Search This Blog

Monday, October 24, 2022

UTAMU WA ZEGE - 4

 





    Chombezo : Utamu Wa Zege

    Sehemu Ya Nne (4)


    SEBASTIAN alifanya kile alichokijua. Alimshika kila mahali Sara ambaye na yeye alirudisha mapigo kwa ufundi wake. Aliutumia vizuri ulimi wake na kinywa katika kuiburudisha nafsi ya Sebastian na kumlegeza kwa maneno matamu. Wote walifurahia siku hiyo. Ya kwanza kukutana miili yao kama wapenzi. 


    Sara alifurahia zaidi. Upole wa Sebastian alihisi haupo tena. Hakuwa Sebastian yule aliyemzoea. Si mwongeaji sana bali wa vitendo. Kweli alitenda. Akatenda vile alivyokaribishwa atende. Sara alifurahi sana.
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    *****
    Jumamosi jioni Sara alirudi nyumbani akiwa anaongozana na Sebastian. Siku hiyo Jane hakutoka zaidi ya kubaki nyumbani kwa ajili ya maandalizi ya mgeni wa Sara. Alitamani sana kumwona shemeji yake. 


    “Karibu shemu,” Jane alimkaribisha Sebastian ndani kwa furaha wakati Sara akitoa mizigo ndani ya gari. Sebastian alionekana nadhifu sana machoni mwa Jane. Jane alifurahia sana ujio wa shemeji yake.


    “Sara alimtambulisha Sebastian kwa Jane. Baadaye alimtambulisha Jane kwa Sebastian. Utambulisho kwa Jane ulikuwa ni sawa na kukumbushia kwani tayari Jane alishajua nini kinachoendelea.


    Jane aliwaacha sebuleni na yeye alikwenda jikoni kumalizia shughuli zake. Sara na Sebastian walipanga mikakati ya kufunga ndo mapema ili waweze kuishi pamoja. Sara alitaka Sebastian ahamie kwake ili wakae katika nyumba yake na alifikiria kumpangishia chumba Jane ili aweze kujifunza maisha akiwa peke yake. Suala hilo alipanga kumwambia. Alijua Jane atafurahia. 


    Baada ya chakula cha jioni, Sara alimsindikiza Sebastian na kurudi. Jane alikuwa ametulia juu ya sofa akitazama TV huku akinywa juice.


    Alirudi akiwa na uso wa furaha, furaha ambayo hata Jane aliitambua na kuiona wazi. Alipita huku akimwangalia Jane na kutabasamu huku akielekea chumbani kwake.


    Alikumbuka na kurudi tena. Alitaka kuongea na Jane kuhusu walichopanga na Sebastiani.


    “Mdogo wangu. Kuna kitu nataka nikuambie, najua utafurahi.”


    “Niambie tu dada Sara,” Jane aliitika kwa furaha na hamu ya kutaka kujua Sara alichotaka kumwambia.


    “Nafkiria nikupangishie chumba. Nataka ujitegemee na kujifunza mengi ukiwa mwenyewe baada ya mimi kuolewa. Ila si kuondoka kabisa. Wikiend utakuwa unakuja kututembelea na tutakuwa tunatoka pamoja. “


    “Sawa dada Sara, mi nakusikiliza wewe. Na pia ni vizuri kuwapa nafasi wapendanao.” Jane alisema huku akicheka. Sara aliamka na kuelekea chumbani kwake. Alikuwa akicheka huku akiwa ni mwenye furaha sana.


    “Ndiyo mpaka unasahau kuniaga dada Sara?” Sara alicheka sana na kurudi hatua mbili nyuma kabla hajaingia chumbani kwake.


    “Jamaaani, yaani mdogo wangu nisamehe, nahisi hii siyo furaha ni kuchanganyikiwa, Good night,” Sara alimuaga Jane huku akitabasamu na kuingia ndani. Alimwacha Jane akicheka tu. Jane naye alizima Tv na kuingia chumbani kwake kwenda kulala.


    *****
    Baada ya mwezi mmoja Sara na Sebastian walifunga ndoa. Harusi ilifana kwelikweli. Jane alifurahia sana. wakati huo alikuwa amehamia Magomeni na kuanza maisha yake. Aliwapisha wanandoa wafaidi ndoa yao. Sara alitamani sana aendelee kuishi naye lakini kwa Jane aliona ni bora kuwapisha ili na yeye akaanze maisha yake. 
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Aliwaaga vizuri siku ya kuondoka na wote walishirikiana kuhamisha mizigo ya Jane ikiwa ni pamoja na kununua samani za ndani ambazo Sara alizigharimikia akisaidiana na Sebastian. Jane alifurahi sana na kuwashukuru wote. Alipata nyumba maeneo ya Magomeni Mapipa.


    Kila wikiendi alienda nyumbani kwa Sara kwa ajili ya kujumuika pamoja nao. Siku moja moja walitoka pamoja kwa ajili ya matembezi. 


    Mtaani aliipokuwa akiishi, alipata usumbufu sana kutoka kwa wanaume. Ni kutokana na alivyo. Wengi walimtamani pasipo na uhakika wa kuambulia hata jibu. Magari yalipishana sana kila mmoja akijaribu bahati yake.


    Kwake hakujali kwani sifa za wanaume alizifahamu na hivyo hakuhitaji kuusumbua moyo wake. Wakati mwingine aliwacheka wale waliojidai kuja kwa moyo wote na kuwaona kwamba wamekosea njia.


    Wengine walidiriki hata kumtukana baada ya kuambulia patupu. Hakuumia kwani alijua ni maneno ya mkosaji. Alitaka kuwa na msimamo. Alisimama na msimamo wake. 


    Lifti za magari ya kifahari yaliyokuwa yakielekea mjini hazikupita mbali. James alikuwa akihesabu tu magari yanayomchukua Jane, mteja wake mkubwa sana wa chipsi mayai hasa usiku pindi Jane anaporudi akiwa na njaa. 




    *****
    James alikumbuka siku ambayo alimuuliza Jane swali na kuahidiwa kuwa ataambiwa. Ni siku kama hiyo ambapo Jane alionekana tena mnyonge akiwa amesimama nje ya lango la kuingilia uani huku akimtazama James ambaye alikuwa akiendelea na shughuli zake huku wakati mwingine akimwangalia Jane. Ni Jane ndiye aliyekuwa wa kwanza kumfuata James. Hakutaka kuumia zaidi.


    “James, kijana mtaratibu, anayejali, mwaminifu na anayejua kujituma….itakuaje siku moja kama atakuwa mume wangu wa ndoa. Nitafanyaje ili nimpate James. James… James, sidhani kama ulinidanganya kwamba una mwanamke mwingine…lakini mbona sijawahi kukuona naye? Leo sitaficha ukweli juu ya moyo wangu… nakupenda sana James. Japo watu watatushangaa na kujiuliza maswali, sitojali. Kama ukinikubalia ombi langu, nitajiona nimepata kile nilichokuwa nakitamani toka nijue nini mapenzi na nini kupendwa,” Jane alikuwa akiwaza huku akimfuata James ambaye alikuwa amesimama akimwangalia Jane akija.


    Ilikuwa ni asubuhi sana James akitayarisha vyombo kwa ajili ya kufungua biashara yake. Jane bila kujali alimfikia James na kumshika mikono.


    “Nitakuchafua Jane, mikono yangu michafu,” James aliongea pasipo kujua ni nini kinachoendelea kwa Jane. 
    “James,” aliita Jane.


    “Dada Jane mbona unaonekana kama kuna kitu kinakutatiza, ni nini? Tafadhali dada Jane, kuna nini?” Jane alimkumbatia kwa nguvu sana James.


    “James…. Nakupenda sana,” Jane alimtamkia James neno ambalo James hakuamini.James alibaki akimwangalia Jane. Alikuwa kama hamwoni, midomo ilianza kutetemeka kwa woga. Jane machozi yalimtoka huku akilia kwa sauti ya kwikwi. Alimkumbatia tena James.
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    “Tafadhali James…. Nifanye nijisikie mwanamke kweli. Sihitaji mwanamume mwingine zaidi yako. Nakuambia hivi kwa sababu nakuheshimu sana na najua unaniheshimu pia. Usifikirie lingine lolote zaidi ya kukubali ombi langu. Nakupenda sana James,” Jane alijibandua kwenye mwili wa James ambaye alikuwa akitokwa na jasho huku asijue aongee nini. Jane aliondoka na kumwacha James akiwa hana la kusema. Aliondoka kwa kukimbia na kuelekea ndani kwake. Ilikuwa ni asubuhi sana na hivyo hakukuwa na watu katika eneo la nyumba yao. 


    James alipatwa na woga sana baada ya kumwona Jane akikimbia na kuelekea ndani. Aliamua kumfuata Jane ili akajue kilichomsibu zaidi. Alifika hadi mlangoni kwa Jane na kugonga mlango. Jane alikuwa akilia sana kwa kwikwi. James aliingia ndani ili kumbembeleza Jane anyamaze. 


    “Dada Jane, kuna nini?” wakati huo Jane alikuwa bado anaendelea kulia.


    “Tafadhali dada Jane.,” James alimshika Jane na kumwamsha. Alimweka sawa na Jane alikaa huku akitokwa na machozi. 


    “James, siamini wakati nakuambia maneno yangu hukuweza kunijibu chochote. Kama hunipendi naomba uniambie James.”


    “Hapana dada Jane, sikuelewa nikujibu vipi. Dada Jane, sikuwa nimejitayarisha kwa maneno uloniambia. Naomba kwanza uwe sawa alafu tutayaongea vizuri,” James alimpooza Jane ili waweze kuongea vizuri. Jane alimshika mikono James ambaye na yeye alikubali Jane afanye hivyo. 


    “Dada Jane, nadhani tutaongea baada ya mi kumaliza kazi zangu. Tafadhali, tufanye jioni,” James alisimama na kumuaga Jane ambaye alionekana kukubali kwa shingo upande. Hakuridhika na alichosema James. Hakutaka kwenda kokote zaidi ya kuwa na James siku hiyo. James alitoka na kwenda kuendelea n shughuli zake. 


    Jane hakukubali. “Hapana James, siwezi, leo hutofanya chochote, kama hela yako nitakupa ya siku nzima. Leo nataka kuwa na wewe. Si kitu….tutaenda sehemu kuongea. Siwezi kuwa mwenyewe na wewe upo,” Jane alijisemea mwenyewe huku akifunga mlango na kutoka kumfuata tena James.


    “James, sikubaliani na maneno yako,” sauti ya Jane ilimshtua sana James ambaye alikuwa ameegemea kibanda chake asijue la kufanya huku akiwaza yale aliyoambiwa na Jane.


    “James, kama ni kukulipa ntakulipa gharama zote za leo. Ninachokuomba ni mi na wewe tutoke leo. Nina mengi sana ya kuongea na wewe James. Naomba ufanye hivyo. Sitakuruhusu kupika leo James.”


    James akuwa na ajizi. Ilibidi afanye vile alivyoambiwa na Jane kama ombi. Alicheka na kumfinya shavuni Jane na wote wakakubaliana watatoka. Jane haraka alianza kuchukua vitu vya James na kuviingiza ndani. 


    Hakujali watu waliokuwa wakipita na kuwatizama. James alibaki akimshangaa sana Jane. Hapo ndipo alipogundua kwamba Jane anampenda sana. 


    “Siwezi nikaipoteza hii bahati,” aliwaza James.




    *****
    Ilikuwa ni siku nzuri sana kwa Jane. Alifurahia kutoka na James. Alimkaribisha kwanza ndani baada ya kuweka vitu vya James. Alifungua kabati na kutoa nguo ambazo alikuwa amemnunulia James. James alishangaa kuziona zile nguo.


    “Za nani?” alihoji James.


    “Ni za kwako James, n’likununulia nkaziweka. Napenda uzivae leo.”
    Jane alimshika James mkono na kumvuta hadi bafuni. Walioga pamoja huku Jane akifanya utundu wake. Alitaka kumwonyesha James kwamba alimpenda sana na angefanya chochote.


    “Hapana James, sio leo. James alikuwa tayari kutekeleza lile lipendwalo na wanaume pale wanapokutana na wanawake.


    “Basi usinfanyie hivyo, sitaweza kuvumilia. Taratibu.” James alimsihi Jane asiendelee kufanya alichokuwa akifanya. Jane alitulia huku akicheka taratibu. james alitoka kule bafuni. Alimwacha Jane akimalizia kuoga. Alivaa zile nguo na kukaa juu ya kiti akimsubiri Jane atoke.
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Jane alitoka. Alitoka mtupu. Hakudiriki kumwogopa James kwa chochote kwani alijua tayari ni wake. Alitembea hadi alipokuwa amekaa James. Alimpa taulo na kumwomba amfute maji. James alifanya hivyo huku akipitiisha mikono yake katika maungo ya Jane. 
    Alimaliza na kumpa taulo. Jane aliifuata meza na kuchukua mafuta. Alimpa tena James. 


    “Nipake mafuta,” James alicheka kidogo, aliona Jane amejawa na vituko. Alifanya kama Jane alivyotaka. Pumzi zilikuwa zikimtoka sana James. Alishindwa kujizuia. Alimnyanyua Jane na kumpakata.


    “Jane, hii ni mara yangu ya kwanza kuona mwili wa mwanamke. Mwili wako ndio wa kwanza machoni mwangu. 
    “Hata mimi James. Na pia, sijawahi kutumika. Naomba uwe wa kwanza kuzindua.”


    “Kuzindua?”


    “James, huelewi. Sijawahi kulala na mwanamume. Wewe ndo utakuwa wa kwanza.”


    “Jane, inamaana…james alishindwa kuendelea. Hakuamini aliyokuwa akiyaona kwa Jane. 


    “Jane, usintanie. Sikuamini. Wewe si mtu wa kunidanganya mimi.”


    “James,” aliita Jane. Alinyanyuka na kumfata alikokaa. Alimkumbatia na kumwambia.


    “James, naona hutaniamini. Lakini nakuhakikishia utaniamini.
    Jane na James walitoka pamoja. Jane alimpigia simu Sara kumjulisha kwamba wikiendi hiyo asingeweza kwenda kwake kwani alikuwa na mgeni. Kwa Sara haikuwa tabu kwani alielewa Jane naye ana marafiki. 


    Jane alifurahia sana siku hiyo kwa kuwa na James. Wateja wa James wengi walijiuliza kulikoni leo.


    “James anaumwa au vipi, kapatwa na tatizo gani kwani?” mmoja wa wateja wake alisema. 


    “Nimemwona na yule dada anayeishi naye huku ndani. James kaotea leo mtoto, chipsi ndo hauzi tena.”


    “Hee! Kupata mwanamke ndo aache kuuza chipsi….makubwa,” mama mmoja aliyekuwa na mtoto wake mgongoni alishangazwa na kauli ya yule mteja wa James.


    “Jamani msifuate ya watu, auze asiuze kwani nyie mtamzuia?Fanyeni mambo yenu. Kama kapata mwanamke au ni dada yake, hayawahusu. Kila mmoja anayake. Siyo kuwekeana vikao kumjadili James na mdada wa watu,” Omary ambaye ni fundi viatu karibu na kibanda cha James aliwawakia kuacha kujadili mambo yasiyowahusu. 


    Wote walibaki kimya. Omary aliwatazama kwa mshangao kwa kutoelewa kinachowafanya wajadili mambo ambayo si yao. Kinamama walishajazana na kujua kulikoni. 


    Wengi hawakumpenda Jane na hivyo walitaka kujua ni nini kinachoendelea baina ya James na Jane kwa kuhofia labda Jane anataka kumchafua James kutokana na tabia ya Jane ya kuletwa na magari ya kila aina na kupelekwa kazini. 


    Walitamani siku moja afanye kosa ili wamshambulie. Kauli ya Omary fundi viatu iliwakatisha tamaa. Wote waligeuka kufuata mambo yao.


    *****
    Jane na James walikuwa wanakula raha ufukweni mwa Bahari ya Hindi. Jane ndiye aliyekuwa na furaha wakati wote. James alijiona mgeni kwenye mapenzi. Hakujua aongee nini, wakati wote alikuwa akimsikiliza Jane ambaye alionekana akimwelekeza James kila kitu.


    “James, tuyaache ya nyumbani… hujawahi kweli kuwa na mpenzi?” alihoji Jane.


    “Kweli dada Jane. Sijawahi. Na sijawahi kuja huku na mtu yeyote.”


    “Sitaki tena hilo neno dada, mi ni mpenzi wako James.”


    “Samahani mpenzi. Hilo ndo jina ambalo nilizoea kukuita pindi nikuonapo. Ntajaribu kulisahau.Sawa da….samahani, sawa mpenzi.” Jane alicheka sana.
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    “Usijali, utalizoea tu James. Twende tukakae pale karibu na wanapouza urojo tuongee mengi juu yetu mpenzi.
    Walikaa karibu na muuza urojo. Kila mtu aliagiza na kuanza kunywa taratibu huku wakiendelea na mazungumzo.


    Alikuwa ni James wa kwanza kumwelezea Jane juu ya maisha yake tangu akiwa mdogo. Mazingira aliyoishi mpaka kufikia alipo.


    *****
    James ni mzaliwa wa Tabora. Kabila lake ni Mnyamwezi. Miaka ishirini na sita iliyopita ndiyo alizaliwa. Alikuwa ni mweupe kiasi na aliyeonekana kivutio kwa baadhi ya wanawake walioishi naye mtaa mmoja. Pengine ni kwa vile James hakupenda kufuata wanawake na hakujihusisha nao hata walipoonyesha tamaa ya kuwa na James. 


    Ni wateja wake wengi waliojaribu hata kumuhonga lakini ustaarabu wake ulifanikisha lengo lake la kufanya kazi yake kwa bidii pasipokujali watu.


    Dar es Salaam alikuja akiwa na miaka saba. Alikuwa akiishi na mjomba wake Mbiro katika nyumba ambayo anaishi mpaka sasa. Wazazi wake wote walifariki kwa ugonjwa wa Ukimwi wakati James akizaliwa. 


    Kwa bahati nzuri James yeye hakupata maambukizi kutoka kwa mama yake na hivyo alizaliwa salama. 
    Hakuweza kusoma hata darasa moja.Baada ya kifo cha wazazi wake. James alilelewa na shangazi na mjomba. Kwa bahati mbaya shangazi yake naye alifariki kwa ajali baada ya basi kupinduka. 


    Mjomba wake James alimchukua James na kuhamia Dar es Salaam. Hakuwa na uwezo wa kufanya kazi baada ya kubakiwa na mguu mmoja kutokana na kukatwa mguu wake mmoja baada ya kuugua ugonjwa wa ajabu ambao ulipelekea kukatwa. Huko Dar es Salaam Mbira aliishi kwa kuombaomba. Walikuwa wakila na kulala popote. James hakupenda maisha aliyoishi na mjomba wake. Alitamni sana kumsaidia. 


    Kazi yao ya kuomba waliifanya kwa muda wa miaka miwili. James alijiunga na kikundi cha vijana wenzake cha kuuza maji katika vimfuko. Alikutana na Ramson ambaye alikuwa rafiki yake. Waliuza maji pamoja na baadaye waliamua kuchanga hela zao kwa ajili ya kupangisha chumba. 


    Walifanya hivyo kwa ajili ya mjomba wake James ambaye alikuwa hana uwezo wa kutembea na hakupata msaada wa kiti cha magurudumu. Walipata chumba Kinondoni na hivyo mjomba wake alipata pa kupumzikia. Kila siku James na Ramson walikuwa wakiondoka asubuhi na kurudi usiku.


    Maisha yaliendelea na wakaamua kuanzisha biashara nyingine ya kuuza mayai. Biashara ambayo iliwaingizia kipato zaidi ya walichokuwa wakiingiza mwanzo.Hiyo iliwasaidia kufikiria mbali kwani waliamua kufanya makubwa zaidi. 


    Waliamua kuachana na biashara ya kuuza mayai kisha baada ya muda wakahamia Magomeni Mapipa na kufungua kibanda cha kuuzia chipsi.


    James alipata pigo kwani mjomba Mbiro alifariki baada ya kuugua kwa muda mfupi. James hakuweza kumsafirisha na hivyo alizikwa Dar es Salaam.


    James na Ramson waliendelea kuishi pamoja huku wakiendelea na biashara yao ya kuuza chipsi. Iliwasaidia sana kupata pesa kwa ajili ya kulipia chumba walichokuwa wakiishi pamoja na huduma nyingine. Mambo yalivyozidi kuwa mazuri kwao, Ramson alimshauri James wafungue kibanda sehemu tofauti ili kila mmoja aweze kupata wateja wengi. 


    James alikubaliana na Ramson. Ramson aliomba yeye ndo ahamie sehemu nyingine na amwache James. Walikubaliana na hivyo James aliendelea kuishi Magomeni na Ramson alihamia Mwenge. 


    Aliishi mwenge kwani angekuwa karibu na wazazi wake ambao pia walimtegemea. Aliahidi kumtembelea James mara kwa mara na pia James liahidi kwenda kumtembelea.


    PAMOJA NA MANENO YA MAJIRANI…..


    JAMES ANAKUBALI OMBI LA JANE. JANE ANAFURAHI NA KUTOKA PAMOJA. 
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    ANAMWELEZEA JANE MAISHA YAKE YA NYUMA….


    JE JANE NA JAMES WATAFAIDI PENZI LAO AU KUNA VIKWAZO VYA MAJIRANI


    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog