Search This Blog

Monday, October 24, 2022

PENZI LA MKE WA BABA - 4

 





    Chombezo : Penzi La Mke Wa Baba

    Sehemu Ya Nne (4)



    Mama alipo sema nifanye nae mapenzi, moyo wangu ulikataa kabisa, nikamwambia

    kwamba, “mama hivi we ni mtu gani ulie kosa hata punje ya huruma, yaani baba

    anaumwa amezidiwa ndani ebu msikie anavyo lia, alafu wewe unasema tufanye

    mapenzi, mimi sitaki bhana na kama umeshindwa kumuuguza baba yangu naomba

    uniambie" mama akasema, “hivi wewe bado ni mtoto ehh! Sasa baba yako kuumwa na

    sisi kufanya mapenzi vinaingiIiana vipi, kumbuka nimeisha kuzalia mtoto, hivyo wewe

    ndiyo mume wangu wa halali, hivi unazani mimi ni mjinga nikuwache siku zote hizo

    hatujakutana kimwili alafu wanawake wengine waniibie burudani yangu" nilikataa

    kufanya lile tendo ila mama alinisukuma kitandani na kuniingiza majaribuni nikajikuta

    nafanya anacho kitaka, wakati bado tunashiriki tendo nilimsikia baba akisema

    kwanguvu kwamba, “mwanangu Meshack najisikia vibaya njoo chumbani" nilitamani

    kwenda ila lile tendo lilikuwa limeninogea nikajikuta napuuzia maneno ya baba yangu

    mzazi bila kujua kuwa najitengenezea laana mbaya maishani mwangu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mama alipo rizika akasema, “dahh! Mpenzi wangu nakupenda, unanirizisha Meshack,

    ngoja nikamuangalie baba yako" nikasema, “sawa hamna shida" mama alipo ingia

    chumbani akamkuta baba ameanguka chini kichwa kimepata vidonda alafu mdomoni

    kuna matawi yametokeza, kumbe ni lile peazi lilikuwa linachanua kichawi ili baba afe

    haraka kusudi mama awe huru kufanya mapenzi na mimi.



    Nilipo ona vile, nikajua moja kwa moja kuwa baba amechezewa kichawi, ndipo

    nikaanza kulia, baba akasema huku machozi yakimtoka kwamba, “Meshack

    mwanangu mimi siwezi kupona lazima nife tu,tazama nilivyojawa na matawi mdomoni

    mwangu na kibaya zaidi najihisi kama kuna mizizi tumboni mwangu, sijui alie nifanyia

    hivi nimemkosea ninijamani, kwanini asinisamee tu natamani kuishi, nimlee mtoto

    wangu". Siri ya ule ugonjwa alikuwa anaijua mama na kipindi sisi tunalia mama

    alikuwa kimya tu haongei chochote. Mungu alisaidia akaamka salama, ndugu na

    wafanyakazi wenzake baba walipo kuja kumtazama, kila mtu alikuwa analia tu sababu

    ya vidonda vibichi alivyo kuwa navyo na matawi ya peazi. Ilipofika usiku baba

    akaanza kulia akisema, “nakufa, nakufa, nakata roho Meshack" huku akifumba macho

    polepole..







    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mama alifurahi sana akijua kuwa hari ya baba alipo fikia ni lazima akate roho tu, na

    kibaya zaidi alikuwa anasingizia majirani kuwa, “yaani hawa majirani zetu wabaya,

    wanamuona mume wangu anapata maendeleo wanaamua kumfanyia uchawi wa namna

    hii" nilishikwa na uchungu sana kumuona baba alie nizaa na kunilea kwa shida na raha

    leo hii anataka kufariki kizembe wakati mimi ndiyo kijana wake alie nitunza kusudi

    nimsaidie pia kwenye matatizo, ndipo nikapata wazo la kwenda kutafuta viongozi wa

    dini mda huohuo usiku kusudi waje kumuombea baba huenda angepona, na wakati huo

    baba yupo hoi anakaribia kufa. Nilibahatika kupata mchungaji mmoja hivi alie kuwa

    maarufu sana kwa kuponya watu, ingawa nilipata shida sana kumpata kwasababu

    ilikuwa ni usiku na mimi nilikuwa sipendi kwenda kwenye nyumba za ibada. Vule

    mchungaji alipo fika mlangoni kwetu akasema, “bwana Meshack, mnaishi vipi kwenye

    hii nyumba, mbona imejawa mizimu na vitu vya kishirikina, hamuishi wenyewe hapa,

    mnaishi na vitu vya ajabu sana" mama alipo muona mchungaji alinuna mno akasema,

    “Meshack nahisi tumbo linaniuma, ngoja nikaangalie dawa dukani", “mama utapata

    wapi dawa sahivi uoni ni usiku sana, ebu tujumuike kumfanyia baba maombi

    asiendelee kuteseka hivi", “mimi naondoka bhana" alisema mama.



    Mchungaji aliomba sana, akaimba mpaka nyimbo za kumsifu Mungu, tulishangaa wote

    kusikia baba analia kama ndege, huku damu zikiendelea kumtoka, mchungaji

    hakukata tamaa alifanya maombi sana na kukemea mizimu na mapepo yaliyo kuwa

    yametawala nyumba yetu, baada ya dakika chache baba akaanza kuongea sauti ya

    kike kwamba, “msitufukuzeee, msituue sio sisijamani, tunaungua moto, sisi

    tulitumwa na malikia tumsumbue huyu baba mpaka afe" mchungaji akawauliza,

    “mnatokea wapi?" Walisema “tunatokea msituni, tunalima sana matunda ya peazi,

    msituue, leo ilikuwa sherehe kubwa ya kuula mwili wa huyu baba" mchungaji aliomba

    mpaka baba akaacha kuongea na akapona palepale. Baba akaanza kujishangaa huku

    akijiangalia akasema “mwanangu Meshack nimekuwaje hivi, mbona mwili wangu

    unaharufu sana, na hata nguo yangu ya ndani nahisi sijabadilisha siku nyingi mimi"

    mama alipo ingia ndani akijua kuwa baba amekufa.







    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mama alishangaa kuona baba amepona alafu lengo lake la kumuua halijakamilika.

    “mke wangu hupo mama, nina siku nyingi sana sijakuona" mama alijilazimisha kuweka

    sura ya furaha ingawa ilikuwa ni ngumu kwake lakini alijitaidi kufurahi kinafiki kuwa

    mume wake amepona ila kwa upande mwingine ilimuuma sana kuona bado baba ni

    mzima wa afya, ndipo mama akamjibu baba kwamba, “mume wangu mbona kila siku

    tupo wote, inakuwaje unasema unasiku nyingi hujaniona" mchungaji akasema, "jamani

    mimi nawaacha nataka kuondoka lakini, mnatakiwa kuja kanisani kwangu, na

    msisahau kumuomba Mungu maana katika maisha sio kila mtu anafurahia kuona mtu

    anafanikiwa labda katika biashara, masomo, na maendeleo kwa ujumla na kitu kingine

    huwezi kupendwa na kila mtu, alafu umzaniae kumbe sie" kipindi namsindikiza

    mchungaji akaniambia kwamba, “Meshack kuwa makini na mke wa baba yako maana

    kitendo mnacho kifanya sio kizuri kabisa Mungu hakipendi", “naomba usimwambie

    baba yangu mchungaji, na nakuwahidi kuwa siwezi kurudia hii dhambi ya kuendelea

    kufanya mapenzi na mke wa baba yangu".



    Siku moja nikiwa nyumbani mwenyewe maana baba alikuwa ameenda kwa mchungaji,

    mama alikuwa sokoni na pale nyumbani nilibaki mimi na mtoto wangu tu maana

    alikuwa amelala, nilijiuliza maswali sana, “hivi siku baba akigundua kuwa mimi na

    mke wake ni wapenzi atachukuwa hatua gani? Au labda huyu mtoto baba anae

    mpenda sana, hivi akijua sio wake ni wangu ni laana gani nitaipata mimi, hapana

    itabidi tu nimnyonge mtoto kisha ninyamaze kimya wakija watajua labda ni ushetani

    bado umetawala humu ndani" baada ya kuwaza vile niliamka kisha nikaingia chumbani

    kwa baba yangu, kusudi nimuue mtoto wangu alafu baada ya siku chache nifanye

    mpango wa kutafuta sehemu nyingine ya kukaa kusudi mimi na mama tusiendelee

    kufanya mapenzi, kipindi nipo chumbani, nilimtazama mtoto kwa huruma sana na nafsi

    yangu ilikuwa inanizuia kumuua lakini nafsi nyingine ya kishetani ilikuwa inasema,

    “bora mtoto afe maana ni mdogo sana, lakini sio kuja kuumbuka badae itakuwa ni

    aibu" nilichukuwa mswaki wa baba ili niusukumie kwenye mdomo wa mtoto mpaka afe

    ila nikaona wanaweza kunigundua, ndipo nikamsogelea mtoto karibu ili nimnyonge

    afe.





    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Wakati nimeshika shingo la mtoto ili nimbane kwanguvu afe moyo wangu ukasita

    kidogo, ila nikasema, “kama nimepanga kuua wacha niue tu, mtoto mwenyewe mdogo

    hatambui chochote bhana" ndipo nikasogeza mkono kwa nguvu zangu zote kuua, mara

    ghafla nikasikia mlango unafunguliwa, kumbe alikuwa ni mama amerudi kutoka

    sokoni, alinikuta chumbani akauliza, “tatizo nini, mbona umeingia chumbani?"

    nilimdanganya kwamba, “mtoto alikuwa analia hivyo nilikuwa nambembeleza alale

    tena" na hiyo ndiyo ilikuwa pona pona ya kumuua mtoto. Niliamua kuomba likizo

    kazini maana mda mwingi nilikuwa sina raha nawaza kwamba baba akitugundua mimi

    na mama itakuwaje? mda mwingine hata hamu ya chakula nilikuwa sina sababu ya

    mawazo. Mama aliamua kurudi kwa mganga wake ili ampe dawa ya kumuua baba

    kabisa kusudi asipate hata muda wa kuombewa, lakini kwa bahati mbaya yake,

    alimkuta yule mganga amefariki dunia sababu ya maombi ya yule mchungaji.



    Siku moja asubuhi baba alijiandaa kusudi aende kazini, baba alikuwa amependeza

    sana siku hiyo maana alikuwa amevaa suti yake nzuri nyeusi pamoja na begi lake

    mkononi. Alipo toka nje na kuondoka baada ya masaa machache mvua kubwa ikaanza

    kunyesha. Nilishangaa kuona mama anakuja chumbani kwangu na kulazimisha kuwa

    anahamu ya kufanya tendo, “mama leo mimi sifanyi uchafu wako na ukilazimisha

    namwambia baba","mwambie tu, siogopi, tena ukisema na mimi namwambia ukweli

    kuwa mtoto sio wake".



    Niligopa kusikia kuwa atamwambia baba kuwa mtoto ni wangu, ndipo nikakubali

    kufanya na mke wa baba mapenzi, kipindi tunacheza mechi mama alikuwa anafurahi.

    Nilijikuta naburudika sana ndipo nikajitahidi kufanya mama afurahie zaidi. Kumbe

    kipindi baba yupo njiani kutokana na maombi yake kwa mchungaji na kumuomba

    Mungu sana, nahisi Mungu alimpa ufunuo wa kumfanya arudi nyumbani mda huo,

    kibaya zaidi wakati nafanya mapenzi na mama hatukufunga mlango. Wakati nipojuu

    ya mwili wa mama naburudika, nilishangaa kuona mlango unafunguliwa na baba ndipo

    akatufumania mimi na mke wake tuna fanya mapenzi! mama aliruka na kuzubaa kwa

    aibu, nilishindwa piajinsi ya kujitetea, Ndipo baba akasema.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Dahh! Vaani Meshack mwanangu unalala na mama yako, unanivua nguo Meshack",

    “hapana baba, nisamee ni mama alinilazimisha kufanya hivi" nilimjibu hivyo huku

    mwili wangu wote ukiwa unatetemeka, sehemu zangu za siri zikiwa zimesinyaa yaani

    ilikuwa ni aibu tupu, maana nilijua fika kuwa siku ya mwizi imenifikia, “Meshack

    mwanangu, nimekulea kwa upendo wote, nimekusomesha kwa pesa zangu kwa tabu

    sana, haya ndiyo matunda ninayo vuna kwako, unakula ninapo kula, ehh laana gani

    hizi Meshack, nimemkosea Mungu nini mimi?" alisema baba huku machozi

    yakimtiririka, “nisamehe baba siwezi kurudia, ni shetani tu". Mama alikuwa amezubaa

    akashindwa hata kuwamka ili avae nguo maana alikuwa bado uchi kama mimi, baba

    akasema, “nimeamini maombi yanasaidia sana, nilijikuta narudi nyumbani bila sababu

    maarumu, kumbe huu ushenzi ndiyo unatendeka ndani ya nyumba yangu, mmenivua

    nguo leo, yaani sikutegemea kama kijana wangu ungeweza kufanyajambo kama hili,

    kumbe ndiyo maana mchumba wako alikukimbia, yaani nakulazimisha kuoa kila siku

    hutaki kumbe unazini na mke wangu, hivi kumbe ndiyo maana mke wangu kipindi

    anajifungua alikuwa anakutaja sanajina, leo ndiyo nimejua kumbe hata mtoto sio

    wangu", “hapana mume wangu mtoto ni wako" alisema Fey, baba alitoka chumbani

    kisha akaingia chumbani kwake kwa hasira, kipindi hicho sisi tupo chumbani, kisha

    baba akakaa ndani.



    “Mama unaona ulicho fanya sasa, hivi naificha wapi sura yangujamani, nimekuzuia

    kila siku hii tabia lakini umekuwa ukinilazimisha kila siku, tazama aibu iliyo tupata,

    nitaishi vipi sasa hapa nyumbani, ni bora nitoroke tu, siwezi kuvumilia hili swala hata

    kidogo" mama akasema, “usiondoke mpenzi wangu, baba yako siku hizi ni mtu wa

    kanisani sana, naamini atatusamehe, maana wanafundishwa kusamehe, kisha

    tutaendelea kujivinjari bila mtu yoyote kugundua, najuajinsi ya kumlaghai baba yako

    wewe subiri".





    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mama alitoka chumbani kwangu kisha akaenda kwa mume wake ili aombe msamaha

    maana alikuwa anajua udhaifu wa baba, baba alikataa kabisa kumsamehe, kipindi

    wanaendelea kugombezana, mtoto akaamka kisha akaanza kulia, sasa kwakuwa baba

    alikuwa amezoea kumbeba mwanae kila aamkapo, hivyo mama akahisi hata siku hiyo

    itakuwa hivyohivyo, lakini cha kushangaza alimwambia mama kwamba, “mchukue

    mwanao kisha utoke kwangu".



    Mama alimchukuwa mtoto, ili aniletee chumbani, lakini cha kushangaza alipo ingia

    chumbani kwangu akakuta tayari nimeisha toroka. Niliamua kupanga chumba sehemu

    nyingine, ili nisionane na baba kwanza maana nilijua kuwa lazima amekasilika sana,

    kumbe baba alichukia sana akaenda sehemu niliyo kuwa nafanyia kazi kisha

    akawambia mambo niliyo yafanya, sasa kwakuwa bosi wa ofisini kwetu alikuwa

    anafahamiana na baba, wakaamua kuniachisha kazi, niliishiwa pesa huku kazi pia

    sina, ndipo nikaamua kutoroka na kwenda mkoa mwingine mbali kabisa na nyumbani

    kusudi nisiweze kuonana na baba.



    Kumbe kipindi hicho chote mke wa baba alikuwa hana sehemu ya kuishi, maana

    kumbe hata ndugu na marafiki wa mke wa baba walikuwa wana taarifa kuwa yeye na

    mimi tumefumwa ugoni, hivyo ndugu zake pia wakamfukuza ndipo mke wa baba

    akakosa muelekeo wa maisha kabisa.



    Nilikimbilia mkoa wa Mara, mpakani mwa Kenya na Tanzania (sirari) ili nisijulikane

    nipo wapi kabisa, pesa yangu iliisha nikabaki bila chochote mfukoni, ndipo nikajaribu

    kutafuta kazi kwenye offisi za uhamiaji kule kule mkoa wa Mara kusudi niweze kukidhi

    mahitaji yangu. Mungu alisaidia nikapata kazi maana walipenda vyeti vyangu

    kwasababu nilikuwa na matokeo mazuri ya shule.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Maisha yaliendelea, lakini nilikuwa nakosa raha mda wote, kila ninapo kaa

    nakumbuka tu dhambi niliyo ifanya nyumbani, nilijikuta naanza kunywa sana pombe,

    mshahara wangu wote unaishia kwenye (bar) kutokana na kunywa sana pombe

    ikanifanya nikawa nachelewa sana kazini, walijaribu kunionya sana ikashindikana,

    hata kuna mda mwingine nilikuwa nazubaa kila mda ofisini maana nilikuwa najikuta tu

    namuwaza baba yanguje ananifikiriaje?.







    Nilipewa barua pia ya kufukuzwa kazi pale ofisini hapo ndipo nilichoka kabisa, maana

    nilijua fika kuwa maisha yangu yatakuwa ya tabu sana.



    Siku moja nilimpigia rafiki yangu simu ili anipe habari za huko kwa baba yangu niweze

    kujua anaendeleaje, akasema, “dahh, Meshack umeharibu sana huku ndugu yangu,

    baba yako ameisha mfukuza mke wake pamoja na mtoto, maana anasema mtoto ni

    wako, na kibaya zaidi ni kwamba, mama yako pamoja na mtoto wanaangaika sana

    huku, leo utamkuta mama yako sehemu za pombe, kesho utamkuta anafanya kazi za

    kupasua kokoto na mtoto wake mgongoni, siku zingine anakuta amebakwa na vijana

    wa mtaani, huwezi kuwamini sahivi mama yako anavuta sigara hadharani,jitahidi

    urudi ukomboe familia ndugu yangu". Nilipo sikia yale maneno palepale nikakata simu

    maana niliona kabisa kama baba na upole wake wote ule kamfukuza mama na mtoto,

    basi hawezi kunisamehe hata kidogo. Kwasababu kipindi nina kazi nilikuwa nakunywa

    sana pombe, hivyo hata nilipo kosa pesa wale walevi wenzangu nilio kuwa

    nikiwanunulia wakaanza kuninunulia pia, sasa kutokana na shida na ukosefu wa kazi

    ulio kuwa unanikabiri, mmoja wawale walevi wenzangu akaamua kunipa gari lake

    kusudi niwe nampelekea watoto wake shule kisha atakuwa ananilipa kila baada ya

    mwezi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku moja nipo njiani napeleka watoto shule, kwa bahati mbaya niliona kama kuna

    gogo katikati ya barabara, hivyo nikalazimisha kukwepa lile gogo kumbe pembeni

    kulikuwa na baba yuko na familia yake wanatembea, kwa bahati mbaya nikamgonga

    na kumpasua mguu wake. Niliogopa kuwa naweza kukamatwa ndipo nikaachana na

    Vule baba akiwa analia nikawasha gari na kukimbia. Vule baba alishindwa kutibiwa ule

    mguu ndipo wakaamua kumkata hivyo basi nikawa chanzo cha kumfanya awe kilema,

    siku moja nilikutana naye barabarani akiwa anatembelea gongo, nikashikwa na moyo

    wa huruma ili nimuombe msamaha lakini nikaogopa kabisa kumfata. Kumbe ndugu wa

    Vulejamaa walichukia sana kwa kitendo nilicho mfanyia ndugu yao ndipo wakaanza

    kufanya mikakati ya kunifanya kitu kibaya ili walipize na wao kisasi.





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog