Chombezo : Facebook Chatting
Sehemu Ya Pili
(2)
Leo hii, vita vya
chini chini vimeanza, vita ambavyo sitotaka kuwaambia marafiki zangu mpaka pale
ambapo ningekamilisha ‘mission’ yangu na kuwa naye. Hebu jifikirie kwanza,
Dorcas angetoka vipi? Angeweza kuanzia wapi kunikataa na wakati nilikuwa na
maneno mengi ya kuandika? Sikuona angetokea wapi, ila kama atanikubali, siku ya
kuonana sijui ingekuwaje kama atagundua kwamba ni mimi atafanyaje? Ila hiyo siyo
ishu, ishu kubwa ni kumfanya aangukie kimapenzi kwenye mikono yangu iliyo salama
juu ya maisha yake......thats all.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
MIMI: (Nikalog out
na kulala huku nikisubiri kesho nianze pale
nilipoishia)
Siku iliyofuata, nakumbuka kabisa
sikuwa na fedha kwenye line yangu ambayo nilikuwa naitumia sana kuunganisha na
huduma ya internet. Siku hiyo nilikaa katika hali ya unyonge kupita kawaida,
akili yangu ilikuwa ikimfikiria Dorcas tu. Sikujua ningepata vipi fedha ya
kujiunga na internet kwani muda wa kifurushi nilichokuwa nimenunua muda wa
kujiunga, ulikuwa umemalizika jana usiku.
Kwa sababu nilikuwa mjanja
nikaanza kuwasiliana na baba, mzee Chilongani na kisha kumwambia kwamba nilikuwa
na shida ya kiasi cha shilingi elfu thelathini. Japokuwa alinihoji maswali
mengi, nilimjibu kisomi mpaka akanitumia kiasi hicho ambacho nikaamua kuchukua
kifurushi cha mwezi mzima cha Vodacom, sikutaka tena kupata usumbufu wa kutokuwa
na huduma ya internet katika harakati zangu za kumtia mikononi
Dorcas.
Nilijiunga na huduma ya mwezi mzima ya
Internet ya Vodacom na kisha kuanza kufungua akaunti facebook. Kwa wakati huo,
akili yangu ilikuwa ikifikiria maneno mengi matamu ambayo nilipaswa kumwambia
Dorcas katika kipindi ambacho ningemkuta online. Baada ya kufungua mtandao wa
facebook, nikaanza kuangalia listi ya marafiki zangu ambao walikuwa online,
walikuwa nane tu kwani kipindi hicho nilikuwa na marafiki 102
tu.
Kati ya watu ambao walikuwa online, Dorcas
hakuwepo kabisa, nilinyong’onyeaje. Ikabidi nizuge zuge na marafiki ambao
walikuwa online kwa wakati huo kwa kupiga stori mbili tatu. Nakumbuka ilipofika
saa 9:17 alasiri, Dorcas akaingia online. Kwanza nikashtuka sana, mapigo yangu
ya moyo yakaanza kudunda kwa kasi ya ajabu, sikutakiwa kuhofia chochote kile,
nikaamua kumpa hi.
MIMI: Mambo Dory! (Nilimsalimia
huku nikitoa tabasamu kana kwamba alikuwa akiniona).
DORCAS: Poa.
Mzima Brother?
MIMI: Nipo poa. Nimekusubiri sana
online.
DORCAS: Acha kunidanganya Brother.
MIMI:
Nikudanganye ili iweje? Kwani kunatolewa tuzo kwa atakayemdanganya
mwenzake?
DORCAS: Hahaha! Hujaacha tu maneno yako?
MIMI:
Maneno gani?
DORCAS: Si hayo hapo unayoongea.
MIMI: Mbona
yapo kawaida tu. Hebu acha nikuulize kitu kimoja. Uliniota jana
usiku?
DORCAS: Hapana.
MIMI: Dah! Kwa hiyo uliniacha nikuote
wewe tu bila kuniota?
DORCAS: kwani uliniota?
MIMI: Yeah!
Nilikuota sana. Nilikaa nawe sana tukipiga stori. Nilifurahi
sana.
DORCAS: Uliota tukipiga stori wapi? Humu
facebook?
MIMI: Hapana. Ulikuja nyumbani.
DORCAS:
Kwenu?
MIMI: Yeah!
DORCAS: Mmmh!
MIMI: Mbona
unaguna tena?
DORCAS: Siamini.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
MIMI: Huamini
nini?
DORCAS: Kama nilikuja kwenu.
MIMI: Je nikikwambia
kwamba ulikuja nyumbani na kuingia chumbani kwangu na kuanza kupiga stori
chumbani humo, utaamini?
DORCAS: Acha utani bwana.
MIMI:
Kweli tena. Halafu nikwambie kitu?
DORCAS: Niambie.
MIMI:
Asilimia mia moja za ndoto zangu huwa kweli.
DORCAS: Hahaha! Kwa hiyo
unamaanisha hata hiyo itakuwa kweli?
MIMI: Wewe
unaonaje?
DORCAS: Haitoweza kuwa kweli.
MIMI: Okey! Tufanye
haitoweza kuwa kweli. Ila ukiulizwa kama ungependa iwe kweli,
utakubali?
DORCAS: Inategemea.
MIMI: Inategemea na
nini?
DORCAS: (Kimyaa)
Dizaini nikaliona
swali langu ambalo nilimuuliza lilikuwa gumu kujibika, nilikuwa nikimuona
akilini akiwa anafikiria jibu la kunipa. Wala sikuwa na wasiwasi kabisa,
nilikuwa najiamini sana, hivyo nikakaa kimya na kuanza kumsikilizia angejibu
nini. Ghafla katika hali ambayo sikuitegemea, akatoka
online.
Nilionekana kuchukia sana, kwa nini Dorcas atoke online na
wakati alijua fika kwamba nilikuwa online kwa ajili yake, nilinyong’onyea sana.
Mara ghafla huku nikiwa simuoni online, nikashtukia napokea meseji kutoka
kwake.
DORCAS: Samahani Brother.
MIMI:
Samahani ya nini tena Dory?
DORCAS: Nilikuwa Intenet Cafe, nilichukua
nusu saa kwani kuna kitu nilikuwa namtumia kaka kwenye email yake, muda
uliniishia. Kwa sasa natumia simu yangu.
MIMI: Usijali. Upo wapi
now?
DORCAS: Nipo kwenye daladala naelekea nyumbani.
MIMI:
Take care njiani.
DORCAS: Usijali wangu. Nikifika home
nitakushtua.
Mimi: Poa.
Hiyo ndio hatua
ambayo ilikuwa ikiendelea. Kutoka kuitwa Brother mpaka kuanza kuitwa ‘wangu’.
Hapa ngoja nikwambie kitu. Kwangu mimi, hasa katika kipindi kile cha nyuma kabla
sijazoea, nilikuwa nikiona kuitwa ‘wangu’ lilikuwa jina moja ambalo lilikuwa
likinichanganya sana. Mtoto wa kike aniite ‘wangu’? Anamaanisha nini aisee? Kwa
nini niwe wake? Kila nilipojiuliza, nikabaki na mshangao wenye furaha moyoni
mwangu.
Siku hiyo sikutaka kutoka online. Japokuwa
nilitakiwa nionane na Rich Carter Jr saa kumi jioni lakini siku hiyo nikaamua
kumchunia. Nilichokifanya ni kuizima simu yangu. Katika kipindi hicho, Dorcas
alionekana kuwa muhimu sana kuliko Rich Carter Jr. Rafiki alikuwepo tu, hata
kama ningekataa kuonana naye siku hiyo wala asingekasirika sana kwa sababu yeye
yupo maishani mwangu.
Ila hali ilikuwa tofauti na Dorcas. Kama
angekuta kwamba sipo online au amenitumia meseji halafu imekaa muda mrefu bila
majibu ingekuwaje? Ningemkasirisha kitu ambacho sikutaka kitokee. Kwangu, hasa
kwa wakati huo, Dorcas alionekana kuwa kama yai au sahani ya udongo ambayo
ilitakiwa kushikwa kwa uangalifu mkubwa sana. Kama kawaida, mara baada ya kufika
nyumbani kwao, nikakuta meseji ikiingia kutoka kwake, kwa haraka haraka
nikaifungua.
DORCAS: Nimefika salama
wangu.
MIMI: Mungu amejibu maombi yangu.
DORCAS: Maombi gani
tena?
MIMI: Nilikuwa namuomba akulinde njia nzima.
DORCAS:
Kwa hiyo wewe mwanamaombi siku hizi?
MIMI: Yeah! Halafu dizaini kama
Mungu anajibu kila ombi ninaloomba.
DORCAS: Ahahaha! Kwani
ulikwishawahi kumuomba maombi gani ambayo aliwahi kukujibu?
MIMI: Kuna
siku nilipiga goti na kumuomba kwamba anipe bahati ya kuchati na msichana mzuri.
Jana amenipa.
DORCAS: Hahahaha! Msichana gani huyo
nimjue?
MIMI: Wewe.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
DORCAS:
Hahahaha!
MIMI: Unanicheka?
DORCAS: Hapana wangu. Nimefurahi
tu. Endelea kuomba tu.
MIMI: Yeah! Jana nilipiga tena
goti.
DORCAS: Uliomba nini?
MIMI: Niweze kukutana na huyu
msichana niliyeanza kuchati naye jana. Ila kwanza kabla ya kukutana tuwe
wapenzi.
DORCAS: Una utani sana Brother.
MIMI: Kweli tena.
Namsubiria ajibu maombi yangu. Natumaini atajibu hivi soon.
DORCAS:
Ombi lako hilo bila kufunga na kuomba sijui kama litajibiwa.
MIMI: Kwa
nini?
DORCAS: Ni ombi moja ambalo linahitajika kuwa na nguvu
sana.
MIMI: Litafanikiwa tu. Au wewe hauamini hilo?
DORCAS:
(Kimyaa)
MIMI: Swali gumu?
DORCAS: Hapana. Omba
sana.
MIMI: Nikuulize swali?
DORCAS: Uliza.
MIMI:
Unanipenda?
DORCAS: Kama rafiki wa facebook tu.
MIMI: Hebu
chukua sekunde kumi za kuzungumza na moyo wako juu yangu.
DORCAS:
Hata nikichukua dakika kumi, bado wewe ni rafiki yangu tu.
MIMI:
Nikwambie kitu Dorcas.
DORCAS: Niambie.
MIMI: Ukweli ni
kwamba unanipenda. Nadanganya?
DORCAS: Hahaha!
MIMI:
Nimekwishazungumza na moyo wako. Unaonekana kuwa mnyonge sana, moyo wako
ulihitaji furaha ya kipindi kirefu sana, unayapenda sana mapenzi japokuwa wakati
mwingine unaona kwamba mapenzi hayakupenda, labda umekata tamaa na kujiona
kwamba una bahati mbaya sana katika masuala yote ya mahusiano. Labda umelia
sana, au umehuzunika sana moyoni mwako kwa sababu ya mapenzi. Moyo wako nauona
una kidonda kikubwa sana, kidonda ambacho hauamini kama kuna siku kitakuja
kupona. Ngoja nikwambie kitu leo, mimi ndiye ambaye nitakuwa dawa kubwa sana ya
kukiponyesha kidonda chako moyoni, kidonda ambacho kinaweza kuoza na kuuharibu
moyo wako wote. Nitakuwa na uwezo wa kuja na kufanya kazi kubwa ya kukurudishia
furaha yako iliyopotea......ila yote yatawezekana kama utafanya kitu kimoja
tu.
DORCAS: Kitu gani?
MIMI: Kunipa ruhusa ya kuingia moyoni
mwako na kuufungua ukurasa mpya wa kimapenzi. Tunaweza kuufungua
sasa?
DORCAS: Naogopa.
MIMI: Unaogopa
nini?
DORCAS: Utaendelea kuumiza.
MIMI:
Unaniamini?
DORCAS: Nakuamini.
MIMI: Basi fanya kama
nilivyokwambia. Niruhusu sasa.
DORCAS (Kimyaa)
MIMI:
Dorcas.
DORCAS: Abee.
MIMI: Nakupenda
sana.
DORCAS: Nafahamu sana. Najua kwamba unanipenda sana. Kila siku
umekuwa ukiniambia neno hilo. Nakumbuka ulikuwa ukikaa sana uchochoroni kwa
ajili yangu, wakati mwingine ukinisindikiza shuleni na hata dukani na kuniambia
kwamba unanipenda. Nilikuwa nikikufikiria sana, sikuamini kama kweli ulikuwa
ukinipenda ila mpaka nilipohama Tandale ndipo nilipoamini kwamba unanipenda.
Yaani ilikuwa ni sawa na kitu ambacho unacho, huwezi kukiona thamani yake mpaka
unapokipoteza. Najua unanipenda Nyemo, najua unanihitaji sana.
MIMI:
(Kimyaa)
Kwanza nikashtuka, kumbe nilikuwa
nikizuga muda wote huo na wakati Dorcas alikuwa akijua kwamba mtu ambaye
nilikuwa nikijiita Brother Prince nilikuwa mimi. Moyo wangu ukaanza kujisikia
aibu, nilitamani niache kuchati naye muda huo huo. Nilijihukumu moyoni kwa kuona
kwamba inawezekana Dorcas alianza kuniona mimi malaya kwa kuwadandia wasichana
wa Facebook.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
DORCAS:
Nyemo.
MIMI: (Huku nikijisikia noma moyoni) Naam.
DORCAS:
nakupenda sana.
MIMI: Dah!
DORCAS: Nini
tena?
MIMI: Nikuulize kitu?
DORCAS:
Uliza.
Kwanza nikakaa kimya
kwa muda, kichwa changu hakikuwa kikionekana kuwa sawa kabisa katika muda huo.
Ni kweli kwamba nilikuwa nikitamani sana kuwa na Dorcas kwa sababu tu nilikuwa
nampenda sana tena toka kitambo, sasa swali ambalo lilikuja akilini mwangu kwa
wakati huo, ni kwa jinsi gani alikuwa amefahamu kwamba mimi nilikuwa Nyemo na
wakati nilitumia jina langu la A.K.A? Kila nilipojiuliza, nikakosa
jibu.
MIMI: Umejua vipi kama ni
mimi?
DORCAS: Nilikuwa na machale.
MIMI: Acha kunitania
Dorcas...machale gani hayo yaliyokufanya unitambue?
DORCAS: Si kwa
sababu ulikuwa unanipenda.
MIMI: Si kwamba nilikuwa. Nakupenda mpaka
sasa.
DORCAS: Nashukuru kusikia hivyo.
MIMI: Ila bado
haujanijibu Dorcas.
DORCAS: Hiyo ni kwa sababu natumia akaunti mbili.
Kuna kipindi nilikutumia meseji kwa kutumia akaunti yangu nyingine na kisha
kukutumia ombi la urafiki, ukanikubalia. Sasa uliponitumia urafiki kwa kutumia
akaunti hii, nikaona ‘matual friend’ akiwa mmoja. Nilipocheki, nikakuta ni
akaunti yangu nyingine. Kwanza nikashtuka, sikujua kama nilikwishawahi kuwa na
rafiki mwenye jina hilo. Nilipoangalia meseji za kule, nikagundua kwamba ni
wewe.
MIMI: Mmmh!
DORCAS: Nini tena?
MIMI: Wewe
mjanja sana.
DORCAS: Kawaida tu Nyemo.
MIMI: Sawa. Ila mbona
haujanijibu? Upo tayari?
DORCAS: Tayari nini?
MIMI: Kuwa na
mimi.
DORCAS: Mmmh! Unataka nipigwe tu.
MIMI: Na nani
tena?
DORCAS: Msichana wako.
MIMI: Yupi?
DORCAS:
Una marafiki wengi sana Nyemo, kuna wasichana wengine wanapenda sana kufuatilia
hadithi zako, sasa unafikiri watajisikiaje kama wakiona nipo na
wewe?
MIMI: Watajisikia kawaida kwani hawajawahi kuniambia kwamba
wananipenda.
DORCAS: Hahaha! Hapana bwana Nyemo. Kwa hiyo
wangekwambia?
MIMI: Ningekataa.
DORCAS: Kwa nini
sasa?
MIMI: Kwa sababu moyo wangu upo kwako.
DORCAS: Nyemo
unataka kunitafutia ugomvi bwana. Sipendi maneno maneno bwana. Nianze
kuzungumziwa sana kisa natoka na wewe. Wasichana sisi tuna mambo sana Nyemo.
Acha niwe peke yangu kwa sasa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
MIMI: Hicho ni kitu
ambacho sitaki kitokee. Najua kwamba inawezekana kuna msichana au wasichana
wanapenda kuwa na mimi, okey, hiyo ni hali ya kawaida kutokea facebook japokuwa
sitaki itokee kwa sababu napenda kufanya mambo yangu kwa uhuru facebook, lakini
watakwambia maneno gani na wakati uhusiano wangu ni kati yangu na wewe tu.
Usiwaogope bwana, wataongea sana mchana, usiku watalala tu.
DORCAS:
Ila kila siku nitakuwa nikiumia sana Nyemo.
MIMI:
Kivipi?
DORCAS; Mtu akitokea na kuanza kukuita ‘wangu, kipenzi,
sweetie’ na majina mengine kwenye comment, unafikiri
nitafurahia?
MIMI: Ni majina ya kawaida tu, labda uwe na wivu
kupitiliza.
DORCAS; Wivu ndio mapenzi Nyemo. Kama nisipojisikia wivu
kwako, hiyo inamaanisha sina mapenzi kwako. Ili nijulikane kama nina mapenzi,
wivu muhimu.
MIMI: Kumbe ndivyo ilivyo?
DORCAS:
Yeah!
MIMI: Sawa, nimekuelewa. Nipe jibu la uhakika sasa....upo
tayari?
DORCAS: Dah!
MIMI: Nini tena?
DORCAS:
Mambo magumu sana Nyemo. Nauonea huruma moyo wangu tu.
MIMI: Usijali.
Nitaujali na kuulinda.
DORCAS: Kabla sijakujibu naomba nikuulize swali
moja.
MIMI: Uliza tu.
DORCAS: Umekwishawatongoza wasichana
wangapi humu facebook?
MIMI: Mmoja tu. Wewe.
DORCAS: Hahaha!
Na umekwishawahi kutongozwa na wasichana wangapi humu facebook?
MIMI:
Hakuna hata mmoja.
DORCAS: Una rekodi ya kutongozwa na msichana yeyote
maishani mwako?
MIMI: Hapana.
DORCAS: kwa hiyo huwa
unatongoza wewe tu?
MIMI: Maswali yamekuwa mengi kweli
Dory.
DORCAS: Hahaha! Mbona unaonekana kulikimbia swali. Nijibu
kwanza.
MIMI: Kwa hiyo kisa nataka cha uvunguni, kwanza sharti
niiname?
DORCAS: Ndio.
MIMI: Sijazoea kutongoza. Huwa
najisikia aibu sana.
DORCAS: Sasa mbona mimi
umenitongoza.
MIMI: Sijakutongoza.
DORCAS: kumbe umefanya
nini hapo?
MIMI: Nimekukumbusha tu juu ya upendo ambao nilikuwa nao
juu yako toka zamani.
DORCAS: Hahaha! Wewe mwanaume mjanja sana. Yaani
unakwepa kwepa.
MIMI: Huo ndio ukweli. Upo tayari?
DORCAS:
Naomba unipe muda.
MIMI: Muda! Wa nini tena?
DORCAS:
Kujifikiria.
MIMI: Yaani hata ukumbusho wangu pia unahitaji
kufikiriwa?
DORCAS: Ndio.
MIMI: Ukinijibu hapa hapa kuna
nini?
DORCAS: Kuna mengine si ya kujibu haraka haraka
Nyemo.
MIMI: Kwa hiyo unakwenda kuomba ushauri kwa
mama?
DORCAS: Umejuaje! Si unajua kila kitu lazima
nimshirikishe.
MIMI: Hebu acha zako. Niambie basi kwanza nijue ni nini
hatma yangu, kama kujiua au kuendelea kuvuta pumzi.
DORCAS: Hahaha!
Ujiue kisa mapenzi?
MIMI: Yeah! Sasa kama mtu unampenda halafu yeye
hakupendi, unategemea nini? Kujiua tu.
DORCAS: Sasa mbona hukujiua
toka zamani?
MIMI: Nilikuwa sina akili ya kujiua. Ila sasa hivi
ninayo. Ukinikataa tu, najiua, nishachoka maisha ya kukataliwa na mtu
mmoja.
DORCAS: Owkey..Usijali. Tutaongea zaidi baadae. Nataka kwenda
kusuka.
MIMI: Daah! Naomba kwanza unipe jibu langu.
DORCAS:
Itakuwa ngumu kwa sasa. Unaonaje tukionana baadaye.
MIMI: Tuonane
wapi?
DORCAS: Unapajua nyumbani?
MIMI:
Hapana.
DORCAS: Njoo hapa magomeni Mapipa then nitakufuata
kituoni.
MIMI: Sasa hivi?
DORCAS: Usiwe na haraka.
Nikimaliza kusuka nitakushtua.
MIMI: Poa.
DORCAS: Kwa
heri.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
MIMI: Ila namba
yangu si unayo?
DORCAS: Sina. Hebu nipatie.
MIMI: 0716
008866
DORCAS: Mtoto wa Tigo.
MIMI: Kama kawa
mchumba.
DORCAS: Basi baadae.
MIMI:
Pwaxxxxx
Kilichofuata baada ya hapo ni Dorcas
kutoka online. Moyoni nilijisikia amani kupita kawaida, furaha ambayo ilikuwa
imetoweka ikaanza kurudi. Dorcas yule ambaye nilikuwa nikimfuatilia kwa kipindi
kirefu, leo hii alikuwa ameamua kukutana nami na kisha kukaa pamoja na
kuzungumza. Kiukweli nilikuwa katika mudi nzuri sana, yaani kwa hali ya furaha
ambayo nilikuwa nayo katika kipindi hicho, hata kama ungekuja kwangu na
kuniambia nikukopeshe 10,000/=, nisingekukopesha, ningekupa kama rafiki yangu
kutokana na furaha ambayo nilikuwa nayo.
Hii
facebook hii...yaani hawa wasichana hawawezi hata kujishika kabisa. Kipindi cha
nyuma kabla ya kuanza kumfuatilia Dorcas, wala hawakuwa wakinifuata fuata ila
baada ya hapo ndipo nao wakaonekana kubadilika kiasi ambacho mpaka nikaanza
kuiona facebook kuwa chungu. Mapenzi haya + facebook = bado nusu yanitoe roho
hasa mara baada ya kuingia katika mahusiano na huyu Dorcas ambaye kwa wakati huo
nilikuwa namuita moyoni ‘QUEEN OF MY
HEART’.
Nilionekana kuwa mwingi wa presha, muda
wote nilikuwa naiangalia simu yangu tu, sikujua ni muda gani ambao mtoto Dorcas
angepiga simu ile. Macho yangu yalikuwa kodokodo kila wakati. Nilikuwa na hamu
kubwa ya kuonana na Dorcas kuliko mtu yeyote katika dunia
hii.
Kuna kitu kimoja ambacho kilikuwa kikiniudhi
sana na ninaamini kwamba hata wewe kimekwishawahi kukutokea mara nyingi sana.
Utakuta mtu unasubiri simu ya mtu muhimu sana, halafu katika kipindi hicho hicho
mtu mwingine anaanza kukupigia simu, unakuwa kwenye hali gani? Sasa hicho ndicho
kilichokuwa kikinitokea katika wakati huo.
Sijakaa
vizuri, Vonso, rafiki yangu kapiga, sijakaa vizuri, Shedrack Joshua kapiga,
sijakaa vizuri, utakuta nae Muksin Muhinga nae kapiga, siku hiyo nilikuwa
nikikasirika sana kiasi ambacho nilitamani kuwatukana. Katika kipindi hicho,
sikutaka kupokea simu ya mtu yeyote yule, simu ambayo nilikuwa nikitaka kuipokea
ni ya msichana Dorcas tu.
Saa 11:20 jioni, simu yangu ikaanza kuita
tena, nilipoiangali, ilikuwa ngeni, unafikiri nilifikiri nani hapo?
Nilipoipokea, sikio langu likakutana na sauti nzuri, sauti nyororo ambayo
sidhani kama nilikwishawahi kuisikia sehemu yoyote zaidi ya waimba kwaya hasa
wale wanaoimba sauti ya kwanza. Alikuwa
Dorcas.
DORCAS: Mambo!
MIMI (Huku
nikitoa tabasamu kana kwamba Dorcas alikuwa akiniona): Poa. U
mzima?
DORCAS: Mzima. Otea unaongea na nani.
MIMI: Naongea
na Malaika wangu, Dorcas.
DORCAS: Hahaha! Upo wapi?
MIMI:
Nipo home.
DORCAS: Unaweza kuja sasa hivi au upo bize?
MIMI:
Naweza. Sipo bize wala nini, yaani hapa nilikuwa nasubiria simu yako
tu.
DORCAS: basi poa. Nakusubiria hapa Mapipa.
MIMI: Poa.
(Nikakata simu)
Vitu vingine si lazima nikuambie
ni kwa jinsi gani katika kipindi hicho nilikuwa na uharaka. Nilivaa nguo fasta
fasta halafu mbaya zaidi, kila nguo niliyokuwa nikiivaa niliiona kuwa haijanikaa
vizuri na wakati siku nyingine zilionekana kunikaa vizuri. Kiu yangu katika
kipindi hicho ilikuwa ni kumuona Dorcas kwa mara nyingine tena, katika kipindi
ambacho ningekaa nae chini na kuanza kuzungumza
nae.
Nilipotoka nyumbani, sikuaga, nikachoma
mazima na kukimbilia tigo pesa. Sikutaka kwenda mifuko mitupu au labda ningekuwa
nakutana na rafiki yangu Babi De Councious. Nikatoa shilingi elfu kumi na tano
na kisha kuchukua bajaji.
Nadhani hiyo ndio
ilikuwa siku ya kwanza kukodi bajaji kutoka Tandale mpaka Magomeni. Japokuwa
Dorcas alikuwa akiijua hali yangu ni ya kawaida lakini siku hiyo nilitaka
kuonekana tofauti kidogo. Bajaji ilichukua dakika tano, ikafika Magomeni Mapipa
na kisha kuteremka.
Macho yangu yalipotua kwa
Dorcas, alionekana kuwa mrembo sana asikwambie mtu. Alikuwa amevaa kipedo cha
jinzi fulani zile laini laini, kishati kidogo cha rangi ya pinki pamoja na raba
fulani simpo sana huku kichwani akiwa amevaa kofia fulani za kisista
duu.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
MIMI:
Duh!
DEREVA BAJAJI: Vipi?
MIMI: Demu mwenyewe yule pale.
Kulalaleki, kawa mkali ile mbaya.
DEREVA BAJAJI: Yupo wapi? Yule
mwenye hijabu?
MIMI: Hapana. Yule aliyevaa kipedo.
DEREVA:
Duuuh!
MIMI: Vipi?
DEREVA BAJAJI: Mmmh! Yule demu mkali
aisee.
MIMI: Ndio huyo bwana. Chukua kwanza hii hela yako then
tutaonana nyumbani (Nilimwambia huku nikimgawia fedha zake)
DEREVA
BAJAJI: Poa (Akaipokea fedha ile na kisha mimi kushuka
chini)
Nikaanza kupiga hatua kumfuata Dorcas, kwa
mbali nilikuwa nikitetemeka huku kijasho chembamba kikinitoka. Kwa mbwembwe
zake, Dorcas aliponiona, akapiga uyowe mkubwa na kisha kuja kunikumbatia kwa
furaha. Nilijisikiaje aibu.
Dorcas alikuwa akinukia kupita kawaida,
pafyumu yake ambayo alikuwa amejipulizia siku hiyo nadhani sijawahi kuisikia
sehemu yoyote ile.
MIMI: Mmmh! Unanukia vizuri
(Nilimwambia karibu na sikio lake huku akiwa kanikumbatia)
DORCAS:
Asante
MIMI: Natamani nikubebe juu, na hivi ulivyokuwa
mwembamba.
DORCAS: Hahaha (Alitoa kicheko fulani cha kizushi na kisha
kujitoa kifuani mwangu)
Kilichofuata mahali hapo
ni kwenda kwenye ule mghahawa uliokuwa katika jengo lililokuwa na internet ya
Virus na KISHA Dorcas kumuita mhudumu.
DORCAS:
naomba Mirinda nyeusi pamoja na kababu. Msikilize na huyo mume wangu (Dorcas
alimwambia mhudumu yule)
MIMI: Naomba bia. Pombe kali yenye kilevi
kuanzia 5%.
DORCAS: Wewe Nyemo.
MIMI:
Naam.
DORCAS: Wewe si umeokoka.
MIMI:
Najua.
DORCAS: Pombe ya nini sasa?
MIMI: Hahaha! Nilikuwa
namzingua. Naomba uniletee juisi ya maembe pamoja na chipsi.
MHUDUMU:
Aweke kila kitu kwenye chipsi?
MIMI: Yeah! Mwambie aweke kila kitu.
Mpaka sumu.
MHUDUMU na DORCAS: Hahahaha (Mhudumu akaondoka mahali
hapo)
Hiyo ndio tabia yangu, huo ndio muonekano
wangu wa kila siku. Mara kwa mara ninaonekana kuwa mcheshi huku nikijaa utani
bila kutambua kama hiyo ni siku ya kwanza kukutana nawe au la. Kila nilichokuwa
nikikifanya mahali hapo ni kumruhusu Dorcas aendelee kujua kwamba sikuwa
nimebadilika, nilikuwa Nyemo yule yule ambaye nilikuwa nikimfuatilia toka
kitambo. Vinywaji na vyakula vikaletwa mahali pale na kisha kuanza
kula.
DORCAS: Naomba uniambie kuhusu mapenzi
(Dorcas aliniambia huku akiniangalia)
MIMI: Mapenzi ni kama kiti cha
basi.
DORCAS: Sipendi kusikia msemo huo.
MIMI: Okey! Mapenzi
ni kama maua.
DORCAS: Bado sijaridhika.
MIMI: Sasa unataka
nikwambie mapenzi ni kama nini?
DORCAS: Jaribu kutunga. Wewe si
mtungaji.
MIMI: Okey! Mapenzi ni kama darasa.
DORCAS: Ndio
kwanza nasikia kwako.
MIMI: Si umeniambia nitunge?
DORCAS:
Yeah! Endelea.
MIMI: Tufanye mapenzi ni darasa, wewe ni mwanafunzi.
Mara kwa mara unapokwenda shule, unapenda kuliweka darasa katika hali ya usafi.
Unapofunga shule au kumaliza, huwa unatamani sana kama ungerudi shuleni, si ndio
hivyo?
DORCAS: Ndio.
MIMI: Sawa na mapenzi. Unapokuwa haupo
kwenye mapenzi, huwa unatamani sana urudi tena katika mapenzi kama unavyotamani
kurudi darasani unapomaliza shule.
DORCAS: Kidogo naanza
kukupata.
MIMI: Unapopata nafasi ya kurudi darasani, unajisikia mwingi
wa furaha kwa sababu unakutana na watu tofauti tofauti ambao ulikuwa umezoeana
nao. Si ndio hivyo?
DORCAS: Yeah!
MIMI: Unapokuwa darasani
unaongea na wenzako kwa furaha, mwalimu wa somo usilolipenda anapoingia, huwa
unajisikiaje?
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
DORCAS:
Vibaya.
MIMI: Hao ndio vidudumtu kwenye mapenzi. Huwa mara kwa mara
hawapendi wakuone kwenye furaha, unapojaribu kufanya hivi, wao watataka kufanya
kile, utakapojaribu kufanya kile, wao watataka kufanya hiki. Waepuke sana watu
hawa, huwa si wema sana, huwa ni wabaya ambao wanaweza kuharibu kila
kitu.
DORCAS: Mmmh! Una maneno mengi sana Nyemo. Ila ulichosema
kuhusu watu hao, ni cha ukweli kabisa.
MIMI: nawajua sana. Ninaposema
kwamba leo nataka kukaa na mpenzi wangu niyafurahie mapenzi, wao watakasirika tu
huku wakihoji kwa nini nikae na mpenzi wangu.
DORCAS: Nimekuelewa.
Hebu kwanza tuachane na hilo. Nikuulize swali?
MIMI:
Uliza.
DORCAS: Unanipenda?
MIMI: Sawa na kuulizia makofi
polisi.
DORCAS: hahaha!
MIMI: Sawa na kuulizia ushungi
Pemba.
DORCAS: hahahah!
MIMI: Ni sawa na kuulizia bunduki
jeshini.
DORCAS: hahaha! Acha kunichekesha Nyemo. Hebu nijibu
kwanza.
MIMI: kwani si tayari nishakujibu.
DORCAS:
bado.
MIMI: Swali lako ni sawa na kuulizia mapenzi juu ya Dorcas
moyoni mwa Nyemo. Nakupenda, nakupenda sana, nakupenda zaidi ya unavyofikiria,
nakupenda zaidi ya unavyojipenda, ninakupenda zaidi ya marafiki zako
wanavyokupenda.
DORCAS: Huo umekuwa kama wimbo Nyemo. Sound
nyingi.
MIMI: Huu ni kama wimbo, naamini hilo. Kila siku umekuwa
ukiambiwa kwamba unapendwa na watu wengi kiasi ambacho umeona kwamba neno
‘nakupenda’ kuwa kama wimbo masikioni mwako. Ila nataka kukwambia kitu kimoja.
Neno hili limekuwa wimbo kwako, lakini leo huu wimbo umekuwa remix masikioni
mwako.
DORCAS: Unamaanisha nini?
MIMI: Msanii anapotoa wimbo
na kisha kutoa remix yake ina maana kwamba kuna vitu alikuwa amevisahau
hakuviweka sasa anataka kuviweka katika remix yake. Hiyo ni sawa na mimi. Wengi
wamekwambia kwamba wanakupenda ila kuna vitu hawajavisema
kwako.
DORCAS: kama vipi?
MIMI: Kupendwa zaidi ya
unavyojipenda. (Nilijibu, akatoa tabasamu ambalo likanifanya nimpende
zaidi)
Ukinisikiliza, nilikuwa naongea kiutani
sana ila kumbuka kwamba ndio nilikuwa nazidi kupiga hatua zaidi na zaidi.
Nilikwishamsoma Dorcas kwa kipindi kirefu sana, hakuwa msichana wa kumwendea
sana siriasi, unamuwekea utani, unamchombeza kwa maneno haya, unamfurahisha
hapa, unamchekesha kule. Hiyo ndio hatua ambayo nilikuwa nikiifanya kwani
nilijua kwamba kama ningekuwa naongea huku nikiwa siriasi, kumpata kwangu
ingekuwa ndoto ya mchana.
DORCAS: maneno yako matamu sana, yanafanana
na post zako unazoziandikaga kwa facebook.
MIMI: Tabasamu lako zuri
Dorcas, linafanana na maneo uliyoniandikia jana kwamba unanitakia ‘FURAHA YA
SIKU YANGU YA KUZALIWA’.
Siku hiyo ikaonekana kuwa
siku ya furaha katika maisha yetu wote wawili, tulikula na kunywa huku tukipiga
stori za kizushi mahali pale. Dorcas alionekana kuwa mwenye furaha kubwa sana
kiasi ambacho hakutana nitoweke mbele yake. Tulitumia muda wa saa moja na nusu
kukaa pale na ndipo tukahitaji kuondoka mahali hapo. Kwa mara ya kwanza,
nikambusu Dorcas shavuni mwake jambo ambalo lilionekana kunifurahisha kupita
kawaida. Ukurasa mpya wa mahusiano ya kimapenzi ulikuwa umefunguliwa mahali
hapo.
DORCAS: Usiniumize.
MIMI: Nami
natakiwa kukwambia maneno hayo hayo.
DORCAS: Naijua facebook. Japo una
marafiki mia moja na kadhaa lakini unaweza kupata marafiki wengi zaidi kutokana
na uandishi wako. Kuwa makini na watoto wa kike.
MIMI: Usijali Dorcas.
Siwezi kufanya jambo lolote baya, hasa kukusaliti wewe (Nilimwambia huku nikitoa
tabasamu pana ambalo lilimfanya kuniamini
zaidi).
Kiukweli tofauti na watu wengine, Dorcas
sikutaka kumchezea na kumuacha, hapana, nilikuwa nikimaanisha mapenzi yale
ambayo nilikuwa nimemwambia, hata kama ingewezekana, basi haikuwa budi kumuoa.
Siku hiyo tukaongea mengi na hatimae kuagana. Sikutaka kuondoka nyumbani,
nilichokifanya ni kumng’ang’ania kwenda naye huko alipokuwa akiishi, tukaenda na
kupaona na ndipo nilipoondoka kuelekea
nyumbani.
MIMI: Nitakupenda mpaka nakufa
(Nilijisemea ndani ya daladala katika kipindi naelekea nyumbani kana kwamba
Dorcas alikuwa pembeni yangu)
Mahusiano yale
yaliendelea zaidi na zaidi, sikuachana na uandishi wa hadithi humu facebook,
bado nilikuwa nikiendelea nao kama kawaida. Watu walinipenda, watu walipenda
kusoma simulizi zangu ambazo nilikuwa nikiziandika katika staili ambayo ilikuwa
ikinishangaza hata mimi mwenyewe. Nikazidi kupata marafiki zaidi mpaka ndani ya
wiki moja kupata marafiki zaidi ya 500. Kazi ya uandishi ilikuwa ngumu sana
lakini sikutaka kuiacha, bado nilikuwa nikiendelea nayo kama kawaida jambo
ambalo lilikuwa likinipa marafiki wengi.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
JULIET: Unajua sana
Nyemo. Nafurahi sana kila ninaposoma simulizi zako, yaani kama naangalia muvi
Mlimani City.
MIMI: Asante. Ila kawaida tu, namshukuru Mungu kwa hiki
kipaji.
JULIET: Yaani kama na mimi ningekuwa najua kuandika kama wewe,
ningefurahi sana.
MIMI: Tofauti na kipaji, wakati mwingine ukijifunza
unaweza.
JULIET: Sasa mimi nitajifunza wapi?
MIMI: Kupitia
hadithi nyingi. Jitahidi kusoma hadithi mbalimbali. Ukiona kwamba unataka
kuandika hadithi kama za Nyemo, basi penda kusoma hadithi za Nyemo, ukiona
kwamba unapenda kuandika hadithi kama za Sultan Tamba, pendelea sana kusoma
hadithi zake.
JULIET: Na kama nikisoma hadithi za
wote?
MIMI: Utachanganyikiwa. Katika maisha ya mwandishi, wengi
hushindwa kuandika hadithi za aina tofauti. Mungu amegawa vipaji ila
kavitofautisha tu.
JULIET: Kivipi?
MIMI: Kuna mwingine
anaweza kuandika hadithi kuhusiana na mambo ambayo huwezi kuyafikiria kabisa,
mfano ninavyoandika, huwezi kujua ni staili gani ninayotumia, naweza kukuandikia
vitu ambavyo havipo katika jamii ya Kitanzania, huwa ninafurahi kuandika
kuhusiana na mambo ya nje, huo ndio uandishi, nazunguka duniani kote. Ila katika
hili, kuna mwingine anaweza kuandika hadithi ambayo inahusu jamii inayomzunguka
tu, kutoka nje ya jamii inayomzunguka inakuwa ngumu sana kwani kuandika kuhusu
jamii tofauti na hizi za Kiafrika, basi inabidi Mungu awe amkupa kitu kingine
cha ziada sana.
JULIET: Mmmh! Umetoa maelezo marefu
sana.
MIMI: Hiyo ni kwa sababu unataka kujifunza.
JULIET: Na
mbona hauandiki hadithi kuhusiana na jamii inayotuzunguka, hadithi zako nyingi
zinakwenda nje ya Afrika?
MIMI: Nilikwishawahi kuandika hadithi kama
Maria, mwanzo mwisho ilizungumzia maisha halisi ya Mtanzania, ila baadae
nikajuta.
JULIET: Kwa nini?
MIMI: Huwa sipendi kuziandika
hadithi hizo humu Facebook japokuwa ninazo nyingi. Humu facebook, ngoja niwe
naziandika hizi hizi za kwenda nje, zile zinazohusu jamii husika ya Mtanzania,
ningependa kuzifanyia muvi na si kuzirusha hewani, ndio maana nafanya hivyo.
Watu wabaya wanaweza kukopi na kupaste, ili kuwachanganya, acha niwaandikie
mpaka za nje, kama wana uwezo, waigize huku wakisafiri kwenda nchi
mbalimbali.
JULIET: Hahaha! Mtoto mjanja wewe.
MIMI: Kawaida
tu.
JULIET: Asante kwa muda wako.
MIMI:
usijali.
Huyu msichana ndiye alikuwa wa kwanza
kabisa ambaye alikileta kitu fulani moyoni mwangu, kitu ambacho kilionekana kuwa
doa katika mahusiano yangu na Dorcas. Kwangu mimi, nilikuwa nachukulia kila kitu
kuwa kawaida sana lakini kumbe mwenzangu alikuwa tofauti na mawazo yangu.
Mawasiliano yangu na Juliet yalikuwa yakiendelea kama kawaida kwa njia ya inbox.
Kitu ambacho kila siku alikuwa akikifanya ni kuniomba namba ya simu, sikuwa
mwepesi, nilikuwa nikimyima sana ila kutokana na wadau wengi kunisumbua kwamba
walikuwa wakitaka kunipongeza kupitia simuni, nikaiweka namba yangu hadharani
jambo ambalo likaonekana kuwa kosa kubwa. Usumbufu ukaanza rasmi kutoka kwa
Juliet,
MIMI: Unasemaje?
JULIET: Sauti
yako nzuri. Naweweseka kila ninapoisikia.
MIMI: Ok! Usijali. Kawaida
tu.
JULIET: Kwani yangu sio nzuri Nyemo?
MIMI:
Nzuri.
JULIET: Hauweweseki?
MIMI:
Ndio...siweweseki
JULIET: Naomba kitu kimoja kutoka
kwako.
MIMI: Kitu gani?
JULIET: Naomba
tuonane.
MIMI: Haiwezekani. Nipo bize sana kwa sasa.
JULIET:
Hata kwa dakika kumi tu.
MIMI: Hapana Juliet, nafikiri kuwasiliana
simuni na facebook kunatosha.
JULIET: Hapana bwana, nataka kumuona mtu
ambaye kila siku anaufanya moyo wangu kufurahia. Naomba
tuonane...nakuomba.
MIMI: Haiwezekani. Sipo Dar, au uje huku mkoani
Kagera ninapoishi (Nilidanganya)
JULIET: Upo Kagera?
MIMI:
Ndio.
JULIET: Mbona umeandika unaishi Dar?
MIMI: Niliamua
kuandika hivyo ili watu wengi waone nilikuwa nikiishi katika jiji
hilo.
JULIET: Nahisi unanidanganya.
MIMI: Kweli tena. Sioni
haja ya kukudanganya.
JULIET: Sawa. Naweza kuja huko Kagera kesho
kuonana nawe?
MIMI: Kuja Kagera? Kesho? Mvua zinasumbua sana huku,
barabara mbovu.
JULIET: Usijali. Nitakuja na ndege.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
MIMI:
Mmmh!
JULIET: Nini tena?
MIMI: Hakuna kitu. Usijali. Unaweza
kuja.
JULIET: Sawa. Nitakuja na ndege ya saa nne asubuhi. Ngoja
nimwambie baba anikatie tiketi kabisa.
MIMI: Poa. (Simu
ikakatwa).
Dizaini sikuwa sawa katika hali hiyo,
nikaanza kujiuliza kuhusiana na Juliet, mpaka kufika hapo, kuna kitu ambacho
nilikuwa nimekifikiria kwa kuona kwamba juliet alikuwa ametoka katika familia
ambayo ilikuwa ikijiweza sana kuhusiana na mambo ya
fedha.
Ila, sikutaka kuamini, nilikuwa naona
kwamba msichana yule alikuwa muongo, nilitaka kuona kama kweli ingewezekana
kusafiri mpaka Kagera kwa ajili ya kuniona. Usiku wa siku hiyo, niliiona post
yake akiwa ameandika ‘Nakwenda Kagera kesho, nahitaji maombi yenu’. Nilishtuka
sana, nikaona kwamba Juliet alikuwa akimaanisha kile ambacho alikuwa ameniambia,
nilichokifanya, nikaLIKE na kisha kuendelea na mambo
yangu.
Kutokana na usiku uliopita kuchelewa
kulala, asubuhi ya siku hiyo niliamshwa na mlio wa simu yangu ambayo ilikuwa
ikiita, nikaamka na kisha kuangalia kioo cha simu ile, namba haikuwa
imehifadhiwa simuni lakini kwa kuiangalia tu, nilikuwa nikiijua, ilikuwa ni
namba ya Juliet. Huku nikionekana kuwa katika uchofu, nikabonyeza kitufe cha
kijani na kisha kuipeleka sikioni.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
****************************************
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment