Search This Blog

Monday, October 24, 2022

USIKU WA BALAA - 3

 





    Chombezo : Usiku Wa Balaa

    Sehemu Ya Tatu (3)



    ILIPOISHIA



    Sikuamini kama nilikuwa nimepata wasaa mzuri kama ule. Sikutaka hata kujishauri mara mbilimbili. Nilichokifanya ni kuchomoka mbio huku nikiwa uchi kama nilivyozaliwa.



    Nilitoka nje kwa spidi kali na kulakiwa na jua kali kuashiria kwamba ilikuwa mi mchana mchanga kabisa. Watu wengi pia walikuwa wakiendelea na shughuli zao huku nje. Mimi sikuwajali, bali ni kuzicharaza mbio kali huku nikiwa uchi wa mnyama.



    SASA ENDELEA



    Yaani hapa sikuijali fadhaa ambayo ningeipata bali nilichokiona cha muhimu kwa wakati ule ni kuukoa uhai wangu ambao ulikuwa hatarini.



    Licha ya uhai, kitendo ambacho alitaka kunitenda yule bwana mume wa Nancy hakikuwa cha kiungwana. Yaani mwanaume mzima niingiliwe kinyume cha maumbile! We haiwezekani hata kidogo. Ni bora niikubali na kuibeba fedheha kuliko kulawitiwa.



    Kitendo changu cha kutoka ndani ya nyumba ya Nancy nikiwa uchi wa mnyama huku nikikimbia sana kiliwastaajabisha watu wengi ambao walikuwa wakiendelea na shughuli zao.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wengi wao kwa muda fulani waliziacha shughuli zao na kuyatupa macho yao kwangu huku wakiiachama midomo yao kwa fadhaa. Watoto ndio walivunjika mbavu kwa kicheko huku sasa wakianza kunikimbiza huku wakipiga kelele.



    Niligeuka nyuma na kuliona kundi la watoto pamoja na watu wazima wakija kwangu kwa kasi huku wakipiga kelele za kunizomea. Katika mlango wa nyumba ya Nancy, nilimwona yule mume wa Nancy akiwa amesimama mlangoni huku akiwa amefura kwa hasira.



    Wengine miongoni mwa waliokuwa wakinifukuza walidhani huenda mimi nilikuwa ni mwendawazimu na wengine walifahamu fika kwamba mimi si mwendawazimu. Baadhi walinifahamu fika kwamba mimi ni kiwembe na siku hiyo walitaka kunikomesha kwa kipigo kitakatifu ili niachane na tabia ile mbovu kabisa ya uzinzi.



    Kelele za umati ule wa watu zilizidi kugonga katika mboni za masikio yangu na kunizidishia hofu. Kuna nafsi moja iliniambia nisimame huenda wale watu wangenisitiri japo kwa mavazi lakini kwa upande mwingine kuna msukumo ulikuja na kuniambia niendelee kuzicharaza mbio kwani watu wale wangeniteremshia kipigo cha hali ya juu na kitakatifu kabisa.



    Nikairuhusu miguu yangu iweze kunichukua kwa kasi ya ajabu kuelekea mahali ambapo niliona pangekuwa na usalama wa kutosha. Kundi lile la watu halikuacha kunifukuza bali lilizidisha kasi huku kelele nyingi za hamasa ya kunishika zikitawala.



    Unajua mimi si mtu wa mazoezi hata kidogo. Masuala ya kukimbiakimbia hayakuwa kabisa moyoni mwangu. Nilishangaa sana siku ile jinsi nilivyozifukua mbio kali mithili ya swala. Sifahamu zilitoka wapi zile mbio.



    Spidi yangu ilikuwa ni kubwa kabisa. Na nahisi kama ningelishiriki mashindano yam bio ya dunia basi nchi ya Bantu tungeunyakua ubingwa

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sikutaka kabisa kuelekea katika mtaa ambao nilikuwa nikiishi kwani niliona huko nitaadhirika sana. Ningeuficha wapi uso wangu kwa jinsi nilivyokuwa maarufu. Nikaamua kuuchukua upande wa mtaa mwingine ambao ulikuwa tofauti kabisa na ule mtaa ambao ninaishi.



    “Jamani Ima mimi mbona leo naadhirika mchana kweupe. Nitafanya nini mimi kuisitiri aibu hii inayonikumba?”. Nilikuwa nikijiuliza swali hili la msingi pindi nilipokuwa nikishindana na lile kundi la watu waliokuwa wakinifukuza.



    Pia nilizidi kumwomba mwenyezi Mungu aweze kuniokoa katika dhahma hii iliyokuwa ikija nyuma yangu. Sikutaka kabisa watu wale wanitie mikononi maana wangenimaliza kwa kipigo.. Lahaula! Leo mbona kazi ipo.



    Mungu si Athumani. Ghafla mbele yangu niliiona nyumba ambayo ilikuwa imeachwa mlango wazi. Ilikuwa ni nyumba ya kawaida kabisa ambayo ilionesha kuwa ilikuwa ikimilikiwa na watu wenye kipato cha chini kabisa kimaisha.



    Akili ilinichemka haraka sana mithili ya jungu la maharage lililoinjikwa katika mafya. Maamuzi niliyoamua kuyachukua kwa wakati ule ndiyo ambayo niliyafanya. Sikutaka kufikiri mara mbilimbili kwani muda wa kufanya hivyo haukuwa rafiki kabisa kwangu.



    Nilizama ndani ya nyumba ile pasi hata kubisha hodi. Sikufahamu ni nani walikuwa wakiishi katika nyumba ile na walikuwa ni watu wa aina gani bali nilichojali mimi ni stara na kuokoa maisha yangu tu.



    Lilitokea jambo ambalo sikulitarajia hata kidogo kutokea katika nyumba ile niliyoivamia mithili ya mwizi wa karanga katika shamba la mzee Maina.



    Wakazi wa nyumba ile walikuwa wametulia tuli juu ya mkeka walioutandika huku wakiwa wameuzunguka ugali mkubwa ambao walikuwa wakiutafuna kwa raha zao.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa kuwa sikuitarajia hali ile, nilijikuta nimejikwaa kwenye miguu ya mmoja wa wanafamilia wale. Kujikwaa kule kulisababisha niudondokee ule ugali huku mjomba akiwa amejichomeka kwenye ugali ule ambao ulikuwa ni wa moto kiasi.

    ********************

    Nilizinduka ghafla kutoka katika usingizi mzito ambamo nilikuwa nimetopea. Kwa pupa niliyafikicha macho yangu ili yaweze kuona lakini ilikuwa hola!. Giza nene ndilo ambalo lilikuwa limetawala katika eneo lote ambalo nilikuwa nipo kwa wakati ule.



    Wakati wote huo kumbukumbu zangu zilikuwa zimepotea na sikutambua ni nini ambacho kilikuwa kimenitokea mpaka nikawa katika hali ile. Mwili wangu wote ulikuwa ukitetemeka kwa baridi kali ambalo lilikuwa likiyatafuna maungo yangu.



    Baada ya muda fulani ndipo kumbukumbu zikaanza kunirudia taratibu. Nikaanza kulikumbuka sakata la aibu ambalo lilikuwa limenitokea mchana wa leo na kuniletea dhahma kubwa sana pale mtaani.



    Nikaanza kujiuliza hivi ni kwa nini niliendekeza sana uzinzi? Pia nikajiuliza ni kwa nini nisioe ili kuepukana na majanga kama aya ambayo yalikuwa yakinipata mara kwa mara?.



    Hatimaye nikajijibu mwenyewe kwamba ulimwengu wenyewe ulikuwa umetawaliwa na warembo wenye mvuto hivyo nilikuwa sina jinsi bali kuwafaidi warembo hawa ambao mwenyezi alikuwa ametujalia.



    Pia niliona kuoa kungeninyima uhuru wa kuwatafuna hawa warembo ipasavyo. Nikahitimisha kwa kusema hakukuwa na sababu muhimu ya mimi kuoa.

    *****************

    Nilipata aibu kubwa sana ambayo nilishindwa kabisa kuibeba. Aibu hii ilinifanya nishindwe kwenda kazini kwa kuhofia macho ya majirani pale mtaani kwani ile skendo ilikuwa imeenea kwa kila mtu kuanzia watoto, vijana mpaka watu wazima.



    Hatimaye nilifanikiwa kuhama mtaa ule ambao nilikuwa nikiishi bila ya kufahamika na majirani kwamba nilikuwa nimehamia wapi. Tukio la kufumaniwa kwangu lilikuwa ndiyo habari ambayo ilikuwa ikizungumziwa pale mtaani nilipokuwa nikiishi awali.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Jiji la Kano ni kubwa sana. Nilipata nyumba maeneo ya Mwambani. Niliamini kabisa habari za kule nilikotoka hazingeweza kufika huku hata kidogo. Niliamini huku nitaishi kwa raha mustarehe huku nikiendelea kuyafaidi maisha bila ya bughudha yoyote ile.



    Kuna jambo moja zuri sana ambalo lilinivutia katika mtaa huu ambao nilihamia kwa sasa. Mtaa ulikuwa umebarikiwa watoto warembo wenye kukonga nyoyo. Kila eneo nililokatiza ilikuwa ni lazima nikutane na warembo kama si wawili basi ungekutana na mmoja.



    Niliona huu ndio mtaa ambao nilikuwa natakiwa kuishi mtu kama mimi. Yaani mtaa ulikuwa na huduma muhimu na za msingi kama hizi? Kweli niliona bahati imeangukia mikononi mwangu. Niliamini hapa sasa zeze lilikuwa limempata mpigaji na kama ni zumari basi lilikuwa limempata mpulizaji.



    Nilianza kujilaumu kwa muda wote ambao nilikuwa nimeupoteza kwa kuishi katika mitaa ambayo haina huduma nzuri na za msingi kama hizi zinazopatikana katika mtaa huu.



    Warembo wa mtaa huu walianza kukipagawisha kichwa changu kabisa. Nilitamani niwamiliki wote kwa wakati mmoja.



    Nikakaa chini huku kichwa changu kikiwa kimeitamalaki mipango na mikakati mingi ya kuweza kuwapata warembo hawa wa kimataifa. Nilikiamini sana kichwa changu kwa kuweza kupanga mipango na mikakati mingi ambayo mara nyingi huzaa matunda.

    ***************

    Leo hii nilikuwa nimetulia tuli ndani ya gari aina ya Toyota Land cruiser huku macho yangu yakiwa makini na barabara na mikono yangu ikicheza na usukani. Mkono wangu wa kushoto ulikuwa ukifanya kazi ya kukichezea kirungu cha gia huku ule wa kulia ukiwa umekamata usukani imara kabisa.



    Wimbo laini kutoka kwa mwanamuziki wa kimataifa Celine Dion uitwao “You are my angel” uliendelea kuziburudisha ngoma za masikio yangu.

    Nilkuwa katika moja ya safari ya kuyatekeleza majukumu yangu ya siku katika kampuni ambayo nilikuwa nikiifanyia kazi.



    Mimi nilikuwa ni mesenja na kazi yangu ilikuwa ni kutumwa na bosi wangu mahali mbalimbali katika jiji la Kano kuchukua na kupeleka mizigo na vifurushi mbalimbali. Pia mara nyingine nilikuwa nachukua na kupeleka ujumbe mbalimbali.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Safari yangu ilikuwa ikinipeleka katika mtaa wa Mwaloni mahali ambapo bosi wangu alikuwa amejenga makazi yake na alikuwa akiishi na mkewe. Nilikuwa nimetumwa na bosi wangu kwenda kupeleka mizigo fulani huko na kisha nirudi ofisini.



    Mawazoni mwangu nilipanga kuupeleka mzigo ule wa bosi haraka kisha nirejee kazini haraka sana. Sikupenda kuupoteza muda wa kazi hata kidogo.

    ****************

    “Oooooh! Karibu sana Ima”. Ilikuwa ni sauti ya Meselina mke wa bosi wangu ikinikaribisha kwa kunirai rai.



    “Ahsante sana mama, nimekwishakaribia”. Nilimjibu Meselina huku mwili wangu nikiusogeza kuuingiza ndani ya nyumba ile ya kifahari iliyosheheni fanicha mbalimbali za kifahari.



    “Ima nilikwishakukataza kuniita mimi mama. Yaani kwa umri wangu huu mimi naweza kuwa mama yako?”.



    “Hapana nisamehe!”. Niliomba radhi kudhihirisha uungwana wangu.



    “Napenda sana kama ukiniita Meselina”.



    “Usijali Meselina. Itikadi itazingatiwa”. Niliongea huku mwili wangu nikiubwaga juu ya mojawapo ya sofa za kifahari zilizokuwemo mle ndani.



    “Bosi kanituma nije nikuletee mzigo huu”. Nilimkabidhi mfuko wa plastiki uliokuwa mikononi mwangu ambao ulikuwa umesheheni madikodiko mbalimbali.



    “Ahsante Ima”. Aliupokea mfuko ule na kuupeleka jikoni kisha akarejea pale sebuleni.



    “Sasa Meselina mimi naona bora nikuache niwahi kazini”. Nilimuaga Meselina.



    “Hapana huwezi kuondoka hivihivi Ima. Ngoja upate juisi ya baridi ili ulitulize hili joto kali la hapa Kano”.



    “Hapana Mese, nitakunywa siku nyingine”. Nilisisitiza nikihofia kuchelewa kurudi kazini.



    “No! noooo! Ima. Unywe leo”. Mese aliongea huku akiwa amenikata jicho moja ambalo lilikuwa kubwa na limelegea ambalo lilinifanya nisalimu amri kabisa na kuketi tena juu ya sofa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati huohuo Meselina alikuwa amekwenda katika friji na kuchukua bilauri na kulileta mezani. Kisha akaenda kabatini na kuchukua glasi na kuja nayo pale mezani kisha akamimina juisi na kunikabidhi. Naye pia akajimiminia katika glasi yake kisha tukagonga chiazi na kuanza kuzinywa.



    “Ima nisubiri kidogo, naja sasa hivi”.



    “Ok Meselina, wala usijali”.



    Meselina aliondoka na kuelekea upande wa veranda ya nyumba ile ambako kulikuwa na vyumba vingi.



    Niliendelea kuburudika na sharubati ile baridi ambayo kiuhalisia ililipooza koo langu kutokana na joto kali la jiji la Kano.



    Baada ya dakika kama tano Meselina alirejea pale sebuleni. Safari hii kidogo alinishangaza na kuniacha nikiwa nimebung’aa. Meselina alikuwa amebadili mavazi yake na sasa alikuwa katika vazi moja la khanga tu ambalo liliyachora vilivyo maumbile yake.



    Meselina alikuwa ni mwanamke mrembo sana. Alikuwa ni mwanamke mwenye sura nzuri sana yenye mvuto. Rangi yake ilikuwa ni ya maji ya kunde yenye mvuto. Kifua chake kilikuwa kimebebwa na matiti ambayo yalikuwa yanapendeza kuyatazama.



    “Ima yaani siku hizi kuna joto sana”. Meselina aliongea huku akikaa katika sofa lillilokuwa mkabala nami huku akiitanua miguu yake na kuifanya kanga aliyovaa isiweze tena kuyasitiri mapaja yake yaliyokuwa yamenona haswa.



    Macho ya tama yalinitoka pima. Niliamini kabisa Meselina alikuwa akinifanyia makusudi kabisa. Sasa kichwa change kilianza kuchanganyikiwa kabisa.



    “Ni kweli meselina. Siku hizi kuna joto sana aisseh!”. Nilimjibu huku nikiwa sijielewielewi kwani sasa midadi ilianza kunipanda.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ghafla Meselina alisimama na kuja kukaa pale ambapo nilikuwa nimekaa mimi. Miili yetu sasa ilikuwa imegusana na kusababisha shoti fulani mithili ya umeme katika mwili wangu. Hali yangu sasa ilianza kuwa mbaya taratibu.

    ****************



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog