Chombezo : Usiku Wa Kigodoro
Sehemu Ya Tatu (3)
ILIPOISHIA: Alimwalia James kwa macho yaliyojaa furaha, akamkumbatia na kumsogeza kifuani pake kisha kuanza kumpa mabusu mfululizo.
SHUKA NAYO MWENYEWE…
“Mbona umeonekana kuwa na furaha ghafla, vipi kwani?” aliuliza James baada ya kumwona Lina akihema kwa nguvu na kumvutia kwake kumpa mabusu mfululizo…
“Hamna mume wangu jamani, siku hazilingani hata siku moja, nikoje kwani mume wangu?” Sasa Lina alipata hata muda wa kusema neno ‘mume wangu.’
“Uko happy ghafla.”
“Aaah jamani baby. Lina alizidi kumbusu James mpaka wakajikuta wamezama kwenye ulingo mwingine kabisa wa mahaba mazito juu ya kitanda.
Lina siku hiyo alimfanyia mambo makubwa ya kimapenzi James kama siku yao ya kwanza kukutana ilivyokuwa.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kila hatua, Lina alihakikisha anatoa kilio cha mahaba huku akimsifia James kwamba ni mwanaume bora kwake licha ya kwamba alijua furaha yake inaweza kuwa ya muda mfupi kuliko kilio kitakachofuata mbele yake siku chache zijazo.
Lina alilala kwa furaha siku hiyo, usiku alipata hata muda wa kuchati na mumewe, Semi kwani James aliwahi kulala akijua ana safari ya kumpeleka stendi Lina asubuhi kwa safari ya kwao, Korogwe.
Kulikucha salama, Lina alijiandaa kwa safari, akapakizwa kwenye gari na James hadi Ubungo.
“Baby mpe pole sana mama, mwambie nampenda panapo majaliwa nitamuona siku moja na Mungu atamsaidia afya njema,” alisema James wakati Lina akijiandaa kupanda basi ndani ya stendi ya Ubungo.
Walipeana mabusu ya nguvu ndani, gari lilikuwa na vioo visivyoonwa ndani yaani ‘tintedi.’
Walipanda wote ndani ya basi baada ya kukata tiketi, Lina akakaa kwenye siti yake huku James akisimama pembeni akizidi kumwombea dua njema kwa safari yake. Baada ya dereva kuingia na kuingiza gia, James alimbusu Lina mbele za watu, akashuka.
Cha kwanza baada ya James kushuka, Lina aliingiza mkono kwenye mkoba wake na kutoa kitita cha pesa alizopewa na James kikiwa ndani ya bahasha. Alihesabu mpaka alipoweka kituo, tayari alishajua amepewa shilingi milioni moja na laki tano.
“Mh!” aliguna Lina, akaangalia juu ya gari kisha akawaangalia abiria wenzake na kuwaona hawana maana, maskini wakubwa.
Basi liliondoka Ubungo, likashika Barabara ya Morogoro na kusogelea mataa ya Ubungo. Mungu ibariki, taa zikaruhusu magari kupita, dereva alivusha gari na kuishika njia ya kwenda Kimara…
Ah! Konda samahani, mzigo niliokuwa nakwenda nao Korogwe nimeusahau nyumbani jamani,” alisema kwa sauti Lina huku akiwa ameshasimama na kutembea kwa kasi kuelekea mlango mkubwa.
Abiria wengine walimpa pole wengine walimshangaa kwa kuhoji iweje mtu asafari mpaka ndani ya basi kumbe anachokipeleka amekiacha nyumbani? Waliona ni usanii mtupu.
“Shusha konda, samahani sana,” alisema Lina.
Dereva akaweka gari pembeni maeneo ya Kimara-Rombo, Lina akashuka huku konda akimkazia macho kuamini kwamba huenda atadai nauli lakini wala!
Akiwa chini ya sasa, Lina aliangaza pembeni na kuona Bajaj…
“Tafadhali nipeleke Kijitonyama.”
Lina alipofika nyunbani kwake, yaani kwake na Semi, alizama ndani akiwa haamini kilichotokea. Alishika simu na kumtwangia Eg kumpa mkasa wote, Eg alishangaa sana. Hakuamini kile alichokuwa anasimuliwa na Lina.
“Sasa mpendwa wangu, ukimwambia umefika si atataka kuzungumza na mama?” aliuliza Eg.
“Nitamwambia hawezi kuongea kwani si nimemwambia mama anaumwa, sijasema anafanyiwa bethidei!”
“Hapo sawa. Kwa hiyo sasa upo nyumbani?”
“Nimejaa tele, nabadili nguo nakwenda kazini.”
Ghafla Lina akakumbuka kwamba, James huwa anakwenda sana kazini kwake na ndiko walikokutania, itakuaje akifika na kumkuta?
Alifikiria kutuma udhuru kwa mabosi wake lakini akaona kwamba ataonekana mvivu maana siku mbili tatu zilizopita alishatoa udhuru mwingine.
“Mh! Sasa itakuaje? Hapa mawili, nitoe udhuru au niende. Lakini nikienda akitokea James nimeumbuka,” alisema moyoni Lina.
Muda huohuo meseji ikaingia kwenye simu yake, akajua ni James lakini sivyo, alikuwa bosi wake…
“Lina hakikisha unafika kazini leo, kuna kazi nyingi sana zimelala. Usikose.”
Lina alijishika kichwani, akajikuna kidogo, akahema…
“Nahisi nimepatikana leo, sina ujanja. Miongoni mwa hizo kazi nyingi anazosema bosi ni pamoja na za James,” alisema moyoni Lina huku akikosa amani ya moyo.
Lina alibadili nguo, akaondoka kuelekea kazini. Ile anaingia tu ndani ya geti, James anapaki gari nje…
“Mungu wangu ndiyo mambo niliyoyakataa haya,” alisema Lina akikimbilia ndani, akaenda kuingia kwenye chumba cha kuchemshia chai ambako mchemsha chai alimshangaa…
“Lina vipi tena, unakimbizwa?”
“We acha tu! Naomba utoke, mfuatilie kaka mmoja anaingia, naamini atakuwa ameshika brifkesi, jua anaingia wapi, anatoka muda gani,” aliagiza Lina.
“Pole na kuumwa mama?”
“Aaa…santé saa…na.”
“Basi sawa mama, we pumzika tutawasiliana tena baadaye.”
“Ha…haya…aa.”
Lina aliipokea simu na kuangua kicheko ambapo mwanamke huyo naye aliungana naye kwa usanii walioufanya.
“Daa! Jamani! Ama kweli dunia tambara bovu,” alisema mama mpika chai…
“Umeona ee?”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nimeona Lina.”
“Sasa mama wewe utanisaidiaje katika hili?”
“Hili suala ni gumu sana mwanangu, tena gumu kwelikweli. Ila cha kufanya wewe kuwa muwazi kwa James, mwambie ukweli wako.”
“Hee! Si atanipeleka polisi?”
“Akupeleke polisi kwa kosa gani?”
“Nimemtapeli.”
“Sasa unadhani nini kitafuata katika maisha hayo ya kukwepakwepa, kujifichaficha? Kwanza unaelewa kuwa huyo James karibu kila baada ya siku mbili anakuja hapa ofisini…”
“Ndiyo hapo sasa mama.”
“Ndiyo maana nimekwambia hivyo au we una mawazo gani Lina?”
Lina alitulia kidogo kisha akamkodolea macho mama mpika chai na kumwambia…
“Nimuue mmoja.”
“Eti?” alishtuka mama mpika chai.
“Bila hivyo hili suala haliwezi kumalizika kirahisi hata siku moja, mi najua.”
“Sasa unataka kumuua nani kati ya James na Semi?”
“Hapo ndipo penye mtihani mkubwa.”
“Mh! Lakini hilo wazo umelitoa wapi wewe binti?”
“Mimi mwenyewe nimewaza hivyo. Unajua hii ni kesi kama nitaamua kumuweka wazi James na ni kweli ndiye anayetakiwa kuwekwa wazi…”
“Basi kama ni hivyo hata kumuua muue yeye,” mpika chai alisema.
Lina alionekana kusita kukubaliana na maneno ya mama huyo kwamba kama ni kufa afe James…
“Lakini mama, unajua mimi nahisi kama mapenzi yangu makubwa yapo kwa James na si Semi…”
“Una kichaa?”
“Kwa nini?”
“Sasa huo si ndiyo usaliti! Unampenda mwanaume wa pembeni zaidi kuliko mumeo? Ndiyo maana ndoa zinawashinda siku hizi.”
Lina alirudi kwenye meza yake bila kupata mwafaka wa namna ya kumaliza utapeli wake kwa James huku kichwa kikiwa kimejaa mawazo…
“Ukweli pale nimejibu sivyo, lakini ndiyo uhalisia wenyewe. Lazima mwanaume mmoja afe ndipo mimi niweze kuwa huru na si vinginevyo. Nani atanielewa siku ikijulikana nini kilitokea? Nitaonekana mwanamke wa ajabu sana mimi.”
***
Mchana wa siku hiyo, James alikutana na Kindaundau mjini, yule mwanaume aliyekwenda kuchukua mzigo ofisini kwa Lina ulioachwa na mume wa Lina, Semi…
“Bwana leo afadhali tumeonana, nataka tuzungumze,” alisema Kindaundau…
“Hebu tukakae kwenye mgahawa wa maana,” alisema James. Kila mmoja aliingia kwenye gari lake na kwenda kwenye mgahawa mmoja maarufu kwa jina la Mashefa!
“Kwanza nina swali lilelile la siku zile,” alianza kusema Kindaundau…
“Lipi?”
“Kuhusu mwanamke uliyemuoa…”
“Kwani Kindaundau unataka kujua nini zaidi rafiki yangu?”
“Nina wasiwasi na jambo fulani.”
“Kuhusu mke wangu?”
“Ndiyo…”
“Kuwa..?”
“Unasema anaitwa Lina si ndiyo?”
“Ndiyo! Anaitwa Lina Joseph Ambakucha, ni mzaliwa na Kijiji cha Kilole, Korogwe mkoani Tanga…”
“Sasa sikia James, mimi nina rafiki yangu anaitwa Semi…”
“Semi?” alihoji kwa mshtuko James…
“Ndiyo, Semi.”
James akakumbuka aliona jina la Bro Semi kwenye simu ya Lina…
“Enhe, kafanyaje?”
“Semi ana mke, anaitwa Lina Joseph Ambakucha. Mimi sijawahi kumwona ila kuna wakati Semi alikuwa anafukuzia mkopo mkubwa benki, Lina alikuwa mmoja wa watu wanaotakiwa kutia sahihi kwenye fomu. Kwa sababu tulikuwa tukienda benki kila siku nikalizoea hilo jina.
“Halafu juzi nadhani, nilikwenda kuchukua mzigo wangu ofisini kwa huyo Lina aliuacha mumewe, huyo Semi…”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kindaundau,” aliita James akiwa na sura yenye mshangao...
“Naam bosi.”
“Unasema?”
“Ndiyo hivyo, jaribu kuchunguza nini kinaendelea kati yenu.”
James alikuwa kama ameganda kwa muda akiwaza, akaangalia juu, kulia na kushoto kisha akamwangalia Kindaundau…
“Kuna mambo unayasema kama yana ukweli fulani. Mfano, unalitaja jina la Semi, naamini kama ni Lina mke wangu, amemsevu kwa jina la Bro Semi…lakini hebu nikuulize Kindaundau…wewe ndiye ulikwenda kuchukua huo mzigo kazini kwa Lina halafu ulimkuta mlinzi?”
“Ndiyo.”
“Halafu uliongea kwa simu na Lina akiwa hayupo kazini?”
“Ndiyo mimi. We umejuaje kwanza? Halafu umenikumbusha kitu James…baada ya mimi kuongea na Lina tu, wewe ukanipigia simu.”
“Ndiyo! Nilikuwa naye mimi alipomuuliza jina lako mlinzi akalitaja la Kindaundau nikakukumbuka na yeye Lina nilimwambia huyo mtu Kindaundau namjua na namba zake ninazo ndiyo maana nikakupigia.”
“He! Kumbe!”
“Mimi nashukuru sanasana ndugu yangu Kindaundau kwa kunihabarisha hili japokuwa nimeumia sana. Lina! Mke wangu, kumbe ana mume mwingine? Ina maana mimi si mume halali? Siamini hata kidogo. Da! Nitaua mwaka huu Mungu nasema, siwezi kuwa mwanaume bwege mimi.”
“James acha jazba.”
“No Kindaundau. Mimi ni mtu na pesa zangu. Anapotokea mwanamke anakufanyia hivi unadhani nini kitatokea hapo?”“Ni kweli kinaweza kutokea kikubwa. Lakini mimi nakushauri…”
“Unanishauri nini Kindaundau, we umeshaniambia niachie mimi. Kwanza huyo Lina kaniambia anakwenda kumwona mama yake Korogwe anaumwa. Kuna uwezekano hajasafiri…hebu mpigie huyo Semi muulize kiaina ujue mkewe yuko wapi?”
“Da! Bwana James, unavyodhani inawezekana kweli nikamuuliza swali kama hilo?”
“Naamini ukiongea naye mawili matatu atasema jambo ambalo litakupa mwanga.”
“Sawa, ngoja nijaribu.”
Kindaundau alimpigia simu Semi akiwa ameweka loud speaker…
“Hujambo bwana Semi?”
“Sijambo, vipi Kindaundau? Mzima wewe?”
“Mimi mzima bwana. Uko nyumbani nini? Maana wakubwa kama nyinyi si ajabu uko nyumbani na shemeji mnakula bata tu.”
“Nipo mkoa bwana, maisha haya bila kutafuta huwezi kuyamudu kaka.”
“Shemeji vipi? Umesafiri naye?”
“Hamna, yuko kazini saa hizi.”
“Poa, nilidhani upo Dar nikupe dili, basi ukirudi nitafute tuongee.”
“Sawa mkuu.”
Baada ya kukata simu, Kindaundau na James walitazamana…
“Kazini hayupo maana mimi nimetokea huko,” alisema James…
“Basi atakuwa amesafiri kweli?” alisema Kindaundau…
“Haiwezekani asafiri halafu huyo Semi asijue, ni ngumu.”
“Mh! Mpigie basi umuulize aliko.”
“Hapana, nitamshtua mapema sana. Mimi nataka niende naye polepole hadi aingie kwenye kumi na nane yeye mwenyewe.”
“Na kweli, ni wazo zuri sana. Ukifanya papara unaweza kupoteza ushahidi lakini ukienda naye polepole itafika mahali kila kitu kitakuwa kweupe.”
Baada ya hapo, waliagana lakini James hakutaka kuondoka na kumruhusu Kindaundau kuanza kutoka. Nyuma, James alizama kwenye kumfikiria Lina kama habari alizozipata ni za kweli!
“Mimi nahisi Kindaundau amechanganya majina. Siku hizi majina yanafanana sana. Unaweza kuwapata Lina Joseph Ambakucha hata saba, tatizo liko wapi? Na kama kweli ni Lina mke wangu, kwa nini amsevu mumewe kwa jina la Bro Semi…
“Halafu, mpaka nifunge ndoa na mke wake, yeye Semi alikuwa wapi? Tena ndoa ilitangazwa kwa siku ishirini na moja kanisani. Itakuwa si kweli.”
Hata hivyo, nyuma ya mawazo yake hayo, James alipata mawazo mengine yanayompa ushahidi kuwa ni kweli Lina aliyemsema Kindaundau ndiyo Lina wa Semi.
“Lakini si nilimsikia Lina akizungumza na mlinzi wa kazini kwake na akamtaja Kindaundau? Inawezekana ikawa ni Lina huyu kweli. Hata mahudhurio yake kwenye fungate hayakuwa mazuri, lakini ninavyojua mimi mwanamke akishafunga ndoa kukaa honeymoon ni kazi ndogo, sasa yeye kila siku alikuwa akitoa sababu.”
***CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Lina alitoka kazini jioni na kurudi nyumbani kwake kwa Semi lakini huku akiwa na wasiwasi kwamba, endapo James atampigia simu na kutaka kuzungumza na mama yake atampa nani, maana mama mpika chai alikuwa ameshaachana naye.
Pia alishangaa sana kwani James hakumpigia simu kwa muda mrefu wakati si kawaida yake.
Alifika nyumbani kwa Semi na akili moja tu kwamba, James akipiga simu asipokee kesho yake akienda kazini ndiyo atampigia na akitaka kuzungumza na mama yake atampa mama wa chai.
***
Ilikuwa usiku wa saa tano Lina akiwa kitandani kwake na kanga moja tu, James hakumpigia simu. Akaingiwa na wasiwasi, akampigia akiamini kwamba kama atataka kuongea na mama yake atamwambia amashalala. Simu ya James iliita mara nane bila kupokelewa…
“Mh! Kuna kitu,” alisema Lina akianza kuogopa.
Usiku ulipita lakini Lina hakupata usingizi kwani kila wakati alikuwa akishtuka na kuiangalia simu yake kama ataona missed calls au meseji za James…
“Hivi huyu ana nini? Mbona si kawaida yake?” alijiuliza Lina huku akiwa na mawazo kibao kichwani mwake.
***
Kulikucha, Lina alitoka kitandani huku mwili ukikataa kwani hakuwa amepata usingizi mzuri usiku uliopita kwa kumuwaza James.
Alijiandaa kwenda kazini huku akili ikimwambia ni siku nyingine ya mpambano ambapo itabidi atumie akili sana kuwepo kazini ili asibambwe na James.
Alipofika kazini tu, alipitiliza hadi kwenye chumba cha mama mpika chai…
“Shikamoo mama nanihi…”
“Marhaba, mbona leo upo kama umechoka sana?”
“Ni kweli kabisa. Yaani sijalala.”
“Kisa?”
“Kisa ni James. Toka jana hajanipigia simu wala kunitumia meseji, nimempigia simu hajapokea. Mpaka kunakucha hajawasiliana na mimi.”
“Unahisi nini?”
“Nahisi kuna kitu.”
“Kitu kama kipi?”
“Nahisi ameambiwa mchezo na mtu.”
“Mchezo gani?”
“Si kunioa mimi wakati nina ndoa nyingine?”
Lina hakutaka kujadili sana na mwanamke huyo, akatoka kwenda kwenye meza yake ambapo alikaa akitupa macho getini. Uzuri wake, meza yake akikaa alikuwa akiliangalia geti kwa mbele hivyo, mtu yeyote aliyeingia ilikuwa lazima amuone.
Aliwasha kompyuta lakini ile anaanza kushika makaratasi tu, James aliingia getini, Lulu akatoka mbio hadi kwenye chumba cha mama mpika chai…
“Kaja…kaja, ndiyo anaingia…”
“Nani?”
“Si James!”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kwa hiyo?”
“Naomba uende mama. Mpaka atakapoondoka ndiyo urudi.”
“Chai?”
“Nitapika mimi.”
Mama huyo alitoka, akamkuta James ndiyo anaingia mapokezi…
“Karibu sana.”
“Asante. Za kazi?”
“Kazi nzuri.”
“Naona bibie hajarudi.”
“Ee, bado.”
“Oke. Meneja yupo?”
“Yupo ofisini kwake.”
James alipitiliza hadi ofisini kwa meneja huyo.
Baada ya dakika tano, meneja alitoka peke yake na kwenda hadi kwenye chumba cha jiko…
“Lina yuko huku?” aliuliza akifungua mlango.
“Nipo bosi, nakunywa chai.”
“Leo chai unanywea huku?”
“Nimeona ninywee huku bosi.”
“Kuna mgeni kule kwangu, mletee maziwa ya moto bila sukari wala kitafunwa,” alisema bosi huyo huku akitoka. Lina alitazamana na mwanamke huyo kisha akasema…
“Siri inafichuka sasa. Nifanyaje mama nanihi?”
“Mh! Sijui mwenzangu. Na wageni wa kwa mabosi wewe ndiyo unayetakiwa kuwapelekea mahitaji yao, nikienda mimi si itakuwa balaa? Si unakumbuka siku ile nilipeleka kahawa kwa mhasibu wakaniwakia?”
Lina alianza kulia. Aliandaa maziwa huku machozi yakimchuruzika mashavuni, moyoni aliilaani sana siku ya kwanza kukutana na James ambapo ilikuwa kwenye ofisi hiyohiyo.
Alibeba maziwa hayo yaliyokuwa katika kikombe cha dongo na kukiweka kwenye sinia na kwenda nayo. Alipofika mlangoni alisimama, akasali kwa muda kisha akafungua mlango na kuzama ndani.
James alikuwa ameinama akisoma Gazeti la Daily News ambalo ni pana sana hivyo alilishika pembe ya kulia na kushoto kiasi kwamba hakuinua macho kumwangalia Lina.
Lina aliweka sinia na kutoka haraka sana na wakati anafunga mlango akageuka kumwangalia James, bado alikuwa amezama kwenye kusoma gazeti hilo.
Hakuondoka, akasimama na kuchungulia ndani kupitia tundu za funguo kwenye kitasa, akamwona James akiweka gazeti mezani na kupeleka mkono kwenye kikombe cha maziwa.
“Kwa hiyo ile fedha iliyozidi nikupe wewe au mista Brown?” aliuliza James, Lina akaondoka zake. Aliingia kwenye chumba cha chai na kumkuta mama mpika chai akimsubiri kwa hamu kubwa.
“Enhe? Imekuaje?”
“Huwezi amini, nimeshinda mtihani mmoja, bado wa pili. Nimeingia, nimeweka maziwa, nimetoka James hajaniona. Kainama anasoma gazeti.”
“Kweli?”
“Kweli kabisa, sasa nasubiri kwenye kutoa sinia na kikombe.”
“Kwanza unatakiwa urudi mapokezi, uliona bosi amekuja huku ina maana amekupigia simu sana mapokezi hukupokea.”
“Mh! Huo ni mtihani mwingine,” alisema Lina akionekana ana wasiwasi kupita kawaida.
Baada ya nusu saa akiwa bado kwenye jiko, alisikia simu ya mapokezi inaita…
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mh! Naitwa sasa,” alisema Lina huku akijishika kifuani kama ishara ya kuogopa.
Alitoka hadi mapokezi, akapokea…
“Haloo bosi.”
“Njoo uchukue vitu vyako.”
Lina alikata simu, akatembea kwenda chumbani huku moyoni akisema…
“Liwalo na liwe tu, sasa nitafanyaje? Kwanza ni afadhali ajue ili hili zigo linitue, nitaishi kama mkimbizi hadi lini sasa?”
Lina aliingia kwenye ofisi ya bosi wake huyo akapata mshtuko kutomuona James…
“Chukua vyombo vyako bwana,” alisema bosi wa Lina huku akiwa ametumbulia macho vyombo hivyo. Lina alitamani sana kumuuliza aliko mgeni, lakini kwa sababu ya cheo alishindwa. Akatoka haraka mpaka jikoni…
“Nikwambie kitu mama angu, sijamwona James kule kwa bosi,” alimwambia mama wa Chai…
“Mh! Ina maana ameondoka au?”
“Sidhani, nahisi amekwenda chooni.”
Dakika tatu mbele wakasikia watu wakitoka huku wanaongea…
“Hao wanatoka sasa,” alisema Lina.
Ni kweli, bosi wa Lina alikuwa akimsindikiza James huku wakiongoea mambo mbalimbali ya biashara.
Lina alipotoka, alisimama mapokezi na kumwona James akiishia na gari lake huku bosi wake akirudi…
“Lina,” aliita bosi huyo.
Lina moyo ukamlipuka lip!
“Abee bosi.”
“Unamfahamu mtu anaitwa James?”
Lina alitaka kuanguka chini, alihisi haja ndogo lakini akajikaza…
“Ni yupi huyo bosi?”
Lina alipojibu hivyo, bosi wake alikaa kwenye kiti cha wageni lakini kabla hajasema neno akasimama akimwambia…“Hebu twende ofisini kwangu kwanza.”
Lina alisimama, bosi wake alitangulia mbele, yeye akafuata nyuma. Alijua ishu imeshasanuka, ameshagundulika ni muongo, tapeli mkubwa.
“Karibu,” alisema bosi huyo.
“Asante.”
Bosi huyo alimwangalia kwa muda Lina kisha akaanza…
“Humjui James?”
“Yupi huyo bosi?”
“We unamjua James yupi?”
“Mimi namjua James kijana mmoja anakujaga hapa.”
“Leo kaja?”
“Sina hakika.”
“Huna hakika? Kwani maziwa ulimletea nani?”
“Bosi, nilipoleta maziwa nilimkuta mgeni anasoma gazeti la Daily News, wala sikumwona sura. Nilipofuata vyombo sikumkuta, labda alikuwa chooni. Kwa hiyo sijamwona.”
“Oke. James huyo unayemsema wewe ni nani yako?”
Lina alikaa kimya kwa muda akijiinamia…
“Bosi ni stori ndefu.”
“Kama ipi Lina? Mbona una hatari wewe msichana?! Yaani na uzuri wako wote unakuwa tapeli wa mapenzi?”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nimekosa bosi.”
“Umekosa nini sasa?”
“Nimekuwa mwongo kweli.”
“Mimi nilikuwa sijui lolote, leo ndiyo kaniambia unajua mimi nimefunga ndoa ya Lina? Nikamuuliza Lina gani? Akasema Lina mfanyakazi wako. Nilishtuka sana. Mimi ninavyojua wewe umefunga ndoa na Semi, sasa kusikia umefunga na mwanaume mwingine da..!
“Nikamuuliza unaishi naye? Akasema ndiyo, ila kasafiri kwenda kwao Korogwe, Tanga mama yake ni mgonjwa. Kidogo niseme yupo na nikuite mbele yake lakini nikajua kuna siri imefichwa, ndiyo maana kumbe hukai mapokezi ulimwona akiingia, si ndiyo?”
Lina alikubali kwa kutingisha kichwa juu kwenda chini na kurudi tena juu kuashiria amekubali alichoambiwa.
“Hebu niambie, nini kilitokea?” aliuliza bosi huyo huku akijiweka vizuri.
Lina naye alikaa sawa, akamwangalia bosi wake huyo kisha akaangalia ukutani. Aliporudisha macho kwa bosi wake akafunguka kuanzia mwanzo wa kukutana na James kazini hapo, ndoa hadi siku hiyo ambayo James alimwambia yeye yupo Korogwe...
“Mh! Lina, mbona una hatari wewe halafu mambo yenyewe mazito. Sasa unadhani nini kitatokea mbele?” aliuliza bosi huyo huku akimkazia macho Lina…
“Hata sijui bosi. Lakini nimeamua kukwambia ukweli wote ili kama unaweza kunisaidia ufanye hivyo.”
“Mh! Cha kukusaidia sina Lina, naamini ni wewe kujisalimisha kwa James na kumwambia ukweli maana yeye ndiyo hana ndoa na wewe na si Semi…”
“Je, nikimwita mbele yako nikatubu kwake?”
“Unahisi itawezekana? Hilo ni suala la kijamii zaidi tena kifamilia. Kulizungumzia ofisini si sahihi, mbaya zaidi kitendo hicho kinaichafua kampuni.”
Lina alijiinamia kwa muda akitafakari jambo huku akiwa hana la kusema na bosi wake huyo alikuwa akimwangalia tu huku akipangapanga vitu mezani kwake japokuwa havikuwa katika mpangilio mbaya.
“Unamjua nani katika marafiki wa James?” aliuliza bosi huyo.
“Hakuna.”
“He! Kweli? Mbona ni tatizo kubwa sana. Yeye anamfahamu nani kwenye ukoo wako?”
“Hakuna.”
“Mh!”
Wakati wanaendelea kuzungumza, mara mlango uligongwa, bosi akauliza nani?
“James.”
“Mh!” aliguna kwa mshtuko Lina lakini kwa sababu alishamweleza bosi wake kila kitu ikabidi bosi huyo aamue kwa busara kumchukua Lina na kumwingiza chooni mwake kisha akafungua mlango kumkaribisha James...
“Vipi bwana James?”
“Nimesahau ile kadi ya namba za kule Marekani.”
“Oooh, hii hapa,” alisema bosi huyo akiwa ameufungua mlango kwa uwazi mkubwa, James akaingia kuichukua kadi hiyo, akaondoka lakini safari hii hakusindikizwa.
Bosi alimfuata Lina, akamtoa chooni…
“Unajua kwa nini niliamua kukuingiza chooni ili usionane na James?”
“Naamini hukupenda niumbuke.”
“Hilo ni mojawapo lakini pia sababu kubwa umeniambia kila kitu, nikajua akikuona humu ndani inaweza kuwa balaa zito,” alisema bosi huyo akiwa amekaa.
Lina alikosa amani ya moyo, alijikuta akiwa mdogo kuliko inavyotakuwa kuwa. Aliamini uzuri wake ndiyo kisa cha yote, akajichukia ghafla.
“Nashukuru sana bosi, lakini sijajua nitamalizaje hili tatizo.”
“Mtegemee Mungu litaisha, lakini ikiwa tu kama ndani ya moyo wako utakiri kwamba ulichofanya sicho.”
“Nakiri hata sasa bosi kwamba nilichofanya sicho kabisa.”
“Basi kaendelee na kazi.”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Lina alisimama huku bosi wake akimwangalia kwa macho makavu kabisa, akaenda kwenye eneo lake la kazi, alikaa kwa hali ya wasiwasi, lakini aliamini anaanza kupata mwanga wa tatizo.
“Lakini lazima James atakuwa amejua kitu, haiwezekani asinipigie mpaka kunakucha halafu tena mpaka saa hizi, si kweli, amesikia kitu,” alisema Lina. Mara palepale simu ikaingia, James alipiga…
“Mh! Hatajwi,” alisema…
“Haloo baby?” alipokea Lina…
“Yes d, nimekususa leo.”
“Nimeshangaa, nikasema huyu mume wangu vipi tena,” alisema Lina huku akisimama kwenda jikoni. Alijua lazima atamuulizia mama…
“Vipi mama anaendeleaje?”
“Kidogo nafuu.”
“Nipe nimsalimie.”
Lina alishamminya mama wa chai, akampa simu naye akaigiza. Walizungumza kwa sekunde kama kumi na tano kisha James akaomba kuongea tena na Lina, simu ikarudishwa…
“Sasa unarudi lini, si kazini uliomba ruhusa ya siku chache tu?”
“Nitarudi kesho.”
“Oke, halafu leo nilikwenda kazini kwenu, nikamkuta yule mmamamama, sijui anafanyaga kazi gani?”
“Ee, mama yetu huyu bwana, anapikaga chai,” alisema Lina lakini akashtuka kwamba ameongea kitu cha kujikamatisha kule kusema ‘mama yetu huyu’ wakati yeye yuko mbali na ofisi, angesema ‘mama yetu yule’.
Baada ya kukata simu alimwambia yule mwanamke alichozungumza na James. Pia alimwambia alichomsimulia bosi wao.
***
Lina alikuwa nyumbani kwake usiku, mumewe alisharudi. Wakiwa sebuleni wamekaa, mumewe akasema…
“Yule rafiki yangu Kindaundau anasema ana shida sana na mimi. Sijui ana shida gani maana namuuliza ni nini anasema mpaka tukutane laivu.”
“Mh!” Lina aligunia moyoni, alijua kumekucha sasa…
“Kwani mna dili lolote kwa sasa?” aliuliza Lina akiwa anaangalia chini.
“Hatuna. Halafu yule ana kawaida moja, akiwa na tatizo anasema nashangaa hili anasema si la kuongea kwenye simu.
Kesho yake ilikuwa sikukuu, Lina aliwasiliana na James akamwambia ndiyo anapenda gari Korogwe kurudi Dar, James akamuuliza ataingia saa ngapi ili akampokee…
“Kwenye saa nane,” alidanganya Lina…
“Basi linaitwaje?”
“Burudani.”
“Basi utanikuta stendi Ubungo.”
“Sawa baby.”
***
Saa saba mchana, Semi alimwambia mkewe Lina waende wakale Mlimani City. Lina alitaka kuchomoa lakini akahisi mumewe hatamwelewa kwani ni kawaida yao sikukuu kutoka kwenda kupata lanchi au dina mahali.
Walifika Mlimani City, wakaa kwenye meza ya peke yao kabla hawajasikilizwa, Semi alimpigia simu Kindaundau na kumwambia kama yupo jirani aende hapo. Akamjibu ampe dakika kumi na tano tu.
***CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Saa nane kamili, James alifika Ubungo stendi bila kumpigia simu Lina. Alitaka akishafika ndiyo ampigie.
Aliegesha gari mahali, akashuka na kutembeatembea huku sasa simu ikiwa sikioni akimpigia Lina.
Lina akiwa na mumewe, Semi alipata mshtuko mkubwa sana kuona simu ya James, akakumbuka kwamba alimwambia atafika Dar saa nane.
Kwa upande wake, James alishangaa kupiga simu ya Lina mara tatu bila kupokelewa. Mara, akaliona basi la Burudani likiingia, akalifuata.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment