Search This Blog

Monday, October 24, 2022

JICHO LA KAMORE - 3

 





    Chombezo : Jicho La Kamore

    Sehemu Ya Tatu (3)



    “Dada umeanza masikhara yako,” Suzana alisema. “Awe fisadi wa EPA, awe ni muuza ‘unga’, au hata awe ni jambazi sisi havituhusu. Muhimu ni kumlia vyake shosti.”



    “Ni kweli,” Martha aliafiki. “ Na sasa usimlee. Mwambie akununulie nyumba...”



    “Nyumba!” Suzana aliachia kinywa wazi.



    “Ndio,” Martha alisisitiza. “Akununulie nyumba au akupe milioni mbili, tatu hivi. Hapo, uongo, hutakosa kibanda kwenye mapori ya Mbagala, na hasa kwa kuzingatia kuwa siku hizi watu wengine wanapachukulia Mbagala kama eneo maalum la kuhifadhia mabomu ambayo huenda yakalipuka siku yoyote.”



    “Dada na maneno yako,” Suzana alisema huku akiachia tabasamu la mbali.



    “Ni kweli mdogo wangu! Mbagala ya leo sio ya jana. Yale mabomu yamewatia hofu wenye mioyo myepesi, na kwa hali hiyo hawataki tena kuchukua viwanja huko.”



    Ukimya ukatawala kwa muda. Kisha Suzana akahoji, “Lakini dada milioni mbili au tatu mbona ni nyingi sana? Hatanishtukia?”



    “Akishtuka, achana nae,” Martha alisisitiza. “Kuna wanaume milioni nyingi tu hapa Dar na wana pesa zao zisizo za mafungu, wanawatafuta wa kuzitumia. Nakwambia usimchekee! Akijitia kushtuka unamwaga tu! Akafie mbele!”



    “Ok, nitajaribu.”



    *****



    JAPO Suzana alionyesha kutatizwa na pendekezo la Martha, hata hivyo dakika chache baada ya kuachana alilitafakari kwa makini pendekezo hilo na kugundua kuwa hakukuwa na kazi ngumu mbele yake. Alijiamini!



    Akiwa yu mkamilifu wa kila idara maungoni mwake, Suzana hakukiona kikwazo kitakachomfanya Kamore asite kumpa kitita kizito cha pesa. Hata kama hatakuwa nazo, atazisaka, apende, asipende, alisema kimoyomoyo. Kitu kimoja kilimtia kiburi cha mafanikio ya suala hilo. Mwili wake! Aliamini kuwa pumzi zake, utaalamu pamoja na utundu aliojaaliwa ni vigezo vitakavyomfanya Kamore asalimu amri baada ya kupewa zawadi ambayo amekuwa akiililia mithili ya mtoto aliliavyo titi la mama.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alikuwa na kumbukumbu ya wanaume wawili ambao walimfanya ajiweke katika daraja la kwanza siku alipodiriki kustarehe nao, kila mmoja kwa siku yake.



    Kuna mmoja, pandikizi la mtu, ambaye aliwahi kufanya kazi ya ulinzi milangoni katika kumbi za burudani. Huyo 'baunsa,' na 'ubaunsa' wake alilazimika kubwaga manyanga siku walipojichimbia gesti. Aliiinua mikono katikati ya dimba, Suzana akaachwa na kiu yake!



    Mwingine alikuwa ni mwanamuziki wa bendi moja ya Kikongo yenye maskani yake jijini Dar es Salaam. Huyo alijitahidi kidogo, Suzana akaburudika kidogo. Lakini ili adhihirishe kuwa yu mrembo hadharani na fundi chumbani, hakumruhusu Mkongo huyo avae nguo zake kwa kujidai. Hapana. Alihakikisha anautumia hata ule ujuzi wake wa ziada, Mkongo wa watu akajikuta 'akinena kwa lugha.'



    Kumbukumbu hiyo ilimfanya Suzana acheke kimoyomoyo pale alipokumbuka kuwa siku ya pili Mkongo huyo aliandamana naye hadi kwa mkurugenzi wa bendi ambako alimtambulisha rasmi kuwa ndiye Mama Watoto na kuomba mkopo wa pesa kwa madai ya kumpeleka mama mkwe hospitali. Mkurugenzi alipomhoji ni kiasi gani cha mkopo aliohitaji, Mkongo akatamka kuwa ni shilingi 200,000. Dakika iliyofuata pesa hizo zikawa katika himaya ya Mkongo, na dakika kama kumi baadaye, wakiwa wameshatoka kwa mkurugenzi, pesa zote hizo zikahamia kwa Suzana.



    Ajabu! Kazi ndogo tu ya saa moja hivi, ndani ya chumba cha gesti fulani ikamwingizia Suzana kitita cha shilingi 200,000! Itakuwa Kamore!



    Kwa ujumla alimchukulia Kamore kama vile kumsukuma mlevi aliyechuchumaa. Dawa ni ileile, kiuno chake! Kwa hilo alijiamini. Mwili wake ni ngao aliyoitegemea, utundu wake kitandani ukiwa ni silaha aliyoiamini. Kipi kimshinde?



    Pendekezo la Martha, la kumtaka amwambie Kamore kuwa amnunulie nyumba au kumnunulia kiwanja na kumkabidhi pesa za ujenzi lilipaswa kufanyiwa kazi kwa utaratibu mzuri na kwa umakini wa hali ya juu. Siyo kwa pupa au shinikizo.



    Hivyo, jioni ya siku hiyo, Kamore alipofika kwa Suzana alipokelewa kwa namna ya kipekee. Hakuruhusiwa kufikia sofani kama ilivyokuwa ada. Mikono ya Suzana ilimdaka. Mikono hiyo laini, yenye joto linalosisimua, ilimpapasa usoni kabla hajavutwa na kupigwa busu la kinywani, busu lililodumu kwa takriban dakika nzima kabla Suzana hajamkokota hadi kitandani ambako alimfanyia yale ambayo Kamore alishayazoea; kutomaswa huku kupapaswa hapa, kunyonywa kule na kadhalika na kadhalika.



    Yalikuwa ni mateso yaburudishayo, lakini siku hii Suzana alizidisha utundu kiasi cha kuiduwaza akili ya Kamore. Na aliendelea kuduwaa hata pale Suzana alipochojoa nguo zote na kumrushia mpira wa kiume, akidhihirisha kuwa yu tayari kwa lolote. Haikumwingia akilini Kamore kuwa hayo yanayotokea ni hali halisi.



    Hapana, alihisi yu ndotoni. Ndiyo, kwa sekunde chache alihisi yu ndotoni au alimwona Suzana akiigiza tamthilia ya mapenzi. Mshangao wa Kamore uliongezeka, pale Suzana alipomfuata na kumchojoa nguo huku akimnong'oneza, “Leo ni siku yako mpenzi...Nifanye utakavyo...chukua chochote katika mwili huu...niko tayari kwa lolote...”



    Haikuwa rahisi kwa Kamore kuyaamini masikio yake. Sasa walikuwa na zaidi ya mwezi, tangu kila mmoja wao alipoanza kumwita mwenzie, 'mpenzi.' Katika kipindi chote hicho, Suzana alikuwa mgumu, tena 'chuma cha reli.' Hakuwa tayari kufanya mapenzi kikamilifu zaidi ya kuchezeana tu maungoni. Lakini jioni hii, alikuwa tofauti na siku takriban arobaini zilizopita. Leo alikuwa mtupu kama alivyozaliwa, akionesha bayana kuwa yu tayari kwa lolote!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kamore alijihisi yu ndotoni. Ndiyo, kwa sekunde chache alihisi yu ndotoni au anaigiza tamthilia ya mapenzi. Lakini ndoto hiyo au tamthilia hiyo haikudumu hata kwa sekunde kumi, ilitoweka kama ilivyoingia. Sasa akajua ni kipi kinachoendelea. Siyo ndoto wala tamthilia. Papohapo akamvuta Suzana na kumkumbatia.



    Ikafuata hatua nyingine.



    *****



    NI njaa iliyowazindua. Ilikuwa ni saa 2:30 usiku. Zaidi ya saa moja walikuwa wamejifungia chumbani humo, wakifanya kila waliloliweza, na kila walilolijua katika kuzikonga nyoyo zao. Suzana alijua ni kipi cha kumfanyia mtu wa aina ya Kamore. Hivyo, nyenzo zake kuu zikiwa ni nguvu na ujuzi, pale tu walipokiangukia kitanda alifanya mengi ambayo Kamore hakukumbuka ni mwanamke gani mwingine aliyewahi kuyafanya. Japo hakuwa na idadi kamili ya wanawake waliokwishamchojolea nguo, hata hivyo aliamini kuwa huyu Suzana ni zaidi ya wengi.



    Zaidi ya wote!



    “Naamini sikukosea kukupenda, Suzy,” lilimtoka Kamore huku akimtazama Suzana kwa macho ya kumtukuza. “Leo nd'o nimegundua kuwa u mzuri zaidi ya wazuri. Wewe sio binadamu wa kawaida. Huenda kuna makosa fulani yaliyotendeka mbinguni, na makosa hayo yakasababisha uzaliwe hapa duniani, dunia yenye kila aina ya uozo. Ulistahili uwe miongoni mwa jopo la malaika wa Mungu, Suzy.”



    Yalikuwa ni maneno yaleyale ambayo Suzana alishayasikia mara nyingi, maneno ambayo kwa kiasi kikubwa huyachukulia kuwa ni unafiki mtupu. Unafiki wa wanaume. Alishachoka kuyasikia. Lakini kwa siku hii, na usiku huu, alijenga imani kuwa kuna asilimia zisizopungua tisini za ukweli katika maneno haya ya Kamore. Hili lilidhihirika katika maneno na macho yake.



    Ndipo Suzana alipokumbuka kuwa huu ulikuwa ni muda mwafaka wa kutekeleza lile alilokubaliana na Martha. Akitumia mpangilio mzuri wa sentensi, alimweleza Kamore juu ya ama kununuliwa nyumba ama kiwanja ama fedha taslimu za kutosha kutekeleza moja kati ya hayo.



    Kwa muda mfupi kimya kilitawala, Kamore akilitafakari ombi hilo. Lilikuwa ni ombi zito ambalo hakulitegemea. Afanye nini? Atamke bayana kuwa hana uwezo huo? Hapana. Hakukubaliana na hilo. Kumtamkia kiumbe wa aina hii, msichana mrembo, mwenye kila sifa zinazomstahili mwanamke mzuri, kwamba hana uwezo wa kulitekeleza ombi lake, aliona kuwa ni zaidi ya kujidhalilisha.



    Angeishusha hadhi ya uwanaume wake. Na akiwa ni mwanamume aliyehitaji kila mwanamke autukuze uwanaume wake, uwanaume wa hadharani na sirini, hakuwa radhi huyu Suzana awe mwanamke wa kwanza kumdharau.



    Japo alikuwa na hakika kuwa kwa usiku huo, kesho au hata keshokutwa asingeweza kulitekeleza ombi hili, hata hivyo alikuwa na imani kuwa uwezekano wa kupatikana kitu kama shilingi milioni tatu au nne ulikuwepo. Ni kwa kuamini hivyo, ujasiri ukamjia na kujikuta akimtupia swali Suzana: “Ni eneo gani unalolipenda?”



    “Mbagala.”



    “Mbagala ipi?”



    “Maji Matitu.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kamore alifikiri kidogo na kuona kuwa, kuanza kutafuta nyumba au kiwanja ni kazi kubwa japo inawezekana. Nafasi ya kufanya kazi hiyo ilikuwa haba. Hivyo, aliamua kuzitafuta pesa na kumkabidhi Suzana ili achague mwenyewe lipi afanye kati ya hayo.

    Aliamini kuwa utaratibu huo utakuwa mzuri kwani utampa uhuru Suzana, uhuru wa kuchagua kiwanja katika eneo atakalolipenda au kununua nyumba yenye ubora utakaomridhisha.



    “Nitakutafutia pesa, mpenzi,” alimwambia. “Kwa huko Mbagala milioni tatu si zitatosha?”



    “Zinatosha,” Suzana alijibu kwa unyonge japo moyoni aliachia kicheko kikali.



    “Ok, ni suala dogo sana hilo.”



    “Kwa hiyo nitegemee lini?”



    “Nipe siku mbili, tatu hivi.”



    Suzana alimtazama Kamore kwa macho yaliyozungumza mapenzi. Akambusu kwenye paji la uso, kisha akampapasa mahala fulani, upapasaji uliomfanya Kamore atoe mguno hafifu na kushusha pumzi ndefu.



    Wakakumbatiana.



    *****



    UNUNUZI wa kiwanja cha ujenzi wa nyumba au kununua nyumba iliyokamilika, vyote huhitaji pesa nyingi. Kwa jiji la Dar es Salaam, takriban kila kitu hugharimu pesa ambazo kiwango chake huwa juu ukilinganisha na mikoa mingine. Kamore alilitambua hilo fika, hivyo ikamlazimu kufikiri kwa kina jinsi ya kuishughulikia ahadi aliyoitoa kwa Suzana. Hakupenda kujidanganya kuwa kiasi cha pesa alizozitaka Suzana ni kidogo. Hapana, ni pesa nyingi.



    Japo mara kwa mara, kwa kutumia kalamu yake alifanikiwa kupata pesa za ziada, nyingi, hata hivyo haikuwahi kutokea hata mara moja akajipatia shilingi milioni moja kwa mkupuo. Pesa alizozipata ziliwahusisha pia Meneja Utumishi na Meneja Masoko, na mgawo wa pesa hizo ukiwa haumpendelei yeyote kati yao kwa viwango. Waswahili husema waligawana “sawa kwa sawa.” Lakini hili suala la Suzana lilihitaji zaidi ya shilingi milioni moja.



    Zaidi ya milioni mbili!



    Ni milioni tatu!



    Hapo akalazimika kuusumbua ubongo maradufu, akifikiri njia nzuri ya kulipatia ufumbuzi suala hilo haraka iwezekanavyo. Ndipo alipomkumbuka Samba, rafikiye waliyesoma pamoja sekondari huko Marangu. Kwa sasa Samba naye alikuwa akiishi jijini Dar es Salaam, akijishughulisha na kazi hii na ile, mradi mkono uende kinywani. Na huu ulikuwa ni mwezi wa tatu hawajaonana. Lakini hilo halikuwa tatizo, alijua jinsi ya kumpata.



    Siku iliyofuata, akiwa ofisini, alimpigia simu na wakakubaliana kuonana saa 10 jioni, Magomeni Mapipa kwenye kijibaa fulani kisichokuwa na wateja wengi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Maisha ya Samba yalikuwa ya kupata pesa bila utaratibu maalumu au ulio wazi. Yalikuwa ni maisha yenye mfumo mgumu kiasi cha kuyafanya makali yake yadhihirike kutokana na mavazi pamoja na afya yake. Makali hayo ya maisha yalimfanya hata ashindwe kupanga chumba. Bado alikuwa akiishi kwa mjomba wake, Mabibo. Ilikuwa ni kila kukicha anaingia mitaa ya katikati ya jiji ambako alifanya mipango ya kupata pesa kwa ule mfumo unaoitwa 'mishen-tauni.'



    Yalikuwa ni maisha ya kubahatisha, na hata Kamore alitambua kuwa Samba mwenyewe hakuyapenda. Aliamini kuwa kumhusisha katika mpango huo ingekuwa ni njia mojawapo ya kumkwamua na kujikuta akipiga hatua moja mbele kuelekea mafanikio maishani.



    Na akilini mwa Kamore aliamini kuwa, mbele ya mpango mzuri utakaompatia pesa nyingi, Samba asingeweza kufikiri kama ni vema kushiriki au la. Hiyo ni moja.

    Pili, alilazimika kumtumia Samba kutokana na uzito wa uhusiano wao. Huu ulikuwa ni mpango mzito, mpango uliopaswa kumshirikisha mtu wa karibu sana, mtu atakayeweza kuitunza siri kwa gharama yoyote ile.



    Kwa sababu hii ya pili, kwa vyovyote vile mtu pekee aliyestahili kushirikishwa alikuwa ni Samba. Vinginevyo, labda awe ni mdogowe wa kiume au mkewe, kama angekuwa ameoa. Lakini hakuwa na mke wala hakuwa na mdogo wa kiume. Alikuwa ni mziwanda, nduguze wanne wa juu walikuwa wa kike na watatu kati yao walikuwa wameolewa na waliishi huko Marangu huku yule mmoja, wa nne kuzaliwa alikuwa nje ya jiji la Dar es Salaam. Yeye alikuwa wa tano kuzaliwa.



    Kamore hakutaka hawa nduguze wa kike wautambue mpango huo. Hakuwa na sababu nzito ya kutotaka wajue; basi tu. Kichwani mwake hakuamini kuwa kumshirikisha ndugu wa kike au hawara katika suala zito la pesa, tena suala lenyewe liwe la mbinu zisizo halali, utakuwa ni mwanzo mzuri wa mafanikio. Hapana.

    Aliamini kuwa kuwashirikisha watu wa aina hiyo, matokeo yake yatakuwa mabaya, iwe leo, iwe kesho, mwezi ujao hata mwaka ujao. Ndiyo maana kamfuata Samba. Na hakutaka wazungumzie hapo nyumbani.



    “Tunaweza kutoka?”



    “Poa tu,” Samba alijibu. “Nilikuwa hata sina pa kwenda, na hapa ghetto pa'shanichosha.”



    “Ok, twende hapo mtaa wa pili. Kwani u'shaacha bia?”



    Samba alicheka. “Ni kukosa pesa tu, mwanangu. Jiji hili ni chungu ka' nini! Kila ishu inagusa pesa. Na huu mtikisiko wa uchumi duniani sijui nd'o unachangia kutulostisha? Pesa ya bia itatoka wapi?”



    “Kuna baa gani hapa jirani?”



    “Siyo mbali, ni hapo mtaa wa pili.”



    “Poa, twen'zetu.”



    Dakika chache baadaye walikuwa mtaa wa pili, wakaingia katika baa moja ambayo haikuwa na watu wengi. Kamore aliyahitaji mazingira ya aina hiyo kwa wakati huo; sehemu isiyokuwa na kelele ghasia zinazoweza kumwathiri kisaikolojia katika maongezi yao.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakachagua meza iliyokuwa tupu na ikiwa pia iko mbali na meza zenye wateja wengine. Ni wakati wakimsubiri mhudumu awahudumiie vinywaji, ndipo Kamore alipoamua kupasua jipu. “Nakuhitaji kwa suala moja nyeti lakini lenye faida kwetu wote,” Kamore alisema. “Kwa ujanja wako na elimu yako, nadhani haitakuwa kazi ngumu kwako.”



    “Ni kazi gani hiyo?” Samba alihoji huku akimtazama kwa macho makali.



    “Siyo kazi kubwa,” Kamore alijibu kwa sauti ya chini na kusita. Mhudumu alikuwa mbele yao akiviweka mezani vinywaji walivyomwagiza.



    Walipobaki peke yao, Kamore alinong'ona, “Nataka risiti.”



    “Risiti?!”



    “Yeah, nataka risiti,” Kamore aliiendeleza sauti yake ya chini lakini safari hii akionyesha kuwa anasisitiza. Akachomoa kijikaratasi kidogo kwenye mfuko wa shati na kumpatia Samba. “Nataka risiti kama hii.”



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog