IMEANDIKWA NA : GLOBAL PUBLISHERS
*********************************************************************************
Chombezo : Chuzi Ndo Hilo, Hakuna Kuonja!
Sehemu Ya Kwanza (1)
“Jamani, huyu kijana anaitwa Musa. Namtambulisha kwenu. Yeye ni mpangaji mwenzenu hapa,” alisema mama mwenye nyumba akiwa amesimama sanjari na Musa.
Mbele ya Musa alisimama baba Shua na mke wake, mama Shua.
Binti yao mdogo, Shua alikuwa akichezacheza chini ya miguu ya wazazi wake hao.
Baba na mama Shua walitoka kufunga ndoa kama miezi tisa iliyopita. Wakati wanafunga ndoa, mama Shua alikuwa na mimba ya miezi saba tumboni ya mtoto huyo...
“Yeye bahati mbaya hana mke wala mchumba kwa mujibu wa maelezo yake,” aliongeza mama mwenye nyumba huyo.“Sawa, karibu sana Musa,” baba Shua alimkaribisha kwa furaha ya kuungaunga.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Moyoni alimuona Musa ni kijana kama yeye. Sasa kuishi na kijana vile kwenye nyumba moja na yeye alitoka kufunga ndoa alihisi kama ni kujitafutia majaribu yasiyokuwa na ulazima.
“Lakini mama siku nyingine tuletee mpangaji mwenye mke. Unajua mpangaji singo kama huyo tatizo linakuja kuwa kwenye zamu za usafi, huwezi kusema afanye usafi. Matokeo yake mke wangu ndiyo atakuwa na kibarua kizito cha kufanya usafi,” alisema baba Shua...
“Lakini mume wangu kwenye nyumba nyingine siku hizi, mpangaji kama ni singo anatoa pesa kwa ajili ya kununulia mafagio na vifaa vingine vya kudekia,” alidakia mama Shua.
Yeye aliyatafsiri maneno ya kwenye sauti ya mumewe kama ndiyo ujumbe wake halisi lakini hakujua moyoni alikuwa akiwaza kitu kingine kabisa.
“Yeah! Yeah! Nitakuwa nikitoa kila mwezi elfu ishirini ya mafagio,” alisema Musa...
“Umeme je? Maana umeme hapa ni elfu hamsini kwa mwezi,” alisema mama mwenye nyumba.
“Sawa, nitakuwa nikitoa elfu ishirini na tano,” alikubali Musa...
“Halafu mbali na umeme, maji kila mwezi ni elfu ishirini,” aliongeza baba Shua.
“Hakuna shaka. Nitatoa elfu kumi.”
“Kwa hiyo una maana nje ya kodi, kila mwezi utakuwa ukitoa shilingi elfu hamsini na tano?” mama mwenye nyumba aliuliza kwa sauti ya kutaka jibu la haraka...
“Ndiyo mama, wala hakuna shida.”
Baba Shua aliumia moyoni kutokana na kitendo cha Musa kujifanya ana pesa sana...
“Huyu kijana anajifanya anazo. Kila kitu anatoa. Anataka kuniletea majaribu tu hapa,” alisema moyoni...
“Mh! Kaka anaonekana ana pesa. Yaani mafagio tu elfu ishirini. Ina maana umeme hata angeambiwa laki moja angesema atatoa nusu yake. Hiyo ishirini ya mafagio itakuwa yangu,” alisema moyoni mama Shua.
Musa alihamia hapo usiku wa siku hiyo na kuanza maisha mapya. Yeye alichukua chumba kimoja na sebule, safi kabisa.
***CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Asubuhi akiwa anapiga mswaki, mama Shua alitokea, akamsalimia...
“Za asubuhi shemeji?”
“Salama tu shemeji. Umeamkaje wewe, mista na mtoto?”
“Hatujambo...hivi kazi unafanyia wapi shemeji?”
“Aaa...!” kabla hajamaliza kusema baba Shua akatokea, Musa akatumia hekima, akaacha kusema na kujibalaguza akiwa ndani ya bukta tu, tena tumbo wazi...
“Bwana Musa za asubuhi?” baba Shua alimsalimia.
“Salama kaka, umeamkaje?”
“Salama. Ungekuwa unapigia mswaki ndani bafuni. Hapa nje naona kama itakuwa usumbufu kwako. Mara mtoto wangu Shua atatoka, mara atakuganda na wewe unataka kuwahi kazini.”
“Oo! Oke...oke. Sawa! Nimekupata ndugu yangu.”
Lakini kutoka moyoni, baba Shua hakupenda jamaa apige mswaki uani huku tumbo linaonekana wakati mke wake anafanya usafi. Aliamini anaweza kujaribiwa.
Baba Shua alizama ndani, uani akabaki mama Shua na Musa...
“Mimi nafanya kazi kwenye kampuni moja ya simu za mikononi,” alisema Musa kwa sauti ya kawaida...
“Ala! Sawa,” alikubali mama Shua.
Wiki moja ilikatika tangu Musa ahamie kwenye nyumba hiyo.
Siku moja Musa wakati anatoka kwenda kazini alikutana na mama Shua akitoka bafuni kuoga. Alikuwa ndani ya kanga moja tu, aliyoipitisha kifuani kukatizia kwenye nido. Kuona vile Musa, mwili ulimsisimka.
Hata walipopishana, Musa hakukubali. Aligeuka kumwangalia huku akitingisha kichwa cha kuashiria kuhamasika naye…
“Du! Bonge la mwanamke kumbe. Sijawahi kumwona vizuri kama leo,” alisema moyoni Musa akiondoka zake.
Alipofika nje, alisimama kwanza. Akaendelea kumuwaza mama Shua, akataka kurudi akiamini atamkuta ameshajipamba au kuvaa tayari kwa kuondoka.
Kweli, Musa alirudi ndani. Akajipitishapitisha kwake, mwishowe akatoka. Akakutana tena na mama Shua akiwa ndani ya gauni refu mpaka chini miguuni lakini likiwa limemchora mwili wake wote na kuonekana vizuri.
Waliongozana kutoka nje…
“Kumbe shemeji na wewe unafanya kazi?” Musa alimuuliza mama Shua.
“Ee! Nipo Jiji.”
“Oke. Mzee ameshaondoka?”
“Yeye anaondoka saa tatu.”
Baba Shua alitoka mbio mpaka nje, akamwangalia mkewe, alishapotea machoni. Akampigia simu…
“Upo wapi mama Shua?”
“Nakaribia kituoni baba Shua. Vipi, nirudi?”
“Hapana. Vipi, huyu kijana ameshaondoka?” aliuliza kwa makusudi baba Shua. Lengo lake lilikuwa kujua kama waliongozana.
Baba Shua, ni mwanaume aliyetokea kumpenda sana mkewe. Tangu uchumba wao mpaka ndoa, hajawahi kupunguza mapenzi yake kwake.
Kikubwa ni kwamba, mama Shua ameumbika jamani! Kuanzia kiunoni kwenda miguuni alikatika vizuri. Ungeweza kusema alijengeka kwa mfano wa kinu. Kifua chake, licha ya kuwa na mtoto mmoja, hakikuwahi kuchakaa. Kilikuwa kama cha msichana aliyemaliza masomo ya sekondari mwaka jana.
Macho ya mama Shua, kama alipaka rangi pembeni yake alitaka mwenyewe, kwani yeye kiasili ni mweupe lakini pembeni ya macho ni mweusi hivyo kumfanya aonekane kama amepaka wanja muda wote.
Wanasema wowowo, wengine wana majina yao mbalimbali. Kwa mama Shua wowowo lilikuwepo jamani. Akitembea akiwa amejifunga kanga au akiwa amevaa suruali au sketi achilia mbali gauni. Wowowo lilimpendeza sana na kuvutia wanaume wengi.
Tabasamu lake liliweza kumfanya mwanaume ahisi amekutana na yule malkia aliyewahi kushika nafasi ya kwanza kwa uzuri, Cleopatra wa Misri aliyekuwepo kipindi kirefu nyuma.
Baba Shua aliujua uzuri wa mke wake kwani mara nyingi, kila wanapokuwa pamoja, wanaume wamekuwa wakimwangalia sana na hivyo kujua kwamba, mke wake ananyendewa na wanaume kibao.
“Sijajua kama ameondoka au la!” alisema mama Shua wakati ukweli ni kwamba walikuwa wote. Alijua akisema wapo wote, mume wake asingependa.
Baba Shua alikata simu, mama Shua akamgeukia Musa…
“Mume wangu alitaka kujua kama umeshaondoka nyumbani,” alisema mama Shua…
“Ana shida na mimi?”CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Sijajua,” alijibu mama Shua lakini ukweli aliujua.
Mbele, karibia na kituo cha daladala, mama Shua alimuaga Musa kwamba anapanda daladala hapo…
“Twende nikupe lifti, nipo na gari nimelilaza hapo mbele,” alisema Musa huku macho yake yakitalii kwenye mwili wa mwanamke huyo mrembo…
“Mh! Ngumu sana bwana. Wambeya wakiniona itakuwa ishu.”
“Kwani mtaa huu una wambeya?” aliuliza Musa.
“Utakosa kweli?” aliuliza mama Shua…
“Mh! Hatari!”
Basi, mama Shua akashika njia kufika kituoni, Musa naye akashika njia kwenda alikolaza gari.
Mbele kidogo, mama Shua aligeuka kumwangalia Musa ambaye naye pia aligeuka kumwangalia mama Shua, wakakutana macho. Mama Shua akakimbiza macho yake mbele, Musa yeye aliachia tabasamu pana…
“Da! Noma kweli. Amejua nimegeuka kumwangalia. Lakini hakuna noma, hata yeye amegeuka kuniangalia,” alisema moyoni Musa…
“Mh! Si atajua niligeuka kwa ajili yake,” alisema moyoni mama Shua.
***
Jioni, Musa ndiye aliyetangulia kufika nyumbani. Akafanya utafiti na kubaini kuwa, kwa jirani yake kulikuwa na mtoto Shua na msichana wa kazi tu. Baba Shua na mama Shua walikuwa hawajarudi.
Lakini akiwa chumbani kwake anasikiliza muziki sanjari na kuupumzisha mwili kwa kazi za mchana kutwa, mama Shua aliingia. Yeye Musa aliweza kumwona kupitia dirishani kwake, akamchungulia anavyofika mpaka kuzama ndani…
“Da! Mpangaji mwenzangu yupo vizuri sana. Jamaa ameibua kifaa cha uhakika,” alisema moyoni Musa.
Mama Shua alipobaini kuwa, Musa alisharudi lakini mumewe alikuwa bado alichukua karatasi na kalamu, akaandika namba zake za simu, akamuita msichana wa kazi na kumpa maagizo…
“Dada!
“Abee.”
“Nenda kwa huyo kaka. Mpe hii namba yangu ya simu. Mwambie awasiliane na mimi, kuna utaratibu nataka kumpa kuhusu usafi wa nyumba.”
Msichana wa kazi aliipeleka ile karatasi kwa Musa, akagonga mlango kwa dalili za kunyenyekea…
“Karibu,” aliitikia Musa kule ndani huku akitoka na kufungua.
“Dada amesema nikupe hii karatasi. Ina namba zake za simu.”
“Oke, mwambie asante sana eee…”
“Sawa. Amesema uwasiliane naye akupangie utaratibu wa usafi,” aliongeza msichana wa kazi huku akiondoka zake.
Musa alishtuka kidogo kusikia anatakiwa kuwasiliana na mama Shua ili ampangie utaratibu wa usafi…
“Mh! Mbona kuhusu usafi tulishamalizana? Au kuna lingine?” alijiuliza Musa akirudi ndani.
Alizisevu zile namba kwenye simu yake kwa jina la Mpangaji. Kisha akamtumia meseji akimwambia…
“Nimepata namba, asante sana. Mimi Musa, mpangaji mpya.”
Mama Shua alipoipata namba ya Musa, akaachia tabasamu laini sana na kumjibu…
“Asante. Nilipenda tu kukupa namba yangu kwa ajili ya mawasiliano kama ikibidi.”
“Da!” Musa alishangaa sana. alihisi ameokota dhahabu juu ya mchanga.
“Mawasiliano ni muhimu sana. mimi tena jamani!”
“Teh! Teh!” mama Shua alijibu kwa kicheko…
Basi, Musa na mama Shua waliendelea kuchati weeee! Mpaka giza lilipoanza kuingia ambapo baba Shua alirudi kutoka kazini kwake akiwa amechoka sana…
“Huyu kijana mgeni amerudi?” aliuliza baba Shua huku akikaa hata kabla ya salamu kwa mke wake…
“Nadhani, sijafuatilia,” alisema mama Shua…
“Amesharudi, si saa zile mimi nilikwenda,” alidakia dada wa kazi ambaye alikuwa anapita na shughuli zake…
“We dada,” baba Shua alimuita ili amsikie vizuri kutokana na kauli yake kwamba alisharudi na yeye alikwenda kule…
“Abe.”
“Ulikwenda kufanya nini?” aliuliza baba Shua…”
“Nilikuwa napita kwenda nje nikamwona amerudi,” alijibu msichana wa kazi na kuukimbia ukweli. Alijua akisema ukweli atavuruga maana mhusika mwenyewe aliyemtuma alisema hajarudi na hajafuatilia.
“Oke, sawa.”
***CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Usikuwa wakiwa wamelala, baba Shua alimwamsha mke wake…
“Mama Shua…mama Shua…”
“Abee…abee.”
“Naomba tuongee kidogo.”
“Sawa,” alikubali mama Shua huku akigeuka kulala sawasawa…
“Humu ndani kuna mpangaji kama sisi…”
“Ndiyo…”
“Sasa nataka kusema kuwa, tupo familia mbili tofauti…”
“Ni kweli mume wangu…”
“Sasa msimamo wangu ni huu. Kila familia ibaki kuwa kivyake. Sitapenda kuona mazoea yoyote kati ya familia yangu na yule bwana, nadhani nimesikika.”
“Nimekusikia mume wangu. Lakini ina maana hata salamu nisimpe?”
“Salamu mpe. Sitaki mazoea yale ya ndani kabisa, sipendi hata kusikia.”
“Nimekuelewa mume wangu.”
“Ndiyo hivyo basi.”
***
Asubuhi kulikucha, Shua alitoka uani akiwa hajavaa nguo. Musa alikuwa uani wakati huo na mama Shua alikuwa akitoka chumbani kwenda uani…
“He! We Shua kwa nini unatembea bila nguo?” mama yake alimjia juu japo Shua hakuwa mtoto mwenye kujitambua…
“Ha! Mchumba unanidhalilisha bwana, hujavaa nguo?! Basi sitakuoa,” alisema Musa akimtania mtoto huyo ambaye hajui lolote…
“Unaona sasa, unakosa mchumba hivihivi mwanangu?”
Musa alikwenda kuoga, akarudi kujiandaa. Mama Shua naye alijiandaa. Kwenye kutoka, baba Shua alisimama nje. Kwa hiyo Musa alipotoka alikuwa kasi kuashiria anawahi. Mama Shua alipotoka yeye, mumewe alimsemesha maneno mengi yaliyomfanya apitishe dakika tano nzima.
Alifanya hivyo ili kumpa Musa nafasi ya kufika mbali ili mama Shua akitoka wasiongozane.
Mama Shua alipotoka, alikimbia, baba Shua akamuuliza…
“Mbona unakimbia? Unamuwahi nani?”
“Jamani baba Shua kwani we’ huoni kwamba nimechelewa mume wangu?”
“Sasa ndiyo ukimbie? Si utembee kwa haraka tu. Unakimbia kama vile kuna mtu anakusubiri?”
“Mh! Baba Shua bwana. Mbona umekuwa hivyo mume wangu?” alihoji mama Shua huku akiangalia simu yake…
“Unachati na nani na we unasema umechelewa kazini?”
“Baba Shua, sichati na mtu. Nimeangalia tu simu.’’
Mbele ya safari akiwa ameshapotea machoni mwa mume wake, mama Shua alimtumia meseji Musa…
“Umeshatimua?”
“Niko barabarani tayari. Vipi? Kwema?”
“Kwema. Ah! Mista alinipotezea dakika kidogo, ndiyo nafika kituoni.”
“Pole sana. Baadaye basi nitachati na wewe.”
“Sawa, usijali.”
***
Musa alipofika kazini alimsimulia mfanyakazi mwenzake, aitwaye Miayo kuhusu mama Shua na akaomba ushauri…
“Musa, huyo mwanamke anakutaka. Hilo liko wazi kabisa. Lakini sasa mwepuke. Unajua mke wa mtu ni sumu inayoua mara moja?”
“Ndiyo, lakini sasa Miayo, si anajileta mwenyewe?”
“Musa….ulitaka ushauri au ulitaka nikuunge mkono?”
“Nilitaka ushauri.”
“Ndiyo huo nimekupa. Utajaza mwenyewe.”
Waliachana na kila mmoja akaendelea na kazi. Kichwani, Musa aliazimia kutembea na mama Shua. Kwanza alimwona ni saizi yake licha ya kwamba yeye alishapata mtoto mmoja huyo Shua…
“Nikishinda mara moja tu si mbaya. Lakini lazima nicheze naye mechi. Mtu anajikomba mwenyewe, mi kosa langu nini sasa?” alijiuliza, akajipa ujasiri.
Akiwa kwenye kuwaza hayo, mara meseji ikaingia, Musa akaifungua haraka sana…
“Vipi, umekula?” ilitoka kwa mama Shua…
“Haya sasa! mambo kama haya ya kuulizana kama nimekula halafu nimwache? Aaa! Wapi! Hata shetani atanicheka,” alisema moyoni Musa.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ndiyo nataka nitoke nikale, karibu sana,” alijibu Musa... “Kale bwana! Mwili haujengwi kwa simenti wala matofali, unajengwa kwa misosi mbalimbali. Mimi ndiyo natoka kula naingia job sasa.” “Poapoa.” Moyoni mama Shua alijua wazi kwamba, anatengeneza msala kati yake na mumewe. Alijua mumewe akibaini ukaribu wake na mpangaji huyo patachimbika. Tangu afunge ndoa na mumewe huyo haijawahi kutokea wakatibuana kuhusu mapenzi au uaminifu. “Mh! Yaani baba Shua akijua tu, imekula kwangu. Mbona atanitoa roho!” alisema moyoni mama Shua huku akijipanga kwamba, kuanzia siku hiyo aanze kuidhibiti simu yake kwa kiwango cha kimataifa ili mumewe asije akaidaka na kukutana na uozo wake na Musa. *** Ilikuwa saa tisa na nusu, mama Shua alimtumia meseji Musa... “Mimi natoka job now . Wewe je?” “Hata mimi mama. Ndiyo niko nje hapa.” “Kituo wapi?” aliuliza mama Shua... “Mh! Nataka nipite Morocco nikapige kituo pale Makumbusho.” “Nije nikujoini?” “Mh! Utaweza?” “Naweza, kwa nini nisiweze? Kwani kuna kikwazo gani?” “Njoo.” “Poa.” Musa aliendesha gari huku mawazo yake yote yakiwa kwa mwanamke huyo. Na yeye alianza kuweka akili sawa kwamba, wanakokwenda lazima hakutakuwa na mwisho mzuri... “Lakini yule ni mke wa mtu. Hivi tunaweza kuwa kwenye uhusiano kwa muda gani bila mume wake kujua?” alijiuliza Musa huku mikono ikiwa kwenye usukani. Alifika Makumbusho, akatafuta baa nzuri na kukaa hapo. Alimtumia meseji mama Shua ya kumwelekeza... “Poapoa. Na mimi ndo’ nashuka hapa kituoni,” alijibu mama Shua. Kwa uelewa wake, mama Shua alikwenda moja kwa moja hadi kwenye baa hiyo na kuungana na Musa. Kabla hajakaa, alivuta kiti, akamsogelea Musa, akampiga busu... “Mmwaaa...” Musa alishtuka kidogo, akataka kukwepa lakini aliogopa kumtia aibu mgeni wake huyo. Kikubwa alichokiwaza yeye ni kwamba, mbona hakuna mawasiliano ya kimapenzi? Sasa mabusu yanatokea wapi tena! “Mmmm...asante sana,” alisema Musa huku akitegesha shavu waziwazi ili apigwe busu hilo. Mama Shua alikaa. Akamwangalia Musa kwa macho ya kulegea kama vile ndiyo yupo eneo la tukio. “Vipi, pole na kazi,” alisema mama Shua... “Nimepoa, pole na wewe.” “Hata mimi nimepoa.” *** Kule nyumbani, baba Shua aliwahi kurudi na kushangaa siku hiyo, mkewe amechelewa na wala hajatoa taarifa yoyote. Alishika simu na kumwendea hewani... “Haloo,” alipokea mama Shua baada ya kumtahadharisha Musa kukaa kimya, mumewe anapiga... “Huko wapi, mbona umechelewa?” “Niko kwenye daladala baba Shua.” “Uko kwenye daladala! Mbona nasikia muziki? Siyo baa hapo?” “Hapana, sema tu daladala linapita nje ya baa moja hapa.” “Wapi?” “Eee...eee...Makumbusho.” “Yaani upo mahali hupajui sawasawa mpaka unajifikiria?” “Jamani baba Shua, mbona hivyo?” Baba Shua alikata simu. Mama Shua alikaa sawasawa, akamwangalia Musa kama anayesema... “Mbona hunitongozi?” “Vipi, mista nini?” “Ah! Ana mchecheto kama nini!” “Wahi basi, mimi bado nipo.” “Kweli, ngoja nipande basi hapa.” Musa alimkatalia kupanda basi, akampa pesa achukue Bajaj ili awahi... “Ooh! Jamani! Asante! Sasa itakuaje?” “Si tutawasiliana.” “Ukija home nishtue basi.” “Ili tuchati?” “Eee.” “Wee! Unataka kupigwa wewe.” “Hakuna. Ila we ukifika nishtue tu.” “Poa.” *** Baada ya kufika nyumbani, mama Shua alimpandishia mume wake... “Yaani wewe unataka hata kama nachelewa dakika kumi nikwambie? Mbona una wivu wa kijinga sana wewe baba Shua?” Baba Shua hakuwahi kusikia maneno kama hayo kutoka kwa mkewe, alikazia macho simu yake... “Mama Shua...” “Nini?” “Leo unanijibu hivyo mimi?” “Ah! Umenikera sana baba Shua ndiyo maana.” “Ndiyo unijibu hivyo mama Shua?” “Nisamehe kama umekereka baba Shua.” “Unajua umechelewa kwa muda gani?” “Nusu saa tu.” Baba Shua aliinyakua simu ya mkewe na kukimbia nayo mpaka chumbani...
Mama Shua alitoka mbio kumfuata nyuma yake huku akimsema vibaya kwa kitendo chake hicho...
“We baba Shua ndiyo nini hivyo? Baba Shua bwana, nipe simu yangu.”
“Aha! Kumbe hii simu ina mambo yako ndani siyo?” aliuliza baba Shua kwa sauti iliyojaa hasira...
“Wala hakuna kitu kama hicho.”
“Sasa kwa nini unaing’ang’ania kama haina mambo mabaya?”
“Si yangu lakini! Kwani mimi nimeitaka simu yako?”
“Shika yangu hiyo. Kaa nayo na mimi nakaa na yako.”
Mama Shua alikumbuka kuwa, kila meseji aliyoipokea kutoka kwa Musa aliifuta na hata zile alizokuwa akituma yeye pia alizifuta. Kwa hiyo akawa hana wasiwasi kwa hilo, bali wasiwasi wake ni kuhusu Musa kama atatuma meseji wakati simu anayo mume wake...
“Haya kaa nayo...kaa nayo...” alisema mama Shua huku yeye akiisusa simu ya mume wake.
Baba Shua alikaa kitandani na kuanza kusoma meseji mbalimbali za mkewe, alizotumiwa na alizotuma. Hakuona ya mapenzi. Akaanza kusachi majina yaliyoseviwa, akatafu ta jina la Musa, kumbe mkewe alimsevu Musa kwa jina la Karibu Mgeni. Akimaanisha Musa alihamia pale muda si mrefu.
Wakati baba Shua amekazana kusaka herufi M, K ya karibu aliipa kisogo na hivyo kumnusuru mkewe katika mtego mbaya wa usaliti.Mama Shua akawa hachezi mbali na mumewe. Alikuwa akijifanya kupanga nguo kwenye kabati huku muda mwingi alimkazia macho mumewe ili aone kama atabadilika uso ajue tayari amekumbana na meseji ya Musa.
***
Musa alipomaliza bia zake nne kwenye baa hiyo aliondoka. Safari yake ilikuwa ni kurudi nyumbani. Aliwaza kumtumia meseji mama Shua lakini moyo ukasita, akakumbuka mazungumzo yake na mwanamke huyo wakiwa wanaagana pale baa...
“Basi ukifika nyumbani nishtue.”
“Ngoja nikifika ndiyo nitamshtua,” alisema moyoni Musa akiwa tayari barabarani.
Ile anaingia tu, anakutana na mama Shua. Mama Shua akamsogelea kwenye sikio na kumwambia...
“Usitume meseji mpaka nianze mimi.”
Musa alikubali kwa kutingisha kichwa tu huku akimtumbulia macho mwanamke huyo.
Mama Shua alirudi tena chumbani. Mumewe akampa simu yake...
“Huna namba ya huyu kijana mgeni?”
“Sina.”
“Haya.”
***
Saa moja jioni, baba Shua alipata wageni wawili anaofanya nao kazi. Kwa hiyo mama Shua akapata nafasi ya kukaa chumbani akiwa na shughuli zake na akatumia nafasi hiyo sasa kuwasiliana na Musa...
“Mambo? Sikuwa na simu mimi ndiyo maana muda ule nikakwambia usitume meseji mpaka nianze mimi. Niambie.”
Musa aliisoma meseji ile na kumjibu kwa kifupi sana...
“Miss u.”CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Miss u 2. Umelala?”
“Hapana,” Musa akamjibu.
“Unafanya nini?” Mama Shua akamtumia meseji ya kumwuliza.
“Nipo baa ya nyuma huku nimekuja kula mishikaki mara moja.”
“Mh! Jamani! Umenitajia mishikaki, mate kinywani yamenijaa.”
“Nikuletee?”
“Utaweza kweli?”
“Nitaweza. Si nikifika naiweka sehemu nje halafu nakujulisha!”
“Sawa, niletee hata miwili.”
“Mitamu sana. Miwili haitoshi, nakuletea mitano.”
“Du! Haya, sawa. Asante sana.”
Musa aliagizia mishikaki sita. Akafungiwa kwenye mfuko wa rambo.
Lakini mama Shua akakumbuka kwamba, akiletewa hiyo mishikaki atailia wapi? Maana mume wake akiona atamuuliza alikoitoa kwa usiku ule. Lakini pia kumkataza Musa asinunue aliona atatoa picha mbaya, akaacha. Liwalo na liwe.
Musa alipofika nje, akauweka mfuko wa rambo juu ya meza ya plastiki iliyochoka, kwenye kona kabisa ya nyumba, akamtumia meseji mama Shua...
“Mzigo wako upo kwenye meza ya plastiki nje kwenye kona.”
Mama Shua alitoka haraka, akaenda nje kwenye meza na kuchukua mfuko kisha akasimama kulekule nje na kutumbukiza mkono mfukoni na kuchukua kipande kimojakimoja cha mshikaki na kukipeleka mdomoni. Mpaka akamaliza mishikaki yote sita.
Alirudi ndani akiwa anajifuta mkono huku akisahau kwamba, mishikaki inanukia...
“Mh! Nasikia harufu kama ya mishikaki,” alisema mgeni mmoja wa baba Shua wakati mama Shua akipita. Wote wakasema kweli.
***
Asubuhi kulikucha, Shua na mama yake walikuwa uani. Musa alipotoka kwenda kuoga akaanza kumtania Shua...
“Mchumbaaa...umeamkaje wewe mchumba?”
Shua aliachia tabasamu tu akiwa hana la kujibu...
“Mwambie nimeamka poa, sina hela ya nyama leo.”
“Sawa mchumba...nikupe shilingi ngapi ya nyama?”
“Mwambie elfu kumi.”
“E...fu ku...mi,” alisema kwa tabu Shua huku akiuma vidole. “Basi mchumba usiwe na wasiwasi , nikiwa natoka kwenda kazini nitakuachia.” “Mwambie ukaniachie pale dukani kwa Mangi,” alisema mama mtu... “Aachie kwa...Mangi,” alisema Shua kwa kufuata maelekezo ya mama yake.
¤¤¤¤
Musa aliingia kuoga. Baada ya dakika sita tu, akatoka. Alirudi chumbani kujiandaa, akatoka zake. Nje alimkuta baba Shua. Akamsalimia kwa furaha... “Mkubwa umeamkaje?” “Salama kaka, umeamkaje na wewe ?” “Niko fiti. Kumekucha.” Mara, mama Shua alitoka akiwa ameshajipigilia tayari kwa kutoka kwenda kazini... “Za asubuhi?” Musa alimsalimia mama Shua kama vile hawajuanagi... “Salama tu, umeamkaje anko?” “Ah! Kumekucha, nimeamka salama.” Musa aliondoka kwa kasi, nyuma baba Shua akaanza... “Kwani yule kijana ni anko wako?” “Kwa nini?” “Nimesikia umemsalimia ukisema ‘umeamkaje anko.’” “Ah! Baba Shua jamani. Basi nisamehe mimi...halafu nimechelewa, naondoka.” “Ngoja kwanza. Umechelewa kivipi? Unamuwahi nani? Mbona jana ulichelewa zaidi ya leo!” “Jamani baba Shua, kwani unataka kuniambia nini?” “Nakushangaa ukisema kwamba unaondoka. Au kuna mtu unamuwahi mahali?” “He! Mtu gani sasa jamani?” “Unamjua wewe .” “Wala hakuna mtu ninayemuwahi . Niamini baba Shua jamani.” Mama Shua aliondoka. Ilibidi atembee kwa mwendo wa polepole ili mumewe asimwelewe vibaya . Akiwa anapita duka la jirani, akaitwa... “Mama Shua.” Aligeuka... “Kuna pesa nimeambiwa nikupe wewe ,” alisema muuza duka... “Na nani?” aliuliza mama Shua... “Kaka mmoja simfahamu.” “Shilingi ngapi?” “Elfu kumi.” “Ooo! Nimeshamjua. Asante sana,” alishukuru mama Shua. Hakuamini kama mazungumzo ya Musa na binti yake, Shua yalikuwa siriasi kiasi cha kuacha pesa dukani kweli. Yeye alijua wapo kwenye utani tu. Mbele, mama Shua alimpigia simu Musa... “Haloo...” “Nashukuru sana wangu. Kumbe ulifanya kweli? Mi nilijua unataniana na binti yangu tu...teh! Teh! Teh!” alisema na kucheka mama Shua... “Usijali my love, tupo pamoja.” “Poa, kazi njema.” “Poapoa.”
*****
.
Kama ilivyokuwa jana yake, mchana wa saa saba, mama Shua alimtumia meseji Musa... “Wangu umekula?” Muda aliijibu haraka sana meseji hiyo... “Yap! Wewe?” “Mimi ndiyo nakula sasa, njoo ule.” “Sina hela.” “Mimi ninayo.” “Teh! Teh! Endelea tu bhana, baadaye.”
. ***CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
.
Kwa kawaida, mama Shua hutoka kazini saa tisa na nusu. Siku hiyo ilipofika saa nane akamtumia meseji Musa... “Nimeboreka na kazi leo, natamani kwenda kupumzika mahali mpaka muda wa kazi ukiisha ndiyo nirudi nyumbani.” “He! Pole sana. Sasa ukapumzikie wapi, baharini?” “Hapana...” “Baa?” “Hapana, sitaki baa.” “Porini?” “Teh! Bhana mi sitaki utani wako. Porini kwani mi swala?” “Wapi sasa? Labda ukapumzikie gesti!” “Hayo maneno.” “Kwa hiyo unakwenda kupumzika gesti?” “Natamani iwe hivyo .” “Du! Hongera, mpaka nakutamani.” “Unanitamani nini sasa?” “Unavyopumzika na mimi ningekuwepo.” “Njoo.” “Kweli?” “Kha! Mbona hujiamini wewe !” “Oke utaniambia wapi upo!” “Poa.” Muda huohuo mama Shua alikusanya vilivyo vyake na kubeba mkoba wake begani, akaaga kwamba anajisikia vibaya , hivyo anakwenda kupumzika. Aliingia katikati ya jiji na kusaka hoteli, akaipata. Alipolipia na kuoneshwa chumba, akamtumia meseji Musa... “Oya! Nipo Greenland Hotel. Rum namba 17.” “Naifahamu, nakuja mama. Da! Mwili mzima umesisima.” “Mwili umesisimka kisa nini?” “Si nakuja kupumzika na wewe . Najua nitapata joto lako, utanibusu midomo, utanivua shati...da!” Mama Shua alipokuwa akiisoma meseji hiyo, naye mwili ulimsisimka... “Da! Bwana Musa, njoo.”
*****
.
.
Baba Shua akiwa kazini kwake , alipokea barua iliyomtaka asafiri kwenda Arusha kikazi kwa siku saba... “Da! Jamani hakuna mtu mwingine anayeweza badala yangu?” alimuuliza bosi wake mmoja... “Hakuna. Kajiandae, kesho asubuhi unaondoka.”.
Kwa baba Shua, ni mara ya kwanza kuonesha kwamba hapendi kusafiri kikazi. Mara zote, amekuwa akifurahia safari hizo kutokana na kulipwa posho ya safari ambayo humsaidia.
Alibaki akijifikiria kiasi cha dakika tatu nzima na mabosi wake walionesha hawana habari naye tena.
Aliondoka akiwa mnyonge. Mawazo makubwa kwake ilikuwa ni jinsi gani atasafiri na kumwacha mkewe, mama Shua kwenye nyumba ile ambako kuna mpangaji mpya, kijana na mtanashati…
“Hivi kweli yule kijana hawezi kuniingilia kwa mke wangu?” alijiuliza baba Shua.
Aliwaza na kuwaza, ikafika mahali akakubali kwamba lazima asafiri kwani kazi ndiyo inamuweka mjini lakini huku moyoni akipanga kwamba, mkewe huyo atakwenda kumwacha kwa kaka yake…
“Mama Shua na Shua watakwenda kukaa kwa bro mpaka nirudi. Hii balaa,” aliwaza mwenyewe.
Alimtumia meseji mke wake…
“Mama Shua mimi kesho asubuhi nina safari ya kikazi, nakwenda Arusha kwa siku saba.”
“Mh,” aliguna mama Shua. Moyoni alifurahia sana, akasema…
“Kwa siku saba! Du! Nitafaidi sana na Musa.”
Palepale, badala ya kumtumia meseji mumewe kumjibu, alimtumia meseji Musa…
“Wangu, kuna uhuru f’lani unakuja mkubwa sana.”
Musa aliisoma meseji hiyo lakini hakuuelewa huo uhuru, akauliza…
“Upi huo wangu?” “Mista ana safari ya Arusha, atakaa kwa siku saba.”
“Du! Kweli huo ni zaidi ya uhuru,” alijibu Musa.
Baba Shua alishangaa kuona mkewe anachelewa kujibu meseji yake wakati si kawaida yake. Akampigia…
“Haloo,” alipokea mama Shua…
“Wewe vipi, umepata meseji yangu?”
“Nimepata mume wangu, nilikuwa bize kidogo, samahani,” alijibu mama Shua…
“Oke, basi endelea,” alisema baba Musa na kukata simu.
Mama Shua aliendelea kuchati na Musa…
“Kwa hiyo wangu angalia ni jinsi gani tutakuwa huru. Labda wewe ubanwe.”
“Mimi nibanwe na nani wakati nipo singo. Labda wewe…”
“Hata mimi nitabanwa na nani kama mume wangu hayupo. Labda wewe.”
Baada ya kuchati sana na Musa, mama Shua ndiyo akamgeukia mumewe…
“He! Siku zote hizo jamani! Si afadhali zingekuwa siku mbili au tatu tu! Loo!”
“Ndiyo hivyo, ndiyo kazi. Nitafanyaje sasa? Lakini itabidi we ukakae kwa bro, Buguruni,” meseji ya baba Shua ilisema hivyo. Mama Shua alishtuka kusoma meseji hiyo, akakosa raha. Akaiangalia simu yake kwa muda kama haamini kuwa ndiyo iliyoleta meseji ile.
Alichoka kabisa, hakumtumia meseji mume wake ya kumwambia sawa, wala hakumtumia meseji Musa ya mwendelezo wa kuchati kwao.
***CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Muda wa kutoka kazini ulipofika, mama Shua aliondoka kimyakimya. Hakumjulisha Musa wala mume wake. Alifika nyumbani akiwa mpole. Furaha yake ilipotea…
“Kwanza baba Shua ye hakumbuki tu. Mke wa kaka yake hatupatani kama nini…sasa anaposema akaniache kule kwa siku saba anatafuta nini kwa yule mwanamke?”
Baba Shua aliporejea alimkuta mkewe amesharudi, akafurahi sana…
“Kumbe umesharudi mke wangu? Pole na kazi.”
“Nimepoa, lakini kichwa kama kinagonga kwa mbali.”
“Umekunywa dawa?”
“Bado, ila kikiendelea hivihivi nitakunywa.”
***
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment