Chombezo : Jamani Antiii...Nishushe Ununio
Sehemu Ya Tatu (3)
“Hapana bosi, mimi sina uhusiano wowote na mtu yeyote hapa ofisini zaidi ya kusalimiana na kushirikiana kikazi, hayo mengine yanabaki kuwa maneno ya watu wasiokuwa na kazi za kufanya mkuu, siko hivyo kabisa na niko hapa kikazi na si mambo mengine, nina familia yangu hivyo najiheshimu kuliko ambavyo yeyote anaweza kudhani,” Vivian alizungumza mfululizo kiasi cha kuwafanya meneja na Bigambo wabaki wamemkodolea macho wasiamini wanachokisikia, kwani tangu Vivian ajiunge na kampuni hiyo, tabia yake ilikuwa ya ukimya wa kupitiliza na neno pekee alilolitoa kupitia midomo yake minene ni salamu na kicheko cha tabasamu.
“Sawa, nimekuelewa,” meneja ambaye hadi hapo alikuwa ameishiwa pozi la ukali aliokuwa nao awali alisema kwa sauti ya upole na kumgeukia Bigambo ambaye hakuonesha wasiwasi wowote. “Nimesikia kuwa una uhusiano usiofaa na Vivian na unajua kabisa utaratibu wa ofisi yetu haturuhusu mapenzi vinginevyo wahusika wafanye kwa siri na wafanikishe iwe hivyo, imekuwaje Bigambo?CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Halafu kwa nini uongozi uendelee kuingia kwenye malumbano na wewe tu kila siku? Wewe ni mtu gani usiyebadilika Bigambo? Nakuhakikishia awamu hii tukikuondoa hutarudi tena ofisini hapa, kama ulivyozoea kuingia na kutoka na hutakuwa na mtu wa kumlaumu,” alisema meneja huku akimtazama Bigambo kuanzia chini magotini alivyokuwa amekaa hadi utosini. “Sina uhusiano wowote na huyu dada kama alivyoeleza yeye, isipokuwa humu ofisini kuna watu wana tabia za kiswahiliswahili sana, wasione watu fulani wenye jinsi mbili tofauti wako karibu wanaanza kuzusha ya kwao, sasa wewe unawezaje kuthibitisha kwamba mimi na Vivian tuna uhusiano usiofaa?” Bigambo alimalizia kwa swali ambalo mfanyakazi wa kawaida hawezi kumjibu mwajiri wake. Ujasiri wa Vivian ulimpa nguvu sana Bigambo.
Yeye kama mwanaume ikabidi aoneshe nguvu mara mbili yake. Meneja alibaki ameduwaa asijue nini cha kufanya. Swali la Bigambo lilikuwa la kitaalam sana. Ni yale maswali ambayo wadau wengi wa mjini na wenye upeo mkubwa wa mambo maishani huita technical question (swali tata). Ni kweli hakuwa na ushahidi wa moja kwa moja kwamba wale ni wapenzi na badala yake alichokifanya ni kuchukua maneno ya watu waliopika majungu. “Basi niachieni hili nitafuatilia mwenyewe kwa wakati wangu na nataka niwaambieni ukweli kwamba nikibaini ni ukweli nitawarudisheni nyote nyumbani bila maelezo yoyote na huo utakuwa mwisho wenu kuwepo hapa ofisini, mnaweza kuondoka,” alisema meneja huku akichagua makaratasi mezani kwake na kuwa kama ameshaachana na akina Bigambo na Vivian. “Sawa bosi lakini kuna jambo umenishangaza sana kwa kweli, tangu nikufahamu na umakini ulio nao haiwezekani ukafanya jambo hilo,” Bigambo alisema na kumtazama usoni meneja kabla ya kuhamishia macho kwa Vivian aliyekuwa kimya tangu azungumze maneno yale mfululizo. “Jambo gani unataka kusema nini, Bigambo?” Meneja aliuliza na kuacha kufanya chochote zaidi ya
kuweka umakini wote kwa Bigambo na Vivian. “Hivi unawezaje meneja mzima kuchukua maneno ya watu na kuleta kesi ya kututuhumu jambo zito kama hilo? Kwa kiongozi mkubwa kama wewe ni muhimu sana kuwasilisha mambo ukiwa na uhakika nayo kwa maana ya ushahidi wa kutosha kumuweka mtu hatiani,” alisema Bigambo na kumalizia kwa msonyo wa kugandisha ulimi eneo la juu ya taya. “Haya, endeleeni na mambo yenu na kama nilivyosema kwamba nikibaini kama kuna ukweli wa namna hiyo nitachukua uamuzi ambao nimewaambieni,” alisema meneja na kuachana nao kimtindo ambapo alishika simu ya mezani na kunyanyua mkonga na kupiga mahali kwingine ambako Bigambo na Vivian hawakujua. Bigambo na Vivian waliondoka ndani ofisini kwa meneja na kila mmoja wao alikwenda kwenye kiti chake na kuendelea na majukumu ya kikazi. Kila mtu akawa anawatazama kwa macho ya kuibiaibia, lakini Bigambo alitengeneza chuki kali sana moyoni mwake dhidi ya wafanyakazi wenzake, ingawa hakujua ni nani alikuwa amepeleka maneno ya uchochezi kwa meneja lakini alishajua kabisa ofisini kuna watu wenye roho mbaya na husuda kali na hawako tayari kuona mtu akifanikiwa kwa jambo lolote. “Hii ofisi aisee, lakini hakuna shida ngoja kila mmoja afanye maisha yake, kwa sababu hakuna undugu humu ndani yaani mtu anaweza kukuangamiza huku anakuchekea na mwisho wa siku anakuwa wa kwanza kuja kukupa pole ya kinafiki ukishafikwa na makubwa,” Bigambo aliwaza moyoni na kuwatupia watu mbalimbali jicho la chuki. “Pacha vipi, mbona kama una mawazo tele kulikoni tena pacha?” mmoja wa wafanyakazi mwenzao aitwaye Kwere alimsabahi Bigambo kwa shangwe na maneno ya bashasha lakini Bigambo aliitikia kwa sauti ya unyonge bila kumpa ushirikiano wa kutosha kama ilivyokuwaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
imezoeleka. “Nikushukuru sana Kwere, lakini kwa sasa naomba uniache maana siko vizuri sana kichwani,” Bigambo alisema huku akiendelea kufanya kazi zake huku akiwa amenuna kutokana na uchungu ambao alikuwa nao moyoni wa maneno ya kuchongwa ambayo aliyakuta kwa meneja. “Haya bwana pacha, maana leo nakuona hauko karibu na sisi wanyonge,” alimalizia Kwere kwa lafudhi ile ya utani wao wa kila siku, kuvuta maneno na kujaribu kutupia semi mbalimbali za maneno ya Kiswahili, lakini siku hiyo Bigambo hakuwa sawa kabisa. Kwere aliondoka na kumuacha Bigambo akiwaza hili na lile kichwani mwake juu ya namna gani aanze kuishi na wale watu wa ofisini kwake. Ni kweli waliwahi kumuumiza kwa mambo mengi sana lakini kwa hili lilikuwa pigo kubwa kwani kumsemea kwa meneja kwamba ana uhusiano usiofaa na Vivian ilikuwa ni kumharibia kwa sehemu zote mbili. Kwamba anaweza kutimuliwa kazi na kumkosa Vivian ambaye alikuwa amemuonjesha penzi tamu kuwahi kupewa tangu aanze kujihusisha na masuala hayo. Wakati Bigambo akiwazua hayo, ghafla simu yake iliita na alipoitazama kwenye kioo, ilikuwa namba ngeni na akaipokea harakaharaka na kuiweka sikioni huku akisikilizia ni nani alikuwa amempigia na alikuwa na ishu gani. Mpigaji wa simu ile alikuwa Vivian, aliamua kumpigia kwa namba ngeni akiwa na maana kubwa sana. “Enhe, imekuwa hivyo tena? Ayaa kwa nini Vivian? Yeye amekuambiaje?” Bigambo aliuliza kwa hamaki baada ya kuambiwa maneno f’lani na Vivian yaliyochoma moyo wake kwa ncha kali ya kisu chenye moyo mkali.
BIGAMBO alihamaki mno. Maneno ya Vivian yalikuwa yamemuondoa kabisa kwenye mudi ya kufanya chochote. Alichokifanya ni kuzungumza na mmoja wa viongozi wake na kumuomba ruhusa ya kwenda nyumbani kupumzika akisingizia kichwa kinamuuma ingawa ukweli ni kwamba alikuwa na msongo mkubwa wa mawazo.
***
Baada ya kutoka kwa meneja, Vivian alikuwa amechanganyikiwa kupindukia. Tangu aanze kujihusisha na masuala ya mapenzi, hakuwahi kufikishwa kwa kiongozi wake wa kazi hata kabla ya kuanza kufanya kazi hapo. Aliifikiria aibu atakayokumbana nayo pale ofisini endapo suala la kuitwa kwa meneja litawafikia wafanyakazi wenzake.
“Lazima nifanye uamuzi mkubwa bila kujali utamuumiza nani na kwa kiwango gani, lazima niachane na Bigambo na sitaki tena kujihusisha na mapenzi na mfanyakazi mwenzangu kuanzia leo,” Vivian aliwaza huku akishika simu yake na kumpigia Bigambo kwa namba ambayo hakuwahi kumpigia nayo na kumueleza ukweli ambao alitarajia kukutana na lawama lakini hakujali sana kwani alikuwa ameamua kutoka moyoni kwamba ni lazima aachane na Bigambo.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Bigambo aliondoka akiwa na mawazo mengi kichwani mwake. Hakujua ataishije bila Vivian licha ya kwamba walikuwa na muda mfupi sana tangu wafahamiane na kupeana penzi mara moja, lakini mahaba ya mwanamke huyo kutoka Tanga yalimkolea sana kijana wa watu.
“Nitaishije mimi bila huyu mwanamke? Mimi ni kidume, nitambembeleza kwa kila njia kuhakikisha namuweka sawa tena kwenye himaya yangu, siwezi kuruhusu kirahisi hivi aniache, siwezi hata kidogo,” Bigambo naye alipangilia mawazo kichwani huku akidandia daladala, tayari kwenda nyumbani kujilaza ili apunguze mawazo.
Alilala hadi mchana ambapo aliwasha simu yake aliyokuwa ameizima tangu afike nyumbani. Meseji zilianza kumiminika moja baada ya nyingine kutoka kwenye mtandao ukimjulisha namba ambazo zilikuwa zimempigia akiwa amezima simu, namba ya Vivian ilikuwa miongoni mwa namba hizo.
“Mmmh,” Bigambo aliguna kwanza huku akishindwa kuamini kama ni kweli Vivian alikuwa amempigia tena licha ya kumwambia maneno ya kuachana tena kwa sauti kavu isiyokuwa na masihara hata chembe.
“Amenipigia kweli? Anataka kuniambia nini zaidi ya kuniumiza zaidi? Ngoja nimpigie nisikie tena anachotaka kuniambia lakini kama ni yaleyale ya kusisitiza kwamba ameachana na mimi sitampa nafasi ya kumsikiliza, sitaki maumivu tena nikiwa najiandaa kumrejesha, Bigambo aliwaza moyoni na kumpigia Vivian ambapo alikuta namba ikiwa inatumika, hivyo alilazimika kusubiri kwa muda.
Aliagiza chakula na wakati ananawa, simu yake iliita na alipoitazama aliona jina la My Vivian, kama alivyokuwa amelihifadhi kwenye orodha ya majina yake ya simu. Moyo ulimlipuka na kujikaza kiume ambapo aliipokea simu kwa nidhamu zote akijiandaa kusikia lolote kutoka kwa mwanamke huyo mrembo.
“Salama kabisa, nakusikiliza Vivian,” Bigambo aliharakisha ili kujua lengo la Vivian kumpigia tena simu.
“Nilikuwa nimelala ndiyo maana nikazima simu.”
Licha ya kujiapiza kwa dhamira ya kweli kwamba hataki tena mapenzi na mtu wa ofisini, moyo wa Vivian ulikuwa bado na hisia za kimapenzi kwa Bigambo, mwanaume ambaye alimuonesha upendo wa kweli kabisa na hata kwenye uwanja wa fundi seremala, alikuwa akijiweza vilivyo.
“Hapana, zilikuwa ni hasira hizo, naomba tuonane tuzungumze tena ili tuone tunafanyaje, tafadhali naomba my love, nakupenda sana Bigambo nimeulizia nikaambiwa umeomba ruhusa ya kwenda nyumbani kwa kuwa unaumwa kichwa, naomba nije nikuone mpenzi wangu, nakuja sasa hivi nikifika hapo Riverside nitakupigia unielekeze nyumbani kwako,” Vivian alisema mfululizo bila kumpa Bigambo nafasi ya kusema chochote na kisha kukata simu, jambo ambalo lilimuacha njia panda kijana wa watu.
“Duh! Huyu demu kiboko aisee, mbona hii ni ajabu sana? Yaani ametoka kunitamkia maneno makali muda siyo mrefu akinitaka niachane naye halafu sasa hivi anataka tuzungumze tena na anadai ananipenda sana, mapenzi ni kitu cha ajabu sana jamani,” Bigambo alijisemea moyoni huku akifurahi kimyakimya.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Dakika 45 baadaye, simu ya Bigambo iliita tena na alipoitazama mpigaji alikuwa ni Vivian, akatabasamu na kuipokea haraka sana.
“Umefika? Basi njoo hadi pale pa siku ile nitakufuata nikupeleke nyumbani,” Bigambo alijibu na kuanza kujisogeza kwenye ile baa waliyokaa na Vivian kwa mara ya kwanza walipokutana kwa ajili ya mazungumzo na kuishia kufanya kweli.
Vivian alitembea kwa haraka, moyoni akiwa na shauku ya kumuona tena Bigambo. Nafsi ilikiri kabisa kwamba alimpenda mno mwanaume huyo, ingawa walikuwa na muda mfupi tangu wakutane. Muda mfupi alifika na kumfahamisha Bigambo ambaye alifika na kumchukua hadi nyumbani kwake.
“Pole kwa kuumwa na kichwa baba,” Vivian alianza mazungumzo kwa maneno hayo huku akimshika kichwani Bigambo, ambaye alibaki ametulia kimya bila kupinga chochote.
“Lakini Vivian, mbona umeniumiza sana moyo leo, ni kwa nini uliamua kunieleza maneno makali namna hiyo?” Bigambo naye alijibaraguza ingawa moyoni alifurahia sana kitendo cha Vivian kumtafuta na hatimaye kukaa pamoja, tena ikiwa chumbani kwake.
“Tuachane na hayo baba, ndiyo maana nimekuja tuyamalize, unajua maneno ya meneja yalinichanganya sana na kujikuta nikijawa na hasira kali lakini baada ya kutafakari kwa kina nimegundua kwamba nakupenda sana mpenzi wangu na kamwe siwezi kuishi bila penzi lako, nisamehe kwa kukuumiza baba yangu, sitarudia kweli tena,” Vivian alisema huku akimpapasa Bigambo kichwani na kuyachezea masikio kwa kuyaminyaminya na kuyakanda, kitendo kilichoanza kuamsha hisia za mambo f’lani kwa Bigambo.
“Sawa, nimekuelewa lakini siku nyingine tusiumizane hivi bwana, sawa mama?” Bigambo alisema ingawa sauti yake ilitoka kwa tabu kutokana na kuanza kuelemewa na mahaba mazito.
Ili kutoonekana goigoi au mshamba wa mambo hayo, Bigambo naye alianza kujibu mashambulizi kwa Vivian. Alipeleka mkono wa kulia shavuni kwa Vivian na kuanza kupapasa taratibu lakini hakuishia hapo na badala yake alihamishia kiganja shingoni na kuwa kama anacharaza gitaa, kufikia hapo Vivian akaanza kufumba na kufumbua macho kwa tabu kama anayenyemelewa na usingizi mzito.
“Oooh, baba jamani,” Vivian alianza kulalamika na kujikunjakunja huku naye akiendelea na zoezi la kupashana joto. Ilifika mahali mpambano ulikolea na kwa pamoja wakajikuta wakiwa hoi na kilichoendelea kilimtosha kila mmoja wao.
Mtanange aliouonesha Bigambo kwa Vivian haukuwa wa nchi hii. Alifanya kwa makusudi ili arejeshe adabu na kweli alifanikiwa kwani alifanya kwa kiwango ambacho hata yeye alishangaa mno.
Baadaye walipitiwa na usingizi mzito ambapo walishtuka ikiwa ni saa mbili kasoro dakika kadhaa usiku. Bigambo akitarajia baada ya kukurupuka, Vivian angeanza harakati za kuondoka, lakini ndiyo kwanza mama wa watu akaendelea kujilaza huku akijibaraguza kwa maneno yasiyokuwa na msingi wowote.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Niambie my love,” Vivian alisema huku akimshika Bigambo kichwani na kuzichezea nywele ambazo zilikuwa zinaanza kuota kwa mbali.
“Nakusikiliza mama yangu,” Bigambo alijibu akitarajia kusikia neno la ‘nataka kuondoka’ kutoka mdomoni kwa Vivian, lakini alichokisikia ni kingine kabisa.
“Tunakula nini usiku huu kabla ya kulala mume wangu?’ Vivian aliuliza swali ambalo Bigambo hakulitarajia kabisa na kujikuta akitabasamu.
“Wewe unataka tule nini?” Bigambo naye alimuuliza.
“Nakusikiliza wewe baba.”
“Kwani unalala hapa?” Bigambo aliamua kutoa dukuduku lake.
“Ndiyo mume wangu au hupendi nilale na wewe jamani, sema basi niondoke?” Vivian alisema na kuinuka kabla ya kukaa sawa kitandani na kumtazama Bigambo kwa jicho la kusikilizia jibu lake.
Kabla Bigambo hajajibu chochote, ilisikika sauti ya jirani wao ikimuita Bigambo.
“Wewe Bigambo wewe?”
“Naam.”
“Njoo kuna mgeni huku nje.”
“Ni nani huyo?”
“Wifi amekuja,” sauti ya nje ilisikika na hapohapo Vivian akamtazama Bigambo kwa hamaki huku akishindwa kuamini alichokisikia.
“Unajua Mungu anatuvumilia kwa mengi sana, mama yangu vile, wewe niamini mimi,” Bigambo alikomelea maneno hayo yasiyofaa na kusikilizika kwa mtu mwenye akili timamu isipokuwa mlevi tu mwenye kuzidiwa na kimea kikali.
“Kweli eeh, unajua kila nikikuangalia nakutafakari sana na kuona kama wewe siyo binadamu wa kawaida, yaani nakuona kama kiumbe cha ajabu au mtu aliyewahi kuzaliwa, akafa na kufufuka tena, yaani unaishi kwa mara ya pili,” Vivian naye alijibu maneno ambayo waliokuwa wamekaa meza ya jirani kwakinywa maji na soda walianza kucheka kufuatia maneno ya Vivian kutoka kwa mpangilio usioeleweka.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakati wakiendelea kunywa, ghfla kuna mtu alisimama mbele yao na kumshika Vivian bega na kumuuliza alikuwa akifanya nini hapo na aliyekuwa amekaa naye ni nani kwake? Mkononi alikuwa na kitu kilichowashtua wote wawili.
VIVIAN aliamka kabisa na kubaki ameshika kiti kwa mkono mmoja. Midomo ikimtetemeka kwa hasira isiyosimulika. Mtu aliyekuwa amesimama mbele yao alikuwa ni Jisu, yule fundi aliyemtengeneza mlango siku ya ugomvi wake na mzazi mwenzake, na mwisho wa siku wakaishia kushiriki dhambi tamu kutokana na kuzidiwa na kushawishiwa na vimea vya Reds na Nyagi.
Mkononi mwa Jisu kulikuwa na mzinga mkubwa wa nyagi, tena ikiwa haijafunguliwa lakini kwa macho ya harakaharaka ni kwamba Jisu alikuwa chakari kwa ulevi kwani hata ongea yake iliashiria jambo hilo kwa uwazi kabisa na pia hakuacha kuyumba na kujiweka sawa kila mara, alikuwa twiiiii, kama siyo bwiiiiiii achilia mbali bwaksiiiiii, maisha ya mitungi yana raha na karaha zake jamani.
“Sasa wewe umefuata nini huku?” Vivian alimuuliza Jisu huku akimtazama kuanzia chini hadi juu akimtathmini kwa namna alivyokuwa amevaa. Kwa kweli uvaaji wa Jisu siku hiyo haukuendana na Vivian kabisa, alikuwa amepigilia yeboyebo chafu, shati chafu na suruali chafu ambayo urefu wake haikufika hadi mwisho wa miguu, kifupi siku hiyo Jisu alikuwa hovyo sana hata kuelezea kwa maandishi nashinda, natamani ungekuwepo siku hiyo msomaji na kujionea mwenyewe lakini hata hivyo kwa maelezo hayo naamini tayari umeshapata picha kamili ya tukio lenyewe.
“Nakuuliza wewe halafu ni mambo gani haya ya kufuatanafuatana hadi huku baa au kwa sababu unanidai pesa yako ya mlango? Sema ni kiasi gani nikulipe uniondolee kiwingu chako hapa bwana huoni kama niko na mume wangu?” Vivian aliendelea kumdhiti Jisu kwa maneno mfululizo lakini moyoni akiomba Jisu asije akaropoka maneno makali ambayo yataanika ukweli wote kwamba licha ya kumuonesha dharau zote hizo lakini Jisu alishaonja asali ya Vivian na sasa alikuwa akitafuta njia ya kuchonga mzinga mzima kabisa.
“Ina maana kweli leo hii unakuwa na maneno makali namna hiyo kwangu? Ama kweli nyie wanawake ni watu wa ajabu sana, haiwezekani tukiwa kitandani unakuwa unanibembeleza kwa maneno makali yenye ushawishi mkubwa sana na heshima tele lakini leo unaniona kama takataka eti kwa sababu nimekukuta una mwanaume mwingine ambaye kwangu ni boya tu,” Jisu alianza kuropoka na mbaya zaidi alikuwa akitoa maneno hayo kwa sauti kubwa na kuwafanya watu wa meza zingine waache kwa muda kile walichgokuwa wanaongea na kufanya na badala yake wakaelekeza masikio yao kwenye meza ya akina Vivian ili kuambulia uhondo zaidi kutoka kinywani mwa Jisu.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Unasemaje wewe? Umechanganyikiwa nini? Hebu tupishe hapa unatuletea kiwingu tu wenzio tuna stress za maisha maana wewe kila kitu kwako kiko sawa tu kwa kuwa huna majukumu ya kifamilia zaidi ya starehe,” Vivian alikomelea msumari wa kummaliza nguvu Jisu.
Wakati wote huo Bigambo alikuwa kimya akisikilizia maneno ya wote wawili. Moyoni alibaki njia panda asijue ukweli ni upi na uongo ni upi kwenye majibizano ya Vivian na Jisu lakini kama mwanaume aliona kabisa kukaa kimya isingekuwa busara na hata majirani waliokaa karibu naye achilia mbali wahudumu wangemshangaa sana kwa kushindwa kuonesha uanaume wake.
“Kwani huyu ni nani?” Bigambo aliuliza bila kuwatazama wote machoni lakini kwa asili ya swali lenyewe, ilikuwa ni rahisi kabisa kugundua kwamba swali lile lilimlenga Vivian atoe ufafanuzi wa kina juu ya ujio wa Jisu.
“Brother sikiliza, mimi siyo kwamba nimelewa au siyo, lakini ukweli ni… niiii…..niniiii kwamba huyu mwanamke huyu hajatulia kabisa hata kidogo na nitaeleza yote hapahapa leo lakini sema nini, wewe endelea kuwa naye lakini kaka hauko peke yako na mimi nilishakula mzigo tena kwa mazingira ya ajabu ajabu sana yaani kifupi ni kwamba mwanamke huyu ni zaidi ya maharage ya Lindi achana na yale ya Mbeya,” Jisu aliporomosha maneno hayo yenye kuumiza na kumfanya Vivian abaki kimya tena akiwa ameinamisha uso kwa aibu.
“Mimi nilijuana naye siku ya ugomvi wake na mwaname aliyezaa naye na kwa sababu kulitokea na fujo hadi za kuvunjiana mlango mimi sikuwepo lakini kwa kuwa watu wanajua mimi ni fundi, wakaniita na kumtengenezea mlango, lakini wakati naanza kufanya matengenezo, aliniaga kwamba anafuata pombe ili wakati natengeneza akute anatuliza mawazo na akaamua kuninunulia na mimi mzinga wangu kama huu, lakini tuliapoanza kunywa tu, akiwa na nusu chupa akaanza kuonesha udhaifu mkubwa kwa kunitega kwa mapozi na maneno matamu sasa bro kama unavyojua na mimi ni mwanaume niliyekamilika unadhani nini kilitokea, njiwa alijileta mwenywe, nikachinja lakini tukiwa ndani aligongewa na mjumbe wetu wakaongea hapo nje, nikapata nafasi ya kuchungulia nikawaona wakifanya uchafu wao bandani kule uani, sasa huyu ni mwanamke ndugu na wewe umekaa naye kwa kujiachia kabisa,” Jisu aliamua kumwaga ugali wote baada ya Vivian kuanza kwa kumwaga mboga.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Maneno ya Jisu yalimwingia sawasawa Bigambo na kwa kutambua umuhimu wa Jisu, alimshukuru na kumuomba namba yake ya simu ili wazungumze kesho yake. Lengo la Bigambo kufanya hivyo ni kutaka kujiridhisha kama kweli Jisu ataweza kuyaongea hayo siku iliyofuata akiwa na akili zake timamu na ndipo achukue uamuzi mzuri, lakini moyoni alianza kuumia kama kweli yaliyosemwa na Jisu ni uhalisia mtupu.
Jisu aliaga lakini kabla hajaondoka alimgeukia tena Vivian na kumtazama usoni. Wote wakakutanisha macho, lakini Jisu aliachia tabasamu la kilevi bila kujua kabisa kwamba alichokifanya kilikuwa ni zaidi ya mauaji ya halaiki. Kumchomea Vivian kwa Bigambo, mwanaume aliyempenda kwa moyo wa dhati lilikuwa ni pigo jingine mujarabu kwa Vivian.
“Mimi naondoka, lakini tafadhali sana antiii, usinielewe vubaya na huu usiwe mwisho wa penzi letu, naomba sana ulilinde penzi hili na hakika nitafurahi sana kama ukinishusha Ununio, hahahaha,” alisema Jisu na kumalizia kwa manenon hayo ya kicheko cha kujilazimisha kilichoungwa mkono na wateja wengine kwenye meza za jirani, ambao walishaanza kukubaliana na maneno ya Jisu kama kweli Vivian hakuwa mwanamke aliyetulia na ndiyo maana hakubisha chochote kuhusiana na maneno ya Jisu.
***
Ofisini maneno yalianza kuenea kuhusiana na meneja kuwaita Vivian na Bigambo ofisini na kisha kuwaonya kuhusiana na mahusiano yao. Watu walifurahia sana kwani asili ya watu wa ofisi ile ni kwamba walifurahia sana kuona mtu akipatwa na matatizo ingawa wakiwa naye huonesha upendo na huruma lakini hayo yote huwa ni unafiki mkubwa kabisa.
“Oya, kimenuka tena kwa jamaa yenu,” Neymo, kijana mdogomdogo aliyekulia maisha ya uswahilini yenye maneno mengi ya kitaa, alianzisha mjadala huo wakati wa kifungua kinywa akiwa na rafiki yake Elino, kijana ambaye waliendana kwa tabia na matendo kwa kujiona kama wajuvi wa mambo na wakali wa kitaa.
“Eeh mwanangu, jamaa haishiwi na majanga kabisa na kwa hili tuone kama atachomoka tena,” Elino alishadadia wakimnanga Bigambo ambaye alikuwa ameonywa na meneja kwa tabia ya kuonesha hisia za kimapenzi na Vivian ikiwa ni kinyume kabisa na maadili ya kazi. Lakini wakati wanajadili, ghafla aliingia Bigambo akiwa amejawa na huzuni kubwa huku uso wake ukichakazwa na machozi.
Wote walishtuka na kumzunguka Bigambo. Kama nilivyosema , wengi wao walikuwa wanafiki wakimuoneshea huruma machoni lakini moyoni wakimcheka kwa dharau na dhihaka kubwa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nini tena mshikaji wetu? Nini kimekukuta wangu?” Darwin mmoja wa wafanyakazi wenzake na Bigambo ambaye kwa umri alikuwa mtu mzima licha ya mwili wake kuonekana kijana alimfariji kwa upendo mkubwa na kutoka moyoni mwake, hata Bigambo mwenyewe hakuwa na shaka na upendo wa Darwin.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment