Search This Blog

Monday, October 24, 2022

NATAKA KUZAA - 1

 







    IMEANDIKWA NA : JENIPHER ALPHONCE



    *********************************************************************************



    Chombezo : Nataka Kuzaa

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    Ilikuwa ni siku ya jumatatu, tarehe tano mwezi wa kumi mwaka 2015. Asubuhi ya saa mbili ilinikuta mimi na familia yangu tukiwa mezani tukipata kifungua kinywa. Ilikuwa ni asubuhi yenye furaha na bashasha.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mimi, baba yangu, mama yangu na wadogo zangu wawili mapacha Pink na Pinto tulikuwa tukinywa chai tukiongea mambo mbalimbali.



    Ni siku hiyo ambapo hata wadogo zangu hawakutamani kwenda shuleni, wazazi wangu pia hawakwenda kazini hiyo siku.



    Yote yalikuwa ni maandalizi ya kunipeleka chuoni ambapo kwa mara kwanza nilikuwa naingia chuo kikuu cha Dar Es Salaam kusomea kozi ambayo ilikuwa ni ndoto yangu na ya wazazi wangu, kozi ya udakatari. Hakika ilikuwa ni siku ya furaha sana.



    “Sociolah unajisikiaje mwanangu?” mama aliniuliza.



    “Mmmh mama sijui hata jinsi gani nikuelezee.” niliongea huku nikichekacheka. “Nimefurahi sana kwasababu ni leo ambayo siku natimiza ndoto zangu na zenu pia, najua jinsi ambavyo mimi najisikia na nyie mnajisikia hivyohivyo.” niliongea na kumalizia kwa cheko pana, wote walicheka isipokuwa wadogo zangu ambao walikuwa bize wakichezacheza michezo yao hapo mezani.



    Baba yangu Michael Kindamba ambaye alikuwa ni daktari wa Muhimbili alisema huku akitafuna chakula mdomoni, “hamna Sociolah sisi tuna furaha sawa lakini furaha yetu haiwezi kuwa kubwa kuliko furaha yako.”



    Mama yangu Anastazia Kimbamba ambaye alikuwa ni mhadhili wa chuo kikuu cha Dar Es Salaam kwa masomo ya uchumi alicheka,



    “ni kweli lazima furaha yako imetuzidi ila unajifanya kama hujafurahi vile Sociolah.” aliongea na kumalizia kwa kucheka.



    Hakika ilikuwa ni siku ya furaha sana kwetu.



    Pink na Pinto hawakuwepo mbali hawakutaka kwenda shule hiyo siku waling’ang’ania kuja chuoni kunipeleka kwaajili ya usajili.



    Tuliondoka nyumbani kwetu maeneo ya Mbezi beach na kuelekea chuo kikuu cha Dar Es Salaam.



    Ndani ya gari nilikaa nyuma na wadogo zangu ambao hawakuishiwa fujo, hakika walikuwa watoto watundu sana, mara zote nilijaribu kuwaongoza “usifanye hiki, usifanye kile” walikuwa wabishi ingawa walileta furaha sana katika familia yetu.



    Mimi na wadogo zangu tumepishana umri mkubwa sana wazazi wangu walisubiri sana kabla ya kuwapata wadogo zangu.





    Mimi nina umri wa miaka ishirini na moja na wadogo zangu wana umri wa miaka kumi na moja hivyo tulikuwa tumepishana miaka kumi kati yetu.



    Tulifika chuo kikuu cha Dar Es Salaam na kuelekezwa katika ukumbi wa Nkuruma ambapo shughuli za usajili zilikuwa zikifanyika.



    Mama yangu alikuwa mfanyakazi wa chuo kikuu cha Dar Es Salaam kwahiyo haikutuwia vigumu sana kufanya usajili.



    Niliweza kuchukua fomu ya kujiunga na kisha nikafanya usajili wa bima na pia nikaenda kupiga picha za vitambulisho.



    Baada ya hapo nilielekea benki kwaajili ya kulipia ada pamoja na hostel. Nilikuwa



    nimepangiwa kukaa hostel za mabibo.



    Baba yangu hakupenda nikae hostel.



    “Mwanangu si uwe unakaa hapa hapa nyumbani nitakupa gari utakuwa unaenda nalo chuoni mimi sipendi ukae mbali na sisi.”



    “Mmmh baba itaniwia vigumu sana kama nitakaa hapa nyumbani kwa maana wakati mwingine tutahitaji kuwa na discussion nitapata shida baba, kila weekend nitakuwepo hapa nyumbani usijali kuhusu mimi alafu saa hizi baba mimi nimeshakua hivyo siwezi kuendelea kukaa hapa nyumbani kudekadeka tu.” niliongea huku nikicheka baba naye alicheka.



    Mama alinisapoti, “anachokiongea Sociolah ni ukweli muache aende akakae hostel na kila weekend awepo hapa nyumbani” mama aliongea tulikubaliana.



    Baada ya kutoka Benki tulienda café kula hakika ilikuwa ni furaha sana tulikula katika café iliyokuwa inaangaliana na shule ya biashara pale chuo kikuu cha Dar Es Salaam.



    Tulirudi Nkuruma kwaajili ya kumalizia Shughuli za usajili.



    Nilibaki nimesimama mlangoni pale Nkuruma, baba na mama yangu waliingia ndani kwaajili ya kuangalia ni nini kilichokuwa kinaendelea.



    “dada… dada….njoo ucheke.” Pink na Pinto waliniita.



    “hawa watoto wasumbufu kweli wameona nini?”



    “njoo…” nilisita kwenda lakini sikuwa na budi kwa vile baba na mama walikuwa ndani ya ukumbi ule na mimi nilikuwa nimesimama mlangoni nilisogea hatua chache na kisha kuwafikia Pink na Pinto.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Angalia pale” niliangalia lakini sikuonakitu.



    “we dada huoni angalia bwana mwenyewe asije akatuona” Pink aliongea huku akicheka.





    Niligeuka na kutazama pale ambapo walikuwa wakinionesha hakika kilikuwa ni kichekesho cha mwaka nilishindwa kujizuia kucheka.



    Alikuwa ni mkaka ambaye amesimama huku akiwa hana hili walalile. Alikuwa akibonyeza simu yake ambayo sikusita kuitambua kwamba ni nokia ya tochi. Hakika jinsi alivyokuwa amesimama na muonekano wake ilikuwa ni kichekesho tosha watu wengi walikuwa wakimuangalia na kucheka alikuwa amevaa tshirt ya light blue iliyopauka, alikuwa amevaa suruali aina ya bwanga rangi ya kijivu alikuwa amechomekea tshirt yake ndani ya suruali hiyo.



    Chini alivaa raba nyekundu, mkononi alikuwa ameshikilia tranka lake na kichwani alikuwa amevaa kofia aina ya pama.



    Hakika alionekana kama mkulima aliyekuwa akielekea shambani au mganga wa kienyeji aliamua kuvalia vizuri, nilishindwa kujizuia nilicheka kisha nikawavuta wadogo zangu kuelekea ndani ya ukumbi, nikawakamea



    “sio vizuri kumcheka mtu”



    “dada kwani huku mnakujaga na matranka?” waliniuliza, nikawaambia



    “hebu acheni huko muacheni mtoto wa watu mnamcheka mnamcheka nini baadae atakuja kuwa mtu mkubwa mpaka mtashangaa niliongea”



    “Mmmh” waliishia kucheka tu ingawa ilikuwa ni kichekesho lakini sikupenda kuwadharau watu.



    Baada ya shughuli za usajili kuisha tulirudi nyumbani tukiwa tumechoka huku tukifurahia safari ile.



    Baada ya kuoga tulipata chakula cha jioni kilichoandaliwa vema na mfanyakazi wetu wa ndani aliyekuwa ni msichana wa makamo tuliyezoea kumuita Linah ingawa jina lake aliitwa Paskalinah.



    Baada ya chakula cha jioni tulikaa verandani tukiongea mambo mbali mbali kuhusiana na siku yetu iliyopita. Pink aliyekuwa akichezea simu ya baba alimgeukia mama na kumuonyesha kitu mama alicheka hadi machozi yakamtoka.



    “Nini unacheka mama” baba aliuliza.



    “Mwambie Pink akuonyeshe” alijibu huku akifuta machozi.



    Pink alimpa simu baba.



    “Imetoka wapi hii” baba aliuliza kwa mshangao uliofuatiwa na kicheko.



    “Mimi ndo nilipiga” alijibu Pink kwa kiherehere.



    “Jamani kuna watu ni vituko” mama alisema “Ni nini?” nliuliza.



    “Si ni yule mkaka wa chuoni niliekuonesha” Pinto alidakia.





    Nlichukia, nikanyanyuka nilipokaa hadi kwa baba aliyekuwa ameshika simu nikaichukua kwa nguvu nikafuta picha zote walizompiga yule kaka.



    “Sio vizuri kumbeza na kumcheka mtu kwa muonekano wake hamjui hata katokea wapi wala anaenda wapi (niliongea kwa hasira) sijapenda…. Pink na Pinto acheni hiyo tabia”



    Wote walishikwa na butwaa nadhani hawakuamini kama ningeweza kumtetea mkaka yule aliyekuwa kituko na ambaye sikuwa nikimfahamu hata kidogo. Sikujali niliirudisha simu kwa baba na kuelekea chumbani kwangu kupumzika sikutaka kuendelea kuwepo hapo.



    “Mmemskia dada yenu.… siku nyingine msirudie” mama aliongea



    sikujishughulisha kuendelea kusikiliza maongezi yao nilibamiza mlango wa chumba changu.



    Ratiba za chuo zinaanza kwa uwepo wa semina elekezi mbalimbali.



    Kila siku mama yangu alikuwa akiondoka na mimi kutoka nyumbani hadi chuoni aliniacha mahali husika na kisha kuelekea ofisini kwake.



    Nilikuwa nikiangalia mazingira mbalimbali ya pale chuoni kwetu, nilizunguka sehemu moja hadi nyingine ili kuweza kuyafahamu mazingira vizuri.



    Katika kipindi hicho cha semina elekezi ndipo nilipokutana na Melania na Fety wasichana tuliopangiwa nao chumba kimoja katika mabweni ya Mabibo. Niliweza kufahamiana nao pale nilipoenda hapo kwa ajili ya kukabidhiwa chumba kwa kuwa wao walikuwa wamekwishahamia kwenye mabweni ya Mabibo wakati mimi nilitokea nyumbani katika kipindi chote cha semina elekezi.



    Melania na Fety niliona wanafaa kuwa marafiki zangu, hakika walikuwa wasichana warembo sana kwenye macho yangu niliona ni wao tu hakukuwa na wengine zaidi yao walipenda kutabasamu wakati wote iliwafanya wazipendezeshe sura zao nzuri sana niliwapenda sana wasichana hao hawakuonesha kuringa na hao ndio wakawa marafiki zangu.



    Mimi na Melania tulikuwa tukisoma kozi moja wakati Fety alikuwa akisomea uchumi. Melania alikuwa akitokea hapa hapa Dar lakini Fety alikuwa akitokea Morogoro. Siku ya jumapili niliohamia rasmi katika mabweni ya Mabibo.



    Siku ya Jumatatu tulianza masomo rasmi siku hiyo ilikuwa ya kufurahiwa sana, nilifurahia kila kitu tulichokuwa tukifundishwa darasani.



    Siku ya jumanne tulikuwa na kipindi saa mbili asubuhi. Niliwahi kuondoka Mabibo nikiwa na Melania na kisha tukaingia darasani.





    Nilikuwa napenda sana kukaa mbele ili niweze kuelewa vizuri kile mwalimu alichokuwa akifundisha tulipofika mlangoni Melania alianza kucheka.



    “anacheka nini huyu” nilimshangaa nilimuona kama mwendawazimu. “gosh… kuingia darasani tu anacheka.”



    Tuliwahi dakika kadhaa kabla mhadhiri hajaingia nikaachana naye kwa kuwa yeye hakupenda kukaa mbele, nikaelekeza macho yangu kwenye viti vya mbele ili kupata nafasi na hapo ndipo niligundua kwa nini Melania alikuwa anacheka.



    Kwanza sikuamini macho yangu kile nilichokiona mbele yangu kilinichekesha na kisha kilinishitusha. Alikuwa ni yule mkaka ambaye nilikutana naye siku ya kwanza nilipofika hapa chuoni



    “haa inamaana na huyu anasoma udaktari, mbona makubwa” alikuwa bize kuangalia mbele kana kwamba mwalimu alikuwa tayari ameingia na anafundisha, alionekana kituko kwa maana huko nyuma watu wengi walikuwa wakimuongelea yeye na kumcheka.



    Siku hiyo alivaa tshirt kubwa jeupe ambayo rangi yake ilionekana kufifia, alivaa suruali nyeusi iliyopauka pamoja na makubazi miguuuni, hakuacha ile kofia yake. Alikuwa ni mzuri wa sura lakini vituko vyake kwa kweli vilinichosha, “huyu mkaka anashida sana.”



    Ilikuwa  imebaki siti  moja  tu pembeni yake nafikiri  watu hawakupenda  kukaa



    karibu naye kwa vile nilikuwa nikipenda sana kukaa mbele nilienda kukaa palepale,



    “hi” nilimsalimia.



    “hallo” aliongea.



    Alikuwa na sauti nzuri sana tofauti na muonekano wake ilinibidi kucheka. Alitabasamu tu na kisha kuendelea kuangalia mbele, nilivutiwa kufanya naye maongezi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Unaonekana kufurahia sana kuwepo hapa” alivua kofia yake na hapo niliushuhudia uzuri wake mwingine, alikuwa na nywele nzuri ambazo ziliupamba uso wake.



    “Huyu mkaka ni mzuri au anafanya kusudi ili watu wasijue kwamba yeye ni mzuri.” Niliongea mwenyewe na nafsi yangu nilionesha tu tabasamu.



    Alilamba midomo yake na kisha akanigeukia kwa tabasamu pana, “naitwa Franklin” aliniambia.



    “ooh Frank nice name” nilimjibu kwa aibu.





    “Ni ndoto yangu ya muda mrefu sana kuja kusomea udaktari lazima niwe na furaha” alinijibu kwa ufupi huku jibu lake likiwa limejitosheleza niliachia tu tabasamu.



    Mara ghafla meseji iliingia kwenye simu yangu, alikuwa ni Melania:



    “Sociolah umechanganyikiwa hujui kama unajiharibia CV yako kila mtu anakucheka huku nyuma.”



    Na muda huo ndipo mhadhiri aliingia, nilishindwa kumjibu nikatoa madaftari yangu na kisha kuanza kumsikiliza mhadhiri. Mhadhiri alianza kufundisha.



    Mkaka yule ambaye nilimtambua kwa jina la Frank alionekana kuwa makini darasani, alisikiliza kila pointi ambayo mwalimu alikuwa akiongea na alionekana kuelewa sana.



    Nilitumia muda mwingi kumuangalia.



    Mhadhara ule ulinipita kwani sikuelewa vitu vingi.



    Baada ya kipindi kuisha nilibaki tu nikimshangaa, alikusanya vitu vyake huku akionekana akijivuta vuta sana. Watu walianza kutoka nje. Melania alikuja na kusimama pembeni yangu. Frank alikusanya vitu vyake na kisha akasimama aliachia tabasamu na kuvaa kofia yake



    “see you” aliongea huku akiachia tabasamu.



    Nilitabasamu tu na kushindwa kumjibu na kisha alitoka.



    Nilisimama kwa ajili ya kutoka nje melania alinivuta na kunikalisha chini kisha akakaa pembeni yangu,



    “Sociolah unapatwa na ugonjwa wa akili wewe ni wa kuongea na huyu mtu aliyekuja na matranka hapa chuoni” aliniongelesha kwa ukali akionesha kuwa yuko siriazi.



    “aah.. Melania sio kwamba…. Sio kwamba…..” nilishindwa cha kuongea.



    “sio kwamba nini kila mtu huko nyuma anasema kuhusu wewe kweli Sociolah unafikiri una hadhi ya kuongea na huyo mkaka kwani ulikosa sehemu za kukaa mpaka ukae hapo si ungekuja hata ukae kule nyuma”



    “Melania huyu mtu ni mwanadarasa mwenzetu swala la kukaa naye karibu na kuongea naye nadhani hayo ni maamuzi yangu binafsi uniache kwani kuongea naye nimepungiwa nini acha watu waongee kwani wao wakiongea mimi napungukiwa na nini sitaki mtu afuatilie maisha yangu. Melania niko huru kuongea na mtu yoyote ambaye mimi namtaka kwahiyo kwa hili naomba uniache.” niliongea kwa msisitizo sana.





    “kwa hilo naomba uniache” alifuatilizia maneno yangu huku akibana pua. “unafikiri kwamba muonekano wako ni rahisi sana kwa hicho unachokifanya utapata shida hapa ni chuoni Sociolah” aliongea.



    “Haaa..” nilivuta pumzi tu nikishindwa nini cha kumjibu, “twende tukale” nilimjibu.



    “fikiria sana nilichokwambia hupaswi kuwa na ukaribu na huyo mtu” aliongea.



    Ni kweli hatukuendana kabisa na Frank lakini hata hivyo Frank alionekana alikuwa ni mtu mpole na asiye na hatia, kwanini astahili hivi, kwanini kila mtu anamtenga alionekana kukosa marafiki hapa chuoni nadhani kisa kikiwa ni kuja na tranka, nadhani taarifa zake zilienea chuo kizima, ilinitia huzuni sana huyu mtu anahitaji faraja ingawa mwenyewe anaonesha kutokujali kabisa.



    Niliondoka nikiwa na mawazo mengi tulimkuta Fety akitusubiri kwa ajili ya kuelekea café.



    Tuliingia café na kuagiza chakula.



    Wakati naendelea kula nikiwa na mawazo mengi nilishitukia kumuona Fety na Melania wakicheka huku wakioneshana kitu.



    “nyie mbona mnachekacheka si mniambie na mimi nicheke” niliwambia. Melania alicheka kwa sauti mpaka alipaliwa Fety alichukua maji na kumpa “Fety what’s wrong” nilimuuliza Fety. “kushoto kwako” aliniambia.



    Nilibaki tu nikishindwa kumuelewa,



    “kuna nini huko kushoto kwangu”



    “geuka uangalie” niligeuka, nilishindwa kujizuia nikacheka hakika kilikuwa ni kituko cha mwaka.



    Kwa kweli nilishindwa kujizuia kucheka, hakika kilikuwa ni kitu cha kuchekesha kuliko vyote ambavyo niliwahi kukutana navyo katika maisha yangu. Nilicheka sana lakini mwishowe niliingiwa na huruma,



    “hivi huyu mtu ana akili kweli? Hajui kama anafanya haya mambo mbele za watu ona watu wanavyomuangalia.” Niliongea kwa sauti.



    Fety na Melania walinigeukia na kunitazama wakiwa wameduwaa.



    Kushoto kwangu alikuwa Frank, alikuwa akinywa chai pamoja na sahani ya matunda. Matunda yale yalikuwa ni mchanganyiko wa matikiti, machungwa, mananasi na maparachichi.



    Lilikuwa ni tukio la kushangaza sana mtu kunywa chai na matunda. Kila mtu alikuwa akimtazama yeye na kumuongelea yeye. Tukio langu la kukaa naye mbele





    darasani na kisha kuongea naye mawili matatu lilikuwa kama gumzo pale chuoni. Watu wote walikuwa wakiongea wakimtazama na kisha walinigeukia mimi na kucheka, hakuonekana kujali kwani alikuwa akilamba michuzi ya matunda iliyokuwa ikichuruzika mikononi mwake bila haya wala aibu huku akipigia miruzi kana kwamba yuko peke yake.



    “ooh gosh hii ni aibu.” Niliwaza.



    Nilinyanyuka kwa hasira sana. Melania aliongea kwa kupaniki,



    “kwani wewe ni ndugu yako?” Nilimuangalia kwa jicho kali na kisha nikaenda nilipokuwa nataka kwenda.



    Nilijongea moja kwa moja hadi kaunta walipokuwa wakiuza vitafunwa, niliagiza chapati mbili na andazi moja na kisha nikampelekea mezani kwake nikamuwekea kwa hasira na kurudi kukaa kwenye meza yangu.



    Hata sikujua ni nini kilichonivuta kufanya hivyo ingawa aibu yake ilikuwa kama yangu pia kwa maana tu nilijiweka karibu naye asubuhi ya siku hiyo.



    Moyoni mwangu nilijisikia vibaya sana kwa nini nilikaa karibu yake asubuhi ya siku hiyo.



    Aliniangalia na kisha akatabasamu tu.



    Dakika mbili si nyingi chapati zile zilikuwa zimeishia mdomoni mwake, alizikunja chapati zile mbili na kuzitafuna kwa mikupuo miwili tu zikawa zimeisha.





    Kicheko cha watu kiliongezeka sasa hivi walishindwa kujizuia kucheka kisirisiri walicheka kwa sauti kubwa. Nilinyanyuka kwa hasira na kuondoka



    “kwa kweli nimejiingiza kwenye mkenge, mama yangu akisikia kwamba nafanya mambo ya ajabu hapa chuoni hakika baba hatonielewa anaweza akachukua hatua kali.”



    Niliondoka nikiwa na mvurugiko wa mawazo kutoka café mpaka kwenye madarasa yetu, nilichagua darasa ambalo halina watu na kisha nikakaa.



    “oooh my god! Huyu ni mtu wa aina gani hivi hajui kama yuko katika jamii ya watu anapaswa kuwa na heshima na adabu mbele za watu. Kwanini anafanya mambo kama chizi alafu ananiingiza mimi kwenye mkenge huu, Shiit…” Nilijawa na hasira sana kuwa karibu naye nilikumbuka maneno ya Melania: “utajutia hapa ni chuoni.”



    Ningejua ningemsikiliza Melania sijui kwanini niliruhusu kuwa karibu na huyu mkaka.





    Watu walianza kuingia darasani kila mtu akiliongelea tukio lile nilibaki kimya nilikuwa nimekaa kwenye siti za mbele kama kawaida na mhadhara ulikuwa unakaribia kuanza.



    Watu waliingia, Melania aliiingia darasani pia hakutaka hata kunisemesha alienda kukaa siti za nyuma kabisa.



    Nilikuwa nimejiinamia kwenye kiti nikiwa na huzuni, mawazo pamoja na hasira. Ghafla nilihisi mtu amekaa pembeni yangu.Sikujushughulisha kumuangalia niliendelea tu kuwaza na kuwazua.



    “hello” sauti yake ilinishitua.



    Niligeuka kwa mshituko huku nimetoa macho nikimtizama,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “ahsante kwa breakfast” aliongea na kisha aligeuka kutazama mbele kama ilivyokuwa kawaida yake kana kwamba anamsikiliza mhadhiri.



    Nilishikwa na hasira sana nilinyanyuka kwa hasira nikavuta begi langu na kisha kujongea kuelekea nyuma kila mtu alibaki ananishangaa.



    Nilifika mpaka viti vya nyuma ambapo Melania alikuwa amekaa aliniangalia kana kwamba anamuona mwendawazimu.



    “sogea huko” nilimuambia. Alisogea na kisha nikakaa nikalaza kicha changu kwenye meza.



    Mchanganyiko wa hasira, mawazo ulinifanya nisielewe mhadhara ule.



    Mhadhara ulipoisha tu mhadhiri wetu alinichagua kuwa mwakilishi wa darasa ama CR. Nafikiri ilitokana na kwamba alikuwa akifahamiana na mama yangu hivyo baada ya kujua kwamba niko katika darasa lake aliamua kunichagua mimi kuwa CR.



    Kiukweli akili yangu haikuwepo kabisa hapo darasani, mhadhiri alipoondoka tu nilibeba begi langu na kisha kuondoka sikutoa vitu vyangu kabisa tangu tumeingia hapo darasani.



    Niliondoka moja kwa moja hadi Shuttle point kwa ajili ya kusubiri gari kuelekea Mabibo.



    Gari lilipofika tu nilipanda wa kwanza na kisha nikakaa siti ya mbele kabisa sikutaka kukaa karibu na mtu yoyote.



    Melania hakuwepo mbali ingawa hatukuweza kuwa karibu kivile, alikuwa akiniangalia kile nilichokuwa nikifanya huku akinishangaa.



    Gari lilipofika Mabibo sikutaka hata kuagiza chakula nilishuka na kisha kuelekea chumbani kwetu mabweni ya Mabibo Block A, Room namba 147. Nilivyofika tu niliingia na kulala sikuvua hata viatu nililala navyo.





    Fety ambaye alikuwa ameshafika bwenini alibaki akinishangaa, “una nini wewe we Sociolah…. Sociolah…..” sikutaka kugeuka.



    Melania alifika, alifungua mlango na kisha akaenda kukaa kwenye kiti alivuta pumzi na kushusha.



    “Kuna nini jamani? Mmepigana nyie? Mmegombana? Kuna nini?” Fety aliuliza maswali mfululizo sikutaka kuendelea kumsikiliza niliamua kuutafuta usingizi. Nadhani Melania alimuelezea kila kitu kwa maana nilipokuja kuamka baada ya kuhisi njaa Fety hakuwa tena akiuliza maswali.



    Niliamka nikiwa na uchovu sana, “nyie mimi nina njaa twendeni tukale.” “Ndiyo unakumbuka saa hizi kwamba hujala.”



    “aah twendeni bwana tukale” tulijiandaa na kisha kutoka nje.



    Tulitoka hadi café ambapo walikuwa wanauza chakula, niliagiza chipsi kuku na kisha kukaa nikisubiria chakula changu. Melania na Fety waliagiza chakula na kisha kukaa pamoja.



    Tulianza kula huku tukiongea mawili matatu ingawa bado nikihisi uchovu mwingi na kichwa kikiniuma,



    “Mungu wangu balaa gani tena hili?!!” nilishituka.



    Frank alikuwa akija kuelekea upande wetu, watu wote mule ndani ya café waligeuka na kutuangalia sisi. Melania alionesha kuchukia sana, kwa hakika alikuwa hampendi sana Frank.



    “Anakuja kufanya nini huyu tena” niliwaza bila majibu.



    Frank alisogea hadi upande wetu



    “haloo” alinisalimia mimi tu.



    “Unataka nini?” nilimuuliza kwa sauti iliyopoa “samahani dada nilikuwa naomba….”



    Melania alisimama na kuanza kumrushia matusi,



    “wewe umechanganyikiwa mbona unapenda kushobokea watu usiowajua eenh yani kuongeleshwa tu kidogo basi ndiyo unafikiri kama umeunga ukoo kwanini unapenda kumsumbuasumbua rafiki yangu, samahani wewe hauko kwenye level zetu naomba uachane na sisi tena umkome Sociolah.”



    “aah nilikuwa sijui anaitwa nani kumbe anaitwa Sociolah.” Frank aliongea, nilizidi mkushangaa.



    “Frank kuwa na akili sikia nikuambie sitaki ukaribu na wewe naomba kuanzia leo usinizoee.” Nilipatwa na ujasiri wa kuongea.



    “usijali.” Alisema.



    Watu wote walikuwa wakituangalia sisi mule ndani



    “shiit… nilishindwa hata kula nilinyanyuka na kuondoka kuelekea chumbani kwangu.



    Nafsi ilinisuta sana kumtukana ingawa nahisi alistahili sana matusi yale, “Yani yupo kama hayupo sijui kama ana akili sawasawa huyu.”



    Nilifika chumbani kwangu na kujilaza, muda haukupita Fety na Melania waliingia nao walikuwa wamepaniki sana.



    Ilikuwa ni kwa mara ya kwanza Fety anamuona lakini ilionesha kiasi gani hampendi. Walikuwa wakiongea maneno ya kulaani kitendo cha kutuijia pale usiku ule,



    “tumemuacha pale mezani maana anatushobokea sijui hata ameona nini, anafikiri sisi ni level sawa na yeye, fyuu…” mwishoni alifyonza.



    Niligeukia upande wa pili usiku huo ulipita.



    Niliamshwa na pilikapilika za Melania na Fety pamoja na mwanachumba mwenzetu ambaye aliitwa Monica. Kiukweli nilikuwa nimechoka sana na nilihisi njaa,



    “Kuna nini jamani mbona vuruguvurugu?”



    Melania alikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa, alikuwa akirusharusha nguo huku na kule, akipangua vitu na kuharibu mpangilio mzima wa chumba chetu.



    “Kuna nini?” Niliuliza bila kujibiwa. Monica na Fety walikuwa kimya tu.



    Nilinyanyuka na kukaa.



    Nilijinyoosha, “aanh…, nasikia njaa hatari.” Melania alinigeukia na kunitazama kwa jicho kali, “Unawaza kula tu huwazi hata ni nini kimetokea.” “Si nimeuliza sipati jibu” Niliuliza kwa kupaniki.



    “Kama hamtaki kunijibu mimi nifanyeje? Halafu matatizo yenu mimi hayanihusu kama nasikia njaa mbona nyie hamjali.” Fety alinikonyeza. “Kwani kuna nini?” Niliuliza.



    “Melania haioni simu yake.”



    “ooh…” Kwakweli nilishituka sana.



    Melania alikuwa akiipenda sana simu yake aina ya Samsung S6 ambayo alipewa zawadi na mama yake kwa kuchaguliwa kujiunga na chuo kikuu cha Dar Es Salaam, ilikuwa ni simu nzuri na mpya kwahiyo sikushangaa kuona Melania





    amechanganyikiwa kuipoteza simu yake ile, ilikuwa ni nzuri sana hata mimi nilikuwa nikiipenda.



    “Mmmh…. Patamu.” Nilisema.





    Kiukweli Melania alikuwa amechanganyikiwa alitimuatimua vitu vyote na hakufanikiwa kuipata ilinibidi tu na mimi nijitahidi kumsaidia kuitafuta kwa maana alikuwa na hasira zisizo za kawaida



    “Simu yangu nani kaiba jamani….?” Alikuwa akipiga kelele kama chizi.



    “Jamani muda wa kipindi umekaribia mnaonaje tukaenda na tukarudi huku kuja kuitafuta, kwani mara ya mwisho ulikuwa nayo wapi?”



    “Hata sikumbuki mimi nimechanganyikiwa kabisa hapa.” Melania alisema.



    “Mimi nakumbuka ilikuwepo hapa jana.” Fety alisema.



    “Basi itakuwepo hapahapa twendeni tukahudhurie kwenye kipindi turudi tuendelee kuitafuta.” Nilipendekeza.



    Melania alikubali ingawa kwa shingo upande.



    “Mimi bila simu yangu hata sijihisi kuwa niko vizuri.”



    “mmh…” Nilitabasamu tu kwa pembeni maana angeniona ingekuwa ni kesi nyingine.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Tuliondoka na kwenda chuoni, muda wote alikuwa amekasirika hakutaka hata kujiongelesha na mtu.



    Tulihudhuria kipindi hiko cha saa nne na baada ya hapo tulitoka na kuelekea Café



    kwa ajili ya kupata kifungua kinywa.



    Melania aligoma kuagiza kitu chochote,



    “Sasa utakaa bila kula jamani mbona unakuwa hivyo” nilimuongelesha Melania kwa namna ya kumshawaishi.



    “Siwezi hata kula chochote, Sociolah simu yangu ni kila kitu kwangu najisikia vibaya sana bila kuwa nayo.”



    “Usijali utaipata kula basi.” Nilimshawishi.



    “Usinilazimishe kula Sociolah wewe kwasababu hujapoteza kitu hivi unafikiri ingekuwa ni ya kwako ungekula wewe, hebu niache usinisumbue.”



    Kwa kweli nilinyoosha mikono juu kwa maana Melania alikuwa ni mtu ambaye asiyeshawishika, akiweka msimamo ni mgumu sana kuubadilisha.” Fety alijaribu, “Kula basi hata kidogo”



    Alinyanyuka tu na kuondoka hatukujua ameelekea wapi.





    “Kuwa makini naye sana Sociolah akiwa na hasira huyo anaweza kummeza mtu.” Fety aliongea tulicheka.



    Hazikupita dakika mbili Melania alirudi akiwa na glasi ya juisi, nilijua ni juisi ya maembe pamoja na ukwaju, juisi ambayo wote tulikuwa tukiipenda sana. Wakati huo nilikuwa nikinywa chai yangu na chapati, Fety alikuwa akinywa chai na maandazi.



    Tukio la ghafla lilitokea na la kushangaza. Wakati Melania anafika mezani kwetu Frank naye alifika mezani kwetu, nilibaki na mshangao nilishindwa kuongea chochote.



    “Samahani, mambo.” Frank alimsalimia Melania.



    Nilimuona Melania hasira zikimzidia na ghafla alimmwagia ile juisi aliyokuwa



    nayo Frank, alimmwagia juisi yote kwenye shati lake jeupe la mikono mirefu



    ambalo alilivalia na suruali yake ya bluu, hakuchomekea na chini alikuwa amevaa



    malapa bila kusahau kofia yake.



    Masikini ya Mungu roho iliniuma sana.



    “Melania umefanya nini?” Melania aliniangalia tu kana kwamba anaongea na mimi kupitia macho na alipokwisha kumaliza aliondoka bila kusema chochote. Frank alibakia amejiinamia tu nilimuonea huruma lakini nilishindwa cha kufanya. Fety alitoka pale alipokuwa amekaa hadi karibu ya Frank



    “Ndiyo ukome.” Alimuambia na kisha kuondoka.



    Nilimuangalia Frank kwa huruma sana, nilishindwa kufanya chochote nikabeba begi langu na kisha kuondoka.



    Nilikuwa nikimfuata Fety alipokuwa akielekea, tulienda hadi yalipokuwa madarasa yetu. Tulikaa eneo la Vibweta.



    “Melania kwanini umalizie sasa hasira zako zote kwa Frank? Kakufanya nini lakini?” Hakunijibu kitu.



    “Yani hasira zako za simu ndiyo unakuja kummalizia Frank ona ulivyomuaibisha mkaka wa watu jamani kwa nini lakini?” Alisonya tu.



    “Angalia sasa sijui hata anakaa wapi masikini, umemmwagia juisi atatembeaje hapa chuoni kumbuka kwamba bado hatujamaliza vipindi kwanini lakini?” Niliendelea kufoka tu huku ikionesha kumba Melania hakuwa akinisikiliza hata kidogo.



    “Shiit…. Fety tumchangie Melania hela akanunue simu, hata kwa kipindi kifupi tu,



    mimi nitatoa baadhi ya hela nilizokuwa nazo.” Niliongea kwa hasira bila kujua.





    Nilifungua pochi yangu na kuanza kutafuta wallet yangu ambayo niliyokuwa nikihifadhi kiasi kikubwa cha hela. Hiyo ilikuwa ni hela ya matumizi ya wiki hili ambayo nilipewa na mama kiasi kama laki tano hivi. Lahaula..! Haikuwepo!



    Nilichanganyikiwa, nilitupa kila kitu kilichokuwepo kwenye pochi yangu na sikufanikiwa kuiona hiyo wallet.



    “Mungu wangu wallet yangu iko wapi?” Kila mtu alishituka.



    “Sioni wallet yangu jamani, nani kachukua?”



    “Hapana.” Kila mtu alijibu.



    “Shiit..” Nilishindwa cha kuongea hasira zilinikaba kooni.



    “Nyie au tunaibiana sisi kwa sisi.” Fety alisema.



    “Hata mimi naijiwa na mawazo hayo, haiwezekeni jana simu ya Melania imepotea leo wallet yako imepotea, kuna nini kati yetu?”



    “Mungu wangu nitaishije mimi bila hizi hela, nitamuambia nini mama? Hakika hawezi kunielewa… Hawezi kunielewa kabisa.” Nilichanganyinkiwa si kidogo. “Haaa….” Nilivuta pumzi na kushusha sikuwa nikielewa nini cha kufanya.



    Niliingia darasani lakini hakika sikuambulia chochote.



    Muda wa vipindi ulipoisha tulirudi bwenini kwetu Mabibo.



    Kwa kweli sikuwa na nguvu za kumsaidia Melania kutafuta simu yake kila mtu alichanganyikiwa kwa kiwango chake.



    Weekend nilirudi nyumbani, kwa kweli nilikuwa nashindwa jinsi ya kumuanza mama, naanzaje kumuomba mama hela.



    Melania naye hakufanikiwa kuipata simu yake hakika alikuwa na majonzi sana. Weekend kwangu ilikuwa chungu sana maana kila mara nilipokuwa nikijaribu kutafuta njia ya kupata hela nilishindwa, mwisho wa yote nilimkumbuka mpenzi wangu Patrick, niliamua kumtafuta.



    Nilikutana na Patrick kiasi kama miezi sita iliyopita, wakati huo ndiyo nilikuwa tu nimemaliza kidato cha sita katika shule ya sekondari ya Ifakara Girls iliyopo Ifakara mjini.



    Nilikutana na Patrick katika moja ya sherehe ambazo baba alikuwa amealikwa, baba alipenda kuhudhuria na mimi.



    Patrick alikuwa ni mhasibu wa TANESCO pale Ubungo mataa na alikuwa akiishi Shekilango.



    Alikuwa amepanga nyumba moja kubwa ambayo ilikuwa inajitegemea kwa kila kitu, nilimpenda sana Patrick.





    Tatizo moja tu alikuwa nalo Patrick alikuwa ni mtu asiyeishiwa na ubize, kila wakati yuko bize, asipokuwa bize na kazi basi yupo bize na marafiki, asipokuwa bize na marafiki basi na kitu kingine chochote tu ilimradi yuko bize muda wote. Siku ya jumamosi niliamua kwenda kwake.



    Patrick alikuwa hafahamiki kwetu hivyo nilidanganya nyumbani kuwa ninaenda kwa rafiki yangu, mama aliniruhusu.



    Niliondoka hadi kwa Patrick sikutaka kumuambia kwamba naenda.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku hiyo ya jumamosi Patrick hakuwepo nyumbani, kwakuwa ninafahamu sehemu ambayo Patrick huwa anaweka funguo yake nilifungua na kuingia ndani na kisha nikampigia simu.



    “Patrick niko kwako nakusubiri.”



    “Sociolah mbona umekuja bila kuniambia leo mimi siko nyumbani siku nzima.” “Patrick you are not serious”



    “Sociolah niko bize sana naomba tu uende nyumbani.” “Patrick nina shida ndiyo maana nimekuja.”

    “Sema unataka shilingi ngapi.” Kiukweli ilinikera sana.



    Mbali na kuwa nilikuwa nikihitaji hela lakini pia nikihitaji faraja kutoka kwake.



    “Sawa.” Nilikata simu.



    Sikuwa na pa kwenda niliamua tu kumalizia tu siku yangu hapo, niliingia chumbani kwake na kulala.



    Jioni ilifika Patrick hakuwa kweli amerejea niliondoka na kuelekea nyumbani. Nilipofika sikutaka hata kula niliingia chumbani kwangu na kulala, mama alikuja kuniamsha,



    “Sociolah amka uende kula.”



    “Mama nimechoka sana.”



    “Nimesema amka uende kula, siku hizi umekuwa mvivu sana kula sijui una matatizo gani Sociolah, utakonda chuo hakihitaji mchezomchezo kula mwanangu.” Sikutaka kubishana naye nilielekea sebuleni nilikula kidogo na kisha kurudi chumbani kwangu.



    Nilipofika tu nilikuta simu yangu inaita alikuwa ni Patrick, nilipotaka tu kupokea ilikata, nilikuta simu zisizopokelewa saba na meseji tano, zote zilikuwa za Patrick, alipiga tena nilipokea.



    “Hello.”



    “Am sorry Sociolah nilikuwa niko bize na saa hizi nimerejea nyumbani ulikuwa na tatizo gani.”



    “Patrick….”



    “Nakusikiliza.” Aliongea.



    Patrick ni mtu ambaye ananisikiliza sana na kunijali na alikuwa akinipenda sana na zaidi ya yote alikuwa ana malengo mazuri tu na mimi ila ubize wake ulinikera sana. “Niambie Sociolah shida ni nini mama?”



    “Patrick kuna mambo yananichanganya sana nilikuwa nahitaji faraja kutoka kwako



    ingawa uko bize sana. Hata hivyo nilikuwa nahitaji pesa maana nimeibiwa hela



    zangu na siwezi kumuambia mama.”



    “Unahitaji kama shilingi ngapi?”



    “Yoyote tu mimi siwezi kukupangia.”



    “Umeibiwa shilingi ngapi?”



    “Nimeibiwa kama laki tano hivi.”



    “Pole, nitakutumia.”



    “Nitashukuru sana.”



    “Aya, usiku mwema.”



    “Patrick hautaki hata kuongea na mimi kidogo.”



    “Kuna kazi nafanya hapa mama, nitakupigia nikimaliza.” Nilijua kwamba hatonipigia kwa maana hamalizagi kazi zake. “Sawa usiku mwema.”



    Alikata simu yake.



    Kwa kiasi Fulani nilijihisi afueni.



    Haikupita dakika kadhaa Patrick alinitumia laki tano, nilifurahi sana.



    Siku ya jumapili nilirejea bwenini kwetu Mabibo na siku ya jumatatu tuliingia kwenye vipindi kama kawaida.



    Melania bado hakuwa amepata simu yake hivyo alikuwa mtu mwenye Hasira



    muda wote na manung’uniko.



    “Usijali utapata.”



    Ilipofika saa sita kasoro dakika tano tuliingia kwenye semina.



    Kiongozi wa semina ile alitupa maelekezo machache kuhusu semina yetu na kisha akatugawa katika makundi kwa ajili ya kazi ya kuwasilisha. Daktari Kisayeye alianza kwa kuongea.



    “Makundi yapo matano kundi la kwanza mtawasilisha jumatatu ijayo, kundi hili lina watu wanne, Sociolah Kivamba”



    “Mmmh..!” Kwanza nilishituka lakini pia nilifurahi kuwa wa kwanza kuwasilisha kazi bila kuwa na uzoefu wowote ilikuwa siyo jambo dogo.



    “Melania Petro”



    “Woow...!” Nilifurahi sana…. Nilifurahi kuwa na Melania katika kundi moja.



    “Innocent Chande.” Hata sikuwa nikimfahamu ni kwa mara ya kwanza nimekutana naye.



    Watu wote tuliotajwa ilibidi tusimame ili tufahamiane alisimama huyo Innocent, alikuwa ni mkaka mzuri sana nilifurahi kuwa naye Kundi moja alikuwa mtanashati mno.



    “Na wa mwisho atakuwa ni Franklin Kazimana.” Nilihisi kuzimia.



    “Frank tena?!”



    Melania ambaye uso wake ulipambwa na Tabasamu ulibadilika ghafla, alichukia kupita maelezo nilishindwa hata kumtazama usoni.



    Daktari Kisayeye aliendelea kutaja watu katika makundi yao tofauti tofauti.



    Kiukweli nilianza kuichukia ile semina yetu.



    Kiongozi wetu alipoondoka tu Melania alikuwa wa kwanza kutoka darasani. Innocent aliniita, “Sociolah.”



    Niligeuka na kumfuata.



    “Unajua tuna kama siku chache tu hivi kabla hatujawasilisha kazi yetu inabidi tukutane tuanze kupanga mikakati, mbona mwenzio amekimbia.”



    “Aanh.. atakuwa hajisikii vizuri, tunakutana lini?” “Kwani nyie mnakaa wapi?” Aliuliza. “Tunakaa mabibo.”



    “Basi tukatane leo saa moja Mabibo.”



    “Sawa.” Niliongea na kuondoka, nyuma yake nilimuacha Frank akipiga hatua kumkaribia Innocent, niliwaacha waendelee na maongezi yao na mimi niliondoka. Baada ya kumaliza vipindi vyote tulirejea Mabibo.



    Saa moja kamili ya siku hiyo ilitukuta katika Vimbweta vya Block A.



    Melania alikuwa bado amenuna.



    “Huyu mwalimu shetani kweli akachagua watu akaona bora atuweke na huyu chizi.”



    “Melania acha bwana aaah.”



    “Mimi sijui kama nitakuwa Comfortable kwa kweli na huyu taahira huyu.” Frank na Innocent walikuwa wakipiga hatua wakijongea upande wetu.



    Melania alivuta mdomo baada ya kumuona Franklin, hakika alikuwa akimchukia sana.





    Franklin na Innocent walijongea mpaka kwenye vimbweta ambapo sisi tulikuwa tumekaa na kisha wakaketi.



    Franklin alibakia kimya tu wakati Innocent alitusalimia kwa uchangamfu wote na sisi tuliitikia kwa kuchangamka pia.



    Mara zote Innocent alikuwa ni mcheshi sana, Melania hakuishiwa kucheka lakini kila tu alipogeuka na kukutana na Frank alivuta tena mdomo. Tulianza kujadiliana swali letu tulilopewa na mwalimu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hapo niligundua kitu kingine kuhusiana na Frank hakika huyu kaka alikuwa ni jiniazi sana, alikuwa anamuelewa mwalimu zaidi ambavyo ni kawaida, aliweza kuyakumbuka maneno yote ambayo mwalimu alikuwa akiyaongea darasani nilimuelewa zaidi Frank kuliko nilivyokuwa nikimuelewa mwalimu alipenda kuongea kwa mifano, alielezea swali zima peke yake wala hakuna aliyekuwa akichangia na alielezea kila kitu kwa kweli ilikuwa ni ajabu sana. Mara zote Melania alikuwa amekasirika.



    Mara ghafla Melania alikunja sura nikashangaa “kwanini?” Kumbe aliona mabaki ya maharage kwenye meno ya Frank wakati Frank akiongea, nilishangaa sana kwanini Melania anamchunguza sana huyo mkaka wa watu.



    Melania alikaa katikati yangu na Innocent wakati Frank alikaa katikati yangu na Innocent.



    Tuliendelea kujadiliana hadi tulipofikia mwisho, baada ya hapo tuliagana na kila mtu kupewa kazi ya kufanya.



    Simu yangu iliita alikuwa ni daktari Kisayeye.



    “Hujambo Sociolah.”



    “Sijambo, shikamoo daktari.” Nilimsalimia. “Marhabaa, najua mnajiandaa na kazi niliyowapa.” Ndiyo.”



    “Sasa ili kuweka urahisi za kupata taarifa zote za kitaaluma ungetengeneza kikundi cha WhatsApp ili taarifa ziweze kuwafikia watu wengi kwa wakati mmoja, fanya hivyo mwanangu.” Aliongea daktari Kisayeye. “Sawa mwalimu nitafanya hivyo.”



    “Aya usiku mwema binti yangu.”



    “Ahsante na kwako pia.” Nilishukuru na kukata samu.



    Wakati huo Melania hakuwepo, Frank alikuwa tu amesimama kana kwamba hajui aelekee wapi. Innocent aliniita.



    “Sociolah kwani Melania ana nini?”



    “Kafanyaje kwani?” Niliuliza.



    “Kamsonya mkaka wa watu kiasi kwamba mpaka watu wote wameshituka wakamgeukia.”



    “Achana naye ana matatizo yake.” Niliongea kisha nikamuangalia Frank alibakia tu amenitolea macho kana kwamba hajui anaongeleshwa nini, nilimuangalia tu huku nikishindwa cha kuongea na mimi nikaondoka.



    Nilifika chumbani kwangu Melania alikuwa ana hasira bado nilijua sababu kubwa ni kwamba bado hakuwa amepata simu yake. Nilitengeneza kikundi cha WhatsApp kama nilivyoelekezwa na daktari Kisayeye, niliweza kuwaunga wanafunzi nilikuwa nikisoma nao darasa moja wale wachache ambao nilikuwa na namba zao na kisha nikaweza kuwaunga wengine waliobakia kwa kutumiwa namba zao. Kikundi kilikamilika, mtu mmoja tu hakuwepo kwenye kikundi naye alikuwa ni Franklin na Melania ambaye simu yake ilipotea ingawa nilimuunga.



    Mara baada ya kuwaunga wanafunzi kutoka katika darasa letu kila mtu alikuwa akimuulizia Franklin.



    “Yuko wapi matranka.” Mtu mmoja aliandika meseji, mtu huyo alikuwa akipenda sana utani, kila mtu alicheka.



    “Aah usikute atakuwa anapaka rangi tranka lake.” Mtu mwingine alituma meseji, watu waliendelea kucheka, kiukweli mimi iliniuzi sana nilichukia mno.



    “Hebu kuweni na heshima nyie.” Nilituma hiyo meseji.



    “Aah CR unamtetea mtu wako.”



    “Sio kwamba namtetea mjifunze kuheshimu hali za watu nyie ni watu wazima kwanini mnakuwa mnafanya mambo kama watoto wa sekondari hebu kueni basi.” Niliongea.



    Innocent naye alikuja juu.



    “Acheni mambo ya ajabu nyie yule ni mtu tena kawazidi vingi tu, msimchukulie kirahisirahisi kama mnavyomuona achaneni naye fanyeni mambo yenu.” Innocent alimtetea.



    “Sawa tumemsikia CR na handsome wa darasa.” Alionge msichana mmoja ambaye alikuwa anapenda sana utani na kisha watu wakaacha kumjadili Frank.



    Siku zilienda hatimaye siku ya kuwasilisha kwetu iliwadia tuliwasilisha vizuri. Daktari Kisayeye alimfurahia sana Franklin, hakusita kuelezea sifa zake mbele ya darasa.





    “Huyu mwanafunzi ni mwanafunzi bora na hajawahi kutokea hapa chuoni nitakupa zawadi kwa maana umeweza kuongelea kila kitu ambacho ninachokitaka umegusa maeneo nyeti sana, hakika wewe ni bora.” Alimsifia.



    Hakuna aliyejishughulisha kupiga makofi, hata nilipoanzisha hakuna mwingine aliyenifuatia, niliamua kuacha.



    Mara baada ya kuweza kuwasilisha tulitoka darasani Melania alikuwa hakuwa katika hali ya kawaida, aliniita.



    “Sociolah, mimi bila simu yangu kwa kweli maisha hayaendi.” “Usijali nitakufanyia mpango upate simu nyingine, usijali.” “Mama hawezi kunielewa nimepoteza simu nzuri hivi.” “Usijali utapata simu nyingine.”



    “Sawa mimi nataka tu nirudi bwenini Mabibo.” “Turudi tu hata mimi nimechoka.”



    Tulianza safari ya kutoka darasani hadi Shuttle Point kwa ajili ya kusubiri magari ya kuendea Mabibo.



    Tulitembea kwa hatua za kichovu sana hatimaye tulifika Shuttle Point. Wakati tukisubiri gari na hapo ndipo tulipomuona mwizi wa vitu vyetu, alikuwa ameshikilia simu ya Melania pamoja na wallet yangu mkononi akituijia mbele yetu. “Mwiziiii……” Ghafla bila kutarajia Melania aliita.



    Watu waligeuka na kutazama ni nani aliyekuwa mwizi wetu. Bila kuchelewa mwizi alishikwa na watu na muda si muda akaanza kupigwa.



    Mambo yalikuwa yakitokea harakaharaka kiasi kwamba sikuweza hata kunyanyua mdomo, nilibaki tu nikiwa nimetoa macho.



    Melania aliendelea kupayuka, “mwizii….. Mwizi…..”



    Watu walifika na kumvuta Shati Frank, nilishangaa vitu vyetu vimefikaje kwenye mikono ya Frank.



    Wakati nikiwa bado sielewi nini kimetokea ghafla alitokea Innocent alipangua watu waliokuwa wamemshika Frank na kisha akamvutia mikononi mwake.



    “Nini…. Kuna nini?” Aliwauliza.



    “Huyu jamaa ameiba vitu vya watu.” Akamgeukia Frank na kumtazama. “Mna uhakika kwamba ameiba?”



    “Ndiyo si hivyo hapo kavishika mkononi.”





    Wakati sisi tukitokea madarasani kwetu kwa ajili ya kuelekea Shuttle Point kupanda gari Frank alikuwa akija mbele yetu huku akiwa ameshikilia wallet yangu na simu ya Melania.



    “Mna uhakika na wewe unamuitia mwizi mtu kabla hujamuuliza.” Innocent aliendelea kufoka.



    Melania alinyamaza, tulishindwa cha kuongea tukabaki tukitazamana.



    Na wale watu waliokuwa tayari wameshamshika Frank na kutaka kumpiga walibaki wameduwaa.



    “Mmemsikiliza alichowaambia hivi unafikiria angekuwa ameiba angekuwa amevishikilia tu hivi anatembeatembea navyo.” Innocent aliongea hakuna aliyejibu. “Kwani amevipaje vitu vyetu.” Niliweza kuuliza. “Waambie Frank.” Alisema.



    Alishikwa na kigugumizi Frank, nilishangaa Frank huyu mwenye kuweza kuongea ameshikwaje na kigugumizi. Mwishowe aliweza kuongea.



    “Sociolah siku ile wakati ulivyokaa pale mbele halafu ukanyanyuka kwa hasira na kuelekea nyuma ulidodosha wallet yako.” Nilishangaa sana wala sikuwahi kuhisi kama ningeweza kuwa nimedondosha wallet yangu pale.



    “Jioni ya siku ile nilikufata pale mgahawani ili nikukabithi wallet yako lakini mlinitukana na kisha mkaondoka kabla sijakukabithi wallet yako na baada ya hapo mliondoka wote Melania alisahahu simu yake pale mezani, nilichukua siku ile na nikaja pale mgahawani na nikataka kuwakabidhi mkanimwagia juisi.”



    Kwa kweli ilikuwa ni aibu kubwa sana mbele za watu kila mtu alitutazama kwa jicho kali tulishindwa kunyanyua sura zetu.



    “Nimeamua kuwakabidhi kwa maana kila wakati nikitaka kuwakabidhi huwa hamtaki. Bahati mbaya simu ya Melania ilizima mda mrefu tu, nikaichaji kwa chaja ya mwenzangu kule chumbani lakini wala mimi sijui kuifungua simu yake, ningeweza kuwajulisha kwamba simu ninayo lakini ilishindikana.” Nilishindwa cha kuongea kwa kweli ilikuwa ni aibu sana nilitazama kando.



    “Wallet yako hii hapa hakikisha kama iko salama na Melania simu yako hii hapa iangalie pia.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Aliipokea kwa fujo na papara zote aliikagua simu yake ilikuwa kama ilivyokuwa cha zaidi alikuwa ameichaji. Aliifungua na kukuta kila kitu kiko salama wala havikufunguliwa, kwa kweli nilishindwa hata kufungua wallet yangu.





    “Fungua Sociolah uangalie.” Nilifungua, nilikuta fedha taslimu shilingi laki tano kama zilivyokuwa kila kitu changu kilikuwepo na hakuna kitu kilichopunguka wala kuongezeka, nilishangaa sana.



    Melania alishindwa hata kumshukuru Frank alihisi aibu aliondoka ghafla huku akilia na kukimbilia kwenye gari.



    Watu waliokuwepo wameanza kukusanyika pale walianza kuondoka na mwishowe tulibaki mimi, Frank na Innocent.



    Innocent alinitazama tu nilinyanyua uso na kuwakuta wamesimama mbele yangu kana kwamba hawana mahali pa kwenda.



    “Ahsante Frank, and am sorry for everything.” Niliweza kusema.



    “Usijali.” Alivyomaliza kusema aliondoka.



    Innocent alibaki akinitazama tu.



    “Kuwa makini.” Aliongea na kisha kuondoka.



    Niliwaangalia hadi walipoishilia kwa aibu nilitoka pale na kuingia kwenye gari sikutaka hata kwenda kukaa karibu na Melania. Gari lilipojaa dereva alikuja na tulianza safari ya kuelekea Mabibo.



    Tulipofika Mabibo habari ile ilikuwa gumzo katika kikundi chetu cha WhatsApp.



    “Kumbe jamaa alikuwa mwizi duuh!” Mtu mmoja aliongea.



    “Hamna wewe hukuona vizuri wala hukusikia mchezo mzima ulivyokuwa wamemsingizia tu, CR umemsingizia mtoto wa watu kaiba jamani.” “Sio mimi.” Nilijitetea.



    “Ni Melania.”



    “Aah na wewe si mlikuwa naye bana mnanyanyasa sana mtoto wa watu.” Aliongea “Ila kajamaa kanaweza kuwa kaizi hadi mkopo apate tutakuwa tumepigika vibaya, hivi hayupo humu.”



    Mdada aliingia, “hana simu ya WhatsApp.”





    “Msijali boom litaingia hivi karibuni na atanunua simu yake.” Innocent aliandika. “Halafu jamaa acheni dharau za ajabu ajabu mimi kitendo kilichotekea leo sijakipenda, sio leo tu nawaona jinsi mnavyomchukulia Frank.” Innocent alikuja juu.



    “Ni sawa Frank ametokea kwenye Familia ya kimasikini lakini jamaa anajua ni nini kimemleta hapa, subirini tu mwenzenu anaishi maisha ya shida subirini hata apate basi boom lake aweze kununua simu sio vizuri kumsema mtu kulingana na





    sehemu tulizopo wengine hapa wana maisha magumu kwao lakini bado wanaigiza bora Frank anaishi maisha yake halisia.” Aliongea kiukweli maneno yake yalinigusa.



    “Amepata mkopo?” Niliuliza.



    “Ndiyo amepata na wameshasaini boom wanasubiri tu liingizwe.” “Sawa.” Nilijibu.



    Muda ulienda na tulianza mitihani yetu ya kwanza ubize uliongezeka kati yetu na matukio ya ajabu ajabu hayakuwepo na ilikuwa kwa nadra sana kukutana na Frank aidha darasani au kwenye korido za darasa zetu. Mara nyingi tulikuwa tuko bize sana.



    Niliweza kuona Frank akiwa na simu mpya aina ya Tecno Y3+, nafikiri aliinunua baada ya kupata boom lake hata mavazi yake pia yalianza kubadilika kidogo ingawa bado alikuwa akivaa kiushamba ushamba lakini alikuwa na afadhali sio kama hapo mwanzo.



    Siku zilisogea na hatimaye sikukuu za Christmas na mwaka mpya zilikaribia, hapo tuliweza kufunga kwa muda wa wiki mmoja na nusu. Baada ya kufunga nilirudi nyumbani.



    Ilikuwa ni siku ya ijumaa ambapo Christmas ilikuwa ni jumatatu nilikuwa tu nyumbani sina cha kufanya niliamua kuvuta madaftari yangu na kuanza kupitia pitia kuna sehemu ilinishinda, niliamua kuuliza kwenye kikundi cha WhatsApp hakuna aliyeweza kunisaidia.



    Nilikuwa nikihitaji sana kujua hiko kitu lakini hakuna mtu aliyeweza kunijibu. “Jamani naombeni basi mnijibu.”



    Wengine walicheka na wengine waliondoka kabisa hewani.



    Nikaamua kutoka hewani na kukaa nilishindwa kuendelea kusoma kwa maana kilikuwa ni kitu cha muhimu sana baada ya muda niliamua kurejea hewani nilishangaa nilishangazwa kukutana na jibu kutoka kwa Frank, alielezea vizuri kiasi kwamba nilielewa.



    “Ahsante sana Franklin.” Niliongea.



    “Usijali.” Alisema.



    Niliona haitoshi nikaamua kuingia sehemu yake ya ujumbe mfupi, “Thank Frank.”



    “Usijali Sociolah.” Alijibu kwa ufupi.



    “Well... Unaonekana uko makini sana darasani.” Niliamua kuendeleza maongezi yetu.



    “Aah Sociolah si nilishakuambia.”



    “Yes I appreciate you.”



    “Do you appreciate me.”



    “Yes I do.”



    “Thank you.”



    “Well.”



    Ilikuwa ni siku ya jumamosi nilitoka nyumbani eneo la Mbezi beach na kuelekea Mabibo hostel kwa ajili ya kusuka. Nilikuwa nikipendelea sana kusuka kwenye saluni za Mabibo hasa hasa saluni flani hivi ambayo nilikuwa nimeizoea sana walinihudumia kwa ucheshi na mara zote walikuwa wananishauri jinsi ya kutunza nywele zangu na mtindo mzuri wa kusuka mara zote nilipenda kusuka kwenye saluni hiyo.



    Na siku hiyo niliamua kwenda kushonea weaving refu.



    Niliondoka nyumbani nikiwa nimevaa gauni langu la rangi ya maruni lililokuwa fupi kidogo, jepesi na mikono yake ilikuwa ni miembamba sana, chini nilivaa viatu vya wazi.



    Sikutaka kuondoka na gari niliamua kupanda usafiri wa jumuiya.



    Nilifika Mabibo mida ya saa nane nikaelekea dukani, nikanunua weaving na baada ya hapo nikaelekea saluni kwa ajili ya kusuka.



    Nilimaliza muda ulikuwa umeenda kidogo kiasi kama saa kumi na moja za jioni baada ya hapo niliamua kwenda kumsalimia Monica chumbani kwetu kwa maana hakuwa ameondoka kwa ajili ya likizo. Watu wengi hawakuwepo mule ndani nafikiri asilimia kubwa ya watu walikuwa wameondoka kwa ajili ya likizo.



    Nilienda moja kwa moja hadi chumbani kwetu niligonga sana lakini mlango haukufunguliwa, nilijaribu kumpigia simu Monica hakuwa akipatikana sikujua alikuwa ameelekea wapi hata hivyo haikuwa na umuhimu sana niliamua kutoka zangu na kurejea nyumbani.



    Nilipofika nje ya block yetu nilishangaa kuona giza limetanda kulikuwa na wingu zito lililoashiria kwamba mvua itanyesha muda si mrefu nilishangaa sana.



    “Hizi mvua za ajabu ajabu zinatokea wapi dakika mbili tu kuingia ndani na kutoka ndiyo wingu limejaa hivi, eenh!” Nilishangaa.



    Nilipiga hatua za haraka haraka kwa ajili kuondoka wala sikufika mbali mvua ilianza kunyesha kwa nguvu zote kana kwamba ilikuwa inazuia nisiondoke.



    Mvua kubwa ilinyesha radi zilianza kupiga na upepo mkali ulivuma nilikuwa nikitembea kwa shida nilianza kuogopa kila mtu alikuwa akikimbia na kujificha,





    nilishindwa niende wapi nilibakia tu nimechanganyikiwa nilikuwa sijui hata naelekea wapi.



    Mara gafla nakutana na Frank akitokea getini akiingia ndani alikuwa ameshika mwamvuli na alikuwa akitembea kwa hatua za haraka haraka.



    “Frank..” Niliita baada ya kuonyesha dalili za kutaka kunipita.



    “Sociolah unaenda wapi?”



    “Naenda nyumbani.” Niliongea kwa kutetemeka.



    “Na mvua hii..? Huko nje hakufai kabisa.”



    “Sasa nitakaa wapi na kule chumbani kwetu hakuna mtu.”



    Radi kubwa ilipiga nilikimbia kwa nguvu zote na kwenda kumkumbatia Frank nikijificha kwake.



    “Aah, twende kule kwetu mvua ikiisha utaondoka.” Hata sikujishughulisha kufikiria hakika nilikuwa nikiogopa radi kuliko kitu chochote.



    Tulitembea kwa hatua za haraka haraka huku nikiwa nimejifunika katika mwamvuli wa Frank hadi tulipofika kwenye block yao, Frank alikuwa akikaa block C.



    “Unakaa Room namba ngapi?” Nilimuuliza. “Nakaa room namba 415.” Alisema. “Huuu…! Ghorofa ya tatu?” “Ndio.”



    “Sasa huko si karibu sana na radi.” Nilimuuliza, alicheka.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Karibu na radi..?! Mmh!”



    “Mimi ninaogopa radi jamani twende haraka.” Nilisena.



    Tulipanda ngazi haraka haraka hadi kufikia ghorofa ya tatu, tuliingia umo nilishangaa kukuta hakuna mtu.



    “Frank wenzio wako wapi?”



    “Wameondoka wote wameenda likizo.”



    “Aanh! We Frank si unatokea Morogoro? Kwanini hukuenda likizo sasa si hapo tu karibu?” Nilimuuliza.



    “Kama ningeenda likizo unafikiri leo ungepata wapi hifadhi.” Aliongea kitu kilichonifanya nijisikie aibu sana niliishiwa namna ya kutaka kuendelea kuongea naye, maswali yote yaliniisha niliamua tu kunyamaza kimya.



    Niliamua kutoa simu kwa ajili ya kumpigia mama ili nimwambie nimekwama Mabibo kutokana na mvua na radi.



    Lahaulaa…!!



    Simu ilizima.



    “Mungu wangu nitatoaje taarifa nyumbani?” Nilibaki tu nimeshangaa. “Hauna chaja?”



    Nilifungua pochi yangu na kutoa chaja yangu, chaja yangu haikuwa ikitumia USB niliichomeka na kuanza kuchaji. Hazikupita dakika mbili umeme ulikatika.



    “Ooh my God! Niliishiwa puimzi nilibaki tu nimesimama uko chumbani kana kwamba sijui nifanye nini.



    “Nitafanyaje Frank?”



    “Hauna USB?” Aliniuliza.



    “Si unaona kabisa chaja yangu haina USB.” “Basi pole.” Alisema.



    “Ooh my God….!”



    “Bahata mbaya hata mimi chaji yangu haina USB ningekuunganishia kwenye kompyuta yangu ungechaji.”



    “Ooh, usiongee basi.” Nilishikwa na hasira.



    “Aanh, ngoja ninyameze kimya.” Alivuta kiti na kukaa.



    Nilienda kukaa pembeni ya kitanda na baridi lilianza kuwa kali na mvua haikuonyesha dalili ya kukatika. Nilianza kutetemeka, nguo yangu nyepesi ilinisaliti.



    “Frank hauna koti?” Hatimaye nilishindwa kuvumilia. Aligeuka akanitazama na kisha akaachia tabasamu murua.



    “Kwa kweli sina, ningekuwa nalo ningekuwa nimekwishakupa muda mrefu sana nakuona jinsi unavyoteseka na baridi.” Maneno yake yalinitia faraja ingawa hayakuweza kunisaidia.



    “Ooh…” Nilikuwa nikitetemeka mpaka meno yakingongana.



    Frank hakuwa mchafu kama alivyozoeleka, mavazi yake tu hayakuwa nadhifu, kitandani kwake palikuwa pamepangiliwa vizuri, shuka lililopauka rangi na mto ulionesha kwamba umechoka kulaliwa kwakuwa umetumika muda mrefu ulikuwa na kila dalili zote za kulegea pamoja na blanketi ama shuka zito zito.



    “Chukua blanketi hilo ujifunike.” Alisema.



    Nilivuta bila kuuliza nikalichukua nikalifunika, nikiwa nimekaa pembezoni mwa kitanda.



    Giza nalo lilianza kuingia na umeme ulikuwa umekatika.



    “Frank hauna hata tochi.”



    “Hapana sina.”



    Nilizidi kuchanganyikiwa sikuwa hata najua ni nini cha kufanya.



    “Hebu niazime simu yako basi nipige simu nyumbani.” Alinipa.



    Kwenye kioo cha simu yake Frank aliweka picha yake hakika alionekana ni mkaka mzuri na wa kuvutia kuliko wote niliowahi kukutana nao nilimfaninisha na ile picha hakika walifanana sana ingawa picha ilionekana kuwa na uzuri, nilimuangalia tu bila kukoma wakati Frank alikuwa akitazama nje, mvua nayo ilizidi kuongezeka.



    Nilibonyeza namba za simu za mama yangu na kisha nikapiga.



    “Halloo…”



    “Hallo.”



    “Mama.”



    “Mwanangu Sociolah uko wapi? Tumekaa hapa tunamashaka sana juu yako, uko salama mwanangu.” Mama aliongea mfululizo.



    “Niko salama mama lakini niko Mabibo nimeshindwa kuondoka huku kwasababu ya mvua.”



    “Uko mahali salama mwanangu?” Nilimuangalia Frank.



    “Ndio mama.”



    “Naomba tu usirejee nyumbani maana huku njiani hapafai ni maafuriko kila kona kuna magari yamesombwa hapo na abiria, ningeweza kuja kukufuata mwanangu lakini nahofia usala wako na wangu pia, kama uko salama endelea kukaa mvua itakapoisha nitakuja mwenyewe kukuchukua mwanangu, sawa.” Mama aliongea na kisha simu ikakata ghafla, simu ya Frank nayo ilikuwa imezima chaji.



    “Oooh…” Nilivuta pumzi na kuzishusha.



    Baridi ilianza kuwa kali ilinilazimu kupanda kitandani kabisa, nilivua viatu vyangu na kisha nikasogea hadi mwisho wa kitanda.



    Frank naye alianza kutetemeka nilimuonea huruma.



    “Frank…” Nilimuita, alinigeukia.



    “Unahisi baridi?”



    “Hapana, kawaida tu.” Alijinyoosha kuonesha kuwa yuko kawaida ingawa nilimuona kabisa alikuwa akiteswa na baridi ile. Radi ziliendelea kupiga nilizidi kupiga kelele.



    “Sasa Socialah kelele za nini?”



    “Wewe huoni radi zinapiga?”



    “Kwahiyo ukipiga kelele ndiyo radi zinaacha?” Niliamua kunyamaza tu kimya.



    Giza lilizidi kuwa zito mule ndani.



    “Frank giza linazidi.”



    Alinyanyuka bila kuongea chochote, alienda kufungua kabati lake na kisha kutoa kompyuta yake ndogo, alikuja na kuiweka pale kitandani, aliiwasha na kisha kuweka filamu ya kiamerika.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Filamu hiyo ilikuwa ikiitwa “Perfect Match.”



    Kwa kiasi Fulani mwanga wa kompyuta ile ulileta mwangaza mule ndani.



    “Sogea huko.” Aliniambia.



    Nilisogea na kisha akaja kukaa pembeni yangu, nilimuonea huruma jinsi alivyokuwa akitetemeka.



    “Chukua blanketi.” Nilimuambia.



    “Hapana, usijali niko salama.” Aliongea.



    Muda ulizidi kwenda filamu ilikuwa nzuri sana ambayo ilinifanya muda mwingine niachie kicheko cha nguvu, alikuwa akinitazama tu.



    Muda ulizidi kwenda nilianza kuhisi kuchoka, usingizi ulianza kunivamia kwa kasi. Nilishindwa kuendelea kujizuia, nilijikuta nimedondokea begani kwake na kisha nikadondokea moja kwa moja kwenye mapaja yake.



    Miale ya jua isiyo na nguvu iliniamsha kutoka usingizini, kabla sijafungua mboni za macho yangu niliachia tabasamu ambalo ni kwa nadra sana kuonekana usoni kwangu. Niliendelea kutabasamu hali ya kumbukumbu ya kilichotokea usiku uliopita ikipita katika akili yangu.



    USIKU ULIOPITA



    Usingizi mwingi ulinielemea, nadondokea begani mwa Frank na mwishowe ninadondokea mapajani kwake. Sijui ni nini lakini nahisi ni nguvu ya asili kati ya mwanamke na mwanaume.



    Frank alisogeza kompyuta, akaiweka juu ya meza na kunisogeza vizuri ili nilale vizuri. Wakati huo niliweza kufumbua macho yangu, nilikuwa nikimtazama Franklin kwa ukaribu zaidi. Hakika alionekana ni kiumbe kipya mbele yangu.



    Franklin uzuri wake ulizidi mara elfu ya jinsi alivyo, macho yake makubwa, pua yake ndogo iliyopamba vyema uso wake pamoja na lipsi zake pana ambazo muda wote zilionekana kung’aa lakini kutokana na matunzo hafifu mara nyingi ulikuwa ukipauka.



    Usiku huo uling’aa mithili ya Tanzanite.



    Alikuwa na nyusi nyingi zilizojaza vyema juu ya macho yake, rangi yake nyeupe ya kuvutia ilizidi kumpamba, alikuwa na nywele nyingi nyeusi ambazo hakuzinyoa





    katika mitindo ya ajabu, nywele zake zilikuwa zimenyolewa kwa msawazo na wakati huo zilikuwa zimekuwa kidogo, ziliongeza haiba yake vizuri.



    Bila kutaraji nilijikuta nimemshika shingoni tulitazamana kwa muda hakuna aliyeweza kuongea lolote niliweza kuzihisi pumzi zake na bila shaka na yeye aliweza kuzihisi za kwangu.



    Nilishindwa tena kuendelea kumtazama nilimvutia kwangu na yeye alikuja kama aliyekuwa akisubiri kuanzwa.



    Frank aliufanya usiku wangu uwe ni wa kukumbukwa ingawa alionekana mshamba lakini alikuwa mjuvi.



    “You are awesome.” Niliongea kwa sauti ya kukata kata pale tulipofika mwisho.



    “Thanks.” Aliongea.



    Nilijihisi nimekamatika kwenye mikono yake. Na kama ni kuzama penzini basi kwa wakati huo nilikuwa nimezama kabisa.



    Sikujali kelele alizokuwa anapigiwa Franklin, sikujali dharau zote wala sikujali nini ambacho kimetokea kabla ya wakati huo. Sikujali watu wangenichukuliaje wala sikujali maisha baada ya hapo na pia sikujali muonekano wa Franklin nilichokuwa nikikifahamu kwa wakati huo ni kwamba ninampenda Franklin ingawa nilishindwa kumwambia.



    Baada ya safari hiyo Franklin alinibusu kwenye papi za midomo yangu na kisha akanibusu kwenye paji langu la uso na kunilaza kifuani kwake na hapo ndipo nilipoamkia asubuhi iliyofuata.



    Baada ya kumbukumbu hiyo kupita kwenye akili yangu hatimaye nilifumbua macho. Nilimsawili mwili wake uliojengeka vyema nadhani ni kutokana na shughuli za hapa na pale.



    Franklin hakuwa na mwili wenye manyama uzembe kama ilivyokuwa kwa Patrick, alikuwa na mwili uliojengenga vyema ambao vijana wa saa hizi wamezoea kuita wa “Six pack.”



    Alikuwa haishi hamu kumtazama tofauti na vile alivyokuwa akionekana katika mavazi yake ya ajabu ajabu. Franklin alikuwa ni aina ya wanaume ambao wangeweza kusumbua mjini kama tu angejali muonekano wake.



    Baada ya kuridhika na utalii wangu katika mwili wa Franklin niligeuka na kumtazama machoni hali nimelala kifuani kwake.



    Alionekana  kama mtu  mwenye  dalili  za  kutoka  usingizini  na  mara  si  mara



    alifumbua macho nilikwepesha macho yangu na kuyafumba kwa kuwa sikutaka



    ajue kwamba niliwahi kuamka.



    Alinibusu kwenye paji la uso.



    “Nimekuona.” Akaniambia nilishindwa kujizuia nikacheka na kisha nikafumbua macho.



    “Umenionaje?” Niliuliza kwa aibu za kike.



    “Nimekuona usingizini.” Nilicheka.



    “Usiku wako ulikuwaje?” Nilimuuliza.



    “Best.” Alijibu.



    “Wa kwako je?” Aliniongeza na swali jingine.” “Awesome.”



    “Well, umeamka poa mama?” Aliongea kwa sauti nzito ya kiume.



    “Ndio.” Nilijibu na kisha nikaachia tabasamu la mwaka.



    Alinibusu tena kwenye paji la uso na kisha alinyanyuka kutoka kitandani.



    Franklin alikuwa amevaa boksa chakavu nilimtazama alivyokuwa akitembea kana kwamba ni mfalme aliyekuwa akiingia katika hekalu lake, alitembea kwa hatua za pole pole hadi kwenye kabati lake, alifungua na alitumia dakika kadhaa hapo kabla ya kuondoka na kurudi tena kitandani.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sikuwa najua haswa ni nini alienda kufanya, alirudi akakaa pembeni yangu. Wakati huo nilikuwa na nguo ya ndani pekee na shuka lililonistiri, nilikuwa nimelishikilia kifuani kwangu nikiwa nimekaa pembezoni mwa kitanda. Alikuja na kuniangalia akaachia tabasamu nikatabasamu pia. Akanyanyuka na kisha akaelekea mahali ambapo zilikuwa zimetundikwa nguo kadhaa. Alichukua bukta akavaa iliyoonyesha miguu yake mizuri iliyojaa vyema kisha akachukua na shati ambalo lilikuwa na mikono mifupi akavaa, alitoka na ndoo mbili za maji.



    “Frank….” Nilimuita



    “Yes.” Aligeuka.



    Nilichukua tshirt kubwa kubwa lililokuwa katika nguo zilizokuwa zimetundikwa mahali hapo nikampelekea.



    “Vaa ili.” Alicheka tu, akachukua akalivaa na kisha akatoka nje.



    Nilirudi na kukaa pale nilipokuwa nimekaa nikitabasamu tu bila mpangilio wala sababu ya msingi.



    Dakika kama tano zilipita Frank aliingia, alikuwa amebeba ndoo mbili zenye maji.





    “Sociolah hamna watu huku kwahiyo ungeenda kuoga, nitakupeleka.” “Lakini sina mswaki wa ziada.”



    “Sijui unaweza kusubiri niende kufuata kule nje.” Niliachia lile shuka lililokuwa likinistiri na kunyanyuka.



    Frank alitoa macho kana kwamba hakutarajia kuniona mimi katika hali ya utupu, hilo nililitarajia. Nilipiga hatua za kiuvivu nikijongea upande wake, nilimkaribia na kusimama karibu yake kana kwamba aliyekuwa akinisubiri, Frank alinipokea kwa mikono miwili alinivuta karibu yake nikiwa na nguo ya ndani pekee.



    Alinishika kiuno mikono yake ya kiume ilikamata kiuno changu sawia nilihisi kutetereka.



    “Frank…..” Niliita kwa sauti iliyopwaya.



    “Nitaoga, nitapiga mswaki nikifika nyumbani usijali.” Hakunijibu.



    Alinivuta na kisha tukapeana busu refu bila kujali hatukuwa tumeswaki asubuhi hiyo, lilikuwa zuri sana sikutamani aniachie lakini busu lile lilidumu kwa sekunde chache tu na kisha Frank aliniachia.



    “Sociolah, umeme umesharudi weka simu chaji uwasiliane na mama.”



    Kama alinizindua usingizini, niliondoka na kisha nikalifuata shuka langu, nikalichukua na kisha kujistiri. Nikachomoa chaja kutoka kwenye pochi yangu na kisha nikachomeka simu yangu chaji.



    Baada ya kuanza kuingiza chaji nilitafuta nguo zangu, nikavaa na baada ya hapo nilisogea pale ilipo simu yangu ilikuwa ikipeleka chaji kwa haraka sana niliamua kuiwasha hivyohivyo. Nilipoiwasha tu meseji kadhaa ziliingia kulikuwa na kiasi kama meseji kumi na tano wakati meseji tisa zote zilikuwa ni za mama, sikujishughulisha kusoma. Nikaingia kwenye orodha ya majina na kulitafuta jina la mama. Kabla sijabonyeza simu iliita alikuwa ni mama nilipokea harakaharaka.



    “Hello Sociolah, uko wapi? Mwanangu nimeshafika hapa Mabibo.” Aliongea kwa haraka.



    Nilishikwa na kigugumizi nikashindwa cha kuongea, nikamtazama Frank alikuwa amesimama pembeni yangu.



    “Uko sehemu gani?” Nilimuuliza.



    “Niko hapa nje getini.” Mama alisema.



    “Ok, nipe dakika tano mama nakuja.”



    “Sawa nakusubiri mwanangu.” Aliongea na kukata.



    Niligeuka na kumtazama Frank.



    “Nasikia mama yako ni mhadhiri wa pale UDSM.” Frank aliuliza.



    “Yes.”



    “Hongera.” Alisema.



    Nilikusanya kila kitu changu na kisha nikasimama, nikamsogelea Franklin alinibusu kwenye paji la uso.



    “Bye.” Alinambia, nilitabasamu.



    “Tutawasiliana.” Nikaongea



    “Nikusindikize?” Aliniuliza wakati nilipofika mlangoni.



    “Hapana usijali.” Niliongea kwa upole nikaachia na tabasamu kali na kisha nikatoka.



    Nilitembea hatua za kivivu hadi getini mama yangu alikuwa amesimama getini akinisubiri, alinipokea mkoba wangu.



    “Ulikuwa salama mwanangu.” Aliniuliza.



    “Ndiyo mama.”



    Tulienda mpaka kwenye gari, alinifungulia mlango wa gari nikaingia ndani na kisha akaingia kwenye siti ya dereva na safari ya kuelekea nyumbani ikaanza. Mahusiano yetu yalizidi kustawi tulikuwa tukitumiana jumbe fupi mara kwa mara huku tukiongea mambo mbalimbali, Frank alikuwa ni mcheshi sana na nilifurahia nyakati zote tulizokuwa pamoja tulikuwa tukiongea kuhusu maswala mbalimbali na alikuwa akinichekesha sana, nilipenda sana kuwa karibu naye.



    Siku moja kabla ya siku kuu ya krismasi nyakati za jioni nilikuwa nikiongea na Frank.



    “Frank naomba tutoke kesho.”



    “Tunaenda wapi Sociolah.”



    “It will be a surprise.” Nilimuambia. “Unataka nikakutie aibu huko unakoenda.” Nilicheka “Hahahah….. Kwanini?”

    “Sociolah mimi na wewe tunaendana kweli?”



    “Haaa.. Usijali kuhusu hilo wewe sema kama uko tayari.” “Mimi niko tayari, lakini….”



    “Usiseme lakini kama umekubali kubali tu.”



    “Sawa niko tayari.”



    “Vizuri.”



    “Lakini mimi sina nguo ya kuvaa Sociolah nitakutia aibu.”





    “Aisee ukikubali sema umekubali usitoe lakini sawa, vyovyote vile utakavyo vaa mimi sitakuwa na shida navyo.”



    “Aaah wewe unasema tu wewe ngojea hiyo kesho wewe mwenyewe utajuta.” “Hahahah kwanini?”



    “Sociolah….” Sauti ya baba ikitokea ndani iliniita.



    “Frank I will call you later.” Nilimwambia. Nilikata simu na kisha kuelekea ndani. “Yes dad.”



    “Kesho tutaenda kusherekea sikukuu ya krismasi kwa baba yako mkubwa Oysterbay.”



    “Noo dad.” Niliongea.



    “Nini… Kuna nini?”



    “Baba mimi siwezi kwenda Oysterbay.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kwanini…? Utaenda.” Aliongea baba na kisha kuondoka.



    “Baba…..  Baba….”  Niliita  hakugeuka,  nilibaki  nimekaa  tu,  machozi  yalianza



    kunitoka na kisha kilio cha chini chini kilianza kusikika.



    “Sociolah  ….  Sociolah  una  nini  mwanangu,  unalia  nini?  Kuna  tatizo?  Baba



    amekupiga?”



    “Mama mimi nilikuwa na udhuru kwamba kesho sitaenda Oyster boy.” “Kwanini Sociolah hujui familia nzima tunatakiwa tuwepo.”



    “Hapana mama nilitamani niwepo lakini nina sehemu ninataka kwenda.”



    “Sehemu gani? Huwezi ukaahirisha ukaenda siku nyingine Sociolah huoni umuhimu wa siku ya kesho kuwepo kule.”



    “Mama kuna sherehe ya rafiki yangu na mimi ndiyo namsimamia.” Ilinibidi kudanganya.



    “Baba yako amesemaje?”



    “Baba hajataka hata kunisikiliza ameondoka tu.”





    “Ngoja nitajaribu kuongea naye halafu nitakuja kukwambia.”



    Nilitoa tabasamu la ushindi nilijua tu hakuna kitakachoharibika, baba huwa hasumbui mbele ya mama anampenda sana.



    Nilifurahia na kisha kuelekea chumani kwangu, nilibeba wallet yangu na kisha kuelekea Mlimani City. Nilichukua bajaji ambayo ilinifikisha kwa haraka Mlimani City.



    Nilimchagulia Fank nguo nzuri ambazo nilihisi ni saizi yake na zingeweza kumtosha nilimchagulia Suruali nyeusi nzuri, shati la mikono mirefu la rangi ya





    Maruni, tai nyeusi na kiatu kizuri sana cheusi niliamini vingempendeza sana nikamnunulia na vest pamoja na marashi na boxer nzuri nikavifunga vizuri na kisha kuelekea nyumbani.



    Nilipofika chumbani kwangu mama alikuja.



    “Eenh umetuletea zawadi gani?”



    “Aanh hamna mama hizi ni zawadi kwa ajili ya sherehe ya kesho.”



    “Aanh sawa baba yako amekuruhusu uende ila amesikitika sana kwamba hutokuwepo kule.”



    “Mama hata mimi pia nilitamani kuwepo lakini ndiyo hivyo tu mama naomba umuambia baba anisamehe siku nyingine haitotokea tena nilimuambia mama.” “Sawa.”



    Mama aliondoka alipoondoka tu Pink aliingia chumbani kwangu.



    “Wewe kwanini umeingia chumbani kwangu bila hodi ukinikuta sijavaa?”



    “Si umeingia sasa hivi hujavaa hujavaa nini.” Pink aliongea, nilicheka tu kwa maana alikuwa ni mkorofi na mwenye maneno mengi sana kuliko pacha wake Pinto. Pinto alikuwa mpole tu ila alikuwa mtundu na mara nyingi sana akiwa na Pink basi hapo mambo lazima yaharibike, mara nyingi sikupenda kuongozana nao hao wote wawili kwa maana lazima tukio litokee.



    “Aya niambie umefuata nini?”



    “Wewe dada nilikusikia unasema kesho utatoka out na mtu kwenye simu.” aliniambia.



    “Keleleee…, Nyau wewe.”



    “Aaah mama amekataza kuniita nyau.” Pink alisema.



    “Toka chumbani kwangu.”



    Mama aliita kwa sauti kutokea jikoni. “Kuna nini..?”



    “Mama dada Sociolah ananiita….” Nikamziba mdomo haraka.



    “Kelele.. Usimuambie mama chochote hata usimuambie kama umenisikia nikiongea kwenye simu umesikia.”



    “Nipe hela.” Alisema, sikuwa na jinsi. Pink kwa ninavyomjua angeenda kusema.



    Nilitoa noti ya elfu kumi na kumpa.



    “Usiseme sawa.” Alitoka chumbani kwangu. Mama aliongea.





    “Kuna nini?”



    “Hamna Pink alikuwa ananisumbua sumbua kidogo.”





    “Huyu Pink naye bwana.” Mama alitoka na kisha kuendelea na shughuli zake. Siku hiyo usiku huo tulielekea kanisani kwa ajili ya mkesha wa sherehe za krismasi tulisali na baada ya hapo ilipofika saa sita kamili nilitoka kanisani na kumpigia simu Frank

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Marry Christmas.”



    “Oooh thank you, niko kanisani hapa nimetoka nje mara moja tu na simu yako imeingia.”



    “Kanisa gani umeenda?”



    “Aanh niko tu kwenye jumuiya ya hapa hapa Mabibo kuna baadhi ya watu wapo hapa tumekutana.”



    “Aanh ibada ilikuwaje iko?”



    “Vizuri tu nimefurahia na wewe uko wapi?” Frank aliniuliza.



    “Niko kanisani nimetoka mara moja, hata hivyo ibada imeisha tunaelekea nyumbani.”



    “Ok Sociolah uwe na usiku mwema, ahsante sana.” “Ahsante pia.” Nilikata simu.



    Safari ya kuelekea nyumbani ilianza njia nzima niliwaza siku ya kesho, sijui itakuwaje, nitafurahi sana kuwa karibu yake. Tulitoka.



    Usiku huo ulipita.



    Asubuhi, mama, baba, Pink, Pinto na dada wa kazi Linah walijiandaa na kisha kuondoka.



    “Unaweza kutumia hiyo gari nyingine.” Baba alisema.





    Waliondoka na kisha kuniacha peke yangu nilioga huku nikiimba nyimbo mbalimbali, nilizunguka zunguka nikatafuta chai nikanywa.



    Nilipanga mtoko wetu uanze saa nane za mchana hivyo nilijizungusha zungusha hapo nyumbani muda ulipowadia niliaandaa vitu vyangu, niliandaa gauni zuri sana lenye kitambaa chepesi ya rangi ya Maruni nilinunua katika moja ya maduka ya Mlimani City lilikuwa ni gauni zuri sana nilivaa gauni hilo na kiatu kirefu sana cha rangi nyeusi, nilijipulizia marashi mazuri ya kike na shingoni nikavaa cheni niliyopewa zawadi na mama yangu ambayo ilikuwa imenakishiwa kwa dhahabu.



    Nilitoka na kuelekea mabweni ya Mabibo nilielekea moja kwa moja hadi chumbani kwa Frank, nilimkuta Frank amevaa fulana kubwa kubwa nyeusi yenye maandishi meupe ambayo sikujishughulisha hata kuyasoma, alikuwa amevaa na





    suruali ya kitambaa ambayo haikufika vizuri kwenye vifundo vya miguu kwa kweli nilishindwa kujizuia ilibidi kucheka.



    “Unacheka nini sasa?” Aliongea kwa sauti yake nzuri ya kiume.



    “Sasa ndiyo umevaa nini?”



    “Mimi si nilikwambia.”



    “Kwahiyo hapo ndiyo umeshajiandaa kwa ajili ya mtoko?” Niliongea huku nikicheka.



    “Eenh hapa bado kuweka viatu tu alivuta viatu vyake raba nyeupe, nilicheka nikamrushia ule mfuko.



    “Vaa hivyo.”



    Alifungua.



    “Woow nguo nzuri hivyo umepata wapi?”



    “Punguza maswali bwana Frank vaa tuondoke muda unaenda.” Niliongea, alitabasamu tu.



    Alijizungusha mara mbili mule chumbani kisha akanijia. “Sociolah unaweza kunipisha nivae.” Nilicheka. “Unaniogopa au unanionea aibu mimi?” “Nina aibu.” Aliongea huku akiinama.



    “Vaa tu wala hamna shida.” Alivua nguo mbele yangu na kisha kuvaa, hakika alipendeza sana zaidi ya sana.



    Nilitoa yale marashi niliyomnunulia na kisha nikampulizia.





    “Aah.. Sociolah ndiyo nini hivyo.” Nilicheka.



    “Si ili unukie vizuri.”



    “Aisee kweli nimekuwa nanukia kama maua fulani hivi.” Nilicheka tu.



    Alipendeza sana zaidi ya sana, mtu yoyote ambaye angemuona angehisi ni mvulana mtanashati kutoka kwenye familia tajiri. Hata hivyo nywele zake hazikuniridhisha tulitoka bwenini, nadhani watu walishindwa kumtambua kama ni Franklin yule aliyekuja na tranka chuoni.



    Tulipofika nje nilitafuta saluni nzuri ya kiume, tuliingia humo akatengenezwa nywele zake ambazo zilipunguzwa kwa mtindo mzuri, zilipakwa mafuta na kung’aa. Alipunguza nywele za pembeni na kisha nywele za kati kati ziliachwa kwa wingi hakika alipendeza sana, baada ya hapo alifanyiwa Scrub alionekana





    kuwa kamili, Frank alikuwa amependeza, niliona Frank ni mwanaume mzuri kuliko wote ambao nimekutana nao kila mtu aliyetuona nahisi alitutamania. Tuliondoka na kuelekea Blue pearl Hotel pale Ubungo. Tulipofika tulichagua sehemu nzuri iliyokuwa pweke ingawa siku hiyo ya sikukuu watu walikuwepo hata hivyo tulikuwa tumejitenga na watu.



    Tuliagiza vyakula kadri tulivyoweza ingawa Frank alionekana mshamba mshamba kwani tulipofika tu aliagiza pilau nyama nilicheka.



    “Tuletee mbuzi choma na ndizi.” Nilisema. “Aaah!!” Aliachia tu mdomo, nilicheka. “Frank unatumia wine?”



    “Aaah hapana wee…” Aliongea nilicheka. Muhudumu alishindwa kujizuia ilibidi na yeye acheke.



    “Mimi niletee tu pepsi.” Alisema, nilicheka.



    “Ok, mimi naomba uniletee dompo.”



    “Dompo!! Hiyo soda mbona sijawahi kuisikia.”



    Nilisema “Frank shiiii….”



    Muhudumu alicheka, nilimuambia



    “Ok nenda tukikuhitaji tena tutakuita.” Aliondoka.



    Tulikula, tulikunywa hadi jioni ilipofika. Giza lilianza kuingia.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilikuwa nikimshawishi sana Frank kunywa dompo.



    “Nipe nionje kidogo.”



    Alikunywa.



    “Mmmh chungu ila tamu.”



    Nilicheka.



    “Kunywa bwana.”



    “Kwani imetengenezwa na nini?”



    “Acha maswali maswali bwana wewe kunywa.” “Sasa si najua tu lakini Sociolah.”



    “Kunywa bwana aanh, ayo maswali mengine kamuulize mhadhiri.”



    Alicheka, aliendelea kunywa. Haukipita muda alianza safari za kwenda chooni kila muda, niliishia tu kucheka.



    “Sociolah mimi nahisi usingizi.” “Usingizi…!!” Hebu jikaze turudi bwenini.”

    “Siwezi Sociolah nahisi usingizi sana.” Alianza kulalia meza.



    “Mmh…” Niliguna.



    “Muhudumu….” Nilimuita muhudumu aliyepita karibu yangu.



    “Naomba utuchukulie chumba.”



    Nilichukua chumba kwa ajili yetu na kisha nilimuomba muhudumu anisaidie kumkokota Frank hadi chumbani kwetu.



    Tulifika chumbani Frank alijilaza kitandani, alifumbua macho na kuachia tabasamu.



    “Frank.” Nilimuita.



    “Vipi?” Aliongea kwa sauti iliyoonesha kilevi.



    “Unajisikiaje?”



    “Niko fresh tu.”



    Alinyanyuka na kusimama.



    “Aaanh Frank siyo wewe uliyekuwa umelewa?”



    “Nilikuwa tu nina usingizi mimi sijalewa.”



    “Oh God, sitaki kuamini, nini hasa lengo lako?”



    “Kulala.”



    Macho yangu yalikuwa kama yakiishiwa nuru, nilimtazama Frank katika macho yaliyokuwa yakisinzia.



    “Frank.” Nilimuita, hakunijibu badala yake alianza kupiga hatua za polepole akisogea upande wangu, nilirudi nyuma hatua moja kumzuia asifike.



    “Frank.” Nilimuita lakini hakuitikia ,alizidi kusogea na mimi nilizidi kurudi hadi nilipogota ukutani



    “Frank.” Alizidi kuja upande wangu.



    Nilinyoosha mikono yangu kumzuia.



    “Frank.”



    Aliidaka mikono yangu na kisha kuibabatiza ukutani na kisha alisogeza midomo yake karibu na ya kwangu.



    Lilifuatiwa na busu refu lililodumu kwa dakika chache na kisha aliniachia.



    “Sociolah.” Aliniita.



    Nilishindwa kujibu wala kunyanyua uso wangu.



    “Say something.” Aliniambia.



    “Nakupenda.” Nilijibu kwa sauti ya pole pole.



    Alinifuata akaninyanyua na kisha kunitupia kitandani, alivua nguo zake na kisha kunifuata pale kitandani nilihisi aibu sana hata hivyo nilifurahia kitendo kile kilichokuwa kikitendeka pale.





    Frank alinipa kile ambacho nilikuwa nikistahili kukipata, hakika ulikuwa usiku wa kukumbukwa sana.



    Tulipomaliza kufanya kile kilichotokana na asili ya maumbile nilijilaza kifuani kwake.



    “Frank… Nakupenda.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Sociolah.” Aliniita.



    “Yes.”



    “Ooh… Basi.” Alinyamaza.



    “Nakupenda pia.” Alijibu.



    “Frank kuna kitu ulikuwa unataka kuniambia ni nini?”



    “Hamna kitu mama.”



    “Bwana niambie.”



    “Sogea huku nikuambie.”



    Nilitoka kifuani kwake na kisha kulala pembeni yake.



    “Aanh nilitaka kukuambia…..”



    Alinivuta na kisha ndimi zetu zikakutana, baada ya busu hilo refu aliniachia.



    “Mmmh…” Nilishindwa hata cha kuongea.



    “Umefurahi.” Nilicheka tu, nikampiga kofi dogo shavuni.



    Na kisha usiku ule ulipita, wala sikukumbuka kurejea nyumbani usiku huo. Nilikuja kuamka ilikuwa asubuhi siku iliyofuata saa nne, niliamshwa na mlio wa simu.



    Frank alikuwa bado amelala niliamka na kuvuta simu yangu ambayo ilikatika muda huo huo. Ilikuwa ni simu kutoka kwa mama nilishituka.



    “Kumbe sikurejea nyumbani usiku uliopita mbona mama atanitafuna, nitaenda kumuambia nini?”



    Kuhamaki nilikuta simu zisizopokelewa 52 na meseji 72 na zote zilikuwa za mama “Mungu wangu…. Mungu wangu…..”



    “Frank…. Frank….” Niliita.



    “Mmmh” Aliitikia tu kwa kukoroma.



    “Niache nilale Sociolah nina usingizi.”



    “Saa nne saa hizi.” Aligutuka.



    “Sasa usiku huu unataka uende wapi?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Siyo saa nne ya usiku Frank ni saa nne asubuhu, Frank be serious…” Niliongea.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog