Search This Blog

Monday, October 24, 2022

TOROJO BAMIA ( WINGA TELEZA ) - 5

 





    Chombezo : Torojo Bamia (Winga teleza)

    Sehemu Ya Tano (5)



    “Jamani mpenzi waambie wenzako muifanye kesho. “

    “Bebi kazi hiyo ndiyo inatupa jeuri ya mimi na wewe kufanya yote haya.”

    “Basi nipe hata chozi la mnyonge, hali ni mbaya,” Lily alilalamika alikuwa kama kachambia pilipili.

    “Bebi nachelewa wananisubiri,” MJ alisema huku akivaa haraka na kwenda kumbusu Lily aliyekuwa kwenye hali mbaya.

    ***

    MJ alionekana baada ya wiki na kusingizia alikuwa amesafiri nje ya nchi kutokana na simu yake kutopatikana hewani. Lily aliamini kabisa MJ alikuwa nje ya nchi.

    Tabia za MJ kila kukicha zilikuwa zikimtesa Lily, hata haki ya kitandani hakuipata kama zamani, ilionesha huanza kutumika kwa wanawake wengine ndipo huenda kwake.

    Mara nyingi amekuwa akiachwa njiani na MJ ambaye huonekana amechoka hata akijitahidi kumuamsha mnara ilishindwa kusoma network ulikuwa chini.

    Siku zote Lily alimvumilia MJ kwa vile alikuwa akimpa kila alichotaka. Lakini karaha za mapenzi zilikuwa kubwa sana zisizo vumilika. Siku mmoja wakiwa katika maandalizi kuupanda mnazi wa raha, simu ya MJ iliita. Kama kawaida aliomba radhi na kunyanyuka kitandani akimwacha Lily na hamu zake.

    MJ alikuwa ameitwa na demu wake mwingine ambaye naye alikuwa nazo.

    “Jamani mpenzi mateso gani haya?”

    “Bebi nakuja leo narudi.”

    “Lakini kumbuka unanitesa, zimepanda wewe unaondoka, huna hata huruma jamani,” Lily alilalamika mpaka machozi yalimtoka.

    “Narudi mpenzi sichukui hata dakika tano.”

    “Mmh! Mimi nitafanyaje,” Lily alikubali shingo upande.

    MJ alivaa pensi tishat na sandoz na kutoka kuelekea alipoitwa. Alipotoka Lily hakukubali alipitia gauni la kulalia bila kuongeza kitu ndani. Kuvaa viatu au ndala aliona anachelewa, alimfuatilia kwa nyuma. Kuchukua gari lake aliona mpango wake atavurugika alitoka hadi nje na kukodi teksi na kumfuatilia MJ ili ajue anakwenda wapi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya mwendo mrefu kidogo alimuona MJ akipaki gari pembeni ya gari lingine. Baada ya muda alimuona msichana aliyekuwa amevaa nusu uchi akitelemka kwenye gari iliyokuwa imesimama na kuingia kwenye gari la MJ.

    Alitulia kuangalia baada ya kuingia yule msichana MJ ataelekea wapi. Alipanga kama anakwenda hotelini basi fujo atakazomfanyia lazima uhusiano wake na Mj ufe siku ile, kwani alikuwa amechoka kugeuzwa futio la miguu.

    Alitulia zaidi ya robo saa kusubiri gari la MJ liondoke, lakini alishangaa kuona muda unakatika bila gari kuondoka wala mtu kutoka. Alijiuliza anafanya nini muda wote wasiwasi wake ilikuwa labda anafanya biashara zake.

    Kilichomshtua zaidi ni mavazi ya yule msichana alivyovaa ya nusu uchi. Wazo la kufanya mapenzi kwenye gari hakuwa nalo. Alimweleza dereva waendelee kusubiri mpaka waone mwisho wake. Baada ya nusu saa alimuona yule msichana akishuka nguo yake ikiwa imepanda upande mmoja na kalio moja kuwa nje. Kingine kilichomshtua alikuwa ameshikilia kufuli mkononi kuonesha kwenye gari kuna kitu kilikuwa kikiendelea.

    Kabla hajafika kwenye gari lake MJ alimwita aligeuka wakati huo MJ alikuwa ametelemka na kumfuata yule msichana.

    Alimsogelea na kumla denda na kuanza kupapasana huku MJ akizinyanyua nguo za yule msichana na kumfanya abakie makalio nje na kuonyesha hakuwa na kitu kingine zaidi ya kufuli alilolishika mkononi.

    Lily roho ilimuuma sana, alishangaa kuwaona wakiingia kwenye gari la yule mwanamke na kupoteza tena zaidi ya dakika ishirini, Lily akiwa anashuhudia.

    Wazo la kwenda kufumania alikuwa nalo lakini wasiwasi wake uwezo wa yule mwanamke. Pia ilionesha ni mwanamke wake wa muda mrefu hivyo asingefanya lolote. Alijikuta akimkumbuka Shuku na kujuta kujiingiza kwa MJ mwanaume mwenye tamaa ya wanawake.

    Baada ya muda MJ alitelemka kwenye gari akiwa amesahau kufunga zipu. Aliishika suruali kwa mkono na kuingia ndani ya gari lake. Baada ya muda magari yote yaliondoka kwa kila moja kufuata njia yake.

    Lily roho ilimuuma na kulia peke yake kilio cha kwikwi. Dereva wa teksi alishtuka kumuona akilia huku akiwa hajui nini kilichokuwa kikiendelea. Muda wote alikuwa akishangaa matukio aliyoyaona hata vazi la Lily lilimshangaza kuvaa gauni la kulalia bila kitu ndani tena bila hata viatu.

    “Dada vipi?”

    “Inatosha leo atanitambua,” Lily alisema kwa hasira.

    “Yule ni shemeji?”

    “Siyo muhimu kujua naomba unirudishe nyumbani.”

    Dereva hakumjibu kitu aligeuza gari na kumrudisha alipomtoa. Walipofika Lily aligundua hakuwa na fedha alitoka yeye kama yeye bila kuchukua hata senti tano.

    Alimuomba dereva akachukue fedha ndani huku akimweka dereva katika wakati mgumu kutokana na nguo aliyokuwa amevaa dodo zilizo jaa na kusimama vyema kifuani na makalio yaliyokuwa wakipishana wakati wa kutembea kama abiria wa Mbagala wakigombea kuingia ndani ya daladala zilimuweka kwenye wakati mgumu dereva wa teksi.

    Baada ya kumpa chake alirudi ndani kuendelea msiba wake. Baada muda akiwa amejilaza kitandani akilia, MJ alirudi na kwenda moja kwa moja kwa Lily akiwa ameisha vua nguo na kujilaza pembeni yake.

    “Bebi nini tena? Usilie nimerudi.”

    Lily alitamani kumfukuza lakini alishindwa kwani hali yake kwa siku ile ilikuwa mbaya shetani mpenda shari alikuwa amepanda alitakiwa kushushwa. Alipanga baada kuzishusha ampe ukweli na kisha kila mtu ashike hamsini zake.

    “Mpenzi mbona unanitesa hivi?” Lily alilalamika.

    “Jamani si nimerudi.”



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Basi nipe raha zangu,” Lily alilalamika kama mtoto wa paka mwenye njaa aliyemuona mama yake. Kwa kinyaa alichokiona kama si kuzidiwa na mahanjamu asingekubali kuutoa mwili wake kwa MJ, kwa vile alijua anakula makombo japo harua haina makombo.

    Kutokana na kuzidiwa na kiu ya dafu, Lily aliuvamia mnazi wa MJ ulikuwa umeinama na kuuupa mshikemshike, haukuchukuwa kunyanyuka. Aliurukia mnazi kama nyani mzoefu, hakusubiri usimame vizuri aliuparamia hivyohivyo.

    MJ naye hakuwa mbali alianza kumsindikiza taratibu Lily aliyekuwa akitatalika kama bisi kwenye kikaango cha moto. Kutokana na kushikika hakutaka kutoa pasi baada ya kuuchukua mpira toka upande wa goli lake na kukimbia nao huku akiwapita mabeki waliokuwa wanamsindikiza.

    Lily aliingia ndani ya kumi na nane na kutazamana na golikipa. Wakati anakiandaa kupiga bao ghafla chombo cha MJ kilizimika ghafla na kumfanya Lily apige kelele za kukatishwa raha zake zilizokaribia kuwa utamu.

    “Jamaniii, MJ ndo nini?”Lily alilalamika kama mtoto aliyenyang’anywa pipi.

    Kwa haraka aliruka toka juu ya mnazi na kujitahidi kuunyanyua chuma kikiwa bado moto. Lakini ilikuwa kazi ngumu kila alivyojitahidi ilikuwa kazi bure. Alijikuta akitumia zaidi ya nusu saa kutaka kuunyanyua mnazi kwa kila mtindo anaoujua huku jasho likimtoka, kwa kupapasa kunyonya kuugusisha hasi na chanya lakini wapiii! Mtalimbo uliendelea kulala dolo.

    “MJ unanifanyia nini lakini? Kama hunitaki si ungeniambia kuliko kunipaka upupu ushindwe kunikuna ni mateso gani haya jamani,” mtoto wa kike alilia madafu.

    “Siyo sikutaki bali hali ndiyo ilivyokuwa hata mimi sikutegemea,” MJ alijitetea.

    “MJ umetumika?”

    “Sijatumika mpenzi wangu ni uchovu tu.”

    “Muongo umetumika!”

    “Sijatumika mpenzi.”

    “MJ mbona unanitoa thamani hivyo? Yaani utumike kwa wanawake zako kwanza ndipo uje unipake makombo?” Lily alizidi kulalamika kwa uchungu huku hamu zake zikiwa juu.

    “Hakuna mpenzi ni uchovu kazi zetu nazo zinatuchosha sana,” MJ alijaribu kujitetea.

    “MJ usiniudhi, biashara gani ya kufanya ngono na wanawake kwenye gari?”

    “Sasa nani kafanya mapenzi kwenye gari?” MJ alijifanya hajui kitu.

    “MJ mi si mtoto mdogo, ninachokisema kikuhadithiwa bali nimekishuhudia mwenyewe kwa macho yangu.”

    “Lily umeshuhudia wapi?”

    “Kwani leo ulienda wapi?”

    “Kwenye biashara zangu.”

    “Na yule mwana mke uliyefanya naye ngono kwenye gari lako kisha mkahamia kwenye gari lake?”

    “Mwanamke! Mwanamke gani?” MJ alijifanya kushangaa.

    “Unaniuliza mimi wakati wa kufanya uchafu wenu tulikuwa pamoja?”

    “Wee nani kakwambia uongo huo?”

    “Usingekuwa uongo kama ungekidhi haja zangu, jamani kumbe kila siku naachwa njia panda kumbe kuna watu wanaokutumia kisha unamalizia kunisha makombo.

    “MJ kama ulijua bado una hamu na wanawake zako kwa nini umenitoa kwa Shuku?”

    “Lily mbona umefika mbali.”

    “Siyo mbali, MJ sikutegemea mwanaume mchafu kiasi hiki, yaani unatoka kwa wanawake zako ndiyo unakuja kwangu, mimi Lily? Hata siku moja haitatokea tena.

    “Sikiliza MJ, sijafikia hatua ya kuteswa kiasi hiki, jamani kila siku nakuwa kama nichambia pilipili na kuniacha njia panda maji moto na vidole ndivyo vimekuwa wapenzi wangu kuna faida gani kuwa na mwanaume kama wewe?” Lily alisema kwa sauti ya kilio huku akimwaga chozi.

    “Lakini Lily unakosa nini kwangu?”

    “MJ kumbe unaninyanyapaa kwa ajili ya kuwa napata kila kitu? Basi unajidanganya sana. Kuanzia leo huu mwili utaona kama kituo cha polisi kwa muuza bangi.”

    “Kama umeamua poa.”

    “Nilijua lazima utasema vile kwa vile una shehena ya wanawake.”

    “We si umeamua poa.”

    “Na si kuugusa mwili huu naomba kila mmoja ashike ustaarabu wake.”

    “Hata hiyo haina noma.”

    “Poa, ukitoka hapa tusijuane siwezi kuna na mwanaume malaya kama wewe.”

    “Umalaya umeuona kwangu, usingekuwa malaya usingemuacha Shuku.”

    “Nakuapia nitamtafuta Shuku kwa gharama yoyote ili kurudisha penzi letu la kweli kuliko wewe tapeli mkubwa.”

    “Kwa taarifa yako Shuku ameoa,” MJ alimkatisha tamaa Lily.

    “Hata akioa haikuhusu.”

    MJ hakulala kwa Lily aliondoka usiku ule na kwenda kulala kwake. Lily alibakia na mateso yake na kuamua kuchemsha maji ambayo kidogo yalimsindikiza mpaka kupata usingizi kwani hali ilikuwa mbaya. Alikuwa kama mtu aliyechambia upupu na mkunaji alikuwa amekatika kucha. Baada ya kupewa kampani na maji moto kama mzazi aliyejifungua aliapa kumtafuta Shuku kwa gharama yoyote.

    *****

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Shuku baada ya kutoka kwa MJ aliamua kuhama kabisa eneo alilokuwa akiishi na kuhamia sehemu ambayo hakumweleza mtu aliamua kuishi maisha yake. Baada ya kutulia kwa muda aliingia kwenye kazi ya kulangua mazao na kuyauza sokoni Kariakoo kwa vile alikuwa na mtaji wa kutosha toka kwa MJ.

    Maisha yake kila kukicha yalimnyookea, aliweza kuyaendesha maisha yake bila kumtegemea mtu yoyote. Lily akiwa na dada yake sokoni Kariakoo alishtuka kumuona mtu kama Shuku akiwagawia watu fedha baada ya kushusha mazao kwenye gari.

    “Shuku,” alimwita kwa sauti ya mshtuko.

    Shuku bila kuitikia japo sauti haikuwa ngeni aligeuka na kumwangalia anayemwita na kukuta ni Lily.

    “Vipi Lily?”

    “Samahani Shuku nina mazungumzo na wewe.”

    “Ngoja nimalize kazi yangu.”

    “Hakuna tatizo nakusubiri.”

    “Sawa.”

    Lily alisogea pembeni kumsubiri Shuku huku akishangaa kumuona akiwa katika afya zuri zaidi kuliko ya awali. Kingine kilichomshtua na fedha nyingi aliyoshika mkononi aliyokuwa akiwagawia watu walionekana wakivuja jasho baada ya kazi nzito ya kupakua magunia kwenye gari.

    Baada ya kugawia washusha mzigo alimwita dereva wa gari.

    “Saidi unanidai shilingi ngapi?”

    “Laki mbili.”

    Shuku alihesabu laki mbili na kumpatia dereva kisha alirudisha fedha iliyobakia kwenye pochi na kumfuata Lily aliyekuwa haamini hali aliyomkutana nayo tofauti na alivyofikiria.

    Kilichomshangaza zaidi ni kauli ya MJ kumshangaa rafiki yake kuondoka kwa ajili ya mwanamke na kuacha gari na fedha taslimu milioni kumi. Aliamini hasira zake ndipo zilingemfanya arudi katika maisha ya kubangaiza na kuchoka kama mpira wa makaratasi.

    Baada ya kusogea kwa Lily alimsalimia.

    “Za siku?”

    “Nzuri sijui wifi hajambo?”

    “Halafu nikujibuje?”

    “Kama hajambo au tayari anakula udongo?”

    “Kwa kweli sina jibu, vipi MJ hajambo?”

    “Mmh! Yule mwanaume hafai.”

    “Kwa nini?”

    “Yule mwanaume malaya hatari.”

    “Umejua leo?”

    “Hata sijui, unajua alinieleza mengi kuhusiana na wewe. Kwa kweli aliyonieleza yaliuumiza sana moyo wangu. Lakini kumbe alitengeneza uongo.”

    “Uongo upi?”

    “Kuwa wewe unamtegemea na pia una tabia ya kuwatia wanawake mimba na kukimbia, eti mpaka unakwenda kwake ulikuwa umekimbia mimba nne.”

    “Aisee,” Shuku alijikuta akiangua kicheko.

    “Usicheke Shuku, MJ amekusema mengi mabaya lakini kumbe ilikuwa njia ya kunipata.”

    “Lakini imekusaidia leo una gari na nyumba tatizo lipo wapi?”

    “Nimeamua kuachana naye.”

    “Halafu.”

    “Nirudiane na wewe.”

    “Mmh! Mbona ngumu.”

    “Usifanye hivyo Shuku japo nasikia umeoa lakini bado nakupenda.”

    “Lily sina gari sina nyumba tutaishije, nami kabwela?”

    “Nisamehe kwa maneno yale ilikuwa hasira tu, Shuku nipo radhi kuishi maisha yoyote ili tu nisikupoteze mpenzi wangu. Nipo tayari kuuza magari yangu yote ili kukuongezea mtaji kwenye biashara zako nami kuwa mama wa nyumbani.”

    “Lily kwa vile nipo kazini nitafute baadaye tutazungumza vizuri.”

    “Shuku nipo tayari kukusubiri muda wowote.”

    “Hapana nipe nafasi nifanye kazi, nimekwambia nitakutafuta kwa hiyo vuta subira.”

    “Sawa nimekuelewa.”

    Lily aliondoka na kumwacha Shuku akiendelea na kazi zake, wakati huo gari lingine kutoka shamba lilikuwa likiingia.

    ****

    Shuku akiwa anamalizia kazi alijiuliza maswali mengi juu ya kutafutwa na Lily mwanamke aliyemshusha thamani. Hakutaka kuumiza kichwa aliendelea na kazi zake na baada ya kazi aliamua kurudi zake nyumbani kupumzika kwani alikuwa amechoka sana baada ya kufanya kazi kwa wiki mbili bila mapumziko.

    Kutokana na uchovu alisahau hata kuwasiliana na Lily, kwa vile hakupenda usumbufu baada ya kuoga na kula alipanda kitandani na kuzima simu zote kabla ya kulala. Toka Shuku aondoke kwa MJ hakuwa na mwanamke mwingine, alitulia atengeneze kwanza maisha yake, hivyo alikuwa akikaa na kulala peke yake, akili yake aliiekeleza kwenye kutafuta ili asiipate aibu kama iliyomkuta kwa swahiba wake MJ.

    Upande wa pili Lily alitegemea kupata simu kutoka kwa Shuku, lakini muda ulikatika bila kuona simu ikiingia. Aliamua kumpigia baada ya kuona muda umekwenda sana, lakini alipopiga simu haikuwa hewani.

    Lily alijikuta akichanganyikiwa na kuona kama Shuku ameamua kumpotezea. Alijikuta siku ile inakuwa chungu kwake kitanda kilikuwa kichungu alitapatapa kitanda kizima kama mzazi mwenye uchungu. Hakukubali kila dakika alipiga simu ya Shuku ambayo haikuwa hewani.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Lily alijikuta akikesha kuitafuta simu ya Shuku iliyokuwa haipatikani. Hakujua kama Shuku baada ya kutoka kwa MJ alibadili hata namba ya simu ili tu asiwasiliane na MJ.

    Lily baada ya kumkosa kwenye simu aliamka siku ya pili asubuhi kwenda kumtafuta Shuku. Baada ya kuoga bila kutia kitu kinywani alielekea sokoni Kariakoo kumtafuta Shuku. Alipofika sehemu aliyomkuta Shuku jana yake alimtazama huenda atamuona.

    Magari yaliyotoka shamba aliyaona yakipakuliwa, lakini Shuku hakumuona. Alijikuta akikaa zaidi ya saa mbili bila kumuona. Ilibidi amfuate kijana mmoja aliyekuwa pembeni ya gari akijifuta jasho baada ya kumaliza kupakuwa mizigo.

    “Samahani kaka yangu.”

    “Bila samahani dada yangu,” jamaa alijibu kwa ustaarabu kwa kujua labda anatafutwa mtu wa kumbebea mizigo yake.

    “Eti kaka yangu, Shuku yupo wapi?”

    “Shuku Zungu la roho?”

    “Yule aliyekuwa akisimamia upakuaji wa gari la mazao jana.”

    “Ndiyo huyo Zungu la roho.”

    “Kwa nini mnamwita hivyo?”

    “Yule dada ukifanya naye kazi utafurahi, wote tunapenda kufanya naye kazi.”

    “Kwa nini?”

    “Yaani hata siku akiwa hana kazi ukikutana naye akimuomba hela anakupa, pia hata kazi zake hana longolongo kwenye malipo.”

    “Kwani yeye huwa anafanya kazi gani hapa?”

    “Yule jamaa, zamani nakumbuka tumepiga naye sana kazi hapa kijiweni. Baada ya muda alipotea na kurudi akiwa na fuba la maana na kuanza kufuata mazao shamba. Alianza na gari moja sasa anapiga mpaka gari sita peke yake.”

    “Kwa hiyo, hiyo ni kazi yake au ameajiliwa?”

    “Yake mwenyewe, tena nasikia kuna mkoko wa nguvu anavuta muda si mrefu.”

    “Usiambie!” Lily alishtuka.

    “Dada kweli anayetoa Mungu humpa, yule jamaa ni zungu la roho kweli tofauti na wengine.”

    “Leo mbona simuoni?”

    “Mmh! Sidhani kama leo atakuja.”

    “Kwa nini?”

    “Jana kamaliza mzigo naona leo anapumzika kisha anaingia shamba.”

    “Shamba kufanya nini?”

    “Kukusanya mazao, wiki mbili zote alikuwa akija mjini alfajiri na kurudi kwake jioni.”

    “Sasa nitampataje?”

    “Labda uende kwake, zaidi ya hapo sijui namna ya kumpata.”

    “Huna namba yake ya simu?”

    “Mmh! Sina.”

    “Kwake unapajua?”

    “ Napajua, kwani we nani yake?”

    “ndugu yake, naomba unipeleke.”

    “Sister si unajua ndo gari la kwanza.”

    “Una maana gani?’

    “Yaani nikiondoka huku nyuma kazi zitanipita.”

    “Wala usihofu, kwani kila gari mnashushia shilingi ngapi?”

    “Elfu hamsini watu watano.”

    “Kwa siku mnashusha magari mangapi?”

    “Kuwa tunagawana, unaweza kushusha magari matatu mpaka manne kwa siku.”

    “Basi mi nitakupa elfu hamsini kunipeleka kwa Shuku tu.”

    “Utani huo sister.”

    “Kweli kabisa, ukifikisha na kunionesha anapokaa Shuku nakupa kisha tunaachana.”

    “Hakuna tatizo ngoja nikawaage wenzangu kisha nibadili nguo kisha nikupeleke.”

    “Haya fanya haraka.”

    Yule kijana alikwenda kuwaaga wenzake na kurudi akiwa amebadili nguo.

    “Sister tunaweza kwenda.”

    “Wawoo! Jamani kumbe kijana mzuri hivi?”

    “Sister yale ni mavazi ya kazi, baada ya kazi tunajichanganya kama kawa.”

    “Poa basi twende, kwani anakaa wapi?”

    “Keko Toroli.”

    Waliongozana hadi kwenye gari, mshikaji naye alishtuka kumkuta mwanamke mrembo akiendesha benzi.

    “Duh! Dada upo sawa.”

    ”Usikonde kaka yangu vitu vya kawaida, unaitwa nani vile?.”

    “Hashimu, Dada kwako vya kawaida wakati wengine hata baiskeli ndoto.”

    “Kwa vile unatafuta utapata tu kaka yangu usikate tamaa, funga mkanda basi tuondoke.”

    “Mmh! Kama nimo kwenye ndege vile.”

    Lily alichekea rohoni hakujibu aliwasha gari na safari ya kwenda kwa Shuku ilianza.

    Walipofika Keko Hashimu alimuelekeza Lily sehemu anapoishi Shuku. Walipokaribia alimuonesha nyumba kwa mbali.

    “Dada naomba unishushe hapa nyumba anayoishi Shuku ile pale yenye vioo vya tinted.”

    “Anaishi na nani?”

    “Mmh! Mara nyingi huwa namuona peke yake.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Si nasikia ameoa?”

    “Ndo nasikia kwako.”

    “Basi nashukuru,” Lily alisema huku akivuta mkoba wake na kuhesabu elfu hamsini kama alivyomuahidi. Alimuongezea na elfu tano ya nauli.

    “Na hii elfu tano ya nauli." ”Asante dada yangu."

    Hashimu aliteremka kwenye gari na kumwacha Lily aende peke yake. Baada ya kubaki peke yake aliendesha gari taratibu kuelekea kwenye nyumba aliyoelekezwa anakaa Shuku.

    Alilipaki gari pembeni ya nyumba ile ambayo ilionesha anakaa mtu mmoja tena mwenye uwezo kutokana jinsi ilivyokuwa. Alijikuta akiingia wasiwasi labda yule kijana amemdanganya. Lakini alisema yote atayajua hukohuko.

    Alitembea huku akiwa na mawazo mengi kama kweli Shuku anakaa pale, huenda yupo kwa ndugu yake kama alivyokuwa kwa MJ. Alipofika alibonyeza kengele iliyoita kwa muda mara alisikia sauti za miguu zikisogea mlangoni. Alitulia amuone anayefungua mlango ni nani.

    Mara mlango ulifunguliwa na kujikuta akitazamana uso kwa uso na Shuku aliyekuwa kwenye vazi la bukta kifua wazi. Shuku alipomuona Lily hakushtuka alimkaribisha ndani. Lakini Lily alijikuta akishika mkono kifuani kwa mshtuko.

    “Karibu,” Shuku alimkaribisha.

    “Asante Shuku nimekaribia.”





    Mara mlango ulifunguliwa na kujikuta akitazamana uso kwa uso na Shuku aliyekuwa kwenye vazi la bukta kifua wazi. Shuku alipomuona Lily hakushtuka alimkaribisha ndani. Lakini Lily alijikuta akishika mkono kifuani kwa mshtuko.

    “Karibu,” Shuku alimkaribisha.

    “Asante Shuku nimekaribia.”

    Shuku alimwacha Lily aingie ndani na kufunga mlango kisha aligeuka na kumkuta tayari mgeni wake amekaa kwenye sofa. Lily baada ya kukaa alizungusha macho katika sebule iliyokuwa na kila kitu kwa matumizi ya mwanadamu.

    Lily bado alikuwa na maswali mengi kichwani kuhusiana na vitu alivyoviona sebuleni pia nyumba ilikuwa ikitumia kiyoyozi. Wazo lake aliamini kabisa pale Shuku atakuwa anatunzwa na mtu na wala si kwake.

    Wakati wakiwa kwenye maswali yasiyo na majibu, Shuku alimuaga na kwenda chumbani mara moja na kumfanya Lily kuwa na uhuru wa kufanya uchunguzi wa kina.

    Macho yake yalipatwa na mshtuko baada ya kuona picha kubwa ya Shuku ikiwa ukutani kuonesha yeye ndiye mwenye nyumba. Lakini bado hakuamini mawazo yake huenda kaachiwa nyumba mwenye mji yupo nje ya nchi.

    Baada ya muda Shuku alirudi sebuleni na kumuuliza mgeni.

    “Mgeni unatumia kinywaji gani?”

    “Chochote utakacho nichagulia wewe mwenyeji wangu.”

    Shuku hakujibu kitu alikwenda kwenye friji na kumletea takira na kumfanya Lily ashtuke.

    “Shuku hii ya nani?”

    “Si umesema nikuchagulie kinywaji, unashangaa nini, au nimekosea?”

    “Shuku hiki ndiyo kinywaji changu kimefikaje kwako?”

    “Sasa huo ugomvi, kwani kinywaji hiki kimetengenezwa kwa ajili yako tu?”

    “Hapana, lakini najua hunywi kinywaji hiki kimefikaje kwenye friji yako.”

    “Ni kweli sinywi, lakini nyumba yangu inatembelewa na wageni wengi hivyo najitahidi kuweka vinywaji vingi. Ili ukija kama wewe basi upate kinywaji chako.”

    “Hapana Shuku una mwanamke anayekunywa kinywaji hiki.”

    “Sina.”

    “Unanidanganya Shuku una mwanamke mwingine,” Lily aliangua kilio cha wivu.

    “Sasa Lily hata kama ningekuwa na mwanamke wewe anakuhusu nini?”

    “Sikubali Shuku wewe bado mpenzi wangu sikubali mwanamke mwingine akuchukue.”

    “Kwa taarifa yako, sina mwanamke wala wewe huna nafasi tena kwangu.”

    “Shukuu, sikubali. Kumbe MJ alinidanganya na kusababisha tuachane.”

    “Kwani nilikufuata kukulilia?”

    “Hapana najua nimekukosea Shuku wangu, nahitaji kurudi kwako, nimeisha jua mbaya wetu, hata shoga zangu walinieleza MJ si mwanaume bali muharibifu.”

    “Muharibifu vipi wakati kakununulia nyumba na magari ya kifahari?”

    “Lakini hana upendo ambao kwako nimeamini upo ambao nitaupigania kwa nguvu zangu zote hata kufa, lakini nikurudishe mikononi mwangu." ”Lily mbona umechelewa.”

    “Nimechelewa kivipi?”

    “Mimi nimeishaoa." ”Etiii nini Shukuuu! Mungu wangu nakufa," kauli ile ilimfanya Lily aanguke chini na kupoteza fahamu.

    Shuku alishtuka kumuona Lily akianguka kama mzigo, alipomsogelea aligundua amepoteza fahamu. Alijalibu kumpa huduma ya kwanza ambayo ilikuwa mtihani kwani wakati wa kumhudumia Lily alikuwa ametandaza miguu na gauni lake fupi kupanda juu na kuyafanya mapaja kuwa wazi na njia ya kuelekea ikulu ilikuwa ipo wazi.

    Jicho la Shuku lilipotua kwenye mapaja laini ya Lily alijikuta akimeza funda la mate ya hamu na kuendelea kumuhudumia. Baada ya muda Lily alirudiwa na fahamu.

    “Vipi?” Shuku alimuuliza akiwa amemshika kichwani.

    “Safi,” Lily alijibu kwa sauti ya chini huku akimuangalia kwa jicho la kuihitaji huruma.

    “Tatizo nini?”

    “Naomba kwanza uniingize chumbani nilale.”

    “Kwani unajisikiaje?”

    “Mwili umechoka sana mpenzi wangu.”

    Kauli ya kuitwa mpenzi japokuwa Shuku hakuipenda lakini hakuwa na jinsi kwa vile alitaka Lily awe kwenye hali nzuri.

    “Lily twende hospitali.”

    “Ukinipeleka hospitali nitakufa.”

    “Hapana utapata tiba nzuri.”

    “Shuku kabla ya kunipeleka hospitali naomba ninale kidogo.”

    “Kwa vile hapa sebuleni kuna upepo mzuri lala hapo kwenye kochi.”

    “Shuku nasikia joto sana.”

    “Nikusogezee feni?”

    “Hapana nataka nijimwagie maji.”

    “Bafu lipo huko,” Shuku alimuonesha bafu kwa kidole.

    Lily baada ya kufanikiwa kumdanganya Shuku amepoteza fahamu, alijifanya kujinyanyua kwa shida. Shuku alimsogelea na kuingiza mkono chini ya kwapa na kumsaidia kumshikilia. Walitembea taratibu huku Lily amekilaza kichwa kwenye kifua cha Shuku ana kutonga kama mtu anayeumwa sana.

    Shuku alimfikisha nje ya bafu na kumweleza aingie.

    “Lily ingia uoge mi nipo sebuleni.”

    “Hapana shuku naomba unishikilie nijimwagie maji.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Sasa utaogaje nami nipo?”

    “Shuku kipi kigeni kwako katika mwili wangu, hebu nisaidie bwana.”

    Shuku hakuwa na jinsi aliingia naye bafuni, Lily aliamini ile ndiyo sehemu ya kuhakikisha anabakia kwa Shuku baada ya kuliona penzi lake lilikuwa halina maisha. Kwa makusudi alizidondosha nguo kwenye maji.

    “Mungu wangu, sasa itakuwaje?” Lily alijifanya kushtuka.

    “Lily hebu jimwagie kwanza maji ili kuupa nguvu mwili.”

    Lily aliamalizia kufuli na mkanda na kufanya mambo yawe wazi kama jua la mchana linavyoangaza pembe zote za dunia.

    Shuku alizidi kumeza mate ya uchu huku akijikaza kuhakikisha hafanyi lolote kwa Lily. Lakini katika kambi yake ya jeshi hali ilikuwa mbaya baada ya kamanda mkuu kutaka kutoka nje ya kambi baada ya kuona anafanyiwa dhihaka.

    Lily alijifanya hana hata nguvu za kufungua bomba.

    “Shuku nifungulie maji.”

    Shuku wakati akifungua maji Lily aliteremka chini na kuingiza mkono kwenye kichaka na kumtoa nyoka aliyekuwa na hasira. Shuku alishtuka lakini alikuwa amechelewa kwani tayari Lily alianza kuchana mistari kwa ufasaha zaidi kwa vile maiki ile alikuwa ameizoea. Alijikuta akibembea juu kwa kwa juu kama shati lililo juu ya enga.

    Lily suala na kujimwagia maji aliliweka pembeni na kuhakikisha mpaka wanatoka bafuni penzi lake lizaliwe upya.

    “A..a..shiiii! Lily,” Shuku alitatalika huku amekishika kichwa cha Lily kama mpiga ngoma kujikuta akimwaga uno la juujuu. Ghafla Shuku aliwasikia wazungu walisogea kwa mbali na kujikuta akichanganya miguu kama mtu anayetaka kufumua shuti kali.

    Kwa haraka Lily aliitoa maiki mdomoni na kuuingia mwiko kwenye chungu. Kwa vile mchicha ulikuwa umekolea nazi, Shuku alijikuta akipiga mikono minne ya kasia na chombo kufika pwani.

    Kwa vile Shuku alikuwa na nguvu pia ugwadu wa muda mrefu alijikuta akipiga two in one (mbili kwa moja) watoto wa mjini wanasema mumo kwa mumo.

    Lily naye alikuwa kama samaki aliyekuwa akitatafuta maji kwa muda mrefu siku ile alikuwa ameyapata. Moyoni alijiapiza mpaka wanatoka bafuni lazima Shuku amrudishe mikononi mwake. Mtoto wa kike alijituma, kila kasia zilivyokuwa zikipigwa ndivyo wazimu ulivyompanda. Mikono alishika kichwani na kuinama kama anatafuta kitu alichokidondosha chini alijipindua nyuma kama nge aliyepandwa na hasira anamvizia mtu kumgonga na kuiacha nyonga laini ifanye kazi.

    Shuku alishangazwa na kujiuliza mara mbilimbili, Lily ana mfupa au kafunga feni. Walijikuta wakienda sambamba kila mtu akiwa na hamu na mwenzake baada ya kumkosa kwa muda mrefu.

    Lily aliamini mkunaji wa upele wake unamsumbia toka alipokuwa na MJ alikuwa amerudi. Shuku naye baada ya kutoa kipigo cha pweza alikumbuka mtu anayempa shuruba nzito ametoka kwenye ugonjwa.

    Alijikuta akipunguza kasi kitu kilichomshtua Lily na kulalamika.

    “Shukuuu unafanya niniii?”

    “Lily si unaumwa?”

    “Utaniudhi! Nani kakwambia mi naumwa? Hebu nipe raha zangu zimezikosa muda mrefu.”

    Mwanaume hakutaka kulemba tena, siku zote mtoto hatishiwi ubwabwa ndicho chakula anachokipenda. Chombo kikarudishwa kwenye maji na kupiga kasia mtindo mmoja mpaka walipojikuta wakiangukiana baada ya kila mmoja miguu kupoteza uwezo wa kusimama kwa muda mrefu. Kwa vile ulikuwa mpambano wa kushtukiza, baada ya kuoga walirudi ndani na kupanda kitandani kujipumzusha na kujikuta wakipitiwa usingizi mzito.

    Wa kwanza kuamka alikuwa Lily, bado hakuamini kama kweli Shuku ameoa, ili kupata uhakika alianza kupekua kwenye kabati iliyokuwa wazi.

    Alichambua kwenye nguo labda atakuta nguo za kike, lakini hakuona kitu. Alichukua albam na kuangalia picha na kushangaa kukuta picha zake na Shuku za zamani wala hakukuwa na picha za mwanamke mwingine pia kulikuwa na picha alizopiga Shuku akiwa shamba alipokuwa akienda kukusanya mazao.

    Baada ya kufanya upekuzi wake uliochukua chini ya dakika kumi bila kuona alichokikusudia. Alijikuta akijiuliza huyo mwanamke aliyemuoa Shuku yupo wapi na mbona hakuna picha wala nguo zake na kwa nini picha zake iwepo kwenye albam ya Shuku na si ya huyu mwanamke wake.

    Alijikuta akikosa jibu la moja kwa moja, kuwepo kwa picha zake ilionesha Shuku bado ana mapenzi na yeye lakini mbona kamwambia ameishaoa? Alijikuta akichanganyikiwa na kushindwa kuelewa hatima yake kwa Shuku.

    Alijiuliza akiamka atamwambia nini ikiwa tayari amemtamkia ameoa. Alirudi kitandani na kukaa pembeni ya Shuku aliyekuwa bado amepitiwa na usingizi baada ya shambulizi ya kushtukiza lililomchosha sana.

    Lily alianza kulia kilio cha sauti ya chini iliyomshtua Shuku kwenye usingizi.

    Aliposhtuka na kumukuta Lily amekaa kitandani akilia, aliuliza.

    “Lily unalia nini?”

    “Najua nitakufa Shuku.”

    “Utakufa! Kivipi?”

    “Utaniua wewe Shuku.”

    “Mimi nikuue wewe! Kivipi?”

    “Hunipendi.”

    “Mimi na wewe nani hampendi mwenzake?”

    “Wewe Shuku, kwa nini kila mara unapenda kunidanganya?”

    “Kukudanganya kivipi?”

    “Shuku huna mwanamke.”

    “Nani kakwambia?”

    “Shuku nimekufuatilia muda mrefu ndiyo maana hata wewe kukubali kufanya mapenzi na mimi ulijua huna mtu.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hiyo siyo sababu.”

    “Shuku kweli huna mwanamke, nakuapia hapa sitoki tena, mi ndo nimefika,” Lily alisema huku akijilaza juu ya Shuku ambaye hakupata nafasi ya kuzungumza kitu.

    Mtoto wa kike akaanza utundu uliomfanya Shuku asisimke kwa vile alikuwa na ugwadu wa muda mrefu, chombo hakukichelewa kukolea moto.

    Mtanange wa bafuni japokuwa palichimbika bila jembe lakini ilikuwa kama kupasha moto mwili. Mchezo ulihamia kwenye uwanja wa vita wa sita kwa sita.

    Lily alimkalia juu Shuku na kuanza kufanya utundu uliomdanya aliruke kama kalalia siafu.

    Alijiteremsha kuufuata mdomo wa Shuku ambao aliupata na kuifanya igandane,

    Shuku naye alitii amri kwani sumu ya hamu ilikuwa imemtawala mwili mzima naye alipitisha mkono shingoni kwa Lily na kumvutia kwake na kuanza kubadilishana mate.

    Kwa umbile na uwezo wa Lily ulimfanya Shuku asahau maudhi yote ya zamani ya mpenzi wake. Lily alimpindua Shuku na yeye kuwa chini na kuikutanisha miguu yake mgongoni kwa Shuku kama mtoto wa nyani.

    Kama kawaida Lily alikanyaga mpira na kumfanya Shuku autafute kwa muda kwa muda mfupi. Hakuchelewa kuupata alipoupata naye akajibu mashambulizi kwa pasi fupifupi zilizomfanya Lily alalamike.

    “Jamani Shuku mpenzi wangu siyo hivyoo au hufurahii kuwa na mimi.”

    “Nafurahia mpenzi wangu.”

    “Sasa mbona unanibania nipe raha zangu nilimezikosa muda mrefu.”

    Mtoto wa kike alilipandisha jicho pumzi zilimtoka kwa shida chini nyonga ilifanya kazi kama nyoka anavyosafiri kwenye majani.

    Aliamini hakuna njia nyingine ya kujirudisha kwa Shuku ni kumpa penzi shatashata lisilochanganywa na maji. Shuku aliyekuwa kama mbwa kwa chatu anapokutana na Lily naye aliyeuanza mchezo kwa kusuasua alirudi mchezoni.

    Alianza kutandaza soka safi huku akitawala sehemu ya kiungo na kumfanya Lily autafute muda wote. Baada ya Lily kupata kipigo cha pweza alijikuta akitoa siri ya MJ.

    Shuku alimchanganya Lily na mtindo wa Punzu magulu remix. Alijikuta akihama katika dunia aliyoizoea na kujikuta akitokwa na maneno kama mvua.

    “Shuuuukuuu aashiii, unajuaaa, Shuku unajuaaa. Shuku niliota kutu kupakwa shombo na MJ leo chuma kimapata msasa safishaaa mpenziii.”

    Lily alilalama huku akiiachia nyonga izungumze na Shuku naye alikuwa amemisi maini ya Lily kwa muda mrefu mwiko ulifanya kazi ya kuyageuza kwa mahiri mkubwa. Alijigeuzia atakavyo, mpaka wanakwenda mapumziko Lily alikuwa ndwembwendembwe.

    Baada ya mpambano wa kukata na shoka Lily aliangua kilio kilichomshtua Shuku.

    “Lily unalia nini?”

    “Kwa nini ulinidanganya?”

    “Kukudanganya kivipi?”

    “Kwa nini hukuniambia ukweli mwanzo wa penzi letu?”

    “Nilijua nitakukosa, Lily nilikuwa nakupenda sana.”

    “Kwa hiyo sasa hivi unipendi?”

    “Narudi mimi na wewe nani hampendi mwenzake?”

    “Wewe.”

    “Nani aliyemsaliti mwenzake?”

    “Wewe.”

    “Kwa nini?”

    “Hakuniambia ukweli kitu kilichosababisha niyaamini maneno ya MJ.”

    “Kwa nini ulimuamini?”

    “Mitego niliyokutega ndiyo iliyokunasa, kwa hiyo yote aliyoniambia niliyaamini. Ona raha hizi nilizipoteza Shuku nazidi kukulaumu kunidanganya.”

    “Sasa kama uliyaamini tatizo nini?”

    “Nimegundua MJ si mkweli mgombanishi kupitia fedha zake. Shuku yote umesababisha wewe,” Lily aliendelea kumlaumu Shuku.

    “Lakini uli...”

    “Shuku usiseme lolote kila siku nitakulaumu wewe.”

    “Basi yamekwisha.”

    “Shuku unanipenda?”

    “Zaidi ya kukupenda.”

    “Naomba usinidanganye ili nami nidumu kwenye penzi lako. Mimi si mpenda fedha kama unavyodhani bali naogopa kudanganywa.”

    “Nimekuelewa mpenzi wangu.”

    “Kama umenielewa nipe haki yangu.”

    Shuku hakuwa na hiyana kwani hata yeye aliumia kuachwa na Lily mwanamke ambaye kwake ndiye aliyekuwa chaguo la moyo wake. Kazi ikawa bandika bandua kila mmoja alitaka kuonyesha anajua mapenzi mpaka raha ikageuka karaha na kuamua kupumzika wakiwa hoi.

    ***

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Penzi lilirudi kwa kasi huku Lily akimganda Shuku kama luba ili kuhakikisha hampotezi. Baada ya muda Lily aliuza nyumba na kuhamia kwa Shuku kujipanga na ndoa yao. Kila kitu kilikwenda kama kilivyopangwa. Siku ilipofika ilifungwa harusi ya kifahari huku MJ akichangia kwa kiasi kikubwa na siku ya harusi aliitumia kuomba msamaha kwa maharusi.

    Shuku hakuwa na hiyana na rafiki yake alimsamehe huku akimpa onyo akimfuata tena mkewe atamteremsha mshipa. MJ alimwambia rafiki yake kuwa kuoa kwake kumpa fundisho kubwa hivyo naye aliamua kumtafuta mwanamke mmoja na kufunga naye ndoa kuanza maisha mapya.

    Mpaka sasa hivi maisha yanakwenda Shuku na Lily wana mtoto mmoja na mke wa MJ anakula maembe mabichi na mate yanamjaa mdomoni.

    MWISHO ---------MWISHOOOOOOOOOOOOO.........MWISHOOOOO

0 comments:

Post a Comment

Blog