Search This Blog

Monday, October 24, 2022

JASHO LA MASUMBUKO - 2

 





    Chombezo : Jasho La Masumbuko

    Sehemu Ya Pili (2)



    MUDA mfupi baadaye binti mmoja akaingia, akamtupia macho kidogo Masumbuko kisha akayahamishia kwa Chausiku.



    “Na huyu ni Mwanahawa,” Chausiku aliendelea huku akimtazama Masumbuko. “Anaitwa Mwanahawa. Ni mdogo wangu, baba mmoja, mama mmoja.”



    Masumbuko aliitika kwa kutikisa kichwa huku akimtazama Mwanahawa. Huyu Mwanahawa alifanana sana na Chausiku. Lakini kufanana huko kulikuwa ni kwa sura tu, kwa maumbile walitofautiana sana.



    Chausiku alikuwa ni mnene, tipwatipwa wakati Mwanahawa alikuwa na mwili mdogo lakini katanuka mapajani na kulitengeneza umbo la 'nane.' Akilini mwa Masumbuko, Mwanahawa alivutia zaidi na hata angestahili kushiriki kwenye kinyang'anyiro chochote cha ulimbwende.



    Hata hivyo hakupata muda wa kumtazama zaidi Mwanahawa, mara Chausiku akamuuliza, “Na wewe jina lako ni nani?”



    “Masumbuko.”



    “Masumbuko?” Chausiku alimuuliza, akionekana kutomwamini.



    “Ndiyo, Masumbuko.”



    “Ok,” Chausiku aliitika huku akitikisa kichwa na papohapo akamgeukia Mwanahawa. “Mwanahawa, huyu ni, mfanyakazi wetu mpya. Atakuwa akiwalisha ng'ombe...” akasita na kumtazama Masumbuko. “ Ulishawahi kuchunga ng'ombe?”



    “Ndiyo. Nzega kuna ng'ombe wengi. Nimeshachunga ng'ombe, mbuzi na hata kondoo.”



    “Basi hiyo nd'o kazi ninayoweza kukupa. Utaiweza?”



    “Ndiyo, mama.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ok, Mwanahawa kamwonyeshe chumba chake cha kulala. Kisha umpeleke bafuni akaoge na umpe nguo nyingine. Hizi alizovaa zichomwe moto.”



    “Sawa dada,” Mwanahawa alijibu kwa kunyenyekea.



    “Halafu, najua ana njaa. Mtayarishie chochote. Mwenyewe unajua utakachomwandalia. Kila kitu kipo.”



    “Sawa, dada.”



    Chausiku akamrudia tena Masumbuko. “Wewe pumzika. Lakini ningependa ujue tu kuwa hapa ni kwa nani. Ni kwa Waziri wa Misosi na Maraha. Anaitwa Kisu Makalikuwili. Unamfahamu?”



    “Ni'shamsikia redioni akitangazwa,” Masumbuko alisema huku akiyaepuka macho ya Chausiku aliyekuwa akimtazama sawia.



    “Basi hapa nd'o kwake,” Chausiku alikazia. “Uko nyumbani kwa waziri! Lakini kwa sasa hayupo. Yuko kwenye mkutano nje ya nchi. Nitamtaarifu kwa simu juu ya ajira yako. Na kwa kuwa umetoka mikoani, najua hatakuwa na kipingamizi chochote. Hawapendi vijana waliokulia hapa Dar na kulizoea jiji. Nakuomba tu ufanye kazi kwa bidii, na uwe na tabia njema. Ukiwa na tabia mbaya atanilaumu mimi. Umesikia?”



    “Ndiyo, mama.”



    “Haya, tutaonana jioni.”



    Akatoka huku mwili wake ukiendelea kutikisika kwa namna ya kipekee, na kuwa kama aliyeamua kuutikisa makusudi kwa madhumuni aliyoyajua mwenyewe; Pwata...! pwata...! pwata....!



    Muda mfupi baadaye masikio ya Masumbuko na Mwanahawa yalinasa ngurumo ya Mercedes Benz ikilalamika nje ya geti.



    **********



    MWANAHAWA alifanya kama alivyoagizwa. Kwanza alimwonyesha Masumbuko chumba cha kulala. Chumbani humo kulikuwa na kitanda kikubwa cha futi sita kwa sita, sofa moja dogo, televisheni ndogo, kabati kubwa la nguo na vikorokoro vingine vilivyoongeza unadhifu wa chumba hicho.



    Baada ya hapo alimwonyesha bafu ili akaoge. Bafu lenyewe lilikuwa ni chumba tu kisichokuwa na kitu chochote. Mtu ilibidi uminye kidude fulani ukutani, na hapo sinki kubwa lingetokea ardhini. Baada ya shughuli zako zote, unakanyaga kidude kingine sakafuni, sinki litazama polepole na kupotea machoni pako.



    Kuzijua kanuni hizo kulihitaji kufundishwa. Masumbuko asingeweza kuzijua kanuni hizo; alifundishwa na Mwanahawa.



    Baada ya kuoga alivaa nguo nyingine alizopewa na Mwanahawa kisha akaenda sebuleni ambako alipata kifungua kinywa; maini ya kukaanga, maziwa moto na mayai ya 'macho ya ng'ombe.'Wakati akiendelea kupata stafutahi hiyo, Mwanahawa alikuwa chumbani kwake ambako alibadili mavazi na kurejea kwa Masumbuko.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Awali alikuwa amevaa gauni zito la kitambaa kilichoshonwa kwa namna isiyovutia. Lilikuwa ni gauni mahsusi kwa shughuli za nyumbani.

    Sasa alibadilika. Alikuwa amevaa kijipensi kifupi na blauzi yenye matundu madogomadogo. Vititi vyake vichanga vilituna kwa kiburi kifuani kama vile vinamdhihaki yeyote yule avitazamaye.



    Alimkuta Masumbuko katulia sofani akionekana dhahiri kuleweshwa na shibe nzito.



    “Kama unajisikia uchovu, unaweza kupumzika,” hatimaye Mwanahawa alimwambia huku akimwelekeza kitanda. “Mi' niko jikoni naandaa chakula cha mchana.”



    Kabla ya kuondoka aliiwasha televisheni na kuweka kituo fulani kilichoporomosha muziki mfululizo. Kisha akatoka huku akitabasamu kwa mbali, tembea yake ikiwa ni ya kujitingisha kivivuvivu.



    Masumbuko akabaki akiikodolea macho televisheni kwa dakika chache kisha usingizi ukamvaa. Alizinduka saa 10 jioni. Alilala zaidi ya saa nne! Akafikicha macho na kuketi kitandani. Akatupa macho mezani na kulishuhudia dude ambalo pia lilikuwa geni machoni pake. Dude hilo lilifanana na meli.



    Kando yake kulikuwa na kipande cha karatasi chenye maandishi: UKIAMKA CHAKULA KIPO MEZANI. BONYEZA KIDUDE CHEUSI. CHAKULA HICHO NIMEKIPIKA MAHSUSI KWA AJILI YAKO. KARIBU, MASU.



    Masumbuko aliguna, akatabasamu kidogo. Akajitoa hapo kitandani na kwenda bafuni kunawa. Aliporejea chumbani alibonyeza kile kidude alichoelekezwa na mara lile dude lote likasambaratika polepole na kwa utaratibu maalumu.



    Ikazuka milango minne, kila mlango ukijifungua taratibu. Ndani yake kulikuwa na vyakula vya aina mbalimbali; wali kwa pande la kuku wa kukaanga, mboga za majani, maharage, juisi ya nanasi na matunda mengine kadhaa.



    Alikula kama mwenye njaa ya siku mbili, na alipomaliza alivirudisha vyombo mahali pake. Dude lile likajifunga na kuanza kupiga king'ora. Muda mfupi baadaye Mwanahawa akaingia na kulitwaa.



    Hazikupita hata dakika kumi Mwanahawa akarejea chumbani humo, safari hii akiwa amejifunga kanga mbili pekee. Moja ilikomea kifuani na nyingine alijitanda mabegani.



    Marashi mazuri yalikijaza chumba hicho mara tu alipoingia. Kwa mwendo wa kusuasua, mwendo wa kujidai alikwenda kuketi kwenye sofa lililokuwa mbele ya Masumbuko. Na mara tu alipoketi kanga moja ilijikunja, sehemu kubwa ya mwili wake ikawa hadharani; mamiguu manene na mipaja mibichi itamanishayo.



    Masumbuko hakuweza kujua kama Mwanahawa alifanya hivyo kwa kudhamiria au ilitokea kama bahati mbaya tu. Akabaki ameduwaa, asiweze kutamka chochote wala kufanya lolote.



    Mwanahawa hakuonyesha kujali wala hakuchukua hatua zozote za kuirekebisha hali hiyo. Zaidi, aliachia tabasamu laini, tabasamu ambalo lilijieleza bayana ni kipi alichokihitaji.





    Masumbuko hakuwa mbumbumbu hata asitambue Mwanahawa ana njaa ya aina gani. Kaa yake na tazama yake vilitosha kutoa taswira halisi. Na ndipo alipoamua kuchokoza. Akamkonyezea jicho na kumwashiria kwa mkono aje aketi pale kitandani. Mwanahawa akajitia kukataa kwa kupandisha mabega juu.



    Haikuwa ishara ya dhati. Masumbuko aliamini hivyo. Kwa mara nyingine akamwashiria kumfuata pale kitandani. Na safari hii Mwanahawa hakupandisha mabega bali alicheka kidogo huku akimtazama Masumbuko kwa namna ivutiayo na mara kwa mara akimtazama kwenye maungio ya mapaja na kiuno ambako kulikuwa taswira iliyomvutia na kumsisimua zaidi binti huyo.



    Masumbuko alikuwa kifua wazi, akiwa na bukta pekee, vazi lililoshindwa kusitiri kikamilifu mabadiliko yaliyojitokeza maungoni mwake kutokana na mhemko uliomvamia pale aliloshuhudia umbo maridhawa la Mwanahawa. Na Mwanahawa alibaini kuwa Masumbuko yu ‘mahututi’ akatamani amvamie haraka laskini akajitahidi kuilinda heshima ya ‘mtoto wa kike.’



    Ukimya ukaendelea kutawala ndani humo. Masumbuko akamkonyezea jicho kwa mara nyingine. Sasa Mwanahawa hakucheka, badala yake aliinamisha uso na kutazama sakafuni kisha kwa sauti isiyokuwa na nguvu yoyote, akasema, “We, Masu, n'takusemea kwa dada.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kauli hiyo haikuweza kumtisha Masumbuko hata kidogo. Alijua kuwa hiyo ni moja kati ya kanuni za wanawake wenye aibu ya kutamka bayana kumkubali mwanamume. Hivyo, aliamua kutoka kitandani na kumfuata pale sofani, akamwinua na kumkumbatia kisha akaivuta kanga iliyomzingira mwilini, akaitupa kitandani.



    Mwanahawa akabaki 'mweupe.' Na ni hapo Masumbuko alipothibitisha hisia zake kuwa kilichomleta msichana huyo chumbani humo ni 'tiba.'





    Ndiyo, alihitaji tiba ya moto wa ujana uliokuwa ukimuunguza. Kwa nini basi asimsaidie binti mpole na mrembo kiasi kile? Alichofanya ni kumkalisha kitandani na dakika kadhaa baadaye walikuwa katika hatua nyingine, Masumbuko akijitahidi kutoa tiba mbadala lakini iliyo mahsusi kwa wagonjwa aina ya Mwanahawa. Na ni siku hiyo Masumbuko alipobaini kuwa kakumbana na 'mgonjwa' mtundu kupindukia.



    Huku ulimi wa Mwanahawa ukiwa kinywani mwa Masumbuko na wakati huohuo kamziba masikio kama vile asisikie vilio na mihemo ya raha za ujana, Masumbuko hakutofautiana na kijipande cha karatasi juu ya kifua kichanga na laini cha Mwanahawa!



    Alirushwa huku na huko, akapelekeshwa kama boya kwenye bahari yenye hasira; sauti ikamkauka na macho yakamtoka pima kama chura anayekaribia kufa! Kwa jumla hakutarajia kukutana na hali hiyo. Hivyo, akajitahidi naye kuuonyesha uwanaume wake katika kuilinda hadhi yake. Akajitahidi kufanya kila alichokijua, akitumia pumzi nyingi na ujuzi aliojaaliwa!



    Walitumia takriban nusu saa wakivitesa viungo vyao kwa namna iliyozikonga nafsi zao na wote waliridhika!



    Baada ya kuoga Masumbuko alitulia chumbani humo akimsubiri mwajiri wake ampe majukumu ya ajira yake.



    **********



    MAMA mwenye nyumba, Chausiku, mke wa Waziri wa Misosi na Maraha Kisu Makalikuwili, alirejea saa 3:45 usiku. Masumbuko akiwa chumbani alisikia geti likifunguliwa ngurumo ya gari ikivuma kwa nguvu. Yeye akaendelea kutulia tu chumbani humo. Nusu saa baadaye akasikia mlango wa chumba alicholala ukigongwa.



    Akainuka na kwenda kufungua. Akashangaa pindi alipofungua na kumwona Chausiku mlangoni. Na si kwamba alishangazwa tu kwa kumwona Chausiku mlangoni, bali pia ni jinsi alivyokuwa. Chausiku alikuwa amejifunga kanga moja tu kutoka kifuani! Mwili wake teketeke, uliong'ara, ulikuwa umepuliziwa manukato yaliyovutia, yakajaa chumbani humo.



    Wakati Masumbuko akiwa bado amepigwa butwaa, Chausiku alipitiliza moja kwa moja kitandani. Akajipweteka kivivuvivu, tabasamu likichanua usoni pake. Kisha akasema, “Sasa njoo. Funga mlango kwa komeo uje tuongee.”



    Masumbuko alitii. Lakini badala ya kumfuata mwajiri wake pale kitandani, yeye aliketi sofani.



    “Unakaa wapi huko?” Chausiku aliuliza kwa ukali wa kuigiza. Haikuwa dhahiri kuwa alifoka kutoka moyoni. Akaongeza, “Nimesema njoo hapa tuongee. Hapo ndio hapa?”



    Sasa Masumbuko akalihama lile sofa na kumfuata mwajiri wake pale kitandani.



    “Sikia Masumbuko,” alianza kuzungumza. Sauti yake ilikuwa ya upole na ya chini. “Mchana nimeongea na mzee kwa njia ya simu, na amekubali ufanye kazi hapa. Utakuwa unalisha ng'ombe na kutusaidia kazi fulani-fulani. Mzee ni mkorofi na hataki mchezo, ndiyo maana tuko wawili tu katika jumba hili. Kwa kweli ana wivu sana! Hivyo, akiwepo jitahidi kuonyesha heshima ya hali juu sana.”



    Akasita na kumtazama Masumbuko kwa makini zaidi huku sasa lile tabasamu lake likizidi kupungua.



    Kisha, akaendelea, “Mshahara wako utakuwa ni shilingi laki moja kwa mwezi. Na utafanya kazi kwa usimamizi wangu. Elewa tu kwamba kazi hizi za kuchunga ng'ombe au mbuzi siyo za mshahara mkubwa kama huu niliokupangia. Wengi hulipwa kati ya shilingi elfu arobaini hadi hamsini tu. Wewe nimekuongeza ili ufanye kazi kwa uaminifu na kujituma zaidi. Umenielewa?”



    “Nimekuelewa, mama.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hata hivyo,” Chausiku alisema, “Ipo kazi nyingine muhimu zaidi ya hiyo ya kuchunga mifugo. Ndiyo maana nimeamua kukulipa laki nzima! Kazi hiyo,” akasita na kumeza funda la mate. Akaangaza macho pande zote za chumba hicho na zaidi akayatupa macho mlangoni kisha akamrudia Masumbuko. “Kazi hiyo nitakuomba uifanye kwa nguvu na bidii zako zote kuanzia usiku wa leo. Wewe umetoka bushi ambako hakuna magonjwa mengi ya zinaa. Kwa hiyo kuanzia leo utaanza kunisaidia.”



    Yalikuwa ni maneno ambayo Masumbuko hakuyaelewa. Ni kazi gani hiyo aliyopaswa kuifanya kuanzia usiku huo? Ina maana pia atakuwa anafanya kazi ya ulinzi? Na kazi hiyo ina uhusiano gani na kumwambia tena eti yeye ametoka 'bushi' ambako hakuna magonjwa mengi ya zinaa? Magonjwa ya zinaa na ajira yake vina uhusiano gani? Wapi na wapi?



    Alijiuliza maswali mengi ambayo hakufanikiwa kupata majibu yake. Na hata Chausiku alibaini kuwa bado hajamwelewa. Lakini hakuwa na wasiwasi kuhusu hilo. Alijua kuwa muda mfupi baadaye ataelewa.



    “Mume wangu ni mtu wa safari za mara kwa mara,” Chausiku aliendelea. “Na hata akiwepo hana lolote la maana, ni mnene sana na utu uzima wake umempunguzia pumzi. Sijui kama unene wake nd'o chanzo cha matatizo aliyonayo au utu-uzima wake nao umechangia kumpunguzia pumzi.”



    Kufikia hapo akajiepusha kutazamana na Masumbuko ana kwa ana. Kwa mbali alihisi kuona haya. Akainamisha uso kidogo kisha akapiga moyo konde na kuamua kupasua jipu. “Kwa hiyo nategemea wewe unisaidie. Nitakutunza na kukupa mahitaji yote muhimu, ilimradi usihangaike na mijanamike ya hapa Dar. Umenielewa vizuri?”



    Sasa Masumbuko alimwelewa. Ndiyo, alimwelewa vizuri, lakini ulikuwa ni mtihani mgumu kwake. Tangu alipoingia humo hakutarajia kuambiwa maneno hayo, tena kuambiwa na mama mwenye nyumba wake! Mwajiri wake! Akubali au akatae?



    Chausiku hakumpa muda wa kutafakari zaidi. Mara aliinuka, na bila hata ya aibu aliitoa ile taulo aliyojifunga mwilini na kuirusha kitandani. Akawa amesimama mbele ya Masumbuko, mtupu kama alivyozaliwa, akitikisa guu la kushoto kwa fahari na kiburi. Macho ya Masumbuko yakatambaa kutoka kichwani hadi miguuni. Akaitazama mipaja ile minene ilivyotikisika.



    Akiwa ni mwanamume mkamilifu, Masumbuko alihisi mifereji myembamba ya barafu ikipanda na kushuka kupitia uti wa mgongo. Akajiona yu kama mtu aliyepigwa shoti ya umeme.



    “Njoo...njoo, mpenzi…baby…” Chausiku alimwambia huku akipanda kitandani.



    Masumbuko akazinduka. Akachojoa nguo na kujitupa kifuani pa Chausiku.



    Chausiku!



    Mke wa waziri!



    Aliondoka chumbani humo alfajiri ya siku ya pili huku akimwambia Masumbuko, “Mwanahawa atakupa shilingi elfu ishirini. Kazi yako ni nzuri. Ukizoea utakuwa mzuri zaidi.”



    **********



    MWAKA ulikatika Masumbuko akiwa katika ajira hiyo, ajira yenye majukumu mawili tofauti. Akawa akiendelea 'kuwatibu' Mwanahawa na dada yake, Chausiku kwa zamu, tiba ambayo aliitoa huku kila aliyetibiwa akisisitiza siri kutunzwa.



    “Usimwambie Mwanahawa...” mara kwa mara Chausiku alimwonya Masumbuko.



    “Usimwambie dada... wala usionyeshe hali yoyote inayoweza... kumfanya akatushtukia...” Mwanahawa naye alisisitiza, msisitizo ambao aliutoa hususan wanapokuwa katikati ya starehe.



    Masumbuko alibadilika; alinenepa, akanawiri na kunang'anika. Kwa nini asipendeze ilhali kila alichokihitaji alikipata? Haya maisha aliyoishi hapa hayakutofautiana na kuishi paradiso. Naam, alistahili kupendeza.



    Hatimaye Waziri Kisu Makalikuwili mume wa Chausiku alirejea kutoka katika moja ya safari zake za ndani na nje ya nchi. Siku hiyo alionekana kuelemewa na uchovu mwingi, na hata hakuonekana kuchangamka.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya mlo wa usiku alikaa kidogo kwenye sofa na kutazama televisheni kwa muda mfupi kisha akaenda chumbani kulala.

    Mkewe alishangaa. Hiyo haikuwa kawaida ya mumewe kuwahi kulala, hususan siku anayorudi kutoka safari. Mara kwa mara alipokuwa akitoka safari, baada ya kula aliketi sofani akinywa toti kadhaa za pombe kali. Usiku huu hakufanya hivyo.



    “Leo hata hataki kunywa whisky!” Chausiku alimwambia Mwanahawa kwa mnong'ono.



    “Ni ajabu,” Mwanahawa alisema.



    Wakati huo Masumbuko alikuwa amekwishaingia chumbani mwake kulala. Mwanahawa na Chausiku wakabaki sebuleni kwa muda mfupi kisha kila mmoja akatokomea chumbani kwake.



    Chausiku alipoingia chumbani tu alimuuliza mumewe, “Vipi sweet, mbona leo mapema?”



    “Uchovu tu,” mzee Kisu Makalikuwili alijibu huku kajilaza chali kitandani, macho kayafumba kama aliyetopea usingizini.



    “Lakini kumbuka tuna miaka mitatu sasa,” Chausiku alisema. “Tuna miaka mitatu, na hatuna mtoto. Inabidi tujitahidi.”



    Mzee Kisu Makalikuwili alimsikia, akamwelewa. Lakini hakuwa timamu kisaikolojia siku hiyo. Alifumbua macho na kumtazama kidogo mkewe kisha akayafumba tena.



    “Umeyadharau niliyokwambia, eti?” Chausiku alimuuliza.



    “Sijayadharau maneno yako,” Mzee Kisu Makalikuwili aliyafumbua macho tena na kumtazama Chausiku sawia. “Nimekuelewa. Lakini kwa leo, acha nipumzike.”



    Chausiku ambaye wakati huo alikuwa amejitanda kanga moja tu bila hata ya nguo nyingine huko ndani, alisema, “Ok, nakuacha upumzike.” Akasonya na kupanda kitandani.



    Dakika takriban kumi zilikatika huku wakiwa wamelala katika kitanda chao kikubwa na cha kifahari kupindukia. Hatimaye waziri Kisu Makalikuwili akaanza kukoroma. Chausiku akamtazama kwa hasira kupitia mwangaza hafifu wa taa iliyomulika humo chumbani.



    Kwa mara nyingine akasonya. Akalitazama dari kwa jicho kali, kisha taratibu akajitoa kitandani kwa kunyata.



    **********



    WAKATI usiku ukiwa ni mtulivu, jumba zima la Kisu Makalikuwili likiwa kimya, mlango wa chumba cha Masumbuko uligongwa taratibu. Masumbuko aliusikia na akaelewa. Akajitoa kitandani taratibu na kuufungua. Chausiku akajitoma ndani!



    Ujio huu wa Chausiku chumbani humo haukumshangaza Masumbuko. Hii haikuwa mara ya kwanza kwa Chausiku kuja nyakati kama hizo. Alishakuja mara nyingi, na kilichomleta ni kile alichomwambia Masumbuko siku ya kwanza ya ajira yake; kumpa penzi.



    Ndiyo, halikuwa ni jambo la kumshangaza Masumbuko, lakini kwa siku hii na usiku huu lilimshtua na kumtisha. Iweje huyu mwanamke amjie wakati huu ambao mumewe yupo? Hii siyo kumhatarishia uhai wake?



    Akaduwaa na kubaki akimkodolea macho Chausiku. Akiwa bado

    katika hali hiyo, Chausiku akamvamia na kumkumbatia, kisha akambusu shavuni. “Nimeliacha limelala. Tufanye haraka mpenzi,” alimwambia Masumbuko huku bado akiwa amemng'ang'ania.



    Masumbuko alijitutumua, akamsukuma. Akamuuliza, “Mama, huoni kuwa hii ni hatari?!”



    “Acha utoto Masumbuko!” Chausiku alimkunjia uso. “Mimi nd'o namjua yule. Akilala, amelala. Zinduka yake ya kwanza ni baada ya saa nzima.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Masumbuko alishusha pumzi ndefu na kubaki akimtazama Chausiku. Chausiku, ambaye sasa alizidisha uchokozi. Zaidi ya kumkumbatia, aliipitisha mikono kifuani kwa Masumbuko na mkono mmoja ukashuka chini zaidi ambako ulipenyezwa ndani ya bukta kisha ukaanza kutalii kwa namna ya kipekee.



    Kama kuna mtu ambaye Masumbuko alimchukulia kama mtaalamu wa michezo ya mapenzi basi ni huyu Chausiku. Japo alikuwa na mwili mkubwa na akiwa na uvivu wa kiwango fulani kitandani, hata hivyo alijua 'kumtayarisha' mwanamume. Kwa hilo Masumbuko alimvulia kofia.



    Chausiku alijua kuitumia mikono yake kupita kila yalipohifadhiwa mashetani ya mwanamume rijali. Na hakuwa na hiyana kuutumia ulimi wake kunyonya sehemu yoyote ya mwili wa mwanamume aliyemwingia moyoni.



    Ni kutokana na uwezo wake huo wa kuchezea mwili wa mwanamume, Masumbuko hakuwahi kujisikia kukinaishwa naye. Tangu alipoanza kufanya ngono na Happy huko Nzega, hakuwahi kutembezewa ulimi kutoka kwenye paji la uso hadi nyayoni, ulimi huo ukilamba na kunyonya popote palipostahili kulambwa na kunyonywa.



    Kabla Happy hajaondoka kwenda Marekani walifanya mapenzi zaidi ya mara kumi. Siku nyingine walikuwa wakitumia hata zaidi ya saa nzima wakiwa katika starehe hiyo. Lakini Happy hakuwa na cha ziada, zaidi ya kuchojoa nguo na kumkaribisha Masumbuko katikati ya miguu yake kisha akatulia kama maji mtungini, akimwacha Masumbuko ahangaike kivyake.



    Happy alikuwa ni mzuri sana kwa sura na umbile, lakini hakujua kuvitumia vidole vyake na kinywa chake hususan ulimi kama huyu Chausiku, mke wa waziri.



    Dosari pekee aliyokuwa nayo Chausiku ni ile ambayo pia Happy alikuwa nayo. Uzito. Ndiyo, alikuwa mzito wakati wa kile kipindi maalumu. Hakuweza kuvishughulisha vilivyo viungo vyake isipokuwa tu kulialia na kubwatabwata kwa sauti iliyotoka kwa taabu, akimsifia Masumbuko katika utendaji na kukisifia kila kiungo cha Masumbuko.



    Kwa hapo ndipo alipotofautiana na mdogo wake, Mwanahawa ambaye hakujua au hakuwa na muda wa kuchelewa kwa kumwandaa mwanamume, lakini alijua kumpokea na kumridhisha vilivyo pindi alipomkaribisha katikati ya miguu yake. Alikuwa mwepesi, alikuwa mjuzi wa 'miondoko' na alijaaliwa pumzi.



    Kwa kipindi hiki kifupi ambacho Chausiku alikuwa amemdhibiti Masumbuko kilitosha kuulegeza msimamo wa Masumbuko kwa asilimia tisini na tano. Fikra za kuyahatarisha maisha yake zikatoweka pale Chausiku alipomchojoa ile bukta na kuanza kuutembeza ulimi wake wa moto chini ya kitovu.



    Masumbuko hakustahimili, alijikuta akiangukia kitanda, Chausiku akamfuatia na kuendelea kuutumia ulimi huo kwa namna iliyomtia wazimu wa aina yake Masumbuko. Mwanamke akawa anahema kwa nguvu huku akishuka taratibu kutoka kitovuni na kugota pale alipopakusudia. Sasa akawa kama aliyepagawa, akigugumia kwa nguvu, akionekana kama anayetaka kutamka neno fulani lakini asiweze, akawa ameng’angania, mkono ukiwa umeshika na kinywa kikibugia.



    Masumbuko akachanganyikiwa, akawa akikunja uso na kuukunjua kwa maumivu yenye raha. Akazisukasuka nywele nyingi na timtimu za Chausika na kuzidi kukikumbatia kichwa chake akihimiza kuendelezwa hicho alichokuwa akifanyiwa.



    Naam, hatimaye kikafikia kipindi ambacho Masumbuko alianza kuitetea ajira yake, kitanda kikawalaki kwa shangwe na kuuhimili mshikemshike uliozuka.



    **********



    MAPENZI kati ya Chausiku na mfanyakazi wake, Masumbuko yalipamba moto siku hadi siku. Ingekuwa siri, lakini haikuwa. Mwanahawa alijua mapema kuwa kuna zaidi ya ajira ya kulisha mifugo kwa Masumbuko.



    Ndiyo, alilibaini hilo siku moja alipotaka kuingia chumbani kwa Masumbuko usiku saa 6 lakini akasita baada ya kusikia miguno na minong'ono isiyo ya kawaida kutoka huko chumbani. Mlango ulikuwa umefungwa, hivyo alichungulia kwenye tundu la kitasa na kubahatika kushuhudia kila kilichokuwa kikiendelea humo ndani.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Aliwaona viumbe wawili wakiwa tupu kama walivyozaliwa, kitandani wakifanya waliyokuwa wakiyafanya. Zaidi, aliweza kuziona hata sura zao kwa usahihi! Mmoja alikuwa ni Masumbuko na mwingine alikuwa dada yake tumbo moja, Chausiku!



    Japo Mwanahawa alijua, lakini hakuwahi kuitoa siri hiyo, na wala hakutaka Chausiku ajue kuwa anajua. Hata hivyo, hiyo haikuwa sababu ya kuifanya siri hiyo iliyohifadhiwa katika kuta za jumba hilo isitoke nje na hatimaye kuyafikia masikio ya wasiohusika na macho ya wasiopitwa na jambo.



    Siku moja Masumbuko alitoka na Chausiku, wakaenda eneo la Tegeta na kukaa katika baa moja maarufu. Hapo walijipatia vinywaji kwa muda mrefu. Hatimaye wakachangamka. Wakajisikia huru kufanya chochote katika uhuru wao.



    Ni katika uhuru wao huo, walifikia hatua ya kukumbatiana na kupigana busu bila ya kujali macho ya wambeya wachache waliokuwa katika eneo hilo.



    Waliowaona hususan wale waliomfahamu Chausiku walishangaa.



    “Yule si ni mke wa Waziri Kisu Makalikuwili?” mmoja alimuuliza mwenzake.



    “Ni mwenyewe!”



    “Kumbe hajatulia! Cheki anayofanya na yule bwa'mdogo.”



    Wengi waliwaona, wengi wakawashangaa. Na ni vituko vyao hivyo vilivyowafanya wale walioshuhudia wasimulie kwa wengine mitaani.



    Huo ukawa mwanzo wa tetesi hizo kuzagaa. Hatimaye habari hizo zikamfikia waziri Kisu Makalikuwili. Naye hakuzichukulia kama uzushi, hapana. Alitulia akazifanyia kazi taratibu.



    Usiku huu aliorejea kutoka ng'ambo ya nchi, alikuwa amepokea tena taarifa hizo za ajabu kuhusu mkewe. Na hata alipoamua kulala, mawazo yake yote yalikuwa juu ya taarifa hizo. Na wakati alipofumba macho akikoroma mithili ya mtu aliyetopea usingizini, ndipo alipomwona mkewe akitoka taratibu chumbani.



    Ni hapo ndipo alipoanza kuziamini zile taarifa alizozipata. Naye akajitoa kitandani taratibu, akaifungua saraka moja ya kabati. Akaitoa bastola kisha akaanza kumfuata mkewe kinyemela.



    Hakuyaamini macho yake pale alipomshuhudia mkewe, Chausiku akiingia ndani ya chumba cha mfanyakazi wao, Masumbuko.

    Masumbuko! Kisu Makalikuwili aliwaza kwa hasira.



    *****MAMBO YAMEKUWA MAMBO! WAZIRI KALISHTUKIA DILI. NI KIPI KITAKACHOTOKEA HUKO CHUMBANI KWA MASUMBUKO?



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog