Search This Blog

Monday, October 24, 2022

KANGA MOJA KIUNONI...MBENGEMBENGE - 5

 







    Chombezo : Kanga Moja Kiunoni...Mbengembenge

    Sehemu Ya Tano (5)



    ILIPOISHIA  Mfaume alibaki akitoa macho na mdomo wazi huku akiangalia umbo lile la mama Mei, umbo alilolifaidi usiku kucha, hakuamini hata kidogo maneno ya mama Mei kama kweli mumewe amesharudi. SASA JIACHIE MWENYEWE... ALICHOKIFANYA alipiga hatua kama mtu anavyonyatia kwa kumfuata mama Mei kwa nyuma lakini kabla hajaufikia mlango wa mama Mei, mlango ukafunguliwa, baba Mei akachomoza. “Umeshaniwekea hayo maji bafuni?” Mama Mei akabaki na kigugumizi akijishikashika vidole huku akimwangalia Mfaume kisha akarudisha macho na kumuangalia mumewe... “Yapo tayari bafuni,” alisema. Baba Mei alishangazwa na hali ile ya mkewe, lakini hakumuuliza wala kujihoji sana mwenyewe, alijiandaa akaenda kuoga... “Nimegundua huyu

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mfaume ni kimeo naye... sasa namwambia pale halafu haamini, anatakaje?” alijisemea moyoni mama Mei. Mume wake, alikwenda kuoga, akarudi ndani na kuendelea na maisha ya nyumbani... “Mke wangu niambie, habari za hapa?” “Njema mume wangu, pole na safari...” “Nimepoa sana. vipi maisha ya siku mbili tatu?” “Maisha yapo salama baba Mei, nilikumisi sana yaani...” “Mimi je, hapa naomba jiandae uje kitandani,” alisema baba Mei huku akielekea chumbani akiwa ndani ya taulo... “Sawa mume wangu, nakuja.” Baba Mei alipofika kitandani alilala akiangalia juu. Uchovu alikuwa nao lakini pia alipenda kumpa burudani mkewe kwani ni siku kadhaa zilipita tangu aondoke. Mama Mei yeye, hakuwa kivile kwani tangu mume wake aondoke, alishadondoka na mzee mwenye nyumba na usiku wa kuamkia siku hiyo alidondoka na Mfaume. Kwa

    hiyo hakuwa mhitaji sana, ila asingeweza kujionesha. Alijiandalia maji, akaenda kuoga kisha akarudi chumbani akiwa amefunga mlango mkubwa ili asitake bughudha na mtu. Alipanda kitandani mama Mei, akambusu mume wake, akamwambia anampenda sana... “Hata mimi nakupenda sana baby,” alisema baba Mei. Walishikana, wakakumbatiana, wakapigana mabusu mpaka ikafika mahali, kila mmoja akawa moto tayari kwa mpambano wa mechi. Kazi ilikuwa nzito kwa baba Mei lakini kwa uzoefu wake, hakumwona mkewe kama alimmisi sana kama inavyokuaga mara nyingi anaposafiri nje ya nyumbani kwa siku kadhaa... “Mh!” Aliguna baba Mei... “Vipi mume wangu, nini kinakugunisha?” mama Mei alimuuliza mumewe... “Hapana.” Lakini muda mwingi, baba Mei alikuwa akiguna mpaka ikafika mahali, mama Mei akaanza kuhisi kitu kutoka kwa mume wake kwamba,

    amemgundua kuwa, alichepuka akiwa hayupo! Mchezo ulikwenda hivyohivyo mpaka wakamaliza dakika za uwanjani..! *** Mzee Hewa alikuwa hajui lolote kuhusu ujio wa baba Mei. Yeye alijua ni amani tu. Usiku huo hakuwa tayari kulala bila kumpata mwanamke huyo. Na alitamani sana alale naye usiku kucha akijua atakubaliwa.   Aliamka mzee Hewa, maana alishapanda kitandani kujipumzisha kama siyo kulala. Akavaa msuli wake na singilendi kwa juu, akafungua mlango na kutoka. Alitembea kwa busara zake zote ili jamii nyingine inayoishia kwenye nyumba hiyo isijue lolote. *** Kwa upande wake, Mfaume alikuwa na wakati mgumu sana. Alijua toka moyoni mwake kwamba, baba Mei aliingia shaka kwa kitendo cha kumwona yeye amesimama jirani na mke wake... “Da! Ile ishu pale haikukaa sawasawa hata kidogo. Jamaa kama ameshtukia f’lani hivi. Ila

    inabidi kuwa kauzu. Kwani nini kitapotea kwangu?” alisema mwenyewe Mfaume. *** Mzee Hewa alishika kitasa cha mlango wa kwa mama Mei, akakizungusha lakini akabaini mlango huo ulifungwa kwa ndani. Akaamua kugonga. Alianza kugonga polepole mwishowe kwa sana ili asikike kule chumbani aliko... “Nani anagonga?” aliuliza baba Mei... “Mh! Sijui nani?!” mama Mei alijibu akiamini hawezi kuwa mtu anayemtafuta yeye pia akawa anajiandaa kutoka kitandani... “Ngoja niende mimi,” alisema baba Mei akitoka kitandani. Alivaa taulo, akaenda kufungua mlango huku akiwa hajui atakutana na sura gani. Kwachakwachakwacha, mlango ulifunguka. Hamadi! Sura ya baba Mei hii hapa Mzee Hewa akashtuka kwani wakati mlango unafunguliwa alishaweka sura ya tabasamu akijua atamwona mama Mei. Kwa hiyo alipokutana na sura ya baba Mei ghafla, alikunja sura ghafla...





    “HAA! Hujambo bwana mdogo?” mzee Hewa alisalimia huku uso wake ukiwa haujakaa sawasawa... “Sijambo mzee, shikamoo...” “Marhaba, za safari bwana?” “Ni njema mzee wangu...vipi, nikusaidie nini?” Mzee huyo alibabaika kwa mbali hali iliyomshangaza sana baba Mei...“Nilitaka kujua kama kuna gesi maana jiko langu la gesi lime...aaah! Nataka kuazima kibiriti kwa mama! Oooh! Nimepitiwa, kuna maji ya baridi ya moto? Ha! Mimi naye kwa kusahausahau sijambo kidogo...naulizia milango kama mmefunga.” Baba Mei alibaki akimtumbulia macho tu huku akijiuliza ni kitu gani kinamfanya mzee huyo ababaike kusema kama kweli aligonga mlango akiwa na shida ndani kwake... “Mzee wangu kwani kuna nini, sikuelewi...” “Haa! Nilikosea kijana kugonga kwako, nilikusudia mlango ule,” alisema mzee Hewa huku akiondoka kurudi kwake. Ile baba Mei anageuka tu, mama Mei anatoka chumbani... “Vipi, ni nani?” alimuuliza mume wake... “Ah! Mimi sijamwelewa mzee wako...nadhani kuna kitu zaidi ya ujio wake,” alijibu baba Mei huku akiingia chumbani moja kwa moja. Mama Mei naye alifuata na kumkuta mume wake akiwa amelala akiangalia juu kwa mawazo... “Yule mzee asitake kuleta longolongo, kwa vyovyote vile alimfuata mke wangu. Inaonekana hakujua kama mimi nimerudi,” alisema moyoni baba Mei... “Baba Mei kwani kasemaje?” “Nani?”

    “Mzee mwenye nyumba?” “Ah! Mimi sijamwelewa hata kidogo. Kwanza nahisi shida yake kubwa ni wewe ila mimi niliingilia kwa bahati mbaya tu...” “Kwani amesemaje?” “Hakuna kilichoeleweka... alipokutana macho na mimi, kwanza akashtuka sana. baada ya salamu akaniuliza habari za safari nikamwambia nzuri, akasema nilitaka kujua kama kuna gesi maana jiko langu la gesi lime...akasita, kisha akasema nataka kuazima kibiriti kwa mama! Akaacha, akasema oooh! Nimepitiwa, kuna maji ya baridi ya moto? Pia akaacha akasema naulizia milango kama mmefunga...” “Khaa! Ndiyo nini sasa?” aliuliza mama Mei huku akionesha kushangaa. Lakini moyoni alijua moja kwa moja kwamba, mzee huyo alikuwa na shida na yeye ila hakujua kama mume wake alisharejea... “Mimi sijui ndiyo nini!” alisema kwa mkato baba Mei na kugeukia kwingine hali iliyompa ishara mkewe kwamba, kuna jambo mumewe amejifunza kuhusu ujio wa mzee mwenye nyumba.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mama Mei alibaki kimya. Alitamani sana kumsemesha mume wake lakini angemsemesha nini wakati mumewe amehisi jambo? Kumsemesha kungemfanya ajulikane kwa undani zaidi. Usiku wa manane, baba Mei alishtuka na kujikuta akimuwaza mzee Hewa, lakini pia akapata na mawazo kuhusu ule ukaribu aliouona kati ya mkewe na mpangaji mwenzao, Mfaume... “Inaonekana kuna kitu kilikuwa kikiendelea wakati mimi sipo. Mbona huyu mke wangu kama amekuwa mwenyeji sana na hawa watu?” alijiuliza. Kitabia, baba Mei si mtu wa kukurupuka! Mambo yake mengi hupenda kuyafanya kwa polepole na utaratibu huku akihakikisha kama ni jambo analipata kwa ukamilifu akitumia mahesabu ya mwaka! Alijichanga akili, akaamua kuweka mtego wa makusudi ili kujua kama kweli mke wake ana jambo la ziada au la, ni mawazo yake tu! *** Kulipokucha, mama Mei alitoka kitandani na kuendelea na kazi nyingine za kila siku za nyumbani kwake.

    Asubuhi hiyo, alikuwa amekunja sura vibaya sana. hakumchangamkia mtu yeyote ndani ya nyumba ile maana alijua wanataka kumweka pabaya! Baba Mei alipoamka, alikwenda kuoga na kurudi ndani. Alivaa, akaenda sebuleni kunywa chai! Hapo alimwita mkewe... “Abee...” “Njoo mara moja.” Mama Mei alipofika alikaa akimwangalia mume wake kwa macho yaliyojaa wasiwasi... “Mimi jioni leo nasafiri tena, nakwenda Tanga halafu Arusha,” alisema baba Mei kisha akamwangalia mkewe ambaye aliachia sura ya tabasamu kutoka ile ya wasiwasi... “He! Yaani unaunga mume wangu?” “Ndiyo kazi sasa mke wangu, nitafanyaje?” “Kweli lakini,” alisema mama Mei huku akiachia tabasamu pana... “Kwa hiyo nilitaka ulijue hilo tu mke wangu maana nikiondoka nikirudi jioni ni safari,” alisema baba Mei na kuendelea kunywa chai... “Sawa mume wangu, safari njema,” alisema mama Mei naye huku akiondoka. Baba Mei alimwangalia mkewe akatingisha kichwa huku moyoni akisema...



    “UNGEJUA siendi kokote na leo lazima ukweli ujulikane wala usingenitakia safari njema. Halafu utanitakiaje safari njema kabla sijaondoka? Hii inaonesha furaha yako ilipo.” *** Ilikuwa jioni ya saa kumi, baba Mei alisharudi na sasa alikuwa akiondoka zake kwa safari kama alivyomwambia mama yake asubuhi. Mama Mei alimsindikiza hadi nje kwenye gari ambako pia alikuwepo mzee Hewa na Mfaume wakiongea kabla ya Mfaume hajatoka kwenda zake kazini... “Jamani nasafiri kidogo, nitakuwa sipo kwa siku kama nne hivi,” alisema baba Mei huku macho yakiangalia pembeni kabisa kwa vile hakuwa na mazoea ya kusema uongo mkubwa kama ule. Mzee Hewa na Mfaume wakaonesha furaha ya waziwazi wakimtaka Mungu amtangulie... “Sawa bwana, safari njema, sisi tupo tu tunasogezasogeza maisha na uzee huu,” alisema

    mzee Hewa akijifanya amechoka kwa umri ilimradi asifikiriwe vibaya maana, lile tukio la jana yake usiku kwenda kugonga mlango wa mama Mei kisha aliyetoka ni baba Mei akakosa cha kusema, bado lilikuwa likimtokota moyoni kwa dhamira mbaya... “Haya, nashukuru sana mzee Hewa...” “E bwana uende salama, sisi tupo kama hivi, tukitoka asubuhi hii kurudi usiku...da! hizi kazi bwana,” alisema Mfaume, naye aliamua kusema hivyo ili kujenga mazingira yenye kuweka amani kwa baba Mei. Mama Mei alisimama kwenye mlango wa gari, akawa anaongea na mumewe maneno ya mwishomwisho kabla hajaianza safari... “Nitakumisi sana darling, nitakukumbuka. Lakini nakuombea kwa Mungu, akutangulie katika safari yako, iwe njema na mwisho kabisa uhakikishe unasali kabla ya kulala ili kumwomba Mungu akulinde, lakini mwisho kabisakabisa usikose kuwasiliana na mimi mkeo ujue naendeleaje lakini mwisho kabisakabisakabisa take care,” alisema mama Mei na kumbusu mumewe...

    “Mmmm...mwaaa...” “Mmm...mwaaaa...aaa,” alirudishia baba Mei, akawasha gari na kuondoka. Nje ya nyumba alikuwepo mzee Hewa tu, kwani Mfaume alishaondoka zake kwenda kazini. Na alikuwa akienda huku njiani akisema moyoni kwamba, siku ile ndiyo nzuri kwa kulala na mama Mei mpaka kunakucha kama jana yake... “Lakini jamaa namuonea kwelikweli, yaani akiwa hayupo tu, mke wake anakuwa msosi wangu...aisee mi kama ni hivi sioei. Uaminifu ni sifuri kabisa,” alisema moyoni Mfaume. *** “Sasa naona mambo mazuri,” mzee Hewa alimwambia mama Mei... “Halafu we mzee Hewa umenikera sana jana usiku,” mama Mei alikumbuka... “Kuhusu nini binti mzuri?” “We unakujaje kugonga mlango kwangu bila kuchunguza kwanza bwana...” “Mimi sikujua kama mwenye mali karudi. Usipige kelele sana binti, mishipa itapasuka bure ufe tukupoteze binti mzuri kama wewe. Ningejua mmiliki karudi hapa mlangoni nisingepita achilia mbali kugonga mlango,” mzee Hewa alisema akiingiza na

    kautani kwa mbali, mama Mei akajikuta akiachia kicheko na si tabasamu... “Haya...haya...sasa unasemaje?” “Nasemaje? Jana nilikumisi sana ndiyo maana nikaja kugonga. Walahi nimelala mwili wote unauma maana sikupata usingizi nilipokuta mwenyewe yupo...” “Kwa hiyo?” “Kwa hiyo? Kwa hiyo nini sasa, si ndiyo muda wetu huu?! Paka ametoka sasa ni nafasi yangu mimi panya.” Mama Mei akacheka huku akimpa mkono mzee huyo ili agonge, akagonga waaa! “Sasa mzee Hewa?” “Nakusikiliza wewe...” “Mimi naingia ndani,” alisema mama Mei... “Na mimi nakufuata nyuma.” Kweli, mama Mei aliingia, mzee mwenye nyumba akamfuata kwa nyuma huku udenda wa mahaba ukimtoka kinywani. Mama alijua nyuma anafuatwa, alipofika kwenye usawa wa mlango wa mzee Hewa, akafungua na kuingia mwenyewe. Kitendo hicho pekee kilimfanya mzee huyo ajikute anataka kukata roho kwa tamaa...

    “Da! Mpaka anatangulia mwenyewe, watu tuna bahati zetu bwana,” alisema moyoni akifuatia kwa nyuma. Mzee Hewa alijiona bado kijana mbichi kuona mwanamke kama mama Mei anamshobokea, kwake ilikuwa ngekewa ya karne. Alifunga mlango, akamkuta mama Mei amesimama katikati ya sebule. Mzigo mzigo kweli, kila idara ilikamilika. Mguu uliokanyaga chini ulishiba kwa kuumbwa...kiuno kama cha mtu wa kuchorwa, kifua ni mwanamke mwenye kujielewa, usipime bwana... “Haa! Haa!” mzee Hewa alianza kuonesha uchu wake kabisa. Alimfuata na kumkumbatia kwa kumuweka kifuani mzimamzima. Mama Mei hakutaka kuonesha kwamba, hajakubali kukumbatiwa, akatoa ushirikiano kwa yeye naye kumkumbatia... “We mama Mei,” sauti ya baba Mei iliita kwa nguvu mlangoni kwake akiwa amesimama...

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MAMA Mei aliruka kutoka sehemu aliyosimama na kwenda kusimama sehemu nyingine na kusema... “Mungu wangu.” Mzee Hewa yeye alichoka kabisa, miguu ilianza kunyong’onyea yenyewe kwani alijua kuna kosa amelifanya... “Ilitakiwa nisubiri mpaka masaa yapite mengi ndiyo ningemuita ndani huyu mwanamke, nimefanya makosa sana,” alisema moyoni mzee huyo. Baba Mei aliendelea kuita akiwa ndani kwake sasa. Alishangaa kutomwona mkewe ndani, hadi chumbani. Mlio wa milango ilisikika ikifunguliwa ndani hali ambayo ilizidi kumuumiza mama Mei. “Sasa mzee Hewa itakuaje? Maana sijui kwa nini baba Mei amerudi?” alisema mama Mei akitetemeka. Hali ilizidi kuwa tete baada ya Mfaume naye kurudi muda huohuo na kukutana na baba Mei akitoka ndani kwake huku akiendelea kuita akienda uani... “Za saa hizi kaka?” alisalimia Mfaume... “Njema bwana...huyu sijui ameenda wapi? Kuna maagizo nataka kumpa nilisahau,” baba Mei alisikika akisema... “Au kaenda dukani...maana mimi nilimuacha wakati natoka kwenda kazini na nimerudi mara moja kuna kitu nimesahau,” alisema Mfaume akiwa hana shaka kwamba, mama Mei anaweza kuingia ndani kwa mzee Hewa. Ni kweli, kurudi kwa baba Mei muda huo ambao ni dakika chache baada ya kuondoka hakuingiliani na mpango wake wa kumuweka mtegoni mkewe huyo. Alitoka hadi nje akasimama akishikashika simu yake. Hakumpigia simu mkewe kwani aliikuta chumbani. Lakini kwa mbali, baba Mei

    alihisi jambo. Ni baada ya dakika tano kupita bila mama Mei kurudi. Alirejea tukio la mwenye nyumba wake huyo na kwenda kugonga mlango wake jana yake usiku... “Au...mh! Inawezekana kweli? Kwamba awe ameingia ndani kwa mzee mwenye nyumba?!” aliwaza mwenyewe baba Mei akiwa bado amesimama pale nje. Aliamua kurudi na kukaa sebuleni mahali ambapo, mkewe hata kama angekuwa amekwenda mkoani, ili arudi ilikuwa lazima apitie pale! Mfaume aliondoka zake akiwa hana hili wale lile kwake aliamini mama Mei alikwenda dukani au gengeni ambako angerudi na kumkuta mumewe amesharudi. “Mzee Hewa, itakuaje sasa? Mimi nahisi kuna mambo mazito sana,” alisema mama Mei kwa sauti ya chini kabisa wakiwa chumbani sasa maana pale sebuleni walipokuwa awali pasingewezekana. “Naona mimi nitokee nikaangalie mazingira, maana kama kuna ukimya au wewe unasemaje?” alishauri mzee

    Hewa... “Mh! Mkionana hawezi kujua kitu kweli?” mama Mei aliingia shaka kidogo... “Hawezi! Ataingiaje shaka wakati hajui kama upo kwangu?” “Haya nenda basi.” Mzee Hewa alitoka na wakati akifungua mlango wake, baba Mei alisikia, akatoka haraka kumchugulia... “Kumbe wewe mzee, namtafuta mama Mei, kuna maagizo nataka kumpa. Sijui kaenda wapi?” aliuliza baba Mei... “Labda kaenda shamba...Eh! Sorry kwani na yeye alikuwa hasafiri? Aah! Mimi naye, siku mbili hizi sijui nikoje! Nilitaka kukwambia huenda amekwenda dukani baba Mei.” “Mh!” Baba Mei aliguna kwanza, hakujua ni kwa nini mzee Hewa huchanganyikiwaga akiongea na yeye. Mzee huyo alipitiliza  mpaka nje, lakini hakuchukua muda, akarudi mpaka ndani kwake. Akafunga mlango kwa woga, akaenda mpaka chumbani kwake huku akihema... “Vipi mzee Hewa?” mama Mei alimuuliza... “Yaani mambo ni mazito sana binti...” “Kivipi?” “Nimejichanganya tena...” “Kivipi mzee Hewa jamani?”“Nimekutana na mumeo, akaniuliza wewe umekwenda wapi, kuna maagizo anataka kukupa, alisahau, nikamwambia labda umeenda shamba... akaguna!” “Jamani jamani mzee Hewa... sasa mimi tangu lini nikaenda shamba hapa mjini. Hata kama lingekuwepo kweli hilo shamba, ningeenda muda huuhuu wakati yeye ametoka?” “Nisamehe sana binti.” Mama Mei alianza kulia. Mumewe kule sebuleni, alibaki amekaza macho akiwaza hili na lile. Shaka kuhusu mzee Hewa iliongezeka mara dufu. Aliamini kwa asilimia tisini na tano kwamba, mkewe alikuwa ndani kwa mzee huyo kwa alivyomsoma. Hata kama angeambiwa aweke pesa ya mshahara kupingana na mtu kwamba, mkewe hakuwemo ndani kwa mzee Hewa, angekubali kuweka akijua yeye angeibuka mshindi... “Lakini tabu yote ya nini wakati sasa ukweli umejiweka wenyewe kuhusu mke wangu. Kwa nini nisiende kumgongea yule kikongwe nimwambie nina wasiwasi mke wangu yumo chumbani mwake? Akigoma nimlazimishe kuingia hata kwa mabavu, maana hana nguvu za kinizuia!” alisema moyoni baba Mei na kusimama kwenda. Alifika mlangoni, akagonga na kuita... “Ngo ngo ngo! Wenyewe!”



    ABA Mei hakuwa na wasiwasi wakati wa kugonga mlango huo kwani aliamini alichokiwaza ni kweli na kweli kabisa. Kazi ikawa kule chumbani, mama Mei na mzee Hewa walisikia sauti ya baba Mei kugonga na kuita ‘wenyewe’... “Mama weee! Mume wangu huyo anagonga,” alisema mama Mei huku machozi yakifika kwenye ncha ya kidevu chapuchapu! “Hebu tulia kwanza we binti, ngoja nikamfungulie, labda ana shida yake,” mzee Hewa alimwambia mama Mei huku na yeye akitetemeka... “Vipi, hajarudi shemeji?” Mfaume alimuuliza baba Mei alipomwona amesimama mlangoni kwa mzee Hewa akiwa amerudi kwa mara ya pili baada ya kuondoka na kurudi. Alikuwa amesahau kitu kingine...

    “Hajarudi bwana, ndiyo nataka kumwachia maagizo huyu mzee akirudi ampe mimi naondoka,” alisema baba Mei maneno ambayo yalifika hadi ndani kwa wawili hao wakapata nguvu kwamba, kumbe alikuwa akigonga ili aache maagizo kwa baba mwenye nyumba. Mzee Hewa alikwenda kufungua mlango haraka sana huku akiachia tabasamu tayari kwa kuchukua maagizo. “Kwacha...kwacha...kwacha,” mzee huyo alifungua mlango wake kwa komeo. Alikutana macho na baba Mei, akazidisha tabasamu na kusema... “Karibu sana baba Mei.” Wakati huo, Mfaume alikuwa ameshachukua alichokitaka na sasa anaondoka zake na alikuwa akifunga mlango... “Mzee Hewa,” alianza kwa kuita baba Mei... “Ndiyo bwana, nakusikiliza...” “Naomba umtoe mke wangu haraka sana kabla sijaingia mwenyewe ndani,” alisema baba Mei akitumia sauti ya upole sana lakini yenye kila dalili ya hasira na maumivu ya wivu... “Khaa! Kwani amesema yupo ndani kwake?” “Yupo ndani kwako, ndani kwake wapi sasa we mzee,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    umeanza kunichanganyia maneno kama kawaida yako siyo?” Mzee Hewa alianza kutetemeka, alijua kimenuka! Kumbe alichofikiria sicho. Kwa upande wake, Mfaume aliposikia maneno ya baba Mei hakutoa hata mguu mmoja pale mlangoni, aliendelea kusimama kusikia kilichopo... “Mh! Mbona madai makali sana! Ina maana huyu mzee anaweza kuwa na uhusiano na mama Mei kweli?” alijiuliza Mfaume. Yeye lengo lake lilikuwa kuhakikisha kama kweli, mama Mei anaweza kuwa na mzee huyo. Kwa uzee wake, na ujana wa mama Mei na sura yake ya utoto wa mjini na ujanja haikuwa rahisi kwa Mfaume kuamini kwamba, wawili hao wanaweza kuwa wapenzi. Kule chumbani, mama Mei alisikia kila kitu kwani mlango wa chumbani kutokea sebuleni ulikuwa wazi. Mwili wake ulilowa jasho la wasiwasi na woga. Usaliti ulimtafuna waziwazi, akakumbuka nyumba kadhaa walizoishi na mumewe huyo tangu wafunge ndoa, hazikukosa kelele za usaliti, baba Mei akimtuhumu mkewe

    huyo. Mzee Hewa aliganda mlangoni, ikabidi Mfaume aingilie kati kwa kushauri... “Mzee, kama ni kweli mtoe mke wa watu, kama si kweli mwambie si kweli.” “Si kweli, hayupo,” alisema mzee Hewa kwa nusu kujiamini... “Basi mwingize mpaka chumbani kwako akahakikishe mwenyewe kwa macho yake. Maana unaweza kusema si kweli yeye akaona unamdanganya,” alisema Mfaume kwa sauti ya kimbeyambeya huku uso wake ukiwa kama anayesema... “Leo nitaona mengi.” Baba Mei alimsukuma mzee huyo bila kutaka kuweka mjadala mrefu kwani kwa uzoefu wake na usomi wake, alishajua mzee Hewa anaujua ukweli kuhusu mkewe... “Wewe mkeo hayupo humu ndani bwana...unanionea tu... toka...kama ni kodi ya nyumba naomba nikurudishie uhame mara moja,” alisema mzee huyo akimfuata kwa nyuma. Baba Mei hata kabla hajafika chumbani, mama Mei alianza kulia kwa sauti... “Nisamehe mume wangu... naomba msamaha sirudii tena jamani! Ooo! Shetani wewe

    ni kwa nini mimi tu?” alisema mwanamke huyo. Sauti yake ilitoka mpaka nje, ikamfikia na Mfaume... “Hee! Ina maana kweli?” alijiuliza Mfaume... “Umenichosha we mwanamke. Hufai na wala hutakuja kufaa hata siku moja...unafanya mambo kama mtu mwenye akili pungufu! Hujitambui, hujifahamu wala hujihurumii,” baba Mei alimvurumishia maneno mazito na makali huku akimuwasha makofi kama siyo vibao... “Jamani basi....basi jamani! Baba Mei basi bwana, namna hii unaweza kuua hivihivi,” Mfaume alisema baada na yeye kuamua kuingia mpaka chumbani... “Hapana bwana, huyu mwanamke kusema ule ukweli ni matatizo juu ya matatizo... mimi ndiyo najua kila kitu. Kuaga kwangu kwamba nakwenda safari haikuwa jambo la kweli, nilitega tu,” baba Mei aliamua kufunguka... “Hodi nyumba hii,” sauti ya Jombi ilisikika akiingia...



    SAUTI ya Jombi ilionesha au kuashiria kwamba alikuwa chicha kwa pombe kwani ilitoka kwa kukatikatika. “Karibu,” Mfaume ndiye aliyeitikia hodi ya Jombi.

    Wakati akipita kwenye korido, Jombi alikuwa akipepesuka na kuyumba huku akitema mate chini na kushikwa na ile hali ya kutaka kutapika, walevi wanajua... “Iiik...ikiii!” alifanya hivyo. Mbaya zaidi alikuwa ametumbukiza mikono mfukoni hivyo kuzidi kupoteza uwezo wa kujimudu kuwa imara wakati wa kutembea. “Una shida gani wewe?” Mfaume alimuuliza baada ya kumwona akiwa katika hali ile mbaya... “Kuna mtu...kuna mtu namuulizia bro,” alisema Jombi. hali aliyokuwa nayo ilimshangaza kila mtu kwani kwa muda ule wa asubuhi halafu mtu awe amelewa vile, ilikuwa kama ameamka nazo kama siyo kuzianzia mapema... “Nani?” Mfaume alimuuliza. Lakini kabla hajajibu, baba Mei alitoka akiwa amemeshika mkewe kwenye nywele akimvuta... “We ni malaya tu, huwezi kunitenda hivi hata siku moja. Mwanamke gani wewe hutulii? Hilo liumbo lako ndiyo unitese namna hii?” alikuwa akisema baba Mei. Mzee Hewa yeye alifuata mpaka sebuleni na kusimama. Alijisikia aibu kubwa kwa mtu kama Mfaume kwani walizoeana kuitana baba, mtoto. Sasa leo baba kuonekana anazini na mwanamke wa ndani ya nyumba tena binti kama wa kumzaa mwenyewe, kwa kweli aliumia sana... “Si huyu hapa, mama Mei,”

    alidakia Jombi baada ya kumwona mama Mei akitoka akiwa chini ya ulinzi. Jombi hakujali kuwa, mazingira pekee yalionesha kuna tatizo, akamfuata mama Mei na kumuuliza baba Mei... “Broo kwani nini?” “Nini kuhusu nini?” baba Mei alitaka kujua akiwa amesimama kidogo. Mfaume alizidi kuwasha moto, akasema... “Huyu dogo kaja anamuulizia shemeji.” “We unamjua huyu mke wangu?” baba Mei alimuuliza Jombi...



     “Namjua, mimi nimekuja kwa ajili yake...unajua naiti moja nimewahi kupinduka ndani kwake au siyo bwana... lakini nilikuwa chenga sana sikufanya lolote...sasa samtaimu mambo kama yale ni kupanga siku mwafaka,” alisema Jomho bila woga wala simile hata kufumbafumba macho hakukuwepo. Mfaume akawa wa kwanza kubaini kuwa, mwanaume aliyemwona usiku fulani akiingia kwa mama Mei na akamwona asubuhi akitoka ni huyo... “What?” Baba Mei aliuliza kwa ukali akimaanisha nini? “Ndiyo hivyo bro,” Jombi alikazia.



     Mama Mei alikuwa kimya wakati huo akilia chini kwa chini kwani sasa ilifika hatua akawa hajui alie, anyamaze kimya au ajitetee. Baba Mei alimwingiza ndani mkewe kisha akamwita Mfaume na akamwomba amwite na mzee Hewa lakini pia akamtaka na Jombi aingie. Jombi alikuwa wa kwanza, akakaa kwenye kochi dogo pembeni ya mlango... “Ungekuja tu baba, mambo tayari yameharibika, hakuna jinsi,” alisema Mfaume akimwambia mzee Hewa... “Hapana mzee wangu, hii ni aibu kubwa sana kwangu. We unadhani mimi nitakuwa mgeni wa nani katika dunia ya watu waadilifu? Nimechafuka hivihivi najiona,” alisema mzee huyo akitokwa machozi... “Baba, kama dunia ya watu waadilifu haupo, utakutana na ile yenye daraja lako, hakuna aliyekuchafua, umejichafua mwenyewe. Lakini mimi kama mimi, lawama zangu ni kwa mwanamke...

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Unataka kuniambia mama Mei ameshindwa kuwa na adabu kwako. Siamini kama wewe ndiyo uliyeanza kumtaka...kama ni wewe basi kuna eneo la kurekebisha mzee wangu...kwa hiyo we twende usipandishe hasira za baba Mei bure,” alisema Mfaume. Mzee Hewa aliposikia neno usipandishe hasira za baba Mei bure, mwenyewe akasimama kwani alijua anaweza kung’olewa meno. Waliingia, wakakaa... “Baba mimi sina maneno mengi sana, huyu mwanamke kuanzia leo ni wa kwenu. Wewe na huyu kijana hapa. Maana nimemuuliza kama kweli amewahi kuingia kwangu kulala amethibitisha kwa kuonesha chumba na kilipo kitanda japo amesema mengine hakumbuki kwani aliingia akiwa amelewa... “Kwa hiyo baada ya kusema hayo, mama Mei nakutaka uchukue kila chako uondoke. Amua kwenda kwa mzee huyo au kwa huyu kijana. Chaguo ni lako.



     Damu zote mbili umezipata, changa na iliyozeeka,” alisema baba Mei akisimama na kuufungua mlango ukakaa wazi. Mama Mei hakuwa na jinsi, aliingia ndani, chumbani akafungasha kila alichotaka... “Ukiweza niachie nguo zangu tu. Vitu vyote chukua, kitanda chukua, makabati chukua, makochi chukua, kila kitu, kasoro kile ambacho huwa navaa mimi... “Naweza kulala chini nikaanza upya kuliko kuwa na hivyo vitu halafu niko na wewe. Amani hakuna.” Mama Mei alishindwa kujizuia na kuanza kulia huku akisema... “Wanaume wameniponza mimi, nilikuwa nikivaa kanga moja na kutembea wanaona wowowo langu likifanya mbengembenge, wakawa wananitamani kumbe wananivunjia ndoa yangu...we mzee Hewa wewe nakulaani, hata wewe Mfaume pia umo, umeshalala na mimi.” He! Wote walishtuka, Mfaume akataka kutoka lakini baba Mei akamzuia na kumwambia awe na amani tu, kwani na yeye pia amepewa mwanamke huyo awe wake! Ama kweli, mwanamke mpumbavu huivunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe! Mama Mei aliamini kule kupendwa ndiyo maisha kumbe ndiyo kujiangamiza.



    MWISHO!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

0 comments:

Post a Comment

Blog