Search This Blog

Monday, October 24, 2022

NAMPENDA ADUI YANGU - 2

 







    Chombezo : Nampenda Adui Yangu

    Sehemu Ya Pili (2)





    Ilipoishia...



    Moyoni alivunja dhana ya uoga na kujikuta akiweka dhamira ya kuhakikisha anampata kimapeanzi katika siku za usoni. Heshima aliyo jijengea kwa rafiki yake John anaipoteza ndani ya dakika chache za maamuzi yake.

    Hatimaye safari inakamilika baada ya kuwafikisha wanafunzi hao shule ya Northern England katika jimbo la Middlesbrough nchini Uingereza na anawaachia fedha za kutosha, hata hivyo Juliana hukugundua jambo lolote lililokuwa kichwani mwa mjomba wake Carlos.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    * * * *

    Endelea....





    John alikuwa amejijenga katika biashara zake akiwa na uwezo wa kuingiza Tanzania kontena tano za mzigo wa nguo. Nguo alizonunua Dubai nchini United Arab Emirates (U.A.E). Hakuwa na shaka kwa mahitaji ya familia na ndugu zake walioishi kwao wilaya ya Moshi vijijini mkoani Kilimanjaro. Siku zote alimtegemea mtoto wake wa kwamza Juliana akiamini akisoma atakuwa tegemeo la familia. Alimpenda sana kitu kilichomfanya amtimizie mahitaji yake yote aliyohitaji. John alibahatika kupata watoto wawili tu, Juliana na Kenny aliyekuwa na umri wa miaka mitano.

    Mr Carlos baada ya kurudi Tanzania alielekea moja kwa moja nyumbani kwake Mikocheni na kulakiwa na mkewe. Hakupenda watoto wake wawepo nyumbani hivyo kujenga mazingira ya wanawe kutojua shughuli alioifanya, ikiwa ni pamoja na vikao vya ujambazi. Kudhihirisha hilo hata mtoto wake wa mwisho aliyekuwa na miaka minne kati ya watoto wake watatu alikuwa amepelekwa shule ya bweni, watoto wake hao walikuwa ni Jane aliyekuwa masomoni Uingereza, Steve aliyekuwa na miaka kumi na wa mwisho aliitwa Mary.

    Carlos aliendeleza shughuli zake na kundi lake la ujambazi la Tanzania Gangstars kwa umakini mkubwa. Dhamira yake ya kumpata Juliana kimapenzi bado ilimkaa kichwani na aliwaza kuifanikisha kwa njia yeyote. Anaendeleza urafiki wa karibu na John asiye tambua dhamira ya Carlos kwa mwanae Juliana. Miezi sita baadae Jane na Juliana wanarejea tena Tanzania kwa ajili ya likizo yao nyingine tena. Ujio wao unakuwa wa faraja kwa Carlos ambaye sio kwamba alimkumbuka mwanae tu bali pia ilikuwa wakati wa kuhakikisha anampata Juliana.

    Kadri siku zilivyokuwa zinaenda Carlos alitafuta njia ya kumpata Juliana lakini hakufanikiwa, mpaka akaanza kupoteza matumainia ya kumpata, muda mwingi Jane alikuwa na Juliana kama ilivyo kuwa kawaida yao. Siku moja ya Jumapili wakati Mr Carlos akiendesha gari lake kutoka kwenye geti la nyumba yake ya kifahari. Ikiwa yapata saa tisa na nusu alasiri mara tu baada ya kutoka nje ya geti hilo alishuhudia gari dogo “Toyota mark II” likiwa na uelekeo wa kuingia nyumbani kwake. Alifunga breki za gari lake na kuziba sehemu ya mbele ya geti hilo. Hatimaye ile “Toyota mark II” nayo ilisimama na alishuka msichana mmoja mrembo na mrefu aliyependeza kwa nguo alizovaa. Toka chini mpaka juu alivaa mavazi yenye rangi nyekundu ikiwa ni pamoja na pochi aliyoishika mkononi, Mr Carlos moyo wake ulilipuka kwa furaha baada ya kugundua alikuwa ni Juliana.

    Juliana alisogelea kwenye gari lake na kumsalimia Mr Carlos ikiwa ni baada ya kumpa fedha dereva taksi wa “Toyota mark II” ambaye aligeuza gari lake na kuondoka.

    “Anko unaenda wapi tena? Mimi ndiyo nakuja kwenu hivyo” alimuuliza Juliana, Mr Carlos ambaye mawazo yake tayari yalishafika mbali akiamini ni lazima siku hiyo afanye mapenzi na Juliana hata ikimbidi atumie nguvu ya ziada . “aah! huko hakuna mtu Jully” alimjibu Mr Carlos akiwa ameutupisha jina hilo kama ilivyokuwa kawaida yao. Carlos alimueleza Juliana kuwa Jane alikuwa ameondoka na mama yake na kumuahidi angempeleka sehemu waliyokuwapo kwa mapumziko. Baada ya kusikia hayo Juliana alifungua mlango wa nyuma wa gari aina ya “Toyota Surf” na kukaa katikati ya viti vyake.

    Mr Carlos aliendesha gari kuliondoa mlangoni alipo liegesha na kuliegesha tena pembeni kidogo. Alimueleza Juliana kuwa anaenda kuchukua fedha hivyo asubiri kidogo jambo ambalo alimuelewa mjomba wake. Alibaki ndani ya gari hilo ambalo vioo vyake havikuruhusu mtu wa nje kona yaliyokuwa ya kijiri ndani ya gari hilo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mr Carlos alitumia mlango mdogo wa geti la nyumba yake aliingia na kunyoosha kuelekea sehemu ya chini ya nyumba yake. Mara baada ya kuingia katika sehemu hiyo ambayo ni maalumu kwa vikao na vijana wake aliongoza mpaka kwenye stoo ya silaha. Punde alipofungua alichukua begi dogo na kuweka bastola ikiwa na risasi alichukua bomba la sinidano na kufyonza aina fulani ya dawa iliyokuwa kwenye kichupa kidogo. Baada ya dawa hiyo kumtosha nayo aliiweka kwenye lile begi, aliongeza kisu, kiberiti pomoja na misokoto miwili ya bangi. Alianza kuondoka katika sehemu hiyo ya chini ya nyumba yake baada ya kufunga milango yote. Taratibu alisogelea geti na kumuaga mlinzi kwa mara ya pili ambaye naye pia alikuwa ni jambazi. Alipenda kuajili watu hao ili kutunza siri za kazi zake. Alilisogelea gari lake na kufungua mlango wa nyuma wa gari hilo ambako Juliana alikaa akimsubiri. Mara baada ya kufungua alikaa siti ya pembeni na Juliana akasikika kwa sauti ya chini akimueleza Juliana “kuna majambazi wamevamia eneo hili” aliongea akiwa amemgeukia dada huyo, “unasemaje majomba….” Alishtuka Juliana na kuuliza sentensi ambayo hakuimalizia, Mr Carlos alimbana mdomo wake kwa mkono wa kushoto uliokuwa na kitambaa chake cheupe. Juliana alijaribu kutoa mkono huo lakini ilishindikana, kwa kasi Mr Carlos alitoa bomba la sindano kwenye begi lake na kumchoma kwenye moja ya mishipa ya Juliana ya shingoni. Alimbana zaidi kwa mikono miwili ili asiweze kujitoa, kwani Juliana aliagaika kwa kila namna ili ajinasue kwenye mikono ya Mr Carlos.

    Dakika tano baadae Juliana alitulia kabisa hakuchezesha hata mkono wake. Ni muda ambao Mr Carlos alishuka na kufunga milango sawasawa kabla ya kuzunguka upande wa pili wa uskani na kuwasha gari, aliliondoa kwa kasi eneo la nyumbani kwake. Baada ya masaa matatu walikuwa eneo la kilometa kadhaa kando ya mto Ruvu mkoani Pwani. Alikuwa katika eneo lililokuwa na vichaka vingi ambalo halikuwa ma makazi ya watu. Juliana alilazwa katikati ya siti za nyuma za gari la Mr Carlos, alionekana kuwa katika usingizi mzito. Hakuwa amevaa nguo hata moja, alikuwa mtupu kama alivyozaliwa. Mr Carlos ndiye aliyemvua nguo hizo na aliziweka pembeni kidogo mwa gari hilo mara baada ya kufunga milango yote ya gari lake. Mkononi alikuwa ameshika msokoto wa bangi akiuvuta akiwa ameegemea gari lake. Mwanzoni hakupanga kumuua Juliana ila alifikiria kufanya hivyo ikabidi. Alipanga kuongea na Juliana ili awe msichana wake wa starehe ya ngono. Mara baada ya kumaliza kuvuta misokoto miwili aliyokuwa ameiweka awali nyumbani kwake alimsubiri Juliana azinduke kutoka usingizini. Ilikuwa yapata saa kumi na mbili na nusu, alihisi gari lake likitikisika hivyo haraka akaingia kwenye gari alimuona Juliana akiwa amezinduka lakini alijishangaa.Baada ya kutoelewana maongezi yao yaliyojaa ubishani kwa muda mrefu, Mr Carlos alichukuwa jukumu la kuanza kumbaka. Masaa matatu baadae alikuwa ameshatimiza zoezi lake, muda huo Juliana alikuwa ameshapoteza fahamu.

    Mr Carlos alichukua simu yake na kumpigia kijana wake aliyemuamini James na kumuelekeza sehemu alipo, akimtaka aende eneo hilo la Ruvu, baada ya zoezi la kupiga simu aliizima kabisa. Masaa mawili baadaye James alikuwa amewasili eneo husika na kuelezwa yote yaliyokuwa yametokea. Lengo la Mr Carlos lilikuwa ni kutaka kumuua Juliana, alitaka amsidie kumtupa msichana huyo katika mto Ruvu. Baada ya kuelewana vizuri Mr Carlos alitoa kisu kilichokuwa na ncha kali kwenye begi lake na kuingia ndani ya gari na kumtoa Juliana. Mara baada ya kumtoa Juliana alimueleza James kuwa amzibe mdomo Juliana ambaye alikuwa bado kapoteza fahamu. Bila ya huruma Mr Carlos alimshindilia Juliana kisu alichokielekeza kifuani mwa msichana huyo mara tatu. Walimshikilia kwa muda kidogo wakati akijaribu kujitupa huku na huko na mwishowe alituria kabisa. Walimbeba juujuu kuelekea upande ambao kulikuwa na mto Ruvu, wakiziacha gari zao zikiwa hazijawashwa hata taa moja na kufanya eneo hilo kuwa la giza. Baada ya kutembea kwa muda mfupi waliufikia mto huo na kuurusha mwili wa Juliana kwenye maji. Walirudi kwa kukimbia eneo waliloacha magari yao, Mr Carlos alichukua jukumu la kuchoma nguo ambazo awali alimvua Juliana.

    “James hii ni siri, kama zilivyo siri zetu za ujambazi” alisikika Mr Carlos akimweleza James “bila shaka” alijibu James kikamavu kumhakikishia bosi wake kutovuja kwa siri hiyo, waliwasha magari yao na kuondoka kwa kasi eneo hilo na safari ikaanza ya wao kurudi jijini Dar es salaam.

    * * * *CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Saa kumi na moja asubuhi simu ya Mr Carlos iliita ikiwa ni dakika chache tu tangu aiwashe mara baada ya kusoma jina anagundua ni rafiki yake Mr John Mushi. Bila uoga anaipokea “haloo” “haloo vipi Mr Carlos nimekutafuta sana toka jana” aliuliza Mr John sauti iliyomfikia Carlos kupitia spika yake ya simu.

    Pole rafiki yangu nilichoka sana, jana hivyo ikanibidi nizime simu mapema na kulala, kwani vipi?”aliuliza Mr Carlos ingawaje jibu alilijua

    “Juliana hakurudi jana nyumbani, kwani hakuja kwenu”? “hapana hakuja…..” alijibu Mr Carlos ambaye baada ya kujua tatizo la rafiki yake John Mushi alimuahidi angekuwa nyumbani kwake baada ya muda mfupi. Alimweleza John kuwa hilo lilikuwa tatizo kubwa na lilihitaji ufumbuzi wa haraka.Mr Carlos alimuaga mkewe na kuondoka alfajiri hiyo akimweleza kuwa rafiki yake John alikuwa na matatizo

    Hakuchukua muda mrefu sana Mr Carlos alikuwa akipiga honi ya gari yake mbele ya geti la nyumba ya John Mushi iliyokuwa Kimara Baruti, mara baada ya geti hilo kufunguliwa aliendesha gari lake mpaka sehemu ya kuegesha magari. Alipokelewa na John aliyekuwa nje wakati huo, ambaye alimueleza kwa uchungu hofu yake kwa mwanae ambaye hakurudi nyumbani.Mkewe na mwanae mdogo Kenny walikuwa wakilia kutokana na hofu ya uhai wa Juliana. John na Carlos waliongozana mpaka ndani na kuanza kushauriana juu ya jambo hilo, tayari simu ilikwisha pigwa kituo cha polisi kutoa taarifa ya kupotea kwa Juliana jambo ambalo John alikuwa ameshakwisha lifanya. Taarifa hiyo kituo cha polisi haikusaidia kwani mpaka inatimia saa tano asubuhi, hapakuwepo na taarifa zozote za kupatikana Juliana. Mr Carlos aliyeonekana kuwa na majonzi makubwa alishirikiana bega kwa bega na rafiki yake kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo, hatimaye Mr Carlos anaamua kuchukua jukumu la kugharamia matangazo katika vituo vya televisheni na radio kutangaza kupotea kwa Juliana. Matangazo hayo nayo hayasaidii lolote kwani hakuna taarifa zinazopatikana.

    Maelezo ya mlinzi wa Mr John anadai siku ya tukio la kupotea kwa Juliana aliondoka akidai angerudi baada ya muda mfupi na hajui kilichoendelea. Mchakato wa kumtafuta Juliana unaendelea pasipo mafanikio, hata siku nne zinapita bila kupatikana kwake. Tayari vijana kadhaa wasio na ajira wanaoishi maeneo ya Kimara Baruti wanakamatwa, likiwa ni shinikizo la Mr Carlos. Alidaiwa huenda vijana hao waliokaa vijiweni walihusika kwa namna moja au nyingine hivyo walitaka maelezo yoyote kutoka kwa vijana hao.

    Hata hivyo hakuna lililofanikiwa, siku ya tano zilipatikana taarifa za kutolewa mwili wa msichana ulioharibika vibaya katika mto Ruvu. Jambo lililomfanya Mr John kuhitaji kuutambua mwili huo, aliongozana na rafiki yake Carlos mpaka katika hospitali kuu ya taifa ya Muhimbili.Mara baada ya John Mushi kuuona mwili huo akiwa rafiki zake kadhaa akiwemo Mr Carlos hakutambua chochote. Hiyo ilitokana na kuharibika kwa mwili huo ambao hata sura yake haikueleweka hata kidogo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Madaktari walichukua jukumu la kuanza kufanya uchunguzi wa mwili huo. Masaa nane baadaye wanatoa taarifa kuhusu mwili huo kuwa ulikuwa wa Juliana. Walidai alibakwa kabla ya kuuawa kwa kuchomwa na kisu chenye ncha kali kifuani mwake. Taarifa hizo zinammaliza nguvu John Mushi haamini aaliyoyasikia lakini anajikaza kiume akisaidiwa na rafiki zake wakiongozwa na Mr Carlos. Mikakati ya mazishi inaanza kufanyika ikiongozwa na Mr Carlos ambaye anagharamia mambo mengi muhimu ya msiba huo. Baada ya maandalizi yote kukamilika mwili huo unasafilishwa kuelekea mkoani Kilimanjaro kwa maziko.

    Familia ya Mr John inajawa na majonzi ikiwa ni pamoja na ndugu na jamaa waliojumuika katika msiba huo wa kusikitisha. Jane analia kwa uchungu akiwa haelewi kisa cha kifo cha rafiki yake waliyejaliana kama ndugu. Baada ya mazishi kufanyika wilaya ya Moshi vijijini eneo la Kibosho ,watu wanatawanyika na siku kadhaa baadae John anarudi jijini kuendeleza shughuli zake.hasira zake ni kwa mtu aliyemfanyia kitendo cha unyama mwanae.Anawahimiza askari wa jeshi la polisi kuendeleza jitihada kuhakikisha aliyehusika na mauaji hayo ya kinyama anakamatwa.

    John hakusahau fadhila alizofanyiwa na mr. Carlos katika kipindi kigumu cha kumtafuta mwanae ikiwa ni pamoja na gharama alizogharamia katika msiba.Anaandaa siku maalum ambayo anaenda na familia yake nyumbani kwa mr.Carlos kushukuru fadhira zake. Bado mr.Carlos anamuahidi kuendelea kushirikiana naye kuhakikisha aliyehusika na tukio hilo anakamatwa .

    Mwezi mmoja baadae hali ya kiafya ya John inadhoofu kwa kiasi fulani hii ilitokana na kutopata taarifa zozote za muuaji wa mwanae. Lakini anafarijika na mawazo tofauti aliyoona yanamjenga aliyopewa na rafiki yake wa karibu mr.Carlos.

    * * * *



    Katika matendo mengi ya kinyama aliyoyafanya katika maisha yake , mr.Carlos hakuna hata mkasa ambao ulimgusa zaidi ya ule aliomfanyia Juliana. Hiyo yote ilitokana na ukaribu wake na John Mushi, ikiwa pamoja na msichana huyo aliyekua akiwa anamuona tangu utoto wake. Hata hivyo jambo hilo halimuumizi kichwa na analichukulia kama la kawaida tu . Katika upelelezi wa kesi hiyo Mr. Carlos anachangia kuudhoofisha baada ya kumshauri John wasubiri ushauri wa polisi , jambo hilo linasababisha ufuatiliuaji mubovu wa kesi hiyo unaofifia siku hadi siku.

    Baada ya muda mrefu kuwa na rafiki yake, akimfariji kwa matatizo aliyoyapata. Mr Carlos anaamua kuandaa mbinu za kufanya ujambazi katika kiwanda cha pamba mkoani Mwanza. Kufanikisha hilo anaamua kusafiri kwa ndege hadi mkoni Mwanza na kuanza upelelezi wake mwenyewe na kubaini mapungufu ya ulinzi wa kiwanda hicho. Anampigia simu kijana wake anaemuamini zadi James na kumueleza juu ya ujambazi aliotaka waufanyae.

    James anawapigia simu majambazi wenzake na kuwaeleza wakusanyike nyumbani kwa Mr. Carlos maeneo ya Mikocheni. Masaa mawili baadae tayari vijana wa Tanzania Gangster walikuwa nyumbani kwa Mr. Carlos wakishiriki kikao cha mbinu za kuvamia kiwanda cha pamba. Ilikuwa yapata saa saba na nusu usiku, Mr. carlos aliawafundisha mbinu kadhaa za kufanikisha ujambazi huo. Mbinu ambazo alizitoa akiyakumbuka vizuri mazingira ya kiwanda hicho. Baada ya masaa mawili ya maelekezo aliyoyatoa Mr. Carlos, alitoa maagizo kuwa ujambazi huo ufanyike ndani ya siku tano. Kazi ilianza siku iliyofuata kwa kundi la watu saba kusafiri kuelekea mwanza. Mr carlos aliwachagua watu aliyowaamini sana wakiongozwa na James. Aliwapa silaha za kufanikisha zoezi hilo kama ilivyokuwa kawaida yake.

    Majambazi wengine ambao hawakuchaguliwa kuelekea mkoni Mwanza, walielezwa waendelee na shughuli nyingine za unyang’anyi jijini, siku iliyofuata wale majambazi walianza safari kwa kutumia magari mawili kuelekea Mwanza. Walipenda kutumia magari kutokana na usafiri huo kuwa na ukaguzi hafifu wa polisi ukilinganisha na usafiri wa ndege. Moyoni Mr carlos alianza kuingiwa na furaha na kuamini kupata mamilioni ya fedha. Hiyo ilitokana na uwezo wa kundi lake ambalo halikushindwa jambo lolote kirahasi. Anaamua kuendelea na shughuli zake kama kawaida akisubiri siku tano alizitoa kuleta mafanikio.

    Siku ya tano ambayo ndiyo siku ya ujambazi alikuwa nyumbani kwa Mr. John pamoja wakiangalia televisheni sambamba na kubadilishana mawazo.Ilikuwa yapata saa nane mchana kituo hicho kilisitisha matangazo mengine. Mtangazaji alieleza kulikuwa na habari za ujambazi zilizo wafikia kutoka mkoani Mwanza Mr John na Carlos wote walikaa vizuri kusikiliza habari hiyo. Mtangazaji alieleza kuwa watu tisa wakiwemo polisi wanne na majambazi watano walikuwa wamefariki. Alidai tukio hilo lilitokea katika kiwanda cha pamba mkoani Mwanza. Majambazi wawili kati ya hayo saba walitoroka kwa gari na mmoja wao akiwa kujeruhiwa mguu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Taarifa hiyo ilimfanya Mr Carlos kutoa jasho kila sehemu ya mwili wake. Usoni alitokwa jasho kama alikuwa ametoka kuoga, ni jambo ambalo Mr John alishangaa na hakupata jibu. Mr Carlos aliondoka nyumbani kwa Mr John bila kumuuaga jambo ambalo hakupata jubu. Mr carlos aliondoa gari lake kwa hasira na moja kwa moja kuelekea nyumbani kwake, mara baada ya kufika nyumbani kwake na kumpa taarifa hizo mkewe alianza kumtafuta James kwenye namba yake ya simu,hakupatikana. Hofu ilimjaa moyoni akiwaza kama kulikuwa na vielelezo vyovyote vinavyo mtambulisha yeye na tukio hilo. Kitu kilichomuudhi zaidi ni kutofanikiwa kwa zoezi hilo. Aliona kama ni kudhoofu kwa kundi lake la Tanzania Gangster. Alijaribu kwa muda tofauti kupiga namba za majambazi wengine alizokuwa nazo hazikupatikana hewani.

    Siku moja baadae jeshi la polisi mkoani Mwanza lilieleza kuendekea na zoezi lake la kuwasaka majambazi wangine waliotoroka. Ni siku ambayo alipokea simu kutoka kwa rafiki yake John akitaka kujua sababu ya mshtuko wake. Mr Carlos alimueleza Mr John alishtuka kutokana na sababu yake ya kuwa mmoja ya wamiliki wa kiwanda kilichovamiwa cha pamba. Alimueleza alikuwa na hisa nyingi katika kiwanda hicho,sababu ambayo Mr John aliiridhia na kumpa pole kwa mkasa huo. Hiyo yote iltokana na imani aliyomjengea rafiki yake, na hakutaka kujua jambo zaidi.

    Siku ziliendelea kuongezeka bila ya polisi kuwakamata majambazi waliotoroka. Mr Carlos naye hakupata simu kutoka kwa vijana wake James na Tabayu walio kimbia. Alitambua kuwa hao ndio walio pona kwenye mkasa huo baada ya majina ya waliofaraiki kutangazwa na yao kutokuwepo. Hatimaye wiki mbili zilikatika bila taarifa yeyote ya majambazi waliotoroka.



    * * * *





    James na Tabayu walikuwa katika kijiji cha Kibiri kilichokuwa karibu na jangwa dogo la Njiri kusini mwa nchi ya Kenya. Walikuwa kwa babu mmojo mwindaji aliyeishi kwenye pori dogo pembeni ya kijiji hicho. Walifika eneo hilo baada ya safari ya misukosuko iliyofuatia baada ya kushindwa kwa jaribio la ujambazi, mara baada ya kushindwa na kukimbia mkoani Mwanza walielekea mkoani Mara na kutelekeza gari lao kabla ya kusafiri kwa mabasi. Waliunganisha safari yao mpaka eneo hilo kuuhofia usalama wao. Hawakuwa na simu kwa vile ya simu ya James waliyoitumia zaidi aliipoteza katika purukushani hizo za kuukimbia mkono wa jeshi la polisi

    James alikuwa ameumizwa na risasi liyopenya sawasawa kwenye goti lake la kushoto.hakuna huduma yeyote aliyoipata wakihofia wakienda hospitali wangehitaji maelezo ya kutosha. Babu mwenyeji wao ambaye aliishi peke yake aliwaelewa maelezo yao kuwa walivamiwa na majambazia nyumbani kwao. Babu huyu alichukua jukumu la kufanya jitihada za kuitoa risasi hiyo katika mguu wa James. Alifanya jitihada hizo kwa kutumia mjani ya porini, baada ya jitihada zake za siku ya tatu, anafanikiwa kuitoa risasi kwenye mguu uliokwisha anza kuoza. Tabayu hakufanya jambo lolote zaidi ya kutaka kujua hatma ya mguu wa James. Baada ya kutoa risasi hiyo James akaanza kutumia majani ya porini katika jitihada za yule babu za kuuponya mguu wake. Majani hayo hayakumsaidia kitu zaidi ya mguu huo kuendelea kuoza kwa kasi. Tabayu anaamua kuchukua jukumu la kuondoka porini pale na kwenda kijiji cha karibu ili kufanya mawasiliano na Mr Carlos. Hilo lingewezekana kwa kuwa alikuwa na kadi ya mawasiliono ya bosi wake. Anaanza safari kuelekea kijiji hicho na kutumia mwendo wa saa moja.

    Mara baada ya kupata sehemu ya kupiga simu katika kijjiji hicho, anampipgia simu Mr Carlos na kumueleza mkasa mzima ulivyokuwa. “kwa hiyo mguu wa James unaendelea kuoza” aliuliza Mr Carlos, “ndiyo….” alijibu tabayu, “kwani huna hata bastola?” aliuliza tena Mr carlos, “ninayo bosi kwani ulitakaje”

    “kama unayo unasubiri nini mmalize kwa kumuua, kwenye kundi la Tanzania Gangster hatukai na walemavu ” alisikika Mr Carlos akimuagiza Tabayu. Mr Carlos alimtaka Tabayu mara baada ya kumuua James arudi haraka Dar es salaam. Tabayu alianza tena safari ya kurudi porini alikomuacha James. Kazi aliyo agizwa na bosi wake ilikuwa ngumu na hakufikiria kuifanya hata kidogo. Alimuheshimu sana James japokuwa Tabayu alikuwa katili aliona ni vigumu kumuua bosi wake James kwani aliwaongoza vizuri katita matukio mengi ya ujambazi na aliwapa fedha za kutosha zilizokuwa zikitlewa na Mr Carlos. Kichwani aliwaza jambo la kumuepusha James katika adhabu ya kifo. Mara baada ya kurudi nyumbani kwa yule babu, aliamua kuongea na James wakiwa peke yao. Alimueleza kila kutu alichoelezwa na bosi wao Mr Carlos jambo ambalo lilimsikitisha sana James. Hakuamini aliyoyasikia kuwa auawe ni agizo kutoka kwa bosi wake aliyemfanyia kazi ya ujambazi kwa miaka zaidi ya kumi na nane.Bado walikuwa na fedha za kutosha zilizobaki katika maandalizi ya ujambazi mkoani Mwanza katika jaribio waliloshindwa. Siku iliyofuata baada ya kumwachia fedha babu aliyewahifadhi walianza safari. Wakati wote huo James anasaidiwa kutembea kwa mguu mmoja mwingine ukiwa ameunyanyua juujuu. Walipanga kuingia Tanzania kwa njia za ubatili katika mpaka wa Tanzania na Kenya wa mkoa wa Kilimanjaro.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya safari ya muda mrefu yenye misukosukowanafanikiwa kufika Moshi mjini mkoani Kilimanjaro.Tabayu mapema anampeleka James hospitali ya Mawenzi ili aweze kupata matibabu. Madaktari wanatoa maelekezo kuwa James anatakiwa kukatwa mguu kwa vile ulikuwa umeharibika sana. James haamini maelezo hayo, baada ya majonzi ya muda mrefu anawaruhusu wamukate, kutokana na maumivu makali aliyokuwa akiyapata. Baada ya zoezi hilo Tabayu anampa fedha zote zilizobaki ambazo walikuwa nazo na kumuongeza nyingine kutoka kwenye akaunti yake ya benki. Kwa ujumla anapata kiasi cha millioni tano ikiwa ni baada ya kulipa fedha zote za matitabu. Tabayu anamuaga na kumueleza kuwa anakwenda kwa Mr Carlos kwani kutofanya hivyo kungeibua picha mpya kwa bosi wao. James anamshukuru tabayu kwa msaada wake zaidi ikiwa ni kukaidi agizo la kuuawa kwake. Anamuacha akiuguza mguu ampaka atakapo ruhusiwa.



    * * * *

    Mr Carlos anachukulia kushindwa jaribio lake la ujambazi kama changamoto anaendelea na kazi yake hiyo. Katika harakati zake hizo anapata mkufunzi wa ujambazi katoka bara la Asia ambaye anawapa vijana wake mafunzo ya wiki mbili. Kazi inaendelea kwa kasi ileile, anaanza kulisahau jina la James kufuatia maelezo ya kuuawa na Tabayu. Ni taarifa ambayo aliwaeleza mara baada ya kuripoti, Mr carlos hakuumia moyoni kufariki kwa James ingawa alifanya naye kazi kwa miaka mingi. Aliamini kuwa kama James angekuwa hai asingeweza kuwasaidia jambo lolote zaidi ya kuvujisha siri kwa vile angekuwa mlemavu.

    Baada ya kulazwa katika hospitali ya Mawenzi mjini Moshi kwa mwezi mmoja hatimaye James anaruhusiwa kuondoka. Alikuwa amepewa gongo la kumsaidia kutembea kwa vile alikuwa amekatwa mguu wake wa kushoto.alipanda basi kuanza safari kuelekea jijini Dar es salaam. Hakuwa tayari kurudi katika nyumba yake aliyojengewa na Mr Carlos maeneo ya kinondoni. Kwani kufanya hivyo aliamini ni kuhatarisha maisha yake. Alimtambua vizuri Mr carlos na alielewa kuwa nyumba hiyo tayari ipo mikononi mwa jambazi mwingine.

    Katika maisha yake yote James hakujijenga hata kidogo akithamini zaidi pombe na starehe ya kubadilisha wanawake wa kila aina. Hadi wakati huo hakuwa ameoa au kuishi na Familia, alichofanya ni kwenda kupanga nyumba maeneo ya Manzese na kufungua biashara ya kuuza mahitaji ya nyumbani. Biashara hiyo ilikuwa ndogo ambayo ilimtosha kuendesha maisha yake.

    Mwezi mmoja baadae akiendelea na biashara hiyo, anaingiwa na hisia ya uovu wa Mr Carlos. Hiyo yote inatokana na matendo yake ya kinyama ikiwa ni pamoja na kutaka yeye auawe. Mtu pekee ambaye anaona anafaa kuutoa uovu huo ni Mr John Mushi ambaye mwanae Juliana aliuawa mbele ya macho yake. Anaanza jitihada za kuipata namba ya simu ya Mr John Mushi na mwishoni anapata njia. Anamtumia kijana mmoja kwenda kwenye maduka ya nguo ambayo yalikuwapo Kariakoo yakiwa maarufu katika mtaa wa Msimbazi.

    Kijana aliyemtuma anafanikiwa kuipata namba ya simu ya Mr John Mushi. Siku hiyohiyo iliyokuwa Jumapili anampigia simu akimueleza angeenda kwa Mr John Mushi. Lengo kubwa alisema alitaka kumwambia mauaji ya mwanae Juliana. James hakutaja jina lake na aliahidi kuwasilisha ujumbe huo kwa Mr John Mushi saa tano usiku. Alichomuambia Mr John Mushi atulie asubiri ujumbe wa kumtaja muuaji wa mwanae. James hakuwa na shaka kwani nyumba ya Mr John Mushi alikuwa anaifahamu vizuri kwani walienda mara nyingi na Mr Carlos alipokuwa akitumikia kundi la Tanzania Gangster.

    Mr John Mushi alikuwa nyumbani kwake akisubiri kwa hamu saa tano usiku ifike, tayari alishamwaleza mlinzi juu ya ujio wa mgeni wake huyo. Hasira alizokuwa nazo kipindi cha msiba wa mwanae zinaanza kumrudia. Anawaza kuhakikisha muuaji ananyongwa katika kufuata misingi ya sheria za nchi ya Tanzania. Ilipofika saa nne usiku anakumbuka kitu muhimu ambacho alikuwa amekisahau. Alikuwa hajamtaarifu Mr Carlos ambaye alikuwa rafiki yake wa karibu katika kipindi chote kigumu cha msiba wa mtot wake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA



0 comments:

Post a Comment

Blog