Search This Blog

Monday, October 24, 2022

GUBERI LA KIMANYEMA - 4

 





    Chombezo : Guberi La Kimanyema

    Sehemu Ya Nne (4)



    Alikuwa kalazwa juu ya kitanda cha kamba kilichotandikwa shuka nyeusi. Alipozungusha macho kushoto na kulia akawaona wanawake watatu wakiwa wamesimama huku wakimtazama, nyuso zao zikimdhihaki. Akashangaa, akaduwaa. Zaidi, alishtuka baada ya kubaini kuwa miongoni mwa wanawake hao ni Hidaya binti Sufiani. Akamkodolea macho zaidi, akihisi kuwa yu ndotoni.

    “He..he..he..!” Hidaya aliachia kicheko cha dhihaka. Akaendelea, “Hata ukinikodolea macho mwanahizaya we, ng’o! Huniwezi! Labda unipige na radi ya kimanyema kama unaweza. Na huniwezi!”

    Yalikuwa ni maneno yaliyomtoka Hidaya kwa sauti iliyojaa kejeli na dharau isiyo kifani. Na bado akaendelea kumtazama huku akitabasamu, tabasamu lisilokuwa na taswira yoyote ya upendo.

    Bado Kiwembe alihisi yu katika ndoto isiyopendeza. Alikuwa mtupu kama alivyozaliwa, kafungwa kamba mikono na miguu na kamba hizo zikiwa zimeshikwa na matendegu ya kitanda hicho. Ni kipi kilichotokea hadi akjikuta katika hali hiyo? Hakuweza kujua.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ni hapo alipoamua kuzirudisha kumbukumbu zake nyuma. Na kwa kuwa ukweli ni kwamba hakuwa ndotoni, kumbukumbu hizo zilimjia mara moja, zikianzia pale Lango La Jiji, Magomeni Mikumi.

    *****

    SURA ya yule mwanamke mrembo, ambaye alijitambulisha kwa jina la Husna Abdilatif ilimjia kichwani. Ni Husna huyo aliyemfanya achukue muda mrefu ndani ya ukumbi wa Lango La Jiji, na ni Husna huyohuyo aliyemfanya ajikute anakunywa bia nyingi usiku huo wa jana.

    Husna!

    Husna alikuwa na mengi mazuri, zaidi ya uzuri wake wa hadharani. Kiwembe hakushindwa kukumbuka jinsi mwanamke huyo alivyouchezea mwili wake kwa namna ya ajabu, akitumia kila kiungo cha mwili wake katika kumdhihirishia kuwa ni mwanamke aliyehitimu fani ya kumstarehesha mwanamume ‘mwenye njaa.’

    Ndiyo, alikuwa ni mwanamke wa kipekee akilini mwa Kiwembe, mwanamke ambaye alifanya kila aliloweza, na kwa ujumla alionesha dhahiri kuyamudu na kuyazoea mengi japo baadhi yake yalitisha.

    Kwa Kiwembe, ilikuwa ni mitindo ya kuliwaza na kusisimua, mitindo ambayo aliipata wakati fulani siku kadha wa kadha kwa wanawake tofauti. Ni wengi waliomchezea maungoni kwa kadri walivyoweza, lakini huyu Husna alikuwa zaidi yao. Zaidi ya wote waliotangulia!

    Kwa ujumla, kadri vidole laini vya Husna vilipokuwa vikipapasa hapa na kutomasa pale, ulimi wake wa moto ukizuru kila sehemu iliyohifadhi ‘umeme’ Kiwembe alihisi pumzi zikimpaa, akachanganyikiwa kiasi cha kutoyajali macho ya ‘wambea’ waliowatazama kwa uchu na mshangao.

    Pia alikumbuka kuwa waliondoka pamoja hadi katika nyumba fulani ambayo Husna alidai kuwa ni ya mama yake mdogo. Na wakati walipokwenda hapo Husna alikuwa amebeba chupa mbili za bia ambazo walitazamia kuzinywa kama ‘lala salama’ kabla ya hatua muhimu iliyowakaabili.

    Kumbukumbu zilizidi kumjia akilini, kwamba, katika nyumba hiyo mama mmoja mwenye umri usiopungua miaka sitini ndiye aliyewakaribisha. Na walikaribishwa katika chumba maridadi na kilichokuwa na kitanda kikubwa, kitanda kilichotandikwa shuka nyeupe, safi za hariri.

    Ni kama vile chumba hicho kilikuwa maalum kwa kazi maalum kwani hakukuwa na kitu kingine chochote zaidi ya kitanda. Lakini kwa usiku huo, Kiwembe akiwa na uchu mkali wa ngono, hakushangazwa na sura ya chumba hicho; alikihitaji kitanda na alimhitaji Husna, basi.

    Ndiyo, kwa Kiwembe huo ulikuwa ni usiku mwingine mzuri kupindukia. Kiwembe alijitahidi kuuonyesha ule urijali wake uliowawehusha wanawake wengine ambao idadi yao hakuikumbuka. Ndiyo, alijitahidi, lakini hii ilikuwa ni siku nyingine kwake. Huyu alikuwa ni zaidi ya yule Husna aliyekuwa akimfanyia vituko vya kupagawisha kule Lango La Jiji.

    Alikuwa ni Husna mwingine! Husna aliyedhihirisha kivitendo jinsi alivyofundwa, akafundika. Alifanya yote aliyoyajua na yote aliyoyaweza, akihakikisha Kiwembe hapati nafasi ya kufurukuta. Na alifanikiwa; Kiwembe hakumudu.

    *****

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    AWALI haikumwingia akilini Kiwembe kuwa vituko vya Husna tangu Lango La Jiji hadi humo chumbani vilikuwa na dhamira maalumu, dhamira ya kumteka kimwili na kiakili hadi ajikute katika hali asiyoitegemea asubuhi hii.

    Sasa alijenga hisia kuwa Husna atakuwa amehusika kwa namna moja au nyingine katika tukio hili la kufungwa kamba mikononi na miguuni. Lakini mbona Husna mwenyewe hayupo? Kati ya hawa wanawake waliomzunguka, Husna hakuwepo. Atakuwa wapi?

    Alijiuliza maswali mengi kwa muda mfupi na hakuweza kupata majibu yoyote. Akabaki akiwakodolea macho wanawake hao.

    “Kiwembe,” Hidaya aliuvunja ukimya. “Kuna kabila moja lenye methali ya Mwana wa Mwalika Ngoma Hatahiriwi Jioni. Mimi naiheshimu sana methali hiyo. Naiheshimu kwani wewe ndiye ‘mwalika ngoma.’ Umetualika ngoma, tumeicheza wote na matokeo yake wote twayafahamu.”

    Alitamka maneno hayo huku machozi yakimtoka, akionyesha dhahiri kuumia moyo. Ukimya ukatawala tena.

    Wakati Kiwembe akiyatafakari maneno hayo, mara akamwona mwanamke mmoja wa makamo akiingia. Huyo alikuwa ni Bibi Siyajali, mkunga wa jadi. Mkononi alikuwa na bisibisi, kifaa kilichomshtua na kumtia woga Kiwembe.

    “Vipi, wanataka kunitahiri upya?” alijiuliza kimoyomoyo huku akimkodolea macho Bibi Siyajali.

    Bibi huyo aliachia tabasamu hafifu, tabasamu ambalo badala ya kumfanya apendeze, lilisababisha atishe kutazamwa mara mbili. Sekunde chache baadaye tabasamu hilo likafutika ghafla na nafasi yake kutwaliwa na kicheko kikali ambacho kama lile tabasamu, hiki nacho hakikuwa kicheko cha kupendeza wala kutoa taswira kuwa mchekaji kafurahi.

    Alitisha!

    Hakutofautiana na yule mwanamke aliyeishi zaidi ya miaka mia mbili, Gagula wa nchi ya Wakukuana aliyeipamba simulizi ya Mashimo ya Mfalme Suleiman. Bibi Siyajali aliendelea kucheka huku akimsogelea Kiwembe.

    Kiwembe aliogopa, na alikuwa na haki ya kuogopa. Bibi huyo mrefu sana, mweusi tii na mwembamba kupindukia hakuwa akifanana na binadamu wa kawaida.

    Alikuwa na kidevu kirefu kilichoshuka kwa chini. Meno yake meusi, yaliyoungua mithili ya mbegu za ubuyu na mashavu yake yaliyosinyaa na kubonyea kwa ndani kiasi cha kushangaza huku macho yake madogo yaliwaka kwa ukali wa kuogofya. Naam, hakuwa ni mtu wa kutazamwa mara mbili.

    Kiwembe hakupenda kuendelea kumtazama bibi huyo, lakini alipotaka kuyahamisha macho, mara akamwona anamwinamia na bisibisi yake mkononi. Kiwembe alishusha pumzi ndefu, akayafumba macho na kuyafumbua.

    Akashangaa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Bibi Siyajali alikuwa akimpapasa katika sehemu zake za siri kama vile atafutaye kitu. Ulikuwa ni upapasaji wa taratibu uliomfanya Kiwembe ayapeleke mawazo yake mbali. Anataka penzi? Alijiuliza, mshangao ukiwa bado umemtawala. Akafumba tena macho na kufinya mdomo kwa raha aliyoihisi.

    Alipoyafumbua tena macho alimwona Bibi Siyajali akianza kumpapasa kwa kutumia ile bisibisi. Bisibisi maalum, kwa kazi maalum. Mshangao ukamzidia Kiwembe, mshangao ulioiduwaza akili yake kiasi cha kujikuta akimwacha Bibi Siyajali aendelee kufanya alilotaka kulifanya.

    Naam, na Bibi Siyajali aliendelea kumpapasa Kiwembe taratibu, akitumia hiyo bisibisi yake maalum, akiutafuta mshipa alioujua mwenyewe. Hatimaye alipoupata, akaubana kwa koleo.

    Ilitosha.

    *****

    ILIKUWA ni kazi ndogo sana kwa Bibi Siyajali, lakini ikiwa ni kazi iliyomwingizia maelfu ya shilingi. Ndiyo, ilikuwa ni kazi ndogo na yenye faida nzuri kwa Bibi Siyajali lakini kwa upande wa pili ikiwa ni kazi iliyozua maumivu makali kwa Kiwembe, maumivu yenye kuzaa madhara yasiyopatiwa ufumbuzi.

    Sasa Kiwembe akawa kama beberu la mbuzi lililominywa mshipa wake wa siri na likawa ‘ndafu dume’ lisiloweza kitu.

    Hiyo ndiyo ilikuwa kazi ya Bibi Siyajali, mkunga wa jadi wa enzi hizo kabla hajajiingiza katika kazi hii ya kuwahasi wanaume, kazi aliyopewa kwa mkataba maalum wa malipo mazuri kutoka kwa wanawake wenye mioyo ya visasi kwa watu vichaa vya mapenzi kama Kiwembe.

    Kilikuwa ni kipindi kigumu kwa Kiwembe. Aliyafumba macho na kuyafumbua haraka. Akapepesa kama anayekaribia kuiaga dunia. Akajaribu kufurukuta, asiweze; kamba za mikononi na miguu zilimdhibiti vilivyo. Akashusha pumzi ndefu huku jasho likimtiririka mwili mzima.

    Hidaya, Sakina na Siamini walikuwa wametulia tuli wakimtazama. Kati yao, ni Hidaya pekee aliyeonesha kulichukulia uzito tukio hilo. Yeye alikuwa akifuta machozi kadri yalivyojiunda machoni sekunde hadi sekunde.

    Hatimaye alisema, “Kiwembe, naomba sana…naomba unisamehe kwa tendo hili. Ni udhaifu wetu kukoseana na kisha tukaombana radhi. Huo ni udhaifu wetu wanadamu. Najua fika hukupenda kufanyiwa tendo hili, lakini ni vizuri pia ukitambua kuwa usilolipenda wewe kutendewa, usimtendee mwenzio.”

    Alishusha pumzi ndefu, akapenga kamasi kisha akaendelea, “Usifadhaike sana, Kiwembe. Najua unaniona mie ni mkosaji na mbaya wako namba moja. Lakini kumbuka kuwa ni vema kuwaomba msamaha wote tuliowakosea na kisha, ikibidi, tukatubu kwa Mwenyezi Mungu. Naomba sana unisamehe, Kiwembe.”

    Hayakuwa ni maneno ya kumwingia akilini Kiwembe hata kidogo! Msamaha! Hidaya anaomba msamaha! Anaomba msamaha kwa tendo analotambua fika kuwa lina madhara makubwa, madhara yasiyoweza kupatiwa ufumbuzi! Haya maneno yanamtoka moyoni kwa dhati au ni unafiki mtupu?

    Kwa kiasi kikubwa Kiwembe alijiona kakumbwa na fedheha, kashfa na aibu. Ya nini kuishi katika hali hii? Alijiuliza.

    Uwanaume ni ndevu za kidevuni? Hapana.

    Uwanaume ni shati? Hapana.

    Uwanaume ni suruali? Hapana.

    Uwanaume ni maungo ya kiume ya sehemu za siri? Hapana.

    Ni wanawake wangapi wenye ndevu videvuni mwao? Ni wanawake wangapi wavaao mashati huku wengi wao wakifanya hivyo bila ya kujua na badala yake hujiona kuwa wamevaa blauzi? Ni wanawake wangapi ambao huvaa suruali za kiume ama kwa kudhamiria au kwa kutojua?

    Ni wanaume wangapi mijini ambao wameumbwa kiume, miili iliyokakamaa, mikubwa, wakiwa wakamilifu katika maungo ya sehemu zao za siri lakini wakiwa na tabia zote za kike huku sehemu hizo za siri zikiwa ni ‘mapambo’ tu?

    Ni hili swali la mwisho lililomfadhaisha. Sasa hakujiona kuwa ni mwanamume aliyekamilka. Ni robo ya mwanamume.

    Simanzi ikamjaa. Akafumba tena macho kwa nguvu. Kwa takriban dakika moja alikuwa katika hali hiyo. Alipoyafumbua, akaona mlango ukisukumwa. Husna Abdilatif akaingia!

    Ni yule aliyemtesa, mateso yaburudishayo.

    Wakatazamana kwa sekunde chache huku tabasamu la mbali, tabasamu lililojaa dhihaka, likichanua usoni pa Husna Abdilatif. Kisha akasogea kitandani hapo na kuketi kando ya Kiwembe.

    Hakuishia kuketi tu, bali alianza kuzifungua kamba huku “pole” zikimtoka, pole zilizofuatishwa na vijikofi vya mahaba. Vilikuwa ni vijikofi ambavyo kwa Kiwembe ambaye wakati huo akili yake ilikuwa imerufaika, hakuweza kutambua kama ulikuwa ni unafiki mwingine.

    Hakuijua kazi ya Husna!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Husna aliyamudu maisha ya jiji la Dar kwa kazi ya kukodiwa kwa masuala nyeti tu; kuwakomesha wale waliostahili kukomeshwa. Alikubaliana na ‘wenye shida’ kwa malipo maalum, malipo makubwa, nusu kabla ya kukamilika kwa kazi na nusu ya mwisho, baada ya kazi.

    Alichohitaji ni kujua tu kwamba mlengwa anapatikana wapi, na akishampata ampeleke wapi. Akishayajua hayo, kazi iliyobaki mwachie yeye. Kama siyo leo, basi kesho atakuwa kishamtia mikononi. Na kama hakumpata, basi labda mlengwa huyo atakuwa mfu.

    Hivyo ndivyo alivyoishi Husna Abdilatif , mwanamke mzuri kwa sura na umbo, aliyeziteka vilivyo nafsi za wakware wa Magomeni kwa vaa yake, tembea yake na hata cheza yake pale kikundi chochote cha taarabu kinapotumbuiza Lango La Jiji.

    *****

    KAMBA zilifunguliwa taratibu na Husna Abdilatif. Zoezi hilo lilipokamilika, bado Kiwembe hakuwa na nguvu ya kufanya chochote. Hata nguo alivishwa na Husna Abdilatif.

    Kwa jinsi alivyojihisi vibaya, hakuwa tayari hata kumtazama usoni mwanamke huyo. Akauinamisha uso kwa huzuni, akahisi uso huo ukiwa mzito na wenye makovu bwerere.

    Huku akiwa bado kauinamisha uso, sauti ya Hidaya, sauti yenye majonzi mazito iliyafikia masikio yake na kumchoma moyo kwa maneno mazito yaliyomtoka Hidaya. Yalikuwa ni maneno ambayo hayakuwa hata na chembe ya uongo.

    “Kiwembe,” ndivyo Hidaya alivyoanza. “Siwezi kukuhurumia sana kwani yote haya umeyataka mwenyewe. Na kuanzia sasa huna chochote uwezacho kuhusu mwanamke, kimapenzi. Pole sana. Lakini ukumbuke Kiwembe, mimi niliachika kwa ajili yako, nawe ukanikimbia,” akashusha pumzi ndefu na kumeza mate.

    Kisha akaendelea: “Kwa ajili yako nilijikuta nikiyaanza maisha mapya na magumu kupita kiasi. Nikawa changudoa wa barabarani na kwenye mabaa maarufu. Ni nani asiyenijua pale Kinondoni Road? Ni nani asiyenijua pale Milambo na Ohio Street? Maeneo ya Masaki na Oysterbay ni’shayachezea vibaya sana.

    Baa za Buguruni, Sinza na hata za hapa Magomeni ni’shazizungukia kwa sana tu.

    “Nilikuwa mtu wa kulala usingizi mchana na kukesha usiku. Siku nyingine nililazimika kutumia gharama ili tu niingie Las Vegas Casino au Billcanas katika kusaka wanaume wenye pesa. Mwili wangu ulishageuka jamvi. Sikujali kuwa mwanaume huyu ni msafi au mchafu. Nilijali pesa.

    “Sikujali kuwa mwanaume huyu anahitaji mapenzi ya aina gani, nilijali uzito wa pesa yake. Ndio, nililazimika kujali pesa ili niweze kula. Na kwa misingi hiyo, kuna wakati nililazimika kuwakubalia wanaume watatu waniingilie wote pamoja na kwa wakati mmoja, huku kila mmoja akitumia njia yake. Hao walinipa pesa nyingi zaidi ya wengine.

    “Lakini hayakuwa maisha ya kujivunia hata kidogo! Kupewa shilingi elfu hamsini au hata laki moja kwa minajili ya kufanya mapenzi machafu halikuwa jambo la kujivunia hata kidogo, lakini ningefanyaje wakati nilihitaji pesa?

    “Baadhi ya wanaume wakware hawakuwa tayari kufanya mapenzi kwa njia ya haramu, lakini pia hawakuwa radhi kutumia njia ya kawaida. Wao walihitaji kuhusisha tupu zao na kinywa changu katika tendo la kukidhi haja zao, na sikuwa na nguvu za kuwakatalia wakati wameshanionyesha au kunipa elfu kumi au ishirini.

    “Kinachoniumiza moyo ni kutoweza kuwashinikiza wateja wangu wote watumie kondomu. Ni wachache tu, tena wale waliokuwa wakipenda kufanya mapenzi kwa njia ya kawaida ndiyo waliojali kutumia kondomu. Lakini wale wa makundi mengine mawili kamwe hawakunielewa nilipowatamkia vitu hivyo.

    “Kiwembe, sikustahili kufikia mkondo huo wa maisha. Nilikuwa mke wa mtu, nikiishi katika jumba la kifahari, nikichezea pesa lukuki na gari la kutembelea nilikuwa nalo.

    “Kiwembe, huruma yangu kwako leo imenifikisha katika shimo lililojaa kila aina ya takataka. Na kwa kweli mpaka sasa sijiamini kuwa ni mzima. Sina uhakika kuwa bado sijaukwaa Ukimwi! Sijui!

    “Niliyoyafanya ni mengi na makubwa, na zaidi yanaunda historia ya kutisha kwangu Hidaya bint Sufiani. Na yote hayo umeyasababisha wewe…Wewe! Wewe! Wewe Kiwembe….” Sauti ikamkwama ghafla. Akatwaa leso na kuyafuta machozi yaliyokuwa yakichuruzika mashavuni. Kisha akamtazama tena Kiwembe, safari hii kwa jicho la uchungu na hasira.

    “Kiwembe,” aliendelea, “kilichotokea hapa ni kulipa fadhila kwa wema ul’onitendea. Usiwe na hofu yoyote; kufa, hufi. Lakini pia yasingekukuta haya yaliyokukuta kama letu lingekuwa moja. Tatizo, wewe ulijitia hamnazo, hata ukakimbia hoteli uliyopanga. Ni ujanja huo? Mbona Husna kakuleta?

    “Hivi ulimchukulia Husna kama dagaa au samaki wa Mugebuka au Kuhe wa Ziwa Tanganyika, ukamtegemea kumvua kiulaini, eti?”

    Akacheka kwa dharau.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Huyu ni Papa, rafiki yangu,” aliendelea. “Unaweza kumwita Papa au Nyangumi. Sasa kakuvua wewe. Upi ujanja, kupata au kuwahi? Tena itakubidi uvae sidiria kama sisi wenzio maana ile hazina yako iliyokufanya uitwe MWANAMUME i’shapata ajali. Tena ni ajali mbaya mwenzangu.

    “Nenda Muhimbili, Hindu Mandal, TMJ, Aghakhan, KCMC, hata kwa Mtakatifu Thomas- Uingereza tuone ka’utapona. Ni heri aliyepatwa na ajali ya gari akafa, kuliko wewe mwenzangu ambaye utabakia kulishuhudia jua likichomoza na kuzama bila ya faida yoyote kwako. Utaishia kuwashuhudia wanawake wenye mapaja makubwa na laini, na wenye makalio makubwa ambao hutaweza kuwafanya lolote.

    Utawashuhudia warembo wenye matiti yanayostahili kunyonywa, macho yanayoshawishi na midomo inayostahili kubusiwa na hata kukufanyia mambo mengine ya kukufurahisha. Kwa kweli utaishia kula kwa macho tu huku wale wanaostahili kuitwa “WANAUME” ndiyo wakiwafaidi kwa jinsi wanavyotaka.

    “Unasikia Kiwembe, maadam sasa roho yangu imesuuzika, nategemea baada ya siku chache n’takwenda Kigoma kwa mume wangu, Khalifa Mwinyimkuu nikamwangukie na n’naamini atanisamehe kwani unyumba wa watoto haufi. Na nikikubaliwa, nitawahadithia wenzangu kuwa tujiepushe na watu wa aina yako, tuwaheshimu waume zetu, nao watuheshimu wake zao.”

    Hidaya alikuwa akiongea kama mwendawazimu mwenye maneno ya hekima, maneno yaliyomtoa machozi Kiwembe.

    Naam, Kiwembe alilia!

    “Twende mgonjwa wangu,” alizinduliwa na Husna Abdilatif aliyemshika mkono na kumvuta kistaarabu.

    Wakatoka ndani ya chumba hicho huku Kiwembe kajiinamia.

    Hidaya na Bibi Siyajali wakashikana mikono, nao wakatoka taratibu, nyuma yao, wanawake wengine, Sakina na Siamini waliwafuata kimyakimya.

    Nje ya nyumba hiyo waliagana, kila mmoja akatokomea kivyake.

    *****



    ILIMWIA vigumu Kiwembe kuamini kuwa tendo lile alilotendewa kule Magomeni Mikumi lilimwondolea ile hadhi kamili ya uwanaume wake. Lakini ile risala ya Hidaya ilimwondolea matumaini ya kujipa imani kuwa yale yaliyotokea asubuhi hiyo ya kipekee yalikuwa ni ndoto tu.

    Akiwa chumbani mwake, Zanzibar Hotel, muda mfupi baada ya kuteremka katika teksi aliyokodi pindi tu alipoagwa kwa busu la kinafiki la Husna, Kiwembe alijikuta akivamiwa na mawazo kichwani mithili ya malaya wa barabarani wanavyovamia gari lililosimama katika ‘viwanja’ vyao.

    Yalikuwa ni mawazo yaliyoshonana kichwani mwake na kumpa taabu ya kupanga lipi aanze kulitafakari na lipi lifuate. Kila aliloamua kulipa kipaumbele, liliruka na badala yake likaja jingine.

    Siku hiyo hakutoka kabisa hotelini hapo. Alishinda kutwa, na usiku ulipoingia alishuka kwenye ukumbi wa vinywaji ambako alikunywa toti kadhaa za pombe kali kisha akala kuku mzima kabla hajapanda tena ghorofani kwake.

    Siku ya pili aliamua kutoka. Aliamua kwenda pembezoni mwa jiji ambako asingepata bughudha yoyote. Alihitaji kupata utulivu kichwani na aliamini kuwa hapo katikati ya jiji, sehemu ambayo kuna idadi kubwa ya watu, wanawake kwa wanaume wanaomfahamu hapafai katika kipindi hiki ambacho ameathirika kisaikolojia kwa kiwango kikubwa.

    Hivyo, asubuhi pwee, akaondoka hotelini hapo na kwenda kituo cha daladala kupata usafiri wa Kimara. Siyo kwamba alikuwa na uhaba wa fedha uliosababisha asubiri daladala. Hapana. Mfuko wake ulimruhusu kukodi teksi hadi Mwanza ambako angeishi kwenye hoteli ya hadhi ya juu zaidi mkoani humo, kwa wiki nzima kisha akarejea tena Dar kwa teksi vilevile au hata kwa Ndege.

    Hakufika Kimara. ‘Mashetani’ yake yalimtuma ateremkie Magomeni Mapipa ghafla, ambako aliivaa mitaa miwili mitatu na kuweka kituo katika baa moja yenye dalili zote za ‘kuchoka.’

    Hapo alikunywa supu na kushushia soda baridi taratibu, macho yake yakimpitia huyu na yule ilhali akili yake ikiwa kama vile imesimama kufanya kazi. Alikaa hapo kwa zaidi ya saa mbili na soda mbili zikawa zimeteremka tumboni mwake.

    Hatimaye alijing’atua na kurudi barabara ya Morogoro kusubiri usafiri uleule wa daladala ili arudi Zanzibar Hotel. Dakika mbili zilizomkuta kituoni hapo zilitosha kuyabadili mawazo yake, na sasa akajikuta akivamiwa na wazo la kutembea taratibu hadi huko hotelini kwake.

    Alitambua fika kuwa ingemlazimu kutumia zaidi ya nusu saa kufika hotelini hapo. Hata hivyo hakujali. Aliamua hivyo kwa kuwa aliamini hiyo itakuwa ni mbinu mojawapo ya kumpa wazo zuri la nini afanye baada ya mkasa ule uliomkumba kule Magomeni Mikumi. Mkasa uliompotezea ‘uwanaume’ wake!

    Mvurugiko wa mawazo kichwani mwake ulisababisha hata mwendo wake ubadilike. Alitembea kama kipofu, mara kadhaa akikoswakoswa na waendesha baiskeli na wakati mwingine akijikuta akipigana vikumbo na watu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alipokuwa akilivuka daraja kubwa eneo la Jangwani, maarufu kwa jina la “DARAJA LA KAJIMA” mara akasikia honi kali ya gari nyuma yake. Alipogeuka aliliona gari dogo, la kisasa, Honda jekundu likimwashia taa kubwa na kuzima papohapo.

    Akashangaa na kubaki akilikodolea macho zaidi. Akamwona mwanamke mrembo nyuma ya usukani, akitabasamu. Kiwembe alishangaa, akamtazama mwanamke huyo kwa makini akijaribu kuvuta kumbukumbu ni wapi waliwahi kuonana.

    Hakukumbuka chochote, na zaidi aliamini kuwa hamtambui mwanamke huyo. Japo alishawaangusha wanawake wengi kitandani kwake, hata hivyo hakuwa ni mtu wa kupoteza kumbukumbu ya sura ya yeyote katika msururu wao.

    “Nakwenda mjini, kaka, ingia twende…” tayari mlango ulishafunguka, hii ikiwa ni ishara rasmi ya kumtaka Kiwembe apenye katika kiti cha mbele.

    “Aaah… asante, sina haraka, nashukuru sana kwa msaada wako,” Kiwembe aliiruka lifti hiyo.

    Mrembo yule aliachia tabasamu la mbali huku akiendelea kumtazama Kiwembe. “Hata mimi sina haraka, kaka’angu,” hatimaye alisema. “Usihofu, twende unipe kampani.”

    Moyo wa Kiwembe uliachia mapigo ya woga. Paa! Pa! Pa! Kwa ujumla hakuwa mtu wa kumwamini mwanamke yeyote kwa kipindi hicho. Hata huyu alimfikiria kuwa ni mwenzake Husna Abdilatif. Katumwa!

    Hata hivyo akapiga moyo konde na kutoa kauli iliyoonesha jinsi alivyo mzoefu wa viumbe wa kike.

    “Usijali mtoto mzuri, naingia kwa heshima yako tu,” alisema huku akiingia garini. Akaongeza, “Sitaki kukuudhi. Mrembo wa aina yako hapaswi kukwazwa kwa namna yoyote ile. Kumkwaza mrembo wa aina yako ni kosa la jinai hapa duniani na hata huko mbinguni.”

    Ilikuwa ni kauli yenye woga wa asilimia mia moja moyoni, japo kinywani hakutoa taswira yoyote ya aina hiyo.

    Gari liliondoka. Ukimya ukatawala wakati wakiwa wanasogea taratibu kwa kufuata foleni. Hatimaye ni mrembo huyo aliyeuvunja ukimya huo.

    “Mwenzangu unaitwa nani?”

    Kiwembe alikohoa kidogo. Akainamisha kichwa mapajani mwake.

    “Mimi naitwa Suzana,” mrembo aliendelea. “Waweza kuniita Suzy tu kwani ndivyo wengi walivyozoea kuniita. Naishi Mbezi Mwisho.”

    Sasa walikuwa wakivuka taa za makutano ya Barabara za Morogoro, Swahili na Umoja wa Mataifa.

    Kiwembe alikuwa kimya kama mfiwa anayepelekwa kwenye mazishi ya mama yake mzazi. Na katika ukimya huo, alikuwa akijing’ata kidole kama msichana atongozwaye.

    Suzy alimtazama kidogo na kushangazwa na ukimya wake. Akajihisi mnyonge, na kujiwa na hisia kuwa Kiwembe anamchukulia kuwa ni mwanamke ‘anayejigonga’. Lakini wakati akiwaza hivyo, mara Kiwembe akaipata sauti yake.

    “Naitwa Kiwembe.”

    “Kiwembe?” Suzy alihoji kwa mshangao.

    “Ndiyo, Kiwembe.”

    “Jina la pili?”

    “La pili?!”

    “Ndiyo,” Suzy alijibu. “Yaani kwa mfano, mie nimekwambia naitwa Suzy. Jina langu halisi ni Suzana Andrew. Nd’o maana nakuuliza na wewe; Kiwembe nani?”

    “Yaani jina la baba’angu?”

    “Nd’o maana’ake.”

    “Sawa, nimekuelewa,” Kiwembe alisema kwa sauti ya chini akionekana dhahiri kunyong’onyea. Akaongeza, “Kwa kweli sina jina la baba.”

    “Una maana gani?”

    “Nasikia wazazi wangu walifariki wakati ningali mdogo.”

    Suzy alitikisa kichwa kwa huzuni. Kisha kwa sauti ya upole alisema, “Pole sana kaka’angu. Hii ndiyo dunia. Leo tupo, kesho hatupo. Dunia siyo yetu, sote tutaiacha kila mtu kwa siku yake. Yote ni mapenzi ya Mungu. Pole sana, Kiwembe.”

    “Asante.”

    Suzy hakupenda kuendeleza mazungumzo yasiyo hata na chembe ya furaha. Haraka akamtupia swali Kiwembe: “Unaishi wapi, kaka’angu?”

    Kiwembe alishtushwa na swali hilo. Akashusha pumzi ndefu akifikiria jibu la kumpa Suzy. Amwambie anaishi wapi? Kariakoo? Hapana. Kwa upande wake alikiona kitongoji cha Kariakoo hakina hadhi; ni eneo lililofurika msongamano wa majumba na uswahili mwingi. Magomeni? Labda. Kidogo alipaona Magomeni ni sehemu yenye hadhi japo kabla hajahamia Kinondoni alipachukulia kuwa ni kitovu cha majambazi sugu.

    Hatimaye akaamua kutotaja makazi ya bandia. Akatoboa ukweli: “Niko Zanzibar Hotel.”

    “Zanzibar Hotel? Una maana kule Zanaki Street?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ndiyo.”

    Suzy aliguna huku akimtazama kwa jicho la wizi. “Kwa nini unaishi hoteli? Kwani we’ ni mgeni hapa?”

    “Ndiyo, nimekuja kwa shughuli za kibiashara.”

    “Kutoka wapi?”

    “Tanga,” Kiwembe aliongopa.

    “Ok,” Suzy alisema huku akikanyaga breki.

    Katika kipindi hicho Kiwembe akawa akimtazama Suzy usoni, kifuani hadi nyayoni kwa chati na kwa makini sana. Hakushangazwa na vazi hili la Suzy. Lilikuwa ni gauni jekundu, fupi ambalo kwa wakati huo Suzy akiwa garini lilijivuta na kuyaacha wazi mapaja yake makubwa

    Kiwembe hakushangazwa na vazi hilo kwani kwa jiji la Dar, ni vigumu kutembea mitaa miwili au mitatu bila ya kupishana na mwanadada ambaye kama hatakuwa amevaa suruali ya kitambaa chepesi iliyombana sana, basi atakuwa amevaa gauni au sketi fupi sana.

    Alivutiwa na umbo la Suzy, lakini hakuwa na ule moyo wa ujasiri kama alivyokuwa kabla ya siku hiyo.

    Hata hivyo alijipa ujasiri wa bandia kwa kumuuliza, “Unaonaje ka’ leo ungenikaribisha kwako, nipajue, ili siku nyingine kama utaridhia, niwe mgeni wako badala ya kutumia gharama kubwa kuishi hotelini?”

    Aliuliza hivyo akitarajia kukumbana na pingamizi kali au la wastani kutoka kwa Suzy. Lakini haikuwa hivyo. Suzy aliachia lile tabasamu lake kwa mara nyingine kisha akasema, “Wewe tu. Kwa bahati nzuri siishi kwa wazazi wangu. Nimejitahidi kununua kijibanda kidogo cha kunihifadhi.”

    “Uko peke yako?”

    “Peke yangu.”

    “Kwa nini?”

    “Kwani ulitegemea niishi na nani mwingine?” Suzy alicheka kidogo. “Nyumba nimenunua kwa pesa zangu. Sasa nani mwingine ambaye ni lazima niishi naye?”

    “Mumeo.”

    Kwa mara nyingine Suzy akacheka. “Labda,” alisema. “Lakini kwa kweli sina mume wala mchumba…”

    “Lakini una boy friend?”

    “Niliwahi kuwa naye, lakini…” Suzy alisema na kusita ghafla.

    Walikuwa wamefika kwenye makutano ya barabara za Morogoro, Mazengo na Msimbazi. Suzy akakanyaga breki na kusubiri ruhusa ya taa.

    “Lakini …” Kiwembe alichokoza akimbana kuhusu kauli aliyoisitisha punde.

    “Aah, tu’shavunja mkataba,” Suzy alijibu kwa unyonge.

    “Kwa nini?”

    “Basi tu. Tuliamua.”

    “Kwa nini mliamua hivyo, au ni kutokana na sababu zisizoweza kuzuilika?”

    “Ndivyo ilivyokuwa.”

    Kiwembe alimtazama Suzy kiwiziwizi na kumwona kabadilika usoni. Akahisi kuwa huenda hakufurahishwa na maswali au udadisi wake. Kwa kuepusha kumwudhi zaidi, akaamua kutosema lolote tena.

    Ukimya ukatawala. Mara taa zikawaka. Suzy akamtazama Kiwembe usoni. Kiwembe naye akamgeukia. Macho yao yakagongana. Suzy akaachia tena lile tabasamu lake la ‘kuua.’ Kisha akasema, “Samahani kaka Kiwembe, nimefuata vifaa fulani hapa Kariakoo, mtaa wa Sikukuu. Sitachukua zaidi ya robo saa, tutakwenda kwangu Mbezi Mwisho ukapaone.”

    Yalikuwa ni maneno yaliyomchanganya Kiwembe kwa kiasi kikubwa. Hakuwa ni mtu wa kukaa chumbani na mwanamke yeyote mwenye mvuto mkali, na aache kumpapasa au kumtomasatomasa baada ya kumshushia maneno yenye mtiririko uwezao kumlainisha kwa haraka.

    Lakini kwa siku hii, hakuwa yule Kiwembe halisi, Kiwembe aliyekuwa na uzoefu wa kutoifunga zipu ya suruali yake. Huyu alikuwa ni Kiwembe mwingine, Kiwembe ambaye tayari kishaipata ajali kubwa na ya kusikitisha.

    Hii kauli ya Suzy ilimfanya amchukie Suzy na pia akajichukia mwenyewe. Lakini alilazimika kuimeza chuki hiyo, na badala yake, naye akatabasamu kidogo, hili likiwa ni tabasamu lililojaa unafiki mtupu.

    “Samahani da’Suzy,” hatimaye alisema. “Kwa leo labda tuahirishe. Tufanye kesho jioni….”

    “Kwa nini?” Suzy alimuuliza huku akimtazama kwa mshangao.

    “Ni ghafla mno.”

    “Hapana, sio ghafla, Kiwembe,” Suzy alisema. “Ingekuwa ghafla ungependekeza iwe leo? Au huniamini? Unahofia kuwa kuna mwanamume kwangu?”

    “Hapana, sina maana hiyo, Suzy.”

    “Ila?”

    “Kuna suala moja ni’lopaswa kulitekeleza leo hii. Tena ni nyakati hizihizi.”

    Wakati huo Suzy alikuwa ameegesha gari mwanzoni mwa mtaa wa Sikukuu. Akamtazama Kiwembe kwa macho makali kidogo, kisha akauliza, “Kwa hiyo inakuwaje?”

    “Tufanye kesho.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kesho?!”

    “Ndio, kesho,” Kiwembe alijibu kwa msisitizo. Akaongeza, “Kwa leo acha niteremkie hapa.”

    Suzy alikunja uso. Akapumua kwa nguvu na kutulia akikodoa macho mbele bila ya kutamka chochote. Hatimaye aliuliza, “Kesho, saa ngapi?”

    “Jioni. Tufanye kati ya saa kumi na saa kumi na mbili kamili.”

    Wakati Kiwembe akitamka hivyo alishafungua mlango na kuonyesha dalili ya kutoka.

    “Subiri,” Suzy alimzuia. “Unaweza kunipa namba yako ya simu?”

    “Simu yangu imeibwa juzi,” Kiwembe aliamua kuongopa. Simu ilikuwa mfukoni mwa suruali. Na aliomba Mungu isitokee ikaita. Akaongeza, “ Ndio niko kwenye pilikapilika kutafuta simu nyingine.”

    Suzy alifikiri kidogo kisha akasema, “Nipe namba ya chumba chako.”

    “Namba kumi.”

    “Usitoke!”

    “Sitatoka!”

    Kiwembe hakutoa ahadi hiyo kwa dhati. Athari zilizompata zilishamfanya ashindwe kujiamini. Hakuwa tayari kuchojoa nguo zake akiwa na mwanamke faraghani bila ya uhakika wa kutimiza hicho kilichowakutanisha.

    Hivyo, pindi tu walipoachana, alikwenda moja kwa moja Zanzibar Hotel, chumbani mwake ambako alishinda kutwa huku akiwa mnyonge. Usiku ulipotinga akaambulia usingizi wa maruweruwe, usingizi ambao hakumbuki ni lini aliupata kwa mara ya mwisho.

    Ni usiku huohuo wa usingizi wa mang’amung’amu ndipo alipojiwa na wazo jipya, wazo la kuondoka jijini Dar es Salaam. Ndiyo, aikimbie Dar es Salaam na kurudi Kigoma katika kitongoji kilekile cha Ujiji ambako angeishi tena na Mama Kadala, guberi la Kimanyema lililomwonyesha dunia ya mapenzi kabla ya kufikia umri wa kulijua na kulionja penzi.

    Kulipopambazuka tu akajihimu kufika kituo cha Reli ambako baada ya kuzungumza na mmoja wa wafanyakazi wa hapo, hatimaye akajikuta akikabidhiwa tikiti ya daraja la kwanza ya treni iliyotazamiwa kuondoka jiono ya siku hiyo.

    Aliporudi hotelini alijiandaa kwa safari hiyo akidhamiria kukabidhi chumba kabla ya saa 10 jioni ili Suzy asimkute hapo. Naam, kila jambo lilitekelezwa kwa jinsi alivyopanga.

    Akaikimbia Dar es Salaam.

    *****



    ***MASKINI KIWEMBE yanamtokea puani sasa………..

    Hali hii hadi lini…………JE nini mwisho wa kiwembe????



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog