Chombezo : Chuzi Ndo Hilo, Hakuna Kuonja!
Sehemu Ya Nne (4)
Mama Shua alijikuta akiingia wasiwasi, akatoka kwa kasi huku macho pima… “Mungu wangu…Mungu wangu. Yule mzee kaniona tena jamani, kamtumia mama meseji,” alisema moyoni mama Shua huku akiseti simu yake ili ampigie mdogo wake… “Selina, mama kanitumia ujumbe tena. Inaonekana yule mzee ameniona tena. Mimi nilikuja hapa kuonana na mwanamke mwenzangu, wala si Musa…” “Musa ni nani kwani dada?” mdogo wake alimuuliza. “Ha! Nilikosea.” Mama Shua alikata simu, akatoka hadi nje kabisa na kusimamisha teksi tayari kwa kurudi nyumbani kwake. “Hivi yule mzee ananitafuta nini mimi? Ana maana gani kunifuatilia kiasi hiki?” alijiuliza akiwa anapanda kwenye gari hilo. Alisahau kabisa kumpigia simu Musa kumjulisha mpaka Musa alipopiga yeye… “Uko wapi baby?” “Ah! Baby nimepata dharura bwana, nimeondoka. Please tukutane kesho baby au nyumbani nitakwambia.” “He! Dharura gani mpaka unafikia hatua ya kuondoka bila kuniambia mapema. Mimi nimeingia mpaka hotelini sasa.” “Sikia Musa, twende kwingine tukatafute hoteli nyingine.” “Kama wapi?” “Popote pale lakini si hapo,” alisema mama Shua na kukata simu ili asome meseji ambayo iliingia wakati anaongea na Musa… “Umeona aibu kuingia hotelini na kuamua kuondoka siyo? Ungeingia tu. We mtoto huo mwenendo wako kama utaendelea kuwa hivyo sijui kama utadumu kwenye ndoa,” ni ujumbe uliotoka kwa mama yake. Mama Shua aliishiwa nguvu kabisa kiasi kwamba alitamani ardhi ipasuke sasa ili afie humo. Mara, Musa akampigia simu… “Haloo Musa…” “Ee, sasa sikia. Nakwenda Makumbusho, tukutane kule,” alisema Musa… “Sawa. Sehemu gani?” “Pale baa. Lakini tukitoka pale tunakwenda gesti, sawa?” “Sawa baby.” Mama Shua alihisi mwili unamsisimka kwa maneno ya Musa, akajikuta anaachana na wazo la kwenda nyumbani. Akamwambia dereva ampeleke Makumbusho. Alifika Makumbusho, akashuka. Akatembea hadi kwenye baa hiyo lakini hakumkuta Musa, akampigia simu. “Uko wapi sasa, mbona hapa baa haupo?” “Nilikuja kuchukua chumba huku gesti.” “Wapi nije?” Musa alimwelekeza mama Shua. Wakati anakwenda, njiani mama Shua alikasirika sana kuhusu yule mzee na mama yake hivyo akaamua moyoni kwamba akikutana na Musa ampe mahaba mazito kama kulipa kisasi kwa mama yake na yule mzee. Mama Shua aliingia, akapita kwenye korido mpaka kwenye chumba kwa mujibu wa maelekezo ya Musa. Akazama ndani. Ile anafika tu, akiwa bado amesimama alimkumbatia Musa na kumpiga mabusu kibao, mara akaomba denda, wakazama kwenye denda kwa muda wa kama dakika tano nzima huku wakitoa miguno ya mmmhCHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/…mmmh! Mama Shua, wakiwa bado wamesimama, akapeleka mkono kwenye suruali ya Musa na kuanza kumfungua kizuio chake kisha akamshusha suruali hadi chini. Baada ya hapo akamvua shati, mara akamvua singilendi mpaka Musa akabaki mweupe. Musa naye kuona hivyo, akaanza na yeye mpaka mama Shua akabaki mweupe kama yeye. Wote wakabaki weupe, wakapanda kitandani. Mama Shua alikuwa akihema sana hivyo kumfanya Musa naye kuambukizwa na mhemo wake, hawakuchukua muda wakaingia kwenye uwanja na kuanza kucheza. Mama Musa huku akijua kwamba Musa atafika haraka safari yake ilibidi aanze kumsemesha… “Unajua mwenzako nina msala…” “Msala gani?” “Mama angu amejua mimi ninaingia hotelini pale. Kuna mtu ananionaga. Sasa leo pia kaniona. Akamwambia mama, mama akanitumia meseji nzito sana. Yaani jamani.” “Mh! Kwa hiyo?” “Kwa hiyo nini sasa. Nilitaka kwenda nyumbani lakini nikajua wewe utakwenda pale na wanawake zako.” “Umeanza baby. Kwa nini tusisubiri tumalize ndiyo uanze kunishutumu?” “Hakuna bwana, we unapenda sana wanawake. Mi unanikera sana ujue.” “Uliwahi kuniona na mwanamke wapi?” “Najua tu. We endelea.” Ilifika dakika ya kumi siku hiyo, mama Shua ndiyo aliyeanza kutangaza nia kwa Musa ikabidi Musa naye ahemuke na kutangaza na yeye wakafika mwisho wa mchezo. *** Waliendelea kulala humo chumbani huku mama Shua akimtekenyatekenya Musa mpaka Musa akawa ngangari tena. Wakaingia tena uwanjani. Safari hii, mama Shua alimsemesha sana Musa maneno ya kila aina… “Siku nikikuona na mwanamke mwingine Musa utanijua mimi ni nani!” “Kivipi?” “Nitakufanyia fujo hata mbele za watu mimi sitajali ujue… ohooo.” “Haitatokea.” “Haitatokea kwa sababu unajificha sana si ndiyo?” “Hamna,” alisema Musa hapohapo akatangaza nia. *** Mama Shua aliingia nyumbani akijifanya mnyonge kwamba, hajisikii vizuri maana alimkuta mume wake amesharudi na amekaa sebuleni. Lakini mumewe hakumuuliza mbona mnyonge, alimwangalia tu. “Hivi baba Shua mimi naumwa hata kuniuliza hutaki? Hayo ni mapenzi gani lakini? Ina maana wewe uumwe mimi nikae kimya nakuangalia tu utajisikiaje?” “Kama unaumwa si ungeenda hospitali?” “Kwani sijaenda?” “Pale gesti Makumbusho ndiyo hospitali?”
Mama Shua alishtuka sana kumsikia mumewe akisema hivyo, akajikuta anamtumbulia macho.
Kusema amuulize kama alimwona alishindwa kwani alijua lazima mumewe amemwona akiingia au akitoka kwenye gesti hiyo ya Makumbusho…
“Au kama hajaniona yeye kuna mtu amemwambia,” alisema moyoni mama Shua huku akiwa na uso wa aibu…
“Da! Nimeumbuka hivihivi…yaani hapa napotea huku najiona,” mama Shua aliendelea kusema moyoni na kuingia chumbani huku miguu yake ikikosa nguvu ya kutembea…
“Hizi salam zikifika kwa mama ndiyo tabu,” aliendelea kusema moyoni mama Shua huku akilitupa begi lake chini.
Jambo lililomshangaza sana ni kuona mumewe amelichukulia suala la yeye kuingia gesti Makumbusho kama utani…
“Ina maana awe ameniona au ameambiwa halafu aniulize kirahisi vile? Haiwezekani,” alisema moyoni.
Baba Shua aliendelea kukaa sebuleni bila kumfuata mumewe chumbani, alikuwa akiwaza…
“Huyu dawa yake ni moja tu. Ni kumtema. Nikisema nimvumilie nitakufa kwa presha. Hivi kwa nini ananifanya mimi mtoto mdogo? Atakapokuwa mbali na mimi ndiyo atajua umuhimu wa kuheshimu ndoa yake.”
***
Kule chumbani, mama Shua alikaa kitandani akiendelea kuwaza na kujiuliza maswali kadhaa kichwani…
“Na kama aliniona yeye mwenyewe si ina maana aliniona nikiwa na Musa? Da! Nimeumbuka kwelikweli.”
***
Musa naye alikuwa chumbani kwake. Alihisi joto la mahaba, akatamani amwite mama Shua walicheze libeneke ili alale usingizi mnono. Akamtumia meseji…
“Baby.”
Mama Shua hakuchukua muda kuijibu meseji hiyo, tena kwa haraka sana…
“Niambie baby! Siko poa sana.”
“Pole baby, unaumwa?”
“Hapana… basi tu.”
“Sasa si uje, nimekumisi sana.”
“Da! Musa bwana…unanipa majaribu ujue.”
“Kwa nini?”
“Si hivyo unavyoniita…mista yupo ujue…”
“Kha! Kwani hata juzi si alikuwepo…mbona ulikuja…njoo bwana…mara moja tu…”
Mama Shua hakumjibu Musa, akavua nguo na kuvaa upande mmoja wa kanga huku moyoni akisema… “Musa naye…yaani kila saa anataka.”
Alitoka sebuleni, akamkuta mumewe amekaza macho kwenye tivii akiangalia taarifa ya habari, akatoka kwenda uani.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Aliweka maji bafuni, akasimama kwa muda akiwaza akaingie chumbani kwa Musa au la!
“Lo! Mbona shughuli…lakini na mimi kama namuhitaji Musa…ngoja nimwambie awe tayaritayari ili nikifika tu chapuchapu ili niwahi kutoka.”
Alirudi chumbani, akamtumia meseji Musa…
“Baby, mlango uwe tayari na wewe pia uwe tayari…nikifika tu chapuchapu ili nitoke.”
“Poa,” alijibu Musa.
Mama Shua alitoka, akajifanya anakwenda uani. Akasimama kwenye mlango wa Musa, akashika kitasa, akafungua, akazama ndani…
“Baby yaani hapa hakuna kupoteza muda, jamaa amekaa sebuleni.”
“Poapoa,” alisema Musa huku akifunga mlango.
Mama Shua alijivua ile kanga na kuitupia kwenye kiti, akajipeleka kitandani mwenyewe huku akiwa anahema kwa kasi.
Hakukuwa na maandalizi wala kupandishana joto, waliingia uwanjani moja kwa moja na kuanza kulisakata kabumbu harakaharaka. Safari hii, mama Shua hakuwa na haja ya kumsemesha Musa ili achelewe matokeo yake akamhamasisha ili amalize mchezo haraka. Kweli ikawa hivyo tena wote kwa pamoja.
Baada ya hapo, mama Shua aliiokota kanga yake haraka, akajifunga kifuani na kutoka kinyemela huku akiurudishia mlango polepole ili usisikike.
Alishtuka kumsikia mumewe anaoga yale maji aliyoyaweka yeye…
“Mh! Ina maana…si atajiuliza mimi niko wapi?” alijiuliza mwenyewe mama Shua huku akitetemeka.
Alikwenda chumbani, akakuta nguo za mumewe ziko chini…
“Ina maana hapa atajua nilikuwa wapi! Chooni ndiyo bafuni kulekule. Jiko liko ndani na limefungwa. Na kama ni jikoni alipokuwa akienda kuoga si angeniona. Da!”
Alishika simu yake, akamtumia meseji Musa…
“Da! Nahisi kama nimeumbuka.”
“Kivipi baby, nikupigie simu?”
“Hapana! Ila kuna ishu kubwa sana.”
“Da! Baby, unanitisha. Jamaa kajua?”
“Atakuwa kajua.”
Mara, baba Shua aliingia akitokea bafuni kuoga. Akajifuta maji kwa taulo, akavaa bukta kisha akatoka kwenda kukaa sebuleni…
“Mh! Ina maana hajajua? Mbona haniulizi?”
Mama Shua naye akatoka kwenda kutenga maji mengine akaoga na kurudi chumbani.
Hakuwa na namna, alipanda kitandani kulala huku moyo ukimwenda kwa kasi ya ajabu…
“Lakini mimi nimeanzisha tabia gani jamani? Mbona zamani sikuwa hivi, sasa itakuaje?” Alipitiwa na usingizi. Alipokuja kuamka, mumewe alikuwa pembeni amelala akiangalia juu na magoti yakiwa juu kwa maana kwamba hakuwa usingizini…
“Baba Shua…”
“Mm…”
“Mbona hujalala?”
“Ungekuwa wewe ungelala?”
“Ningekuwa mimi kivipi sasa?” “Wewe ungekuwa umeniona mimi nikiingia chumbani kwa mwanamke mpangaji mwenzetu na ukasikia kitanda kinalia na mimi natoa sauti za mihemko ya mapenzi ungepata usingizi?”
Mama Shua alishtuka sana, akaamka na kukaa kitandani. Alitingisha kichwa kama vile alisikia vibaya… “Sijakuelewa baba Shua.” “Hujanielewa nini sasa? Wewe umeingia chumbani kwa yule kijana. Umekula uroda, unabisha? Au ulitaka nisimame mlangoni kwake ndiyo ujue kwamba nimejua umeingia kule?” Mama Shua alikaa kimya. Baba Shua akajipinda na kuangalia upande mwingine kuuchapa usingizi huku akimwacha mkewe bado amekaa akiwaza na kuwazua… “Da! Yaani nilidhani ni siri lakini kumbe nimeonwa? Hivi ni kweli ameniona au anahisi tu? Lakini nawezaje kusema si kweli ila anahisi wakati mimi mwenyewe najijua kweli niliingia chumbani kwa Musa? “Ila sasa kama baba Shua aliniona kwa nini hakuchukua hatua palepale? Lakini pia kama angeamua kunichukulia hatua je, mimi nilikuwa tayari kwa kuchukuliwa hatua?” Yote hayo aliyawaza mama Shua huku akijisikia aibu mwenyewe. Usingizi ulimkatika, akatoka kwenda chooni. Alipokuwa akipita kwenye mlango wa chumba cha Musa, alihisi kichefuchefu. Akajutia. Lakini wakati anatoka chooni kuingia ndani, akakutana na Musa naye akiwa anatoka kwenda chooni… “Vipi baby?” Musa aliulizia kwa sauti ya chini. “Poa,” mama Shua alijibu kwa mkato, Musa akamshika mkono kumzuia asiendelee mbele… “Wewe huogopi?” aliuliza mama Shua… “Niogope nini sasa?” “Bwana, mwenzio nina msala chumbani kwa mume wangu.” “Msala gani?” “Nitakwambia.” “Sikia…sikia baby…” “Sema, nakusikiliza…”CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Twende chumbani kwangu.” “Ha! We saa hizi wakati nimekwambia kabisa kwamba nina msala…” “Sikiliza baby, ukiamua kula nguruwe kula aliyenona. Kama una msala malizia kula raha ili msala uwe mdogo,” alisema Musa… “Una maanisha nini?” “Namaanisha twende chumbani kwangu tukajirushe, msala utaushughulikia kesho.” Maskini mama Shua, eti maneno hayo tu alijikuta akishawishika na kukubali kuingia chumbani kwa Musa… “Lakini kama saa zile Musa, iwe chapuchapu! Sawa?” alisema mama Shua huku akiwa anaitupa kwenye kochi kanga moja aliyovaa. Walipanda kitandani na kwa vile walikuwa wanaibia mechi, hakukuwa na maandalizi, palepale wakaingia uwanjani na kuanza kulisakata kabumbu kwenye uwanja wa sita kwa sita.Kweli, safari hii mama Shua alionekana kucharuka sana kitandani kwa sababu alitembea kwenye ile dhana ya Musa kwamba kama kuna msala, ajirushe tu kesho yake atashughulikia msala wake. Ni dakika chache za wizi lakini mama Shua alizitumia vizuri kuliko Musa kwani alipata ushindi wa kwanza, kufumba na kufumbua akapata ushindi wa pili kabla Musa hajapata ushindi wa kwanza kwa mbwembwe. Baada ya kumaliza, mama Shua alisimama, akavaa kanga yake huku akisindikizwa na Musa kutoka. Lakini kushika mlango hivi, kumbe umefungwa kwa nje… “Haa!” mama Shua alihamaki kwenye masikio ya Musa ili asisikike… “Vipi?” “Mlango umefungwa kwa nje…” “Hamna bwana…nani afunge?” alisema Musa huku akishika kitasa… “Mungu wangu, kweli mama Shua. Unadhani atakuwa nani?” “Nahisi ni mume wangu. Nani mwingine humu ndani anaweza kufunga mlango kwa nje?” alisema mama Shua huku akianza kutetemeka. Mbaya zaidi, simu yake aliiacha chumbani. Moyoni alisema afadhali angekuwa nayo, angempigia msichana wake wa kazi amfungulie. Lakini akili ikakumbuka kwamba, namba za dada wa kazi anazo kichwani hivyo akamwomba simu Musa ili ampigie… “Sasa kama jamaa amesimama mlangoni si atakusikia?” Musa aliingia wasiwasi… “Nitaongea kwa sauti ya chini sana.” Mama Shua alimtajia namba Musa, akaziandika kwenye simu yake na kumpigia. Simu ilipoita, Musa akampa simu mama Shua… “Haloo…we nani?” dada wa kazi aliuliza kwa sauti ya juu maana hakuwa na namba za Musa… “Sikia dada, mimi mama Shua…” “A…aaa…vipi dada, uko wapi kwani?” “Sikia…toka chumbani, nenda kwenye mlango wa yule kijana mpangaji mgeni, kama mlango wake umefungwa kwa nje mfungulie, sawa?” alisema mama Shua katika mazingira ambayo, dada wa kazi hakujua kama bosi wake huyo alikuwa ndani ya chumba hicho… “Sawa dada.” Msichana wa kazi alitoka, akaenda lakini alishtuka kumkuta baba Shua amesimama mlangoni, akajifanya anakwenda chooni… “Shikamoo baba…” “Unaamkia sana, we pita na hamsini zako.” Msichana wa kazi alipita akitetemeka. Alijilazimisha kujisaidia kisha akarudi ndani. Alichukua simu akatuma tafadhali nipigie kwenye namba ya Musa. Musa akampa simu mama Shua, akapiga… “Dada hujatoka tu?” “Nimetoka mama, baba amesimama katikati ya mlango, akaniambia niendelee na hamsini zangu.” “Ulimwambia unataka kufungua mlango..?” “Hapana, sijamwambia. Nilimwamkia akasema ninaamkia sana.” Mama Shua akakata simu, akakaa kitandani na kuanza kuporomosha machozi huku akimlaumu Musa... “Nilikwambia nina msala Musa hukutaka kunielewa. Unaona sasa?” “Sasa si wakati wa kulaumiana huu mama Shua, tuangalie itakuaje?” “Sasa unadhani itakuaje na mtu kasimama mlangoni!” Pale nje, baba Shua aliwaza kuwagongea mlango wawili hao ili ijulikane moja.
Aliwaza sana, akaamua kwamba amwambie msichana wake wa kazi ni marufuku kufungua mlango wa chumba cha Musa endapo ataambiwa afanye hivyo…
“Ngo ngo ngo,” aligonga.
Msichana wa kazi akafungua na kusimama mlangoni…
“Dada, mama Shua ameingia kwenye chumba cha yule kijana mgeni…”
“Haa! Kufanya nini?”
“Anajua mwenyewe…sasa sikia, akikupigia simu ukamfungulie mlango usiende maana ni mimi nimefunga kwa nje…”
“Ha! Sasa dada kaenda ndani kwa watu kufanya nini tena jamani? Halafu mbona ni usiku sana?”
“Mama Shua si mwaminifu,” alisema baba Shua huku akiondoka kurudi chumbani kwake.
Alipanda kitandani kulala, akaanza kuwaza kabla ya kuupata usingizi…
“Siwezi kuwa na ndoa tena…na nikisema nimvumilie nitakuwa mwanaume wa ajabu wa kwanza hapa duniani,” alisema moyoni baba Shua. Usingizi ukampitia haraka.
***
Kule chumbani, mama Shua na Musa walikaa tu juu ya kitanda. Muda mwingi mama Shua alikuwa akimwaga machozi. Kuna wakati alimwingiza akilini mama yake mzazi, akajikuta akiogopa zaidi…
“Musa, unadhani itakuwaje sasa?”
“Kuhusu nini?”
“Mimi naachwa mwenzako. Kwani we hujui?”
“Da! Sasa tufanyeje mama Shua?”
“Mi sijui.”
Hakuna aliyelala, muda mwingi walikuwa wakisinzia lakini bila kulala. Mama Shua hakumpigia tena simu msichana wake wa kazi baada ya kujua kuwa, mumewe amesimama mlangoni…
“Yaani najuta mimi najuta! Nilikuwa nakosa nini kwa mume wangu mpaka kujikuta natumbukia kwenye penzi la nje. Nitamwambia nini mama?” alisikitika mama Shua huku machozi yakiufunika uso wake.
Jogoo la kwanza liliwika, mama Shua akashtuka sana…
“Umesikia jogoo hilo?” alimwambia Musa…
“Kumekucha,” alisema Musa huku akiuendea mlango na kujaribu tena kuufungua, akakuta umefungwa vilevile. Akarudi kitandani huku akisikitika sana…
“Da! Mlango bado umefungwa mama Shua…mumeo sijui amenikusudia nini mimi! Mwenyewe najuta sana na hii hali…unadhani nitaendelea kuwa mpangaji kwenye nyumba hii?”
“Uendelee, usiendelee mimi sijui Musa. Kwani sitakuwepo tena.”
Kulikucha kabisa, mlango bado ulifungwa kwa nje. Msichana wa kazi wa mama Shua alishaamka na kuendelea na kazi zake za kila siku huku akijua mama Shua yumo chumbani kwa Musa. Alijiuliza mengi moyoni.
Jua lilichomoza, mama Shua akapata wazo kwamba achukue simu ya Musa, ampigie baba Shua na kumwomba afungue mlango atoke, achukue mizigo yake na kuondoka kabisa lakini Musa akagoma kumpa simu yake…CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Noo mama Shua…siwezi kukupa simu yangu wakati najua yule ni adui yangu…siwezi. Kama anataka tufie humu ndani poa tu. Kama amepanga kuniua mimi sasa nitafanyaje?” alisema Musa akiwa amekasirika sana. Kwake, ilifika mahali ikawa liwalo na liwe.
Jua lilitoka kabisa, baba Shua alitoka chumbani na Shua, akaenda kuufungua mlango na kumwingiza Shua ndani…
“Nenda kwa mama yako.”
Mama Shua alishtuka sana kumwona mtoto wake akiingia na mlango ukiwa umefunguliwa. Alimkumbatia na kuanza kulia huku akisema…
“Mwanangu, nimekutenda vibaya sana. Utahangaika sana kwa sababu ya akili mbaya ya mimi mama yako.”
Shua hakujua lolote. Alibaki akimwangalia mama yake kwa macho ya mshangao…
“Mamaa,” aliita Shua, mama Shua akazidisha kilio kumsikia mtoto wake akimwita mama.
Shua aliachana na mama yake, akamfuata Musa…
“Chumba…”
Musa alikasirika sana, akatamani kumpiga. Shua alimwita Musa chumba kutokana na maneno yake siku za nyuma akimtania Shua kwa kumwita mchumba.
***
Baba Shua alikwenda kuoga, akavaa na kuondoka zake huku pesa za matumizi akiwa amemwachia msichana wa kazi.
***
Muda f’lani, mama Shua alisimama mlangoni akimlia taiming msichana wake wa kazi akipita…
“Dada,” alimwita alipopita…
“Abe…shikamoo dada…eti kwa nini upo huko?”
“Hayakuhusu…baba Shua ameondoka au yupo?”
“Ameondoka.”
“Kweli?”
“Kweli ameniaga, ameniachia pesa za matumizi.”
Mama Shua alirudi chumbani, akamchukua Shua na kutoka akiwa hana hamu tena na Musa.
Aliingia chumbani kwake. Kitu cha kwanza ni kuangalia simu yake, akaikuta. Akashangaa sana kwani aliamini jambo ambalo angelifanya baba Shua ni kuondoka na simu hiyo.
Aliipekua ndani na kubaini kwamba, haijachunguzwa kwani baadhi ya meseji zilikuwa za jana yake usiku na hazikusomwa.
“Mh! Sasa hapa dawa ni kumwomba radhi baba Shua. Mimi ni mkewe wa ndoa, binadamu hukosea, hiyo ni kawaida. Naamini atanisamehe tu. Nitamwambia sirudii tena, nimwahidi uaminifu,” alisema moyoni mama Shua.
Amwombeje samahani? Aliamua kumwandikia ujumbe wa simu badala ya kumpigia akiamini kwa kusoma atamwelewa vizuri zaidi kuliko kumwendea hewani. Kwanza anaweza asipokee hata hiyo simu yake. Aliandika:
“Baba Shua, najua kosa langu, nimekutenda vibaya sana mume wangu. Nakiri kosa moja kwa moja. Niko chini ya miguu yako mume wangu, nisamehe sanasana! Sitarudia tena, ni shetani tu alinipitia. Sasa nimejitambua ujinga wangu. Please mume wangu. Nisamehe saba mara sabini.” Akatuma.
Baba Shua hakujibu meseji hiyo. Ilifika mahali, mama Shua akaamini kuwa, mumewe alikuwa bize hivyo hajaona meseji yake, akaamua kubipu. Lakini licha ya kubipu, bado mumewe hakumpigia…
“Sijui kama nina ndoa tena! Ina maana baba Shua amebadilika kiasi hiki? Yaani ajue jambo zito kama la mimi kulala na mwanaume mwingine halafu aendelee na shughuli zake? Lazima kuna jambo baya sana anataka kunifanyia,” alisema moyoni mama Shua.
Siku hiyo aliamua asiende kazini. Aliamua kukaa nyumbani huku kazini kwake akiaga kwa uongo kwamba anasumbuliwa na kichwa.Kingine kilichokuwa kikimpa wakati mgumu mama Shua, aliamini kwamba mume wake atapeleka habari zake nyumbani kwao kijijini jambo ambalo anajua linaweza kusababisha kifo cha ghafla cha mama yake mzazi…
“Yaani afadhali haya mambo tuyaongee wenyewe, akisema anampigia simu mama kumwambia nimempoteza mama yangu. Lakini hivi mimi hii tabia nimerithi kutoka kwa nani? Kwa baba au mama?
“Mbona sijawahi kusikia hadithi yoyote inayosema mama alikuwa mhuni au baba alikuwa mhuni. Au wananificha? Au mimi nimeathiriwa na mazingira?” alijiuliza yote mama Shua.
***CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kule kazini, baba Shua muda mwingi alikuwa mwenye mawazo. Aliiona meseji ya mke wake, lakini hakutaka kumjibu. Na aliona alipobipu lakini pia hakutaka kumpigia.
Mara simu yake iliita, akaangalia skrini na kushtuka sana baada ya kuona jina la Maua.
Maua ni msichana aliyekuwa na uhusiano na baba Shua kabla ya kukutana na mama Shua.
Baba Shua alimpenda sana Maua kiasi kwamba, alikuwa tayari kwa ndoa naye lakini alipotokea mama Shua, alijikuta akitekwa na kumsahau Maua.
Uhusiano wao ulikufa polepole mpaka kila mmoja akajikuta akichukua hamsini zake. Baadaye, baba Shua akamuoa kwa ndoa mama Shua…
“Haloo,” baba Shua aliipokea simu ya Maua…
“Haloo…mzima wewe?”
“Mimi mzima. Sijui wewe?”
“Mimi pia mzima. Niko hapa kwenye mgahawa jirani na kazini kwako, nikasema nikupigie ili kama hutajali uje tushiriki kifungua kinywa cha pamoja.”
“Wapi? Hapo Bianca?”
“Ndiyo.”
“Nakuja Maua.”
“Karibu sana.”
Baba Shua alifunga mlango wa ofisi, akaenda Mgahawa wa Bianca na kukutana na Maua.
Ni Maua bila kujali kuachwa, alipomwona baba Shua alisimama, akamkumbatia na kumpiga mabusu mawili ya nguvu…
“Mmm…mwaa….mmmwaa.”
“Asante Maua…za siku nyingi?”
“Njema, sijui wewe?”
“Mi mzima sana Maua.”
“Nakuona umenawiri mpenzi…ni hiyo ndoa au nini?”
“Ah! Maua…nadhani ni wakati wa mwili wenyewe tu. Ndoa si sababu…”
“Kwa nini Benny?”
“Ah! Nimeingia chaka Maua.”
“Umeingia chaka! Kivipi Benny?”
“Maua…nimeoa malaya.”
“Ha..! Benny…unajua hilo neno ni zito sana…umeoa malaya?”
“Niamini mimi Maua…ngoja nikupe mkasa mzima,” alisema baba Shua na kuanza kumsimulia mkasa mzima Maua kuhusu mke wake, mama Shua.
Baba Shua alitumia kama nusu saa nzima kusimulia kisa cha mama Shua na Musa. Hata alipomaliza, alihema kwa kasi kubwa ya kusimulia…
“Lo! Asee! Kwa hiyo huyo kijana Musa ndiyo mwiba kwenye ndoa yako? Sasa umeamuaje?” aliuliza Maua.
“Maua, ungekuwa wewe ndiye umekumbana na kisanga hiki hata kwa jinsia yako ungeamuaje?”
“Ningeamua kusamehe.”
“Hapana! Ni ujinga wa hali ya juu. Haiwezekani.”
“Sasa wewe unataki kufanyaje?”
“Hakuna ndoa Maua. Mwanamke anakuletea mwanaume mpaka ndani, wewe upo. Unamsema lakini bado anaendelea tu!?”
“Niachie mimi, nitaamua,” alisema baba Shua uso wake ukionekana kuwa makini sana.
“Da! Pole sana Benny. Mambo mengine vipi lakini?” Maua aligeuza kibao cha mazungumzo…
“Poa sana. Sikutegemea kama leo utanipigia, nimefurahi sana.”
“Kweli? Hata mimi nimefurahi sana wewe kukubali mwaliko wangu. Maana bwana, mtu akishakuwa kwenye ndoa, hataki tena ahadi, hataki mtoko.”
Baba Shua alicheka, akamuuliza…
“Bado unaishi Temboni?” baba Shua alimuuliza Maua…
“Kulekule lakini nyumba kama ya tano toka pale nilipokuwa nikikaa zamani. Karibu sana Benny…”
“Nitakuja siku moja…”
“Lini nijiandae.”
“Ujiandae kwa kufanyaje? Umfukuze shemeji uliyenaye sasa hivi?”
“Ha! Wala! Mimi pale haingii mwanaume labda awe ndugu yangu.”
“Mbona mimi unaniruhusu nije kuingia?”
“Sasa wewe historia yako kwangu ni tofauti na wengine. Wewe ni kama mtalaka wangu. Kwa hiyo una nafasi yako ya pekee.”
“Basi nitakuja wikiendi hii,” alisema baba Shua…
“Mimi sitaki uje wikiendi hii…”
“Unataka lini?”
“Leo!”
“Mh! Mbona ghafla sana Maua?”
“He! Jamani! Kwani nyie wanaume mna ghafla?”
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Eee! Ratiba zikiingiliana ni ghafla tu.”
“Ina maana Benny huwezi kuua ratiba zako kwa mwaliko wangu mimi?”
“Kwani umenialika au umeniomba nije nikutembelee?”
“Haya, nakualika sasa. Leo naomba uje nyumbani kwangu.”
“Sawa, kuna siku nitakuja…”
“Mimi nataka uje leo bwana.”
“Mh! Maua bwana…nikisema ghafla ndiyo hupendi…oke, nitakuja leo.”
“Saa ngapi?”
“We unataka saa ngapi?”
“Mimi nataka ukitoka kazini nikufuate twende wote mguu kwa mkono.”
Baba Shua hakuwa na jinsi, alikubali…
“Basi nitakujulisha nikiwa natoka,” alisema.
“Sawasawa.”
Walipomaliza kupata chochote, walisimama wote, wakatoka huku Maua akiwa ametangulia mbele.
Baba Shua alishangaa sana kwa namna Maua alivyobadilika. Alikuwa akitembea kwa mwendo wa kujisikia, alinawiri, alinenepa kidogo na alitakata…
“Da! Huenda ningekuwa na Maua mambo yasingekuwa hivi yalivyo sasa na mama Shua. Halafu demu kapendeza ile mbaya, suruali imemkaa kama amezaliwa nayo,” alisema moyoni baba Shua huku mwili ukianza kumsisimka kwa kumfikiria Maua alivyo kwa siku zile na moyoni akawa anakumbuka zamani za mapenzi yao motomoto.
Nje, waliachana. Maua akaingia kwenye gari lake na kuendelea na safari zake lakini huku akimsisitiza baba Shua kumfuata baadaye, baba Shua alikubali akarudi kazini kwake huku akisema moyoni…
“Kumbe Maua ana gari! Aisee! Lakini huenda huyu Maua akanisaidia kunipunguzia stresi. Kama tutaishi kama zamani itakuwa poa sana. Naweza kuendelea na mama Shua kwa vile nimefunga naye ndoa lakini huyu Maua akawa ndiye chaguo langu.”
Kusema kweli kwa muda wa siku kadhaa nyuma za mshikemshike wake na mkewe mama Shua na Musa wake, siku hiyo baba Shua alijisikia ana amani sana baada ya kukutana na kipenzi chake Maua.
***
Kwa upande wake, Maua aliondoka naye barabarani akiwa na mawazo kibao kuhusu baba Shua…
“Naamini sasa Benny anajutia uamuzi wake wa kunimwaga mimi na kumchukua huyo malaya wake,” alisema moyoni Maua…akaendelea…
“Na safari hii nikimdaka, hachomoki, kweli kabisa.”
***
Saa kumi kamili ya alasiri, Maua alimpigia simu baba Shua…
“Mm…vipi Benny? Hujatoka tu?”
“Ndiyo natoka Maua.”
“Kwa hiyo?”
“Njoo basi twende.”
Maua alichoma mafuta mpaka ofisini kwa baba Shua, akamchukua kwenye gari lake mpaka nyumbani kwake.
Walishuka wote, wakatembea kwenda ndani huku Maua akiwatambulisha majirani kwa baba Shua…
“Jamani! Mama Kise, huyu anaitwa Benny…ni mchumba wangu. Alikuwa nje kwa masomo, sasa amerudi.”
“Oooo! Karibu sana,” majirani walimkaribisha baba Shua.
Kwa jinsi alivyo, mwonekano na mavazi, kweli baba Shua alionekana kufananafanana na mtu aliyetoka nje ya nchi.
Ndani, walifikia sebuleni. Maua alionekana mwenye furaha sana kwani walipofika tu sebuleni, alimbusu baba Shua kisha akampa denda la mbali sana, wakakaa…
“Karibu sana baby, hapa ndiyo kwangu…dada,” Maua alimkaribisha, akamuita msichana wa kazi…
“Abee dada…”
Msichana wa kazi alitokea kutoka uani…
“Msikilize mgeni anakunywa nini? Lakini acha tu, namjua huyu nitamhudumia mwenyewe,” alisema Maua akisimama na kwenda kwenye friji.
***
Ndani ya saa moja, Maua alimkaribisha baba Shua chumbani…
“Njoo upaone mahali anapolala ubavu wako,” alisema Maua.
Baba Shua akiwa ameshakunywa wine glasi mbili, hivyo amechangamka kidogo, alimfuata Maua kwa nyuma hadi chumbani…
“Da! Chumba kama cha waziri wa fedha,” alitania baba Shua, Maua akacheka.
Ni kweli kilikuwa chumba kizuri, kilichosheheni kila kinachohitajika kwa ajili ya chumba.
Kitanda cha kisasa kilichozibwa na godoro kubwa, kabati kubwa la nguo, redio yenye kutumia CD sita na kiyoyozi cha ndani kwa ndani, vyote hivyo vilikifanya chumba hicho kuvutia zaidi.
Baba Shua alifikia kujitupa na kunesanesa kidogo huku akimsifia Maua kwa kujitahidi kutengeneza maisha yake vizuri…
“Da! Umejitahidi sana baby wangu…hongera sana…”
“Asante sweet, lakini siku zile tukiwa bado wote uliweza kunipa njia ya namna ya kutumia fedha. Kwa hiyo kwa kutumia maelekezo yako nikawa nimejifunza jinsi ya kubana matumizi,” alisema Maua huku akiachia tabasamu laini na kumwangalia baba Shua.
Walizungumza mengi chumbani, mwishowe walijikuta wamejitupa wote kitandani. Walichezacheza wakiwa kwenye nguo, baadaye Maua alitoka kitandani na kwenda kufunga mlango kwa funguo…
“Kwarakacha…kwarakacha…kwacha!” Msichana wa kazi aligunia moyoni. Kwake lilikuwa tukio geni sana kumwona bosi wake akiingia chumbani kwake na mwanaume. Hajawahi kuona!Simu ya baba Shua iliita, akaitupia macho na kuona jina la mke wake, akaipuuza…
“Baby mbona hupokei simu?” Maua alimuuliza
“Ah! Si yule malaya anapiga…”
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ungepokea sasa…unajua anataka kukwambia nini?”
“Achana naye,” alisema baba Shua akianza kukunja sura.
Maua baada ya kauli hiyo, hakutaka kupoteza muda, akapanda kitandani na kuanza kumvua nguo baba Shua huku tayari akiwa na mihemko ya kimahabamahaba…
“Baby,” aliita Maua kwa sauti yenye kuashiria kubembeleza mwana…
“Niambie Maua…”
“Nikupe dawa ya kumwacha mke wako?” aliuliza Maua kwa sauti iliyotoka nje kwa kupitia tundu za pua…
“Kama ipi Maua?”
“We sema uko tayari au hauko tayari?”
“Niko tayari…kwa mambo anayonifanyia? Aisee niko tayari…hivi hapa ninavyojua mimi kwa sababu ameshatekwa na huyo Musa wake hataweza kurudi kwenye reli ninayoitaka mimi kama mume.”
“Da! Aisee pole sana. Basi mimi nitakupa…lakini nikwambie mapema, hiyo dawa si ya mitishamba wala vidonge vya hospitali.”
“Ni dawa gani sasa jamani Maua mpenzi wangu, hebu niambie kidogo basi…”
“Wala usiwe na wasiwasi Benny kwani wewe si unahisi mkeo anakusaliti?”
“Maua si kwamba nahisi, ni kweli ananisaliti. Nimekwambia anaingia chumbani kwa mpangaji mwenzangu nikiwa namwona kwa macho yangu halafu unasema nahisi, maana yake nini? Halafu yule kijana tangu anahamia pale siku ya kwanza nilimuazia vibaya kwamba atakuwa ananisaliti na mke wangu, sijui kwa nini niliwaza hivyo?!”
“Huenda ni akili yako ilijiongeza tu. Wapo watu wameumbwa hivyo. Wanajiongeza wenyewe hivyo huwa hawahitaji kuongezwa.”
“Oke, sawa…sasa niambie hiyo dawa ni ipi?”
“Nitakwambia, we tuendelee kuwa pamoja tu,” alisema Maua huku akimshika mikono baba Shua na kuanza kumnyooshanyoosha. Pia akahamia sehemu mbalimbali za mwili na kumkandakanda huku akimpongeza kwa maneno ya mahaba…
“Benny…”
“Niambie Maua…”
“Unajua namshangaa sana huyo mke wako…”
“Kwa nini? Japokuwa hata mimi mwenyewe namshangaa…”
“Yaani mwanaume mzuri kama wewe anakutenda hivi?! anajua thamani ya mwanaume kweli? Tatizo binadamu wengi wanapenda kupata lakini hawawezi kutumia…
“Utakuta watu wanapishana kwenye maofisi kutafuta kazi lakini wakishapata hawatendi. Mimi huwa naamini watu wengi wanatafuta ajira na siyo kazi…”
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Una maanisha nini Maua kwa huo mfano wako?” aliuliza baba Shua…
“Namaanisha kwamba, siku hizi wanawake wengi wanatafuta kuolewa lakini si ndoa…”
“Ha! Maua, kuolewa na ndoa si jambo moja mpenzi wangu?”
“Hapana Benny! Kuolewa ni mwanamke kumpata mwanaume wa kuishi naye akahesabiwa yeye ni mke wa fulani. Ndoa ni zile taratibu zilizopo. Yaani uvumilivu, uaminifu na tendo lenyewe.
“Sasa kama mke anaingia kwenye chumba cha mwanaume ndani ya nyumba moja hiyohiyo, huyo anaijua ndoa kweli? Si alitafuta kuolewa tu!”
Benny alimwelewa vizuri Maua kiasi kwamba alimkisi kama ishara kwamba, amemkubali. Maua naye akambusu Benny, kisha wakazama kwenye tukio lingine la denda! Kwa dakika kadhaa hakuna aliyekuwa akiongea.
Kila mmoja aliguswa na hisia za mapenzi yao miaka miwili nyuma ambapo walikuwa moto.
Kutokana na hali hiyo, walifika mahali kila mmoja alifanya anachotaka kwa vitendo bila kutoa sauti.
Mfano, Maua alipotaka Benny ageuke alimshika na kumgeuza, Benny akajua na kuendelea kujigeuza mwenyewe.
Benny naye alipotaka Maua alale chali, alimshika akaashiria kumlaza, Maua akalala mwenyewe huku akiyakaza macho kwa mwelekeo wa mwanaume huyo kama anayeuliza ‘kuna lingine?’
Hali iliendelea hadi wakafika mahali wakajikuta tayari wapo uwanjani na mechi imeanza.
Siku hiyo, Maua alitumia ufundi wake wote kuhakikisha anakidhi hitaji la mapenzi kwa Benny. Ilifika mahali hata Benny mwenyewe alishangaa kuona mambo makubwa kwa Maua. Akajiuliza amepatia wapi uzoefu huo?
Kingine alichokifanya Maua siku hiyo ni kwenda sambamba na Benny huku akiendelea kumsifia kwa mambo mbalimbali, akikumbushia hata madogo tu aliyoyafanya Benny zamani kuhusu yeye.
Ukichanganya na sauti aliyokuwa akiitumia sasa, weee! Benny namaanisha baba Shua, alisahau kabisa kama alifunga ndoa na sasa ana mtoto mmoja wa kike anaitwa Shua.
Kichwani alianza kumsahau ghafla mama Shua. Ile hali ya kuumia moyo kwa sababu ya usaliti wake ilianza kumtoka na kujiona kama kawaida. Akili yake ya wivu ilianza kuhamia kwa demu wake huyo…
“Maua,” aliita huku mikiki ya mpira ikiwa inaendelea…
“Abee…”
“Unajua nikija kukuona na mwingine nitakasirika..?”
“Ukiniona na mwingine au na mwanaume mwingine? Maana unaweza kuniona nikiwa na shoga yangu Hadija, pia utakasirika sweet?” aliuliza Maua.
Hapo ni baada ya mechi yao kufika mwisho na sasa walikuwa wamepumzika huku wakihema kwa kasi ya shughuli pevu…CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment