Search This Blog

Monday, October 24, 2022

NATAKA KUZAA - 2

 





    Chombezo : Nataka Kuzaa

    Sehemu Ya Pili (2)



    “Frank…. Frank….” Niliita.



    “Mmmh” Aliitikia tu kwa kukoroma.



    “Niache nilale Sociolah nina usingizi.”



    “Saa nne saa hizi.” Aligutuka.



    “Sasa usiku huu unataka uende wapi?”



    “Siyo saa nne ya usiku Frank ni saa nne asubuhu, Frank be serious…” Niliongea.



    Alishituka na kisha akanigeukia, alinitazama kana kwamba anaona mwandawazimu na kisha aligeuka pembeni na kuvuta simu yake na kuangalia muda.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Aanh! Saa nne asubuhi!” Alibaki tu ameshangaa.



    “Frank ona.” Nilimuonesha simu zisizopokelewa kutoka kwa mama pamoja na meseji zake.



    “Ooh God! Aisee wewe Sociolah unapendwa, simu zote hizo na meseji kibao



    kutoka kwa mama yako, yani ningekuwa mimi nisingepata hata meseji.”



    Ilinibidi  kucheka  maana  nilishindwa  kujizuia  na  kisha  nikamchapa  kofi  dogo



    shavuni.



    “Frank hivi unafikiria is it fan…. Naenda kumuambia nini mama?!”



    “Aaah sory.” Aliongea huku akiinama chini.



    Nilisikitika.



    “Nifundishe cha kwenda kuongea nyumbani basi.” “Sociolah…” Aliniita.



    “Eee..” Niligeuka na kumtazama, kila mara macho yetu yalipogongana nilihisi macho yangu yakipotelewa na nuru.



    Kana kwamba alikuwa akitaka kuongea kitu halafu ghafla akaghairi tulibaki tu tukitazamana.



    Sikuwa na kitu chochote mwilini mwangu zaidi ya shuka lililokuwa limenistiri, alisogeza mkono wake hadi kwenye mapaja yangu, nilifumba macho.



    Mkono wake mwingine ulitua moja kwa moja tumboni kwangu na kuanza kutalii maeneo mbalimbali.



    Sikuweza kuzuia kitu chochote na hatimaye tulifanya tena kitendo kile.



    Tulipomaliza nikiwa kifuani kwake.



    “Frank, niambie basi nikamwambie nini mama.” “Kwani uliagaje?”



    “Nilimuambia naenda kwenye party.”



    “Muambie party ilichelewa kuisha ikabidi ulale huko huko kwasababu uliona ingekuwa siyo vizuri kurudi usiku nyumbani.” “Mmh sijui atanielewa.”



    “Wewe kamjaribu kumuambia hivyo.”



    “Poa nitafanya hivyo, ngoja nijiandae niondoke.” “Ok poa.”



    Nilifungua wallet yangu na kumpatia laki moja na nusu.





    “Take care of your appearance.” Alicheka. “Hahahaaa.. Si ulipenda boga, penda na ua lake.” “Bwana acha utani.” Nilisema “Mimi sitanii.”



    “Sawa.”



    Baada ya kuoga pamoja nilimchukua Frank hadi bwenini, nikamshusha mbele ya block yao na kutoka kuelekea nyumbani sikutaka kupokea simu hadi nifike. Nilipokaribia kufika niliamua kuizima kabisa, nilipiga honi na geti lilifunguliwa mara moja, familia nzima ilitoka na kusimama nje kana kwamba walikuwa wakinisubiria mimi.



    “Sociolah uko salama mwanangu.”



    Mama aliniambia.



    “Niko salama mama.”



    Mwili wangu ulikuwa na uchovu sana sikutaka mama agundue hilo.



    “Nenda ndani kapumzike.” Nilienda ndani.



    Nilioga na kisha kulala.



    Mama aliniacha nilale.



    Niliamka baadae, uchovu ulikuwa umeniisha hakuna aliyeniuliza nilikuwa wapi wala kwanini sikurudi usiku uliopita, nadhani mama alikuwa ana mashaka sana na hali yangu huko nilipo, katika hali kama hizo mama huwa haniulizi. Siku zilipita na hakuna aliyeuliza kuhusu mahali nilipokuwepo.



    Uhusiano wangu na Frank ulizidi kustawi.



    Siku moja tulikuwa tukiongea na Frank.



    “Frank unajua nakupenda halafu hata sijui ni kwanini.” “Love doesn’t ask why.” Aliniuliza. “Unanipenda?” Nilimuuliza.



    “Nakupenda lakini….” Alimalizia na viemoji vilivyokuwa vikionesha huzuni.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kuna nini?”



    “Kuna kitu nataka nikuambie Sociolah.”



    “Nini Frank niambie.”



    Subiri usiwe na haraka…



    “Nitakuambia tu wala usijali.”



    “Ndiyo ninakusikia niambie.”



    “Hiki nitakuambia siku nyingine ngoja leo nikuambiae kingine.” Nikacheka.



    “Sasa ndiyo nini?”



    “Ok, nikuulize kitu?”



    “Hivi umejiandaaje na maisha baada ya kurudi chuoni?” “Aanh wewe niachie mimi nitajua jinsi ya kufanya.”



    “Mmmh, sawa, ila mimi ningependelea tusiwe na ukaribu kabisa watu wasije wakahisi chochote kati yetu.”



    “Frank niachie mimi najua jinsi ya kufanya, chochote kile nitakachofanya wakati tukiwa chuoni wewe kichukulie kama ni maamuzi yangu sawa.” “Haya.”



    “Mwaka mpya tutatoka tena au vipi?”



    “Wee.. Kazi ya kuomba ruhusa nyumbani unaijua ilivyo ngumu.” “Hahaha.. Mmmh… Toroka uje.”



    “Bwana.., unataka mimi nifukuzwe nyumbani, sijui lakini nikipata nafasi tutakuwa pamoja.”



    “Nilienjoy sana ile siku Sociolah natamani ijirudie tena.” “Hata mimi pia, sijui kama nitapata hiyo nafasi.” “Sociolah…” Niliitwa na baba. “Nitakupigia baba kaniita.”



    “Hahaha… Haya msalimie baba mkwe.”



    “Wee…eenhe.”



    Alicheka tu na mimi nilikacheka na kukata simu. Niliondoka hadi sebuleni ambapo baba alikuwa akiniita. “Haya niambie una udhuru gani?”



    “Kwanini baba?” Niliongea huku nikicheka. “Mwaka mpya tutakuwa na wageni hapa nyumbani.” “Aaah.. Nitakuwepo baba nilijua tunaenda sehemu.”

    “Kwahiyo kama tungekuwa tunaenda sehemu inamaanisha usingeenda.”



    “Hapana baba nilikuambia kwamba udhuru hautojitokeza tena, nitakuwepo na wala tungekuwa tunaenda popote pale tungekwenda.”



    “Sawa binti yangu, jiandae tu kwa ajili ya kupokea wageni.” “Sawa.”



    Siku zilijongea na hatimaye sikukuu ya mwaka mpya ilifika.



    Nilipewa kazi ya kufanya usafi nyumbani kuhakikisha mazingira yote yako safi na ya kupendeza kwa ajili ya wageni ambao waliotarajia kufika hapo mchana.





    Binafsi nilikuwa napenda sana swala la usafi na nadhani ndiyo sababu kubwa iliyomfunya mama akanipa hiyo shughuli.



    Mama na dada Linah waliingia jikoni wakati baba alikuwa amekaa nje barazani alisoma magazeti.



    Nilifanya kazi zangu pole pole kwa kuwa sikuwa na haraka yoyote, nilisafisha mazingira ya nje, nikasafisha ndani na kisha nikaanza kupamba sebuleni kwetu kwa ajili ya wageni nikitayarisha vitu mbalimbali ambavyo vingetumika na wageni katika siku hiyo.



    “Nyie nini?” Nilimsikia mama akiongea, nilijua tayari wakina Pink tayari wameshafanya mambo.



    “Hawa watoto bwana wajinga kweli.” Niliongea “Nini…? Kuna nini?” Mama alikuwa akionge.



    “Ona… Ona… Sikia huyu hapa mbishi.” Pink aliongea.



    “Kafanyeje?” Mama alimjibu.



    Sikusikia sauti zao tena ingawa nilivutiwa sana na mazungumzo yao nilikuwa nakitaka kujua wamefanya kitiu gani.



    Niliendelea na shughuli zangu, wakati huo nilisogea chumba cha maakuli kwa ajili ya kupanga vyombo ambavyo vingetumika kwa ajili ya maakuli siku hiyo, hapo niliweza kusikia kilichokuwa kikiongeleka kule jikoni.



    “Huyu anabisha kwenye hii simu ya dada Sociolah huyu siyo Matranka.” “Mungu wangu! Wamepataje simu yangu hawa?!” “Siyo yeye.”



    “Muangalie vizuri, wewe si unamkumbuka?” Sikusikia mama akiongea chochote.



    Nilisogea hadi kwenye mlango wa kuingilia jikoni na kisha kuchungulia kwakuwa ulikuwa wazi kidogo, mama alichukua simu na kisha kuangalia, kama alikuwa akivuta fikra.



    “Anafanana naye.”



    “Ni yeye mama.”



    “Ni yeye, Pinto mbishi kweli.”



    “Halafu huyu hapa ndiyo alikuwa anaongea….” Nikaingia ghafla.



    “Kuna nini kwenye simu yangu?”



    Mama alikata haraka na kisha akanipa.



    “Sijui hawa watoto walikuwa wanachezea simu yako.” Aliongea mama na kisha kugeukia upande mwingine na kuendelea na shughuli zake.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Wewe Pink mara ngapi nimekuambia kuhusu swala la kuchezea simu yangu kwanini hunisikii.”



    “Pinto huyo ndiyo mbishi, mimi nilimuambia huyo Matranka anabisha ndiyo nikaja kumuuliza mama.”



    Nilishindwa cha kuongea, nilitoka nje haraka na kuelekea chumbani kwangu na kisha kujifungia. Baada ya muda mama aliingia chumbani kwangu, alinikuta kama niliyechanganyikiwa.



    “Sociolah nini mwanangu?”



    “Hamna kitu mama.”



    “Najua kuwa hamna kitu lakini kwanini hali yako imebadilika ghafla.”



    “Mama mimi sipendi jinsi wakina Pink wanavyowadharau watu, kwani Matranka ana nini na akiwepo kwenye simu yangu kuna nini si ni mwanafunzi mwenzangu na pia haitwi Matranka anaitwa Frank, kwanini lakini anakuwa hivi na wewe kama mama badala ya kuzuia unawasapoti watoto.”



    “Sasa mwanangu mimi nifanyeje wewe umeacha simu yako bila kuweka password na watoto wameifikia wanaichezea, sasa mimi nifanyeje.”



    “Hata kama mama lazima kuwakemea.” “Sijui tu kwanini unamtetea huyo Frank.”

    “Hapana mama naweza kumtetea mtu mwingine yoyote.”



    “Sijawahi kukuona katika hali hii Sociolah, mimi ni mama yako.” Mama aliniambia.



    Niliamua kunyamaza na kugeukia upande mwingine.



    Sikutaka tena kuendelea kukaa sebuleni.



    Wageni walifika hata sikutoka kuwasalimia nadhani waliniulizia maana muda kidogo Pink aliingia chumbani kwangu kuniita.



    “Wewe dada unaitwa na baba mdogo, kasema hajakuona siku nyingi kakumisi.” “Nakuja.” Alitaka kutoka nikamuita.



    “Wewe Pink njoo, ulikuwa unatafuta nini kwenye simu yangu.”



    “Si nilikuambia, Pinto alikua anabisha yule siyo yule mkaka tuliyemkuta na matranka siku tuliyokuja mara ya kwanza chuoni kwenu.”



    “Kwahiyo kama ndiyo yeye ndiyo inakuaje.”



    “Huyo Matranka…...”



    “Siyo Matranka, Frank.”



    “Matranka.”



    Pink alinibishia, nilishikwa na hasira kiasi cha kutaka kumpiga kofi.





    “Matranka, mimi namjua Matranka majina mengine siyajui.” Aliongea. Nilivuta hasira zangu, nilitamani kukitafuna kiumbe kile lakini nilishindwa. “Ok nenda ila usiseme chochote kama nimekuuliza.”



    “Kwani dada amefuata nini kwenye simu yako au na wewe unataka matranka?” “Ndiyo nataka tranka niwekee nguo zangu.”



    Pink alicheka kicheko cha kimbea na kisha kugonga mikono yake.



    “Halooo…aya.. Sawa.”



    Alitoka nje huku akicheka, nilisikitika tu.



    Baba yetu mdogo aliyekuwa akiishi maeneo ya Kimara na baba yetu mkubwa ambaye alikuwa akiishi Oysterbay.



    Wote walikuwa ni watu waliokuwa na nafasi nzito serikalini, walikuwa wakijiweza na mipango yao ilikuwa kwamba kila kwenye sherehe basi wanakwenda kutembelea familia moja wapo.



    Nilifika sebuleni na wala sikuwa hata nimejiandaa vizuri.



    “Sociolah” Baba aliniita.



    “Unaumwa?”



    “Hamna baba sijisikii tu vizuri.”



    “Basi pole, ungeenda kukaa nje upate hewa safi.” “Usijali baba nitakuwa salama.” “Kajiandae basi ujumuike na wageni.”



    Niliondoka na kuelekea chumbani kwangu, nilioga na kisha kubadilisha nguo, nilivaa nguo nzuri ambayo baba alininunulia kwa ajili ya sikukuu hizo. Nikatoka nikaenda kujumuika nao sebuleni.



    Wote kati yao niliwatambua isipokuwa mtu mmoja tu ambaye sikumtambua.



    Katika siku kama hiyo huwa wanafanya kama sherehe fulani hivi fupi.



    Walianza na utambulisho.



    Baba alitutambulisha familia yake yote, baba mdogo alitambulisha familia yake yote na kisha baba mkubwa alitambulisha familia yake.



    Ni mtu ambaye sikumtambua alikuwa ni mvulana wa makamo alionekana kuwa na maisha mazuri hakutambulishwa, nilibaki nimeshangaa.



    “Sasa kama hajatambulishwa amekuja hapa kama nani?” Baada ya kumaliza utambulisho baba alisimama. “Mbona kuna mgeni mwingine hafahamiki hapa?”



    “Huyu bwana ni mwenzangu tunataka kuanzisha naye biashara mpya ni kijana mwenye mafanikio sana na alikuwa nje ya nchi kwa muda mrefu na sasa amerejea



    hivyo nimependa naye ajumuike pamoja nasi kwa maana muda si muda mtasikia



    tunafanya mambo makubwa sana ni kijana mwenye hari ya mafanikio na mchapa



    kazi, mimi binafsi namkubali sana.”



    “Karibu sana kijana wangu.”



    “Ahsante, naitwa Kelvin.”



    Walipeana mikono na mama na watu wengine waliopenda kumpa mikono.



    Baada ya salamu fupi ulifika muda wa maakuli, tulisogea mezani na kisha kuanza kupata chakula, siku hiyo alipikwa mbuzi mzima.



    Kulikuwa na vyakula vya aina mbali mbali hata sikufurahia kuvila. “Sociolah, unaumwa mwanangu.” “Hapana mama.”



    “Hebu kakae nje upate upepo kidogo.”



    “Pink alikuwa akiniangalia tu kwa macho yake makavu.”



    “Huyu mtoto ana laana kweli.” Nilisema kimoyomoyo, nilinyanyuka bila hata kugeuka na kuondoka zangu kuelekea nje.



    Nilienda kukaa bustanini nikiwa nimeshikilia simu yangu, nilimtumia meseji Frank lakini hakujibu.



    Nilibaki nikiwa na lindi la mawazo yaliyochanganyika na huzuni na ghafla niliguswa begani.



    “Mama nahitaji kuwa peke yangu naomba uniache” Niliongea.



    “Sociolah..”



    Ilikuwa ni sauti ya kiume ambayo sikupata kuisikia kabla, niligeuka haraka na kumuangalia, alikuwa ni Kelvin.



    “Kelvin karibu.” Niliachia tabasamu la kulazimisha.



    “Tayari nishakaribia.”



    Alivuta kiti na kukaa mbele yangu, alikuwa akinitazama usoni, niliinamisha uso wangu ambao ulikuwa umejawa na huzuni.



    “Pole.”



    “Pole ya nini?” Nilimuuliza.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Pole ya mambo ambayo yanakukwaza.”



    “Aanh.. Usijali nipo kawaida.”



    “Nakuona haupo kawaida Sociolah, anyway. Mimi nafanya biashara na baba yako na muda siyo mrefu tunataka kuanzisha kitu hapa nchini. Nimetokea Marekani nilikiuwa nakaa kule na familia yangu yote ipo kule na ndiyo maana sikukuu ya mwaka mpya sikuwa hata na sehemu kwenda nilikuwa sina kampani ndiyo





    nimefika tu nchini, kwa kulitambua hilo baba yako aliamua tuungane kwa pamoja.”



    Sikuelewa mantiki ya vyote hivyo alivyokuwa akiniongelesha nilitabasamu tu kumuonesha kwamba tuko pamoja ingawa sikuwa nikivutiwa na kile alichokuwa akiongea.



    “Sawa nashukuru.”



    “Una ndoto gani Sociolah?”



    Nilicheka.



    “Unafahamu hata nini ninasomea?”



    “Najua… Najua unasomea udaktari.”



    “Sasa kuniuliza nina ndoto gani unamaanisha nini? Si unafahamu kabisa



    ninasomea udaktari.”



    “Hahaha…”



    Alicheka kana kwamba ananicheka.



    “Mbona mimi nina taaluma ya udaktari tena ni daktari mzuri tu wa upasuaji lakini



    ninafanya biashara.”



    “Aanh.”



    “Sociolah mbali na kuwa daktari unataka nini?” “Nataka kuzaa.”



    Alishituka halafu akacheka.



    “Unataka kuzaa?”



    “Ndiyo.”



    Alicheka kama anacheka kwa dharau na kisha akatikisa kichwa chake. “Nilizani naweza kukusaidia kutimiza ndoto zako, sijui kama naweza.” Niliachia kicheko cha nguvu.



    “Ahsante nashukuru.”



    Nafikiri yupo mtu ambaye atakuwezesha uzae Sociolah.” “Yes..”



    “Baba anamjua?”



    Nilipojibu swali la mwisho nilijibu kwa bashasha zote lakini lile tabasamu liligandia kati na kisha kutoweka kabisa, nilishindwa cha kumjibu, alitabasamu. “Anyway not a problem, mimi siwezi kwenda kumuambia.”



    “Hata kama nazani hawezi kupaniki sana kwasababu umri umeenda pia.” “Sociolah wewe bado ni mdogo sana.” “Udogo wangu nini mimi?”



    Alicheka.



    “Anyway keep it up. Unampenda sana rafiki yako wa kiume.” “Siyo rafiki yangu wa kiume ni mpenzi wangu.”



    “Aanh sorry na ahsante kwa kunirekebisha, vizuri, mpende sana na hakika yeye atakufanya utimize ndoto yako ya kuzaa.”



    “Ooh well Thank you. Aanh…. What about your….”



    “Mimi ndoto yangu ni…”



    “Sijaongelea kuhusu ndoto.”



    Nilimkatisha, alicheka.



    “Ok uanongelea kuhusu swala la familia si ndiyo?” “Ndiyo.”



    “Aanh kwa sasa hivi…. Hahaha….”



    Alicheka na kisha kuishia kati.



    “Unataka kunidanganya?”



    Nilianza kumzoea.



    “Hapana, ni kwamba baba yangu na mama yangu wote ni watanzania na baba yangu ni daktari. Muda mrefu sana baba yangu alikuwa akifanya kazi Tanzania. Niliondoka Tanzania nikiwa mdogo sana yapata nikiwa kama nina miaka mitano, nilielekea Marekani, nimeishi kule miaka yote na mara chache nilikuwa nakuja likizo kutembelea ndugu jamaa na marafiki. Nilikutana na baba yako pia muda mrefu kidogo uliopita wakati huo ndiyo naanza masomo yangu ya udaktari. Lakini kwa vile tulikuwa na ndoto za kufanana tulikuwa tunawasiliana muda mwingi na hatimaye tukaweza kupanga kitu ambacho tunataka kukifanya na mpaka sasa nimeweza kumaliza masomo yangu. Nimeajiriwa na maisha yangu najitegemea nimeamua kuja Tanzani ili nifanye kitu ambacho nilikuwa nataka kufanya na baba yako, lakini kitu kikubwa sana nampenda mama yangu.”



    “Huyu mbona anaanza kujibu maswali ambayo mimi sijamuuliza.” Niliongea mwenyewe na nafsi yangu, ila niliendelea tu kumsikiliza mwisho wake ulikuwa ni nini.



    “Mama yangu ni mwanamke ambaye wa utofauti sana kati ya wote amabao nimewahi kuishi nao uko marekani hivyo nataka kuoa mwanamke wa kitanzania. “Hahaha…” Nilicheka wala sikuwa najua kama huo ndiyo ulikuwa mwisho wa hadithi yake.



    “Ooh nice, Nakutakia kila lakheri.” Niliongea.



    “Kelvin…” Baba aliita.



    “Naona ushapata rafiki.”



    “Yeah Sociolah is so Charming, nimefurahi sana kumfahamu.” “Naona hata homa imepoa.”



    “Hamna baba, nimefurahi pia kumjua Kelvin.”



    Baba alikaa pembeni yetu tulizungumza mawili matatu.



    “Unajisikiaje saa hizi mwanangu.”



    “Basi twendeni ndani tukaendelee na mazungumzo yetu.” Tulinyanyuka wote kwa pamoja na kuelekea ndani



    “Naona Sociolah amepata rafiki maana anakuwa mpweke sana.”



    “Mpweke tena! Inamaanisha baba amemleta Kelvin ili awe rafiki yangu fine lakini.”



    Muda ulizidi kwenda na hatimaye tulifungua chuo, tulifungua ilikuwa ni siku ya jumatatu yapata kama tarehe tano hivi mwaka 2016.



    Ilikuwa ni furaha kurejea chuoni kwangu mimi ingawa mama hakutaka kabisa. “Sociolah mwanangu vutavuta kidogo. kwani kuna nini mimi nitakuwa nakupeleka chuoni.”



    “Mama nimewamisi hata marafiki zangu, na pia nataka tukaanze kusoma mama.” “Sociolah kwani mimi nikikutoa hapa nyumbani kukupeleka chuoni na kukurudisha utakuwa husomi?”



    “Mama nitakosa majadili na wenzangu.” “Utajadili na nitakuwa nikikusubiri mwanangu.” “Aanh…” Nilishindwa cha kujitetea.



    “Kaa tu hata wiki moja tu halafu wiki ijayo unarudi sawa.” “Sawa mama.” Niliitikia kwa shingo upande.



    Nilitoka na kwenda chumbani kwangu.



    Siku iliyofuata asubuhi kabisa mama alikuja kuniamsha.



    “Jiandae twende chuo.”



    Niliamka kiuvivu uvivu nikaoga nikavaa vizuri nikabeba begi langu la madaftari. Nikapanda kwenye gari. Mara zote mama yangu alipenda nikae kwenye siti za nyuma kwa maana yeye alikuwa anasema kwamba wewe mwanangu ni mtoto wa mfalme na malkia hivyo hupaswi kukaa mbele. Siti ya nyuma ni sehemu ambayo wanatakiwa wakae watoto wa kifalme. Na mimi nilifurahia sana, nilifungua mlango wa nyuma na kisha kuketi.



    Mama aliingia na safari ya kwenda chuoni ilianza, nilikuwa nikiwaza maisha yataendaje huko.





    Alinileta hadi kwenye madarasa yetu na mara zote yeye alikuwa akinifungulia mlango wa gari. Alishuka watu wote macho walielekeza kulipo gari letu nilikuwa nikiwaangalia tu kupitia dirishani mama alifungua mlango na kisha nikashuka.



    “Uwe na siku njema mwanagu.” Aliongea na kisha akanikumabtia na kunibusu shavuni na kisha akafunga mlango.



    “Kuna tatizo lolote?”



    “Hapana mama.”



    “Unahitaji hela?”



    “No.. Ninazo mama.”



    “Sawa.” Nilipiga hatua za kivivu kuelekea darasani.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilikutana na Melania alikuja akanikumbatia kwa nguvu zote.



    “Wewe mtoto umekaa nyumbani wiki moja tu umenenepa hivyo?”



    “Nimekumisi sana Melania.”



    “Jamani si urudi Hostel.”



    “Mama kaniambia nirudi wiki ijayo.”



    “Jamani tumekumisi.”



    “Vipi mpo wote mmeshafika?”



    “Yeah na Fety yupo yani kakumisi kweli na Monica wote.” “Nitarudi bwana hata usijali sawa.”



    Muda wa kipindi ulianza tuliingia darasani, nilijaribu kutupia jicho kila kona kumtafuta Frank lakini sikumuona.



    “Yuko wapi huyu?”



    “Melania alihisi kwamba kuna mtu namtafuta na ilionekana darasani kwetu kote ni



    Frank tu ndiye ambaye hakuwepo kwa maana darasa letu hallikuwa na watu wengi.



    “Unamtafuta Frank?” Melania aliuliza.



    “Nilicheka tu.”



    “Hapana lakini simuoni.”



    “Sijui yuko wapi?”



    “Anaumwa.”



    Mtu wa tatu aliitikia kutoka pale tulipokuwa tumekaa alikuwa ni Innocent “Ooh Innocent I miss you, Frank anaumwa ?” “Yeah anaumwa.”



    “Anaumwa nini?”



    “Hajisikiisikii anaona uchovuichovu anahisi ana malaria.” “Ameenda hospital?”



    “Heeee….  Maswali  yote  hayo  ya  nini?  Unataka  kujua  nini  kuhusu  Frank?”



    Melania aliingilia.



    “Kwani vibaya kumjulia mtu hali kama anaumwa?” “Innocent alitabasamu.



    ‘Vizuri umejibu vizuri sana Sociolah.”



    “Eenhe niambie ameenda hospitali?”



    “Nimemuacha chumbani sijui kama ameenda hospital.”



    “Aanh sawa.” Nilitaka kuongea neno lakini niliogopa uwepo wa Melania niliamua kunyamaza.



    Tulipotoka darasani nilianza kumkwepa Melania. Siku hiyo tulikuwa tukimaliza vipindi vyetu saa kumi za jioni.



    Nilimkwepa Melania dakika mbili tu tulikuwa tumepotezana nilikimbia haraka Shuttle Point na kupanda gari za Mabibo.



    Sikutaka kumuambia Frank kama kwake, nilitaka iwe surprise niliposhuka kwenye gari pale Mabibo nilimnunulia juisi ya azam kubwa, nikamnunulia matunda aina ya tufaha (Apple.), nikanunua na chakula, nilinunua Chipsi na kuku nusu na maji ya kilimanjaro makubwa. Nikafikiria kitu gani ambacho sijanunua, nilikaa nikawaza nimnunulie nini.



    “Si anaumwa ngoja nimnunulie glucose.”



    Nilienda kumnunulia glucose kisha nikakumbuka kujinunulia mafuta yangu ya karafuu kwa ajili ya kujikandia na kutoka kisha kuelekea chumbani kwa Frank. Nilifika pale niligonga mlango, nilifunguliwa na mtu mwingine ambaye sikuwa nikimfahamu na ndiyo ilikuwa mara kwanza kuonana.



    “Karibu mrembo.” Alinikaribisha kwa bashasha zote.



    “Ahsante.”



    Kabla sijaingia nilimuuliza.



    “Frank yupo?”



    “Yeah yupo.”



    “Naweza kuingia kuja kumuona?” Niliongea kwa sauti ya chini wala sikutaka Frank ajue kama niko hapa mlangoni.



    “Ingia.”



    Alishangaa sana kwa kweli, nahisi nilikuwa mtu wa kwanza kuja kumtafuta Frank zaidi ya Innocent ambaye ndiye aliyekuwa rafiki yake, yeye peke yake. Mkaka alibaki ameshangaa tu niliingia hadi kitangani kwa Frank ambapo alikuwa amelala na kujifunika shuka mwili mzima nilikaa pembeni yake na kisha kumbukumbu ya





    usiku ule ambao tulikuwa pamoja kitandani hapo ilinijia, nilibaki tu nikitabasamu. Yule kaka alikuwa amesimama mlangoni na wala hakuwa amefunga mlango, niligeuka na kumtazama nikaachia tabasamu alitabasamu na kisha kuja mpaka kwenye meza. Alichukua chukua baadhi ya vitu, alikusanya vingine aliviweka vizuri kisha akaniaga.



    “Natoka.”



    “Mbona unanikimbia.”



    “Hamna nilikuwa najiandaa kutoka.”



    “Aaah, sory Frank amekula?” Niliuliza.



    “Hapana nilikuwa nataka pia nikamtafutie RB huko nje.” “RB?” Nilicheka.



    “Ok fine, nimemletea chakula usinunue, sawa.” “Hamna shida.” Alisema na kuondoka.



    Hata mimi pia nilitamani aondoke ili atuachie nafasi, aliondoka. Nilienda mlangoni nikafunga mlango na kisha nikasogea pale kitandani alipo Frank,



    “Frank.” Niliita wala hakutikisika, nilimvuta shuka bado hakuamka, nilimbusu shavuni aliachia tabasamu.



    “Sociolah.” Aliita akiwa bado hajafungua macho niliachia tu tabasamu. Alifungua macho kichovu na kisha akageuka upande wangu.



    “Yes darling.” Nilifurahia sana kuitwa hilo jina mwili mzima ulinisisimka.



    “Hata hujaniambia kama unaumwa.” Alicheka tu.



    “Sikutaka upate shida yoyote, siku ya kwanza kwenda chuo halafu upo nyumbani isigekuwa vizuri.”



    “Jamani nani kakuambia isingekuwa vizuri?” “Sorry kama nimekosea.” “Usijali, unajisikiaje?”



    “Najisikia vizuri kwasababu umekuja.”



    “Hauko serious.”



    “Nilijisikia kuumwa sana lakini umekuja nimepata hata afadhali.” “Hahaha…” Nilicheka.



    “Amka ule basi mpenzi wangu.”



    Alijitahidi kunyanyuka ingawa alionekana kama akipata maumivu. “Frank what is wrong.”



    “Mwili mzima unauma Sociolah..”



    “oooh pole..”



    “Aaah.. Joto limekuwa kali sana.”



    Chumbani kwao hakukuwa na feni.



    “Utafanyeje? Uvue basi shati.”



    “Eenh… yani mara nasikia baridi kali mara nasikia joto kali itakuwa ni malaria.” “Nikupeleke hospitali?”



    “Mimi naogopa sindano bwana.”



    “Utakufa.”



    “Eeenh najua nitakufa.”



    “Usiseme hivyo bwana ukifa utaniacha mimi na nani?”



    “Si na baba yako.”



    “Hahaha…” Nilicheka.



    “Ngoja nifungue mlango kidogo.”



    Nilifungua mlango na kuacha nafasi kidogo ili hewa iingie mule ndani. Alivua shati na kisha kubakia kifua wazi, alijitahidi kukaa pale kitandani na kisha nilifungua chakula nilichokuwa nimemletea na kuanza kumlisha taratibu.



    “Wewe Sociolah chakula kitamu.”



    “Kula sasa upate nguvu mgonjwa sawa.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nakula mama.”



    Hakika alikuwa anakula kana kwamba ndiyo anakula siku ya kwanza. “Frank kula taratibu basi.”



    “Yani nahisi kama kitapotea vile.”



    Nilicheka.



    “Hebu kula bwana.”



    Pamoja na ugonjwa wake alijitahidi sana kuchangamka, alikula kadri alivyoweza na mara tu aliniambia kwamba nimetosheka.



    “Frank.” Nilimuita.



    “Unajisikiaje sasa?”



    “Sasa najisikia afadhali ila mwili unauma uma.”



    “Ok lala nikumassage.”



    “Eeenh.. Unifanyeje?”



    Nilicheka.



    “Nikukande.”



    “Sasa hapa hakuna heater ya kuchemshia maji au unataka unikande na maji ya baridi.”



    “No…. Nakukanda kwa mafuta.”



    “Mafuta gani? Mimi natumia baby care.”



    “Ninayo ya kwangu usijali.”



    Niliongea huku nikicheka.



    “Ok, nilaleje sasa?”



    “Lala kifudifudi.”



    Alilala kifudifudi na kisha kugeukia ukutani.



    Nilinyanyuka na kisha nikapandisha gauni langu juu na kisha kumkalia kiunoni. “Unaumia.”



    “Hapana.” Alijibu kwa sauti iliyofifia.



    Nilifungua mafuta na kisha kujimwagia kwenye mikono na kuanza kumpaka yale mafuta huku nikimsugua taratibu aliishia tu kuguna.



    “Ukijisikia kuumia uniambie.”



    “Aaah naumiaje na mikono yako ilivyo milaini hivyo.” Nilicheka, niliendelea kummassage.



    “Frank siku nyingine ukiwa unaumwa uniambie, sawa.”



    “Nitakuambia usijali.”



    “Sawa.”



    “Umekunywa dawa yoyote.”



    “Nimekunywa tu panado.”



    “Lakini Frank kwanini umekataa kwenda hospital.” “Nilisha kuambia naogopa sindano.”



    Nilicheka tu.



    “Sawa lakini I hope mpaka kesho utakuwa unajisikia vizuri unaweza ukaja chuoni, mimi nimetoroka tu hapa mama atakuja kunichukua saa kumi.” “Sociolah kwanini umetoroka?”



    “Don’t ask me why.”



    Alicheka kidogo tu na kisha akanyamaza kimya.



    Niliendelea na kazi ya kumkanda nikimpapasa maeneo mbali mbali ya mwili wake kwa ajili ya kuondoa uchovu.



    Ghafla mlango ulifunguliwa kwa pupa na mtu ambaye alifungua mlango aliingia, nilihisi tu ni yule mkaka ambaye nilimkuta hapo chumbani maana mambo yake yalionekana kufanyika rafu rafu sana, hakupiga hodi wala nini aliingia tu.



    “Hey what is wrong?” Niliongea huku nikijaribu kushusha gauni langu. La haulaaa…!!!!!!!!





    Kinyume na matarajio yangu yule mtu hakuwa yule mkaka niliyemkuta pale chumbani alikuwa ni Innocent. Hakika alipigwa na butwaa sana kuniona mule chumbani kwa maana alibaki ameachia mdomo wazi huku amesimama pale mlangoni kana kwamba mtu ambaye anataka kukimbia lakini akaishiwa nguvu.



    “Sociolah...” Alipata nguvu ya kuongea niliachia tabasamu.



    “Yes..”



    “Unafanya nini hapa?”



    Huku nikiwa na tabasamu lililoupamba uso wangu. “Kwani kuna tatizo lolote mimi kuwepo hapa?” Alishangaa tu.



    Mkononi alikuwa ameshika mfuko alifunga mlango na kisha kusimama. “Sijaelewa maana ya uwepo wako hapa, umekuja kufanya nini?Nani aliyekuita humu? Na umeingiaje kwenye hiki chumba? Na umejuaje kama Frank anakaa humu?”



    Aliuliza maswali mfululizo na ambayo yalionesha hayana mwisho.



    “Hey stop... Mimi ni CR nimekuja kumuangalia memba wangu wa Darasa anaumwa.”



    “Aaah Sociolah!!” Alishindwa tena kuendelea kuniongelesha. “Au bado mnania mbaya na Frank umekuja kumfanyia nini?” “Eeeh.... Eeeh....” Frank anageuka na kumtazama.



    “Kama angekuwa na nia mbaya wewe unafikiri angenishinda?” “Anafanya nini sasa hapa?”



    Frank aliachia tabasamu tu, nilinyanyuka mgongoni kwake na kisha kukaa.



    Frank naye alijitahidi kunyanyuka akakaa na kisha akazungusha mkono wake kiunoni kwangu akanivutia kwake, nikamuegamia begani.



    “Sapraizi...” Frank aliongea.



    “Whaat?!..... Mimi sielewi mnataka kujaribu kunionesha nini? Am i dreaming?”



    “Vyovyote vile.”



    “Ahaa... Kwanza Frank si unaumwa.”



    Innocent alianza kuishiwa point alipiga hatua zilizoonesha kuchoka hadi karibu na meza alivuta kiti na kukaa huku akitutazama.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ndiyo anaumwa.” Nilijibu.



    “Sociolah mimi bado nashindwa kuelewa hebu basi nielezeeni niwaelewe.”



    “Am.... Dating.... Frank” Nilijibu.



    “Tangu lini?”



    “Tuna about a month.”



    “Aaah!” Huku akijawa na mshangao aliachia tabasamu. “Aisee... Mimi siamini acheni kunidanganya.” “Unataka tufanye nini ili uamini?”



    “You guys kissing each other....”



    Nikamuangalia Frank alikuwa ameachia tabasamu lake zuri kabisa kwa kweli nilisahau kama pembeni kuna mtu ingawa katika hali ya kawaida ningeona aibu. Nilimvuta Frank karibu yangu na kisha tukafuatia na busu zito na refu sana, tulijisahau kama pembeni yetu kuna mtu.



    Aaah.... Basi inatosha inatosha.”



    Innocent alisema na hapo akatushitua. “Kwahiyo mnafanya kama mnanikomesha vile.” “Aaah.... Hamna wewe si hutaki kuamini.” “Aaah kwahiyo ilikuaje kuaje hasa.”



    Nilicheka.



    “Unataka ujue ili iweje yani?”



    “Mimi bado mmeniacha na bumbuwazi nashangaa sana hata sijawahi kuhisi na ndugu yangu Frank hata kuniambia!”



    Aliongea Innocent kwa bashasha zote. “Nilikuwa nasubiri kitu kama hiki kitokee.” “Hongera sana Sociolah mama, wewe ni mtu mzima.” “Mmmhh..” Niliachia tu kicheko.



    “Ok basi kama umepata mtu wa kukuangalia acha mimi niondoke.” “Aaah no mimi nimetoroka tu chuoni.”



    “Hata mimi nimetoroka maana Frank alinitumia meseji hajisikii vizuri nimemletea dawa hizi hapa atumie.”



    “Kwasababu uko naye hapo unamuangalia acha mimi nirudi chuoni kuliko tukae hapa tukakosa vipindi wote.”



    “Hahaha... Aya nenda kasome halafu mimi utakuja kunielekeza si eti eeh.” Niliongea.



    “Sawa bwana.”



    Alindoka nilifungua baadhi ya dawa na kumpatia Frank.



    Tuliendelea kupiga stori za hapa na pale huku tukiwa tumejilaza pale kitandani. “Frank kuna kitu ulisema unataka kuniambia.”



    Alicheka.





    “Mimi naumwa bwana unaniambia vitu gani hivyo badala ya kunifariji unaanza kuleta mambo ya ajabu.”



    “Hasa kwani hicho si unakijua wewe mimi sijui kama ni cha ajabu pengine ni kizuri kinaweza kukufanya upone.”



    “Hahaha aya bwana nitakwambia siku yake mama usiwe na papara sawa.” “Aaah.. Hasa siku yake siku gani?”



    “Sikia Sociolah yani ni kama embe saa hizi halijaiva litakuwa chungu lina uchachu subiri liive na utakula.”



    “Bwana sasa si bora usingeniambia ukasubiri siku ambayo unataka kuniambia.” “Sorry mama kwa hilo samahani.”



    “Mmmh mimi nimekasirika.”



    “Usikasirike basi mke wangu.”



    Nilishituka na kumgeukia na kumuangalia.



    “Umeniita nani?”



    “Sociolah.”



    “Bwana siyo hivyo.”



    “Kweli nimekuita Sociolah.”



    “Hamna hujaniita hivyo yani kama umesikia kitu kingine basi ni mawazo yako mimi nimekuita Sociolah.”



    Alinifanya niamini kweli ameongea hivyo.



    “Mmmh mimi sidhani bwana halafu wewe unapenda sana utani.” “Sasa kama umenisikia unataka tena nini.” “Hahaha.” Nilicheka.



    “Mimi nataka tu urudie, rudia basi mpenzi wangu.”



    “Nimekuita Sociolah.”



    “Bwana siyo hivyo.”



    “Sasa umuamini mume wako?”



    Niligeuka na kumtazama nikashindwa cha kuongea.



    “Eti mke wangu huniamini.”



    “ahaa...” Nilitabasamu tu.



    “Nakuamimi mume wangu.”



    “Sawa nakupenda.”



    “Nakupenda pia.”



    Nikajilaza kifuani wake ghafla simu yangu ilita.





    Niliivuta haraka haraka nilijua tu ni Melania alikuwa akinitafuta, hakuwa ni Melania alikuwa ni mama.



    “Mwanangu...” Aliniita tu nilivyopokea simu.



    “Yes mom.”



    “Nimepatwa na dharula naelekea ofisini kwa baba yako kwahiyo naomba uchukue usafiri utakaokurudisha nyumbani kama huna hela ya kutosha niambie nikutumie.” “No mom ninayo hela ya kutosha.”



    “Ok fanya hivyo mwanangu sorry kwa usumbufu.” “Usijali mama naelewa.”



    “Aya ahsante binti yangu uwe na wakati mwema.”



    Aliongea na kukata simu, hakujua tu kuwa amenipa furaha sana nilijua tu kama mama angechelewa kurudi nyumbani hivyo nilikuwa na muda mrefu wa kukaa na Frank siku hiyo.



    Nilikaa hadi jioni na kisha nilitoka na kurudi nyumbani niliwakuta wakina Pink na dada Linah.



    “Baba mbona hajarudi wala mama.”



    “Mama na baba wameenda kazini.”



    “Oooh mimi nimeshawamisi.”



    “Umewamisi nini?”



    Pink na Pinto walianza kujibizana niliwaacha tu na kuelekea chumbani kwangu. Niliingia chumbani kwangu na kupitiliza bafuni kwakuwa bafu lilikuwa lilikuwa chumbani kwangu yani master bedroom.



    Nilioga kuondoa uchovu na nilitoka nilimkuta Pink alikuwa ameshikilia simu yangu sikioni.



    “Aaah..! Pink unafanya nini?” Niliongea. “Baby wako alipiga.” Huku akinipa simu yangu. “Nini?!!”



    Aliongea, “Mimi nimeingia nimekuta simu yako inaita umeandika my oga, oga si



    maana yake Oxygen eeenh.”



    “Haaa..!!”



    “Nimepokea akaniambia baby, hii hapa.”



    Simu ilikatika.



    “Jesus..!!!!”



    “Pink..... Pink.... Nakuomba usiseme usimuambie baba kitu chochote sawa.”



    Alipandisha mabega juu na kubinua mdomo wake na kisha alitoka nje.



    Siku iliyofuata asubuhi na mapema mama alinipeleka chuoni.



    Tulifika alinishusha kama kawaida mbele ya darasa letu watu wengi walikuwa wamesimama mbele ya darasa letu wakituangalia, nilishuka moja kwa moja Melania alikuwa akinisubiri.



    “Sociolah..” Aliniita, nilihisi kama tayari wameshapata taarifa kuhusian na kilichotekea jana ambacho Innocent alikishuhudia.



    “Are you fine?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Yes i am.”



    “Uliyekuwa unamuulizia amekuja mwanafunzi wa darasa lako.” Nilicheka tu.



    “Kama amekuja basi ni vizuri.”



    “Jana ulienda wapi?”



    “Aaah...” Nilishindwa cha kumjibu.



    “Aaah... Hata sijisikii vizuri leo.” Niliamua tu kumchanganyia mada.





    “Una nini kwani?”



    “Hamna sina kitu ila tu najihisi kuchoka choka.”



    “Basi pole tulia usizungukezunguke sawa eeeh.”



    Nilikuwa nikipenda sana jinsi ambavyo walikuwa wakinijali.



    “Nimemmisi sana Fetty.”



    “Jana si ulikimbia wenzako tumeenda mgahawani tukajua tutakuwa pamoja hukuwepo.”



    “Ila leo nitakuwepo tutakula pamoja.”



    Na kweli ulipowadia muda wa kwenda kunywa chai tuliondoka pamoja na kumkuta Fetty akitusubiri, alinikumbatia kwa nguvu zote watu wote walikuwa wanajua ni kiasi gani tulikuwa tukipendana. Tulipata chakula na kisha tuliendelea na ratiba nyingine za chuoni.



    Tuliingia kwenye kipindi cha saa sita na hapo tulikutana na Franklin, alikuwa amevaa zile nguo ambazo nilimnunulia siku ya krismasi hakika alionekana mtanashati, Melania hakuamini macho yake, niliona alipomuona aliachia mdomo huku akiwa ametoa macho na kushindwa kuongea chochote wala kupiga hatua alibaki amesimama.



    Frank aliachia tabasamu nilishindwa kujizuia nilitamani sana kujifanya hatuko pamoja lakini ilishindikana.



    “You look very nice today.”



    “Thank you.” Frank alijibu, tabasamu lake lilikuwa zuri sana.



    Watu waliacha walichokuwa wakifanya na kutuangalia.



    Alibaki amesimama tu akinitazama na mimi wala sikuondoka tulibaki tumesimama



    kama majitu.



    Innocent alinijia.



    “Haa.. Aisee...!! Ngoja niwapige picha ya ukumbusho.”



    Watu wote walinigeukia na kunitazama, alitoa simu yake nzuri aina ya Samsung na kutupiga picha. Tukaweka mapozi nikamsogelea Franklin nikamuegamia kifuani nguo zake zilikuwa zimefanana kidogo na nguo nilizokuwa nimevaa siku hiyo, nilikuwa nimevaa suruali nyeusi iliyonibana vizuri na shati ambalo lilikuwa limekaa kifasheni jeupe lenye maua ya maruni na chini nilivaa viatu vya wazi vyeusi tulipendeza hakika.



    Tuliweka mapozi mbalimbali ya kupiga picha hakuna mtu ambaye alionekana kufanya jambo jingine zaidi ya yote watu wote walikuwa wakituangalia sisi wengine walidiriki kutoa simu zao na kutupiga picha pia.



    Melania alishikwa na bumbuwazi tu asijue afanye nini, tulipiga picha hadi zoezi lilipoonekana kumalizika.



    Innocent alituletea picha ambazo alitupiga ili tuangalie, zilikuwa picha nzuri sana.



    “Jamani naziomba.” Nilimuambia.



    Melania aliniangalia kwa jicho kali na kisha kuingia darasani.



    “Aya mimi nawaacha.” Innocent aliongea nakuondoka, nilitabasamu na



    kumuangalia Innocent mpaka alipopotelea na kisha nikamgeukia Frank.



    “Mambo?”



    “Poa.”





    “Unaendeleaje leo?”



    “Naendelea vizuri, Sociolah ahsante for you company.” Nilicheka tu.



    “Ok.”



    “Naenda.”



    “Sawa.” Nilijibu.



    Ni kama nilikuwa nikulazimisha uelewa wangu kwenda mbali na Frank.



    Wakati tunapishana nilishindwa hata kuacha nafasi kati yetu nilijikuta namgonga, nilirudi nyuma kidogo na kumtazama usoni, aliachia tabasamu na mimi niliachia tabasamu pia, akasogea pembeni na mimi nikasogea pembeni.



    “Pita.”



    “Pita wewe.”



    “Hahaaa...” Nilicheka.



    “Basi tupite wote.”



    “Sawa.”



    Tulibaki tumesimama tu tulicheka na kisha tukapita.



    Niliingia darasani na yeye alitoka nje sikutaka kwenda kukaa na Melania ambaye alikaa nyuma, nilitafuta siti ya mbele na kisha kukaa.



    Baada ya muda Frank alirejea alikuja kukaa kiti cha pili kutoka kwangu,



    nilimuangalia halafu nikaachia tabasamu hali kati yetu niliweka begi langu na yeye



    aliweka la kwake.



    Mwalimu aliingia.



    Baada ya kipindi kuisha, kipindi ambacho kilikuwa cha mwisho kwa siku hiyo watu walianza kutoka darasani kwa mafungu na kisha kuondoka kabisa. Sikuonyesha dalili yoyote ya kuondoka wala Frank hakuonesha dalili yoyote ya kuondoka, niliona watu wamepungua darasani nikamgeukia Frank alikuwa akiniangalia tu muda mrefu.



    “Oooh kuna nini?” Nilimuuliza.



    “Umependeza.” Aliniambia.



    “Aaah sijakuzidi wewe.”



    “Hahaa...”



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alicheka tu.



    Nilikuwa napenda sana alivyokua akicheka cheko zuri sana.



    Nilimgeukia na yeye alinigeukia, akanyoosha mikono yake kwa ishara ya kutaka nimpe mikono, nilimpa.



    “Nakupenda sana Sociolah.” Aliniambia.



    “Nakupenda pia.”



    “Nafurahia sana umekuja katika maisha yangu ingawa....”



    Nilimziba mdomo kwa mkono wangu.



    “Hakuna kilichoharibika wala kitakachoharibika, kila kitu kitakuwa sawa.” “Jana uliniogopesha sana Sociolah.” Frank aliongea. “Kwanini?”



    “Nimepiga simu umepokea nakuita baby huitikii halafu ghafla nasikia unagombana na mtoto.”



    Nilicheka.



    “Simu alipokea mdogo wangu anaitwa Pink, kuna siku nitakukutanisha naye.” “Sawa nitafurahi sana kumuona inaonekana ni mtu ambaye anapenda utani naamini tutafurahi kuwa pamoja.”



    “Hahaha..... Hamna shaka usijali tutaonana sawa.”



    “Ok.”



    Alitupia macho nyuma yangu na mimi nilitupia macho nyuma yake hakukuwa na mtu tuliona kama nafasi, tulisogeleana karibu na kutaka kubusiana.



    “Hey stop...” Sauti kali ilipenya kwenye masikio yetu tuligutuka na kugeuka kule sauti ilipotokea.



    Kumbe wakati wote Melania hakuwa ameondoka alikuwa amekaa pale pale alipokuawa amekaa na akituangalia.



    “Unafanya nini Sociolah?”



    “Hahaha...” Nilicheka



    “Nothing..”



    “Nothing...! Unamaanisha ulichokuwa unafanya hapa eti ni nothing Sociolah usiwe mjinga. Wewe toka hapa, uko kama kinyago.”



    “Hey.... Shut up...” Nilimuambia



    “Shut up nini siwezi kuvumilia kuona upuuzi kama huu toka mbele yangu.” Alimfukuza Frank.



    Frank alibeba begi lake na kisha kuondoka. “Sociolah unachanganyikiwa eeeh?!” “Hapana kwani kuna nini kibaya?” “Ulitaka kufanya nini pale?” “Nothing.”







    Nilibeba begi langu na kuondoka.



    Moja kwa moja nilienda nyumbani wala sikutaka kuulizia kumsikiliza Melania.



    Nilipofika tu Fetty alinitafuta.



    “Umemfanya nini na Melania wewe?”



    “Kuna nini kwani?”



    “Melania kasema anakuchukia.”



    “Haaa! Kwani nimefanya nini?”



    “Mimi sijui.”



    “Any way nikija naamini tutasolve ni maugomvi tu ya kawaida.”



    “Sawa take care.”



    “Hamna shida.”



    Mwishoni mwa wiki mama aliniambia niwapeleke watoto beach nilichukia sana maana nilikuwa sipendi kutembea na wakina Pink



    “Mnataka beach gani?”



    “Tunataka utupeleke Mikadi.”



    “Mtaenda wenyewe mimi simpeleki mtu Mikadi.” “Nini.... Mama kasema utupeleke.”



    “Mkitaka kwenda beach nawapeleka Kunduchi huko kwingine mtajua wenyewe



    sipeleki mtoto wa mtu.” Niliongea.



    “Aaah... Mama kasema utupeleke.”



    “Mtajua sasa kama mnataka kwenda beach twendeni.” Pinto akaitikia, “Twende.”



    “Mimi hata nilikuwa sitaki kwenda Kunduchi.” “Mimi sitaki kuendesha gari umbali mrefu.” Walijiandaa, nikawabeba na kisha kuwapeleka.



    Tulienda moja kwa moja mpaka kunduchi beach, walibadilisha nguo zao na kasha kuanza kuogelea.



    Pink na Pinto walikuwa wakipenda sana kuogelea na zaidi ya sana walikuwa wakipenda kuogelea baharini.



    Waliogelea huku nikiwa nimekaa pembeni nilitandika kitenge changu na kisha nikatoa dompo nikawa nakunywa taratibu kabisa huku nikichat.



    Nilimtafuta Frank lakini hakuwepo hewani nikawa nachat tu kwenye makundi mbalimbali.



    Mara ghafla Pink na Pinto walikuja huku wakikimbia kwa kasi.



    “Dada..... Dada.... Tukuchekeshe.”



    “Mnichekeshe nini?”



    “Angalia pembeni yako.”



    Nilitupia macho pembeni ambapo Pink na Pinto walikuwa wanapazungumzia nusu nizirai.



    Sikutaka kuamini macho yangu kwamba alikuwa ni Frank.



    “Mungu wangu! Amefuata nini huyu hapa, kwanini hajaniambia kama anakuja huku, haaa!”



    Akili yangu ilichanganyikiwa sana.





    Na hapo hapo Frank aligeuza macho yake na yaligongana na ya kwangu nilikimbiza ya kwangu pembeni haraka nilikuwa nimeshachelewa. Frank alinyanyuka pale alipokuwa na kusogea upande wetu.



    Kila mara nilipokuwa nikimuona huyu mwanaume moyo wangu ulijawa na furaha sana sikusita kunyanyuka na kumkimbilia kisha tukakumbatiana na kuninyanyua na kunizungusha baada ya kunishusha alinibusu kidogo mdomoni.



    “Naona uko na watoto, ndiyo wakina Pink wenyewe?” “Yes, njoo ujuane nao.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Tulivyofika pale Pink alibaki ametoa macho tu kama haamini.



    “Shikamoo anko.” Pinto alisalimia.



    “Marhaba.” Frank alimshika shavu Pinto, Pink alicheka.



    “Shikamoo.” Pink alisalimia.



    “Marhabaa wewe ndiyo utakuwa Pink si ndiyo.” “Ndiyo mimi.” Alimjibu.



    “Mzoee tu Pink.” Pink aliniangalia kana kwamba anataka kuniambia kitu nilimuangalia.



    “Nini?”



    “Hamna kitu.”



    “Hahaha...” Nilicheka.



    “Karibu tukae, nyie nendeni mkaoge.”



    Pink aliniangalia ni kama ana jambo alikuwa anataka kuniambia na kisha akaondoka.



    Frank alilala pembeni yangu tukawa tunaongea mambo mbalimbali yaliyokuwa yakituhusu.



    “Frank mimi nataka tukimaliza kusoma tukae pamoja.” “Inategemea Sociolah.”



    “Lakini Frank hujawai kuniambia kuhusu familia yenu.”





    “Kwahiyo unataka nikuambie hapa sasa hivi?” “Kama inawezekana”



    “Ok mimi nakaa na mama yangu ni mkulima tunaishi zetu huko Ifakara.” “Aaah.. Sasa wewe ni kabila gani?”



    “Mimi ni msukuma, mama yangu alihamia Ifakara kwasababu alisikia ardhi ya kule ina rutuba sana kwahiyo alienda kule kwa ajili ya kufanya kilimo.”



    “Ok, mpo wangapi kwenu?”



    “Tuko watatu na mimi ndiyo wa kwanza.” “Woow..”



    “Na wadogo zangu wawili wakike na wa kiume.” “Well.”



    “Mmoja anaitwa Fiona na mwingine anaitwa Furaha.” “Aahaa, sasa kati ya hao nani wa kiume.” “Furaha ndiyo wa kiume.”



    “Hahaha... Mbona mmempa jina la kike.”



    “Mmmh jina la kike kwani lina matiti?”



    Nilicheka sana.



    “Wewe Frank wewe acha utani.”



    “Serious nakuambia.”



    “Aya bwana nimefurahi kujua familia yako, si kunasiku utapenda twende Ifakara.”



    “Aaah lakini haiwezekani acha tu.”



    “Kwanini haiwezekani Frank.”



    “Wewe unaweza kwenda Ifakara? Umezoea vumbi wewe?” “Hahaha vumbi tu, Sema kingine.” “Kuna kuchota maji utaweza wewe?”



    “Nitaweza.”



    “Aya unakaribishwa.”



    “Ahsante nitakuja.”



    “Nitafurahi sana.”





    “Ok.”



    Tuliendelea kufurahi, kwa kweli siku yangu ilikuwa ya furaha sana. “Frank kesho naweza kurudi Hostel.” “Kweli?”



    “Yeah.”



    “Basi itakuwa vizuri.”



    Mara Pink na Pinto walirudi.



    “Vipi?”



    “Tumekuja kupumzika kidogo.”



    “Mimi nataka kutembea tembea.” Niliwaambia.



    “Mnaenda wapi sasa?”



    “Tunazunguka hapo tu kidogo.”



    “Mmmh... Sisi tunataka kula Icecream.” Walianza kulalamika.



    “Mnataka hela?” Niliwapa elfu kumi.



    “Mbona unawapa hela kubwa hivyo.”



    “Wataenda kunisemea kwa mama nimewanyima hela we waache tu.”



    “Nyie kwenu mnadekezwa sana.”



    “Hamna kawaida tu.”



    “Frank kwanini hujaniambia kuhusu baba yako.” Aligeukia pembeni.





    “Baba... Baba alifariki wakati tuko wadogo kabisa.” “Oooh pole.... Pole sikutegemea kukuumiza.”



    “Wala hata hujaniumiza ila utaniumiza tu endapoo.... Aaah.... Twende basi



    tukatembee.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Endapo nini mbona humalizii.”



    “Twende tukatembee.”



    “Mmmh sawa.”



    Tulinyanyuka na kuanza kupiga hatua za kichovu kutembea.



    Tulitembea na kila mtu aliyetuona hakuacha kuhisi kwamba sisi ni wapendanao wa muda mrefu, tulitembea huku tumeshikana mikono na mara nyingine nilikuwa nikicheka na kumuegamia kifuani Frank.



    Wakati mwingine alikuwa akinikumbatia kutokea nyuma na tukitembea kama kumbikumbi, mara nyingine alinibeba, alinibusu, alitangulia mbele yangu akanishika mikono huku akinitazama na kisha kunivuta, mara nyingine tulikimbizana ilikuwa ni furaha sana tupo pamoja.



    Wakati huo kwa pemeni kulikuwa ni kama watu wakifanya sherehe tulipita pembeni yao huku tukiendelea kukimbizana kama watoto.



    “Sociolah...”



    “Yes Frank.”



    Nilimgeukia Frank ambaye nilihisi alikuwa ameniita, nilimkuta Frank ameshikwa na bumbuwazi tu.



    “Nini...?” Alinigeukia na kunitazama mimi.



    “Si umeniita.”



    Frank hakunijibu.



    “Bae si umeniita mbona usemi kitu?”



    Alitikisa kichwa kwa ishara ya kukataa.



    “Hasa kaniita nani au nimesikia vibaya?”



    Alinyanyua mkono wake ishara ya kunioneshea wapi mtu aliyeniita alitokea, niligeuza macho yangu na kutazama kule ambapo Frank alikuwa akinionyesha. Nilihisi kizunguzungu kana kwamba ningepoteza fahamu muda wowote ule. Nilijishika kichwa kwa kuwa sikuamini mtu ambaye nilikuwa nikimuona mbele yangu. Kitu cha kwanza kilichofanya nisijiamini nilikuwa sina neno la kumuambia kwa wakati huo, ningemuambia nini katika mazingira hayo ambayo alinikuta nayo, ambayo bila shaka yalionesha kwamba nina uhusiano wa kimapenzi na Frank. Ningemuelezea nini hadi anielewe, ningefanya maamuzi gani ya haraka hapo. Hakika lilikuwa tukio la kuchanganya akili zangu, nilijikaza.



    Wala haikuhitaji maelezo aliyekuwa mbele yangu alikuwa ni Patrick, ingawa kwa wakati huo sikuwa nikimpenda kabisa Patrick, kukutana naye katika hali kama hiyo kulinishtua.



    “Sociolah unafanya nini hapa na wewe ni nani?” Aliniuliza.





    Nilimuangalia Franklin uso wake ulionekana kuhamanika sana alishindwa kitu cha kuongea.



    Nilipatwa na ujasiri wa aina yake ambao mpaka leo sikumbuki niliupataje





    “Oooh Patrick mambo?” Nilimuuliza alishindwa kunijibu alikuwa akiniangalia mimi na kisha akimuangalia Franklin.



    “Sociolah mimi sielewi nielezee.”





    “Aaah Patrick kitu gani ambacho huelewi?”





    “Huyu ni nani? Nijibu Sociolah.”





    “Aaah usipaniki nisikilize kwa makini Patrick, mimi kutoka kwako sikuwa nikihitaji hela kwa sababu kama hela kwetu tunazo zinatutosha. Kutoka kwako nilikuwa nahitaji mapenzi na muda wako lakini wewe hivyo vyote hukuvijali sijui ulikuwa unaniwazia nini sawa kuna wakati nilikuwa sina hela na nikaja kwako kukuomba hela lakini haimaniishi kwamba nilikuwa sina uwezo wa kupata hizo





    hela nilikuwa nao sana, kitu ambacho nilikuwa nikikihitaji kutoka kwako ni faraja na muda wako lakini wewe huna mimi siwezi. Nimeenda sehemu ambayo ninapata faraja na pia ninapewa muda.”



    “Sociolah...” Alionekana kuchanganyikiwa hadi ashindwe cha kuongea.





    “Si ungeniambia tu mama mimi nakupenda.”





    “Hapana, hakuna nafasi tena, am sorry Patrick, bye....”





    Niliondoka alinivuta Frank naye alinivuta upande mwingine.





    “Muachie nimekwambia.” Patrick aliongea kwa hasira.





    Frank aliachia tabasamu lake lililonimaliza kabisa ingawa nilikuwa radhi kuelekea kwa Frank lakini moyo wangu haukuwa umefanya chaguo.



    “Muache mke wangu.” Frank aliongea.





    “Si ameishakuambia, kuna cha ziada ambacho unataka kumuuliza muulize kiupole ama sivyo hali ya hewa itabadilika sasa hivi.” Aliongea Frank kwa msisitizo.



    Patrick alionekana kutetereka, nilimjua alikuwa siyo mgomvi wala hawezi maswala ya ugomvi, kwa upande wa Frank sikuwa nikijua kama alikuwa akiongea siriazi ingawa alionesha kuwa hatanii.



    “Muache..” Frank alirudia.





    Patrick aliniangalia.





    “Sociolah ndiyo kusema.....”





    “Tumeachana.”

     CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Aliishia kati na kushindwa kuendelea na mimi niliamua kumalizia ili kuondoa utata.



    “Sitaki kuamini macho yangu.” Aliniachia mkono wangu na kisha kufunika macho yake kwa viganja vyake alipokuja kufunua macho yake Frank alikuwa amenishika kiuno na tulikuwa mita kadhaa kutoka pale alipokuwa tulishaondoka muda mrefu.



    “Sociolah....” Alibakia akiniita,  nilipunga mkono bila  kugeuka huku tukizidi



    kuongea kwa ishara ya kwaheri.





    Tulizunguka zunguka hadi muda ulipokuwa umeenda sana na kisha tukarejea pale tulipokuwa tumewaacha wakina Pink.



    “Mpo salama.”





    “Ndiyo.”





    “Ok.”





    “Tunaondoka saa hizi tunarudi nyumbani sawa.”





    “Eeeh dada mimi nimechoka.” Pinto alisema.





    “Sawa na anko Frank tunaenda naye?” Pinto alisema baada ya kuona tunaelekea kwenye gari.



    “Ndiyo.”





    “Anaenda mpaka nyumbani?” Nilicheka.





    “Eee tunaenda naye.”





    “Haaa! Pink alihamaki.





    “Nini na wewe.”





    “Eehe dada huyu hapo ndiyo yule ambaye my oga eeh?” Aliuliza.





    Nilicheka nilicheka sana mpaka nilishindwa kujizuia nikaegamia usukani mara baada ya kuingia kwenye gari huku nikiendelea kucheka, Frank naye alicheka.



    “Pink unapenda sana utani.”





    “Mimi sitanii.” aliongea huku akionesha msisitizo.





    “Eeee.. Ndiyo yeye.” Niliitikia.





    “Ooh.. Ila anafanana na na....” Aliamua kuishia kati.





    “Halafu dada huyu si ndiyo.....” Pinto alimziba mdomo.





    “Nini.... Nini.... Pink usije ukanifanya nikakupiga hapa sasa hivi unataka kuongea



    nini?”





    “Akaa nimekosea twende.” Aliongea.





    Nilijuta sana kuwa na mdogo ambaye ana maneno mengi kama Pink mara mia Pinto nilichukia nilishika usukani wa gari na kuondoa gari kutoka pale Kunduchi beach.



    “Sikia Pink nampeleka kwanza Franklin hostel.”





    “Si umesema tunaenda naye nyumbani.”





    “Nilijua tu hatuwezi kwenda naye, mmmh heri ninyamaze.” Pink aliongea.





    Niliamua kucheka ili kumpa imani Frank naye alicheka baada ya kuniona mimi nimechaka.





    “Pink bwana una utani sana.” Alicheka tu Pink na kisha hali ya ukimya ilitawala katika gari.



    Niliendesha gari kwa umakini sana huku nikiwa na mawazo mengi hadi tulipofika katika mabweni ya mabibo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Niliingiza gari hadi ndani kabisa giza lilikuwa tayari limeisha ingia nilizima taa za kwenye gari na kisha kumbusu Frank mdomoni.



    “Byee.”





    “Ok byee.”





    “Aya.”





    Frank alishuka huku kuonyesha kutoridhika hata mimi nilitamani kuendelea kuwa naye.





    Niligeuza gari na safari ya kuelekea nyumbani ilianza, kila nilipokuwa nikimuangalia Pink kupitia kioo cha pale mbele alikuwa tu akiangalia dirishani.



    “Pink.” Nilimuita.





    “Bee dada.”





    “Unajisikiaje?”





    “Nahisi usingizi dada,”





    “Usijali tutafika nyumbani sasa hivi na utaenda kupumzika mdogo wangu sawa, usiongee kitu chochote kuhusu anko Frank.”



    Ni kama nilimshitusha Pinto.





    “Kwanini dada mbona mzuri au kwasababu baba atamjua ndiyo Matranka.” Aliongea.



    “Kelele.... Nishawambia siyo Matranka niliwambia anaitwa Frank.”





    Pink hakujibu chochote alionekana kuelemewa na usingizi.





    Hii ilikuwa mbaya sana kwangu kama asingenisikia angeweza kuongea.





    Tuliendelea na safari hadi tulipofika nyumbani na baada ya kufika nyumbani wakina Pink walikuwa wamechoka sana, walioga na kisha kulala.



    Asubuhi ya siku iliyofuata ilikuwa ni siku ya ijumaa nilienda chuoni kama kawaida Melania hakutaka kuniongelesha kabisa. Ulipofika wakati wa mwenda kunywa chai nilimkuta Fetty akiwa anatusubiri nilikuwa wa kwanza kumfikia Fetty na Melania alikuja na kutupita tu.



    “Mmmh shosti hali mbaya.” Fetty aliongea.





    “Yani Melania usiku kucha anaongea tu anakutukana, analia.”





    “Sasa mimi nimefanyaje lakini.” Niliongea sijui.





    “Kwa kweli na wala hata sijui nifanyeje hali mbaya nitakuja jumapili tutasolve hayo mambo yote.”



    “Sociolah usijidanganye kwama Melania atakusikiliza mi naona ukija ugonge mara mbili.”



    “Weee...!”





    “Kweli mtafute Monica akuambie kila kitu hali ni mbaya anasema yani lazima akufanyie kitu kibaya.”





    “Mungu wangu! Amepatwa na nini Melania kwani shida iko wapi si ni jambo tu la kukaa chini na kuongea.”



    “Kasema hataki kusikia chochote kuhusu wewe.”





    “Shit... Nitakuja na nitahakikisha tatizo linaisha,”





    “Mmmh...Sawa.” Melania alikaa mbali na sisi siku hiyo.





    Nilikunywa chai tukiwa na Fetty tukiongea mawili matatu, na baada ya hapo niliachana na Fetty na kisha kuelekea darasani.



    Melania aligoma kabisa kuzungumza na mimi, watu wengi walikuwa wakiongea kuhusu sisi kila mtu akitaja sababu yake nilinyamaza tu kimya bila kuongea chochote.



    Nilirudi nyumbani baada ya vipindi kuisha, nashukuru Mungu Pink ana Pinto hawakuwa wameongea chochote kile.



    Siku ya jumapili mama alinipeleka hostel.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Nilikuwa naogopa, alinishusha mpaka nje ya bweni letu.





    “Nakupeleka mpaka chumbani kwenu.”





    “Nilihofia hali ambayo mama anaweza akaikuta kule.”





    “Aaah.. Mama usijali unaweza tu ukaenda nashukuru nimefika salama naweza kubeba na mabegi haya na nikafika usijali mama.”



    “Sawa uwe na wakati mwema mwangu, kuwa makini sawa eee.”





    “Aya mama usijali.”





    “Sawa.” Alinivuta karibu na kisha kunibusu kwenye paji la uso mara nyingi mama alikuwa anapenda sana kunibusu kwenye paji la uso aliniambia inaonesha ni kiasi gani ananipenda.



    Nilimuangalia hadi alipopanda kwenye gani na kisha kuondoka, nilivuta begi langu kivivu na kiunyonge kuelekea chumbani kwetu.



    Nilipofika mlangoni nilisita kufungua malango.





    Na wakati najiuliza niingia au nifanyeje mlango ulifunguliwa na kisha Melania alichomoza.



    Alinipandisha na kunishusha na kisha akaachia msonyo ambao hata sikuwahi kujua kama Melania alikuwa akiweza kuachia msonyo wa aina ile. Alinisukuma na kisha alipita kuendelea na safari yake.



    Nilibaki tu nimeshikilia begi langu, nilisimama mlangoni kwa dakika kadhaa.



    Alipita moja ya watu ambao walikuwa katika vyumba vya jirani.



    “Aaah Sociolah umerudi mbona umesimama tu hapo mlangoni?” Mlango ulifunguliwa na kisha Monica alitoka.



    “Sociolah....” Alinifuata na kunikumbatia. Nilimkumbatia.



    “Mbona huingii?”



    “Naingia.”



    “Umekutana na Melania?” Aliniuliza.



    “Yeah nimekutana naye.”



    “Vipi kakusalimia?”



    “Hamna kanipita tu.”



    “Oooh pole, ingia ndani basi upumzike.”



    Nikaingia ndani.



    Monica kwa kifupi alianza kuniambia hali halisi ilivyo humu ndani. Alieleza jinsi ambavyo Melania alikuwa akiongelea kuhusu ugomvi uliokuwa baina yetu, alielezea vitisho vyote ambavyo Melania alikuwa akiwaambia kuhusu mimi na mwisho aliniambia kwamba nina wakati mgumu sana.



    “Sociolah sijui kama amani itakuwepo humu ndani.”



    “Aah achana naye mimi naamini kwamba kila kitu kitakuwa sawa wala hata usijali.”



    Nilipanga vitu vyangu haraka kwenye kabati na kisha kutoka.



    “Nitarudi muda si mrefu.” Nilimuaga na kuondoka.



    Nilitoka moja kwa moja hadi chumbani kwa kina Frank sikutaka hata kumuambia kama nimefika. Niligonga mlango na kisha kuingia ndani.



    Frank alikuwa na Innocent walikuwa katikati ya majadiliano, waliponiona walifurahi sana. Nilienda pale alipokuwa amekaa kwenye kiti kwa nyuma yake nilimkumbatia kutokea nyuma na kisha nikambusu shavuni na baada ya hapo nikasogea kitandani na kukaa kwani kiti chake kilikuwa karibu sana na kitanda.



    “Mambo.”



    “Poa, mzima?”



    “Mzima sijui wewe.”



    “Naona umerudi mama.”



    “Eeee nimerudi.”



    “Hakuna shida karibu sana.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ahsante.”



    Frank alionesha ucheshi wa hali ya juu nilimpenda, alizidi kunivutia kila siku.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog