Chombezo : Mapigo Ya Moyo
Sehemu Ya Tano (5)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mchana wa siku hiyo aliwasili Dar mapema akiwa na uchovu mkubwa wa safari ndefu ipatayo masaa nane njiani.
Alipofika kwao alikula na kulala. Alikurupuka saa nne usiku. Alienda kupata chakula cha usiku. Alipomaliza aliingia bafuni kuoga na kujitupa kitandani na kuchukua simu yake na kumpigia Neila.
“haloow”
Ilisikika sauti ya mwanaume na kumfanya Frank ashangae na kuangalia kwenye kioo cha simu yake labda atakua amekusea namba. Lakini alikuta ni jina la mpenzi wake ndio limejitokeza.
“ namuomba mwenye simu” aliongea Frank kwa hasira.
“wewe kama nani mpaka unawapigia wake za watu usuku kama huu?” aliongea mwanaume upande wa pili na kumfanya Frank aishiwe nguvu. Alijikuta amekata simu bila ya kutegemea. Alipojaribu tena kupiga simu haikupokelewa. Alilipopiga mara tatu ndio ujumbe wa simu kutopatikana ulipomjia masikioni mwake.
Hakutegema kama Neila angeweza kumfanyia yale. Moyo ulimuuma kupita kiasi. Hakula wala kulala. Kutwa alikua analia kila akikumbuka ahadi mbali mbali waliahidiana na Neila.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Siku tatu baadaye, Frank alimpigia simu Neila. Ilikuwa kama bahati baada ya kuisikiia ikiita kwakua siku zote toka siku ile ilikuwa haipatikani.
“haloo mpenzi.” Aliongea Frank baada ya Nila kuipokea ile simu na kukaa vizuri.
“haloo Frenk” aliitikia Neila kama vile hakukuwa na tatizo lolote lililotokea baina yao.
“kwanini unanitesa Neila?” aliuliza Frank kinyonge.
“nakutesa?, kivipi yaani.” Aliongea Neila na kucheka.
“unajua fika kuwa siwezi kuishi bila ya kuwa na wewe. Na unajua jinsi gani ninavyokupenda na sitamani hata siku moja itokee tukahitilafiana. Kwanini umempa mwanaume simu yako anitukane?” aliongea Frank na ishara za kuwa alikua analia zilijitokeza kutokana na sauti yake.
“ngoja nikuambie ukweli. Mimi sikupendi hata kidogo na sijawahi kukupenda. Ila nilifanya yote kwakua ulikua unahitajika sana na timu ya chuo pia nilijua kwanini ulikua unafeli mitihani. So nikaamua kukusaidia angalau na wewe ufanye vizuri mitihani yako. Lakini swala la kukupenda halikuwepo. Haya ni mengineyo tu. Nikupe taarifa tu kuwa mimi ni mke wa mtu. Kwa hiyo nakuomba ukome kunipigia simu sababu hujui umenigombanisha kwa kiasi gani na mume wangu. Tumejuana kuchuo chuo na tumeachana kichuo chuo. So, sahau kuhusu mimi. Siku njema”
Neila aliongea kwa hasira na kuonyesha wazi kuwa alikuwa havutiwi hata kidogo na Frank. Mpaka anamaliza kuongea na kukata simu, Frank alikua haamini alichokisikia. Aliona kama yupo ndotoni. Lakini alipofikicha macho yake haikuwa ndoto. Bali ni hali halisi. Alipigwa na butwa na kujikuta machozi yenyewe yakimtiririka mashavuni.
Frank alilia sana mpaka mama yake alisikia kilio cha mwanae. Kwakua alikua mooto wa pekee, wazazi wake hawakuvumilia hali ile. Walimfata na kumgongea chumbani kwake.
“vipi mwanangu?” aliuliza mama yake akiwa nje huku akisubiri kufunguliwa mlango.
“fungua mlango basi, sisi wazazi wako utuambie yanayokusibu.” Aliongea baba yake Frank
Frank alifungua mlango na wazazi wake wakaingia ndani. Alilia wakati wote na wazazi wake walimbembeleza sana. Baada ya muda, alinyamaza na kuwaelezea wazazi wake kuanzia mwazo toka anakutana na Neila mpaka hapo walipofikia.
Wazazi wake walimuonea huruma lakini hawakua na jinsi. Zaidi ya kumshauri atafute msichana mwengine kwakua yule hakua bahati yake.
`“mi nampenda sana Neila baba, sijaona bado msichana mzuri na mwenye vigezo kama vya Neila.” Alizidi kuongea Frank na kuwafanya wazazi wake na wao kuchoka. Maana Frank hakusikia la muadhini wala kengele ya kanisa kwa kumuweka Neila nafasi zote za wasichana aliowahi kuwa nao.
Baada ya wiki moja, Frank alishindwa kuvumilia. Alimpigia simu Neila ambaye aliipokea baada ya kuita mara kadhaa.
“umesahau nini?” CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hayo ndio maneno aliyokutana nayo Frenk baada tu ya kupokelewa simu yake.
“jamani Neila, hata salamu.”
Aliongea Frank. Hakika moyoni alijisikia vibaya kujibiwa vile.
“kama kwako ina umuhimu sawa. Ila kwangu mimi sioni kama kuna umuhimu wa kusalimiana na mtu kama wewe.” Aliongea Neila kwa nyodo.
Kilikuwa kitu kama upinde uliokuja kwa kasi na kuuchoma moyo wa Frank. Alitamani hata kulia kutokana na maumivu ya moyo anayoyapata kutokana na kauli za Neila.
“usinifanyie hivyo Neila, unaniumiza.” Aliongea Frank na kuanza kulia.
“mimi sikuumizi Frank, unajiumiza mwenyewe, unafikiri kama usingenipigia simu yote haya unge yapata?... sipendi ukaribu na wewe Frank mbona unalazimisha kitu ambacho hakiwezekani?” alifoka Neila.
“nimekupigia kwa sababu nilikua na shida kidogo.” Aliongea Frank kwa sauti iliyohuzunisha huku matamshi yake yakimjulisha wazi Neila kuwa alikua analia muda huo.
“shida gani ambayo unadhani mimi naweza kukusaidia. Onyo, iwe ya msingi na isihusiane na mapenzi.” Aliongea msichana huyo mwenye mapozi yote 66. hakika Frank alipatikana kwa huyu binti kiasi cha kumfanya kulia kila wakati kama mtoto mdogo.
“nahitaji kuonana na wewe” aliongea Frank huku akiwa makini kusikiliza maamuzi ya Neila.
“mimi sihitaji kuonana na wewe.” Aliongea Neila kwa lafudhi ya dharau.
“usikatae Neila, ni muhimu sana. Nakuomba usikatae wito, kataa maneno yangu nitakayokuambia tutakapoonana.” Aliomba Frank.
“kwani huwezi kuongea kwenye simu?” aliuliza Neila.
“si rahisi kumaliza yote ninayotaka kuongea na wewe kwenye simu.” Aliongea Frank.
“mume wangu akiniruhusu nitakuja.”
Aliongea maneno hayo Neila na kumfanya Frank kuganda kwa muda bila kuongea kitu chochote. Baada ya hapo ni kilio cha kwikwi ndicho kilichosikikika na kumfanya Neila kukata simu.
Frank alitulia kwa siku mbili na kumtafuta tena Neila. Mara kadhaa alikataliwa ombi lake la kuonana na Neila. Frank hakuchoka mbali na maudhi na maneno ya karaha ya Neila yaliyomuumiza roho lakini aliendelea kumsumbua mpaka Neila akakubali kuonana na Frank.
Siku waliyoahidiana kukutana, Frank alifika mapema na saa limoja baadae Neila alifika eneo la tukio. Alikua na muonekano tofauti. Alivaa nusu kanzu kama za kihindi na Panjabi. Aliutupia mtandio shingoni na kuziacha nywele zake nyingi zikiwa zimedizainiwa kwa style ya pekee. Kati kati zilipakwa brich rangi ya zambarau aliyometisha kuanzia nguo, hereni mpaka rangi ya kucha zake.
Frank alipigwa na bumbuwazi baada ya kumuona Neila akiwa amependeza mpaka basi.
Alimsalimia kiouga na baada ya hapo alimpeleka sehemu tulivu na kukaa nae.
“naomba tukakae sehemu ambayo haina watu wala mwanga mkali, sipendi kuonekana kwa sababu najulikana sana maeneo haya.” Aliongea Neila baada ya kuonana na Frenk.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Bila kubisha, Frenk alikubali kuwa maamuma na kumfata Neila na kwenda sehemu aliyoitaka yeye. Walichagua sehemu tulivu na kukaa huko peke yao.
“nina saa moja tu ya kukaa hapa na wewe.” Aliongea Neila na kuangalia saa yake iliyokuwa inasoma saa mbili na robo usiku.
“kwanza nashukuru kwa kukubali wito. Nimekuita hapa nikueleze ya moyoni mwangu. Neila sina haja ya kurudia kukuambia kama nakupenda, ila unafahamu kwa kiasi kikubwa jinsi ullivyoniteka na jinsi nilivyokuwa sina hali kwako. Nipo tayari hata kubadili dini na kuwa muislamu na kuswali swala tano kama utanipa nafasi myingine kwenye moyo wako.”
Aliongea Frank huku analia na kupiga magoti. Alilia na kumuangalia Neila kwa macho ya huruma.
“yaani umeniita ili nije kuusikia upuuzi huo unaouongea?” aliongea Neila bila kuonyesha kujali kilio cha Frank.
“nakupenda sana. Amini hivyo.” Aliongea Frank huku akiwa pale chini alipopiga magoti.
“mimi sikulazimishwa kuolewa. Nimeolewa na mtu ninayempenda sana. Frank huna hadhi ya kuwa na mimi. Na sisemi hivyo kwakua tu nimeolewa, hata kama ningekuwa sina mpenzi basi wewe usingekuwa na nafasi kwangu. Yaani hata kama nikizaliwa upya bado nikikutana na wewe nitakukataa. Kuonyesha kuwa sikupendi, geuka nyuma uone.”
Aliongea Neila na kumfanya Frank ageuke nyuma. Aliona kundi la watu Tisa walioshika kila aina ya zana wakija upande wao wakiongozwa na jamaa mmoja mwenye asili ya kiarabu akiwa amevalia suti ya khaki huku akiwa ameshika mkongojo ulionakshiwa na dhahabu.
Kundi hilo lilifika eneo hilo na kusimama mbele yao. Yule mwarabu alimfata Neila na kumkumbatia kisha akampiga busu. Baada ya hapo alimtaza Frank aliyekuwa ameduwaa pale chini alipopiga magoti.
“we vipi hapa.” Aliuliza yule mwarabu kwa ukali.
“ndio huyu mtu mwenyewe anayenisumbua kila siku mume wangu,” aliongea Neila kauli zilizomfanya Frank kupatwa na kitete. Alarm ya hatari ilianza kulia kwenye kichwa chake kila akiutazama umati uliokuja pale haukuwa na amani kwake. Alitamani kukimbia, ila njia zote zilizingirwa na wale watu. Alitamani kupiga kelele, lakini eneo hilo halikuonekana kuwa na watu karibu.
Mawazo ya kufanyiwa kitu kibaya yalianza kuingia haraka ubongoni kwake. Hisia za uoga zilianza kutanda katika kila kona ya mwili wake. Vipele vya uoga vilimtoka mwili mzima na kwa mbali kijasho chembamba kikaanza kumtoka.
“sasa kijana utajuta kumfahamu huyu binti.” Aliongea yule mwarabu na kumsogelea Frank aliyekuwa ameganda kama ziginari pale chini. Alimtandika ngumi moja takatifu iliyompeleka Frank mpaka chini.
Bila kuchelewa, wale wengine walianza kumpa kipigo cha haja Frank kwa magongo waliyonayo na wengine kumcharanga sehemu kadhaa na mapanga. Dakika mbili tu zilitosha kumuacha Frank akiwa hoi pale chini.
“ukome kufuata wake za watu.” CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Aliongea yule mwarabu na kuondoka na kundi lake huku Neila akiwa amemlalia asishuhudie tukio alilofanyiwa Frank.
Kipigo walichompa Frank kilimfanya apoteze fahamu. Aliokotwa na wasamaria wema waliokuwa wakipita eneo hilo na kumpeleka hospitali.
Taarifa za kuumizwa kwa mtoto wao wa pekee ziliwafikia wazazi wa Frank na kwenda mbio hospitali waliyoelekezwa kuwa Frank yupo.
“vipi hali yake Dokta.” Aliuliza mama yake Frank baada ya kumuona daktari aliyekuwa ana muhudumia Frank.
“hali sio nzuri sana. Kwakua amepigwa sana maeneo ya kichwani, ndio sababu itakayomfanya kuchelewa kupata fahamu.” Aliongea daktari na kuwaangalia wazazi wa Frank walioonyesha kuchanganyikiwa.
“sasa baba unatusaidiaje?” aliongea mama yake Frank kinyonge
“kina kipimo cha bodymass index ndio tunachoenda kumpima muda huu ili tujue mwili wake mzima umepata majeraha kiasi gani.” Aliongea Daktari na kuingia kwenye chumba alichotaka kuingia awali. Wazazi wa Frank walirudi kwenye benchi kusibiri majibu ya kipimo hicho.
“mwanangu sijui kama atapona.” Aliongea mama yake Frank na kuanza kulia.
“mmh mke wangu. Unajichulia ukifanya hivyo. Chamsingi ni kumuombea dua apone na kuwa mzima kama zamani.” Aliongea baba yake Frank na kumbembelea mkewe.
Masaa manne baadae, Daktari aliwaita na kuwapa majibu wazazi wa Frank.
“majibu yanasema kuwa amevunjika mbavu mbili za kushoto kutokana na kupigwa na kitu au vitu vizito. Kubwa zaidi ni kuwa damu imevuja kwenye fuvu lake la kichwa. Cha kuchukuru mungu ni kwamba damu hiyo haijachanganyika na ubongo. Maana ingekuwa hivyo tungekuwa tunaongelea habari nyingine hapa. Nimewaita ili msaini kama mnakubali mtoto wenu afanyiwe operation kubwa ya kichwa ili tunusuru maisha yake.”
Aliongea Daktari na kumfanya mama yake Frank kuanza kulia.
Baba yake Frank aliamua kuanguka saini yake na Frank akapelekwa kwenye chumba maalumu cha kufanyia upasuaji.
Wiki tatu baadae, Frank alipata fahamu kwa mara ya kwanza na kuwafanya wazazi wake kumshukuru mungu kwa kumuamsha tena mtoto wao na kumpa uhai.
Frank akiwa kitandani. Alikumbuka mbali sana toka anaanza mapenzi. Alikumbuka idadi ya wasichana waliokuwa wakilia na kumpigia magoti bila kosa lolote kumfanyia. Hakuamini kuwa mapenzi hayo hayo ambaye yeye alishayapatia yangewaza kumchenjia na kutaka kumpotezea uhai.
Roho ilimuuma sana baada ya kumkumbuka Lulu. Hapo aliamini kuwa huyo ndio alikuwa chaguo lake ambalo mungu amemuandikia. Aliamini kile kilichomtokea ni adhabu kutoka kwa mungu kwa kumkataa mwanamke aliyekuwa na ndoto za kuishi naye bila kuhitaji kitu chochote kwake. Kuna wakati alikua anaamini kuwa toka aanze mapenzi, hakuna msichanana ambaye alikua na malengo naye kama Lulu. Mbali na kumtukana na kumdhalilisha, bado alikua anamuhitaji hata kwakua spare tyre.
Taratibu moyo uliokufa ulianza kurudisha matumaini baada ya picha ya Lulu kuganda ubongoni.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“mama , naomba muite Lulu aje kuniona.” Aliongea Frank baada ya mama yake kuletea chakula cha mchana.
“halafu sijamuona siku nyingi sana huyo msichana na hata nyumbani haji kuni salimia kama zamani. Nitamuonea wapi mimi?” aliongea mama yake Frank kwa sauti ya utaratibu.
“ni muhimu sana mama, nenda hata kwao.” Aliongea Frank na mama yake akakubali kufanya hivyo.
Saa moja usiku, mama yake Frank aliwasili hospitali akiwa ameongozana na Lulu. Walifika mpaka kwenye kitanda cha Frank ambaye alikuwa amelala muda huo. Lulu alishangaa kumuona Frank akiwa na bandeji mwili mzima. Ilikuwa si rahisi kumtambua kwa haraka kwa jinsi alivyoviringishwa bandeji hio mpaka usoni na kuacha mdomo, Pua na macho tu.
Mama yake Frank alimuamsha taratibu Frank. Alipoamka, alistaajabu Frank kumuona Lulu akiwa analengwa lengwa na machozi baada ya kumuona. Kingine kilichomshangaza ni jinsi Lulu alivyo vaa. Alikua kavaa nguo ndefu na kutupia ushungi aliojitanda vizuri. Muonekana wake ulizidi kuwa mzuri. Alikuwa kanenepa kiasi na kufanya Shape yake kuongezeka na kuwa bomba zaidi.
Macho ya Frank yalimuangalia na kujilaumu moyoni kumtesa msichana mzuri kama huyo.
“pole Frank.” Aliongea Lulu baada ya kumuona Frank akimuangalia.
“ahsante, nimeshapoa baada ya kukuona tu.” Aliongea Frank na mama yake akaamua kuondoka kwakua alijua kuwa maongezi yanayoendelea yalikuwa hayamuhusu.
“jamani nini tena kimekupata?” aliongea Lulu na kuonyesha ishara za kujali.
“ni mitihani tu ya dunia .” aliongea Frank na kumuangalia Lulu kwa macho ya haya.
“pole, mungu atakujaalia tu utapona.” Aliongea Lulu kwa hali ya kumuonea huruma Frank.
“Lulu, najua kuwa kwa sasa unaweza kuwaza kwa nini nimeamua kukuita. Kusema ukweli, yule msichana niliyekuambia kuwa ni chaguo la moyo wangu. Ndio aliyenisababishia yote haya. Nilipotea njia. Ila kwakua yameshanikuta makuu ndio namekukubuka na kuona thamani yako ikiwa juu ya maisha yangu yaliyobakia. Ni wazi kuwa nakupenda ingawaje nilihisi utakuwa unanibana na kutokuwa huru kuwa na wasichana wengine. Ila nakuapia kuwa hivi sasa najutia kwa kila nilichokutendea na naomba uupokee moyo wangu mkosefu mbele yako wewe uliyejaa uvumilivu na mapenzi ya kweli juu yangu. Nakutamkia kauli kutoka moyoni kuwa nahitaji msamaha wako ili niwe wako kwa mara nyingine.”
Aliongea Frank maneno hayo huku machozi yakimtoka na kumfanya Lulu mwenye machozi ya karibu kuanza kulia na yeye.
“Frank hakuna mwanaume duniani niliyeiweka rehani roho yangu kwake kama wewe. Ulinifunba macho na kuwa sioni kwa penzi lako. Ni wewe ndiye uliyenifundisha na kunionjesha matamu ya mapenzi. Na ni wewe pia ndio uliyeniingiza kwenye dimbwi la wanaolilia mapenzi na kuniumiza moyo zaidi ya nilivyoumia siku waliyokufa wazazi wangu. Kwanini Frank uliamua kunitenda?? Kwanini uliamua kuninyanyasa kwa maneno yaliyonifanya nitamani kuupoteza uhai wangu??? Kwanini ulinitamkia kuwa mimi si chaguo lako?? Kwanini Frenk??” CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Aliongea Lulu maneno hayo kwa uchungu na kumfanya machozi yaliashiria uchungu uliopo moyoni mwake kumwagika kama maji.
Hali hiyo nayo ilizidi kumuumizi Frank na kumfanya nae azidi kulia kwa uchungu. Kila akisemacho Lulu kilikua cha ukweli.
“naomba unisamehe Lulu. Unaniumiza sana kila ukinitajia mabaya niliyokufanyia.” Aliongea Frank na kuendelea kulia.
“mi nimeshakusamehe Frank, ila siwezi kuwa na wewe tena. Hivi ninavyokwambia tayari mimi ni mchumba wa mtu na mwezi ujao tunafunga ndoa. Najua inakuuma sana, lakini halikuwa lengo langu kukuumiza. Ila toka uliponiambia kuwa mimi si chaguo lako. Mapenzi yangu kwako niliyatua siku ile ile. Nimempata Mpenzi mwengine. Ananipenda na mimi nampenda pia. Na kuhakikisha hayo, nimeshabadilisha hadi dini na hivi sasa naitwa Salma.”
Aliongea Lulu na kumfanya Frank azidi kulia. Hakukua na wa kumlaumu, zaidi alijilaumu mwenyewe kwa kuacha mbachao kwa msala upitao.
Kwa shingo upande, Frank alikubaliana na matokeo na kumuomba Lulu ampe nafasi japo ya kuwa kaka yake kwakua aliamini ni faraja tosha kuwa karibu na msichana huyo hata kama sio tena mpenzi wake.
Lulu alikubali urafiki wao uendelee kama kaka na dada. Alizidi kumtembelea hospitali na Frank alipata faraja kila alipomuona Lulu.
Harusi kubwa kati ya Salim na Salma ( Lulu ) ilifungwa na watu mbali mbali wakiwemo wazazi wa Frank walihudhuria na kufurahia pamoja. Frank alishindwa kuhudhuria harusi hiyo kwakua alikua bado kitandani.
Baada ya kumaliza saba. Salma na mume wake walimtembelea Frank Hospitalini.
“Huyu ndio kaka yangu wa hiyari niliekuambia, anaitwa Frank.” Alitambulisha Salma baada ya wote kusalimiana.
“nashukuru kukufahamu.” Aliongea Frank na kutabasamu.
“Frank, huyu ndio mume wangu. Anaitwa Salim.” Aliendelea Salma na utambulisho.
“Salim, Salma… majina na hata mlivyo mmeendana pia. Hongera Salma.” Aliongea Frank na wote wakafurahi.
“ila nina ombi kwako Salim. Nakuomba uwe mwaminifu na mwenye mapenzi ya kweli kwa Salma. Huyu ni zaidi ya mke umepata. Ni zaidi ya mshauri pia ni zaidi wanawake bora ambao ulishawahi kukutana nao. Nitaumia sana nikisikia chochote kibaya kikitokea kwa huyu dada na wewe ndio ukawa msababishaji…. Ni hilo tu. Zaidi ya hayo nawatakia maisha mema na mungu awajaalie kizazi chema.” Aliongea Frank kwa uchungu moyoni lakini akiwa na tabasamu la plasitiki usoni.
Wote walicheka na Salim alimyamyuka na kumpa mkono Frank.
“nimekulewa. Nakuahidi kumpenda mpaka pumzi yangu ya mwisho wa uhai wangu.” Aliongea Salim na wote wakacheka. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
*********************** MWISHO****************
0 comments:
Post a Comment