Chombezo : Mapigo Ya Moyo
Sehemu Ya Nne (4)
Kipenzi cha warembo aliingia chuoni na kushangiliwa na madada wengi baada ya kumuona Frank akiwa amepona kabisa. Idadi kubwa ya watu waliomlaki ilizidi kumpa faraja Frank. Katika watu wengi aliokutana nao, mtu mmoja ambaye alimkumbuka kipindi chote cha likizo ilikua bado hakumtia machoni.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwa mbaali alizisikia kelele za watu waliomzunguka na kumkumbatia mtu aliyeshuka kwenye gari aina ya Land Rover . alishawishika kumsogelea mtu huyo maarufu pale chuoni. Baada ya kuwapangua watu kadhaa waliokuwa pale, alipagawa baada ya kumuona Neila akiwa amependeza sana. Alikua amevaa nguo ndefi ya rangi ya blue na kiremba kilichofungwa vizuri. Shingoni alikua na kidani kama cha wanawake wa kihindi wanavyopenda kuvaa.
Mapigo ya moyo yalianza kumuenda kasi baada ya msichana huyo ameachia tabasamu na kuelekea upande wake.
Kwa mapozi yote 66, Neila alimsogelea Frank na kumpa mkono wake kwa mara ya kwanza. Frank aliushangaa ulaini wa mkono wa Neila mpaka akawa anahisi labda atakuwa anamuumiza. Ulikuwa laini zaidi ya pamba na mweupe ambao haukuwa na alama yoyote zaidi ya mistari kadhaa iliyojichora alama ya ( M ) kwenye kiganja chake.
“assalaam aleykum” ilisikika sauti tamu ya Neila na kumshtua Frank aliyejawa na mawazo ya ghafla baada ya kugusana viganja vyao.
“waaleykum salaam” aliitikia Frank kwa kubabaika kidogo kwakua salamu hiyo hakuizoea.
“kayfal-khali” aliongea Neila na kumtazama Frank kwa macho malegevu yaliyo zidishwa uzuri na kope za bandia.
“twayib” alibahatisha Frank na kumfanya Neila acheke.
“waoooh… una kumbukumbu sana. Nice.” Aliongea Neila na kuendelea kufurahi hali iliyozidi kummaliza Frank.
Urafiki wa kawaida kati ya Frank na Neila uliendelea mpaka walipobandikiwa matokeo yao. Frank ndio alikuwa wa kwanza kwenda kuangalia.
“yes, nimewaburuza tena.” Alishangilia Frank baada ya kuwa wa kwanza tena.
Marafiki kadhaa walimpongeza na baadae wazo la kumuangalia Neila likamjia.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Walitafuta jina la Neila na baada ya kumuona alicheka.
“sio mbaya lakini, ameshika nafasi ya 6.” Aliongea kwa Dharau baada ya kuona kampita masomo yote tena kwa point nyingi.
“hongera, umekuwa mtu wa 6.”
Aliongea Frank baada ya kumuona Neila amejiinamia. Neila alinyanyuka akiwa na sura nyingine tofauti na ile aliyoizoea. Hali iliyomfanya Frank ashangae.
“ hapa shuleni kila mtu ameletwa na mzazi wake, so matokeo yangu hayakuhusu. Ni nani amekuambia alikua anahitaji umuangalizie matokeo yake?.. kuongoza mitihani isiwe shida kwa wengine. Siku nyingi sana nilikua siipendi tabia yako ya kujisikia ndio maana nikakwambia ufute yako. Nikafikiri umejirekebisha kumbe ndio tabia uliyozaliwa nayo. Unafikiri sijakusikia ulipokuwa unajitamba eti nilifikiri nimepata mpinzani kumbe yule dada boya tu… acha shobo mtotoo wa kiume, fuata yako halafu tusijuane coz tumekutana chuoni tu hapa.”
Maneno yale ambayo yalisika na umati mkubwa waliokuwa pale kutokana na Neila kuongea kwa nguvu, ndio kulikomfanya aumie sana rahoni na kupata aibu kubwa.
Furaha yote aliyokuwa nayo juu ya kufaulu vizuri iliyeyuka kama barafu kwenye jua kali. Aliulaumu sana mdomo wake kwa kuropoka mambo ambayo yangemshusha maksi kwa Neila.
Tukio hilo lilimkosesha raha Frank. Hakupenda kumchukiza Neila hata kidogo. Alijua kuwa kumuuzi binti huyo ni sawa na kujipa adhabu kali inayomuumiza mwenyewe.
Urafiki ukafa kinamna hiyo. Hakukua na salamu wala maongezi yoyote kati yao. Awapo Frank sehemu yoyote, basi Neila hakusogeza miguu yake pale. Na hata kama Neila alikua anapiga story na watu mbali mbali, basi akija tu Frank yeye huondoka eneo hilo.
Unyonge mkubwa ulimpata Frank na kujiona kuna kitu anakosa kutoka katika maisha yake. Alijiridhisha kwa kuwachukua marafiki wa karibu wa Neila na kutembea nao. Hiyo ndio ilizidi kumpunguzia maksi Frank na kuzidi kuchukiwa na Neila.
Uwezo wake wa kusakata kabumbu ulipungua kiwango siku hadi siku. Kuna wakati hakua msaada kabisa kwa timu yao ya chuo. Kocha wao alimuita na kumuuliza ni nini tatizo.
“Neila,….. huyu ndio ananifanya kila nikifanyacho nikione kibaya kwangu. Ananiumuzi sana moyo wangu.” Alilalamika Frank kwa kocha wake ambaye alimuelewa vizuri.
Kutokana na kocha huyo kumtegemea sana kiungo wake mshambuliaji, aliamua kulibeba jukumu hilo na kumfuata Neila na kuongea nae.
“kuwa naye ni swala gumu sana Mr. Jocob. Mimi siwapendi watu wenye dharau na kujiona wapo juu kuliko wenzao. Watu wenye kutumia kitu walichonacho kwa ajili ya kuwanyanyasa wenzao mimi huwa siivi nao. Kati ya hayo yote, hakuna hata category moja wapo ambayo Frank hayupo. Kingine ni Malaya mbwa. Kwa mambo hayo tu, hana kibali hata cha kuipokea salamu yangu. Tena mfikishie habari kuwa hana hadhi hata ya salamu yangu.” CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Aliongea Neila na kuondoka zake. Kocha alibaki hoi na hakujua ni njia gani nyingine anayoweza kutumia kwa mrembo huyo mwenye msimamo wa hali ya juu.
Taarifa zilifika kama zilivyotumwa kwa mlengwa. Hapo Frank alianza kujirekebisha kwa kuachana na wasichana wake wote aliokuwa nao. Alin`gata line na kununua nyingine ambayo aliwa save watu muhimu kwake tu.
Mabadiliko ya tabia ya Frank hayakuzaa matunda, kwani tayari kulikua na ukuta mkubwa aliouweka mrembo huyo ambao ilikua ngumu Neila kujua kama yeye amebadilika.
Mitihani ya kumaliza semester nyingine ilifika na yeye kuanguka kutoka nafasi ya kwanza mpaka ya ishirini na mbili.
“dah, mwanangu Neila katuongoza. Kashika nafasi ya kwanza.”
Aliongea mmoja wa marafiki zake wa karibu waliokuwa wote bweni moja.
Mpaka wanafunga chuo hakukua na salamu wala ukaribu tena na mrembo Neila. Mawazo yaliumaliza mwili mzuri wa kuvutia na kuwa mwili ambao hata yeye mwenyewe hakuutamani.
Frank alikichukia kioo kutokana na kumuonyesha jinsi alivyopuputika.
Alirudi nyumbani na kila aliyemuona alimshangaa. Lakini hawakujali sana baada ya kupewa taarifa za uongo juu ya ugumu wa masomo yao.
Lulu hakuchoka, bado siku hiyo alienda dukani na kununua maua mazuri na midoli. Alipofika kwa kina Frank, alpokelewa vizuri na mama yake Frank na kuingia ndani.
Frank aliyapokea yale maua na kuyaweka mezani. Aliendalae kulala huku akiugulia maumivu kama ishara ya kuumwa.
“umeshaenda hospitali?.. usipuuzie, inaweza kuwa malaria.” Aliongea Lulu kwa sauti iliyoashiria kujali.
“samahani sana. Nashukuru kwa zawadi yako, ila nakuomba uniache nipumzike.” Aliongea kwa upole Frank na kujifanya amezidiwa.
Baada ya Lulu kuondoka. Alitoka sebuleni na kumfata mama yake.
“mtu yeyote akija kuniulizia mwambie sipo.”
Aliacha maagizo hayo frank na kurudi chumbani kwake.
Usiku ulizidi kuwa mrefu kwa Frank kwa kuwa mawazo ya Neila yalitawala kichwa chake.
Baada ya wiki moja kupita, Frank alipigiwa simu na rafiki yake kipenzi.
“oyaa, mbona kimya sana bro?” aliongea rafiki yake huyo baada ya salamu ya vijana.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“hamna bwana, si unajua muda huu nautumia kupumzika baada ya kuumiza kichwa muda mrefu chuo?” aliongea Frank
“ kesho njoo fun city kuna party ndogo ya wanafunzi wote wa chuo chetu tunaoishi dar” aliongea yule rafiki yake.
“mtonyo shilingi ngapi?” aliulizia Frank kutokana na kupenda mambo ya kujirusha hususani kipindi kile cha upweke kwake.
Siku ya siku ilifika, na Frank akajipigilia nguo zilizomkaa vizuri kiasi na kwenda Fun city. Alikutana na wanafunzi wengi na wote wakafurahi kuonana. Keki kubwa ililetwa mbele ya meza .
“jamani, tumteue nani ili atulishe keki?” aliongea maneno hayo Mc wa tafrija ile iliyowasuuza roho wanafunzi wote waliohudhuria pale.
“FRANK!!!”
Wengi walisikika wakilitaja jina hilo.
“kwakua wengi wape, basi Frank umepita. Unatakiwa utulishe keki umati wote uliokuwa hapa. “ aliendelea kuongea mshereheshaji huyo mwenye mbwe mbwe za kila aina. Hakika aliiwezea ile party na kuwafanya waliohudhuria kuburudika.
“sijui nimuanze nani?” aliuliza Frank baada ya kukubali majukumu yale ya kuwalisha keki wenzake.
“mimiiiiii” walijibu wote kwa pamoja.
“basi pangeni msitari mmoja. Atakayekuwa mwisho ndiye atakuwa wamwisho kula keki.” Aliongea Frank na kauli yake ikasikilizwa na umati wote ukapanga mstari mmoja.
Baada ya zoezi hilo la kulishana keki kukamilika, mshehereshaji alichukua tena kipaza na kuendelea na ratiba zingine.
“sasa Frank unatakiwa ufumbe macho na wewe ulishwe keki” aliongea mshereheshaji na Frank alitii kwa kufumba macho.
Mtu aliyeteuliwa kumlisha keki Frank, alienda na kumlisha keki kisha mshereheshaji akamruhusu Frank afumbue macho.
“MY GOD, I CAN`T BELIEVE!!!!!”
Ulikua mshangao mkubwa sana baada ya Frank kumuona Neila akiwa pale na ndio aliyemlisha keki. Akiwa katika taharuki, Neila alimfata na kumkumbatia na kufanya umati wote uliokuwa pale kupiga makofi, miluzi na vifijo. Machozi ya furaha yalimtoka Frank bila ya kutegemea.
Kiukweli ilikua ni zaidi ya Surprise kwa Frank. Hakutegemea kabisa kuwa karibu na Neila tena hata kwa sekunde moja. Huzuni yote aliyokuwa nayo ilitoweka na furaha ikaanza kuenea moyoni mwake kwa kasi.
Baada ya zoezi la kulishana keki kukamilika baada ya Frank kujibu mapigo kwa kumlisha Neila kwa style ya aina yake.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mziki mkubwa uliwashwa na wote wakaanza kusakata rumba huku Frank akipata nafasi ya dhahabu kwa kuruhusiwa kumshika Neila popote atakapo.
Baada ya party hiyo kuisha mishale ya saa nne usiku. Watu waliokuja na usafiri wao walipanda kwenye magari yao. Na waliobakia walipanda usafiri wa pamoja.
“unaonaje ukipanda kwenye gari niliyokuja nayo. Nitakupeleka mpaka kwenu.” Aliongea Frank alipokuwa anatoka huku akiwa amemganda Neila kama ruba.
“noo, hata mimi nimekuja na usafiri wangu.” Aliongea Neila na kumkata maini Frank.
Usiku huo ulikua wa faraja sana kwa Frank ambaye alirudi nyumbani kwao akiwa na furaha isiyokuwa na kifani.
“hallow”
Aliitikia Neila baada ya kuipokea simu ya Frank.
“niambie, umeshafika nyumbani?” aliuliza Frank baada ya kupanda kitandani.
“nimefika muda kidogo, na hivi sasa ndio napanda kitandani kwa ajili ya kulala. Maana nimechoka sana.” Aliongea Neila kwa mapozi na matamshi yaliyomvutia kwa kiasi
Kikubwa Frank.
“sijui kwanini, leo nakiona kitanda kikubwa sana” aliongea Frank na kumfanya Neila acheke.
“kwanini?” aliuliza Neila huku akiendelea kucheka.
“hata mimi mwenyewe sijui kwanini.” Aliongea na kicheko kwa wote kikachukua nafasi.
“usiku mwema bwana , mwenzio nimeelemewa na usingizi.” Aliongea Neila
“poa, sleep well” aliongea Frank na kukata simu. Alifurahi sana kuwasiliana na mrembo huyo aliyeziteka hisia zake kuikweli kabisa.
Mapenzi ya simu ndio yalikuwa na nafasi kwa Neila. Na kila Frank alipopanga kukutana na Neila, alipanguliwa na sababu mbali mbali zilizofanya wasionane mpaka wanafungua chuo.
“jamani Frank si ulisema ukirudi likizo utanipa msimamo wako juu yangu. Mbona kila nikija chenga zinakuwa nyingi mara unaumwa mara hujisikii kuongelea maswala ya mapenzi… kwanini unanitesa mwenzio.”
Alilalamika Lulu baada ya kuonana na Frank. Ni kipindi kirefu hawajaonana kutokana na Frank kutotaka kuonana nae.
Hata wakionana basi Frank huzua sababu yoyoye ilimradi asikae nae na kumsikiliza.
“Lulu, mimi si mwanaume unayestahili kuwa na wewe. Nitakuumiza bure. Kuna mtu nampenda kuliko wewe na huyo sitaki kumuuzi kwa kumgonganisha na mwanamke mwengine. Mimi si Frank yule uliyemzoea. Mimi ni Frank mwengine niliyeamua kuishi katika misingi ya kutokuwa na wanawake wengi kama awali. Na mwanamke mwenyewe sio wewe. Kwa hiyo sioni pa kukuweka Lulu. Nisamehe kwa kukupotezea muda na bikira yako, ila ni dhahiri mungu hajapanga mimi nikuoe wewe. Usilazimishe kitu ambacho hakiwezekani. Nilikupenda awali ambapo nilikuwa play boy na baada ya kukufunua tu basi upendo ulikufa pale pale kitandani. Baada ya hapo ulikuwa taka taka kwangu. Sasa nimeingiwa na moyo wa kupenda, lakini kwa bahati mbaya wewe sio chaguo la moyo wangu.” Aliongea Frank na kumfanya Lulu atokwe na machozi.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“nakupenda sana Frank, ila kwa kauli ulizoamua kunitamkia muda huu. Nimeamua kunyoosha mikono juu. Pendo langu la dhati nalifukia ardhini leo hii na kuanza maisha yangu upya……. Na nakushukuru kwa yote uliyonitendea. Nakushukuru kwa katambua kuwa umeivunja ahadi yangu na kuniharibia usichana wangu. Nakutakia maisha mema na huyo unayemuita chaguo la moyo wako.”
Aliongea Lulu kwa uchungu na kuondoka huku analia. Farnk hakujali, alitoka na kufunga mlango wake na kuchukua simu yake na kutafuta jina lililoandikwa NEILA na kupiga.
“ kama masihara mpenzi wangu, wiki ijayo tunarudi tena mjengoni.” Aliongea Frank baada ya salamu.
“umeona eeh.. nilivyokumiss naona wiki yenyewe nyingi.” Aliongea Neila na kumfanya Frank atabasamu.
“unarudi lini huko bagamoyo angalau hata nikuone kabla ya kwenda chuo?” aliuliza Frank huku akigalagala kitandani kwa utamu wa kuongea na Neila mwenye sauti ya ushawishi wa kutamani kuongea nae muda wote hata kama huna cha maana unachotaka kuongea nae.
“ sirudi Dar, yaani nikitoka huku naonganisha moja kwa moja chuo.” Aliongea Neila kwa sauti ya kudeka.
“haya , nilikuwa nakusalimia tu. Si unajua mimi ni mgonjwa wa sauti yako. Kila muda natamani kuisikia tu.” Aliongea Frank na kutabasamu.
“kama kila muda unatamani kuisikia, nikuambie ufanye nini?” aliongea Neila na kumfanya Frank akae kwa umakini na kusikiliza kitu atakachoambiwa.
“ hebu niambie basi.” Aliongea Frank kwa pozi na yeye za kisharo.
“chukua simu yako record sauti yangu. Kila ukitaka kuisikia utakua unasikiliza muda wote.” Aliongea Neila na wote wakacheka.
Siku ilipowadia Frank alifika chuoni mapema na Neila akafika siku inayofuata. Hakika kila mmoja alionekana kummiss mwenzake. Walikumbatiana na kupigana mabusu yasiyo na idadi.
Frank na Neila walikua wapenzi waliopendezana na watu wote waliowaona walikiri kuwa walikua wanaendana. Mwili wa Frank ulifutuka na kuwa zaidi ya alivyokuwa mwanzo. Alirudi tena gym na kutengeneza mwili wake vizuri
Kutokana na huo ndio ulikuwa mwaka wa mwisho pale chuoni. Frank aliandikwa kwenye kumbukumbu za wanafunzi waliokipa chuo mafanikio makubwa na kukitangaza hadi nje ya nchi kutokana na kiwango cha hali ya juu alichonacho Frank kama mchezaji wa mpira wa miguu.
Yote hayo yaliwezekana kwakua alikua amempata mwanamke aliyeumiza hisia zake kwa muda mrefu.
Walimaliza mitihani yao ya mwisho na kurudi makwao. Lakini Neila hakurudi na Frank kama Frank mwenyewe alivyotarajia. Alichukuliwa na mtu aliyekuja na Land rover na kuondoka naye.
Kipindi chote walichokuwa chuo. Kitu ambacho kilichomfanya Neila kuonyesha kukasirika ni swala la kufanya mapenzi. Kwakua Frank alikua haambiwi wala haoni kwa Neila, alikubali kukaa kipindi chote hicho bila kumjua Neila baada ya kuvua nguo yukoje.
Kila alipomuhitaji Neila, aliishia kula denda na kuambiwa mambo mazuri hayahitaji haraka.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Siku waliyopanga kuzindua penzi lao kwa kulala pamoja mpaka asubuhi ilikuwa ni siku hiyo kwa malengo ya kuondoka pamoja. Zoezi lao limefeli kwakua kuna mtu aliyetambulishwa kuwa ni kaka yake wa damu ametumwa na wazazi wake kuja kumchukua.
Frank aliumia kidogo roho lakini alipiga moyo konde na kuamini watakuwa wote kwakua hakukua na hililafu yoyote na msichana huyo aliyeyabadilisha maisha yake kwa kiasi kikubwa. Aliamini yeye ni sawa na Playstation Game na Neila ndio kashika padi. Hivyo alikuwa anamuendesha atakavyo.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment