Search This Blog

Monday, October 24, 2022

NATAKA KUZAA - 4

 





    Chombezo : Nataka Kuzaa

    Sehemu Ya Nne (4)



    Nilioga na kisha kutoka.



    Nilimkuta amesimama chumbani kwangu nilikohoa kwa ishara kwamba nataka kuvaa hivyo anipishe.



    Alitoka nje nilivaa haraka haraka na kisha nilifungua mlango alirejea. “Sasa nikumiminie juisi yako si ndiyo toto?”



    Siku hiyo Kelvin hakuondoka nyumbani tulishinda siku nzima hadi wazazi



    waliporejea.



    Walitukuta bustanini.



    “Nimefurahi sana jamani, ahsante sana Kelvin kwa kumuangalia mwanangu.” “Aanh usijali mzee wangu tuko pamoja.”



    “Huyu arejee chuoni sasa ameshakuwa yuko vizuri.” Nilimuangalia Kelvin.



    “Wewe Sociolah hutaki kurejea chuoni?”



    “Hamna naenda, kwanini nisiende sasa hivi nimeshapona niko vizuri.” Ilipofika jumapili jioni nilijiandaa kwa ajili ya kwenda Hostel. Moyo wangu ulikuwa ukipiga kwa nguvu sana.



    Baba alionekana yuko bize akiandaa hiki na kile.



    Sikuwa na amani yoyote kurejea kule, sikutaka kuamini kwamba kungekuwa salama kwangu.



    Nilitembea kwa hatua za kiuchovu mara baada ya kushuka kwenye gari sikutaka mtu yoyote anipeleke.



    Nilitembea moja kwa moja hadi chumbani kwetu, mikono ilikuwa ikitetemeka na



    miguu yangu ilikuwa haina nguvu.



    Nilifungua mlango pole pole huku nikiingia.



    Nafsi yangu ilikuwa imegoma kabisa kuamini kama kuna usalama humo ndani.



    Mapigo ya moyo yalienda kasi nilihisi kupungukiwa na pumzi.



    Nilijikaza na kuingia ndani wala sekunde haikufika nilipoingia tu mashaka yangu yalithibitika.



    Niliporomoka moja kwa moja na kuelekea chini hata hivyo nilidakwa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilikuja kushituka baadae nikiwa hospitali ya chuo.



    Nilichanganyikiwa sana kujikuta niko hospitalini.



    Pembeni yangu alikuwepo nesi na pia niliweza kumtambua Kelvin. “Mungu wangu balaa gani tena hili!”



    Nilishindwa kuelewa.



    “Ameamka.” Kelvin alisema.



    Nesi alikuja harakaharaka.



    “Unajisikiaje saa hizi?”



    “Najisikia vizuri.”



    “Unaitwa nani?”



    Nilimtazama Kelvin nilihisi kusahau jina langu.



    “Naitwa nani?”



    “Aanh ok, endelea kupumzika.”



    Nililala huku nikiwa najiuliza maswali.



    “Naitwa nani mimi? Mimi?”



    “Naitwa nani?”



    Nilishangaa sana niliweza kumtambua Kelvin lakini nilishindwa kutambua jina langu.



    “Oooh My God!”



    Nilikaa hospitali kwa siku mbili mfululizo.



    Na baada ya hapo niliruhisiwa kurudi.



    Muda wote Kelvin ndiyo alikuwa akiniangalia nilimuomba sana asitoe taarifa nyumbani, baba angekasirika sana kwasababu kwanza angetaka kujua sababu ya kunifanya nizimie mara baada ya kufika hostel. Wala sikuwa tayari kusema nilichokikuta.



    Kelvin alinirudisha moja kwa moja hadi chumbani kwetu.





    Niliwakuta wanachumba wote wakiwa wamekaa huku kukionesha kwamba hakuna dalili ya amani.



    Alinileta mpaka kitandani kwangu akanikalisha huku akinionesha upendo wa aina yote.



    “Unajisikiaje sasa Sociolah?”



    “Najisikia vizuri tu.”



    “Mimi sitaki nikuache naona hali yako siyo nzuri.” “Aaanh niko salama wala usijali.”



    Niliongea huku nikionyesha kwamba sina usalama wowote.



    “Tell me exactly what happen Sociolah.”



    Niliona watu wakiwa wamevuta midomo sana, nadhani hawakutegemea kwamba kwa wakati huo mapema hiyo ningekuwa na Kelvin.



    Nafikiri kwa Melania kuweza kumchukua Frank ilikuwa ni dharau kubwa kwangu na aliamini kwamba nitaumia sana na hicho kitendo alichonifanyia lakini kuniona napata faraja kwa mtu mwingine nadhani ilimchukiza sana.



    Aliondoka kimya kimya wala hakuonesha dalili ya mazungumzo humo ndani kila mtu alinyanyuka na kuondoka tulibaki mimi na Kelvin.



    “Ulipokuwa unatoka pale siku tunakurudisha hostel na baba nafsi yangu ilikuwa inakataa kabisa kukuacha mwenyewe, ulivyokuwa ukishuka kwenye gari nilikuwa nikikuangalia kwenye kioo ulivyokuwa unatembea, niliamua kumdanganya baba kuna kitu nataka kuja na nilimuambia aende tu nitarudi mwenyewe nyumbani. Nilishuka kwenye gari na kisha kuja chumbani kwenu, nilisimama hapo huku nikikuona ukisita kufungua mlango na mara bada ya kuamua kufungua mlango uliingia ndani na kisha kudondoka. Nilikuwahi na kukudaka hakuna hata mtu ambaye alishituka chumbani kwenu, una nini na wanachumba wenzio? Leo umerudi baada ya kulazwa siku mbili lakini hakuna hata mtu ambaye anakupa pole, Kwanini?”



    “Haaa..” Nilivuta pumzi huku machozi tayari yakishaanza kunitoka. “Mimi sitaki ulie Sociolah sitaki ulie kabisa, niambie tatizo ni nini?” “Chanzo cha matatizo yote ni mahusiano yangu.”



    “Unataka kuniambia ni Frank ndiye ambaye amesababisha hali ya chumba kuwa hivi?”



    “Yes ni yeye.”



    “Oooh pole sana Sociolah, lakini usijali niko na wewe wakati wote ukinihitaji nipo.”



    “Ahsante Kelvin.”



    “Leo nitakaa na wewe mpaka jioni nihakikishe umelala.” “Sawa.”



    “Kwani ni kitu gani kilikufanya uanguke?” Aliniuliza.



    “Nilimkuta Melania na Frank humu ndani walikiwa kitandani wamelala.” “Walikuona?”



    “Hapana wote walikuwa wamelala usingizi sidhani kama walikuwa wakiniona.” “Aanh pole sana.”



    Aliendelea kunihudumia mpaka ilipofika saa tatu usiku nilihisi usingizi. Alinihadithia hadithi mbalimbali za kuchekesha wakati huo watu wote walikuwa wamesharudi hadi nilipopitiwa na usingizi ndipo alipoondoka.



    Niliamka asubuhi kiuvivu kwa ajili ya kujiandaa kuelekea chuoni, wenzangu wote walikuwa wameshaondoka.



    Nilifika kwenye kipindii kwa kuchelewa sana niliingia.



    Pale ambapo nilizoea kukaa kwenye viti vya mbele alikuwa amekaa Melania na pembeni yake Frank alikuwa amekaa Frank alikuwa bize sana kumsikiliza mwalimu.



    Huku Melania akionesha kila aina ya utundu kwa Frank watu wote darasani waligeuka na kunitazama hadi dokta Kiseyeye alinitazama huku akisita kuendelea kufundisha nilionekana kudhoofu na kutokuwa na Furaha. Innocent siku hiyo alikuwa amekaa nyuma kabisa.



    Nilipiga hatua za kivivu mpaka nyuma na kisha kukaa pembeni ya Innocent.



    Niliweka begi langu na kisha kulalia meza.



    Sikujua hata kipindi kimeisha saa ngapi ni Innocent ndiye aliyeniamsha alikuwa amesimama na msichana mmoja mzuri ambaye nilizoea kumuona hapo darasani wala sikuwahi kumjua alikuwa ni nani.



    “Amka Sociolah muda umeisha.”



    Niliamka huku nikifikicha macho nilikuwa na wimbi la usingizi.



    “Hujalala usiku?”



    Watu waliokuwa pembeni yangu walicheka.



    “Nililala.”



    “Sasa CR unasinzia darasani sisi wengine inakuaje?”



    Nilishindwa hata cha kujibu sikutamani kuongea na mtu yoyote hata hivyo sikuweza kuwakimbia niliamua kunyamaza kimya.



    “Mimi nakusalimia tu naona tangu umeingia unapiga mbonji darasani.”



    “Sijisikii kusoma leo.”



    “Si urudi.”



    “Hata kurudi pia sijisikii.”



    “Mmmh ok Sociolah nitakutafuta baadae sawa.” “Hakuna shida.”



    Aliondoka na kisha kumuacha yule msichana amesimama pembeni yangu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alikuwa muoga sana na alikuwa mrembo.



    Kwa mana alikuwa amegwaya tu asijue cha kuongea.



    “Vipi?” Nilimuuliza.



    “Safi, mambo?”



    “Poa.”



    “Sociolah.”



    “Eee..”



    “Naweza kuwa na wewe?”



    “Kuwa na mimi kiaje?”



    Alingata midomo huku akishangaa na kutoa macho.



    “Kuwa na mimi kiaje?”



    Nilimuuliza tena.



    “I mean twende tukanywe wote chai.”



    “Aanh hakuna shida twende.”



    Tulinyanyuka na kisha kuelekea.



    Nilipata faraja kwamba hatimaye nimepata mtu mtu wa kuwepo karibu yangu kwa maana kila mtu alionekana kunicheka na kunikebehi.



    “Si alikuwa anaringa, vizuri kula na wenzio bwana.” Tuliondoka hadi mgahawani. Niliagiza juisi tu.



    “Kwanini huli?”



    “Si ninakunywa.” Nilimjibu.



    “Halafu hata sijakujua unaitwa nani kila siku nakuona darasani sijajua kabisa wewe ni nani.”



    “Aanh mimi naitwa Christina.”



    “Oooh Christina nimefurahi sana kukujua.”



    Niliongea huku nikijitahidi kuonesha hali ya furaha ingawa sura yangu ilinisaliti. “Sociolah mimi nimekupenda muda mrefu tu lakini nilikuwa nashidwa kukuambia, nimekupenda kweli.”





    “Aah jamani Christina ahsante nimefurahi sana wala usijali.” “Lakini kuna kitu nitakuambia baadae sawa.” “Kitu gani?”



    “Nishakuambia baadae kwahiyo usubiri,”



    Tulitoka mgahawani tukiongozana huku tukiongea mambo mbalimbali.



    Tulitembea kwa hatua za kichovu mpaka tulipofika darasani.



    Nilimkuta mama akiwa ananisubiri.



    “Sociolah naomba nikupeleke nyumbani mwanangu.” “Kuna nini mama?”



    “Naomba nikupeleke nyumbani sawa.”



    “Mama sijamaliza vipindi.”



    “Nimesema naomba nikupeleke nyumbani, umebakiza vipindi vingapi?” “Vitatu.”



    “Panda kwenye gari twende.”



    Nilipanda kwenye gari na kisha kuelekea hostel za Mabibo.



    “Mama kwani huku ndiyo nyumbani?”



    Hakunijibu.



    Aliingiza gari moja kwa moja na kisha kwenda mpaka mbele ya bweni letu, alisimamisha gari.



    “Shuka.”



    Nilishuka.



    Tuliongozana mpaka chumbani kwangu.



    “Fungua mlango.” Nilifungua.



    Aliingia akachukua kiti, akapanda juu na kuvuta mabegi yangu mawili makubwa ambayo nilikuwa nikitumia kuwekea nguo zangu wakati nilipokuwa nikirudi nyumbani wakati huo yalikuwa tupu.



    Nilibaki nimesimama nikimshangaa mama nisijue nini anataka kufanya.



    Alivuta mabegi na kuyashusha chini.



    “Naomba funguo ya kabati lako.”



    Nilimpa alifungua kabati langu na kisha kuanza kutoa nguo huku akizirushia kwenye mabegi yangu.



    “Mama ni nini unafanya?”



    “Subiri utakuja ujue baadae.”



    Alirushia nguo zangu zote na vitu vyangu vyote vilivyokuwa kwenye kabati kwenye mabegi.



    Alifunga kabati, akafunga na mabegi yangu.



    “Kuna kitu chochote cha muhimu humu ndani ambacho unakihitaji zaidi ya hivi nilivyoweka?”



    Niliendelea kumshangaa.



    “Mama unafanya nini?”



    “Nakurudisha nyumbani najua huwezi kukaa hapa.” “Hapana mama mbona mimi nakaa vizuri.”



    “Sociolah usijitafutie matatizo yasiyokuhusu nimeshasema huwezi kukaa hapa na nina ushahidi kwamba huwezi kukaa hapa kwanini uishi katika maisha magumu kiasi hiki nakurudisha nyumbani utapata kila kitu unachokitaka lakini siyo kukaa hapa.”



    Nilishindwa kuelewa kama niko tayari kurudi nyumbani au bado ningependa kuendelea kukaa hapo.



    Hata hivyo niliona bora nikapumzike nyumbani endapo ningeona ugumu wowote ningeweza kurudi.



    “Lakini mama usikabidhi chumba change.” “Sawa nimekuelewa.”



    Alipakia kila kitu changu ambacho nilikuwa nikihitaji na chenye umuhimu na

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kisha tulitoka na kuelekea nyumbani.



    Wadogo zangu walifurahi sana.



    “Dada tulikuwa tunakumisi bora umerudi.” Pink alisema.



    “Nitaondoka mimi.” Nilitania.



    “Uondoke uende wapi hiloo umekuja na mabegi yako yote.” “Kwani unafikiri nikija na mabegi yote ndiyo siondoki?”



    Tuliendelea na utani mdogo mdogo na wadogo zangu. Nilijisikia amani sana.



    Jioni ya siku hiyo Kelvin alikuja.



    “Aanh Sociolah umehama hostel bila kuniambia.”



    “Hata sikutegemea kuhama mama kanihamisha tu ghafla.”



    “Sawa bwana nilikupitia pale twende kwenye sherehe ya rafiki yangu nikashangaa haupo.”



    “Si ungenitafuta kwenye simu kabla hujaja.” “Nilitaka kukusapraizi.”



    “Ulitaka kunisapraizi mimi halafu sasa imegeuka sapraizi kwako mwenyewe.” “Umeona eenh.”



    Tuliongea huku tukicheka.



    “Kajiandae basi.”



    “Ngoja nimpigie simu kwanza baba nimuage.” “Baba nimeshamuambia anajua.” “Aanh basi hakuna shida.”



    Nilienda nikatafuta nguo ambayo ilifanana na nguo yake ambayo aliyokuwa amevaa nilichagua iliyokuwa nzuri kabisa. Tulitoka na kisha kuelekea kwenye sherehe hiyo.



    Ilikuwa ni sherehe ya siku ya kuzaliwa ya moja kati ya marafiki zake.



    Niligundua kuwa Kelvin ana marafiki wengi tena ni watu wakubwa na wenye pesa zao.



    Rafiki yake huyo alikuwa akitimiza miaka kadhaa na alikuwa na mke mzuri na mtoto wao mmoja ambaye alikuwa bado mdogo.



    Wakati wapo mbele wakishukuru watu Kelvin aliwatazama kwa huzuni. “Una nini Kelvin mbona umepoteza furaha yako ghafla?”



    “Aanh hamna.” Alilazimisha kucheka. “Naweza kukuona wala usinidanganye hapa.” “Kweli Sociolah niko na amani kabisa.”

    “Mmh labda kama umeamua kunificha lakini kama unanificha na mimi nitakuficha



    vitu vyangu sawa.”



    “Natamani kuwa na familia.”



    Mwishowe aliamua kuongea.



    “Marafiki zangu karibia wote wana familia zao, baba alikuwa akinipigia kelele kila siku kuhusu swala la kuwa na familia nikiona marafiki zangu ile hamu ya kuwa na familia yangu na mimi inazidi najua siku nitakuwa nayo itakuwa furaha yangu kubwa sana nitaipenda na nitailinda kwa nguvu zangu zote.”



    Nilicheka.



    “Yani wewe unapoteza furaha kwasababu ya kutokuwa na familia, si nikuomba Mungu tu atakupa familia nzuri na imani utafurahia mwenyewe.”



    “Nasubiri sana na ahsante kwa kunipa moyo.” “Sawa tuwahi basi kurudi nyumbani.” “Ok.”



    Tulienda mpaka nyumbani.



    Alinisindikiza hadi mlango wa nyumbani kwetu.



    “Sociolah.” Aliniita.



    “Mimi sitaki kuingia na mimi nataka niwahi nyumbani kweli nimefurahia sana



    kampani yako leo.”



    “Hakuna shida.”



    Alinishika kiuno na kisha kinivuta nilishangaa ni kitu gani ambacho anataka kukifanya.



    Alinivuta hadi nilipofika karibu yake kabisa.



    Nilikwepesha uso wangu na kisha kumuegamia begani, sikutaka kitu ambacho alitaka kufanya kitokee.



    Baada ya hapo aliniachia na kisha kunitazama nilijilazimisha kutabasamu.



    “Uwe na usiku mwema.”



    “Ahsante.”



    Aligeuka, nilimtazama mpaka alipoishia getini nilifungua mlango na kuelekea ndani.



    Baba alikuwa bado hajalala.



    “Habari za kwenye sherehe mwanangu.”



    “Salama tu nimefurahia.”



    “Kelvin alikuacha urudi mwenyewe?”



    “Hapana baba ameishia hapo nje.”



    “Aanh ningemtafuta usiku huu.”



    “Usimsumbue baba amechoka ndiyo maana nimemuambia aende.” “Hakuna shida kapumzike sasa binti yangu.” “Ahsante baba.”



    “Usiku mwema.”



    “Usiku mwema pia.”



    Niliondoka na kisha kuelekea chumbani kwangu.



    Niliingia kuoga na kisha kutoka.



    Na baada ya hapo nilipitiwa na usingizi mzito.



    Nilikuja kuamka ilikuwa ni asubuhi ya siku ya pili yake.



    Nilikuwepo tu nyumbani na hata wazazi nao walikuwepo wala walikuwa hawajaondoka.



    Niliamka na kisha nilipiga mswaki na kuoga na baada ya hapo nilitoka nje kila mtu alikuwa yupo bustanini.



    Nilitoka nje nikiwa nimevaa gauni jepesi jeupe lilinipendeza sana na lilikuwa likinibana.



    Nilijisikia tu kuwa na amani kwenye nafsi yangu.





    Nilitoka nje wala sikuwa nikijua kama watu wapo huku nikitembea kwa hatua za mikogo nikiimba kwa sauti ya chini kwa furaha.



    Nilikwisha sahau maswaibu yote niliyowahi kupitia na wakati huo nilikuwa na furaha ya aina yake.



    Nilitembea nilipofika mlangoni nilianza kutembea usawa wa kuelekea bustanini.



    Hapo ndipo nilipokutana na familia yangu yote nilisimama nikishangaa kuwaona



    wakiwa wapo wote.



    Ghafla geti lilifunguliwa.



    Kelvin aliingia alikuwa ameva suti nzuri sana iliyompendeza ilikuwa ni suti ya rangi nyeupe huku ndani akiwa amevaa shati la rangi ya maruni.



    Alivaa mkanda mweusi ambao aliumechisha na rangi ya kiatu chake hakika alipendeza kuliko siku zote nilizowahi kumuona.



    Alikuwa ameongozana na watu wawili amabao kwa kuwatazama tu ilikuwa rahisi kujua kwamba walikuwa ni watu matajiri.



    Walikuwa wakitembea kwa kujipanga na mara baada ya kutokeza wote walisimama.



    Nilikuwa mita chache kutoka kwao na wao walikuwa mita nyingi zaidi kunizidi kutoka walipo wazazi wangu kila mtu alibaki kuwatazama tulingojea kwa hamu kujua ni nini wanataka kukifanya.



    Kelvin alipiga magoti na kisha alipokea ua kutoka kwa mmoja kati ya watu waliokuwa nyuma yake.



    “Sociolah....” Aliniita.



    Nilibaki nimeshangaa wala sikujua nini anataka kuniambia.



    “Will you marry me?”



    Nilichanganyikiwa sana kumtazama.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Niligeuka na kumtazama baba alionekana kufurahia sana.



    Nilijua huo ni mtego tu nimewekewa siku zote baba hakutaka kuonesha kwamba Kelvin ni mtu ambaye amechaguliwa kwa ajili yangu hivyo aliruhusu kitu kama hicho kifanyike kwasababu kwanza ningechukulia heshima kwao na kisha ningeweza kujikubali.



    Pamoja na yote yaliyotokea bado sikuwa kabisa nimemchukia Frank bado nilimpenda na nilikuwa tayari kumpa nafasi nyingine kama angekubali makosa na kuamua kubadilika.



    Swala la kuingia katika mahusiano mapya na Kelvin sikuliafiki hata kidogo.



    Nilipigwa na butwaa huku nikibaki njia panda nilishindwa nini cha kujibu.



    Kila mtu aliyekuwa pale alionekana kufurahia nilichanganyikiwa sana.



    Baba alinionesha ishara za kukubali.



    Machozi yalianza kunibubujika taratibu.



    Nilipatikana.



    “Kwanini baba hataki kunielewa?”



    Nilizidi kuchanganyikiwa.



    “Ooh...” Nilivuta pumzi.



    Nilimtazama mama mama naye alionekana kufurahia kitendo kile.



    “Ooh my God. Sasa huyu Kelvin ana akili kweli.” Nilianza kuwaza.



    “Anawezaje kuja kunipropose mbele ya wazazi wangu? Kama nikimkataa je atafanyeje? Aanh ninaimani anajiamini siwezi kukataa ndiyo maana amekuja kunipropose mbele ya wazazi wangu.”



    “Haaa.....” Nilibaki tu nikivuta pumzi na kushusha.



    Nilimtazama tena baba sura yake ilishabadilika lile tabasamu lake lilikuwa limepotea na sasa ananiangalia kwa sura ya kunishurutisha ambayo inaonesha kwamba haitaji mzaha wa aina yoyote ile. Niliogopa.



    “Baba hii ni destiny yangu.” Nilitamani kumuongelesha lakini hata hivyo nilishindwa.



    Baba alionesha kwamba hataki utani katika hilo swala macho yake aliyakaza kwangu hakika niliogopa.



    “Je nikubali halafu baadae nije nikatae, nifanye nini mimi sitaki kumsaliti Frank hata kama amenisaliti yeye, nifanye nini sasa.”



    Nilishindwa cha kujibu.



    Nilimuangalia mama machozi yalianza kunitoka.



    Niliwaangalia wakina Pink sura zao zilionesha kujawa na huzuni.



    Niligeuka na kumtazama Kelvin alionesha kupoteza tumaini huku machozi yakianza kumtoka.



    Marafiki zao nao walikuwa kama watu wasioamini kilichokuwa kinatokea.



    Niligeuka na kumtazama baba uso wake uliingiwa na huzuni tena.



    “Yes i will.” Niliongea.



    Kama mtu asiye tarajia baba aligeuka na kunitazama nilimuangalia kwa jicho kali kuoneha kwamba sikupendezwa na wala sikuwa tayari kwa hiyo harusi bali nilifanya kwa sababu yake.



    Aligeuza uso wake na kutazama pengine mahali ambapo hapakuwa na mtu yoyote.



    Kelvin alinyanyuka na kuja mpaka nilipokuwa.



    Alinikabidhi ua, nililichukua na kisha alinikumbatia sikuonyesha dalili yoyote ya furaha.



    Alipomaliza kunikumbatia nilijilazimisha kutabasamu wala hakujali hicho kitu. Marafiki zake walikuja na kunipongeza walinipa kiasi kikubwa cha pesa kama pongezi.



    Wazazi wangu nao wakaja kunikumbatia.



    Baba alionesha kuwa na furaha iliyozidi kipimo, mama yangu naye alibaki njia panda akiwa hajui kama afurahi au akasirike au awe na huzuni kwa maana bado alishindwa kuelewa hasa kwamba nimekubali kwa kupenda au kwa kulazimishwa. Kina Pink nao walikuwa wakifurahia hata sijui walikuwa wamefurahia nini niliwatazama kwa jicho kali.



    “Nini sasa dada?” Pink aliongea.



    “Kwani nini?”



    Nilimuashiria anyamaze.



    Alinyamaza.



    Tulielekea ndani ambapo dada Linah alikuwa tayari ameshaandaa chakula cha asubuhi na siku hiyo baba alisema kwamba tutaenda kupata chakula cha mchana na cha jioni katika hotel.



    Tulielekea Kunduchi beach kwa ajili ya kwenda kupata chakula.



    Tuliondoka na kisha kuelekea huko.



    Nilijitahidi sana kuweka tabasamu huku nikipanga kwenda kumuuliza Kelvin na zaidi ya sana nimuombe avunje huo uchumba ambao ameuanzisha.



    Tulipofika kule tulikaa chini na kuagiza vyakula. “Baba nataka kwenda kuangalia samaki.” “Nenda, Kelvin msindikize mwenzio.” Nilimshika mkono na kisha kunyanyuka.



    Mama alionekana kufurahi kweli kwani aliamini nilikuwa na furaha ya hali ya juu.



    Nilimshika mkono Kelvin na kisha tulielekea mahali ambapo samaki walikuwepo.



    Tulipofika pale niliendelea kumvuta kumuelekeza sehemu nyingine kabisa.



    “Sociolaha samaki si hawa.”



    “Ndiyo nimewaona.”



    “Sasa nini kingine?”



    “Kwani nini? Mimi si nilikuwa nimekuja kuangalia samaki si nimeshawaona twende sehemu nyingine.” Niliongea kiukali kidogo.



    Tuliondoka na kisha kuelekea baharini.



    Tulipofika kule baharini nilimvuta kwangu hadi akaja mbele yangu. “Kelvin unafikiri kitu ulichokifanya ni sahihi?”



    Aliachia tu tabasamu.



    “Sikia nikuambie Kelvin kuja kunipropose mbele ya wazazi wangu ukaamini kwamba sitakataa umeshafeli mimi siko tayari kuwa na wewe wala siko tayari kuolewa na wewe na unafahamu kabisa kwamba sikupendi unajua fika kwamba ninampenda sana Frank na wala si wewe, kuwa na matatizo na Frank haimaanishi kwamba ndiyo mahusiano yetu yamekufa. Nimewakubali kwasababu ya baba, naomba uende ukamuambie baba kwamba ninavunja huu uchumba na usimpe sababu kwamba mimi nimekataa sijui tunaelewana.”



    Alicheka.



    “Sociolah nitakufanya kuwa mwanamke mwenye furaha kuliko wanawake wote, siyo sawa na familia hiyo ya kimasikini nitakupa kila unachotaka nitakupeleka kila sehemu unayoenda. Nakupenda sana Sociolah.”



    “Sitaki.. Sitaki.. Kelvin mimi sikupendi siwezi kuwa na furaha kuwa na wewe.” “Aanh usifikirie tu ila ukweli upo kwamba utafurahi wala usijali we niruhusu tu utafurahia mwenyewe.”



    “Sitaki... Sitaki.... Kelvin.”



    “Hakuna shida.” Alianza kuondoka.



    “Naenda kuwaambia wazazi wako.”



    “Nooo Kelvin subiri... Subiri.”



    Alishapiga hatua nyingi niliendelea kutembea huku nikichanganyikiwa.



    Tulienda hadi mezani.



    “Baba kuna kitu nataka nikuambie.” Kelvin aliongea.



    “Ongea tu wala usiwe na shida yoyote.”



    “Aanh ni kuhusu uchumba wetu mimi na Sociolah ambao tumeuanza rasmi leo.” Baada ya kuongea hivyo alinitazama, sura yangu ilionesha kujawa na huzuni. Nilimsisitiza kwa kila namna asiongee alichokuwa akitaka kukiongea.



    “Kelvin stop.” Niliongea kwa sauti ya chini huku nikimtazama usoni.



    Macho yangu yote yaliashiria kwamba asiongee kitu chochote hata hivyo alionesha kwamba hanielewiali.



    Aliniangalia tu na kisha kuendelea na kile alichokuwa anataka kukiongea.



    “Aanh baba kitu ambacho nilikuwa napenda sana kusema ni kwamba nampenda sana Sociolah na nitamuoa muda wowote kuanzia sasa wala sitaki izidi miezi sita.





    Kwahiyo naomba kila kitu kifanyike haraka haraka ikiwemo maswala ya kuvalishana pete ya uchumba pamoja na kutoa mahari ili tupate baraka zenu na pia tuweze kuandaa mipango ya harusi.”



    Mama alifumbata uso wake katika viganja vyake vya mikono, chembechembe za machozi zilianza kumtoka.



    Baba yangu alibakia kimya asijue nini cha kuongea, nilichanganyikiwa zaidi ya ambavyo ilitakiwa.



    “Huyu mwanaume ni mjinga nini?!”



    “Kelvin.....” Niliita kwa ukali, baba alinigeukia na kunitazama.



    Niliyameza maneno yangu na kisha kuinama chini.



    “Hata Sociolah mwenyewe haamini.”



    Baba aliupasua moyo wangu kwa maneno yake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Sisi tunakupa Baraka zote mwanagu hata ukitaka ufunge ndoa leoleo sisi wala hatuna shida.” Baba aliongea.



    Nilichukia sana nilimuaangalia Kelvin kwa uso wa chuki, alitabasamu tu na kisha kugeukia upande mwingine.



    Siku hiyo ilimalizika kwa furaha kwa upande wao huku ikimalizika kwa maumivu



    sana kwa upande wangu.



    Tulirudi nyumbani.



    Asubuhi yake mama aliniamsha mapema nilijiandaa na kisha kuongozana naye kuelekea chuoni.



    Wakati tupo tukisubiri foleni maeneo ya Mwenge.



    “Sociolah...” Mama aliniita.



    “Abee mama.”



    “Una furaha katika uchumba wako?”



    Sikumjibu nilinyamaza kimya.



    Kama mtu asiye jali jibu langu mama aliendelea kuongea.



    “Nataka nikupe gari yako mwenyewe uwe unakuja shule mwenyewe, wewe ni



    mchumba wa mtu sasa unatakiwa uwe huru siyo nikubanebane unapanga maisha



    yako sasa.” Mama aliniambia.



    “Nitafurahi mama.” Nilimuambia.



    “Utanipa gari gani sasa?”



    “Usiwe na haraka, nitakupa gari dogo.”



    “Mama mimi silitaki gari dogo nataka kubwa nyeusi.” “Wewe gari kubwa ya nini na uko peke yako?”



    “Lolote utakalonipa mama nitachukua.” Niliongea



    Mama hakutaka tena kuendelea na mazunumzo mengine na mimi nilikuwa bize nikichati.



    Aliendelea kuendesha gari hadi tulipofika chuoni.



    Alinipeleka kwenye madarasa yetu na kisha kunishusha



    “Bai mama.” Nilimuaga mara baada ya kushuka chini ya gari.



    “Sociolah..” Aliniiita.



    Nilirudi.



    “Umependeza mwanangu.” Aliniambia.



    “Ahsante mama.”



    “Uwe na wakati mwema.”



    “Ahsante mama.”



    Mama aliondoa gari nilimtazama mpaka alipopotelea na kisha kugeukia kuelekea usawa wa madarasa yetu na hapo ndipo nilipomuona Frank.



    Alikuwa amesimama mlangoni akinitazama muda wote, macho yetu yalipogongana.



    Alipeleka macho yake pembeni kwa huzuni nilimuangalia kwa hasira na kwa jicho kali na kisha nikatembea hatua za haraka haraka na kuingia darasani.



    Sikutaka tena kukaa viti vya mbele nilienda moja kwa moja mpaka viti vya nyuma na kukaa.



    Watu walianza mazungumzo ya chini chini kabla ya dokta Kiseyeye kuingia darasani.



    “CR baada ya kipindi naomba uje ofisini kwangu.”



    Aliendelea na kipindi wakati huo Melania aliingia kwa kuchelewa sana na kwenda kukaa kwenye kiti ambacho mara zote nilikuwa nikikaa mimi. Nilisikia minongono ya watu.



    “Kiti cha malkia kimechukuliwa bwana.”



    Sikujali.



    Nilishapoteza vipindi vingi sana nilitaka kuwa makini sana darasani sikuruhusu akili yangu itawaliwe na maneno yao.



    Vipindi viliendelea hadi wakati ambao tulikuwa tunaenda kunywa chai.



    Christina alikuja.



    “Mambo?”



    “Poa Christina.”



    “Sijakuona muda mrefu sana, tangu ile siku sijakuona tena sijui umepotelea wapi?”



    “Aanh niliondoka nilienda nyumbani.”



    “Nimekuja chumbani kwenu kukutafuta lakini nikaambiwa kwamba umeondoka



    na kila kitu chako.”



    “Kweli bwana nimehama.”



    Innocent alisogea upande wetu.



    “Nimesikia umehama hostel.”



    “Ndiyo nimehama.”



    “Aanh.., ndiyo umemkimbia Melania mke mwenzio.” Innocent alisema. Nilimtazama Innocent kwa macho makali kuashiria usaliti wake kwangu sikuufurahia hata kidogo.



    Alinivuta pembeni na kumuacha Christina amesimama pembeni yetu. “Sociolah nahitaji muda kuzungumza na wewe.”



    “Sihitaji Innocent mlichonifanyia dharau zenu nimeziona sihitaji muda wa kuongea na wewe kabisa, siyo wewe wala huyo mwenzio fanyeni mambo yenu na mkiniona mnifanye kama hamjawahi kunijua, sijui unanielewa?” “Sasa Sociolah kwani mimi kosa langu ni nini?”



    “Huna kosa lolote kosa lako ni kuja kuniomba muda wa kuongea na mimi. Sihitaji kuongea na wewe.”



    Niliongea kwa hasira huku nikiondoka.



    “Sociolah nisikilize basi kuna kitu cha muhimu nataka nikuambia.”



    “Hakuna umuhimu wowote ambao unaweza kuniambia mimi nikakuelewa fanya mambo yako h ilo ndiyo la muhimu lililobakia sasa kwako achana na mimi ukiniona jifanye kama hujawahi kunijua.” Niliongea kwa ukali na kwa msisitizo.



    Niliondoka haraka na kumshika Christina mkono na kisha kumvuta kuelekea mgahawani.



    “Kuna nini kwani?”



    “Aanh.. Mimi namshangaa sana huyu Innocent ni mnafiki kupitiliza kipindi kile wakati niko na Frank....”



    Roho iliniuma sana kuona kwamba ilishakuwa wakati uliopita.



    “Kipindi kile wakati niko na Frank alijifanya ananipenda sana lakini sasa hivi ameshakuwa adui yangu halafu bado anahitaji muda wa kuongea na mimi.” Niliongea kwa kirefu bila kupumzika.



    “Aanh Christina...” Nilimuita.



    “Sorry kwa kukuongelesha kwa hasira hivyo najua haya yote hayakuhusu wewe.”

     CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mimi ningefurahi kama ungemsikiliza Innocent.”



    Niligeukia upande mwingine tulikuwa tukipita kwenye daraja kwa ajili ya kuelekea mgahawani.



    “Christina kama unataka kugombana na mimi ndani ya Sekunde mbili hizi basi endelea kumtaja huyo mtu katika masikio yangu, naomba twende.”



    Christina hakuongeza neno.



    Tuliondoka kwa hatua za kiuchovu huku kila mmoja akiwa kimya vitu kadhaa vikipita katika ubongo wangu.



    Tuliongozana hadi tulipofika mgahawani niliagiza chai yangu na yeye aliagiza ya kwake.



    Nilishindwa hata kula mawazo mengi yalinitawala juu ya ugomvi uliotokea hapo asubuhi.



    Mara ghafla simu yangu iliita alikuwa ni Kelvin. “Heloo..” Nilisema mara baada ya kupokea simu. “Uko wapi mchumba wangu?” “Niko chuoni.”



    “Nahitaji kuja kukuona.”



    “Samahani sehemu ya kuja kuniona sio chuoni njoo nyumbani wakati wowote nikiwepo.”



    “Lakini nimekumisi sana Sociolah hebu punguza hasira.” “Hapana utakuja kuniona nyumbani akili yangu haiko sawa.” Nilimuambia.



    “Hakuna shida mama ila tuliza akili sawa mama.” “Sawa.” Nilikata simu.



    Christina alikuwa akiniangalia.



    “Sociolah kuna wakati katika maisha inakubidi uwe shujaa na kuikabili kesho yako.”



    Niliamua kwa dhati kuyasikiliza maneno yake.



    “Ndiyo.”



    “Jua kesho yako inataka nini na kisha itafute kesho yako.” Niliendelea kumsikiliza. “Katika maisha Sociolah huwezi kufika kama unapitia kwenye njia usiyoijua na maanisha kufika pale ambapo wewe unataka kufika. Mwisho wa safari utafika lakini unaweza kufika kituo ambacho hujataka kufika kwasababu kama mtu anataka kuelekea Mwanza halafu akapita njia ya Arusha sidhani kama atafika. Namaanisha kwamba kuna ndoto zetu, kuna kesho yetu ambayo tunaitazama lakini





    hatuwezi kuifikia kama tu tutapita katika njia tofauti. Eti kwasababu katika ile njia ambayo itakufikisha kule unapoenda kuna matatizo, kuna miiba imesonga.” Nilishindwa kumuelewa alichokuwa anamanisha.



    “Unamaanisha nini?”



    “Usijali utanielewa tu polepole.”



    “Mimi bado umeniacha njia panda tena.” Niliongea huku nikitasamu.



    “Sociolah unafahamu ni kitu gani unakipenda katika maisha yako, kitafute hicho hata kama kuna shida kiasi gani usikate tama pambana upate kile kitu ambacho unakipenda.”



    “Unamaanisha nini?” Nilimuuliza.



    “Unampenda sana Frank mtafute Frank wako achana na wengine.”



    “Christina naona unanipanda kichwani, sitaki mtu anifanyie maamuzi ninajua mwenyewe ninachokifanya.”



    Nilinyanyua pochi yangu na kusimama.



    “Kuanzia leo nione kama hujawahi kunijua.” Niliongea maneno hayo huku moyo ukiniuma sana.



    “Kila mtu nampoteza kwa ajili ya nini sasa?” Nilijiuliza huku nikiondoka.



    Safari yangu iliishia katika vibweta vilivyo karibu na daraja.



    Nilikaaa pale machozi yakinitiririka, moyo wangu uliniuma sana.



    “Lakini Christina anaongea ukweli, hata hivyo si mimi niliyemkataa Frank, Frank ndiye aliyenikataa mwenyewe. Mimi bado nampenda siwezi kumlazimisha anipende kama yeye ameamua kufuata njia yake muache aende mimi siwezi kumlazimiasha anipende siwezi kwenda kumbembeleza Frank ni mtu mzima yule anajielewa mimi namuacha.”



    Niliondoka na kuelekea darasani vipindi vyote vilivyofuataia sikuweza kupata chochote.



    Mwisho wa vipindi nilinyanyuka kiuchovu nikaenda kumsubiria mama.



    Hata hivyo nilivyotoka tu nje ya darasa letu nilikutana na gari ya Kelvin.



    Nilishangaa sana nilienda mpaka dirishani.



    “Kelvin ...”



    “Yes mama.”



    “Mama atakuja kunichukua.”



    “Nimeshaongea naye mimi ndiyo nitakayekuchukua.”



    Nilizunguka ili kupanda kweye gari ya Kelvin na hapo nilimuona Franklin alikuwa kutoka kwenye kona akituangalia.



    Hata hivyo mboni zake hazikuonesha kuhisi chochote kwa maana alikuwa



    akitutazama kama mfu.



    Sidhani hata kama aliniona.



    Nilimshangaa kwa dakika chache na kisha nikaamua kuondoka, nilipanda kwenye gari na kuondoka na Kelvin.



    Alinirudisha mpaka nyumbani na huo ndiyo ulikuwa utaratibu wake siku zote kila mara alikuja kunichukua chuoni na kisha kunirudisha nyumbani.



    Baada ya wiki mbili kupita Kelvin alinivalisha pete ya uchumba hata hivyo sikuwa na furaha kabisa katika uhusiano wangu huo kila mara nilipokuwa naye niliingiwa na hasira tofauti na ninavyokuwa karibu na mtu wangu. Siku moja mama aliniita.



    “Sociolah, sioni kama una furaha.”



    Niliamua kumuamini mama yangu.





    “Mama naomba tukaongelee chumbani kwangu.” “Hakuna shida.”



    Tuliondoka na kisha kuelekea chumbani kwangu. “Mama sina amani kabisa kwenye moyo wangu.” “Kwanini mwanangu?”



    “Mama sina amani kabisa kwamba nakuja kuolewa na Kelvin siyo mwanaume



    ambaye ninampenda mama.”



    “Kwanini?”



    “Hayupo moyoni mwangu kila nikijitahidi kumpenda nashindwa mama kumbuka maisha ya ndoa mama nikishaingia kwenye ndoa ni kwamba mpaka kifo kitatutenganisha hapo ndipo malengo yalipo na kesho yangu ilipo mama. Endapo nikichagua mtu ambaye hayupo moyoni mwangu itaniharibia maisha yangu yote yaliyobakia mama. Mimi sidhani kama niko tayari kuolewa na Kelvin.” Mama alinisikiliza na kisha aliinamisha uso wake kwa huzuni.



    “Sijui hata nikuambie nini binti yangu lakini mimi ni mama yako wala sikulazimishwa kuolewa na baba yako.Na mimi sidhani kama baba yako pia anafahamu kwamba wewe hupendi kuolewa na Kelvin. Nahisi kuna kitu, nitakuja kukuambia kila kitu ambacho kinaendelea siwezi kukubali mwanangu ukaingizwa katika msala huu nitahakikisha nakuponya kwa gharama yoyoyte ile binti yangu. Ungenambia tangu mwanzo Sociolah wangu.” “Mama niliona kila mtu yuko upande wa Kelvin.”



    “Hivi mwanangu mimi niwe upande wa Kelvin?! Kelvin nimembeba mimi miezi



    tisa tumboni kwangu kweli mwanangu?”



    “Nisamehe mama.” Nilijibu kiupole.



    “Sawa nitahakikisha kila kitu kinakuwa sawa.”



    Mama aliondoka na kuniacha nikihisi kupunguza mzigo mzito niliokuwa nimeubeba hata Kelvin alipokuja nilikuwa na Furaha sana.



    Pete ambayo alinivalisha kidoleni ilikuwa ya thamani sana ilikuwa imenakishiwa kwa madini ya almasi hata hivyo kwangu niliona kama mzigo tu.



    Wiki iliyofuata nikiwa chuoni tulikuwa tuna muda mrefu kabla hatujaingia kwenye kipindi sikuwa na rafiki yoyote niliamua kutembea peke yangu.



    Kwa mbali niliweza kumuona mtu kama Frank na Melania wakiwa pamoja roho iliniuma sana hata hivyo nilivutiwa kuwaangalia walichokuwa wakikifanya.



    Frank alikuwa akitembea kwa hatua ndefu sana mbele huku Melania akimfuata nyuma bila shaka walikuwa wana ugomvi.



    Walikuwa mbali sana kutoka kwangu kiasi kwamba nisingeweza kusikia kitu walichokuwa wakikiongea lakini niliona jinsi ambavyo Melania akijaribu kumvuta Frank kana kwamba anambembeleza kitu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilifurahi sana kuona kwamba katika mahusiano yao hakuna amani nilidhani kivuli changu kilikuwa kikiwaandama.



    Niliamua kuachana nao na kisha kuendelea na mambo yangu.



    Siku hiyo ilikuwa ya furaha sana kwangu niliingia darasani huku nikiwa nimefurahi mno.



    Kila nilipomuoana Melania nilijihisi kucheka sana watu wengi walitabari kwamba siku hiyo isingeisha salama Melania angeweza kunipiga.



    Frank alionekana kuwa na hasira muda wote na hakuna mtu ambaye angeweza kunifuata kuniuliza kwa maana ilionekana darasa zima liko peke yao likiwa kama kikundi kimoja kinachosaidiana na mimi nilikuwa niko kwenye kikundi changu peke yangu yani jeshi la mtu mmoja.



    Niliamua kujipa mwenyewe raha kwa maana sasa mambo yangu yalikuwa yakienda vizuri.



    Mama ananisikiliza na uhusiano mpya ambao ulianzishwa kwa lengo la kuniumiza mimi una matatizo.



    Tuliendelea na masomo kama kawaida huku nikiwa na furaha sana na siku hiyo mama ndiye aliyekuja kunichukua.





    Mama alinipakiza kwenye gari lake. “Sociolah nimemzuia Kelvin kuja kukufuata.” “Mmmh kwanini?”



    “Basi tu nimemuambia atakuchukua pale atakapokuoa.” “Aanha atanioa kweli?”



    “Sidhani kuna kitu nahisi kama hakiko sawa.” “Kwanini mama?”



    “Aanh naona Kelvin huwa naona anakuja muda mrefu kabla ya wakati wako wa kutoka sijui huwa anafanya nini humu ndani.”



    “Labda anakuja kunichunguza chunguza njia zangu.” “Hahah sidhani.” Mama alicheka. “Yawezekana mama.”



    “Kelvin anakupenmda sana hata hivyo nashindwa kuelewa mimi, kuna vitu vinanichanganya sana mwanangu unajua tangu mwanzo nilikuwa na hisia ambazo haziko vizuri, nitaendelea kufuatilia kati ya baba yako na huyo Kelvin nijue nani ambaye yuko chini ya hii ndoa yako.”



    “Mama mimi najua kabisa baba ndiyo anataka mimi niolewe na Kelvin kwasababu si ni rafiki yake wanataka kuanzisha biashara yao wote.”



    “Biashara!” Mama aliongea kwa mshituko kidogo “Ndiyo Kelvin ndiyo aliyeniambia.”



    “Mwanangu jaribu kukaa sana na Kelvin kwa muda mrefu halafu uongee naye umchunguze chunguze si mchumba wako eeenh eenhee ongea naye.” Nilicheka.



    “Mama bwana leo umekunywa nini? Maana una furaha kweli na unachekesha.” “Hahaha, hamna binti yangu jaribu kufanya hivyo sawa.” “Aya mama.”



    Tulipofika nyumbani Kelvin alikuwepo.





    Sura yake haikuonesha kuwa na amani kabisa.



    Tulipata muda wa kuwa peke yetu.



    “Kelvin una nini leo.”



    “Nimeshangaa sana mama kunizuia kuja kukufuata kuna nini?”



    “Aanha nimeongea na mama amesema kwamba anahitaji muda wa kuwa na mimi kabla sijaolewa anadhani atanimisi sana mimi naomba umpe ruhusa ya yeye kufanya hivyo.” Alicheka sana mpaka machozi yalianza kumtoka.





    “Nilidhani ndiyo anajiandaa kuvunja uchumba wetu nimeumia sana Sociolah.” “Usijali ni kawaida tu.”



    “Aanh Kelvin unapenda tuishi wapi mara baada ya kufunga ndoa.”



    “Aaanh Sociolah mimi sitaki tukae karibu na wazazi ningependa sana kukaa Dar na pia natamani sana kwenda kuishi na wewe Marekani.”



    “Aaaha mimi sitamani kwenda nje ya nchi kabisa.” “Hata mimi sitamani kuondoka Tanzania Sociolah.” “Na mimi sitaki kuishi nje ya Dar.”



    “Nafahamu hilo, mama anakaa mbezi si ndiyo?” “Yeah.”



    “Mimi nitakupeleka kukaa sehemu nyingine mbali huko.” “Hahaha..” Nilicheka.



    “Yani kiasi kwamba mama akija anajifikiria kwanza napoteza mafuta kiasi gani.” Aliongea kwa ucheshi sana nilicheka mno.



    “Kelvin unatamani tuzae watoto wangapi?”



    Niliongea huku nikionesha kuwa na hali ya furaha nikifurahia maongezi yetu.



    Nilishangazwa na ukimya uliotawala.



    Kelvin alinigeukia na kunitazama.



    Niliona kuna kitu usoni mwake ambacho kilinipa taarifa kwamba Kelvin alikuwa



    hakufurahishwa na kile kitu ambacho nilikionge na zaidi ya sana kilikuwa



    kimemuumiza.



    Nilipatwa na kiulizo.



    “Sociolah kuzaa ni mipango ya Mungu.”



    “Aanh idadi yoyote ile ya watoto mimi nitafurahia. Ila kuhusu swala la watoto mke wangu nakuachia wewe ukitaka uzae watoto ishirini, ukitaka uzae kumi ukitaka tusizae.”



    “Haaa hivi kuna mwanamke ambaye hapendi kuzaa?” Nilimuuliza Kelvin.



    “Wapo. Wewe usione unapenda kuzaa basi ndiyo ukadhania kila mtu anapenda wengine hawapendi.”



    “Mimi nataka kuzaa.” Nilisema.



    “Basi tutazaa mke wangu.”



    “Siku moja unipeleke kwako sijawahi kufika kabisa.” “Aanh hilo tena wala usitie shaka tutaenda.”



    Siku iliyofuata nilielekea chuoni watu wengi walikuwa hawajawahi kuniona nikiwa na pete yangu ya uchumba.





    Siku hiyo habari zilisambaa chuo kizima kwamba nimevalishwa pete ya uchumba na hakuna mtu alikuwa akijua ni nani ambaye amenivalisha pete ya uchumba. Nilishangaa sana kwamba Melania alikuwa akifurahi mno nazani alifurahia sana kuona kwamba vita ya kumgombania Frank inaelekea mwishoni.



    Nilipita na pete yangu ile ya uchumba yenye thamani sana kwa mbwembwe zote kuonesha kwamba mimi ni zaidi yao.



    Mara zote Christina alikuwa akinitazama tu nilikuwa nikimuangalia nikimuona kama na yeye ni mmoja kati ya vibaraka wa Frank.



    “Ama kweli Matranka sasa amekua hadi anaweka vibaraka wa kunifuatilia fuatilia mimi, ameshindwa.” Niliendelea kuwaza.



    Nilifurahia sana maisha ya kuwa peke yangu pale chuoni.



    Hakuna mtu ambaye alikuwa akinifuatilia wala kunifanya niwe na mawazo.



    Niliishi mwenyewe na wakati huo tayari nilikuwa nina gari yangu.



    Hivyo nilienda chuo mwenyewe na kurudi mwenyewe na mizunguko yangu yote ningefanya nikiwa peke yangu.



    Maisha yaliendelea siku zilizidi kukatika sikuona dalili ya uchumba wetu kusitishwa kama mama ambavyo alikuwa ameniahidi. Nilipatwa na mshangao sana.



    “Mama kanisaliti?!!”



    Nilizidi kuchanganyikiwa hasa pale Kelvin alipokuja na tarehe yetu rasmi ya kufunga ndoa na siku ya kutoa mahari.



    Alinieleza kwamba sherehe ya harusi yetu haihitaji mchango wowote kamati tu pekee ilitosha kukusanya fedha ambazo zingetumika katika sherehe ya harusi yetu. Huku fungate likipangwa kufanyika katika moja ya visiwa ambavyo ningechagua mwenyewe.



    Nilitamani sana kumfuata mama na kumuuliza hata hivyo mama alionekana kuwa bize muda wote.



    “Mungu wangu mama naye amekuja kunidanganya hapa nitashangaa tu siku ya harusi imeshafika. Aanh dunia imenisaliti mimi.”



    Furaha yote niliyokuwa nayo ilianza kutoweka.



    Siku zilizidi kukimbia, siku yangu ya kutolewa mahari ilizidi kukaribia nilizidi kukosa amani.



    Wala sikuwa nikielewa jinsi masaa yalivyokuwa yakipita.



    “Aanh Mungu wangu dunia imenisaliti sasa.”



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilikuwa nikijifungia ndani muda wote mara baada ya kutoka chuoni sikutaka kufanya mawasiliano na mtu yoyote.



    Siku ya siku nilipokea meseji nilipofungua tu simu yangu nilikutana na ujumbe mfupi.



    “Mambo? Ni mimi Christina. Najua kwamba hukunipa namba yako ya simu lakini niliitafuta na kufanikiwa kuipata. Mimi siko upande wa Frank hata hivyo siko upande wa mchumba wako wa sasa. Ninachotaka nikuambie ni kwamba kuna kitu kipo nyuma ya pazia na ambacho wewe hukijui. Naweza kusema kwamba nafahamu kwa uchache sana. Jaribu kumchunguza mchumba wako vizuri halafu jaribu kuangalia ukweli kwamba Frank amekukosea na amekifanya hiki kitu kwa ridhaa yake kwa maana sidhani kama tangu lilipotokea tatizo hili umewahi kuongea naye, pengine ana kitu cha kukuambia. Ninamjua vizuri sana Frank sidhani kama Frank anaweza kufanya kitu kama hiki namjua Frank tangu tukisoma naye shule ya msingi mpaka hapa tuko pamoja lakini mchumba wako naweza kusema kama namfahamu kidogo nimewahi kumuona siku moja hapa chuoni lakini nilimuona katika sehemu mbili tofauti zinazonipa mashaka na ndiyo maana nimeamua kukutafuta.



    Sasa mimi ninachokushauri ninaomba umtafute Frank uongee naye kama utapata huo muda. Na pia kaa vizuri na mchumba wako mchunguze vizuri.”



    Aliandika meseji ndefu niliisoma na kisha nikaipuuzia.



    “Fyuuu wote walewale tu.”



    Hata hivyo maneno ya kwenye ujumbe ule yalikataa kufutika akilini kwangu kabisa.



    “Sidhani kama amekurupuka kuandika meseji kama ile.”



    Nilikumbuka kipindi chote ambacho tulikuwa pamoja na maneno yake yote ya



    busara ambayo alikuwa akiniambia.



    Akili yangu ilikosa utulivu kabisa.



    “Huyu Kelvin ana nini?! Mbona nazidi kuchanganyikiwa sasa.” Niliamua kufanya uchunguzi wangu kwa chinichini. Nilimpigia simu na kumuomba niende kwake.



    Alikubali alikuja kunifuata nyumbani na kisha kunipeleka nyumbani kwake. Kelvin alikuwa akiishi kwenye nyumba nzuri sana ya kifahari na ya kitajiri. Alikuwa na magari mengi huku nyumba yake ikinakishiwa na vitu vingi sana vya thamani.





    “Kelvin uliwezaje kupata hivi vitu vyote jamani?” Nilizidi kuchanganyikiwa katika mazingira yale.



    “Mimi nimfanya kazi tena ninafanya kazi kwa bidii sana Sociolah na yote ni kwa ajili ya familia yangu.”



    “Aanh so nitakuja kuwa malkia kwenye hii nyumba.” Uzuri wa ile nyumba ulinichanganya.



    “Ndiyo, nilikuambia nitakufanya kuwa mwanamke mwenye furaha sana naamini ndoto yako itatimia.”



    “Nitafurahi sana Kelvin, ninakupenda.” Nilijikuta tu nimeongea.



    “Aanh, nakupenda pia.”



    Alinizungusha sehemu mbalimbali za nyumba ile na mwisho kabisa tuliishia chumbani kwake.



    Kilikuwa ni chumba kizuri sana ambacho kingemfanya mkaaji wake asipende kwende sehemu nyingine yoyote angetamani akae siku zote ndani ya chumba hicho bila kutoka nje.



    “Kelvin nahitaji kitu cha baridi kama juisi hivi.” “Aanh sidhani kama kuna juisi.” “Kamtengenezee mkeo.” Nilimuambia.



    “Hakuna shaka dakika chache tu nitakuwa nimerejea.” Aliondoka.



    Alipoondoka nilianza kutembea nikikisanifu chumba kile.



    Huku nikiwaza mambo mbalimbali mara baada ya kuhamia katika chumba hicho. “Hapa nitapanga viatu vyangu, hiki kitanda nitakisogeza upande wa kule halafu hizi karatasi zilizokuwepo hapa juu nitaziweka kabatini.”



    Kulikuwa  na  karatasi  ambazo  zilikuwa  ziko  juu  ya  meza  yake  meza  ndogo



    iliyokuwa pembeni ya kitanda.



    Nilizichukua na kuzipeleka kabatini.



    Nilifungua kabati lile la kisasa ambalo nilikuwa na vioo pande zote.



    Nilitafuta sehemu ya kuweka zile karatasi.



    Nilipekua pekua na kubahatika kukutana na bahasha.



    Nilifungua bahasha ile huku nikiziweka sawa zile karatasi na kutaka kuziingiza ndani ya ile bahasha.



    Niligundua kitu kwenye zile karatasi ambacho kilivutia sana kusoma.



    Nilisoma zile karatasi chache zilizokuwepo pale juu ya kabati.



    Nilijikuta mikono ikitetemeka.





    Niliirudisha ile bahasha iliyokuwa kwenye kabati na zile karatasi nilizozikuta juu ya meza nilizirejesha mahali pake.



    Nilifungua mlango na kisha kutoka, niliweza kumuona Kelvin akiwa jikoni akiandaa juisi.



    Nilipita moja kwa moja hadi getini niliita bajaji iliyokuwa ikipita karibu na kisha kuondoka kuelekea nyumbani.



    Nilipofika nyumbani nilimkuta mama kama aliyechanganyikiwa.



    “Mwanangu...” Aliniita mara baada ya kufika nyumbani.



    Kabla sijamjibu alinishika mkono na kunipeleka chumbani kwangu.



    Nyumbani alikuwepo dada Linah peke yake.



    “Kuna nini mama?” Nilimuuliza mara baada ya kuingia chumbani.



    “Mwanangu tarehe za siku ya kutoa mahari pamoja na siku ya kufunga harusi zimerudishwa nyuma sijui sasa ni kwa nini wanataka kuharakisha sana.” “Mama kuna kitu…”



    “Sikia nikuambia mwanangu wewe acha usiongee chochote najua umekutana na kitu ambacho siyo cha kawaida, la muhimu ni kwamba usioneshe hali yoyote ya kuchanganyikiwa jipe moyo mkuu mimi na wewe tupo pamoja tumekuwa kitu kimoja maana nimegundua kuna kitu hakiko sawa kabisa endelea na uchunguzi kimya kimya na mimi nitaendelea kufuatilia sababu za kurudishwa nyuma. Baba yako hatoi ushirikiano wa aina yoyote sijui hata ana mawazo gani na wewe.” “Mama naogopa.”



    “Usiogope mwanangu kila kitu kitakuwa sawa, sawa?” “Sawa mama.”



    Nilibaki chumbani nimelala tu.



    Simu iliita nilijua tu ni Kelvin aliyekuwa akinipigia sikutaka kupokea simu yake.



    Simu iliita na mwishowe niliamua kupokea.



    La haula!! Ni mama yake na Franklin alikuwa akipiga simu.



    Nilipokea.



    “Haloo, shikamoo mama.”



    Niliongea ingawa moyoni mwangu nilikuwa na hasira.



    Hata hivyo nilifikiria ni hasira za aina gani nimchukie mama yake Frank yeye amefanya nini.



    “Mwanangu hujambo?”



    “Sijambo mama za siku?”



    “Nzuri, nimekuwa nikikutafuta kwa muda mrefu sana.”



    “Nipo mama za siku? Unaendeleaje na hali yako?”



    “Salama tu nilienda shambani ndiyo nimerudi wiki hii hii, nimekuwa nikihangaika kukutafuta.”



    “Aanh mama nilikuwa na mambo mengi nipo bize kidogo.” “Aanh usijali mwannagu nimekupatia gunia moja la mpunga.” “Aanh ahsante mama nitakuja kulichukua.” “Lipo tu hata usijali.”



    Nilitegemea muda wowote mama angeniuliza sababu ya sisi kuachana hata hivyo mama hakuongea alinisalimia kunijulia hali na baaada ya hapo alikata simu.” Nilibaki nimelala tu nyumbani.



    Na jioni Kelvin alikuja nyumbani alinikuta nimelala.



    “Sociolah kwanini umeondoka bila kuniaga, mmh?”



    “Am sorry Kelvin niliondoka bila kukuaga mama alinipigia simu kunatatizo kidogo nirudi.”



    “Kwani limeshashughuliwa, kuna nini?”



    “Hamna lilikuwa tu ni tatizo la kawaida limeshashughuliwa wala usipate shida.”



    “Ungeniaga basi tungekuja wote jamani mama anaweza akanifikiria vibaya.”



    “Hamna usijali.”



    “Ok niambie.”



    “Safi.”



    “Sasa juisi yako atakunywa nani?”



    Nilijikuta nacheka.



    “Kwani si ipo nitakuja kuinywa.”



    Tulikaa mpaka usiku baba aliporejea waliongea mawili matatu na kisha aliaga.



    Nilimsindikiza.



    “Nitakuja kesho.”



    “Nitafurahi sana.”



    “Karibu.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kama nilivyomuahidi kesho yake nilienda.



    Tuliingia jikoni, tuliandaa chakula, tulikula, tulicheza michezo mbalimbali, tuliongea mambo mengi na baada ya hapo tulipitiwa na usingizi.



    Hata hivyo sikuwa nimelala kabisa nilimsubiri pale alipopitiwa na usingizi kabisa kiasi cha kutoshitukia kitu chochote niliamka na kuendelea kukaguakagua. Nilifungua kabati kwenye zile bahasha nilizozikuta, niliichukua na kisha kuiingiza kwenye pochi yangu.



    Baada ya kuingiza kwenye pochi yangu.



    Nilipotaka kushika simu yake aliamka.



    “Vipi haujalala?”



    “Nimeshituka sasa hivi.”



    “Nilikuwa nataka kuangalia muda.”



    Alichukua simu yake na kisha kuiweka pembeni.



    “Saa hiyo hapo Sociolah.”



    Niligeuka na kuangalia.



    “Aanh hatujalala sana ila nasikia uchovu ngoja nikaoge.” “Twende tukaoge wote.”



    “Hapana tutaoga wote mara tukishafunga ndoa, kwani unaharakia wapi na mimi ni mkeo.”



    Aliniangalia na kisha kutabasamu.



    Alikuwa na macho mazuri sana ambayo yalimfurahisha mtu ambaye alikuwa akitazama.



    Nilinyanyuka na kisha kuelekea bafuni.



    Nilioga na kisha kutoka.



    Mara nyingi nilikuwa nikimkwepa hata hivyo hakuweza kugundua alizania tu ni michezo ya kimahaba.



    Jioni ilipofika nilirejea nyumbani nikiwa na amani kidogo.



    Usiku mama alikuja chumbani kwangu wakati watu wote walipokuwa wamelala. “Vipi niambie kuna maendeleo?”



    “Ndiyo mama nimepata document ambayo nafikiri itasaidia.” “Sasa mimi ninakushauri nenda ukashughulike na kompyuta yake.” “Mmmh, sawa nitajaribu mama hakuna shida.”



    “Nimepata maendeleo kidogo lakini najua nikichanganya na ya kwako tutafikia



    kitu nilichotaka tufikie mwanangu sawa.”



    “Ndiyo mama.”



    Siku iliyofuata nilielekea chuoni.



    Niliwahi sana kufika chuoni nilielekea kwenye viti vya nyuma na kisha kukaa. Nilijiinamia tu nikiwa na mawazo mengi mara ghafla nilisikia watu wakizozana mbele.



    “Sitaki nimeshakuambia sitaki kwanini unielewi?” Nilivutiwa kuangalia kitu ambacho nilikuwa nikikiona.

    Nilishangaa sana kukuta ni Franklin na Melania ndiyo walikuwa wakigombana.



    Niliponyanyua uso wangu waliniona.



    Franklin alitoka nje kwa hasira huku akimuacha Melania.



    Melania alinisonya na kisha kuondoka.



    Nilicheka kwa furaha sana na kwa dharau.



    “Mmmh ulidhania mimi nilikuwa nafaidi sana.” Niliongea mwenyewe.



    “Kila shetani na mbuyu wake ulidhania zile raha nilizokuwa napata mimi utazipata na Frank ulifikiri kila mtu ni mimi? Pengine kuna vitu vyako mimi nilikuwa navipenda Melania havipendi sasa ndiyo utakapoonja joto la jiwe.”



    Vipindi viliendelea huku nikiwa na furaha sana.



    Mara nyingi nilicheka mwenyewe kila nilipokumbuka migogoro kati ya Frank na Melania.



    Nilirudi nyumbani huku nikipanga mkakati wa kuchukua kompyuta ya Kelvin.



    Nilimpigia simu Kelvin.



    “Kelvin nimekumisi.” Niliongea mara baada ya kupokea simu yake. “Mimi pia, niko bize sana leo bado niko kazini.”



    “Naomba ukitoka upitie hata nikuone tu jamani.” “Wala usijali nitapitia.”



    Alipitia kama alivyosema.



    Alikuwa amebeba mgongoni begi ambalo mara nyingi walikuwa wakitumia wanachuo, begi hilo lilifanana sana na la kwangu.



    Nilitoka naye mpaka bustanini na kisha tukaanza kuongea mambo mawili matatu. “Kelvin samahani ngoja nikakuletee juisi, samahani nisamehe.”



    Alicheka.



    “Usijali mke wangu.”



    Nilinyanyuka na kisha kuelekea ndani.



    Nilichukua begi lake na kulipeleka chumbani kwangu na kisha nikachukua begi langu la madaftari na kuliweka pale.



    Tuliongea na baadae alichukua begi lake na kisha kuondoka.



    Nilianza kushughughulikia kompyuta yake ambayo haikuwa imefungwa.



    Niliingia moja kwa moja kwenye email.



    Nilihisi kudondoka.



    “Mungu wangu tumekwisha!!”



    Nilipiga ukelele wa nguvu mama alinisikia na kuja.



    Hata hivyo sikutaka mama aone, nilifunika kompyuta ile ndogo harakaharaka. “Nini mwanangu.”





    “Aanh mama nahisi kichwa kinaniuma sana naomba uniletee dawa.” Aliniletea dawa na maji, nilikunywa na kisha alikaa pembeni yangu. “Hupaswi kuwa hivyo mwanangu lazima ujipe moyo mkuu.”

    “Najitahidi  mama  lakini  naona  kama  mambo  yananizidia.  Mama  mimi  naona



    tutafute  njia  nyingine  ya  kuhangaikia  haya  matatizo  ama  sivyo  naona  kama



    tutajiingiza kwenye shida.”



    “Usiogope.”



    “Hapana mama mimi naona tuachane na Kelvin tusiendelee kumfuatilia mama hata kama bila ushahidi mimi ndiye ninayefunga ndoa nitakataa.”



    “Mmmh, vyovyote vile unavyosema wewe siwezi kukupinga.”



    “Sawa acha nimpigie simu.”



    “Wa nini?”



    “Aje achukue begi lake.”



    “Aanha sawa hakuna shida.”



    Nilimpigia simu.



    “Heloo..”



    “Heloo baby.”



    “Ooh, niambie ushanimisi.”



    “Hamna umesahau begi lako nilichanganya nikachukua la kwako nikadhani la kwangu ujue mabegi yetu yamefanana.”



    “Aanh halafu hata sijaangalia. Basi naomba usilifungue nitakuja kulichukua



    kesho.”



    “Hakuna shaka.”



    Nilifunika ile kompyuta na kisha kwenda kukaa kitandani.



    Mawazo yalikuwa mengi sana nilishindwa kujua ni nini nifanye.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Usiku ule ulipita tu wala sikuweza kupatwa na usingizi..



    Nilimpigia simu Kelvin mara baada ya kukucha.



    “Mimi naenda nalo chuoni utakuja kulifuata.” Alikuja chuoni kulichukua. Sikuwa na furaha kabisa.



    “Unaumwa?” Aliniuliza.



    “Hapana niko kawaida tu.”



    “Mmh nakuona kabisa unaumwaumwa.”



    “Hamna kweli siumwi nipo kawaida.”



    “Sawa hakuna shida.”



    Alichukua begi lake na kisha kuondoka.



    Nilihisi maumivu makali sana ya kichwa, niliamua kupanda gari yangu na kisha kuondoka.



    Nilitoka kwenye madarasa yetu na kisha kuelekea nyumbani.



    Hata hivyo nilitaka nikanunue maji kwa maana kichwa kilikuwa kikiniuma sana.



    Nilielekea mgahawani na nikapaki gari yangu.



    Nilishangaa kuona gari ya Kelvin ikiwa maeneo hayo.



    “Inamaanisha huyu hajaondoka anafanya nini hapa?!”



    Nilikumbuka mama alivyoniambia kwamba Kelvin huwa anawahi kuja mapema sana.



    “Mmh, ngoja niangalie nini anafanya.”



    Nilitembea kwa hatua za pole pole huku nikiangalia ni nini kilichokuwa kikitokea. Niliingia ndani ya mgahawa niliangaza macho huku na kule sikuweza kumuona nilitoka nje na kujiuliza ameelekea upande gani.



    Nilitoka na kisha kuingia mgahawa namba mbili nako hakuwepo.



    Niliangaza macho pande zote, nilizunguka mpaka nje lakini pia sikuweza kumuona.



    Nilirudi mpaka pale magari yalipokuwa yamepaki.



    Niliangalia, nilishuka na kisha kuelekea chini. Nilitazama pande zote hata hivyo hakuwepo. “Ameelekea wapi?!”



    Nilidhani pengine ameelekea kutoa hela katika ATM iliyokuwa ubavuni mwa duka la vitabu.



    Huko nako hakuwepo.



    Nilisimama kwenye uchochoro uliokuwa katika kati ya kituo cha posta na duka la vitabu nikiwa sijui la kufanya.



    “Ameelekea wapi sasa?!”



    Nilitoa simu ili nimpigie.



    Nilijionya kwamba kumpigia simu kungekatisha kile kitu ambacho alikuwa anakifanya katika maeneo hayo sikutaka nimpigie simu nilitaka nikutane naye bila kujua ili asitambue kama nilikuwa namfuatilia ili na mimi niweze kujua ni nini anafanya mahali hapo.



    Nilibaki nimeishikilia simu nikiwa nina mawazo mengi.



    Mara simu yangu iliita.



    Nilishituka sana nikihisi kwamba ni yeye ndiye alikuwa akipiga simu.



    Wala hakuwa yeye alikuwa ni mama yake na Franklin.



    Nilishangaa sana.



    “Huyu mama anataka nini kwangu mbona ananizoeazoea hivi!” Nilipokea simu nikiwa na hasira.



    “Hujambo mwanangu.”



    Mama aliongea kwa sauti ya unyonge.



    “Sijambo mama shikamoo.”



    “Marhabaa nadhani u mzima.”



    “Ndiyo mimi niko mzima.”



    “Masomo yanaendeleaje binti yangu.”



    “Yanaendelea vizuri tu nashukuru Mungu.”



    Niliongea huku nikiwa na shauku sana ya kukata hiyo simu niendelee na uchunguzi wangu niliona kama ananipotezea muda.” “Wote huko wazima?” Mama aliongea.



    “Ndiyo wote wazima familia yote nzima kila kitu kipo salama.” “Basi nashukuru Mungu.”



    “Ahsante sina shaka na nyie wote ni wazima.” “Hapana.” Mama alisema. “Kuna nini?”



    “Mmmh…” Mama alivuta pumzi tu.



    “Mama kuna tatizo gani?” Nilimuuliza.



    “Binti yangu mawazo yangu yote yamethibitika na mashaka yangu yote.” Nilishindwa kuelewa nini alikuwa anamaanisha.



    “Nafikiri nilikuambia mwanangu katika mahusiano kwa watu wa aina mbili tofauti yanahitaji uvumilivu na uaminifu sana. Sina shaka kwa sasa hivi hauko tena na Frank maana kila nikimuuliza amekuwa akinizungusha tu sijui tatizo ni nini. Lakini siamini kama ni Frank ndinye ambaye ni chanzo cha haya yote. Nilijaribu kuongea na rafiki yake na Frank siku ambayo Frank alikuwa naumwa amenieleza kitu ambacho kimenipa mwanga nina imani kubwa siyo frank ambaye amefanya hivyo. Umekosea sana kufanya maamuzi bila kuchunguza.”



    Alizidi kuichanganya akili yangu.



    “Hapana mama ni Frank mwenyewe ndiye ali….”



    “Sikiliza binti yangu jaribu kukaa na Frank na ukishindwa jaribu kuangalia mwenyewe kwa macho yako kuchunguza ili upate ukweli usikimbilie kufanya maamuzi kabla ya kuwa na uhakika unaweza ukawaumiza watu wengine na kujiumiza wewe mwenyewe.”





    “Sisi huku nyumbani tuko salama. Fiona na Furaha wote wanakusalimia uwe na siku njema.” Alikata simu.



    Nilibaki tu nimeishikila simu pale sikioni kana kwamba bado anaendelea kuongea.



    Moyo ulikuwa ukinipiga kwa kasi sana.



    Nilishindwa kuelewa.



    “Mama anamtetea Frank anajua alichokifanya mwanaye. Eti nimuulize nimuulize nini sasa?”



    Maswali kadhaa yalipita kichwani mwangu huku nikiwa bado nimeshikilia simu pale sikioni mwangu.



    Macho yangu hayakubanduka katika gari la Kelvin.



    Na ghafla mlango wa gari ile ulifunguliwa simu yangu ilikuwa bado imeganda sikioni kwangu kana kwamba imepigiliwa na misumari.



    Hata hivyo nilishindwa kuelewa ni kwa namna gani ilinitoka na kuanguka moja kwa moja mpaka chini mara baada ya mlango wa gari kufunguliwa na kisha watu waliokuwemo mule ndani kutoka.



    Melania na Kelvin walishuka kutoka ndani ya ile gari.



    Macho yangu yalishindwa kuamini kilichokuwa kikionekana mbele nilirudi kinyumenyume hadi nilipogota kwenye geti lililokuwa likizuia duka la vitabu lililokuwepo nyuma wangu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Machozi yalianza kunitoka kidogokidogo hata hivyo niliwahi kuchomoa leso yangu iliyokuwa kwenye mfuko wa suruali yangu ili kuyazuia machozi hayo yasionekane na wapita njia waliokuwa wakipita hapo mara kwa mara.



    Niliwatazama nilishindwa kuelewa nikitugani ambacho Kelvin na Melania walikuwa wakikifanya ndani ya lile gari.



    Nilipiga hatua za kinyonge huku nikiwa nimeisahau simu yangu pale chini.



    Hata hivyo nilisimama na kisha kugeuka na kurudi tena pale nilipokuwa nimesimama kabla ambapo paliniwezesha kuona kilichokuwa kikiendelea. Melania kwa wakati huo alikuwa akipandisha ngazi kuelekea mgahawani.



    Na Kelvin aliingia kwenye mlango wa dereva na kisha kuwasha gari yake na kuondoka.



    Kwa namna yoyote ile Melania angegeuka nyuma angeniona hivyo niligeuka harakaharaka na kuanza kupiga hatua za pole pole.



    “Dada dada.....” Nilisikia nikiitwa.



    Niligeuka.



    Nilisha ngaa kukuta ni Tina.



    “Oooh kumbe ni Christina.”



    Nilibaki nikimshangaa huku nikiwa sijui kama niondoke au niendelee kusimama mahali hapo.



    “Oonh ulikuwa umesahau simu yako hapa Sociolah.” Nilibaki nikiishangaa ile simu kana kwamba ndiyo naiona leo. “Au siyo ya kwako?”



    Niliichukua kwa kasi kutoka mkononi mwake.



    Kioo chake kilikuwa kimeharibika sana kilikuwa na mipasuko mingi kiasi kwamba sikuweza kuitambua kama ni ya kwangu.



    Niliiwasha, picha yangu nzuri niliyoipenda ilitokeza kwa juu.



    Nilishindwa kuongea roho iliniuma sana kuona simu yangu kuona imepasuka vile.



    “Ni ya kwangu.” Niliongea kiunyonge.



    “Pole Sociolah. Maneno yangu niliyokuambia ile siku hayajabadilika bado endelea kuyafikiria.” Aliondoka kana kwamba mtu ambaye ananihukumu.



    Niliumia sana moyoni mwangu.



    Machozi yalinitoka.



    Watu waliokuwa wakipita mahali pale waliendelea kunishangaa.



    Nilipiga hatua za haraka kuliendea gari langu nikiacha kabisa kununua maji.



    Nilisikia baadhi ya watu wakiongea.



    “Analia kwasababu amedondosha simu yake imepasuka.” “Simu yenyewe aina gani?”



    Waliendelea kujibizana.



    “Ni Samsung S6 kitu kama hiko.”



    “Bonge la simu hata ningekuwa mimi ningelia aisee.”



    Niliachana nao na kisha kuingia kwenye gari langu machozi yalinitoka mfululizo.



    Nililia... Nililia... Nililia tena.



    “Sasa mbona maisha yangu yameisha haribika mpaka kufikia hapa Kelvin ataniua



    mimi, atamuua baba yangu, atamuua mama yangu, atamuua Pink, atamuua Pinto.



    Ooh maskini wadogo zangu.”



    Nililia nililia sana.



    “Kelvin kwanini umetuchagua sisi? Tumekukosea nini lakini?” Nililia sana.



    Hadi nilipitiwa na usingizi.



    Nilikuja kushituka baadae muda ulikuwa umeenda sana.



    Nilihisi uchovu.





    Nilikuna kichwa huku nikijaribu kuweka sawa kumbukumbu zangu. “Imekuaje tena nikalala ndani ya gari?”



    Kumbukumbu zanagu zilianza kunirejea polepole wakati huo niliingiwa tena na hasira nilikasirikia maisha yangu nilikasirikia kila kitu. Nilitazama jinsi simu yangu ilivyokuwa haitamaniki.



    Niliwasha gari kwa hasira na kuendesha kwa mwendo wa kasi sana kuelekea nyumbani.



    Nilipofika nyumbani nilipitiliza moja kwa moja chumbani kwangu.



    Sikukaa hata muda mrefu mlango wa chumba changu uligongwa kwa nguvu.



    “Sociolah fungua mlango.” Alikuwa ni baba.



    Nilinyanyuka  kwa  uchovu  nikikimbilia  kanga  iliyokuwa  pembeni  yangu  kwa



    maana nilikuwa tu na gauni jepesi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilifungua mlango.



    Baba aliingia kwa hasira zote ilibidi nimpishe. “Umechanganyikiwa wewe?” Nilishangaa.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog