Search This Blog

Monday, October 24, 2022

JASHO LA MASUMBUKO - 3

 





    Chombezo : Jasho La Masumbuko

    Sehemu Ya Tatu (3)



    USIKU huu aliorejea kutoka ng'ambo ya nchi, alikuwa amepokea tena taarifa hizo za ajabu kuhusu mkewe. Na hata alipoamua kulala, mawazo yake yote yalikuwa juu ya taarifa hizo. Na wakati alipofumba macho akikoroma mithili ya mtu aliyetopea usingizini, ndipo alipomwona mkewe akitoka taratibu chumbani.



    Ni hapo ndipo alipoanza kuziamini zile taarifa alizozipata. Naye akajitoa kitandani taratibu, akaifungua saraka moja ya kabati. Akaitoa bastola kisha akaanza kumfuata mkewe kinyemela.



    Hakuyaamini macho yake pale alipomshuhudia mkewe, Chausiku akiingia ndani ya chumba cha mfanyakazi wao, Masumbuko.

    Masumbuko! Kisu Makalikuwili aliwaza kwa hasira.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    **********



    MASUMBUKO alimpokea Chausiku, mke wa waziri maungoni kwa nguvu ya ajabu. Akaingia katika kitengo kingine cha ajira yake, akidhamiria kuiondoa kabisa kiu ya Chausiku. Lakini hakufika mbali, mara mlango ukasukumwa! Mumewe Chausiku, waziri, Kisu Makalikuwili akaingia, bastola mkononi!



    “Niwaue?!” lilikuwa ni tamko lake la kwanza. Uso wake ulibadilika. Hakuwa yule Kisu Makalikuwili ambaye wakati alipotoka safarini alikuwa na uso uliopooza, ukidhihirisha uchovu mkubwa uliomwandama.



    Huyu alikuwa ni Kisu Makalikuwili mwingine. Uso wake uliashiria kifo dakika yoyote. Ilikuwa dhahiri hakuwa akifanya masikhara. Kwa ujumla alitisha.



    “Niwaue?” kwa mara nyingine aliwauliza.



    Hakuna aliyemjibu. Walengwa walibaki wameduwaa, jasho chepechepe likimtoka kila mmojawao.



    “Nawauliza kwa mara ya mwisho, niwaue?”



    Chausiku alianza kulia. Na hakikuwa kilio cha kimyakimya, kilikuwa cha sauti, kilio cha majuto. “Nisamehe...nisamehe mume wangu...” alisihi.



    Kisu Makalikuwili akasonya. Akaushusha mkono. Kwa upande wa Masumbuko, hali ilikuwa ni mbaya zaidi. Alihisi kuwa huo ndiyo mwisho wa maisha yake. Akawakumbuka wazazi wake kule nyumbani, Nzega. Akamkumbuka Happy, mtoto wa daktari Mkombo.



    Sasa akajikuta akisali kimoyomoyo, akimwomba Mungu amsamehe dhambi zake zote alizowahi kuzitenda. Zooote! Ikiwemo hii ya uzinzi iliyomfikisha katika fumanizi hili la aibu!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mara ghafla tena mlango ukasukumwa na Mwanahawa akaingia! Papohapo akamrukia Kisu Makalikuwili na kumpora ile bastola. “Hapana shemeji... hapana... usiue!” alibwata kwa sauti kali huku akiwa ameshasimama mbali na Kisu Makalikuwili.



    Ni hapo Masumbuko alipozinduka. Akakurupuka kutoka kitandani na kumpiga kumbo kali mzee huyo. Akafungua mlango haraka na kutoka nje mkuku! Alikuwa uchi kama alivyozaliwa.



    Kitu kimoja kilimsaidia. Kwa muda wa miezi miwili sasa nyumba hiyo haikuwa na mlinzi. Yule aliyepangiwa hapo na serikali aliacha kazi bila taarifa, na hakukuwa na mlinzi mwingine aliyeletwa. Hivyo, Masumbuko alikuwa na ahueni, vinginevyo angekumbana na vikwazo hapo getini.



    Alipolifikia geti alilifungua haraka na kutoka nje. Hakujali anakwenda wapi, alijali kuisalimisha roho yake. Muda mfupi baadaye alikuwa mbali na jumba hilo, sehemu isiyokuwa na nyumba hata moja.



    Akatulia na kupatazama huko alikotoka. Akashusha pumzi akiamini kuwa sasa yu salama salimini. Sehemu hiyo ilitawaliwa na miti mingi. Akazunguka hapa na pale na kufanikiwa kupata vipande vya mashuka chakavu ambayo hata hivyo yalimsaidia kwa kujihifadhi mwilini. Kisha akapanda katika mti mmojawapo na kutulia akisubiri kupambazuke.



    Hatimaye mapambazuko yalijiri. Lakini Masumbuko hakuharakisha kuteremka. Alitulia palepale mtini akiliangalia jumba lile la Kisu Makalikuwili kwa mbali. Ilipokaribia saa 2 akamwona waziri Kisu Makalikuwili akitoka huku akiendesha gari lake, Jeep Cherokee.



    Hakuweza kuijua hatima ya sekeseke la jana yake. Ilikuwaje? Je, waziri huyo aliwaua Chausiku na mdogowe? Na kama hakuwaua alichukua hatua gani zaidi?



    Mara akajikuta akinong'ona kama mwendawazimu, “Wakubwa wana mbinu zao za kutatua matatizo yao ya ndani. Hawapendi mambo yasambae. Wanaogopa watu wa magazeti wasije wakajua; itakuwa aibu kubwa.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Punde akawaona Chausiku na mdogowe, Mwanahawa wakitoka nje ya geti. Walikuwa wakiangaza angaza macho kama wanaotafuta kitu. Masumbuko akajiwa na nguvu mpya. Akapaza sauti, “Niko huku! Niko huku!”



    Chausiku na Mwanahawa walishtuka, wakaangaza macho kule mtini. Walipomwona, walicheka. Mwanahawa akamfuata huku Chausiku akirudi ndani. Muda mfupi baadaye Chausiku akatoka, mkononi akiwa na begi kubwa. Naye akamfuata Masumbuko hukohuko mtini.



    “Teremka, basi, usiogope,” Chausiku alimwambia.



    Akateremka. Hata hivyo bado hakuonekana kujiamini. Aliwatazama wanawake hao kama wageni kwake, na hakukosa kuangaza macho huku na kule kila baada ya sekunde chache, akihisi kuwa bado hatari inamnyemelea.



    “Usihofu, mpenzi,”Chausiku alimwambia huku akimkabidhi begi. “Hakuna tatizo tena. Pole sana na sakata la jana. Humo kuna nguo zako zote.”



    Kisha akamkabidhi bunda la noti na kuongeza, “Ni laki tano. Ukajianzishie kijimradi cha kukuendeleza huko mbele ya safari. Halafu,” akasita na kumshika mkono. Akamvuta pembeni.

    Hakutaka mdogo wake ayasikie hayo mengine aliyotaka kuongeza.

    “Mie nimeambiwa nihamie Rome, Italy. Kule kuna nyumba zetu mbili. Moja ndiyo nitakayokwenda kukaa. Na ubaki ukijua kuwa nina mimba yako changa! Namwomba Mungu nijifungue salama. Nakuheshimu kwa kunipatia ujauzito huu. Yule mzee angenifanya nife sina hata mtoto. Masumbuko nitakukumbuka! Na nitakapojifungua tu, nitakujulisha.”



    Wakabaki wanatazamana, nyuso zao zikionyesha majonzi ya kutengana. Mara Chausiku akamkumbatia na kumbusu kinywani, busu lililodumu kwa takriban nusu dakika.



    Wakati huo Mwanahawa alikuwa kimya, akiwatazama. Simanzi ilikuwa bayana usoni pake. Machozi yalimlengalenga machoni. Mara tu Chausiku alipomwacha Masumbuko, Mwanahawa akamwita kwa upole, “Masu.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Masumbuko akamfuata. Mwanahawa akampa bahasha na kuondoka bila hata ya kutamka neno jingine. Masumbuko alipoifungua bahasha ile akakuta kuna fedha taslimu shilingi 300,000 na kijikaratasi chenye maandishi: MASUMBUKO, MPENZI, NINA MIMBA YAKO YA MIEZI MINNE.



    Kwa mbali Masumbuko akahisi kizunguzungu. Akashusha pumzi ndefu huku akivaa nguo zake. Dakika kumi baadaye zilimkuta barabarani akiitoka Bunju bila ya kujua aendako.



    **********



    JOTO la Dar es Salaam lilikuwa ni kali asubuhi hiyo. Masumbuko alitembea huku akijifuta jasho usoni. Hatimaye alitokea kwenye Barabara ya Bagamoyo. Hapo alitulia kwa dakika chache kabla hajapata usafiri wa daladala iliyompeleka Mwenge ambako alichukua usafiri mwingine wa kuelekea Posta.



    Hadi wakati huo hakuwa na uamuzi afanye nini na aweke wapi maskani yake baada ya kuharibu mambo kule kwa mwajiri wake. Alipoteremka pale Posta Mpya akaanza kutembea akielekea baharini. Ni kama vile alikuwa amechanganyikiwa. Japo alikuwa na pesa mfukoni hata hivyo bado hakujiamini. Hakuwa na dira yoyote inayoeleweka.



    Hakufika mbali mara akakutana na Balinzigo, kijana aliyekuwa akiishi Nzega miaka kadhaa iliyopita. Balinzigo alikuwa ni mfanya biashara ndogondogo maarufu kwa jina la 'machinga.' Alikuwa akitembea mitaani akiuza sketi, suruali na blauzi. Mara nyingi alikitumia kituo cha daladala cha Posta Mpya kwa kuwa huwa kuna mkusanyiko mkubwa wa watu hususan wanawake.



    Baada ya Masumbuko kumweleza kuhusu mkasa uliomkumba, wakakubaliana ahamie kwa Balinzigo, eneo la Vingunguti ambako yeye angekuwa mtu wa tano katika chumba hicho kidogo kwenye kijumba kichakavu.



    Naam, Masumbuko akawa ameingia katika mkondo mpya wa maisha. Sasa naye akajiunga na Balinzigo katika biashara hiyo ya nguo. Miezi mitatu baadaye akawa mzoefu katika biashara hiyo. Lakini tofauti na matarajio yake, matumizi yalikuwa makubwa kuliko mapato.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wenzake katika nyumba hiyo walikuwa watu wa starehe. Japo hawakuwa na kipato kikubwa, hata hivyo hawakujiweka nyuma katika mambo ya 'kujirusha.' mara kwa mara walipenda kuhudhuria kwenye kumbi mbalimbali ambako bendi za dansi au taarabu zilitumbuiza. Pia walikuwa watu wa pombe na wanawake. Hivyo kipato kidogo kilichopatikana walikigawanya kwa kula na kustarehe.



    Masumbuko akiwa ni mgeni katika makazi hayo, na wao wakiwa ndiyo waliomfundisha jinsi ya kufanya biashara hiyo, alishindwa kuwaepuka kwa asilimia mia moja. Hivyo siku moja-moja naye akawa akijiunga nao kwenda baa na katika kumbi za muziki kuburudika.



    Hatimaye akajikuta akisaliwa na akiba ya shilingi 50,000 tu huku suruali, mashati, sketi, blauzi na sidiria vikiwa havinunuliwi kwa kasi ya kuridhisha.



    Ndipo ikaja siku.



     Mvua ilikuwa imenyesha mchana kutwa siku hiyo. Masumbuko alihisi kuandamwa na homa kwa mbali, hivyo tangu asubuhi hakutoka kwenda kwenye mizunguko yake. Wenzake wote walikuwa wametoka.



    Ilikuwa ni jioni, saa 10. Bado manyunyu yaliendelea kudondoka. Akiwa amesimama mlangoni akiwa hana la kufanya, mara akamwona kijana mmoja akimjia na bahasha ndogo mkononi.



    Kijana huyo alipofika, bila hata ya salamu alimpa Masumbuko bahasha hiyo huku, kwa sauti kavu na nzito, akisema, “Shika barua yenu hii. Ni ya chinga mwenzenu mwenye jina hilo.”



    Masumbuko aliipokea bahasha hiyo na kuuliza, “Nani kakupa?”

    “Demu mmoja bomba kishenzi,” kijana huyo alimjibu huku akimtazama kutoka juu mpaka chini. “Alikuwa akiendesha mzinga wa gari, mwanangu.”



    Masumbuko alizidi kumtazama kijana huyo kwa makini zaidi. Alionyesha dhahiri kuwa ni kijana aliyeishi katika mazingira magumu. Nguo zake zilikuwa zimechanikachanika hapa na pale na nywele zikiwa timutimu. Macho yake yalikuwa mekundu na uso ulioshupaa, uso ulioikumbatia dhiki ya muda mrefu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Naam, ulikuwa ni uso uliokata tamaa ya maisha, uso wenye dalili zote za kikatili. Akayarejesha macho kwenye ile bahasha na kukuta juu kumeandikwa jina lake: MASUMBUKO kwa wino mwekundu. Akashtuka na kushangaa. Akaguna.



    “Kishaondoka?” akamuuliza kijana huyo.



    “Kasepa longi kichaa wangu, taimu ileile baada ya kunipa hiyo bahasha.”



    “Na amepajuaje hapa?”



    “Maswali mengi ya nini?” kijana huyo alibwata. “Kama barua hiyo inawahusu chukueni, kama haiwahusu basi itupe! We' vipi? Achana na mimi! Mie kanibamba kwenye mishemishe zangu, akanidakisha kitu kidogo baba’ake nikamkubalia ombi lake.”



    Sauti yake kavu na nzito, sauti isiyotofautiana na mlio wa bundi mzee, kwa kiasi fulani ilimtisha Masumbuko. Na kwa upole, akijaribu kuepusha shari, alisema, “Basi, imefika. Asante sana.”



    Kijana huyo aliondoka bila ya kuaga, na wala hakugeuka nyuma. Masumbuko akairudia ile bahasha na kuuangalia ule mwandiko kwa makini. Ulikuwa ni mwandiko mgeni kwake. Hakuweza kukisia ni nani aliyeandika.



    “Hii ni barua ya ajabu,” alinong'ona. “Kwa nini mwandishi atumie wino mwekundu?”



    Hakupata jibu.



    Mara alikumbuka kuwa huwa kuna mbinu za mauaji kwa kutumia barua. Unafungua barua, unakumbana na unga wenye manukato ya kuvutia, lakini harufu hiyo nzuri inakuondolea uhai dakika chache baadaye.

    Au, unaifungua na kutokea mlipuko mkubwa, mlipuko huo unakusambaratisha kiasi cha mwili wako kubaki ni vipande vidogovidogo vya nyama visivyopungua milioni moja. Kwa ujumla eneo palipotokea mlipuko linakosa taswira yoyote ya kuwepo kwa mwanadamu sekunde chache zilizopita.



    Lakini ni binadamu gani mwenye akili timamu atakayediriki kumuua 'chinga' kwa teknolojia ya aina hiyo? Alijiuliza na kuamini kuwa siyo rahisi kwa mtu wa aina yake kutegeshewa kifo kwa mfumo huo.



    Kwa tahadhari kubwa aliifungua bahasha ile mithili ya mwindaji hodari mwenye silaha duni akimwandama simba mwenye watoto.



    Hakuyaamini macho yake baada ya kuifungua bahasha hiyo. Ndani kulikuwa na kipande cha karatasi kilichokunjwa mara moja, na alipokikunjua ndipo aliposhtuka. Ilikuwa ni barua, na juu ya barua hiyo kulikuwa na anwani ya mwandishi. Ni jina la mwandishi huyo ndilo lililomshtua moyo.



    Ndiyo, alishtuka sana, lakini pia alifarijika. Ilikuwa ni barua kutoka kwa yule binti, binti mzuri ambaye vijana wengi wa Nzega walimchukulia kama mrembo wa dunia aliyekamilika katika kila hali hivyo haikuwa rahisi kwa mtu wa aina ya Masumbuko kuweza kumpata. Binti aliyewafanya vijana hao wamdhihaki Masumbuko kabla na hata baada ya binti na wazazi wake kuondoka nchini.



    Ni Happy Mkombo!



    Naam, ilikuwa ni barua ya pili kutoka kwa Happy, baada ya ile aliyomwandikia mara tu walipofika Marekani. Baada ya barua ile Happy alipotea! Masumbuko alimjibu haraka barua yake. Kisha akamwandikia nyingine baada ya mwezi mmoja.

    Kimya.



    Akaandika nyingine tena.



    Kimya.



    Hakuchoka, akamwandikia barua ya nne.



    Kimya.



    Masumbuko alishaangaa, na nguvu zikamwisha. Akakata tamaa. Sasa leo ndio anaipata barua kutoka kwa Happy, na tena barua yenyewe inaletwa kwa mazingira ya kutatanisha. Barua ya pili baada ya miezi tisa!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mshangao uliompata haukudumu sana nafsini mwake, bali furaha ilitwaa nafasi haraka kiasi cha kujikuta akiibusu barua hiyo huku kimoyomoyo akijiuliza, Happy karudi kutoka California? Na kama ndiye kwa nini amtume kijana yule mchafumchafu? Kwa nini asije mpaka hapa nikamwona? Na je ni kweli Happy sasa ana gari au kakodi?



    Labda ni yeye. Lakini kama kweli ni yeye, atakuwa amepajuaje huku Vingunguti ambako kwa mtu wa aina ya Happy hatakosa kupafananisha na makazi ya mataahira?



    Mnyororo mrefu wa maswali ulijinyonganyonga kichwani mwake. Kwa shauku kubwa akarudi chumbani na kuketi kitandani ili aisome barua hiyo kwa utulivu, barua kutoka kwa yule ampendaye. Akilini mwake alihisi kuwa huenda pia barua hiyo ilikuwa na mnyororo mwingine mrefu wa majibu.



    “WA ZAMANI, MASU,” ndivyo barua hiyo ilivyoanza. “NAJISIKIA AIBU SANA KUKUANDIKIA BARUA KIDUDUMTU KAMA WEWE. NINAYO MENGI YA KUFANYA KULIKO KUPOTEZA MUDA KUKUANDIKIA BARUA, MBWA WEWE! VIPI HALI YAKO YA UHOHEHAHE? NASIKIA ETI SIKU HIZI UMEKUWA 'CHINGA-BOY' WA KUZURURA NA MIGUO MITAANI KA' CHIZI. I SEE, POLE SANA.”



    Ulikuwa ni mwanzo mbaya, mwanzo wa kutisha akilini mwa Masumbuko. Barua ya Happy, mtu aliyemwahidi ndoa, tayari ilianza kumzingua. Alihisi mate machungu mdomoni, kizunguzungu kikamvaa kwa mbali. Jasho jembamba likamtoka pajini mwa uso. Akajifuta jasho hilo kwa kutumia kiganja cha mkono wa kulia. Akashusha pumzi ndefu na kuendelea kusoma.



    “NAKUFANYIA HESHIMA KUBWA SANA KUKUJULISHA YAFUATAYO:

    KUANZIA SASA UTAMBUE KUWA MIMI SIO MCHUMBA WAKO TENA. ETI UCHUMBA! ULIKUWA NI UCHUMBA GANI AMBAO HADI LEO WAZAZI WETU HAWAKUWA NA TAARIFA NAO? WEWE! KOMA KABISA! TENA ISHIA HAPOHAPO! UNITOE KABISA MAWAZONI MWAKO. HIVI UTANIPA NINI KATIKA MAISHA YANGU?



    KWA SASA NIPO HAPAHAPA DAR, NINA MIEZI KAMA MITANO HIVI TANGU NIREJEE KUTOKA CALIFORNIA. VILE VIJIBARUA VYAKO VICHAFU ULIVYONIANDIKIA VILINITIA AIBU NA KUNIKERA SANA. HUNA AKILI NA HUNA ADABU, MASUMBUKO!



    BAHATI MBAYA YAKO HUNA SIMU. NINGEKUTWANGIA NIKIWA HUKOHUKO NA NIKAKUMWAGIA MANENO YALIYOKUSTAHILI SIKU ZILEZILE, TAAHIRA WE!



    WAKATI HUU NIANDIKAPO BARUA HII, NIKO ZANGU COCO BEACH NAPUNGA HEWA. SI UNAJUA TENA MAMBO YA PESA! NI KULA RAHA KWA KWENDA MBELE. SINA MIGUO MINGI YA KISHAMBA KAMA WANAVYOVAA HAO MALAYA ZAKO WA USWAZI, AKHA! MWENZIO NIMEJIVALIA KICHUPI CHA PINKI AMBACHO KIMELIFICHA LILE TUNDA BIVU, ZURI ULILOLIONJA KWA MARA YA KWANZA KIMAKOSA, BWEGE WE!



    MASUMBUKO, ILE MIPAJA MINENE, MIEUPE, MILAINI, IKO PEUPE IKIPAPASWA NA KIJANA MZURI WA KIARABU, ABOUBAKARY. NI MWANAMUME ANAYEJUA MAPENZI NI NINI NA ANAJUA KUMFURAHISHA MWANAMKE. SIYO KAMA WEWE MSHAMBA WA KILA FANI. MBWA JIKE WE!



    NIMEMWACHIA ABOUBAKARY MIPAJA HII, ANAIMINYAMINYA, NA WAKATI MWINGINE ANAVUKA MIPAKA NA KUFIKA KULE KWENYE KISIMA CHA UVUGUVUGU. ABOUBAKARY ANAJUA KUNIBUSU ANAVYOTAKA NA KUNINYONYA ANAVYOPENDA. HATA MIMI NAMFANYIA YALE YANAYOSTAHILI KUMFANYIA. YOTE! MAPENZI NI UCHAFU; SIO UCHAFU KAMA WAKO WA NGOZI NA MAVAZI MBWAKOKO WE!



    MASUMBUKO, KANDO YETU KUNA GARI DOGO, JEUSI, BMW. HILI NI GARI LANGU, MASUMBUKO. NI ZAWADI NILIYOPEWA NA BABA YAKE ABOUBAKARY. NA LIMEINGIA NCHINI BURE BILESHI! DADADADADEK! HALIKULIPIWA USHURU HATA SENTI MOJA! KWA HIYO MASUMBUKO UTAMBUE KUWA SASA MIMI NI MALI YA WATU, MSHENZI WEE! TENA NI MALI MUHIMU NA ADHIMU.



    WE PAKASHUME USIYE NA MKIA, UKIBAHATIKA KUNIONA POPOTE PALE, FANYA KAMA VILE HUNIJUI; USIPOTEZE HATA MUDA WAKO KUNISALIMIA KWA SABABU SANASANA UTAAIBIKA; SITAIPOKEA SALAMU YAKO. SINA HAJA NA SALAMU YAKO KONOKONO MWENYE HARUFU MBAYA WE!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MASUMBUKO, MTOTO MIE SIKU HIZI SITAKI KERO YA MIJASHO KWA KUGOMBANIA MIDALADALA YENU! HIVI WABONGO BADO HAMJAFIKIRIA NJIA NYINGINE YA KUSAFIRI BILA KUGOMBANIA DALADALA? HUU UMASKINI WENU UTAISHA LINI?



    MASUMBUKO, NAKUOMBA SANA UICHUKULIE BARUA HII KAMA AGANO LA MILELE. NILIPOKUSHAURI UKATAFUTE MAISHA SIKUTARAJIA KUWA UNGEKUWA 'CHINGABOY.' HIVI ULIKOSA KAZI NYINGINE YA KUFANYA? SHAURI YAKO, UTAENDELEA KUWA MASUMBUKO KAMA ULIVYO, NA UTAENDELEA KUSUMBUKA MPAKA KUFA KWAKO, KENGE MWEUSI WEE!



    POLE! NAKUPENDA LAKINI AKHA! UMASKINI WAKO, UMASKINI WAKO MASU!



    KWA HERI!



    NI MIE HAPPY (SUPER QUEEN).



    Masumbuko alianguka chini na kuzirai!



    Fahamu zilimtoka Masumbuko. Alipozinduka giza lilikuwa limekwishatanda humo chumbani. Umeme haukuwepo ndani ya nyumba hiyo ambayo lilikuwa ni banda tu lililosimama kwa mikogo tosha. Na alikuwa peke yake, wenzake wote walikuwa hawajarudi kutoka kwenye mihangaiko yao.



    Akahema kwa nguvu na kujitingisha kidogo, kujitingisha kulikosababisha jeshi kubwa la mbu livume chumbani humo. Akasonya na kufungua mlango kisha akatwaa shati na kuanza kulipunga huku na kule akiamini kuwa kwa njia hiyo huenda akawafukuza mbu hao.



    Ni kama vile alikuwa amechanganyikiwa. Na kwa ujumla alikuwa amechanganyikiwa. Bado hakuwa timamu kiakili. Kwake, dunia ilikuwa imegeuka jehanamu. Barua ya Happy, barua ambayo haikutofautiana na jisu kali lenye makali kuwili ilikuwa imeurarua vibaya sana moyo wake.



    Akajiuliza, huyo Aboubakary yukoje? Ana macho sita na miguu minne tofauti na watu wengine? Mara machozi yakamtoka. Alilia kwa uchungu mkubwa, akiona kuwa hakuna njia yoyote ya kuweza kumwondoa katika mkondo huo wa maisha.



    Akajikuta akinong'ona, “Ama kweli duniani kuna watu. Mie hapa nagugunwa na mbu, njaa imenisakama huku wengine wanahonga gari!



    “Kwa nini mie niwe maskini hivi? Nina mkosi? Nimelaaaniwa? Ni kwa sababu sina ajira ya uhakika wa kipato? Hapana. Umaskini huu unawapendelea wachache, akina Kisu Makalikuwili. Yeye kochi lake moja tu la kwenye ile sebule yake linatosha kunifanya 'chinga' mimi niwe kwenye kundi la wenye nazo.



    “Hebu fikiria hilo jumba lake la huko Italia, limemgharimu shi'ngapi? Yule ni fisadi mkubwa. Atakuwa amepata wapi pesa za kujenga au kununua jumba hilo? Atakuwa amepata wapi kama sio wizi mtupu? Ndio, ni wizi mtupu! Wizi mtupu! Wanaifilisi nchi kwa kula pesa ya kodi inayotolewa ana walalahoi.



    “Halafu eti kwa ushenzi wao wanasema kuwa sisi chinga tuondoke hapa mjini. Ng'o! Hatuondoki Tutabanana hapahapa!”



    Mara akapiga ngumi kiganjani na kusonya kwa nguvu. “Umaskini huu!” aliipaza sauti kidogo. Kisha akaanza kulia kwa sauti ndogo, kilio kilichoambatana na kwikwi.



    Naam, simanzi ilimtawala kutoka utosini hadi nyayoni. Akilini mwake, neno UMASKINI lilimtisha mithili ya kifo.



    Aliitafakari ile barua ya Happy kwa uchungu usiomithilika. Happy, binti mzuri, mrembo kupindukia, aliyetegemea kufunga naye ndoa pindi atakaporejea kutoka Marekani, leo anamwasi kwa barua yenye kila chembe ya dhihaka!

    Kwa Masumbuko huo ulikuwa ni usiku mrefu kupindukia. Hakumbuki kama aliambulia lepe la usingizi.



    ***********



    ASUBUHI ya siku iliyofuata, Masumbuko alipiga moyo konde akatafuta kalamu na karatasi na kuamua kuijibu ile barua. Aliamua kufanya hivyo baada ya mmoja wa wakazi wa nyumba hiyo kumwambia kuwa kijana aliyeleta barua ile hufanya kazi ya kuwasaidia mafundi ujenzi katika majengo mbalimbali yanayoendelea kujengwa hapo Vingunguti.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Na siku hizi anasimamia lile jengo la mzee Kisura,” kijana mmoja kati ya wale anaoishi nao alimwambia.



    Hili jengo la mzee Kisura halikuwa mbali kutoka hapo. Hivyo, haraka Masumbuko alishika karatasi na kuanza kuandika barua hiyo.



    MPENDWA, MKE WANGU MTARAJIWA, HAPPY, BARUA YAKO NIMEIONA, NIMEISOMA NA KUIELEWA VIZURI. NAOMBA UTAMBUE KUWA UAMUZI ULIOUCHUKUA NI WA KILIMBUKENI SANA, HAPPY.



    NAAMINI HUO UZURI WAKO NDIYO UNAOKUZUZUA. JIHADHARI, UKIMWI UTAKUONDOA.



    MIE NIMEKUKOSEA NINI HAPPY? UMASKINI WANGU NI KOSA LANGU MIE? NILIUOMBA UMASKINI? MIMI NI MASKINI, SAWA. LAKJINI UKAE UKIJUA KUWA MIMI NI MASKINI KWA KUWA ABOUBAKARY NI TAJIRI.

    MIE NATEMBEA KWA MIGUU AU NAPANDA DALADALA KWA KUWA NYIE MNATESA NA MAGARI YENU YA KIFAHARI.



    HAPPY, INATIA AIBU SANA KAMA UMEAMUA KUWA MALAYA WA KUSTAREHESHA WAPITA NJIA. SHAURI YAKO, HAPPY, LAKINI NAAMINI IPO SIKU MAJI YATAKUFIKA SHINGONI; UTANIKUMBUKA NA UTAYAKUMBUKA MANENO YANGU HAYA.



    NI MIMI MUMEO MTARAJIWA, MASUMBUKO.



    Aliikunja barua ile, akaitia ndani ya bahasha na juu akaandika: MPENZI HAPPY. Baada ya hapo, alitoka taratibu hadi kwenye hilo jumba aliloambiwa kuwa ujenzi wake unaendelea na kwamba yule kijana aliyeileta ile barua ndipo anapofanya kazi.



    Alimkuta akiwa na karai la zege kichwani. Hakumwita, alivizia hadi pale watakapokutanisha macho ili amwite kwa ishara. Muda mfupi baadaye jambo hilo lilitokea. Alimpungia mkono na kijana yule hakukaidi, alitupa karai lile la zege ambalo wakati huo halikuwa na kitu, akamfuata Masumbuko.



    “Vipi, mwanangu?” ilikuwa ni kauli ya kwanza ya kijana huyo mara tu alipomfikia Masumbuko.



    “Poa. Tunaweza kuongea kidogo?”



    “Zungumza tu, kuna ishu gani?”



    “Unanikumbuka?”



    Kijana yule alimkazia macho Masumbuko kisha akatikisa kichwa na kusema, “Nikumbushe.”



    “Ni mimi uliyenipa barua jana pale kwenye nyumba ya Mama Kuruthumu,” Masumbuko alimfahamisha.



    Kijana yule akatabasamu kwa mbali na kutikisa kichwa. Kisha: “Kwa hiyo vipi kwani?”



    Masumbuko aliingiza mkono mfukoni na kuchomoa noti ya shilingi 2000. Akampatia yule kijana akiambatanisha na ile barua huku akisema, “ Naomba umpelekee huyo demu aliyekupa. Unaweza kumwona?”



    Noti ile ilikuwa ni silaha kubwa ya kummaliza nguvu huyo kijana, nguvu za kupingana na Masumbuko kuhusu matakwa yake. Aliipokea na kusema, “Hakuna noma, mwanangu. Mbona shwari tu! Lakini saa hizi niko mzigoni. Mwenyewe si unaniona.”



    “Siyo lazima sasa hivi,” Masumbuko alisema. “We' dunda mzigo tu. Hiyo ni ishu ya baadaye. Lakini unaweza kumwona ndani ya siku mbili, tatu, hivi?”



    “Hakuna noma, nitajitahidi,” kijana yule alijibu. “Huwa hakosi kule Coco Beach hasa siku za wikiendi. Na leo ni Jumamosi, kwa vyovyote atakuwepo. Nikitoka hapa jioni nitazungukia huko.”



    “Poa. Kwa hiyo tutawasiliana vipi?”



    “Si unakaa pale pale kwa Mama Kuruthumu?”



    Masumbuko aliitika kwa kutikisa kichwa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Basi us'konde. Kesho nitakuja kukwambia kama nimempata au bado.”







    **********





    WIKI nzima ilipita baada ya siku Masumbuko alipompa kijana yule barua kwenda kwa Happy. Aliridhika baada ya kijana yule kumjia siku ya pili na kumtaarifu kuwa alimwona Happy na akampatia barua ile. Kwamba Happy ataichukulia vipi ile barua, halikuwa ni suala la kukisumbua kichwa chake hata kidogo. Alichohitaji ni barua kumfikia mlengwa.



    Hii ilikwa ni siku ya nane. Saa 6 kasoro dakika chache ilimkuta Masumbuko akiwa kwenye mihangaiko yake ya kutafuta wateja wa nguo alizozitembeza mitaani.



    Mchana huu alikuwa eneo la Upanga, Barabara ya Allykhan. Doti chache za vitenge zilikuwa mkononi mwake. Jua lilikuwa kali na lilimshushia miali yake mithili ya tanuru. Alilowa chepechepe! Isitoshe, alikuwa hajatia kitu tumboni tangu asubuhi.



    Katika tembeatembea yake, akiwa kandokando ya barabara hiyo, alipita katika sehemu iliyokuwa na bomba la maji machafu. Bomba hilo lilikuwa limepasuka na hivyo kusababisha dimbwi la maji barabarani.



    Maji hayo yalitoa harufu kali na iliyochefua mioyo ya wapita njia wengi.

    Masumbuko alijitahidi kulivuka eneo hilo haraka huku kaziba pua yake. Lakini hakwenda mbali mara akashtushwa na honi ya gari nyuma yake. Alipogeuka akauona mkono wa mtu ukimwashiria kwenda.



    “Biashara!” alinong'ona. “Huenda nikapata walao hela ya kula. Mungu nisaidie.”



    Haraka akafukua mbio akilifuata gari hilo dogo, jeusi, aina ya BMW. Alikwenda akiwa na matumaini makubwa ya mafanikio. Lakini kabla hajalifikia, mara gari hilo nalo likaanza kumfuata. Likawa linasogea polepole, kisha likaongeza mwendo ghafla likiyasogelea yale maji machafu.



    Kwa kuchukua hadhari, Masumbuko alirudi nyuma akiepuka kurushiwa yale maji machafu. Lakini alikuwa amechelewa sana! Gari lile lilikuja upande uleule aliokuwepo, kwa kasi zaidi, likaingia kwenye dimbwi na kuyarusha yale maji kwa nguvu kubwa!



    Yakampata Masumbuko sawia! Mwili wake wote, na vile vitenge vikalowa maji yaliyochanganyika na vinyesi!



    Halafu, polepole, na kwa madaha tosha, gari hilo liliondoka huku likipiga honi ya ajabu, honi yenye mdundo kama wa muziki wa kinanda kipigwacho na mpiga kinanda mahiri.



    *****HAYA! KIJANA MASUMBUKO AKIWA KATIKA MISHEMISHE ZAKE ZA KUSAKA PESA ANAKUMBWA NA GHARIKA HIYO. JE, ATACHUKUA HATUA GANI?

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog