Chombezo : Sex Machine
Sehemu Ya Nne (4)
Catherine akiwa anaikanya ardhi ya nchi hiyo ya Obama, kwa upande mwingine, Sex machine alikuwa anaikanyaga ardhi hiyo hiyo uwanjani hapo. Kila mmoja alichukua usafiri wake na kuondoka uwanjani hapo safari ikiwa ni sehemu moja utofauti ni kwamba huyu mmoja, alikuwa anakwenda kufanya ngono na shoga kikongwe na huyu mwingene, alikuwa anakwenda kumuuwa shoga huyo kabla hata sex machine haja mgusa. Lakini wote walikuwa wanatakiwa kuingia ndani ya hoteli hiyo ya V Ice.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Gari ya kwanza kufika kwenye hoteli hiyo ya hapo jijini Miami, ilikuwa ni ile iliyombeba Catherine. Alishuka garini humo na kukamilisha malipo kisha akaingia ndani ya hiyo hoteli. kila kitu alikuwa anakijua kwahiyo haikumpa tabu. Alifika mapokezi na kufanya itifaki za hapo alipomaliza wakati anaondoka, kijana mtanashati mwenye suti safi alikuwa naye anaingia mapokezi kukamilisha utaratibu wa kukamilisha kupata chumba. Catherine akageuka na kumtazama huyo kaka bila kificho chochote kwenye sura yake na kutabasamu huku anaondoka. Chriss alikuwa anaongea na dada wa mapokezi lakini akili yake yote ilikuwa ikimfikiria huyo dada. Ni kama sura hiyo anaikumbuka, aliwahi kuiona mahali lakini akivuta picha ilikuwa haiji.
"ni wapi nilipata kuiona sura hii mbona kama inanijia kumbukumbu zake. Ni wapi jamani?" alijiuliza. Ghafla akakumbula tukio moja ambalo lilimtokea sehemu fulani huko nchini Uingereza ndani ya jiji la London. Tukio hilo ni tukio la kutekwa kwake na mwana dada Moline kisha akaja kuokolewa na huyo dada na yeye kumsaidi Moline. Kila awapo huyo dada kuna tukio linafanyika, akaweka imani hiyo. Kwahiyo hata hapo huwenda kuna kitu kikatokea. Labda ni hatari kwake. Aliwaza. Alipomaliza kuwaza hivyo, huku nako alikuwa amesha maliza kujaza na yeye kukabidhiwa kadi ya chumba. Akatoka hapo akiwa na tabasamu ili asiweze kushtukiwa na dada wa hapo mapokezi, tabasamu likiwa kama fimbo ya kumnyong'onyeza dada huyo. Alipofika kwenye lifti akakuta inatumika akajua huo ni mchezo kachezewa. Kumbukumbu za kuuwawa kwa mashoga zikamjia, akawaza kuwa hata hapo huwenda hilo tukio linaweza kutokea. Akaamua kutumia mazoezi ya mbio kwa kupanda ngazi, alitumia muda mrefu lakini alifanikiwa kufika juu ambako chumba cha mteja wake kipo. Kipindi hiki kilikuwa si cha yeye kuchukua chumba bali ni kutoa tu maelezo mapokezi kuwa kuna mwenyeji wangu yuko chumba namba fulani. Kwahiyo hata kuchukua hicho chumba ni geresha tu ili kuwafanya wafanyakaxi wa hoteli hiyo wadiweze kumtilia mashaka. Akakitazama hicho chumba na kugusa kitasa.
TURUDI DAKIKA TANO NYUMA.
Catherine alipotoka pale mapokezi, alielekea kwenye lifti na kuiruhusu lifti hiyo impeleke flow namba tano, lifti hiyo iliporuhusiwa, ikatii. Alipofika flow husika, hakutoka kwenye ile lifti. Aliharibu kwanza system ya kuiendesha lifti ile kisha akatoka na kuelekea kwenye chumba husika. Ndiyo maana hata Sex machine alipofika kwenye ile lifti akaona kuwa inatumika lakini si hivyo. Lifti hiyo ilikuwa imeshaharibiwa zamani. Catherin alikwenda hadi kwenye mlango husika na kunyonga kitasa mlango ulikuwa umefungwa kwa ndani lakini aliyepo ndani humo, akajua kuwa ni mgeni wake, akafungua mlango. Catherine alimsukumia huyo mzee kwa ndani kisha hakufunga mlango bali aliurudisha tu. Na kumgeukia mzee yule kikongwe asiye na haya wala soni, asiyetulia na kufanya ibada kwa ajili ya kutubia dhambi zake. Badala yake anazidi kufanya mambo ambayo alikuwa akiyafanya toka ujani mwake, huku yakiwa ni mambo ya kiharamu kabisa yasiyompendeza Mungu.
"huna bahati leo na sikuachi hai" alisema Catherine. Yule mzee akataka akimbilie kwenye kengele ya kupiga alam ili kutoa taarifa kuwa ameingiliwa na muuwaji. Alikosea. Nasema alikosea kwa sababu alikula mtama mmoja wa nguvu kutoka kwa mwanadada huyo kisha akamnyanyua na kumuwekea kisu shingoni. Nakuuwa si kwa kukuonea bali kukubali kwako, kufanya mapenzi kinyume na maumbile na ikiwa Mungu hapendi. Ulifnya kwa muda mrefu sana huu mchezo lakini huku ridhika na hukutaka kuacha. Unaamua kufanya mchezo huo mchafu hadi muda ambao ulipaswa kupiga magoti chini na kumuomba Mungu akusamehe kwa kujifananisha na wanawake na kuthubutu hata kukubali kuunyima haki mwili wako kama mwanaume na ukageuzwa kinyume na maumbile. Kama ungeniambia kuwa nikikuacha hapa utaacha huu mchezo, nisinge thubutu hata kukuwekea hiki kisu kooni lakini kitendo chako cha kukimbilia kengele ili tu utoe taarifa kwenye ulinzi wa hii hoteli kwa kuhisi nakuonea, Nakuapia. Kisu hiki hakirudi mahali kilipotoka bila kumwaga damu yako na Mungu ananiona kuwa sikuonei. Utaacha huu mchezo mchafu?" alisema mengi Catherine kisha akamuachia swali la kumtega.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"kama unaniachia niachie tu lakini tayari mimi nimekwisha kuuzoe huu mchezo na leo ni siku ya kuufurahia mchezo huo kutoka kwa kijana anayesifika kwa kujua kukuna kutoka tanzania, please, niache wee muwaji kisha uende na sitatoa taarifa popote pale." aliongea mzee huyo ambaye hakuwa tayari kuiacha kazi hiyo ambayo kwake ni kama ibada.
"basi ngoja ufe kama uko tayar..!" alikwama kidogo baada ya kuona kitasa cha mlango kimeguswa. Akajua kuwa kijana amewadia sasa ni lazima apambane ili achomoke pia amsaidie na Sex machine. Kijana Sex machine alipofungua tu mlango na kuingia ndani, aliushudi mwili wa mzee aliyepatakiwa kuja kumchambua nywele za makalio na kumuingilia kinyume, ukiwa unadondoka chini huku akimuona mtu ambaye amejificha sura kwa kitambaa cheusi akiwa amekamata kisu huku mikono yake ikiwa imevikwa gloves. Dada yule alikiachia kile kisu na kuanguka mwilini mwa yule mzee aliyekufa kwa kuchinjwa kisha akajiweka katika mkao wa kupambana. Sex machine akaweka brifcase chini na kumkabili huyo muuwaji. Ulikuwa ni mkono mkali sana kila mmoja alionesha weledi katika nyanja hiyo ya mapambano. Dada alipeleka mashambulizi makali kwa lengo la kupima uwezo wa kijana huyo, akakuta mapigo yake yote yamepanguliwa na.kupewa pigo moja la komfuu. Catherine aliserereka na kupiga mweleka mbaya, Sex machine akawahi pale chini ili kumdhibiti lakini Catherine akakataa na kumtoka kijana huyo na kumpiga pigo ambalo Sex machine aliliona akakwepa. Pigo hilo lilikuwa limepigwa kwa umaridadi sana hivyo Sex machine wakati anakwepa, alikutata na kitu kingine kilichomtupa kitandani na hapo hapo Catherine akakimbilia mlangoni na kuufungua mlango huo lakini kabla hajatoka, alisema.
"njia ninayopitia ni hapo kwenye dirisha. Kuna kamba itakayonifikisha chini na kutoweka eneo hili naomba na wewe utumie njia hiyohiyo kwani mimi ndiye niliyeharibu ile lifti ya kuja huku juu. Pia walinzi wanaokiongoza hiki chumba na hoteli nzima hii kwa kamera maalumu za ulinzi, wamesha kitilia mashaka hiki chumba na mimi nitakapotoka tu watahakikisha wanaweka ulinzi kila kona. Kwa kukusaidia my love naomba tutoke wote ili usije kuingia kwenye mikono ya polisi wa Marekani. Muda watakao utumia kupanda ngazi kuja hapa ufanye ndio muda wa kufikiri na kutoa maamuzi, Tutaonana my love" aliposema hayo Catherine, hakusubiri kitu kingine, alitotoka na kuchumpa dirishani kwa kutumia kamba maalumu aliyoiweka hapo kwa kuishikisha mahali akapotea. Camera zilikuwa zimesha msoma huyo mtu aliyeruka hapo kwahiyo kwa haraka sana hali ya hatari ikamfikia kila raia anayehusi na ulinzi ailiomo humo ndani mwa hoteli maana haikujulikana ni nini kimekwenda kutukia mule ndani ya kile chumba. walinzi walianza kuja ...............
walinzi walianza kuja hadi kwenye lifti walipofika hapo kwenye lifti wakakuta imeharibika, hapo wakajua hali si shwari huko juu.
Muda huo Sex machine hakungoja kusikia tena maelezo mengine alitoka mbio huku akisiki ving'ora vya hatari vikilia. Alikwenda hapo dirishani kweli alikuta kamba. Alibinjuka na kutembea na hiyo kamba lakini hakufika chini alijipushi kwenye jingo moja na kutembea juu ya paa la jingo hilo na kuchumpia upande wa pili. Huko alikuta watu wachache ambao walikuwa na mishe zao. Huku nyuma mambo yalikuwa si shwari walinzi wale walikuwa wanakuja huku kwa mbali kukisikika sauti za ving'ora vya gari za polisi. Chriss alidandia pikipiki aliyoikuta imeegesha hapo na kuwasha kwa haraka bila hata kumuomba muhusika na kutoweka. Kwa mbali Catherine naye aliondoka baada ya kuona Sex machine amefanikiwa kuwatoroka walinzi na askari waliokuwa wanakuja mahali hapo.
Catherine alipotoka hapo, kitu pekee alichokifikiria ni kwamba, lazima Chriss akitoka pale ni katika Hoteli ambayo ndiyo atakayokwenda kukutana naye kwa ajili ya kazi inayofuata na kazi hiyo, mhusika mkuu alikuwa ni yeye hivyo, alipiga mwendo wa haraka sana hadi katikati ya jiji hilo la Miami. Aliitafuta hoteli husika na kuelekea hadi hapo. Gari aliyopanda ilipomfikisha hapo ikamuacha na yeye kuingia ndani ya hoteli hiyo ya kifahari sana. Alilipia Chumba alichopanga kukutana na Sex Machine na kwenda kutulia akimsubiri mtu huyo.
Chriss alikimbiza pikipiki hilo alilolikwapua kwa ajili ya kumtoa kwenye lile sekeseke, hadi alipofika katikati ya jiji. Hapo alilitelekeza lile pikipiki na kuingia kwenye Saloon moja kubwa mjini hapo. Akatengeneza nywele kwa mtindo mwengine na kuchonga ndevu vizuri kwa mtindo wa 'O' kisha akatoka humo ndani akiwa tofauti kidogo. Alipotoka ndani ya Saloon hiyo, alielekea moja kwa moja hadi kwenye duka kubwa la nguo linalopatikana mjini hapo. Alinunua nguo za gharama na za kileo. Alinunua Jeans nyeusi, akachukua na fulana ya rangi nyeupe pee!, akaingia kwenye chumba cha kubadilishia nguo. Akabadili nguo hizo chini akapiga raba safi nyeupe kisha kuchukua na kapelo. Alipotoka hapo, hakuna hata aliyedhani kuwa huyo ndiye yule aliyehusishwa na vurugu baada ya mauwaji yaliyotukia kwenye hoteli ya V. Alikuwa ni kijana bomba wa kileo kabisa, ambaye ukiangalia mavazi, mwendo, na jinsi alivyotoka na pigo zake, huwezi kuamini kama ni yeye yule wa mwanzo na si kuamini tu, hata kumtambua ingekusumbua. Brifcase lake la gharama lilikuwa mkononi, alikuwa akitembea kwa mwendo wa kuringa lakini wa haraka kidogo na muda wote alikuwa akiangalia saa yake ya mkononi. Alikatiza nje ya nyumba moja ya biashara ambayo ilikuwa wazi akataka kuingia humo lakini akasimama ghafla baada ya kuona matangazo na matukio ya mchana yakirushwa kwenye chombo kimoja cha habari. Kubwa na lililomvutia ni taarifa ya kifo cha yule kikongwe kule hotelini. Kifo chake kikawapa watu hisia tofauti baada ya muuwaji kutokujukikana, wengi walisema muuwaji ni mwanamke ambaye hakuonekana sura kutokana na kujiziba sura wakati wa kutoka humo hotelini kwa kutumia njia za panya. Wengine wakasema ni mwanaume ambaye sura na muonekano wake vikaonekana na ni mara baada tu ya mwanamke huyo kutoka ndipo naye akatoka kwa kupita njia moja ya kuruka dirishani kwa kamba. Picha yake ikaoneshwa kwenye luninga hiyo, hakuwa akionekana sura vizuri ni kama alikuwa akiikwepa kamera hivyo kuonekana sura yake kwa uchache sana. Alitabasamu Chriss baada ya kuutazama muonekano wake wa mwanzo na huo kisha akaondoka hapo kwa kuchepukia mtaa wa pili kisha kuvuka barabara na kueleke upande mwingine kabisa mbali na eneo hilo. Alizipita kona kadhaa kisha kuibukia mbele ya hoteli kubwa ambayo ndiyo aliyokuwa akiitaka. Alizama ndani na kaufanya kila alichotakiwa kufanya. Akapelekwa mahali chumba kilipo. Akaingia akajifungia ndani ya chumba hicho kimya. Alilipia chumba hicho kwa muda wa siku tatu kwani hapo alikuwa na kazi kubwa sana ya kufanya. Ya kwanza ilikuwa ni kukutana na mwanamke mmoja tajiri sana ambaye alikuwa akihitaji huduma ya ngono na ni ndani ya hoteli hiyohiyo kwenye chumba ambacho kiko mkabala na chumba chake. Pili ilikuwa ni lazima afanye mauwaji kwa mfanya biashara mmoja mkubwa na tajiri sana ndani ya mji huo wa miami na Marekani kwa ujumla. Mwisho ni kufanya mauwaji ya meneja wa hoteli ambayo amefikia. Hakuwa akijua kuwa anachokipanga yeye na wengine wanapanga mipango yao. Hivyo kwake ikawa ni ngumu sana kupata kujua nini kitakwenda kumtokea.
Chriss alishusha pumzi nzito sana baada ya kufikiria kazi hizo zote zilizoko mbele yake huku mtekelezaji akiwa ni yeye. Alichoka sana lakini hakuwa na budi zaidi ya kuhakikisha zote zinafanyika na kwa weledi wa hali ya juu mno. Alinyanyua mkono na kuangalia muda, ilikuwa imetimu saa kumi na mbili za jioni. Muda huo ndio mda ambao alitakiwa kuingia ndani ya chumba cha pili kwenda kumkamua mtu.
"leo nina hamu sana ya ngono, natumai itakuwa ni gemu tafu sana kwangu na huyo mwanamke lazima asimulie. Ninauchu sana kama nyapara aliyefungiwa chumba cha peke yake kwa miaka mingi" aliwaza kijana huyo huku akijinyanyua mahali hapo alipokuwa amekaa, akaelekea mlangoni na kushika kitasa cha mlango huo. Alikuwa katika vazi hilo hilo na wala hakuwa na sababu za kufanya chochote kuhusu ulinzi kwani chumba hicho alichokuwa akienda hakikuwa na mwanaume zaidi ya mwanamke pekee hivyo hata walinzi wa hapo, pengine hawakuweza kulitilia shaka jambo hilo. Aliufunga mlango wake vizuri na kupiga hatua za kuhesabia hadi ulipo mlango wa chumba cha huyo dada. Akakikamata kitasa cha mlango na kukinyonga, kitasa kikanyongeka na mlango ukaachia, akausukuma bila ya kuwa na presha wala wasiwasi wowote. Alipoingia ndani ya hicho chumba, alikutana na mtoto mkali sana. Alikuwa ni mrembo kweli huyo binti aliyemkuta humo ndani na alikuwa katika mavazi ya kutega sana. Alikuwa amevaa bikini nyekundu chini na juu alikuwa amekiziba kifua chake kwa sidiria nyekundu. Alikuwa amekaa kitandani lakini akiwa amempa mgongo Criss. Harufu kali ya uturi ikazikumba pua zake. Urembo wa mtoto huyo kwa nyuma tu ukawa umeweza kuzinyanyua sehemu za kazi za kijana huyo. Akaanza kuhisi hamu ya hatari sana na hali hiyo inapomtokea kijana huyo, hakuna kitu anachokisikiliza zaidi ya kutekeleza kile kinachotakiwa kutekelezwa. Alipiga hatua moja mbele, akavuta ya pili. Binti huyo alikuwa hapo hapo na wala hakugeuka nyuma.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"karibu sana handsome boy ndani ya historia mpya ya maisha yako" maneno hayo yakamfanya kijana huyo kusimama ghafla. Kwa nini alisimama? Kilichomsimamisha siyo sauti nzuri ya dada huyo laa!, bali kilichomfanya hasa asimame ni kusikia kuwa anakaribishwa kwenye historia mpya ya maisha yake. Tena sauti hiyo akiwa anaikumbuka kabisa. Ni sauti aliyokutana nayo ndani ya hoteli ya V. Na ni sauti hiyo hiyo mbayo, mmiliki wake, alikuwa akipambana naye kule hotelini. Anakumbuka kuwa alimtahadharisha akimbie, leo hiyo hiyo kabla hata ya kupinduka kwa jua, anamkaribisha kwenye historia mpya ya maisha yake. Ni historia ipi hiyo?
"ni nani?" alijiuliza.
"na kwa nini anikaribishe kwa mtindo huo?" alizidi kujiuliza mawazoni Chriss.
"mbona umesimama? Karibu nipo hapa kwa ajili yako boy." alizidi kuongea dada huyo safari hii akiwa anasimama taratibu lakini akiwa bado amempa mgongo kijana huyo. Umbo mwanana kabisa, makalio yaliyovibwa na kutengeneza mlima mzuri wa wastani lakini ulionona na kuufanya uvutie kuutazama ama kuuminyaminya. Mkanda mwembamba uliopita katikati ya mapande hayo mawili makubwa ya nyama, uazidi kumfnya Sex machine azidi kukodoa macho ya kumtamani dada huyo lakini hakutaka kukurupuka kwanza kwani hali ya hewa ya mahali hapo hakuielewa.
"ni nani wewe?" aliamua kuuliza Chriss lakini swali lake halikupata jibu na badala yake huyo dada akageuka na kumtazama usoni. Mshtuko mkubwa ulimkumba Chriss, macho yakamtoka asiami hicho alichokutana nacho mahali hapo.
"vipi, hata huku upo? Inamaana umesha uwa na huku? Wewe ni nani kwani?" aliuliza maswali mfululizo huyo kijana lakini ndiyo kwanza huyo dada alitabasamu. Kimya kifupi kikapita huku dada huyo akimkodolea macho huyo kijana, yalikuwa ni macho yaliyoangaliwa kidadisi sana. Chriss alishangaa kumuona dada huyo, chozi likimdondoka machoni mwake huku akionekana akiwa ni mwenye kutabasamu muda wote.
"jina langu ni bikini nyekundu, hilo ndilo jina langu na nipo hapa kwa ajili ya kupata huduma yako Chriss"
"whaat!? Umeniitaje?" aliuliza kijana huyo akiwa ni mwenye mshangao mkubwa.
"Chriss, si ndilo jina lako, au wewe ni nani labda, haujifahamu" alisema Catherine au bikini nyekundu kama alivyojitambulisha mahali hapo. Chriss alifkiri kwa muda halafu kitu kama sindano ikachoma ndani ya moyo wake, yalikuwa ni maneno machache lakini yalimuingia akilini vizuri sana. Akafikiri ni wapi alipata kulisikia jina hilo akiitwa. Alifikiri kwa haraka sana, akakumbuka ni siku ambayo alikuwa akifanya mapenzi na Suzane, aliitwa jina hilo hilo la Chriss lakini alipotaka kujua zaidi kuhusu jina hilo, binti yule hakumuweka wazi zaidi ya kuzuga na kujifanya ni kama amechanganya. Leo jina hilo hilo analikuta kwa huyo binti anayejiita bikini nyekundu. Akamtazama vizuri machoni. Mungu wangu! Alikuwa ni yule aliyemuokoa kule London. Akaona kama ndoto ya mchana ikiwa inamletea maluweluwe machoni mwake. Akataka kusema kitu lakini alichelewa, binti huyo alimsogelea na kuanza kumzunguuka, alimzunguuka taratibu huku akiwa anamtazama kwa makini sana.
"karibu uufaidi mwili wangu Sex machine kwani kumbuka kuwa upo hapa kwa ajili ya kuwatumikia mabwana wako, ukumbuke kuwa wanakuona kila unapokwenda na kila unachokifanya bila ya wewe mwenyewe kujua. Umekuwa kama Mbwa ambaye hana mfugaji wewe mwanaume" hayo yalikuwa ni maneno yenye kumuumiza kupita kawaida. Yalikuwa ni matusi mazito kwake. Ni kweli alikuwa hana sauti kwa watu wanao mtuma lakini si kwa kutukanwa namna hiyo. Akamgeukia akiwa ni mwenye ghadhabu sana, ni dhahiri alitaka kumrarua huyo binti lakini hakuwahi na badala yake aliwahiwa na maneno na bikini nyekundu.
"nimelipa pesa nyingi sana kwenye kampuni yenu kwa ajili ya huduma yako, hebu fikiria ni
hebu fikiria ni hasira kiasi gani utakazo wapa waliokutuma kwa kumpiga mteja ambaye robo tatu ya pesa bado hajalipa?" alisema binti huyo kwa kujiamini huku akiwa anamtazama usoni kijana huyo ambaye alikuwa akitweta kwa hasira. Ni kweli aliyoyasema huyo msichana na ni kweli tupu kuwa atakuwa amekwenda kinyume na mkataba wake unavyomtaka afanye.
"ni kweli anayosema huyu dada lakini mbona kama anajua vingi kuhusu mimi, yeye ni nani kwani na huyu ndiyo yule niliyekutana naye kule na kuniokoa, mbona ananichanganya sasa?" alijiuliza Chriss. Hakuwa na jibu na kila alipotaka kumuuliza ni kama dada huyo alikuwa akienda na hisia zake kwani alikuja na kumkumbatia kwa nyuma na kumwambia.
"nataka kuona unavyowadatisha wanawake wengi kila kona ya dunia" kisha baada ya kusema hivyo, alimkumbatia kwa nguvu nyuma yake na kumwambia tena.
"ooouh! Nina muda mrefu sana sijapata kugusa joto la mwanaume, leo ni zamu yangu na nataka unifanyie kila aina ya manjonjo hadi nikukumbuke kila wakati" alikuwa akimnong'oneza sikioni ili tu kuziamsha hisia za mwanaume huyo. Chriss hata awe na hasira kiasi gani lakini anapoguswa na kifua laini cha mtoto wa kike, basi hasira zote huyeyuka kama unga wa muhogo kweye upepo. Chriss alishaanza kupandisha joto na mara tu vazi lake likaanza kazi ya kurekodi lakini hapo hapo Catherine, akanyofoa kidude fulani kwenye vazi la Sex machine. (SMC). Catherine alikuwa amemkumbatia Sex machine hapo nyuma kwa makusudi makubwa kabisa. Alikuwa anajua kuwa muda wowote vazi alilolivaa SM, linafanya kazi yake. Joto lilipanda kwa nguvu sana hadi Sex machine akageuka na kutaka kumkamata huyo binti na kumlaza kitandani. Binti huyo akaidaka mikono ya huyo kijana na kuiweka pembeni na kuanza kumpa mate. Alitumia muda wa kama dakika tatu kufanya hivyo hadi SM akapagawa kabisa na kuhitaji kuzitoa nguo za huyo binti kifuani. Binti akagoma na kumrudisha nyuma kwa nguvu hadi sex Machine akashtuka na kupatwa na mshangao.
"mimi ni wako na nakuhitaji kweli boy lakini si sasa" alisema huyo dada Chriss akataka kumfuata kwa kasi kwa ajili ya kwenda kutumia nguvu ili tu kumla uroda. Akili ilishamruka kwa wakati huo, hakuwa yeye kabisa mahali hapo alichokihitaji ni ngono tu na si kitu kingine. Alikuwa hajui pia kama hilo vazi alilopewa alivae, lilikuwa likimrekodi na kurusha picha kwenye ofisi za kampuni anayofanyia kazi. Pia hata hivyo kwa wakati huo alikuwa hajui kama kwa wakati huo, kile kifaa kinachotumika kurusha picha hizo kimesha ng'olewa na huyo dada na kuharibiwa kabisa. Simu yake iliita kwa fujo sana na kumshitua. Ilikuwa imewekwa vibration na kufanya mtetemo wa aina yake kwenye mfuko wa suruali aliyokuwa amevaa. Hapo alikuwa bado yupo na nguo zake za kawaida akiwa hajavua nguo hata moja. Akamtazama huyo binti kwa udadisi wa hali ya juu huku akiwa sasa hana imani naye kabisa. Alipoitazama simu hiyo ilikuwa ni private number. Akaiweka sikioni.
"Sex machine, fanya kila njia umuangamize huyo dada au kama itashindikana potea kabisa mahali hapo, hapo hapakufai kabisa, fanya haraka" ilikuwa ni sauti ya bosi wake. Joesan. Chriss alipoirudisha hiyo simu mfukoni alimfuata huyo dada huku akiwa si yule aliyekuwa amepandwa na pepo la ngono bali huyu alikuwa ni wa kutaka kuuwa. Catherine huo mchezo akaujua tayari, kwani kitendo cha vazi kuanza kurusha picha na kisha kukata ghafla, alijua mapema kuwa kitawachanganya wana kampuni wa huko. Catherine akawa makini zaidi kwani tayari uwezo wa huyo kijana alishaujua na alijua kabisa kuwa kijana huyo anauwezo mkubwa kuliko yeye. Akatakiwa kutumia akili zaidi kuliko nguvu kwani kama ataleta kujua mahali hapo, atafeli na hatobaki hai, tayari kijana huyo bila shaka ameshapewa go aheed ya kuuwa. Chriss alikuja na stail ya karate, akampelekea binti huyo makonde ya nguvu lakini hakuwa amepata hata moja, mapigo yote yalipishwa na kupiga hewa. Catherine akapanda hewani na kudansi kama wale wanawake wa kichina wanavyo dansi kwenye nyimbo zao za asili kisha akashuka na kunyooka kama nyoka wa jangwani na kumpa kijana huyo pigo zito la kushtukiza lakini aliliona akahama kushoto. Pigo hilo likasugua kidogo kwenye paji lake la uso. Catherine akapinduka upande wa pili na kusimama katika mtindo wa kupendeza kabisa. Wakageukiana na kutazamana. Chriss alizunguuka kwa kasi kama kimbunga akiwa anamfuata Catherine kwa kasi sana. Catherine akajua kuwa pigo hilo ni pigo la kifo na mpigaji amedhamiria kuuwa. Akacheza na akili yake kwa haraka sana. Hali ya hatari ilisha jionesha mahali hapo. Alijiandaa akiwa anamsubiri huyo kijana hivyo hivyo. Chriss alipomkaribia Catherine, binti huyo aliruka pembeni kwa haraka sana na kuangukia kitandani. Lakini wakati anaruka pembeni, alifanikiwa kumchoma kijana huyo na kitu chenye ncha kali. Alibingilia kwa haraka sana na kusimama pembeni akiwa na kitu kama kisu mkononi mwake. Chriss akajitazama pale alipohisi pamekwaruzwa na kifaa hicho chenye ncha kali. Damu zilikuwa zikimtoka sehemu hiyo yenye jeraha, alimtazama binti huyo kwa hasira sana na kumfuata kwa kasi ya hatari sana lakini kabla hajamfikia, akaanza kuhisi kizunguzungu, macho yalianza kuhisi giza, hatimaye yalianza kuwa mazito na kujikuta akianza kuona nguvu zikimtoka na mwili kuwa mzito. Miguu ikamsaliti kwa kushindwa ama kukataa kuubeba mwili, akadondoka chini kama mzigo wa mawe, akatulia kimya na kusahau yote ya duniani kwa muda. Catherinr alisogea hadi dirishani na kuchungulia nje kisha akanyanyua simu na kuiweka sikioni.
"fanyeni haraka na muhakikishe mnakuja kama wauguzi kuna kazi natakiwa kuimalizia kwa mtindo huo" alisema na kuishusha simu chini na kumsogelea Chriss, alimuangalia jinsi alivyo lala pale chini na kusema.
"huu ni mwanzo mzuri sasa unarudi kama zamani" alipomaliza kusema hivyo akakumbuka kitu, mh!, akagumia na kusogea tena pale dirishani. Akaona magari mawili, moja likiwa la wagonjwa na jingine likiwa ni gari ya kifahari aina ya Rolls Royce Phantom V12 6.7. Zikiwa zinaingia kwa pamoja ndani ya uzio wa hoteli hiyo. Kila moja ilielekea katika maegesho ya magari na kutoka watu watatu kwenye ile gari ya wagonjwa wote wakiwa ni wanaume. Wakaelekea moja kwa moja kwenye mlango mkuu wa kuingilia ndani ya hoteli hiyo. Wengine wawili wakatoka kwenye ile Rolls, hawa wakiwa ni mwanamke na mwanaume. Mwanaume akionekana ni mzungu na mwanamke akiwa na asili ya kichina au ki korea. Wakionekana kuwa na mshangao mkubwa baada ya kuona wauguzi wakiingia mule ndani wakiwa na machela. Muda wote huo Catherine alikuwa pale pale kwenye lile dirisha akizidi kufuatilia matukio hayo kwa umakini mkubwa kisha akajitoa pale dirishani baada ya kujiridhisha.
"natakiwa kumsaidia huyu kijana kuuwa ili nizidi kuwachanganya wakina Joesan, lazima nihakikishe nauwa wote waliotakiwa kuuwawa. Si katika kazi yangu lakini haina jinsi. Maana ukitaka kumkamata mwizi, huna budi kushirikiana naye. Naanza na huyu Meneja wa hii hoteli kisha anafuatia huyo mwingine. Lazima nianze na huyu meneja maana nataka nikitoka hapa sirudi tena." alisema Catherine na kwenda kukaa kwenye kitanda akisubiri watu wake.
Wale wauguzi walipofika mapokezi, wakazuiwa na kuhojiwa ni wapi wanaelekea na kufanya nini?
"kuna mgonjwa wetu tunamfuata huko juu ni mgonjwa sana na amepoteza fahamu, alikuwa yupo na mkewe kwahiyo tupo hapa kwa ajili yake" walijibu namna hiyo baada ya kuulizwa.
"chumba namba ngapi?"
"chumba namba 26" walijibu lakini badala ya kuruhususiwa, yule binti akanyanyua simu na kupiga mahali.
"njooni eneo hili kuna jambo haliko sawa kidogo" alitoa maelekezo dada huyo wa mapokezi kisha akaendelea kusubiri. Baada ya sekunde kadhaa, askari wawili waliohusika na ulinzi wa hoteli hiyo walifoka nahali hapo. Wakapewa maelezo na kuwageukia wale
jamaa kisha wakauliza.
"kwanini hizo taarifa hazikufika kwenye ofisi zetu kwanza huo siyo utaratibu"
"utararatibu huo ni wa kwenu nyinyi na wateja wenu, sisi hapa tumekuja kwa ajili ya mgonjwa wetu. Na sioni sababu ya kutuchelewesha hapa ikiwa tumesha wapa maelezo tayari" alifoka mmoja wa hao wauguzi akiwa na hasira sana mahali hapo. Akaongezea.
"tambueni kuwa huyo mgonjwa akipatwa na tatizo zaidi, mtawajibika. Msifikirie kuwa huyo ni kama wateja wenu hawa mliowazoea, huyo ni mtu muhimu sana" alipomaliza kusema hivyo, wale walinzi wakagwaya na kuamua kuwapisha watu hao. Walipita kwa kasi sana huku askari hao wakiwa wanafuata nyuma.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
walipofika kule juu wale askari walisimama mlangoni na wale wauguzi wakapiliza hadi ndani ambako walimchukua Chriss na kumuweka kwenye machela hiyo walioingia nayo hotelini hapo.
" hakikisheni anafika shimoni haraka sana na adhibitiwe vizuri kabla hajaamka, akiamka huyo kabla ya kufika shimoni shughuli yake siyo ndogo" alisema Catherine. wale jamaa waliovaa kiuguzi, wakatoka mule ndani. Walipofika chini wakiwa wanataka kupitia kwenye mlango mwingine, wakazuiwa.Wakasimama wakimsubiri mtu huyo aliyewazuia mahali hapo. Alikuwa ni yule mzungu. Alionekana akiwa amekasirika sana huku akiwa na mshangao ndani yake.
"nini kimetokea ndani ya hoteli yangu na huu utaratibu ni wa namna gani?" aliuliza mzungu huyo. Kabla hajajibiwa akamuona mwanamke ambaye alikuwa amevaa kofia kubwa la urembo na mawani ya jua akiwa anafika mahali hapo. Vile alivyo na nguo alizovaa ilikuwa ni vigumu sana kumgundua ni wa kike au wa kiume. Sauti pekee ndiyo ambayo itakujuza kama ukimpa nafasi ya kuongea.
"wewe ni kama nani unayeuliza?" aliuliza Catherine akiwa amejificha kwenye hiyo kofia na mawani kwa ajili ya kuto kujulikana vizuri. Yule mzungu alimgeukia yule mwanamke na kumtazama kwa hasira sana na kujibu kwa jeuri. Alijua kuwa ni mwanamke baada ya mtu huyo kuongea.
"mimi ndiyo meneja wa hoteli hii na ni wajibu wangu kuuliza endapo kama kuna jambo haliko sawa"
"ni sawa na unahaki hiyo lakini si kwa afya ya mume wangu, isitoshe nakushangaa unafoka wakati mume wangu amepatwa na tatizo ambalo halijawahi kumtokea hata siku moja katika maisha yake? Nisikilize vizuri, nina wasiwasi na hoteli yako haiko katika usalama wa afya za watu" aliongea kwa sauti ya juu sana na yeye pia Catherine kisha .....................................
Catherine kisha sauti yake ikabadilika na kuwa kama ya kunong'ona hivi, ilikuwa inzito kidogo na kusema jambo hilo ambalo lilimshtua sana huyo meneja. Alionekana kuwa na hofu sana. Ni tatizo gani hilo lililomkumba huyo mteja wake? Alijiuliza sana pasipo kuwa na jibu zuri. Akiwa bado anazidi kushangaa asijue ni nini cha kufanya kwa wakati huo, Catheri akawageukia wale watu wake na kuwaambia kuwa waondoke na wamuwahishe kwenye matibabu haraka kwani alikuwa na mashaka makubwa sana na afya ya mume wake huyo. Wale wauguzi wakaondoka. Yule mzungu akageuza shingo lake huku na huko kuangalia kama kuna mtu yeyote amesikia hayo maneno kwani endapo kama kuna mtu atakuwa amesikia basi alikuwa na hofu nyingine ya kupata wageni ambao wangekuja kuiukaguzi, hilo likawa ni jambo asilotaka litokee kabisa.
"na...naomba...ka...ma kuna uwezekano tukaliongelee hili jambo kwenye ofisi yangu si hapa kwani hapako kiusalama kabisa mahali hapa" alikuwa mpole kabisa tofauti na alipokuwa akiongea hapo mwanzo, sauti yake ilikuwa imeshuka na akionekana ni mtu mwenye wasiwasi mkubwa. Catherine alimuangalia baba huyo wa kizungu na asiwe na kitu cha kuongeza alijua tayari ameshamvuta mtu huyo kwenye kumi na nane zake na kilichobakia ni kumaliza kazi tu.
"sina imani tena na usalama wangu pia, naweza kumkosa mume wangu mimi" alisema Catherine huku akiwa analia kabisa akionekana ni mtu mwenye uchungu mkubwa. Jambo hilo likamfanya mzungu huyo kuzidi kuchanganyikiwa mahali hapo.
"unataka tufanye nini sasa madame? Niko hapa kwa lengo la kutaka......kutaka kutatua hilo tatizo na inabidi tupate mahali kwa ajili ya kuliongealea hilo swala" alisema mzungu huyo akionekana kuguswa sana na hilo jambo.
"ok, nadhani ingekuwa ni vizuri kama tukizungumzia kwenye gari yangu ama yako kama umekuja na gari" alisema Catherine akiwa katika harakati za kufuta machozi yaliyokuwa yameloanisha mashavu yake. Mzungu huyo alifikiri kwa muda kidogo lakini hakuwa na njia nyingine ya kuchagua zaidi ya hiyo ambayo mteja wake amechagua. Akamwambia kuwa basi waelekee kwenye gari yake. Wakatoka na kuingia kwenye gari ya meneja huyo na kuanza kulizungumzia hilo jambo. Kitu ambacho meneja huyo hakukigundua ni mwanadada huyo kuchezea begi lake la mkononi (hand bag). Yeye alijua kuwa ni maongezi yaliyo na umuhimu mkubwa kutokana na mteja wake kulia kwa kupatikana kwa matatizo ya mumewe na ikiwa ni kitu ambacho ni kigeni sana kutokea kwenye hoteli hiyo. Catherine alikuwa amevaa gloves maalumu kwa ajili ya kazi lakini Meneja huyo alijua labda dada huyo amevaa mavazi ya urembo. Kumbe dada huyo alikuwa kazini na hapo ikiwa ni katika harakati za kutimiza mauwaji. Hapo alikuwa akifungua chupa fulani iliyopo kwenye bag lake hilo, akajimiminia unga kiasi wenye rangi ya manjano. Unga huo ulikuwa ni sumu hatari sana inayouwa kwa haraka sana kama utafanikiwa kuuvuta kwa wingi kwenye mapafu yako. Catherine alipohakikisha kuwa unga huo uko tayari kwenye mkono wake, akaendelea kuonge maneno machache huku hali ya huzuni bado ikiwa machoni mwake. Lakini baada ya muda mdogo mbele, akawa tofauti, akabadili hata sura na maneno aliyokuwa akiyaongea hapo yakampa mshangao bwana huyo. Ghafla, Catherine alimpiga pigo moja kwenye mbavu na kabla mzungu huyo hajatoa ukelele, alimziba pua na mdomo kwa kutumia ule mkono ulio na unga ule wa sumu. Akawa anambana na kumuachia kwa awamu, kitendo hicho kilimfanya mzungu huyo kuivuta hewa kwa nguvu sana mara tu anapoachiwa bila kujua kuwa alikuwa akiiruhusu sumu hiyo ijae kwenye mapafu yake. Hazikupita hata dakika mbili mzungu huyo akatulia.
"inabidi ufe ili tuikamilishe misheni yetu kwa haraka na bila usumbufu wowote. Utanisamehe sana kwa kuyakatisha maisha yako." alisema Catherine na kuzivua zile glove akazitia kwenye bag lake na kutoweka taratibu kwa kujifucha ficha ili asipate kuonekana. Alipofanikiwa kufika barabarani, alitazama saa yake na kugundua kuwa kwa muda huo windo lake la pili liko njiani kuelekea kwenye mkutano kama ambavyo Sex machine alivyopewa maelekezo na mabosi zake. Kifo sasa kilikuwa kinamuwinda Milkao, tajiri na mfanya biashara mkubwa. Catherine alikodi tax na kuondoka eneo hilo kwa kutoa maelekezo wapi anatakiwa aende. Alipofika mbele kidogo, alimuwekea bastola ya kichwani yule dereva na kumtaka aipaki gari hiyo kando ya barabara. Suka hakuleta ubishi mbele ya chuma hicho cha baridi, akasogeza gari pembeni kisha kusimama. Tendo bila kuchelewa, pigo moja zito la kitako cha bunduki lilimuendea yule dereva tax kisha akakaa yeye kwenye usukani. Akaliondoa gari kwa kasi kubwa, kasi ambayo ilikuwa marambili ya ile aliyokuwa akiitumia dereva au mmiliki wa gari ile. Muda mchache tu alikuwa nyuma ya msafara wa mfanya biashara huyo aliyekuwa akielekea mkutanoni. Ulikuwa ni msafara wa magari matatu, aliipiga fimbo gari yake hadi akafanikiwa kuupita huo msafara kisha akasimamisha gari yake kwa mbele. Msafara huo ulipofika hapo ukasimama wakashuka walinzi wa mfanya biashara huyo na kwenda kumkalipia mtu huyo aliyewasimamisha bila mpangilio mahali hapo. Catherin akiwa katika muonekano ule ule wa awali, akawa anabishana nao huku yeye akilalamika kuwa gari yake ilikuwa ni mbovu. Bila kuwa na mashaka na mtu huyo wakiamini kuwa huwenda kweli gari yake itakuwa mbovu, aliwazuga kwa kuwaabia huenda ni mwendo mkali aliokuwa akiutumia tofauti na uwezo wa gari yake. Akawambia watu hao wasubiri ajaribu kuliwasha kama linaweza kuwaka. Wakakubali na kumruhusu mtu huyo ambaye kwa wakati huo alikuwa amevaa koti refu na kofia yake kubwa kama kawaida huku yule dereva wa ile gari akiwa amemlaza vizuri nyuma ili asiweze kuonekana kwa urahisi. Gari hiyo ikawaka lakini pasipo na mataajio yao dada huyo aliirudisha gari hiyo nyuma kwa kasi kubwa na kusimama sawa na gari ya mfanya biashara huyo ambaye muda wote alikuwa akiangalia muda. Kitendo cha kusimama ghafla kiliwashtua sana na hawakukitegemea. Sauti za kutosha za milio ya risasi iliwafanya wakabaki kinywa wazi, kilikuwa ni kitendo cha ghafla sana na hawakuwa wanakitarajia kama kinaweza kutukia mahali hapo, hata walipokuja kutoa mitutu yao ya bunduki, tayari gari ilishageuzwa na kuondolewa eneo hilo kwa kasi kubwa huku nyuma akiwaacha wale jamaa wasijue cha kufanya kwani gari zao zote zilikuwa zimetolewa upepo kwa risasi na bosi wao akiwa na matundu ya risasi kichwani. Walidata, walichoka na hawakujua wakimbize kwa miguu au wapige kelele ya kuwa wamevamiwa na majambazi. Na wangempigia nani hizo kelele ikiwa hapo walipo wapo kwenye mbuga ndogo. Hoi.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"nifungueni hapa kabla sijafanya kitu kibaya, nasema nifungueni" alipiga kelele Chriss mara baada ya kuzinduka kutoka kwenye usingizi wa nusu kifo. Alikuwa akipiga kelele bila kujua anampigia nani kwani hapo alipokuwa amefungwa hapakuwa na mtu hata mmoja, alikuwa mwenyewe tu ndani ya chumba hicho ambacho hakikuwa na vitu vingi zaidi ya kiti chake alichofungiwa nacho.
Muda ulikuwa umekwenda sana na muda huo ikiwa tayari imetimia saa mbili kasoro za usiku. Nchini Tanzania ndani ya mji wa Morogoro, mr. Kim alikuwa amekaa kwenye luninga akiafuatilia habari kwenye kituo kimoja cha kimataifa kilicho kuwa kikirusha habari za moto, yaani habari zulizotokea punde. Alijikuta akiwa na furaha kubwa mara tu alipopata taarifa za vifo vya watu wake. Habari hiyo ilikuwa inasema kuwa 'MUUWAJI ASIYEFAHAMIKA AVAMIA MIAMI.' Asababisha vifo vya watu watatu, viwili vikiwa vimetokea kwenye hoteli tofauti na kimoha cha tajiri mkubwa na mfanya bishara maarufu, kikiwa kimetokea barabarani wakati mfanya biashara huyo akiwa anaelekea katika mikutano yake ya kibiashara. ilikuwa ni shangwe kubwa sana kwa Kim tena kusikia kuwa ni muuwaji asiyefahamika, hilo lilikuwa ni jambo ambalo hakuwahi kulitegemea kabisa kama atakuja pata muuwaji hatari kiasi hicho, furaha yake ikamfanya hata asiwe na muda tena wa kuangalia mwishilizio wa habari hiyo ambayo ilimuonesha mtu ambaye hakufahamika. Yaani mwanamke si mwanamke na mwanaume si mwanaume.
"D.A, zamu yako ndiyo inayofuatia mshenzi mkubwa wewe, huwezi kunifanya nikaishi bila amani na nina hakika utakufa tu na ukifa wewe hakuna kima yoyote atakaye nigusa, ha ha haaa!" alisema hivyo Kim na kuangua cheko kubwa sana. Lakini wakati yeye anasema hayo na kucheka, Father D.A alikuwa akitabasamu na kuzungumza maneno nachache tu kwa utaratibu sana.
"kwanini huendi kinyume na maamuzi yako wewe binti?" alijiuliza hayo father baada ya kumuona yule anayesadikika kuwa ni muuwaji, ambaye hakuwa ameonekana sura hata nusu na hakufahamika hata kidogo. Alifanya hayo yote kitaalamu sana.
Kwa kim kulikuwa ni furaha tu na majira hayo hayo, alimpigia simu Joesan na kumpa hizo habari za kuwa Chriss yupo hai na amefanikisha kufanya mauwaji ya watu aliotaka wauwawe, laiti kama angejua kuwa aliyefanya mauwaji yale ni binti hatari wa hasimu wake mkubwa toka zamani bwana D.A. Laiti kama angelijua hilo, sijui angetapika au sijui angefanya nini. Joesan alizipokea taarifa hizo akiwa haamini kabisa maana tangu hapo alijua kuwa kijana huyo yupo kwenye mikono ya watu makini na hatari hivyo hata afya yake ilikuwa mashakani. Alizichukua taarifa hizo kama zilivyo na kumjulisha kila mwana kampuni ile hasa wale wa kitengo chao. Taarifa hizo zikapokewa vizuri na kila mfanya kazi lakini Tai akajua kuwa hata kama akiwa hai huyo SM basi ana kazi ya kuunda tena vazi jingine maana hilo halitakuwa vazi tena. Taarifa hizo zilipofika kwa mzee Rafael hakushangaa sana na kuwaambia hata yeye amezishuhudia kwenye luninga. Furaha ilikuwa kubwa kweli kwa kuwa hai kwa SM lakini walakini na sintofahamu, ilikuwa kwa mzee Rafa. Hakuamini hata kidogo kama aliyefanya mauwaji yale ni SM. Hakuwa na imani hiyo hata kidogo kwani kila alivyomuangalia muuwaji huyo anayehisiwa na jeshi la polisi la nchi ya marekani, alibaki na maswali, alikuwa hafanani hata kidogo na umbo la SM. Hata kidogo. Alitabasamu kwa chati na kujikohoza kidogo akitoa harara kwenye koo lake kisha akatulia kitini.
"wanasheherekea pasipo kujua ni nani aliyefanya hayo. Mbona mimi sina imani kabisa na hiyo habari, mbona SM hapatikani hewani au ndiyo alipoteza simu kwenye mapambano, Chriss ninayemjua mimi. Haya basi kama amepoteza simu kwenye mapambano mbona hata mtandao ukimtafuta kwa kutumia kifaa maalumu alichowekewa kwenye vazi lake ..........
pia hapatikani. Inamaana kuharibika kwa vazi ndiyo kuharibika kwa kifaa cha GPS? Wajipange, wajue wapo na mtu makini sana anayewafuatilia na kama ni hivyo tumekwisha au tutakwisha wote" aliwaza mzee huyo kwa kujiuliza wingi wa maswali. Rafael hakuwa mtu wa mchezo mchezo ni mzee asiyependa ujinga kabisa na haamini jambo kirahisi.
"nilikuwa mafia tangu nikiwa kijana mdogo hivyo najua mbinu nyingi sana za ki mafia, natamani kuwafumbua macho hawa wajinga lakini sijui dhamira ya huyu mkorea ndani ya Taifa langu. Kama ameweza kuwaharibu vijana wengi kuwa mashoga, hashindwi kuliteketeza Taifa hili. Nasema sijui anampango gani na Taifa langu la hapo baadaye nachelea kusema kuwa naweza kuwa nimechangia kuliharibu Taifa langu mwenyewe kisa pesa. Hapana sitaki kuchangia kuliuwa Taifa langu mwenyewe kwa kufuata matakwa ya mgeni. Japo nimefanya uharamia sana na mauwaji ya kutisha, sasa inatosha, siko radhi tena. Kwa macho tu matendo yake yanajionesha kuwa, hadi hapa alipofikia, hana nia nzuri na Taifa hili, ni vijana wangapi wa kiume ambao walitakiwa kuwa na wake zao na kujenga familia, leo hii wamekuwa mashoga kupitia yeye. Nani ataamini kama kijana Chriss alikuwa ni msomi mkubwa mwenye shahada ya sayansi ya kompyuta, angalia alivyomgeuza kuwa mashine hatari ya ngono na kifaa kibaya sana cha kufanya mauwaji. Niko tayari kuuwawa na hao walio na mpango mzuri na taifa hili kama wataamua kututeketeza wote lakini si kumfungua masikio Mr. Kim." aliwaza mengi sana mzee Rafa kisha aliamua kuzima luninga yake na kuingia chumbani na kwenda kuukabidhi mwili wake kwenye kitanda ili kuupitisha usiku huo.
**********************************************
"ooh! Vizuri sana boy kama umeamka, habari yako?" aliongea Catherine akiwa ameingia ndani ya chumba hicho tena akiwa na yale mavazi yake ayapendayo. Alikuwa amevaa bikini nyekundu kama kawaida na akiwa mbele ya kidume hicho cha kazi.
"nimeamka ndiyo na nataka unifungue hapa niondoke kistarabu tu" alijibu Chriss akiwa na ghadhabu za kuzidi.
"huwezi kufunguliwa hapo kirahisi hivyo na ukitaka kuondoka kistarabu utaondoka tu na tutaondoka wote, sory" alijibu Cathetine.
"aisee nitawauweni kama ugonjwa uliovamia mifugo" aliongea SM lakini hakuna aliyemjibu tena mahali hapo. Badala yake Catherine alimgeukia kijana mmoja na kumwambia kuwa amchukue huyo SM na ampeleke kwenye chumba cha kazi. Kijana huyo akatii, akasukuma kiti hicho alichofungiwa SM huku yeye akiwa anafuata nyuma. Alipofika huko ndani kwenye hicho chumba, akaomba aitiwe dokta. Baada ya muda mfupi daktari alifika hapo na kusimama mbele ya dada huyo.
"Chars nadhani mtu mwenyewe ni huyu hapa, anatakiwa kufanyia kazi ili arudi kwenye hali yake ya awali" aliongea hivyo na kumtazama Chriss usoni. Chriss alikunja sura na kuvimba kabisa.
"mnataka kunifanyia nini nyie watoto wa changudoa?" aliuliza.
"tunataka kukufanya uwe mtu tena Chriss"
"mmeambiwa na nani kuwa hapa nilipo ni mnyama?"
"huwezi kujitambua hata kidogo kuwa uko katika hali gani kwani hata kichaa hajitambui kuwa yeye ni kichaa bali anayemtazama na kumshangaa ndiye anayemuona ni kichaa huku yeye akijiona ni mzima wa afya kabisa.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"upo katika matatizo makubwa sana Chriss" alisema Catherine. Hili jina Chriss ndilo lililokuwa likimuumiza kichwa kijana huyo. Kwake ni mara ya pili sasa analisikia tena likitajwa na watu wawili tofauti, mmoja akiwa ni Suzane na wa pili ni huyo binti asiyemuelewa ni nani kwenye maisha yake. kwani amekuwa akikutana naye mara kwa mara na kumuokoa pia kwenye matatizo, alijiuliza sana kuhusu huyo binti lakini hakuwa na namana. Alikuwa hajitambui na alishapandikizwa sumu ya ubishi mwilini mwake.
"sitaki chochote kutoka kwenu, naomba mniachie kwa upole tu niondoke zangu, nawaahidi kuwa mkiniachia kwa upole, sitawauwa hata mmoja lakini mkikaidi ni wazi hakuna atakayenizuia mimi tena kuwauwa ninyi" alizidi kuwaka kijana huyo.
"sikiliza Chriss, wewe hapo ulipo huwezi kutoka hadi utakapokuwa sawa ndipo utakuwa na ruhusa ya kutoka, hivi ni mwanadamu gani anayejitambua, anaweza kufanya mapenzi hadharani kama mnyama huku akiwa amezunguukwa na watu, ni kiumbe wa namna gani wewe usiye na maamuzi yako bali unaishia kuendeshwa tu kila siku na hao unaowaita mabosi zako." aliongea Catherine kwa hisia kali sana lakini ni kama alikuwa akitwanga maji kwenye kinu au ni sawa na mtu anayempigia Mbuzi gitaa kwa kutegemea Mbuzi huyo anengue.
"ni wazi hakuna kiumbe yeyote mwenye akili timamu anayeweza kufanya hivyo ila kwa mimi chizi na nisiye na akili ni kawaida sana na naifurahia kazi yangu na unabahati sana wewe malaya, ningekunyonya hadi visivyo nyonywa maana nilikupania kupita kiasi pengine hata....!" hakufika hata mwisho wa kauli yake, konde zito likamuangukia Chriss, damu zikamtoka mdomoni, yalikuwa ni maneno yenye kuumiza sana. Catherine alinyanyuka hapo akiwa anafuta machozi na kwenda kwenye kioo kikubwa na kukiwasha kioo hicho, ilikuwa ni luninga kubwa. Picha mjongeo zikaanza kuonekana , alioneka kijana huyo akiwa anafanya mapenzi hadharani huku akiwa amezunguukwa na watu wakimtazama. Hadi pale alipomaliza na kupigiwa makofi kisha akaonekana akifanya mapenzi na wanawake si chini ya kumi na wawili, wote akiwaingilia kwa njia tofauti halafu luninga hiyo ikazimwa. Baada ya kuizima luninga hiyo, Chriss aliangua kicheko kikali sana alicheka huku machozi yakimmwagika, alikuwa amechanganyikiwa kijamna huyo. Hakuamini kama kazi ile aliyokuwa akiifanya ilikuwa iko katika rekodi. Inamaana hakuwa akijificha chumbani na mambo yakaishia chumbani, kumbe hadharani, mitaani itafikia hatua watu wataangalia ujinga na ushenzi ule aliokuwa akiufanya. Alimkumbuka Sauda mpenzi wake. Ni vipi kama Sau wake ataona hizo video. Ni wazi zile ndoto za kuwa mkewe zitanyakuliwa na upepo mithili ya kifaranga cha njiwa kibebwavyo na kunguru na kukiachia kutokana na kushindwa nguvu ya kukibeba kifaranga hicho kisichojua kutumia mbawa zake kuruka. Hebu fikiria kifaranga kiachiwe kutoka umbali wa nguzo ya umeme halafu kiangukie kwenye jiwe kama si lami. Ni wazi penzi lake litakufa kifo kibaya sana. Alicheka sana Chriss mwishowe akalia kabisa. Usiombe kufikia hatua ukacheka kicheko cha namna hiyo, kicheko kikali chenye maumivu, kicheko kinachodhihirishwa na sauti tu lakini moyo na sura zikiwa zinalia kwa uchungu mkubwa. Chris alijikuta kwenye maumivu makali mno ya moyo. kicheko kile kilimliza hadi Catherine mwenyewe mahali hapo.
"madame, anaweza akapata matatizo ya ubongo kutokana na kuzidiwa na mawazo, tumchome sindano tu kama vipi?" alisema dokta Chars.
"najua Chars kuwa wewe ni dokta na ndiyo maana umeliona hilo na mimi nataka nimchanganye zaidi akose kabisa neno la kusema ndipo tutafanya yetu." alisema dada huyo huku akiwa anafuta machozi.
"ok" alijibu Chars.
"nyie malaya nitawauwa kama jinsi ninavyo lichana karatasi, tafadhali nifungueni niondoke, hasa wewe malaya wa kike mwenye nyeg*, usiponifungua hapa nitahakikisha unalala na mimi kwa siku tatu mfululizo tena ukiwa maiti yaani nakuingilia hivyo hivyo ukiwa wa baridi mjinga wewe, unafikiri nipo hapa kwa ajili ya k*m* yako peke yako" maneno hayo yalimfanya Catherine awe kama amepigwa na shot ya umeme, kifua kilimpanda juu na kushuka chini kutokana na ghadhabu zilizomjia ghafla, alimsogelea kijana huyo akamshushia makonde mazito hadi akazuiwa na Chars.
"basi muache madame, hatuendi hivyo na siyo lengo la kumuweka mtu huyo hapa"
"haiwezekani Chars, mtu upo kwa ajili ya kumsaidia halafu anakudharau, anakutukana, inauma sana." alisema Catherine.
"sawa lakini hata kama utampiga hadi kufa, huwezi ukalibadilisha tusi au matusi aliyokutuakana kuwa salamu, hayo ni maneno na yamesha toka tayari." alizidi kusihi Chars.
"unanijua mimi ni nani wewe, unanijua mimi, hivi unajua kama mimi ndiye niliyebeba historia nzima ya maisha yako. Hujui ndiyo maana una kiburi, nimeuwa Meneja wa hoteli ile ambayo tulikutana mimi na wewe hii yote ni kutaka nikufikishe kwenye historia ya maisha yako na kuwamaliza wabaya wako ambao wewe unawaabudu. Nimemuuwa Milkao tayari" aliongea kwa hasira kuu Catherine tena akiwa anafoka kabisa. Maneno hayo yakamfanya Chriss kutoa macho, hakutegemea kama kazi aliyoambiwa aitekeleze, dada huyo ameifanya.
"inamaana amenisaidia kufanya mauwaji, ni nani huyu dada, mbona kila wakati ni mtu wakunisaidia tu. Historia, historia ya maisha yangu? Ni kweli sijifahamu? Lakini mbona anajua mengi sana yanayonihusu mimi? Ni nani kwani huyu binti?" alijiuliza mawazoni kijana huyo lakini akiwa anahangaika angalau apate hata jibu moja la maswali aliyojiuliza, Catherine akaendelea.
"kazi ya kusafirisha mzigo wa madawa ya kulevya utaifanya wewe na hapo ndipo utakapomjua baba yako ni nani. Najua hata sura ya baba yako huijui hapo ulipo, unamjua baba yako wewe? Unamjua baba yako nakuuliz........!!?
" inatoshaaaaaa! Inatosha, basi inatoshaa. Nifungulieni hapa niwauwe, nifungulieni nasema na nitawauwa wote halafu na mimi najiuwa nifungulieni!!" alikuwa akipiga kelele bila mpangilio ni wazi sasa yale maneno yalimuingia na yalikuwa yanaukweli ndani yake lakini hakuwa akijitambua hakujua kwa nini ana moyo wa namna ile, moyo usiokubali kujitambua yeye ni nani, kweli alikuwa akimaanisha kuwa hakuwa na haki ya kuishi tena na aliona ni bora kufa tu kabisa. Hapo ndipo alipokuwa akipasubiria Catherine.
"mchome sasa hiyo sindano na tumpeleke kwenye mtambo" aliongea na daktari akafanya yake alichukua chupa ya dawa na kuichanganya kisha akaivuta kwa bomba la singano na kumchoma kijana huyo. Baada ya sekunde kadhaa, usingizi ukamkamata, wakamfungua zile kamba na kumvua nguo zote kisha walimlaza kwenye kitanda cha matairi na kumpeleka kwenye mtambo.
"madame huoni noma kumtazama kijana huyu akiwa mtupu bila nguo?" alitania daktari. ............................
Catherine akatabasamu na kuzidi kumtazama kijana huyo alivyo mzuri wa maungo.
"tena hakikisha anakuwa kama zamani nina mpango naye mkubwa sana hapo baadaye" alisema Catherine akiwa amezidi kutabasamu. wakafika mtamboni. Wakampandisha kwenye kitanda cha chuma, kitanda hicho kilikuwa ni sawa na kile alichotengenezewa SM japo hiki kilikuwa mfano wa sanduku la duara na lilijengwa kwa kioo kigumu sana kiasi cha kumuona mwili mzima mtu akiwa ndani ya sanduku hilo. Walipomuweka hapo, sanduku hilo likajifunga kisha daktari huyo akavuta kiti akaka na kukipampu, kikapanda juu taratibu kiti hicho hadi kikawa usawa na kompyuta kubwa inayotumika kuendeshea mtambo huo. akawasha hiyo kompyuta na kuisubiri ijifungue yenyewe na kujiweka tayari kisha akaingiza nywila na kuanza kazi ya kuichezea compyuta hiyo. Kitanda kile kilichokuwa kimeubeba mwili wa Chriss kilizunguuka kwa mzunguuko wa kwanza ,pili na tatu na kila mzunguuko uliokuwa ukizunguuka ulikuwa ukienda na kasi yake hadi unafika mzunguuko huo wa tatu, kasi ilikuwa kubwa sana kisha kikatembea na kwenda kuingia ndani kabisa ya mtambo huo. Kila alipokuwa akibonyeza vitufe vya kompyuta hiyo, ndipo mitambo hiyo ilivyozidi kujikonecti. Akaanza kubonyeza vitufe kadhaa, hapo sasa mambo ndipo yalipoanza kuwa magumu, chumba kizima kiliwaka taa nyekundu zilizokuwa zikiwaka na kuzima huku zikitoa mlio wa alarm za hatari. Dokta Chars alikuwa amechanganyikiwa, alibonyeza kila kitufe kwa haraka sana lakini mambo yalikuwa magumu haswa.
"vipi Chars?" aliuliza Catherine.
"amewekewa kitu cha hatari sana kwenye ubongo wake, kitu hicho ndicho kinacho contral akili yake kwa sasa na hata kama ungekuwa ukiongea naye kwa kipaza sauti bado tusingeweza kumbadilisha. Kinatumia mjongeo wa mapigo ya moyo na kuchukua taarifa ubongoni kisha kuzichuja." alieleza Chars.
"kwaiyo hicho ndicho kinachosababisha hii hatari inayojionesha?"
"ndiyo, kwani pia ni mtego mbaya sana wa kuweza kumuuwa wakati wowote na muda wowote watakapo hitaji. Kinauuwezo wa kuibana mishipa ya damu yote inayopeleka damu ubongoni na ikasitisha zoezi hilo la kusafirisha damu kwa harka mno, kitu ambacho kingeleta zaidi ya madhara. Huyu walimtengeneza lakini walikuwa na wasiwasi naye huwenda angewageuka hivyo, wamemuwekea kifo kibaya sana ambacho ni kwa sekunde tu kinaweza kupasua kichwa chake. Hapa niliingia katika program ya kuweza kukitoa kitu hicho kwa kukivuta karibu na mshipa mkuu wa damu ili tuweze kukinyonya kwa bomba la sindano, ndiyo maana kikanitahadharisha. Ni kidogo sana kama kipande kidogo cha punje ya mchel............! My god!" alistaajabu Chars baada ya kompyuta yake kumuandikia neno Danger kisha kuweka alama nyekundu kama mshale kuelekea kwenye sanduku lililokuwa likionekana hapo kwenye kioo cha kompyuta yake. Akabonyeza kitufe kingine, ikamuandikia Wait kisha kikaweka giza kioo kizima. Chars akabaki kushika kichwa huku Catherine akiwa mdomo wazi, hapo neno Mungu nisaidie likatawala. Kompyuta ilikaa hivyo kwa muda wa dakika tano kisha ikawaka na kuandika neno Continue huku ikimtaka abonyeze inter, akafanya hivyo na muda huo huo taa zile nyekundu zilizima na kwenye kioo cha kompyuta kukakaa mistari miwili mwekundu na manjano kisha ule wa manjano ukaondoka na kubaki mwekundu. Ule mwekundu ukawa unasogea taratibu na nyuma kuchora kijani.
"tumefanikiwa" alisema Chars huku akimuangalia Chriss kupitia kioo, akamuona bado anapumua.
"duh! Afadhali maana nilikuwa nimeshaanza kuandaa machozi, kwahiyo atachukua muda gani hadi kuwa yari?" alisema Catherine na kuuliza.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"atachukua muda wa masaa manane kwa mujibu wa mashine yangu hapa"
"si unasema kuwa huo mstari mwekundu ukiisha ndiyo kazi imekwisha, sasa mbona unaniambia masaa manane tena na ikiwa unatembea kwa kasi hivyo."
"ukifika katikati huo mstari huta tamani kubaki humu ndani utakwenda taratibu sana" aliongea daktari na kuendelea na kazi yake kama ada. Mara wakiwa bado wana piga stori, kuna mtu aliingia humo ndani na kusema.
"madame, njoo kwenye ofisi yangu kuna jambo haliko sawa na linanichnganya" Catherine hakungojea, alitoka humo kwenye hicho chumba cha mitambo na kuelekea huko alikoitwa.
"wameshajua kuwa mauwaji yale yalifanywa na mtu makini sana hivyo serikali imeamua kuweka watu makini kumfuatilia mtu aliyesababisha mauwaji" alisema kijana huyo aliyefahamika kwa jina moja la Amiri mara baada ya Catherine kufika kwenye ofisi yake.
"mbona sikuelewi unachokimaanisha Amiri, wamegundua nini?" aliuliza Catherine kwa kutokuelewa na mshangao wa aina yake.
"nadhani unajua Madame kuwa kamera zetu za ulinzi nimeziunganisha na system ya kamera za CCTV za jiji hili"
"najua!" akajibu Catherine na kumfanya Amiri kijana makini anayeijua kuichezea compyuta kama ana lana nayo, kuendelea kusema.
"kuna wapelelezi kama watatu au wanne wanafuatilia hili tukio la mauwaji."
"umejuaje Amiri?" Catherine akadakia kwa swali la kushtukiza.
"tazama hapa kwenye kioo cha hapo juu, unamuona huyo jamaa aliyevaa koti jeusi?"
"ndiyo nimemuona" alijibu Catherine baada ya kuyahamishia macho yake kwenye kioo cha kompyuta kubwa.
"sasa kuna huyo halafu kuna huyu hapa mwenye shati la drafti kisha huyo mwenye nguo nyeusi tupu kama anakwenda msibani nadhani wote umewaona vizuri?"
"ndiyo, Amiri nimewaona" alijibu Catherine, Amiri akaendelea kusema.
"nimekamata harakati zao kupitia kamera zangu na kilichofanya niwagundue kuwa wanafuatilia muuwaji, ni kuchunguza alama muhimu alizoacha muuwaji"
"unasemaje Amiri? Kwaiyo inakuwaje?" aliuliza akiwa katika taharuki kubwa Catherine.
"wanafuatilia hizi picha zilizopigwa na kamera zao za ulinzi na kwa bahati nzuri hawaja pata sura yako halisi, hapo hata mimi nikupe pongezi kwani hata vyombo vya habari vilivyorusha matukio ya mauwaji sambamba na picha ya wanaemhisi kuwa ndiye aliyesababisha mauwaji hayo, hakuweza kuionesha sura yako na pia hawana uhakika kama muuwaji ni mwanaume au mwanamke. Picha wanazozifuatilia hata mimi ninazo na hazita wasaidia sana kwenye upelelezi wao ila kinachonitia wasiwasi ni kufuata hatua zako kupitia uelekeo wako"
"hapo hata mimi ndipo panapo nichanganya Amiri, itakuwaje sasa na ndiyo kwanza Chriss yupo kwenye mtambo na mtambo huo unamaliza kazi baada ya masaa nane?" aliuliza Catherine akiwa amekusanya lundo la hofu na kuto kuelewa. Kijana Amiri akashusha pumzi ndefu na kusema.
"wamefikia hapa kwenye hii hoteli inayotoa huduma za asili ya wahindi. Hapa ambapo ulitelekeza lile gari baada ya kutoka kufanya mauwaji ya yule mfanya biashara, wameiona hiyo gari na hapa ndiyo wamechoka. Wamewasiliana kisha bilashaka wakakubaliana wapumzike. Kwaiyo huyu mwenye koti jeusi, ametulia kwenye hoteli hii na hawa watatu sijui wawili wapo kwenye hoteli moja. Sioni wakim
jongea tena, bila shaka watalala hapa ili kesho wavamie huku tulipo"
"inamaana wamesha gundua kuwa tupo huku?" akauliza Catherine.
"hapana hawaja gundua ila kesho ninaimani kuwa watafika hapa kwa sababu kuna kamera tatu za mwisho za CCTV kutoka hapo walipo hadi hapa na ninaimani lazima watajua kuwa ni njia ipi uliyopitia, hiki ndicho kinachofanya niamini kuwa kwa kesho tutavamiwa bila chenga." alipomaliza kusema hivyo Amiri, Catherine alihema kwa nguvu hadi kifua chake kikapanda na kushuka. Alikuwa na hofu kubwa sana na maisha ya Chriss kwani kitendo cha kumtoa kwenye mtambo uliokuwa ukirudisha akili yake, ni kumfanya kijana huyo kuwa chizi mazima. Alifurahi sana kusikia kuwa kunauwezekano wa watu hao wanaodhaniwa kuwa ni wapelelezi, kufika siku inayofuata. Alimgeukia tena Amiri na kumuuliza.
"kutoka hapo hadi hapa wanaweza wakachukua muda gani?"
"ni muda mfupi sana lakini nadhani hadi ikifika majira ya saa moja na nusu au mbili kasoro, watakuwa hapa"
"wametukosa." alisema Catherine akiwa anajiamiani sasa na kumfanya Amiri abakie na tabasamu usoni.
"hakikisha unazidi kuwafuatilia ikiwezekana hata usilale kabisa, utakwenda kulalia kwenye ndege. Fuatilia nyendo zote za hao jamaa hatua kwa hatua, hapa sisi ikifika kesho saa moja kamili tutakuwa hatupo. Ngoja nikawashtue Zomba na Jay wajiandae pia nijue kwa upande wao ni vipi wamejiandaa" alisema Catherine na Amiri akajibu poa. Catherine akatoka mule ndani na kuingia kwanza kwenye chumba cha kubadilishia nguo kisha akatoka na kuelekea kunako chumba cha hao vijana. Ulikuwa ni muda wa jujiandaa kwani muda wowote wangeweza kuvamiwa.
"niambie Zomba?" alisalimia mara tu baada ya kufika hapo.
"tuko safi madame vipi maendeleo yanavyokwenda?" alijibu Zomba na kurudisha tena salamu kwa dada huyo.
"huko yanakwenda vizuri ila ni maandalizi ya kutimka hapa ifikapo kesho mapema kwa sababu wapelelezi wameshamwagwa kila kona na wanatufuatilia, hofu yangu ni kwamba tusije tukaishia kwenye mikono yao ikawa noma. Tanzania haita tuelewa kwa kufanya mauwaji ya watu wasio na hatia, serikali yetu haitajua kuwa tunampango gani wa baadae na taifa letu na badala yake watatuona ni magaidi. Vipi gari ya kututoa hapa shimoni iko poa?"
"kwa hilo usitie shaka madame mtoto yuko safi na hapo alipo miguu inamuwasha kwa safari" alijibu Jay na kumfanya Catherine kuwa na amani. Akamalizia.
"jiandaeni kwa safari kuanzia sasa hakikisheni hakuna harufu yenu itakayo bakia humu na kuwapa mwanga hao paka ya kutufuatilia, nadhani mnajua kuwa wapelelezi wa nchi hii wakoje?" alipomaliza kuwauliza swali hilo baada ya kuhitimisha, vijana wakamtoa wasiwasi kisha wakatoka hapo na kwenda kuweka mambo yao katika hali ya usawa huku Catherine akirudi kwenye chumba cha mitambo.
"Chars, hebu angalia kwenye kioo cha hiyo compyuta hapo naona kama huo mstari umesimama?" aliongea Catherine baada tu ya kuingia humo ndani...................
"nilikuambia madame kuwa ukifika katikati huo mstari utachukia hata kuutazama. Hapo ulipo unakwenda ila ndiyo unakwenda taratibu mno." alijibu Amiri huku akiacha kazi aliyokuwa anaifanya mahali hapo.
"nenda kalale tu madame hapa kila kitu kitafanyika, hakuna sababu ya wewe kuwepo mahala hapa kwanza ulikuwa na kazi ngumu sana leo"
"ni kweli Amiri lakini sidhani kama nitapata usingizi, natamani huyo kijana atoke hapo hata sasa hivi, ameteseka sana isitoshe tayari wapelelezi wa nchi hii wanajaribu kupita nilipopita, bilashaka kesho watakuwa hapa"
"unasemaje madame?" aliuliza kwa kushtuka Chars.
"ndiyo hivyo Chars" alisema dada huyo.
"asante kwa kunifumbua, hawakuti kitu hapa hiyo kesho" alisema, akavuta hewa kidogo kisha akasema tena.
"usijali madame kwa imani na uwezo wa Mungu, hapa hakuta haribika kitu na atarudi kama alivyokuwa mwanzo."
"sawa lakini kiukweli nitabaki na wewe hapa na sitaweza kwenda kulala hata kidogo"
"sawa lakini inabidi utazame pembeni maana ukiutazama huu mstari utazidi kukuchanganya na kukupa usingizi" aliongea Amiri na kumfanya Catherine kucheka. Walikaa hapo kwa muda mrefu huku kila mmoja akiwa na shughuli yake kwenye compyuta yake. Hakuna aliyekuwa akimsemesha mwenzake. Muda mfupi mbele, kimya kikatanda kabisa kwani tayari binti huyo alishapitiwa na usingizi mahali hapo.
"mapenzi ni kitu kizito sana na usiombe mapenzi yakaushambulia moyo wako kwa kasi ya namna hii, yaani hata kwenda kulala hataki. Anaonekana anampenda sana huyu kijana japo sina hata historia yao, lakini hapa bila kificho kuna mapenzi ndani yake." alisema Amiri na kutabasamu kisha akageuka na kuitazama Compyuta yake kubwa inavyofanya kazi.
Asubuhi kulipokucha, bado mawasiliano ya Sex machine yalikuwa ni magumu sana. Saa kumi na mbili Joesan alikurupuka kutoka kitandani na kumruka Merina kisha akaikamata simu yake na kumpigia kijana huyo, majibu yalikuwa ni yaleyale ya jana kuwa namba hiyo ilikuwa haipo hewani alichoambiwa ni kuacha ujumbe ili anayempigia akiwa hewani aukute ujumbe huo. Joesan alitamani simu yake aipige chini kwa ghadhabu. Hiyo ilikuwa ni too much sasa kwa kijana huyo kutokuwa hewani kwa muda wa siku nzima. Hata kama atakuwa amekamilisha mauwaji lakini ndiyo asipatikane.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"atakuwa ameuwawa nini na yeye mbona kama moyo wangu hauko na amani" alijisemea kwa sauti kubwa pasipo kutarajia kabisa.
"ondoa shaka my dear, hawezi kufa kirahisi hivyo yule ni mtu makini sana, subiri tu atakutafuta" sauti kutoka kwa Merina ambaye alikuwa akibingilia kitandani, ikamshtua. Joesan akageuka na kumtazama binti huyo ni kama hakujua anaongea kitu gani. Aliwaza mengi sana bwana huyo. Kwanza ni huwenda Sex machine ameuwawa, pili labda huwenda ametekwa na kuingia kwenye mikono ya watu wasioleweka na tatu au labda atakuwa ameumia vibaya na kushindwa hata kutembea. picha zote hizo asizozipenda zilimjia kichwani mwake.
"ni bora basi angekufa akiwa tayari ameshasafirisha ule mzigo kuliko kufa akiwa hata mzigo hajausafirisha. Nimepoteza pesa nyingi sana kwa kutegemea kuingiza mabilioni ya shilingi kama ule mzigo ungefika nchini Brazil. Hawata nielewa hawa jamaa kama atakuwa amekufa huyu mpuuzi. Usife leo Sex machine, kufa baada ya kurudi Brazil. Kufa ukiwa tayari umeniweka kwenye kilele cha kuwa bilionea mkubwa kabisa Afrika nzima. Ndiyo utakufa Sex machine na utakufa kwa mikono yangu pindi tu nitakaporidhika na kile ulichoniingizia lakini si leo. Najua hadi utakapokufa, utakuwa unapesa nyingi sana kwenye akaunti yako ambayo kampuni inakulipa. Hizo zote zitakuwa chini yangu." aliwaza Joesan akiwa ameikamata simu yake mkononi kama vile anaesubiri simu itakayoingia. Akajaribu tena kupiga lakini hakuna kilichobadilika kamwe.
Wakati Joesan akiwa anawaza muda huo wa saa kumi na mbili asubuhi, huku mambo ndiyo yalikuwa yanawamba.
"wamebakisha mwendo mfupi tu hadi kufika hapa na wanakuja kwa kasi sana bila shaka wameshajua kuwa tuko hapa." alisema Amiri akiwa anaitazama kompyuta yake. Muda huo huo Chars akaingia ndani hapo akiwa na Chriss tena akiwa mpole sana na mtu anayeshangaa ni mahali gani alipo.
"kijana yuko tayari madame" alisema Chars.
"ok. well done, Chars. Hatuna muda tena hapa mambo yamesha haribika. Zomba na Jay nendeni mkaandae gari tafadhali, wamefikia wapi kwa sasa Amiri?" aliongea mambo mengi kwa wakati mmoja, alitoa maelekezo kwa vijana wake na kuuliza hili na lile.
"wamebakisha kamera moja tu ya ulinzi na muda wowote nitakuwa siwaoni hiyo itamaanisha kuwa watafika hapa ndani ya dakika arobaini na tano." alisema Chars akiwa ananyonya kitu fulani kwenye kompyuta yake na kuiacha iendelee kunyonya.
"haribu system zote na kila kitu, hakikisha tukitoka hapa shimoni na shimo nalo linadidimia, hawatakiwi kujua kabisa kama kuna watu walikuwa wakiishi hapa au kuna kitu kilikuwa kinaendelea mahali hapa na wakijua basi wakute emty hakuna hata harufu yetu" alitoa maelekezo Catherine. Muda wote huo Chriss alikuwa kama haeliwi kilichokuwa kinaendelea mahali hapo. Alijiona kama mgeni vile. Alikuwa akikumbuka mengi sana yaliyopita na mara ya mwisho alikuwa katika kampuni ya Joesana akiwa amekubali kuwa Sex machine pasipokujua kama alikuwa amekubali kubadilishwa akili. Kitendo cha kujikuta hapo, kilikuwa kikimpa maswali mengi sana na hakuwa na muda wa kuuliza kwani kila mtu alikuwa busy mahali hapo.
"yes, nimemaliza kuchukua silaha zangu za kazi kwenye kompyuta sasa naangusha system zote chini" alisema Amiri na kuanza kazi hiyo na kwa wakati huo akiwa hawaoni kabisa hao jamaa.
"madame mtoto yuko tayari kwa safari" alikuja Zomba na kusema maneno hayo.
"madame gari zimesha fika karibu na mlango wa kuingilia humu shimoni" alisema Amiri na akiwa tayari amesha haribu kila kitu.
"nimeshaziba mlango wa kuingilia humu na itawapa shida kidogo kuweza kuingia, pia tayari nimesha weka hali ya hatari humu ndani kama mnavyoona taa hizi nyekundu zinavyo waka na kuzima muda wowote kuanzia sasa shimo hili linaporomoka. Twendeni garini" aliongea Amiri na muda huohuo wote wakaongoza mahali ilipo gari yao ya kuwatoa humo shimoni. Shimo ambalo liliandaliwa maalumu kwa ajili ya kumrudisha Sex machine kwenye maisha yake halisi. Shimo ambalo mtengenezaji wake na muanzilishi akiwa ni Father D.A. Ambaye alilitengeneza shimo hilo kwa sababu zake binafsi lakini zenye mantiki na misingi mikubwa kama hiyo. Kelele za kuvunjwa kwa mlango huko juu walizisikia lakini hawakuwa na muda wa kuogopa kitu kama hicho, walikimbia mahali lilipo gari. Walitembea kwa miguu kwa umbali mdogo huku wakipita kwenye njia mithili ya handaki hadi walipolikuta gari hilo. Ilikiwa ni gari aina Land Rover ya kizamani sana lakini ni yenye nguvu mno. Gari hiyo ilifanyiwa mautundu na vijana wawili Zomba na Jay, vijana wenye utaalamu mkubwa wa kuyafanya magari watakavyo na wanauwezo wa kuibadilisha gari katika muundo wautakao wao wenyewe. Wakaingia kwenye gari hiyo na Jay ndiye aliyekaa kwenye usukani wa gari hiyo. Huku nyuma shindo kubwa lilisikika na vumbi nene likaibuka.
"shimo limeanza kushuka sasa kwa sauti hiyo itakuwa vigumu kujua nini kinaendelea huku chini" alisema Amiri na mara Chars naye akasema.
"Jay hakuna kupoteza muda washa gari tuondoke hapa kwa kasi kubwa kwani kama shimo limeanza kushuka, inamaana ya kuwa muda si mrefu mlipuko mkubwa utaibuka kutoka kwenye mtambo"
"what??" akang'aka Catherine akifuatiwa na Zomba.
"ndiyo, nimeuseti ule mtambo kuwa baada ya shimo kuanza kutitia ndipo nao utakapolipuka" aliongea Chars gari ikiwa tayari umesha ingia kwenye njia ya huko chini ya ardhi ili kuweza kuwatoa humo shimoni. Mlipuko mkubwa ukarindima eneo hilo tena ukiwa ni mlipuko wa aina yake kabisa. Ulikuwa ni mlipuko ambao haukutarajiwa kutokea mahali hapo. Askari kadha waliokuwa juu ya shimo hilo walipoteza maisha pasipo kutarajia. Gari yao ilizidi kukata njia. Kulikuwa na giza kubwa mno lakini Jay, aliweza kutembea kwa mwendo mkubwa kutokana na taa za gari hiyo kuwa na mwanga mkali sana. Chars alikuwa ameshika kitu mfano wa saa ya ukutani mkononi mwake kisha akairusha nje ya lile gari.
"nini kile ulichokitupa?" aliuliza Catherine ambaye alikuwa amekaa karibu na Chriss.
"hilo ni bomu la masaa nililolibuni kama wiki mbili zilizopita, nilijua kuwa siku kama hii ingetubidi tuondoke, litalipuka baada ya dakika kumi na tano" alisema Chars kwa kujiamini sana.
"unaakili kweli Chars?" aliuliza Catherine akiwa anajiweka vizuri kitini. Alikuwa ni kama hawelewi vijana wake kuhusiana na hayo wanayoyafanya. Chriss alikuwa kama mtu anayeangalia sinema ya kusisimua, hakuwa akijua chochote.
"ninazo madame na kumbuka kuwa hawatakiwi hata kujua kama kuna njia humu chini. Hilo ni moja na pili, ukumbuke kuwa, askari wote wa mji huu watajaa hapa, halafu kumbuka hatutapaa mbali sana kutoka hapa, japo ndege tukayoitumia imefanyiwa utundu na hawa wachawi lakini pia ni moja ya kuwafanya wasione kama kuna ndege inapaa, hiyo itakuwa ni hatari kubwa sana kwetu. Hivyo basi, dakika kumi na tano baada ya hapa, sisi ndiyo tutakuwa tunaruka. Huku kwa muda huohuo bomu linalipuka unadhani macho yao yatakuwa wapi kama si hapa kwenye bomu? Na watakapokuwa wanadili na kuushangaa mlipuko, huoni kama sisi tutupaa bila kugundulika?" aliongea Chars kwa kujiamini sana. Catherine hakuona hata sababu ya kujibu hilo swali na badala yake alijilaza kitini tena akiwa na tabasamu pana. Kwa hakika alikubaliana na moyo wake kuwa hakuwa na vijana wa daraja dogo, alikuwa na vijana wa daraja la juu na wanaojua nini wanapaswa kufanya. ..................
Gari ilizidi kukimbia, giza lilikuwa nene sana ndani ya barabara hiyo ya chini. Chriss alikuwa ni mtu wa kushangaa maajabu yote aliyokuwa akiyaona mahali hapo. Baada ya mwendo huo mfupi wa kutembea chini kwa chini, walikuja kuibukia kwenye mbuga moja kubwa sana hapo ndipo kasi ilipoongezwa mara dufu. Gari hiyo ilikimbia kwa kasi kubwa sana huku nyuma ilitimua vumbi kubwa, hakuna mtu aliyekuwa akiongea mahali hapo hadi wakafika nje ya mji kabisa. Huko wakakuta ndege ambayo ilikuwa imeandaliwa maalumu kwa safari hiyo na ndege hiyo ilikuwa imehifadhiwa chimbo la hatati ambalo hata ingekuwaje isingeweza kuonekana na ilikuwa ni ndege iliyofanyiwa mautundu na wataalamu wawili Zomba na Jay. Ilikuwa ni ndege ya pekee sana, umbo lake la nje lilifanana kabisa na ndege za kivita. Waliitia moto ile gari ikawa inaungua taratibu na wao wakakimbilia kwenye ndege. Walipopanda ndani ya ndege hiyo, Zomba akaanza yake kwa kuipa uhai ndege hiyo ambayo ilikimbia kwa umbali mdogo uliokuwa uko tambarale na kupaa kwa kasi kubwa na muda huo huo huku nyuma kule shimoni, mlipuko mwingine mkubwa uliibuka na kusababisha mtafaruku mkubwa kwa wanausalama wa nchi hiyo ambao waliamini kuwa hali hiyo imesababishwa na matukio ya kigaidi. Habari zilisema kuwa ni baada ya wanausalama kugundua chimbo la maharamia hao muda mfupi nyuma na walipoamua kuvamia na kwenda kuwashtukiza ndipo kukatokea milipuko hiyo. Hivyo wanaamini huwenda magaidi hao wameamua kujitoa muhanga baada ya kugundua wamevamiwa na hawana pa kutokea.
Chars na Amiri waligongeana mikono wakati ndege yao ikiwa tayari ipo angani, walihakikisha ndege hiyo haionekani na rada ya aina yoyote ile kwani endapo ingeonekana ingekuwa ni habari nyingine kabisa na ingesababisha wao kupatikana kiurahisi. Tukio lililotokea Marekani lilikuwa limeenea duniani kote na kila upande ulikuwa macho kuangalia kama hao waliosababisha mauwaji hayo ambayo yaliongezeka kutokana na milipuko ile miwili kama wataweza kuonekana. Ndege hiyo ilishusha mbawa zake kando ya msitu mkubwa wa nchini Brazil kisha watu wote wakashuka ndegeni na kuingia ndani ya msitu huo. Ndani ya ndege alibakia Zomba pekeyake ambaye alikuwa akiharibu ndege hiyo kwa mfumo alioutengeneza yeye mwenye na kuiacha mahali hapo ndege hiyo ikiwa haina faida tena, akashuka na kuelekea upande ambao wenzake walikimbilia. Catherine akatoa ramani na kuitandika chini, wakaizunguuka ramani hiyo wote kisha Catherine akasema.
"tutapita katikati ya huu msitu ili tuweze kuwakwepa askari wanaohusika na usalama wa huu msitu kisha tutakuja kutokea hapa" akaonesha hapo walipotakiwa kufika halafu akaendelea.
"tutaiacha hii njia mnayoiona ambayo ni rahisi sana kutufikisha barabarani, sisi tutapita hii. Tunafanya hivyo kwani hapa ndipo tutakapo kutana na gari ambayo fadha ametuma watu wake kuja kutuchukua" akamaliza.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"huu msitu siyo ule unaopatikana wale nyoka wakubwa, Anaconda?" aliuliza Amiri na kuwafanya watu wote hapo wacheke.
"acha woga mtoto wa kiume wewe" Jay akamwambia.
"ni umbali gani kutoka hapa tulipo hadi kufika hapo kwenye hiyo gari" aliuliza tena Jay.
"ni kilomita mbili na nusu tu kama tutatembea kijeshi na itatupasa tutembee hivyo kwa sababu ninyi nyote mnatakiwa muondoke leo hii na ndege ya saa kumi kuelekea Afrika ya kusini kisha Nairobi kwenye kambi yetu ya muda ambapo ndipo tutakapoifanya kazi yetu ya mwisho. Hapa nitabakiwa na Chriss pekee ambaye anatakiwa kufanya kazi amabayo hajaimalizia" aliposema hivyo hakuna aliyesubiri amri nyingine, safari ya kuukata msitu huo ikaanza. Walitembea kwa muda mrefu huku wakibadishana mawazo na kuchangamshana ikiwa ni mbinu ya kujipunguzia hofu. Msitu ulikuwa mkubwa na wenye kutisha sana. Wote walikuwa matumatu kutokana na hofu juu ya msitu huo wa aina yake. Kila mtu kwenye safari hiyo alikuwa akipiga soga na mwenzake. Chars alikuwa akipiga stori na Amiri, Zomba yeye alikuwa na Jay. Chriss akajikuta yupo na Catherine.
"hupendi kuongea au hujisikii kuongea chochote na mimi maana tokea tumeanza hii safari umekuwa kimya tu?" aliuliza Catherine huku akijaribu kuongeza mwendo kumfikia Chriss maana yeye ndiye aliyekuwa mwisho kuliko wenzake wote.
"najiona niko tofauti sana na nyinyi na ndiyo maana niko kimya" alijibu kijana huyo.
"kivipi?"
"sijui mwanzo wala mwisho na nimejikuta tu nipo na nyinyi" aliongea Chriss huku akizidi kutembea kwa kasi.
"ni stori ndefu sana Chriss na inahitaji muda kuweza kukuhadithia, nitakupa kwa uchache tu tukifika mahali salama na stori kamili ni hadi tukiwa Nairobi."
"huwezi kunigusia japo kwa uchache angalau?" aliuliza Chriss akiwa amesimama ghafla na kumuangalia binti huyo amabaye kwake alimsoma kama kiongozi wa kundi hilo dogo. Kitendo kilichopelekea hadi Catherine kusimama.
"Chriss, naomba uwe mpole na pia fahamu kuwa ni hitoria ndefu ambayo pengine haitakuwa nzuri sana kwako, wewe ni mtoto wa kiume hivyo unatakiwa uwe na subira" alisema Catherine huku akimpita kijana huyo na kuendelea na safari. Chriss akabaki hapo amesimama kwa muda mfupi kabla ya kuwakimbilia wenzake.
"madame, nafikiri hadi hapa tulipo tumebakiza hatua chache tu kuweza kufika mahali ilipo gari?" aliongea Chars ambaye ndiye aliye kuwa kiongozi mbele yeye pamoja na Amiri.
"tazama hapo bondeni upande wa kushoto, umeiyona hiyo pick up nyekundu?"
"ou! Kumbe tumefika tayari" alidakia Zomba na kukimbilia mahali lilipo gari, kila mtu alikuwa na furaha kubwa sana baada ya kuiona gari hiyo. Walikuwa wamechoka sana. Walifika hadi hapo na Catherine akaongea na mtu waliyemkuta hapo kisha wote wakapanda nyuma ya hiyo gari na kujituliza. Walikuwa wamechoka sana japo ilikuwa ni safari fupi lakini kwa mwendo walioutumia haukuwa wa kawaida hata kidogo. Gari hiyo ilitiwa moto hadi mjini. Walipofika mjini, Zomba, Amiri, Chars na Jay. Hawakupoteza muda walikamata gari iliyowafikisha uwanja wa ndege huko wakapanda ndege ambayo ilikuwa ikielekea Afrika ya kusini.
Catherine na Chriss walichukua hoteli kwa ajili ya kazi ya kumalizia. Usiku wa siku hiyo, Catherine alikuwa chumbani pamoja na Chriss wakiwa wanajadili jambo. Kwanza kabisa Catherine alichokifanya ni kumkabidhi Chriss simu yake. Chriss akashangaa baada ya kupewa simu hiyo lakini kabla haja uliza ndipo akapewa muktassri wa kile alichokuwa hakijui.
"unakumbuka nini Chriss hapo ulipo? Yaani namaanisha kuwa mara ya mwisho unakumbuka ulikuwa wapi?" alianza kwa swali binti huyo. Chriss akafikiri kwa muda na kusema kuwa kwa mara ya mwisho anakumbuka kuwa alikuwa kwenye kampuni anayofanyia kazi mjomba wake Joesan.
"unakumbuka ulienda ndani ya kampuni hiyo kwa lengo gani?" lilikuwa swali jingine?
"ilikuwa ni kwa ajili ya kwenda kupewa kazi"
"unaweza kuniambia kazi ambayo mjomba wako alitaka kukupa?" Chriss alifikiria kwa muda baada ya kuulizwa swali hilo kisha akainama chini kwa aibu ni kama hakuwa tayari kusema.
"unatakiwa kuwa huru kwa kila jambo kama kweli unataka kujua ni kwanini kwa mara ya mwisho uwe Morogoro na kisha uje ujikute Marekani" alizidi kumchimba kijana huyo Catherine. Chriss akayanyanyua macho yake na kumwambia kuwa yuko tayari kumwambia japo aliona si sahihi kusema hivyo kwani ilikuwa ni kazi ya aibu sana ila hakuwa na jinsi, alitaka kujua mengi kutoka kwa dada huyo.
"Sex machine" alijibu Chriss kisha kugeukia pembeni.
"najua na najua ulipambana kufa na kupona ili upite kwenye mtihani wako wa kwanza kama Sex machine na ukashinda. Joesan alikufanya kweli kuwa kifaa cha ngono na hukuwa ukijitambua kama wewe ni kifaa cha ngono na ulikuwa ukifanya ngono kwa kumuingizia pesa nyingi yeye na watu wake." maneno hayo yakamfanya kijana huyo kushtuka na kumuangalia huyo binti kwa macho makavu ni kama hakuamini hayo aliyokuwa akiyasikia.
"nilikuwa mashine ya ngono kweli? Kivipi? Mbona sikumbuki kama niliwahi kufanya ngono hata siku moja?" alijikuta akiuliza maswali mengi sana kijana huyo, ni wazi aliona binti huyo anamdanganya.
"Joesan alikubadilisha kwa mtambo maalumu ambao ulibadilisha ubongo wako na kukufanya usikumbuke kitu chochote katika maisha yako zaidi ya taaluma uliyokuwa nayo"
"hapana unanidanganya Joesan mjomba wangu, hawezi kufanya hicho kitu hata kidogo. Joesan mjomba wangu anigeuze akili na kunifanya nisijue kitu chochote? Si kweli wewe mwanamke ni muongo na mnavyoonekana mna ajenda kubwa sana na mimi, mnataka kuniingiza kwenye mambo yenu ya kigaidi mnayoyafanya, mnataka na mimi niwe gaidi kama nyinyi si ndiyo?" aliongea mambo mengi sana Chriss, hakutaka kumuelewa binti huyo hata kidogo na hakuwa akiamini kila kilichokuwa kikiongelewa hapo. Aliamini hao ni magaidi na wanataka kumuingiza kwenye huo ugaidi na alisema hivyo kutokana na kile alichokishuhudia kule shimoni.
"sikiliza Chriss, sisi hatuna nia mbaya na wewe hata robo na badala yake wale uliowaona niko pamoja nao, wamejitolea kunisaidia katika harakati hizi za kukukomboa wewe kwenye mateso uliyokuwa ukiyapata pasipo kijitambua huku.............!!"
"wewe ni muongo na sitaki kujihusisha na mambo yenu, naomba uniache nitoke humu ndani na niende ninapopajua mimi, huwezi kumzushia mjomba wangu kuwa ameweza kunifanyia hayo, Joesan ananijali na kunipenda sana" Chriss alimkatisha Catherine na kusema maneno hayo huku akiwa tayari amesimama kutaka kutoka humo ndani.
"nisikilize Chriss, Joesan sisi hatumzushii na hata kama tutamzushia hatotusaidia chochote kile katika maisha yetu. Ila ukumbuke kuwa Joesan hakukufanya tu kuwa mashine ya ngono bali alikufanya Punda yaani alikugeuza kifaa hatari cha kusafirisha madawa ya kulevya..........
Sitaki uzidi kuniona mimi ni muongo au nazidi kumzushia mjomba wako. Chukua hiyo simu hapo chini ambayo ulitaka kuirudisha kwangu na uiwashe kisha utampigia Joesan. kwanza unakumbuka kwenye simu yako ulimsevu jina gani Joesan?" alisema Catherine na kumuuliza swali. Chriss akasema alimuhifadhi kwa jina la Uncle. Catherine akamwambia kuwa hapo kwenye hiyo simu hakuna jina la uncle wala shangazi, kuna majina matano tu. La kwanza ni Boss, ambaye ndiyo Joesan, la pili ni Suzane, tatu Merina, nne ni Honey na tano ni mzee Rafa. Hayo ndiyo majina pekee yaliyokuwamo humo kwenye hiyo simu, akamwambia kuwa, hilo kwanza ni ajabu la kwanza. Chriss hakutaka kuamini moja kwa moja, akaamua kuiwasha simu hiyo. Ilipowaka, kweli alikutana na majina hayo, hilo halikumshangaza sana pengine pia yaweza kuwa ni mchezo wao ili kumchanganya. Bado kichwa chake kilikuwa kigumu kuamini.
"hapo unatakiwa umpigie Joesan ambaye kwenye simu hiyo umemsevu kama Boss. Ukisha mpigia jifanye ulikuwa katika hali mbaya sana baada ya kupambana na yule adui wa kike na kushindwa kabisa kuendelea kubaki ndani ya hiyo hoteli kwa siku hiyo nzima, nasema hivyo kwa sababu sisi siyo tulio kuleta Marekani, bali aliyekuleta Marekani ni huyo anko wako na alikupeleka marekani kwa kazi maalumu, hivyo mwambie ulitekeleza mauwaji ya meneja wa hoteli kwa sumu na kwenda kumvamia mfanya biashara yule halafu ukazima kabisa simu ili kuzuia kufuatiliwa na watu wabaya ili uweze kujitibu kwa urahisi. Nakufundisha haya kwa sababu huwenda akakuuliza kuhusiana na mimi maana mimi ndiyo ulikuwa mteja wako wa mwisho kufanya ngono baada ya shoga ambaye nilimuuwa mimi kwa mikono yangu, sikutaka uthubutu kufanya mapenzi ya jinsia moja. Pia hawakujua kama mimi ndiyo nilikuwa na mpango wa kukukomboa na kukutoa kwenye kifungo walichokufunga. Baada ya hapo ndipo utakapojua kuwa Joesan si mtu mzuri kwako hata kidogo. Lazima atakuambia kesho uende Ufarasa ukachukue mzigo wa madawa ya kulevya." alimpa malezo kijana huyo. Chriss ni kama alianza kumuelewa huyo dada na alikuwa akijifikiria jinsi ya kupiga hiyo simu. Liwalo na liwe kinachotakiwa kujulikana ni ukweli na hujihakikishia kuwa kweli huyo atakuwa ni Joesan yule anayemjua yeye maana sauti ya mjomba wake bila hata kuelezwa aliijua kinaga ubaga. Akapiga hiyo simu. Simu ya upande wa pili ikaita mara ya kwanza na mara ya pili ikapokelewa.
"Sex machine!" sauti hiyo iliita kwa mshangao mkubwa. Ilikuwa ni sauti ya Joesan kabisa. Chriss alitaka hata kuiachia hiyo simu kwa jinamizi kubwa la mshangao lililomkumba, ni kweli yeye alikuwa ni Sex machine pasipo kujitambua.
"yes, Boss" aliitikia Chriss.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"ulipatwa na nini SM hadi unafanya kampuni inachanganyikiwa kwa muda wa siku tatu nzima hauko hewani, hadi tulijua labda yule shetani wa kike alikuzidi maarifa. Nini tatizo Sex machine?" Chriss kiukweli alijikaza kiume lakini kama asingejikaza, hata hiyo simu angeshindwa kuidhibiti. Alikuwa akijihisi vibaya sana moyoni mwake. Ilibidi ajibu kama alivyoelekezwa na Catherine kwa muda huo. Maongezi yalikuwa marefu na mwisho akamwambia Mzigo aliotakiwa kuufuata nchini Ufaransa bado unamsubiria hivyo anatakiwa kesho atake asitake, ni lazima aende Ufaransa kuuchukua mzigo huo na aupeleke nchini Brazili. Chriss akajibu sawa lakini alikuwa akiumia sana kwa hizo amri alizokuwa akipewa hapo. Alikuwa Sex machine kweli, pia alikuwa msafirisha madawa ya kulevya. Alimtazama yule binti aliopo hapo na kujikuta akitamani hata kusema jambo kwa ajili yake lakini hakuwa na uwezo wa kufanya hivyo, midomo ilikuwa mizito na kooni alikabwa na dukuduku zito. Alijiona si yule Chriss wa zamani, alijiona hana thamani tena kwenye hii dunia, alikuwa amepoteza nguvu kabisa. Alitamani kulia lakini amlilie nani sasa.
"Joesan, ulisema unanipenda sana na hupendi nipatwe na matatizo katika maisha yangu, kumbe ulikuwa unanidanganya na kuzugisha ili niingie kwenye kazi zako za kishetani. Sikatai ni kweli nilikubali kuwa Sex machine lakini si kwa kutokujitambua" aliwaza Chriss akiwa amenyong'onyea kabisa.
"hutakiwi kufa moyo, hii ni vita kubwa sana na walikuwa na mpango wa kukutumia vile watakavyo wao hadi kifo chako." akashtuka Chriss na Catherine akaendelea. Joesan ana kundi kubwa analofanya nalo biashara hizi. Ni makundi matatu kama sikosei na a........oooh shit! hebu ngoja, sogea hapa karibu usikie hizi sauti." alisema Catherine na muda huo huo Chriss akasogea na kuchukua ear phone moja na kuiweka sikioni. Walisikia kila kitu kilichokuwa kikiongelewa hapo hadi mwisho. Chriss alijikuta anachoka kabisa.
"huyu aliyekuwa anaongea na Joesan hapa anafahamika kwa jina la BC (Black Clockodile). Anajiita Mamba mweusi kwa lugha yetu ya taifa. Huyu ni miongoni mwa kundi lake linalohusika na hii biashara. Anamwengine yuko huko Urusi na mwengine yuko huko Ufaransa ambako unatakiwa uende kesho. Wanafurahi kwa kuwa wamejua uko hai na wanaweza kuendelea kufanya biashara zao vile watakavyo wao."
"siendi" alisema Chriss.
"oooh no, ni lazima uende Chriss. Kama nilivyokuambia kuwa hii ni vita na wapiganaji wa vita hii kubwa ni wewe na mimi wengine watakuwa wanatupa msaada tu." aliongea Catherine.
"nitaendaje sasa madame na mimi siyo sex machine tena?" aliuliza Chriss.
"utakwenda kwa kujifanya kuwa wewe ni Sex machine kama wanavyokufahamu na utauchukua huo mzigo kisha hapo ndipo tunapoharibu kila kitu na mipango yao yote. Mzigo hautafika wanapotaka uende sisi tutauharibu na kisha tutampigia mmoja baada ya mwingine na kumchonganisha na mwingine. Yaani tutampigia Joesan na kumwambia kuwa mzigo umevamiwa na kundi la BC na kutoweka nalo, kisha tunampigia Yule wa Urusi na Ufaransa na kumwambia kuwa vijana wa wa BC wamevamia na kupora mzigo. Tutafanya hivi kwa sababu kundi la BC ni kubwa kuliko makundi yote. Najua watapigana wenyewe kwa wenyewe kwa kudhulumiana huku sisi tukirudi Tanzania kwenda kujua nini kitafuata." aliposema hivyo akatulia huku akimuangalia kijana huyo usoni.
"Joesan si anaweza kunitumia mimi kupambana na hao wenzake?" aliuliza Chriss.
"sidhani kama atawahi, muda huo sisi tunaweza kuwa tumeshaharibu kwa upande wao." Chriss akakubali kuubeba uhalisia na kukubali kwa moyo wote huku akiwa na dhima ya kutaka kujua sababu kuu ya Joesan kufanya yote hayo. Kikao hicho cha usiku kikafungwa kwa makubaliano kuwa Chriss atakwenda Ufaransa na kisha kurudi Brazil Tena ambako wangefanya yao. waliagana baada ya hapo na kila mmoja akaelekea kwenye chumba chake kwa ajili ya kuupitisha usiku huo.
******************************************************************************
"sasa nimeamini mkuu kuwa huyu kijana ni levo nyingine kabisa, sikutegemea kama atakuwa hai hadi sasa. Kwa usalama wa nchi kubwa kama Marekani, ukiambiwa ameweza kuwatoka askari hatari na makini na kuweza kufanya mawasiliano na mimi?" alisema Joesan alipokuwa amemtembelea mr. Lee kwenye moja ya jingo lake la siri.
"mimi nilikuambia Joesan kama unakumbukumbu nzuri, niliwahi kukuambia kuwa yule kijana ni mtu hatari sana. Na sifa aliyonayo ni ya ujasusi yule. Kikubwa ni kuwa makini laa sivyo tutatafutana endapo atakutana na watu tofauti au akikutana na mahasimu wetu." aliongea mr. Lee.
"nitahakikisha hilo halitokei kirahisi, nitafanya kila mbinu ilimradi Sex machine abaki kuwa Sex machine pasipo kujitambua" walizidi kuongea namna hiyo mida hiyo ya asubuhi bila kuwa na wasiwasi kabisa, walikuwa katika furaha kubwa kupita kawaida.
"na safari hii akiwa hapa, nitamtuma akamuuwe yule mzee nisiyependa kulisikia hata jina lake, namchukia sana D.A lakini huu ndiyo mwisho wake wa kujidai." alizidi kusema kwa tambo mr. Kim.
Taarifa za kuwa Sex machine yuko hai na muda si mrefu atakuwa Tanzania, zilifika ndani ya kampuni na wafanyakazi wote wakaelezwa jinsi ambavyo kijana huyo hatari alivyoweza kutoka kwenye sekeseke la kukaribia kutekwa. Wafanyakazi wote walikuwa katika furaha kubwa baada ya sintofahamu ya muda wa siku mbili zilizopita. Kila mmoja akarudi kwenye nafasi yake ya kazi kwa kuamini hakuna kilichoharibika. Pamoja na furaha kuwagubika wafanyakazi hao, kuna mmoja hakuwa na amani kabisa na ukweli kuwa eti, Sex machine yu katika uhalisia ule wa awali. Alikuwa na furaha kubwa machoni kwa kumtazama tu lakini moyoni alikuwa na zaidi ya lundo kubwa la maswali mfululizo. Waswahili na wabobezi wa kiswahili hasa wale wanayoijua lugha hii ngumu nje na ndani yake, walipata kusema haya. 'moyo huteta fikira, na fikira huleta neno upendapo kulitamka' Unaweza usielewe ni kwanini walipata kunena maneno haya yenye fumbo kubwa. Je, unadhani waliondoka bila kulifukunyua neno hilo kwa kina hadi kulipatia maana? Si kweli waliacha maana japo maana hizo ni nyingi lakini kubwa ni hii. Hakuna asonekaye pasi na kuushirikisha moyo, hakuna awazaye, bila ya kuushirikisha moyo na moyo unapowaza ama kuteta, huleta fikira, hizi hujaa kifuani na kuleta kero kubwa kwa muwazaji na hatimaye hujikuta akitamka neno pasipo hata kufanya maamuzi kwa wakati mwingine. Napata picha ya hayo kupitia mzee Rafael, mzee ambaye kichwa chake hakilali pasipo kuwa na jambo lenye kutafakariwa ndani yake. Alipokuwa ofisini kwake mzee huyo, alikuwa katika tafakuri nzito iliyopelekea kutamka neno moja tu kutoka kinywani mwake na sidhani hata kama alipanga kulitoa neno hilo kwa majira hayo.
"tumekwisha!" ndilo neno lililotoka kinywani mwa mzee Rafa kisha kulilazimisha tabasamu na kujizunguusha pale kwenye kiti chake muda huo wa asubuhi na kuendelea kuwaza.
"bado nakitafakari kinasa sauti nilichokigundua chini ya meza yangu, pili mtu aliyefanya mauwaji ya meneja wa Hoteli huko Miami. Mwanamke, yule ni mwanamke, kuanzia mwendo hadi haiba yake. Japo alijaribu kujificha kidogo lakini kwa mtu kama mimi nilifanya shughuli hizi na maharamia wengi wa kike, najua mbinu na hata aina yao ya mauwaji. Inamaana mkuu na unyama wake wote ameshindwa kumng'amua kuwa yule hakuwa Sex machine?" Mawazo yalikuwa yakitiririka kichwani mwa mzee huyo mithili ya jasho mwilini. Hadi muda huo wa saa tano, bado hakuwa amefanya kazi yoyote ile zaidi ya kuwaza...............
"Pol, wewe ndiye utakayekiongoza kikosi chote kitakachohakikisha mzigo wote wa DF unaingia mikononi mwetu mara tu utakapoingia Brazil. Kikubwa ni kwamba mzigo huo uvuke salama kutoka ufaransa hadi Brazil kisha baada ya kutoka uwanja wa ndege, sisi tunafanya uvamizi wa ghafla na kutoweka na mzigo. Wazo langu la kutaka kumteka huyo kijana ili awe miongoni mwenu nimelifuta, hakikisheni hammuui hadi mzigo mmeuti mikononi mwenu. Nitakuwa nyuma yenu, mtakapohitaji msaada, nitawasliaidia" aliongea BC akiwa kwenye eneo lake kubwa kama uwanja wa basket ball, akitoa maelekezo kwa vijana wake. Alikuwa anadhamira kubwa ya kuuteka mzigo huo wote kisha ampe kesi Sex machine kuwa amevamiwa na kuporwa mzigo huo. Lakini hawakuwa na lengo la kumuuwa kijana huyo bali walichokihitaji wao ni mzigo tu. Lakini kama atakuwa mkaidi basi wahakikishe anakufa lakini wakiwa tayari wanamzigo.
"mkisha uchukua huo mzigo nadhani mnajua ni wapi mimi na nyinyi tutakutana, hivyo sitegemei kama kutakuwa na shida sana. Ninyi mko wengi sana, siamini kama mtu mmoja anaweza kuwashinda nyinyi mlio zaidi ya ishirini." alizidi kuongea kwa tambo kubwa sana bwana BC. Kweli kwa wakati huo wanapanga mipango ya kuuteka mzigo atakaoubeba Sex machine, kijana Chiriss alikuwa angani akielekea nchini ufaransa ambako alitakiwa kuufuata mzigo kuelekea nao Brazil kama ambavyo biashara hiyo ilivyozoeleka. Safari hii ulikuwa ni mzigo mkubwa sana ambao ulikuwa ukisafirishwa kwenye begi kubwa la kuvaa mgongoni. Hawakujua kuwa wanayempangia huo mpango hakuwa Sex machine tena, SM wanaomjua wao hakuwa huyo kiakili bali kimwili tu. Huyo alikuwa ni mtu mwingine kabisa kiakili, mwenye mipango mingi ya kutaka kuijua historia yake kwa nguvu zote pia kujua ni kwanini Joesan mtu aliyekuwa akimheshimu kama ndugu wa mama yake kwa jinsi alivyoelezwa, awe na roho mbaya kiasi cha kutisha tena si cha kutisha tu, bali cha kumbadilisha hata yeye kuwa Sex machine. Huyu alikuwa na mpango wa kuuteketeza huo mzigo kwenye kina cha bahari kisha kuzusha kuwa vijana wa BC wamemvamia. Huku nako vijana wa BC wako uwanja wa ndege wa New York, wakielekea Brazil kwa lengo la kuupora huo mzigo huku BC mwenyewe akiwa nyuma kwa kuwafuatilia kwa njia azijuazo mwenyewe. Nini kitakachokwenda kujiri huko.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ndege kubwa kutokea Brazil ilishusha mabawa yake ndani ya uwanja wa Charels de Gaulle na kuzikanyagisha tairi zake kubwa ndani ya barabara safi kisha kukimbia kwa kasi kubwa kabla ya kuelekea kwenye eneo la kusimamishia ndege. Abiria walishuka mmoja mmoja na kuelekea mahali pa ukaguzi. Ambako alikaguliwa na kutoka maeneo yenye usafiri kisha akachukua usafiri hadi katikati ya mji ambako alikuta mtu ambaye alimchukua hadi kwenye himaya ya mr. Santiano. Bwana moja katilli la Kifaransa.
, ambalo linaweka tamaa mbele kuliko utu. Mara njingi hakupenda kulitumia jina lake la kweli ambalo amelikatish kwa kujiita T. Ano. Jina maarufu na la kibiashara. Huyu ndiye yule bwana ambaye aliunda kundi la watu wanne akiwemo BC, Chalco na J. Chriss alizama ndani na kumkuta mtu huyo mrefu na mwenye mwili wa mzoezi ambaye hakuwa na maongezi mengi mahali hapo. Alikabidhi mzigo na kumucha kijana huyo aondoke bila kumwambia chochote kwani alijua ni wapi mzigo ulitkiwa kwenda. Moyo wa Chriss ulikuwa ukienda mbio sana, alijiona ni kama hakuwahi kubeba madawa hata siku moja katika maisha yake, hiyo aliona kwake ilikiwa ni mara ya kwanza kabisa. Hofu yake yote ilikuwa ni jinsi gani angeweza kupita kwa usalama ndani ya uwanja wa ndege wenye ukaguzi mkali kama wa Charels. Alijipa moyo na kukaza roho. Aliyakumbuka maneno ya Catherine kuwa alikuwa ni kifaa hatari cha kusafirishia madawa ya kulevya pia alikuwa ni mashine ya ngono. Aliamua kubeba uhalisia, hakutaka kufeli kwa kujipa hofu kizembe kwani aliamini kosa moja ambalo angelifanya, angekuwa ameharibu utaratibu mzima. Pia alifikiri kuwa akili yake ndiyo ambayo haijawahi kufanya hiyo biashara lakini mwili wake uliwahi hivyo akapiga moyo konde.
"lazima nifike Brazil na huu mzigo ili nijue mengi kuhusu mimi, huu ni wakati wangu wa kujua kuwa Joesan ni nani kwenye maisha yangu, kwanini hana huruma na mimi?" aliwaza Chriss alipokuwa ndani ya Tax akiwa anaelekea uwanja wa ndege.
"Siku zote mimi ndiyo namaliza kazi, utajiri wangu huu unazidi kukuwa mkubwa kwa kasi kubwa kwa sababu ya kuwageuka wenzangu. Nadhani mnajua kawaida yetu?" alisema bwana huyo wa kifaransa, bwana mwenye tambo kubwa na tamaa za kuzidi. Alisema na kuuliza swali akiwa mbele ya kijana wake mmoja akisubiri jibu kutoka kwa kijana huyo.
"ni kuuwa na kusafiri na mzigo" alijibu kijana huyo.
"napenda watu wenye kumbukumbu kama wewe, ni watu muhimu sana kwangu," akaweka koma na kuwageukia vijana wake wengine. Akasema.
"nakiamini kikosi changu huwa hakikuni nazi, ninapokituma huwa kinafanya kweli. Hakikisheni huyu shoga mwenye ngozi nyeusi akipanda ndege ya mbele nyinyi mnakuwa nyuma. Tulimuuwa Cat bila kugundulika, tukatembea na mzigo. Tukamchinja Jojo kwa kifo kibaya sana baada ya kuleta ubishi pia tukaondoka na mzigo, hawakuweza kunigundua wala kujua kuwa mimi ndiye ninayewageuka. Na leo anakufa SM pia tunateka huu mzigo. Nataka niwahiidi kitu kimoja, tukifanikiwa kuondoka na mzigo huu, ninyi nyote ni matajiri na kazi ya madawa ya kulevya tunaacha kabisa kwa sababu huu ni mzigo mkubwa kuliko yote tuliyowa kuipora, ila muhakikishe huyu kijana wanayemsifia ambaye kwangu ni kama malaya niliyelala naye na kumfanya ninavyoweza halafu nikamtoa bila malipo, lazima afe na kumuanika bila nguo hadharani ili kuwaonesha kuwa sisi ni mafia na kazi hizi hatubahatishi." alijitapa T. Ano na kuwaamrisha vijana wake kumi na wawili waelekee air port kwa njia tofauti na wao wataondoka na ndege ya pili baada ya aliyopanda SM kwani tayari ameshafanya malipo yote ya safari hiyo. Kazi si ndogo, tena si ndogo abadan, kizaazaa kikubwa kinachokwenda kukutana na kijana Mdogo wa kitanzania, kijana ambaye hajui kama kuna makundi mawili yote yakiwa ni hatari na yanayouhitaji mzigo huo mkubwa wa madawa ya DF. Mzigo uliyobeba utajiri mkubwa. Ikumbukwe kuwa, T. Ano ndiye aliyefanya mauwaji ya Sex machine wa awali na kusababisha Joesan kuingia kwenye matatizo makubwa na Mkuu wake wa kazi na leo tena mambo yaliyowahi kujitokeza miaka iliyopita yanataka kujirudia. Ni vipi kama Chriss akiuwawa, je, Mr. Lee atamuelewa Joesan tena? Haijulikani, hapo ni utata kila kona.
Roho ya Chriss ilikuwa nyeupe kabisa baada ya kufanikiwa kupita kwenye ukaguzi pasipo kutambulika na hiyo ni baada ya kufanya ujanja na akili kubwa ya kuzaliwa ndipo akafanikiwa. Alikuwa ndani ya ndege akisubiri ndege hiyo iiyache ardhi hiyo ya Ufaransa. Dakika tano mbele alikuwa angani akiwa na furaha kubwa kwa kufanikiwa kupita sehemu moja na kuwaza jinsi atakavyotoka kwenye uwanja wa Brazil salama na kwenda kuuteketeza mzigo huo. Hakujua kama nyuma yake kuna ndege ambayo anapishana nayo dakika kumi tu na hiyo pia ikiwa na watu wenye mpango kabambe na mzigo huo ambao yeye anampango wa kuuteketeza. Lakini kwa upande mwingine wa anga kulikuwa na ndege ya shirika la kimarekani nayo ikiwa imewabeba vijana ishirini nao pia wakiwa na lengo na mzigo huo.
Baada ya masaa kadhaa ya kuwa angani, ndege iliyombeba Chriss, ilitua bila shida kwenye uwanja wa kimataifa wa nchi hiyo ya Brazil. Kijana huyo alishuka na kutoka salama kwenye uwanja huo na kuelekea kwenye gari ambayo alikuwa na maelekezo nayo. Ndani ya gari hiyo alikuwamo mwanadada Catherine ambaye alikuwa akifanya mawasiliano na kijana huyo kila hatua aliyokuwa akipiga na kila wakati.
"kweli Chriss ulitengezwa kwa kazi hii maalumu, hata kama wasingekuingiza kweye mitambo na kukubadilisha akili, bado wewe ni mtu hatari. Mafunzo ya kijasusi ambayo Joesn alikupa, yamekufanya umekuwa ni sumu kali" aliongea Catherine akiwa ameegamia usukani wa gari.
"na huyo mshenzi alifanya yote hayo kumbe alikuwa na malengo maalumu?" aliuliza Chriss.
"haswaa!" alijibu Catherine baada ya Chriss kuongea hivyo.
"wapi tunakwenda kuuwangamiza huu mzigo wa madawa?" aliuliza Chriss.
"inabidi tuelekee kwenye kina kirefu cha bahari ambacho hakina watu karibu na kuutupa huu mzigo, lakini tutautupa tukiwa tumeufunga pamoja na jiwe zito ili kuufanya uzame na kuto kuonekana mazima" alisema Catherine na kuliondoa hilo gari taratibu.
"anaeleke upande wa beach ya Copa, vipi kwani ndiyo ambako huu mzigo unatakiwa kwenda?" aliuliza mtu mmoja nyuma ambaye alikuwa pembeni ya dereva na gari yao ilikuwa na vijana kumi wa BC huku nyuma kukiwa na gari nyingine inayofanana na hiyo, ambayo nayo ilibeba vijana kumi na kutimiza idadi ya vijana ishirini.
"haijalishi, tunachotakiwa kufanya ni kuhakikisha mzigo unaingia mikoni mwetu kabla haujafika kwa tajiri" alijibu mtu mwingine. Gari ile ya Chriss na Catherine ilipoondoka, walisubiri magari mengine mawili yatangulie ndipo wao wafuate nyuma lakini kabla hawajaondoka hapo, gari moja nyekundu ikawatangulia kisha na ya kibuluu nayo ikapita mbele kwa kasi. Vijana wale wa BC wakapatwa na mshtuko na wasielewe hizo gari ni kwanini zilikuwa zimewapita hivyo baada ya kutangulia gari mbili baada ya ile iliyokuwa na windo lao.
"kakikisha unazipita hizo gari mbili kamanda, hiyo gari ya huyo SM isituache sana." alisema mtu mmoja wa gari ya nyuma kupitia kifaa cha mawasililiano. Hao walikuwa ni vijana wa BC. Hawakuwa wakijua kuwa hizo gari nyekundu na kibuluu zilizowatangulia zilikuwa ni za watu wanaoutaka huo mzigo pia. Safari ilikuwa ndefu kidogo, walikimbia kwa mwendo mkali sana lakini pamoja na kufuatiliwa nyuma na vikundi viwili tofauti, hakuna aliyegundua hata mara moja. Huku nyuma zile gari zilikuwa zikichezeana mchezo wa kushangaza sana. Kwani zile gari nyekundu na za kibuluu za vijana wa T. Ano, .......
hawakukubali kuziruhusu gari nyingine ziwapite hata kidogo hivyo wakati gari ya vijana wa BC zilivyokuwa zikitaka kupita wao walikuwa wakitanua na kufanya gari hizo zisiweze kupita. Vijana wa BC walijenga mashaka makubwa sana juu ya gari hizo nyekundu na kibuluu lakini kwa vijana wa T. Ano, wao waliona ni kama mchezo wa kuigiza tu na muda wote walikuwa wakicheka kwa jinsi walivyokuwa wakiwafanyia vituko wenzao wakidhani ni watu wa kawaida tu wa barabarani kumbe walikuwa ni watu wenye nia na dhamira moja.
"ha ha ha haaa!, wooouuuuu!, yeeaaaaa!" walikuwa wakifurahi namna hiyo vijana hao huku wakihakisha gari iliyoko mbele hawaipotezi. Ilikuwa ni vigumu sana kugundulika kwani mbele yao kulikuwa na gari kama mbili ama tatu kabla ya gari zao.
"kiongozi, wanakwenda wapi hao mbona kama wanachukua njia isiyo sahihi?"
"hata mimi nashangaa ujue, mimi nilijua wanakwenda beach lakini si hivyo"
"tuwe makini kiongozi hawa inawezekana walikuwa na mpango wao hebu waambie jamaa nyuma waandae vifaa vya kazi" walikuwa wakiongea vijana wa mbele wa T. Ano. Muda huo huo wakawasiliana na vijana wa nyuma na kuwaambia kuwa waandae mashine za kazi kwani muda wa maangamizi unawadia, huko mbele hakukuwa na njia iliyokuwa inakwenda mbali sana hivyo walijua tu gari hiyo kunasehemu itakuwa inaelekea.
Wale vijana wa BC walivyoona zile gari nyekundu na kibuluu nazo zimeingia njia ambayo gari iliyombeba SM imeleekea huko, walijawa na wasiwasi mkubwa hivyo hawakutaka kuufuta msafara huo. Wakaamua kupita njia nyingine ili kuweza kutokea kwa mbele.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Catherine alipoifikisha gari mbele, ilikuwa si mbali sana na zilipo kuta za bahari. alisimamisha gari na kushuka na begi moja dogo la mgongoni na kuelekea upande ilipo bahari ambapo kulikuwa na kijumba kimoja kirefu kwenda juu. Kijumba hicho kikiwa ni sehemu moja wapo ya utalii ama sehemu ya matembezi ya watu mbalimbali. Alifika ndani ta kijumba hicho huku nyuma Chriss alikaa upande wa dereva na kuiondoa gari hiyo kuendelea mbele zaidi.
"hapa sielewi kiongozi, vipi huyu mrembo tumuuwe?" aliuliza kijana mmoja.
"hapana huyu hana sumu na inaonekana ni kama hana analolijua, huwenda alipewa lifti tu, hebu tumfuatilie huyo wa mbele ambaye ndiye target yetu kubwa." alisema huyo aliyeitwa kiongozi. Safari ikazidi kwenda mbele zaidi.
Chriss alifika hadi mwisho wa njia ile kisha akashuka na lile begi na kusogea nalo hadi kweye ukuta wa bahari ile, huko ndiko kulikoaminika kuwa na kina kirefu sana cha bahari kwani kulikuwa na mabango mbali mbali yaliyokuwa yakionesha tahadhari. Alichukua jiwe kubwa kiasi na kuliifunga kwenye lile begi kisha kusimama pale juu ya ule ukuta huku akiwa amelishika lile begi kutaka kuliachia majini.
"anampango gani kiongozi" aliuliza yule jamaa aliyekuwa muongeaji kila wakati.
"huyu mshenzi hafichi bali anaupoteza kabisa huu mzigo, kuweni makini hata kama mkimpiga risasi muhakikishe lile begi linabaki nje ya maji." alisema huyo kiongozi.
"tufanye nini sasa?" aliuza tena.
"piga risasi moja pembeni, lazima atashtuka na kugeuka nyuma, hapo tutavunja miguu. Tukifanya hivyo, ataangukia kwa mbele na hapo ndipo tutammaliza kabisa." alisema kiongozi huku wakiwa kwa juu kidogo wakimtazama kijana huyo kwa jinsi alivyokuwa amesimama pale kwenye ukuta wa bahari ile tayari kabisa kuuteketeza mzigo ule.
Kwa upande wa vijana wa BC, walikuwa tayari wamefika kwa mbele kidogo lakini walikuwa wakiwaona wale jamaa ambao walikuwa wakizitazama nyendo nzima za Chriss.
"hao jamaa kumbe siyo wema kwetu pia, inavyoonekana hata wao wanashida na huo mzigo" aliongea kijana mmoja upande ule wa wale vijana wa BC.
"nini kifanyike kamanda?" swali hilo aliulizwa mkuu wa kikosi.
"haraka sana shambulia watamuuwa yule na sisi tutaukosa mzigo." sauti ya kushambulia ilitoka.
Kwa majira hayo hayo, Catherine naye alishuhudia lile tukio la wale vijana wa T. Ano lakini hakujua ni jinsi gani angeweza kumsaidi Chriss. Alibaki ametuliza jicho lake kwenye lenzi ya bunduki yake ya kudungulia lakini bado alikuwa katika sintofahamu. Kumbe alikuwa ameyatilia mashaka yale magari na ndiyo maana akashuka pale, kilichomshtua ni kwamba hakutegemea kuona kundi la watu wale ambao walikuwa si chini ya kumi na wawili.
"my god" aliishia kusema hivyo. Alitaka kumjulisha kuwa pale alipo yupo kwenye hatari lakini aliogopa kumchanganya. Aliishia kuita tu Chriss, kwa kutumia vifaa vya kunasia sauti walivyokuwa navyo,
" Chriss". Sauti ile ndiyo iliyomfanya Chriss agande na kushindwa kulitupa majini lile begi kwa haraka.
"kuna ni............!" sauti yake haikufika mwisho, mlio mkali wa risasi ukasikika na kisha miliyo ya risasi kulindima mahali hapo. Chriss alishangaa asijue la kufanya ni kama alipigwa na bumbuwazi la nguvu mahali hapo.
Wale vijana wa T. Ano kabla hawaja ruhusu risasi kumuelekea Chriss, tayari wao walikuwa wamekwisha wahiwa na vijana wa BC. Sasa hapo ikawa ni kutupiana risasi na kwa kuwa vijana wa T. Ano, hawakuwa wamelitegea lile tukio, walipukutika kwa muda mfupi lakini hata hivyo hawakukoma kupeleka mashambulizi na kujihami.
"usishangae Chriss, yupo mmoja hapo amekulenga tupa majini hilo begi na ujirushe kichakani" ilikuwa ni sauti kutoka kwa Catherine na wakati anamaliza kusema, alichia risasi kwa kutumia bunduki yake ya kudungulia aliyoifunga kiwambo cha kuzuia sauti na kumlenga kijana ambaye alikuwa amemlenga Chriss. Chriss alishautupa ule mzigo baharini na kujirusha kichakani, risasi kadhaa zikapita pale alipokuwa amesimama, hakusubiri, alitambaaa kama nyoka kwa haraka na speed kali, huwezi amini kama yule alikuwa ni binaadamu kwa jinsi alivyokuwa akitambaa hapo kichakani. Vijana wa BC walikasirika sana baada ya kumshuhudia SM akiuwachia ule mzigo baharini, waliamua ni bora kumuuwa tu kwani kilichokuwa kimewapeleka hapo walishakikosa hivyo hawakuona sababu ya kumuacha hai msababishi wa jambo hilo. walichelewa, Chriss alijirusha kando na risasi zao kupiga hewa na hata walivyomtafuta kupitia lenzi za bunduki zao waliambulia hewa kwani kijana huyo aligeuka na kuwa kama nyoka kwa haraka sana kwa jinsi ambavyo alivyokuwa akitambaa mithili ya nyoka. Kukawa hakuna njia nyingine zaidi ya kutupiana risasi na mahasimu wao. Ilikuwa ni vita kubwa kila kikundi kilikuwa imara sana. Kikundi cha T. Ano kilipunguwa sana lakini hakikuwa lelemama na bila shaka ndiyo maana hata T. Ano mwenyewe alikiamini sana kikosi chake. Vita hiyo haikukoma hata kidogo hadi kukawa kimya kabisa bila kusikika mlio wa risasi hata mmoja, vijana wote wa makundi hayo tofauti waliuwana. Alibakia mmoja tu mahali hapo ambaye alifahamika kwa jina la kiongozi lakini hakuwa na uwezo wa kufanya lolote kwani mwili wake wote ulikuwa umejaa matundu ya risasi. Alijivuta taratibu na kwa tabu hadi pale alipokuwa amesimama Chriss na kuushika ule ukuta wa kingo ya bahari. Hapo hapo alianza kuhisi maumivu makali na hatimaye akadondoka akiwa ameulalia ule msingi roho ikiwa inauwacha mwili wake kwa maumivu makali mno. Kimya kikatanda mazima.
Chriss yeye alikimbia hadi alipokutana na Catherine.
"hongera sana kijana, tunaingia kwenye gari hiyo na kupotea mahali hapa kabla wanoko wa mji hawaja jaa" alisema Catherine, wakakimbilia kwenye hiyo gari na kubomoa mahali fulani ndani ya ile gari, wakaunganisha waya. Mara gari hiyo ikaunguruma, Catherine akakamata usukani na kuliondoa gari hilo kwa kasi kubwa mahali hapo.
***********%%%%%%%%%************%%%%%%%%%*************%%%%%
Kimya kizito kilitanda ndani ya hoteli moja ndani ya mji mmoja mkubwa hapo Brazil, hakukuwa na mtu yeyote aliyekuwa akiongea na si kuongea pekee, bali hata wahusika walio ndani ya chumba hicho cha hoteli, kila mmoja alikuwa amekaa upande wake. Chriss alikuwa dirishani akiwa kama mtu anayeushangaa mji mkubwa wa Brazil na Catherine yeye alikuwa amekaa kwenye kochi moja lililopo chumbani hapo. Kimya hicho kilichukua muda wa kutosha hadi pale sauti ya mhemo mkubwa iliposikika. Hapo ndipo ikawa mwisho wa kimya hicho kwani yule mtu ambaye alishusha pumzi hizo ambaye alikuwa ni Chriss, aliamua kuuvunja kabisa ukimya huo.
"sijaelewa huu mchezo ulivyochezwa Catherine, ni wakina nani wale waliovamia mpango wetu wa kuyateketeza yale madawa ya kulevya" aliuliza Chriss. Catherine akashusha pumzi nzito sana kisha akasema.
"bila shaka hawa watakuwa ni vijana wa mmoja kati ya vikosi hivi vinne vinavyoshirikiana"
"na kile kikosi chengine? Vilikuwa viwili vile kumbuka?" alihoji zaidi Chriss.
"hapo ndipo ninapochanganyikiwa lakini kimoja wapo kinaweza kuwa ni kikundi kilichogeuka kama sio viwili."
"unamaanisha kuwa walikuwa na mpango wa kugeukana?" aliuliza tena kwa mshangao Chriss.
"ndivyo ninavyofikiri mimi"
"sasa tunafanyaje, bado ule mpango wa kumwambia Joesan kuwa tumevamiwa na kikosi cha BC upo?"
"ndiyo ule mpango upo, tena utakuwa rahisi zaidi kwani ninaushahidi wa kumpa Joesan." aliongea Catherine huku akitoa kifaa kidogo mfukoni mwake, mithili ya memori kadi na kukipachika kwenye kadi lida kisha akaichomeka kwenye kompyuta yake mpakato. Picha mbalimbali zikawa zinaonekana kwenye ile kompyuta moja baada ya nyingine.
"ungelikuwa bado haujarudi kwenye hali yako ya kawaida, pengine labda ungeweza kuwafahamu.................
hawa watu lakini kwa nini walikuwa wengi hivi?" alisema Catherine kisha akauliza swali ambalo kwa kijana Chriss pia lilikuwa gumu.
"hebu ngoja, rudisha nyuma hiyo picha?" aliongea Chriss baada ya kuiona picha moja mahali hapo. Catherine akarudisha. Chriss akaitazama picha hiyo kwa umakini kisha akasema.
"huyu jamaa nimemkuta Ufaransa. Hapa sasa nimepata picha kuwa hivi vikundi vimegeukana na ninawasiwasi na hicho kingine pia kama siyo cha Mrusi basi ni cha BC." aliweka tuo Chriss kisha akaendelea kuuliza.
"kumbe uliwapiga picha aisee uko vizuri, uliwezaje sasa?" aliuliza kijana huyo na kutulia.
"niliwapiga kwa ile bunduki ya kudungulia, ni bunduki ya aina yake sana ambayo inauwezo mkubwa. Haijawahi kutokea bunduki yenye uwezo mkubwa namna hii. Inanguvu ya kupiga mbali pia inauwezo wa kuchukua picha za mnato japo hazina ubora sana kulingana na umbali uliotumika lakini tukimtumia hizi picha Joesan, anaweza kuwafahamu na kujua kuwa hawa ni kina nani kama ambavyo wewe umeweza kumfahamu huyu mmoja. Aliongea dada huyo na kumgeukia Chriss kisha akamwambia kuwa hakuna sababu ya kuchelewa, muda huohuo wafanye mawasiliano na kutuma hizo picha. Chriss akakamata simu na kulicheki jina la bosi kisha akalipigia. Akamueleza kila kitu kuhusu kupotea kwa mzigo na jinsi alivyo vamiwa lakini hakusema kama wako wawili na alikuwa na mpango wa kwenda kulitupa lile bag baharini bali aliamua kuwabebesha mzigo mazima vijana wale waliovamia. Joesan hakuelewa hilo jambo, matusi mazito mazito yakamtoka na kumuona kijana huyo ameanza kuwa mzembe. Alitukana sana Joesana, hakutaka hata kumpa nafasi tena kijana huyo ya kuongea, alimuona ni kiumbe mpumbavu kabisa tena alivuka hadi mipaka na kumuambia ni mara mia hata angekufa yeye kuliko kupotea kwa huo mzigo. Chriss hapo ndipo alipojiaminisha kuwa Joesan alikuwa ni kiumbe mbaya sana tena hakuwa na nasaba za kibinadamu japo alivikwa ngozi ya ubinadamu na kila kitu kinachofanana na binadamu lakini kwa hakika aliamini kabisa kuwa huwenda bwana huyo ndani alikuwa na damu ya kiumbe hatari kabisa hapa duniani. Joesan alisema haoni sababu ya kumuacha hai kama kapoteza huo utajiri lazima angemuuwa tu. Chriss alitamani kulia lakini hakuwa na moyo wa kike, moyo unaoshindwa kuhimili maumivu, Chriss alikuwa na moyo mgumu tena moyo wenye kuwa na subira ndani yake.
"ngoja nikutumie picha za watu walionivamia bosi na kutaka kuniangamiza." alisema Chriss akiwa anapambana na kifusi cha ghadhabu na hasira kilichojenga kichuguu kizito kifuani mwake. Joesan akamwambia azitume picha hizo na pia ajiandae kufa. Chriss aliikalia kompyuta yake ya kazi na kuichukua ile chiipu na kuanza kuzituma hizo picha, alituma picha zote hakuacha hata moja kisha akatulia kimya kusikilizia nini kitajiri baada ya picha hizo kumfikia mlengwa. Dakika kumi nyingi, Joesa alipiga simu na kumfanya Chriss kushtuka kidogo, alipomuangalia Catherine alimkuta akiwa ni mwenye kutabasamu.
"wamenigeuka washenzi wale, nasema haiwezekani, wamenigeuka aaaaghr!, Chriss sahau maneno yangu niliyoyasema hapo awali kwa sababu ya hasira. Panda ndege uje hata kama umekatika kichwa. Unahaki ya kushindwa kijana wangu, washenzi wale ni makatili na najua ulishindwa kwa sababu walikufanyia ambush lakini na sema wamekanyaga nyoja hatari mkiani ni lazima tuwamalize wote wajinga wale" alisema mithili ya mtu aliyedata Joesan, alikuwa akiongea maneno mengi bila mpangilio maalumu, ni wazi ya dhahiri kabisa alikuwa amepandwa na hasira mara zaidi ya nyingi. Chriss alitabasamu kisha akauliza.
"ni nani na nani hao walio nivamia boss" akauliza kwa kutega Chriss. Joesan akajibu kuwa ni kikosi cha T. Ano na BC. Chirss aliishusha simu chini na kuhema kwa nguvu sana huku wakicheka na kufurahi. Catherine wewe ni hatari sana aisee, nazidi kukukubali kila wakati, ni mwana mipango mzuri mno" alisifia Chriss akiwa anakwenda kumkumbatia dada huyo.
"kazi imebaki ndogo Chriss, wewe si wa kutumwa huku tena kuja kufanya mauwaji haya kwani si kazi yako hata kidogo. Hapo ulipo unakazi kubwa mno. Cha kufanya ni kuwachonganisha wenyewe kwa wenyewe wamalizane" alisema Catherine kwa kujitapa baada ya kutoka kifuani mwa kijana huyo.
"kivipi?" aliuliza Chriss.
"ingia hapo kwenye simu yako kuna namba, umeihifadhi kwa jina la Chalco, hiyo niliijenge mashaka muda tu japo sikutaka kukuamhia mashaka yangu, nafikiri hiyo hata upande wa whatsApp bila shaka ulishawahi kuitumia lakini hata kama hukuwahi kuitumia kwa WhatsApp, inabidi leo itumike. hebu ingia kwanza faster" alisema Catherine. Chriss hakusubiri, alifanya alivyoelekezwa na kukuta kweli namba hiyo inatumika huko pia.
"tuma hizo picha na umuandikie na maelezo. Mwambie kuwa hilo kundi limekuvamia na kuondoka na mzigo wote na hata kukukosakosa kukuwa japo umepambana vya kutosha. Sasa tunauhakika wa kufanya hivyo kwwni tukimwambia huyo ni wazi mambo yataharibika. Alipomaliza kutoa maelekezo hayo, muda mfupi kazi ikawa imekwisha.
" sasa hapo hatokujibu lakini naamini kwa huyo jamaa kutakuwa na kikosi cha kutosha na kwa ninavyowajua warusi, hawezi kukubali kushindwa au kudhulumiwa kikondoo, lazima atataka kulipa. Unafikiri wewe utahusika tena, hiyo ni vita ya wenyewe sisi tunakwenda kambini leo kwa ajili ya mambo mengine." alimaliza kuongea namna hiyo Catherine kisha akanyamaza na kumuangalia kijana huyo aliyeko hapo mbele yake. Macho yake ya kulegea kidogo yakamfanya Chriss kuachia tabasamu pana kabisa usoni mwake.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"umekuwa wa tofauti sana na nilivyokuacha, ile alama yako ya kwenye shavu la kushoto haipo tena, imefutika kabisa." aliwaza Catherine alipokuwa akimuangalia kijana huyo kisha akasema.
"acha mimi nikaoge na wewe pia kama utapenda, leo tunatakiwa kuwa Nairobi ili kesho kutwa uwe Tanzania kwa ajili ya mpango wako" alisema Catherine akiwa amekaa tayari kufungua mkanda wa vazi lake la suruali ili kuweza kulivua aelekee bafuni. Chriss alikuwa akiona kama masihara yaliyokuwa yanafanyika mahali hapo hivyo akawa amemkazia macho, hakuwa akipepesa hata mara moja. Catherine akalishusha vazi hilo hadi chini kidogo ya kiuno na kusitisha hilo zoezi.
"kwaiyo unataka kuona hadi hii nguo itakapotoka mwilini au?" aliuliza Catherine, Chriss akabaki akijitafuna kwa aibu. Ni kweli alikuwa akimtazama sana dada huyo pindi alipokuwa akiishusha suruali hiyo. Aibu yake ilimfanya ashindwe kabisa kumtazama dada huyo akabaki akitazama chini.
"nipe mgongo kabisa Chriss, hapo sina imani na wewe kabisa, nataka kuvua nguo zote" aliposema hivyo, Chriss aligeuka na kumpa mgongo binti huyo. Catherine alivua nguo zote na kujifunga kijitaulo kidogo kilichoishia juu ya mgoti na kumwambia Chriss kuwa anaweza kugeuka sasa. Chriss akageuka na kumtazama binti huyo ambaye alikuwa ameshampa mgongo Chriss. Kilikuwa ni kijitaulo kifupi sana hivyo mapaja yote yalikuwa wazi kwa asilimia kubwa sana. Kifuani hakuwa amevaa kitu, alikuwa ameiachia mikono yake na kukishikilia kile kijitaulo, hakuweza kuona kifua cha binti huyo Chriss kwani tayari binti huyo alikuwa akipiga hatua za madaha kabisa kuelekea ndani ya bafu hilo. Mwendo wake wa maringo ndiwo uliokuwa ukimpa maswali kijana huyo. Catherine alikuwa akirusha miguu kama hataki kuikanyaga sakafu ya humo ndani kwa jinsi alivyokuwa akitembea. Nyama zake za nyuma zilikuwa zikitikisika kwa uzuri wa kinamna namna kabisa. Chriss alijikuta akimeza mate kwa matamanio makubwa mno.
"majaribu haya sasa, inamaana hajui kama hapa ndani pana mwanaume au ni vipi? amenifanya nimeanza kumtamani sasa, wewe muache andelee kunitania tu, nitamlamba ohoo! Ananifanya hadi nimesimamisha kabisa aisee" aliwaza Chriss mara tu binti huyo alipopotelea bafuni.
Alipotoka huko bafuni, Chriss naye alipambua nguo na kubakiwa na boksa, yeye hata hakuona aibu mahali hapo na hata pia hakumzuia binti huyo asiangalie. Aliingia bafuni kuoga huku nyuma akiwa ameacha maswali mengi sana na mawazo ya kuzidi kwenye kichwa cha Catherine.
"Chriss unanichanganya sana na umbo lako hadi najihisi kuwa na wewe karibu lakini si sasa, hadi pale utakanijua mimi ni nani kwenye maisha yako na utakapo jijua wewe ni nani pia ndipo nitakapo kupa huu mwili. Nakupenda sana Chriss na nauahidi moyo wangu kuwa ipo siku kichwa changu kitalala kifuani mwako na pia mwili wangu utakuwa faraja yako." aliwaza Catherine akiwa tayari ameshavaa nguo zake na kuwa tayari kwa safari.
Saa 18:30 jioni. Ndege kubwa iliyokuwa ikitokea South Africa, ilikanyaga katika ardhi ya Kenyata na kukimbia kwa kasi kubwa. Ilikuja kisimama mahali ambapo ndipo zinaposimamia ndege hizo kubwa za abiria kutokea mataifa mbalimbali. Chriss na Catherine walikuwa miongoni mwa wasafiri waliokuwa wakitokea nchini Brazil kupita Afrika ya kusini kisha Nairobi Kenya. Walishuka taratibu wakiwa ndani ya mavazi yao ya kawaida sana, kila mmoja akiwa amekamata mzigo mkononi mwake, Catherine alikuwa amebeba mdoli mkuwa wa Simba pamoja na kibegi chake kidogo cha mkononi. Chriss yeye alikuwa amekamata begi lililokuwa limemeza Kompyuta mbili mpakato, ya kwake na ya Catherine huku mgongoni akiwa amebeba begi jingine lililokuwa limeficha mavazi yake ya kazi ambayo alikuwa akiyatumia kipindi ni Mashine ya ngono. Walifanya itifaki za hapo uwanjani kisha wakaelekea mahali ilipo gari moja ndefu sana. Hii ilikuwa ni Benzi, milango sita yenye rangi ya Creem ambayo ilikuwa imeigamiwa na kijana mdogo aliyeyaficha macho yake kwenye mawani ya macho na kofia ya kapelo.
"hizi kofia siyo type yako Amiri, mbona unapenda kulazimisha vitu" alisema Catherine baada ya kumkaribia kijana huyo kisha akaivua hiyo kofia na kuitupia kichwani mwake. Nako haikudumu sana, ilichukuliwa na Chriss na kuipachika kwenye kichwa chake.
"hata wewe unalazimisha, mijinywele yote hiyo na kofia wapi na wapi" alisema Chriss.
"mh! Haya chukua wewe mwenye kichwa cha kuvaa kofia.....Amiri, ona huyu jamaa ameimaindi pia kofia yako"
"hapo sisemi kitu tena, mimi nimekuja kuwapokea tu. Najua mmetoka mbali na safari ..........
na safari yenu ilikuwa moja sasa siwezi kujua mlianza kuchokozana wapi" alitania Amiri.
"acha ujinga Amiri, umeshaanza uwenda wazimu wako" alisema Catherine. Wote wakaangua kicheko kikubwa sana wakiwa tayari wameshapakia garini. Safari ikaanza namna hiyo. Walifika Nyumbani kwa Father D.A, wakashuka garini na kuingia ndani ya jingo hilo. Vijana watatu wakatoka ndani ya huo mjengo na kuja kuwalaki.
"karibuni sana nyumbani, karibu madame, karibu sana kiongozi" walikaribishwa namna hiyo. Chriss alishangaa sana kupewa majina mbalimbali ya uongozi. Hakuwa akielewa ni kwanini vijana hao walikuwa wakimheshimu hivyo ghafla. Alikuwa ni mtu asiye na msaada wowote kule shimoni hadi wanafika Brazil, sasa iweje awe ni mtu wa kupewa heshima na vijana hao. Wakiwa wanazidi kujuzana hali na habari, Sauti ya mtoto wa kike iliyokuwa inatoka ndani iliwashtua wote hapo na kujikuta wakigeuka kumtazama binti huyo mdogo ambaye alikuwa akipiga kelele kwa kuliita jina na Dada. Alikuwa ni Mery. Alikuja hapo na kumrukia Catherine kwa furaha kubwa kabisa. Catherine alimzunguusha binti huyo kwa furaha sana. Akamkabidhi ule mdoli kama zawadi kwake.
"niliku miss sana mdogo wangu, hujambo?" alisema Catherine.
"hata mimi nilikumiss sana Dada, sijambo umeniletea zawadi gani, unakumbuka?" alisema Mery kisha kudai zawadi yake ambayo ndiyo akiyoahidiwa na dada yake tukiutoa huo mdoli.
"kama hakuna?"
"kama hakuna nitalia sana kwa sababu uliniahidi" alisema Mery. Lakini muda wote huo wakati Catherine na Mery wakiwa wanazungumza mahali hapo, Chriss alikuwa kama amepigwa sindano ya gazi mwilini mwake. Muda wote huo yeye alikuwa akishangaa tena akiwa anamshangaa huyo binti mahali hapo. Ni kama alikuwa akimkumbuka lakini kumbukumbu zikawa zinakataa. Alikuja kuacha kushanga pale ambapo Catherine alipoanza kumuuliza Mery kama hao watu waliopo hapo amewazoea na kama anawafahamu kwa majina pia.
"umesha wazoea wajomba wote?"
"ndiyo, nimeshawazoea tayari na wananipenda"
"unawafahamu kwa majina?"
"ndiyo, nawafahamu"
"hebu nitajie mtoto mzuri nikakupe zawadi yako" alisema Catherine na kumfanya Mery kuanza kuwataja watu hao kwa majina na kuwagusa kabisa akiwa bado yupo kwenye mikono ya dada yake.
"huyu hapa ni Uncle Charls, huyu hapa ni uncle Zomba, huyu hapa ni uncle Amiri na huyu hapa ni uncle Jay na......na...nahu.....huyu ni.....kakaaa, kakaaaaaa, oooh my God, my brother Chriss. I miss you very much my brother" alipiga kelele Mery hadi kina Zomba wakajikuta wanapigwa na taharuki kubwa mahali hapo. Mery aliruka kutoka mikononi mwa Catherine na kumrukia Chriss ambaye alimuwahi kwa kumdaka. Ilikuwa ni furaha kubwa sana iliyozirudisha kumbukumbu za Chriss mazima. Machozi yalimmwagika kijana huyo. Alijiona amerudi tena duniani baada ya kupotea katika sayari hiyo ki fikra na kiuhalisia takribani mwaka mmoja na miezi mitano. Alilia Chriss, alilia sana, hakujua hata amshukuru vipi Catherine kwa kumkutanisha tena na mtu aliyekuwa anampenda sana. Machozi yake hakuna aliyeweza kuyarudisha kwenye chemchem yake huko yalikotoka. Hata Catherine alipojaribu kumpa maneno ya kumtia nguvu na ushujaa bado Chriss alikuwa anadukuduku kubwa mno.
"asante sana dada kwa kuitimiza ahadi yako. Asante kwa kuniletea kaka Chriss" alisema Mery. Vijana wale wanne wakaungana na kumpigapiga mgongoni ikiwa ni moja ya kumpa uvumilivu kijana huyo. Mery alishindwa kujua acheke kama alivyokuwa akicheka mara tu alipomuona kijana huyo au aliye kama anavyolia kijana huyo ambaye ndiye kaka yake wa ukweli, japo hawakuzaliwa pamoja lakini historia zao zilifanana na hicho ndicho kilichomfanya Chriss kulia kwani aliamini kabisa Joesan na mkewe, hawakuwa uwezo wa kupata mtoto. Hivyo hata uchungu wa wa mtoto hakuwa nao. Sasa kama amethubutu kumgeuza yeye kuwa mashine ya ngono, inamaana huyu angekuja kuwa kahaba wa kimataifa.
"kuna muda unaweza ukajihisi umetengwa na dunia, kutokana na matatizo yanavyokuandama peke yako" sauti nzito ilisema kutokea nyuma. Sauti ambayo ilikikata kilio cha Chriss ghafla. Sauti hiyo baada ya kuweka koma, ikaendelea.
"matatizo ni ya wengi lakini yanatofautiana, yanatofautiana ndiyo, hata mimi nakubali. Yatofautiana kivipi?" akaiacha alama hiyo ya kuuliza mtu huyo ining'inie mahali hapo kwa muda kisha akairudia na kuifanyia kazi.
"yatofautiana kwa sababu kila anayekutwa na tatizo au matatizo, hujiona yeye ndiye mwenye matatizo makubwa kuliko wenzake wote waliowahi kukumbwa na matatizo kama yake au pengine kuzidi yake." mtu huyo akaweka kituo kikubwa hapo na kuja mbele ya hao vijana ambao walikuwa wakimsikiliza bila kugeuka. Alipofika mbele ya macho yao, akanyanyua macho na kumtazama moja kwa moja Chriss.
"kijana, yaliyokukuta ni makubwa sana na laiti kama ungeyajua, usingelia bali ungeomba kuirudisha nyuma historia hiyo na isingewezekana. Karibu sana katika maisha mapya, maisha ambayo ndiyo ulipaswa kuishi toka zamani" alipomaliza kusema hivyo mzee huyo, aliitupia mikono yake nyuma kwa mtindo wa kupendeza kabisa na kuondoka hapo kwa hatua tatu mbele. Chriss akamkimbilia na kutaka kujua ni nini kingine kipo nyuma ya pazia lakini mzee huyo aliongeza mwendo na kuzidi kuondoka mahali hapo. Chriss alipotaka kukazana ili kutaka kumshika mzee huyo, alikutana na mikono laini ya kike iliyomshika bega na sauti tamu kupenya katika masikio yake.
"yule hawezi kuongea tena na wewe, alichotaka kufanya hapa ni kukupa nguvu na moyo wa kujikubali na kuamini kuwa wapo wenye matatizo makubwa zaidi yako. Kuwa na moyo wa kiume ili uweze kukubaliana na mengi. Yule ni master wa Tempo si chini ya nne, ni mwingi wa kufikiri na kujua njia za kumtoa mtu kwenye majonzi na uchungu alionao. Pia ndiyo maana akakuacha kwanza ulie kwa muda ndipo akupe haya maneno ambayo kwa mtu mpambanaji kama wewe, usingeweza kuminyana na badala yake ungechukua muda kuyatafakari." aliongea Catherine. Yalikuwa ni maneno ambayo kama si mpambanaji ungeweza kuona labda binti huyo amekudharau lakini yalikuwa ni maneno kuntu sana na yenye kumtoa mtu kwenye huzuni aliyonayo, kumrudisha kwenye hali ya kawaida. Chriss alijua kweli pengine kuna mengi zaidi ya hayo anayoyajua yeye, alichofanya ni kuwatazama watu walioko hapo kila mmoja. Kila aliyemtazama alikuwa akitikisa kichwa chini juu kuonesha kuwa yaliyokuwa yamezungumzwa na dada huyo, yalikuwa ni mambo ya msingi sana. Akakirudisha kichwa kwa Mery, akakuta binti huyo anamtazama kwa macho ya kumwambia 'kaka mwanaume wa kweli halii bali anacheka hata asikiapo mama yake mzazi amefariki kwa kuuwawa, ili tu kuupa moyo faraja ilihali unaumia'. Alimsogelea binti huyo na kumbeba kisha akampiga busu la kwenye paji la uso na kumwambia.
"nitazame ninavyocheka, hivi ndivyo nilivyo mdogo wangu, kilio kile kilikuwa ni cha kukukumbuka tu, kwa sababu sikupata kukuona muda mrefu na nakuahidi kuwa sitalia tena kwa sababu sitakubali kukaa mbali nawe tena"
"kweli kaka Chriss?" aliuliza Mery akiwa analirudisha lile tabasamu lililokuwa limefifia
baada ya kumshuhudia kaka yake akilia.
"kweli kabisa Mery, niamini mdogo wangu, nakupenda sana" alisema Chriss huku na yeye akirudisha tabasamu. Mery akasema.
"sasa nakuamini, na nakupenda pia kaka" kisha akamrudishia kaka yake busu la shavuni.
********************%%%%%%%%%%%%****************
"Rafael, nimewaiteni hapa ninyi watu watatu kwa sababu maalumu" aliongea Joesan akiwa kwenye kiti cha ofisi yake, akaendelea.
"nadhani mnakumbuka kilichotokea nyumbani kwangu siku tatu ama nne kama siyo tano zilizopita." akaweka tuo na kuwatazama watu hao waliokuwa wakimsikiliza kwa makini kabisa. Watu hao wakatikisa vichwa vyao ikiwa ni ishara ya kuwa kilichoongelewa hapo kimeeleweka. Joesan akameza mate kidogo na kutulia kwa kama sekunde kadhaa, akamtazama kila mmoja kwa nafasi yake. Alimtazama Rafa, akarudi kwa Suzane na mwisho alimtazama Merina. akaendelea.
"kile kifo kilichomtokea mke wangu, hakikuwa kifo cha kawaida hata kidogo, ni kifo cha kupangwa na binadamu wenye mpango maalumu. Niseme tu kitu kimoja, waliotekeleza hayo mawaji si watu wa mzaha. Wana uweledi wa kuuwa na wanatumia akili nyingi na nguvu ndogo sana. Sitaki kuwasifia hao wauwaji mahala hapa, bali nilichowaitieni hapa ni kwamba sasa ndiyo ule wakati wa ninyi kufanya kazi yenu. Kila mmoja akae kwenye jukumu lake." aliongea hivyo Joe kisha akaita.
"Suzane," Suzane akaitikia, kisha bwana Joe akaendelea.
"ni wakati wa kuzifungua kucha zako ulizozificha muda mrefu. Kuwa tayari kwa kazi muda wowote, kuna watu wananusa harufu yetu na wewe Rafael, hakikisha vijana wako wanakuwa tayari kwa kazi kuanzia sasa. Merina wewe kazi yako ni moja tu ya kuhakikisha usalama wangu maana sina imani tena. Sex machine anaingia kesho kutwa hapa, nadhani akija yeye atakuwa na jukumu lake" alisema Joesan na kutulia kimya kama anayetaka kusikia nini kitachangiwa hapo. Alipoona hakuna cha zaidi, aliwaamuru warudi nafasi zao za kazi na yeye akabaki akiwa anatafakuri nzito mahali hapo.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"sikuwa nimewaza tofauti hata kidogo, nilijua tu kuwa kuna zaidi ya umeme, nilijua tu kuna kitu kiliendelea. Na sasa wamsubiri huyo Sex machine wao ili tujue kama kweli ni yeye au tayari ameshabadilishwa" alikuwa akiwaza mzee Rafael mara tu alipokuwa ameingia kwenye ofisi yake. Akili yake iligoma kabisa kumkubalia kuwa eti, Sex machine alikuwa yupo kama alivyokuwa hapo nyuma, aliamini kabisa kuwa kwa muda huo walikuwa na ..........
, Sex machine alikuwa yupo kama alivyokuwa hapo nyuma, aliamini kabisa kuwa kwa muda huo walikuwa na wakati mgumu sana na walipaswa kujipanga. Cha kushangaza hakupenda kile anachokihisi kuwaambia mabosi wake, haikujulikana ni kitu gani kilichofanya abaki nayo hiyo siri. Pengine kuna mengine au ni yale yale tunayoyajua.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment