Search This Blog

Monday, October 24, 2022

JASHO LA MASUMBUKO - 4

 





    Chombezo : Jasho La Masumbuko

    Sehemu Ya Nne (4)



    MASUMBUKO alijitahidi kulivuka eneo hilo haraka huku kaziba pua yake. Lakini hakwenda mbali mara akashtushwa na honi ya gari nyuma yake. Alipogeuka akauona mkono wa mtu ukimwashiria kwenda.



    “Biashara!” alinong'ona. “Huenda nikapata walao hela ya kula. Mungu nisaidie.”



    Haraka akafukua mbio akilifuata gari hilo dogo, jeusi, aina ya BMW. Alikwenda akiwa na matumaini makubwa ya mafanikio. Lakini kabla hajalifikia, mara gari hilo nalo likaanza kumfuata. Likawa linasogea polepole, kisha likaongeza mwendo ghafla likiyasogelea yale maji machafu.



    Kwa kuchukua hadhari, Masumbuko alirudi nyuma akiepuka kurushiwa yale maji machafu. Lakini alikuwa amechelewa sana. Gari lile lilikuja upande uleule aliokuwepo, kwa kasi zaidi, likaingia kwenye dimbwi na kuyarusha yale maji kwa nguvu kubwa!



    Yakampata Masumbuko sawia! Mwili wake wote, na vile vitenge vikalowa maji yaliyochanganyika na vinyesi!



    Halafu, polepole, na kwa madaha tosha, gari hilo liliondoka huku likipiga honi ya ajabu, honi yenye mdundo kama wa muziki wa kinanda kipigwacho na mpiga kinanda mahiri.



    Jirani na eneo hilo kulikuwa na kijiwe cha vijana ambao hujulikana kama 'kula kulala.' Wazazi wao wana uwezo mkubwa wa kipesa. Vijana hao, baada ya kupata stafutahi makwao, hukutana katika kijiwe hicho na kupiga stori hadi mchana wanaporejea tena makwao kwa ajili ya maakuli.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa mwonekano, vijana hao walikuwa 'hawajambo.' Mavazi yao yalikuwa ya thamani kubwa na mikufu ilining'inia kwenye shingo zao. Baadhi yao walitoga hereni masikioni huku nywele zikiwa zimesukwa kawa mitindo ya kipekee.



    Kila walipokutana, stori zao ziliegemea miji ya Pretoria, Johannesburg, London, Paris, New York, Amsterdam na kwingineko. Lakini ukweli ni kwamba kati yao hakukuwa na aliyewahi kufika huko.



    Hivyo ndivyo vijana hao walivyolijenga taifa lao. Ndivyo walivyojifunga mikanda, na ndivyo walivyoibeba misalaba yao.



    Waliishuhudia zahama iliyomkumba Masumbuko, wakabwata: “Oyaa! Oyaa! Msh'kaji! We chinga acha kulemaa. Kula naye sahani moja demu huyo...”



    Kilichofuata ni kama vile ilikuwa nyota njema kwa Masumbuko. Wakati lile gari, BMW likiondoka, mara gari kubwa la mizigo likatokea mbele yake likiingia katika barabara hiyo ya Allykhan. Wakati likiingia taratibu likawa limeziba barabara yote na hivyo kulazimisha magari mengine yote kusubiri. BMW lililomrushia maji machafu Masumbuko lilikuwa miongoni mwa magari hayo.



    Kwa hasira za kiwango cha juu, hasira za karne nyingi, hasira za mtu aliyekata tamaa ya maisha, Masumbuko alivirusha vile vitenge bila kujali vitatua wapi na kwa nani, ni kama vile aliviona ni minyororo iliyomnyima uhuru wa kufanya kile akipendacho.



    Kilichofuata baada ya kuvirusha vitenge hivyo ni wepesi mithili ya radi; akatimua mbio kama kichaa na sekunde chache baadaye akawa ameshalifikia lile gari, BMW. Alitisha! Mwili wake wote ulikuwa umetapakaa maji yaliyochanganyika na kinyesi! Inzi walimwandama! Alitoa harufu kali na mbaya kupindukia.



    Uso wake uliodhihirisha mateso ya jua kali, ulitisha zaidi ya kifo. Macho yake yalikodoa kwenye gari hilo bila ya kupepesa. Alitisha kutazamwa. Alionyesha dhahiri kuwa alikuwa tayari kwa lolote!



    Naam, alikuwa tayari kwa lolote.



    Tayari kuua.



    Tayari kufa.



    Wakati huo pia, lile kundi la vijana wa kijiweni lilikuwa likisogelea katika eneo hilo, baadhi yao wakiwa wameokota vile vitenge vilivyorushwa na Masumbuko.



    Mara tu Masumbuko alipolifikia gari lile alivurumisha ngumi kwenye kioo cha dereva, kioo ambacho wakati huo kilikuwa kimefungwa.



    Kikasambaratika!



    Papohapo akatumbukiza kono lake la kulia na kukishika kichwa cha dereva huyo. Akakiinua na kumtazama usoni. Akakutana na uso wa kike, uso wenye ngozi laini iliyomeremeta.



    Naam, alikuwa ni msichana mrembo ambaye Masumbuko hakutegemea kukutana naye. Macho ya binti huyo yalikuwa makubwa, yaliyojaa huba. Kijiblauzi chake kilionekana kushindana na vititi vichanga vilivyochongoka kama mikuki.



    Lile bonde la vititi hivyo pale kifuani lilionekana kama konde zuri lililostahili kwa kilimo cha mbogamboga. Sketi yake ilikuwa fupi, nyeusi iliyoyaacha hadharani mapaja yake manene.



    Macho yao yalipokutana, mrembo huyo alitabasamu, tabasamu lililotengeneza vijishimo viwili katika mashavu yake laini. Akayalegeza yale macho yake ya 'kichawi' kisha akamkonyeza Masumbuko huku, kwa sauti nyororo akisema, “Vipi, brother, una matatizo gani? Please, acha kuzitibua nywele zangu.”



    Alikuwa ni Happy!



    Happy Mkombo!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Masumbuko aliduwaa. Akahisi kuwa yu ndotoni. Lakini kumbukumbu ya ile barua yenye tani elfu nyingi za kashfa, barua aliyopewa na yule mbeba zege majuzi, ilipomrudia akilini, akauweka kando ustaarabu. Akawa kama kichaa aliyekunywa gongo na kuvuta bangi.



    Akamshika Happy kwa nguvu zaidi na kumvuta kutoka mle garini. Alipokwishamfikisha nje tu, akamtwisha gumi zito usoni. Happy hakustahimili, alianguka chini mithili ya papai bovu, tii!



    “Ndiooo! Mkomeshe! Wakome haoo!” walioshuhudia walimuunga mkono Masumbuko.



    “Akomeshwe! Anaringia gari alilopewa kwa umalaya wake!” wengine walibwata.



    Happy hakunyanyuka. Alibaki pale chini akikoroma huku damu ikimtoka kwa wingi mdomoni. Ndiyo, konde moja tu lilikuwa limefanya kazi yake, konde la mtu mwenye uchungu wa maisha, mtu ambaye kila kukicha hajui kama atakula, na atakula nini, mtu atokaye jasho kutwa nzima na kuambulia vijisenti vya kula.



    Naam, lilikuwa ni konde lililokusanya maguvu ya kihistoria nyuma yake haidhuru hata kama limeangukia ndipo, sipo. 'Kombora lililokosea shabaha halimdhalilishi aliyelirusha, maadam lilmedondokea upande wa adui. Hivyo Masumbuko hakuona aibu kwa kitendo kile.



    Punde akazuka kijana mrefu, mweupe, nywele nyingi zilizosokotana na pua ndefu iliyopinda. Alikuwa ni wa asili ya Uarabuni. Mara sauti yake kali iliyojaa ghadhabu ikapaa hewani: “Nipisheni...! Nasema nipisheni! Yuko wapi huyo mbwa koko aliyempiga Baby sexy Queen?”



    “Mimi hapa!” Masumbuko alimjibu kwa kiburi. Na hasira zikiwa bado zimeutawala ubongo wake, alikunja ngumi kwa mara nyingine akijiandaa kwa shambulizi jingine, safari hii akidhamiria kumshushia 'mvua ya makonde' mwarabu huyo.



    Hakuipata nafasi hiyo. Tayari kijana huyo wa Kiarabu alikwishaitoa bastola na kufyatua risasi. Masumbuko alihisi joto kwenye sikio la kushoto, akajitupa chini haraka. Risasi hiyo ilikuwa imelipapatiza sikio, lakini hakuumia sana.



    Kwa muda shwari ikatawala. Lakini kulikuwa na kama sekunde tano au kumi tu za shwari hiyo, halafu kama vile roho mbaya amepita, wale vijana waliokuwa pale pamoja watu wengine waliofika walimkamata huyo kijana wa Kiarabu na kumnyang'anya ile bastola.



    Kilichofuata hakikutofautiana na taswira ya watu wanaomshambulia kibaka anayejulikana mitaani kwa kuwapora watu. Kila mmoja aligombania kupata nafasi ya kumpiga kijana huyo. Dakika kumi baadaye zilimkuta kijana huyo akiwa maiti!



    Kilikuwa ni kitendo cha haraka mno. Jinsi alivyokumbwa na mvua ya vipigo haikuwa ni hali ya kuelezeka kwa urahisi. Na tandabelua hiyo haikuishia kwenye mwili wa kijana huyo pekee. La hasha. Dakika chache baadaye zililikuta gari lile la kifahari likipigwa mawe kama vile linanyeshewa mvua.



    Yalikuwa ni mawe yaliyorushwa kwa shabaha ya ajabu kutoka katika mikono sugu ya watu wenye hasira.



    Muda mfupi baadaye BMW ile ilikuwa haitazamiki, haitamaniki. Haikutofautiana na gofu. Na kama vile haitoshi, 'msamaria' mwema mmoja aliyekuwa kifua wazi huku kalowa jasho chepechepe alitoa kibiriti na kulitia moto tangi la mafuta.



    Petroli ikachekelea!



    Eneo zima likatanda moshi mzito, moshi mweusi uliojiviringa kwenda juu kama vile kumjulisha anayedaiwa kuishi huko kwamba, nchi aliyoiumba imejaa dhuluma na uonevu, na sasa watu wamechoka.



    Naam, petroli ile haikuuangusha umati uliokuwa umekusanyika pale. Iliungana nao, ikaruka kutoka gari moja hadi jingine. Sasa kukawa na mfumka wa watu. Walikuwa wanakimbia kuelekea sehemu nyingine ya barabara. Masumbuko akaungana nao.



    Na huku kulikuwa na kasheshe mpya. Watu wenye roho zilizotoneshwa majeraha walikuwa wamelizingira 'shangingi' Toyota Land Cruiser jipya ambalo ndani yake kulikuwa na mwanamume mmoja mnene kupindukia.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mwanamume huyo alikuwa upande wa kiti cha abiria. Alikuwa akiongea kwa dharau huku kabinua mdomo juu: “Nyie vibaka kwa nini mnakosa adabu? Tuwaite polisi?”



    Lilikuwa ni kosa kubwa! Umati wa watu ulipandwa na hasira maradufu. Subira ikakosekana. Mawe mengine yakalivaa gari hilo. Wakati huo dereva wa 'kibonge cha mtu' huyo alikwishateremka na kutokomea katika kuyalinda maisha yake.



    Masumbuko naye alijipenyeza na kuliangalia gari hilo. Akahisi siyo gari jipya machoni mwake. Akaziangalia nambari zake za usajili. Akaguna. Akamtazama huyo mtu mnene aliyekuwa ndani. Akamtazama vizuri na kumtambua.



    Alikuwa ni yule Waziri wa Misosi na Maraha, Kisu Makalikuwili!

    Masumbuko akaduwaa.



    *** *** *** *** *** ***



    NA huku kulikuwa na kasheshe mpya. Watu wenye roho zilizotoneshwa majeraha walikuwa wamelizingira 'shangingi' Toyota Land Cruiser jipya ambalo ndani yake kulikuwa na mwanamume mmoja mnene kupindukia.



    Mwanamume huyo alikuwa upande wa kiti cha abiria. Alikuwa akiongea kwa dharau huku kabinua mdomo juu: “Nyie vibaka kwa nini mnakosa adabu? Tuwaite polisi?”



    Lilikuwa ni kosa kubwa! Umati wa watu ulipandwa na hasira maradufu. Subira ikakosekana. Mawe mengine yakalivaa gari hilo. Wakati huo dereva wa 'kibonge cha mtu' huyo alikwishateremka na kutokomea katika kuyalinda maisha yake.



    Masumbuko naye alijipenyeza na kuliangalia gari hilo. Akahisi siyo gari jipya machoni mwake. Akaziangalia nambari zake za usajili. Akaguna. Akamtazama huyo mtu mnene aliyekuwa ndani. Akamtazama vizuri na kumtambua.



    Alikuwa ni yule Waziri wa Misosi na Maraha, Kisu Makalikuwili!



    Masumbuko akaduwaa.



    Akayahamishia macho katika kiti cha nyuma. Huko kulikuwa na mtu, mwanamke ambaye Masumbuko hakufanikiwa kumwona vizuri kiasi cha kuweza kumtambua.



    Vurugu iliendelea. Mara gari hili nalo likatiwa moto na watu wale wenye hasira. Yule mwanamke aliyekuwa kule nyuma alifungua mlango na kutoka mbio. Na Waziri huyo alipoona maisha yake yako hatarini naye alikurupuka na kutoka. Lakini hiyo haikuwa salama yake, kwani muda mfupi baadaye naye mawe yalishindana moja baada ya jingine yakitua mwilini mwake huku akiwa chini.



    Alikufa huku kaachia kinywa wazi, haja kubwa na ndogo vikiwa vimemtoka kwa mkupuo! Kwa kiasi kikubwa mwonekano wake ulitisha.



    “Mtie moto!”



    “Achomwe...!”



    “Mchinjeni!”



    Kelele zilizizima kutoka katika kundi lile la watu wenye hasira.



    Masumbuko alizifananisha na kelele zile za Mafarisayo wa enzi za kale waliokuwa wakimzomea Yesu na kumdhihaki huku wakipaza sauti: Asulubiwe...! Asulubiwe...!



    Mara akajitokeza msamaria wa pili, na kwa mara nyingine tena petroli ikachekelea! Waziri wa Misosi na Maraha, Kisu Makalikuwili akaivishwa!



    Ghafla king'ora kikasikika. Umati uliokuwa katika eneo hilo ulikitambua king'ora hicho, hivyo ulitambua fika ni kipi kitakachojiri muda mfupi ujao. Kila mmoja akafukua mbio akielekea alikoamini kuwa kuna usalama.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Lakini walikuwa wamechelewa sana. Kila upande kulikuwa na askari waliovalia rasmi; kofia za chuma vichwani, bunduki mikononi, virungu na bastola viunoni.



    Masumbuko naye aliwaona. Akatafuta upenyo, na kwa bahati yake akaupata. Akatoka mbio na kutokomea. Lakini hakwenda nyumbani moja kwa moja. Alihofia kukutwa na askari huko maskani kwake na kutiwa mbaroni.



    Hivyo alikwenda hadi kwenye bustani iliyo jirani na kituo cha daladala cha Fire ambako alikaa hadi jua lilipotokomea. Kisha akatembea taratibu akikifuata kituo cha mabasi yaendayo Vingunguti. Moyoni alikuwa na uchungu wa kudhalilishwa na Happy kwa kumwagiwa maji machafu na kupoteza vitenge vyake doti tano ambavyo alivitegemea kama nguzo ya kumpatia pesa.



    Lakini hakuwa na la kufanya zaidi ya kujichunga zaidi kwani aliamini kuwa tayari ameshaingia kwenye kundi la wahalifu kufuatia mshikemshike wa mchana huo. Hivyo alirudi nyumbani kwa hadhari kubwa, akijisikia hata kutokula.



    Alilala njaa!



    **********





    SIKU iliyofuata magazeti kadhaa yalitangaza kwa kirefu juu ya tukio la siku iliyopita. Gazeti moja litolewalo na shirika moja la Haki za Binadamu liliandika: HATIMAYE WALALAHOI WACHARUKA. Jingine lilisema: KIBOPA MBADHIRIFU AONJA CHUKI ZA WAVUJA JASHO; AGEUZWA KIFUSI CHA MAJIVU BARABARANI.



    Lingine liliandika: MAJAMBAZI YAZUSHA GHASIA...



    Ilimradi kila gazeti liliandika kivyake. Hata hivyo ukweli ulibaki palepale. Kwamba, kiongozi mmoja wa ngazi za juu serikalini, kiongozi ambaye alitumia mamilioni ya fedha za Watanzania kwa manufaa yake, ameuawa.



    **********





    SEKESEKE la siku iliyopita lilimwathiri sana Masumbuko kisaikolojia. Hivyo, asubuhi hii hakuwa na wazo la kutoka. Aliamua kujipumzisha. Lakini wakati akiyatafakari yaliyojiri jana yake, mara wenzake walioishi hapo wakaingia huku mmoja wao akiwa na gazeti mkononi.



    “Masu, mwanangu vipi bado umelala?” yule mwenye gazeti alimwambia. “Amka ucheki hapa!”



    Masumbuko aliamka. Akakabidhiwa gazeti. Akalipokea huku mikono ikimtetemeka. Katika ukurasa wa mbele kulikuwa na picha kubwa ambayo aliitambua mara moja kuwa ni yake. Juu ya picha hiyo kulikuwa na maandishi makubwa: ANATAFUTWA NA POLISI.



    Maelezo yaliyofuata yalimchanganya zaidi.



    MASUMBUKO MALIYATABU, MWENYE PICHA HAPO JUU, ANATAFUTWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA UJAMBAZI WA KUTUMIA SILAHA.



    MTUHUMIWA JANA ALIMVAMIA MWANAMKE MMOJA JIJINI DAR ES SALAAM KWA NIA YA KUPORA GARI HUKU AKIWA NA BASTOLA. JARIBIO HILO LILISABABISHA VURUGU KUBWA VIKIWEMO VIFO VYA WATU KADHAA.



    KATI YA VIFO HIVYO NI KILE CHA ABOUBAKARY NASSOR, AMBAYE NI MTOTO WA KIUME WA TAJIRI MKUBWA MWENYE VIWANDA VYA NEPI NA CHUPA, ABDULRAHMAN NASSOR. KIFO KIBAYA ZAIDI KATIKA HUJUMA HIYO NI KILE CHA ALIYEKUWA WAZIRI WA MISOSI NA MARAHA, MHESHIMIWA KISU MAKALIKUWILI (MUNGU AIWEKE MAHALI PEMA PEPONI)....



    ZAWADI NONO YA SHILINGI MILIONI KUMI (10,000,000/=) ITATOLEWA KWA YEYOTE ATAKAYEFANIKISHA KUKAMATWA KWA MHALIFU HUYO.



    Tangazo lilikomea hapo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Masumbuko aliwarushia hilo gazeti bila ya kutamka chochote.



    “Umeelewa?” mmoja wa walioleta gazeti hilo alimuuliza.



    “Kuelewa nini?”





    “Hili tangazo.”



    Masumbuko hakujibu.



    Mara sauti za mbwa wakibweka zikasikika huko nje. Masumbuko na wenzake wakashtuka, wakatazamana. Mara wakakurupuka na kukimbilia dirishani kuchungulia.



    Naam, katika nyumba ya tatu tu kutoka hapo, askari polisi wawili waliovalia sare, virungu mikononi, bastola viunoni na mbwa wawili walioshiba wakiwa kando yao, walikuwa wakimhoji bi kizee mmoja aliyeishi mtaani hapo.



    Ghafla msichana mmoja alitokeza uchochoroni. Uso wake ulikuwa umevimba, bandeji na vipande vya plasta viliusakama.



    Ni Happy!



    Masumbuko aligwaya. Akatambua kuwa ni kweli anasakwa.

    “Kimbieni!” aliwaambia wenzake.



    Hawakukimbia, zaidi walimtazama kwa mshangao.



    “Kimbieni!” Masumbuko alirudia, safari hii kwa msisitizo.



    “Kwani sie tuna kosa gani?” mmoja wao aliuliza.



    “Kimbieni!”



    Safari hii walitii. Wakatoka mkuku wakitumia mlango wa uwani.



    Masumbuko alibaki palepale dirishani akiangalia mahojiano kati ya wale askari na yule bibi kizee. Ilivyoonekana, mahojiano yale hakwenda vizuri kwani alimshuhudia askari mmoja akimkwatua ngwala yule bibi kizee. Bibi kizee alipaa juu kisha akarejea chini kwa kishindo tii!



    Hakutikisika tena!



    Tukio hilo lilipenya moyoni mwa Masumbuko mithili ya msumari wa moto. Akatoka mbio akiwafuata wale askari. Happy ndiye aliyekuwa wa kwanza kumwona. Na kwa sauti iliyojaa kiwewe akawaonyesha wale askari huku akibwata, “Jambazi lenyewe ni hilo!”



    Muda mfupi baadaye Masumbuko akajikuta amezingirwa na mbwa huku bastola mbili zikimtazama.



    “Mikono juu!” akaamriwa. Kisha virungu vikaanza kumshukia mfululizo mithili ya mvua ya masika. Ni kama vile askari hao walidhamiria kumuua.



    Matumaini ya kuishi maisha ya uhuru yakaanza kutoweka akilini mwa Masumbuko. Hata hivyo hakuwa tayari kutiwa mbaroni na kupelekwa kituo cha polisi. Aliyajua ambayo yangefuata baada ya kufikishwa huko kituoni. Tuhuma ya mauaji ingekuwa juu yake.



    Hivyo akaamua kujikumbusha kareti na judo alizojifunza wakati akiishi Bunju. Akawaza kuwa askari polisi wengi huwa hawana mazoezi ya kutosha. Wakishatoka Moshi kwenye mafunzo basi, hujipweteka. Zaidi, hubakia kuwaghasi raia kwa kuwapiga virungu na kula rushwa.



    Imani hiyo ilimwongezea ujasiri. Akamvaa yule askari aliyekuwa mbele yake na kumpiga ngwala ya nguvu. Hakubisha; alikwenda juu mzima-mzima na alipokuwa akirejea chini alipokewa na teke zito la kichwani. Dakika iliyofuata alikuwa akijinyoosha chini huku akitoa mkoromo wa kutisha.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kisha akatulia!



    *****KIMENUKA! HAPATOSHI HAPO! NI KIPI KITAKACHOFUATA?



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog