Chombezo : Usiku Wa Kigodoro
Sehemu Ya Tano (5)
ILIPOISHIA
“Mh! Hebu soma meseji hii,” Lina alisema akimpa simu Eg.
“Kuna nini umesahau kwangu we binti,” Eg aliisoma meseji hiyo kwa sauti huku akitingisha kichwa. Alipomaliza, alimwangalia Lina kisha akasema…
“Unajua kama angeandika meseji hii huku hujui shemeji Semi atasemaje hapo sawa. Lakini sasa, Semi naye kaonesha kukwazika, ndiyo nahisi pana tatizo hapo.”
“Sasa Eg hebu nishauri, nifanyaje sasa?”
“Aisee sina cha kukushauri shoga yangu. We cha kufanya ni kumwachia Mungu tu, yeye ndiye anaweza kulitatua tatizo lako lakini kwa akili zetu hakuna kitu. Unajua nini Lina?”
“Niambie…”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kama angetokea mmoja wao ndiye akawa amegundua kuwa upo kwenye ndoa nyingine, yaani awe Semi au James isingekuwa tatizo lakini sasa wamejua wote halafu kwa siku moja,” alisema Eg na kuzidi kumpa maumivu mwenzake.
Lina alilia sana, alifika mahali sauti ya kilio chake ilionekana kama amefiwa na mzazi wake.
“Lina shoga yangu, maisha yako hivyo, nilishakwambia mbona. Leo unalia, kesho utafurahi. Cha msingi we mwombe Mungu tu,” alisema Eg naye akisikitika. Lakini moyoni alijua alichokifanya Lina, yeye asingediriki kukifanya hata iweje!
“Unajua Eg maisha yangu yamebomoka?”
“Ni kweli Lina. Maana hali yenyewe ndiyo hivyo tena.”
“Da! Sijui nitafanya nini mimi Lina? Hivi, ni kwa nini nilikubali kuingia kwenye ujinga kama ule?”
“Ni shetani tu shoga yangu.”
***
James alikuwa ameweka laptop kwenye mapaja yake akiandika. Alionesha hana amani kivile, mfanyakazi wake mmoja wa ndani akamfuata na kusimama pembeni yake, akamuuliza…
“Bosi, shemeji vipi, jana uliondoka naye lakini hukurudi naye, kuna tatizo?”
“Hebu waite wenzako wote niwaambie kwa pamoja,” James aliagiza.
Wafanyakazi wake wote, hadi wa getini walifika na kukaa kwa adabu…
“Jamani nataka kutoa tamko. Lina si mke wangu tena?”
“Umemfumania bosi?” waliuliza kwa pamoja.
“Hapana, ila imekuja kubainika kumbe ana mume wa ndoa kama mimi.”
“Eee?” waling’aka wote wakamtumbulia macho.
“Jana nilipoondoka naye tulikwenda kukaa Mlimani City ili tupate chakula cha pamoja, akaja bwana mmoja akasema amenifumania mimi na mkewe. Nilimwambia ni mke wangu akasema ni wake, tena wamefunga ndoa kanisani…”
“Ye Lina alisemaje?” mmoja wa wafanyakazi aliuliza.
“Hakusema kitu, alibaki analia. Kwanza alizimia, alipozinduka akaondoka mbio.”
“Aaa! Itakuwa kweli.”
“Siyo itakuwa, ni kweli. Nilikwenda hadi nyumbani kwa yule bwana, nilikuta picha yao ya harusi ukutani.”
“Mh! Hiyo kali. Sasa aliwezaje kuwa na wewe halafu ana mume nyumbani? Au waliachana?”
“Hawajaachana.
Kuna mchezo alikuwa akinifanyia Lina, anaaga anakwenda kulala hospitali kuna mgonjwa kumbe anakwenda kwa mume wake, kule nako anaongopa anakwenda kulala hospitali kumbe anakuja kwangu. Yaani sijui ni kituko gani hiki! Kuna mambo makubwa mengi tu. Alisema anasafiri kwenda kwao, hakwenda alirudi kwa mume wake…
“Sasa mbona amerudi na vitu?”
“Kanunua sokoni ili niamini ametoka safari. Nimejua kila kitu chake.”
***
Semi siku hiyo alishinda ndani tu, alikuwa akiwasiliana na ndugu zake mbalimbali na kuwapa taarifa ya alichokifanya Lina. Wengi walishtuka sana, wengine walisema hawajawahi kusikia achilia mbali kuona…
“Labda ungeniambia aliomba talaka kwako ili akaolewe na mwanaume mwingine, lakini kufunga ndoa nyingine na ya kwanza ipo na tena anaishi na wanaume wote kwa nyakati mbalimbali, sijawahi kusikia,” alisema kaka yake Semi, anaitwa Trela!
“Ndiyo hivyo kaka. Hivi hapa ninachotaka ni kufanya utaratibu wa talaka mahakamani,” alisema Semi…
“Hata mimi naunga mkono mdogo wangu. Kwani kuna kila dalili kwamba huyo mwanamke angeweza kukuua wewe ili abaki na mume mmoja.”
“Ni kweli kaka.”
***CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Lina alikuwa ameduwaa, simu yake ikaita. Aliichukua haraka akiamini inaweza kuwa imetoka kwa mmoja wa waume zake. Kuangalia skrini lilijitokeza jina Boss!
“Mh! Eg bosi wangu anapiga simu.”
“Pokea.”
Lina akapokea…
“Haloo bosi…”
“Wewe uko wapi?”
“Nipo mahali bosi.”
“Upo mahali? Kivipi?”
“Bosi nina matatizo makubwa sana, siko nyumbani niko kwa rafiki yangu. Zile ndoa zote zimevunjika bosi wangu. Maisha yangu yameharibika bosi wangu, Lina si Lina tena,” alisema mrembo huyo huku akianza kulia tena.
“Ilikuwaje tena Lina?”
“Nilikuwa na James tumekaa Mlimani City tunakula, akatokea Semi…”
“Duu! Hiyo kali. Kwani hukujua kama Semi ataweza kuja?”
“Alikuwa Zanzibar kumbe akarudi bila kuniambia, ndiyo na yeye akaamua kuja Mlimani City…uuuuwi! Eeee! Najiua bosi,” alisema Lina huku akilia
“Lina,” aliita bosi wake…
Abee bosi…”
“Kujiua si sababu wala dawa kwani wako waliokufa bila kukumbwa na mkasa kama wako. Mwombe Mungu akusaidie kwa namna yoyote ile,” alisema bosi huyo na kukata simu baada ya kubaini kwamba, Lina alikuwa akiendelea kulia.
“Mjinga sana huyu mtoto...ala! Yeye alitarajia nini sasa. Wenzake wakirubuniwa sana wanachepuka tu, sasa yeye mpaka kuamua kuolewa kabisa, hata kama ningekuwa mimi ndiyo mume wake nisingemwacha,” alisema bosi huyo huku akifikiria namna ya kumsimamisha kazi Lina.
***
Semi alikuwa safarini kwenda Korogwe, nyumbani kwa akina Lina kuweka wazi mambo ya mtoto wao. Safari yake hiyo hakumwambia Lina wala mtu mwingine yeyote yule.
Alifika saa kumi na mbili jioni na kukaribishwa kwa mshangao mkubwa maana mara zote anazoendaga, Lina huwajulisha kwanza…
“Karibu baba, za mjini? Mbona ghafla sana,” alisalimia mama Lina huku baba Lina akimwekea kiti.
Walichoona kimepungua au kuna jambo ni baada ya kumwona hajashusha zawadi yoyote kama walivyozoea kumwona akienda.
Baada ya salamu na mazungumzo mengine ya hapa na pale, Semi akaanza…
“Wazee kama mnavyojua, mshenga wangu alishafariki dunia hivyo kuna mambo yamenifanya nije mwenyewe hapa nyumbani…”
“Ndiyo ndiyo,” alisherehesha baba Lina huku mama akikaa vizuri…
“Nataka kuweka wazi kwamba Lina si mke wangu tena…”
“Eee!!” alishtuka mama mtu akamtumbulia macho Semi…
“Lina si mke wangu tena, iwe kwa talaka mahakamani au bila talaka. Nasema hivyo kwa sababu amefanya jambo moja la ajabu sana ambalo sijawahi kulisikia likifanywa sehemu nyingine hapa duniani.”
“Amefanyaje tena baba?” aliuliza baba mtu huku akianza kuhisi maisha magumu kwani msaada wa Semi kwao ni mkubwa sana tangu amemuoa binti yao…
“Lina amefunga ndoa na mwanaume mwingine, anaitwa James. Suala hilo halina ubishi kwake wala kificho, hajasingiziwa wala kuonewa…”
“Ngoja kwanza mkwe,” alidakia baba Lina…
“Eee…”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ina maana Lina amefunga ndoa na mwanaume mwingine wakati ndoa yake na wewe haijavunjika au imevunjika kwanza?”
“Amekwenda kanisani akiondokea kwangu, aliniambia anakwenda kwenye sherehe ya rafiki yake akaniomba alale hukohuko kumbe ndiyo wamekwenda kupumzika na huyo mumewe mwingine.”
Semi alihisi wazazi hao wa Lina hawataweza kumwelewa hivyo aliamua kuanika mkasa mzima mwanzo hadi mwisho na jinsi yeye alivyojua na alivyokaa na James na kumweleza ilivyokuwa.
Mama Lina aliangua kilio kikubwa sana kama amefiwa na huyo Lina, baba akachukua simu palepale na kumpigia Lina, ikawa hivi…
“Shikamoo baba,” Lina alisalimia baada ya kupokea simu…
“Lina,” aliita mzee huyo.
“Abe baba…”
“Una baba yako mwingine zaidi ya mimi?”
“Sina baba mwingine zaidi ya wewe baba, kuna nini?”
“Mumeo yuko hapa nyumbani. Sasa tambua mwenyewe kaleta habari gani kwetu?”
Lina alikata simu, akaizima kabisa…
“Vipi tena shoga?” Eg alimuuliza…
“Nimekwisha Eg…”
“Kivipi?”
“Semi yuko nyumbani Korogwe.”
“Mungu wangu! Kimenuka Lina, kila kitu sasa wazi hadi kwa wazazi, maskini shoga yangu wewe, utafanyaje sasa?”
“Eg mimi nakwambia sina namna, ni kujiua tu,” alisema Lina akasimama…
“Unakwenda wapi sasa Lina?”
“Nakwenda kujiua Eg, baki salama.
Niliipenda dunia na mambo yake lakini kifo nacho kimenipenda zaidi. Sina jinsi, simchukii Semi kwa kitendo chake cha kwenda kusema nyumbani wala simchukii James kwa kunitumia ile meseji bali najichukia mwenyewe kwa uamuzi wangu ulioshindwa kuangalia mbele ya safari.
“Nilidhani binadamu kuheshimika ni neema ya Mungu kumbe ni jinsi unavyoweza kutengeneza maisha yako mwenyewe. Mimi si wa kuheshimiwa tena. Kwanza niheshimiwe kwa ajili ya kitu gani nilichokifanya. Nikifa Eg nakuagiza wewe nizikwe kokote kule na vyovyote vile.
Lakini pia kukwambia kwamba uwaambie ndugu zangu wamuombe mume wangu wa ndoa halali, Semi asimamie mazishi yangu,” Lina aliondoka kwa kasi Eg alimfuata nyuma akimzuia kuondoka.
Kwa vile Eg alikuwa ndani ya kanga moja tu, alishindwa kutoka hadi nje, akarudi kuvaa gauni na kutoka mbio lakini alikuta Lina ameshapanda Bajaj…
“Nipeleke Kijitonyama,” alisema Lina akimwambia dereva wa Bajaj.
Lina alirudi nyumbani kwake, akakuta mlango umefungwa kwa nje. Alilijua hilo baada ya kuambiwa Semi yupo kwako, Korogwe.
Alikwenda mtaa wa pili akamwita fundi na kumwomba auvunje mlango ili aingie ndani. Fundi hakuwa na maswali kwa vile anamfahamu Lina kuwa ni mke wa Semi, akauvunja, akapokea malipo yake, Lina akazama ndani.
Alichukua chupa tupu ya bia akaipasua na kusaga vipandevipande ili avinywe. Aliona ni vema akanywea maji, akafuata maji kwenye glasi.
***
Akili ilimruka Eg, kwamba Lina atakuwa ameshika uelekeo gani, akahisi nyumbani kwake, yeye akakodi bodaboda…“Please anko nikimbize Kijitonyama haraka sana,” Eg alimwambia suka.
Bajaj iliendeshwa kwa mwendo wa kasi kidogo hadi Kijitonyama nje ya nyumba ya Lina, Eg akashuka bila kulipa nauli na kukimbilia ndani ili kumuwahi Lina kabla hajajimaliza kama alivyoahidi mwenyewe kwamba anakwenda kujiua.
“Lina...Lina…” aliita Eg kwa sauti ya juu akikimbilia chumbani, alisukuma mlango na kumkuta Lina anaweka vipande vya chupa kwenye kikombe ili avinywe.
“Wee…weeee, acha hivyo Lina…Lina,” Eg alimrukia Lina wakaenda wote sakafuni…
“Lina noo! Usifanye hivyo tafadhali,” alisema Eg akimpokonya glasi Lina.
Cha ajabu Lina akaanza kulia kwa sauti ya juu kama vile amesikia habari za msiba wa mama yake mzazi.
Kusikia mayowe hayo, yule dereva wa Bajaj nje akawasha Bajaj yake na kutimua mbio. Haikujulikana mara moja kisa cha kukimbia vile wakati yeye alipeleka abiria pale.
Baadhi ya majirani walifika kutaka kujua kulikoni Lina akaangua kilio vile. Wengi walijua amepatwa msiba mzito, kama si baba, mama. Lakini ndani ya moyo wake, Lina ndiyo alianza kuingiwa na hisia za kitendo alichokifanya ndiyo maana akalia sana. Alipata hisia kali na kujilaumu kwa kumfanyia mumewe, Semi kitendo kibaya kama kile.
“Hodi wenyewe,” majirani walibisha hodi.
Eg akatoka akiwa ameshika glasi iliyokuwa na vipande vya chupa ndani ambapo Lina alitaka kuvinywa…
“Karibuni.”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Jamani mbona tunasikia kilio, vipi tena?”
“Ah! Amepata taarifa si nzuri sana.”
“Kafiwa.”
“Ndiyo.”
“Na nani?”
“Shangazi yake kijijini. Ndiye aliyemlea.”
“Oh! Mpe pole, shangazi akishakulea huyo ni mama mzazi kabisa,” alisema mama mmoja jirani. Kwa ubinadamu, majirani hao walitoa michango mbalimbali. Wengine walifungua vitenge wakatoa elfu kumi, wengine elfu ishirini. Jumla zilipatikana laki moja, Eg akasema moyoni…
“Ama kweli kufa kufaana lakini huku si kufa kufaana bali wajinga ndiyo waliwao.”
Walipoondoka, Eg alimwaga zile chupa kwenye taka, akarudisha glasi mahali pake na kurudi chumbani. Hakuwahi kuingia chumbani kwa Lina ndiyo mara ya kwanza siku hiyo.
Kwa haraka sana Eg aliamua kutumia ufahamu wake kumpigia simu Semi ambaye muda huo alikuwa gesti amejipumzisha baada ya kumalizana na wazazi wa Lina. Baba wa Lina alikuwa akimtafuta kwa simu binti yake bila mafanikio baada ya kuzima simu.
“Shem…” aliita Eg…
“Ndiyo shem, mzima?”
“Mzima wapi bwana, kuna matatizo huku!”
“Matatizo gani?” alihoji Semi bila kuonesha dalili ya mshtuko.
“Mkeo ametaka kunywa vipande vya chupa.”
“Kisa?”
“Nadhani kwa yaliyotokea shem.”
“Sasa shem akinywa yeye ndiyo nimekunywa mimi? Na nikinywa mimi ndiyo amekunywa yeye sidhani kama ni shida.”
“Ni shida! Unajua tuko ndani ya nyumba yako?”
“Ndani ya nyumba yangu, mmeingiaje?”
“Sijui, mi nimemkuta ndani akiwa ameshika glasi ina vipande vya chupa tayari kwa kuvibugia.”
Kuna sauti ilipita kwenye kichwa cha Semi ikisema…
“Umefanya mangapi katika maisha yako ambayo ni machukizo kwa Mungu mbona umesamehewa? Jaribu kusamehe na wewe. Mbona Zanzibar una mwanamke. Morogoro una mwanamke. Tanga ulikwenda ukaishi kwa mwanaume siku saba nzima tena ukiwa na huyuhuyu Lina, samehe bwana.”
“Sikia shem. We si upo hapo?”
“Ndiyo.”
“Kwanza hebu niambie ukweli, Lina alilala kwako jana?”
“Hapana, nimekuja baada ya kumkosa kwenye simu ndiyo nikajua labda anaumwa, nikaja na kumkuta na glasi…
“Nilipomuulizia akanisimulia matatizo makubwa sana…”
“Ina maana ulikuwa huyajui shem?”
“Nilikuwa siyajui hata moja, nimeshangaa sana sana, tena sana.”
Kwa mbali, Semi alianza kumwamini Eg japo awali alijua ni mulemule tu. Aliamini zaidi baada na yeye kukumbuka kwamba akiwa na wazazi wa Lina, Korogwe alikata simu akazima.
Pia alianza kuamini alipobaini kwamba Lina hakuwa kwa Eg lakini akaingiwa na wasiwasi kwamba kama hakuwa kwa Eg alikuwa wapi!
“Sasa sikia shem?”
“Ndiyo shem…ndiyo shem…nimekuelewa shem…sawa shem….eee, sawa shem….oke shem…”
Muda wote, Lina alikuwa akisikiliza baada ya kugundua kuwa, Eg alikuwa akiongea na mumewe lakini hakujua walikuwa wakiongea nini ila kwake yeye ilikuwa ni hatua kama kweli Semi amepoteza muda wake kumsikiliza Eg ambaye ni rafiki yake kipenzi.
Eg alipomaliza kukata simu tu, Lina akamuwahi hata kabla hajapumua…
“Naamini ni Semi huyo?” aliuliza kwa haraka Lina.
“Ndiyo mwenyewe.”
“Amesemaje? Niambie tafadhali…”
“Anasema mimi nisiondoke hapa nikuangalie mpaka yeye aje kesho,” alisema Eg na kumfanya Lina kuwa na matumaini kidogo kwamba huenda msamaha ukatembea kama si kupita.
“Anaweza kunisamehe kweli kwa jinsi ulivyoongea naye?”
“Anaweza. Tena uwezekano ni mkubwa kuliko unavyofikiria.”
“Mh! Ikiwa hivyo kweli Mungu ni mwema kwangu,” alisema Lina.
“Lakini Lina,” aliita Eg…
“Niambie.”
“Mimi nina wazo…”
“Lipi hilo Eg?”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kwa nini tusiende kwa yule padri aliyekufungisha ndoa ukatubu yote kisha yeye akamwita Semi kumpa maelekezo ya msamaha kwako?”
Lina aliangalia juu kama anayejiuliza jambo fulani. Alionesha kukubaliana na maneno ya Eg. Alimkumbuka padri huyo ambaye siku si nyingi zilizopita alikutana naye mjini akamuuliza…
“Ndoa yako inasemaje? Bado iko imara?”
“Iko imara Faza Denis.”
“Mungu awabariki sana.”
“Amina Faza Denis.”
“Eg ni kweli Eg. Mimi pia nakubaliana na wewe,” alisema Lina baada ya kuwaza kwa muda mfupi.
***
Ilikuwa jioni ya saa kumi na moja, walikwenda kanisani kuonana na Faza Denis ambaye aliwapokea kwa mikono miwili huku akimpongeza Lina kwamba amenawiri, mumewe anamtunza vizuri.
“Enhe, Lina nikusaidieni nini? Mwenzio anataka kufunga ndoa kama wewe?” aliuliza Faza Denis…
“Hapana Faza Denis. Nina matatizo makubwa sana sana sana tena sana…”
“Ndani ya ndoa? Maana sitarajii umeniletea matatizo ya kiofisi.”
“Ndani ya ndoa Faza Denis.”
“Mumeo Semi yuko wapi?”
“Yuko ukweni kwake, Korogwe.”
“Una maanisha kwa wazazi wako?”
“Ndiyo.”
“Haya, nakusikiliza,” alisema Faza Denis huku akikaa sawasawa kwenye kiti, kiganja cha mkono wa kulia akakitumia kushikilia kidevu…
“Huyu ni rafiki yangu mkubwa, anaitwa Agnes. Mimi nimezoea kumwita Eg, wengine wanamwita hivyo. Kanisindikiza hapa…
“Faza, kuna tukio nimelifanya ndani ya ndoa limeniletea hali mbaya sana pengine hata ndoa yangu kutaka kuvunjika…”
“Ni lipi hilo Lina? Unanitisha hata mimi kiongozi wako wa kiroho.”
Lina alianza kusimuliza kisa kizima cha James kwake mpaka kufunga naye ndoa nyingine.
Wakati anasimulia, kuna muda Faza Denis alitingisha kichwa kusikitika, wakati mwingine alitumbua macho. Pia kuna wakati alitumia kiganja cha mkono wa kulia kujifuta uso kama vile alikuwa na jasho.
Ilifika mahali Faza Denis alilaza mikono yake yote kwenye meza kama aliyekuwa akitaka kumsikiliza kwa karibu Lina. Kuna kipindi Lina alisema maneno yaliyomfanya padri huyo kumwangalia Eg kama anayemuuliza ‘eti ni kweli?’ Eg naye akawa anasema ni kweli kwa kutingisha kichwa juu, chini.
“…hayo ndiyo yaliyotokea Faza Denis mpaka leo hii. Kama si huyu Eg ningekuwa mfu saa hizi. Nakuomba sana tena sana, natubu ni kosa lakini niombee kwa Mungu anisamehe na mume wangu pia anisemehe, nimekosa mnisamehe wote,” alimaliza Lina kisha padri akahema kwa nguvu…
“Lina!” aliita Faza Denis.
“Abee faza.”
“Pole sana. Najua mapito yako yote yalikuwa yamesimamiwa na shetani. Hukuwa na uwezo wa kumshinda kwa sababu ana nguvu sana kwako.
Wewe ukilala huombi, ukiamka huombi wala kumshukuru Mungu. Mara ya mwisho kukuona kanisani siku ile ulipokuwa umemsindikiza yule binti wa mzee Mchemsho aliyetaka cheti chake cha ubatizo hapa, sijakuona tena…
“Sasa kwa sababu umetubu ina maana umelijua kosa lako na Mungu anasema siku zote kwamba, kila mwenye kuomba msamaha asamewehe hata saba mara sabini kwa saa ishirini na nne.
“Nitampigia simu Semi ili akifika tu aje kuniona tuyaongee haya mambo.
Nitamwambia ulikuja kutubu kwangu. Ila kabla hamjaondoka niwaombee kidogo,” alisema Faza Denis huku akiweka mikono sawa kwa maombi. Alimshika kichwani Lina, akamwombea kwa dakika kama tatu kisha akampa mkono wa baraka aondoke.
***
Semi alikuwa amekaa kwenye kiti jirani kabisa na Faza Denis, Lina alikuwa pembeni, Eg naye pembeni lakini jirani na Lina, James hakuachwa nyuma maana aliitwa na faza huyo japokuwa walikuwa hawajuani lakini James aliitikia wito…
“Nadhani bwana James utakuwa unajua kisa cha kukuitia?” aliuliza padri huyo.
“Sikuambiwa, ila nilipokuta haya mazingira nimejua,” alijibu James…
“Asante sana kwa uelewa. Napenda vijana wenye uelewa kama wako…Semi unajua?”
“Na mimi kama huyu bwana James…”
“Nashukuru, lakini Lina na Eg mnajua kila kitu?”
“Ee tunajua kila kitu faza,” walijibu kwa pamoja wawili hao.
“Mimi sina maneno marefu, kesi iliyopo hapa ni ya ndoa mbili. Kesi hii imeletwa na Lina mwenyewe ambaye ndiye mhusika.
“James ni kweli mnamo mwezi mmoja uliopita ulifunga ndoa na Lina?”
“Ni kweli faza, tena ilikuwa ndoa halali kabisa kwa wakati ule.”
“Unaposema ilikuwa ndoa halali kabisa kwa wakati ule una maana gani?”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nina maana wakati nafunga naye ndoa sikujua kama ana mume mwingine kabla yangu. Ila baada ya kutokea lililotokea ndiyo nimejua kumbe nilikuwa siko sawasawa,” alisema James na kuashiria ukomavu wa busara.
“Vema sana, sasa nilichotaka ni hicho, kwamba bwana James atambue kuwa ndoa haikuwa yake, kaingilia. Lakini pia napenda nijua kwako Semi, uko tayari kumsamehe mkeo? Maana kwa upande wake ameshalijua kosa lake na ndiyo maana alikuja kutubu kwangu na nikamfanyia maombi.”
“Kusema kweli baba paroko nampenda sana mke wangu lakini alichokifanya sijakubaliana nacho, nahisi ni zaidi ya usaliti. Kwa hiyo kusema nimsamehe hapana,” alisema Semi kwa sauti ya upole kabisa.
Lina alianza kudondosha machozi huku akionekana uso umevimba. Eg yeye, moyoni alisema…
“Kama anachomoa si James ajichukulie mke tu!”
“Kwa hiyo unataka kuniambia kwamba haupo tayari kwa ndoa?” aliuliza padri.
“Ndiyo, sipo tayari,” Semi alisisitiza.
Padri, Eg, Lina na James wakaangaliana huku nyuso zao zikionesha mshangao mkubwa lakini Semi hakuonesha kushangazwa na mishangao yao.
Ukimya ulitawala kwa muda, padri ndiye akaukata kwa kuuliza…
“Kuna mwenye nyongeza?”
James alikataa kwa kutingisha kichwa, Eg akataka kusema lakini akaacha, Lina yeye ni machozi tu. Semi midomo ilimchezacheza kwa hasira.“Basi sawa, nifunge kikao. Lina, pole sana, mimi sina jinsi tena, mumeo kaamua hivyo,” alisema padri huku akisimama.
James alikuwa wa kwanza kuondoka baada ya kumpa mkono paroko huyo, Semi akasimama, naye akampa mkono paroko na kuondoka, Lina na Eg walibaki. Lina kilio kama kawa huku akisema…
“Faza, ina maana kweli sina ndoa tena?”
“Ndoa ipo, maana alichokiunganisha Mungu mwanadamu asikitengue, ila mumeo hataki kuishi na wewe. Mimi nilichojifunza kwake ni kwamba bado ana hasira ya tukio, ngoja atulie lakini na wewe mwombe sana Mungu,” alisema padri.
“Ni kweli kabisa Lina, shemeji bado hayuko sawa. Unajua jambo lenyewe zito,” alisema Eg huku akitangulia kuondoka mbele ya Lina ambaye bado alikuwa anamwaga machozi.
Je, unajua nini kilitokea hapo? Usikose kusoma kwenye Gazeti la Risasi, Jumatano ijayo.
Mama Kisamvu, mtoto Muhogo, ni shiida!
“
Samahani, sijui mwenzangu unaitwa nani?”
“Juliana Anold.”
“Unaishi wapi?”
“Ilala.”
“Ilala kubwa, Ilala gani?”
“We tambua ni Ilala,” alijibu Juliana huku akimwangalia kijana aliyekuwa mbele yake kwenye foleni ya benki akimuuliza.
“Oke, mimi naitwa Bitungu, naishi Temeke, lakini Ilala huwa nafikafika sana ndiyo maana nikataka kujua wewe unaishi Ilala gani?”
“Mimi naishi Ilala tu.”
“Oke, tuyaache. Una boifrendi?”
“Ninaye ndiyo.”
“Anaishi wapi?”
“Temeke.”
“Temeke ipi?”
“Temeke tu.”
“Mh! Oke, tuyaache hayo, naweza kupata namba ya simu?”
“Ya huyo boifrendi wangu au?”
“Ya kwako, boifrendi wako mimi ya nini?”
“Nitajie zako, nitakubip,” alisema Juliana kwa sauti yenye utulivu maana ni eneo la benki.
Bitungu alimtajia Juliana namba zake za simu, baada ya hapo wakaendelea kutembea kwenye foleni.
Juliana ndiye aliyeanza kuhudumiwa, alipotoka akampa mkono wa bai kijana huyo huku akichia tabasamu la ‘nakuacha’.
***
“Juli,” mama yake alimwita siku ya pili yake tangu mrembo huyo kukutana na Bitungu…
“Natoka mara moja, lakini nitachelewa kurudi.”
“Hivi mama, kila siku unapenda kutoka muda huu, kurudi unachelewa mpaka unagombana na baba huwa unakwendaga wapi kwani?”
“Wee mtoto, acha maswali yako. Unapatia wapi ubavu wa kuniuliza maswali kama hayo mimi mama yako?”
“Nisamehe mama.”
“Tena koma kabisa, usirudie tena.”
***
“Baby, unajua nilikumisi sana? Hatujaonana tangu lini?” mama Juliana alimwambia mpenzi wake ambaye ni dogodogo.
Lina na Eg walitoka, ilibidi Lina aende nyumbani kwa Eg kuishi huko ambapo baada ya wiki mbili alipokea barua kutoka mahakamani ikimtaka afike kwa tarehe aliyopangiwa bila kukosa akiwa analalamikiwa na James.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Lina alifika tarehe hiyo akiwa na Eg, wakamkuta James amejaa tele. Malalamiko ya James kwa Lina mahakamani hapo ni kuamua kufunga ndoa batili na James huku akijua ana mume halali na hivyo kumsababishia hasara na kumchanganya akili mwanaume huyo.
Lina alikana mashitaka na kesi inaendelea huku Semi naye akimfikisha kwenye mahakama nyingine akidai talaka, nako kesi bado inaendelea. Kesi zote zimemkalia vibaya Lina, anakabiliwa kutoa talaka kwa Semi na kuamriwa kulipa gharama alizozitoa James kwa ajili ya ndoa yao.
Ama kweli, kabla ya kutenda fikiri kwanza, ikibidi hata mara saba mpaka kumi au kushirikisha watu wenye hekima zaidi yako.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment