IMEANDIKWA NA : IRENE MWAMFUPE
*********************************************************************************
Sehemu Ya Kwanza (1)
Wakati akijiandaa kusema alichokuwa amekusudia, ghafla Jagadi alitokeza na kuwatazama wote wawili kwa jicho la ‘duh mara hii mmeshakuwa na ukaribu huo’.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
TEREZA NAYO SASA…
WOTE walishtuka. Vivian akamtazama Bigambo usoni kisha akayarudisha kwa Jagadi aliyekuwa bado anawatazama kwa zamu. Lakini hakuacha kutoa tabasamu. Alichofanya Bigambo ni kuendelea na ratiba zingine. Akawa anakagua chupa za asali kabla ya kikao cha kujadili ubora wa asali ya siku hiyo.
“Huyu mbona ametuangalia sana?” Vivian alimuuliza Bigambo huku akiachia tabasamu lake lenye kusahaulisha kabisa adha za foleni za asubuhi.
“Sijui, labda ana mambo yake,” Bigambo alijibu lakini moyoni aliujua ukweli kwa nini Jagadi aliwatazama kwa jicho lile.
“Watu wana mambo ya Kiswahiliswahili, huwezi kuwatazama watu kwa jicho la hivyo,”Vivian alisema na kuendelea na zoezi lake la kutazama asali huku mazungumzo yakiendelea.
Muda wa kikao uliwadia na watu wote walijumuika pamoja kwenye meza kubwa na ya kisasa kabisa, tayari kwa kujadili bidhaa ya siku hiyo. Mwenyekiti wa siku hiyo aliitisha kikao na wajumbe wakawa tayari. Vivian na Bigambo walikaa pamoja, lakini macho ya wajumbe wengi wakiwa wanaume hayakubanduka kwa wawili hao.
Kikao kiliendeshwa haraka na shughuli zingine zikaendelea. “utanitafuta baadaye tukutane kwa ajili ya kuzungumza,” Vivian alimwambia Bigambo ambaye hadi wakati huo walikuwa wamekolea kwenye urafiki mkubwa.
“Poapoa, nitakutafuta,” Bigambo alijibu haraka kisha kuendelea na majukumu yake, ambapo Vivian naye alitoka na kwenda kwenye mizunguko yake ya kusaka matangazo kwenye makampuni mbalimbali mjini.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Siku nzima Bigambo alishinda na furaha isiyoelezeka. Uzuri wa Vivian ulikuwa umetikisa kabisa ukuta wa ubongo wake, moyoni alitamani jioni ifike mapema ili awasiliane na Vivian kabla ya kukutana na kufanya naye mazungumzo ya kuupendezesha moyo.
Kazi zilifanyika. Hatimaye jioni ikawadia na Bigambo alimpigia simu Vivian ili kujua mahali alipokuwa.
“Ndiyo nimefika hapa River- Side, wewe uko kwa wapi?” Vivian alimuuliza Bigambo na kusikilizia jibu lake ili aone kama ataweza kumsubiri au atachelewa.
“Ndiyo najiandaa kutoka ofisini, lakini sitachelewa sana mama,” Bigambo alisema na kunyanyuka kitini kwake kwa ajili ya kujiandaa kuondoka.
“Mbona bado uko mbali sana na mimi nataka niwahi nikapike au tuonane kesho basi,” Vivian alijibu ingawa hakuwa na msimamo sana juu ya pendekezo lake la kuonana siku inayofuata.
“Hapana V, nafika sasa hivi mama kwani nitachukua bodaboda ili nikuwahi, sawa?” Bigambo alikoleza wakati akishuka ngazi za ofisini kuelekea chini tayari kwa kuchukua usafiri ili amuwahi Vivian.
“Basi jitahidi si unaona muda nao umesonga na hivi nilivyochoka na mizunguko ya leo ndiyo basi kabisa,” alichagiza Vivian kisha kukata simu.
Bigambo alitembea haraka hadi kuwafikia watu wa bodaboda na kuelewana na mmoja wao ampeleke River- Side. Dakika ishirini baadaye Bigambo alikuwa ameshafika River-Side.
Uko upande gani?” Bigambo aliuliza baada ya Vivian kupokea simu.
“Nimesimama kwenye hii stendi ya magari ya kwenda Makoka, hapa mwanzoni karibu na bucha, ukisogea utaniona nimesimama karibu kabisa na vijana wa bodaboda,” Vivian alisema.
“Okey, sikiliza…”
“Ndiyo.”
“Rudi nyuma kidogo.”
“Halafu.”
“Mkono wako wa kulia kuna baa moja inaitwa kwa Mama John, karibu tu na mahali uliposimama, utanikuta hapa.”
“Sawa,” Vivian alijibu na kuanza kurudi nyuma kama alivyoelekezwa na Bigambo.
Muda mfupi baada ya maelekezo hayo, Bigambo na Vivian walikuwa wamekaa meza moja wakitazamana kwa nyuso za furaha na uhuru wa nafsi.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nimechelewa?” Bigambo aliuliza japo moyoni aliamini kabisa kwamba swali lake halikuwa dhahiri kwani alitumia muda mfupi sana kutoka ofisini Sinza-Kumekucha hadi hapo River-Side.
“Wala,” Vivian alijibu kwa sauti ya chini na aibu za kikekike zikiutawala uso wake.
“Jamani karibuni,” ilikuwa ni sauti ya mhudumu akiwasikiliza kwa kinywaji.
“Mimi nipe Dompo na huyu nadhani Savanna au mama?” Bigambo aliagiza kwa mbwembwe kwani siku hiyo alikuwa vizuri mfukoni kutokana na posho ambayo huwa wanapewa kila wiki kazini kwao, alikuwa nayo, pia jioni ya siku hiyo alikutana na mkurugenzi mlangoni wakati anaingia ofisini na kupewa zaidi ya shilingi elfu 40 ikiwa ni pongezi kwa kufanya kazi nzuri sana jana yake.
“Sawa,” Vivian aliinama kuashiria kabisa kwamba Bigambo alikuwa ameotea aina ya kinywaji akipendacho.
Mhudumu aliondoka kufuata vinywaji.
“Bigambo bwana,” Vivian alisema bila kumalizia sentensi yake.
“Vipi tena Vivian?”
“Wewe mtundu sana jamani.”
“Kawaida mama.”
“Nikuulize kitu?”
“Uliza tu Vivian, sidhani kama kuna swali utauliza halafu nisiwe na majibu yake.
“Umejuaje kama napenda kunywa Savanna?”
“Nimeotea tu jamani, nimekosea?”
“Hapana, basi tu nimependa,” Vivian alisema na kuachia kicheko cha kukenua meno bila kutoa sauti.
Vinywaji vililetwa na kuwekwa mezani. Wateja wa jirani wakawa wanaitazama Dompo ya Bigambo kwa kuisindikiza kwa macho kabla haijatua mezani kwa wahusika.
“Karibuni jamani,” mhudumu aliwakaribisha kwa bashasha kubwa huku akifuta meza kwa uchangamfu mkubwa.
Vinywaji vilianza kunywewa na hadi wakati huo si Bigambo wala Vivian aliyefungua mdomo kumwambia mwenzake kwamba anamhitaji.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ila Bigambo wewe ni mwanaume wa tofauti sana,” Vivian alianzisha mazungumzo, tayari akiwa na Savanna tatu kichwani huku Bigambo akiwa ameshabugia glasi zaidi ya nne za kinywaji chake. Wote walishaanza kuchangamka kwa vileo.
“Kwa nini Vivian?”
“Mchangamfu na mtu unayejali sana,” Vivian alisema huku akimpa Bigambo mkono wa shukrani lakini kutokana na umbali uliokuwepo mkono ulipelea na kutaka kuanguka kutokana na kuegemea sana wakati wa kutoa mkono huo.
“Ooh, pole sana Vivian,” Bigambo alisema.
“Asante.”
“Sogea huku,” Bigambo alisema huku akiweka kiti kingine karibu kabisa na mahali alipokuwa amekaa na kumtaka Vivian akaribiane naye ili waweze kuongea kwa uhuru zaidi. Hilo halikuwa na kipingamizi na Vivian alilitii mara moja ambapo sasa walikaa kwa ukaribu mkubwa ambao ilikuwa rahisi kwa kugusana kwa wakati wowote na mahali popote.
“Unajua Vivian,” Bigambo alisema huku akipekea mkono wake wa kulia kwenye mapaja ya Vivian akitegemea pengine atakutana na upinzani mkubwa lakini hali haikuwa hivyo na badala yake Vivian alitulia kama anayesikilizia jambo.
Bigambo kuona hivyo, akazidisha mbwembwe ambapo sasa alianza kuutembeza mkono kwenye mapaja ya Vivian kwa mikogo na mtindo wa kutekenya, hali ambayo ilimfanya Vivian kufumbafumba macho na kuweweseka kwa uwazi kabisa huku naye akijisogeza zaidi kwa Bigambo. Vivian hakukomea hapo, naye alianza utundu wa kiaina kwa kumshika Bigambo maeneo ambayo yalimfanya adate.
Vinywaji viliendelea kunyweka. Bigambo alikuwa akikaribia kuimaliza Dompo na tayari kichwani walishaanza kuwa wawili.
“Vivian,” aliita Bigambo huku akimtazama usoni.
“Bee…”
“Nataka nikueleze ukweli kabisa kutoka moyoni.”
“Sema tu B.”
“Nataka tuingie ndani tukazungumze kwa uhuru maana macho ya watu.” Bigambo alisema na kushindwa kufunguka kwa uwazi.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Jamani Bigambo huko ndani si ndiyo tutazaa na mengine?”
“Mengine kama yapi jamani?”
“Aaah, unajua bwana.”
“Hapana, hatuwezi kufanya chochote kwa leo zaidi ya kuwa na uhuru tu,” Bigambo alisema huku akizungusha mkono wake kiunoni kwa Vivian ambapo alijikuta akigusa vitu vigumu viamshavyo hisia za ndani kabisa za mwanaume yeyote rijali.
“Sa…saaawa Bigambo lakini tusifanye looo….loteee,” Vivian aliitikia kwa maneno ya kukatakata kwa maana ya kuzidiwa na vitu viwili ambavyo ni Savanna na kule kushikwa kiunoni na Bigambo.
Walinyanyuka na kuingia ndani ya baa hiyo ambapo kwa upande wa kushoto kulikuwa na gesti.
Walichukua chumba kimoja na kuzama ndani ambapo si Vivian wala Bigambo aliyekuwa na uwezo wa kujizuia kwa lolote.
“Bigambo,” Vivian aliita na kujiegemeza zaidi kifuani kwa Bigambo huku akihema kwa pupa ikiwa ni pamoja na kuendeleza utundu wake mwilini kwa Bigambo muda mfupi tu baada ya kuketi kitandani.
Kuona hivyo, Bigambo alijiweka sawa na kumgeukia Vivian. Akanyoosha mikono na kuyaparamia maembe mawili na kufanya kama anayabonyeza ili kuona kama yameiva na yanafaa kuliwa.
Vivian aliruka na kutoa kilio kilichomfanya Bigambo aangue kicheko cha nguvu.
Acha mambo yako bwana, ngoja niondoke,” Vivian alisema huku akikanyaga mguu kwenye kigingi cha kukanyagia kabla ya kukaa vyema kwenye kiti cha pikipiki, ambapo yule kijana hakuwa na muda wa kupoteza zaidi ya kutia gia na kuondoka kwa kasi na kumuacha Bigambo akikodoa macho huku akicheka na kujisifia moyoni kwa namna ambavyo ameweza kumpata Vivian kwa urahisi na wepesi wa namna hiyo. Kwa upande wa Vivian, kichwani alikuwa na maswali mengi ambayo hayakuwa na majibu kwa wakati huo. “Hivi kweli mimi Vivian nimekuwa mtu wa kupatikana kwa mwanaume kirahisi namna hii? Ama kweli Bigambo ni kiboko lakini hata hivyo amesaidiwa sana na utundu wake pamoja na ile hali ya kunijali, maana nina siku nyingi sana sijaoneshwa upendo wa namna hii kwenye mapenzi, Bigambo ananifaa sana kwenye maisha yangu ya ndoa, tena ni mtu mwelewa kwa mambo mengi ya kimaisha,” Vivian alikuwa akiwaza kabla ya kufika nyumbani kwake ambpo alikuta mtu amesimama wima akimngoja kwa hamu na shauku kubwa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
VIVIAN alishtuka sana, kitendo cha kuona mtu amesimama wima mlangoni mwake, kilimgutua kutokana na ukweli kwamba hakutarajia kabisa, licha ya kwamba hadi wakati huo hakuwa amejua ni nani alikuwa amesimama mlangoni kwake. “Aaah, jamani umenishtua sana sasa mbona hujaniambia kama unakuja au simu yangu huna?” Vivian alisikika akimlalamikia mtu huyo baada ya kujua ni nani. Jamaa aliyekuwa amesimama mlangoni kwa Vivian alikuwa mzazi mwenzake na mwanamke huyo, ambaye uhusiano wao ulishaanza kuyumba ingawa ana haki zote za kuja nyumbani kwa Vivian wakati wowote kwa lengo la kumjulia hali mtoto ingawa wakati mwingi huwa yuko shule.
“Kwani jamani kila nikija hapa ni lazima nitoe taarifa au kuna mabadiliko mapya tena kwenye mji huu, halafu muda kama huu unatoka wapi Mama Edson au unataka kutumia mwanya wa kutofautiana kwetu kama njia ya kujipatia uhuru uliopitiliza, haiwezekani nakuambia,” mwanaume huyo alianza kutiririka maneno mengi tena bila kuzingatia vituo na koma kama siyo nukta. “Hivi Raphael, tangu lini tukaanza kuwekeana masharti nyumbani kwangu? Wewe si una kanuni ya kuja hapa Jumamosi na kuondoka Jumapili ili upate nafasi ya kuzungumza na mwanao, sasa leo kimekuleta nini? Yaani unataka nikose hata uhuru wa kazi zangu za kiofisi kwa sababu ya kukuwahi wewe ambaye sina mkataba na wewe zaidi ya kuja hapa kumjulia hali mwanao?”
Kwanza nataka tuanze utaratibu mpya wa kumsalimia Edson, kwani kwa mtindo huu hapana kabisa jamani, aaah,” Vivian naye alijibu kwa maneno mengi na sentensi ndefu zenye kuchosha kusikiliza. “Utaratibu gani unaotaka uanzishe kuhusu mimi kumjulia hali mwanangu?”
“Uwe unakuja na kuondoka, masuala ya kulala hapa wakati mimi na wewe siyo mke na mume sitaki tena kwa kweli,” Vivian alikazia tena huku akiwa amesimama wima karibu kabisa na mwanaume huyo ambye jina lake ni Raphael kama alivyomtaja. “Unasemaje wewe nyang’au?” “Unaniitaje Raphael?” “Wewe nyang’au tu, tena usinipandishie nisije nikakubadilikia sasa hivi nikakuwasha makofi bure, umenielewa?” “Babu wee, achana na mimi bwana, mwanaume gani usiulizwe, yaani kuniijia usiku nyumbani kwangu tena bila taarifa wakati namba yangu ya simu unayo halafu unataka usiulizwe, ulishawahi kutoa hata senti tano yako kwenye kulipia kodi ya hii nyumba? Tena angalia kabisa usije ukanitibua usiku huu,” Vivian alisema huku akipiga hatua kuingia ndani akimuacha Raphael peke yake nje ya mlango. Wakati Vivian akiingia ndani, ghafla simu yake iliita na alipotupa macho kwenye kioo, aliona jina la Bigambo wangu, bila kujiuliza mara mbilimbili alipokea na kupeleka sikioni tena kwa sauti ya kudeka kulikopitiliza.
“Yes, baby wangu jamaniiii,” Vivian alianza kwa maneno hayo huku akizidisha kuibana sauti yake isitoke kwa ufasaha kwenye mdomo na badala yake ibanane kwenye zile tundu mbili za pua. “Niambie mama.” “Nipo baby wangu, niambie unafanya nini kwa sasa?” “Niko tu nyumbani Vivian, wewe umeshafika,” Bigambo aliuliza akiwa amekaa ndani kitandani kwake, muda mfupi baada ya kutoka bafuni kujiweka sawa kwa uchovu wa mechi kali aliyotoka kupiga na Vivian. “Ndiyo naingia sasa hivi lakini kuna mtu ameniudhi sana baba yangu.”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nani tena huyo jamani mama?” “Aaah nitakuambia wangu, kuna watu duniani wakiingia maishani mwako huwa ni kama laana na kuna wengine wakiungana na wewe maishani mwako kama ulivyofanya kwangu baba huwa ni baraka kubwa, sasa huyu aliyenikera sasa hivi ni wale watu wa kundi la kwanza nililokueleza,” alisema Vivian wakati wote huo Raphael akiwa nje akisikiliza kila kitu kilichokuwa kinazungumzwa na Vivian na Bigambo, kwani simu ya Vivian ilikuwa na sauti kubwa hata kama haijawekwa mfumo wa sauti ya nje (loud speaker). Haisra zilizidi kumpanda Raphael. Ni kweli kabisa hana uhusiano wa ndoa na Vivian baada ya kuachana kwa tofauti za kibinadamu na kukubaliana kulea mtoto wakiwa mbalimbali na kisha baadaye kuzaa suala la kulala pamoja baada ya siku moja kunywa pombe na kupitiliza ambapo waliamua kukumbushia penzi lao na kuanzia siku hiyo walianza tabia ya kulala pamoja kila Raphael alipokwenda kumjulia hali mwanaye.
“Unajua nitaonekana mwanaume mjinga sana kama nitatoka hapa bila kumuwasha japo vibao viwili huyu mwanamke, hata kama siishi naye lakini heshima ya kwamba nimezaa naye inabaki palepale na anapaswa kuniheshimu na siyo kunioneshea dharau za wazi namna hii kwa kuzungumza na wanaume kwenye simu ilhali anajua kabisa mimi nipo hapa,” aliwaza Raphael huku akijiandaa kuingia ndani. * * * Wakati Vivian akizungumza na simu, alifunga mlango kwa komeo wakati Raphael akiwa amezama kwenye lindi la mawazo mengi, hivyo hakushtukia wala kujua ni saa ngapi Vivian alifunga mlango wa kuingilia ndani ya nyumba hiyo yenye chumba kimoja na sebule ukichilia mbali chumba cha nje ambacho kiko maalum kwa ajili ya wageni. “Sasa baby, unaonaje kama nitapika kwanza ndipo tuongee baadaye nikiwa kitandani mume wangu?” Vivian alisema akimwambia Bigambo kupitia simu, katika kumalizia mazungumzo yao ya wakati huo. “Sawa mama na mimi ngoja nikaangalie chakula huko nje ndipo nije nilale.”
“Jamani baby, hivi huwa haupiki?” “Sipiki na sina mpango huo.” “Ndiyo maana hunenepi mume wangu, sasa hivi nimeingia maishani mwako nitahakikisha unanunua vyombo kama huna ili niwe nakuja kukupikia mwanaume wangu, sawa baba?” “Mmmh…,” Bigambo aliishia kuguna. “Unaguna nini?” “Si maneno yako jamani.” “Yamefanyaje?” “Hayo ya kunipikia, hakika nitanenepeana sana.” “Sana, huo mwili siyo
wako.” “Sawa, tutaona mama.” “Okey, baadaye basi baba, nitakutafuta nikiivisha.” “Sawa mke wangu,” Bigambo alimalizia na maneno hayo bila kujua kwamba anampa wakati mgumu sana Vivian ambaye alikuwa amempenda kupitiliza kutokana na mavituz kama siyo majambozi ambayo alikuwa amemuonesha muda mfupi uliopita, kwa hiyo hata ile jeuri ya kumjibu maneno makali Raphael ilitokana na kuvimbishwa kichwa na penzi tamu la Bigambo. Raphael alihamaki baada ya kuusukuma mlango na kugundua kwamba umeshafungwa kwa ndani, ni hapo ndipo hasira yake ikazidi kupanda maradufu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Wewe Vivian wewe, hivi unawezaje kunifungia nje wakati unajua kabisa niko hapa kwa ajili yako?” Raphael alianza kulalama tena huku akiutingisha mlango kama anayetaka kujiridhisha kama kweli Vivian alikuwa amemfungia kwa nje. “Bab wee, umekuja kwa ajili yangu au kwa ajili ya mwanao na unajua kabisa kwamba siku kama hizi anakuwa yuko shule, mwenzangu labda ulikuwa na safari zako ndiyo maana ukaamua kunishtukiza kuja kwangu bila kunitaarifu, halafu nakuuliza na badala ya kujibu kistaarabu eti unaanza kunipandishia maneno ya jeuri ya kimfumo dume, sasa wewe si ulianza, mimi namalizia ukurasa,” Vivian alisema huku akitweta na kuhema. Raphael alirudi nyuma na kuukanyaga mlango kwa nguvu huku akitamka maneno ambayo yaliwafanya hata majirani washtuke na kuamka kabisa ili kuja kutuliza soo la varangati ambalo alikuwa amelianzisha Raphael nyumbani kwa Vivian
WATU walijaa, wakiwemo majirani na wengine wapita njia ambao walivutiwa na varangati la Raphael nyumbani kwa Vivian. “Jamani kuna nini tena hapa?” ilikuwa ni sauti ya mjumbe wa nyumba kumi, ambaye kiumri alikuwa mzee wa makamu lakini mwenye kuogopeka sana mtaani kutokana na utemi wake kwani alikuwa ni mstaafu wa jeshi mojawapo la ulinzi na usalama hapa nchini.
“Mzee wangu mimi hunijui eti,” Raphael alidakia huku akiachana na mlango na kumsogelea mjumbe, ambaye alikuwa amejiandaa kwa lolote lakini lengo kubwa likiwa ni kuamua kesi na makelele yale. Kabla mjumbe hajajibu chochote, Vivian alitoka ndani akiwa amefura kama mbogo jike aliyeibiwa watoto mwituni.
Hakutaka kuuliza chochote, mkononi alikuwa na mwiko ambapo aliuinua na kumpiga nao kichwani Raphael, ambaye aliudaka na katika kunyang’anyana huku damu nyingi zikimchuruzika, wote wawili walijikuta wakipelekana hadi chini na kuanguka kama mzigo wa viazi vitamu. “Mshenzi kabisa wewe, niacheni nimuoneshe adabu mbwa koko huyu anayelazimisha mapenzi ki-nguvu,” Vivian sasa alikuwa amechanganyikiwa na kwa wakati huo alikuwa amedhamiria kuzua ugomvi wa aina yake na alikuwa tayari kwa lolote hata kama ikiwa ni kulala polisi.
“Jamani mbona mnatiana aibu hapa?” mjumbe alisema huku akitumia nguvu zake zote kuwaachanisha Raphael na Vivian. Wakati Vivian na Raphael wameangushana chini, Vivian alitumia mwanya huo kupenyeza kisawasawa mkono wake wa kushoto na kulishika shina la makao makuu ya mkuu wa kaya wa Raphael na kuanza kuyakamua vilivyo, kitendo kilichomfanya Raphael kunyoosha mikono juu akiomba yaishe na kwamba hatarudia tena kufanya chochote. “Nasema achaneni vinginevyo nitatumia nguvu na mamlaka yangu kuingilia ugomvi huu na mnajua hatutamaliza salama,” alisema mjumbe na kwa sauti hiyo wote wawili waliachiana huku Raphael akiendelea kuvuja damu nyingi kichwani na mwili ukiwa umegwaya kutokana na aina ya mkabo aliofanyiwa na Vivian.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mjumbe, huyu mwanaume ana matendo mabaya sana na mimi simtaki kuzaa naye isiwe tabu, ni kweli nyote mnajua kabisa kwamba kila mara huwa mnamuona anakuja hapa na kuondoka, yote hayo ni kwa sababu ya mtoto wake ambaye huwa anakuja kila Jumamosi na kuondoka Jumapili, sasa hivi sitaki awe anakuja kwangu na kulala,” alisema Vivian huku akihema kwa nguvu kabla ya kuendelea…
“Leo amekuja bila kunitaarifu, nimekuta amesimama hapa utafikiri mwizi na nilipomuuliza kulikoni aje bila kunitaarifu kupitia simu yangu eti hilo ndilo kosa langu na sasa hivi ameharibu mlango wangu, mimi sitaki kabisa na leo sijui itakuwaje, anitengenezee mlango wangu ndipo aondoke na kuanzia leo sitaki kumuona nyumbani kwangu, kama ni mtoto nitalea mwenyewe,” alisema Vivian na kumtazama mjumbe kama anayesema; “sijui unasemaje mjumbe kwa hilo.”
“Jamani, mimi sitaki kabisa ugomvi na huyu mwanamke, niko tayari kutengeneza mlango na nitakuwa nakuja kumsalimia mwanangu kila Jumapili na kuondoka,” alisema Raphael huku akiingiza mkono mfuko wa nyuma ambapo alichomoa noti nyekundu kama kumi na kumkabidhi Vivian ambaye alianza kulegeza na tabasamu likaonekana kwa mbali.
“Sawa, hata mimi sina shida na chochote lakini mzazi mwenzangu amenikosea na mimi sijawahi kumkosea heshima kabisa na hata yeye ni leo tu lakini kama alivyosema kwamba yaishe basi na yaishe kweli na mimi anisamehe kama kuna mahali nimemkosea na kumvunjia heshima,” alisema Vivian na kuwashangaza watu waliokuwepo kweye tukio hilo kutokana na kubadilika ghafla kwa msimamo wake, kwani mwanzoni alionekana kutokuwa na masihara hata kidogo, lakini baada ya kupewa kiasi kikubwa cha pesa na mzazi mwenzake, alibadilika ghafla sana na kuonesha furaha na huruma ambazo zilikuwa zimemezwa na harufu za noti!
“Sawa, kama mmeamua kumaliza wenyewe aibu hii mimi nadhani hakuna shida ingawa mngeweza kukaa wenyewe na kuelewana kuliko kama hivi mmejaza watu na kuwapa faida ambayo haikuwa na maana yoyote,” alisema mjumbe na kumalizia kwa msonyo huku akijiandaa kuondoka lakini Raphael akawahi kutupia neno la mwisho.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Basi mjumbe utusamehe sana kwa haya yote na usumbufu, kuna wakati binadamu tunapitiwa kwa makosa mengi sana kama hivi, tusamehe wanao, nimejifunza mambo mengi kwa muda mfupi huu lakini kubwa ni kuwa na uwezo wa kujizuia na kukubaliana na matokeo halisi, kama hivi mimi nalazimisha mapenzi,” alisema Raphael. “Haina shida, mimi naondoka bwana nyie malizieni hayo mengine, sasa wewe Vivian utapata wapi fundi wa mlango sasa hivi,” mjumbe aliuliza huku akijiandaa kuanza kupiga hatua kuondoka.
“Kuna kijana mmoja yuko pale nyuma naona wameenda kumuita naamini ataw
eza kurekebisha maana ni komeo tu ndilo limelegea na kung’oka misumari miwili ya kulishikia,” alijibu Vivian huku akimtazama Raphael. Raphael aliingiza tena mkono mfukoni na kutoa noti nne nyekundu na kumkabidhi mjumbe huku akiendelea kumuomba msamaha tena mjumbe kwa usumbufu mkubwa na kujaza watu mtaani kwake. “Oooh, asante sana mwanangu kwa hapa sasa hakuna shida, sasa wewe si utakwenda kutibiwa kidogo au unasemaje?” mjumbe naye alichangamka sana baada ya kushikishwa wekundu wanne na Raphael, meno yote yakawa nje huku bashasha zikiongezeka kwa sana.
“Ndiyo, ngoja niende pale pharmacy nikawekewe bandeji maana sijaumia ni kijeraha kidogo tu cha kupigwa na mwiko, lakini sijaumia sana,” alisema Raphael huku akijikung’uta suruali yake kwa vumbi alilogalagazwa na Vivian. “Ni vizuri kama tutabadilishana mawasiliano maana hakuna ubaya kwa kujuliana hali,” mjumbe ambaye ukiondoa ubabe na umahiri wake mtaani hapo, sifa nyingine aliyotambuliwa na wakazi wa eneo hilo ni upigaji wa masanga, yaani unywaji wa pombe kupitiliza ingawa hakuwa mtu wa fujo akiwa ameweka mambo hayo kichwani zaidi ya kuwa mtu wa utani na maneno mengi yenye elimu ndani yake, aliendelea kushadadia na kujiweka kwa ukaribu zaidi na Raphael kwa lengo la kujihakikishia ulaji kwa nyakati zijazo. “Haina shida mzee, chukua namba yangu,” alisema Raphael na kumtajia mjumbe namba zake
za simu kabla ya kuondoka na kuwaacha watu wa eneo hilo wakijadili mambo mbalimbali kuhusiana na tukio lake na Vivian. Watu walitawanyika, sasa Vivian alibaki na fundi wa mlango ambaye alikuwa akiukagua mlango wote ili ajue pa kuanzia. “Sasa fundi itakuwa ni kiasi gani jamani?” Vivian alimuuliza huku akimtazama kwa umakini kijana huyo. Ni kweli aliwahi kumuona lakini hakuwahi kuzungumza naye na kuna siku fundi huyo aliwahi kukutana na Vivian uchochoroni na kumsalimia lakini Vivian hakuitikia licha ya salamu hiyo kutolewa kwa sauti ya juu kabisa na fundi. “Hapana, hebu ngoja kwanza nitengeneze ndipo nikuambie ni kiasi gani maana kwa sasa naweza kusema kumbe nikawa nimekupiga sana au umenipiga, kazi ikikamilika nitapima na kisha kukupa bei yangu, lakini naamini kabisa haitakuwa kubwa. “Sawa, ngoja nichukue bia moja au mbili hapo jirani nijipoze kidogo maana kwa varangati hili dah,” alisema Vivian huku akimtazama fundi. “Kwani kimetokea nini anti, maana sikuwepo nyumbani na nimerudi muda huu na kusimuliwa kwa juujuu tu,” fundi aliuliza. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/“Wewe acha tu, nyie wanaume mna maana nyie basi,” alisema Vivian. “Sasa ukisema hivyo utakuwa umekosea.” “Basi nitakuja kukusimulia nikirudi, wewe unakunywa bia gani nikuletee japo mbili za kutuliza koo lako?” “Mimi anti huwa sinywi bia zaidi ya Nyagi tu,” fundi huyo ambaye jina lake halisi aliitwa Jisu alisema huku akimtazama Vivian kwa macho ya kudadisi atasema nini. “Mmmh, basi sawa ngoja nikakuletee kubwa moja kabisa ili uburudike vya kutosha, unachanganya na soda au maji?” “Vyovyote hata kavu huwa napiga,” alisema Jisu na kumfanya Vivian acheke na kuondoka kwenda kwenye grosari.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment