Search This Blog

Monday, October 24, 2022

NATAKA KUZAA - 5

 





    Chombezo : Nataka Kuzaa

    Sehemu Ya Tano (5)



    Nilipofika nyumbani nilipitiliza moja kwa moja chumbani kwangu.



    Sikukaa hata muda mrefu mlango wa chumba changu uligongwa kwa nguvu.



    “Sociolah fungua mlango.” Alikuwa ni baba.



    Nilinyanyuka  kwa  uchovu  nikikimbilia  kanga  iliyokuwa  pembeni  yangu  kwa



    maana nilikuwa tu na gauni jepesi.



    Nilifungua mlango.



    Baba aliingia kwa hasira zote ilibidi nimpishe. “Umechanganyikiwa wewe?” Nilishangaa.



    “Hivi hiyo ndiyo spidi ya kuendesha kweli umepewa gari unaanza kujifanya chizi.”


    Mama alibaki ameshangaa alikuwa akijaribu kumzuia baba asinifikie kwa maana hasira za baba zilionesha wazi kwamba anaweza kunipiga muda wowote.


    “Kuna nini kwani baba Sociolah?”


    “Umeona jinsi alivyokuwa anaendesha gari huko njiani kama chizi anaendesha gari kama yuko kwenye mashindano hivi unafikiri hiyo barabara nimejenga mimi.” Baba aliendelea kufoka.


    “Lakini baba Sociolah umeshawahi kumsikiliza binti yako kweli?”


    “Nimsikilize nini ana sababu gani ya kuendesha gari vile eeeh? Kama amechoka si akajitumbukize tu baharini kuliko kuendesha gari vile mwishowe apate ajali aharibu hadi na magari yangu.”


    Baba aliongea maneno yake na mimi niliinama tu na kushindwa kumjibu chochote. Ni kweli nilikuwa nimekosea ingawa baba angejaribu kuisikiliza sababu yangu angeniruhusu hata niongeze spidi zaidi ya ile ambayo nilikuwa nikiendesha kwa wakati ule.


    Aliongea nilimuacha aongee kila kitu ili hasira zake zipungue. Hasira zake zilipopungua kidogo aliondoka na kuniacha na mama. “Mwanangu una nini?”
    “Mama mimi kusema kweli siwezi chochote mama siwezi mimi siwezi.”


    “Usijali mwanangu pumzika ngoja nikakuandalie chakula nitakuja kuongea na wewe baadae.”


    Wakati mama anatoka alipishana na Kelvin.


    “Niambie mpenzi wangu.” Alisema Kelvin mara baada ya kufika karibu pale kitandani ambapo nilikuwa nimeketi.


    “Salama tu hakuna tatizo.”


    “Mbona unaonekana haupo sawa, mimi sipendi wazazi wanakukemea kemea wewe ni mke wa mtu tayari.”


    “Usijali ni mambo ya kawaida si unajua wakati mwingine nakosea kwa hiyo usijali


    bado mimi ni mtoto wao. Na tangu nilivyokuacha chuoni kichwa kinaniuma sana


    nahitaji muda wa kupumzika.”


    “Ooh pole sana pole.”


    “Wala hakuna shida usijali.”


    Tulikaa tukiongea mawili matatu huku tukipanga maisha yetu baada ya ndoa. Nilikuwa nikimchora tu jinsi alivyokuwa anaongea sikutaka agundue chochote. “Sociolah muda si muda unaenda kuwa mke wangu natambua kwamba tarehe za ndoa yetu zimerudishwa tuna kama wiki mbili tu kisha tutafunga ndoa naomba uwe siriazi.”


    Nilitabasamu.


    “Niko siriazi kwani kuna tatizo lolote?” “Hakuna ila inaelekea wewe unataka matatizo.” “Matatizo gani?” Alicheka. “Nimekuletea zawadi.”


    “Zawadi gani?”


    Alifungua begi lake na kisha kutoa boksi ambalo mara nyingi sana lilikuwa likitumika katika kuwekea zawadi.


    “Mmmh zawadi gani niambie kwanza kabla ujafungua.” Nilinyanyuka na kisha kuketi kitandani.


    “Sapraizi... Nakupa ufungue mwenyewe.” Niliichukua na kisha kuifungua kwa kiherehere.


    Kitu nilichokutana nacho hakikunishangaza wala haikuwa sapraizi kilinivuruga akili.


    Ilikuwa ni simu nzuri sana.


    Aina ya iphone 7.
     CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Moyo ulinilipuka puuu.... Na kisha nikamtizama.


    “What the hell.” Nilimuuliza


    “Haujafurahia?” Nilishikwa na kigugumizi nilishindwa niongee nini. “Nimefurahia lakini. Ahsante.”


    Nilishidwa kumalizia kitu ambacho nilitaka kukiongea.


    “Ahsante Kelvin simu nzuri nimeipenda.


    “Badilisha laini yako sasa hivi weka kwenye simu mpya.” Alisema.


    Nilisita kutoa simu yangu ambaye kioo chake kilikuwa kimeharibika vibaya. “Nitaweka baadae ngoja niiweke kwanza chaji.” “Hapana nimeishaichaji wewe badilisha sasa hivi.”


    Niliitoa simu yangu, nikitegemea mshangao kutoka kwake hata hivyo Kelvin hakushangaa.


    Alinisaidia kuifungua na kisha kutoa laini zangu na kila kitu ambacho kilikuwa kwenye simu yangu na baada ya hapo aliweka kwenye simu hiyo mpya na kisha kunikabidhi.


    “Enjoy.”


    Alisema mara baada ya kunikabidhi ile simu.


    Mambo yote yaliyokuwa yakitendeka hapo yalinivuruga akili yangu.


    Nilishindwa kuelewa jinsi dunia alivyokuwa ikienda nilibaki tu nikimtazama ingawa sijui kama nicheke au ninune au nikasirike. Alinigeukia na kisha kuniangalia.


    “Sociolah tuweke utani pembeni.”


    Niligeuka na kumtazama.


    Nikiachilia mbali kuiangalia simu mpya ambayo nilikuwa nimepewa.


    Sura yake ilionesha kwamba haitaji utani wa aina yoyote.


    “Aanh kama nilivyokuambia kwamba wewe ni mke wangu mtarajiwa Sociolah nataka unisikilize kwa makini na unielewe na unitii kama mumeo mtarajiwa.” Nilitabasamu kwa kulazimisha.


    “Nakusikia, nakuelewa na ninakutii.”


    “Ok sociolaha naomba urudishe document ambazo umechukua kule nyumbani.” Moyo ulinipasuka paa....


    Macho yalinitoka pima nisijue nini cha kusema.


    “Na usitake kuniambia kama hujachukua.” Aliendelea.


    “Nafahamu fika kwamba umechukua kama umesoma kama hujasoma naomba uzirudishe. Sijui unanielewa? Usitake kutumia hizo document kuzuia ndoa hiko


    kitu hakiwezekani nakuonya usije kujaribu. La muhimu ukitaka nikuoe au nisikuoe zirudishe hizo document ulipozichukua kabla sijabadilika na kuwa Kelvin mwingine mara moja. Baba yako ananisikiliza mimi na wala siyo wewe kwa maana hiyo basi rudisha document. Ninakuonya ujanja ujanja wowote ule utakupoteza wewe na familia yako.”


    Kila kitu ambacho nilitamani kukiongea kwa wakati huo kilishindwa kupita mdomoni nilibaki tu nimetoa macho nisijue ni nini cha kuongea. Nilitamani kuongea kitu chochote lakini nilishindwa.


    Aliendelea kuniangalia kwa macho yake makali.


    “Ni lini utazirudisha document zangu?” Aliniuliza.


    “Naongea na wewe sociolah.” Alinikemea.


    “Sirudishi.” Nilipata ujasiri wa kujibu.


    Alicheka.


    “Sina utani na wewe ninazitaka zile document mara moja.” Na mara mlango ulifunguliwa nilishukuru Mungu.


    Ni mama ndiye aliyeingia na alikuwa amebeba chakula.


    “Unaendeleaje saa hizi mwanangu?”


    “Naendelea vizuri.”


    “Nashukuru Kelvin yuko hapa anakutia moyo, si ndiyo? Lazima ujisikie vizuri.” Mama aliongea maneno yake yalinifanya nijisikie vibaya sana.


    Nilimuangalia Kelvin na kisha nikamfinya mama mkono mama alinitazama. Nilimuangalia Kelvin ambaye alikuwa akitazama dirishani huku akionekana kuwa na wimbi la mawazo.


    Nilimnong’oneza mama kuwa abaki na mimi wakati huo.


    Mama alikaa kitandani alianzisha mazungumzo yasiyoeleweka na Kelvin. Waliongea vizuri kana kwamba hakuna kitu nambacho kilipita ndani ya dakika chache zilizopita.


    Nilimuonya mama asije kutoka mule ndani.


    Mama alikaa mpaka ilipofika usiku mnene.


    Kelvin aliaga.


    “Kichwa kinaniuma sana Kelvin siwezi kukusindikiza.” Nilimuambia.


    “Nitarudisha vitu vyako.” Nilisema.


    “Utarudisha vitu gani?” Mama aliuliza.


    Kelvin alidakia harakaharaka.


    “Aaa hamna mama.”
    “Aya sawa.”


    Kelvin aliondoka.


    Nilirudi chumbani kwangu na kujitupia kitandani.


    Wala sikumbuki ni muda gani ambao nilipitiwa na usingizi.


    Nilikuja kuamka nikiwa nimechelewa sana ilikuwa kiasi kama cha saa nne asubuhi.


    Niliamka kiuvivu na kuelekea bafuni.


    Nilioga huku maneno ya Kelvin yakipita akilini kwangu na ile taswira ya sura yake nayo ilijirudia kwenye kichwa changu.


    Nilikuwa nikivuta pumzi na kuzishusha mara kwa mara sikutegemea kama


    nitaingia kwenye mtihani mzito.


    Niliamua moja kwa moja kumkabili baba.
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Nilifunga safari hadi ofisini kwake na wala sikuelekea chuoni.


    “Baba....” Nilipofika tu nilimuuliza.


    “Binti mbona umekuja ofisini bila kuniambia?”


    “Baba ni jambo la kushitukiza samahani kwa kuja ofisini kwako bila kukupa taarifa.”


    “Aanh usijali lakini hapa ni kwako mwanangu.” “Ahsante baba nina maswali kadhaa ninataka nikuulize.” “Ndiyo.”


    “Baba umejuana vipi na Kelvin?”


    “Hahaha unataka kwenda kumsapraizi nini?” Nilicheka.


    Hata hivyo sikutaka baba ajue kama kuna kitu kinaendelea.


    “Ndiyo baba.”


    “Kwanini usimuulize mwenyewe nafikiri angekuambia.”


    “Hapana baba yeye ana nafasi yake na wewe una nafasi yako wewe ni baba yangu siku zote utabakia kuwa baba yangu lakini mimi Kelvin nimemjua hivi karibuni nadhani niko na uhuru sana na wewe kuliko na yeye.” Alicheka tu baba.


    “Aanh Kelvin nilijuana naye kwa mtandao. Nilikuwa nikijaribu kutafuta promo kwa ajili ya dawa zangu mpya ambazo ninataka kuzitengeneza. Hizi dawa naweza kuzisambaza sehemu mbali mbali za dunia. Kwahiyo kupitia yeye ingekuwa rahisi sana kuzifikisha nje ya nchi kwasababu yeye ana kampuni yake ya usafirishaji kwa maana hiyo basi tulikubaliana biashara. Mimi ningezalisha bidhaa zangu na kuzisafirisha kwa kutumia kampuni yake mpaka nje ya nchi hasa Marekani kwasababu kule amewekeza na ana miradi mingi. Inamaanisha dawa hizo


    zingewafikia watu wengi na pia zingesaidia kupata hela nyingi. Ni hivyo tu mwanangu.”


    “Ilikuwaje baba mpaka ukamuamini kumuingiza kwenye biashara zako.”


    “Kwanza nilijenga ukaribu naye, nikamuamini, ni mtu muaminifu sana, ni mtu mzuri sana hata alipokuja kuniambia kuhusu swala la kutaka kukuoa kwa kweli nilijua mwanangu anaenda kwenye mikono salama.” Nilicheka ndani ya nafsi yangu.


    “Kumbe baba ni mjinga hivi?” Niliwaza.


    “Aanh baba unaamini kabisa kwamba Kelvin ananifaa?”


    “Ni kweli anakufaa kwa sababu ukiwa naye kwa sasa swala la pesa siyo shida utapendeza sana binti yangu, utaenda kila unapopataka, utapata kila unachokitaka.” “Mmmh baba mbali na hiyo Kampuni ya usafirishaji ya Kelvin kuna shughuli nyingine ambayo Kelvin anaifanya?”


    “Kwa kweli sijui na wala sijawahi kumuuliza.” Baba alijibu.


    Niliona baba anatoa majibu marahisi kwa maswali magumu.


    Nilijua baba hajui chochote kuhusiana na Kelvin.


    Nilibaki nikivuta pumzi na kuzishusha huku nikikuna kichwa.


    “Kuna nini?”


    “Aanh baba mimi nadhani umekosea sana kumuamini Kelvin.” Nilijikuta tu naongea.


    “Kwa nini?”


    “Kelvin hakupaswa kunioa.”


    Baba alitabasamu.


    Nilishindwa kuelewa kama ni alikuwa akielewa kitu ambacho nilikuwa nikimuambia, alitabasamu kwa dharau au kufurahia kile kitu ambacho nilikuwa nikimdokezea.


    “Baba ni lazima unielewe.”


    “Sikia Sociolah. Nilimpa nafasi Matranka aje akutane na mimi anielezee mikakati yake yote ya maisha pamoja na wewe. Nilimuita aje aniambie ana malengo gani na wewe hakuja mpaka leo. Bado unataka kuendelea kuwa naye?”


    Akili yangu ilivurugikwa sana na maneno ambayo baba alikuwa akiongea.


    “Ina maana ni kweli baba alimuambia Franklin kwamba wakutane na anafurahia sana kwa kuwa tupo pamoja. Kwa maana hiyo Frank hakunidanganya.” Maswali hayo yalipita kichwani kwangu.
    “Sikiliza nikuambie Sociolah nimekuweka kwa Kelvin uko mikono salama sitaki


    tena kusikia habari za Matranka.”


    “Hapana baba nisikilize.”


    “Nakusikiliza lakini usije ukasema chochote kuhusu Kelvin ninamfahamu.” Niliona nimeshidwa kupata msaada kutoka kwa baba yangu mzazi. Nilibaki nikiwa nimechanganyikiwa nisijue nini cha kufanya.


    “Sociolah una matatizo gani?”


    “Baba...” Nilimuita tu.


    “Ninaondoka.” Nilijikuta nimesema.


    “Una nini binti yangu.”


    “Naondoka baba tutaonana baadae.”


    Nilinyanyuka na kisha kuondoka.


    Baba alinipigia simu sana wakati niko njiani hata hivyo sikuzipokea.


    Niliendesha mpaka nilipofika maeneo ya chuoni.


    Nilipitiliza hadi katika kumbi za yombo na kisha kupaki gari langu.


    Sikushuka niliendelea kuwaza na kuwazua mahali pale.


    Mara ghafla simu yangu iliita.


    Alikuwa ni mama ndiye ambaye amepiga simu.


    “Sociolah...” Mama aliniita.


    “Ndiyo mama kuna nini?”


    “Uko wapi?”


    “Niko chuoni.”


    “Ulienda ofisini kwa baba yako.”


    “Ndiyo mama nilienda.”


    “Umeongea naye nini?”


    “Nilienda kumuuliza kuhusu Kelvin.”


    “Uko salama lakini?”


    “Niko salama mama.”


    “Sina imani kabisa kama uko salama naomba urudi nyumbani.”


    “Mama mwili wote una tetemeka tangu nimefika hapa chuoni sidhani kama naweza kuendesha gari naomba nipumzike. Nitarudi baadae.”


    Mama aliendelea kuniongelesha huku akitaka kujua hali yangu lakini ghafla simu iliyokuwa sikioni mkwangu ilianguka na kuangukia pembeni ya kiti nilichokuwa nimekalia.


    Hiyo ilikuwa ni mshituko mara baada ya kuwaona wote watatu.
    Ilikuwa ni gari ya Kelvin iliyokuwa ikikatiza mbele yangu.


    Dereva alikuwa ni Kelvin huku Melania akiwa amekaa pembeni yake na nyuma alikuwa ameketi Frank.
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Nilishindwa kuelewa kuna mahusiano gani kati ya hao watu watatu wote hao kwangu wameshakuwa watu wabaya.


    “Simtaki Frank, simtaki na Kelvin.”


    Niliongea pasipo kujua kwamba simu yangu ilikuwa bado haijakatika. “Nini Sociolah, kuna nini mwanangu?”


    Sauti ya mama ilinishitua.


    Niliokota simu na kisha kuweka sikioni.


    Niliangua kilio cha nguvu.


    “Usilie mwanangu subiri nakufuata hapo sasa hivi sawa.” Niliendelea kulia mule garini.


    Nusu saa ilipopita mama alikuwa amefika.


    Alikuwa amepanda pikipiki nilishangaa alipitaje pale.


    “Mwanangu uko salama?”


    “Niko salama.”


    Macho yalikuwa yamebadilika rangi na kuwa mekundu.


    Uso wote ulivimba alinikumbatia kwa upendo huku akionesha dalili zote za huzuni machozi yakimlengalenga.


    Aliniamishia upande wa abiria na kisha kuketi kwenye kiti cha dereva na safari ya kurudi nyumbani ilianza.


    Tulipofika nyumbani tulimkuta baba akiwa ameshafika.


    Alikuwa sebuleni tu akisimama huku akitembea tembea huku na huku.


    “Nyie mlikuwa wapi na kwanini hampokei simu? Sociolah una matatizo gani? Mimi ujinga ujinga wa aina yoyote ile sitaki kuusikia si unanielewa.”


    Mama alichukizwa sana na hali hiyo.


    “Baba Sociolah kila siku nakuambia hujawahi kumsikiliza binti yako siku utakapoamua kumsikiliza utakuwa umechelewa. Umekuwa mtu wa kupiga piga tu kelele. Huamini familia yako unamuamini mtu mwingine, unamsikiliza sana mtu mwingine kuliko kuisikiliza familia yako. Hivi unafikiri sociolah akiwa na shida aende kwa nani kama siyo kwako? Sipendi hiyo tabia muache binti yangu ni mtu mzima sasa si anaelekea kuwa mke wa mtu muache usimuingilie. Kumpigia pigia simu kila saa unatafuta nini?”


    “Yeye alikuja ofisini kwangu kufanya nini?”
    Baba na mama waliendelea kujibizana.


    “Kwani hamkuongea? Inamaanisha haukusikia maswali yake? Haujui kabisa kwamba alikuwa anaongea kuhusu nini?”


    Baba alinyamaza kimya ni kama alitafuta neno la kusema halafu akashindwa.


    Aliondoka moja kwa moja kuelekea chumbani kwake.


    Mama alinipeleka chumbani kwangu na kunilaza.


    Nilishindwa kujua jinsi ya kutoka katika shimo hilo ni bora baba yangu angekuwa akinielewa ingekuwa ni rahisi kama baba hanielewi, hamuelewi hata mama. Nilikuwa nina mtihani mzito sana mbele ambao uliitaji kuwa na moyo mkuu. Siku hiyo nilitoka kuungana na familia yote kwenye chakula cha jioni.


    “Dada kama hukai hapa.” Pink alisema.


    “Mmh..” Nilijilazimisha kutabasamu.


    “Sasa dada ukiondoka hapa sisi tutakumbuka sana jamani uwe unakaa na sisi.” Waliendelea kuongea.


    “Msijali.”


    “Kila saa tu unalala, kila saa tu umejifungia chumbani, kila saa tu uko chumbani ukitoka zako chuoni unaenda moja kwa moja kulala sijui kwa nini.” Pink aliendelea kuongea.


    Baba alikuwa ananikazia macho.


    Na mimi nilijilazimisha kutabasamu kwa kila hali.


    Mama alikuwa akinitazma huku akiangalia hatua zangu nadhani alikuwa akijiandaa kwa lolote ambalo lingetokea hasa katika kunitetea. Tulikula na tulipomaliza niliamua kutoa vyombo siku hiyo.


    Nilibeba vyombo na kuelekea jikoni.


    Nilipotaka kuondoka dada Linah aliniita.


    “Dada Sociolah.” Aliniita.


    Niligeuka na kumtazama.


    Hata hivyo sikuwa na mazoea naye niliamua kumsikiliza.


    “Nini?”


    “Samahani.” Aliongea.


    “Mchumba wako alikuja leo asubuhi.”


    Nilishangaa.


    “Anakujaje bila kutoa taarifa na anajua kabisa wakati huo mimi sipo nyumbani na hakuna mtu anayekuwepo nyumbani?”


    “Sijui. Alikuja akaomba kuingia chumbani kwako nikamruhusu aingie nadhani kuna kitu alikuwa anakitafuta.”


    “Mmmh... Kuna kitu alikuwa anakitafuta chumbani kwangu?!” Nilimuuliza. “Ndiyo.”


    “Nitakuja kuongea na wewe baadae usilale kabla ujaniona.” Niliondoka na kurudi mezani.


    Huku nikijitahidi kuonesha hakuna kitu kilichokuwa kikiendelea ingawa uso wangu ulinisaliti.


    “Dada..” Pinto aliniita.


    “Bee.”


    “Kuna kitu Pink anacho anataka kukuonesha.” “Kitu gani?” Nilimuuliza. “Pink si useme.” Pinto alisema.


    “Pink sema kabla sijakusema.” Pinto aliendelea kulalama.


    Pink alibaki tu ameniangalia.


    Macho yake yalionesha uoga.


    “Si useme kuna nini?”


    “Hawa watoto bwana wanasumbua tu.” Mama alisema.


    “Kweli mama anacho.” Pinto alisema.


    “Unaogopa kuniambia?”


    “Ndiyo utanichapa.” Pink alisema.


    “Hamna sikuchapi.”


    “Utanichapa wewe.”


    “Basi mpe mama.”


    Alimuangalia mama.


    “Mmh.. Sema hapa mimi nitamuambia dada asikuchape hawezi kukuchapa mimi nipo.”


    “Kuna kitu nilichukua.”


    “Kitu gani?”


    Na hapo ndipo niligundua kwamba muda wote alikuwa amefumbata mkono wake nyuma, mkono wake wa kushoto.”


    “Mimi nilichukua kitu chumbani kwa dada Sociolah leo nilivyotoka shuleni.”


    “Kitu gani?” Nilimuuliza.


    “Kilete hapa.” Mama alisema.


    Pink alishuka kwenye kiti kiuchovu hadi alipo mama.
    Alifumbua kiganja chake cha mkono wa kushoto na kisha kumkabidhi mama.


    Kila mtu alishituka.


    “Umepata wapi umesema?” Baba aliuliza. “Chumbani kwa dada Sociolah.” “Wewe kwanini ulichukua?”


    “Mimi nilikuwa nimeifananisha na risasi ndiyo maana nikaichukua. Niliichukua ili


    nimuulize Pinto.”


    “Pinto kakuambiaje?”


    “Kasema ni risasi.”


    “Sociolah risasi za nini?” Baba aliniuliza.


    “Baba mimi sijui chochote sijui imefikaje chumbani kwangu.” “Kwani nani ambaye anakaa kwenye chumba chako?” “Ni mimi baba kiukweli sijui.”


    “Sociolah....”


    Kila sehemu ya mwili wangu ilikuwa ikitetemeka.


    Bila shaka hiyo risasi iliachwa na Kelvin pale alipokuja chumbani kwangu.


    “Hebu ilete.” Baba alisema.


    Mama alimkabidhi risasi ile.


    Aliichunguza na kisha akaelekea chumbani kwake.
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Pink alikuwa amejikunyata pale bila shaka alionekana kuwa na hatia sana.


    “Nendeni mkalale.” Mama alisema.


    Walinyanyuka na kisha kuondoka.


    “Huu... Unafikiri imetoka wapi?” Mama alivuta pumzi ndefu na kisha kuniuliza. “Sikutaka kumuambia kuhusu ujio wa Kelvin hapo nyumbani.” “Sijui mama.”


    “Au ni ya baba.”


    “Inawezekana.”


    “Lakini kama ni ya baba imefikaje chumbani kwako.” “Nashindwa kuelewa hapo mama.”


    “Basi tuone, ngoja mimi niende chumbani baba yako atakuwa na hasira sana.” “Sawa mama. Usiku mwema.”


    Mama alinyanyuka na kisha kuelekea chumbani.


    Nilibaki sebuleni huku mawazo yakiwa mengi.


    Dada Linah baada ya kunisubiri muda mrefu jikoni alikuja sebuleni kuniangalia.


    Alinikuta bado nimekaa kwenye chumba cha kulia chakula.
    Alikuja na kukaa mbele yangu.


    Kuketi kwake kulinizindua katika mawazo nilishituka kama nimeona jini.


    “Dada kuna nini?” Aliniambia.


    “Aanh hamna umenishitua sikukuona wakati unakuja.” “Mbona nimekaa hapa kama dakika nzima.” “Mawazo tu.”


    “Unawaza kwasababu Kelvin alikuja hapa nyumbani bila kukuambia.”


    “Hamna nimewaza ni kitu gani alikuwa anatafuta. Kuna kitu aliondoka nacho?” Nilimuuliza.


    “Sidhani. Alikuja hajabeba kitu na akaondoka hivyohivyo.”


    “Dada inaonekana kabisa humpendi Kelvin. Naona tangu muanze uchumba wenu


    umekuwa huna amani.”


    “Niambie, alionekanaje?”


    Sikujibu swali lake bali niliuliza swali langu. “Yani sura yake wakati anakuja ilikuwajekuwaje?”


    “Kiukweli Kelvin ni mtu ambaye anapenda sana kutabasamu lakini hakuwa katika hali hiyo mimi mwenyewe ilinishangaza.”


    “Ok nina amani tu katika uchumba wangu, ninashukuru kwa taarifa usiku mwema.”


    Niliongea na kisha kunyanyuka kuelekea chumbani.


    Mawazo mengi yalinitawala.


    Niliamua kumtafuta.


    “Kelvin nimekumisi jamani mbona siku hizi huji kuniona?” Nilisema mara baada ya kupokea simu.


    “Mambo mengi si unajua naandaa harusi yetu.” “Najua lakini hata kunipigia simu.” “Samahani kwa hilo.”


    “Lakini hata ulikuwa hunikumbuki si unajua mimi niko chuoni.”


    “Uwe na amani Sociolah.”


    “Usijali. Ahsante.” Niliongea.


    “Basi hakuna shida nikutakie usiku mwema upende kulala mapema.” “Ahsante ila usisahau kurudisha document zangu.” “Mmmh..” Kwa kweli hapo alinikera sana.


    “Ulivyokuja kuzitafuta leo hukuziona.” Niliamua kumjibu.


    “Acha utoto Sociolah huniwezi ila nakuweza.” Aliongea na kisha kukata simu.


    “Mungu wangu! Ngoja tu nizirudishe.” Niliwaza. Kwa upande mwingine ukikataa kabisa nisizirudishe. “Natakiwa niwe na akili sana.”


    Asubuhi ya siku iliyofuata nilimpigia simu.


    “Kelvin naomba uje chuoni.”


    Alikuja.


    “Document zako hizi hapa sikuzifungua nadhani nilizibeba kwa makosa. Hata hivyo nimeshangaa sana umepaniki mno sijui hata kuna nini humo.”


    “Samahani sana ni vitu vya kibiashara unajua kama vinapotea lazima mtu


    uchanganyikiwe, samahani sana.”


    “Usijali kuhusu hilo.”


    “Naomba nisome.”


    “Aanh utasoma baadae saa hizi soma desa.” Aliongea kiutani.


    “Kelvin mimi nakupenda nashangaa unanifanyia vitu vya ajabu siku mbili hizi


    umekasirika sana nimeshangaa.”


    “Aanh hamna nikawaida tu.”


    “Tunakaribia kwenye ndoa lakini juzi nimekuona mtu tofauti kabisa.” “Nilichanganyikiwa kwenye mambo ya kibiashara Sociolah.” “Sawa hakuna shida.”


    “Ilimradi saa hizi nimeshakurudishia document zako uwe na amani. Nataka kumuona Kelvin wangu wa siku zote nilimuambia.” “Hakuna shida.”


    “Ok acha nikuache”.


    Alinikisi mdomoni na kisha kuondoka.


    Nilimtazama huku nikitabasamu mpaka alivyopotelea.


    Alipoingia kwenye gari yake na kuondoka niliachia msoyo wa nguvu na kisha


    nikaendelea na shughuli zangu.


    Sikutaka kuendelea tena kumfatilia.


    Siku zilijongea.


    Walitoa mahari na utambulisho hatimaye siku ya harusi yetu ilikaribia.


    Maandalizi yote yalikwishafanyika.


    Shera langu lilinunuliwa kwa gharama kubwa sana.


    Na lilibuniwa Marekani huko waliko wazazi wake.


    Cha kushanganza Kelvin alisema kwamba wazazi wake hawataweza kuhudhuria kutokana na kubanwa na majukumu hata hivyo aliniambia mara baada ya kufunga ndoa tungeenda kuwasalimia.”


    Nilijitahidi kuwa na furaha na kila mtu alionesha kuwa na furaha hata hivyo maumivu ya kichwa yalikuwa yakinisumbua mara kwa mara. Nilikosa muda wa kuwa na mama.


    Siku ya harusi yetu ilifika.


    Ratiba ya harusi yetu ilikuwa tayari imeshapangwa.


    Asubuhi takribani mida ya saa mbili ningeelekea saluni kwa ajili ya maandalizi yote ya kupambwa na kisha kuvaa.


    Baada ya hapo ningepata chakula cha mchana na kisha kuelekea sehemu mahususi ambapo tulitarajia kufunga harusi yetu.


    Harusi yetu ilipangwa kufungwa katika hoteli ya Sea cliff.


    Tungefunga ndoa yetu saa kumi na moja za jioni.


    Na mara baada ya kutoka hapo tungeelekea Palachi dream city kwa ajili ya kupiga picha za harusi yetu.


    Na mara baada ya hapo tungerejea Sea cliff kwa ajili ya sherehe zilizoandaliwa na mara baada ya sherehe tungeelekea visiwa vya Mbudya kwa ajili ya kulala usiku huo.


    Kesho yake tungeelekea Marekani tiketi tayari zilishaaandaliwa.


    Ndoa yetu ilikuwa gumzo mjini.


    Ulinzi uliwekwa kila sehemu.
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Vitu mbalimbali vilikuwa vimeandaliwa kwa ajili ya sherehe hizo.


    Kadri muda ulivyozidi kujongea ndivyo nilivyozidi kupoteza amani mwili ulikuwa ukinisisimka bila sababu.


    “Sasa ninaenda kuungana na kuwa mwili mmoja na huyu mwanaume. Mwanaume ambaye hayupo kabisa moyoni mwangu.”


    Kelvin alitamani kuona ndoa yetu ni ya kipekee sana.


    Mara zote alikuwa akinipigia simu kuniuliza kama niko tayari na jinsi ambavyo nilikuwa nikijisikia.


    Simu zilizidi kunichukiza.


    Mapema nilijiandaa na kwenda saluni nilipambwa nikapambika.


    Akili yangu iligoma kuamini mwisho wake ninaangukia katika mikono ya Kelvin mtu ambaye nilikuwa simpendi.


    Sijui ni kitu gani ambacho kingetokea mara zote nilikuwa nikiomba muujiza utokee.


    Iwe kama Kelvin ameamua kughairisha ndoa hiyo.


    Hata hivyo kadri ya muda ulivyozidi kwenda ndivyo nilivyogundua kuwa hiko kitu hakiwezi kutokea.


    “Mungu wangu usiniache.” Nilisali sara zote nilizozijua hata hivyo muda uliendelea kunisomea.


    Muda ulipowadia nilitoka moja kwa moja na kuelekea Sea cliff wakati huo nikimsubiri aje kwa ajili ya kufunga ndoa.


    Marafiki wengi sana wa Kelvin walikuwepo kushuhudia harusi ya rafiki yao.


    Baba alialika marafiki zake.


    Mimi peke yangu sikupata nafasi ya kualika mtu yoyote.


    Sikuwa na marafiki kwa wakati huo wale ambao nilisoma nao hawakuwepo pamoja nami nilitamani ningekuwepo na rafiki hata mmoja tu ambaye angehudhuria katika harusi yangu, mpaka siku ya harusi inakaribia sikuweza kumpata yeyote wa kuhudhuria katika harusi yangu. Mwili wote ulikuwa ukisisimka.


    Nilikaa katika chumba cha hoteli ile nzuri huku nikisubiri muda wa harusi ukaribie. Nilishindwa kupata hata chakula cha mchana hakikuwa na ladha yoyote kinywani mwangu.


    Msichana ambaye alikuwa akinisimamia mara zote alikuwa akinitia moyo.


    “Ni kawaida sana inatokea katika harusi nyingi mtu anapokuwa anajiandaa kufunga ndoa anakuwa kama na uoga fulani hivi kwahiyo ni kawaida mimi hata sikushangai.”


    Na wasichana ambao waliandaliwa kwa ajili ya kunisindikiza walikuwa ni wasichana wazuri sana ambao sijui wapi walipotokea.


    “Sijui Kelvin aliwapata wapi kwanini asingewaoa mmoja kati ya hao mbona ni wazuri na wamenizidi.” Nilishindwa kuelewa.


    Hata hivyo nilijipa imani kwamba ndoa hiyo haitafungwa.


    Muda ulipowadia baba alikuja kunichukua.


    “Kila mtu ameshafika, marafiki zako wapo, ndugu na jamaa wote wapo muda si muda ndoa itaanza kufungwa furahi mwanangu.” Baba alisema.


    Nilijitahidi kutabasamu huku nikijiuliza ni marafiki zangu gani ambao wamehudhuria katika harusi yangu.


    Hata hivyo sikutilia maanani zaidi ya sana hofu iliyokuwa ndani yangu.
    “Uwe na amani binti yangu kila kitu kitakuwa sawa.”


    “Kwahiyo mama yuko huko kwenye watu?” Nilimuuliza huku nikishindwa kuelewa kitu ambacho nilikuwa nikikiongea.


    “Ndiyo, mipango inasema mimi ndiyo nitaingia na wewe.


    “Mchungaji ameshafika?”


    “Mchungaji yupo.”


    “Aanh zimebaki dakika ngapi kabla ya kufunga harusi?” Baba aliangalia saa yake.


    “Imebaki robo saa.”


    “Kelvin ameshafika?”


    “Kelvin hajafika bado. Mimi niko hapa na wewe Kelvin akifika tu tunaenda.” “Sawa baba.”


    Ilikuwa imebaki robo saa tu kufika saa kumi na moja kamili za jioni Kelvin alikuwa bado hajafika. Sijui alikuwa wapi na wala sikujua alikuwa akifanya nini. Tuliendelea kumsubiri kwa takribani saa lizima.


    Ndipo alipowasili kwa maana muda huo tuliitwa mimi na baba kwa ajili ya kuelekea katika bustani ya hoteli ya sea cliff kwa ajili ya kufunga harusi hiyo. Nilitembea kwa hatua za kichovu kana kwamba ninasukumwa. Watu walikuwa ni wengi na nilipendeza sana.


    Harusi yetu ilipangwa kwa rangi ya maruni na yeupe pamoja na rangi nyeusi rangi ambazo nilikuwa nikizipenda sana.


    Hakika walipendeza na bustani nayo ilipendeza kila kitu kilikuwa kimepangwa katika mpangilio.


    Sehemu ya harusi yetu kulitengenezwa jukwa kidogo lililokuwa limepambwa na maua juu mpaka chini.


    Ilikuwa ni sehemu nzuri sana ambayo mara zote niliishia kuifikiria tu mawazoni na siku hiyo nilikuwa nikiitazama kwa macho.


    Na zaidi ya sana ni mimi ambaye ilikuwa ikinihusu.


    Viti vilipangwa vizuri kana kwamba ni kanisa dogo.


    Moyoni mwangu nilimsifia mpambaji.


    Hata hivyo nafsi yangu haikufurahia nilichokuwa nikikitazama.


    Muda mchache baadae nitaenda kuwa mke halali wa Kelvin.


    Baba ndiye aliyekuwa akitumia nguvu zote kunivuta ili kusogea mbele ama sivyo nisingeweza kutembea.


    Nilitambea kwa hatua za kichovu mpaka kufika mbele na nilipofika pale baba alisimama pamoja nami.


    Wala sikuwa nimemuona Kelvin alikuwa amesimama upande mwingine.


    Hakika alikuwa amependeza sana alionekana mzuri zaidi ya ambavyo nilikuwa


    nikimuona siku zote.


    Alipodolewa akapodoka.


    Nilishangaa kwamba kumbe tayari ameshafika mbele.


    “Na tuanze ibada yetu.” Mchungaji aliongea.


    Niligeuka ghafla na kumtazama.


    Mchungaji alihisi kwamba ninamtazama.


    Macho yangu yalikataa kuondoka kwake.


    Hadi mchungaji alihisi kwamba ninamtazama.


    Alinitazama kana kwamba ananiuliza kuna shida gani binti.


    Msimamizi wangu alinishitua.


    Niligeuka na kumtazama na kisha nikaachia tabasamu kidogo.


    Baba alirudi kitini na sisi tuliruhusiwa kukaa kwenye viti vilivyokuwa vimeandaliwa hapo mbele na kisha mchungaji alianza kuhubiri. Alihubiri kwa muda mrefu kidogo.


    Mpaka kufikia saa kumi na mbili na nusu ndipo tulipokuwa tukiingia sehemu ya kufunga harusi.


    Kila mara nilikuwa nikimkata jicho mchungaji kana kwamba namuomba asifungishe ndoa hiyo na yeye alibaki na sintofahamu akishindwa kujua ni kipi hasa nilichokuwa nikikihitaji.


    Hata hivyo muda wa kufunga harusi ulifika.


    Wakati mchungaji anataka kuanza kufungisha ndoa yetu Kelvin aliomba aseme kitu.


    Bila hiyana mchungaji alimpa ruhusa ya kuongea.


    Alisafisha koo lake kidogo.


    Hapo moyo wangu ulikuwa ukienda kasi mithili ya treni ambayo imekosa dereva.


    Nilifikiri pengine anataka kughairisha ndoa yetu.


    Hata hivyo nafsi yangu ilikosa kabisa utulivu.


    Aliendelea kupoteza muda bila kuongea chochote.
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Nilishindwa kumuelewa ni kitu gani hasa alichokuwa anataka kukiongea.


    Alivuta muda na kisha kuongea.


    Kila mtu alitega sikio lake kumsikiliza.


    “Naomba nichukue nafasi hii kumshukuru kila mtu ambaye amehudhuria katika harusi yangu na pia niwashukuru marafiki zangu ambao mmenishika mkono katika kipindi hiki ambacho tulikuwa tuko pamoja katika maandalizi ya harusi yangu mpaka yameweza kufanikiwa. Nashukuru Mungu kwa sababu nimepata neena nina kibali na wakati huu naenda kumfanya Sociolah kuwa mwanamke wa maisha yangu.” Alianza kwa kuongea.


    Nafsini mwangu nilikuwa na huzuni na uchungu sana.


    Nilitamani maneno yake yabadilike ikibidi hata anitukane mbele za watu ilimradi tu ndoa ile isiwepo, mawazo ambayo hayakuwepo akili kwake hata kidogo. “Napenda kuwashukuru sana wazazi wangu, wakwe zangu kwa kumlea Sociolah kwa maadili na ninaamini kwamba anaenda kuwa mke mwema kwasababu ananisikia, ananitii na kuniheshimu. Napenda kuwashukuru sana kwa hilo. Nadhani watu wengi wanaweza kuwa wanashangaa imekuwaje nikaongea maneno haya kabla sijafunga harusi yangu lakini kuna kitu nataka nimuahidi Sociolah mbele yenu kwa sababu ni mwanamke wa maisha yangu. Nadhani kila mtu hapa anatamani kuwa na mwanamke mzuri kama Sociolah, mnaweza mkamchukulia kama alivyo lakini ni zaidi ya jinsi alivyo. Ni mpole, mcheshi, mzuri, ana akili na sifa nyingine nyingi sana nikizitaja sitoweza kuzimaliza. Tumepitia mengi katika mahusiano yetu Sociolah amekuwa akiniheshimu, akinijali, akinisikiliza, akinisaidia pia katika mambo mbalimbali. Wanansema kwamba katika kila maendeleo ya mwanaume kuna mwanamke nyuma yake basi Sociolah alikuwa nyuma yangu.”


    Alianza kuongea maneno mengi kiasi kwamba nilihisi kuchafukwa na moyo, sifa ambazo hata hazikunihusu, sifa ambazo hazikuwa za kwangu. Vyote alivyokuwa akiviongea vilikuwa ni vya uongo.


    “Basi nishukuru kila mtu ambaye amehusika katika makuzi ya Sociolah ambaye yuko mahali hapa na ambaye hayupo kwa maana mmemfanya kuwa mke mwema na mimi nafurahia kwa hilo. Ahsante sana wakwe zangu, ahsante familia ya wakwe zangu wote na watu wengine. Na pia nitoe shukurani zangu za dhati kwa marafiki zangu ambao wao wamekuwa mstari wa mbele katika kuifanya harusi yangu kuwa kama ilivyo kwasababu nao pia wanampenda Sociolah. Kwa maana hiyo wakajitoa kwa hali na mali kwa ajili ya harusi yetu. Kwa hilo nafurahia sana. Nashukuru sana, nashukuru uwepo wenu nafurahia kila kitu.


    Kabla sijafika mbali basi nilisema kwamba nataka nimuahidi kitu Sociolah kabla hatujafunga ndoa na hiko ni kitu ambacho kitasimamia ndoa yetu siku zote.
    Mke wangu mtarajiwa Sociolah.”


    Hatimaye aliniita.


    Ni msimamizi wangu ndiye alikuwa amenishikilia pengine hivyo ningekuwa tayari nimeshaporomoka chini.


    Sikuhisi hata kama mwili wangu ulikuwa na nguvu hata kidogo.


    Mama yangu alikuwa amesimama pembeni akiniangalia.


    Nilitamani kumuambia mama afanye kitu kabla ya dakika chache zijazo ambapo ndoa yangu ilikuwa imefungwa.


    Hata hivyo naye alisimama tu kana kwamba mtu ambaye hajui ni nini cha kufanya. “Mungu wangu, Mungu wangu mama naye ananisaliti hivi kweli?!”


    Baba alikuwa anafuraha zote, wadogo zangu walikuwa wamependeza sana.


    Nilisimama tu na gauni yangu kama ndege asiyejua aendako.


    Shela lile lilipendeza lakini niliona kama vile nimevikwa sanda naenda kuzikwa. Na kelele za watu wote waliokuwa wakifurahia pale niliona kama vilio. Nilinyanyua uso wangu na kumtazama Kelvin ambaye alikuwa akisubiri muitikio wangu.


    Aliachia tabasamu ambalo kwangu nililitafsiri kama dharau kubwa. “Hatimaye sasa ndege mjanja nimenasa kwenye tundu bovu.” “Sociolah...” Aliniita tena na kunizindua kutoka katika lindi la mawazo. “Bee.” Niliitika huku sauti yangu ikionekana kupwaya.


    “Ahsante kwa kunichagua kuwa mume wako.” Aliongea na kisha kumalizia na kicheko hafifu.


    Vyote hivyo kwangu nilivitafsiri kama dhihaka.


    “Naomba nikuahidi kitu mbele ya kadamnasi. Nataka useme ni kitu gani unakitaka chochote kile unachokitaka kiseme kabla hatujafunga ndoa nitaishi maisha yangu nyote nikikupatia hicho kitu chako unachokihitaji. Nataka nikufanye kuwa malkia wa dunia, nataka nikufanye kuwa mtu mwenye furaha, nataka nikufanye kuwa mwanamke wa pekee katika dunia yote.”


    Nguvu mpya zilinirejea.


    Niliutoa mkono wangu kutoka pale nilipokuwa nimeshikiliwa na yule msimamizi wangu.


    Nilisimama kikakamavu kama wanajeshi waliokuwa wakikaguliwa na mkuu wa nchi.


    Tabasamu lilichanua usoni mwangu tabasamu lililomaanisha dharau na dhihaka zaidi ya yeye alizokuwa akinionesha.
    “Mimi siyo mrahisi kiasi hiki.” Niliongea na nafsi yangu.


    Kila mtu alitarajia kusikia kitu ambacho ningekitaja, kitu ambacho ninakitaka.


    Kila mtu alikuwa na shauku sana ya kujua.


    Kwangu mimi nilikuwa na furaha sana kwa maana huo ndiyo wakati niliokuwa nikiusubiria.


    Nilitasua midomo yangu na kusema kile ambacho nilichokuwa nakitaka na kukihitaji kutoka kwa Kelvin.


    “NATAKA KUZAA.”


    Kila mtu alishitushwa siyo tu na jibu langu bali na watu wawili waliokuwa wakisogea mbele kwa kasi huku mmoja akionekana amemkosea mwenzie.


    Huku na yule ambeye amekosewa akiwa na hasira kali zaidi ya mbogo aliyejeruhiwa.


    Hata mimi pia nilishangaa.


    Katika kutahamaki Melania alisukumwa kwa nguvu na kuja kudondokea mbele yangu.


    Frank alionekana ni mtu mwenye hasira sana.


    Nilishangaa.


    “What the hell!” Nilijikuta nimeropoka.


    “Nyamaza Sociolah.” Frank alisema.


    “Mungu wangu! Frank unawezaje kuniambia ninyamaze kimya hii ni harusi yangu. Kwanini unakuja kuniharibia harusi yangu?”


    Niliongea kwa hasira.


    “Unafikiri kuna harusi tena mahali hapa, Sociolah ongea ukweli unaifurahia hii harusi.”


    Nilishindwa kuelewa.


    Nilimtazama Kelvin ili nisikie neno lolote kutoka kwake kuhusiana na uvamizi huo wa ghafla.


    Mkono mmoja alikuwa ameshika kiunoni na mwingine alikuwa ameshika kichwani.


    “Kelvin ongea chochote.” Nilimuita.


    Kelvin lishusha mkono wake kutoka kichwani mpaka usoni na kisha kufunika macho yake.


    Hali hiyo ilinivuruga sana.


    Watu waliokuwa wamekaa kwenye viti kwa utulivu walisimama.


    “What the hell?!”
    Baba naye aliingilia kati.


    “Kuna nini?”


    “Nisikilizeni.”


    Frank alisimama.
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    “Kaeni chini.” Aligeuka na kuwaambia wale watu ambao walikuja kushuhudia harusi yangu.


    “Msiwe na shaka harusi yenu itaendelea kama kawaida lakini kabla harusi haijaendelea nataka kusema kitu.”


    Baadhi ya watu ambao walionekana kumuelewa Franklin walikaa.


    Wengine waliona kama ni mwendawazimu ambaye hajui anachokifanya na muda si muda angejutia kitu ambacho alikuwa anakifanya wakati huo kwa maana Kelvin asingeweza kumuacha salama.


    “Naomba niongee ukweli kwa sababu siwezi kukaa kimya siku zote najua nina haki ya kuongea ukweli. Kukaa kimya kuna niumiza mimi, kukaa kimya pia kunaharibu maisha ya watu wengi. Siwezi nimeshakaa kimya sana na sasa hivi siwezi kuendelea kukaa kimya tena.” Aliongea Frank.


    Nilimshangaa.


    Alianza kwa kuelezea mkasa mzima.


    Alielezea kila kitu ambacho kilitokea.


    Aligusa hisia za wengi.


    Aliibua machozi ya wengi.


    Aliibua hasira za wengi.


    Na zaidi ya sana alitupeleka katika mwisho wa mchezo wote.


    FRANKLIN KAZIMANA.


    “Miezi kadhaa nyuma nakumbuka mara ya mwisho nilikutana na baba yake Sociolah wakati tupo kwenye sherehe ya rafiki yetu Innocent. Baba yake aliniita akaniambia anahitaji kuongea na mimi kama niko tayari kumuoa binti yake. Nilikubali na nilimuambia kwamba nitamtafuta. Na siku hiyo tulirejea bwenini kwetu Mabibo nilishindwa kuongea na Sociolah ilikuwa ni usiku sana na nilimuahidi kwamba kesho yake tungeongea.


    Aliamka asubuhi sana na kunipigia simu nilimuambia aje chumbani kwangu na alikuja lakini wakati tunaongea ghafla simu yake iliita nadhani alikuwa ni baba ambaye alikuwa akipiga simu. Baada ya maongezi mafupi sijui ni nini walikuwa wakiongea Sociolah alinigeukia kwa mshangao na kuniuliza kitu ambacho baba alikuwa ameniambia. Nilimuelekeza kile kitu ambacho nilikuwa nimeambiwa na


    baba yake Sociolah bwana Michael Kivamba. Lakini Sociolah aliondoka akiwa na hasira iliyochanganyika na huzuni sijui ni kwanini.


    Any way nilikaa nikiendelea kufikiria. Hata hivyo niliamua kuondoka ili niende nikamuulize Sociolah ni kitu gani kimetokea. Wakati najiandaa kuelekea kwa Sociolah mlango uligongwa, nilifungua. Walikuwa ni watu ambao sikuwahi kukutana nao hata siku moja na kwa mara ya kwanza tulikuwa tumekutana kwa hiyo siku. Naweza kumtambua huyo mtu ni bwana harusi wetu.”


    Maneno hayo yalinishitusha sana.


    Niligeuka na kumtazama Kelvin.


    “Kelvin ni wewe?!”


    Ni kama Franklin hakunisikia aliendelea kuongea.


    “Nilimkaribisha vizuri alipofika alitoa bastola na kuiweka mezani aliniambia maneno ambayo sitakaa niyasahau. “Bwana Franklin kijijini kwenu ulikotoka hamna wasichana wa hadhi yako.” Na hivi ndivyo Kelvin alivyoanza.


    “Naona unahangaika sana na wasichana ambao siyo taipu yako. Kwa amani au kwa shari sitaki nikuone una ukaribu wowote na Sociolah.” Nilijaribu kujitetea nilipigwa sana, nilipigwa sana sana na kisha simu yangu ilichukuliwa na nikatishiwa maisha yangu endapo nitaendelea kumfuatilia Sociolah basi ndiyo ungekuwa mwisho wa maisha yangu.


    Sikukubali kirahisi hata hivyo nilipigwa mpaka nilipopoteza fahamu.


    Nililazwa siku zote na wala Sociolah hakuwahi kuja kuniangalia. Nilijua fika kwamba sina changu kwa wakati huo inapaswa mimi kuendelea mbele. Masikini mimi nani ambaye angenisikiliza.”


    Aliongea Franklin kwa hisia zote kiasi cha kila mtu aliyekuwa pale kumwaga machozi huku nikibeba ushindi kwa kumwaga machozi zaidi ya wote.


    “Zaidi ya sana hazikupita siku nyingi nilipata tena ugeni wa bwana Kelvin na safari hiyo alikuwa ameongozana na Melania.”


    Niligeuka kwa ghadhabu na kumtazama Melania ambaye alikuwa bado yuko chini aliinamisha uso wake kwa aibu na majuto.


    “Wakanipa mkakati mzima wakanichagulia namna ya kuishi nionekane kwamba nina uhusiano wa kimapenzi na Melania. Hali yangu ilikuwa mbaya bado kwa majeraha niliyokuwa nayo hata hivyo nilikuwa nina uhakika wa asilimia zote kwamba tayari sina Sociolah wangu tayari ameshaenda. Nilitaka kubisha hata hivyo niliambiwa kwamba maisha yangu yote yapo mikononi mwao, familia yangu yote wangeweza kuitekeketeza endapo nisingekubaliana na matakwa yao.


    Niliamua kukubali wakati huo ningemtafuta Sociolah ili anipe mustakabali mzima lakini Sociolah hakuwa tayari kuzungumzia hili swala. Alinibebesha mimi mzigo wa lawama zote, mimi nimemkosea sana. Kumtafuta Sociolah pia kuliniwia vigumu kwasababu tayari sikuwa na simu yangu ilinibidi kuanza upya na namba yake sikuwa nayo.


    Kila kumbukumbu zangu zilizokuwa zikimhusu Sociolah zilichukuliwa.


    Kipigo kikali pia kiliniogopesha, kilinionya kukaa mbali na Sociolah kwamba Sociolah siyo wangu tena.


    Roho iliniuma sana kusikia Sociolah anaolewa na Kelvin. Kwa ninavyomjua Kelvin hapaswi kuwa mume wa Sociolah lakini kama Sociolah unampenda mnaweza mkafunga ndoa.”


    Machozi yalinitoka mfululizo niliongeza spidi ya kulia.


    “Mimi siwezi kuzuia ndoa yenu.” Aliongea Frank kwa sauti iliyochanganyika na kilio.


    Niliinama huku nikijutia kufanya maamuzi bila kuongea na Frank.


    Nilimuonea sana, nilimpa hukumu kwa makosa yasiyostahili na sasa nilikuwa nikijihisi hatia ndani ya nafsi yangu.


    “Hakuna shida kama unaolewa, olewa tu Sociolah mimi nitamtafuta tu masikini mwenzangu huko.”


    Harusi iligeuka eneo la msiba.


    “Nimeshatua mzigo wangu.” Frank aliendelea.


    “Siku zote nilikuwa nikionekana kama mwanamke vile nisiye na maamuzi, nisiye na msimamo wala kutetea kile ambacho nakipenda. Nimenyamaza kimya kwa muda mrefu sana lakini siwezi kukaa kimya muda wote.


    Sociolah bado nakupenda sijafanya yote hayo kwa mapenzi yangu ila nililazimishwa na kuwekewa mazingira ya kufanya hivi pamoja na hayo yote ninakuhitaji nimekuja kutetea penzi langu lakini kama uko tayari kuolewa na Kelvin olewa.


    Furaha yangu mimi ni kukuona wewe kuwa na furaha ukifurahia maisha, kama una


    furaha na Kelvin olewa naye tu.”


    “Noooo..!!”


    Nilitoa ukelele wa ghadhabu kuonesha ni kiasi gani nilikua naipinga harusi hiyo. “Hata kama Frank usingekuja kwenye harusi, hata kama kuna nini kingetokea nisingekuwa tayari kuolewa na Kelvin. Mimi ni mpumbavu kiasi gani nijue
    madhabi yote ya Kelvin na bado nihitaji kuolewa naye. Yeye ni nani? Anafikiri


    mimi ninaweza kumuogopa kwa kiasi hicho hapana.” Niliongea kwa ghadhabu.


    “Sikuwa tayari tangu mwanzo kuolewa na Kelvin na yeye mwenyewe anajua hilo


    lakini bado aliendelea kunilazimisha. Nilishamuambia kwamba simpendi lakini


    bado aliendelea kung'ang'ania kufunga ndoa na mimi. Kitu hicho kilinipa mashaka


    sana ni kwanini atake kumuoa mwanamke ambaye anafahamu fika kwamba yeye


    hayupo moyoni mwake.


    Hali hiyo ilinipa maswali.
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Nilianza kuonesha wasiwasi wangu kwake. Niliamua kumchunguza kimyakimya na nilipata majibu. Mara ya kwanza kabisa kwenda nyumban kwa Kelvin niligundua vitu ambavyo vilinichanganya.


    Kwanza kabisa nilikutana na karatasi juu ya meza ambazo nahisi alizisahau kuziondoa ilikuwa ni ripoti ya daktari ambayo ilionesha Kelvin hana nguvu za kiume kabisa kabisa. Nilipatwa na mashaka. Inakuwaje Kelvin atake kunioa wakati anajua kwamba hana nguvu za kiume. Nilipofungua kabati lake nilikutana na document ambazo zilionesha kampuni feki ambayo alikuwa ameianzisha. Kampuni ambayo alikuwa akimdanganya baba yangu kwamba anafanya nayo kazi kwa kweli hakuna kampuni ya usafirishaji ambayo Kelvin anaimiliki. Na document zote ambazo zilikua feki nilizichukua na ninazo. Yale makaratasi ambayo nilikurudishia kwenye ile bahasha hazikuwa zile document ambazo nilizichukua Kelvin.”


    Nilimgeukia Kelvin na kumuambia huku nikimshushua. “Ni mitihani yangu ya semister iliyopita.” Niliongea.


    Kelvin alijipiga kofi la nguvu sana kichwani.


    “Na ile siku nilibadilisha begi lako makusudi wala haikuwa bahati mbaya mimi kuchanganya mabegi. Nilichukua komputa yako na nikafungua nikakutana na email zote ambazo mnazitumia kuwasiliana na wenzio. Tangu mipango yenu yote mliyoipanga nimeiona na ninayo.


    Wewe na marafiki zako zote waliopo hapa nchini na huko nje ya nchi. Kelvin huna wazazi nje ya nchi. Usidanganye umma kwamba umezaliwa Marekani na kukulia Marekani. Wazazi wako umewatelekeza hapa hapa Tanzania.”


    Kelvin alishindwa kustahimili alijikuta ameporomoka hadi chini.


    “Hao huko nje ya nchi ni mabosi zako ambao wamekutuma uje huku Tanzania uangalie uwezekano wa kuleta dawa za kulevya na kwa maana hiyo ukamtafuta


    mtu mjinga kuliko wote ukampata baba yangu na familia yangu. Ukaweza kumdanganya ili uitumie project ya baba ya dawa zake kujifanya unazipeleka nje ya nchi na kuleta huku malghafi na misaada mingine. Usafirishe madawa yako ya kulevya ili ikitokea umekamatwa basi baba aonekane ndiye mbaya.”


    Baba alishituka kiasi kwamba alijikuta amesimama kwenye kiti alichokuwa amekaa.


    “Yote kwa yote ulitaka kunioa mimi ili uchukua utajiri wa baba yangu ambao ameufanyia kazi yeye mwenyewe kwa maana unajua mimi ndiyo mrithi wa kila kitu cha baba.


    Mara baada ya kunioa ungechukua utajiri wa baba yangu wote kwa kunilazimisha mimi nimuambie baba aniandikie urithi na baada ya hapo ungeweza kufanya chochote katika pesa za baba yangu.


    Unataka kubisha?”


    Nilimuona Kelvin akitetemeka mwili mzima nadhani alishndwa ni nini akiongee kwa wakati huo.


    “Ningekuwa mjinga kiasi gani mimi kuolewa na shetani, wewe na shetani si mnatoka familia moja.”


    Niliongea kwa hasira huku nikichukua ua mbalo nilikua nimeshikilia na kumpiga nalo kichwani.


    Hasira zilikuwa zimenikaba sana.


    “Nilinyamaza siku zote sio kama mimi ni mjinga lakini sikutaka uaibeke katika watu wachache.


    Marafiki zako nawajua na ninafahamu kwamba mnahusika nao katika ishu ya madawa ya kulevya na mambo mengi ya kitapeli.


    Lakin mimi nilitaka uaibike hapa mbele ya kila mtu ambaye ulimuona wa thamani sana kumualika kwenye harusi yako.


    Sikukupenda tangu mwanzo na wewe unafahamu hilo. Unafahamu ni kiasi gani umeweza kumdanganya baba yangu mpaka hata hii harusi leo ikafikia lakini nakuhakikishia kwa asilimia zote kwamba hakuna harusi kati yangu mimi na wewe. Mimi sio mjinga, sikupendi na hauko kabisa moyoni mwangu.”


    Niliendelea kumshushua pale mbele za watu. Na zaidi ya sana nakuhakikishia kiama chako kimefika.”


    “Nikuambie, hakuna mtu mjinga hapa mjinga ni wewe uliyeamini kwamba nitakunyamazia kimya.”


    Mama naye alinyanyuka.


    “Mtoto mdogo kama wewe unafikiri unaweza ukaniweza mimi, mtu mzima kama mimi na akili yangu tena nimeelimika kuliko wewe. Unafikiri ni kwa njia rahisi ungaweza kunishinda. Nilikuwa tu nimenyamaza kimya nilikuandalia mpango kabambe kuonesha kwamba kutoa funzo kwako na kwa wengine kwamba utu uzima dawa.


    Nimekufatilia sana jinsi ulivyokuwa ukimdanganya mume wangu hadi akaweza kukuelewa.


    Umetumia mbinu nyingi na pesa zako chafu kutudanganya lakini hata siku moja sikuweza kukuamini.


    Mara zote nilikua nikishangaa wewe ni mtu wa aina gani na nashukuru Mungu kupitia binti yangu Sociolah nimeweza kukujua. Na leo mwisho wako ndiyo umefika.”


    Mama alichukua pochi yake na kumtupia Kelvin.


    Pink na Pinto walivua viatu vyao na kumpiga navyo.


    Mama aliwazuia, walienda kuchukua viatu vyao na kuvivaa.


    “Hata hatukupendi.”


    Walimuambia.


    Kila mtu alishikwa na hasira mahali pale watu wote walinyanyuka na kwenda kumpiga Kelvin.


    Kila mtu alimpiga na kitu chochote kile kadri alivyoweza mpaka wanakuja kumzuia tayari Kelvin alikua ameshaumia alikuwa na majeraha kadha wa kadha. Wakati wakiendelea kutuliza ghasia nilisogea pale alipokuwa amekaa Franklin kwenye kiti.


    Nilipiga magoti mpaka chini.


    “Naomba nisamehe Frank.”


    “Usijali mrembo wangu.”


    “Naomba nisamehe Franklin nimekosea sana kwa kufanya maamuzi bila hata kukuuliza naomba nisamehe kwa yote.”


    “Usijali hata mimi pia nimekukosea na ninapaswa kuomba msamaha, nimekua muoga sana kushindwa kulitetea penzi langu. Naomba nisamehe sana mke wangu.”


    “Naomba tusikilizane.”


    Baba aliongea.


    “Binti yangu kwanza naomba unisamehe sana kwanza kwa kutokukusikiliza na pili kwa kutokukuamini. Nimejifunza vitu vingi sana lakini huyu mtu alikuwa ni zaidi


    ya mnyama alinishawishi vitu vingi sana mpaka nikajikuta naisahau hata familia yangu.”


    Baba aliongea huku akionesha dalili za kutaka kulia.


    Nilitamani hata kumtukana lakini ndiyo hvyo sikuwa na jinsi, yeye alikuwa ni mzazi wangu.


    Nilibaki tu nikiendelea kumsikiliza alichokuwa akiongea kwa wakati huo. “Naomba unisamehe sana binti yangu pia naomba Frank anisamehe kwa vile nimemkosea sana. Frank ni kama mwanangu lakini nilimdharau, na mambo mengine kadha wa kadha ambayo siwezi kuyazungumzia. Naomba familia yangu yote inisamehe.” Aliongea baba.


    “Naomba harusi iendelee kufungwa lakini sasa bwana harusi atakuwa amebadilika siyo Kelvin tena bali atakuwa ni Frank.”


    Nilihisi mwili mzima ukisisimka kwa kauli hiyo.


    Nilitegemea kurudi kwa Frank lakini sikutegemea kwamba ni tungefunga ndoa siku hiyo hiyo.


    Nilifumba macho huku nikisikilizia utamu wa kauli hiyo.


    “Kama watakuwa tayari lakini.” Baba aliendelea.


    “Kama hawatokuwa tayari sawa pia, lakini siku yoyote mtakapokuwa tayari mtaniambia msihofu.”


    Nilimgeukia Frank na kumtazama na yeye alikuwa akisubiri kusikia kutoka kwangu.


    Nilimuangalia tu nikajikuta nacheka.


    Alinininyanyua pale nilipokuwa nimepiga magoti na kisha tukaelekea mahali palipoandaliwa kama dhabahu kwa ajili ya kufunga harusi yetu. Mchungaji alisimama na baadhi ya watu walirejea kama kawaida.


    Ndani ya dakika chache zilizofuatia mpangilio wa vitu ulikuwa umerejea sawa. Hata hivyo Kelvin na watu wake walikuwa tayari wameshawekwa chini ya ulinzi na maafisa wa polisi ambao mama alikuwa amewaita kwa kazi maalumu ya kuwakamata wauza unga.


    Nilishukuru sana kwa jitihada ambazo alikuwa amezifanya kwa maana peke yangu nisingeziweza.


    Wakati mwingne nilimuona kama msaliti lakini mama yangu alibaki kuwa mama


    yangu huku akisimama upande wangu na kunitetea kwa ajili ya kutimiza kile


    ambacho nilikuwa natamani kukifikia.


    Aliweza kujua mipango yote ya Kelvin.
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Aliweza kujua mahusiano yaliyopo kati ya Kelvin na Melania na ndiyo maana aliniambia kwamba Kelvin alikuwa akiwahi sana kuja chuoni.


    Kwa maana hiyo wakati huo alikuwa akipata muda wa kukutana na Melania na


    kupanga mipango yao michafu.


    Nilishukuru sana kwa jitihada zake.


    Mama yangu alikuwa na furaha isiyokuwa kifani kuona nimesimama mbele na


    mwanaume nilikuwa nikimpenda.


    Kila mtu alifurahia.


    Melania naye alikuwa amewekwa chini ya ulinzi.


    Mchungaji aliendelea kufungisha ndoa yetu.


    “Ndiyo nakubali.” Nilijibu kwa furaha zote pale nilipoulizwa kama nipo tayari


    kuishi na Frank kama mume wangu.


    Na yeye aliitikia hivyo hivyo.


    Ilikuwa ni furaha sana.


    Baada ya kubarikiwa na kuwa mume na mke hatukutaka chochote kiendelee.


    Tuliondoka huku tukikataa kuhudhuria sherehe ambayo ilikuwa imeandaliwa.


    Tulienda moja kwa moja visiwani Mbudya kwa ajili ya kupumzika usiku huo.


    Ulikuwa ni usiku ulioshamiri mahaba na mapenzi moto moto.


    Tuliogea mambo mengi, tulicheka, tulikumbushana vitu vingi, tulilia, tulifuta machozi na kufungua ukurasa mpya.


    Nafsi yangu iligoma kuamini kama ni kweli nimekuwa mke wa Frank rasmi.


    Hata hivyo ndivyo ilivyokuwa.


    Asubuhi ya siku iliyofuata tulikuwa na uchovu mwingi pamoja na hayo yote hatukusita kuondoka kisiwani hapo na kuelekea nyumbani kwetu. Tulikuwa mume na mke lakini hatukuwa na makazi rasmi.


    Tulipokelewa kwa bashasha zote.


    Wazazi wangu ambao walionekana walikuwa na uchovu mwingi.


    Ilikuwa ni siku ya jumapili.


    Hawakwenda kanisani.


    Tulikaribishwa chai.


    Tulikunywa.


    Mara zote baba alikuwa akiniangalia kana kwamba anataka kusema kitu.


    “Binti yangu bado najihisi hatia sana, mwanangu Frank sijui nitazisafishaje hizi dhambi ambazo ninazihisi ndani yangu. Naomba mnisamehe sana.” “Baba.” Nilimuita.
    Frank aliendelea.


    “Usiwe na shaka baba makosa tumeumbiwa binadamu, sisi wote tumekosea kwa namna moja au nyingine kila mtu hapa ana makosa. Mimi kwa moyo mweupe nimekusamehe baba wala sina kinyongo na wewe sijui Sociolah.”


    “Mimi sina shida na baba nimeshamsamehe.” “Sema tu umekosea Frank.” “Nimekosea nini baba?”


    Frank alionekana kushitushwa sana na maneno hayo ya baba. “Umemuita Sociolah kwa jina lake, huyu ni mkeo sasa.” Aliongea baba na sisi wote tulianza kucheka.


    Tuliongea mambo mengi na kisha baba alituita. “Nimeamua kuwapa nyumba yangu ya kule Tabata bima.” Kiukweli nilishindwa kufurahi nilijikuta nacheka.


    Hiyo ni nyumba ambayo baba hakutaka mtu yoyote aende, alikuwa akiipenda sana nyumba yake na alisema atakapostaafu ndiyo ataenda kuishi kule.


    Hivyo hakutaka mtu yoyote aende akakae ni yeye mwenyewe ndiye aliyekuwa akienda kuiangalia na endapo ingehitaji usafi basi angeenda na wafanyakazi kule kwa ajili ya kuifanyia usafi.


    Lakini aliamua kuikabidhi kwetu hakika lilikuwa ni jambo la kipekee sana.


    Mama yangu naye alicheka kwa kuwa hakuaminh'.


    “Baba Sociolah unakumbuka hiyo nyumba ulisema hutampa mtu yoyote.” “Sina jinsi naona kama ni sehemu ya kuomba msamaha.” Baba alisema.


    “Aaanhaa Baba hakuna haja nimewapa kwa moyo mweupe wanangu muende kuishi kule. Mnajua nyie mmeshakuwa mume na mke lakini sasa mmoja anakaa kwangu mwingine anakaa Mabibo, mimi sitaki kukaa na mke wa mtu hapa.” Baba aliongea, tulicheka.


    Baada ya maongezi mengi Pink na Pinto walikuja kuungana na sisi. “Mimi nilikuwa napenda sana kumtania huyu.”


    Pink alisema huku akimnyooshea kidole Franklin.


    Kiukweli akili yangu ilichoka kujua kwamba Pink muda wote alikuwa akipenda kumtania Frank.


    Mara zoe nilikuwa nikihisi anamaanisha.


    Ilikuwa ni furaha sana.


    Walifurahi sana kuwa naye karibu hata tulipotaka kuondoka ilituwia vigumu kwa maana Pink na Pinto waligoma kabisa kutuachia.


    Nilitoka na baadhi ya vitu vyangu vichache na kisha kuchukua gari moja wapo ambayo baba alitupa.


    Tulielekea moja kwa moja Tabata bima.


    Tulipofika kule nyumba yetu ilikuwa imekaa barabarani tu.


    Ilikuwa nzuri sana.


    Tuliingia na kuanza kuikagua.


    Ilikuwa ni safi hivyo hatukuwa na haja ya kufanya usafi.


    Mara baada ya kupanga vitu tulitoka na kuelekea Mabibo.


    Baadhi ya watu walikuwa na taarifa za lile tukio lililotokea.


    Nilielekea moja kwa moja chumbani.


    Nilipofungua mlango nilikutana na Melania.


    Nilipoingia ni kana kwamba kulikuwa kuna kikao kilikuwa kinaendelea.


    Mara baada ya kuingia kila mtu aliinamisha uso wake kwa huzuni.


    “Karibu mume wangu.” Nilimuita.


    Frank aliingia ndani.


    Watu wote walionesha nyuso za huzuni.


    Sikuwa na chochote nilichokuwa nimeenda kukifanya mule ndani.


    Hata hivyo nilienda tu ili kuonesha katika ile vita waliokuwa mameianzisha mimi ni mshindi.


    Melania alishuka kwenye kiti alichokuwa amekaa kisha kupiga magoti. “Naomba unisamehe rafiki yangu.”


    “Wewe shetani leo umekumbuka kuomba msamaha.” Nilimuambia. “Naomba nisikilize basi usinihukumu.”


    “Mimi nikuhukumu wewe? Sina huo muda.” Nilijibu kwa nyodo.


    “Nisikuhukumu Melania, si unajihukumu mwenyewe kwa nafsi yako. Unaona hata haya. Mimi nikuhukumu wewe sina huo muda.” Nilijibu kwa nyodo.


    “Naomba nisikilize hata mara moja tu. Kiukweli mimi sijawahi kumjua Kelvin vizuri alikuja mara baada ya ugomvi kati yangu mimi na wewe. Ni kweli niliongea yale maneno kwa hasira kwamba nitakukomesha kwa kumchukua Frank. Nilikuwa nafahamu fika kwamba Frank anakupenda sana wewe na wala asingekubali kuwa na mimi.


    Hata hivyo Kelvin ndiye aliyebadilisha msimamo wangu.


    Yeye alikuja kuniambia kwamba Sociolah ni mkewe mtarajiwa lakini kuna mtu ambaye anamsumbua sana ambaye ni Frank.


    Alinipa pesa, aliniahidi kwamba endapo nitamsaidia ataniongezea zaidi na pia ningeweza kumpata Frank.


    Na pia aliniambia kwamba Frank ananipenda sana mimi na sio wewe ila Sociolah tu ndiyo ambaye anamng'anga'ania Frank.


    Kwa maana hiyo basi endapo mimi ningempata Frank wewe ungetulia na kukubali kuolewa na yeye.


    Na aliniambia kwamba anakupenda sana hataki kukupoteza.


    Nilifanya hivyo kama kisasi kwako kwa zile tu hasira zisizokuwa na maana. Naomba unisamehe sana.”


    Nilishangazwa sana na taarifa hiyo mpya.


    “Kumbe huyu Kelvin alikuwa mshenzi kiasi hiki. Mimi siwezi kuwaamini wewe wala yeye. Muendelee na maisha yenu.


    Mimi wala sina mpango na wewe, sihitaji marafiki. Nyie wote humu ndani ni wanafiki tu sijaona rafiki hata mmoja.”


    Monica na Fetty waliangua kilio cha nguvu.
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    “Hapana Sociolah usiseme hivyo.”


    “Nisiseme hivyo nini na nyie wote ni wale wale sina rafiki mimi najua nimekuja tu kuwaonesha kwamba mipango yenu wote imeshindwa. Mimi na Frank sasa ni mume na mke.”


    “Tunajua hilo na tunajutia nafsi zetu.” Fetty aliongea.


    “Sijui ni pepo gani alinikumba hata nikafanya hivyo kila mara nilipokuwa nakifikiria nilihisi hatia ndani yangu. Moyo wangu ulikuwa ukiungua kila siku hata hivyo sikupata nafasi ya kuongea na wewe. Naomba nisamehe Sociolah, haya yote ni makosa ambayo tumeumbiwa binadamu na ni makosa ambayo tunafanya, kama tusingefanya sisi basi angefanya mtu mwingine yoyote. Naomba msamaha wako Sociolah.”


    Nafsi yangu iligoma kabisa kuwaamini wala kuwasamehe.” “Hapana siwezi kuwasamehe.”


    “Mke wangu.” Frank aliniita, niligeuka na kumtazama.


    “Samehe.” Aliniambia.


    “Hapana siwezi, siwezi.”


    “Samehe Sociolah. Usiposamehe hutokuwa na amani katika maisha yako. Katika maisha yetu niseme mimi na wewe sasa ni mwili mmoja. Samehe waliokukosea ili na wewe upate nafsi ya kusamehewa.”


    Aliniambia maneno ambayo yalinitikisa.
    Hata hivyo nafsi haikuwa radhi. Niliumizwa sana na kitendo ambacho walinifanyie.


    “Samehe saba mara sabini.” Ilikuwa ni sauti ya msichana.


    Nilishangaa.


    “Ni nani uyu.“


    Bila shaka alikuwa ni Christina.


    “Tina.” nilimuita.


    “Samehe Sociolah, kwa maneno yote ambayo uliwahi kunimbia mabaya na yenye kuumiza, nilisamehe. Samehe hawa ni marafiki zako.” Nilishindwa cha kujibu. Nilivuta pumzi ndefu na kisha kwenda kumkumbatia kwa nguvu zote.


    “Ahsante Christina, nakupenda.” Nilimuambia.


    “Nakupenda pia Sociolah.”


    Hapo ndipo nilipomuona na Innocent kwa pembeni.


    “Nisamehe Innocent.”


    “Usijali Sociolah. Nilitamani sana kuja kukuambia nini ambacho kimetokea hata hivyo hukunipa nafasi lakini yote kwa yote nilijua kwamba hata mimi ningekuwa katika hali kama yako ningekuwa kama wewe lakini muda umefanya maamuzi. Hakuna kilichoharibika ila samehe Melania, samehe Fetty, samehe Monica.” Nilimkumbatia Innocent na kisha nikageuka.


    “Samehe mke wangu.” Frank aliniambia.


    Nilipiga hatua pole pole hadi pale alipokuwa amepiga magoti Melania.


    Nilipiga magoti na kisha kumkumbatia.


    Alilia kwa uchungu sana.


    Niliwakumbatia wote kwa ishara ya kuwasamehe.


    Nilimfuta machozi Melania.


    Alikaa pembeni yangu huku akilia.


    “Nisamehe sana.”


    “Nimekusamehe Melania. Nawapenda sana marafiki zangu.” Niliwakumbatia wote na kisha wote wakanikumbatia.”


    Tuliongea mawili machache huku wakinipa hongera nyingi kwa kufunga ndoa. “Jamani umefunga ndoa hakuna hata rafiki aliyehudhuria.”


    “Baba amesema kwamba tutafanya ibada ya kubariki ndoa yetu kwa maana hata wazazi wa Frank hawajaweza kuhudhuria. Msijali mtakuja kama kawaida.” “Tutafurahi sana.”


    Tuliongea mengi na hapo ndipo nilipogundua kwamba Christina ana mahusiano na Innocent.
    “Nampenda sana Christina.” Innocent aliongea.


    “Ni msichana mzuri sana. Nafurahi kwamba matatizo yako wewe na Frank yamenileta mimi pamoja na Christina.”


    Niliishia kucheka.


    “Hongereni.”


    “Ahsante.”


    “Na mkifanya ndoa yenu na sisi muda si muda tutafunga ya kwetu.” Nilicheka.


    Furaha yetu iliendelea kwa muda mrefu hadi sasa.




    NIMEZAA.




    “Mke wangu mimi napenda tuendelee kuzaa tu.”


    “Aanh mimi nimeshachoka Frank huyu mtoto wetu wa tatu ni wa mwisho. Hawa mapacha Fancy na Fantasy wenyewe hawajakua vizuri.”


    “Watakuwa tu wala usijali ila tungeongeza wengine wawili wangefika watano hivi ingekuwa sawa.”


    “Aanh hapana kwa kweli huyu atakuwa ni wa mwisho sitazaa tena, watatu wanatosha.”


    “Wachache bwana tuongeze ongeze familia iwe kubwa.” “Hapana sitaki tena.”


    “Shauri yako Biblia inasema tuzae tuongezeke.” Frank aliongea kwa utani.


    “Tumeshajaa duniani hata hakuna haja ya kuongeza watu wengine.”


    “Aaanh wapi, tumejaa tumejaa wapi? Bado bwana bado sana. Tufyatue tu mpaka kieleweke.”


    Aliongea kwa utani na mimi nilicheka kwa sauti.


    “Tulale sasa mke wangu.”


    Alinibusu shavuni na kisha tukalala.
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/


    MWISHO.


0 comments:

Post a Comment

Blog