Chombezo : Nataka Kuzaa
Sehemu Ya Tatu (3)
“Mambo.”
“Poa, mzima?”
“Mzima sijui wewe.”
“Naona umerudi mama.”
“Eeee nimerudi.”
“Hakuna shida karibu sana.”
“Ahsante.”
Frank alionesha ucheshi wa hali ya juu nilimpenda, alizidi kunivutia kila siku.
“Aaah ngoja niwaache.” Innocent alisema.
“Aaah mwanangu unaenda wapi sasa na hatujamaliza?” “Nitakuja baadae.” Innocent alisema.
Alinyanyuka akanikonyeza akaachia kicheko na kisha kuondoka, nilicheka tu.
Tulibaki peke yetu.
“Frank nina tatizo.”
“Tatizo gani tena mimi naweza kukusaidia?” Nilicheka kidogo.
“Unafikiri msaada wa aina gani hata mawazo yako ni ya muhimu tena zaidi ya sana ndiyo ninayohitaji, mimi na Melania tuna ugomvi na sijui kwa nini.” Alikuna kichwa na kisha akakikumbatia kichwa chake kwa mikono yake.
“Huyu msichana sijui ana matatizo gani, mbona anakuwa na mambo ya ajabu, kwanza kwanini ananichukia mimi, mimi nimefanya nini.” Aliongea kwa sauti yake nzuri ya kiume.
“Sijui.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Aaah nashindwa kuelewa kabisa, hivyo ndiyo mlikuwa hivyo tangu mwanzo.” “Mimi na yeye tumejuana tu hapa chuoni nashangaa amebadilika wala hakuwa vile kila mtu anashangaa.”
“Ok hamna shida, mimi niko tayari kukabiliana naye wala hanitishi.” “We unasema, mimi nakaa naye chumba kimoja unafikiri nitaishije.” “Akikusumbua njoo kaa kwangu.”
Nilicheka sana.
“Frank acha utani bwana.”
“Mimi nakuambia kweli.”
“Frank nataka tutoke.” Nilimuambia.
“Twende wapi tena.”
“Nataka twende mlimani City.”
“Sijawahi kufika hilo eneo.”
“Twende, jiandae tuondoke.”
“Nijiandae nini sasa na nipo tayari.”
Nilishindwa kujizuia nikajikuta nimecheka, alikuwa amevaa tshirt kubwa refu ambalo lilikuwa limekaribia kumfikia magotini lilikuwa jeusi na lilikuwa na nembo flani ivi ambayo nilishindwa kuielewa kifuani. Na chini alikuwa amevaa suruali ya kitambaa ambayo haikumfika kwenye vifundo vya mguu.
“Badilisha bwana.”
“Au nivae zile za sikukuu.”
“Hahaha Frank jamani sasa si zitapauka.”
Alicheka na kisha alibadili na kuvaa nguo ambazo zilonekana kumpendeza. Tuliondoka na kuelekea Mlimani City, nilipitia Bank na kuchukua hela kutoka kwenye akaunti yetu. Mama hakupenda nitumie hela kwenye akaunti yangu binafsi hivyo alifungua akaunti ya familia ambayo kila mtu alikuwa akichukua hela mimi, baba na yeye.
Aliniambia bado nilikuwa mdogo sana kumiliki pesa zangu mwenyewe hata hivyo aliniambia kwamba akaunti yangu ipo tayari na kila mara alikuwa akiweka pesa kwa ajili ya matumizi yangu ya baadae.
Nilichukua kama kiasi cha laki sita na kisha kuelekea Mlimani City tukiwa na Frank.
Nilipanga kwenda kumnunulia baadhi ya nguo ambazo angekuwa anazivaa hapo chuoni.
Tulizunguka maduka mbalimbali kuchagua nguo ambazo zilimpendeza nilihakikisha kwamba atakapovaa hizo nguo kila mtu ageuze macho yake kumtazama.
“Utapendeza kweli ila usiibwe tu.” Frank aliinua macho yake akaniangalia. “Naanzaje.”
Nilicheka tu.
“Kwanini usiibwe.”
“Huu ni mziki mnene Sociolah siwezi kuibiwa kirahisirahisi.” Aliongea huku akitabasamu.
Tulitoka mlimani City na kisha tukaelekea sehemu kupata chakula Fair delight pembeni ya Mliman City.
“Chakula kitamu.” Aliongea.
Tulipata chakula na baada ya hapo tulirejea mabwenini kwetu Mabibo ilikuwa kiasi kama saa tatu, nilipitiliza moja kwa moja chumbani kwa Frank hakuna mtu ambaye alikuwepo chumbani kwake. Alianza kuzijaribu zile nguo ambazo nilimnunulia siku hiyo.
“Kuna nini kingine unahitaji?”
“Hamna.”
“Hamna, unaona kama simu yako ni nzuri?”
“Nzuri tu inaingia WhatsApp, inaingia Insta sijui wapi.” Aliongea.
Nilijikuta tu nacheka.
“Kama ni nzuri sawa.”
Mama alipiga simu sikupokea.
“Mbona hupokei?”
“Mama huyu nitaongea naye baadae.”
Tuliendelea kuongea maongezi ya hapa na pale tukipiga story mbalimbali hadi ilipofika saa tano.
“Frank mimi nahisi usingizi nataka kwenda kulala.” “Ngoja nikusindikize.”
Alinitoa hadi mbele ya mabweni yetu alinibusu kwenye paji la uso na kisha kuniacha niliingia bwenini kwetu.
Mimi na Melania tulikuwa tukilala vitanda vya chini, Monica na Fetty walikuwa wakilala vitandanda vya juu.
Niliingia nikakuta Monica akiwa kitandani kwake juu Fetty na Melania walikuwa mezani.
Sijui walikuwa wakiongea nini au walikuwa wakifanya nini, niliingia, Fetty alinyanyuka kuja kunikumbatia Melania alimvuta mkono na kumkalisha kwenye kiti.
“Unaenda wapi?” Alimuuliza.
Kwa kweli sikuwahi kumshuhudia Melania akiwa katika hali kama hiyo, hali hiyo ilinifanya nimjue Melania ni mafia kwa maana ile sauti yake ya upole ilibadilika.
Fetty hakuwa na jinsi alirudi kitini na kukaa nilicheka kwa upole kiasi kwamba Melania asingeweza kunisikia.
“Hi..” Nilisalimia.
Aliitikia Monica nadhani Fetty aliogopa kuitikia.
Niliingia kitandani kwangu na kisha kujilaza.
Asubuhi ya siku iliyofuata tulikuwa tuna kipindi cha saa mbili asubuhi niliamka niliwakuta tayari wote wameshaamka nilielekea bafuni kuoga na baada ya hapo nilirudi chumabani kwangu kujianda. Walitoka dakika tano kabla yangu, tulipanda wote gari moja hadi chuoni.
Tulishuka na kisha kuelekea yalipo madarasa yetu, walikuwa hatua zisizopungua kumi na tano mbele yangu.
Melania akiwa na baadhi ya watu wa darasa letu.Tulipofika karibu na madarasa
yetu kila mtu alikuwa akishangaa.
Nilishindwa kujua kuna nini.
Lakini ghafla nilimuona Melania akisita, mshangao alioupata sikuwahi kumuona nao hata siku moja.
Ilinibidi kuwa mdadisi ni nini kinatokea na nini kilichomfanya Melania akashangaa kiasi hiko.
Hakika Frank alikuwa amependeza tofauti na hata vile alivyokuwa akizijaribu zile nguo. Kitu pekee nilichokijua ni kwamba Frank alikuwa mbunifu sana ila alikuwa akishindwa kupata mavazi mazuri. Nilimnunulia nguo katika pea lakini alijua kuchagua nguo zinazoendana hakika alipendeza sana.
Melania alikuwa mbele yangu nilitazama jinsi watu walivyokuwa wakimshangaa Frank kila mtu akitamani kupiga naye picha, alionekana ni mwanaume wa kileo ambaye kila msichana angetamani kuwa naye. Niliachia tu tabasamu na kisha kuongeza hatua zangu, nilimpita Melania kwa hatua za pole pole nilipita mahali ambapo Frank alikuwa amesimama na kisha kuingia darasani.
“Basi basi inatosha.” Frank alisema na kisha akaniungia tela nyuma yangu. “Sociolah...” Niligeuka na kumtazama na kisha nikaendelea kupiga hatua hadi kwenye sehemu ambayo nilizoea kukaa mara zote.
Hata hivyo nilikuta vitu ambavyo vilionesha kuna mtu tayari ameshakaa. Viti vyote vya mbele vilikuwa vimewahiwa kitu ambacho siyo kawaida mara zote nilizoea kukaa mbele na hakuna mtu ambaye alikuwa anaweza kukaa kwenye kiti ambacho nilikuwa nakaa.
“It is yours.” Alisema Frank.
“Frank.” Nilimuita.
Watu walianza kuingia darasani nilinyanyua vile vitu na kugundua kwamba havikuwa ni madaftari. Nilikaa, alikuja kukaa pembeni yangu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Zilikuwa ni bahasha mbili nilichungulia ndani ya bahasha moja nikakuta kadi nzuri sana niliifunga bahasha na kisha kuweka kwenye begi langu nikamgeukia Frank. “Mwalimu ameingia.” Aliniambia, nilicheka tu na kisha kumtazama mwalimu. Mwalimu alivyoingia tu alimuita Frank.
“Franklin Kazimana.” Aliita.
Frank alisimama.
“Baada ya kipindi uje ofisini kwangu na Cr nitahitaji kukuona baada ya kipindi.” Watu wote walicheka darasani.
“Mnacheka nini?” Aliuliza mwalimu yule ambaye alikuwa ametuzoea wanafunzi wake.
“Hamna kitu.” Alituangalia tu na kisha kuendelea.
Mara baada ya kipindi.
“Frank twende.” Nilimuita tulinyanyuka kwa hatua za polepole kuelekea ofisini kwa mwalimu.
Tulifika ofisini kwa mwalimu.
Mwalimu yule alikuwa akituangalia tu.
“Frank nataka niwape kazi ya kufanya kuna mashindano ya madaktari wanafunzi kutoka vyuo mbali mbali nataka mkashiriki lakini wewe pekee ambaye ninakuamini nataka ukatuwakilishe Frank.” Daktari aliongea. Daktari Kiseyeye alionekana kuwa makini sana.
Frank aliniangalia.
“Hamna shida, yanahusiana na nini?”
“Nitakuja kukupa maelezo kwa njia ya maandishi ilimradi umekubali hakuna
shida.”
“Sawa.”
“Sociolah nataka uwatangazie test watu wako, wiki ijayo kutakuwa na mtihani wajiandae nitatoa kwenye module ya kwanza niliyofundisha.” “Sawa mwalimu.”
“Kitu kingine nataka kujua kwanini watu walicheka darasani baada ya kuita Sociolah?”
Nilitabasamu na kisha nikamuangalia Frank.
“Hapana sijui mimi, ni bora tu ungewauliza wenyewe.”
“Hamna shida mnaweza mkaenda.”
Tulitoka tulishikana mikono tukitembea mpaka mgahawani kwa ajili ya kupata chai.
“Leo tutakunywa chai pamoja.” Nilimuambia. “Hakuna shida.”
Aliagiza yeye chai mimi niliagiza juisi.
“Kunywa chai Sociolah.”
“Aaah, mimi sipendi sana kunywa chai ujue.” “Shauri yako mwili haujengwi kwa matofali.” “Hahaha kama juisi ni matofali sawa.”
Tuliendelea na mazungumzo ya hapa na pale tukifurahia na kucheka.
Nilipopiga jicho pembeni yangu niliweza kumuona Melania akituangalia kwa jicho kali, nilikatiza tabasamu langu usoni na kisha kubaki nikimshangaa alinyanyuka ghafla na kuondoka.
Kila mtu mule mgahawani alishangaa hakuna aliyejua sababu yake na mimi niliamua kumpotezea na kuendelea kuongea na Frank kana kwamba sikumuona. Tuliendelea na vipindi hadi vilipoisha.
Nilimuacha Melania awahi kuondoka nilimsubiri Frank huku nikimchelewesha ili tusiwahi kuondoka.
“Kwanini hutaki kuondoka?”
“Mimi sitaki kuongozana na Melania na wala sitaki kwenda kule chumbani kwetu si unajua tuna ugomvi.”
“Basi twende ukakae chumbani kwetu.” Aliongea.
“Ni wazo nzuri.”
Tuliondoka hadi mabibo na kisha tukaingia Complex kwa ajili ya kupata chakula cha mchana. Tulikula chakula cha mchana na kisha kuelekea chumbani kwa Frank. Marafiki zake walikuwepo.
“Aaah jamaa umependeza kweli yani leo kila mtu darasani anakuzungumzia wewe wasichana sio kujigonga huko aisee jamaa una nyota kweli.”
Aliongea mmoja wapo kati ya watu ambao ni wakazi wa chumba cha Frank kabla ya kuniona nikiingia.
“Niliachia tu kicheko.”
“Shukrani zote zimuendee mama hapa.” Aliongea Frank huku akinioneshea mimi niliinama kwa aibu.
“Aaah...Aisee... Huyu ni bonge la mke Frank usiache.”
“Naanzaje asa kwa mfano?” Aliongea.
Niliachia tu kicheko huku nikitazama chini.
Nilikaa chumbani kwa Frank hadi wakati wa usiku ulipofika. “Nataka kupumzika nimechoka.” Nilimuambia Frank. “Hakuna shida ngoja nikupeleke.”
Alinisindikiza hadi nje ya chumba chetu, alinibusu na kisha kunitakia usiku
mwema.
Akaondoka.
Nilimuangalia hadi alipopotelezea huku nikitabasamu mwenyewe.
“Hakika hapa nimefika nampenda sana Frank.” Niliongea.
Niligeuka na kushika kitasa cha mlango ili nifungue kwa ajili ya kuingia ndani nilipominya kitasa cha mlango ulifunguka na kisha nikasikia kilichokuwa kikiongeleka mule ndani.
“Yeye si anajifanya mjanja nitamkomesha.”
Nilivutiwa kujua ni nani tena ameingia kwenye ugomvi na Melania.
“Hamna usimfanyie kitu kibaya.” Fetty alisema.
“Nyamaza.. Mimi ndiyo Melania sishindani na vitoto vidogo.” Nilifunga mlango nikijiuliza maswali yasiyo na majibu.
“Melania amegombana na nani tena, kumbe ana tabia za ugomvi hivi? Kama ni hivi sitaweza kupambana naye namuacha kama alivyo akiamua kunisikiliza nikiomba yaishe sawa asipoamua sitajali.”
Nilifungua mlango na kuingia sikujua wanaongea nini lakini wote watatu Melania, Fetty na Monica walikuwa wameinamia simu ya Fetty kuangalia walichooneshwa na Fetty.
Nilipoingia kila mtu alikurupuka kwa haraka na kuanza kufanya vitu ambavyo havikuleta maana, nilibaki nimeduwaa.
Hali niliyoikuta mule chumbani ilinitisha sana, nilishindwa kuelewa na kubaki nimesimama tu katikati ya chumba nikiwa kama mtu nisiye sina muelekeo. Monica alitoka pale walipokuwa wameinama wakiangalia kitu na kukimbia moja kwa moja kwenye kitanda changu alichukua shuka langu na kisha kujifunika mwili mzima.
Melania alinyanyuka pale alipokuwa amesimama na kisha kuelekea kwenye makabati na badala ya kufungua kabati lake alifungua kabati la Fetty na kisha alijiweka bize kana kwamba kuna kitu anakitafuta kwenye kabati la Fetty.
Fetty aliiziba simu yake kwa nyuma, aliiweka nyuma yake ili nisione ni nini kilichokuwa kinatokea, nilibaki nimeshangaa. Kila mtu alijiweka bize kama vile hawakutaka nijue ni nini kilichokuwa kikiendelea mule chumbani.
“Unatafuta nini kwenye kabati langu?” Fetty alimuambia Melania.
“Aaah... Eeee....Mmmh ...”
Melania aliishia kuguna tu na kisha alifunga kabati la Fetty na kufunga kabati lake. Hali hiyo ndiyo ilizidi kunichanganya zaidi, nilifungua mlango na kuubamiza kwa nguvu na kisha kuondoka sikutaka kuendelea kuwepo mahali pale.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Niliondoka moja kwa moja hadi chumbani kwa Frank, nilifungua mlango bila kubisha hodi.
Frank alikuwa yupo kifua wazi huku chini akiwa amevaa kaptula ya michezo. Niliingia na kwenda moja kwa moja kitandani kwa Frank nilikaa na kujiinamia huku nimefumbata uso wangu katika viganja vya mikono yangu.
“Nini Sociolah kuna nini?” Frank aliniuliza sikutaka hata kumjibu. “Niambie mama kuna nini?” Alikuja kukaa pembeni yangu. “Hapana Frank naomba nipe muda nipumzike nitakuambia kila kitu.”
Niliwakuta watu wote waliokuwa wakiishi katika chumba cha Frank nadhani na wao pia walitaka kujua nini kimetokea kwa maana waliacha kufanya walichokuwa wakikifanya na kuniangalia mimi.
“Ok basi pumzika.” Frank alisema.
Alinilaza pale kitandani na kisha kunifunika shuka nilipitiwa na usingizi.
Nilikuja kushitushwa baada ya kuota ndoto ya kutisha na muda ulikuwa umeshaenda sana.
“Nini?” Frank aliniambia baada ya kushituka usingizini.
“Sociolah una nini lakini?”
“Frank nimeota ndoto ya kutisha sana.”
“Ndoto gani?”
“Umeota nyoka wanakukimbiza.”
“Bora hata angekuwa nyoka.”
“Nini hiko ulichoota niambie basi Sociolah.”
Alinyanyuka pale alipokuwa amekaa na kuja kitandani alininyanyua na kisha kuzungusha mkono wake begani kwangu.
“Niambie basi kuna nini?”
“Nimeota unanisaliti, tena na Melania.”
“Aaah...” Alicheka sana.
“Hiko kitu hakiwezi kutokea Sociolah hata siku moja naomba uniamini mke wangu kwanza mimi siwezi kutoka na mwanamke kama yule, mwanamke kama mwanaume.”
Nilishindwa kujizuia ilinibidi kucheka nilisahau shida zote zilizokuwa zikitokea katika chumba chetu.
“Frank mimi sielewi hali ya kule chumbani kwetu.” “Kuna nini kwani?”
“Nimekuja nimekuta kuna kitu wanaoneshana kwenye simu ya Fetty halafu ghafla wote wakaanza kukimbia na kuanza kuact differently, ilinishangaza sana inaonekana kuna kitu walikuwa wakikiangalia kwenye simu ya Fetty na hawataki nijue.”
“Mmmh nini iko?”
“Sijui kwa kweli mimi nashindwa kuelewa.”
Frank alikuna kichwa kana kwamba akijaribu kutafuta majibu, nilibaki tu nikimuangalia ili niweze kusoma alichokuwa akikifikiria sikuweza kufanikiwa. “Twende tukamalizie siku chumbani kwenu.”
Wazo lake lilinifurahisha sana kwa maana kwa kufanya hivyo ningeweza kumuumiza roho Melania.
Tulitoka na Frank hadi chumbani kwetu nilifungua mlango na kuingia, kila mtu alishangaa.
Frank alikuwa kama malaika.
Monica alikuwa bado amelala kitandani kwangu.
“Monii.... Monii....” Nilimuamsha.
“Niache...”
“Monii...”
“Niache nimesema.”
“Monii... Toka kitandani kwangu.” Nilimuambia kwa sauti Frank alicheka.
Alifunua shuka ghafla na kuamka.
“Aaah samahani nilikuwa sijui kama nimelala kitandani kwako.” Nilicheka tu na kisha kumuacha.
“Aya toka.”
Alitoka na kisha kupanda kitandani kwake.
Mimi na Frank tuliingia kitandani kwetu na kukaa.
Tuliongea mawili matatu kwa sauti ya chini ambayo haikusikiwa na mtu yoyote na kisha tukajifunika shuka na kujilaza, tukio hilo lilionekana kuwakera sana.
Kila mtu alipanda kitandani kwake.
Tukiwepo kitandani tuliweza kuongea mambo mengi huku tukicheka kwa sauti walichokuwa wakisikia ni kicheko tu hakuna sauti iliyotoka.
Tuliendelea kuongea hadi muda ulipokuwa umeenda sana. “Twende tukatafute chakula tule halafu unipeleke kulala.” Kabla sijajibu Melania aliachia msonyo wa hali ya juu. Nilitabasamu tu na kisha nikaitikia kwa sauti zote.
“Sawa.”
Nikambusu kidogo mdomoni na kisha kutoka pale kitandani, alitoka kitandani na kisha kuketi katika kingo za kitanda.
Nilinyanyuka na kuelekea kabatini kwangu nilifungua kabati na kutoa shati jingine.
“Nikivaa hili si nitapendeza?” Nilimuuliza Frank.
Kila mtu aligeuza macho yake.
“Yes umependeza, unapendeza katika kila kitu Sociolah.” Frank alisema.
Nilivua shati Frank aliachia tu tabasamu na kisha nikavaa shati lile jingine nililokuwa nimelichagua na baada ya kuvaa nilikusanya vitu vichache na kisha kutoka.
Tulielekea Complex kupata chakula cha jioni.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Tulikula huku tukiongea mawili matatu kila mtu alikuwa akituangalia, tulipiga stori huku tukicheka sana na baada ya hapo nilimsindikiza hadi maegesho ya magari.
Tuliongea mawili matatu na kisha tukaachana alielekea chumbani kwake na mimi nilielekea chumbani kwangu.
Nilipofika mlangoni kwangu kilichokuwa kikiongelewa pale sikutaka kuamini masiko yangu, nilihisi masikio yangu yakinidanganya kwa maana sikutegemea kusikia kitu kama hicho.
Bila shaka ndani ya chumba chetu kulikuwa kuna ugomvi uliokuwa unaendelea bila kuambiwa niliweza kujua kwamba Melania hayupo mule chumbani.
Ni ugomvi uliokuwa ukiendelea kati ya Fetty na Monica sikuwahi kuhisi kama Monica na Fetty wangeweza kugombana kiasi hiko kwanza walikuwa wote ni wapole.
Kwa kiasi fulani mimi na Melania tulionekana tumechangamka sana mbele yao lakini ugomvi ule uliokuwa ukiendelea mule chumani ulinifungua macho kwamba rafiki siyo mtu yoyote yule unayekutana naye ili mtu awe rafiki yako inabidi
kusiwe na sababu ya urafiki wenu kwani ile sababu ikipotea hakutakuwa tena na urafiki kati yenu.
Nilisimama hapo mlangoni muda mrefu, walianzia mbali sana hadi kufikia kwenye ugomvi wao.
“Aaanh kwa uzuri huo lazima tu agombane naye hata ningekuwa mimi lazima ningeingia kwenye ugomvi naye.”
“Mimi ndiyo ninaingia naye kwenye ugomvi.” Fetty alisema. “Eenhe.. Tutabanana hapo hapo hata mimi siachi.” “Nini..? Unaongea nini?”
“Yani nakuambia hivi Melania si amesema lazima atoke na huyo Frank na mimi niko hapo hapo.” Alijibu Monica kwa msisitizo.
“Sikia usitake kujifanya unamjua sana Frank, sisi Frank tunamjua tangu siku ya kwanza hivyo tunaomba ukae mbali naye.”
“Yani hilo utanisamehe kwa kweli mwanaume mzuri kama Frank nani atakubali amuache.”
“Monica huwezi kunitisha kwa chochote pambana na hali yako na mimi nipambane na hali yangu fyuuu.... Tuone kama atakuchukua mtu mwenyewe kama
wewe.”
“Tutajua hapo hapo.”
Waliendelea kutamkiana maneno ya kashfa na ya ajabu nilishindwa kuelewa inamaanisha chanzo cha ugomvi wote huu ni kwamba hawa watu wanamtaka Frank. Hilo lilianza mbali kuwahi kuingia katika akili yangu.
“Inamaanisha Melania kumchukia Frank kote ni kwamba alikuwa anamtaka. Kwanini asingemchukua mapema mpaka unafikia wakati mimi na Frank tuko naye kwenye mahusiano na hata hivyo siwezi kuruhusu hiyo hali nitapambana naye mpaka mwisho na kuanzia sasa nitamkomesha.”
Sikuingia chumbani niliondoka, nilitoka hadi kwenye maegesho ya magari na kisha nikampigia simu Frank.
“Mama umeshanimisi?” Alianza kuongea mara baada ya kupokea simu yangu.
Nilicheka.
“Frank njoo, njoo parking nakusubiri kuna kitu nataka niongee na wewe.”
“Si tumeachana sasa hivi tu jamani.”
“Ndiyo naomba uje.”
Alishuka hadi maegesho ya magari.
“Tutafute sehemu tukae.”
Ilikuwa mida ya saa nne.
Tulikaa nilimsimulia kila kitu nilichokisikia chumbani kwetu, alivuta pumzi na kuzishusha.
“Hao watu wamechanganyikiwa nini, hivi wanafikiri mimi nitaweza kukuacha wewe Sociolah kwasababu ya wale, sikia nikuambie kitu Sociolah wewe ulinipenda wakati mimi sina kitu chochote, ulinipenda wakati nikiwa sina hadhi yoyote hata mbele za watu, ulinipenda wakati kila mtu ananidharau siwezi nikakuacha hata iweje nakupenda sana.”
Maneno yake yalinitia nguvu na jeuri.
“Nashukuru Frank.”
“Nataka tuwaoneshe kwamba mimi na wewe hatutoachana sawa.” Aliongea huku akitabasamu.
“Nitafurahi sana.”
“Usijali.”
Tulitoka pale hadi chumbani, chumba kilikuwa kipo kimya niliingia.
Melania alikuwa amerudi huku kila mtu alikuwa anaendelea na shughuli zake kimya kimya hakukuonekana dalili ya usalama wala amani mule ndani.
Niliingia na kisha Frank alifuatia nyuma yangu alikuwa amenishika kiuno huku
tukitembea kama kumbikumbi.
Frank alikuwa akinitekenya.
“Niache.”
Kila mtu alinigeukia na kuniangalia nilimuona jinsi ambavyo Melania alikuwa amechukia.
Tulienda mpaka kitandani akakaa na kisha nikamkalia kwa juu nikamgeukia na kumtazama na kisha lilifuatiwa na busu refu.
“Aaanh,.. Nakupenda.” Aliniambia Frank mara baada ya kukatisha busu hilo. “Nakupenda pia.”
Alinichapa kofi kidogo.
“Nini lakini.”
Tuliendelea kuongea mawili matatu huku tukicheka kwa sauti.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nahisi usingizi.”
“Kesho tusiende chuo.” Nilimuambia.
“Kweli eeehe.”
“Eeenh...”
Aliitikia, “Hamna shida hatutaenda.”
Nilisahau kama kesho ni mwisho wa wiki (Ijumaa) hivyo nilitakiwa niende nyumbani na mama baada ya kutoka chuoni.
Aliniaga na kusimama na kisha kutembea hadi mlangoni nilisimama na kisha kujongea mahali alipokuwa amesimama pale mlangoni, nilisogea hadi karibu yake alinyanyua mikono yake na kisha kuizungusha kwenye kiuno changu nilichukua mikono yamgu na kuizungushia begani kwake.
Alinibusu na busu hilo lilichukua muda mrefu kidogo. Baada ya sekunde kadhaa aliniachia.
“Uwe na usiku mwema.” Aliniambia.
“Sawa, same.”
Aliondoka nilivuta pumzi na kuishusha na kisha kufunga mlango na kuuegamia macho sita ya watu watatu yalikuwa yakinitazama mimi.
Nilivua nguo zangu na kisha nikachemsha maji na kuelekea bafuni kuoga, niliporudi nilivaa gauni langu jepesi la kulalia la rangi ya pink na kisha niliukumbatia mdori wangu na kisha kulala huku nikitabasamu sikutaka hata kusikia wanaongea nini wala nini kinaendelea.
Asubuhi nilipoamka hakukuwepo na mtu hata mmoja na simu yangu alikuwa akiita. “Sociolaha umenisaliti.” Ilikuwa ni sauti ya Frank mara baada ya kupokea simu yake.
“Kwanini?”
“Si tumekubaliana leo tusiende chuoni, kwanini umeenda?” “Mimi nipo ndiyo kwanza naamka.”
“Mmmh sasa unakuja huku kwangu au nije huko kwako?” “Njoo huku bwana mimi ndiyo kwanza nimeamka.” “Aya sawa.”
Baada ya dakika kadhaa Frank alikuwa amefika chumbani kwetu.
Tulicheza michezo mbalimbali, tulitekenyana, tukakimbizana humo humo chumbani, tuliongea, tukapiga stori, tukalala, tukaamka, tulisahau hadi kula mpaka ilipofika mchana mwingi.
Nilimuita mmoja kati ya wafanya usafi pale kwenye mabweni yetu na kumuagiza atuletee chakula.
Tulikula humohumo ndani tukaendelea na michezo mbalimbali hakika siku hiyo ilikuwa ya furaha sana nilisahau kurudi nyumbani.
Takribani wiki mbili zilipita bila kurejea nyumbani mawasiliano na mama yalikuwa finyu sana.
Mara nyingi kila akipiga simu wakati niko na Frank sikupokea ama ningetoa sababu yoyote ile ya kutokupokea simu yake. Wiki ya tatu iliingia.
Wala sikuwa nikikumbuka kurejea nyumbani siku hiyo haikuwa ya kawaida Frank alinijia na sura ya kichovu sana asubuhi wakati akinipitia kuelekea chuoni.
Ni siku hiyo ndiyo tuliamua kwenda chuoni baada ya kupita wiki takribani mbili mara baada ya kumaliza mtihani hatukuhudhuria tena chuoni.
Tuliwahi kufika mapema mara baada ya vipindi kuisha nilitoka nilimuacha Frank ndani akiongea na baadhi ya watu huku nikiwahi kutoka kwenda kumsubiria nje. La haula!
Nilikutana na mama amepaki gari lake mbele ya darasa letu huku amesimama nje ya gari akiwa amefura.
Haikuhitaji maelezo kwamba alikuja kunifuata alikuja alisimama pale huku akionekana ana hasira sana.
Nilisimama mwenyewe na kuelekea pale.
“Ingia kwenye gari.”
Nilifungua malango wa gari na kuweka begi langu na kisha kupanda sikupata hata muda wa kumuaga Frank.
Safari ya kuelekea nyumbani ilianza.
“Naomba simu yako.”
Nilipojaribu kuchukua meseji nimtumie Frank mama aliniomba simu.
Nilikata haraka na kumpa simu yangu, aliichukua na kuiweka mbele kwenye sehemu ambayo alizoea kuweka simu yake, nilijua tu mambo siyo mazuri.
Tulifika nyumbani hali niliyomkuta nayo baba iliashiria kwamba kuna kitu hakipo sawa.
Haikuwa kawaida kuikuta familia yetu kwa namna hiyo hali hiyo iliniogopesha. Sebuleni alikuwepo baba, Kelvin na Linah dada yetu wa kazi. Mama hakuniweka hata niongee nao neno moja alinipitisha moja kwa moja hadi chumbani. Niliingia chumbani alinikalisha kitandani
“Pumzika mwanangu.” Aliongea na kisha kutoka nje. Nilishangaa, nilikaa takribani nusu saa nzima. Nikafikiria jambo. “Ngoja nimfuate mama anipe simu yangu.” Nilinyanyuka hadi mlangoni. Nilipojaribu kufungua mlango niligundua kwamba mlango umefungwa kwa nje na funguo haukuwepo. Nilirudi na kukaa kitandani.
“Mama anamaanisha nini kunifungia mlango humu ndani, nikipatwa na shida je?”
Niliita.
“Mama....”
Niliita watu wote waliokuwepo humo ndani kwa sauti kubwa hata nilihisi sauti yangu inataka kukauka lakini hakuna aliyeitika wala kunifungulia mlango.
Nilijua tu mambo yamekua mabaya, nilikaa mule ndani, nilizunguka, nilisimama, nikakaa chini, nikarudi kitandani, nikaenda kusimama dirishani, niliingia bafuni na kutoka, nilikuwa sina cha kufanya nilihangaika hadi nilipopitiwa na usingizi.
Nilikuja kuamshwa baada ya kuhisi mlango wa chumbani kwangu umefunguliwa giza tayari lilikuwa limeshaingia.
Waliingia Pink na Pinto nilikuwa nina uchovu mwili mzima nilinyanyuka na kisha kukaa nikafikicha macho yangu na kuwatazama.
“Shikamoo dada.”
“Marhabaa.” Niliitikia kiuchovu.
“Mama kaseme tuje tukuulize utakula nini.”
Nilikasirika sana nilijua mama anahitaji kuniletea simu yangu kumbe anakuja kuniambia kuhusu maswala ya chakula.
“Fyuuu...” Nilisonya mwenyewe.
“Kwani alifikiri mimi nitaishi kwa ajili ya chakula tu mwambie chochote.” Niliongea kwa hasira.
Pink alicheka na kisha walitoka nje, nilijaribu kwenda kufungua mlango nilikuta umefungwa tena.
Nilikaa mwenyewe takribani lisaa lizima lilipita nilitegemea usiku huu nitafunguliwa kwa ajili ya kujumuika na familia nzima kwa ajili ya chakula cha usiku nilichoka kuwaza na kuwazua nini kinaendelea.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Je baba ameshamjua Frank? Je hicho ni kitu ambacho kinamchukiza? Je Melania ameongea na mama kuhusu mahusiano yangu na Frank au kuna nini kinaendela?” Nilishindwa kupata majibu ya haraka.
Muda ulijongea, nilikaa kitandani kwangu pasi na kitu cha kufanya na mara ghafla niliona mlango ulizungushwa kwa ishara ya kwamba mtu anahitaji kuingia nilikaa kitako kuja kujua ni nana alikuwa akiiingia nilipanga kumuuliza maswali yote kwanini nimefungiwa humo ndani kuna nini. Nilikasirika sana kuona ni Pink na Pinto wakiingia.
Waliingia wakiwa wamebeba vitu mbali mbali vilivyoonesha ni chakula cha usiku waliviweka kitandani.
“Dada chakula.” Pink aliongea na kisha walitoka haraka haraka.
“We Pink...” Niliita.
“Baba kasema tusikae huku.”
Nilishangaa.
“Kuna tatizo gani!”
Walitoka haraka haraka.
Mama alikuwa ameniandalia chakula kizuri sana ambacho bila shaka ni yeye mwenyewe aliyekipika niliweza kutofautisha kati ya chakula cha mama na kile kilichoandaliwa na dada yetu wa kazi Linah. Aliniandalia chakula nikipendacho sana ndizi nyama.
Kulikuwa na sahani ya matunda pembeni pamoja na maji ya matunda ya maembe na glasi moja ya maji.
Wala hata sikutamani kuingiza kile chakula mdomoni hata hivyo nilikumbuka kuwa sijala kitu tangu asubuhi ilinibidi kujilazimisha huku nikiwa na mawazo mengi.
Nilijaribu kula kile chakula ambacho kilionekana kuendelea kunishinda na ghafla mlango ulifunguliwa tena waliingia Pink na Pinto huku wakicheka.
“Mnacheka nini?” Niliwambia.
Pink alikuwa anatembea kana kwamba anamuigizia mtu mwenye nguvu nyingi, aliingia ndani na kisha Pinto alifunga mlango haraka haraka.
Pink alionekana kama mtu mwenye hasira sana alifura kana kwamba kuna mtu amemuudhi nani kama mtu mwenye umuhimu mkubwa, ni sawa na bosi ambaye amechukizwa na mfanyakazi wake.
Niliendelea kutazama vituko vyake huku nikihisi kucheka.
Alivimba huku akitanua mikono yake kuonesha kiasi gani ameshikwa na hasira. Pinto alisimama pembeni akimuangalia huku akicheka na mimi niliungana naye kucheka.
Ghafla Pink aliongea kitu ambacho kilinichanganya sana. “Nikimjua nitatenganisha kichwa chake na kiwiliwili.” “Wewe Pink unaongea nini?” Nilimuuliza ghafla. Maneno ya Pink yalinichanganya sana.
“Baba kasema tukuletee simu yako.”
“Hebu njoo kwanza subiri nikuulize.”
“Baba kaniambia nisikae humu ndani.” Walitoka nje.
“Baba alikuwa anamzungumzia nani?” Nilishindwa kuelewa hata hivyo uwepo wa Kelvin ulinipa mwanganza inawezekana kuwa ni mfanyabiashara mwenzie
amemuudhi ninamjua baba yangu akiwa na hasira anaweza kuongea vitu vya ajabu sana na wakati mwingine anaweza kufanya jambo la ajabu pia.
Niliendelea kujilazimisha kula huku maneno ya Pink yakizidi kunisumbua moyoni mwangu ni nani huyu nilizidi kujiuliza maswali.
Nilikula kile chakula nilishindwa kukimaliza nikabaki nimekiangalia tu uwepo wake pale ulianza kunikera harufu yake tayari ilishakuwa mbaya kwangu nilitamani kuvitoa vile vyombo lakini nilikumbuka kwamba mlango umefungwa, ningewezaje kuvitoa?
Nilinyanyuka kwa hasira huku nikizungukazunguka mule chumbani nilienda kwenye mlango na kuufungua kwa hasira zote huku nikitoa ukelele wa ghadhabu. La haula...!!
Mlango ulifunguka saa hizi.
“Mlango haujafungwa ngoja nijifanye napeleka vyombo.”
Nilibeba vyombo vyangu na kuvipeleka jikoni, wakati narudi nilijaribu kuchungulia sebuleni ni akina nani wapo na kama kuna uwezekeano wa kusikia wanachokiongea.
Nilimkuta mama akiwa amekaa peke yake alionekana kuwa na mawazo mengi sana, hali hiyo iliniumiza nilinyata taratibu na kisha kwenda kukaa pale alipokuwa amekaa mama.
Nilimgusa begani aligeuka uso wake ulionesha simanzi sana aliniangalia tu na kisha kuendelea kutazama pale alipokuwa ametazama.
“Mama...”
Aligeuka na kuniangalia machozi yalionekana kumlenga.
“Kuna tatizo gani mama mbona nimechukuliwa chuoni kwa namna kama ile na nimeletwa huku nimefungiwa ndani kuna nini ambacho sipaswi kukijua, kuna tatizo gani mama niambie basi.”
Mama alivuta upande wa kanga ambao alikuwa amejifunga na kufuta machozi yaliyokuwa yameanza kuchuruzika baada ya hapo alinitazama alinyanyua mkono wake hadi shavuni kwangu.
“Mwanangu Sociolah.”
“Bee mama.”
Alitabasamu tabasamu lililoonesha machungu aliyokuwa nayo moyoni.
“Nakupenda sana mwanangu.” Mama aliniambia.
“Nakupenda pia mama, je hilo ni tatizo, kuna kitu unanificha mama naomba uniambie.”
“Sociolah niambie ni mwanaume gani mwenye mahusiano na wewe pale chuoni.” Swali lake lilinishitusha sana sikutegemea kuulizwa swali kama hilo kwa wakati kama huo.
“Mama ni nini hicho unaniuliza.”
“Hakuna cha kuficha Sociolah niambie ni nani?”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilipandwa na ghadhabu sana niliona kama familia nayo imeanza kuniingilia katika mahusiano yangu na Frank.
“Mama mimi nimeshakuwa mtu mzima.” Nilianza kuongea kwa ghadhabu na mimi.
“Hayo maswala mimi siwezi kukuambia na kama mmekaa na baba mnakuwa na huzuni kwasababu ya hilo swala sijui, mimi nimeshakuwa mtu mzima naomba mniache, mniache...”
Niliongea.
“Pumbavu....” Mama alinyanyuka kwa ghadhabu nilishangaa, alisimama mbele
yangu.
“Ninaongea na wewe kama binti yangu nikupendae unanijibu kama unaongea na marafiki zako huku chuoni, sikia Sociolah lazima uwe na adabu mbele yangu.” “Mama kwani nini nimekosa.” Nilimuingilia.
“Kosa langu mimi ni nini mnanichukua chuoni kama mnamchukua mhalifu nakuja huku mnanifanyia mambo ya ajabu ajabu kwasababu gani? Eti kwasababu ya kuwa na mahusiano na mtu kwani ni vibaya kuna shida gani hata kama ninaye.” “Kelele...” Mama alinikatisha.
“Kuanzia leo hutotoka humu ndani, kwenda chuoni utaenda na mimi na nitakurudisha mwenyewe na nitakuwekea mtu wa kukuangalizia mpaka pale utakapo jirekebisha, hiyo ni amri kutoka kwa baba yako na amesema akisikia ujinga ujinga wowote utamkosa huyo mwenzio pumbavu.” Mama aliongea na kisha kuondoka.
Nilibaki nimechanganyikiwa nisijue hata cha kufanya. Niliendelea kukaa pale sebuleni kana kwamba sina sehemu ya kwenda.
“Mungu wangu, Mungu wangu balaa gani tena hili mbona matatizo juu ya matatizo.” Niliendelea kujiuliza.
“Mbona Mungu umeniacha mimi, huku Melania huku nako familia inanifanyia hivi mimi nitaishije jamani.”
Niliendelea kuwaza, niliuma vidole mpaka nikahisi vitakatika. Nilinyanyuka kiunyonge na kisha kuelekea chumbani.
Usiku mzima nilikesha nikilia.
Nilishindwa kujua hatima yangu ni nini?
Niliamua kuacha kama ilivyo usiku ule nilichelewa sana kulala na asubuhi na mapema ilinikuta niko macho.
Siku nzima nilishinda ndani simu yangu haikuwa na laini baba alitoa laini na kisha kubaki nayo nilikaa tu nikiitazama simu yangu. Muda wote nilikuwa ndani.
Afuheni ilikuwa ni kwamba kuanzia siku hiyo iliyofuatia sikuwa nikifungiwa chumbani bali getini alibadilishwa mlinzi ambaye hata sikuwa nikimfahamu na alipewa amri ya kutonifungulia geti hivyo nilikuwa nikikaa ndani nikichoka ningetembea tembea humo bustanini muda wote.
Kwa kuwa baba na mama walikuwa kazini asubuhi hadi jioni wakati Pink na Pinto walikuwa shuleni nilibaki na dada wa kazi mule ndani ambaye na yeye sikuwa nimemzoea sana na wala sikutaka kuwa karibu naye.
Muda na siku vilienda nilishindwa kuonana na Frank wala kufanya naye mawasiliano.
Melania aliendelea kunichukia.
Hali hiyo iliendelea hadi likizo ilipofika.
Ulikuwa ni mwezi wa tatu tarehe tatu. Bado sikuwa na ruhusa ya kutoka nyumbani hata hivyo nilijitahidi sana kuwa binti mzuri ili niweze kuulainisha moyo wa baba anisamehe kutoka katika kifungo hicho hakika alipendezwa sana. Siku yake niliingiwa na ujasiri.
“Baba umenifungia kwa muda mrefu ni lini utaniachia huru.” Niliongea kwa sauti ya upole.
“Oooh binti yangu nitaongea na mama yako na kisha nitakuja kukuambia nini tumeamua.”
“Sawa baba nitafurahi kama utanikubalia.”
Nilirudi chumbani huku nikisherekea ushindi huo, najua kama mama angekubali basi baba asingekuwa na tatizo lolote.
Baada ya nusu saa mama aliingia chumbani kwangu.
Nilikuwa nimekaa kitandani hiku nikisoma soma baadhi ya vitu.
“Sociolah.” Mama aliniita kwa upendo huku akinishika begani.
“Yes mama.” Nilimjibu.
“Unahitaji kutembelea sehemu gani na kiasi gani kwa ajili ya safari yako.” Furaha iliyonijia nilitamani kuruka ruka ila nilijizuia.
“Napenda kutembelea Morogoro na kiasi chochote tu.”
“Kuwa huru binti yangu nimeongea na baba yako vizuri kabisa amesema kipindi chote ulichokuwepo humu ndani umebadilika naona na akili yako pia imerudi tumekufungia sana ndani muda mrefu na saa hizi ni wakati wako wa kuwa huru popote utakapotaka kwenda utaenda sawa mwanangu, usiwe na shaka sema unahitaji kiasi gani?”
“Mama kwa kweli mimi chochote tu nitafurahi najua nyie ni watu mmetembea sana, mimi sijawahi kwenda hayo maeneo kwahiyo sijui ni kiasi gani, naweza nikakuambia kiasi gani halafu ikawa kidogo au nikakutajia kikubwa kuliko unachoweza kunipa.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mama alicheka.
“Taja hicho kikubwa ambacho sisi hatuwezi kukupa tutakupa hichohicho.” Nilicheka tu.
“Nipe laki saba mama.”
“Hakuna shida.” Nilishangaa sana.
Mama alienda na kurudi na kiasi chote cha fedha. “Utaondoka lini?” Aaah nitaondoka siku yoyote tu. “Ila nilipenda sana niende kesho kutwa.”
“Hakuna shida binti yangu kesho nitakukabidhi laini yako.” “Ahsante mama.”
Mama alitoka chumbani kwangu na kisha kuondoka, nilifurahi sana nilichagua nguo nzuri ambazo ningeweza kuzivaa katika safari yangu hiyo nilichukua begi langu dogo na kisha kupanga, niliweka kila kitu changu tayari.
Kesho yake haikukawia, mama alinipa laini, sikutaka kuongea na mtu yoyote niliweka simu yangu chaji na siku iliyofuata nilifanya safari yangu.
Niliondoka nyumbani saa kumi na mbili na nikapanda gari ya saa moja gari lilikuwa likielekea Ifakara safari ilikuwa ndefu na ya kuchosha, nilikuwa sijazoea kusafiri umbali mrefu kwa basi na katika barabara za vumbi nilifika Ifakara nikiwa nimechoka sana.
Sikujua hata wapi nilekee nilitoa simu yangu na kutafuta jina la Frank la haula halikuwepo.
Hata hivyo haikunisumbua kwasababu namba yake nilikuwa nayo kichwani nilibonyeza na kumpigia.
“God, is it you Sociolah?”
“Ni mimi Frank.”
“Nina malalamiko na wewe siku zote ulikuwa wapi?” Alianza kutoa malalamiko yake bila kuchoka.
“Frank stop please.” Alinyamaza.
“Niko hapa Ifakara niko Stand naomba uje unichukue nimechoka.” “Say what!!” Alionekana kushituka sana. “Ndiyo Frank fanya haraka.”
“Sociolah acha utani bwana.”
“Kweli kwanini nikutanie, naomba uje unichukue.” Hazikupita dakika nyingi alikuja.
Alifurahi sana kuniona alinikumbatia kwa nguvu zote.
“Sociolah kwanini umekuja bila kunitaarifu.”
“Hiyo ruhusa yenyewe kuipata ilikuwa shida. Nimekumisi sana Frank wangu ndiyo maana nimekuja.”
“Sociolah unajua mimi kule naishi na mama.”
“Kwani mama ndiyo atatuzuia tusiwe wote.” Nilongea.
“Hamna hali ya kule.”
“Frank umesahau kwamba ulinihaidi siku utanileta Ifakara au kwasababu nimekuja mwenyewe ndiyo umechukia hutaki nifike kwenu niambie kama hutaki nirudi Dar sasa hivi.”
“Hapana lakini isingekuwa vizuri kama nitakupeleka kuishi mazingira kama yale. “Mimi mwenyewe nimekuja nimeamua kuja wewe twende vingine tutajua huko huko.” Tulichukua Taxi na kisha kuelekea maeneo ambayo Frank alikuwa akiishi. Alikuwa akiishi maeneo ya mtaa wa Pogoro.
Maeneo hayo yalikuwa machafu na yenye msongamano wa watu. Kadri tulivyokuwa tukikaribia kwao nilianza kuona ugumu wa kuishi huko hata hivyo maji nilisha yavulia nguo sikuwa na budi kuyaoga. Safari iliishia kwenye nyumba chakavu sana.
Nyumba iliyojengwa kwa matofali ya kuchoma ambayo haikuwa na sakafu ndani yake. Ilikuwa na vyumba vitatu na sebule ambayo haikuonekana kama sebule. Ndani ya sebule hiyo kulijazwa ndoo za maji, meza chakavu na baadhi ya vyombo vichache huku baadhi ya picha zikining’inia ukutani.
Kulikuwa na viti vya mbao ambavyo vingemuumiza makalio ya mtu ambaye angekalia.
Mazingira kwa ujumla yalikuwa machafu, choo kilikuwa nje, na hakikufaa kabisa kwa matumizi ya binadamu kilikuwa choo cha shimo na mimi nilikuwa nikiogopa
sana kutumia vyoo vya shimo uwanja ulikuwa umezungushiwa kwa makuti na hapo ndipo Frank alikuwa amekulia kwa kuwa ni mahali ambapo Frank alikuwa akiishi sikuona shida.
Gari lilipaki mbele ya nyumba na kisha Frank alinishusha alinisaidia kubeba kibegi changu kidogo na kisha kuelekea ndani. Hakukuwa na mtu ndani hapo.
Aliniingiza moja kwa moja hadi chumbani kwake kulikuwa na kitanda chakavu cha futi nne kwa tano. Meza ndogo ambayo juu yake kulikuwa kuna taa aina ya kibatari ,kiberiti, peni na baadhi ya vitu vidogovidogo. Ukutani kulikuwa kuna misumari iliyokuwa imetundikwa nguo ambazo zilionekana kuwa ni za Frank. Kulikuwa na masufuria makubwa ambayo ndani yake kulionekana kuwa na maji.
Pamoja na ndoo.
Frank alinikaribisha ndani ya chumba hicho sikuona sehemu ya kukaa isipokuwa kitandani, nilikaa.
“Frank unahofia kufika kwenu.”
Wala hakutabasamu kama alivyozoea alikuja kukaa pembeni yangu. “Sociolah unaweza kuishi katika mazingira kama haya.”
Nilivua viatu na kujilaza kitandani huku nikitabasamu wala hata sikumjibu.
“Nimechoka Frank nahitaji kwanza kwenda kuoga.” Alitoa macho.
“Nini nipeleke nikaoge bwana.” Nilimuambia.
“Hamna shida.”
Nilifungua begi langu na kutoa kanga mbili nikajifunga na kisha kuelekea bafuni. Bafu ambalo lilikuwa limetengenezwa kwa makuti, ni choo kilichokuwa kimetengenezwa kwa matofali ambacho juu kilikuwa akijaezekwa na bafu hilo lilikuwa limewekwa matofali chini na lilioneka kuwa limechakaa sana na halikuwa zuri kiafya.
Nilioga kana kwamba sioni nilirudi chumbani nikamkuta Frank akiwa amesimama nahisi akiwaza cha kufanya.
“Nini unawaza?” Nilienda huku nikijaribu kumkumbatia kwa nyuma. “Hakuna shida.”
“Mama atarudi muda wowote ule na pia wadogo zangu wapo shule.”
“Natamani sana kuwaona mpigie mama simu muambie awahi kurudi kwani yuko wapi?”
“Aanh yuko kwenye majukumu yake.”
“Hakuna shida akirudi atakula nini?”
Alinyamaza kimya.
“Sitaki kuamini kwamba unasubiri mama aje ndiyo apike acha tabia mbaya twende jikoni.”
Tulitoka hadi nje kulikuwa na kibanda kilichokuwa kimeezekwa kwa majani na palikuwa na mafiga yaliyokuwa meusi na pembeni yake kulikuwa na mfuko mdogo uliokuwa na mkaa mchache ambao haukutosha kupika.
“Frank kuna nini cha kupika.”
Frank alibaki akiniangalia.
“Unaniangalia kana kwamba hunijui mimi ndiyo Sociolah.” Nilimuambia huku nikicheka. Nilifungua wallet yangu na kisha kutoa noti mbili za elfu kumi. “Kanunue mchele wa kutosha, kanunue na nyama na maharage na mboga yoyote ya majani na mafuta na vitu vingine ambavyo havipo, mimi leo sitoki nimechoka.” Nilivuta mkeka na kisha kukaa chini.
Frank aliondoka na baada ya dakika chache alirudi na vitu nilivyomuagiza nilianza kupika kwenye jiko la kuni.
Ilikuwa ngumu sana kwasababu hata kupika kwenyewe nilikuwa sijui vizuri lakini nilijitahidi kwa nguvu zote ili mama atakapokuja afurahie chakula changu.
“Frank tunakula au tunamsubiri mama?” Nilimuuliza mara baada ya kukamilisha mapishi yangu.
“Mimi nina njaa Sociolah.” Aliongea huku akicheka. “Lakini Frank unaonekana umepoteza kabisa amani yako.” “Napotezaje wakati nipo na mke wangu pembeni.” Nilicheka sana. “Hakuna shida.”
Tulikula huku tukiwaachia watu wa pale nyumbani chakula kilichobaki.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Tulikaa na baada ya muda mlango ulifunguliwa.
Wakati huo tulikuwa tumekaa mkekani mlango wa mbele ulifunguliwa.
“Frank.....” Sauti ya mwanamke iliita.
“Frank mama amekuja.”
Frank alinyanyuka na kisha kwenda.
Nilinyanyuka na kumfuatia kwa nyuma mama alikuwa amebeba mzigo mzito kichwani, mizigo ambayo ilikuwa ndani ya ndoo nilishindwa kujua ni nini alimpokea na kumtua mzigo ule.
Mama alionekana kuchoka sana nilimkimbilia na kisha kumshika na kumsaidia kumkalisha kwenye viti vya mbao ambavyo vilikuwa pale sebuleni.
“Ahsante.” Alijibu kwa pole na kisha kunitazama.
“Karibu.” Aliniambia huku alimuangalia Frank.
“Frank huyu ndiyo Sociolah?”
Nilishan gaa kujua mama mtu ananijua.
“Yeah mama ndiyo huyu.”
“Mbona amekuja bila taarifa si angesema anitaarifu nimuandalie chakula jamani.” “Hakuna shida”
“Acha nikakuandalie chakula.”
Mama alitaka kunyanyuka.
“Usijali mama nimeshaandaa.”
Nilijibu.
Ngoja nikuwekee chakula ule au nikuchemshie maji.” Alinitazama huku macho yake yakionesha upendo mwingi. “Usijali mwanagu nitaoga tu maji ya baridi.” “Maji ya moto ni mazuri mama.”
“Hakuna shida.” alinyanyuka huku akionekana kupata nguvu mpya.
Alioga na kisha kupata chakula huku akinisifia kuwa chakula kile kilikuwa kitamu sana.
Baadae familia nzima ilirudi ilikuwa ni familia ndogo tu tulijumuika pamoja na kisha kupata chakula cha usiku. Ilionekana tayari walikuwa wakinifahamu hivyo haikuwa na haja ya utambulisho ilionekana ni familia ya kimasikini lakini yenye upendo mwingi.
Tuliongea mambo mengi tulicheka ulikuwa ni wakati mzuri sana katika maisha
yangu yote niliyowahi kupitia nilifurahia sana kuwa pamoja na familia ya Frank.
“Mwanangu....” Mama aliniita siku moja.
“Unampenda Frank?” Aliniuliza.
“Ndiyo mama nampenda sana.”
Kwanini umeuliza?
“Kama unampenda changamoto zitakazokuijia ni nyingi sana, nakushauri mwanangu usikate tamaa endelea kumpenda kwa moyo wote.”
Aliongea mama Frank huku uso wake ukibadilika kutoka kwenye mtu mwenye furaha hadi kwenye nyuso ya huzuni.
“Mama.” Nilimuita huku nikisogea karibu yake.
“Nampenda sana Frank na kati ya watu wote nimeamua kumchagua yeye sitojali ni nini tunapitia, sitamuacha Frank.” Alicheka. “Usijali mwanangu.”
Alitabasamu kwa huzuni.
“Mama itakuaje na Frank naye akiniacha.” Aligeuka.
“Eenhe Frank kanijia hapa kama amechanganyikiwa Sociolah….. Sociolah….
Sociolah, Sociolah ataniacha mimi mpaka analia.” Mama yake aliongea, nilicheka. “Kweli Frank huwaga analia?”
“Mimi nilikuwa sijawahi kumuona ndiyo kwa mara ya kwanza kumuona analia.” Nilicheka sana.
Na hivyo ndivyo siku zetu zilivyokuwa na mwisho wa siku baba alinipigia simu. “Sociolah mwanangu tumekumisi tunaomba urudi nyumbani.”
“Baba nafurahia sana kuwepo huku baba natamani kuendelea kuwepo zaidi nimewamisi sana pia naomba uniongezee wiki moja tu.”
“Hapana mwanangu wiki moja ni nyingi zaidi naomba urudi nyumbani.” “Nitarudi baba wala usijali.”
“Sawa.” Baba alikata simu lakini alionesha kutokuridhika.
Niliendelea kukaa na Frank Ifakara na familia yake walinipenda sana nilifanya kazi zote za nyumbani ambazo hata kwetu sikuweza kuzifanya. Nilipika, nilifua nguo za familia, nilifanya usafi, nilienda shamba, nilienda kazini kumsaidia mama kuuza vitu sokoni na kufanya shughuli nyingine ndogondogo.
Watu wengi walikuwa wakinishangaa kwa maana sikuonekana kufanania na hali hiyo, hata hivyo Frank alikuwa akijisifia sana na alipenda kutembea na mimi hicho kitu ndicho kilikuwa kikinipa amani sana nilijiona kupendwa sikujali hali ya maisha ilivyokuwa.
Kwa siku chache tulizokuwepo familia ilianza kupendeza.
Tuliweza kula chakula kizuri na hata mavazi pia yalikuwa mazuri mama yake alinipenda sana.
Alinitembeza sehemu mbalimbali za Ifakara tulienda maeneo kama daraja la mto Kilombero ambalo ndiyo kwanza lilikuwa limeanza kujengwa tukaenda na maeneo mengine mazuri ya kuvutia hakika nilijisikia faraja sana hasa kuwa pembeni yake.
Mara kwa mara mama yangu alikuwa akinipigia simu. “Mwanangu tumekumisi tunaomba urudi nyumbani.” “Nitarudi mama wiki hii haiishi lazima niwe nimerudi.”
Niliendelea kuwatia moyo ingawa ilikuwa bado sikufikiria kurudi nyumbani. Ilikuwa ni jioni ya siku moja tulikuwa tumekaa kwenye mkeka, Frank akiwa amejilaza huku kichwa chake akikiegamia katika mapaja yangu. Mama yake alikaa pembeni akisuka ukili, wakati wadogo zake wawili wa Frank, Furaha na Fiona walikuwa wakicheza karata.
Ilikuwa ni usiku mara baada ya kupata chakula cha jioni kwa vile nyumba ya kina Frank haikuwa na umeme tulikuwa tukikaa nje kwenye mbalamwezi tukingojea muda wa kulala.
Nilikuwa nikichezea nywele za Frank wakati simu yangu ilipoita, nilipotazama alikuwa ni baba.
“Pokea simu.” Frank aliniambia.
“Ni baba huyo.”
“Pokea.”
Kila mtu alitega sikio kusikia, nilipokea.
“Haloo baba shikamoo .”
“Sociolah utani na wewe sasa umekwisha muda wa kurudi nyumbani umefika nimekufungia ndani kwa muda mrefu ili ujirekebishe lakini umeonekana bado hujajirekebisha umeshakaa sana na huyo mtu wako sasa ni muda wa kurudi nyumbani usitegemee kwamba mimi ningekuwa mjinga kiasi hicho kuamini kwamba uko mikumi, uko sijui udzungwa unatalii, ninafahamu fika kwamba uko Ifakara naomba kesho ifikapo saa kumi na mbili jioni ufike hapa nyumbani sihitaji maelezo.”
“Baba….” Simu ilishakatwa.
Mchanganyiko nilioupata kwenye akili yangu sikuwahi kuupata siku zote za maisha yangu yaliyopita, nilishindwa cha kuongea machozi yalinitiririka bila kukoma.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Vipi?” Mama Frank aliniuliza, nilishindwa cha kuongea.
Frank alininyanyua na kunipeleka chubani, uso wangu wote ulikuwa umejawa na furaha sasa hivi ulitawaliwa na huzuni. Machozi yalienea kila kona, uso wangu ulipambwa na michirizi ya machozi kana kwamba ni eneo ambalo mto unaanzia.
“Baba anataka nirudi kesho.”
“Aaah Sociolah tumekaa hapa kwa muda wa wiki moja na nusu, you go back home soon I will be back, likizo yenyewe imeshakaribia kuisha wala usijali.” “Nisijali nini Frank? Siwezi kukaa mbali na wewe.”
“Sociolah lazima uangalie hali ya mazingira jinsi ilivyo ukileta ubishi baba anaweza kuzuia hata baadae nishindwe kuishi na wewe please naomba urejee nyumbani.”
Huku nikilia nilikubali kwa shingo upande.
Nilianza kupanga vitu vyangu wakati huo Frank alienda kuwapa taarifa familia yake wote walipatwa na huzuni sana sikuwa na jinsi siku iliyofuata nilirejea Dar es salaam.
Niliogopa sana kufika nyumbani kwani baba alikuwa tayari alikuwa akifahamu nilipokuwepo hata hivyo nilijipanga kupambana naye.
Nilipofika nilipokelewa vizuri na familia yangu yote hata baba alionekana kunifurahia sana.
Pink na Pinto waliniambia kuwa walinimisi sana na walikuwa na wakati wa huzuni sana kuwa mbali na mimi.
Amani ilirejea ndani ya yumba yetu sikuwa nikifungwa tena wala kubanwa mwisho wa siku likizo iliisha na nilirejea chuoni.
Siku ya kwanza mama alinipeleka chuoni mwenyewe kwa gari. Sikutaka kuuliza ni lini nitaenda bwenini kwetu niliamua kunyamaza kimya nione nini kinafuata. Wakati tuko njiani tunarudi mama aliniambia.
“Sociolah lini unarudi bwenini kwenu?”
“Aanh nilikuwa napanga kwenda kesho mama.” Nilimuambia.
“Basi hakuna shida una kipindi saa ngapi?”
“Nina kipindi saa tatu.”
“Basi asubuhi utaenda Mabibo halafu utatokea kule kuja chuoni.” “Sawa mama.” Niliongea kwa furaha sana.
Hata hivyo nilivyokumbuka hali yangu na Melania furaha yangu ilitoweka ghafla.
Siku ya kwanza Frank hakuwepo.
Ilipofika siku ya pili mama alinipeleka bwenini kwetu.
“Mimi nina safari ya kwenda mjini Kariakoo kwahiyo sidhani kama nitakupeleka chuoni, wewe nenda mwenyewe nadhani unaweza kila kitu na hakuna shida yoyote ukihitaji pesa niambie hakuna shida.”
Mama aliniambia, aliondoka na kuniacha.
Nilitoka moja kwa moja hadi chumbani kwa Frank niliwakuta wote wakiwa wamesimama wanaongea huku wakicheka kwa sauti. Nilipoingia Frank alijongea karibu yangu na kunikumbatia na kisha akanibusu kidogo mdomo nilihisi aibu mbele ya marafiki zake.
“Karibu mke wangu, karibu malkia.”
“Ahsante.” Nilisema na kwenda kukaa kitandani.
“Sociolah kuna kadi ya mualiko hapa imetufikia tunataka kwenda kwenye sherehe mwisho wa wiki, utakuwa pamoja nasi?”
“Sherehe ya nini?”
“Huyu hapa rafiki yetu Innocent amepewa kadi ya mualiko kuhudhuria tukio fulani
hivi. Baba yake mdogo anamiliki kampuni, kampuni yao inatimiza miaka mitano
kwahiyo wanafanya anniversary.”
“Frank utaenda?”
“Ndiyo nitakuwepo.”
“Na mimi nitaenda.”
“Nitafurahi sana kuwa na wewe sociolah.” “Woow tutaenda na malkia.”
Watu wote waliokuwepo kwenye kile chumba walifurahia sana kwamba
ningeungana pamoja nao.
Innocent naye alifurahi sana.
“Mimi ndiyo maana nakukubali sana sociolah yani ni msichana ambaye uko
kipekee sana.”
“Wala hata usijali.”
Nilimpigia mama simu na kumpa taarifa ya kuhudhuria kwenye sherehe hizo na yeye bila hiyana aliniruhusu na aliniambia kwamba angemuambia baba.
Siku ya ijumaa niliondoka na Frank hadi Mlimani City kwa ajili ya kuchagua nguo za kuendea kwenye sherehe hiyo.”
Nilichagua gauni jeupe zuri na yeye nilimchagulia shati jeupe ambalo kwa pamoja tulionekana kufanana tulipojaribu nguo zetu tulionekna kufanana sana.
Hatimaye siku ya sherehe ilifika nilijiandaa mapema na mpaka kufikia saa kumi na moja nilikuwa tayari. Nilijipulizia manukato yanayonukia sana.
Nilitoka moja kwa moja na kuelekea chumbani kwa kina Frank niliwakuta wote wakiwa tayari wakinisubiri mimi.
“Madam tulijua utachelewa bwana.”
“I am always punctual.” Niliwaambia.
“I can see, kweli Frank amepata mwanamke.” Niliachia kicheko kidogo na baada ya kuwasalimia nilielekea aliko Frank, nilimkumbatia na kisha tukaongea mawili matatu.
“Tuondokeni.” Innocent aliongea.
“Gari linatusubiri.”
Tulipanda kwenye gari na kisha safari ya kuelekea Serena hotel ilianza.
Njiani kulikuwa na kelele nyingi hata hivyo nilitulia nikiongea na Frank wangu kwa sauti ya chini sana wala sikushughulishwa na kelele zao.
Kwa takribani lisaa limoja tuliweza kufika Serena hotel.
Tuliingia moja kwa moja ukumbini na tayari shughuli ilikuwa imeshaanza.
Vinywaji vilikuwa vya kila aina.
Frank hakuzoea kutumia vinywaji vikali hivyo na mimi sikupenda kutumia kinywaji kikali siku hiyo niliamua kutumia vinywaji laini kama ilivyokuwa kwa Frank.
Tulikaa kwenye meza yetu iliyokuwa na wtu takribani sita huku tukiongea
maswala mbalimbali.
Ratiba ziliendelea kufuatwa.
Tulipata chakula kizuri na wakati shughuli ikielekea mwishoni kabisa walifungua muziki kwa ajili ya kucheza.
“Twende tukacheze.” Frank aliniambia.
“Unaweza…?” Nilimuuliza.
“Sasa kama ningekuwa siwezi ningekuita tukacheze, leo utajua kwamba nina kipaji
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
cha kucheza.”
“Hahaha..” Nilicheka.
“Ok twende ukanioneshe.”
Tulinyanyuka na kisha kuelekea katikati ambapo watu wengi walikuwa wakicheza. Tulianza kucheza waliweka mzika laini ambapo ulipendeza sana kucheza wapendanao.
Alinishika kiuno, akauchukua mkono wangu na kuugusanisha na wake na kisha tukaanza kucheza kama mara nyingi wafanyavyo wazungu, nilikuwa nikipenda sana kucheza hivyo na nilifurahia sana.
Tuliendelea kucheza huku nikizidi kuvutiwa na miziki hiyo, nilijikuta nikipoteza uwiano nilikuwa nikimtazama Frank moja kwa moja machoni kwake. Hisia zilinizidia nikajikuta nazidi kumsogelea usoni kwake hadi pua zetu zilipogusana.
Nilifumba macho kana kwamba ninayesinzia huku nikiwa tayari kwa kitu ambacho kilikuwa kikitokea katika sekunde moja iliyobakia.
Ghafla niliguswa begani nilifumbua macho haraka sana macho yangu yaligongana
na Frank ambaye alikuwa ameshikwa na mshituko, niligeuka haraka na
kumuangalia mtu ambaye amenishika nikiwa na hasira zote kwa kunikatishia
starehe yangu
La haula!!
Nilikutana moja kwa moja na baba, sikutaka kuamini macho yangu nilishindwa cha kuongea midomo ilibaki ikitetemeka tu huku nikihisi haja ndogo ingenitoka muda wowote ule.
Nilimuachia mkono Frank kana kwamba sikuwa naye aaanh maneno yalishidwa kunitoka.
”Aaanh sociolah na wewe umekuja?”
Nilipata nguvu ya kuongea.
“Ndiyo baba niko na marafiki zangu kutana na Frank ni rafiki yangu sana.”
Baba alimuangalia Frank, alimpandisha na kumshusha nilijua tu kesi yake siyo ndogo wala sikupaswa kupaniki nilimuacha baba afanye anavyotaka lakini nisingeruhusu avuke mipaka.
Alimpandisha na kumshusha na kisha alitoa mkono wake na kumshika. “Nimefurahi sana kukufahamu rafiki wa mwanangu mimi ndiyo baba yake na Sociolah.”
Frank hatimaye alipatwa na neno.
“Nashukuru kukufahamu pia.” Frank alijibu kwa sauti ya utaratibu. “Naomba nikuambie neno moja kijana wangu.”
Baba alimuambia Frank.
“Samahani Sociolah dakika moja.” Aliongea baba.
“Hakuna shida.” Alimvuta Frank na kisha kuelekea pembeni.
Waliongea kama dakika mbili tatu hivi na kisha Frank alitabasamu na kurejea pale tulipokuwepo.
“Sasa mimi nilikuwa naondoka kwa bahati nikakuona kwa mbali, si unarudi hostel mwanangu?” Baba aliniuliza.
“Ndiyo baba nimekuja na marafiki zangu wengi tu wengine wapo kule.” Niligeuka kana kwamba ninataka kuwaita.
“Aanh hakuna shida nitakutana nao siku nyingine, nimefurahi kumuona rafiki yako mmoja nafikiri ataenda kuwasalimia na wengine.”
Nilifurahi sana nikiamini kwamba baba hakuongea kitu kibaya na Frank kwa maana Frank naye alionekana kufurahia.
“Aaanh sawa baba siku uje ukutane na marafiki zangu wote hawajawahi kukuona walikuwa wakikusikia tu wanamjua mama lakini wewe hawakutambui baba.” “Usijali binti yangu nitakuja usipate shida.”
Nilifurahi sana kusikia hivyo.
Baba alichomoa kiasi cha pesa na kumpatia Frank, Frank alipokea kwa mikono inayotetemeka.
Sikutaka kuamini macho yangu ina maana baba amempenda Frank kiasi cha kumpatia hela.
“Sociolah uwe na usiku mwema binti yangu acha mimi niende nyumbani.” “Baba mbona mimi hunipi hela?” Niliongea kiutani.
“Hahaha….” Alicheka.
Tayari alikuwa ameshaanza kupiga hatua alirudi na kisha aliingiza mkono mfukoni na kunipatia kiasi cha pesa.
“Hakitoshi?”
“Kinatosha baba ahsante.”
“Aya sawa bai mwanangu.” Aliniaga na kisha akamuaga Frank.
“Bai mwanangu mwingine.” Akaondoka.
Kwa kweli nilitamani kujua baba alimuambia nini Frank. “Frank baba amekuambia nini?” Nilimvuta pembeni. “Niambie basi Frank wangu.”
“Subiri Sociolah usiwe na haraka nitakuambia turudi hostel halafu nitakuambia usijali, sawa mama.”
“Ok, yani najikuta tu siwezi kuvumilia kukusikia natamani kusikia kitu ambacho
baba amekuambia.”
“Usijali utanisikia.”
Tuliondoka tulipanda kwenye gari na kisha safari yetu ya kuelekea Mabibo ilianza. Frank aliniambia kwamba ana usingizi hivyo asingependa kusumbuliwa, alilala na mimi nikamlalia kifuani kwake wala hatukujua safari yetu ilichukua mda gani lakini mwisho wa yote tulifika Mabibo.
Ilikuwa ni usiku wa saa saba tusingepata muda wa kuongea Frank aliniahidi kwamba tutaonge keso.
“Relax mama uwe na usiku mwema.” Alinibusu kwenye papi za mdomo na kisha kuondoka nilienda chumbani kwangu nikiwa na furaha zote.
Nilikuta watu wote wamelala kwa vile nilikuwa nimechoka sana na mimi niliingia kitandani kwangu kulala.
Asubuhi ya siku hiyo aliamka Melania akiwa na furaha sana hata alinisalimia. Nilishangaa Melania ananisalimia kuna nini kimetokea lakini ghafla nilikumbuka kumtafuta Frank wangu nilitaka niamini kama kweli Melania ana nia ya dhati ya kutaka kurudisha urafiki wetu.
Nilimpigia simu Frank.
“Heloo… Heloo…. Baby.”
“Heloo…” Frank alipokea.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Aaanh nataka uniambie ni nini umeongea na baba jana.” “Sociolah siwezi kukuambia kwenye simu njoo chumbani kwetu.” “Ok five minutes niakuwa hapo.” Niliongea. “Hakuna shida.”
Nilijiandaa haraka haraka niloga na kupiga mswaki na kuvaa mavazi mazuri na kisha kujipulizia marashi yaliyokuwa yakinukia sana. Nilijipodoapodoa kidogo na kuhakikisha uso wangu upo vizuri.
Baada ya hapo nilipiga hatua za kivivu na kuondoka kuelekea chumbani kwa kina Frank.
Frank alikuwa bado hajaondoka alikuwa kitandani, alikuwa kifua wazi huku amevaa kaptula fupi. Nilienda pale kitandani na kumlalia.
Watu wengi chumbani kwao walikuwa wameondoka wengi walikuwa wameenda kanisani hivyo kumfanya abakie peke yake chumbani pale. Nilipata wasaa wa kujiachia.
“Eenhe niambie jana baba alikuambia nini maana ulifurahi siyo kitoto.” “Oooh…..” Alivuta pumzi ndefu huku akiachia tabasamu.
“Sociolah nimefurahi sana kukutana na baba yako na huwezi amini baba amesema.”
Simu yangu iliita na alikuwa ni baba aliyepigia simu, nilipokea huku nikimnyamazisha Frank asiendelee kuongea.
“Haloo..” Nilisema mara tu nilipopokea simu.
Baba wala hakunipa muda nivute pumzi alianza kueleza alichokuwa akitaka kuniambia.
“Sociolah unafikia hatua ya kutudharau, hata kutusahau familia yako kwa sababu ya huyo Matranka una akili kweli Sociolaha.”
“Baba....” Niliongea, alinikatisha.
“Sitaki kusikia kuhusu huyo mtu wako na ukitaka ujue upande wangu wa pili endelea kuwa naye, hakufai huyo mwanangu kuna watu wazuri tu ambao wanaweza kukufaa tena kulingana na hadhi yako kwanini umng’ang’anie huyo Matranka, sasa sitaki kusikia ujinga wa aina yoyote ile na wala sitaki kusikia kitu chochote ambacho unataka kuniambia simtaki huyo mtu na sitaki uendelee kuwa naye nafikiri nimeeleweka.”
Alimalizia na kisha kukata simu.
Nilishindwa nini cha kuongea nilimtazama Frank ambaye hakuwa akielewa nini kinaendelea, nilishangaa ni kitu gani ambacho baba alimuambia Frank.
“Frank baba alikuambia nini jana?”
“Aaanh Sociolah.” Aliongea huku akitabasamu wakati huo uso wangu ukiwa umehamanika sana.
“Baba aliniambia amenipenda mno na atafurahi sana kama nitakuwa mkwewe kwahiyo nina asilimia zote za kuja kukuoa Sociolah nimefurahia sana.”
Nilimuangalia kana kwamba ninamshangaa nilinyanyuka haraka na kukusanya vitu vyangu na kisha kurudi chumbani.
Niliingia moja kwa moja na kujitupa kitandani Melania aliachia kicheko cha nguvu. Nililala huku nikilia, machozi yalinibubujika nililia kwa sauti ya chini mpaka nikashindwa tena kujizuia hakuna aliyejishughulisha kuja kunipa pole, siyo Melania siyo Monika wala Fetty.
Roho iliniuma sana ni kitu gani ambacho kinafanya Frank anidanganye kwanini asiniambie ukweli, anafikiri anaweza kunificha hali kama hii. Nilitegemea Frank angekuja muda wowote hata hivyo hakuja.
Nililia hadi nilipopitiwa na usingizi nilipokuja kuamka nilisikia Fetty na Monika wakiwa wanaongea.
“Haiwezekani hii vita lazima tutashinda wote.”
“Siwezi kuruhusu kila mtu anamtaka hapa lazima tumpate wote.” Aliongea Fetty kwa hasira.
“Hata mimi siwezi kukubali mtu mwenyewe wa kumuiba tutampata wote.” Nilishitushwa sana na mazungumzo yao nilinyanyuka kuonesha kama vile nilikuwa macho na nilikuwa nikiwasikia.
Fetty aliachia msonyo wa hali ya juu nilibaki nimeshangaa huku nikichanganyikiwa na nafsi yangu vituko nilivyoviona hapo nilishindwa kuvihimili. Ilikuwa ni siku ya jumapili jioni niliamua tu kurudi nyumbani nilienda moja kwa moja mpaka chumbani kwangu na kujifungia.
Nilipitiwa na usingizi mzito sana hakuna aliyeniona wakati nikiingia.
“Mama.... Chumbani kwa dada Sociolah kumefungwa kwa ndani.”
Nilisikia sauti ya Pink.
“Nani kafunga kwa ndani? Nani ameingia sasa?”
“Mimi sijui.”
Nilishitushwa kutoka usingizini na majibizano yao yaliyokuwa yakiendelea pale mlangoni.
Nilinyanyuka na kisha kwenda kufungua mlango.
“Shikamoo mama.” Nilisalimia kiuchovu.
“Kuna nini?”
“Hamna kitu.”
“Leo jumapili unarudi huku?”
“Mama najihisi kuumwa.”
“Unaumwa nini?”
“Hata sijisikii vizuri.”
“Pole twende ukapumzike basi.”
Baba alitoka chumbani kwake na kisha akasimama mlangoni akituangalia.
Mama alianza kumuelezea shida niliyokuwanayo.
“Sociolah anajihisi kuumwa ndiyo maana amerudi nyumbani.” Baba hakujibu lolote alitembea moja kwa moja kuelekea sebuleni. Mama alibaki ameshangaa kuna nini jamani mbona siwaelewi.
Alinirudisha chumbani kwangu na kisha kunilaza kitandani kina Pink walikuja kukaa pembeni yangu.
“Pumzika mama ngoja nikakuandalie chakula sawa.”
“Sawa.” Niliitikia kinyonge nilishindwa kujua nini kinaendelea.
Usiku huo ulipita wala sikupokea simu ya Frank.
Nilikaa nyumbani takribani siku tano wala simu yangu sikuona meseji wala simu. Nilikuwa nikimuona WhatsApp akiwa hewani lakini bado hakunitumia meseji ya aina yoyote.
Moyo wangu uliugua sana ndani nilishindwa kujua. “Kwani nimemkosea nini Frank kwanini ananifanyia hivi.” Wiki iliisha wala sikupokea simu yake.
Wakati huo Kelvin ndiyo alikuwa mfariji wangu, mara kwa mara alikuwa akija nyumbani kunitembelea na kunijulia hali.
Alikuja mara nyingi wazazi wangu wakiwepo na hata wasipokuwepo.
Tulikaa pamoja tukiongea mengi, alinisimulia mengi kuhusu maisha yake nilijua vitu vingi sana kuhusu yeye zaidi ya yote nilimuamini sana nikamuelezea shida zangu.
Alinishauri mambo mengi kuhusiana na mahusiano yangu nilijikuta namuamini sana.
Siku moja jioni baada ya Kelvin kuwa ameondoka nyumbani nilikaa nikicheza na wadogo zangu wakina Pink hadi waliponiudhi.
“We dada Matranka yuko wapi, yule anko wa siku ile tuliyemkuta kule ufukweni yuko wapi siku hizi mbona hatumoni.”
“Kwani ulienda kwake ukaambiwa hayupo.” Nilimjibu.
“Kwani si alikuwa akikupigiaga pigiaga simu kila siku my oga my oga mbona siku hizi hatumuoni.”
Nilifungua sehemu ya kuhifadhia picha na kuitafuta picha ya Frank na kumuonesha.
“Aya huyu hapa muangalie, umefurahi?”
Nilipoiangaliea ile picha mimi mwenyewe nafsi iliniuma.
“Aya ondokeni.”
“Sasa dada nini jamani....”
“Toka sitaki kuwaona.”
Nafsi iliniuma sana lakini niliapa kwamba sitalia.
Pink na Pinto waliondoka na kuniacha peke yangu nilienda kufunga kabisa mlango kwasababu sikutaka kusumbuliwa.
Nilirudi na kisha kuchukua simu yangu na baadhi ya vitabu nikisoma hadithi huku simu yangu ikiwa pembeni.
Ghafla niliijiwa na wazo nilifungua simu yangu na kisha kuelekea upande wa WhatsApp nikitaka kuweka status mpya.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilivutiwa kuangalia status ambayo Melania alikuwa ameweka kiasi kama cha dakika moja iliyopita.
Nilipofungua sikutaka kuamini kilichokuwa kikionekana pale, ilikuwa ni picha ya Frank huku akisindikizwa kwa maneno “HATIMAYE SASA UMEKUWA WANGU NITAKUPENDA SIKU ZOTE.”
Sikutaka kuamini nilichokuwa nikikiona niliamua kwenda kuangalia na status ambayo ilikuwa imewekwa na Frank.
Niliona ni picha ya Melania lakini haikuwa na maelezo yoyote.
“Mungu wangu!!”
Nilihisi kiza kizito.
Nilikuja kufumbua macho nilikutana na sura sizizopungua tatu zikiniangalia kutokea juu.
Nilishindwa kujua ni mahali gani.
Nilikuja kugundua ni baba, mama, Kelvin, dada Linah huku Pink na Pinto walionekana kuwa na nyuso za huzuni.
Nilikuwa pale pale kitandani kwangu nilipokuwa nimejilaza.
Nilishangaa sana wameingiaje na nilifunga mlango kwa ndani.
Mama uso wake ulionekana kuwa na huzuni sana. Nilipofumbua macho baada ya dakika kadhaa baba alikuwa akiniangalia kwa chuki sana alinyanyuka na kuondoka kisha kuelekea sebuleni.
Mama alimtazama Kelvin na kisha kumuambia.
“Naomba ukaongee na baba yako.”
Kelvin aliondoka.
“Pink, Pinto...” Mama aliwaita walibaki wakimtazama, aliwaangalia tu kana
kwamba hana cha kuwaambia.
Alimgeukia dada wa kazi Linah.
“Wachukue hao wapeleke chumbani kwao na wewe pia ukapumzike.” Nilishindwa kujua saa hiyo ni saa ngapi kichwa kilikuwa kikiniuma sana. Mara baada ya wote kuondoka mama alienda kufunga mlango. “Mmeingiaje chumbani kwangu na nilikuwa nimefunga mlango mama?” Nilimuuliza.
“Kwanza pole binti yangu, nini kimekukuta?”
“Sijui mama, nilikuwa nimelala na nilikuwa nimefunga mlango chumbani kwangu.”
Mama aliniangalia huku akinisikitikia.
“Sociolah ulipiga kelele ndiyo maana tulikuja, kwa bahati mbaya tulikuta mlango umefungwa ilibidi tuvunje mlango na kuingia ndani tukakukuta huna fahamu. Tunashukuru jitihada za Kelvin zimekusaidia kuweza kuamka. Kwa bahati nzuri wakati ulikuwa ukipiga kelele ndiyo kwanza alikuwa amefika. Unajisikiaje saa hizi mwanangu?”
“Mama kichwa kinaniuma sana.”
“Hebu niambie mwanangu ni nini kimekukuta.”
Nilianza kufikiria ni nini kilichokuwa kikipita katika akili yangu kabla sijafikia hatua ya kupiga kelele, machozi yalianza kunitoka mfululizo.
Mama alinisogeza kwake na kunikumbatia na kisha akanifuta machozi.
“Naelewa binti yangu hizo zote ni changamoto za maisha naomba wala usiumie sana mwanagu utapata mtu atakupenda na atakuthamini hawa watu masikini ndivyo walivyo hawajuagi kurudisha shukrani tangu kipindi kile hana thamani yoyote ukampenda hivyo hivyo lakini bado ameshidwa kuthamini mapenzi yako akaamua kufanya vitu vya ajabu kama hivi na kumuumiza binti yangu, roho yangu, moyo wangu, kwa kweli sitamsamehe mimi naomba umsahahu kabisa uanze maisha mapya utapata mwanaume mzuri kabisa binti yangu.”
Mama aliongea maneno marefu ambayo yalikuwa yakizidishi uchungu moyoni mwangu sidhani kama nilikuwa nikimuelewa kwa wakati huo.
Kilichokuwa kikipita akilini kwangu ni usaliti ambao Frank amenifanyia. “Kwanini asingeniaga basi mbona ningemuelewa tu yani baada ya kukubaliwa na baba ndiyo apate jeuri ya kunisaliti? Hivi ni kweli huyu ni Franklin?”
Machozi yalinitoka, mama alinibembeleza hadi nilipopitiwa na usingizi. Nilipokuja kuamka ni asubuhi ya siku iliyofuata wala sikutaka kutoka kitandani kwangu.
Mtu wa kwanza kuja alikuwa ni Kelvin.
“Oooh bibie umeshaamka?”
“Ndiyo niko macho Kelvin.”
“Hakuna shida nimekuletea juisi sema hujapiga mswaki sikupi.” “Hahaha nitaenda kupiga niwekee hapo.”
“Hapana, hadi upige mswaki ndiyo nitakupa juisi yako.”
“Nini lakini si unipe tu kama umeniletea au kama hujaniletea basi chukua mwenyewe.”
“Ni ya kwako nimekuletea lakini kama hujapiga mswaki sitakupa nyanyuka ukapige mswaki.”
“Mimi siendi sasa na mimi.”
Niligeuka huku nikimuangalia, nilikuwa nikiitamani sana ile juisi hata hivyo sikujisikia kufanya chochote asubuhi ile.
“Basi hakuna shida mimi naondoka.”
Alinyanyuka na kuonesha kama anaondoka nilimvuta ule mfuko kwa bahati nzuri hakuwa amejiandaa kwa hilo tukio alidondokea moja kwa moja kitandani.
“Oooh pole, umeumia?” Nilimgusa kifuani.
Alionekana kuuhisi mguso wangu kwani aliachia tu mdomo huku akitoa macho na
kushindwa kuongea chochote.
Nilitoa mkono wangu haraka.
“Umeumia popote.”
“Hapana, kumbe Sociolah ni mchokozi hivyo.” Aliniambia.
“Si ukapige mswaki nikupe.”
“Bwana mimi naona uv ivu.”
“Twende nikupeleke.”
“Twende.”
Sikuwa na jinsi nilisimama alinipeleka mpaka bafuni aliniwekea mswaki wangu
dawa kwa ajili ya kusafisha meno yangu.
Niliendelea kusafisha meno yangu kiuvivu sana.
“Sociolah acha uvivu.”
Alishika mswaki wangu na kutaka kunisaidia kupiga.
“Hapana usijali nitapiga naacha uvivu.”
Niliongea huku nikijaribu kucheka.
Nilipiga mswaki na kisha aliniacha bafuni nioge.
Nilioga na kisha kutoka.
Nilimkuta amesimama chumbani kwangu nilikohoa kwa ishara kwamba nataka kuvaa hivyo anipishe.
Alitoka nje nilivaa haraka haraka na kisha nilifungua mlango alirejea. “Sasa nikumiminie juisi yako si ndiyo toto?”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Siku hiyo Kelvin hakuondoka nyumbani tulishinda siku nzima hadi wazazi
waliporejea.
Walitukuta bustanini.
0 comments:
Post a Comment