Search This Blog

Monday, October 24, 2022

UTAMU WA ZEGE - 5

 





    Chombezo : Utamu Wa Zege

    Sehemu Ya Tano (5)




    MAISHA yaliendelea na wakaamua kuanzisha biashara nyingine ya kuuza mayai. Biashara ambayo iliwaingizia kipato zaidi ya walichokuwa wakiingiza mwanzo. Hiyo iliwasaidia kufikiria mbali kwani waliamua kufanya makubwa zaidi. 
    Waliamua kuachana na biashara ya kuuza mayai kisha baada ya muda wakahamia Magomeni Mapipa na kufungua kibanda cha kuuzia chipsi.
    James alipata pigo kwani mjomba Mbiro alifariki baada ya kuugua kwa muda mfupi. James hakuweza kumsafirisha na hivyo alizikwa Dar es Salaam.
    James na Ramson waliendelea kuishi pamoja huku wakiendelea na biashara yao ya kuuza chipsi. Iliwasaidia sana kupata pesa kwa ajili ya kulipia chumba walichokuwa wakiishi pamoja na huduma nyingine. Mambo yalivyozidi kuwa mazuri kwao, Ramson alimshauri James wafungue kibanda sehemu tofauti ili kila mmoja aweze kupata wateja wengi. 
    James alikubaliana na Ramson. Ramson aliomba yeye ndo ahamie sehemu nyingine na amwache James. Walikubaliana na hivyo James aliendelea kuishi Magomeni na Ramson alihamia Mwenge. 
    Aliishi Mwenge kwani angekuwa karibu na wazazi wake ambao pia walimtegemea. Aliahidi kumtembelea James mara kwa mara na pia James liahidi kwenda kumtembelea.


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    *****
    James aliamka na kumsihi Jane warudi nyumbani. Walikuwa wameshatumia saa tatu kuzungumza. Jane alikuwa akimwangalia James kwa huzuni. Alimwonea huruma maisha yake. Alikumbuka alikumbuka alivyoishi na mama yake wa kambo.
    “Hapana James, tuendelee kustarehe huku….James unakumbuka bado mimi sjakuelezea maisha yangu. Ila ntakuelezea mpenzi.” Jane alianza kumwelezea James juu ya maisha yake hadi alipofika Dar es Salaam. Alimweleza juu ya wadogo zake Neema na Marry jinsi alivyowaacha na kuondoka bila kuagana nao.
    “Hakuna aliyeniona James. Nilitoroka jioni nkaenda kulala kituo cha basi. Sijui kama walintafuta. Lakini ninavyomwelewa yule mama. Sidhani. Roho yake haiwezi thubutu kunitafuta."
    “Jane, maisha yako yanasikitisha sana, hasa mambo ambayo alikufanyia mama yako mdogo. Na kwa nini baba yako hakukujali na wakati we ndo mtoto wake?”
    “James, unajua hakuwa anakaa sana nyumbani, ni mtu wa safari sana. Yule mwanamke alikuwa kamshikilia kiasi kwamba angesema chochote lazima angesikilizwa. Alinisema sana hadi baba kuniona mi kiburi. Na baada ya kuona hakuna anayenijali ndo nikaamua kukimbilia huku ndo n’kakutana na dada Sara siku ya kwanza.”
    “Umenikumbusha sana siku dada Sara alivyotaka kunigonga na gari.”
    “James niliogopa sana siku ile. Na kwa jinsi watu walivyokuwa wamejazana pale nikajua watatushambulia.”
    “Wakuwashambulia alikuwa ni mimi Jane. Na ndo maana niliongea haraka na nyie ili nisiwape nafasi ya kuongea. Sikuumia ndo maana.”
    “James, kwa nini mwanzo hukuikubali ile hela?”
    “Hapana, alikuwa tayari ameniomba msamaha. Je kama ningekufa, ningeipeleka wapi hiyo hela au ningeiona tena. Sikujali hela Jane, nilijali uhai na kusamehe ni jambo la muhimu sana kwetu kwani kuna leo na kesho. Na tayari aliwahi kuja kuniomba msamaha na hapohapo nilifarijika tofauti na mtu mwingine ambaye angekimbia. Ningekasirika sana na hata maumivu labda yangezidi.”
    “Haya James, wewe ni mwanamume unayejali sana, huna tamaa na una utu. Endelea hivyo hivyo mume wangu. Nakupenda sana.”
    “Kweli Jane?”
    “Ndiyo James.”
    Jane alimshika mabega James na kumbusu kisha kulala juu ya kifua chake wakiwa wamekaa katika mchanga wa ufukweni. Waliendelea na zoezi la kupeana mabusu motomoto yaliyowaweka sawa katika hatua ya kwanza na siku ya kwanza katika penzi lao. Jane alimwachia James amshike atakapo. James alifanya hivyo hadi pale alipoona Jane amekuwa mwepesi zaidi. hakujiweza.
    “Jane, tuache. Naona hujiwezi. Hapa si mahala pazuri.”
    ‘James. Nashindwa kuvumilia. Twende nyumbani.
    “Pumzika kwanza Jane. Shusha pumzi kwanza.”
    “Sawa, dakika chache alafu tunaondoka.”
    “Jane, sijazoea haya maisha….naona kama nina mzigo mkubwa nikifika nyumbani.,..wateja wangu watalalamika sana.” James alimwambia Jane huku akiwaza wateja wake ambao hawakuzoea kumkosa katika kibanda chake. Jane alicheka sana.
    “James, yaani we unawaza wateja….kwani unajua watakaa na njaa?”
    “James,” Jane alimwita James kwa sauti ya mahaba.
    “Mpenzi nakusikiliza,” James alimwangalia Jane usoni huku akimsikiliza kwa makini.
    “Napenda uachane na hiyo biashara ya kuuza Chipsi, najua ndiyo iliyokufikisha hapa lakini kwangu mi naona inatosha wewe kufanya tena.”
    “Jane…. Sasa unadhani mimi nitafanya nini nikiacha shughuli yangu. Si nitakaa bure tu. Sitaki kurudi nlikotoka. Tulihangaka sana na mjomba Mbiro.”
    “Simaanishi utakaa bure James, nataka uhamie kwenye biashara ninazofanya mimi.”
    “Kweli Jane?”
    “Ndiyo James.”
    “Jane, sasa itakuaje?”
    “Kwa nini James?”
    “Hapana, nimefikiria tu ni nani atakayekupikia zege usiku ukirudi,” kauli hiyo iliangua vicheko kwa wawili hao. Jane alimwahidi James kufanya naye pamoja katika duka lake na pia kumfungulia lingine ili asimamie.
    James, tuondoke. Sihitaji kuwa hapa sasa. Hali yangu sio nzuri.” Jane alisimama na kumshika James mikono. Walielekea hadi kituo cha Taxi na kupakia.
    “Magomeni Mapipa,” alisema Jane akimwelekeza dereva Taxi awapeleke Magomeni. 
    “Elfu kumi mpaka Magomeni.”
    “Elfu kumi?” alikuja juu James.
    “Tupeleke bana, James. Usijali. Mradi atufikishe nyumbani.
    Dereva Taxi alipiga moto gari. Walitumia nusu saa kufika magomeni. Muda huo hakukua na magari mengi na hivyo ilikuwa ni rahisi kufika.
    Saa mbili na nusu walikuwa wameshaingia ndani.
    James alishajua Jane alichokitaka. Alimbeba juu kitendo kilichomfanya Jane apige kelele kwani hakutarajia James angefanya vile. James alimshika vizuri. Akambwaga kitandani. Jane alifurahia uamuzi wa James. Alikumbuka alivyokataa asubuhi walivyokuwa bafuni. Hakuwa tayari. Sasa anafurahia uwepo wa James. Leo analala naye hadi asubuhi. James sasa alikuwa James. 
    Aliufuata mlango na kuufunga vizuri. Alirudi na kufungua dirisha. Aliweka pazia vizuri na kisha aliifuata swichi ya taa. Aliizima. Kukawa na giza sana. Aliiwasha tena. Alichukua kitambaa kilichokuwa juu ya sofa na kuifunika ile taa. Mwanga ulipungua na sasa kulikuwa na mwanga hafifu. 
    Sasa alimgeukia Jane. Jane alikuwa akimtazama James aliyekuwa akihangaika. Alicheka. Alisimama na kumfuata.
    Alichokifanya kilimstaajabisha James. Alimshika mikono na kuizungusha nyuma ya kiuno chake. Hapo alimpa James uwanja wa kujidai na maungo yake. Alianza kumchojoa blauzi aliyokuwa ameivaa. Kisha akamalizia na sketi fupi iliyokuwa imeremba umbo lake na kuonekana mtanashati. 
    Ikahamia kwa James. Jane alitoa fulana ya James na kuiweka kwenye sofa. Kazi ikawa moja t. miguno baada ya ashiki ilifanya chumba kitii amri ya binadamu wale. Chumba kilisimama. Kilijua kinatumika. 
    Saa mbili ziliwatosha kufurahia uhusiano wao bila kuchoka. Jane alimkumbatia James kwa nguvu na kumbusu. James alikuwa akiangalia sehemu ya shuka ambayo ilikuwa nyekundu. Zilikuwa ni damu. 
    James alitabasamu. Tabasamu lililomfanya Jane aangue kicheko cha furaha baada ya kuona James kakubali kuwa yeye ndiye alikuwa wa kwanza kumega. Alimsifia James kwa alichofanya.
    “Wewe ndiye mwanamume. Mwanamume niliyekuhitaji. Sitakaa nikuache James.”
    Kauli hiyo ilimfanya James afurahi. Hakuamini kwa kile kilichotokea baina yake na Jane, alimsifia sana Jane kwa kile alichompa. 
    Wote walifurahi. Jane aliweka mazingira ya kulala vizuri. Waliingia kuoga na kutoka tayari kulala wote wakiwa na furaha.


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    *****
    Asubuhi, James aliwahi kuamka. Alikumbuka kibanda chake cha chipsi. Haikuwa rahisi kwake kukiacha baada ya kumpata Jane japo alimwahidi atamsaidia. Alimkumbuka rafiki yake Michael ambaye walisaidiana wakati mwingine kuuza. Alitaka atoke ili amfuate aongee naye ili aje afanye kazi katika kibanda chake.
    James na Michael walijuana muda mrefu. Mara nyingi alikuwa akija na kumsaidia kuuza na kupika. James alijua itakua nafasi yake kufanya mengine na Jane wakati Michael akiendelea na shughuli za kibanda. 
    Alimwamsha Jane na kumweleza. Jane aliafiki na kumwahidi kuongeza mtaji katika kibanda chake na si kuacha kabisa.
    “Kweli, nimefurahi na wazo lako James. Itabidi iwe hivyo. Kwanza utakuwa umemsaidia rafiki yako.”
    “Sawa atafurahi sana.”
    “James, nataka tujenge nyumba.”
    “Nyumba?”
    “Ndiyo James, nilishanunua kiwanja. Nadhani ni wakati mzuri wa kuanza ujenzi,” James alimwangalia Jane huku akitabasamu. Alimshukuru sana Jane kwa kuyabadilisha maisha yake japo ni kwa siku moja kuwa naye.
    “James, wewe ni kama wanaume wengine. Kama walikuwa navyo. Hata wewe unastahili. Nmekupenda mimi na kila kitu changu ni haki yako. Tumia uwezavyo kama ulivyoweza kuutumia mwili wangu na kujisikia vizuri. Umenipa raha sana James.




    *****
    Maisha ya Jane na James yalibadilika sana. Watu hawakuamini kama James atamuoa Jane. Wengine walitaka kufanya kila namna wamtoe Jane kwa James. Hawakuamini kama anaweza kuishia mikononi mwa muuza chipsi, James. 
    Ni msimamo wa Jane ndiyo uliompa tumaini la kufunga ndoa James. Kila mmoja alijitahidi kumfanya mwenzake ajisikia na aringe awapo na mwenza wake. Jane alimwonyesha mahaba yote James akiamini ndiye yeye pekee atakayefunga naye ndoa.
    “Haloo, nani mwenzangu?” simu ya Jane iliita na kuipokea. Aliyeongea naye alikuwa ni mmoja wa watu ambao walikuwa wakimfatilia kwa muda mrefu sana kwa lengo la kumtongoza lakini aliambulia patupu kwani kwa kipindi chote cha jitihada zake hakuambulia hata busu. 
    “We nani?”
    “Ina maana Jane leo umenisahau, mi Austin…Austin Michael.”
    “Ahh, mambo vipi Austin, nimkukumbuka, uliwahi kunileta nyumbani mara kadhaa na gari lako.”
    “Ni kweli, nahitaji kuonana na wewe.”
    “Mimi? Kuna nini kwani?”
    “Jane, ni wazi nilishakuambia kwamba nakuhitaji… napenda tuonane tuongelee hilo suala tena.”
    “Tafadhali, siwezi kuja huko na kuhusu mapenzi tayari ninaye mtu na sihitaji mwingine. Naomba tuelewane. Samahani sana,” Jane alimaliza kuongea na kukata simu. James alielewa usumbufu anaoupata Jane kwa wanaume. Hakujali sana kwani alijua Jane alimpenda kwa dhati.
    Kila aliyewaona alijiuliza imekuaje, labda James kamwekea dawa Jane kwenye chipsi. Labda ni zali limemwangukia James. Iweje Jane mtoto mzuri atembee na muuza chipsi? Wenye uwezo wa kifedha na matajiri waliokuwa wakihangaisha magari yao kumpa lifti Jane waliambulia salamu tu na kumfungulia milango ya gari. Sasa wengi wao walianza kumtupia lawama na kumwona tapeli.
    Kwa Jane haikumuumiza kichwa na hivyo aliendelea kujiimarisha na kumpa mapenzi ya kweli James. Alimpenda sana James. 


    *****
    Jane na James waliamua kupanga mipango ya ndoa. Jane alikumbuka sana nyumbani kwao na hivyo aliamua kuondoka ili akawape taarifa juu ya maisha yake na mipango yake ya ndoa. Hakupenda aitelekeze familia yake japo yenyewe ilimtupa kwa mateso aliyoyapata kwa mama yake na kuamua kukimbia.
    Akiwa na usafiri wake binafsI gari aina ya Rav 4, alifika nyumbani Dodoma. Hakuna aliyemtambua kwamba ni Jane. Aliwaona wadogo zake Marry na Neema ambao hawakumtambua kwani alibadilika sana. Aliwaacha wakiwa wadogo. Yeye aliwakumbuka kwani sura zao zilifanana na mama yao. Jane yeye alifanana na baba yake. 
    “Neema na Marry,” Jane aliita.
    “Abee,” waliitikia huku wakimwangalia sana Jane.
    “Mi dada yenu Jane, mnanikumbuka.”
    “Haah, Dada Jane…. Mamaaa, dada Jane amekuja,” Neema alimtambua na kuanza kupiga kelele kumwita mama yake. Mama alitoka na kumwona Jane.
    “Jane…aliita kwa sauti ya mshangao.
    “Shikamoo mama,’ hapo hapo mama yake wa kambo alisahau unyama wote aliomtendea Jane na kumfuata. Alimkumbatia kwa nguvu na kwa muda mrefu. Hakuamini kama siku moja Jane atarejea nyumbani. Hata baba yake Jane alipojua kwamba Jane amerejea nyumbani aliahirisha safari yake ya kwenda Zambia na kurudi nyumbani. Gari alikabidhi kwa dereva mwingine ambaye alielekea nalo Zambia.
    Jane alifurahi kumwona baba ake ambaye alionekana mwenye sura ya aibu aliyeshindwa kuongea na Jane pindi alipomwona. Hakuweza hata kutowa lawama kwa Jane wala kumkaripia kwa nini aliondoka nyumbani.
    “Samahani sana baba na mama,” Jane alikuwa wa kwanza kuomba msamaha kwa baba yake kwa kuondoka nyumbani.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    ‘Nilifanya hivyo kwa ajili ya maisha yan….” 
    “Hapana Jane… ni sisi utusamehe,” mama alimkatisha Jane kabla hajamaliza kuongea. Tulikutafuta sana ila hatukuweza kukupata. Tunamshukuru Mungu umerudi nyumbani na hapa ni kwenu. Karibu sana mwanangu. Sikukutendea haki kipindi ukiwa mdogo, kun a wakati nilikukosa sana katika nafsi yangu na kuumia sana kwa kuondoka kwako. Hata wadogo zako hadi walikusahau kwa kuwa ulikaa muda mrefu sana bila kurudi nyumbani. Mimi na baba yako tuligombana sana kwa sababu yako baada ya kuondoka lakini mwishowe tuliamua kumwachia Mungu… nilimwambia baba ako ipo siku utarudi nyumbani. Nilikosa mwanangu naomba unisamehe.”
    Jane machozi yalimtiririka kwa kauli za mama yake wa kambo. Aliwafuata Marry na Neema na kuwakumbatia na kuwaomba msamaha kwa kuondoka na kuwaacha. Jane alitaka muda ili aongee na baba yake, dhamira kubwa ilikuwa ni kumweleza juu ya maisha yake na hasa kufunga ndoa na James baada ya kumalizika kwa kipindi kifupi cha majonzi kilichotawala nyumba ya mzee Amos.


    *****
    Baada ya mipango kukamilika Jane alirudi Dar es Salaam na kumjulisha James juu ya nyumbani kwao na mipango inavyokwenda. James alifurahia sana. Ndoa ilifungwa nyumbani kwa kina Jane Dodoma. Jane alibadilisha maisha ya nyumbani kwao na kuwachukua wadogo zake Marry na Neema na kuishi nao nyumbani kwake. Aliendelea kuwasomesha na kuwatunza vizuri. 
    James alionekana akiwa na mawazo sana. Hali hiyo ilimfanya Jane amfuate na kumuuliza kulikoni. Alimsogelea James ambaye alikuwa akiitazama nyumba yao pamoja na mazingira ya nyumba yao. Alimwangalia Jane akajitazama tena nay eye kwa jinsi alivyoonekana nadhifu. Hakuamini bado maisha yalivyombadilikia…
    “Ni mimi kweli…..hapana… muuza chipsi mimi?... usawa aliokuwa amegeukia, Jane asingejua kwamba James alikuwa mwenye mawazo ya kutokuamini maisha yake kuwa ya juu hivyo. Alimsogelea taratibu na kuzunguka kwa mbele yake. Macho ya James hayakuwa ya kawaida. Ni mwanamume lakini uanaume aliuweka pembeni na kutiririkwa na achozi… siyo ya furaha tu bali ya kutokuamini juu ya mabadiliko aliyoyapata kutokana na penzi lake kwa Jane na penzi la Jane kwake. 
    “James usifanye hivyo…nini tatizo mpenzi?” Jane aliuliza huku akiwa na huzuni mwingi moyoni.
    “Nakupenda sana Jane. Maisha yangu umeyabadilisha wewe, ni kitu ambacho nakushukuru sana. Siamini kama ni mimi yule aliyekuwa anauza chipsi hadi saa tano za usiku leo maisha yangu yako hivi.”
    “James….hata mimi nakushukuru wewe kwani kama siyo chipsi mayai zako nisingependeza vile kukuvutia wewe hadi ukakubali kuwa na mimi, nakupenda sana James, wewe ndo wangu wa milele.” Alisema Jane.
    Ulikuwa ni usiku ambao ulijawa na furaha hasa baada ya kuwa tayari ni mke na mume. Ni ndoto ya kila mmoja ambayo imetimia. 
    Mume wangu James,” aliita Jane huku akimfuata James ambaye alikuwa amelala. Alifunua shuka na kuingia. Alimkumbatia James na hapo ukawa ni ufunguo mwingine wa kile walichotaka kukifanikisha wakiwa pamoja. 
    Baada ya miezi tisa ya kubeba ujauzito Jane alifanikiwa kupata mtoto mzuri wa kike ambaye alimpa jina la Janeth akimkumbuka mama yake mzazi ambaye alifariki baada ya yeye kuzaliwa na kuishi naye kwa miezi miwili tu. 
    Sara na Sebastian pamoja na mtoto wao ambaye walimpa jina la Jane, walifika na kumpongeza pamoja na James. Kwa kutoa pongezi zake na kukumbuka tukio la kumgonga na gari James. Sara alimpa zawadi ya gari. 
    “James, nakupa hii kama ukumbusho wa lile tukio. Nilijisikia vizuri sana baada ya kunisamehe na kuchukulia ilikuwa ni jambo dogo japo ni hatari na hapo ndipo ukanifanya niwe mwangalifu zaidi. pokea funguo hizi.”
    “Nashukuru sana dada Sara. Siamini haya yote. Mimi James…Muuza chipsi,” wote walicheka.
    “Maisha hubadilika James. Hakuna asiyebadilika…. Nawatakia maisha mema pamoja na mdogo wangu Jane.” 
    “Tunashukuru sana dada Sara.” Jane na James walifurahi sana. 
    Baada ya kujumuika katika chakula cha jioni, Sara na Sebastian waliwaaga kuondoka
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/


    MWISHO


0 comments:

Post a Comment

Blog