IMEANDIKWA NA : INNOCENT A. NDAYANSE (ZAGALLO)
*********************************************************************************
Chombezo : Jicho La Kamore
Sehemu Ya Kwanza (1)
KUNA waliomwona kuwa ni chizi. Wengine walimfananisha na kipofu wa tangu kuzaliwa, kipofu ambaye kwa muujiza fulani amejikuta akifumbuka macho na kuona vya kushangaza na kutamanisha. Walikuwepo pia ambao walimweka katika kundi la limbukeni. Na wapo ambao walimjumuisha na wakware.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Aliitwa Kamore. Alizaliwa Marangu mkoani Kilimanjaro. Aliishi huko Marangu kwa kipindi kile tu cha masomo ya elimu ya msingi, na alipoingia sekondari, wazazi wake nao wakawa wamepata uhamisho wa kikazi kwenda jijini Dar es Salaam. Huko akafikia katika shule ya sekondari ya Benjamin Mkapa.
Mwaka wa kwanza alikuwa yuleyule Kamore aliyeyapenda na kuyajali masomo kwa kiwango kilekile cha juu. Mwaka wa pili, akiwa na umri wa miaka kumi na saba, alianza kubadilika. Ilitokea siku moja akiwa darasani peke yake mara akaingia msichana mmoja aliyekuwa akisoma kidato cha nne. Huyo aliitwa Lightness.
Lightness alikuwa mwanafunzi wa kidato cha nne. Alikuwa ni mrefu kiasi na mwenye macho ambayo muda mwingi huonyesha ‘kuchoka’. Ngozi yake nyeusi, iliyomeremeta, haikuchusha machoni mwa watu. Ulikuwa ni ule weusi wa kupendeza, weusi wa kutakata.
Mara nyingi Lightness alikuwa mcheshi, na maongezi yake yalijaa kauli zisizowakera watu. Ni mara chache sana tabasamu lilikosekana usoni pake. Kwa ujumla alikuwa ni mzuri wa sura na umbo, na uzuri huo ukiongezeka kutokana na ucheshi uliomtawala kila wakati.
-
Siku moja Lightness aliingia ndani ya darasa alilokuwamo Kamore. Ilikuwa ni saa 7 mchana. Wanafunzi wengine walikuwa mapumzikoni. Darasani humo alimkuta Kamore peke yake. Machoni mwa Lightness, Kamore hakuwa mgeni. Alishamwona mara kwa mara wakati aingiapo darasani humo. Na alivutiwa na upole wake na utanashati wake.
Lakini siyo kwamba alipoingia humo alikuwa kamfuata Kamore. La. Alikuwa kamfuata rafiki yake, Loveness. Na hakuwa na haja ya kuuliza kwani, zaidi ya Kamore hakukuwa na mtu mwingine humo ndani. Lakini hata hivyo, Lightness alihoji, “Lightness yko wapi?”
“Nadhani atakuwa amekwenda na Joyce pale kwenye chipsi,” Kamore alimjibu.
“Huwa anakula wapi?”
“Sijui,” Kamore alijibu huku sasa akiacha kusoma kitabu na kumtazama Lightness sawia usoni.
Walipotazamana, kama kawaida yake Lightness alitabasamu, likiwa ni lilelile tabasamu lake ambalo kwa yeyote ambaye hajazoea kukumbana na tabasamu la aina hiyo, kwa vyovyote vile atasisimkwa mwili. Kamore akayaepusha macho yake haraka na kulirudia daftari lake.
“Mbona wewe umebaki?” Lightness alichokoza.
“Basi tu.”
Wakati huo kumbukumbu zilianza kumjia Lightness. Alikumbuka kuwa, mara mbili, tatu aliwahi kuwasikia wasichana wa kidato cha pili wakimzungumzia Kamore; kwamba ana akili sana na hupewa pesa nyingi na wazazi wake. Shilingi 2,000 au 3,000 alizopewa na wazazi wake takriban kila siku, na kila siku vilevile akaziteketeza kwa kununua hiki na kile zilimwongezea hadhi kwa wanafunzi wenzake kiasi cha kumchukulia kama 'tajiri mdogo' darasani humo.
Ni taarifa hizo zilizompa wazo Lightness, wazo la kufanya kile alichozoea kuwafanyia wale walioonekana kama vile ni 'walokole,' watu wanaojitahidi kuzitii Amri zote Kumi za Mungu kwa nguvu zote.
“Nakuuliza wewe, mbona huendi kula?” alimshtua kwa swali hilo.
Kamore alikiacha tena kitabu chake cha Biology. Akamtazama Lightness ambaye kama kawaida yake, tabasamu pevu lilichanua usoni pake.
“Nitakwenda,” hatimaye alimjibu.
“Saa ngapi?” sasa Lightness alikuwa ameshamsogelea na kuanza kumpapasa nywele. Kisha akakipenyeza kidole kimoja katika sikio la kulia.
Kwa mbali Kamore alihisi kusisimkwa mwili. Na hali hiyo haikuwa siri machoni mwa Lightness, alijua kuwa tayari Kamore kachanganyikiwa. Hema yake ilitosha kutoa taswira kuwa leo Kamore kapatikana. Dakika iliyofuata vidole vya Lightness vilikuwa mahala pengine, katikati ya miguu ya Kamore, vikichezea sehemu moja hadi nyingine.
Kamore alizidiwa, akahisi mapigo ya moyo yakizidi kupanda.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Lakini mara Lightness akamwacha na kumwuliza, “Kamore, unaweza kutoroka kabla ya saa kumi?”
Kamore alishusha pumzi ndefu. “Kutoroka?” hatimaye naye akauliza.
“Ndio.”
“Kutoroka kwenda wapi?”
“We, kubali kwanza.”
“Ndiyo, naweza.”
“Ok, utanikuta pale kituoni nakusubiri.”
“Kituo gani?”
Lightness alifikiri kidogo, kisha akasema, “Sokoni Kariakoo.”
“Sokoni?! Mbona mbali sana? Kwani tunakwenda wapi?”
“Kamore una maswali ka' paparazi?” Lightness alimdaka. “Kijana mpole kama wewe, mtanashati, haupaswi kuwa na hofu kama vijana wa bushi. Kwani kuna umbali gani kutoka hapa mpaka sokoni? We' Kamore vipi? Umekua Kamore.”
Kamore aliona haya kidogo. Hakutaka kuonekana mshamba mbele ya Lightness. Akakuna kichwa akifikiri. Lakini Lightness hakumpa muda, akamwuliza, “Kwa hiyo inakuwaje?”
“Poa.”
“Ok, fanya hivi, jitahidi uchomoke saa nane au nane na nusu,” Lightness alisema kwa kujiamini. Kisha akatupa swali, “Una simu?”
Lilikuwa ni swali ambalo Kamore aliona kama vile ni aina nyingine ya udhalilishaji. Wanafunzi wengi shuleni hapo walikuwa na simu za mikononi. Yeye hakuwa nayo. Kutokuwa na simu aliona kama vile ni taswira halisi ya kumweka mtu katika daraja la chini. Mtu maskini, aliyezaliwa katika ukoo wa kimaskini. Unyonge ukamjaa moyoni. Akayaepuka macho mazuri ya Lightness. Kisha kwa unyonge huohuo akajibu, “Sina.”
“Us'jali,” Lightness alisema huku akimpa Kamore simu yake. “Kaa na hii simu yangu,” alimwambia. “Humo nimesevu namba ya simu na jina la Loveness. Nitakapokuwa darasani nitakuwa na simu ya rafiki yangu. Utakapotoka, unipigie au uni-beep. Nitajua.”
“Niku-beep wakati gani?”
“Utakapokuwa umeshatoka darasani. Najua huwezi kukosa mbinu ya kumdanganya mwalimu. Zipo sababu nyingi tu za kutumia. Mtoto wa town huwezi kushindwa.”
Ilikuwa kama walivyopanga. Walikutana kando ya soko la Kariakoo, na ndipo Lightness alipotoboa kuwa alitaka waende Msasani kwa dada yake.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kuna nini?” Kamore alizidi kushangaa.
“Wasiwasi wa nini, Kamore?” Lightness alicheka kidogo. “Mbona hujiamini? Unahofia kuchunwa ngozi? Acha woga, Kamore! Biashara ya kuchunwa ngozi imekwishapitwa na wakati...twen'zetu, au hupendi kutembelea watu?”
Kamore aliufyata. Wakazifuata daladala za Msasani zilizokuwa kwenye foleni zikisubiri abiria. Wakaingia. Nusu saa baadaye walikuwa wakiteremka eneo la Namanga. Wakachepuka mtaa mmoja hadi mwingine hadi walipotua mbele ya nyumba moja maridadi. Lightness akaingia kama kwake.
Ilikuwa ni nyumba kubwa ya vyumba vitatu. Dada yake Lightness alikuwa amepangishiwa na ofisi iliyomwajiri. Wakati walipoingia, dada yake Lightness ambaye kwa siku hizo alikuwa likizo, aliwakaribisha kwa uchangamfu na hakuonyesha kumshangaa Kamore wala kumhoji lolote Lightness.
“Laiti,” dada yake alimwita huku akiwa amebeba mkoba.
Lightness hakuitika, alimtazama tu huku akisubiri kuambiwa alichoitiwa.
“Natoka kidogo,” dada yake alisema. “Najua nitawakuta. Sichelewi sana. Nafika hapo Namanga kucheki vitu f'lani madukani.”
“Poa, dada,” Lightness alijibu huku akimtupia Kamore jicho la chati.
“Kuna juisi, keki na biskuti kwenye friji,” dada yake aliongeza. “ Endeleeni kwa wakati wenu. Nadhani ndani ya nusu saa nitakuwa nimerudi.” Mara akamgeukia Kamore na kumwambia, “Mgeni, karibu sana. Jisikie nyumbani.”
Huku Kamore akiyaepusha macho yake kwa aibu, alimjibu, “Asante sana dada.”
Ni kama vile Lightness alikuwa akiomba dada yake aondoke. Alicheka kimoyomoyo huku akimsindikiza kwa macho wakati akitoka. Wakabaki peke yao; Lightness na Kamore!
Hazikupita dakika mbili mara Lightness akaelekea chumbani ambako alitumia muda mfupi na kutoka, safari hii akiwa ameshachojoa zile sare za shule na badala yake akawa amejitanda kanga pekee mwilini. Akarudi palepale sofani na kuketi na Kamore. Akauanzisha tena ule uchokozi wake, kama shuleni, safari hii akiuzidisha maradufu.
Alipogundua kuwa Kamore kazidiwa alimnong'oneza sikioni, “Twende chumbani.”
Kamore alionyesha kusita, akihofia kukutwa na dada yake Lightness na kuwa ni kadhia isiyostahimilika.
“Unaogopa nini? Dada harudi sasa hivi,” Lightness alisisitiza.
Bado Kamore alionyesha kusita na sasa hata kila kiungo chake kilisinyaa, ule msisimko aliokuwanao ulitoweka.
“Twende, basi,” Lightness alimshika mkono.
Kamore alinyanyuka. Wakaingia chumbani. Kilichoendelea huko ndicho kilichomwingiza Kamore katika dunia mpya ya mapenzi. Akaigundua starehe iliyojificha katika mwili wa mwanamke. Akazibuka mtoto wa kiume.
Miezi mitatu baadaye akawa hashikiki. Alifanikiwa, tena kwa urahisi tu, kustarehe na wasichana wengine wanne wa shule hiyo ya Benjamin Mkapa.
Haijulikani kama Kamore alikuwa mpole, mkimya, mwenye dharau, bozi au bakunja. Lakini kwa ujumla hakuwa mzungumzaji wa kuweza kumfanya msichana mwenye msimamo mkali aulegeze msimamo wake kiasi cha kumchojolea nguo kiulaini kama ilivyokuwa.
Mbinu yake kubwa ilikuwa ni vijizawadi vidogovidogo mathalani viazi mbatata kwa mayai au pesa kidogo kama shilingi 1,000 hivi. Lakini, pamoja na kupenda vimwana, hata hivyo hakuwa mzembe katika masomo. Japo kiwango chake kilishuka kidogo, bado hakuathirika kiasi cha kujikuta akiambulia patupu katika kila somo. Mungu alimsaidia, akapata Daraja la Tatu.
Baada ya kuhitimu kidato cha nne, ndipo akaingia katika mkondo mwingine wa maisha. Dunia ikamkaribisha rasmi. Sasa alitambua fika kuwa alipaswa kupata ajira ili aweze kuyamudu maisha. Ikibidi, ajiajiri kufuatia uhaba wa ajira katika nchi hii.
Akaingia mitaani mtoto wa kiume. Leo alikwenda huku, kesho kule, akisaka ajira katika ofisi mbalimbali.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mgaagaa na upwa hali wali mkavu. Pitapita yake katika kampuni hii na ile, shirika hili na lile na kadhalika, haikuwa ya bure. Mungu alimsaidia, kampuni moja inayojihusisha na usafirishaji wa bidhaa ndani na nje ya nchi ikamkubali. Akayaanza maisha mapya akiwa na uhakika wa kujipatia pesa kila mwisho wa mwezi.
Ile tabia yake ya kupenda warembo sasa ilimea na kustawi kwa kiwango kikubwa. Akiwa ni Mweka Hazina wa MP Brother's co. Ltd, maisha yalimnyookea kwa kiasi kikubwa. Mshahara mnono, marupurupu kibao na mbinu ya wizi wa kutumia kalamu zilikuwa ni nyenzo zilizomwinua kimaisha ndani ya miezi mtatu tu.
Sasa huyu alikuwa Kamore mwingine, Kamore ambaye hakuamini kuwa hutokea mwanamume akakataliwa penzi na mwanamke. Iweje mwanamke akukatae? Mwanamke wa Dar anajua kumkataa mwanamume? Labda. Ndiyo, labda huenda utakapomtongoza akakukataa akidai kuwa yeye ni mke wa mtu. Lakini, kuwa mke wa mtu ni kigezo cha kutomvulia nguo mwanamume mwingine? Hilo halikumwingia akilini Kamore.
Ni wanawake wangapi walioolewa, ambao kwa vishawishi hivi na vile kutoka kwa wanaume hujikuta wakizisaliti ndoa zao? Ni wanaume wangapi wenye ndoa, ambao huvutiwa na wanawake wengine na bila ya kujali kuwa wanawake hao wameolewa, huwashawishi kwa hila nyingi hadi wakafanikiwa kupata wakitakacho?
Tangu alipokuwa akisoma sekondari hadi akaanza kazi hapo MP Brother's Co. Ltd tayari alishawaona wanaume na wanawake, hususan waishio jijini Dar es Salaam, siyo waaminifu katika ndoa zao. Alishashuhudia wanandoa wakipigana baada ya kutokea fumanizi. Alishasoma habari katika magazeti mbalimbali juu ya miparaganyiko ya ndoa kufuatia tuhuma za mmoja kutokuwa mwaminifu kwa mwenzie. Isitoshe, yeye mwenyewe alishadiriki kustarehe na wanawake wawili ambao alitambua fika kuwa ni wake za watu.
Awali wakati akiwatongoza, walikuwa wagumu sana. Lakini alipojipapasa mifuko na kumkatia donge zuri mmoja wao, siku ya pili walitumia zaidi ya saa tatu ndani ya gesti fulani, kila mmoja akimdhihirishia mwenzake uwezo wake katika uwanja wa mapenzi kivitendo.
Wa pili naye hakuwa na kauli baada ya kukabidhiwa bahasha ambayo ilihifadhi shilingi 50,000. Huyo, wala hata hakusogeza siku moja mbele; alijikuta akiropoka, “Tukutane kituo cha daladala, Posta ya Zamani, saa kumi na moja jioni nitakapotoka kazini.”
Walipokutana, mwanamke huyo alisema kile kilichomshtua zaidi Kamore: “Kama kuna gesti nzuri mbali na kwako, na mbali na kwangu, tufanye haraka. Mume wangu anarudi saa mbili usiku. Sitaki akute sijarudi.”
Pamoja na kushtushwa na kauli hiyo, hata hivyo hakuogopa. Nusu saa baadaye walikuwa Mwananyamala ndani ya gesti fulani, wakijisikia huru kustarehe jinsi watakavyo, wakivitesa viungo vyao kwa mateso yaliyozikonga nyoyo zao. Makazi ya mwanamume yalikuwa Magomeni Mapipa na mwanamke, Tandika hivyo hawakuwa na hofu yoyote.
Ni rekodi za wanawake hao zilizomfanya aamini kuwa hakuna lisilowezekana mbele ya pesa. Mbele ya pesa mwanamke yeyote atapatikana, hivyo hakuwa na haja ya kuchukua muda mrefu akibembeleza. Fimbo kuu aliyoitegemea ni pesa; alitumia kiwango chochote cha pesa katika kumfukuzia mwanamke amtakaye. Na kwa hali hiyo, ule utaalamu wake wa kujipatia pesa za ziada kwa kutumia kalamu yake sasa aliuzidisha maradufu. Pesa zikazidi kummiminikia huku wanawake, mmoja baada ya mwingine wakianguka kitandani kila alipowahitaji. Sasa mitaani akawa gumzo. Na ndipo alipopachikwa majina mbalimbali na sifa tofauti.
Yeye hakujali kuzungumzwa kwa namna yoyote, hakujali kupachikwa majina ya aina yoyote wala hakujali kupewa sifa za aina yoyote. Alichojali ni kuwapata wanawake wazuri, wanawake wanaojua nini cha kufanya pale wachojoapo nguo faraghani mbele ya wanaume rijali. Majina ya Lubuli, Kiwembe, Kipanga, Chizi, Limbukeni na Mshamba hayakumwathiri kisaikolojia kiasi cha kumfanya asitishe chochote alichodhamiria kukifanya dhidi ya mwanamke yeyote aliyemvutia.
Hatimaye ikaja siku ambayo alihisi kamwona malaika. Ilikuwa ni saa 10 jioni. Ndiyo kwanza alikuwa ameteremka kwenye teksi iliyomtoa ofisini. Katika nyumba hii ambayo iko katika mtaa wa Idrissa , Kamore alikuwa ni mmoja wa wapangaji wake. Ilikuwa ni nyumba iliyokuwa katika mtaa uliopangika vyema hivyo kuwa rahisi kumwona mtu kwa mbali. Mara tu Kamore alipoteremka garini, alisimama kiambazani na kutupa macho mtaani. Akamwona mrembo huyo ambaye alikuwa umbali wa hatua takriban mia moja hivi.
Alikuwa ni mwanamke mrefu kiasi cha futi tano, mweupe huku umbo lake likiwa ni jembamba kuanzia kifuani hadi nyongani na kutanuka mapajani. Alivaa fulana nyeupe na suruali ya bluu ya kitambaa chepesi iliyombana vilivyo maungoni. Kadri alivyozidi kusogea ndivyo pia Kamore alivyozidi kufaharisha macho yake. Akamtazama vizuri usoni na kuyabaini macho mazuri ambayo ni kama vile yalikuwa yakisihi na kushawishi, macho yenye mvuto wa kipekee, macho ambayo ni kama vile yalikuwa yakimwambia Kamore: “Niko tayari hata sasa hivi.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kifua chake kilibeba matiti ya ukubwa wastani, yaliyoshiba, matiti ambayo kwa Kamore kilikuwa ni kivutio kingine ambacho humsisimua. Alihisi mabadiliko ya mapigo ya moyo pale mrembo huyo alipomtupia macho na kuachia tabasamu dhaifu lililofuatiwa na “Za saa hizi?”
Kamore hakumbuki kama aliijibu salamu hiyo. Kwa ujumla ni kama akili yake ilisimama kufanya kazi. Akabaki akimtumbulia macho mrembo huyo hata pale alipompita. Mwanamume akashindwa kustahimili, akageuka na kuendelea kumtazama, macho yakivutwa na robota lile la kiuno chake.
Mrembo alitokomea machoni mwa Kamore, hakutokomea akilini mwa Kamore. Akiwa na dhamira yake ileile ya kuwafuatilia viumbe wote wazuri, hata huyu mrembo aliamua kumvalia njuga. Akawatumia vijana wa vijiweni kupata taarifa zake sahihi. Siku ya tatu akawa amepata mengi kuhusu msichana huyo.
Aliitwa Suzana. Aliishi mtaa wa pili ambako alipanga chumba. Siyo mke wa mtu. Haikufahamika bayana kama alikuwa na hawara au mchumba. Mara kadhaa alionekana peke yake baa akinywa bia.
Kamore aliyajua mengi zaidi ya hayo, na mengi vilevile
0 comments:
Post a Comment