Chombezo : Facebook Chatting
Sehemu Ya Nne
(4)
Najisikia
nimechoka sana, nimechoka kupita kawaida kwa sababu nilikuwa nimetoka kucheza
mpira uwanjani huku nikiwa nimechafuka kupita kawaida. Ninapofika nyumbani,
ninaoga na kisha kuchukua simu yangu kwa ajili ya kuangalia updates za facebook,
sikukuta hata meseji moja zaidi ya notification tu, tena wala hazikuwa nyingi.
Nilichokifanya ni kuanza kuzugazuga hapa na pale na kisha kutulia. Mara ghafla
nikaona namba moja nyekundu kwenye sehemu ya meseji, kulikuwa na meseji
imeingia, nilichokifanya, nikaifungua na kuanza kuchati na mtu huyo
huyo.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
EDUADO: Mambo vipi
Shahruk Khan.
MIMI: Hahahha! Poa. Inakuwaje wewe
mtu.
EDUADO: Kama kawa. Nilikuwa nakusubiri sana online. Nilikuwa na
mzuka na wewe ile mbaya.
MIMI: Duh! Mzuka na mimi! Kuna nini
tena?
EDUADO: Kuna bonge la kazi hapa. Unataka?
MIMI: Kwa
nini nisitake? Nipe mawasiliano yao niandike barua ya kuomba kazi
fasta.
EDUADO: Hahahaha! Kaka unakosea. Niliposema kazi sikumaanisha
hiyo.
MIMI: Wewe ulimaanisha ipi sasa?
EDUADO: Kazi moja
hivi. Kazi ambayo watu wengi wameishindwa hasa masharobaro.
MIMI:
Hahahaha! Itakuwa kubeba zege hiyo watoto wa mama hawaiwezi. Mimi naiweza, hebu
niambie ni jengo gani.
EDUADO: Sio kazi ya kubeba zege. Kuna mtu
nataka umfanyie kazi.
MIMI: Mtu gani?
EDUADO: Kuna demu
fulani nipo nae hapa UDSM ni mkali ile mbaya. Yaani mkali mpaka nashindwa kusema
ukali wake unafanana na nini.
MIMI: Hebu acha masihala kaka. Kwa hiyo
kama mkali mimi nifanyeje nini?
EDUADO: Huyu demu anaringa mbaya.
Yaani demu ananata utafikiri akanyagi ardhi hii tunayochimbia
vyoo.
MIMI: Ok! Wazuri wapo wengi na hata wenye maringo wapo wengi
pia. Hebu niambie kuhusu huyo. Kwanza anaitwa nani. Nipe maelezo ya
kujitosheleza na sio naanza kumtengeneza demu mkali kichwani mwangu ikawa ndivyo
sivyo.
EDUADO: Huyu demu anaitwa Aziza Moody, anaishi Msasani, baba
yake ni mfanyabiashara mkubwa sana aisee. Ni demu fulani pini…yaani ni pini
sana.
MIMI: Hebu acha masihala. Sasa inakuwaje watoto wa kisharobaro
wamemshindwa.
EDUADO: Huyu demu hafagilii muonekano, ni demu fulani
ambaye anapenda mtu anamfuate kama jinsi alivyo. Yaani kama wewe ni mtu wa
chini, mfuate hivyo hivyo ila tatizo watoto wa hapa chuo wanapenda kumfuata
kisharobaro kaka.
MIMI: Dah! Kwa hiyo kazi unayotaka kunipa ni
ipi?
EDUADO: Umchukue huyu mtoto. Yaani ukifanikiwa, moyo wangu
utakuwa mweupeeeeeee kama theluji.
MIMI: Hahaha! Usitake kunichekesha
EDUADO, hivi unamkumbuka Sikitu?
EDUADO: Sikitu yupi?
MIMI:
Si yule demu wa mwaka jana ambaye ulikuwa unamsifia sanaaaaa kwamba mkali kumbe
wala hakuwa mkali kama ulivyokuwa ukimsifia, mbaya zaidi alikuwa anakaa mbali,
Musoma.
EDUADO: Acha na hayo, yule msahau kwani mimi mwenyewe
alinitumia picha ambayo sio yake. Ila kaka kiukweli Aziza ni demu mmoja mkali
sana. Hapa chuo amekuwa gumzo kila kona, vijana wengi
wamechemka.
MIMI: Sasa kama wengine wamechemka mimi nitaweza
vipi?
EDUADO: Hahahaha! Kaka ninakuamini sanaaaa, wewe mtu unaweza
sana kuongea, unaweza sana kuandika. Endapo kazi nikakupa na kisha ukashindwa,
haki ya Mungu nitajua kweli duniani kuna wasichana wagumu.
MIMI: Kwa
hiyo kazi yako ina malipo au?
EDUADO: Ikitokea umempata, nitakupa
zawadi kaka. Yaani ninachokitaka huyu demu umchukue tu, basiiiiiiii. Anaringa
sana, ananata sana, yaani sijui niseme vipi.
MIMI: Ila si anaringa kwa
sababu mzuri?
EDUADO: Ndio. Ila yeye kazidi.
MIMI: Ila kwa
sasa aisee nahisi nimepoteza kumbukumbu zangu za kuongea na hawa watoto wa kike,
sijui kama nitaweza.
EDUADO: Acha kunitania kaka. Nakuamini sana
kwamba unaweza kuliko mtu yeyote na ndio maana nikakufuata wewe. Hivi haujiulizi
kwa nini sikumfuata Thomas? Thomas kwenye kuongea mkali sana ila kwenye kuandika
hakuna kitu, ila wewe, aisee una kipaji kila kona, nafikiri hata ukimtokea
kiziwi, hachomoiiiiiiiiii.
MIMI: Hahaha! Hebu acha kunipamba. Hebu
niambie, huyo demu yupo Facebook?
EDUADO: Amejaa teleeee…yaani kajaa
teleeee. Anajiita Aziza M Aziza. Ni demu mkali sana. Hebu mcheki
kwanza.
MIMI: Sawa.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Sikutaka kuchelewa,
tayari kichwa changu kikaanza kujazwa na sura nyingi za wasichana wazuri huku
nikianza kuzigawanya kimakundi kwamba huyu alikuwa Aziza mwenyewe huyu hakuwa
mwenyewe. Nilikuwa namfahamu EDUADO toka tupo katika shule ya sekondari ya Mbezi
High School, alipokuwa akisema msichana fulani ni mzuri, mzuri kweli japokuwa
kwa Sikitu alikuwa ameniingiza choo cha kike. Sikutaka kuremba, mara baada ya
kuona majina kadhaa, nikamfuata Eduado inbox.
MIMI: Oyaa
Akshey.
EDUADO: Vipi ushampata?
MIMI: Wamekuja wakina Aziza
wengi hao, mpaka wengine wanakaa India.
EDUADO: Hebu
subiri.
Sikujua alikuwa akifanya nini, kwa sababu aliniambia kwamba
nisubiri, wala sikuwa na presha, nikamsubiri nione angeniambia kitu gani baada
ya hapo. Nilimsubiri kwa kipindi kama cha dakika moja hivi, akanijia tena
inbox.
EDUADO: Umeiona hiyo picha yenye mdoli wa
Barbie?
MIMI: Yeah!
EDUADO: Ndiye yeye huyo. Nyemo huyo ni
demu mkali ambaye sijawahi kuona.
MIMI: Acha utani.
EDUADO:
Sure. Unamkumbuka Silvia wa Mbezi High, sasa Silvia haingii kwa
Aziza.
MIMI: Acha utani kaka. Silvia haingii?
EDUADO: Kweli
tena. Tena hagusi hata robo.
MIMI: Sasa mbona hajaweka picha yake,
nitamjua vipi kama ni mkali. Hebu nipe sifa kwanza manake naona picha zake
kazipiga pini watu wasio marafiki zake wasizione.
EDUADO: Kwanza demu
ni pini sana, demu kwao wana mahela ya kumwaga, chuo anakuja na gari, Verrosa
moja nyeusi, mtoto anamiliki laptop aina ya Apple ile inaayouzwa milioni tatu,
mtoto anamiliki anamiliki iPhone 5 huku akisema kwamba iPhone 6 ikianza kuuzwa
atataka kuanza kuitumia kwani anapenda kwenda na wakati.
MIMI: Kaka
utakuwa unanitania tu.
EDUADO: Kweli tena.Halafu kuna cha
zaidi.
MIMI: Kipi?
EDUADO: Otea.
MIMI: Hebu
niambie kipi?
EDUADO: Ugonjwa wako.
MIMI:Unamaanisha
nini?
EDUADO: Mtoto Mpemba.
MIMI: Hahahaha! Kaka acha utani,
utanifanya nimfuate sasa hivi.
EDUADO: Ndio hivyo. Mtoto ni pini sana,
pini ile iliyosimama.
MIMI: Hahaha! Pini kama ya Blackberry
vile.
EDUADO: Acha kaka. Mtoto ni pini zaidi ya zile za Blackberry.
Kwanza ukimuona tu, mtoto utampenda. Mavazi yake sasa…weeeeeee.
MIMI:
Hebu nipe sifa zake kwa ujumla.
EDUADO: Nisikilize. Mtoto ni wa
kipemba. Ana nywele ndefu zinazomfikia chini ya mabega yake, mtoto ana hipsi
zilizopangika, hapa mashavuni mwake ana vijishimo viwili, lipsi lainiiiii kila
wakati zinang’aaaaa.
MIMI: Kingine?
EDUADO: Mtoto ana sura
zile nyembamba zile, masikio hayaonekani sana, kifuani hapa kumesimama vizuri
sana, mavazi yake huwa ni suruali za jinsi kwa sana.
MIMI: Umesema
anaishi wapi?
EDUADO: Anaishi Masaki.
MIMI: Halafu mimi
naishi uswahilini Tandale. Umesema anamiliki simu gani?
EDUADO:
Anamiliki iPhone 5.
MIMI: Halafu mimi namiliki Huawei. Umesema baba
yake ana gari?
EDUADO: Yeah! Yeye mwenyewe analo.
MIMI: Mimi
sina gari na baba yangu hana hata gari.
EDUADO: Acha kujizarau Nyemo.
Mtoto unang’oa huyu.
MIMI: Usijali. Ushawahi kufika
kwao?
EDUADO: Yeah kaka. Kwanza hiyo nyumba yao….duh! Kuna watu
wanakufuru. Kwanza bonge la nyumba. Limezungushiwa ukuta, jumba lina fensi kwa
juu, ndani kuna kamera, nyumba vigae, ukiingia ndani unakutana na bwawa la
kuogelea. Kuna ungo wa Dstv, kuna bustani kali ya maua mbalimbali, kuna walinzi
wawili ambao wanalinda kwa bunduki kutoka Knight. Yaani wapo
full.
MIMI: Ok! Mimi naishi Tandale. Nyumba yetu ndogo, haina ukuta
wala fensi, haina mlinzi na kama kuogea, tunaogea bafuni na si kwenye bwawa.
Mpaka hapo, nimeshamkosa.
EDUADO: Nyemo. Usiniangushe. Yaani mimi
lengo langu umchukue huyu mtoto tu.
MIMI: Una namba zake za
simu?
EDUADO: Hapana.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
MIMI: Basi ngoja
nifanye mishe halafu nione itakuwaje. Ila wasiwasi wangu ule ule tu, itakuwa
kama Sikitu.
EDUADO: Usijali kaka. Huyu sio kama Sikitu. Kwanza yule
demu mwenyewe alinitaka nikaamua kukurushia wewe. Mimi na demu wa mkoa wapi na
wapi. Ishi Dar tuwe tunamalizana, mambo ya mikoani haya, tigo pesa zinatumika
sanaaaa. Hapa hapa Bongo ndio kuzuri, ukimtaka tu, nauli yako sh 400 kwenda, 400
kurudi. 600 soda yako, 600 soda yake. Mwisho wa siku kwa gharama zote ukitoa
buku tano, michenji inarudi mingi mpaka mfuko unaomba poo kwa kuzidiwa
uzito.
MIMI: Hahaha! Umeonaeeeee. Hakuna gharama kabisa. Ila poa,
usijali. Ngoja nimtumie friend request halafu nianze kumfanyia uninja. Ila
niandalie zawadi
yangu.
EDUADO: Usijali kaka.
Wewe fanya yako, ukimaliza, niache nami nifanye yangu. Au sio?
MIMI:
Poa. Mia mia. Ngoja nianze kazi.
EDUADO: Shwari. Ngoja nifanye yangu.
Nataka nimfuate mtoto Magreth hapa.
MIMI: Ndio yupi
huyo?
EDUADO: Si yule wa facebook wa kipindi kileeeee.
MIMI:
Kwani ushang’oa?
EDUADO: Chezea mimi wewe. Mimi noma…kama ni wembe
badi Gilette.
MIMI: Sasa mbona hujamkata Aziza kama ni
Gilette.
EDUADO: Aziza ana chembechembe za chuma. Ningemkataje? Huyo
nakuachia kama wewe mwenye yale maji ya kuyeyushia vyuma ndio utakwenda nae
sawa.
MIMI: Basi poa. Acha nikufanyie kazi yako mkurugenzi. Kazi hii
niliachana nayo zamani sana ila kwa ajili yako, navaa gwanda nikukamilishie
halafu nisepetue.
EDUADO: Mia mia.
Hapo
nikatulia kwanza. Nikaanza kujifikiria ni kwa jinsi gani nilitakiwa kuanza
kumfuata msichana Aziza. Kitu ambacho kilikuwa kikiniumiza kichwa changu kwa
wakati huo ni kwamba hata Aziza mwenyewe sikuwahi kumuona kwa hiyo niliogopa
kuuziwa mbuzi kwenye kiroba kama ilivyokuwa kwa Sikitu. Ngoja nikupe kijistori
changu na huyu Sikitu.
Eduado alinifuata inbox na kuniambia kuhusu
Sikitu, alimsifia na kumpamba sana, alinifanya nivutiwe nae sana na yeye alitaka
nimchukue, nikasema poa. Mzee nikaanza mishemishe zangu kama Michael Scotfield
wa Prison Break na kweli ndani ya wiki mbili, mtoto akawa mikononi mwangu.
Unajua jinsi mtu anavyokwambia kwamba msichana mzuri hata kama wewe mwenyewe
haujamuona unaanza kumtengeneza msichana wako kichwani, hivyo ndivyo
nilivyofanya kwa Sikitu. Nikamtengeneza Sikitu wangu kichwani, kumbe nilikuwa
namuumba Sikitu wangu bila kujua. Siku aliponitumia picha yake inbox niione mara
baada ya kumlazimisha sanaaa, akanitumia. Alikuwa mrembo lakini hakuwa na urembo
kama ambao Eduado aliniambia. Nikaachana nae.
Sikitu hakukoma, chating
zangu nzuri za inbox za maneno ya hapa na pale alikuwa akizipenda sana, hivyo
alitaka tuendelee kuchati. Haikuwezekana tena, nilimkatia maguu mara baada ya
kuniambia kwamba anaishi Musoma, mbaya zaidi huku Dar hakuwa hata na ndugu kwa
hiyo hakuwa na ndoto za kuja Dar, sasa mimi ningeonania nae wapi? Yaani nisafiri
mpaka Musoma kwa ajili yake? Niliona kuwa suala gumu sana kufanyika. Basi ndio
hivyo, tukapotezana potezana na hatimae mapenzi kutoweka, siku hizi simuoni,
bila shaka, kaniblock.
Baada ya miezi miwili, leo Eduado kaja na mpya,
kaja na demu mpya ambaye wala sijawahi kumuona, huyu anaitwa Aziza. Sikutaka
kufanya vitu kwa presha sana, nilichokifanya ni kumtumia friend request na kisha
nikianza kusubiria majibu. Kila siku nilipokuwa naingia facebook, hakuwa
ameconfirm, sikuwa na shaka, niliendelea kusubiria zaidi na zaidi na baada ya
siku mbili, akaikubali, furaha iliyoje? Hapo ndipo nilipoamua kuuanza mchezo
wangu, mchezo ule ule ambao ulimfanya Sikitu kuchanganyikiwa kwangu, ila kwa
hapa, kutokana na sifa ambazo niliambiwa na Eduado, ilinipasa nitumie mbinu
kubwa zaidi, mbinu ambazo zingeendana na uzuri wake, mtoto wa kipemba bwana,
hakutakiwa kufuatwa kikawaida, nami nikaanza kumfuata kipemba kipemba na mapenzi
ya Kihindi….mtu mzima nikawa najiona kama Shahruk Khan
vile.
****
Mtu mzima nikaingia kazini kwa ajili ya kuanza
kazi yangu ambayo nilikuwa nimepewa ya kuhakikisha kwamba mtoto wa Kipemba,
Aziza anakuwa wangu. Ni kweli kwa mambo ambayo alikuwa amenieleza Eduado
yalikuwa yamekwishanitenga kwa kiasi kikubwa sana kutoka kwa Aziza lakini
ilitakiwa pia nifanye yangu katika kipindi hicho.
Kitendo cha Aziza
kuikubali Friend request yangu kilionekana kuwa kitu kizuri sana, kwa hiyo
nilichokifanya nikajifanya bonge la bwege, nikamfuata kwa wall yake na kuandika
‘thanx A’ na kisha kusikilizia.
Kweli, kama alivyosema Eduado ilikuwa
vile vile, demu hakuiLIKE thanx yangu wala kuitolea comment, nikaona poa, vyote
hivi ni mwanzo wa kumbukumbu zangu nitakazompa hapo baadae. Kwa upande wa
Eduado, hakutaka kujishika, kila siku alikuwa akinisumbua tu kwa
inbox.
EDUADO: Kaka vipi?
MIMI: Kuhusu
nini?
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
EDUADO: Mtoto.
Hujaniambia chochote kile. Umefanikiwa au?
MIMI: Wewe umeniambia mambo
mengi kuhusiana na huyu mrembo, unadhani ningeweza kumamilisha ndani ya siku
tatu?
EDUADO: Hapana. Nilikuwa nauliza manake nimeona hapa sasa hivi u
rafiki yake.
MIMI: Yeah! Ni rafiki yangu ila kila kitu kinatakiwa
kufanywa kimahesabu.
EDUADO: Usianiangushe basi Sharukh
Khan.
MIMI: Hilo usijali.
Katika kipindi
hicho nilikuwa nafikiria mambo mengi sana, huyu mtoto kwangu alionekana kuwa na
pozi ajabu, yaani nilikuwa nikizipitia post za kizushi alizokuwa akiziweka, watu
walikuwa wakicomment halafu yeye hatokei. Hata kama kaweka picha ya mdoli, watu
walikuwa wakicomment halafu yeye hatokei na mbaya zaidi kulikuwa na watu wengi
wanaolike na kucomment jambo lililonifanya kugundua kwamba kuna siku huyu
msichana alikwishawahi kuweka picha na hivyo wanaume kujua ni mzuri na kisha
kuzitoa.
Bado kiu yangu ilikuwa ni kuwasiliana na Aziza tu ambaye
alionekana kuwa mtu wa mapozi sana. Sikujua ningeanzia wapi ila nilichokifanya
ni kuanza kumtumia meseji nione kama angeijibu au
kuipotezea.
**************************
MIMI:
Mambo!
Niliituma meseji hiyo, siku ya kwanza, ya pili, ya tatu mpaka
wiki hadi mwezi lakini meseji ile moja haikujibiwa, mbaya zaidi nilikuwa namuona
online. Sikukoma kidume mimi, bado nilikuwa nikimtumia meseji za kumsalimia
lakini hali ilikuwa vile vile, hakujibu.
Mtu mzima nikaona naumbuka,
kama nilikuwa naitwa Sharukh Khan basi ilibidi niwaonyeshe watu kwamba
hawakukosea kuniita jina hilo, nilitaka kuwaonyeshea dhahiri kwamba mama yangu
alikuwa mtu wa Tanga, kule ambapo mapenzi yalikuwa yamenogeshwa kwa kuwekewa
makorokocho. Nilichoanza kukifanya ni kuanza kumtag picha. Hapa ni lazima
ugundue, picha ambazo nilikuwa nikimtag ni zile ambazo zilikuwa romantic tu.
Picha ambazo zilikuwa zikiwaonyesha wapenzi wakibusiana na kukumbatiana, ndizo
ambazo nilikuwa nikimtag, tena yeye peke yake.
Hahaha! Ule ukaonekana
kama ujinga vile kumbe kwa wakati huo nilikuwa na target zangu kichwani.
Niliendelea na mtindo ule ule mpaka siku ambayo akaonekana kuchoka na
kukasirika, kwa mara ya kwanza akaja inbox, ila sio kiamani kama nilivyotaka,
alikuja kibifu.
AZIZA: Naomba usiwe unanitag
mapicha yako.
Niliisoma meseji ile. Kwanza
nikacheka, kilichonifanya kucheka ni kwa kumuona kwamba alikuwa msichana mjinga
sana, kitendo cha yeye kuniandikia meseji kilionekana kuwa kama kosa kubwa sana,
nilichokifanya, nikaanza kuandika meseji ndefu, meseji ambayo ingemfanya
kunijibu, meseji ambayo isingemfanya kubaki kimya.
MIMI: Kuna vitu
kadhaa Aziza itakupasa uelewe na ninatumaini vitakuongoza katika maisha yako
yote. Jitahidi kuishi lakini kamwe usiwe mbinafsi. Unapopata kitu, usitake kukaa
nacho, jaribu kuchangia pamoja na wenzako. Unapopata chakula, jaribu kumwangalia
yule asiye na chakula na kumgawia, milele atakushukuru kwa ulichomfanyia siku
moja tu alipokuwa na njaa. Unapomuona mtu hana nguo, mgawie nguo na ataendelea
kukushukuru maisha yake yote. Unaniona mimi, mimi si mbinafsi hata mara moja,
katika maisha yangu nimekuwa nikiwapa watu vitu fulani vitu ambavyo hawana
katika maisha yao, nikakuangalia wewe, nikakuona kwamba u masikini sana,
ukijiangalia, unajiona kuwa tajiri, mwenye fedha labda, lakini bado ni masikini,
masikini wa kitu kimoja ambacho ulihitaji mtu mwenye kitu hicho akusaidie,
nikakusaidia lakini unaonekana kuukataa msaada wangu. Kuwa makini Aziza, mara
nyingine msaada huja mara moja na kupotea, unapoutafuta, inawezekana usiuone
tena.
Kwanza nikashusha pumzi nzito, nikaiangalia
meseji ile na kisha kuirudia rudia mara nyingi nyingi na kisha kuituma. Niliiona
kuwa meseji kali ambayo isingemfanya kubaki kimya kwa kutaka kujua ni kitu gani
ambacho alikuwa amekosa katika maisha yake, kilichonifurahisha, akatuma meseji.
Kuna nini tena? Meseji ya pili hiyo, hakujua kwamba ndio mwanzo wa chating
yetu.
AZIZA: Umemaanisha nini?
MIMI: Nimemaanisha kwamba
wewe ni masikini. Tena yule fukara kabisa. Hiyo ndio maana
yangu.
AZIZA: Sijakuelewa.
MIMI: Hebu isome vizuri hiyo
meseji, utaielewa tu.
AZIZA: Nimeirudia zaidi ya mara tano,
sijaielewa, naomba uniambie umemaanisha nini.
MIMI: Nikuulize kitu
kimoja?
AZIZA: Niulize.
MIMI: Unaweza kugundua ni umasikini
wa aina gani umekuwa nao?
AZIZA: Hapana na ndio maana
nikauliza.
MIMI: Inawezekana ukawa na magari, nyumba na fedha ila bado
ukawa masikini, unakubaliana nami?
AZIZA: Hapana.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
MIMI: Kwa sababu
gani?
AZIZA: Mtu ana kila kitu, atakuwaje masikini.
MIMI:
Hahahah! Aziza. Ukisema hivyo unakosea. Kuwa na kila kitu haimaanishi kwamba
wewe si masikini. Unaniruhusu nikuulize kitu?
AZIZA:
Niulize
MIMI: Unaamini katika fedha?
AZIZA:
Yeah!
MIMI: Fedha inaweza kukupa kila ukitakacho?
AZIZA:
Yeah!
MIMI: Unakosea sana Aziza.
AZIZA: Unapokuwa na fedha
unanunua gari ulitakalo, unanunua chakula, unanunua nyumba na mambo mengine.
Kwani nimekosea?
MIMI: Umepatia. Ila unavyoona kila mtu mwenye fedha
huwa na furaha?
AZIZA: Inawezekana.
MIMI: Umekosea.
Umekwishawahi kuwasikia wale matajiri wanaojiua?
AZIZA:
Yeah!
MMI: Sasa wamekosa nini wale katika maisha yao? Wana fedha,
wanaweza kununua kila kitu, wana magari, wanaweza kwenda sehemu yoyote ile. Ila
swali linakuja kwa sababu gani walijiua?
AZIZA: Mmmh!
Sijui.
MIMI: Hahaha! Jibu rahisi sana. Walikosa furaha, amani,
wakakosa mapenzi na mambo mengine. Unapokuwa na fedha, utanunua gari ila kumbuka
hautoweza kununua furaha, unapokuwa na fedha utaweza kumnunua msichana mtaani
lakini ukashindwa kununua mapenzi. Umenipata hapo?
AZIZA:
Kidogoooo.
MIMI: Yeah! Kila mtu hunipata kidogo, ila tukiendelea
kuchati, utanipata sana tu. Utaniruhusu niwe nachati nawe kwa ajili ya kukuambia
mengi usiyoyajua?
AZIZA: Yeah! Ila huwa siwi online muda
wote.
MIMI: Hilo si tatizo. Unachotakiwa ni kunishtua kila unapokuwa
online. Utakwenda kufahamu mengi ambayo haujayajua. Kwani unaishi
wapi?
AZIZA: Nipo Masaki Dar es Salaam.
MIMI: Ndio
maana.
AZIZA: Kwa nini?
MIMI: Usijali. Mtaa unaokaa ndio
nitakaoanza nao siku tukianza kuchati. Kwa sasa nahitaji kusoma, naomba
uniruhusu niondoke.
AZIZA: Ila pleeeaseeee naomba
uniambie.
MIMI: Sijakataa. Nitakwambia tu wala usijali. Wewe ni rafiki
yangu, pamoja kuwa na kila kitu, yakupasa kupata vitu vingine ambavyo haupaswi
kuvinunua. Nitakwambia namna ya kuvipata na inawezekana hata marafiki zako
wakakushangaa.
AZIZA: Mmmh!
MIMI: Usigune. Huo ndio ukweli.
Usiku mwema Aziza.
AZIZA: Nawe pia.
Kuna
nini tena? Nilichokifanya ni kutoka online mpaka saa sita ndio nikaingia tena,
Aziza hakuwepo, nikamtafuta Eduado, nikamuona, hata kabla sijamtumia meseji,
akaniwahi.
EDUADO: Vipi Sharukh Khan. Imekuwaje au
bado?
MIMI: Kwisha habari yake. Anacheza na mwanasaikolojia
nini.
EDUADO: Imekuwaje tena?
MIMI: Wewe usijali. Cha msingi
andaa zawadi yangu.
EDUADO: Umeanza kufanikisha?
MIMI: Ndio
maana yake. Unajua ukimjua mpinzani inakuwa rahisi sana.
EDUADO: Dah!
Wewe noma kaka. Yaani hii kazi nimewapa watu saba, naona wengine wanambwela tu,
wananiambia kila wakimtumia meseji dogo hajibu.
MIMI: Hahahaha! Hata
mimi ilikuwa hivyo hivyo. Nilivyoona anashindwa kujibu, nikatumia plan B. Hapo
ndipo nilipompoteza na kuchati nae sana.
EDUADO: Kwa hiyo ulichati
nae?
MIMI: Yeah! Tena mimi ndiye nimemkatisha. Chezea mimi
wewe.
EDUADO: Hahahah! Ebwana wewe nomaaaaa....sasa hata
kukutambulisha kwa demu wangu mwingine naogopa.
MIMI: Wewe si ulinipa
kazi kaka? Hakuna tatizo. Kazi inafanyika taratibu.
EDUADO: Duh! Kaka
nashukuru sana kwa kunisikiliza. Natumaini mtoto ataeleweka tu.
MIMI:
Amekwishaeleweka. Dogo amekwishaeleweka.
EDUADO: Hahahah! Basi poa
sana, nimefurahi sana.
MIMI: Usijali kaka...hug.
EDUADO:
Poa.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kila kitu
kikaonekana kuwa juu ya mstari, meseji moja ambayo alikuwa amenitumia ikaonekana
kubadilisha kila kitu. Ile meseji ndio ambayo nilikuwa nikiitaka kuiona na kweli
aliituma. Chatting zikawa zimeanza, kwa Aziza, nilihitajika kuwa makini sana
kupita kawaida kwani kwa kufanya vile nilikuwa na uhakika wa kumchukua ili
kumuonyeshea Eduado kwamba nilikuwa Sharukh
Khan.
Sikutaka kuleta shobo tena kwani tayari
nilimuona kuku kuwa wangu kwa hiyo sikutakiwa kumshikia manati kwa kuamini
kwamba jioni ikifika mwenyewe atarudi bandani. Nilipoingia online siku
iliyofuatia, msichana Aziza alikuwepo, kajaa tele ila mtu mzima nikaamua
kuchuna. Katika hili ngoja nikwambie kitu kimoja rafiki yangu hasa mwanaume kama
mimi. Unapoona kwamba kuna msichana fulani unampigia sana misele facebook,
hautakiwi kila wakati umuanze wewe tu, sometimes unamchunia uone je ataweza
kukutumia meseji au la. Ukiona kwamba kakutumia, basi jua kwamba anautambua
mchango wako na hata kwenye ile mishemishe yako anaonekana kuifurahia. Ila
ukiona nae anakaa kimya, mtu mzima poteza kwani si unajua warembo wapo wengi!
Inawezekana haujapangiwa kuwa na huyo.
Nilipomuona Aziza online,
nikamchunia kana kwamba sijamuona huku nikiamini kwamba yeye ndiye alipaswa
kunitumia meseji. Ila katika kipindi hiki hasa siku ya leo, meseji zilikuwa
zikiingia nyingi nyingi hasa kutoka kwa marafiki zangu wengine, bahati nzuri
nilikuwa natumia kompyuta hivyo ilikuwa rahisi
kuwajibu.
IBRA: Mambo vipi kaka!
MIMI:
Poa. Ni aje mkuu?
IBRA: Kama kawa. Upo wapi?
MIMI: Nipo
gheto aiseee nimesizi tu si unajua kijimvua nje kinazingua.
IBRA:
Yeah! Hilo kweli kaka. Hivi unamuona mtu wangu hapo online?
MIMI:
Nani?
IBRA: Tina.
MIMI: Dah! Hapa namuona kwa kuotea, mara
anakuja mara anatoka. Kama vipi mcheki kwa whatsapp.
IBRA: Kwani yupo
huko?
MIMI: Yeah!
IBRA: Dah! Basi nafikiri kule atakuwa
kaniblock mtu mzima. Simuoni kabisa.
MIMI: Hahahah! Kaka pole sana.
Umeblockiwa...hahaha! Tatizo lako uliremba sana kwa kujifanya umeoa, full
mauhakika.
IBRA: Unajua nini kaka, kila siku naamini kwamba mwenda
pole ndiye mla nyama.
MIMI: Usitake kuniambia hivyo. Wahenga wengine
walikuwa wakizingua tu, kidogo naweza kumuamini yule aliyesema chelewa chelewa
utakuta mwana si wako. Si kwamba unamuona kinyonga anatembea taratibu ukajua
hata yeye anajua kwamba anatembea taratibu, mwenzako pale anajiona anakimbia kwa
kasi sana. Hahahaha! Na bado...atakublock mpaka whatsapp.
IBRA:
Akiniblock na huko tena, nitamuona katili sana
kaka.
Huku nikiendelea kupiga stori na Ibra, mara
Emmanuel Solo nae akaingia kwa inbox yangu. Sikuwa na jinsi, nilikuwa nachati
nao huku nikimuona Aziza online ila nami nilikuwa nimemlia pini
tu.
SOLO: Kaka.
MIMI:
Niambie.
SOLO Upo wapi?
MIMI: Nipo gheto. Wewe upo
wapi?
SOLO: Nipo Morogoro kama kawaida yangu.
MIMI: Duh!
Wewe noma. Ndani ya wiki moja umetembea mikoa mitatu. Big Up
mkuu.
SOLO: Kutafuta kaka. Maisha kutafuta. Si unamuona hata Ndimanga
Hassan, anatembea zaidi ya mikoa kumi kwa mwezi, hatutakiwi kukaa sehemu moja.
Hadithi imeishia wapi?
MIMI: Ipi? Zipo nyingi tu.
SOLO: Ile
ya yule msichana mwimbaji wa kwaya aliyekuwa amepanga mauaji kwa mvulana ambaye
alikuwa amemkataa kanisani na kuamua kutaka kumuua nchini
Zambia.
MIMI: Bila shaka unaizungumzia HER HIDDEN FACE, si
ndio?
SOLO: Yeah!
MIMI: Ile ipo sehemu ya tano. Inaendelea
kama kawa.
SOLO: Basi poa. Ngoja niitafute niendelee
kuisoma.
EDUADO: Kaka
MIMI: Niambie
kijana.
EDUADO: Mtoto leo kaja chuo aisee kapendezaje!
MIMI:
Acha utani.
EDUADO: Sure. Mtoto ni noma kaka. Mtoto mrembo mpaka
anajishangaa. Namuona online, ushatupia mambo?
MIMI: Hapana. Nangoja
anianze, asiponianza nampotezea tu kwani si lazima kivile kuchati nae na
kumshobokea.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
EDUADO: Ila kaka
fanya mambo bhana. Huyu demu sitaki umkose kabisa.
MIMI: Usijali kaka.
Huyu mdogo mdogo mwisho wa siku utamkuta gheto kapumzika. Chezea Tandale
wewe.
EDUADO: Hahaha!
AZIZA:
Mambo!
MIMIl Mabaya.
AZIZA: Ubaya wake?
MIMI:
Naumwa.
AZIZA: Nini tena jamani?
MIMI: Maralia. Yaani mbu
mmoja tu jana chumbani kwangu ndio alisababisha majanga yote
haya.
AZIZA: umekunywa dawa?
MIMI: Hapana.
AZIZA:
Kwa nini sasa jamani?
MIMI: Naogopa sana dawa Aziza. Labda uje
uninyweshe kinguvu.
AZIZA: Dah! Pole sana Nyemo. Nitakuombea kwa Mungu
akuponye.
MIMI: Asante sana. Nitafurahi sana.
AZIZA: Aya
nishakushtua. Hebu niambie kuhusu vitu ulivyokuwa ukiniambia.
MIMI:
Tatizo lako unajiamini sana Aziza halafu unafanya makosa sana kila unapoona
kwamba fedha ndio kila kitu. Yaani haujifikirii kama kuna watoto wa matajiri
ambao wanaumwa sana mpaka wanakufa, kama fedha ni kila kitu si
wangepona.
AZIZA: Nafahamu.
MIMI: Basi kama unafahamu,
fahamu pia kuna kitu ambacho ni kila kitu na si fedha kama
unavyofikiria.
AZIZA: Kipi tena.
MIMI: Mungu ndiye kila kitu
katika maisha yetu. Bila Mungu, huwezi kuwa na furaha hata kama una fedha, bila
Mungu huwezi kupona ugonjwa wako hata kama una fedha na kutibiwa na madaktari
wakubwa duniani. Umenipata?
AZIZA: Ndio nimekupata.
MIMI: Au
hadi hapo unataka kubishana tena?
AZIZA: Hapana. Ila unaonekana kuwa
na hekima sana Nyemo.
MIMI: Yeah! Unajua wakati mwingine yatupasa
kuutambua ukweli. Hatutakiwi kuamini sana katika fedha. Ila achana na hayo. Wewe
ni mama wa nyumbani, mwanafunzi wa sekondari au mwanafunzi wa
chuo?
AZIZA: Naonekaje?
MIMI: Profile picha yako ni ya
mdoli, sasa nitajua unaonekanaje?
AZIZA: Hahaha! Usijali. Mimi ni
mwanachuo.
MIMI: Unasoma wapi?
AZIZA:
Mlimani
MIMI: Unasomea nini?
AZIZA: Sheria.
MIMI:
Afadhali.
AZIZA: Afadhali ya nini tena?
MIMI: Uje kuwa
mwanasheria wangu baadae katika kampuni yangu.
AZIZA: Hahahah! Utaweza
kunilipa?
MIMI: Kwa nini nisiweze? Nitakuwa na fedha
mbayaaaaaaa....nitamiliki magari ya kifahari na majumba makubwa
sana....lol
AZIZA: Yote ni mipango ya Mungu ila napenda ulivyoongea
kwa sababu unaonekana una imani ya kupata hivyo, cha msingi yakupasa kujituma tu
na kumtanguliza Allah kwa kila kitu. Naomba nikuulize swali.
MIMI:
Usijali. Uliza.
AZIZA: Unaishi wapi?
MIMI: Tandale kwa
Mtogole.
AZIZA: Kule kwenye wezi wengi na wakabaji?
MIMI: Si
wezi wengi tu, kule kunapodharaulika na watu wenye fedha kama
nyie.
AZIZA: Hahaha! Usiseme hivyo bwana. Ila mbona
umedanganya?
MIMI: Nimedanganya nini?
AZIZA: Kwenye profile
lako. Umeandika unaishi Romania. Ulikuwa unataka kujipaisha nini upate
wanawake?
MIMI: Hapana Aziza. Hiyo imekuja yenyewe
tu.
AZIZA: Kivipi?
MIMI: Nilikuwa nataka kupatambulisha kama
home kwetu ni Tandale. Ila nilipokuwa nikiandika Tandale, haikuwa ikitambulika
kama ilivyokuwa sehemu nyingine. Matokeo yao wao kama facebook wakaniletea
Tandalesti mji fulani kutoka Romania, nikaona sio kesi, nikakubaliana nao, ila
ukiangalia kwa makini, Tandale imetokeza katika jina hilo.
AZIZA:
Yeah! Nimeona. Hebu naomba uniambie mengi kuhusu Tandale.
MIMI: Kama
yapi unataka kufahamu?
AZIZA: Mazingira, watu wa huko na mambo
mengine.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
MIMI: Tandale kama
Tandale mazingira yake mazuri sana, watu full kuyafurahia maisha kama kawa. Kuna
watoto wazuri, watoto ambao wanajitambua wao ni nani na kipi cha kufanya
maishani mwao. Kuna mambo ya Rusha Roho usiku, yaani kwa kifupi kuhusu maisha,
huku tunakula sana bata kuliko kwenu pa kulala saa moja.
AZIZA:
Hahaha! Kwani huko kwenu huwa mnalala saa ngapi?
MIMI: Huwa nikiwa
mgonjwa sana, nawahi kulala kama saa saba hivi.
AZIZA: Saa
saba?
MIMI: Yeah! Ila nikiwa si mgonjwa, mpaka adhana iadhiniwe. Watu
tunatransform usiku kuwa mchana na maisha yanasonga.
AZIZA: U must be
kidding me Nyemo.
MIMI: Huo ndio ukweli Aziza. Siwezi
kukutania.
Unaona jinsi mawasiliano yetu
yalivyokuwa yakienda? Hapo ndipo nilipokuwa napataka sasa. Nilikuwa namletea
sana ucheshi lakini mwisho wa siku kuna kitu nilikuwa nakihitaji kutoka kwake,
namba ya simu tu. Unajua katika maisha ya kuchati facebook huwa yanachosha sana,
kuna kipindi fulani automatically unatokea kummisi mtu fulani na ungependa sana
awe online lakini hayupo online, unapokuwa na namba ya simu, inakupa wakati
mzuri wa kumsikia na kumjulia hali katika kipindi chochote ambacho ungependa
kumsikia.
Ucheshi ndio ulikuwa kawaida yangu ila katika kipindi hiki
nilikuwa nataka kuuleta ucheshi mpaka katika maandishi. Aziza akaonekana
kulifurahia hilo, akaonekana kuanza kunikubali japokuwa hatujawahi kuonana hata
siku moja. Nilikuwa bize na chatting na Aziza, sikutaka kuwasiliana na mtu
mwingine katika kipindi hicho japokuwa nilimuona Eduado, Ibra Akilimia na
Emmanuel Solo walikuwa wamenitumia meseji.
Nilikuwa nikijitahidi sana
kumuingiza Aziza kwenye himaya yangu, yaani aingie bila kupenda na mwisho wa
siku kila kitu kiwe poa sana. Sikujali alikuwa akiishi wapi, sikujali na mimi
nilikuwa nikiishi wapi, kitu ambacho nilikuwa nikikiamini ni kwamba mapenzi wala
hayakuwa na hiyana, yalikuwa hayabagui watu kama tulivyo
wanadamu.
AZIZA: Nikuulize kitu.
MIMI:
Niulize tu.
AZIZA: Unasoma?
MIMI: Hapana.
AZIZA:
Unafanya kazi?
MIMI: Hapana.
AZIZA: Sasa unafanya
nini?
MIMI: Nipo nipo nyumbani. Nilisoma kidato cha kwanza, sikuwa na
fedha za kuniendesha kielimu, nikaachana nayo mpaka sasa hivi. Kuna kipindi
nilipata vijisenti mara baada ya kubeba sana mizigo Tandale sokoni, nikaenda
kusoma English Course.
AZIZA: Kwa hiyo haufanyi kazi?
MIMI:
Yeah! Sifanyi kazi.
AZIZA: Unafanya kitu gani kingine?
MIMI:
Sifanyi chochote kile.
AZIZA: Ila niliona kama unaandika hadithi! Au
majina yamefanana?
MIMI: Yeah! Huwa ninazipost tu.
AZIZA:
Hadithi zile huwa unaandika wewe?
MIMI: Hapana.
AZIZA: Sasa
huwa anaandika nani?
MIMI: Anaandika baba na kisha mimi kuzichukua na
kuziweka facebook.
AZIZA: Unanidanganya Nyemo.
MIMI:
Nikudanganye ili iweje? Kuna tuzo ya uongo wanapewa waongo? Huo ndio
ukweli.
AZIZA: Mmmh! Basi mpe hongera baba yako.
Mimi:
Zimefika.
Wakati mwingine haitakiwi kuwa mkweli
kwa kila kitu. Tayari nilikwishaona kwamba kagundua kwamba sisi ni watu
tunaoishi sehemu mbili tofauti, madaraja mawili tofauti na katika kichwa chake
aliamini kwamba Tandale wanaishi watu masikini japo haikuwa hivyo. Nilichokuwa
nikikifanya ni kuendana na akili yake alivyokuwa ameiweka, nami nikaanza
kujifanya masikini ambaye sikubahatika kusoma kwa kuwa sikuwa na fedha ya
kuniendeleza kielimu. Nikafanikiwa, kwa kiasi fulani aina ya maisha ambayo
nilimpa yalimfanya kuamini kwamba kweli nilikuwa mtoto wa uswahilini,
nilijivunia kuishi Tandale katika uwepo
wake.
Maisha yalikuwa yakiendelea kama kawaida,
kuhusu Aziza, wala sikuwa na wasiwasi kwa kuamini kwamba piga ua huyu mtoto ni
lazima ningemchukua bila tatizo lolote lile. Kila siku nilikuwa nikiwasiliana
nae, alikuwa akionekana kunikubali sana, chatting zangu zilizokuwa zikitabasamu
zikaonekana kuuteka moyo wake. Nilikuwa na marafiki wengi facebook lakini
nikikaa bila kuchati na Aziza sikuwa nikijisikia furaha
kabisa.
Japokuwa Eduado alikuwa amenipa ishu ya kumfuatilia Aziza kama
mchezo fulani lakini kadri siku zilivyokuwa zikizidi kwenda mbele na ndivyo
ambavyo nami nikazidi kufall inlove. Nilikuwa nikipenda sana Aziza, kila
nilipokuwa nikiingia facebook na kumkosa, sikuwa nikijisikia raha
kabisa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kuna nyakati za
shida zikaingia, nyakati ambazo sikuweza kumuona Aziza online. Katika nyakati
hizo maisha yalikuwa ya tabu sana, nilikuwa nikikosa furaha hata katika maisha
ya kawaida. Nilimzoea sana Aziza, nilimpenda sana Aziza kwa hiyo kutokuuona
uwepo wake machoni mwangu kilikuwa ni kitu ambacho kiliniumiza
sana.
MIMI: Eduado vipi?
EDUADO: Poa.
Inakuwaje?
MIMI: Kama kawa. Mbona Aziza simuoni siku
hizi?
EDUADO: Tupo kwenye mitihani kaka.
MIMI: Sasa mkiwa
kwenye mitihani ndio haruhusiwi kuwa online? Mbona wewe upo?
EDUADO:
Mimi si unajua mbishi kaka.
MIMI: Dah! Nimemmisi sana Aziza.
Nimemmisi ile mbaya kaka.
EDUADO: Usijali kaka. Mitihani ikiisha
atakurudi online tu.
MIMI: Poa. Ila mnamaliza lini?
EDUADO:
Wiki ijayo.
MIMI: Duh!
EDUADO: Nini tena
kaka?
MIMI: Nahisi kama nitakufa kwa mawazo. Nahisi nitaweza kufa
kaka.
EDUADO: Usijali kaka. Wewe vumilia tu utakula
mbivu.
MIMI: Poa kaka.
Katika kipindi
hicho ndicho nikajua kwamba moyo wangu ulikuwa ukimpenda sana Aziza. Huyu Aziza
ndiye ambaye alinifanya niwaone wasichana wote kuwa wa kawaida sana, yeye ndiye
aliyenifanya nimuone kuwa msichana mzuri kuliko wasichana wote duniani. Uwepo
wake katika mtandao wa facebook bado nilikuwa nauhitaji sana, nilikuwa
nikijisikia mpweke kupita kawaida. Aziza...Aziza...Aziza...upo wapi wewe
msichana uje kuupoza moyo wangu ulio kwenye maumivu makali?
Siku
zikaendelea kukatika na hatimae siku ambayo ilionekana kunifurahisha ikawadia.
Siku hiyo nikawa kama nimepigwa na mshtuko mkubwa moyoni, sikuamini kile ambacho
kilikuwa kikionekana machoni mwangu, Aziza alikuwa online. Sikutaka kupoteza
muda, sikutaka kuleta pozi, kwa haraka sana nikamtumia
meseji.
MIMI: Mungu wangu!
AZIZA: Nini
tena.
MIMI: Umekuja at last.
AZIZA: Yeah! Nilipotea kwa
kipindi fulani hivi, si unajua mitihani wangu.
MIMI: Pole sana.
Mmekwishamaliza?
AZIZA: Yeah! Tumekwishamaliza. Ila nami nilikumisi
sana.
MIMI: Nashukuru kwa kunimis, ila ulimiss nini kutoka
kwangu?
AZIZA: Chatting zako, meseji zako zimekaa kitofauti sana na
watu wengine.
MIMI: Kivipi?
AZIZA: Zipo kitofauti sana.
Katika maisha yangu nimewahi kuchati na watu wengi sana, ila
zako...dah!
MIMI: Bado haujaniambia kivipi.
AZIZA: Kwanza
hauandiki kimkato kama neno ‘sijui kuliandika cjui’, yaani maneno ya mikato huwa
hauitumii kabisa.
MIMI: Kwani hiyo nayo ni sababu?
AZIZA:
Ngoja nikwambie kitu Nyemo. Hii ni siri ambayo wanaume wengi wamekuwa hawaielewi
na ndipo wanapofanya makosa kila siku.
MIMI: Siri
gani?
AZIZA: Unajua unapochati na msichana yeyote ambaye haujawahi
kuonana nae, unatakiwa kuonyesha nidhamu ya hali ya juu, hiyo ndio sifa moja
kubwa ya kumteka msichana kwa sababu hisia zetu hazitekwi na mambo makubwaaa,
hapana, hivi vitu vidogo vidogo ambavyo wavulana wanavipuuzia ndio
vinatuteka.
MIMI: Kama vitu gani.
AZIZA: Cha kwanza salamu
Nyemo. Hivi unajua kwa sababu gani meseji yako ya kwanza kabisa uliyowahi
kunitumia sijakujibu?
MIMI: Hapana. Sijajua kwa nini.
AZIZA:
Salamu. Wanawake wengi wanalichukulia tofauti neno ‘mambo’. Unapomsalimia
msichana kwa mara ya kwanza kwa kumwambia ‘Mambo’, wanaojibu ni wachache
sana.
MIMI: Kwa nini sasa?
AZIZA: Kwa sababu mwanamke
anapenda kufuatwa kinidhamu.
MIMI: Sasa nilitakiwa kukusalimia vipi
ili ujibu?
AZIZA: Unapomfuata msichana yeyote duniani, anza kwa
kumsalimia ‘Habari yako’ au salamu yoyote iliyokaa kinidhamu. Kidogo ukisalimia
hivyo, kuna asilimia kubwa sana ya msichana kukujibu.
MIMI: Duh!
Kumbeee!
AZIZA: Yeah! Hiyo ni siri ya kwanza Nyemo, wavulana wengi
huwa wanafeli hapo tu kitu ambacho kinawafanya kila siku kulalamika kwamba
wasichana tuna mapozi kujibu salamu zao, hapana, hatuna mapozi bali wanakosea
kusalimia, wanakosa nidhamu katika kusalimia.
MIMI: Nimekuelewa.
Naomba siri nyingine.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
AZIZA: Chatting.
Unajua usipende kuchati na msichana kifupi kama nilivyokueleza toka mwanzo.
Andika neno lote kwa ujumla, unajua unapoandika kifupi, unaupa kazi ubongo wa
mtu kulifikiria neno na matokeo yake akili yake inachoka na kukatisha chatting
na wewe.
MIMI: Ila mimi sijawahi kuchati namna hiyo
Aziza.
AZIZA: Najua. Ila ninakumegea siri juu ya vitu ambavyo msichana
anavipenda na vile asivyovipenda.
MIMI: Dah! Umeifungua akili
yangu.
AZIZA: Ila wewe..dah! Wewe mtu noma.
MIMI: Kwa
nini?
AZIZA: Kama kuna msichana ulichati nae halafu akaonekana kuchoka
na chatting zako, basi hakika hatoweza kuridhika na chatting za mtu yeyote yule
duniani.
MIMI: Hahaha! Kwa nini?
AZIZA: Unaandika maneno kwa
ujumla, hauandiki vifupi, cha kushangaza sasa
MIMI:
Kipi?
AZIZA: Unafuatilia mpaka alama za maandishi. Penye kiulizo,
unaweka, penye nukta, unaweka, penye mkato, unaweka, penye alama ya mshangao,
unaweka. Nimekuvulia kofia.
MIMI: Hahaha! Ni kawaida sana Aziza.
Napenda kuchati na mtu katika staili ya kuandika hadithi.
AZIZA:
Hongera yako. Naomba nikuulize swali.
MIMI: Uliza tu.
AZIZA:
Ulinimis?
MIMI: Sana tu.
AZIZA: Ulimiss nini kutoka
kwangu?
MIMI: Chatting na mambo mengine.
AZIZA: Kama
yapi?
MIMI: Uzuri...koh koh koh
AZIZA: Hahaha! Hebu acha
kunitania, umewahi kuniona mpaka useme mimi mzuri?
MIMI: Unajua
unapoongea na msichana usiyemfahamu simuni halafu ukasikia sauti yake, unajua tu
kwamba huyu mzuri na huyu mbaya.
AZIZA: Sasa kwani mimi umeisikia
sauti yangu?
MIMI: Hata unapochati na mtu, mwandiko wake unajionyesha
kwamba huyu mzuri na huyu mbaya. Ila kuna kingine pia.
AZIZA:
Kipi?
MIMI: Nilichogundua ni kitu kimoja. Wasichana wengi wanaoweka
profile picha zao picha za wanawake maarufu wazuri, huwa wabaya. Ila walioweka
picha za profile zao kama maua au midoli, huwa ni wanawake
wazuri.
AZIZA: Hahaha!
MIMI: Yeah! Hii ni kwa sababu yule
msichana mbaya kamuweka Rihanna kwa sababu anataka kutuonyesha kwamba yeye ni
mzuri ila yule aliyoweka picha ya ua anataka kutuonyesha kwamba yeye ni mtu wa
thamani, mzuri na ananukia kama ua au mdoli. Nililifuatilia hilo kwa marafiki
zangu wengi na nikaligundua.
AZIZA: Kweli wewe mfuatiliaji. Kwa hiyo
ukagundua mimi kuwa ni mzuri?
MIMI: Yeah! Nimegundua hilo kiasi
ambacho kama nitaambiwa niombe kitu kimoja duniani nacho kitafanikiwa, basi
ningeomba kuwa na wewe, basi.
AZIZA: Hahah! Acha utani
Nyemo.
MIMI: Kwani naonekana kutania?
AZIZA:
Yeah!
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
**************************
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment