Chombezo : Nampenda Adui Yangu
Sehemu Ya Tano (5)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ilipoishia…..
Wakati mtu huyo damu zikiendelea kumtoka alingia mwingijne na kuendeleza kupigana.Kenny aliendelea kujipanga sawasawa na kukwepa mateke na ngumi vilivyo rushwa na adui yake huyo.Dakika tano baadaye mtu huyo wa pili naye alianza kuumizwa jambo hilo liliwapa hofu wenzie ambao waliamua kutumia njia nyingine.Wakati Kenny akiendelea kupigana na mtu huyo aliyetambua alikuwa ni kijana wa Mr.Carlos Mato alishtushwa akipigwa kichwani na kitu kizito.Alianguka chini na baada ya muda mfupi alipoteza fahamu.
Endelea…
Watu hao walikuwa ni vijana wa Mr.Carlos ambao walifanya doria kwa siku kadhaa shuleni hapo wakimtafuta.Baada ya kupigana na Kenny kwa muda mfupi na kuona wakizidiwa walikonyezana na mmoja wao alimpiga Kenny na kitako cha bunduki waliyokuwa nayo kichwani.
Walimpakia Kenny kwenye moja ya gari zao mbili aina ya Mercedez Benz walizokuwa nazo katika moja ya buti ya gari hizo.Waliwasha gari zao na kuondoka kwa kasi kuelekea maeneo ya Mikocheni katika makutano yao ya kazi ya ujambazi.Mmoja wao alimpigia simu Mr.Carlos akimweleza juu ya kukamatwa kwa Kenny John Mushi jambo ambalo Mr.Carlos alionesha furaha.Aliahidi kufika katika nyumba yake hiyo ya Mikocheni ihusikayo na vikao vya ujambazi na dawa za kulevya.Baada ya muda kidogo gari hizo Mercedez Benz zilikuwa zikingia katika geti la nyumba hiyo ya Mikocheni ya Mr.Carlos Mato.Mara baada ya kuingia walimshusha Kenny ambaye alikuwa bado amepoteza fahamu na kuanza kumburuza kuelekea katika eneo la chini la nyumba hiyo ya ghorofa.Walimburuza Kenny mpaka kwenye chumba kimoja kilicho kuwa kidogo ndani ya nyumba hiyo, watu walikuwa wengi wakiwa na pilikapilika tofauti. Walimkalisha Kenny kwenye kiti na kumfunga na kamba akiwa amepoteza fahamu hivyohivyo.
Wakati huo walimsubiri Mr.Carlos afike ambaye robo saa baadaye aliwasili na gari lake kwa kasi.Alishuka haraka na kuanza kukimbia kuelekea sehemu ya chini ya nyumba hiyo.Mkononi alikua ameshika bastola yake “Yuko wapi huyo kenge nimmalize mwenyewe ehh!…..”aliuliza Mr.Carlos akionesha hamu ya kumuona Kenny.Aliongozwa mpaka chumba ambacho Kenny alifungwa akiwa amezimia “ehh!huyu ni mwenyewe anafanana kabisa na baba yake niliyemfanyia kitambo….”Aliongea Mr.Carlos akikishika kichwa cha Kenny na kukigeuza kila upande.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Aliagiza walete maji ya baridi ili wamumwagie lengo lake lilikiwa alitaka azinduke.Zoezi hilo lilitimizwa ndani ya dakika kadhaa na Kenny alimwagiwa maji. Baada ya muda mfupi alizinduka na alikutana na sura ya mubaya wake Mr.Carlos “Kijana ndani ya masaa ishirini na nne tutaitumia vizuri hewa unayoitumia…..eeh! hautakuwa hapa utaenda kuongeza orodha ya familia yako”Alisikika Mr.Carlos akiwa amekaza uso na mishipa ikiwa imemtoka kila eneo la uso wake.Mr.Carlos alicheka kidogo kisha akatabasamu aliwakonyeza vijana wake ambao walianza kumpiga viboko kila eneo la mwili wake akiwa amefungwa.Kenny alipiga kelele za kuumia lakini watu hao waliendelea kumpiga.Muda huo Mr.Carlos alikuwa akipiga makofi juu ya kile kilichoendelea,dakika kumi badaaye Mr.carlos aliwataka wamuache.
Walimfungua Kenny na alikuwa amevimba kila eneo la mwili wake “kijana umeona huo ni utangulizi tu ahhh!...”aliongea Mr.Carlos kwa madaha
“siwezi kufa kabla yako …”Aliongea Kenny kwa sauti ya kukatakata baada ya kipigo hicho.Alikuwa amelala katika sakafu ya chumba hicho,Mr.Carlos kwa mara nyingine aliwataka vijana wake wamshushie kipigo Kenny.Jambo ambalo lilitekelezwa walianza kumpiga tena kila eneo la mwili wake akiwa amelala sakafuni kwa mara nyingine tena Kenny alipiga kelele za kuumia na baada ya muda mrefu wa kipigo aliamua kujifanya amepoteza fahamu kwa mara nyingine tena.Jambo hilo liliwafanya waache kumpiga na tayari alikuwa ametokwa damu nyingi eneo lililomzunguka.
Wakati huo ilikuwa yapata saa saba na nusu usiku Mr.Carlos aliwaita nje ya chumba kile vijana wake kadhaa.Aliwataka Kenny akauawe eneo la pembeni kidogo na Dar es salaam na mwili wake uachwe huko huko.Baada ya kushauriana walikubaliana waende kumuulia maeneo ya Kibaha mkoa wa Pwani.Walirudi kwenye kile chumba na Kenny bado alikuwa amelala kama hana fahamu “safari njema Kenny John Mushi….unahitajika mbinguni”Alisikika Mr.Carlos akiongea wakati huo Kenny alikuwa akinyanyuliwa kupelekwa nje.Walimbeba mpaka kwenye zile Mercedez benz zilizomleta na safari ilianza kuelekea maeneo ya Kibaha, Mr.Carlos aliwasha gari lake na kuondoka kuelekea nyumbani kwake akiamini kazi ilikuwa imeisha.
Kenny alikuwa kwenye buti la moja ya gari zilizokimbia katika barabara iliyoelekea Morogoro.Vijana wa Mr.Carlos walitaka kumaliza kazi ya kumuua Kenny ili waendelee na kazi nyingine za Tanzanian Gangstars.Waliamini hakuna kilicho shindikana hivyo walijua Kenny alikuwa na muda mfupi wa kuwapo Duniani.Ilikuwa saa tisa kasoro robo wakati huo gari hizo ziliendeshwa kwa kasi maeneo ya Kimara wakielekea Kibaha.Kenny akiwa kwenye buti kukiwa na joto kali na nafasi ndogo ambayo hewa ilipenya, alijaribu kufungua mlango wa buti hiyo pasipo mafanikio.Hakukubali auawe kirahisi hivyo akiwa hajalipa kisasi kwa muuaji wa familia yake.Alijaribu kupiga mateke mlango wa buti la gari hilo pasipo mafanikio jambo lililompa hofu kuhusiana na maisha yake.
Baada ya dakika kadhaa walikuwa eneo la Mailimoja, kulikuwa na foleni kubwa ya gari zilizotoka mkoani Dar es salaam.Mercedez Benz hizo za vijana wa Mr.Carlos waliokuwa wakimshikilia Kenny ziliingia katika foleni hiyo.Walikua hawaelewi foleni hiyo ilisababishwa na nini muda huo wa saa kumi kasoro.Baada ya kusogea wakiendesha gari zao wakiwa katikati ya foleni hiyo walishuhudia askari wengi wakifanya ukaguzi wa gari moja mpaka jingine.Walitaka kugeuza gari zao lakini haikuwezekana kwa vile walikuwa katikati ya foleni.
Waliendelea kusogea huku wakipanga mbinu za kuvuka kikwazo hicho.Wakiendelea kusogelea ukaguzi huo waliamua kumuita askari mmoja na kumuuliza kilichoendelea wakati zamu yao ikikaribia.Walielezwa kwa ufupi kuwa kuna ujambazi ulikuwa umetokea Dar es salaam masaa machache yaliyokuwa yamepita.Wakati huo Kenny akiwa ndani ya buti la moja ya gari hizo alishtushwa na kupungua kwa kasi za gari hizo alihisi kuuawa kwake kulifuatia.Vijana wa Mr.Carlos Mato walisogeza gari zao na zilianza kukaguliwa .Askari walikonyezana kuonyesha hali ya kutowamini watu hao hiyo ilitokana na mavazi yao ya suti za kufanana na miwani iliyopoteza sura zao.
Walianza upekuzi wa gari hizo kiufasaha wakitaka kuhakikisha kama hazikuwa zinahusika na ujambazi uliotokea.Muda huo Kenny hakuwa na amani akiamini saa ya kufa kwake ilishafika lakini aliwaza kupigana mpaka mwisho wa zoezi hilo ili ashinde.Baada ya ukaguzi wa gari hizo pasipo mafanikio askari walitaka kukagua buti za gari hizo.Jambo hilo liliwatia moyo askari hao kutokana na hofu ilionyeshwa wazi na watu hao.Walikagua gari la kwanza na kuona halikuwa na kitu na waligeukia la pili wakitaka kulikagua.Hapo ndipo hofu ya watu hao iliongezeka kabla askari aliyekagua kufungua buti la gari hilo,walishangaa gari hizo na ziliondolewa kwa kasi eneo hilo la ukaguzi.
Askari hao waligundua watu hao walikuwa ni majambazi waliwasha haraka gari zao na pikipiki na kupiga simu kituo cha polisi cha mbele kuelezea tukio hilo.Nao waliondoa gari zao na pikipiki kufuatilia zile Mercedez Benz mbili.
Vijana wa Mr.Carlos walijitahidi kukimbiza gari zao ili kuukwepa mkono wa polisi ,dakika chache tu tangu wakimbie toka kituo cha kukaguliwa walishuhudia gari za polisi na pikipiki vikija kwa kasi nyuma yao.Waliongeza kasi za gari zao na kuwaacha polisi hao kwa kiasi fulani.Baada ya kukimbiza gari zao kwa kilometa kadhaa walishtushwa na gari nne mbele za polisi zilizopangwa barabarani.Polisi hao walielekeza bunduki zao kwao walisimamisha gari zao na kutoa bastola zao walizozitoa kwenye makoti yao ya suti.Walishuka na kuanza kurushiana risasi na askari wa pande zote, waliokuwa wameziba barabara na wale waliokuwa wakiwafukuzia nyuma.Baada ya kuona walizidiwa walianza kukimbia kuelekea vichakani huku wakiendelea kurushiana risasi.Tayari mmoja wao alikuwa amepigwa na askari hao ambao nao pia askari wawili walikuwa wamepigwa na majambazi waliopambana nao.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
* * * * *
Mary aliendelea vizuri na afya yake na alikuwa nyumbani kwao maeneo ya Mbezi Beach.Moyoni aliumia kitendo cha kupigwa alichofanyiwa na Kenny bado hakujua chanzo chake.Alijilaumu kwa kutumia muda wake na gharama nyingi kumsaidia mtu ambaye hakuwa na msaada kwake.Alijiuliza lengo la Kenny siku aliyompiga lakini hakupata jibu,aliamini wasingetokea watu waliomuokoa siku hiyo asingekuwa hai,kilicho muudhi zaidi alijitahidi kumtoa Kenny katika hisia zake lakini haikuwezekana na dalili zote za kumsamehe zilianza kuonekana.Alitaka kujua sababu iliyomfanya Kenny ampige na alikuwa na lengo gani akilini hakujua alikuwapo sehemu gani.
Siku zote baba yake Mr.Carlos alimweleza Mary kuwa msako wa kumtafuta Kenny uliendelea na hangekuwa na msamaha kwa kijana huyo.Jambo hilo ndilo lililomfanya Mary aamini Kenny akikamatwa angeishia jela kutokana na uwezo wa baba yake.Siku moja ya Jumamosi Mary baada ya kuwa amelala kwa muda mrefu aliamka na kwenda kuoga.Baada ya zoezi hilo alielekea sebuleni kwao na kukaa kwenye sofa. Ilikuwa ni baada ya kumsalimia baba yake Mr.carlos aliyemkuta sebuleni hapo ikiwa ni saa nne asubuhi.Aliungana na baba yake kuangalia televisheni iliyokuwa imewashwa,baada ya muda mfupi ilifika wakati wa taarifa ya habari.Katika muhtasari wa habari hiyo mtangazaji alieleza juu ya watu nane waosadikiwa kuwa majambazi waliouawa maeneo ya Kibaha.
Mr.Carlos alishtuka na kukaa vizuri katika sofa alilokaa akisubiri kwa hamu taarifa ya habari hiyo ianze kutangazwa.Muda huo kijasho chembamba kilianza kumtoka kwani vijana wake aliowatuma wakamuue Kenny John Mushi walielekea maeneo hayohayo ya Kibaha.Taarifa hiyo ya habari ilianza kusomwa ikieleza watu kumi walikuwa wamefariki katika mapigano ya askari na majambazi nane.Wawili kati yao wakiwa askari na majambazi nane waliokuwa wamemteka kijana aliyejitambulisha kwa jina la Kenny John.Mr.Carlos alipandwa na hasira na shati lake jeupe lilianza kulowa jasho lililomtiririka.
Mary alikuwa ameshtuka kusikia jina la Kenny John na alikaa vizuri kuanza kuifuatilia habari hiyo. Mtangazaji aliendelea kwa kusema kijana Kenny John alikuwa amelazwa hosptali ya Muhimbili na alikuwa na mmajeraha mengi. “sasa tumuone Kenny John Mushi aliyetekwa na majammbazi hao”Aliongea mtangazaji huyo na picha ya kituo hicho cha televisheni ikaanza kumuonesha Kenny John aliyekuwa amelazwa huku akihojiwa “aahm! mtu anayehusika na majambazi hawa wote waliouawa mimi namfahamu na ninasuburi nipone ili nimfichue mtu huyu mwenye maovu mengi ambayo nayafahamu…..”Aliongea Kenny John na kutohitaji kuongea zaidi tena,aligeuza kichwa chake upande wa pili wa kitanda alichokua amelazwa.
Taarifa hizo zilimshtua Mr.Carlos Mato na kuanza kupiga makelele kama mtu aliyechanganyikiwa “Hamjamuua kwa nini? Mimi siwaelewi na hiki nini tena…aah!”Alipiga kelele Mr Carlos akitoka nje ya nyumba yake akiwa na hasira kupindukia.Aliwasha gari lake na kuondoka kwa kasi eneo la nyumbani kwake.Wakati huo Mary alikuwa akitokwa na machozi, picha ya Kenny akiwa ameumizwa vibaya ilimfanya amuonee huruma.Kwani alikuwa ameumizwa zaidi ya vile alivyokuwa yeye.Kilichomshangaza ni hasira alizozipata baba yake jambo lililoanza kumtia hofu na kuhisi huenda kulikuwa na jambo kubwa ambalo hakulijua.
Sentensi aliyolalama baba yake ya kutouawa kwa Kenny ndiyo aliyompa wasiwasi zaidi,hakuelewa ni kwanini Kenny apewe adhabu kama hiyo, wazo la kuujua ukweli wa mtu aliyemteka Kenny na sababu iliyomfanya ampige ndivyo vilimkaa kichwani akiwaza kufanya jambo.Alitaka Kenny amweleze vizuri kila kilicho endelea ingawaje hakuwa na uhakika kama mtu huyo alirudi katika hali ya kutomchukia.Jambo lililokuwa gumu kwake ni agizo kwa walinzi wa nyumba hiyo kuwa asiruhusiwe kutoka alilolitoa baba yake.Alianza kufikiria njia ambayo angeitumua kutoka nyumbani kwao hapo lakini hakupata jibu.
Mr.Carlos alikimbiza gari lake na baada ya dakika kadhaa alikuwa Mikocheni katika nyuma yake maalumu kwa vikao vya ujammbazi.Aliwaita vijana wake katika kikao cha dharura muda huo alikuwa amechanganyikiwa akili yake ilikuwa haijatulia vyema aliwataka vijana wake waende wakamteke Kenny John akiwa hospitali. Agizo hilo liliwafanya vijana wake waanze kupanga mbinu za kwenda kumteka Kenny John, baada ya dakika kadhaa walipata njia ya kuitumia.Mr.Carlos alikuwa amepanga kuongozana nao ili kuhakikisha Kenny anatiwa mikononi mwao.
Baada ya kufikiria kwa muda Mary alipata njia ya kuwalaghai walinzi wa getini katika nyumba yao.Aliingia chumbani kwake nakuchukua fedha zote alizokuwa nazo sambamba na kadi ya kuchukulia fedha Benki, aliweka katika suruali aliyokuwa ameiivaa.Baada ya kujianda alianza kutembea kwa kunyata akihofia mama yake kugundua kuwa aliondoka,Kiafya alikuwa akiendelea vizuri na alikuwa na makovu kadhaa usoni na sehemu tofauti za mwilini mwake.Mara baada ya kutoka nnje ya nyumba yao alienda akikimbia katika chumba walichokaa walinzi kilichokuwa getini. Mara baada ya kufika getini hapo alianza kuigiza kwa kulia “Jamani mnisaidie mama kaanguka anaumwa” alisikika Mary akilia akiwa sisitiza walinzi hao.Walinzi hao walitoka mbio kwenye chumba hicho na kuanza kukimbia wakielekea kwenye nyumba hiyo ya Mr.Carlos.Wakati huo Mary nae aliwafuata nyuma akikimbia kwa kasi ndogo tofauti na wao.Hatimaye waliingia ndani kabla yake haraka alichofanya ni kuanza kufunga mlango wa nyumba hiyo.Mara baada ya kufunga mlango huo akitumia funguo zilizokuwa mlangoni hapohapo.
Alitoka mbio mpaka kwenye geti kubwa la kutokea la nyumba yao wakaalo walinzi na kulifungua. Kisha alirudi na kuwashwa gari dogo la kutembelea aina ya Toyota Hilux ambalo awali alichukua funguo zake.Aliondoka kwa kasi eneo hilo la nyumbani akiwaacha walinzi wakipiga kelele za kutaka wafunguliwe baada ya kugundua walikuwa wamedanganywa. Alikimbiza gari hilo lengo lake likiwa ni kufika hospitali ya taifa ya Muhimbili na hatimaye kumpata Kenny.Jambo alilohofia ni jinsi ambavyo baba yake Mr.Carlos alivyoshtushwa na tukio lililokuwa limetokea.Lengo lake lilikuwa ni kumuokoa Kenny na kuujua ukweli wa mambo ambayo yeye hakuyajua.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mwishoe aliifika hospitali hapo akiwa amesimamisha gari sehemu ya mbele ya hospitali hiyo.Alishuka na kuanza kukimbia kuelekea eneo la mapokezi la wagonjwa.Mara baada ya kujitambulisha kama ndugu wa Kenny John alielekezwa wodi alilokuwa amelazwa kijana huyo.Alianza kutembea haraka haraka kuelekea kwenye wodi hilo na hatimaye alipofika aliongoza kitanda namba ishirini na tano kama alivyoelezwa. Lakini kitandani hapo hapakuwa na mtu kama alivyokuwa ameelezwa awali, akahisi kuanza kuchanganyikiwa taratibu.
Lakini kitandani hapo hapakuwa na mtu jambo lililomfanya aanze kumuulizia Kenny John kwa wagonjwa waliolazwa vitanda vya pembeni.Walimjibu alikuwa ameondoka muda mrefu na hawakujua alielekea wapi muda mfupi akiwa hajui jambo la kufanya aliingia askari mmoja ambaye naye alianza kumuulizia Kenny John. “Yuko wapi huyu? nimepewa jukumu la kumlinda au ametekwa tena?”Alilalama askari huyo baada ya kusikia kuwa Kenny John alikuwa ametoka na hakurudi tena.Mkononi alikuwa amebeba juisi ya kopo na chakula alichokuwa amemnunulia Kenny John.
Mary aliamua kuanza kuzunguka kila sehemu ya hospitali hiyo kwa lengo la kumtafuta Kenny lakini hakupata nafasi hiyo ya kumuona.Baada ya kumtafuta kwa muda mrefu pasipo mafanikio aliwasha gari na kuanza kuondoka hospitalini hapo.Mita kadhaa akiiacha hospitali hiyo alipishana na Mercedez Benz mbili zikiwa na kasi kuelekea hospitalini hapo.Alisimamisha gari alilokuwa nalo kwa lengo la kutaka kuwaona watu ambao wangeshuka kwenye magari hayo.Akiwa ametoa kichwa nje akitazama gari zile,alishuhudia watu saba wakishuka kwenye gari hizo.Mwishoe alishuka mtu ambaye alimhisi ni baba yake aliyewaonesha ishara wale wengine wakanza kuelekea kwenye hospitali mtu huyo aliyemhsi baba yake ambaye alimuona upande wa mgongoni tu aliingia tena kwenye moja ya gari hizo.
Mary alishangazwa na kilichokuwa kinaendelea jambo lililomfanya aingiwe na wasiwasi na maneno ya baba yake.Aliamini watu hao walimtaka Kenny, kilichomshangaza ni kujiingiza kwa baba yake katika tukio hilo lililokuwa la kipolisi zaidi.Hakutaka kufuata kumuliza kwani wakati huo alishakuwa na kesi ya kutoka nyumbani kwao.Kikubwa aliamini Kenny hakuwepo hospitalini hapo hivyo wasingemkuta,aliondoa gari lake kwa kasi na kuiacha hospitali hiyo.Jambo aliloanza kufanya ni kumpeleleza Kenny kila sehemu aliyopita aliendesha gari akizunguka maeneo tofauti ya jiji akimulizaa pasipo mafanikio.Aliamua kwenda kituo cha mabasi cha Ubungo akiwa na wazo alilohisi huenda Kenny alikuwa na malengo ya kurudi kwao Moshi. Katika kituo hicho cha mabasi hakumwona Kenny aliendelea na mzunguko katika maeneo waliyowahi kuyatembelea wakati akiwa na uhusiano naye bado hakufanikiwa kumuona.
Baada ya kuzunguka kwa muda mrefu pasipo mafanikio yeyote ilikuwa yapata saa moja kasoro robo.Aliamua kuendesha gari lake kuelekea shuleni ambako awali Kenny John alisoma katika shule ya Azana.Alihisi huenda Kenny alikimmbila eneo hilo kwa vile alifahamiana na wanafunzi wengi.Mara baada ya kufika maeneo ya shuleni hapo alisimamisha gari lake kando ya geti kuu la shule hiyo na alianza kutafuta mbinu ya kumuulizia Kenny.Baada ya dakika kadhaa alimuona kijana mmoja akingia shuleni hapo,akaamua kumuita na kumulizia kuhusu Kenny.Alimjibu amsubiri kidogo aende akamuulize kama alikuwepo shuleni hapo hatimaye kijana huyo alirudi na taarifa za kutokuwapo kwa Kenny John, taarifa hizo zilimchanganya Mary aliyeamua kulala kwenye usukani wa gari alilokuwa nalo.Wakati huo ilikuwa vigumu kwake kurudi nyumbani kwa vile alitoroka na kama angerudi aliamini hangeweza kupata nafasi ya kutoka tena.
Kilichomuuma zaidi hakuelewa hali ya kiafya ya Kenny John na hisia za kuwa huenda alitekwa tena zilianza kumjia kichwani, alijikuta akitokwa na machozi pasipo ridhaa yake wakati huo hakuona jambo jingine la kufanya kwani alikuwa amezunguka sehemu nyingi akimtafuta pasipo mafanikio.
* * * * *
Baada ya kukaa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa masaa kadhaa Kenny aliamua kutoroka.Hiyo yote ilitokana na kuamini kwa vyovyote vile Mr.Carlos angemtafuta baada ya kusikia alikuwa hai, kikubwa zaidi ni vitisho vya kutoa siri za Mr.Carlos ambaye alivitoa wakati akihojiwa na kituo cha televisheni.Huku akiwa anachechemea na kuvimba sehemu nyingi za mwili wake aliwaaga wagonjwa wenzie akidai alielekea chooni.Muda huo askari aliyekuwa akimlinda alikuwa ameondoka akidai alienda kumtafutia chakula.Alijitahidi kutembea na hatimaye alitoka nje na kukodi taski kwa kutumia fedha za watu walizompa baada ya kuona ameumizwa vibaya.Alielekea maeneo ya ufukweni mwa bahari ya Hindi na huko alikaa katika eneo la peke yake akitathimii yote yaliyokuwa yamejiri.Tayari alielewa alikuwa ameanzisha vita na Mr.Carlos na mwisho wa vita hivyo alipaswa ashinde kwa kulipiza kisasi.Muda huo hakuelewa njia ambayo angeitumia kupata fedha za kukamilisha mipango yake dhidi ya Mr.Caarlos.Jambo ambalo aliligundua alikosea na akaanza kujilaumu ni kitendo alichofanya cha kumpiga Mary.Katika wakati huo mguu aliyokuwa nao aliamini Mary pekee alikuwa na uwezo wa kumsaidia kwa jinsi alivyompenda.Lakini tayari alikuwa ameharibu uhusiano wake na Mary hivyo hakuwa na njia nyingine.
Alitamani kupigia simu Mary lakini alihofia asingekubali kuongea naye zaidi hakuwa na simu muda huo.Jambo alilojiuliza kichwani lilikuwa endapo Mary angegundua uovu wa baba yake angekaa upande gani.Hakupata jibu lakini aliamini Mary angekaa upande wenye haki.Baada ya kukaa kwa muda mrefu katika fukwe hizo,alianza kuwaza ni sehemu gani angelala siku hiyo.Hatimaye aliamua arudi shuleni kwao ambako aliwaacha rafiki zake kadhaa ili apate hifadhi ya siku moja. Aliamini siku iliyofuata angejua afanye nini na wazo lake kubwa lilikuwa ni kurudi kwao mkoani Kilimanjaro.Aliondoka maeneo hayo kwa taksi ikiwa ni majira ya saa moja na nusu usiku na safari ilianza kuelekea shuleni kwao.Moyoni hakuwa na amani sana kwa vile eneo hilo la shule ndilo eneoambalo alikamatwa na watu wa Mr Carlos.
Baada ya dakika kadhaa taksi hiyo ilisimama mbele ya geti la shule hiyo kando kidogo kulikuwa na “Toyota Hiliux”.Kenny alishuka ikiwa ni baada ya kumlipa dereva taksi. Huku akichechemea alianza kutembea kuelekea kwenye geti la shule hiyo, akiwa ametembea mita kadhaaa alishtushwa na sauti ya kike iliyomuiita kwa nguvu toka kwenye Toyota Hilux iliyokuwa pembeni kidogo.Alipogeuka alimuona Mary akiwa ameshuka toka kwenye gari hilo na alikimbia eneo alilosimama Kenny na kumrukia akimkumbatia.Wote walianguka chini kabla ya Mary kumsaidia Kenny kusimama.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Tuondoke eneo hili ni hatari”Aliongea Mary akimvuta mkono Kenny kabla ya mazungumzo yoyote.Jambo ambalo Kenny alilitii na waliongozana kwenye gari hilo alilokuwa nalo Mary na waliondoka eneo hilo kwa kasi. “Mary naomba unisamehe kwa yote yaliyotokea”Aliongea Kenny kabla ya yote mara baada ya gari hilo kuondolewa “Mmh! pole wewe kwa yaliyokukuta, mimi nilishakusamehe….ingawaje sielewi mambo mengi” “usijali nitakueleza kila kitu usicho kifahamu”Alijibu Kenny na Mary alikuwa akiendesha gari wakielekea maeneo ya Magomeni.
Walitumia muda kidogo kufika Magomeni kutokana na foleni iliyokuwa barabarani.Mary aliendesha gari mpaka kwenye hoteli moja ambayo alilipia na waliongoza kwenye chumba walicho elekezwa.Jambo alilotaka kujua ni kuhusu mambo yote yaliyo kuwa yametokea ambayo binafsi hayajua.Mara baada ya kuingia kwenye chumba hicho Mary alianza kutokwa na machozi kutokana na jinsi ambavyo alimuona Kenny.Alikuwa ameumia sehemu kubwa ya mwili wake akiwa na majeraha mengi yaliyokuwa yamefungwa.Kenny alimtuliza asilie na alihitaji achukulie jambo hilo ni la kawaida alianza kumsimulia yote yaliyotokea.Alianza kwa kuzielezea familia zao,yake ya John Mushi na Mr.Carlos Mato.Alimueleza Mary jinsi baba yake Mr.Carlos alivyoiua familia yake akianza na dada yake Juliana aliyemubaka kabla ya kumuua..Alimweleza pia alivyochoma nyumba yao na kumuua baba na mama yake na kumaliza kwa kuwaua Babu na Bibi yake.Kenny alimweleza jinsi alivyoipata siri hiyo na kumaliza kuhusiana na jinsi alivyompiga Mary alidai alifanya hivyo kutokana na hasira aliyokuwa nayo.
Alidai katika maisha yake alimchukia Mr.Carlos na familia yake lakini kwa wakati huo hakuona umuhimu kuwachukia watu wasio na hatia.Muda huo Mary alilia kwa uchungu akiwa haamini unyama uliokuwa ukifanywa na baba yake.Jambo ambalo lilianza kumuingia akilini ni kuhusiana na maneno aliyoyataja baba yake kuwa kwa nini Kenny hakuuwawa.Alianza kukubaliana na yote aliyoelezwa na Kenny na alimtaka siku iliyofuata watoe taarifa katika kituo cha polisi. Jambo hilo Kenny alikataa kabisa akimweleza mtandao wa baba yake ulikuwa mkubwa na alishirikiana na maofisa wa polisi.Bado Mary alisisitiza wafanye hivyo, upendo na heshima vyote alivyomjengea baba yake vilikuwa vimepotea ndani ya muda mfupi. Hakumtamani hata kidogo mzazi wake huyo, unyama aliokuwa ameufanya ulikuwa ni mkubwa kupindukia. Kenny alimtaka Mary waongozane wote kuelekea mkoani Kilimanjaro, siku iliyofuata walilitelekeza gari la Mary katika hoteli hiyo waliyofikia. Ikiwa ni majira ya saa kumi na moja alfajiri walikuwa kituo cha mabasi cha Ubungo wakikata tiketi ya basi la kuelekea Moshi. Mara baada ya zoezi hilo walisafiri kwa basi mpaka Moshi na punde walipofika walipanda gari jingine lililoelekea Moshi vijijini kata ya Kibosho.
Mara baada ya kufika nyumbani kwao Kenny alimwelezea pia shangazi yake kuhusiana na mauaji ya familia yao. Shangazi yake alishtushwa na taarifa hizo naye aliungana na Mary kuwa wakatoe taarifa kituo cha polisi. Siku hiyohiyo walitoa taarifa kituo cha polisi Moshi mjini na kuelezwa taarifa hizo zingefanyiwa kazi.
Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro alishtushwa na taarifa alizozipata kuhusiana na Mr. Carlos Mato mtu aliyemuamini kuwa ni mwenye uwezo kifedha. Hakuwahi kufikiria jambo linalohusiana na ukatili kama huo unaomuhusu Mr. Carlos Mato. Kabla ya yote alichukua simu yake na kumpigia Mr. Carlos Mato na kumweleza yote aliyoyasikia. “sasa kamanda nitakupa fedha yoyote lakini ufanye jambo hili siri” aliongea Mr. Carlos Mato “sasa hata nikifanya siri, wewe utafanya nini kwa sababu watu hawa wataenda hata kituo kingine cha polisi” aliongea kamanda huyo wa polisi na kumuuliza Mr. Carlos swali. “Mimi leo hii nitahakikisha nawaua wote” alisikika Mr Carlos Mato aliyeonekana kuchanganyikiwa. “Fanya hivyo lakini mimi nahitaji milioni thelathini” “Bila shaka kamanda nashukuru kwa taarifa yako” aliongea Mr. Carlos akijibu akiwa amechanganyikiwa.
Tayari kamanda huyo wa polisi wa mkoa wa Kilimanjaro aliamini yote aliyoelezwa na kujua jinsi ya kumnasa Mr. Carlos Mato. Aliwaeleza Kenny, Mary na shangazi yake walirudi nyumbani siku hiyo, alituma gari kumi za polisi eneo la Kibosho wilaya ya Moshi vijijini. Aliwataka askari kujificha katika mashamba ya kahawa na miomba kumsubiri Mr. Carlos Mato aende eneo hilo la nyumba ya marehemu mzee Mushi, jambo ambalo askari hao walilitekeleza ikiwa ni baada ya kuyaficha magari yao wakati huo uilikuwa yapata saa tano usiku. Walijificha katika maeneo yaliyozunguka nyumba hiyo yaliyokuwa na giza. Hapakuwa na mwanga hata kidogo kwani hata taa za nyumba hiyo zilizimwa.
Walikaa eneo hilo kwa muda mrefu pasipo Mr. Carlos Mato kutokea eneo hilo, waliendeleza uvumilivu hadi saa kumi na robo usiku walishuhudia Mercedes Benz mbili zikiwasili maeneo hayo na kusimama mbele ya nyumba ya marehemu mzee Mushi. Alishuka katika gari hizo Mr. Carlos Mato na vijana wake sita wakiwa na bastola mikononi mwao walianza kugonga mlango wa nyumba hiyo, wakiwa wanaendelea kugonga walishtushwa na taa kali zilizowaka kutoka maeneo tofauti ya eneo hilo na waliambiwa wanyoshe mikono juu. Mwanga huo ulikuwa mkali na uliwaumiza macho pasipo kuwaona waliowamulika. Mr. Carlos na vijana wake walinyosha mikono juu baada ya kuweka silaha zao chini. Walishuhudia gari za polisi zikisogezwa eneo hilo na walizungukwa na askari ambao pia waliwasogelea.
Mr.Carlos tayari alikuwa mikononi mwa polisi na kesi dhidi yake ilifunguliwa mahakama ya hakimu mkazi ya Kisutu mkoani Dar es salaam. Siku ya kwanza tu ya kesi hiyo kuanza kusomwa, kesi iliyohudhuriwa na mamia ya watu ambao wengine walikuwa nje, Mr. Carlos alikubali kufanya mauaji ya familia ya John Mushi. Alielezea mauaji mengine ya zaidi ya watu hamsini aliowaua na alikubaliana na hukumu yoyote akimaliza kuongea alisema kuwa “ naomba nusu ya utajiri wangu apewe kijana Kenny John Mushi”. Maelezo ya Mr. Carlos Mato yaliwashtua wengi waliohudhuria hukumu ya kesi hiyo waliodhani alionewa. Hatimaye hukumu iliyotolewa dhidi yake ilikuwa ni kunyongwa hadi kufa kufuatia vifungu vya sheria vya nchi ya Tanzania.
Gari la polisi lilisogezwa na Mr. Carlos aliisogelea familia yake na kupiga magoti “nawaomba mnisamehe na ishini katika misingi ya maadili msiwe kama mimi” aliongea Mr. Carlos akiwakumbatia wanawe Jane, Joseph na Mary wakiwa na mama yao wakilia kwa sauti za juu mahakamani hapo. Siyo wao tu hata watu wengine waliotendewa mema na Mr. Carlos walikuwa wakilia kutokana na adhabu aliyohukumiwa. Mr. Carlos alimgeukia Kenny John Mushi aliyeongozana na familia yake naye alimwambia “nisamehe mwanangu …” kabla hajaendelea alivutwa na askari na kuongozwa mpaka kwenye gari la polisi akaondoka nao eneo hilo la mahakama ya Kisutu.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya miaka mitano Kenny na Mary walikuwa wakiishi katika jiji la Paris, Ufaransa na tayari walikuwa wamepata mtoto wa kiume waliyompa jina la Carlos.Familia yao ilijawa na furaha na walishasahau yaliyojiri miaka ya nyuma katika maisha yao.Mwanao walimuita Carlos wakimweka karibu babu yake mtoto huyo aliyekufa kwa kunyongwa.Siku ya Jumamosi mwezi Desemba tarehe thelathini na moja,ilikuwa ni siku ya kuzaliwa kwa Mary, Kenny alimnunulia zawadi nyingi na kabla hajamkabidhi alisikika akisema”Siku zote za maisha yangu niliichukia familia ile na kuwaona wote ni adui zangu,Hata siku moja sikufikiria ingetokea kuwa NAMPENDA ADUI YANGU kutoka kwenye familia ile, Kumbe adui wengine ni wake wema”Alimalizia Kenny na kusisitiza “Nakupenda sana mke wangu……nakupenda…..!” Walikumbatiana wakiwa na furaha.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment