Search This Blog

Monday, October 24, 2022

MAPIGO YA MOYO - 3

 







    Chombezo : Mapigo Ya Moyo

    Sehemu Ya Tatu (3)





    “kama hakuna kilichokuleta ondoka basi maana nina kazi nyingi za kufanya. Sina muda wa kukaa na wewe na kuangaliana kama picha.” Aliongea Frank na kumuangalia Lulu aliyekuwa kama kifaranga aliyenyeshewa na mvua.

    “Frank nimekukosea niini mie?” aliongea Lulu kwa sauti ya upole.

    “hujui kosa lako?” aliongea Frank kwa hasira.

    “sijui kosa langu, ila naomba unisameha kama kweli nimekokusea.” Aliongea Lulu huku akionyesha hali ya unyenyekevu.

    “kosa lako ni kunivulia nguo. Mimi huwa sirudii kufanya mapenzi mara mbili na msichana mmoja. So siwezi kuendelea kuwa na wewe bila kufanya mapenzi. Hilo ndio kosa lako.” Aliongea Frank na kunyanyuka na kuelekea chumbani kwake.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Maneno yale yalikua zaidi ya maumivu ayasikiayo mtu aliyedidimizwa sindano kwenye kidonda kiumacho. Alitoka na kupishana na mama yake Frank nje huku analia.

    “Lulu,…Lulu”

    Aliita mama yake Frank lakini sauti hiyo haikusikika kutokana na maumivu aliyonayo Lulu. Kilio kilidumu njia nzima mpaka alipofika nyumbani kwao ambapo si mbali sana na anapoisha Frank.



    Alifika nyumbani kwao ambapo anaishi na dada yake huku machozi yana mtoka.

    “nini tena mdogo wangu.” Aliuliza dada yake Lulu baada ya kumuona mdogo wake akiingia ndani huku akilia kwa kwikwi.

    “ni..ni..ni.. Fra..nk” aliongea Lulu huku akiendelea kulia kwa kwikwi.



    Dada yake aliamua kuchukua jukumu la kumbembeleza ili awe sawa kwanza ndipo amuulize vizuri. Iliwachukua dakika kumi mpaka Lulu kurudi katika hali yake ya kawaida. Macho yote yalikua mekundu na kumvimba kutokana na kilio cha haja alicholia Lulu.

    “haya niambie mdogo wangu, huyo Frank amekupiga au amekufanya nini?” aliongea dada yake Lulu na kumtazama mdogo wake aliyekuwa amejawa na mawazo.

    “acha tu dada nikapumzike,..sijisikii vizuri.” Aliongea Lulu na dada yake akamuelewa na kuelekea chumbani kwake.



    Mawazo yalimpeleka mbali sana wakati alipomuona Frank kwa mara ya kwanza walipohamia mtaa huo. Ustaarabu na utaratibu wa Frank ulimvutia sana na kuanzisha urafiki wa karibu na kijana huyo. Msaada wa Frank katika masomo yake ndio aliamini yalimvusha kidato cha nne na kuingia kidato cha tano.



    Ukaribu wao ulikua mkubwa na kujikuta wamekuwa wapenzi bila mtu yeyote kumtongoza mwenzie.



    Frank alizoeleka na dada yake Lulu na kuwa na uhuru wa kumchukua muda wowote aliokua anamuhitaji. Hata Lulu alifahamika kwa wazazi wa Frank kama mpenzi wa mtoto wao.



    Kwakua Lulu alikua bado bikira, alimuomba Frank kumvumilia mpaka watakapofikia hatua muhimu kabisa za kuoana kwakua alijiapiza kumpa bikira yake mwanaume atakayemuoa.



    Uvumilivu wa Frank ulimpa asilimia zote kuwa Frank alikua anampenda kweli. Mbali na kusikia tetesi kuwa Frank ni play boy, lakini alizitupilia mbali kashfa hizo na kuziona ni fununu tu. Laiti angekuwa play boy asingekubali kuwa nae kimapenzi kwa miaka miwili bila kumgusa.



    Sms, kadi na maua mbali mbali yaashiriayo mapenzi ndio yalikua chachu ya mapenzi yao. Kila mmoja hakumchoka mwenzake kwa kumuandalia vitu hivyo ambavyo vilikua pambo katika kila chumba cha mmoja wao.



    Alikumbuka alipomaliza kidato cha sita na matokeo yake kuwa mabovu kutokana na kuendekeza mapenzi na kuacha kusoma. Alijilaumu sana lakini Frank alimuhakikishia kuwa akimnaliza chuo atamuoa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku hiyo wakiwa wanacheza chumbani kwa Frank kama kawaida yao. Walijikuta wanazidiwa na Frank kwa mara ya kwanza anafungua utepe wa Lulu. Hayakuwa mategemeo ila Frank alifurahi sana kwakua hakua na imani asilimia zote juu ya kua Lulu alikua kweli ni bikira.



    Kuvunjika kwa ahadi yake ndio kulimfanya Lulu alie akimuomba Frank kutomsaliti na kuoa mwanamke mwengine.



    Leo hii yale aliyoyakataa mwanzo yamejitokeza tena kwa mtu aliyemuamini. Kilio kikaanza tena kuchukua nafasi yake.



    Usiku ule ulikua wamateso sana kwa Lulu. Hakupata usingizi mpaka palipokucha.

    “sasa mdogo wangu usipokula itakuaje?” aliongea dada yake Lulu baada ya kumuona mdogo wake hajala toka jana usiku.

    “sijisikii njaa dada.” Aliongea Lulu huku akikiangalia chakula kama vile uchafu. Hakutamani kitu chochote kipite kinywani mwake.

    “ yaani wewe utakua mjinga namba moja wa mapenzi. Yaani unaacha kula kwa sababu ya mwanaume?... kwanza ulivyo mzuri hivyo unatongozwa na wanaume wangapi kwa siku mpaka huyo mmoja anakuumiza kichwa kiasi hicho?” aliongea dada yake Lulu na kumuangalia mdogo wake ambaye alikua kama mgonjwa kwa siku ile.



    “nampenda sana dada, we hujui mapenzi. Na kama ukipenda kutoka moyoni basi chochote kibaya kikikufika kunachuhusu mapenzi yako ni lazima uwe katika hali kama yangu.” Aliongea Lulu kwa uchungu.

    “ndio maana mimi hizo habari za kupenda sina mpango nazo. Umeona nazidi kuchanika tu. Sasa wewe unakula kwangu, unavaa kwangu na hela za matumizi nakupa. Kinachokufanya ukonde ni nini zaidi ya mapenzi. Basi hayana faida katika maisha yako kwakua hayakupendi. Achana na hizo ishu.” Aliongea dada yake Lulu na kuondoka zake kwakua alishamaliza kunywa chai.



    Maneno ya dada yake hayakumuingia akilini, zaidi alimuomba dada yake amsaidie kumbembelezea kwa Frank.

    “yaani Lulu hujawahi kunitukana tusi kubwa kama la leo. Mi nitaanzaje kumfuata Frank na kumwambia arudiane na wewe?.. wakati mnatongozana nilikuwepo?..nipishe mie.”



    Maneno ya dada yake yaliashiria wazi kuwa hilo zoezi hawezi kulifanya. Wazo lingine likaja haraka kichwani mwake na kuchukua simu yake na kutafuta jina liliandikwa Rose na kupiga.

    “mambo shosti.” Aliongea Rose baada ya kuipokea ile simu.

    “safi, unaweza kuja nyumbani sasa hivi.” Aliongea Lulu baada ya kuitikia salamu.

    “kuna nini?” aliuliza Rose kwa mshangao.

    “we njoo tu shosti.” Aliongea Lulu na rafiki yake akakata simu baada ya kukubali wito.



    Rose aliwasili kwa kina Lulu mapema kama alivyoahidi na kukumbatiwa na rafiki yake huyo mkubwa toka wanasoma.



    Lulu hakuona sababu ya kuficha kwa rafiki yake huyo. Alimwambia kila kitu kinachomsibu na kumuomba amsaidie kama inawezekana.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “usijali rafiki yangu. We nionyeshe mahali anapopendelea kwenda kisha nitajua nimuingie vipi.” Aliongea Rose na kumpa faraja kidogo rafiki yake.

    “nisaidie Rose, nampenda Frank kufa yaani.” Aliongea Lulu na kumfanya Rose acheke.



    Baada ya maelekezo ya kina. Rose alielewa na baada ya kuangalia picha kadhaa za Frank alipata kuikariri sura hiyo kichwani.



    Jioni ya siku hiyo Rose alielekea uwanjani ambapo watu wengi aliwaona wakifanya mazoezi. Wengi walionekana ndani ya jezi za mchezo wa mpira wa miguu. Kwa mbaali alimuona Frank akiwa amejumuika na wenzake kwenye mazoezi hayo huku akiwa na ogo lake mguuni.

    Alimsubiri amalize mazoezi na alipomaliza alimsogelea na kumshika bega wakati Frank alipokuwa anarudi nyumbani kwao. Frank alipogeuka nyuma alikutana na tabasamu zuri la mtoto wa kimbulu. Macho yake yalipogongana na Rose, alipata hisia kali kwakua huyo msichana mrembo alikua mgeni machoni mwake.



    “Mambo” alisalimia Rose baada ya macho yake kugongana na ya mvulana mwenye kila sifa ya uzuri.



    “safi tu.” Alijibu Frank na kuachia tabasamu.

    “nina shida na wewe, sijui tunaweza kuongea?” aliongea Rose na kumuangalia Frank aliyeonekana kutabasamu wakati wote.



    “poa, ila nisubiri kwenye café ile nikaoge fasta nakuja.” Aliongea Frank



    Baada ya makubaliano hayo, Frank aliondoka na yule dada alienda kwenye ile café na kuagiza kinywaji huku akimsubiria Frank.



    Nusu saa baadae, Frank alifika pale akiwa amependeza huku akinukia perfume ya bei mbaya.

    “nimekuweka sana?” aliuliza Frank na kumshtua Rose aliyejiinamia na kuwa bize kubonyeza simu yake. Mshituko ule pia ulifanya moyo wa Rose kulipuka baada ya kumuona Frank akiwa amependeza sana.

    “tunaweza tukaongea hapa hapa au tutafute sehemu nyingine tulivu?” aliongea Frank na kumuangalia Rose machoni. Aibu ya ghafla ikajijenga kwa Rose na kumfanya aangalie chini.

    “popote tu.” Aliijikuta Rose anaongea maneno hayo na kumpa nafasi Frank ya kuchagua.

    “mimi binafsi sijapapenda hapa.” Aliongea Frank na kumuangalia Rose huku akimtathmini.



    Wazo la kutafuta sehemu nyingine lilikubaliwa na zoezi la kutafuta sehemu nzuri lilisimamiwa vizuri na Frank. Walitafuta Hotel iliyokaribu na pale na kwenda kupata chakula cha jioni kwakua kiza kilishaanza kuingia.



    “kuwa huru dada, ingawaje sikufahamu. Ila nimevutiwa na muonekano wako.” Alianza kuchombeza Frank wakati wanapata chakula hicho.



    “kwanini unasema hivyo.” Aliongea Rose na kumuangalia Frank kwa kujiiba maana alishindwa kumuangalia wakiwa wamekutana macho yao.

    “kabla ya sura na umbo zuri ulilojaaliwa na muumba, una sauti nzuri sana inayomshawishi mtu kukusikiliza.” Alisifia Frank huku akimuangalia Rose kwa pozi.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “acha maneno yako.” Aliongea Rose huku akitabasamu.

    “mamaangu nakuapia, nimekutana na wazuri wengi ila wewe ni special.” Aliongea Frank na kumfanya Rose azidi kucheka.



    Waliongea mengi lakini hakuna jambo lolote linalomuhusu lulu kuongelewa pale. Baada ya chakula na maongezi ya hapa na pale, Rose alijitambulisha na kubadilishana namba za simu.



    ************************



    Ni jumapili tulivu isiyokuwa na jua kali wala dalili za kunyesha mvua, wingu lilipendeza kwa idadi ndogo ya mawingu meupa na kufanya sehemu kubwa kuwa rangi ya blue.



    Rose akiwa kwa kina Lulu wanapiga story mbili tatu ikiwemo kazi aliyopewa na rafiki yake kipenzi. Mlio wa simu yake unamgutusha na kuitoa kwenye kipochi chake. Moyo ulimripuka baada ya kuona jina la FRANK likiwa limejitokeza kwenye kioo cha simu yake.

    Alinyanyuka na kwenda kuipokea pembeni.

    “haloo.” Alipokea Rose na kusikiliza upande wa pili ulikuwa unataka kuongea nini.

    “nambie, uko poa?” aliongea Frank na kumfanya Rose atabasamu.

    “niko poa, lete story.” Aliongea Rose kwa pozi za hali ya juu.

    “niseme nini tena wakati sauti yako inazidi kunimaliza mwenzio” aliongea Frank na kumfanya Rose acheke.

    “acha utani bwana.” Alizidisha mashauzi huku akitabasamu.

    “una ishu gain mida hii, maana nimeboreka?” aliongea Frank na kusikilizia matokeo.

    “unataka tutoke nini?” alidakia Rose baada ya kung`amua kitu alichotaka kusema Frank.

    “ndio maana nikakwambia wewe ni special.. una claver zaidi ya Sheddy.” Aliongea Frank na kumfanya Rose azidi kucheka.

    “pande za wapi sasa tunakutana?” aliongea Rase.

    “pale pale kwenye ile café yetu tuliyokutana kwa mara ya kwanza.” Aliogea Frank.



    Baada ya makubaliano hayo, simu ikakatika na Rose akarudi na kuungana na wenzake aliowaacha kutokana na simu hiyo ya private kwake.

    “hata kama unaongea na bamsapu ndio utukimbie?” alitania dada yake Lulu bila kujua kuwa ile simu ilikua ya usaliti kwa mdogo wake.



    “jamani mi sikai, buu buu kanipigia simu kaniambia tutoke. Mnanionaje jamani au nikabadilishe?” aliongea Rose na kuwaangalia Lulu na dada yake.



    “hata hujapendeza shoga, kwa mtoko na mpenzi wako?..twende chumbani nikakutolee nguo ya mtoko.. acha ushamba?” aliongea Lulu na kufanya kicheko kitawale kwa sekunde kadhaa.

    “ndio maana nakupenda shoga yangu.” Aliongea Rose na kuelekea chumbani kwa Lulu na kupewa nguo nzuri ambayo ilimpendeza sana.



    Kwakua Lulu alikuwa hodari katika maswala ya make up, basi alimtengeneza rafiki yake vizuri bila kujua kua huo mtoko ulikua wa kumsaliti yeye. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Hawakukosea wahenga waliposema usilolijua ni sawa na usiku wa giza au moyo wa mtu ni sawa na pori lililojaa giza. Laiti kama Lulu angelijua kuwa Rose anaenda kukutana na Frank tena si kwa kumsaidia yeye, basi asingelimkaribisha na kumpa nguo yake yenye thamani kubwa.

    Rose alimkumbatia rafiki yake huyo kinafiki na kuondoka zake.



    Safari hii Rose alimkuta Frank ameshafika na anakunywa soda taratibu. Mapigo ya moyo yaliongeza kasi kwa Frank baada ya kumuona Rose akitoka kivingine kabisa. Alimsogelea na kumkumbatia.



    Safari iliwapeleka kunduchi beach ambapo walicheza, walikula, waliogelea na mwisho wa yote wakajikuta wamelala kabisa kwenye hotel hiyo ya kifahari.



    Maufundi na maujuzi aliyokuwa nayo Frank hasa kwenye sita kwa sita yalizidi yale ayajuayo kwenye masomo na mpira. Kwa wale ambao hawajawahi kulala kwenye kifua cha Frank walisema ana uwezo mkubwa wa akili za darasani na wale mashabiki wa mpira waliamini hakuna mchezaji hapa bongo anayemfikia Frank kwa kusakata kabumbu.

    Lakini kwa madada waliobahatika kulala nae wote walikiri kuwa ufundi wa kitandani unashika namba moja na mengine ndio yanafuata.



    Hakuna msichana aliye toka kwake bila kutoa machozi japokuwa haikusaidia. Mana kanuni ya Frank halali na msichana mmoja mara mbili.



    Baada ya wiki moja toka Rose akutane kimwili na Frank mabadiliko makubwa aliyaona. Hakupigiwa simu na hata alipopiga yeye simu yake haikupokelewa na mara nyingine alikatiwa smu zake. Hata alipotuma Sms hazikujibiwa.



    Mawazo juu ya makosa aliyomtendea Frank yalimtesa bila majawabu sahihi, aliamua kwenda kwa kina Frank ili mradi ajue ni nini tatizo.



    Wakati alipokua njiani, alipigwa na butwaa baada ya kumuona Frank akiwa na msichana mwengine Bar wakilishana na kupigana mabusu hadharani.



    Kwa hasira na ghadhabu za hali ya juu aliwasogelea walipo na kuwatenganishawalipkuwa wakibusiana.

    “Frank!!!..... unafanya nini?” aliliza Rose kwa hasira.

    “wewe kama nani kwangu mpaka unaniuliza havyo?” aliongea Frank kwa dharau.

    “ Frank. … wewe wakuniambia mimi hivyo?” aliongea Rose katika hali ya kutoamini akisikiacho kutokwa kwa Frank.

    Alichokifanya Frank, alinyanuka na kuwaomba umati uliokuwa pale bar wamsikilize japo dakika moja.

    “jamani samahanini kwa kuwapotezea muda,.. hivi mapenzi yanalazimishwa?” aliuliza Franik baada ya watu wote waliokua pale bar kumgeukia yeye.

    “hapana” sauti za pamoja zilisikika.

    “kuna haja ya kumbembeleza mtu asiyekupenda?” aliuliza tena Frank.

    “hapana” wakajibu tena kwa pamoja.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “basi mshaurini huyu dada, mimi simtaki ananilazimisha kuwa nae wakati nina mpenzi wangu.. niondolee kiwingu dada usije kunifunga hela bure.” Aliongea Frank na kufanya watu wote waliokuwepo kwenye ile bar kumcheka Rose.



    Aibu ya mwaka ambayo haijawahi kumpata toka azaliwe, ndio iliyomfanya Rose aondoke pale bar mbio huku analia.



    Huyo ndio Frank. Hakuna msichana ambaye aliachwa na yeye bila ya kutoa machozi. Baada ya kumuacha Rose tena kwa kumdhalilisha mbele za watu, aliendelea kuwabadilisha kama nguo wasichana waliokuwa na shobo kwake.



    “umefikia wapi shoga yangu, maana hunupi ripoti.” Aliuliza Lulu baada ya kumtembelea shoga yake.

    “shoga tafuta mwanaume mwengine, yule si mwanaume bali ni nyoka. Yaani sijaona mwanaume Malaya kama yule. Yaani badala ya kunisikiliza ninachomwambia kuhusu wewe ananigeuzia kibao na kunitongoza mimi. Ndio maana sitaki hata kuonana naye.” Alijikosha Rose bila kumwambia ukweli rafiki yake yaliyomkuta.



    “kwa hiyo na wewe umeshindwa?” aliongea Lulu huku akiwa hana furaha kama aliyokuja nayo mwanzo.

    “achana nae mwaya, unafikiri samaki ni yeye tu bahari nzima. Wapo wengi tena watamu zaidi yake.” Aliongea Rose na kuonyesha kuchukizwa sana na tabia ya Frank.



    Siku zilikatika bila Lulu kuonana na Frank mpaka siku ambayo Frank alikua anarudi tena chuo.

    “wewe mwanamke, huchoki wala huelewi ukiambiwa kitu. Sikupendi na sikuhitaji hata bure katika maisha yangu. Niseme na kitu gani ndio unielewe?” aliongea Frank baada ya kumuona Lulu akimfata wakati alipokuwa ana paki mabegi yake kwenye gari.



    “Frank, najua hujui mazito yanayonikabili ndani ya mtima wangu. Kila kilichokuwa kwenye mwili wangu nilikupa password zake na ulizifungua utakavyo. Nimekupa mpaka uhuru wa kuingia kwenye ikulu yangu yenye thamani zaidi ya falme za kiarabu. Si mimi Frank ambaye sichoki dharau zako na kukubali kama hunipendi. Tatizo ni moyo Frank. Moyo wangu ndio hausikii wala haoni juu yako. Macho yangu hayaoni kwa wanaume wengine na kukuona wewe tu. Maumivu unayonipa yanapoozwa na sura yako tu ingawaje kauli zako ni mzigo mkubwa uliomulemea kizee jangwani na asiyekuwa na msaada wowote Frank.” Aliongea Lulu huku machozi yanamtoka.

    “Frank tazama machozi yangu angalau kwa jicho la huruma nipate japo faraja. Kwani idadi ya matone ya machozi yangu hayafanani na uzito wa maumivu ya moyo yanimalizayo mwili kila kukicha. Sihitaji kujua nitakuwa nafasi ya ngapi kati ya uwapendao. Ile kunikaribisha hata nje ya moyo wako nitafarijika. Bora uongo utakaonipa faraja kuliko ukweli utakaoniumiza. Nakupenda Frank zaidi ya niwezavyo kukuelezea.”



    Maneno ya Lulu yalipita kama upepo masikioni mwa Frank. Alimtazama na kuyapokea maua aliyoletewa na kuingia nayo kwenye gari.



    “nimekuelewa, nitakujibu nikipata likizo nyingine.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hayo maneno ya Frank kidogo yalimpa faraja Lulu. Baada ya hapo safari ya kuitafuta ubongo kwa ajili ya safari ya Dodoma kuendelea na masomo yake ilianza.



    ********************



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog