Chombezo : Penzi La Mke Wa Baba
Sehemu Ya Tano (5)
Siku moja nipo (bar) nakunywa, pombe zikanikolea sana, kwa bahati mbaya
nikamshika mke wa mtu makalio yake bila kujielewa maana mimi nilihisi huenda ni
dada tu anaejiuza kutokana na mavazi yake aliyo kuwa amevaa. Mume wake alichukia
kile kitendo cha kushika makalio ya mke wake. Ndipo akaongea na vijana wake
wanikate mkono wangu kisha wampelekee. Mimi sikujua na wala sikuwa na taarifa
yoyote kuwa kunamtu anahitaji mkono wangu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Siku moja usiku nikiwa nimetoka kupeleka gari la bosi wangu kwake, nilishangaa
kukutana na vijana wawili barabarani huku wakiwa wameshika panga, “tunataka
mkono wako wa kushoto, tumetumwa na bosi, hatuna shida ya kukuua", walisema
hivyo, “ndugu zangu mkono wangu wa nini tena naombeni mnisamehe bwana,
chukueni hela hii hapa misinikate mkono" wakachukuwa hela kisha wakasema,
“tusipo peleka mkono wako tutakatwa sisi, turuhusu tu tukate mkono wako" niliinama
chini kisha nikawakwepa na kukimbia, nilipo fika mbele kidogo nikakuta ukuta hivyo
nisinge weza kukimbia tena,jamaa mmoja alinyanyua panga kisha akawa kama
anataka kukata shingo langu ndipo nikakinga mkono wangu wa kushoto kweli
ukakatwa na kisha wakauchukuwa ule mkono mpaka wa bosi wao.
Niliangaika sana kuuguza kile kidonda, na nilijua tu kuwa haya matatizo yote ninayo
yapata ni sababu ya laana ya baba yangu mzazi. Bosi wangu aliamua kuniachisha kazi
maana hakutaka tena niwaendeshe watoto wake kwa kutumia mkono mmoja.
Siku moja nikiwa ndani nalia tu, huku nina mawazo chungu nzima, nikaanza
kukumbukajinsi baba alivyo kuwa ananipenda leo hii nateseka na dunia peke yangu
yaani mda mwingine nakosa hata elfu moja mfukoni, wakati najifuta machozi nikasikia
simu yangu inaita nilipo itazama kumbe baba yangu ndiyo alikuwa na shida ya
kuongea na mimi.
Nilipokea simu ya baba kwa furaha nikihisi huenda ana lengo la kunisamee, “hallo
habari Juma, vipi pesa yangu unanipa lini" alisema baba, “hapana baba mimi sio
Juma, ni mwanao Meshack", alinisonya kwanza, “hivi kumbe nimekupigia wewe
mpuuzi, na sitaki kusikia unasema wewe ni mwanangu, nilisha hesabu tangu zamani
kuwa sijawai kuwa na mtoto, na ninaomba kama nikijisahau nikakupigia wewe tena
usipokee simu yangu, tafadhali sana" alisema baba kisha akakata simu, nilichoka
nikajua moja kwa moja kuwa sina msaada tena wa maisha, ndipo nikaamua kutoa
(line) ya simu kisha nikaitupa ili nisipatikane tena kwenye simu baada ya hapo
nikanunua line mpya hivyo mimi na baba tukapoteza mawasiliano ya kwenye simu
tangu siku hiyo.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Sehemu nilipo kuwa nimepanga, kodi ilikuwa imekaribia kuisha na kibaya zaidi sikuwa
na pesa kabisa, ndipo nikaanza kutafuta kazi kila nyumba, niliangaika sana maana
kila mtu alikuwa ananiambia kuwa, “wewe huna mkono mmoja, utafanyaje kazi?" mda
wote nilikuwa nalia mpaka napiga magoti chini kusudi nipate angalau kazi yoyote
niweze kutunza pesa kwa hajiri ya kulipa kodi, nilizunguka sana lakini sikufanikiwa
ndipo nikaamua kurudi nyumbani, kipindi nafika mlangoni kwangu nikakuta mlango
wangu umebomolewa, nilipo ingia ndani sikukuta begi langu la nguo, kumbe wezi
walikuwa wameniibia, kibaya zaidi vyeti vyangu vyote vya shule na kuzaliwa vilikuwa
kwenye ilo begi, hivyo nisingeweza kuomba kazi bila vyeti tena kupitia helimu yangu,
na kila nilipo pata wazo la kuvifatilia, gharama zake zilikuwajuu ya uwezo wangu,
ndipo nikakata tamaa kabisa na maisha, lakini nilikuwa najua haya yote yanayo
nitokea ni laana ya baba yangu mzazi.
Hali iliendelea kuwa ngumu mpaka kula kwangu kukawa kwa tabu sana, kilicho kuwa
kina niumiza sana ni pale kazi zilizo kuwa zinapatikana zili-kuwa za kulima kwenye
mashamba lakini mimi nilikuwa siwezi kulima kutokana ule mkono mmoja kukatwa.
Siku moja nilizidiwa sana maana nilihisi njaa mpaka nikaanza kuhisi mwili unaishiwa
nguvu kabisa, ndipo nikamsimamisha dada mmoja hivi barabarani Mungu saidia
alisimama, “habari dada, ndugu yangu naomba msaada wako, leo siku ya nne
sijaweka chochote tumboni, naomba hela nikale dada", “ehh kaka siku nne hujala,
unaishi vipi sasa?" alijibu hivyo, “nishida tu za dunia dada yangu", “sasa cha kufanya
ni kitu kimoja kaka yangu, twende kwetu nikapike chakula ule maana hapa sijabaki na
hela yoyote kabisa" niliongozana naye mpaka kwao, alipika chakula tukala pamoja na
wazazi wake, familia yao ilikuwa imeshika dini sana, hivyo nikalialia sana shida zangu
mpaka baba wa Vule binti Nancy, akanionea huruma, hata mama Nancy akasema,
“wewe kijana usijali kabisa, utakaa hapa utaishi tu vizuri maana sio vizuri sisi
kubakiza chakula kisha tunatupa wakati wewe unasema unakaa siku nne hujala
chochote".
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilianza kuishi kwenye ile nyumba, ila nilijitahidi sana kufanya kazi nilizo ziweza,
mpaka wazazi wa nancy na Nancy wote wakafarijika mimi kuendelea kukaa kwao.
Niliishi kwa mda sana kwenye nyumba yao, baada ya miaka saba, baba yake Nancy
alifariki dunia hivyo nyumba nzima tukabaki mimi, mama Nancy pamoja na Nancy.
Tuliishi vizuri sana pale nyumbani na walikuwa wananiheshimu sana maana ndiyo
nilikuwa mwanaume nilie kuwa nimebaki kwenye ile nyumba. Siku moja tumekaa
sebreni mama Nancy akaanza kututania kwamba, “hivi nyie wanangu si muoane tu
mniletee wajukuu maana mnapendana sana, mda wote mnafurahi tu, nyie hamjui tu
yaani mnapendeza sana kuwa mke na mume, na mimi natamani sana kuona wajukuu
zangu kabla sijafa".
Kwa mara ya kwanza nilihisi huenda mama anatania, hivyo basi nikaamua kumuita
Nancy pembeni kusudi tuweze kuongea kuhusu ilo swala, sikuwamini nancy alivyo
sema kwamba yupo tayari kuwa mke wangu, “Nancy asante sana kwa kunipenda na
kunikubalia kutoka moyoni mimi kuwa mume wako, nashindwa kuwamini yaani na huu
ulemavu wangu umekubali kuwa mke wangu wa maisha", “mapenzi huwa yanatoka
moyoni Meshack, napenda sana tabia zako tangu nikufahamu, maana kipindi chote
upo hapa sijawai kukuona na tabia mbaya za kubadilisha wanawake".
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mama Nancy alitukubalia hivyo nikaanza kulala chumba kimoja na nancy, nilifurahi
sana maana alikuwa ananifariji sana, mda mwingine nikajisahau kabisa kama kuna
kosa nililitenda kwa baba yangu. Baada ya miezi miwili Nancy alipata ujauzito, Mungu
alisaidia mpaka akajifungua, lakini tulishangaa sana maana mtoto alitoka akiwa
kilema yaani mguu mmoja mfupii mwingine mrefu, Nancy aliumia sana kupata mtoto
wa namna ile ila nilimpa moyo kuwa yote ni mipango ya Mungu, baada miaka miwili
mke wangu alipata ujauzito, nilikwazika sana maana mtoto alie toka tena alikuwa
kilema kama wa kwanza, yaani mguu mmoja mrefu na mwingine mfupi, mke wangu
akauliza, “Meshack mume wangu, hivi kwenye ukoo wenu kuna ndugu wa namna hii,
mbona watoto wetu wote wanatoka vilema" nilimjibu kuwa, “mke wangu kwa upande
wetu sijawai kuona kabisa ndugu zetu wapo hivi labda nikuulize kwenye ukoo wenu
kama wapo wa hivi, maana watoto wetu wote wanatoka vilema tu"tulikosajibu kabisa,
ndipo tukapanga kuwa tutafute mtoto wa tatu kama na yeye atakuwa kilema basi
tuache kuzaa tu, ili tuwalee watoto watatu tu, tuliumia sana maana hata mtoto wa tatu
sawa alikuwa wa kike mrembo sana lakini nayeye alikuwa kilema pia.
Nilikaa nikawaza sana kwanini iwe vile, ndipo nikamuita mke wangu ili nimpe siri kwa
nini tunapata watoto wa namna ile, alipo kuja nikamwambia kwamba, “mke wangu
kuna kipindi nilikuwa dereva wa gari, ila kwa bahati mbaya nilimgonga mtu barabarani
na kumpasua mguu wake, baada ya hapo nilimkimbia, hata sikuwa na punje ya
huruma kuweza kumjulia hari hospitali kipindi anakatwa ule mguu, na kuna siku moja
nilikutana naye barabarani anatumia gongo kutembea nikatamani sana kumuomba
msamaha ila nikaogopa, mimi naomba twende kumuomba msamaha popote alipo
kusudi tusiendelee kupata vizazi vya namna hii, huenda Mungu na yeye pia
atanisamehe, endapo Vule baba akitusamehe kutoka moyoni, mke wangu akasema,
“sawa mume wangu tumtafute, maana hii ni laana"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Tuliangaika sana kumtafuta Vule baba ambae nilimsababishia ulemavu, ilituchukuwa
mda sana kumpata takribani kama miaka mitatu. hila nilijuta sana, kwanini
nimemuomba yule bwana msamaha, maana kipindi nimefika kwake, walikuja ndugu
zake wengi pamoja na majirani zake wa karibu. Kaka yake Vule bwana akasema,
“ulimfanya ndugu yetu awe kilema, ukamkimbia bila huruma, alafu leo unakuja kisha
unajifanya unalia eti unaomba msamaha, hivi ulizani sisi ni wajinga tulipo kaa kimya,
sasa basi msamaha wetu tutakupa lakini kwa sharti moja tu", asante kaka ni sharti
gani hilo" nilimjibu hivyo nikihisi huenda wanahitaji pesa, “unatakiwa kuwacha mguu
wako hapa, yaani tukukate pia mguu ndiyo uwe umesamehewa, maana ndugu yetu
umemfanya kuwa mlemavu kila saa kila dakika anaumia kuupoteza mguu wake na
chazo cha yeye kuwa hivyo ni wewe maana ulimgonga na gari lako, hivyo hatuwezi
kukusamehe kwa maneno lazima damu ikutoke pia", mke wangu akasema, “heee!
Wewe baba ni roho gani hiyo sasa, msameheni mume wangu, kwani hamuoni kwamba
hana mkono mmoja, sasa mkimkata na mguu mnategemea atakuwa ni mtu wa aina
gani, huo sini unyanyasaji, maana hata kama sawa alimgonga na gari, lakini ilikuwa ni
bahati mbaya tu sasa mkimkata mguu mtakuwa mmesaidia nini?".
Nilianza kulia huku nikijua fika kuwa wale watu hawawezi kunisamehe kabisa, “mume
wangu usilie, tuondoke tu na tumkabidhi Mungu hili swala," kipindi tunaamka
kuondoka, nilishangaa kuona napigwa teke, mke wangu akafungwa kamba miguuni na
mikononi kisha akapelekwa chumba ambacho nilikuwa hata sikujui, nilijaribu
kupambana nao lakini kutokana na ukosefu wa mkono mmoja wale vijana walishinda
nguvu kabisa.
Mke wangu alipelekwa kwenye chumba na kubaki na kijana mmoja ndani wa
kumshikilia kusudi asitoke nje kuona ninavyo katwa mguu wangu, maana walijua kuwa
nikakatwa na panga mbele ya mke wangu inaweza kumfanya mwanamke apate
mshituko na kujikuta hata anajifanyajambo baya. Kibaya zaidi wale watu walikuwa
wanakaa nje kidogo na mji hivyo kule kijijini hakukuwa hata na kituo cha polisi cha
kuweza kutusaidia mimi pamoja na mke wangu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Walinishika kwa nguvu kisha wakataka kunifunga kamba mkononi, nilikataa na
kuwanza kupambana nao, walinipiga sana, mwili wote ulijaa damu, nikawa
mnyongeeee! Wakanifunga kamba mkononi, kisha wakanisimamisha kwenye mti,
kiuno changu kikafungwa kamba na niliumia sana maana ile kamba ilinifinya ngozi
mpaka nikaanza kutamani kufa tu, ili niondokane na tabu za dunia.
Kuna kijana aliitwa kuja kunikata mguu wangu na alijulikana kwajina la Osama, alipo
fika akashika shoka kisha akanyanyuajuu, nililia kipindi naona kabisa naupoteza
mguu wangu, “kaka osama, usinikate mguu ndugu yangu nisamee kaka tafadhali",
Vule kaka alikuwa na sura mbaya sana, sura yake ilikuwa imekaa kikatili, alinyanyua
shokajuu kisha akasema, “nakataaaa mguu, navunja mimi," kipindi ananyanyua
shoka lakejuu zaidi kwa bahati nzuri kumbe ule mpini ulikuwa umelegea hivyo kile
chuma cha kukatia kikachomoka na kumuumiza Osama vidole, aliweka shoka chini
kisha akasema, “nani ameleta shoka bovu, mpaka limenigonga vidole" alinuna kisha
akaondoka.
Nilihisi huenda labda wale watu watanionea huruma na kuniacha niondoke zangu
lakini wakasema, “kamuiteni chui aje kumkata huyu kijana haraka" nilipo sikia mtu
amepewajina la chui nikajua lazima nife maanajina lenyewe liliniogopesha. Chui
aliwasili kisha akaweka shoka sawa, “fumba macho" alisema hivyo, “chui sikia
usinikate nitakupa pesa chui, naomba usikate mguu chui, nihurumie kaka", “fumba
macho nimesema" alijibu hivyo.
Nilifumba macho kweli kisha nikaanza kupiga kelele maana nilijua kuwa siwezi
kusamehewa, kipindi nalia nikasikia mke wangu analia pia kutoka kule chumbani,
nilihisi huenda analia kisa kanisikia nalia, lakini kumbe mke wangu alikuwa anabakwa
na Vule kijana alie ambiwa amshike kule ndani kusudi asione ninavyo katwa mguu,
mke wangu aliumia sana kufanyiwa ule uchafu bila idhini yake, lakini hakuwa najinsi
maana Vule kijana alikuwa amemshikia kisu hivyo akakubali tu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Chui alisema, “navunja mfupaa, fumba macho" nilifumba macho na kukaza hisia za
maumivu, chui alinikata mguu mpaka damu zangu zikamrukia usoni mwake, nililia
sana maana alipo kata kwa mara ya kwanza mguu haukutoka hapo hapo hivyo
akakata kama mara tano ndipo mguu ukaachana na mwili, wale watu walikuwa na roho
mbaya sana, maana hawakupata huruma hata kidogo, mimi nilipata maumivu mpaka
nikapoteza fahamu, kumbe wale vijana wakajua nimefariki hivyo wakanibeba na
kwenda kunitupa mbali kidogo na kwao wakanipeleka sehemu zenye vichaka.
Baada ya hapo wakaenda kumwambia kijana alie kuwa na mke wangu amtoe ndani,
walipo ingia wakakuta yupo anambaka mke wangu kipenzi, walimlaumu sana na
kumwambia, “unakosea kufanya hivyo, sisi shida yetu sio huyu mwanamke, shida
yetu ilikuwa mume wake" mke wangu alipo toka tu akakuta damu nyingi nje, alipo
ulizia mimi nilipo wakasema, “tumemtupa vichakani nenda kamtafute" wakati huo
mimi damu zinanitoka mguuni na nimezimia sina nguvu hata kidogo wala sijitambui,
mke wangu alianza kulia sana kisha akaanza kunitafuta nilipo ndani ya hicho hicho
kichaka.
Mke wangu aliangaika sana kutembea umo vichakani akisema,"mume wangu uko
wapi" alirudia sana hayo maneno bila mafanikio, sasa Mungu saidia mke wangu alifika
sehemu akahisi uchovu akakaa chini, kumbe nyuma ya kichuguu alicho kuwa amekaa
nilikuwepo mimi, nilijukuta Napata fahamu huku nikisikia maumivu makari sana, nililia
sana, mke wangu akaogopa akakimbia mbele, alipo rudi kuwangalia ni nani, alisikitika
sana kuniona mume wake nipo chini bila mguu wangu. Alinifata kwa uchungu kisha
akasema, “mume wangu pole sana, tumuachie Mungu yeye ndiyo muweza wa yote,
atakama wangekukata nini kwenye mwili wako siwezi kukuwacha nakupenda sana
mume wangu" nilikuwa na maumivu sana ndipo nikamuegemea mke wangu kisha
tukaanza kujivuta polepole ili niende hospitali, damu zilikuwa zinatoka sana mpaka
nikaishiwa nguvu njiani nikatamani kufa tu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mke wangu alimuona babu mmoja na familia yake wanatoka shambani kulima, aliwaita
kisha akawaomba msaada, ndipo nikasaidiwa na kutibiwa kienyeji kwa waganga wa
kienyeji mpaka nikapona kabisa, lakini nilibaki kilema. Kipindi tupo kijijini watoto
wetu kumbe walikuwa wanateseka sana nyumbani, maana pesa tuliyo waachia iliisha
kwasababu tuliacha hela kidogo tukijua tutawai kurudi nyumbani, hivyo waliishiwa na
wakabaki bila chochote ndani, lakini kilicho wasaidia ni kwamba walitumia ulemavu
wao kuomba msaada barabarani na kweli watu walikuwa na huruma walipo waona wote
watatu ni vilema hivyo basi wakawasaidia.
Hata hivyo mimi na mke wangu tuliondoka na kurudi kwetu, lakini kumbe mke wangu
kipindi amebakwa na VuIe kijana kumbe alipata ujauzito wa VuIe bwana kwa bahati
mbaya.
Kwa mara ya kwanza, sikuweza kugundua kabisa kama mke wangu ni mjamzito, na
sikuwaza kabisaaa!, Kama angeweza kuwa na mimba, maana tulikuwa tuna mda mrefu
sana hatujakutana kimwili kwasababu tulikuwa na uoga kwamba tunaweza kuzaa
mtoto wa nne ambaye ni mlemavu pia. Watoto wangu walishangaa sana kuona baba
yao sina mguu, na kilicho wakwaza zaidi ni pale walipojiona wao ni vilema, na baba
yao pia nimekuwa kilema kama wao, “baba tazama hauna mkono mmoja,juzi tu wewe
na mama mlituaga mnasafiri kwa mda mfupi, tunashangaa umerudi bila mguu mmoja,
kwanini familia yetu ina mikosi" alisema mtoto wa kwanza, “usijali mtoto wangu kila
jambo litokealo huwa ni mipango ya mwenyezi Mungu" alijibu mke wangu. Sasa mimi
kipindi mke wangu pamoja na watoto wanaongea nilikuwa nalia sana machozi
yakinitoka mbele ya watoto, mtoto wangu wa mwisho alikuwa ananipenda sana,
alichukuwa kitambaa na kunifuta machozi, “usilie baba, ukilia, utatuliza na sisi"
alisema “Lidia" mtoto wangu wa mwisho alie kuwa mrembo sana lakini mlemavu pia.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mguu wangu ulikuwa bado haujapona, hivyo hata kujiusisha na swala zima la mapenzi
na mke wangu ilikuwa ni ngumu sana, kwasababu kidonda kilikuwa hakija kauka
vizuri. Kumbe mke wangu alikuwa amegundua kuwa ana mimba ambayo sio yangu,
lakini akaogopa kuniambia akihisi kwamba nikijua nitamuacha na kumtelekeza, hivyo
akaamua kukaa kimya kusudi mimi nisiweze kudungua. Siku moja nilimkuta anakula
maembe mabichi yenye uchachu, “mke wangu kipenzi, naona unakula maembe
mabichi leo, wewe siunasema hupendelei vitu vichachu labda uwe mjamzito"
nilimuuliza mke wangu, “hapana mume wangu yaani huwezi amini leo kunajirani
kapita na maembe hapa, nikammezea mate, uvumilivu ukanishida ikabidi nimuombe
tu embe nile, lakini nililiosha kwanza" alijibu mke wangu. “haya sawa mama watoto,
mimi naenda ndani", akajibu kwa furaha sana, “sawa mume wangu nakuja pia" ndipo
nikageuza gongo langu na kuwanza kurudi ndani polepole.
Siku ziliendelea kwenda, mke wangu akaanza kuwa mvivu sana wa kufanya kazi za
ndani, vyombo vinashinda vichafu, uwanja pia mchafu, kazini hataki kwenda, mda
wote yeye anatapika na kutema mate ovyo. Sikuweza kuhisi hata kidogo kama mke
wangu ana mimba, maana alikuwa sio mtembezi mda wote nakuwa nae nyumbani na
kazini, hivyo swala la mimba nilikuwa sina wasiwasi nalo kabisaaa. Siku moja
alizidiwa sana ndipo nikamwambia kwamba, “mke wangu, hali yako kiafya sio nzuri
itabidi nikupeleke hospitali" mke wangu alichachamaa, “hapana mume wangu, mimi
siumwi, huo ni uharibifu wa pesa, magonjwa mengine mtu unaweza kulala na kunywa
maji mengi ukapona tu", “ sawa mke wangu, ila kama ukizidiwa naomba usikae kimya
niambie kusudi ukatibiwe".
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kumbe mke wangu alikuwa akiamka asubuhi anafunga tumbo lake kwa nguvu sana
kusudi nisiweze kugundua kama mimba inaanza kukuwa, nilianza kumuhisi kuwa ni
mjamzito maana kuna kipindi aliaanza kumchukia sana mtoto wangu wa kwanza nilie
zaa nae, kila akifanya kosa dogo anampiga, anamtukana mpaka matusi mtoto.
Nilimuita mke wangu na kumkalisha chini, “mke wangu, naanza kuhisi vitu vibaya
kwako, hivi ni kweli una mimba kama hisia zangu zinavyo niambia", “heee! Mimba,
mme wangu kwani hiyo mimba umenipa lini, mimi sio mjamzito mume wangu, ni hisia
zako tu" alisema mke wangu, “haya sawa kama huna mimba", nilimjibu mke wangu.
Sura ya mke wangu ilianza kubadilika, akaanza kupata chunusi, kinywa chake kinajaa
mate kwa mda mfupi sana. Sasa kwa sababu haikuwa mimba yake ya kwanza, hivyo
nikajiongeza na kutambua kuwa mke wangu amebebeshwa mimba na mtu tofauti na
mimi. Niliamua kuwa muwazi huku nikitokwa na machozi, “mke wangu, hivi kweli
umeshindwa kuvumilia kidonda changu cha mguu kipone, ili tukutane kimwili,
umeamua kuleta tamaa za mapenzi na kuzini nje ya ndoa, hivi ni pepo gani lililo
kuwasha mpaka ukatoka nje, au kwasababu sina mguu" mke wangu akiwa analia pia
akasema, “nisamehe sana mume wangu, sikutaka kukwambia maana nilijua
nitakuumiza sana roho, kipindi wewe umefungwa kamba ili ukatwe mguu, wale vijana
walinibeba mimi kisha wakanipeleka kwenye chumba na mmoja wao aliniingilia kimwili
bila idhini yangu, ndiyo maana nimepata mimba ambayo sio yako" nilishtuka,
nikajisikia vibaya sana, lakini nikaamua kukaa kimya maana nilikumbukajinsi nilivyo
mpa mke wa baba yangu mimba, leo hii na mimi mke wangu mtu mwingine amemjaza
mimba, ndipo nikaamini msemo usemao kwamba, “malipo ni hapahapa duniani".
Sikuwa najinsi niliamua kuvumilia mpaka mke wangu akajifungua, lakini mke wangu
aliumia sana, maana mtoto alitoka kabla ya miezi yake, na kutokana na kushindwa
kutimiza njia za kumlea mtoto ambaye hajafikisha miezi tisa tumboni, ikampelekea
Vule mtoto kufariki dunia.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwa kipindi nilicho kuwa naumwa huku mke wangu pia ni mzazi, biashara zetu zilikuwa
zinaendeshwa na binamu yake mke wangu, maana mama nancy alikuwa ni marehemu,
sasa siku moja usiku kipindi Vule binamu ameleta pesa za mauzo nyumbani, mimi
nilikuwa sipo pamoja na mke wangu hivyo Vule binamu akamkabidhi ndugu yake mke
wangu mwingine alie kuja kumsaidia mke wangu baada ya kuwa amejifungua, sasa
alie pewa pesa akaamua kukimbia nazo bila kutuaga maana alishikwa na tamaa ya
pesa, Na kibaya zaidi kumbe Vule binamu alie kuwa ameleta pesa za mauzo alipanga
mbinu na majambazi waje kutuvamia kisha wabebe zile pesa zote. Kipindi tumerudi
nyumbani usiku mimi na mke wangu tuliwakuta watoto peke yao nyumbani, na Vule
dada alikuwa ameisha toroka mda mrefu na kibaya zaidi alikimbia na pesa, sasa
kipindi tupo sebreni nilishangaa kusikia, “kaeni chini" mimi na familia yangu yote
tukalala chini, wakasema, “tunaomba pesa zote za mauzo yenu ya leo" nikasema,
“tusamehe ndugu zetu bado binamu hajaleta"jambazi mmoja akasema, “ohh, hamtaki
kutoa pesa ehh! Sasa hawa ngoja niwaonyeshe kazi" alimshika mtoto wangu wa
mwisho ambaye ni lidia, alie penda kunifuta machozi mda wowote yalipo nitoka, Vule
jambazi alimningiiniza mtoto na kumchoma kisu bila huruma, mtoto akafariki mda
huo huo, “kama hamtaki kutoa pesa tutawaua wote, toa pesa" nikasema, “pesa
zingekuwepo ningewapajamani leo binamu hajaleta hela" sasa kumbe wale walikuwa
wanajua kabisa kuwa binamu kaleta hela, lakini kumbe alipo leta alimpa ndugu yake
mke wangu, na Vule naye akakimbia na pesa bila sisi kujua.
Jambazi akasema, “naona mnaleta mchezo na sisi" alimchukuwa mtoto wangu wa
kwanza, alie penda kunishauri na kuniuliza maswali sana kisha akamuua bila huruma
mbele ya macho yangu. Mke wangu alilia sana akasema, “sisi tumetoka hospitali mda
sio mrefu hatujui pesa zilipo" nilitamani kupambana nao lakini nilikuwa sina mkono
wala sina mguu pia, hivyo nisinge waweza maana walikuwa wawili.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kilicho niuma ni kwamba alibaki mtoto mmoja tu, kumbe na 9
yeye alikuwa mjanja alipo ona watoto wenzake wanauliwa
akaamua kusimama na kukimbia, kibaya zaidi alikuwa mlemayu hiyyo kukimbia
kwake kulikuwa kwa shida, ndipojambazi mmoja akamfyatua na risasi, akafa hapo
hapo, Kisha wakasema, “Sasa hivi mmebaki nyie wawili tu, mke na mume, tunaomba
hela, msipo tupa tunawamaliza" nililia, mke wangu akalia, "'tuhurumie, tutawapa pesa
za kesho, pesa ni makaratasi msitutoe roho zetu"jambazi akasema, “wanawake huwa
ni wepesi sana wa kutoa pesa, inaonyesha wazi kabisa, mwanaume ndiyo anafahamu
pesa zilipo, sasa kama anajifanya kuwa yeye ni mbishi tunamuua mke wake mbele ya
macho yake" nilipo sikia hiyyo nilianza kutetemeka, maana nilijua kabisa sina akiba
yoyote ndani ya kuwapa, na pesa za mauzo ni kweli hakuna, nikajutia sana kwanini
nilikuwa sikai na pesa ndani, wakauliza, "“we mwanaume unawaza nini, unazani
unaweza kutukwepa, sisi tunaroho ngumu, tumeisha ua sana, tuna hesabu mpaka tatu
usipo tupa pesa tuna muua mke wako sasa hivi," nilihisi wanatania, “moja...
mbili....tatu" nilifumba macho na kusikia sauti ya mke wangu ikisikika na kupotea
ghafla, nilipo fumbua macho nikakuta kisu kimepitiswa katikati ya shingo la mke
wangu, huku akitoa sauti kama kuku anayyo chinjwa, akaanza kuchezesha sana
miguu mpaka akafariki.
Nililia mpaka nikaishiwa nguvu na sauti ikaanza kukoroma, Jambazi mmoja akasema,
“wewe baki hapa muangalie huyu mjinga, ngoja nikatazame chumbani kama naweza
kupata pesa" kipindi nimebaki na Vulejambazi mmoja nilikuwa naangaliajinsi ya
kumkwepa pale kusudi nisife, kuna kipindi aligeuka nyuma kidogo ndipo nikambonda
na gongo langu kichwani kwake, alianguka na kuzirai hapo hapo, ndipo nikatoka
haraka haraka, maanajambazi mwingine alikuwa bado anakagua yyumba pole pole
kutafuta pesa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kesho yake nilirudi nyumbani kwangu, kuwangaliajinsi ya kuendesha mazishi ya
familia yangu nikakuta ndugu wa mke wangu wapo wote pale, nilichukia sana walipo
niita pembeni na kuniambia, “shemeji Meshack, tunashukuru sana kwa kuteketeza
ukoo wetu, umeua watoto, umeua mke wako, tunashukuru, tulitaka kukufunga lakini
tumemuachia Mungu tu, ila ukoo umekaaa chini na kuongelea hili swala, hivyo basi
kwanzia leo hauruhusiwi kuishi kwenye hii nyumba, na miladi yote ipo chini yetu
tungeomba tu urudi kwenu, maana hata wazazi wako hatuwajui wala kuwatambua,
asante kwa mauaji yako ondoka kabla na wewe hujauliwa,".
Niliogopa sana yale maneno nikaumia zaidi kwanini mimi nafukuzwa bila hata
kumwaga mchanga kwenye makaburi ya familia yangu. Sikuwa najinsi nikaona bora
niondoke kusudi nisije kuuliwa, kama niliyyo katwa mguu na wale watu wengine.
Niliamua tu kurudi nyumbani ili nimuombe baba msamaha, maana laana za dunia
zilinikomesha sana, wakati nipo safarini narudi nyumbani, nilikuwa nazungumza
mwenyewe kwenye basi kama kichaa, kila mtu ananishangaa, kumbe ni damu iliyo
yuja ya watoto wangu na mke wangu kwa ajili ya laana zangu za kutembea na mke wa
baba, ndiyo ilikuwa inanisumbua, nilipo fika Dar es salaam, (ubungo) nikashuka
kwenye basi, nilikutajiji limebadilika, barabara mpya za mwendokasi zimejengwajiji
linayutia sana.
Kipindi nimezubaa naangalia mgari ya mwendo kasi, nilishangaa kuona kijana mmoja
anakuja na kuvuta begi langu kwanguyu kisha akakimbia nalo nilimuona sura yake
yizuri tu, hiyyo nikabaki bila nguo yoyote, na kukimbia nilikuwa siwezi, hata mawazo
ya kupiga kelele kuwa nimeibiwa sikuwa nayo, sababu ya mawazo ya mauaji ya
kikatili kwenye familia yangu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Niliamua kwenda mpaka kwa baba, nilipo fika kwenye geti lake, nilianza kujifikilia
mara mbilimbili, "je nigonge mlango, hivi kweli baba akiniona atanisamehe, acha
nigonge tu mlango, akija nitamwambia, baba nimerudi kwako naomba unisamehe
sitarudia kosa " baada ya hapo nikagonga mlango, kweli mlango ukafunguliwa na
mwanamke mrembo sana, “nikusaidie nini", “dada mimi naitwa Meshack, hapa ni
nyumbani kwetu sijui baba nimemkuta" akasema, “mhhh! Subiri kidogo nakuja" alipo
ingia ndani akaja na mme wake, “yipi kijana umesema wewe unaitwa nani" nikawajibu,
“ohhh! Baba yako alituuzia hii nyumba, na hatujui mpaka leo yupo wapi" nilichoka
sana, ndipo wakanipa msaada wa kulala kwaojapo siku moja kisha kesho yake
nizunguke kumtafuta baba yangu mzazi kusudi anisamehe niondokewe na pepo la
laana.
Nilijaribu sana kumtafuta baba yangu ikashindikana, siku moja kuna shirika moja
liliitisha walemayu wote ili tule na kufurahi kwa pamoja huku huku Dar es salaam,
niliamua kwenda pia maana nilikuwa sina mkono pamoja na mguu, kipindi nipo pale
nimekaaa huku nikisikiliza ushauri wa wageni mbalimbali walio kuwa wamealikwa
kuongea na sisi, nilishangaa kumuona “Fey" akiwa hana miguu yote miwili, akiwa
ameletwa na mtoto wake nilie zaa naye kwenye baiskeli ya vilema, alafu kumbe huyo
mtoto nilipo mtazama yizuri ndiye ambae aliniibia begi langu kipindi nimefika ubungo.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Uvumilivu ulinishinda ikabidi nimfate karibu, “habari dada unanikumbuka,"
aliniangalia akasema, “Meshack ni wewe!"“ndiyo ni mimi mama" alifurahi sana
kuniona, akauliza, “mbona hauna mkono na mguu" nikacheka huku moyo ukiwa
unaniuma sana kisha nikamuuliza, “mbona wewe huna miguu yote pia" akasema, “ni
hadithi ndefu sana Meshack, lakini hii yote ni kutokana na tabia mbaya tuliyo kuwa
tunafanya bila kujua malipo ni hapa hapa duniani, nilikuwa nataka kumuua baba yako,
nikamfanya mpaka akaota peazi tumboni, leo hii baba yako anaishi maisha mazuri tu
alafu mimi nateseka na ulemavu wangu, kama ningekuwa namuheshimu nisinge kuwa
hivi" nikamsimulia pia matatizo yote niliyo pitia na laana zilizo nikuta mpaka akalia,
kisha tukaombana msamaha palepale, kipindi nataka kuondoka akasema, “Meshack
huyu mtoto anae nisukuma na hichi kibaiskeri, ndiyo mtoto wetu tulie msingizia baba
yako, mpaka leo hajawai kwenda shule na ukubwa wote huu" mtoto wangu akasema,
“baba nisamehe najua nilikuibia begi lako lakini nitarudisha tu" tulibadilishana
mawasiliano kisha nikaondoka.
Siku moja nikampigia Fey (mke wa baba) kisha akanielekeza sehemu baba anayo ishi,
nilipo fika nikakuta nyumba yake kubwa sana, walinzi wa kila aina, sehemu za
kuogelea, maua, nyumba nzuri sana yenye mvuto wa kisasa, baba alipo niona
akaanza kusikitika mwenyewe kisha akasema, "'tazama sasa, unatembea na gongo
wakati ulikuwa kijana mzima kabisa, hizo zote ni laana mwanangu, ulimfanya mke
wangu kama mke wako, bila kukumbuka uchungu na nguvu nilizo zitumia kukulea
wewe, ukazaa na mke wangu kipenzi, mkaniona mimi mjinga siwezi kugundua, ukazani
unanizidi akili baba yako, kibaya zaidi mlikuwa mnazini ndani ya nyumba yangu,
mwanangu haya maisha tunapita tu, alafujiulize swali kwamba baada ya kufa utaenda
wapi,je ukiisha enda huko ukiulizwa kwanini ulizini na mama yako utamjibu nini
Mungu" nikamjibu kuwa, “nisamehe baba nimerudi mwanao, ulimwengu umenifunza,
siwezi kurudi kosa, tazama sina mguu, sina mkono, nihurumie baba ulimwengu
umenifunza" baba akasema, mwanangu, “waheshimu baba na mama upate heri na
miaka mingi duniani, nimekusamehe mtoto wangu, sogeza kichwa chako nikushike,
uondokewe na mikosi, na kwanzia sasa unapaswa kumjua Mungu, na umuombe sana
ili akusamehe dhambi zako" nilikumbatiana na baba yangu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alinitafutia mguu na mkono wabandia, nikaanza kufanya kazi nilizo ziweza kutokana
na helimu yangu maana niliyipata yyeti yyangu selikarini, nilianza kupata pesa na
maisha mazuri, ndipo nikaanza kumsomesha mtoto wangu na kumsaidia maisha mke
wa baba bila kuzini naye kama zamani, nilifunga safari ya kwenda kuwangalia
makaburi ya familia yangu. Mpaka sasa naishi mimi na baba nyumbani na
sijabahatika kupata mtoto tena zaidi ya huyu niliye zaa na mke wa baba, na Mungu
saidia baba yangu anampenda sana mjukuu wake, Siwezi kurudi tena kutembea na
mke wa mtu, rafiki, mzazi,jirani au mtu yoyote Yule maana malipo ni hapa hapa
duniani.
******************MwISHo**********************
0 comments:
Post a Comment