Search This Blog

Monday, October 24, 2022

GUBERI LA KIMANYEMA - 2

 





    Chombezo : Guberi La Kimanyema

    Sehemu Ya Pili (2)



    “Hidaya, tafadhali unielewe. Tuko peke yetu muda huu, na tuko ndani ya gari. Hakuna anayetuona. Tafadhali Hidaya, niruhusu nikubusu japo kidogo…”

    “Hilo tu?” Hidaya alimuuliza kwa sauti ya chini.

    “Ni hilo tu, Hidaya, mpenzi.”

    Ukimya mfupi ukatawala. Hidaya akashusha pumzi ndefu. Kiwembe akahisi kuwa tayari kibali kimetolewa. Akautupa mkono juu ya paja la Hidaya, paja lililonona. Mkono huo ukateleza taratibu juu ya paja hilo. Hidaya akabadilika, hema yake ikawa ya taabu. Kiwembe hakuishia hapo, mara akaupeleka mkono kwenye titi moja la Hidaya na kuanza kulitomasatomasa huku akiuwinda ulimi wa Hidaya.

    Muda mfupi baadaye wakawa katika hatua ambayo walishindwa kustahimili, nguo zikachojolewa. Gari la kifahari, Mercedes Benz 320 SE likageuzwa kuwa gesti. Hidaya na Kiwembe wakaifurahia dunia mpya. Huo ukawa ni mwanzo wa uhusiano wa penzi la wizi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Penzi kati yao likakua na kumea. Wiki tatu baadaye walikuwa wameshaingia gesti bubu kadhaa katika maeneo ya Buzebazeba, Mwanga-Majengo na Gungu, wakizifurahisha nafsi zao kwa namna waliyotaka.

    Hata hivyo pamoja na kuwa walijitahidi sana kuufanya siri uhusiano wao wa kiroho na kimwili, wakijinafasi katika gesti za mafichoni, bado hiyo haikuwa ‘dawa’ ya kuwatia upofu watu wachache wanaowafahamu. Umaarufu wa Khalifa Mwinyimkuu na mkewe ulizagaa takriban Manispaa nzima ya Kigoma/Ujiji. Watu wengi waliwafahamu, hivyo kati ya hao, mmoja wao alimwona Hidaya akiingia katika gesti moja eneo la Mwanga- Majengo saa 2 usiku huku akionyesha wazi kuwa hakutaka kutambulika.

    Mwingine walipishana kwenye korido ya gesti fulani katika kitongoji cha Buzebazeba, Ujiji, Hidaya akiingia akiwa amekumbatiana na Kiwembe huku jamaa huyo akitoka.

    Minong’ono ya wambea ikazagaa kwa kila aliyemfahamu Khalifa Mwinyimkuu na Hidaya Sufiani. Minong’ono hiyo iliendelea kuzagaa hata ikayafikia masikio ya Khalifa Mwinyimkuu mara tu alipotoka katika moja ya safari zake za kibiashara. Na kama hakuna siri duniani, ni kipi kingemfanya bwana huyo asipate habari?

    Alizipata! Ndiyo, alizipata, lakini kwa kuwa hakuwa mshiriki sana wa maneno ya hisiahisia, yasiyokuwa na uthibitisho wowote, wala hakupenda kushiriki kwenye vibaraza vya kahawa ambako huenda angezisikia tetesi, alizipuuza habari hizo.

    Siku zikaja, siku zikapita akiendelea kuzipuuza habari hizo. Lakini jambo la kusikia lina maudhi na maumivu yake. Linauma ingawa halitoi damu. Chukulia kuwa siku moja uko na rafiki yako wa karibu, rafiki mliyeshibana, halafu anapita mwanamume mmoja mbele yenu. Baada ya mtu huyo kupita, rafiki yako anakunong’oneza, “Unamwona huyo mshikaji?”

    Labda na wewe unaitika, “Ndio, nimemwona. Vipi?”

    Rafiki yako anakukazia macho na kutamka kwa msisitizo, “Ukae ukijua kuwa huyo nd’o mume mwenzio.”

    Utajisikiaje baada ya kusikia hivyo?

    Japo Khalifa Mwinyimkuu hakuwa mtu wa kupokea habari ambazo hakuzithibitisha mwenyewe lakini taarifa ya rafiki yake mmoja wa siku nyingi kuhusu nyendo za mkewe, hakuichukulia kama aina nyingine ya habari za uzushi na umbea. Hapana, taarifa hiyo aliipa uzito wa juu, akaamua kuifanyia kazi.

    Kila kikeracho moyo kina mwisho wake wa uvumilivu. Khalifa Mwinyimkuu alishindwa kuvumilia zaidi. Akaamua kufanya uchunguzi huo baada ya kuona mabadiliko fulani katika mienendo ya mkewe, Hidaya. Tangu alipotoka safari Hidaya hakuonesha kuwa na furaha wanapokuwa pamoja. Na isitoshe, katika wiki nzima ambayo alikuwa amerudi, Hidaya hakuwa amempa unyumba kwa kutoa visingizio hivi na vile.

    Hidaya alikuwa amebadilika. Hakuwa akimliwaza kama ilivyokuwa kawaida yake. Hawakuwa wakicheka pamoja, wakichekea penzi lao.

    Je, kwa tabia hiyo kwa nini Khalifa Mwinyimkuu asiamini kuwa mkewe ana mwanamume wa nje aliyemmalizia hamu yake ya mapenzi? Ndipo alipoamua kufanya uchunguzi wa kumjua huyo aliyemzuzua mkewe, Hidaya.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Khalifa Mwinyimkuu alishangaa, akasononeka. Akawaza, iweje Hidaya afanye uhuni kiasi hicho? Ni shida ipi inayomsumbua? Hakuwa na familia ya kuitunza. Familia ya ndugu wa mume ilikuwa ikijitunza yenyewe. Kipi sasa kimfanye awe malaya?

    Aliishi katika nyumba kubwa, nzuri iliyoenea kila kitu ndani. Alipewa gari zuri la kutembelea. Ni kipi kingine alichohitaji? Roho ya mtu?

    Hakupata jibu.

    *****

    JAPO Hidaya alimtaarifu Kiwembe bayana kuwa baba mwenye nyumba kishahisi jambo, na kumtaka wasitishe mawasiliano kwa muda, hata hivyo Kiwembe hakukubali. Alishanogewa. Ndiyo, alishanogewa na kwa ujumla wote walinogewa kiasi cha kufikia hatua ya siku nyingine Kiwembe kuja hapo nyumbani ambako alipata maakuli kabla ya kujichimbia chumbani na kufanya yale waliyopenda kuyafanya.

    Hidaya alikuwa mjanja. Alibaini kuwa mumewe kishamhisi siku alipomuuliza maswali ya kimtegomtego kuhusu ratiba zake za kutoka nyumbani. Kwa hali hiyo, siku ya pili tu walipokuwa na Kiwembe katika gesti fulani kwenye kitongoji cha Buzebazeba, ndipo alipoamua kumtaarifu kuhusu hadhari wanayopaswa kuichukua.

    Na ni hapo ndipo Hidaya alipogundua kuwa kwa Kiwembe kutokuwa na simu ni tatizo kubwa. “Ungekuwa na simu…” alimwambia na kuiacha sentensi hiyo ikielea.

    “Ningekuwa na simu, lakini sina, na pesa za kuinunua hiyo simu sina,” Kiwembe alisema kwa unyonge.

    Hidaya alifikiri kidogo kisha akasema, “Any way, nipe siku mbili, tatu hivi. Nitakununulia simu ya bei ya kawaida. Lakini kwa siku tatu tusionane. Usije nyumbani, umenielewa?”

    “Poa,” Kiwembe alijibu kwa unyonge. Akilini mwake hakuwa tayari kumkosa Hidaya hata kwa siku mbili.

    ‘Haiwezekani,’ alijisemea kimoyomoyo. Akajigamba mwanasagamba, kwani sagamba haiogopi lami wala kokoto. Na wala kijiko cha jikoni hakiogopi moto. Kichaa hicho! Kiwembe akafikia hatua ya kuwa na wivu, akitaka penzi analopewa na Hidaya asipewe mtu mwingine! Hata mumewe!

    Ndiyo, alitaka awe yeye tu!

    Yeye peke yake!

    Akawa na hamu ya kuwa naye kila wakati, akifaidi wepesi wake kitandani sanjari na manung’uniko yake ya faraja yaliyomtoka kwa sauti ya kipekee iwezayo kumsisimua rijali yeyote.

    Ni jana tu walipokuwa pamoja, na wakakubaliana Kiwembe asidiriki kutia mguu tena nyumbani kwa Hidaya. Lakini Kiwembe kwa uchu wake na ukichaa wake hakuweza kutii makubaliano yao. Saa 9 alasiri akawa ameshakanyaga nje ya geti la nyumba ya kifahari ya mzee Khalifa Mwinyimkuu. Akabonyeza kengele ya wito.

    Hidaya akiwa hategemei kuwa Kiwembe angethubutu kukiuka makubalianao yao, alikwenda kufungua geti. Mshtuko alioupata baada ya kufungua geti hilo ulikuwa nusura umtoe ruho. Japo wakati huo Khalifa Mwinyimkuu hakuwepo, hata hivyo Hidaya alighadhibika. Hasira zikampanda kwa kiwango cha juu.

    “We vipi?” alibwata huku akimtazama kwa macho makali. “Kwani tumeongeaje jana?”

    Kiwembe hakujibu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nakwambia kwa mara ya mwisho, usije tena, ondoka! Mume wangu akija sasa hivi na kukukuta hapa utasema nini? Ama mimi nitajielezaje?”

    Kufoka kote huko kwa Hidaya, machoni na masikioni mwa Kiwembe ilikuwa kama sinema ifurahishayo.

    “Sikiliza mpenzi, Hidaya,” Kiwembe alisema huku akichekacheka. “Acha jazba. Piunguza ukali. Nakuomba uelewe tu kuwa nisipokuona japo kwa siku moja tu, basi jinamizi huja na kuniiinamia…”

    “Koma!”

    “Tafadhali Hida…”

    “Toka!”

    “Nisikilize taf…”

    “Koma we! Nakwambia tena koma! Uniondolee upuuzi wako hapa!”

    Pamoja na ukali wote huo wa Hidaya, hata hivyo Kiwembe aliondoka huku roho yake ikiwa imesuuzika. Kumwona Hidaya na kuisikia sauti yake ilikuwa ni hatua kubwa sana kwake.

    *****

    SIKU zilipita, wiki zikaenda hatimaye miezi miwili ikakatika. Sasa hali ya amani, furaha na upendo ikarejea ndani ya nyumba ya Khalifa Mwinyimkuu na mkewe, Hidaya. Ule wasiwasi wa kulindana ukatoweka. Kila mmoja akawa na furaha na mwenzake. Lakini Hidaya hakuwa na furaha iliyotimilika. Katika ndoa yao kulikuwa na dosari iliyopaswa kutafutiwa ufumbuzi.

    Ile haki ambayo kila mmoja alistahili kuipata katika ndoa, Hidaya hakuipata. Na kulikuwa na sababu. Khalifa Mwinyimkuu alikuwa ni mwanamume, ndiyo. Lakini alikuwa na udhaifu uliosababisha Hidaya asiifurahie ndoa yake. Kila usiku ulipoingia, na wanandoa hao kulakiwa na kitanda, hakukuwa na chochote cha ziada kilichotokea ambacho kilimfanya Hidaya ajione kuwa yuko katika maisha ya ndoa.

    Usiku ulipita kama ulivyo, mapambazuko yakawakuta kama walivyokuwa. Tatizo la Khalifa Mwinyimkuu kutomtimizia haja zake Hidaya, lilianza baada ya kupata ajali mbaya akiwa safarini Arusha. Miongoni mwa athari zilizomkuta baada ya ajali hiyo ni kupungukiwa na nguvu za kiume kwa kiwango cha juu hivyo kutokuwa na uwezo wa kufanya tendo la ndoa na mkewe kwa kiwango kinachoridhisha.

    Pamoja na amani kurejea ndani ya nyumba yao, hata hivyo bado Hidaya alijisikia kuteseka kwa kukosa kile alichokihitaji. Hali hiyo ikamfanya awe na msukumo fulani uliomtia kishawishi.

    Ndipo ikaja siku. Ilikuwa ni siku ya kawaida tu kwake, akiwa katika safari zake za kawaida za sokoni. Siku hiyo alikwenda katika soko kuu la Kigoma mjini. Wakati alipoegesha gari tu, akamwona Kiwembe hatua chache kando ya gari. Kiwembe alikuwa na safari zake za kawaida zisizokuwa na malengo maalumu. Lakini alipomwona Hidaya akiegesha gari kando ya soko hilo, naye akasitisha safari yake. Akamfuata na kumsalimia.

    Hidaya naye akifurahia kukutana kwao, baada ya kusalimiana akasema, “Kiwembe nimekukumbuka. Lakini hapa wanga wengi. Tuonane wapi? Sema haraka.”

    Kiwembe aliwaza harakaharaka na kukosa jibu sahihi. Angesema wakutane wapi ilhali yeye hana pesa za kukodi chumba gesti?

    “Pesa, Hidaya. Sina kitu.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Usijali,” Hidaya alimdaka huku akiangaza huku na kule kwa kumhofia mumewe.

    Wakakubaliana haraka kuwa siku isiyokuwa na jina wakutane kwenye hoteli fulani wakumbukie.

    *****

    KHALIFA Mwinyimkuu hakuwa mjinga. Pamoja na ukimya wake wote, pamoja na upendo aliouonyesha kwa mkewe kwa siku zote hizo, hata hivyo kwa siri aliendelea kuzifuatilia nyendo zake kwa makini sana. Hakufanya papara, kwa kuwa alihitaji kuthibitisha mwenyewe hicho anachokitilia mashaka.

    Akawapa tenda vijana watatu wa ‘njaa-njaa,’ tenda ya kumfuatilia kwa siri Hidaya. Kila mmoja katika vijana hao akapewa 10,000/-. Naam, pesa ni sabuni ya roho.Vijana hao walipopewa tenda wakaingia kazini. Wakawa wakimfuatilia Hidaya kila alikokwenda, na asubuhi ile ambayo Hidaya alikutana na Kiwembe sokoni, vijana wale wakashangaa na kushtuka. Wakati walipopewa kazi hiyo na Khalifa Mwinyimkuu, aliwadokeza juu tetesi alizowahi kuambiwa kuhusu uhusiano wa Kiwembe na Hidaya.

    Hivyo, kuwaona Hidaya na Kiwembe wakizungumza kuliwafanya wazidi kuwafuatilia, na zaidi wakiwa wanamfuatilia Hidaya. Na taarifa za mwisho zilipomfikia Khalifa Mwinyimkuu, papohapo akaisereresha Land Cruiser barabarani kwenda kushuhudia. Bado hakuwa na papara hata pale alipowaona Hidaya na Kiwembe wakiingia ndani ya hoteli ile nzuri. Alivumilia japo moyo ulimuuma.

    Aliwaona, lakini akawapa muda, wastarehe wapendavyo.





    MLANGO uligongwa mara tatu mfululizo. Kiwembe na Hidaya wakashtuka, wakatazamana. Haikuwa siri, mshangao uliwakumba, hofu ikawatawala. Namna mlango ulivyogongwa iliashiria shari tupu. Kiwembe na Hidaya wakatazamana kama vile wanaoulizana, “Tufanyeje?”

    Na labda walikuwa na haki ya kushangaa na kujawa na hofu. Hii hoteli ya Kimondomondo iko nje ya mji, ni kilometa kadhaa kutoka kwenye makutano ya Barabara za Kasulu na Mwandiga. Ni hoteli iliyokuwa kando ya barabara ya Kasulu, jirani na kijiji cha Msimba.

    Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kukutana hapo, na waliamua kufanya hivyo katika kuepusha uwezekano wa kufumaniwa. Kuendelea kuzitumia gesti za Mwanga, Mwanga-Majengo, Buzebazeba, Gungu na kwingineko katikati ya mji waliona sio vizuri. Walihitaji kupata sehemu iliyotulia na ambayo pia itawafanya akili zao zitulie na wastarehe kwa uhuru.

    Siku hiyo walipokuja hapo Kimondomondo Hotel, Hidaya alilipa gharama zote zilizohitajika ili kuondoa usumbufu wa aina yoyote toka kwa wahudumu. Shilingi 30,000 zikamtoka Hidaya kwa kukimiliki chumba kwa saa 24 tu!

    Takriban nusu saa baada ya kustarehe ndipo waliposikia mlango ukigongwa kwa namna iliyoonyesha kuwa hakuna heri. Vichwani mwao waliamini kuwa hata kama mhudumu angewajia kwa dharau yoyote, basi angegonga mlango huo kwa ustaarabu.

    Ndiyo, walishtuka, wakashangaa, wakaghadhibika na kugwaya. Hidaya aliyekuwa kifuani pa Kiwembe akidhihirisha ule utaalamu na wepesi wa viungo vyake, alisitisha zoezi hilo ghafla. Akaking’atua kinywa chake kilichokuwa kimegandana na kinywa cha Kiwembe, ndimi zao zikisumbuana katika namna iliyowaongezea msisimko.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sasa Hidaya aliikita miguu yake mmoja huku na mwingine huku, hali kadhalika, mikono. Akabaki akimtazama Kiwembe aliyekuwa chali. Kati yao hakuna aliyekuwa hata na kipande cha nguo mwilini.

    Mlango ukagongwa tena! Hidaya akajitoa kabisa kitandani. Akasimama juu ya zulia zito lililoifunika sakafu ya chumba hicho. Akashusha pumzi ndefu huku akitetemeka kwa mbali. Kiwembe naye akajitoa kitandani.

    Mlango ukagongwa tena, safari hii kwa nguvu zaidi.

    “Vaa!” Hidaya alimhimiza Kiwembe huku yeye akiwa amekwishazivamia nguo zake na kuanza kuvaa.

    Muda mfupi baadaye wote walikuwa wameshavaa nguo zao. Wakatazamana kwa hofu.

    Mlango ukagongwa tena, kisha sauti kali ikasikika: “Fungua!”

    Kiwembe akawa akitetemeka. Kiroho kikawa juu. Akatangatanga chumbani humo akitafuta pa kukimbilia, asipaone. Akafungua dirisha la chumba hicho na kuchungulia nje. Akagwaya. Dirisha lenyewe lilikuwa na nondo imara, hivyo ni dhahiri asingeweza kupita. Halafu, chumba hicho kilikuwa ghorofani. Ghorofa ya tatu!

    Chozi likamtoka Kiwembe. Hakujua afanye nini. Akamlaani sana Mama Kadala aliyempachika sifa ya ‘kichaa wa mapenzi’ kwa laana ya mapenzi. Akamlaani Mama Kadala aliyemwingiza katika hatia, jimama lililomshawishi penzi wakati yeye halijui penzi, likamfanya abalehe kabla ya wakati na kukumbwa na kichaa cha mapenzi kiasi cha kuwa ni mtu ‘anayependa’ bila ya kutazama huyu ni nani na ni wa nani.

    Moyo ulimdunda kwa nguvu. Kila alilobuni katika kujiokoa aliona halifai. Akamtazama Hidaya na kumwambia kwa sauti ya kutojiamini, “Fungua.”

    Hidaya akaufuata mlango huku nguvu zikimomonyoka miguuni. Na alipoufungua hakuamini macho yake.

    Khalifa Mwinyimkuu alikuwa mlangoni akiwatazama kwa zamu. Haikuwa siri, macho yake makali yaliitangaza bayana hasira iliyojikita moyoni mwake.

    Na kilikuwa ni kipindi kigumu zaidi kwa Kiwembe. Alichanganyikiwa. Sasa uwanaume wake wote ulitoweka. Mbona wakati anamlia ‘vyake’ alikuwa akimchukulia kama mume mwenzake? Hata akadiriki kumtania Hidaya kwa mzaha wa mapenzi eti ‘nitukanie mumeo…ananikera…ananikosesha uhuru wa kulifaidi penzi lako.’

    Ni muda mfupi tu uliopita Kiwembe alimwambia hivyo Hidaya, na Hidaya naye akafanya kama mpenzi wake alivyotaka. Hidaya! Akadiriki kumkashifu na kumtukana mumewe matusi yenye uzito wa kutosha kuua mtu. Wakati huo ndio walikuwa kwenye kilele cha mapenzi!

    Sasa! Ndiyo, sasa kishayasahau yote hayo. Mwili wote unamtetemeka. Khalifa Mwinyimkuu yuko mbele yao, ni kipi kitakachofuata?

    Khalifa alimkodolea macho Kiwembe. Kisha, kwa sauti nzito, iliyosheheni tani kadhaa za hasira, alisema, “Samahani kwa kukukatiza starehe zako na kukupotezea muda wako. Lakini unanifahamu?”

    Kiwembe alihisi sauti ikimkwama. Akabaki akimkodolea macho Khalifa Mwinyimkuu.

    “Nakuuliza wewe,” Khalifa Mwinyimkuu alifoka. “Nakuuliza kwa mara ya mwisho. Unanifahamu?”

    “Hapana, mzee,” Kiwembe alijibu kwa sauti iliyojaa kitetemeshi. “Kwa kweli leo nd’o mara yangu ya kwanza kukuona.”

    Khalifa Mwinyimkuu aliachia cheko dogo la dhihaka. Kisha: “Unakiri kuwa hii ndio mara yako ya kweanza kuniona. Je, huyo mwanamke?”

    Lilikuwa ni swali gumu kwa Kiwembe. Akashindwa kupata jibu la haraka, akizisoma hasira za wazi katika paji la uso wa Mwnyimkuu. Aliamini kuwa pupa yoyote katika kujibu ingmletea majuto baadaye.

    Khalifa Mwinyimkuu alipoona Kiwembe kawa’bubu’ akafoka tena: “Ok, twendeni!”

    Ilikuwa ni amri ambayo Kiwembe hakuipenda, lakini angefanya nini wakati yeye kashika makali na mpini umekamatwa na mtoa amri?

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ingieni garini!” amri nyingine wakati walipofika nje, mbele ya hoteli hiyo ya Kimondomondo.

    Ndani ya gari hilo wote waliketi mbele kwa amri ya Khalifa Mwinyimkuu, mtu aliyeogopwa kama jicho liogopavyo mchanga. Gari lilisimamishwa nje ya jengo lilelile ambalo Kiwembe alizoea kuliona na mlango uleule ambao alizoea kuugonga na kufunguliwa na Hidaya.

    Kwa amri nyingine Khalifa akawashinikiza kuingia ndani na kuketi sebuleni, katika masofa ya kifahari yaliyoipendezesha sebule hiyo. Lakini sasa ‘wapenzi’ hao waliketi mbalimbali huku Khalifa Mwinyimkuu akiwa ameketi kwenye kiti cha kawaida, akiwatazama.

    “Sikiliza, mjomba,” Khalifa Mwinyimkuu aliukata ukimya uliokuwepo. “Ni ukweli wako tu ndio utakaokuwa kinga ya kunifanya nikuonee huruma. La sivyo, nitakutia kilema sasa hivi; nitayatoboa hayo macho yako yasiyotulia kisha niliteremshe bega la kushoto, halafu nikupindishe kiuno.”

    Licha ya kutamka maneno hayo kwa upole, bado hasira isiyo kifani ilikuwa wazi usoni pake. Macho yake makali ni kama vile yalikuwa yakimwambia “NITAKUUA.”

    Alitisha!

    “Unafanya mapenzi na mke wangu,” aliendelea. “Na muda huu mmetoka kufanya mapenzi. Bisha! Na si unafahamu kuwa ni hatari kucheza na mke wa mtu? Ama hujui kuwa kucheza na mke wa mtu ni sawa na kucheza na kifo? Na hujui kuwa mtu akifumaniwa na mwenye mke, akauawa, muuaji hatakuwa na hatia?

    “Sanasana itaeleweka tu kuwa muuaji kaua bila ya kukusudia kwa uchungu wa mkewe kuchukuliwa na kinyangarika fulani. Na kama ni mimi ndiye nitakayekuwa natuhumiwa kwa kuua mbwa kama wewe, sitakuwa na hofu yoyote. Nina pesa, na mbele ya pesa hakuna linaloshindikana. Hata kwa akili yako finyu najua unalitambua hilo.

    “Unajua hivyo? Kama ni uongo, bisha, ufe. Ok, tuachane na hayo mengine. Kwa kifupi kaa ukijua kuwa kitakachokuponya ni ukweli wako tu!”

    Abishe! Kiwembe aliwaza. Hilo halikukubalika kichwani mwake japo alitambua fika kuwa hiyo ni sheria yake (Khalifa) binafsi na wala sio sheria ya serikali. Alichojua ni kwamba adhabu zinatofautiana kati ya aliyeua kwa kukusudia na yule aliyeua bila ya kukusudia. Lakini wote wana hatia.

    Alikumbuka kuwa aliwahi kusoma gazeti moja na kukuta habari iliyomhusu mama mmoja aliyempiga kofi kali sana la shavuni mwanae mwenye umri wa miaka mitano, kisa, alidokoa kipande cha nyama jikoni. Kofi lile lilizaa kifo cha mtoto yule saa moja baadaye akiwa hospitalini. Mama akabeba kesi ya kuua.

    Kwa Kiwembe aliamini kuwa marehemu alitenda kosa, na adhabu ilikuwa ni moja ya njia ya kumkanya katika ule utaratibu wa ‘samaki mkunje angali mbichi.’ Haikumwingia akilini Kiwembe kuwa mama mwenye akili timamu anaweza kudiriki kumwua mwanaye wa kuzaa kwa kosa la kudokoa kipande cha nyama mekoni.

    Alichofanya mama kutoa onyo, lakini kwa bahati mbaya onyo lenyewe likawa na uzito wa tani nyingi kwa mlengwa.

    Kwa mtazamo wake, Kiwembe, hukumu ya mama huyo ingekuwa ni ya mtu aliyeua bila ya kukusudia. Haya maneno ya Khalifa Mwinyimkuu, hayakuwa na ukweli wowote kichwani mwa Kiwembe. Lakini alihofia kutamka hivyo kwani tayari ameshaambiwa “Kama ni uongo, bisha, ufe.”

    Akabaki kaitumbulia macho sakafu, akiomba ipasuke, adidimie ili ajiepushe na adha ya Khalifa Mwinyimkuu, mtu aliyetisha hata kutazamwa.

    “Nakupa dakika moja ya mwisho,” Khalifa alimtisha.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA ..................





0 comments:

Post a Comment

Blog