ile kitchen party ya Lina, muoaji mwenyewe ndiye yule. Na Semi naye alijua yule mwanamke ameuliza kwa sababu ya ugeni, hajui kama Lina yupo kwenye ndoa ndiyo maana akamwambia Eg, ‘shemeji Eg hujawaambia nini?’

    ***

    Lina aliendelea kujipamba, magari mawili ya kukodi yakafika kwa ajili ya kupelekwa ukumbini.

    Shamrashamra ukumbini zilinoga kama si kuvutia, kwani kila kitu kilikwenda sawasawa. Lina pamoja na kwamba alitegemea michango lakini yeye mwenyewe kwa kupitia kwenye mfuko wa James alichangia fedha kwa kiasi kikubwa na kusababisha bajeti kwenda ilivyopangwa.

    Shughuli ilikuwa nzuri, waalikwa walikula la kunywa na wakasaza huku kila mmoja akimpongeza Lina.

    Lakini muda mwingi wa sherehe hiyo, Lina alipenda kuinamisha kichwa ili kukwepa macho ya watu akiamini pengine kuna ambaye atakuwa anamjua. Mbali na macho ya watu, awali kabisa Eg alishawatangazia waalikwa kuachana na kupiga picha kwa kutumia kamera za kwenye simu zao. Na wala hakukuwa na mpiga picha aliyekodishwa.

    Baada ya shughuli hiyo, Lina alikwenda kulala kwa Eg baada ya kumpigia simu mume wake na akamwambia hatarudi toka Morogoro.

    Usiku Lina alianza kuchati na James…

    “Baby sherehe ilikuwa nzuri sana, nimemaliza kazi bado kwako ndoa wikiendi ijayo.”

    “Niko fiti baby, mipango yote tayari. Tutakwenda fungate wapi baby?” aliuliza James swali lililomuumiza sana Lina kwani alijua kwenda fungate ni kubumbulua mambo kwa mume wake, atamuaga anakwenda wapi!”

    “Popote pale my dear,” alijibu Lina.

    Kama wangekuwa wanaongea kwa sauti angeshangaa kusikia sauti ya Lina inazungumza kwa unyonge wa hali ya juu.

    “Basi niachie mimi, nitachukua hoteli nzuri sana tena kubwa ya hapa mjini. Au unataka twende nje ya mji kama Zenji?”

    “Noo! Hata hapa Dar panatosha sana my love.”

    Walichati mpaka saa tisa kasoro lakini muda mwingi akili ya Lina ilikuwa haipo sawa. Kuna wakati alitamani hata kufunguka lakini alishindwa kwa sababu walishafika mbali na angesababisha mawazo ya James kuamini kwamba wanawake ni wabaya sana.

    Siku ya ndoa ndiyo ikafika sasa, Lina alikuwa anajiandaa kivyake na James kivyake walikubaliana wakutane kanisani na kuungana kuingia ndani kwa ibada ya ndoa.

    “Uko wapi Lina?”

    “Kwa dada, ndiyo tunataka kutoka kwenda saluni my dear.”

    “Lina usinitibue, kwa dada saa hizi wakati unajua kanisani tunatakiwa saa nane kamili mchana, sasa uende saluni saa sita hii utamaliza muda gani? Kanisani utakuja saa ngapi na ndoa itafungwa saa ngapi au hutaki tufunge ndoa Lina?”

    “Nitamaliza mapema tu.”

    Mara Lina akakata simu…

    “Khaa! Yaani Lina kanikatia simu mimi? Ana maana gani?” alijiuliza James. Alipopiga tena iliita bila kupokelewa…

    “Afadhali isingepatikana ningesema chaji imeisha, sasa hapokei ana maana gani?” James aliendelea kuwaza…



    ***************

    ********************

    ***************************

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Lina alichukua Bajaj ambayo ilimfikisha nyumbani kwake akiwa amechoka sana. Ile anaweka simu mezani tu, mumewe Semi akaichukua.

    “Kuna mtu nataka kumpigia nijue alipo halafu simu yangu haina hela,” alisema akiminya vitufe.

    Moyo wa Lina ulilipuka kwani alikumbuka kuwa ndani ya simu hiyo kulikuwa na meseji za James ambazo hakuzifuta na zilisomeka vibaya kama zingeonwa.

    Alitaka kupeleka mkono kumpokonya mume wake lakini alijua akifanya hivyo pia angempa picha mbaya kama nia yake haikuwa kupekua meseji.

    Semi alipiga simu na kuongea na mtu ambapo alisikika akisema…

    “Wee kama nilivyokwambia, hakikisha unatumia kila njia ili tuujue ukweli wa mambo. Unajua hakuna kitu kibaya kama mke awe wako halafu kumbe kuna mwingine anamwona ni mke wake, hiyo ndiyo maana yangu kuu.

    “Sawa kaka, sawasawa, fanya uchunguzi wako halafu utanipa majibu.”

    Lina aliishiwa nguvu, miguu ilimtetemeka, akataka kukaa lakini akajisikia kuumbuka. Alitamani kuuliza kinachoendelea, pia akashindwa.

    Semi hakuwa na nongwa, alimrudishia simu yake huku akimwangalia usoni ambapo Lina aliamua kuukimbiza uso wake pembeni.

    “Pole na starehe,” alisalimia Semi, Lina akashindwa acheke au ajibuje…

    “Nzuri.”

    “Mambo yaliisha salama?”

    “Ndiyo.”

    “Una uhakika?”

    “Ndiyo, kwani umesikia nini?”

    “Nimesikia umenisaliti.”

    Lina moyo ukamfanya paa! Mpaka akajishika kifua kwa hofu…

    “Mungu wangu,” alisema ndani kwa ndani…

    “Pole lakini, maana kulala nje ya nyumbani nako...” Semi alisema huku akicheka, kidogo Lina akajua mumewe anafanya utani kwani kwa anavyomfahamu asingeweza kucheka kama angekuwa analo jambo moyoni.

    Lakini bado yale maneno aliyoongea mumewe na mtu kupitia simu yake kwamba achunguze mtu anaweza kusema ni mke wake kumbe kuna mwanaume mwingine naye anasema ni mke wake yalimtesa akilini.

    Alienda chumbani huku akifungua simu kuangalia namba iliyopigwa, akabaini ni ya mtandao ambao anao na yeye hivyo aliisachi…

    “Issac Majurila ni nani, mbona sijawahi kumsikia,” aliwaza moyoni. Aliamua kumsaka ili kujua mumewe alimwambia amchunguze nani ambaye anaweza kuwa mke wa mtu kumbe kuna mwingine anasema ni mke wake!

    ***

    “He! Kumbe leo ni Jumapili, nilisahau kabisa, nikajua utachelewa kazini,” alisema Semi akiwa ameingia chumbani ambapo hata Lina mwenyewe alishtuka, akakumbuka kwamba, alifunga ndoa jana yake Jumamosi, amelala na James usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili.

    “Mh! Mi mwenyewe kusema za ukweli nilijua leo ni siku ya kazi,” alisema Lina akiendelea kushangaa. Mara simu yake iliingia meseji, akaisoma chapchap...

    “Baby leo ni Jumapili, sasa umeondoka bila kusema utakuja muda gani?”

    Lina aliijibu palepale…

    “Mchana nitakuwa hapo baby, hata mimi nilisahau kabisa kwamba leo ni Jumapili, sijui ni kwa nini wote tulisahau.”

    “Oke, ilitokea tu, uje basi kwa muda huo.”

    Bahati nzuri pale nyumbani napo, Semi aliaga anakwenda kwenye shughuli zake hivyo Lina akabaki yeye na msichana wa kazi tu. Ikawa ni nafasi yake ya kurudi hotelini aliko James.

    Alikwenda sebuleni, akazima tivii maana alimkuta mumewe Semi ameiwasha akitazama mambo mbalimbali. Lina aliizima kwa sababu alihisi inamchanganya, kwa wakati huo alihitaji kutafakari zaidi kwa kitendo alichokifanya.

    Kwanza alijua amemfanyia kitendo kibaya sana James, kufunga naye ndoa ambayo ni batili. Alihisi huruma anatakapogundua wakati mwenzake mapenzi yote aliyaelekeza kwake kama mke.

    Pili, alimini kuwa James anajua amejikomboa kwa kupata mke na yeye anapitia sera za kike maana yake ametoa mkosi, sasa kumbe badala ya kuondoa mkosi amejiongezea…

    “Hivi huu mtego nitawezaje kujinasua nao? Ni kwa nini nimeuingia? Ni tamaa ya hela au mapenzi ya dhati?” aliwaza Lina. Lakini kwa harakaharaka alipata jibu kwamba, zile laki mojamoja kila kukicha zilimchanganya akili licha ya kwamba ni kweli James ni kijana mtanashati sana.

    Lina aliamua kumpigia simu shoga yake, Eg na kumwambia anavyojisikia…

    “Halo Lina…”

    “Eg…”

    “Bee.”

    “Naweza kujiua mwenzio.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “He! Kwa nini Lina, kuna nini kimetokea? Shemeji kajua?”

    “Hapana! Ila…”

    “Ila nini tena Lina?”

    “Unajua nimefanya jambo la kipuuzi sana? James anajua mimi ni mke wake wa ndoa. Halafu sasa, mbaya zaidi ndoa yenyewe ya Kikristo, ni kama loki. Siku akijua nina mume tena wa ndoa nini kitatokea?

    “Mtu mwenyewe ana hela, nahisi atanifunga na hakuna wa kunitetea. Najuta Eg, najuta kabisa. Sijui ni kwa nini na wewe rafiki yangu kipenzi hukinikataza?”

    “Lina, nisingekukataza mtazamo wako na wangu ni mmoja tu. Kama ni kujuta sasa tujute wote, kwani kwa maneno yako ya saa hizi hata mimi nimegundua hilo…”

    “Eg subiri nipokee simu ya James…halooo.”

    “Mke wangu Lina…”

    “Abee baba.”

    “Mwambie dada ukija mchana hakuna kurudi tena huko. Utakuwa unatokea hapa kwenda kazini na kurudi mpaka siku tano tunahamia nyumbani, hivyo ukija beba nguo zako kwenye sanduku chukua teksi.”

    “Mh! Sawa baby.”

    “Mbona umeguna kwanza?”

    “Basi tu, nafikiria jinsi ya kumwambia huyo dada.”

    “Unafikiria jinsi ya kumwambia dada? Kwa nini ufikirie? Mimi si mume wako kwa sasa? Tena wa ndoa.”

    “Ni kweli my love.”

    “Sasa?”

    “Oke, nimekuelewa.”

    James alikata simu na kumwacha Lina katika mawazo kibao…

    “Da! Nimeingia mkenge kwa kweli. Hapa sina cha kujitetea, siwezi kutengua ndoa tena. Imefungwa imefungwa tu. Kinachotakiwa ni kuamua moja, kusuka au kunyoa…

    “Semi mume wangu akijua sijui nini kitatokea. Da! Balaa! Hivi kama ni tamaa, tamaa gani ya hivi mimi Lina mimi? Haya mambo si yanaweza kufika kwa wazazi? Yakifika nitajiteteaje?”

    Lina alikosa ujasiri wa kufikiria kiasi kwamba alianza kutoa machozi mwenyewe…

    “Mungu wangu, nisaidie mimi. Nimekwaa tatizo kubwa.”

    Kwa upande wake James baada ya kumkatia simu Lina naye alizama kwenye maswali kibao huku akikosa majibu ya moja kwa moja…

    “Ni kwa nini Lina anamuogopa dada yake kiasi hicho? Yeye si mke wangu wa ndoa? Sasa nini kitamfanya huyo dada azuie Lina kuondoka?

    “Halafu, kwani mbona siku ya harusi ukumbini sikumwona huyo dada yake akitambulishwa? Maana kama ndiye ameishi naye alitakiwa kutambulishwa kama mzazi wa Lina kwa hapa Dar es Salaam.”

    Kifupi wote walikuwa katika wakazi mgumu sana, kila mmoja alikuwa na maswali yake yaliyokosa majibu ya moja kwa moja kwa pale.

    ***

    Mchana ulifika, Lina mapigo ya moyo yaliongezeka kwa sana. Kila dakika ilipokatika aliitupia macho simu yake akiamini James atapiga…

    “Huyu atapiga sasa hivi,” alisema moyoni. Aliwaza amwambie nini mume wake, Semi ili aondoke kurudi hotelini aliko James lakini pia alijiuliza akienda bila nguo ataelewekaje kwa mumewe huyo?

    Kama aliota, simu ya James iliita. Aliitupia macho kwa dakika moja nzima mpaka akakata. Ikapigwa tena ndipo akapokea…

    “Baby…

    “Mbona hufiki? Nikufuate?”

    “Noo baby, nilikuwa naweka nguo zangu kwenye begi nakuja.”

    “Poa.”

    James akakata simu kwa dalili zote kwamba amekasirika na mwenendo wa Lina kwa siku ile.

    Lina alimpigia simu mume wake ili amdanganye kitu…

    “Baby…”

    “Ee baby…”

    “Kuna balaa juu ya balaa,” alisema Lina…

    “Lipi tena baby?”

    “Yaani Eg ana dada yake alikuwepo kwenye sherehe ya jana, amefika kwake ameumwa ghafla kakimbizwa Muhimbili…”

    “Duu! Balaa. Sasa?”

    “Sasa nakuomba ruhusa niende Muhimbili mchana huu maana Eg naye anakwenda.”

    “Sawa! Lakini huyo atakuwa amekula kitu kibaya, unajua sherehe sherehe hizi mambo hayo hutokea. Ngoja nikupe namba ya Dokta Matingisha ukifika umpigie ili asaidie.”

    “Itakuwa vizuri baby.”

    Lina aliachia tabasamu, akapata akili. Alichukua begi, akatoa kwenye kabati lake nguo za zamani kibao na kuziweka kwenye begi.

    Kama vile hiyo haitoshi, akafunua godoro ambapo pia mlikuwa na nguo nyingine, nazo akazitia kwenye begi mpaka likavimba. Akachukua Bajaj hadi hotelini alipo James.

    ***

    Eg alikuwa hana hili wala lile, simu ya shemeji yake Semi ikaingia kwake…

    “Mh! Huyu shemeji vipi, si kawaida yake kunipigia simu,” alisema moyoni Eg huku akiwaza apokee au la! Akaamua kuipokea…

    “Haloo shem…”

    “Shemeji poleni sana na mgonjwa jamani! Aisee,” alisema mume wa Lina…

    “Mgonjwa?” alihoji Eg…

    “Si Lina ameniambia kwamba…”

    Eg alikata simu haraka sana. Akampigia Lina…

    “Shoga…”

    “Ee shoga vipi?” alisema Lina…

    “Umemwambia shemeji nina mgonjwa?”

    “Ha! Ndiyo Lina, kakupigia? Please mwambie unaye, nimemwambia ni dada yako amelazwa Muhimbili anaumwa sana tumbo la kuendesha na yuko hoi…”

    “Oke, tena huyo anapiga ngoja nipokee…

    “Haloo shem…”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Shem, naona mtandao unasumbua…Lina kaniambie una mgonjwa.”

    “Eee, unajua nilidhani unasema wewe ndiyo una mgonjwa ndiyo maana nikauliza mgonjwa gani?! Dada yangu bwana, anasumbuliwa na tumbo tukamkimbiza Muhimbili.”

    “Da! Poleni sana, lakini Mungu atamsaidia.”

    “Asante sana shemeji.”

    “Oke shemeji. Sisi tupo, yeye kaniambia anakuja Muhimbili.”

    “Ee, na mimi naelekea huko shemeji yangu.”

    “Sawa, baadaye.”

    ***

    Lina alifika hotelini, akasukuma mlango na kuzama kwenye chumba alichomo mume wake wa pili James…

    “Hodi.”



    James alifungua mlango, ukawa wazi mpaka mwisho. Lakini alionekana kukunja sura na kupoteza uchangamfu kuliko siku nyingine.

    “Karibu.”

    Lina aligundua James hakuwa sawa…

    “Baby kama haupo sawa, kuna nini?”

    “Lina, mimi ni nani kwako?”

    “Mume wangu.”

    “Unatakiwa kumsikiliza dada ‘ako au mimi?”

    “Wewe.”

    “Basi naomba unisikilize kuanzia sasa.”

    “Kwani sikusikilizi baby? Mbona mimi nakusikiliza sana jamani.”

    “Lakini si kwa kiwango kinachotakiwa Lina, ongeza usikivu wako kwangu. Mbona mapema sana kuanza kuonesha si msikivu!”

    “Nisamehe mume wangu.”

    “Oke, yamepita nakupenda sana.”

    “Asante baby, nakupenda pia.”

    Walikumbatiana wakaganda kwa muda huku kila mmoja akimtazama mwenzake machoni, mwishowe wakaachia tabasamu laini, wakapanda kitandani ambako Lina ndiye aliyeanzisha kupeana muwashawasha kwa James naye akapokea, wakakukuruka mpaka wakaingia uwanjani kuanza mchezo.

    ***

    Usiku uliingia, Lina alikuwa akipiga mahesabu ni uongo gani atamwambia mume wake akaeleweka ili asirudi nyumbani siku hiyo. Kwa siku hiyo kumpigia asingeweza maana muda wote James alikuwa yuko naye beneti. Akaamua kutuma meseji.

    “Baby, hali ya dada’ke Eg bado si nzuri. Naomba nilale hospitali maana naye Eg ana mgonjwa mwingine pale kwake.”

    Baada ya kutuma meseji hiyo, kila sekunde Lina alikuwa akiiangalia simu yake ili kuona kama meseji ya majibu itaingia.

    Zilikatika dakika kumi meseji yake haijajibiwa, mwishowe akaanza kuingiwa na wasiwasi kwamba huenda mume wake hajapenda ruhusa hiyo na kama ndivyo, ataagaje kwa James ili arudi nyumbani. Mara, meseji ya mume wake Semi iliingia.

    “Sijakubaliana na wewe, Eg aangalie utaratibu mwingine wa mtu wa kulala na mgonjwa wake na si wewe.”

    Ni kujikaza tu, lakini Lina alibadilika rangi muda uleule ila alijichangamsha ili kutompa nafasi James kumsoma. Moyoni alijua kuna ugumu mkubwa kwa James kumkubalia aondoke. Kwanza atasema anakwenda wapi?

    “Mh! Nimeyavulia nguo mwenyewe, lazima niyaoge sasa,” alijisemea moyoni huku akianza kutetemeka mpaka James akajua.

    “Vipi baby mbona kama unatetemeka?”

    “Wala, niko fiti tu.”

    Kwa mbali Lina alipata akili kwamba, amtumie meseji Eg na kumwambia apige simu kwake aseme kuna shangazi mgonjwa amepelekwa Muhimbili muda huo, awahi Muhimbili.

    Baada ya kujiridhisha kwamba itakuwa sawasawa, Lina alituma meseji hiyo kwa Eg ambaye alijibu kwa ufupi poa! Lakini akatuma nyingine akimuuliza apige simu au atume meseji?

    “Piga kabisa,” alijibu Lina.

    Alijifanya anakwenda chooni ili simu ya Eg ikiingia ipokelewe na James na ikibidi ujumbe huo upokelewe na yeyeyeye James.

    Ile anafika chooni tu, simu yake ikaita. James akatupa jicho kwenye skrini, akasoma jina akamwita Lina.

    “Baby…”

    “Abee…”

    “Kaka Semi.”

    Kaka Semi ni mume wa Lina. Wakati anakwenda hotelini hapo aliamua kubadii jina la mume wake, badala ya kuandika My Huzband kama ilivyokuwa mwanzo, akaandika kaka Semi akiamini kwamba anaweza kupiga wakati yeye yupo na James itakuwa soo kuonekana My Huzband!

    Lina alitoka mbio huku mapigo ya moyo yakimwenda kasi kwa sababu hakutegemea kama mumewe angepiga simu muda ule.

    Lina aliipokea simu kutoka kwenye mikono ya James akiwa haamini maana alijua kuwa hata kama James angeamua kupokea na kusema ‘mwenye simu yuko mbali’ au ‘subiri kidogo’ ingekuwa soo kwake.

    Pia alijua kuwa, James angeweza kuipokea simu hiyo kwa lengo la kusalimiana na shemeji yake huyo aitwaye Semi kwa mujibu wa jina la kwenye skrini ya simu.

    Lina alijifanya anaipeleka simu hiyo sikioni huku akiikata halafu akajifanya anaongea.

    “Shikamoo kaka Semi…mimi sijambo, za huko? Hawajambo wote? Sisi tunaendelea vizuri, utakuja lini? Haya karibu sana, shemeji yako utamuona tu ukija, yupo! Haya kwa heri kaka.”

    Alipomaliza kusema kimagirini, alituma meseji kwa mumewe.

    “Kuna daktari kapita wodini, nitakupigia. Lakini pia nitakuja nilikuelewa.”

    Alichokitaka Semi ni hicho kujua kwamba, kukataa kwake Lina asilale hospitali alielewa. Mara, ikaingia simu ya Eg, Lina akiwa amesimama dirishani, James akatupia tena macho na kumwambia...

    “Eg anapiga, ngoja nipokee nimsalimie…shemeji mambo? Ee…yupo…nani? Amelazwa..? Hospitali gani? Hebu ongea na Lina huyu hapa shemeji…”

    “Haloo…amelazwa? Anaumwa nini? Oke, nakuja basi.”

    Lina alikata simu na kumgeukia James…

    “Vipi?” aliuliza James…CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mh! Majanga… itabidi niende hospitali.”

    “Ameniambia aisee. Da! Sasa si itabidi nikupeleke?”

    “Utanipeleka? Si ulisema unapenda wiki nzima ushinde ndani tu!”

    “Ni kweli, lakini sasa wewe utaendaje?”

    “Nitachukua Bajaj…”

    “Kwanza leo nataka kukwambia jambo, mambo ya kupandapanda Bajaj yaishe, sitaki kuona. Nitakununulia gari tukimaliza fungate, kwa hiyo itabidi ujifunze kuendesha…ila leo nenda na teksi,” alisema James huku akimwagiza Lina kutoa pesa kwenye brifkesi…

    “Nichukue shilingi ngapi?”

    “Unayoona inatosha.”

    Lina alitumbukiza mkono akaibuka na shilingi elfu hamsini…

    “Nimechukua hamsini.”

    “Sawa, kawape pole wote.”

    Lina alichukua Bajaj hadi nyumbani kwake ambapo alimkuta mumewe, Semi. Swali la kwanza alilokumbana nalo kwa mumewe ni kuhusu pete ya ndoa na ya uchumba…

    “Baby, hivi hizo pete ulizipeleka tena kwa sonara nini, maana naziona zinang’aa sana siku mbili hizi.”

    “Nilipeleka zikaoshwa. Niliona zimeanza kuingia giza.”

    “Oke, zimekuwa nzuri sana,” alisema Semi bila kujua kwamba zile ni pete mpya ambazo alizinunua James kwa ajili ya ndoa hiyo.

    ***

    Lina amefika kwake, kazi ikawa kumsikilizia James akipiga kuulizia kuhusu mgonjwa. Aliumia sana moyoni kiasi kwamba alitamani kumwandikia meseji amwambie ukweli kwamba yeye ni mke wa mtu, tena kwa ndoa lakini kila alipofikiria kuhusu hilo akiamini hata James alifunga naye ndoa alikosa la kufanya.

    Eg alimpigia simu Lina na kumuuliza kama dili lao lilitiki au la! Alipoambiwa limetiki, akacheka sana na kukata simu huku moyoni akisema…

    “Lakini sisi tuna hatari sana. Ni kweli Lina ataweza kudumu na James kwa muda mrefu bila kujulikana? Sidhani aisee!”

    ***

    Saa kumi na mbili jioni, Lina akiwa chumbani simu yake iliita. Na muda huo aliamua kwa makusudi kuwa chumbani akijua lazima James atapiga…

    “Haloo,” alipokea kwa sauti ya chini, mume wake alikuwa amekaa sebuleni…

    “Vipi mgonjwa?”

    “Mgonjwa hali mbaya James, hivi hapa daktari ndo ameingia sasa hivi.”

    “Mh! Sasa itakuaje? Ahamishwe hospitali.”

    “Sijajua ndugu watasemaje maana waliondoka na hawajarudi. Hivi nilitaka kukwambia naomba nilale nitoke asubuhi kuja huko.”ITAENDELE KESHO.

    “Sawa, lala tu Lina, wale wakija asubuhi wewe unatoka, si ndiyo?”

    “Ndiyo.”

    “Basi hamna shida.”

    Lina alijisikia furaha ya aina yake, kwani alijua amemaliza kazi kubwa sana ya siku hiyo…

    “Kibarua cha leo kimeisha, bado cha kesho, keshokutwa, mtondogoo na siku za mbeleni, sijui itakuwaje!”

    ***

    Asubuhi ya saa kumi na mbili, Lina alitoka na simu yake hadi uani, akampigia simu James haraka ili arudi tena kitandani kulala…

    “Umeamkaje baby?”

    “Nimeamka poa. Vipi mgonjwa?”

    “Mgonjwa hivyohivyo tu, hakulala usiku.”

    “Da! Poleni sana. Wameshakuja hao?”

    “Wako njiani, watafika kwenye saa mojamoja hivi, maana watashinda hapa.”

    “Sawa. Sasa ukitoka si unakuja huku?”

    “Yeah!”

    “Oke poa.”

    “Oke, baadaye basi.”

    ***

    Asubuhi ya siku hiyo, Lina alipotoka kuoga na kuvaa ili aende kwa James alipata wakati mgumu kwani isingekuwa kawaida aende akiwa amevaa nguo nyingine wakati James anajua alikwenda hospitali. Lakini pia isingekuwa rahisi avae nguo zilezile mbele ya mume wake. Kwa siku hiyo, mume alijua anakwenda kazini.

    Ilibidi avae nguo nyingine, akazichukua za jana yake na kuzitia kwenye mkoba na kuondoka zake.

    “Mume wangu baadaye.”

    “Sawa, kazi njema.”

    “Poa.”

    Nje, Lina alichukua Bajaj na kwenda hotelini kwa James. Lakini alimshangaza sana dereva wa Bajaj kwani walipokaribia nje ya hoteli, alimwambia suka huyo asimamishe Bajaj na afungue turubali ili abadili nguo, avae ileile ya jana yake kisha zile alizovaa siku hiyo akaziweka kwenye mkoba…

    “Kwani vipi anti, sijakuelewa?”

    “We acha tu. Nina mambo makubwa sana, usinione hivi.”

    “Mambo gani, siwezi kukusaidia mimi?”

    “Huwezi.”

    Mara, simu yake ikaita, mumewe alipiga…

    “Nakuja hapo ofisini kwako, kuna mzigo nataka kuuacha,” akakata simu.



    LINA alipata mshtuko mpya kutoka kwa mume wake, kwamba anakwenda kuacha mzigo pale, ni mzigo gani huo?

    “Mh!” aliguna huku akimwangalia dereva Bajaj.

    Alishuka lakini alisimama akishindwa kutembea kuelekea ndani ya hoteli kwani alishajua kuna mambo yatakuwa yameharibika.

    “Pole anti, ungenilipa basi mi niondoke zangu.”

    “Suka, hujui kama siko sawa?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Sasa kama hauko sawa anti mimi nifanyaje?”

    “Oke, chukua hela yako uondoke,” alisema Lina huku akimkazia macho dereva huyo.

    Naye akaondoka zake huku akimsonya Lina kwa kutaka kumuwekea kiwingu.

    Lina aliliona geti la hoteli ni kubwa sana kiasi kwamba alitamani hoteli yote ilipuke moto na kuteketea akiwemo James ndani yake ili aondokane na kitendo cha kupata shida ile ambaye ilikuwa ikimnyemelea…

    “Hii tabu nimeitafuta mwenyewe lakini, ninachokipata hapa ni halali yangu, lakini ee Mungu nisaidie,” alisema moyoni Lina wakati akipita kwenye geti dogo la hoteli kuingia ndani.

    Mara mumewe, Semi alipiga simu kwa tafsiri kwamba alishafika kazini kama alivyokuwa amemwambia awali.

    “Siwezi kupokea,” alisema moyoni.

    “Lakini nisipopokea na akiambiwa sijafika kazini itakuwaje? Si atashangaa nimekwenda wapi badala ya kazini, mbaya zaidi sijatoa taarifa kazini kwamba sitaenda au nitachelewa,” Lina alihisi mambo yanazidi kuwa magumu siku hadi siku.

    Lakini aliamua kupokea simu ya mume wake…

    “Haloo…”

    “Niko nje hapa.”

    “Sijafika kazini, nimepitia Mnazi Mmoja, nakutana na Eg mara moja halafu nakuja huko.”

    “Ah! Basi baadaye, mimi napita lakini naacha huo mzigo kwa mlinzi wenu atakuja kuchukua mtu mmoja anaitwa Peter Kindaundau.”

    “Sawa.”

    Kidogo Lina alipumua kwani alilimaliza hilo. Alisifu kitendo cha mumewe kutoingia ndani ya ofisi na kumuulizia kwani ingekuwa ishu sana kuliko vile.

    Alipanda hadi juu kwa James ambapo alipata mapokezi mazuri kwa kukumbatiwa na kupigwa mabusu mfululizo…

    “Mmmm! Mmmwaaaa…”

    “Mmmmmwaaaa, asante sana darling.”

    “Vipi, mgonjwa anaendeleaje?”

    “Nimemwacha hivyohivyo tu,” Lina aliamua kusema hivyo akijua ni akiba, huenda baadaye akaomba tena kwenda kulala hospitali ili arudi nyumbani kwa mumewe mkubwa au wa kwanza.

    Lina alivua nguo zote, akaingia bafuni kuoga, akarudi na kumkuta James akisoma magazeti mbalimbali ambayo aliyaagiza kwa mlinzi wa hoteli hiyo.

    ***

    Ilikuwa saa saba na nusu mchana, Lina alikuwa akipata chakula cha mchana na mumewe, James kwenye mgahawa wa hoteli hiyo, simu yake iliita…

    “Kaka Semi huyo,” alisema James huku akiyatoa macho kwenye skrini ya simu ya Lina na kuachia tabasamu laini. Ilibidi Lina achukue simu hiyo na kuipeleka sikioni mwake…

    “Haloo…”

    “Haloo, Peter ameshakuja yupo hapo nje. Toka!”

    “Sawa.”

    Semi akakata simu.

    Lina alimpigia simu mlinzi wa kazini kwake…

    “Haloo Mzee Kitale.”

    “Haloo.”

    “Kuna mzigo ulipewa na mtu mmoja asubuhi?”

    “Ndiyo. Nipo nao mapokezi, niliambiwa nikupe wewe lakini sijakuona leo mama, vipi unaumwa kwani?”

    “Mi mzima sana, ila kuna mtu mmoja amesimama hapo nje anaitwa Peter Kindaundau, hebu mpe huo mzigo. Lakini hakikisha kwamba ni kweli ni Peter Kindaundau.”

    “Sawa mama,” alisema mlinzi huyo mzee na kukata simu.

    “Akina nani ulikuwa unaongea nao?”

    “Wa kwanza ni bro wangu, Semi…kuna mzigo aliuacha ofisini akasema kuna mtu anaitwa Peter Kindaundau ndiyo ataufuata, sasa kaja.”

    “Huyo Peter Kindaundau namfahamu vizuri sana, si mfanyabiashara kule maeneo ya Kamata?”

    Kwanza moyo wa Lina ulimlipuka lipu! Mpaka James akabaini naye akashangazwa…

    “Vipi, mbona umeshtuka kusikia namfahamu Peter Kindaundau?”

    “Wala, kwanza mi mwenyewe simfahamu hata kwa sura wala namba zake, bro kaleta mzigo nafikiri kwa sababu ya ukaribu kutoka kwake na kwa huyo Peter. Kama ningekuwa namfahamu ningempigia yeye mwenyewe anipe mlinzi nimwelekeze.”

    Wakati Lina anajitetea kwa mapana hayo, mlinzi alimpigia simu…

    “Hebu ongea naye…”

    “Haloo…umepata mzigo aliuacha Semi?”

    “Nimepata ahsante sana.”

    “Haya poa.”

    Simu ikakatwa.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Lina alimtupia macho James, lakini James akaonekana hana wasiwasi tena, akashika simu yake na kuanza kuipekua akiangalia namba ya Peter Kindaundau…

    “Namba yake hii hapa,” alisema James huku akiipeleka simu sikioni mwake.

    “We Kindaundau, sema, za siku?” alisalimia James huku akiweka loud speaker ili Lina naye asikie…

    “Nzuri James, nasikia umefunga ndoa bwana?”

    “Eee, hivi bado nipo kwenye fungate.”

    “Hongera sana bwana.”

    Haja ndogo ilimshika Lina, ilibaki kidogo aiachie, alijua kila kitu kimefika mwisho sasa…

    “Shemeji wa wapi, anaitwa nani?” aliuliza Kindaundau…



    “Mtu wa Tanga huko, anaitwa Lina…”

    “Lina?” aliuliza Kindaundau kwa sauti yenye mshtuko…

    “Eee, Lina,” alijibu kwa kujiamini James huku akiachia tabasamu la amani ndani ya moyo na mkono mmoja ukimshikashika Lina sehemu ya mwili wake kama ishara ya mapenzi ya dhati kama mke wake.

    “Hilo jina kama nalifahamu.”

    “Utakuwa unalifahamu tu, leo si ulikwenda ofisini kwake ulichukua mzigo uliachwa na kaka yake.”

    “Eee, sawa nimekumbuka sana, ni kweli. Kumbe ndiyo shemeji uliyefunga naye ndoa?”

    “Eee…wewe nani alikwambia nimefunga ndoa?”

    “Si Yunus! Yule fundi aliyekujengea tangi la maji nyumbani kwako.”

    “Eee, nilikutana naye siku moja kabla ya ndoa.”

    Wakati wa maongezi hayo, Lina alishamalizika, ilibaki kuanguka chini tu na kukata roho lakini hakuwa yeye hata chembe.

    Kila wakati akili yake ilitafsiri mazungumzo ya James na Kindaundau na kujikuta akizidi kushtuka, mfano…

    “Utakuwa unalifahamu tu, leo si ulikwenda ofisini kwake ulichukua mzigo uliachwa na kaka yake.”

    Lina aliamini kwa maneno hayo tayari Kindaundau alishajua kuna kitu kikubwa na cha siri ndani yake endapo mume wake, Semi alimwambia aende kwenye ofisi hiyo akachukue mzigo ameuacha kwa shemeji yake na si kwa mwanamke tu…

    “Kama Semi alimwambia nenda ofisini kwa mke wangu nitakuachia mzigo pale nimeumbuka, lakini kama alitaja jina tu basi si tatizo,” alisema moyoni Lina akihema kwa kasi kama mtu aliyetoka kukimbizwa na nyoka aina ya chatu.

    Baada ya kukata simu, Kindaundau alishikwa na dukuduku, akawaza…

    “Khaa! Sasa Lina atafungaje ndoa na James wakati ana ndoa na Semi?

    “Ina maana Lina huyu ni wa Semi au mwingine? Lakini atakuwa huyohuyo, James angejuaje leo nilikwenda kuchukua vitu pale kama angekuwa hajaambiwa na Lina mwenyewe? Lazima pana jambo tena zito. ”

    Alijikuta akishika simu na kumtwangia Semi…

    “Kindaundau, vipi?”

    “Ee bwana, ulisema shemeji anaitwa nani?”

    “Anaitwa Lina, kwani hujafika tu hapo kazini kwake?”

    “Nimefika, nilisahau jina.”

    “Anaitwa Lina, we ulizia Lina,” alisema Semi bila kujua nia ya rafiki yake huyo kuulizia jina tena na wala hakujua kama mwenzake alishachukua mzigo saa nyingi sana na kuondoka zake...

    “Hivi ni shemeji kabisa?”

    “Ah! We Kindaundau naye bwana maswali yako kama ya denti wa darasa la nne, sasa hilo nalo swali gani?”

    “Nimetaka kujua tu.”

    “Mke wangu wa ndoa huyo, kwa hiyo usiwe na wasiwasi naye kwamba labda huo mzigo atakuchoma nao kwa polisi, acha woga wewe.”

    “Sawa bwana.”

    Semi alikata simu, mambo mengine yakaendelea. Semi hakuwaza kabisa kwamba simu ya Kindaundau ilikuwa na ishu nzito nyuma yake, yeye alijua kawaida.

    Kwa habari aliyoambiwa na James, Kindaundau akaamini hata James hajui kama huyo Lina ana mume, lakini bado akili ilikataa kwamba, kama ni kweli Lina huyo ni yule mke wa Semi anayemjua yeye na pia mke wa James pia anayemjua, imekuaje mpaka anafunga ndoa na kwenda fungate, Semi awe hajui…

    “Ina maana Semu anajua mke wake amekwenda wapi? Au ameaga anasafiri? Lakini hapana, mbona aliniambia niende kazini kwake nimuulizie si ina maana anajua yupo?

    “Au…” Kindaundau alishindwa kumalizia maneno akajikuta akishika simu na kumtwangia James…

    “Ee, Kindaundau sema.”

    “Hivi huyo shemeji yeye ndiyo uko naye fungate?”

    “Eee, kwani vipi?”

    “Ndoa mlifungia wapi?”

    “Si kanisani, ndoa inafungiwa wapi kwa mimi Mkristo?”

    Lina akajua tayari mambo yameharibika, Kindaundau ameshajua kila kitu kwa hiyo akaanza kufikiria namna ya kumziba mdomo…

    “Oke.”

    “Oke.”

    Baada ya kukata simu na Kindaundau, James alimwangalia Lina huku akiachia tabasamu lenye mshangao wa hali ya juu…

    “Huyu jamaa sijamwelewa.”

    “Kwa nini?”

    “Eti ananiuliza hiyo ndoa ya mimi na wewe nimeifunga kanisani au?”

    “Khaa! Ana maana gani sasa baby?”

    “Si ndiyo maana nimekwambia sijamwelewa.”

    ***

    Lina alianza kuumiza kichwa ni jinsi gani ataipata namba ya Kindaundau kwani walipoongea ilitumika simu ya mlinzi wa getini. Kuichukua kwa James ilikuwa kazi kubwa kumwambia, angetaka kujua ye ya nini? Labda kwa kuvizia akienda kuoga ambapo pia hakujua ameisevu kwa jina gani!

    Kindaundau alimtumia meseji Semi akimwambia anaomba wakutane kwani ana jambo muhimu na nyeti sana anataka kuzungumza naye na ikiwezekana isipite siku hiyo.

    ***CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    James alikuwa bafuni akijimwagia maji, Lina akavuta simu yake na kuanza kusachi majina ili alipate la Kindaundau…

    “Kindaundau…Kindaundau…Kindaundau…”

    Akakumbana nalo limeandikwa…

    “Kindaundau 2.”



    Haraka sana akaisevu namba hiyo kwenye simu yake na kuirudisha simu mahali pake. Akajibalaguza akifikiria namba ambavyo atawasiliana na mtu huyo na kumwambia chondechonde asije akatumbua jipu kama si kidonda.

    ***

    James alipotoka kuoga alijiweka kwenye kitanda na kumwita Lina mke wake ili ambembeleze kwa mahaba mazito kwa wakati ule ingawa pia, Lina alikuwa na mawazo kichwani ya kuangalia namna atakavyoaga na kurudi kwa mumewe Semi.

    “Baby, njoo basi, unajua nimekumisi sana!”

    “Hata mimi my love, nimekumisi pia.”

    “Basi kumbe tumemisiana.”

    “Ni kweli d.”

    Kwa muda huo wakiwa juu ya sita kwa sita, James alikuwa fiti kimahaba lakini Lina alionekana kuwa chini kuliko kiwango chake jambo ambalo lilimshangaza sana James, akamuuliza huku mechi ikiendelea…

    “Nahisi kama hauko sawa dear.”

    “Ni kweli.”

    “Kwa nini? Kuna nini kimetokea?”

    “Ah! Basi tu, sijui leo nimeamkaje?!”

    “Unajisikiaje kwani?”

    “Mwili na akili vyote havipo sawasawa.”

    “Unawaza nini?”

    “Sijui tu.”

    James aliposikia hivyo aliamua kujitahidi mwenyewe na alipomaliza safari yake akajiweka pembeni, naye akazama kwenye mawazo kuhusu Lina…

    “Hii ndoa ipo haipo? Mbona kama sielewielewi…

    “Mtu anasema ana mawazo, mawazo gani sasa wakati mimi nipo na ndiyo kwanza tupo kwenye ndoa mpya tena fungate.”

    Lina aliiona hali ya James akajua naye hayuko sawa kama yeye, lakini alishindwa kumuuliza waziwazi.

    “Lina,” aliita James…

    “Abee.”

    “Naomba leo tuondoke kwenda nyumbani, sina amani tena na hapa hotelini.”

    Lina alishtuka sana lakini kwa siri ili asijulikane, aliamini kitendo cha kwenda nyumbani kwa James ndiyo mambo yatakuwa wazi mapema sana jambo ambalo hakulipenda…

    “Kuna nini kimetokea baby?”

    “Nimeamua hivyo tu.”

    “Ndiyo umeamua, kuna nini?”

    “Hakuna kitu Lina, fuata ninayosema.”

    “Oke, sawa! Nimekuelewa!”

    “Kama umenielewa vizuri, naomba jiandae kwani tunaondoka muda huuhuu, sioni sababu ya kupoteza muda.”

    Lina alijiandaa, akili ilizidi kuvurugika, aibu aliiona mbele ikimnyemelea, angesema nini…

    “Hivi likibumbuluka nitasema nini mimi?” alijiuliza mwenyewe.

    Walishuka hadi kwenye gari la kifahari la James, wakazama humo na kuondoka hadi nyumbani kwa James ambapo Lina alipokelewa kwa shangwe na wafanyakazi wa ndani wa James wakijua amekwenda rasmi na si kama mchumba. Salamu zikawa nyingi, karibu za kumwaga!

    Moyoni Lina alisema…

    “Mh! Mngejua nimelikoroga wala msingenishobokea, yaani nyie mko huru kuliko mimi hapa.”

    Bado Lina alikuwa na mawazo ya jinsi gani ataaga kurudi kwa Semi. Aliona afadhali walivyokuwa hotelini kuliko pale nyumbani.

    “Bosi samahani, alikuja Bryan, akasema ukija muonane, amepata ule mzigo,” alisema mlinzi wa getini akimwambia James.

    James aliachia tabasamu kusikia maneno hayo, palepale alimuaga Lina kwamba anaondoka atarudi ndani ya dakika 50 mpaka saa moja.

    “Sawa baby.”

    ***

    Baada ya James kuondoka, Lina aliingia chumbani, akatoa simu yake huku akifurahi kwamba atapata nafasi ya kuongea na Kindaundau sasa, akapiga simu hiyo lakini haikuwa hewani!

    “Mungu wangu! Au Kindaundau 2 niliyoichukua haitumiki kwa sasa?” alijiuliza mwenyewe Lina huku mapigo ya moyo yakiendelea kumdunda.

    ***

    Katika kuelekea nyumbani kwa Bryan, James alipita mahali akakutana na Eg, rafiki wa Lina akiwa na rafiki zake wawili, wamejikwatua hao mfano hakuna, akasimamisha gari ili kumsalimia…

    “Shemu vipi?”

    “Shwari shemeji yangu, hajambo Lina?”

    “Hajambo, wapi shemeji mbona umependeza sana?”

    “Tunakwenda kwenye kikao cha hawa rafiki zangu, kinafanyika Mikocheni.”

    “Ooo! Sawa! Mgonjwa anaendeleaje?”

    Eg ndiyo akashtuka kusikia habari ya mgonjwa, akakumbuka dili lake na Lina. Kwa jinsi alivyojipara alishindwa kusema mgonjwa bado kalazwa, angeonekana hajali, akasema…

    “Mgonjwa katoka mchana wa leo shemeji, hivi hata Lina hajui lolote.”

    “Ala! Afadhali, poleni sana,” alisema Lina huku akiingiza mkono kwenye mfuko wa shati na kutoa shilingi elfu hamsini, akampa…

    “Ongezea nauli shemeji.”

    “Jamani shemeji, asante sana jamani, Mungu akubariki sana.”

    “Usijali shemeji.”

    ***CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya kuondoka tu, Eg akampigia simu Lina ili kumpa tukio hilo…

    Sasa kaondoka, akirudi nitakwambia ili unipigie simu usingizie yule mgonjwa, kwamba unaniomba nikalale naye ili wewe urudi nyumbani, niweze kurudi kwa Semi la sivyo mwenzio naumbuka…”

    “Shoga pole, haitawezekana,” alijibu kwa mkato Eg…

    “Eh! Eg, kwa nini? Ni wewe au mwingine?”

    “Yaani namaanisha tumekutana na shemeji sasa hivi?”

    “Yupi?”

    “Si James. Sasa hivi, tunaagana ndiyo na mimi nikaamue kukupigia simu. Amesema anakwenda wapi sijui, lakini kwa rafiki yake.”

    “Mh! Alikuuliza kuhusu mgonjwa?”

    “Ndiyo swali lake la kwanza. Kauliza vipi mgonjwa shemeji? Na mimi kwa jinsi nilivyovaa na kujipata leo nakwenda kwenye kile kikao cha akina Mama Mumba, nikajikuta nimemwambia mgonjwa katoka.”

    “Ayaaaa! Umeniua Eg, nitadanganya nini sasa kwa James mpaka anikubalie kutoka na kwenda kulala hukohuko mpaka kesho?”

    “Aisee! Sijui iweje! Halafu mbaya zaidi nilimwambia kabisa kwamba nakwenda kikao cha harusi.”

    Lina alikata simu kwa hasira. Alimchukia Eg. Aliamini anaweza kuwa chanzo cha lolote litakalotokea kwake na James na Semi.

    “Khaa! Sasa huyu mbona amekata simu?” alijihoji Eg akianza kuingiwa na wasiwasi.

    Kwa upande wake, Lina aliamua liwalo kwa siku hiyo na liwe, alishajua kisingizio hakuna tena. Aliamua kupanda kitandani na kujipumzisha huku akiwaza sana kuhusu hatima yake.

    “Sijui nini hatima ya hili sakata langu, nahisi Eg naye ameanza kunikimbia, ni kwa nini amwambie anakwenda kwenye kikao cha harusi wakati anajua yeye ndiyo tegemeo langu la kuondokea kwa James?”

    ***

    James alirejea nyumbani hapo saa kumi juu ya alama. Alipoingia ndani tu aliita kwa sauti ya juu…

    “Baby wa James.”

    Lina alikuwa chumbani kwa hiyo hakusikia, ila mfanyakazi mmoja wa ndani alimwambia bosi wake huyo kwamba, Lina alikuwa chumbani.

    Alikwenda chumbani na kusukuma mlango, akazama ndani na kwenda kumkumbatia Lina…

    “Baby nimekumisi sana…”

    “Mmmh! Jamani baby, hata mimi. Ila sina amani sana dear…”

    “Kisa nini tena?”

    “Nimetumiwa meseji mama anaumwa sana nyumbani, Korogwe! Si unakumbuka hata kwenye harusi yangu nilikwambia hatakuja?”

    “Ndiyo…sasa?”

    “Da! Sijui niende?”

    “Ah! Lina mke wangu, suala la mama kuumwa ni la kuamua uende au usiende? Unatakiwa kwenda, ikibidi hata kesho asubuhi na mapema.”

    “Ooh! Nashukuru kwa ruhusa baby, nilijua hutapenda ukizingatia tumetoka kwenye ndoa juzi tu.”

    “Kutoka kwenye ndoa si ishu Lina, uzima wa mama ni wa mbele. Hata kama tungekuwa tumefunga ndoa leo, usiku ukaambiwa mama anaumwa, ingebidi kwenda.”

    ***

    Usiku uliingia, Lina aliamua kuzima simu ili Semi asimpate moja kwa moja. Alijua angepigiwa na angeshindwa kujibu au kudanganya mbele ya James…

    “Lakini sasa hatima yake ni nini kama hatanipata hewani? Je, atanitafuta kwa Eg? Na kama atakwenda kule halafu asinikute, nini kitafuata? Da! Huu mzigo ni mkubwa sana kwangu, vigumu kuubeba,” aliwaza moyoni Lina kiasi kwamba, James aligundua hilo…

    “Baby, pungumza mawazo. We kesho nenda, asubuhi sana mimi nitakupeleka stendi. Kama ungekuwa unaweza kuendesha gari ungetumia gari moja,” alisema James huku akiwa anamshikashika sehemu mbalimbali mkewe huyo.

    Lakini Lina alikumbuka kitu, akawasha simu ili amtumie meseji Eg kumshawishi wapange uongo mpya kwa mumewe, Semi.

    Hata hivyo, kabla hajamtumia meseji yoyote, meseji iliingia kwenye simu yake, ilitoka kwa mumewe…

    “Baby, pole na kazi! Nimekupigia simu haupo hewani, pole. Mimi niimepata dharura, nakwenda Iringa na wale jamaa wauza madini, tunarudi keshokutwa. Please take care.”

    Lina alihisi ameona nyota ya bahati kwa kupata ujumbe ule kwani ndiyo sababu pekee iliyokuwa na uwezo wa kumpa nafasi ya kulala nje ya nyumbani kwake kwa siku hiyo.

    Alimwangalia James kwa macho yaliyojaa furaha, akamkumbatia na kumsogeza kifuani pake kisha kuanza kumpa mabusu mfululizo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog