Search This Blog

Monday, October 24, 2022

NAMPENDA ADUI YANGU - 1

 





    IMEANDIKWA NA : RAYMOND MWALONGO



    *********************************************************************************



    Chombezo : Nampenda Adui Yangu

    Sehemu Ya Kwanza (1)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ilikuwa siku ya Jumatatu mwezi Julai tarehe mosi, siku ambayo hali yake ya hewa na anga kwa ujumla vilikuwa tulivu. Majira hayo ya saa moja asubuhi hali haikuwa shwari katika eneo la mto Wami mkoani pwani. Katika eneo hilo ilikuwa imetokea ajali mbaya ya gari la mizigo aina ya ‘Scania’ lililogongana uso kwa uso na gari dogo aina ya ‘Toyota land cruiser’ lililokuwa linatoka mkoani Kilimanjaro.

    Ajali hiyo ilikuwa umbali wa nusu kilometa kuufikia mto huo, ‘Toyota land cruiser’ hiyo ilikuwa imeharibika vibaya na kupoteza muonekano ambao ilikuwa nao kabla ya ajali hiyo. Gari hilo liligeuka kuonesha matairi yake juu, kulikuwa na kelele za watu zilizotoka katika gari hilo lililokuwa pembeni kidogo ya barabara hiyo. Kelele hizo zilitoka pia kwenye ‘Scania’ lililoishia kugonga ukuta wa pembezoni mwa barabara mara baada ya kugongana na ‘land cruiser’ hiyo.

    Dakika kumi baadaye lilionekana gari aina ya ‘Toyota hilux’ likija kwa kasi eneo la tukio na lilipunguza kasi yake kadri lilivyosogelea eneo hilo, hatimaye lilisimama kando kidogo na eneo lililokuwa na ajali hiyo. Alishuka kijana mmoja ambaye kwa wastani angekadiliwa kuwa na miaka thelathini katika gari hilo dogo lililotokea upande wa mkoa wa Kilimanjaro wa barabara hiyo. Kijana huyo alitoka mbio mpaka kwenye “Scania” lililokkuwa limegonga ukuta wa pembezoni mwa barabara.

    Mara baada ya kulisogelea alishuhudia dereva wa gari hilo akiwa amebanwa na uskani wa gari hilo kifuani kwake na damu zilimtoka mdomoni hali kadharika puani. Alisikia kelele za mtu akilalamika upande wa pili wa gari hilo aliamua kuzunguka upande huo. Hilo lilifuata baada ya kuamini dereva wa gari hilo alishapoteza maisha punde alipozunguka upande wa pili alishuhudia kijana aliyehisi alikuwa utingo wa gari hilo akiwa amebanwa miguu yake na sehemu ya mbele ya gari hilo iliyokuwa imebonyea kwa kiasi kikubwa. Dakika mbili baadaye akiwa bado anahangaika ni jinsi gani atamtoa kijana huyo walifika askari wa kituo kidogo cha polisi wa eneo hilo la mto wami ambao walisikia kelele za ajali hiyo iliyotokea umbali mfupi na kituo hicho.

    Askari hao walishilikiana na kijana aliyefika eneo hilo la tukio kabla yao kumnasua mtu waliyeamini alikuwa utingo kwa kutumia jeki ya ‘Scania’ hilo kupanua sehemu aliyobanwa muda mfupi ulitumika na zoezi hilo lilikamilika na haraka walimchukua kijana huyo mpaka kwenye gari ‘Toyota hilux’ ya kijana mwokoaji aliyekuwa akitokea mkoani Kilimanjaro. Baada ya kumpakia kijana huyo aliyejeruhiwa walikimbia kuelekea eneo ambalo ‘Toyota land cruiser’ iligeuka juu kuwa chini, na chini kuwa juu walishuhudia mama mmoja akiwa amebanwa na sehemu ya chini ya gari hiyo na tayari alikuwa ameshafariki. Pembeni kidogo mwa gari hilo walimuona kijana mmoja ambaye kichwa chake kilipasuka na damu nyingi ilikuwa imemtoka na kuzunguka eneo alilokuwa. Askari mmoja alimsogelea na kumuangalia mapigo yake ya moyo, mara alipoinuka alitikisa kichwa kuashiria naye pia alishafariki.

    “Nadhani wahanga wa ajali ni hawa tu” aliongea askari mmoja akiwaeleza wenzake jambo waliloafiki lakini wakataka kuchunguza zaidi eneo hilo wakiamini huenda kuna mtu alilushwa mbali na ajali hiyo. Askari mwingine alimuamuru kijana mwenye ‘Toyota hilux’ kuandaa gari lake tayari kwa safari kuelekea hospitali wakiamini hapakuwapo na mtu mwingine.

    Kijana huyo aliingia kwenye gari lake hilo na kuliwashwa akisubili maelezo ya askari. Muda mfupi baada ya askari kuzungukazunguka eneo la tukio alisikika mmoja wao akitoa taarifa ya kumuona mtu akiwa hai akiwa ameumia vibaya. Askari wengine walikimbia na kuelekea eneo hilo na kumbeba mtu huyo aliyevuja damu na mkono wake wa kushoto ulionekana umevunjika na hakuwa na fahamu. Mara baada ya kumpakia kwenye gari safari ilianza kuelekea kijiji cha karibu cha Msata ili kupata huduma ya kwanza kwenye Zahanati ili majeruhi hao wapelekwe hospitali kubwa. Ndani ya gari hilo alikuwamo pia askari aliyeongozana na kijana mwenye gari na askari wengine walibaki eneo la tukio kuweka miili ya waliofariki katika mazingira mazuri.

    * * * *

    “Nashukuru sana ndugu yangu kwa kuniokoa” alisikika kijana mmoja mwenye kifua kipana na misuli akiwa amejiegesha kwenye kitanda chake ambaye alionekana kuvunjika mkono wake wa kushoto pia, uliofungwa ‘P.O.P’ alikuwa anamueleza kijana mwenzie aliyeshiriki kumuokoa katika ajali aliyoipata, ikiwa ni siku nne baada ya ajali hiyo kutokea “usijali ni mambo ya kawaida aahm! Naitwa John Mushi, sijui unaitwa nani?” alijibu kijana huyo na kuuliza swaliCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mimi naitwa Carlos Mato”, waliendelea na maongezi marefu na kufahamiana zaidi John Mushi alikuwa ni kijana aliyekuwa wa kwanza kufika katika eneo la ajali na kumuokoa Carlos Mato akishilikiana na askari wa kituo cha polisi Wami pamoja na kijana mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Joseph Emmanuel. Wote walikuwa wamelazwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili. Joseph alikuwa amevunjika miguu yote miwili wakati Carlos alikuwa na majeraha mengi mwilini na kuvunjika mkono wake.

    Hiyo ndiyo ilikuwa tabia yake John Mushi aliyeishi Kimara- Baruti kuwatembelea wagonjwa wake kila siku kabla ya kwenda kwenye biashara zake kariakoo. Jambo hilo liliwafariji sana Carlos na Joseph na kujenga urafiki baina yao. Baada ya wiki mbili wote walihuruhusiwa, Joseph Emmanuel anaamua kurudi kwao mkoani Mwanza, na Carlos alipelekwa nyumbani kwake Mikocheni kwenye nyumba ya kifahari aliyoijenga. Moyoni aliumia kusikia dereva wake na mama aliyemtaja kuwa ni mfanyabiashara mwenzie walifariki eneo la ajali. Lakini anajiona hana jinsi na kumuachia yote mwenyezi Mungu, kadri siku zinavyoenda John na Carlos wanakuwa marafiki na kufahamiana vizuri hadi familia zao. Carlos anamwonyesha rafiki yake biashara yake ya kuuza komputa aliyoifanyia maeneo ya Posta jijini Dar Es Salaam na kumueleza kuwa pia alikuwa na mashamba ya chai mkoani Iringa.

    Hali kadharika John anamuonesha biashara yake ya kuuza nguo aliyoifanya maeneo ya Kariakoo, wanaishi maisha ya kawaida pasipo mmoja kati yao kutaka kujua maisha ya mwenzie kwa undani zaidi. Carlos muda mwingine anaonekana mhangaikaji wa maisha kwani hata dukani kwake huwezi kumuona zaidi ya watu aliowaajili lakini John mara nyingi anakuwa dukani kwake na ananua mzigo wa nguo zake Dubai nchini United Arab Emirates (U.A.E).

    * * * *

    Carlos Mato alikuwa mzaliwa wa kijiji cha Uwemba wilayani Njombe mkoani Iringa, elimu yake ilikuwa ni kidato cha nne aliyoitimu shule ya sekondari Uwemba. Maisha yake yalikuwa na matatizo mengi yaliyoanza tangu akiwa shule ya msingi. Carlos akiwa shule alitambulika kwa tabia ya uvutaji bangi,wizi na ubabe jambo lililopelekea achukiwe na wanafunzi wenzie kwa vile aliiba vitu vyao, alikuwa na nguvu, kifua kilichojaza, kitu kilichomfanya awe akiwaonea wanafunzi wenziwe katika mambo mbalimbali ya shule hususani kuwapiga.

    Mapema mara baada ya kumaliza shule alikabiliwa na kesi iliyopelekea kushtakiwa kwenda jela miaka miwili kwa kosa la kuvunja duka kijijini kwao na kuiba kila kitu kilichokuwemo, vitu ambavyo vilikamatwa kwenye chumba chake. Baada ya shtaka hilo mtuhumiwa Carlos alianza kutumikia kifungo chake katika gereza la wilaya ya Njombe. Akiwa gerezani anaweza kufahamika haraka kutokana na ubabe wake na moyoni anaingiwa na tamaa ya kuwa jambazi mkubwa zaidi ili aweze kufanikisha ndoto zake za maisha yake. Kifungo alichokipata hakiwi funzo kwake kuachana na wizi bali kinakuwa nafasi kwake kujifunza mbinu mbalimbali za ujambazi kutoka kwa wafungwa wengine ambao walikuwa majambazi sugu. Carlos anajifunza mbinu mbalimbali za ujambazi akiwa na rafiki yake James aliyefungwa kifungo cha miaka mitatu. Baada ya miaka miwili kuisha Carlos anatoka gerezani na taarifa anazozipata kaka yake kati ya watoto wawili waliokuwa wa marehemu mzee Mato alikuwa anaumwa. Siku mbili baadaye anafariki na kumuachia wosika Carlos abadili tabia yake. Zaidi ya hilo anamuachia gari moja “Land rover” na nyumba moja akimpa jukumu la kuhakikisha mama yao anaishi maisha mazuri, hii ilifuatia kutokana na kaka yake kuwa hajaoa na kutokuwa na familia.

    Baada ya kifo cha kaka yake, Carlos anapata upenyo na njia ya kukamilisha kazi yake ya ujambazi. Anaanza kufanya ujambazi mikoa ya kanda ya kusini, akitumia gari alilloachiwa na kaka yake, mahakamani anakuwa akikabiliwa na kesi kadhaa ambazo anazishinda kutokana na ukosefu wa vielelezo kamili vya uhalifu wake. Mwaka mmoja baadaye anamuajili James aliuyemuacha gerezani na kazi yao inakamilika maradufu. Tayari Carlos anafanikiwa kumiliki nyumba kadhaa na maduka wilayani Njombe. Baada ya mafanikio hayo ya miaka kadhaa anaamua kuamia jijini Dar es salaam na kufungua biashara zake sambamba na kuongeza mtandao wake wa ujambazi kwa kuajili vijana wengine wengi.

    Siku ya Jumatatu mwezi Julai tarehe mosi, siku ambayo Carlos Mato alipata ajali ni siku ambayo alitoka mkoani Moshi kufanya utafiti wa kuangalia uwezekano wa kufanya ujambazi katika benki ya Moshi Investment bank (MIB) iliyokuwako Moshi mjini mkoani Kilimanjaro. Alishapata mbinu na kuandaa mipango kabambe ya kuwapa vijana wake ili waweze kupora mamilioni ya fedha katika benki hiyo. Lakini mipango hiyo ilikwamishwa na ajali aliyoipata ya gari lao kugongana uso kwa uso na lori la mizigo. Baada ya miezi mitatu ya kuuguza majeraha yake Carlos anajitambua kuwa alikuwa ameshapona kabisa. Anaona huo ni muda muafaka wa kuendeleza kazi ya kundi lake lililoitwa ‘Tanzanian Gangstars’ zilizokuwa zinafifia wakati wa ugonjwa wake. Anachukua simu kwa nia ya kumpigia kijana wake James aliyemuamini katika kazi. “James nawahitaji haraka nyumbani mikocheni na wenzio wote kwa ajili ya kikao” alisikika Carlos kwa sauti yake ya kukwaluza.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ndiyo bosi nimekuelewa” ulijibu upande wa pili simu, ikiashiria James alielewa

    Baada ya dakika arobaini na tano magari saba ya kutembelea ya aina tofauti yaliwasili nyumbani kwa Mr. Carlos kwa muda tofauti. Vijana hao waliokuwa wakiwasili huku wengi wao wakiwa wamevaa miwani ya rangi nyeusi waliongoza eneo la chini la nyumba ya ghorofa ya Mr Carlos ambalo lilichimbwa wakati wa ujenzi wa nyumba hiyo. Eneo hilo lilikuwa tulivu na hakuna aliyeruhusiwa kuingia humo zaidi ya Carlos na vijana wake. Siku zote Carlos hakupenda kufanyia vikao vya kazi zao sehemu nyingine zaidi ya nyumbani kwake akiamni palikuwa salama zaidi tofauti na mahotelini na sehemu nyinginezo.

    Mara baada ya Mr Carlos kufungua kikao hicho vijana wake walikaa kimya wakijua angetoa mipango kadhaa ya kufanikisha jambo la ujambazi. Hilo ndilo lililotokea, Mr Carlos alitoa mipango kadhaa ya kufanikisha zoezi la ujambazi katika benki ya Moshi Investment bank (MIB) ambayo vijana wake walikubali na alitoa siku mbili za zoezi hilo kukamilika ikiwa ni pamoja na kutoa silaha za kufanikisha ujambazi huo.

    * * * *

    Hali ya hewa ikiwa shwari mkoani Moshi majira ya saa saba mchana lilioneka gari aina ya “Toyota mark II” likipaki mbele ya Moshi Investment bank (MIB) iliyokuwa umbali mfupi tokea eneo iliopo stendi kuu ya mabasi ya Moshi mjini. Walishuka watu watatu, wawili wakiwa wamevaa suti za kiitaliano na mmoja wao alivaa suti wavaazo wachungaji wa madhehebu ya dini za kikristo. Waliongoza kuelekea mlango wa benki hiyo, vijana wawili wenye suti za kiitaliano walimfuata nyuma yule aliyevaa suti zifananazo na za wachungaji wakiwa wamebeba mabegi yenye muonekano wa kiofisi mikononi mwao. Waliongoza mpaka ndani na kuelekea eneo la maelezo ya taarifa mbalimbali zinazohusu benki. Kijana aliyevaa suti inayowiana na za wachungaji alianza kutoa maelezo akiongea na mhudumu wa meza hiyo.

    “Mimi ni mchungaji wa kanisa la Born Again Christianity Church lililopo Kibosho wilaya ya Moshi vijijini”

    “Nakusikiliza unataka nikusaidie nini” alisikika dada huyo aliyekuwa akipanga karatasi mezani”tunapesa nyingi tunataka huduma ya kuwa sehemu tulivu tuhifadhi fedha za kanisa.

    “huduma hiyo ipo ila zinafika milioni ishirini?

    “ndiyo zinafika” alijibu mchungaji kama alivyojitambulisha

    “basi nifuateni………” aliongea dada huyo akimuacha dada mwenzie kwenye meza hiyo, wakati huo kulikuwa na foleni za mistari mitano ya watu waliokuwa wanawapeleka kuhifadhi au kutoa fedha zao katika madirisha madogo ya huduma hiyo.

    Aliyejitambulisha mchungaji na wenzie walimfuata yule dada wa mapokezi ambaye aliwapeleka chumba kimoja pembeni kidogo na madirisha ya kupokelea fedha na alirudi kuendelea na majukumu yake. Katika chumba hicho walimuona mama mmoja aliyekuwa wa makamo, mara baada ya kuvuta viti na kukaa walidai walitaka kuweka fedha milioni themanini. Aliwapa lisiti ya kuwekea fedha “pay-in-slip”, na mchungaji akaanza kuijaza, mara baada ya kuijaza alimkabidhi na kuchukua moja ya begi walilobeba wenzie akaanza kutoa fedha zilizotungwa vizuri ambazo zingekadiliwa kuwa ni milioni moja. Baada ya kutoa mafungu hayo ya fedha mara tano, mara ya sita mkono wake ulitoka na Bastola aliyomuelekezea yule mama kwenye paji lake la uso.

    “kimya! kwa usalama wako usitoe hata miguno ya kelele”, alisikika mtu huyo ambaye awali alijitambulisha kuwa ni mchungaji, wakati hayo yakiendelea wenzie nao walichukua bastola mbili kwenye lilelile begi nao pia walimuonesha yule mama “sasa tunataka utoe fedha zote zilizopo humu ndani” alisikika tena akimuamuru yule mama ambaye alikuwa akitetemeka kupindukia. Amri hiyo alikuwa kama hajaielewa na baada ya dakika kadhaa za kurudiwa amri hiyo, Alianza kutoa fedha ambazo zilikuwepo kwenye chumba hicho, na kuziweka mezani kijana mwenye suti ya kichungaji alimkonyeza mmoja kati ya wale wawili ambaye kwa haraka haraka alizichukua fedha hizo na kuziweka kwenye lile begi lililochukua fedha hizo lililokuwa mezani. Begi ambalo aliweka fedha ambazo pia walikuja nazo na dakika moja baadaye lilikuwa limejaa. Akachukua begi jingine ambalo lilikuwa halina kitu na kuanza kuweka fedha nyingine katika begi hilo.

    “Wewe usilete ujinga hatutaki kumwaga damu” alisikika tena, mara baada ya kuona alitoa fedha hizo kwa kasi ndogo.

    Dakika tano baadaye mabegi yote yalikuwa yamejaa fedha na tayari zilikuwa zinawatosha hawakuwa na begi jingine la kubeba. Walimuamuru yule mama kulala chini kifudifudi, ambaye tayari alikwisha jisahidia haja ndogo, haraka alitimiza amri hiyo. “pesa hizi hazitutoshi! Ebu vamieni na vyumba vingine” alipaza sauti mmoja wa watu hao lengo likiwa kumfanya mama huyo aelewe kuwa bado waliitaji fedha “we mama ukijitikisa tu, nakusambaratisha mgongo wako” alisikika mmoja wa watu hao jambo lililomfanya mama huyo atulie kwa uoga na mwishoe aliishia kupoteza fahamu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Taratibu waliinua mabegi yao na kuufungua mlango polepole na kuanza kuelekea nje mwa benki hiyo, walitoka katika uwazi wa benki hiyo sehemu ambayo shughuli za kibenki ziliendelea, walitembea kiustaarabu na hakuna mtu aliyehisi kuwa walikuwa wameshafanya ujambazi wa fedha nyingi. Hatimaye walifika katika meza ya maelezo na kutoa shukrani zao. Waliongoza na mwendo wao wa polepole mpaka nje kwenye gari lao “Toyota mark II” na kuliwasha na waliliondoa benki hapo kwa mwendo wa taratibu ili wasigundulike na askari waliokuwa nje ya benki hiyo.

    Baada ya kuwa mbali na benki wakiwa wanaelekea barabara inayoenda mkoani Arusha, waliongeza kasi ya gari lao ambayo haikuwa ya kawaida. Dakika ishirini baadaye walikuwa eneo la uwazi la wilaya ya Hai, walipunguza kasi ya gari lao baada ya kuliona gari jingine aina ya “Mercedez Benz” lililosimama pembeni mwa barabara kuelekezwa Moshi mjini. Pembeni mwa gari hiyo alikuwako kijana mwingine ambaye pia alivaa suti akiwaelekeza wasimame.

    Mara baada ya kusimama, haraka walihamia kwenye lile gari aina ya “Mercedez Benz” na waliacha bomu lililobakiwa na dakika nane kwenye ile “Toyota mark II” waliyokuwa nayo awali, waliondoa lile “Mercedez Benz” kwa mwendo kasi wa kawaida wakiwa wanaelekea Moshi mjini ambako ndiko wale vijana watatu walikuwa wameshafanya uharifu. “Du! James we mkali” alisikika kijana jambazi akimpongeza mwenzie James “we unafikili mbinu za Carlos ni za kitoto” walifurahia na kuamini walishashinda mamilioni ya fedha ambayo hata wao hawakujua kuwa zilikuwa shilingi ngapi?. Muda huo walikuwa na lengo la kuutoroka mkoa huo wa Kilimanjaro ili kukamilisha ushindi waliamini bomu waliloliacha kwenye “Toyota mark II” wangewapoteza kabisa askari kama wangejaribu kuwafuatilia.

    Dakika tano baadaye wakiwa usawa wa njia panda ya barabara ielekeayo Kibosho, Moshi vijijini walishuhudia gari tatu za polisi zilizopiga vingora zikielekea barabara ya Arusha ambako ndiko walitokea. Wote walijikuta wakicheka baada ya kuamini hakuna ambalo wangalipata askari hao. Kilichofuata ni kuongeza kasi ili kuachana na mkoa wa Kilimanjaro wakifuata barabara kuu ielekeayo mkoani Tanga na Dar Es Salaam.

    * * * *

    Muda mfupi baada ya mchungaji na watu wake kuondoka, kama alivyoamini dada wa meza ya maelezo. Walifika watu wengine ambao pia walikuwa na pesa nyingi akawa anawaongoza kuelekea kwenye chumba maalum kwa wateja kama hao. Punde tu baada ya kufungua alimuona mama wa makamo waliyemtambua zaidi kwa jina la mama Massawe akiwa amelala kifudifudi huku akiwa amezungukwa na kiasi kidogo cha majimaji. Jambo hilo lilimfanya apige kelele na wafanyakazi wenzie wakaenda mbio kuona ni nini kilichotokea. Wakati huo askari wa benki walikuwa tayari wakijua kulikuwa na tatizo limejitokeza, wafanyakazi hao walianza kumpepelea hewa ili aweze kizinduka, mara tu alipozinduka alisikika akilalamika “majambazi, majambazi …….”. baada ya kutulia kidogo alitoa maelezo juu ya majambazi hao walijitambulisha walitokea katika kanisa la ‘Bom Again Christianity church’.

    Haraka ilipigwa simu polisi na gari mbili za polisi zilifika benki hapo na baada ya uchunguzi wa haraka walibaini gari la majambazi hao lilikuwa limeelekea njia ya Arusha, waliondoa gari zao kwa kasi likiongezeka na jingine la askari wa benki hiyo na kufanya magari hayo kuwa matatu.

    Askari hao walipiga simu kwa askari wa mkoa wa Arusha kuwataarifu wakague kila gari ambalo lingeingia mkoani humo. Kilometa kadhaa toka Moshi mjini wakiwa eneo la wilaya ya Hai walishuudia gari likiwa limelipuka na moto mkubwa ukiwaka waliegesha gari zao umbali mrefu kidogo na kuanza kulitathimini gari hilo ambalo mabati yake yalirushwa kila upande wa barabara hiyo, mmoja wa askari wa benki alidai anaamini lile ndilo gari waliloondoka nalo majambazi katika benki ya Moshi Investment Bank (MIB) na aliamini huenda walipata ajali.

    Mkuu wa kituo cha polisi wilaya ya Moshi mjini aliamuru gari moja la polisi na lile la askari wa benki yaendelee na safari ya kutukuzia majambazi katika barabara ielekeayo Arusha. Hilo lilifuatia baada ya kuhisi ajali hiyo haihusiani na majambazi hao,alibaki na askari wengine ili wafanye uchunguzi katika ajali ya gari lile lililokuwa linawaka moto. Baada ya saa moja na robo la kuwaka gari hilo Afisa mkuu wa polisi alisogea na askari wake eneo lililowaka gari hilo. Hakuna kitu walichokiona kama kielelezo cha jambo lolote zaidi ya kiasi kidogo cha majivu na vyuma vigumu ambavyo havikuungua. Hata ikatimia masaa matatu hapakuwa na taarifa za kukamatwa kwa majambazi eneo lolote

    * * * *CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “niliwaambia vijana wangu, si mmeona? kulipuwa gari la milioni nne na kupta milioni sabini kuna hasara gani?” alisikika Carlos kwa sauti ya kukwaruza akiwa na vijana wake wakipongezana kwa kufanikisha ujambazi wa milioni sabini. Kikao chao hicho kilikuwa kinaendelea muda huo kama kawaida kwenye nyumba yake maeneo ya Mikocheni Dar es salaam. Wakati wakiendelea na kikao hicho alimsifu James ambaye alikuwa anamuamini kuliko wote kati ya vijana wake. Hiyo ilitokana na James kujua mbinu nyingi ambazo waliwahi kujifunza wote walipokutana gereza la wilaya ya Njombe.

    Maisha ya Carlos na kundi lake la ujambazi la Tanzania Gansters yaliendelea kama kawaida huku akijitahidi kuhakikisha siri ya kazi yake hiyo haivuji. Matukio ya ujambazi makubwa yanaendelea nchini Tanzania, kitu kinachowafanya makamanda wa polisi wa mikoa kukosa jibu kabisa. Baada ya miaka kadhaa jina la Carlos Mato linaanza kufahamika na kusikika masikioni mwa watu kutokana na uwezo wake wa kifedha. Watu wengi wanaamini mafanikio yake yametokana na maduka ambayo anayamilikia sehemu tofauti za jiji la Dar es salaam.

    Urafiki wa Carlos Mato na John Mushi ambaye pia alijijenga kiasi Fulani kiuchumi,unakuwa zaidi ya awali. Carlos na mkewe mzaliwa wa mkoa wa Pwani walishabahatika kupata mtoto aliyeitwa Jane. Carlos alimpenda sana mkewe kutokana na usiri mkubwa wa mke wake aliyejua kazi aliyoifanya mumewe. Wakati huo Jane alisoma shule ya msingi ya kimataifa, shule ambayo mtoto wa John Mushi aliyeitwa Juliana pia alisoma. Jane na Juliana walikuwa marafiki kutokana na urafiki wa wazazi wao na walichukuliana kama ndugu wa familia moja.





    * * * *



    Jane na Juliana baada ya kumaliza masomo yao ya awali ya shule ya msingi nchini, walijiunga na shule ya sekondari ya Northern England katika jimbo la Middlesbrough nchini Uingereza. Furaha ndiyo inatawala mioyo yao wakiwa na amani kutokana na kutimiziwa kila kitu walicho kihitaji kutoka kwa wazazi wao. Walikuwa wakirudi Tanzania kila baada ya miezi sita kwa ajili ya likizo. Carlos na John walikuwa wakipokezana kuwapeleka mabinti zao pindi shule ilipokuwa ikifungua. Wakiwa mwaka wa pili wa masomo yao wanarudi likizo nchini Tanzania ya miezi miwili wanaonekena wakiwa na maumbile makubwa kama walizaliwa miaka ishirini iliyopita, uzuri wa sura zao na muonekano wa urembo walionao unakuwa kivutio kwa watu wanaodhani ni mapacha. Hiyo ilitokana pia na kuwa kwao pamoja kila sehemu waliyoelekea. Pamoja na maumbile yao kuwa makubwa wote wana umri wa miaka kumi na sita. Baada ya mapumziko yao hapa nchini Tanzania wanasindikizwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu J.K Nyerere tayari kwa safari kwa kutumia shirika ndege la Tanzania Airways. Familia zote mbili zina jumuika kuwaaga na walikuwa wakiongozana na Carlos ambaye ni baba yake Jane.

    Safari inaanza wakitarajia kupitia miji ya Addis Ababa wa Ethiopia, Cairo nchini Misri na hatimaye London nchini Uingereza. Carlos alikuwa amekaa na Juliana katika siti mbili zilizokuwa zinafuatana, katika muda wote wa safari Juliana aliyekuwa mcheshi aliutumia kumsimlia Mr Carlos mambo mbalimbali ya nchini Uingereza. Safari iliendelea na simulizi zake kwa mjomba wake Mr Carlos kama alivyo mtambua kutoka utoto wake ziliendelea.

    Mr Carlos ambaye kwa muda mrefu alikuwa kimya akimsikiliza Juliana, aliingiwa na tamaa ambayo alijitahidi kuizuia ili isije ikatokea katika maisha yake. Alimtamani kimapenzi mtoto wa rafiki yake wa siku nyingi bwana John Mushi yaani Juliana. Kadri safari ilivyoendelea tamaa hizo ziliongezeka na alijaribu kushiriki mazungumzo yao na Juliana ili kupoteza tamaa zake, haikuwa hivyo. Wakati huo Jane alikuwa siti ya nyuma yao na hakufuatilia maongezi hayo. Baada ya muda mrefu wa ucheshi wake Juliana alisinzia na kuegemea bega la mjomba yake Mr Carlos. Ni muda ambao Mr Carlos aliutumia kuchunguza uzuri wa mtoto wa rafiki yake na kuweza kugundua mengi, kutokana na aina ya nguo ya kubana aliyoivaa Juliana. Moyoni alivunja dhana ya uoga na kujikuta akiweka dhamira ya kuhakikisha anampata kimapeanzi katika siku za usoni. Heshima aliyo jijengea kwa rafiki yake John anaipoteza ndani ya dakika chache za maamuzi yake.

    Hatimaye safari inakamilika baada ya kuwafikisha wanafunzi hao shule ya Northern England katika jimbo la Middlesbrough nchini Uingereza na anawaachia fedha za kutosha, hata hivyo Juliana hukugundua jambo lolote lililokuwa kichwani mwa mjomba wake Carlos.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    * * * *

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog