Search This Blog

Monday, October 24, 2022

FACEBOOK CHATTING - 5

 





    Chombezo : Facebook Chatting

    Sehemu Ya Tano (5)


    Ilipoishia 




    AZIZA: Kweli wewe mfuatiliaji. Kwa hiyo ukagundua mimi kuwa ni mzuri?
    MIMI: Yeah! Nimegundua hilo kiasi ambacho kama nitaambiwa niombe kitu kimoja duniani nacho kitafanikiwa, basi ningeomba kuwa na wewe, basi.
    AZIZA: Hahah! Acha utani Nyemo.
    MIMI: Kwani naonekana kutania?
    AZIZA: Yeah! 
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Songa nayo sasa...


    MIMI: Huwa sifurahii pale ninapokuwa serious halafu mtu ananiona natania. Nipo serius Aziza.
    AZIZA: Sasa umenipendea nini? Hujawahi kuniona wala nini.
    MIMI: Ngoja nikwambie kitu Aziza. Mapenzi ni hisia, mapenzi hayajalishi uwe umemuona mtu au haujamuona, vyote hutokea moyoni. Unapotumia kipindi kirefu kuchati na msichana fulani, automatical moyoni unafall inlove, hicho ni kitu ambacho hutokea kwa binadamu wengi wenye moyo wa nyama kama wa Nyemo.
    AZIZA: Duuh! Hivi naomba nikuulize kitu.
    MIMI: Uliza.
    AZIZA: Unaongea mambo mengi sana mazuri Nyemo. Unaonekana kuwa una kitu cha ziada kichwani mwako.
    MIMI: Hapana, sina kitu cha ziada. Akili nilizonazo mimi ndizo ambazo hata mtu mwingine anazo, tofauti kwenye kuzitumia hizo akili tu.
    AZIZA: Unaonaaa. Kila unachoongea point. Nyemo una kitu cha ziada akilini mwako. Matumizi ya akili yako nayaona kuwa tofauti sana. Wewe genious.
    MIMI: Genious! Acha utani. Niwe vipi Genious na wakati shuleni sijawahi kuingia hata kumi bora?
    AZIZA: Sikiliza Nyemo. Kuna wale genious wa darasani. Haimaanishi ukiwa genious darasani basi hata kwenye kuongea na kuandika utakuwa genious, haiko hivyo. Kwa magenious wamegawanyika. Kuna wale wa darasani na wale wa sehemu nyingine kwenye maisha. Unaweza ukawa genious darasani lakini katika maisha ukawa mbumbumbu. Unakubaliana nami?
    MIMI: Kiasi.
    AZIZA: Hahaha! Usijali. Utanielewa tu. Turudi kwenye mada yetu.
    MIMI: Kwa hiyo hivyo ndivyo mapenzi yalivyo Aziza. 
    AZIZA: Nimekuelewa Nyemo.
    MIMI: Naomba nikuulize swali moja tu.
    AZIZA: Uliza.
    MIMI: Ushawahi kujisikia kitu chochote romantic moyoni mwako juu yangu?
    AZIZA: Swali gumu kujibika Nyemo.
    MIMI: Najua. Hata mwalimu anapoamua kutoa mtihani mgumu, kuna wengine wanafaulu japokuwa ni mgumu. Najua swali langu gumu lakini naona linaweza kujibika kirahisi sana.
    AZIZAl Swali gumu Nyemo.
    MIMI: OK! Ngoja nibadilishe swali. Unanipenda?
    AZIZA: Ninakupenda sana Nyemo. Nahisi katika marafiki zangu wote facebook. U are the best.
    MIMI: Dah! Ushatoka nje ya mada.
    AZIZA: Kivipi?
    MIMI: Hebu turudi ndani ya mada. Unanipenda?


    Swali lile likaonekana kuwa gumu kwa upande wake, nikaona ukimya ukiwa umetawala mahali hapo, nikawa naisubiria meseji yake huku nikionekana kuwa na kiu kubwa ya kutaka kusikia kitu chochote kutoka kwake, hasa jibu la swali ambalo nilikuwa nimemuuliza.
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    AZIZA: Mhh!
    MIMI: Nini tena?
    AZIZA: Una haraka sana Nyemo. Maswali yako mengine yanakufanya nikuone mtu wa haraka mno.
    MIMI: Tatizo muda Aziza. Nahofia kwamba nikichelewa, nitakuta ushachukuliwa kitu ambacho sitaki kitokee.
    AZIZA: Hahaha! What if nikisema sikupendi?
    MIMI: Nafikiria litakuwa neno baya ambalo sijawahi kulisikia katika maisha yangu.
    AZIZA: Hahaha! Nyemo una maneno sana. Hivi unayatoa wapi hayo yote?
    MIMI: Kutoka moyoni mwangu Aziza. Nimetokea kukupenda sana.
    AZIZA: Lakini bado mapema sana.
    MIMI: Najua. Najua kwamba mapema ila kumbuka kwamba vitu vingine ni lazima vifanyike mapema. Nadhani sina makosa juu ya hilo.
    AZIZA: Nikuulize swali?
    MIMI: Niulize.
    AZIZA: Una mpenzi?
    MIMI: Nadhani ningekuwa na mpenzi nisingeweza kukwambia kwamba nakupenda na kukuhitaji.
    AZIZA: Kwa nini usiweze?
    MIMI: Uaminifu. Napenda sana kuwa mwaminifu hasa kwa mtu nimpendae.....thats all.
    AZIZA: Sawa. Ila mbona haujaniuliza kama nina mpenzi au la?
    MIMI: Nadhani sitakiwi kujua kwani kwa upande mwingine nikitokea kujua, nitaumia kitu ambacho sitaki kitokee moyoni mwangu.
    AZIZA: Nakuonea huruma Nyemo.
    MIMI: Kwa nini?
    AZIZA: Unampenda mtu usiyewahi kumuona.
    MIMI: Hahaha! Hilo si tatizo Aziza. Kukuona haijalishi,. Kitu kinachojalisha ni wewe na mimi kuwa pamoja tu.
    AZIZA: Sasa kama nina mpenzi itakuwaje?
    MIMI: Sijajua itakuwaje lakini kitu ninachokihitaji ni kimoja tu, kupata nafasi moyoni mwako, kuthaminiwa na kupewa kipaumbele.
    AZIZA: Kwa hiyo mpenzi wangu nimuache kwa sababu yako?
    MIMI: Simaanishi hivyo Aziza.
    AZIZA: Hiyo ndio maana yake. Yaani nimuache mpenzi wangu.
    MIMI: Wakati mwingine inawezekana. Ngoja nikupe kijistori cha kizushi.
    AZIZA: Aya nipe.
    MIMI: Kuna mwanamke mmoja alikwenda kuchota maji siku moja, alikuwa amechoka na kuchafuka sana. Sehemu alipokuwa amechota maji kulikuwa mbali sana, kichwani alikuwa na ndoo na mkononi alikuwa na kidumu. Bahati mbaya, akajikwaa, ndoo ikadondoka na kupasuka, maji yakamwagika na kushindwa kuzoleka.
    AZIZA: Dah! Alifanya nini sasa?
    MIMI: Kurudi bombani kulikuwa mbali sana na alikuwa amechoka kupita kawaida. Kile kidumu ambacho alikuwa nacho mkononi ndicho kilichomsaidia kuoga.
    AZIZA: Stori nzuri.
    MIMI: Yeah! Ni nzuri na iliyojaa mafunzo. Umejifunza nini?
    AZIZA: Nimejifunza kwamba yatupasa kuwa na kidumu pia katika kipindi tunachokwenda kuchota maji.
    MIMI: Umekuwa mwerevu sana. Nadhani ushajua nimemaanisha nini.
    AZIZA: Hahaha! Kumbe ndio umemaanisha hivyo? Yaani nina ndoo na unataka niwe na kidumu?
    MIMI: Yeah! Ila naomba ufahamu kitu kimoja. Wakati ndoo inapovunjika, kidumu kitaweza kufanya kazi kama ndoo. Kwa hiyo ni muhimu kuwa na kidumu pia japokuwa haulazimishwa kufanya hivyo.
    AZIZA: Nyemo unanifundisha tabia mbaya.
    MIMI: Hapana. Sikufundishi tabia mbaya ila nakupa tekniki nyingine ya maisha. Njia ambazo unaweza kufanya plan B mara plan A inapoonekana kuharibika.
    AZIZA: Ok! Nimekuelewa.
    MIMI: Sasa umechukua hatua gani baada ya kunielewa?
    AZIZA: Inabidi unipe muda wa kufikiria kwanza manake duh! Kuwa na kidumu inahitaji moyo.
    MIMI: Nisikilize Aziza. Unataka kwenda kuomba ushauri wapi? Kwa mama?
    AZIZA: Hapana Nyemo, ila nahitaji kujifikiria juu ya hilo.
    MIMI: Kwani moyo wako unakwambia nini sasa hivi juu yangu?
    AZIZA: Hauniambii kitu chochote.
    MIMI: Unanidanganya Aziza. Hautakiwi kulifikiria jambo hili, unapoamua kufanya maamuzi ya maisha yako yakutakiwa kuwa peke yako Aziza.
    AZIZA: Najua. Sasa wewe unafikiri natakiwa kumuomba ushauri nani zaidi ya mama?
    MIMI: Niombe ushauri mimi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    AZIZA: Hahaha! Aya basi nishauri juu ya hili. Unaonaje, niwe na Nyemo au?
    MIMI: Hahah! Ninachokushauri ni kwamba inakupasa kuwa nae kwani kwa muonekano wake tu anaonekana kukupenda na kukuhitaji sana tofauti ya unavyofikiria Aziza. Usimuumize, mpende, kama ameamua kukupenda, kuutoa moyo wake kwa ajili yako, mfanyie the same.
    AZIZA: Hahaha! U mshauri mbaya sana.
    MIMI: Kwa nini?
    AZIZA: Unanishauri vitu vibaya. Ila ok! Naomba nikufikirie kwani sitaki kukuumiza. Nikisema nitoe jibu langu sasa hivi, utaumia na mimi sitaki uumie.
    MIMI: Sawa. Kama unaona ukitoa jibu la papo kwa papo utaniumiza, basi usifanye hivyo. Kwa hiyo lini utanijibu.
    AZIZA: Wewe unataka lini?
    MIMI: Sasa hivi....lol!!
    AZIZA: Utaumia. Naomba unipe muda. Bado tuna nafasi kubwa ya kuzidi kuwasiliana Nyemo.
    MIMI: Poa. Kama ndio hivyo hakuna noma, acha tuzidi kuwa na nafasi zaidi.
    AZIZA: Umekasirika?
    MIMI: Hapana. Sijakasirika. Kwani umeongea neno lolote la kunikasirisha?
    AZIZA: Hapana ila wanaume wengine huwa ukiwakataa wanakasirika sana na kesho wanakuwekea post.
    MIMI: Acha nao. Hawajui mapenzi, mapenzi yanahitaji subira, mapenzi yanahitaji kujitoa kwa kila kitu, hautakiwi kukata tamaa ila mapenzi pia yanahitajiiiii........
    AZIZA: Yanahitaji nini?
    MIMI: Kuyafuatilia sana kama unafuatilia kazi.
    AZIZA: Hahaha! Una maneno wewe mtoto.
    MIMI: Kawaida tu. Ila kiukweli...dah! hongera.
    AZIZA: Hongera ya nini?
    MIMI: U mzuri sana. Yaani dah! Sijui niseme nini. Kuna mengine nikisema naona kama nitaonekana muongo.
    AZIZA: Hahaha! Kivipi? Niambie tu.
    MIMI: Jana nilipokuwa nikinywa maji, nilikuona kwenye glasi, nilipokuwa najitazama kwenye kioo, nilikuona wewe. Usiku silali, nakuota wewe tu.
    AZIZA: Hahaha!
    MIMI: Maneno ya zamani hayo. Wanawake wa zamani ulikuwa ukiwaambia hivyo....fasta unamchukua. Ila nyie wa siku hizi mmejanjaruka sana.
    AZIZA: Hahaha! Kwa sasa hivi tunajua ukweli kwamba huwezi kuniona kwenye maji.
    MIMI: Ok! Tuachane na hayo. Hivi tunaweza kuonana?
    AZIZA: Kuonana. Mbona mapema sana!
    MIMI: Poa, usijali. Tutaonana tukizeeka kwa sababu ndio utakuwa muda muafaka.
    AZIZA: Hahaha! 
    MIMI: Hiyo ndio maana yake. Yaani kuonana tu unataka tupeane kalenda. Kweli makubwa.
    AZIZA: Usijali. Tutaonana soon. Ngoja nikamilishe vitu fulani hivi vya kifamilia.
    MIMI: Ok! Hakuna tatizo. Unaweza kuchukua muda gani?
    AZIZA: Si muda mrefu, kama siku mbili tatu hivi. Unatamani kuonana na mimi?
    MIMI: Yeah! Ninatamani sana Aziza.
    AZIZA: Ok! Hakuna tatizo. Utaonana na mimi kwa masharti.
    MIMI: Masharti gani?
    AZIZA: Uje nyumbani.
    MIMI: Mh!
    AZIZA: Nini tena?
    MIMI: Kwa nini usije nyumbani. Au unaogopa matope, unaogopa kuchafuka kutokana na matope ya uswahilini?
    AZIZA: Hapana. Nitakuhitaji uje nyumbani.
    MIMI: Unataka nife nini?
    AZIZA: Kwa nini?
    MIMI: Baba yako. Nadhani ataniua.
    AZIZA: Usijali. Ninapokwambia uje nyumbani, namaanisha kwamba siku hiyo itakuwa poa na hakutokuwa na tatizo.
    MIMI: Sawa. Ukiwa na nafasi naomba uniambie. Shida yangu nikuone tu.
    AZIZA: Sawa. Usijali. Tutaonana tu.


    Siku hiyo tulichati sana mpaka saa saba usiku muda ambao alitaka kulala, niliridhika na hivyo kumruhusu kwa moyo mmoja kulala. Siku zikakatika mpaka kufikia siku ambayo Aziza akataka kuonana na mimi. Nakumbuka siku hiyo ilikuwa kama ndoto kwangu, baada ya miezi miwili ya mawasiliano bila kuonana leo hii Aziza akaniambia kwamba alikuwa akitaka kuniona, nilitamani kuruka ruka kwa furaha.
    Siku ya tukio ilipofika, nikaoga na kujiweka makini, nikachukua jinzi yangu na kuivaa, nikachukua raba zangu za kawaida na kuzivaa huku kofia yangu ikiwa kichwani mwangu. Kutoka nyumbani mpaka kwao Masaki wala hakukuwa mbali, nilitegemea kuchukua daladala na hatimae kwenda nyumbani kwao. Mara baada ya kumaliza kujiandaa, nikaingia facebook na kisha kuanza kuwasiliana nae.
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    MIMI: Nipo tayari.
    AZIZA: Ok! Chukua namba yangu. Hii hapa. 0718 069 269.
    MIMI: Ok! Ndio najiandaa kwenda kituoni sasa hivi.
    AZIZA: Kwani umeshatoka nyumbani?
    MIMI: Bado.
    AZIZA: Basi usijali. Nielekeze nije kukuchukua.
    MIMI: Uje kunichukua?
    AZIZA: Yeah! Kuna ubaya?
    MIMI: Yeah! Sijawahi kufuatwa na gari toka nizaliwe.
    AZIZA: Usijali. Leo nitakuwa wa kwanza kukufuata. Umesema Tandale, napafahamu kidogo, nitakuja mpaka kwa Mtogole then unielekeze.
    MIMI: Hakuna tatizo. Nakusubiria.


    Sijui niseme nini aisee, huyu mtoto alikuwa akijiandaa kuja kunichukua nyumbani kwa ajili ya kuelekea nyumbani kwao, nilikuwa na presha sana, sikuwa nikijiamini kwamba nilikuwa mimi Nyemo. Moyo wangu ukawa na dukuduku kupita kawaida, mavazi niliyoyavaa niliyaona kutokuwa fresh hali iliyonifanya kubadilisha mara kwa mara. Sikujua Aziza alikuwa akifanana vipi, uzuri ambao aliusema Eduado, leo nilikuwa nakwenda kuuona kwa macho yangu.


    Kwa sababu aliniambia kwamba angekuja mpaka kwa Mtogole wala sikuwa na wasiwasi, nilichokifanya ni kuelekea katika sehemu ya camp yetu ambayo vijana wengi tulikuwa tukitumia kukaa na kutulia. Siku hiyo, mawazo yangu yote yalikuwa juu ya msichana Aziza ambaye alitarajiwa kufika muda si mrefu, sikutaka kumwambia mtu, nilichotaka kukifanya nilitaka kiwe sapraizi kwa kila mtu mahali pale. Ilipofika saa tisa na robo, simu yangu ikaanza kuita, nikaipokea na kisha kuipeleka sikioni.


    AZIZA: Nimekwishafika hapa kwa Mtogole.
    MIMI: Ok! Unaiona hiyo njia ya vumbi kushoto kwako?
    AZIZA: Nimetokea huku Kijitonyama Sayansi.
    MIMI: Haina noma. Vuka barabara ya lami na kisha ingia katika barabara ya vumbi, nyoosha, hapo mbele njia imegawanyika, panda na hiyo ya kushoto moja kwa moja utanikuta mtu mzima nimejaa tele na wanangu.
    AZIZA: Ok! Nakuja.


    Mapigo ya moyo yakaanza kudunda, kila nilipokuwa nikimfikiria Aziza nilikuwa nakosa amani. Nilikuwa nikijiangalia, japokuwa nilipendeza sana kama siku za sikukuu lakini kwa macho yangu nilijiona bado kabisa. Kwangu, Aziza akaonekana kuwa kama malkia fulani ambaye alikuwa akisubiriwa kwa mbwembwe zote kwangu. Macho yangu hayakutulia, yalikuwa yakiangalia ile barabara ya vumbi ambayo ilionganisha mpaka kwa Mtogole. 
    Baada ya muda, kwa mbaliiiii niliweza kuliona gari moja dogo, Verrosa nyeusi, bila shaka lilikuwa gari la Aziza ambalo alikuwa akilitumia. Ebwana sikufichi rafiki yangu, nilipigwa na butwaa, nikakosa kujiamini. Sikutaka kuwaambia washikaji juu ya Aziza kwa sababu unaweza kuwatambia halafu mwisho wa siku msichana mwenyewe akaonekana kuwa si mzuri, mtu mzima ukaona noma.
    Gari lile likaendelea kuja, lilipofika karibu na pale tulipokaa, nikasimama na kisha kulisimamisha kwa kupunga mkono. Kwanza washikaji wakaonekana kunishangaa, hawakuwa wakifahamu kitu chochote kile kilichokuwa kikiendelea mahali hapo. Nilibaki nikiwa nimesimama nje ya mlango hasa baada ya Aziza kusimamisha gari, sikuweza kumuona kwa sababu vioo vilikuwa tinted. Aliposhusha kioo...MUNGU WANGU!
    Ngoja nikwambie kitu rafiki yangu. Kati ya majini wote wanaojigeuza kuwa mademu na kuua wanaume nyakati za usiku umewahi kuwaona? Kabla sijaendelea, ngoja nikwambie kitu fulani. Mimi kama mimi nilikwishawahi kukutana na msichana ambaye alikuwa jini nyakati za usiku, tena nakumbuka ilikuwa mkoani Kilimanjaro katika kipindi ambacho kulikuwa na tetesi nyingi kuhusiana na majini ambao walikuwa wakiua watu nyakati za usiku, bila shaka ilikuwa 2006 au 2007.
    Usijiulize nilijuaje kwamba huyo mwanamke alikuwa jini. Nilikutana nae usiku katika kipindi ambacho nilikuwa nikielekea Majengo katika kipindi cha likizo, nakumbuka ilikuwa saa mbili usiku, tulifunga shule na kuja Dar es Salaam niliona ningetumia gharama kubwa. 
    Nilikutana na huyo msichana, asikwambie mtu, alikuwa demu mkali sana, ukali wa msichana yule jini sikuwahi kuuona kwa msichana yeyote yule toka nizaliwe, hata demu wangu alikuwa haingii ndani.
    Nilipopishana nae, alikuwa akinukia manukato mazuri sana, nywele zake zilikuwa ndefu, nilitamani kumsalimia, ila nilikuwa dogo, nadhani kama ningekuwa mkubwa, siku hiyo na mimi lazima ningeuliwa tu...yaani ni LAZIMA. Unamwacha vipi msichana mrembo unayepishana nae? Ukimwangalia, mwarabu si mwarabu, mzungu si mzungu na mtu mweusi si mtu mweusi. Nilipopishana nae, nilipiga kama hatua tano, nilipogeuka nyuma ili niangalie umbo lake la nyuma, kajazia vipi, sikumuona, kilichofuata...ni kutoka nduki tu huku nikipiga kelele.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Nilipokuwa nikiwangalia Aziza katika kipindi hicho nilikuwa nikimfikiria yule mwanamke jini wa kule Kilimanjaro. Aziza, aisee Aziza....Mhh! Nadhani Eduado alikuwa mchoyo, hakutoa sifa ambazo alistahili kuwa nazo Aziza, Aziza alikuwa msichana mzuri sana, msichana ambaye....dah! Sijui nizungumze vipi. 
    Hahaha! Kwanza kwa washikaji. Walipoona kwamba nimelisimamisha gari lile, wakataka kuangalia ndani kujua kuna nani, nilikuwa nimewapa mgongo, mlango ulipofunguliwa, Aziza akatoka nje...aiseeee. Si kwa watoto, watu wazima, mababu, wala mademu wengine, wote wakabaki wakimshangaa Aziza, alikuwa mkali mpaka mtu mzima nikawa najipa mapungufu. 
    Ukiachana na zile sifa za uchoyo ambazo alikuwa amezitoa Eduado juu ya Aziza, acha nikwambie jinsi alivyo, umtengeneze Aziza wako kichwani mwako na uone ni jinsi gani alikuwa mrembo.
    Kwanza demu alikuwa Mpemba, kwa hapo sitaki nizungumze sana kwa kuwa wote mnaamini kwamba wapemba wamebarikiwa kwa urembo, mtoto alionekana kuwa baba yake alikuwa mwarabu, tena wa Dubai, mama yake alikuwa Mlangi, vuta picha mtu mzima. Mtoto alikuwa na nywele nyingi sana, hapo ndipo nilipogundua mapungufu ya sifa za Eduado. Mtoto hakuwa na nywele zilizoishia kwenye mabega, mtoto minywele ilikuwa hiyooo mpaka mgongoni huku zikiwa zinang’aa sana. Uso wake ulikuwa mwembamba ambao ulikuwa ukizungukwa na tabasamu pana ambalo lilikuwa likiyafanya meno yake meupeeee kuonekana. Ukiachana na hayo, huyu mtoto alikuwa na kidoti aisee, tena kile kidoto kilichokuwa karibu na pua, kilimfanya kupendeza sana.
    Ukiachana na uso wake auliomfanya kuonekana kama malaika, umbo lake lilikuwa zuri sana. Huwa wapemba ni kama waarabu au wachina, hawana makalio hayoooo tofauti na wanawake wetu weusi, yeye alikuwa mwembamba wa wastani, kifua chake kilikuwa kimesimama. Kwa sababu alikuwa amevaa sketi fupi kiasi, miguu yake haikuwa miguu ya bia, ilikuwa miguu ya watani kidogo. Kila nilipokuwa nikimwangalia, mtoto hakuwa na kovu lolote lile, yaani alionekana kama katengenezwa kupitia Adobe Photoshop na kisha kuja kwangu.


    AZIZA: Wao Nyemoooooo.


    Aliniambia kwa furaha na kisha kunikumbatia. Watu wote ambao walikuwa wakimwangalia Aziza wakaanza kutushangaa, Aziza alionekana kama mzungu, nilionekana kuokota embe katika mti wa mlimao au kujenga nyumba kubwa angani. Aziza alikuwa akinukia vizuri sana, harufu ya manukato yake ikanifanya nifall inlove zaidi na zaidi. Nilitamani kumbeba juu juu. Mademu wa pale mtaani ambao walikuwa wakiniringia sanaaaaaa, katika kipindi hiki walionekana kushikwa na wivu huku mioyo yao ikiukubali uzuri wa Aziza.


    MIMI: Mzima wewe cheupe?
    AZIZA: Mimi mzima.
    MIMI: kweli nilipatia, sikutoka nje hata mara moja.
    AZIZA: Ulipatia nini?
    MIMI: Wanawake mnaoweka picha za midoli na maua huwa mnakuwa wakali sana. 
    AZIZA: Kwani mimi mzuri?
    MIMI: Nilikuwa najiuliza kwamba hivi umezaliwa hapa duniani au umeshushwa kutoka hukooooo.
    AZIZA: Hahaha! Acha hizo Nyemo.
    MIMI: Mtoto unaonekana kuwa mrembo sana, mtoto una mvuto wa ajabu, mtoto unaonekana zaidi ya malkia Cleopatra aiseee...dah! Ulivyonikazia kuwa na mimi sawasawa tu manake ungenisababishia kifo.
    AZIZA: Kivipi?
    MIMI: Mmh! Hapa kifo nje nje aiseee. Tena bora ulivyokuwa na gari manake ungekuwa unatembea kwa miguu, utawafanya hata wale wanaokwenda msikitini kuswali wakatishe safari zao, utawafanya mpaka wale wanaokwenda kanisani kusali wakatishe safari zao kwa muda wakuangalie wewe. Kama vitabu vya dini vinavyosema kwamba ukimwangalia mwanamke na kumtani utakuwa umeshazini nae, haki ya Mungu nina uhakika wewe umeshazini na watu wengi maishani mwako. Umeshazini na mimi, umezini na wale marafiki zangu, umezini na wale mababu waliokaa pale chini wakicheza bao, mbaya zaidi, umezini mpaka na wasichana wenzako....hahahaha! Wamekusaga.
    AZIZA: Yaani yote hiyo kwa sababu wamenitamani?
    MIMI: Ndio. Hebu jiangalie, hivi unaweza kujilinganisha na nani? Hata Beyonce haingiii, labda Alicia Keys ndiye anaweza kuifikia nusu yako.
    AZIZA: Hahaha! Nyemo una maneno matamu. Hebu nisubiri kidogo niende hapo dukani.
    AZIZA: Unakwenda kununua nini? Hakuna pizza wala baga hapo.
    AZIZA: Hahaha! Hebu acha utani.


    Huyu Aziza. Aisee bora alivyoweka picha ya mdoli katika akaunti yake ya facebook manake kama angeweka picha yake basi ingekuwa balaa. Mwendo wake ulikuwa ni wa mapozi kupita kawaida, alionekana kutembea kwa tahadhali ardhini. Nilichokifanya nikayapeleka macho yangu kwa washikaji waliokuwa pale kijiweni, nilijua tu kwamba walikuwa na dukuduku mioyoni mwao.
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    JAFARI: Kaka heshima. Kaka heshima yako...kuanzia leo...hauna mpinzani hapa mtaani aiseeee...duh!
    MIMI: Hahaha! Mtoto umemuonaje.
    JAFARI: Kwanza huyu mtoto umemtoa wapi?
    MIMI: Facebook.
    JAFARI: Duh! Kaka naomba na mimi uniunganishe manake dah!
    MIMI: Kaka mambo hayapo rahisi kama unavyofikiri. Mpaka nimempata huyu mtoto, nimepitia kwenye mabonde, mito majabari mpaka wewe kumuona hapa. Usifikiri ukijiunga leo kesho unampata, unaweza ukawa babu hujaambulia chochote.
    ALLY: Kwani huyu ni wa facebook?
    MIMI: Yeah! Tena yupo mpaka Twitter...yupo kotekote.
    HUSSENI: Ila huyu demu sio mgeni machoni mwangu, nadhani nilishawahi kumuona sehemu.
    MIMI: Acha uongo. Wapi?
    ALLY: Daah! Nshajichanganya. Kumbe kichwani mwangu ilikuwa inakuja picha ya Kajool, yule demu muigizaji wa Kihindi.
    MIMI: Hahaha! 
    JAFARI: Ila Nyemo. Daah! Unapokuwa na mtoto kama huyu, hivi kweli unaweza kutembea nje ya ndoa?
    MIMI: Kaka, sisi wanaume hatufai, hata upewe demu mzuri kama malaika, kesho unalala na rafiki yake...hahaha!


    AZIZA: Nyemo.
    MIMI: Niambie (Huku nikimfuata)
    AZIZA: Tuondoke.
    MIMI: Bila ya kukanyaga nyumbani? Hebu acha zako, twende home.
    AZIZA: Nyemo...nataka tuwahi nyumbani.
    MIMI: Hata kama. Twende mara moja tu.


    Lengo kubwa la kumtaka Aziza twende nyumbani lilikuwa moja tu, kutaka kuwaonyeshea wale wasichana ambao walikuwa wakileta mapozi kwamba huyu msichana alikuja kwa ajili yangu kwani kama nisingefanya hivyo, wangejua kwamba alikuwa mpita njia ambaye alikuwa amesimama kutaka kuulizia kitu fulani. Kwa sababu alikuwa amelipaki gari pembeni, nikawaambia washikaji waliangalie na mimi kuanza kuondoka na Aziza kwenda nyumbani.
    Watu walikuwa wakinitolea macho, wengine walikuwa wakiniangalia kisiri na kunipigia saluti, Aziza alionekana kukimbiza kupita kawaida, urembo wake ulikuwa ni mkubwa kiasi ambacho hakukuwa na mtu aliyefikiria kama ningeweza kuja na msichana mzuri kiasi kile.


    AZIZA: Mazingira ya huku nimeyapenda.
    MIMI: Umeyapendea nini?
    AZIZA: Yametulia sana. Halafu kumechangamka.
    MIMI: Hahaha! Nyie si mmezoea mazingira ya kwenu yapo kimya utafikiri jangwani.
    AZIZA: Yeah! Unajua kule sijui kupo vipi, huwa kunaboa kweli.


    Katika kipindi chote ambacho tulikuwa tukiongea huku tukielekea nyumbani, kichwa changu kilikuwa kikimfikiria baba. Nilijua kabisa kwamba katika kipindi hicho alikuwa nyumbani, kichwa changu kilikuwa kikifikiria uongo ambao nilitakiwa kumpa, uongo ambao ungeendana na ukweli. Nilipofikiria kwa kipindi fulani, nikapata jibu, nikapata kile nilichotakiwa kumwambia baba. 
    Kweli tukafika home, majirani wote wakawa wananiangalia kwa macho ya kunishangaa, Aziza kwao alionekana kuwa tofauti sana, uzuri ambao alikuwa nao ulionekana kuwa wa kipekee sana. Nikaufungua mlango, tulipoingia ndani tu, kizaazaa, baba alikuwa kwenye kochi akiangalia televisheni.


    Nikamkaribisha Aziza, akamsalimia baba na kutulia kochini. Nikamwangalia baba huku lengo langu likiwa ni kutaka kumsoma, hiyo ndio ilikuwa tabia ya nyumbani, muda mwingi watu huwa tunasomana kabla ya kuongea kitu chochote kile. Baba akaonekana kufahamu nilichokuwa nikikifikiria. Akaniwahi.


    BABA: Unaonekana unataka kuniambia jambo, halafu hilo jambo la uongo, hebu niambie sasa nikusikilize.
    MIMI: Hahaha! Tatizo mzee Chilo una presha sana. Wewe subiri kwanza, mbona unakuwa na wasiwasi?
    BABA: Huo mtazamo wako unaoutumia kunitazama. Ok! Karibu mgeni. Sijui unatumia kinywaji gani?
    AZIZA: Hapana. Nimeshiba.
    BABA: Kwani ukinywa kinywaji chochote utavimbiwa?
    AZIZ: Hapana. Nimekwishakunywa.
    BABA: Nyemo, ni kweli anayoyasema?
    MIMI: Hapana. Hapo kakupiga fix.
    AZIZA: Hahaha!
    BABA: Jisikie huru. Uletewe kinywaji gani?
    AZIZA: Maji tu yanatosha.
    MIMI: Ok! Ila kuna maji ya chumvi...utakunywa?
    AZIZA: Mmmh! Maji ya chumvi?
    MIMI: Sasa unashangaa nini? Au haujui kama Dar es Salaam kuna bahari ya Indi?
    AZIZA: Niletee hata hayo nitakunywa tu.
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Mtu mzima nikanyanyuka, kumbuka hapo bado sikuanza kumtambulisha Aziza kwa mzee kwamba alikuwa nani na alifuata nini nyumbani. Juu ya hilo, sikuwa na wasiwasi sana kwani kwa umri ambao nilikuwa nimefikia, mzee hakuwa muongeaji sana zaidi ya kunitaka kuwa makini kila siku kwa kila nikifanyacho. Nilipochukua maji, nimaletea, tena kwa makusudi, nikamletea kwenye kikombe cha plastiki, nilichokuwa nikikihitaji ni kumuonyeshea maisha fulani ya tofauti sana, maisha ambayo alikuwa akiyaamini kichwani mwake kwamba yalikuwa yakiishiwa na watu waliokuwa wakikaa Tandale uswahilini.


    MIMI: Baba huyu ni rafiki yangu anaitwa Judith. Nilisomanae Faraja Seminari ila nilimuacha darasa moja. Kwa sasa yupo hapo I.F.M anasomea sheria.
    BABA: Asante kwa kumfahamu. Karibu Judith na jisikie huru.
    AZIZA: Asante.
    MIMI: Aziza, huyu ndio mzee Chilongani au mzee Chilo. Huyu ndiye ambaye nimemuibia hiki kipaji cha kuandika andika.
    AZIZA: Nashukuru kumfahamu.


    Kwa sababu tulikuwa na safari, hatukutaka kukaa sana mahali hapo, tukasimama na kisha kuaga na kuondoka. Njiani, Aziza alionekana kushangaa sana, hakuamini kama nilikuwa na uhuru mkubwa wa kuongea na mzazi kwa kiasi kile.


    AZIZA: Mbona baba yako unaongea nae namna ile?
    MIMI: Kivipi?
    AZIZA: Ulivyokuwa ukiongea. Yaani kama unaongea na vijana wenzako.
    MIMI: Nisikilize Aziza, mzazi ni rafiki, hautakiwi kumuogopa sana mzazi mpaka kukosa uhuru, wazazi wetu hawakutulea katika mazingira hayo, walitulea katika mazingira ya kirafiki zaidi, mazingira ambayo yametufanya kuwa huru kwao.
    AZIZA: Basi hongereni. Mzee wangu ukae chini na kuongea nae namna ile, mh! Mtu hujiamini. Kwanza akirudi tu, amani nakosa, muda wote utasikia Azizaaaa.
    MIMI: Hahaha! Ila hao wazee ndio fresh. Mzee unakuwa bandidu kama hivyo, hakuna utani, hakuna masihala...hahaha! 
    AZIZA: Kuna uzuri gani? Baba akirudi unajificha chooni. Ngoja nikuulize swali.
    MIMI: Uliza.
    AZIZA: Kwa nini umemdanganya jina langu na kila kitu kuhusu mimi?
    MIMI: Pale ningemwambia unaitwa Aziza, angeshtukia mchezo.
    AZIZA: Kivipi?
    MIMI: Unajua nimesoma seminari, sasa niliposema kwamba nimesoma na wewe, kidogo angetilia mashaka. Nilichokifanya ni kucheza na akili yake kabla ya yeye kucheza na akili yangu, nikamuwahi. Hahaha!
    AZIZA: Nyemo una visa sana.


    Tuliendelea kwenda mtaa wa juu, tulipofika, watu wengine bado walikuwa wakishangaa, wala sikutaka kuwa na wasiwasi, kama kuuza tayari nilikuwa nimeuza sana, nilichokifanya ni kushukuru kwa niaba yake kwa washikaji waliokuwa wakililinda gari na kisha kuingia garini.


    AZIZA: Sasa hapa safari ni kwenda nyumbani. Unatakiwa kuwa huru, baba yangu ni mkali sana ila kwa sasa hayupo. Jiamini, usiwe na wasiwasi. Umenisikia.
    MIMI: Ooopsss...nimekuelewa. Sasa kama akirudi ghafla?
    AZIZA: Usiwe na wasiwasi. Kila kitu kipo under control.
    MIMI: Mmmh! Aya byana japokuwa huwa ninahofia sana kwenda nyumbani kwa mwanamke.
    AZIZA: Hahaha! Kwa nini unaogopa?
    MIMI: Unaweza kugeuzwa mwanamke....hahaha
    AZIZA: Usijali Nyemo. Hakuna mtu anayeishi nyumbani ambaye ametokea Mombasa. Kuwa na amani.
    MIMI: Aya (Nilisema na Aziza kuwasha gari na kuondoka mahali hapo huku nikiwa nimezoa maksi nyingi sana kwa kila aliyeniona na Aziza).
    Ila pamoja na hayo yote yaliyokuwa yakiendelea, nadhani sikutakiwa kwenda kwa kina Aziza. Mungu ametufumba macho kutojua mambo yanayotokea mbele yetu, kama angetupa uwezo, nadhani nisinge kwenda kwa kina Aziza kwani hali ilikuwa ni balaa tofauti na uhakika ambao alikuwa amenipa.....chezea wazee wa kiarabu kwa mabinti zao


    MIMI: Mmmh! Mapigo ya moyo mbona yananidunda hivi?
    AZIZA: Hahaha! Uoga wako tu. Au una BP?
    MIMI: Hapana. Yaani kama kuna jambo baya linakwenda kunitokea.
    AZIZA: Jambo gani na wakati nimekwishakwambia kwamba baba hayupo, nipo peke yangu.
    MIMI: Na mama je?
    AZIZA: Nae hayupo. Yaani kurudi kwao mpaka saa mbili usiku.
    MIMI: Hapo mwake mwake.
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Kiukweli nilikuwa na wasiwasi sana ila Aziza alijitahidi sana kuniondoa wasiwasi. Ngoja nikwambie kitu kimoja, mimi hakuna wazee ambao ninawaogopa kwa mabinti zao kama wazee wa Kiarabu. Huwa hawataki utani kabisa, huwa hawataki ulete masihala kwa mabinti zao hata mara moja. Kukutoa roho kwa sababu umemfuata binti yake wala haoni tatizo hata mara moja.
    Kwa Aziza, akajitahidi sana kuniondoa wasiwasi lakini sikufichi rafiki yangu, hofu bado ilikuwa ikiendelea moyoni mwangu. Nikaona haina noma, mzee wa Kiarabu angenitishaje mimi mtoto wa Tandale na wakati kama fujo nimekwishazizoea? Mzee wa Kiarabu angenitishaje mimi na wakati kama ugomvi Tandale mambo hayo hutokea sana? Nilikuwa nikijipa moyo ila nilipofikiria kwamba wazee wa Kiarabu walikuwa wakitumia hata bunduki kukudedisha, nikaona mweeeee...kazi ipo.
    AZIZA: Tumekwishafika nyumbani. Karibu.
    MIMI: Asante.


    Mlinzi akafungua geti na kisha Aziza kuliingiza gari ndani. Nikabaki nikishangaa tu, sikuamini kama hapa Tanzania kulikuwa na watu ambao walikuwa wakiishi katika majumba makubwa kama ule mjengo aisee. Kulikuwa na bonge la bwawa la kuogelea, bustani kubwa ya maua pamoja na sehemu ya kuegesha magari. Mazingira ya nyumba yakanivutia sana, tukateremka na kisha kuanza kuangalia huku na kule, nilitaka kuyazoea mazingira japokuwa ilikuwa ni mara ya kwanza kwangu.
    AZIZA: Mbona unaangalia hivyo.
    MIMI: Lazima niyazoee mazingira, naangalia vichochoro vya kufanyia uninja wangu mara mzee wako atakapotokea ghafla.
    AZIZA: Acha hizo bwana. Mzee harudi sasa hivi, mpaka saa mbili usiku.
    MIMI: Basi hakuna noma. Kuna nani mwingine ndani ya nyumba?
    AZIZA: Mfanyakazi wa ndani. Wadogo zangu wote wapo shule nchini Kenya.
    MIMI: Hakuna noma.


    Tukaingia ndani na kisha kutulia. Macho yangu hayakutulia sehemu moja, yalikuwa yakiangalia huku na kule kama mtu ambaye nilikuwa natafuta jambo fulani. Sebule ilikuwa nzuri, ilivutia na kupendesha macho ya kila aliyekuwa akiiangalia. Nikakaribishwa katika mkochi mmoja mkubwaaaa, ile kukaa tu, nikayahisi makalio yakiingia ndani kabisa na kuzama kochini.




    AZIZA: Hapa ndipo nyumbani. Karibu
    MIMI: Asante
    AZIZA: Nikuletee nini?
    MIMI: Kwani kuna nini na nini?
    AZIZA: Kuna juisi, soda, maziwa na maji.
    MIMI: Kwa sababu nyumbani ni ngumu sana kunywa maziwa, hebu niletee maziwa.
    AZIZA: Hahaha! Aya. Kuna kingine unachokitaka?
    MIMI: Kama kuna vitafunio itakuwa full mzuka.
    AZIZA: Unataka vitafunio gani?
    MIMI:Kwani kuna nini na nini?
    AZIZA: Kuna keki, mandazi, baga, pizza, chapati
    MIMI: Duh! Utafikiri nimeingia hotelini. Fanya hivi. Kwa sababu sijawahi kula baga zaidi ya kuisikia kwa watu, hebu niletee hiyo na kwa sababu nasikia sikia watu wakitamba facebook sijui pizza tamu, nami niletee kwanza. 
    AZIZA: Utamaliza vyote Nyemo?
    MIMI: Kwani vikibaki si nitabeba! Au hairuhusiwi kubeba?
    AZIZA: Inaruhusiwa.
    MIMI: Basi niletee.


    Usinishangae aiseee, hivi ndivyo nilivyo na nilikwishazoea kuishi maisha ya namna hiyo. Tandale hakukuwa na sehemu inayouza baga wala pizza, kwa hiyo kwa nini nisiagize baga na pizza nami nitoe ushamba mdomoni mwangu? Nikaletewa vitu nilivyovitaka, aiseee, kwanza nikajifanya kutokujua baga ipi pizza ipi, ikanibidi niulize.
    MIMI: Pizza ipi na baga ipi?
    AZIZA: Pizza hiyo ya duara na baga ni huo mkate wenye vitu mbalimbali.
    MIMI: Mweee...kazi ipo. Nahisi leo nitaumwa sana tumbo.
    AZIZA: Kwa nini?
    MIMI: Tumbo langu halijazoea kula vitu hivi Aziza.
    AZIZA: Usiogope, vitu vya kawaida tu.
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Nikaanza kula buana, vilikuwa vitamu sana, tofauti na Aziza alivyofikiria kwamba ningebakisha, haikuwa hivyo, nikala vyote na kushushia na maziwa. Muda wote Aziza alikuwa akiniangalia, sijui alinionaje, sikutaka kujali, nilichokijali ni kupiga msosi tu.
    Hayo ndio yalikuwa matukio ambayo niliyafanya mahali hapo, bado nilikuwa nikitaka kumuonyeshea Aziza kwamba mimi nilikuwa mtoto wa uswahili. Najua wale masharobaro wangeomba maji na pia kama wangeambiwa kuhusu chakula wangesema wameshiba, ila kwangu mimi mtu nisiyekuwa sharobaro, hahaha! Nikaagiza vitu ambavyo vilikuwa adimu kupatikana Tandale.
    Nilichokuwa nikikifanya ni kucheza na akili ya Aziza tu, unajua unapoona umekuwa na msichana wa matawi ya juu halafu wewe unatoka uswahilini, usijifanye matawi sana na wakati kwenu ni wababaishaji tu. Nilitaka kumtia kipofu Aziza, nikajifanya sijawahi kula pizza na wakati mara nyingi nilikuwa nakwenda kuzinunua Magomeni karibu na msikiti wa Kichangani. Nikajifanya kwamba hata baga sijawahi kula na wakati nilikuwa nikipenda kuzinunua pale Kijitonyama katika sheli ya mafuta karibu kabisa na jengo la TTCL. Aziza akaniona kwamba kweli nilikuwa mtoto wa uswahilini


    MIMI: Nashukuru kwa chakula chako na kinywaji chako. Nadhani sasa ni wakati.
    AZIZA: Asante kwa shukuru. Wakati gani?
    MIMI: Wa kuniambia kile ambacho kila siku nilikuwa nikikihitaji sana kwako.
    AZIZA: Kipi?
    MIMI: Kuwa msichana wangu wa dhati.
    AZIZA: hahaha! Hausahau?
    MIMI: Nitasahau vipi na wakati ninakupenda. Then ukiona nakumbuka basi jua kwamba wewe ni mtu muhimu sana kwangu. Kama usingekuwa muhimu, nisingekumbuka.
    AZIZA: Hahaha! Nisikilize Nyemo, najua kwamba unanipenda ila...
    MIMI: Ila nini tena?
    AZIZA: Nahofia.
    MIMI: Unahofia nini?
    AZIZA: Kuwa na wewe. Naweza kufa kwa presha.
    MIMI: Haha! Hakuna kitu kama hicho. Nahitaji kuwa na wewe tu. Hebu fikiria muda wote ambao nimeupoteza kwa ajili yako Aziza, umekuwa rafiki yangu mkubwa, rafiki ambaye sikutaka kumpoteza katika maisha yangu yote.
    AZIZA: Najua. Tuendelee kuwa marafiki.
    MIMI: Nisikilize Aziza. Kila kitu kinakwenda na nyakati pamoja na mabadiliko. Najua kabisa kwamba kabla ya baba yako kumuoa mama yako walikuwa marafiki, si ndio?
    AZIZA: Ndio.
    MIMI: Baadae wakabadilika na kuwa wapenzi, si ndio?
    AZIZA: Ndio.
    MIMIl Na mwisho kabisa wakawa mke na mume. Nimekosea?
    AZIZA: Haujakosea.
    MIMI: Yeah! Hayo ndio maisha yalivyo. Tumekuwa marafiki kwa kipindi kirefu, inatupasa tubadilishe kila kitu kwa wakati huu, kutoka kwenye urafiki mpaka kuwa wapenzi, tukitoka hapo, itatupasa tubadilike pia, tuje kuwa wachumba na hatimae mke na mume.
    AZIZA: Mmmh! Nyemo una malego ya mbali.
    MIMI: Yeah! Hayo ndio maisha yanavyotakiwa kuwa. Hatutakiwi kila siku tufikirie kuhusu hapa tulipo, yatupasa tufikirie kule tutakapokuwa kesho. Ukiona mtu anafikiria zaidi hapa, kidogo atakuwa na matatizo fulani kichwani.
    AZIZA: Naomba nikuulize swali. Unanipenda?
    MIMI: Nadhani macho yangu yanaelezea kila kitu. Siku zote mapenzi ya msichana huonekana katika tabasamu lake ila mapenzi ya mvulana huonekana machoni mwake. Unaona nini machoni mwangu?
    AZIZA: Mapenzi.
    MIMI: Yeah! Hicho ndicho kitu kilichomo moyoni mwako juu yako. Nakupenda sana.
    AZIZA: Najua.
    MIMI: Naomba kitu kimoja Aziza.
    AZIZA: Kitu gani?
    MIMI: Lipsi zako.
    AZIZA: Zimefanyaje?
    MIMI: Nataka kuona ni jinsi gani zilivyo laini.
    MIMI: Unamaanisha nini?
    MIMI: Haujajua namaanisha nini? Subiri.
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Nikainuka pale nilipokuwa na kisha kumsogelea. Lengo langu kubwa mahali hapo lilikuwa ni moja tu, kubadilishana mate na kisha nione lipsi zake zilikuwa laini kiasi gani. Hakuonekana kuwa mchoyo, akanipokea, huku lipsi zetu zikiwa zinatamaniana tu, ghaflaaaaa..............................tukasikia honi ya gari getini. Kwa haraka sana Aziza akainuka na kisha kuchungulia dirishani, geti lilipofunguliwa, alikuwa baba yake.
    AZIZA: Mungu wangu! Baba!
    MIMI: Unasemaje?
    AZIZA: Baba. Baba amerudi.
    MIMI: Amerudi (Nikainuka na kwenda kuchungulia dirishani, gari la baba yake lilikuwa linaingia)
    AZIZA: Mungu wangu! Sijui nifanye nini.
    MIMI: Wewe si ulisema baba yako anarudi saa mbili?
    AZIZA: Ndio. Sijui leo imekuwaje.
    MIMI: Mmmh! Hiki kifo (Nilijisemea moyoni huku nikitetemeka na haja ndogo ikitaka kunitoka)


    Aziza alionekana kama kupigwa ganzi, hakujua ni kitu gani ambacho alitakiwa kukifanya kwa wakati huo, nilimuona akianza kutetemeka huku kwa mbali kijasho chembamba kikianza kumtoka. Hakuonekana kuamini kile ambacho alikuwa akikiona mahali pale.


    MIMI: kwa hiyo?
    AZIZA: Sijui nifanye nini.
    MIMI: Chumba chako kipo wapi?
    AZIZA: Njoo.


    Nikaanza kumfuata kule aliponiambia nimfuate, chumbani. Nilijua fika kwamba katika kipindi hicho akili yake haikuwa sawa, mimi kama ninja nikatakiwa kufanya manuva. Tukaenda mpaka chumbani kwake, alikuwa akiendelea kutetemeka tu. Baada ya kufika chumbani, mtu mzima nikabaki nikikiangalia chumba kile, kilionekana kuwa na mvuto sana.


    AZIZA: Kwa hiyo.
    MIMI: Daah! Ngoja nizame chini ya kitanda (Mtu mzima nikazama chini ya kitanda)


    Huko chini kulionekana kusafi ajabu, kitanda kile kikubwa cha chuma kilikuwa na nafasi ya kutosha kabisa. Kitu cha kwanza nilichokifanya ni kuichukua simu yangu na kisha kuiweka katika Silent. Nilibaki nikijiuliza sana kwamba kwa nini jambo kama lile lilikuwa likinitokea? Kwa nini Aziza alikuwa ameniaminisha sana mimi kwenda kwao mpaka kutaka kuniletea msala? Kila nilichojiuliza nikakosa jibu. Kule chini ya kitanda nikaanza kuchati na Eduado kupitia sms za kawaida.


    EDUADO: Nyemo umefikia wapi?
    MIMI: Kaka acha. Nipo kwao.
    EDUADO: Du! Upo kwao? Wewe noma. Ilikuwaje kuwaje hadi umefika kwao?
    MIMI: Alikuja kunichukua home.
    EDUADO: Sikupatii picha mtu mzima. Leo malovee hapo hapo chumbani kwake.
    MIMI: Haha! Kaka acha. Nipo uvunguni.
    EDUADO: Uvunguni! Kivipi tena?
    MIMI: Baba yake amefika na wakati dogo alisema kwamba anarudi saa mbili usiku. Karudi kwa kushtukiza, yaani hapa nimeingia chumbani kwake na kujificha uvunguni.
    EDUADO: Hahaha! Kaka hiyo kweli noma, sikupatii picha aisee ulivyojipinda huko mtu mzima.
    MIMI: Kaka wewe acha tu, huku ni noma. Ukisikia nimepigwa risasi, usishangae.
    EDUADO: Dah! Ngoja nikuombee Mungu akuokoe.
    MIMI: Wewe unafikiri Mungu atanisaidia hapa? 
    EDUADO: Atakusaidia tu.
    MIMI: Kunisaidia anaweza ila dah! Kaka mimi ni mwenye dhambi. Nafikiri atataka nikamatwe ili nisirudie mchezo wangu.
    EDUADO: Kaka pole sana. Sasa mtoto anasemaje?
    MIMI: Yaani hapa ni kujiokoa mwenyewe. Aziza anazingua, anaonekana kuogopa sana.
    EDUADO: Kwa hiyo utatokaje humo uvunguni?
    MIMI: Ngoja kwanza giza liingie manake huku mtu unaweza kufa.


    Mtu mzima nilikuwa nazidi kutetemeka chini ya uvungu wa kitanda, Aziza hakuwa akitulia, mara aingie, mara atokea hali ambayo ikanionyeshea angetoa boko muda wowote ule. Nilichokifanya nikachukua simu yangu na kisha kuanza kumtumia meseji.
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    MIMI: Nini kinaendelea hapo?
    AZIZA: Baba amekaa sebuleni, amekuja na wageni. Tena wageni ambao watalala hapa hapa nyumbani.
    MIMI: Hilo sio tatizo sana. Wa kike au wa kiume?
    AZIZA: Wa kike.
    MIMI: Duuh! Ila si watalala chumba cha wageni?
    AZIZA: Yeah! Ila wengine watalala katika chumba changu. Mbaya zaidi baba ameniambia nije kusogeza kitanda ili kiingizwe kitanda cha pili.
    MIMI: Duuuh! Leo kazi ipo.
    AZIZA: Mbaya zaidi amemwambia mdogo wangu aje kufagia chumbani.
    MIMI: Mungu wangu! Nimekwisha.
    AZIZA: Naomba uniambie nifanye nini Nyemo.
    MIMI: Kwanza kabla ya yote punguza presha. 
    AZIZA: Sawa.
    MIMI: Najua kwamba leo nakwenda kukamatwa, kabla sijakamatwa naomba uniambie kitu kimoja.
    AZIZA: Kitu gani?
    MIMI: Unanipenda?
    AZIZA: Nakupenda Nyemo.
    MIMI: Upo tayari tuingie katika mahusiano kwa muda mchache uliobakia kabla sijauawa na baba yako?
    AZIZA: Nyemo usiseme hivyo.
    MIMI: Wewe unafikiri nitasemaje? Naomba unijibu. Upo tayari?
    AZIZA: Nipo tayari lakini jua hautokwenda kuuawa.
    MIMI: Nimefanya kila kitu kwa ajili yako, nilihisi mambo haya yatatokea tu toka tulipokuwa tukija. Ila usijali. Ngoja nikuonyeshe jinsi mchezo unavyofanyika Aziza. Nataka nikuonyeshe kwamba huwa sikamatwi kijinga jinga.
    AZIZA: Utafanya nini sasa?
    MIMI: Cha kwanza hakikisha mdogo wako haji kusafisha chumba, akifika chumbani mpokonye fagio, ng’ang’ania kusafisha chumba chako.
    AZIZA: Sawa. Cha pili?
    MIMI: Hakikisha kila unapotoka chumbani, unafunga mlango kwa ufunguo, cha tatu, uache mlango wa jikoni wazi, cha nne mpe taarifa baba yako kwamba kuna mtu alikuja kumuulizia.
    AZIZA: Mmmh! Huyo mtu nani?
    MIMI: Nyemo...ila leo niite jina la Ahmed.
    AZIZA: Akisema yupo vipi?
    MIMI: Mwambie kama jinsi nilivyo. Usitie shaka.
    AZIZA: Kingine nisemeje?
    MIMI: Mwambie kwamba ningekuja baadae kumuulizia tena.
    AZIZA: Mhh!
    MIMI: Usijali. Kila kitu kipo under control.
    AZIZA: Sawa. 


    Baada ya dakika kadhaa, nikasikia mlango ukifunguliwa, nikasikia vishindo vikija kwa kasi, alikuwa mdogo wake ambaye alitaka kusafisha chumba kwa kukifagia, Aziza akafika na kisha kumpokonya ufagio kwa kutaka kufagia yeye mwenyewe. Mdogo wake alipoondoka, akakiinamisha kichwa na kisha kukutana nami.


    *
    MIMI: Vipi huko?
    AZIZA: Bado hali ni ngumu.
    MIMI: Daah! Sikamatwi kijinga hapa. Fanya kama nilivyokwambia, umesikia?
    AZIZA: Sawa.
    MIMI: Nakupenda mpenzi.
    AZIZA: Nakupenda pia (Tukafanya kile tulichotaka kukifanya pale sebuleni....lol)


    Aziza akaondoka, nikaona sio ishu, niliendelea kukaa uvunguni mule. Nazo dakika zilikuwa zikisogea tu, zilisogea zaidi na zaidi, mpaka saa moja usiku inaingia, mtu mzima nilikuwa mule mule ndani chini ya uvungu. Saa mbili kasoro nikaona ungekuwa ujinga, nikamtumia Aziza meseji.


    MIMI: Njoo uvunguni kwanza.
    AZIZA: Sawa.
    MIMI: Ila kabla ya kuja, cheki kuna nani jikoni.
    AZIZA: Yupo mama.
    MIMI: Vizuri sana
    AZIZA: Vizuri?
    MIMI: Yeah! Njoo kwanza huku uvunguni.
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Baada ya muda, Aziza akafika, hakuonekana kuwa na amani.


    AZIZA: Unasemaje baby?
    MIMI: Hapa naondoka na kuelekea jikoni, cha msingi kamtoe mama yako jikoni.
    AZIZA: Mmmh! Nitamtoa vipi?
    MIMI: Kamwambie kwamba baba yako anamuita.
    AZIZA: Eeeh!
    MIMI: Fanya hivyo. Una dakika moja ya kufanya hivyo. Nakwenda kwa muda.
    AZIZA: Hlafu?
    MIMI: Wewe kamwambie hivyo. Akija sebuleni mimi utanikuta nje ambapo huko sebuleni utamwambia baba yako kwamba kulikuwa na mtu alikuja kumuulizia. Umesikia
    AZIZA: Na mama akifika sebuleni na kusema kwamba kaitwa kumbe hajaitwa?
    MIMI: Mwambie uliskia vibaya.
    AZIZA: Sawa.
    MIMI: Kenye ile dakika moja, umebakisha sekunde arobaini. Nenda, ukitoka zima taa ya humu chumbani na uuache mlango wazi kidogo
    AZIZA: Sawa.


    Aziza akaondoka mahali hapo, na kweli akaelekea jikoni na kumwambia mama yake kwamba alikuwa akiitwa na baba yake, nilipomuona mama yake akipita ukumbini kueleka sebuleni, alipopita, nikaufungua mlango na kupita kuelekea jikoni, nikaufungua mlango na kutoka nje kwa nyuma, nikaanza kuambaa ambaa mpaka pembeni ya gari lao.


    MAMA AZIZA: Nimekuja mume wangu.
    BABA AZIZA: Kuna nini?
    MAMA AZIZA: Aziza amekuja na kuniambia unaniita.
    BABA AZIZA: Mimi! Hapana, labda kasikia vibaya.
    AZIZA: Si nimesikia unamuita mama.
    BABA AZIZA: Hapana.
    AZIZA: Basi samahani nilisikia vibaya
    MAMA AZIZA: Usijali. Nipo jikoni naandaa chakula kwa sababu dada wa kazi anaumwa, amelala na huyu Aziza asije akatoa chakula kibichi
    BABA AZIZA: Sawa. Aziza, wapeleke chumbani wageni hawa.
    AZIZA: Sawa. Ila leo kuna mtu alikuja kukuulizia.
    BABA AZIZA: Nani?
    AZIZA: Sijui, ila alisema atarudi usiku.
    BABA AZIZA: Yupo vipi?
    AZIZA: Mrefu kidogo, maji ya kunde halafu ana.........!


    MLANGO: Ngo ngo ngo ngo (Nilikuwa nikipiga hodi huku mlinzi akionekana kunishangaa kwani aliniona ninavyoingia na Aziza, alikuwa hajui sababu kwa nini nilikuwa nimetokea nyuma ya nyumba na kuanza kugonga mlango. Mlango ukafunguliwa, alikuwa Aziza, kama vile sterring, nikaingia ndani, Baba yake Aziza akabaki akiniangalia, sikufichi, nilijiamini kama Van Damme)


    Baba yake Aziza alikuwa amenitolea macho pamoja na wageni wote ambao walikuwa sebuleni, mtu mzima sikutaka kuteteleka hata kidogo, nilionyesha uso wa kujiamini kupita kawaida. Kwa Aziza, kwa mbali alionekana kuwa na hofu kwani alidhani kwamba nisingekuwa na ujasiri wa kusimama na kuzungumza.


    MIMI: Samahani mzee. Shikamoo.
    BABA AZIZA: Marahaba.
    MIMI: Nilikuja katika kipindi kilichopita lakini sikukuta.
    BABA YAKE AZIZA: Sikuwepo. Sawa, umeshanikuta. Kuna nini?
    MIMI: Niliagizwa na mzee Badour wa kule Msasani, ameniambia kwamba leo utatakiwa kufika katika kikao kile cha harusi kinachoendelea (Baba Aziza akaonekana kushtuka)
    BABA AZIZA: Kikao gani?
    MIMI: Kile cha mtoto wake, Farhia.
    BABA AZIZA: Huyo mzee ndiye nani?
    MIMI: Mfanyabiashara mwenzako.
    BABA AZIZA: (Huku akionekana kushangaa zaidi) Alikutuma uje kwangu?
    MIMI: Ndio (Nilijibu huku nikiwa serious)
    BABA AZIZA: Una uhakika ni mimi?
    MIMI: Ndio.
    BABA AZIZA: Yeye alikwambia uende kwa nani?
    MIMI: Kwako.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    BABA AZIZA: Nani?
    MIMI: Mzee Mahmoud.
    BABA AZIZA: Hapana. Mimi sio mzee Mahmoud. Mimi ni mzee Mansour.
    MIMI: Mmmh! Mbona unanichanganya? Hii si nyumba namba 315?
    BABA AZIZA: Hapana. Hii ni nyumba namba 511. Nyumba kuanzia namba 300 zipo kule mbele.
    MIMI: Ok! Basi samahani kwa usumbufu mzee wangu. Nikosea namba, ila nilipomuuliza mlinzi alijibu hapa ni kwa mzee Mansour ila jina likanichanganya, si unajua sisi wengine majina ya kiarabu hatuyajui vizuri.
    BABA AZIZA: Usijali kijana. Najua vijana wa sasa hivi mnakuwa na mambo mengi vichwani. Sawa. Nenda.
    MIMI: Usijali (Nikageuka na kisha kuufungua mlango huku Aziza akibaki kutetemeka tu)
    MLINZI: Ebwanaa vipi tena, mbona sikuelewi elewi?
    MIMI: Hakuna tatizo. Nilikuwa nataka kuonana na mzee Mansour tu.
    MLINZI: Ok! Karibu tena.
    MIMI: Asante.


    Nikashusha pumzi ndefu, sikuamini kama niliweza kutoka katika mikono ya mzee yule aliyeonekana kuwa na hasira kupita kawaida. Nilitembea kwa mwendo wa haraka haraka mpaka kituoni ambapo nikapanda gari na kisha kuelekea nyumbani. Garini, mawazo yangu yalikuwa juu ya ule msala ambao nilikuwa nimenusurika, ulikuwa msala mkubwa ambao ungeweza kunitoa roho kama ningeleta ishu za Kisharobaro kama Eduado. Nilipofika nyumbani, nikaanza kuchati na Aziza.


    AZIZA: Hakuna kama wewe. Umeshindikana mpenzi. Wewe ni genius.
    MIMI: Hahaha! Tena ana bahati leo sikutaka kuleta usanii mkubwa zaidi.
    AZIZA: Mmh! Kwani ungeweza kuleta zaidi ya ule?
    MIMI: Yeah! Mngenibeba pale.
    AZIZAl: Hahaha! Hapana chezea wewe mtoto wa tandale, umeshindikana aisee.
    MIMI: Hahaha! Usijali. Kokote kunapokuwa na ishu zinazohitaji mafunzo ya kininja wewe niite tu, usiogope. Hata ukitaka kuingia Ikulu, wewe niite tu na kila kitu kitakuwa poa.
    AZIZA: Mmmh! Unajiamini wewe.
    MIMI: Acha masihala na mimi.
    AZIZA: Ok! Leo sichati sana ila ningependa kuonana na wewe kesho.
    MIMI: Wapi?
    AZIZA: Popote upendapo.
    MIMI: Poa. Tuonane gesti.
    AZIZA: Hahaha! Acha masihala.
    MIMI: Ndio maana nimekwambia sema wapi. Yaani ni sawa na kuja Tandale halafu nikuulize unakunywa kinywaji gani, je ukisema maziwa, nitayatoa wapi? Ukija huku sikuulizi unakunywa kinywaji gani, nakuuliza unakunywa soda gani.
    AZIZA: Hahah! Wewe mtoto wewe. Najivunia kuwa na mtu kama wewe.
    MIMI: Usijali. Kuwa serious, tuonane wapi?
    AZIZA: Njoo chuo.
    MIMI: Saa ngapi?
    AZIZA: Muda wowote ule.
    MIMI: Poa. Nitakuja saa nne usiku.
    AZIZA: Nini?
    MIMI: Hebu kuwa serious, nije saa ngapi?
    AZIZA: Njoo saa tisa. Unalijua lile jengo la Biashara la UDBS?
    MIMI: Yeah! Si pale karibu na kituo cha polisi, opposite na mini-market?
    AZIZA: Yeah!
    MIMI: Poa nitakuja.
    AZIZA: Usichelewe, kuna bonge la sapraizi nataka kukuonyeshea.
    MIMI: Mmmh! Lipi hilo?
    AZIZA: Nikikwambia haitokuwa sapraizi. Wewe njoo tu.
    MIMI: Poa.


    Kuanzia kipindi hicho sikuonekana kuwa na furaha tena, muda wote nilikuwa nafikiria kuhusiana na sapraizi hiyo ambayo Aziza alikuwa ameniahidi. Sikufichi rafiki yangu, usiku ulikuwa mrefu kwangu. Sikutaka kuchati na Aziza, nililala moja kwa moja mkpaka kesho ambapo nikaamka. Kutokana na ubize wa hapa na pale, nikaenda chuo saa tisa na kisha kumuita aje nje ya jengo lile la UDBS, haukuchukua muda, akatoka huku akiwa na Eduado, wote walikuwa wakicheka jambo lililonichanganya.
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    AZIZA: Karibu mpenzi.
    MIMI: Asante. Mbona mnacheka hivyo mtafikiri mnamwangalia Mr Bean?
    EDUADO: Ungekufa. Watoto wa Waarabu si wa kwenda kuwavaminia kwao. Matokeo yake ukajificha uvunguni, sikupatii picha, ulijikunja kama dawa ya mbu.
    MIMI: Hahaha! Aisee ni noma. Kweli nimeamini mtu akifumaniwa, acha awe mdogo kama panadol.
    AZIZA: Kwanza twendeni tukapate lunch, au Nyemo umeshiba?
    MIMI: Nimekula home ila sijashiba wala nini. Wazo ulilolitoa liko poa. Msosi wapi?
    AZIZA: Kule bondeni.
    MIMI: Wanapakua kingi au nao wababaishaji.
    AZIZA: Kikiwa kidogo utaongeza.
    MIMI: Namna hiyo, hayo ndio maneno. Ila hapa nina 400 ya nauli tu.
    AZIZA: Usijali. Nitakurudisha na gari.
    MIMI: Hapo mzuka zaidi. Itakubidi uniongezee shilingi mia ninunue vocha ya 500 ili niingie facebook baadae.
    AZIZA: Usijali. Nitakutumia elfu kumi kabisa.
    MIMI: Duh! Sasa simu yangu si itazima
    AZIZA: Kwa nini?
    MIMI: Haijazoea kuingiza kiasi kikubwa cha hivyo. Sawa na mgonjwa wa Tandale ukampelekea juisi ya shilingi elfu kumi. Anaweza kufa.
    AZIZA: Hahaha! Kwa nini?
    MIMI: Tumbo limeingiza kitu kigeni kwa hiyo inaweza kuonekana kama asidi.
    AZIZA/EDUADO: Hahaha.
    MIMI: Huo ndio ukweli. Ila nina swali.
    AZIZA: Swali lipi?
    MIMI: Nahisi kama mnanificha. Kuna ishu inayoendelea hapa?
    AZIZA: Muulize Eduado.
    MIMI: Eti kaka kuna nini?
    EDUADO: Aziza anakupenda. Alikuwa akikuhitaji toka zamani ila alikuwa akiogopa kukwambia, akaniambia nifanye juu chini mpaka anakupata.
    MIMI: Unasemaje?
    EDUADO: Ndio hivyo. Anapenda kusoma kila unachokiandika facebook, amekuwa rafiki yako mkubwa, akavutiwa na wewe ila alikuwa akikuhitaji, alichokifanya, akakuunfriend na kisha kujifanya mtu mpya kwako.
    MIMI: Aiseee...duh! kwa hiyo kila kilichokuwa kikiendelea kilikuwa kikijulikana?
    EDUADO: Yeah! Huo ndio ukweli.
    MIMI: Sasa na wewe Aziza ulikuwa unaogopa nini kuniambia?
    AZIZA: Maadili.
    MIMI: Kivipi?
    AZIZA: Msichana hatakiwi kumuanza mvulana.
    MIMI: Hahaha! Ningekuwa na girl mwingine je?
    AZIZA: Ningepigana mpaka nikupate.
    MIMI: Hahaha! Aya buana. Mchezo wenu umefanikiwa na wote mmeshinda. Hebu kwanza ongezeni mwendo washikaji, unajua hapa nina ubao ile mbaya mpaka tumbo linasikia kizunguzungu.
    AZIZA: Mmmh! Kwani tunatembea taratibu?
    MIMI: Mnatembea kama mnamsindikiza Bibi Harusi.


    Hicho ndicho kitu ambacho nilitaka kukwambia kila siku katika maisha yangu. Aziza ndiye alikuwa msichna wangu, nilimpenda na kumthamini sana. Japokuwa alikuwa msichana mwenye uwezo lakini kila alipokuwa pamoja nami alikuwa akionyesha heshima ya hali ya juu japokuwa nilikuwa nikiishi Tandale. Aziza alinipenda, nilimpenda pia, tulifanya mengi sana hasa yale ambayo wapenzi huyafanya faragha. Mpaka leo hii, bado ninampenda mtoto huyu ila cha ajabu....hahaha! hata kwao sitamani kukanyaga.


    Hii ni hadithi ya kutunga, hakuna kitu chochote cha kweli. Ninapoandika facebook chatting, ni kama kuburudishana na si kufundishana kama wengine wanavyodhani. Fasihi andishi kazi yake ni kufundisha, kuonya, kuburudisha na mambo mengine. Kwa upande wa facebook Chatting, tunaburudishana tu na ndio maana hakuna hata sehemu moja kwa siku imepita bila kucheka.
    Nakutakia siku njema. Kama umetokea kuipenda, unajua cha kufanya......Au hadi tukumbushane? 


    ASANTE KWA KAMPANI YAKO......NAMSHUKURU MUNGU KWA KUIKAMILISHA HII HADITHI.
    ENJOY SIKU YAKO.
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog