Chombezo : Guberi La Kimanyema
Sehemu Ya Tatu (3)
“Nakupa dakika moja ya mwisho,” Khalifa alimtisha.
Kiwembe hakuwa na budi kuyavulia maji nguo na kuyaoga. Akaamua kuutapika ukweli ili aijue hatma yake baada ya kuitii amri ya huyu ambaye ni kama vile ndiye aliyekuwa ameishika roho yake.
“Samahani…samahani, mzee” ndivyo alivyoanza kwa sauti yenye mkwaruzo wa mbali. “Wanawake wanaponza. Baadhi yao wanaponza. Aliniambia mwenyewe kuwa hana mume, hajaolewa. Unaona ibilisi huyo wa mwanamke? Unaona? Nilipomuuliza na hapo unapokaa ni kwa nani, eti ni kwa baba na mama yake.”
“Ukamwamini?”
“Sasa kumbe nisingemwamini?” Kiwembe aliyasema maneno hayo kwa unyonge na unyenyekevu uliopandikiza chembe ya huruma kwenye moyo wa Khalifa Mwinyimkuu.
Hidaya ambaye muda wote huo alikuwa amekaa chini akilia, aliangaza macho yake mekundu huku na kule na kufanikiwa kuona ndoo ndogo ya plastiki iliyokuwa tupu. Akaitwaa na kumvurumishia Kiwembe kichwani puu!
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Koma!” albwata kwa sauti kali. “Koma mshenzi we! Mwanga wa mchana we! Sikukwambia kuwa n’na mume wangu ukan’ambia eti tuibe kidogo! Leo unanigeuka?”
Khalifa Mwinyimkuu alinyanyuka na kumzaba kofi kali Hidaya, kofi lililompeleka sakafuni sawia. “Unatakiwa kuwa na adabu ndani ya nyumba hii, mbwa we!” alimwambia huku akimtazama kwa yale macho yake makali na yatishayo.
Hidaya alibaki pale sakafuni akilia kichinichini.
Khalifa Mwinyimkuu akamgeukia Kiwembe. “Mheshimiwa tuendelee na hoja yetu,” alimwambia huku akimtazma usoni.
Kiwembe akayaepusha macho yake na kutazama chini.
“Pamoja na kukuponza,” Khalifa aliendelea. “Mmeshafanya mapenzi mara nyingi sana, na ndiyo maana hata mimi mwenye haki hana hamu nami tena. Hamu yote iko kwako. Ni mara ngapi mmeshafanya mapenzi ya kimwili?”
Kiwembe hakulitarajia swali hilo. Kwa kutojiamini alijibu, “Leo ni siku ya pili tu, mzee…kweli tena, mbona yote ni’shasema?”
Machozi yakamlengalenga Khalifa Mwinyimkuu, hatimaye yakadondoka bila ya kutegemea taa…ta…ta…! Alihitaji ushahidi upi mwingine kwa mtu huyo zaidi ya huo aliousikia na kuushuhudia? Ni kashfa ipi ya penzi zaidi ya hii?
Ni kipi alichokikosa mkewe hata aamue kuutoa mwili wake kwa wapita njia? Hata kama yeye, Khalifa, hana pesa au hamridhishi katika tendo la ndoa, lakini si walikubaliana kuishi pamoja kwa uaminifu, wakivumiliana katika taabu za dunia hii na kusaidiana kupata ufumbuzi wa tatizo lolote katika ndoa yao?
Iweje basi amdhalilishe kiasi hiki? Kuna faida gani kumdhalilisha mwenzi wako katika ndoa kama siyo tamaa, ukosefu wa akili, mawazo finyu na uamuzi wa haraka?
Aliyapangusa machozi, akauinua uso na kumtazama Kiwembe. Akasema, “Kwa taarifa yako bwa’mdogo, kuanzia sasa, muda huu tunapoongea, huyu Hidaya siyo mke wangu tena. Kaa ukijua hivyo. Ni wako. Nimemwacha kuanzia leo, shahidi wa kwanza ukiwa ni wewe. Akitoka hapa atakuja kwako baada ya kumkabidhi talaka yake na kufungasha kila kilicho chake ndani ya nyumba yangu.”
Kiwembe hakutamka chochote. Alikuwa ameinamisha uso kama kondoo, akiitazama sakafu kama vile ndiyo kwanza anaiona.
“Na kutokana na maelezo yako,” Khalifa Mwinyimkuu aliendelea, “huna hatia yoyote kwangu. Unaweza kuondoka, ukamsubiri hukohuko mnakokutania katia nyendo zenu. Sawa?”
Kiwembe hakuyaamini masikio yake. Fahamu zilikataa katakata kuamini kuwa yu huru. Ndiyo, fahamu zilimpotea kwa sekunde chache. Zilipomrudia, aliinyanyua miguu yake aliyoihisi mizito, akaivuta taratibu huku kakiinamisha kichwa chake kama jogoo aliyepigwa na mtetea kuku mke. Bado ni kama vile alikuwa ndotoni. Ametoka mzima ndani ya nyumba ya Khalifa Mwinyimkuu aliyeogopwa kama kifo?
Khalifa Mwinyimkuu alimtazama wakati akiondoka, na alipokwishatokomea, alimgeukia mkewe, Hidaya. “Na wewe kusanya kila kilicho chako, upotee machoni pangu,” alimwamuru. “Chukua kila kilicho chako na chochote kile ukipendacho kikakufae huko uendako.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kilio kikali kikamtoka Hidaya. “Nisamehe mume wangu.. tafadhali nisamehe…ni ibilisi tu kanipitia…” aliomboleza huku akigaragara miguuni pa Khalifa Mwinyimkuu.
Haikuwa kauli yenye nguvu wala hakikuwa ni kilio chenye uwezo wa kuyabadili mawazo ya Khalifa Mwinyimkuu.
Ikabaki ile methali ya “kala yake riziki imemtosha, iliyobaki awaachie wenzake!”
*****
ILIMLAZIMU Kiwembe kuukimbia mji wa Kigoma. Japo hakuguswa hata ukucha na Khalifa Mwinyimkuu siku ile ya fumanizi, hata hivyo hakuwa radhi kuendelea kuishi mjini hapo. Hivyo siku ya tatu, saa 11.00 jioni alikuwa ndani ya treni akielekea jijini Dar es Salaam ambako alijihusisha na utapeli akishirikiana na wakongwe wa kazi hiyo aliokutana nao hukohuko Dar.
Miezi michache baadaye mambo yakawa yamemnyookea vilivyo. Pesa bwerere zikammiminikia. Lakini bado alikuwa yuleyule Kiwembe, kichaa wa mapenzi asiyepitwa na kitu. Alibadilisha wanawake kama nguo. Na hakuwa na muda wa kupanga chumba uswahilini.
Alipoingia jijini Dar, kituo chake cha awali kilikuwa Bongo Guest House katika kitongoji cha Manzese. Uchumi ulipomkubali akapaona Manzese ni makazi ya vibaka. Akahamia Magomeni Mapipa. Alipoanza kuionja ladha ya utajiri, akapaona Magomeni ni kituo kikuu cha majambazi sugu na wafanyabiashara uchwara wa dawa za kulevya. Akahama na kuivaa Kinondoni ambako alifikia Kilingeni Hotel.
Naam, utapeli mdogomdogo alioufanya katika vitongoji mbalimbali jijini Dar ulimwongezea pesa siku hadi siku. Na kazi yake hiyo ya ajabu aliifanya huku na kule, akilazimika mara kwa mara kwenda katika kitongoji hiki au kile ama kwa kutumia gari la kukodi au hata kwa miguu.
Ni katika pitapita yake hiyo ndipo siku moja akakumbana na Hidaya katikati ya jiji, eneo la Posta Mpya. Kila mmoja alishtuka kumwona mwingine. Wakashikana mikono kwa muda bila ya kutamka chochote.
Hatimaye: “Kiwembe, uko huku?” Hidaya alimwanza.
“Niko huku, Hidaya. Vipi, mbona na wewe uko huku?”
“Ndio, na mimi niko huku…” Hidaya alisema, akasita na kukunja uso kidogo. Hakuonyesha kuendelea kuzungumza.
“Unaishi wapi?”
“Buguruni.”
“Kwa nani?”
“Kwangu.”
Kiwembe aliona hali ya kukosa raha usoni pa Hidaya. Hivyo akamalizia kwa kusema, “Tusitupane Hidaya.” Akamtazama mkono wa kushoto na kumwona kashika simu. Akaongeza, “Naomba namba yako.”
Hidaya hakuwa na hiana. Papohapo akamtajia. Baada ya Kiwembe kuingiza namba hizo kwenye simu yake akapiga. Simu ya Hidaya ikaita. “Na mimi hiyo nd’o namba yangu,” hatimaye alimwambia.
“Poa,” Hidaya alisema huku sasa uso wake ukiwa umekiunjuka na kunyesha uchangamfu. Kisha akaongeza, “ Tutaonana basi, Kiwembe. Kumbuka…kumbuka ulivyonichanganya siku zile. Bado nakuhitaji. Usitupe jongoo na mti wake, Kiwembe wangu. Ni matumaini yangu ipo siku tutaonana tena, na siku hiyo haiko mbali.Tutakapoonana tena ndipo tutakapofungua majalada ya kumbukumbu na kuzisoma nyaraka zilizomo.”
Yalikuwa ni maneno matamu sana masikioni mwa Kiwembe, lakini utamu huo ulidumu kwa sekunde tano tu pale kumbukumbu zilipomrudia kichwani, kumbukumbu za tukio lisilosahaulika kule Kimondomondo Hotel, nje kidogo ya mji wa Kigoma.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hata walipoachana Kiwembe hakutaka tena kumkumbuka Hidaya, japo zoezi hilo la kumsahau lilishindikana. Atamsahau vipi ilhali katika kumbukumbu za wanawake aliowahi kustarehe nao, Hidaya alikuwa na mabo ya ziada chumbani?
Hakuweza kumsahau, lakini alijitahidi kutompigia simu, jitihada iliyofanikiwa kwa siku tatu mfululizo na hasa kwa kuwa kila siku jioni na usiku kucha hakuwa akilala peke yake; aliupitisha usiku akiwa na mwanamke mwenye kiu ya bia na uchu wa pesa zake. Hivyo hakuwa na sababu ya kumpigia simu Hidaya.
*****
HII ilikuwa ni siku ya nne. Tangu asubuhi mvua ilikuwa ikinyesha jijini Dara es Salaam. Kiwembe alikuwa juu kabisa ya jengo la hoteli ya Kilingeni ambako pia kulikuwa na baa. Aliketi chini ya mwavuli akinywa soda taratibu huku akiangaza macho huku na kule, akiwatazama wanywaji wengine ambao baadhi walikuwa wakinywa soda na baadhi wakifakamia bia na pombe kali.
Eneo hilo lilichangamka sana. Wanawake warembo nao hawakukosekana. Kuna walioingia na kutoka. Macho ya Kiwembe yaliganda kwa wanawake tu! Tamaa iliwaka usoni pake bila ya kificho. Akamtazama kila mwanamke kwa matamanio makubwa, baadhi yao akiwasifu kimoyomoyo kwa jinsi walivyotembea kwa madaha.
Kuna waliomkosha kwa macho yao ‘yaliyochoka,’ macho ambayo muda wote yamtazamapo mwanamume ni kama vile yanamwambia, “nakuhitaji” au “nakupenda” au “niko tayari hata sasa hivi.” Wengine walibeba matiti yenye ukubwa wa wastani, yenye uhai, yakamtia ushawishi wa kuyanyonya.
Pia walikuwepo wale walioivuruga akili yake pale walipomwachia migongo wakati wakitembea na kuonyesha kuwa walidhamiria kumtesa kwa kuyatingisha makalio yao kiaina kadri walivyonyanyua miguu yao.
Kwa ujumla macho yake hayakutulia. Alimsifu huyu kwa hili na kumkosoa yule kwa lile. Soda yake ilipokwisha, alnyanyuka na kuondoka. Akateremka akielekea chumbani kwake ghorofa ya nne. Ngazini akakutana na wanawake wakipanda kule kwenye ukumbi wa baa. Wote walikuwa wakivutia kwa sura na maumbo yao, lakini kwa asubuhi hii alihitaji kuwa makini, asipaparikie wanawake.
Aliamua hivyo kwa kuwa jana usiku alikuwa na mwanamke mmoja ambaye walitoka pamoja Mango Garden na kuja kutia nanga chumbani mwake hapo hotelini. Kitanda kilipowalaki, Kiwembe akakiona cha moto. Mwanamke alifanya aliyopaswa kuyafanya, akidiriki hata kumwonyesha Kiwembe mitindo ambayo hakuwahi kuifanya kwa imani kuwa ni kinyume na maadili ya Kibantu. Baada ya kufakamia supu asubuhi, kisha akashushia soda, sasa aliamua kurudi chumbani kupumzika.
Alipokwishaingia chumbani alifunga mlango nyuma yake kisha akajitupa kitandani. Pia alihitaji kupumzika ili apange ratiba ya mahangaiko ya kesho katika kazi yake ya utapeli. Lakini haikuwa kama alivyotaka. Muda huohuo simu yake iliita. Akaitwaa na kuitazama kwenye skirini. Akakuta maandishi: PRIVATE NUMBER. Akaguna.
Hakuweza kumjua mpigaji, na hakuwa na sababu ya kutoipokea simu hiyo. Akilini mwake wakati akiitoa simu, alihisi kuwa huenda Kizito, rafikiye aliyeishi Gongo la Mboto ndiye aliyepiga. Kama siye huyo basi ni Kisauti wa Sinza. Wote hao walikuwa washirika wake wakubwa katika shughuli zao za ujanja ujanja.
Alikuwa amezisajili namba za hao rafikize pamoja na majina yao katika simu yake. Ni nani basi huyu aliyepiga? Anataka nini? Na kwa nini afiche namba yake?
Alijiuliza swali hili na lile na kukosa jibu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Simu iliita hadi ikakatika. Ikaanza kuita tena. Akaamua kuipokea.
“Hallow,” alisema kwa sauti ya chini na nzito, akisikilizia upande wa pili.
“Ni Kiwembe sio?” ilikuwa ni sauti nyembamba, ya kike toka upande wa pili.
“Yeah. We n’nani?”
Ukimya mfupi ukapita kisha sauti hiyo laini ya kike ikapenya tena masikioni mwa Kiwembe.
“Rudisha funguo za chumba chako. Hata kama unaweza kulipa shilingi elfu ishirini kwa siku nzima bila ya matatizo, lakini ni vema uangalie mbele…”
“Lakini we n’nani?” sauti ya Kiwembe ilikuwa kali.
“Acha ukali, Kiwembe,” alijibiwa. “Mimi ni yuleyule wako wa siku zote. Ukiniona utanikumbuka. Kiwembe, mpenzi wangu, nakupenda sana. Nakupenda na n’nayajali maisha yako. Tafadhali fanya kama nilivyokwambia. Nitakufuata baada ya robo saa hivi. Ni vema kama utahamia huku niliko.”
“We, n’nani?!”
“Nimekwambia ni yuleyule wako…”
“Wangu?”
“Ndio. Mbona unaonyesha kushangaa. Kwani una wangapi laazizi wangu?”
“Sina nimpendaye,” Kiwembe alijibu kwa hasira.
“Kwa sasa huna, lakini aliwahi kuwapo?”
Kiwembe alizidi kughadhibika. Akataka kumpa jibu mpigaji huyo, jibu baya litakalomfanya akate simu bila kupenda. Lakini aliurudisha moyo nyuma, akaamua kuwa mpole hadi amjue vizuri mtu huyo.
“Yeah, aliwahi kuwapo,” alijibu. “Lakini, tafadhali, n’ambie wewe ni nani? Unanifahamu, lakini mimi sijakufahamu. Huoni kuwa hunitendei haki?”
Kicheko kikali kikatoka upande wa pili. Kisha jibu likapenya masikioni mwa Kiwembe: “Ok, ni yule aliyediriki kukuvulia nguo huku akiwa ni mke wa mtu.”
“Nani?” Kiwembe alibwata. “Haloo… haloo…haloo…”
Simu ilishakatwa.
Kiwembe alibaki kaduwaa. Hakuweza kujipumzisha tena. Akaketi kitandani huku akijiuliza, ni nani mtu huyu? Kumbukumbu zake zisizofutika kichwani zilimwambia kuwa mwanamke aliyefanya naye mapenzi ilhali ni mke wa mtu, ni Hidaya wa Kigoma. Ni majuzi tu, kiasi cha siku tatu zilizopita alipokutana na Hidaya huyohuyo eneo la katikati ya jiji, Posta Mpya. Wakapeana namba za simu zao.
Lakini Hidaya siyo mtu wa kwanza kufanya nae mapenzi huko Kigoma na hata jijini Dar es Salaam. Hakumbuki idadi yao, lakini ni wengi. Na baadhi yao waliwahi kumtamkia kuwa ni wake za watu. Na walipeana namba za simu.
Ni nani basi huyu aliyepiga simu akimtaka arudishe chumba na kwenda kukaa kwake? Jibu la swali hilo halikupatikana. Akajaribu kuwakumbuka baadhi ya wanawake aliowahi kustarehe nao ilhali ni wake za watu. Akavikumbuka vituko vyao vya chumbani, vituko vilivyomfanya awapende au apende kustarehe nao, zaidi ya wale wanawake waliokuwa huru, hawajaolewa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mara akayarejesha mawazo yake Kigoma, na kuikumbuka ile siku iliyomfanya auone mji wa Kigoma mchungu, hususan vitongoji vya Ujiji na Mwanga. Hakupenda kumbukumbu ya kubalehe kifuani pa Mama Kadala irejee kichwani mwake. Hakupenda kukumbuka kuwa kufichuka kwa siri ya penzi kati yake na Sharifa ndiko kulikosababisha apoteze heshima, huduma na fadhila kwa mama ya Sharifa (Mama Kadala).
Ndiyo, hakuyapenda yote hayo. Lakini, zaidi hakupenda kuirejesha kichwani kumbukumbu ya ile siku alipokuwa Kimondomondo Hotel, nje kidogo ya mji wa Kigoma. Siku alipofumaniwa papo kwa papo na Khalifa Mwinyimkuu, mume wa ndoa wa Hidaya binti Sufiani.
Asingeweza kuisahau siku hiyo, lakini pia haikuwa rahisi kuusahau wepesi na utaalamu wake Hidaya binti Sufiani pindi wazichojoapo nguo zao na kujitupa kitandani au popote pale watakapoona panawafaa kwa kile walichodhamiria kukitenda.
Asingesahau!
Na mara akawaza kuwa huenda ni Hidaya aliyepiga simu hiyo. Atakuwa ni yeye? Hakupenda kuamini hivyo. Na kama ndiye kwa nini aifiche namba yake ilhali walipeana namba zao kwa hiari ya kila mmoja?
Alitambua fika kuwa ni yeye aliyasababisha ndoa ya Khalifa Mwinyimkuu na Hidaya ikavunjika. Kama Hidaya na Khalifa Mwinyimkuu waliiishi kwa miaka mitatu, wakilala chumba kimoja, kitanda kimoja, wakiridhishana kimwili, haiwezi kuwa vigumu kwao kuzungumza lolote kwa kuelewana licha ya kutengana katika ndoa yao.
Kwa hali hiyo, hisia zilizojengeka kichwani mwake ni kwamba kulikuwa na mpango mbaya dhidi yake, mpango wa kuhatarisha maisha yake. Akahisi kuwa watakuwa wameungana katika kulipa kisasi.
“Hanipati!” alinong’ona kwa uchungu.
Huku akijifuta jasho usoni, aliirejesha simu mfukoni kisha akatikisa kichwa, uso ukiwa umekunjamana, lakini ukiwa hautoi taswira ya kama amekasirika au kufadhaika. Akajilaza tena kitandani na kuwaza kama ingemstahili kuendelea kuzubaa chumbani humo au aondoke na kwenda sehemu yoyote kuiliwaza akili kwa bia mbili, tatu.
*****
KHASSAM alikuwa miongoni mwa marafiki wa Kiwembe. Alikuwa ni Mtanzania mwenye asili ya Kiasia. Urafiki wa Khassam na Kiwembe licha ya kuwa na ushirikiano katika kazi yao ya utapeli pia ulitokana na mapenzi yao kwa pombe na wanawake. Kila ilipotokea Khassam akawa amepata pesa nyingi, kitu cha kwanza alichofanya ni kumtafuta Kiwembe. Anamtafuta na wakionana, wanakwenda baa ambako watakunywa bia nyingi, watakula nyama choma kwa fujo na hatima ya yote ni kujitwalia wanawake ambao huwa wako tayari kwa yeyote mradi pesa ziwepo.
Asubuhi hii, Khassam ambaye makazi yake yalikuwa maeneo ya Upanga, alikuwa na pesa za kumwaga. Akakodi teksi kutoka mjini huku uchovu uliosababishwa na pombe alizobugia jana yake ukimsumbua kichwani. Alipofika Kilingeni Hotel akakwea ngazi haraka hadi mlangoni pa Kiwembe. Akagonga.
“Nani wewe?”
“Vipi wewe? Umelala” Fungua..kwani una matatizo gani?”
Haikuwa sauti ngeni masikioni mwa Kiwembe. Alimjua mgongaji. Papohapo akafungua mlango.
“Enhe, una nini?” Khassam alihoji huku akimtazama rafiki yake kwa mshangao.
“Tafadhali nipe lifti. Nadhani nihamie Zanzibar Hotel.”
“Kwa nini?”
“Twende, nitakwambia baadaye.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Waliingia ndani ya gari dogo la Khassam na kuelekea katikati ya jiji ambako walifikia Zanzibar Hotel, mtaa wa Zanaki. Zanzibar Hotel ilikuwa imechangamka. Ukumbi wa baa ulifurika watu, wanawake kwa wanaume.
Khassam na Kiwembe hawakwenda hapo kwa minajili ya kujiburudisha kwa vinywaji pekee. Hapana. Walikuwa na jingine lililowapeleka.
Wanawake.
Si mara moja au mbili walishafika hapo na kujipatia vinywaji na hatima yake huondoka na mijimama yenye kuiuza miili yao, mijimama iliyokuwa na mvuto mkali machoni mwa wanaume wapenda wanawake wazuri , na pia ikiwa ni mijimama ambayo haikuwa na kipingamizi chochote kwa aina yoyote ya penzi litakaloombwa na ‘mteja.’ Wao walijali thamani ya pesa. Basi!
Mchana huu wa kijimvua kilicholituliza joto la Dar kwa kiwango kikubwa, waliingia hapo huku Khassam akiwa na mpango uleule wa kusaka mwanamke. Hata hivyo baada ya muda aligundua kuwa rafikiye hakuwa katika hali nzuri kisaikolojia. Na alipomdadisi aliambulia jibu fupi tu, “Sijisikii vizuri kwa leo.”
“Kwa nini? Unaumwa?”
“Hapana. Lakini siko fiti. Nadhani itanibidi nichukue chumba hapa na kupumzika.”
“Kwa nini uhame ghafla pale Kilingeni?” Khassam alihoji kwa mshangao.
“Basi tu.”
“Au kuna ishu iliyolipuka?”
“Hakuna. Nadhani nikipumzika kama saa moja hivi nitarudia kuwa fiti.”
“Ok, hiari yako,” Khassam alisema kwa unyonge huku akigugumia bia iliyokuwa kwenye glasi.
Dakika chache baadaye Kiwembe alikuwa ameshapata chumba hapohapo Zanzibar Hotel. Akajilaza kitandani akijaribu kuuvuta usingizi bila ya mafanikio. Akabaki akigaragara huku akiwaza nini afanye.
Robo saa ikapita.
Nusu saa ikakatika.
Hatimaye saa nzima ikaisha akiwa hapohapo kitandani. Mara akajikuta akicheka. Ndiyo, alicheka kwa kukumbuka kuwa kilichomkimbiza kutoka kule Kilingeni Hotel, Kinondoni ni kumkwepa yule mtu aliyempigia simu, ambaye kwa sauti yake na lafudhi yake hakutofautiana na Hidaya.
Lakini mbona amekuwa mwepesi wa kumkimbia kama vile anamkimbia simba au mnyama yeyote mwenye hasira? Na kweli aliyepiga simu ni Hidaya au ameifananisha tu sauti na lafudhi yake ya Kimanyema?
Kwa kiasi fulani akajiona kuwa kafanya jambo la kipuuzi. Akajitoa kitandani na kushuka ghorofani haraka, moja kwa moja hadi kule baa ambako alimwacha rafikiye, Khassam.
Hakumkuta. Hata hivyo hakujali, wala hakuhangaika kumpigia simu. Alichofanya ni kuagiza bia na kuinywa taratibu, mawazo yake yakiwa yameshatulia na kuamua kurudi kuwatupia tena macho wanawake warembo waliotapakaa ukumbini humo.
Bia mbili zilipokwishapenya kooni mwake, akajisikia kughairi kuendelea kuwemo ndani ya baa hiyo. Akatoka na kuamua kubadili mazingira. Akakodi teksi akielekea Magomeni. Huko alifikia Magomeni Mikumi katika baa kongwe ya Lango La Jiji. Akakuta wingi wa watu, maradufu ya kule Zanzibar Hotel. Zaidi, hapa kulifurika wanawake kuliko kule Zanzibar Hotel. Wanawake waliokuwa hapa Lango La Jiji walivutwa na muziki wa kundi moja maarufu la taarabu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Machoni mwa Kiwembe, wanawake hawa walivutia zaidi kwa mavazi yao na unenguaji wao wa muziki, unenguaji uliomtia ushawishi wa kuwatupia maneno mawili, matatu. Aliketi sehemu ambayo aliweza kuwaona kwa uwazi zaidi watu wote walioingia hata wale waliojimwaga jukwaani kucheza muziki huo wa taarabu.
Bia zikaendelea kutua mezani pake. Mwanamume akaendelea kuburudika huku uchu wa kujipatia mwanamke hapo ukumbini ukizidi kumjaa. Na akaendelea kuwatazama kwa uchu wa matamanio wanawake wote waliomvutia, utazamaji ambao baadhi yao waliugundua na wakaamua kumvalia njuga kwa madhumuni yao binafsi.
*****
“USIZUBAE, usijivunge mwanamume…zungumza kiutu uzima na utapata ukitakacho,” msichana mmoja mrembo alimwambia Kiwembe huku akijipitishapitisha mbele yake. Wakati akitamka hivyo, alimtupia macho ya wizi Kiwembe kisha akaendelea na hamsini zake kwa mwendo wa ‘bata mzoea kupata.’
Kiwembe alimtazama mwanamke huyo kwa uchu zaidi. Naam, kama wale wasichana wengine aliwasifu kwa uzito wa vikalio vyao vilivyoumbwa kama chungu cha mtori, basi huyu alimsifu kwa umbo lake lililo mithili ya mtungi wa kusindika mbege.
Na hakustahimili, alijitoa kitini na kumfuata huku akijiuliza, ni nani atakayekufa kwa ugonjwa wa kawaida? Ni nani, wakati kila mtu hudaiwa kufa kwa Ukimwi?
Eti hata mtu akianguka toka mtini, watu watasema kajiangusha kwa kuwa anajijua ana Ukimwi. Maradhi ya malaria yalikuwapo zaidi ya miaka hamsini iliyopita, yakiua watu na bado yanaendelea kuua na kuwa tishio hadi leo, hadi kesho!
Kansa nayo ikawa muuaji mkubwa, lakini yote hayo sasa hayapewi uzito. Sasa hata mtu akifa kwa kipindupindu itadaiwa kuwa kafa kwa Ukimwi.
Utasikia: “Si uliona yule kijana alivyokaribia kufa? Katapika sana na kuhara kupita kiasi! Akakondaa! Alikuwa nao yulee..!”
Kwa mzee aliyefikia ukomo wa maisha yake, watasema, “Si tulisema! Alikuwa malaya sana mzee yule! Ulimcheki alivyoisha? Alidhani Ukimwi unakopesha! Alikuwa nao, ukawa unasambaa mwilini taratibu.”
Watasema mengi. Tatizo watakuwa wamesahau kuwa yule mzee alikuwa ni binadamu kama binadamu wengine. Alizaliwa, hivyo hakuwa na budi pia kufa. Tena ni heri yeye aliyefika hatua ya kuitwa ‘shaibu,’ mbona wapo wengi ambao hata umri wa miaka hamsini hawakuufikia?
Na tukiachilia mbali umri au rika la mtu, ni nani atakayetikiswa barabara na maradhi fulani na mtu huyo akaendelea kuwa na siha njema, labda zaidi ya alivyokuwa kabla hajaugua? Ama zama zile kabla ya kutangazwa Ukimwi watu walikuwa hawakondi au kuugua na hatimaye kufariki dunia?
Mbona kuna waliokuwa wakikumbwa na maradhi ya kuhara yaliyowaondoa duniani? Mbona wengine walitapika mfululizo hadi wakakumbwa na mauti?
Kiwembe aliwachukia sana wote walioamini kuwa mtu aliyeugua maradhi hayo, yakaudhoofisha mwili wake basi tayari ameshapata Ukimwi. Ndiyo, aliwachukia na akayachukia maongezi yao ambayo aliona kuwa yalilenga kuvuruga harakati zake za kuwafaidi viumbe wa kike.
Ataishi vipi duniani bila ya kustarehe na wanawake warembo kama hawa wanaojipitishapitisha mbele yake, wakiyatikisa maungo yao kwa namna ya ushawishi dhahiri kwa wanaume?
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Akilini mwake aliamini kuwa mwanamume aliye huru, na ana pesa za kutumia, yuko kwernye jiji la maraha na karaha kama Dar, akikosa kustarehe na warembo wa aina hii kwa vyovyote vile atakuwa na hitilafu kubwa maungoni mwake.
Ni nusu ya mwanamume!
Akiwa hapo Lango La Jiji, aliendelea kumtazama mwanamke huyo aliyemtupia maneno ya kumshawishi huku akimtazama kwa macho ya ‘kibiashara’ zaidi. Alikuwa ni mwanamke aliyekamilika kila idara, akiyavuta macho ya wakware wengi waliofurika ukumbini humo.
*****
UFUSKA ulikuwa ndani ya mishipa ya damu ya Kiwembe. Macho yake yakazidi kung’ara kila alipotazamana na msichana yule. Akapiga moyo konde na huku pia kimoyomoyo akisema, “Potelea mbali hata kama hao ndio Papa au Nyangumi wa baharini, sijali. Bahari ikichafuka, nisipoweza kuogelea nitatumia ngalawa na kasia za miti, lakini kujitosa baharini ni muhimu na lazima.”
Aliapa hivyo, na hakukubali kushindwa. Alitaka kuhakikisha kuwa kwa udi na uvumba anaitimiza azma yake. Na akiwa ni mtu wa aina ya kipekee, ambaye tangu abalehe kifuani pa Mama Kadala hakuwahi kukataliwa penzi na mwanamke yeyote, hata kwa huyu ‘Papa wa Nchi Kavu’ hakupata pingamizi lolote kwa mwanamke huyo mrembo kupindukia. ‘Papa’ huyo aliyetingisha Magomeni kwa uzuri wa sura na umbo lake, si mwingine bali ni Husna Abdilatif.
Wakakubaliana kuondoka pamoja baada ya kuhitimishwa onesho la muziki wa taarabu. Na kwa kuukoleza uhusiano wao huo mpya, meza yao haikukauka vinywaji. Kiwembe ambaye hakuwa na kawaida ya kunywa zaidi ya bia tatu, siku hiyo, mbele ya Husna Abdilatif bia tano zilimiminika tumboni!
Ni starehe gani nyingine aliyohitaji zaidi ya hiyo? Ni starehe gani kubwa kwa mwanamume rijali, zaidi ya kuketi na mwanamke mzuri ambaye anajua nini cha kumfanyia mwanamume hata kabla hawajachojoa nguo zao chumbani?
Pamoja na kunywa bia kwa kiwango kikubwa, hata hivyo Kiwembe aliburudika pia kwa utomasaji mzuri wa mwanamke huyo mrembo, Husna Abdilatif, mwanamke aliyefundwa, akafundika.
Hivyo kutokana na starehe aliyoipata, hakuwa hata na kumbukumbu aliondoka vipi hapo Lango La Jiji. Ni pale kulipokucha, akazinduka na kujikuta katika mazingira tete ndipo alipochanganyikiwa. Hakuyaamini macho yake.
Alikuwa kalazwa juu ya kitanda cha kamba kilichotandikwa shuka nyeusi. Alipozungusha macho kushoto na kulia akawaona wanawake watatu wakiwa wamesimama huku wakimtazama, nyuso zao zikimdhihaki. Akashangaa, akaduwaa. Zaidi, alishtuka baada ya kubaini kuwa miongoni mwa wanawake hao ni Hidaya binti Sufiani. Akamkodolea macho zaidi, akihisi kuwa yu ndotoni.
“He..he..he..!” Hidaya aliachia kicheko cha dhihaka. Akaendelea, “Hata ukinikodolea macho mwanahizaya we, ng’o! Huniwezi! Labda unipige na radi ya kimanyema kama unaweza. Na huniwezi!”
Yalikuwa ni maneno yaliyomtoka Hidaya kwa sauti iliyojaa kejeli na dharau isiyo kifani. Na bado akaendelea kumtazama huku akitabasamu, tabasamu lisilokuwa na taswira yoyote ya upendo.
Bado Kiwembe alihisi yu katika ndoto isiyopendeza. Alikuwa mtupu kama alivyozaliwa, kafungwa kamba mikono na miguu na kamba hizo zikiwa zimeshikwa na matendegu ya kitanda hicho. Ni kipi kilichotokea hadi akjikuta katika hali hiyo? Hakuweza kujua.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ni hapo alipoamua kuzirudisha kumbukumbu zake nyuma. Na kwa kuwa ukweli ni kwamba hakuwa ndotoni, kumbukumbu hizo zilimjia mara moja, zikianzia pale Lango La Jiji, Magomeni Mikumi.
*****
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment