Search This Blog

Monday, October 24, 2022

NAMPENDA ADUI YANGU - 3

 







    Chombezo : Nampenda Adui Yangu

    Sehemu Ya Tatu (3)





    Ilipoishia…CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Mr John Mushi alikuwa nyumbani kwake akisubiri kwa hamu saa tano usiku ifike, tayari alishamwaleza mlinzi juu ya ujio wa mgeni wake huyo. Hasira alizokuwa nazo kipindi cha msiba wa mwanae zinaanza kumrudia. Anawaza kuhakikisha muuaji ananyongwa katika kufuata misingi ya sheria za nchi ya Tanzania. Ilipofika saa nne usiku anakumbuka kitu muhimu ambacho alikuwa amekisahau. Alikuwa hajamtaarifu Mr Carlos ambaye alikuwa rafiki yake wa karibu katika kipindi chote kigumu cha msiba wa mtot wake.



    Endelea….

    Anachukuwa simu na kumpigia Mr Carlos akimueleza aende nyumbani kwake kuna mtu anatarajia kutoa siri ya mauaji ya Juliana.

    Taarifa hizo zinamshtua sana Mr Carlos ambaye anaammini hakuna mtu aliyejua siri hiyo zaidi ya James aliyekuwa marehemu. Anabadilisha nguo za kulalia alizokuwa amelala nazo na kuvaa nyingine. Kwa kasi anaondoka nyumbani kwake na gari lake baada ya kumuaga mkewe. Safari inaanza kuelekea Kimara Baruti, akiwa na shauku ya kumjua anayeifahamu siri hiyo. Aliamini akiwahi kufika ingekuwa vigumu kwa mtu huyo kutoa siri hiyo. Tayari alihisi dalili za shari hivyo aliwapigia simu vijana wake kuwa tayari muda wowote kwa kazi.

    Saa tano na dakika tano usiku ule alikuwa katika njia iliyoelekea nyumbani kwa Mr John Mushi akiwa ametanguliwa na taksi mita kadhaa. Hatimaye alipo karibia geti la Mr John Mushi aliona ile taksi ikisimama mbele ya geti hilo. Alichofanya ni kufunga breki za gari lake na alimuona mtu mmoja aliyekuwa na gongo akishuka akiwa amekatwa mguu wa kushoto. Baada ya kumtazama vizuri alibaini alikuwa ni James, yote hayo yaliweza kutokana na taa iliyowekwa nje ya geti hilo. Wakati huo Mr Carlos jasho lilimtoka akiwaza nini cha kufanya, hatimaye James alifunguliwa geti na kuingia na taksi aliyokuja nayo iligeuza na kuondoka.

    Aliwapigia simu vijana wake na kuwaelekeza eneo alipo akiawataka waende na madumu ya mafuta ya petroli pamoja na bunduki za kutosha. Nusu saa baadae gari tano ziliwasili zikiwa na vijana kumi na nne wa Mr Carlo akiwemo pia Tabayu. Mtu aliyeingia kwa Mr John Mushi alikuwa ni James ambaye mara baada ya kuketi ndani kwa Mr John alianza kumsimulia mambo yote yaliyomuhusu Mr Carlos kwa ufupi na alieleza mkasa mzima wa kifo cha mwanae. Baada ya kusimuliwa mambo hayo ilikuwa yapata saa tano na nusu. Akiwa amechanganikiwa, alichukua simu na kupiga kituo cha polisi lakini iliita pasipo kupokelewa. Hasira zilimpanda kwa kiasi kikubwa hakuamini mtu aliyemtegemea kama rafiki yake alifanya unyama wa kutisha kama ule.

    Aliamua kumpigia simu baba yake mzee Mushi na kumwambia maneno matano “Mr Carlos Mato nitakufa naye” baada ya kusema hayo alikata simu

    Mr Carlos baada ya dakika kadhaa za kukaa nje alielewa tayari Mr John Mushi alishaupata ukweli kutoka kwa James. Alichukuwa simu yake na kumpigia kwa makusudi, alipokea na kuzungumza maneno matano tu “Nitakuuwa kwa mkono wangu mwenyewe” maneno hayo yalimpa taswira nzima Mr Carlos aliyewaruhusu vijana wake kuanza kazi.waliongozwa na Tabayu ambaye hakutambua alivamia nyumba ya nani. Walimkamata mlinzi na kumnyonga wakitumia kamba ya katani na kufanikisha zoezi hilo ndani ya dakika kumi.

    Walianza kumwaga mafuta ya petroli kuzunguka nyumba ya Mr John, dakika tano baadae walikuwa wamekamilisha zoezi hilo. Walimwaga petroli zaidi ya madumu kumi na tano. Tabayu aliendelea kumwaga chini mafuta hayo kutoka kwenye nyumba hadi nje alipokuwa anawasubiri Mr Carlos.

    Mara baada ya kukamilisha zoezi hilo la kumwaga petroli Mr Carlos aliwasha kiberiti na kuelekeza kwenye mafuta yaliyomwagwa chini na Tabayu. Punde tu alipoachia njiti ya njiti ya kiberiti aliyoiwasha, moto uliwaka kwa kasi kubwa kuelekea kwenye nyumba ya Mr John. Hatimaye ulikamata nyumba hiyo na kuanza kuwaka kwa kiwango kikubwa. Muda huo Mr Carlos na vijana wake walikuwa wakishuhudia tukio hilo. Baada ya dakika mbili nyumba za majirani zilianza kupiga kelele za yowe. Mr Carlos alichukua bunduki na kupiga hewani risasi zaidi ya kumi na hatimaye kelele hizo zilitulia. Mara aliposhusha bunduki hiyo alielekeza kwenye paji la uso wa Tabayu na alisikika akisema “wewe ni msaliti …….” Hakuongeza jambo zaidi ya kumfyatulia risasi mbili kichwani.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Aliwaamuru vijana wake waondoke eneo hilo haraka, jambo ambalo walilifanya na gari zao ziliondolewa kwa kasi katika eneo la nje la nyumba ya Mr John. Vijana wa Mr Carlos hawakutambua chanzo cha kuuwawa kwa Tabayu walikimbiza gari zao na kuingia barabara ielekeayo Morogoro na kila gari liliendeshwa kuelekea sehemu ambayo dereva wa gari aliamua.

    Mr Carlos aliendesha gari kwa kasi kuelekea nyumbani kwake Mikocheni. Alikuwa amechukizwa na taarifa za uongo ambazo awali Tabayu alizitoa akidai alimuua James. Jambo hilo ndilo lililomfanya amuue Tabayu mbele ya vijana wake wengine wa Tanzania Gangstars. Alilewa alielekea nyumbani kwa ajili ya kujiandaa na msiba mkubwa wa familia nzima ya Mr John Mushi. Ingawaje John Mushi alikuwa rafiki yake, anaamini hakuna urafiki ambao ungeendelea baada ya kugundulika kwa siri zake. Kufa kwa Mr John Mushi na familia yake pamoja na James aliona ni jambo la msingi katika kutunza siri zake.





    Siku iliyofuata vyombo vya habari vilitawaliwa na taarifa za kifo cha Mr John na familia yake. Magazeti ya jioni yalionesha picha ya nyumba ya Mr John ikiwa imeungua na kukosa hata mabaki zaidi ya kuta za nyumba hiyo. Taarifa zilieleza watu watano walifariki katika tukio hilo, mmoja alipatikana nje ya uzio wa nyumba hiyo akiwa amepigwa risasi kichwani. Mwingine ambaye aliyebainika kuwa alikuwa ni mlinzi mwili wake ulipatikana akiwa amenyongwa upande wa ndani katika geti la nyumba hiyo. Taarifa hizo zilitoa maelezo ya awali zikiamini ndani ya nyumba iliyoungua alikuwepo John, mkwewe na mfanyakazi wa ndani wa jinsia ya kike.

    Ukosefu wa taarifa hizo ulitokana na kushindikana kupatikana kwa mabaki ya wahanga hao. Vitu vyote viliungua na kuwa majivu, muda wa saa tano na nusu asubuhi Mzee Mushi na mkewe waliwasili wakiwa na mjukuu wao Kenny kwa usafiri wa ndege wakitokea Moshi. Kenny ambaye alikuwa na miaka saba akiwa ni mtoto pekee aliyebaki wa marehemu John Mushi. Alinusurika katika janga hilo kwa vile alikuwa shuleni katika shule ya East Africa International School iliyokuwa mjini Moshi akiwa darasa la kwanza. Mzee Mushi na mkewe waliona mwanzo wao wa kupoteza mwelekeo wa maisha kwani John alikuwa mwanao pekee aliyekuwa amebaki baada ya wengine kufariki. Mzee Mushi ambaye muda wote alikuwa analia alitatizwa na sentensi aliyoambiwa na mwanae iliyoeleza “Mr Carlos Mato nitakufa naye...”. Hakupata picha yeyote kutoka kwenye sentensi hiyo, kuna wakati alihisi mwanae alimananisha kufa na Mr. Carlos kutokana na urafiki wao wa karibu. Lakini pia alihisi huenda mwanae alimananisha kumuua Mr. Carlos na yeye kujiua. Utata huo unakaa kichwani mwake pasipo kumweleza mtu yeyote na anaamini Mr. Carlos Mato mwenyewe ndiye atakayeelezea jambo hilo.

    Kenny John mwanae John Mushi alilia kwa uchungu akijigongesha kila upande wa chumba kilichokuwa maalum kwa wafiwa katika nyumba iliyokuwa ya jirani yao. Ingawaje alikuwa mdogo, hasira zake na kwikwi vilimfanya aamini kuwa aliweza kulipiza kisasi kwa yeyote ambaye angehusishwa na tukio hilo, kilichomuuma zaidi ni kupoteza familia yake katika kipindi kifupi ikiwa ni baada ya kifo cha dada yake Juliana. Haelewi ataanzia wapi zoezi hilo lakini siri yake hiyo moyoni ndiyo inayompa hasira na kujijengea imani ya kulipiza kisasi.

    Mr. Carlos ndiye aliyehusika na maandalizi ya kila kitu kilichohusu msiba wa rafiki yake Mr John. Jambo hilo linamfanya asitulie muda wote wa msiba huo akitafuta mahitaji tofauti ya msibani hapo. Watu waliokuwa msibani hapo walifurahishwa na upendo aliouonesha. Ikiwa ni pamoja na kuhusika na msiba wa Juliana kwa asilimia kubwa na wakati huu msiba wa familia nzima waliamini Mungu atamzidishia Mr. Carlos kwa wema wake. Kutokana na kukosekana kwa miili ya marehemu Mr. Carlos akishirikiana na familia ya marehemu. Wanashauriana kujenga makaburi katika eneo ambalo janga la moto ulioaminiwa kusababishwa na majambazi lilitokea.

    Halikadhalika wanashauriana kuchukuliwa majivu ili yakazikwe mkoani Kilimanjaro kama kielelezo cha kufariki kwa familia hiyo. Jambo ambalo walianza kulitekeleza haraka, ikiwa ni ujenzi wa makaburi matatu katika eneo la ajali hiyo iliyosababishwa ya moto. Mpaka nyakati za jioni siku hiyo zoezi hilo lilikamilika, inasubiriwa siku iliyofuata ili safari ianze kuelekea Mkoani Kilimanjaro.

    Mr. Carlos Mato kuna jambo lilimtatiza kichwani nalo ni kuhusiana na maduka ya marehemu Mr. John Mushi. Hahitaji maduka hayo yaendelee, anaamini kama yakiendelea kwa kuendeshwa na ndugu wa marehemu Mr. John Mushi lingeweza kutokea tatizo. Jambo alilolihofia ni upelelezi ambao ndugu wa marehemu Mr. John Mushi wangeufanya kupitia fedha ambazo wangelikuwa nazo. Kupoteza ndoto hizo anaelekea kando kidogo na kuwapigia simu vijana wake akiwataka wahakikishe wanachoma maduka yote matatu ya nguo ya marehemu Mr. John Mushi ikiwa pamoja na stoo zake. Zoezi hilo aliwakata lifanyike saa nane usiku wa siku ile, baada ya maelezo hayo alijiona yuko safi akiamini hakuna linaloshindikana kwa vijana wake wa Tanzania Gangstars.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mzee Mushi baada ya muda mrefu wa majonzi, anashindwa kuvumilia anataka kujua ukweli wa kauli ya mwanae. Hilo aliamini liliwezekena kwa vile Mr. Carlos Mato mwenyewe aliyetajwa alikuwepo msibani hapo. Anaamua kumuita kando na kuanza kwa kumuuliza kuwa mara ya ya mwisho alipata kauli kutoka kwa mwanae iliyokuwa “Mr Carlos Mato nitakufa naye…” alihitaji kujua chochote kutoka kwa Mr. Carlos Mato akiamini alitambua kutokana na ukaribu wake na marehemu. Kauli hiyo ulimshtua Mr. Carlos Mato ambaye hakuonesha hali yeyote kwa Mzee Mushi ya mshtuko wake. Baada ya ukimya wa sekunde kadhaa Mr. Carlos anakubali kauli hiyo inaukweli ndani yake. Lakini anamuomba Mzee Mushi atulie na kumuahidi kumjulisha maana yake mara baada ya msiba huo. Mr Carlos anaongeza kwa kusema ukweli wa kauli hiyo ungemchanganya zaidi Mzee Mushi jambo ambalo halikuwa jema wakati huo.

    Siku iliyofuata wakiwa kwenye maandalizi ya safari kuelekea Mkoani Kilimanjaro. Zilipatikana taarifa za kuchomwa moto maduka matatu na stoo nne vyote vikiwa mali ya marehemu Mr. John Mushi taarifa hizo zinaifadhaisha zaidi familia hiyo, Mr. Carlos Mato na marafiki wengine wanashauri tukio hilo lisiwe kikwazo cha kusafirisha msiba huo. Lakini maswali mengi yalikuwa vichwani mwa watu juu ya unyama wa mtu aliyefanya matukio hayo. Hakuna jibu linalopatikana hivyo safari ya kuelekea Moshi, Mkoani Kilimanjaro inaanza na zaidi walitegemea jitihada za polisi kufichua mtenda uovu huo.

    Baada ya msiba Mr.Carlos alirudi jijini Dar es salaam kuendeleza shughuli zake.Kichwani alianza kupoteza kumbukumbu za Jina la rafiki yake Mr.John Mushi aliyemuua.Alimini amepoteza uwezekano wote wa kuvuja siri zake, kitu kilichokuwa mbele yake aliwaza kukuza mtandao wake wa Tanzanian Gangstars.Wema aliokuwa akiuonesha mbele za watu katika msiba unakoma, kwani alishidwa kumsaidia mzazi wa marehemu John Mushi ambaye maisha yalianza kumuwia magumu.Katika kupanua mtandao wake wa Tanzanian Ganastars Mr Carlos aliamua kuanza kuuza Dawa za kulevya.Biashara hiyo aliifanya katika nchi za Pakistani,Iran,Iraq zikiwa miungoni mwa nchi za bara la Asia.Nchi nyingine zikiwa ni Uingereza,Ujerumani pamoja na Marekani na alifanya biashara hiyo karibu kila nchi ya bara la Afrika.

    Lakini pia bado aliendeleza kazi ya kuongoza kundi lake katika matukio ya ujambazi katika ukanda wa Afrika, miezi sita baadae akiwa anaendelea na shughuli hizo alipata kikwazo kutoka kwa mzee Mushi. Alikuwa akimuhitaji kujua misingi ya kauli ya “Mr Carlos Mato nitakufa naye..” Mzee Mushi alikuwa akipiga simu kila siku akitaka kujua kauli hiyo aliyoelezwa na marehemu mwanae inamaana gani



    . Jambo hilo lilimkwaza Mr Carlos ayepanga kuzizimisha kabisa ndoto za mzee huyo. Mzee Mushi katika mawazo yake alikuwa akihisi huenda Mr Carlos alihusika na mauaji ya mwanae kwa namna moja au nyingine. Mr Carlos aliandaa safari mahususi kwa ajili ya kuimaliza familia ya mzee Mushi ambaye alitambua kuwa alikua akiishi na mkewe.

    Alinza safari akiwa na vijana wake wa kazi wawili kuelekea mkoanai Kilimanjaro. Waliondoka jijini nyakati za jioni lengo lao likiwa ni kufika mjini Moshi usiku wa manane.Saa nane usiku Mr Carlos anaegesha gari lake nje ya nyumba ya Mzee Mushi baada ya safari ndefu iliyotawaliwa na kasi kubwa ya gari lake.Aliwaacha vijana wake kwenye gari na kuanza kuelekea kwenye nyumba ya Mzee Mushi. Kulikuwa na giza nene kutokana na tatizo la kukatika umeme katika eneo hilo la Kibosho.Mara alipofika mlangoni Mr Carlos alianza kugonga huku akijitambulisha.Baada ya dakika tano alisikia vishindo vya mtu akitembea kuusogelea mlango huo.Hatimaye alifunguliwa mlango na Mzee Mushi aliyekuwa na tochi mkononi.Hali kadhalika mkewe alikuwa nyuma yake na wote walionekana kujawa na hofu juu ya ujio wa Mr Carlos usiku huo jambo ambalo halikuwahi kutokea awali. Mzee Mushi alimueleza mkewe awashe taa ya mafuta jambo ambalo alianza kulitekeleza mara baada ya kuwasha taa hiyo wote waliketi kwenye viti wakitaka kujua tatizo la ujio wa Mr.Carlos.

    “Mzee Mushi usihofu nimekuja kuwaongeza na mkeo katika idadi ya watu kuzimu hivyo muwe na amani tu”Aliongea Mr.Carlos kauli yenye utata huku akitoa bastola yake kwenye koti lake suti. Wakati huo mzee Mushi na mkewe walikuwa wanatetemeka kiasi cha kulitikisa kochi walilokuwa wamekalia.

    “Lakini kabla sijawaua ninaomba muutambue ukweli huu ili mkiwakuta huko waliotangulia mbele za haki msipate taabu ya kuwauliza.Mimi Mr Carlos Mato ndiye niliyemubaka na kumua mjukuu wenu Juliana na mimi ndiye niliyeiua kwa moto familia ya Mr.John Mushi mengine yanayonihusu nitawasimulia na mimi nikija kuzimu,tangulieni salama”Alimaliza Mr Carlos Mato na kumiminia risasi mbili za kichwa Mzee Mushi kabla ya kumgeukia mkewe kwa risasi hizohizo.Alicheka na kisha kutabasamu,alijisikia fahari kwa matukio ya kila jambo alilolifanya, utu kwake ulikua umeshapotea hakuwa na huruma hata kidogo.Alitoka mbio kuelekea kwenye gari lake ambalo aliwaacha vijana wake.Waliondoa kwa kasi gari hilo kutoka kwenye eneo la nyumba hiyo ya mzee Mushi, Mr Carlos alijisifu akisema “kazi imeisha na hakuna matata”

    * * * * *CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kenny John kama alivyoandikishwa shule akiwa mtoto wa marehemu Mr.John Mushi alibahatika kuupata ukweli aliokuwa akiutafuta siku zote.Baada ya kusoma kwa miezi sita katika shule ya East Africa International School ya mjini Moshi babu yake alishindwa kumudu gharama za shule hiyo.Aliamua kumuandikisha katika shule ya msingi ya wilayani Moshi vijijini katika kata ya Kibosho ili aendelee na masomo.Siku chache za awali akiwa kwa babu yake anakumbana na shida ya kuishi maisha ambayo awali hakuyazoea jambo hilo linamfanya muda mwingi ajifungie chumba alicholala kikiwa karibu na sebule nakulia kwa kwikwi .Jambo hilo mzee Mushi aliligundua na alijitahidi kuwa karibu na mjukuu wake.

    Hasira zake haswa ziko kwa muuaji wa familia yake ikiwa ni pamoja na yule aliyemubaka na kumuua dada yake.Kilichomuudhi ni kutopatikana kwa taarifa zozote juu ya wauaji hao kutoka Jeshi la polisi.Aliamini kama jambo hilo lilifanywa na binadamu kama yeye basi siri hiyo lazima angeigundua.Siku chache akiwa nyumbani kwa babu yake wakati wa usiku wa manane alishtuka usingizini baada ya kusikia mngurumo wa gari.Aliamka na kufunua kidogo pazia la dirisha la chumba alichokua analala alimshuhudia Mr.Carlos Mato aliyemtambua kama mjomba wake akishuka kwenye gari hilo.Mara baada ya kushuka Mr.Mato alianza kutembea akielekea kwenye nyumba hiyo ya babu yake na punde taa za gari hilo zilizimwa.

    Sekunde chache baadaye alisikia kelele za mlango ukigongwa na hatimaye ulifunguliwa na babu yake Mzee Mushi.Alimsikia Mzee Mushi akimweleza bibi yake awashe taa ya mafuta.Alitamani kwenda sebuleni ila kutokana na uchovu aliokua nao alimua kubaki chumbani kwake.Mawazo yake yote yalimfanya awe na furaha akiamini mjomba wake Mr.Carlos Mato huenda alienda kumchukua ili wakaishi wote jijini Dar es salaam.Jambo hilo lilimfanya atege sikio vizuri kusikiliza ambacho kingendelea,hilo liliwezekana kwa vile chumba hicho kiliruhusu kusikika kwa sauti za watu sebuleni.

    Alishtushwa na Sentensi ya kwanza iliyoeleza”Mzee Mushi usihofu nimekuja kuwaongeza na mkeo katika idadi ya watu kuzimu,hivyo muwe na amani tu”Sentensi hiyo ilimfanya Kenny kuamka taratibu na kukaa katika kitanda chake.Mshtuko huo uliongezeka kutokana na maelezo yaliyotolewa na Mr Carlos kuwa yeye ndiye aliyemubaka na kumuua Juliana na ndiye aliyehusika na kifo cha familia yake.Hasira zilipanda na kwikwi kwa pamoja akiwaza kufanya jambo, kabla hajafanya lolote alishtushwa na mlio wa risasi uliosikika sebuleni.Aliishiwa nguvu na kuangukia kitanda chake alibaki ametoa macho hata mdomo ulikua mzito kuongea.Alisikia tu mlio wa gari likiondoshwa mbele ya nyumba yao lakini hakuwa na nguvu ya kuinua hata meno.Baada ya nusu saa watu wengi walikusanyika nyumbani kwao na walimsaidia kwa kumtoa nje ili apulizwe na upepo.Vilio vya watu vilitawala eneo la nyumba ya Mzee Mushi, watu wengi hawaelewi makosa yaliyofanywa na familia hiyo.Zinaibuka hisia kuwa Mr John Mushi huenda alifanya dhuluma ambayo mtu aliyedhulumiwa alikuwa analipiza.Lakini hilo nalo lilionekana siyo kigezo cha msingi cha mauaji hayo katika familia hiyo.

    Baada ya muda mfupi Kenny alirudi katika hali yake ya awali na kuanza kulia kwa sauti ya juu.Alipelekwa mpaka kwenye chumba kilichowekwa miili ya babu na bibi yake wakiwa wamefariki.Alilia akiwakumbatia akiwa haamini kuwa alikuwa nao katika masaa machache yaliyokuwa yameshapita.Hasira zake zinatawala juu ya muuaji wa familia yake Mr.Carlos Mato, alilia akijibamiza katika kuta za chumba hicho.Majirani kadhaa walijitahidi kumtuliza moyoni aliumia sana akiwakumbuka wazazi wake na dada yake Juliana zaidi ni kifo cha babu na bibi yake.Jambo lililomkaa moyoni ni kulipa kisasi kwa mkono wake mwenyewe pasipo msaada wa mtu mwingine.Hataki siri hiyo hata polisi wajue kwani haoni mchango wao kwake.Siku zote hakuhisi na kudhania mtu aliyekuwa akiheshimika kama mjomba yake alikuwa katili kiasi kile.

    Siku iliyofuata taratibu za mazishi zilifanyika na Mzee Mushi na Mkewe wakazikwa.Mara baada ya mazishi polisi walimuita kando Kenny na kuhitaji kutoka kwake chochote kilichohusiana na kifo cha bibi na babu yake.Hakutoa siri hiyo hata kidogo,ingawaje alikuwa na umri a miaka nane wakati huo lakini alikuwa na mtazamo wa mbali.Alijua hata akiwapa siri hiyo askari wa Jeshi la Polisi wangeishia kutomuadhibu Mr.Carlos Mato kutokana na uwezo wake kifedha.Jambo hilo pia aliona lingekatisha jitihada zake za kufanikiwa kumuua Mr.Carlos Mato kwani aliamini angekufa kabla ya Mr.Carlos.

    Jambo lililomdhihirishia Mr.Carlos Mato alikuwa akiigiza katika misiba na kumuona ni muuaji hakushiriki msiba huo kama alivyokuwa akishiriki hapo awali.Baada ya msiba huo Kenny alianza kuishi na mtoto wa babu yake mkubwa.Alikuwa ni mama mtu mzima ambaye katika maisha yake hakubahatika kupata mtoto.Mama huyo ambaye Kenny alimtambua kama shangazi yake alikuwa hana kazi yoyote.Waliishi katika nyumba hiyo ya marehemu babu yake Mzee Mushi wakitegemea shamba la kahawa lililozunguka nyumba hiyo pamoja na mauzo ya ndizi.Kwa vile Mzee Mushi alifanikiwa kuwa na shamba kubwa la migomba ya ndizi kama ulivyo utamaduni wa wachaga.

    Maisha yaliendelea kwa taabu, kila siku mara baada ya kuamka Kenny alijenga utamaduni wa kuitazama picha ya familia yao kabla ya kufariki kwa Juliana. Mara zote alidondokwa na machozi lakini pia hakuacha kuzitazama picha za muuaji Mr.Carlos Mato na kila baada ya kuzitazama alikunja uso kama alikuwa amepigwa.Hasira zake siku zote aliwaza kulipiza kisasi kwa njia yeyote.Aliendelea na msomo katika shule ya msingi Umbwe akijitahidi kujifunza mambo tofauti ili yamjenge katika maisha yake ya baadaye.Siku zote aliamini atafanikiwa kulipiza kisasi kwa kuitafuta elimu na mwisho kuwa na fedha za kutozidiwa na Mr.Carlos.Alielewa wazi asipotafuta maisha yake mazuri hawezi kufanikisha jambo lolote.



    * * * * *CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mr.Carlos moyoni alipata amani akiamini kila kitu alikuwa amekimaliza, jitihada zake ziligeukia katika kundi lake la Tanzanian Gangstars ili kuhakikisha mafanikio katika maisha yake.Aliamua kujenga nyumba yake nyingine maeneo ya Mbezi Beach na ile ya awali ya Mikocheni ilianza kutumiwa kwa shughuli za biashara ya Dawa za kulevya na kuendeleza vikao vya ujambazi.Vyumba vingi vya nyumba hiyo vilihifadhiwa silaha tofauti za shughuli zake.

    Mr.Carlos pia alifungua maabara katika nyumba yake ya awali ya Mikocheni, maabara hiyo ilikuwa maalumu kwa ajili ya upasuaji wa maiti na kuweka dawa za kulevya na kusafirisha kirahisi, alikuwa akinunua maiti kwa wafanyakazi wa hospitali tofauti waliofanyia mochwari.Maiti nyingine alizozinunua zilikuwa ni zile ambazo hazikutambuliwa.Utajiri wake uliendelea kukua siku hadi siku, jambo lililomfanya ajijengee tabia katika jamii ya kutoa msaada mara kwa mara.Jina la Mr.Carlos Mato linakuwa kubwa kila kona ya Tanzania hakuna asiyemtambua hata nchi za karibu.Yote hiyo ilitokana na utajiri wake na ukarimu aliokuwanao kwa raia wa nchi.Wakati huo wanawe walisoma sehemu tofauti bara la ulaya akiwepo mtoto wake wa pili Steven na wa mwisho aliyeitwa Mary. Mwanaye Jane tayari alikamilisha masomo yake na alikuwa akifanya kazi jijini London nchini Uingereza.

    Watu wengi hawatambui siri ya misaada ambayo Mr.Carlos aliitoa kwa watanzania.Alikuwa akitangaza ofa ya kuwapeleka nchini India watu kutibiwa magonjwa ya moyo,mapafu na mengineyo lakini siku zote alikuwa na makusudi yake.Mara nyingi aliwapeleka watu zaidi ya Thelathini kutibiwa nchini India,matatizo hayo ya mapafu na moyo.Lakini kati yao ilikuwa ni lazima itokee watano wanarudishwa wakiwa wamefariki.Taarifa zilizokuwa zinatolewa zilidai walizidiwa sana na madaktari walishindwa kuokoa maisha yao.Lakini ukweli haukuwa huo watu hao waliofariki wengi wao waliuawa kwa makusudi na miili yao ilikuwa ikitumiwa kusafirisha dawa za kulevya kabla ya kurudishwa nchini Tanzania. Jambo hilo halikumharibia Mr.Carlos hata kidogo katika uhusiano wake wakaribu na wananchi.Watu waliamini vifo vya ndugu zao vilitokana na kushindikana kwa jitihada za madaktari wa India.Fedha ambazo Mr.Carlos alizipata kupitia kusafirisha dawa za kulevya zilikua mara tatu ya zile alizozitumia kuwatibu wachache waliorudi salama.

    Hivyo ndivyo maisha ya Mr.Carlos yalivyoendelea pasipo watu kuujua ukweli wake wowote.Alipoteza utu kwake kuua lilikuwa jambo la kawaida, jina la rafiki yake wa enzi hizo marehenu Mr.John Mushi lilipotea kabisa kichwani mwake na hakukumbuka yaliyojiri.



    * * * * *

    Baada ya masomo yake ya shule ya msingi, Kenny John anafanikiwa kufaulu na kuchaguliwa kujiunga shule ya sekondari Umbwe.Shule iliyokuwa Moshi vijijini kata ya Kibosho ambayo ilipakana na shule ya msingi Umbwe aliyoisoma kabla ya kufaulu kwake.Shangazi yake aliyeishi naye ambaye alizoeleka kama mama Mushi alianza jitihada za kuuza kahawa pamoja na ndizi ili kufanikisha kujiunga kwa Kenny kidato cha kwanza kutokana na ugumu wa maisha ilimpasa aanze kuandaa fedha za ada ya Kenny mapema.Wakati huo Kenny alifanya vibarua sehemu tofauti na fedha aliyopata alimpa shangazi yake aongezee kwenye ada.Siku zote alikuwa tayari kufanya kazi yoyote ambayo aliamini ingemsaidia katika maandalizi ya kulipiza kisasi kwa Mr.Carlos.

    Hatimaye alijiunga na shule hiyo ya wavulana ya Umbwe iliyokuwa ya bweni na kuanza masomo yake.Alifurahi sana akiamini ndoto zake za kulipiza kisasi zilianza kukamilika.Akiwa shuleni hapo iliyokuwa na kidato cha kwanza hadi cha sita,mapema alijiunga na kikundi cha wanyanyua vyuma na kuanza kujenga mwili wake.Alifanya hivyo kwa vile alitambua mtihani ambao ungemkabili miaka ya usoni.Hakuishia kujenga mwili kwa kunyanyua vyuma bali pia alisoma kwa bidii ili kukamilisha ndoto zake.Siku zote akiwa shuleni hapo hakupenda kungalia televisheni ya shule kutokana na sababu kubwa ya vituo vingi kumuonesha Mr.Carlos akitoa misaada sehemu mbalimbali.Jambo kubwa lililomuudhi kwa vile alimtambua Mr.Carlos vizuri na aliamini misaada aliyoitoa haikuwa ya bure.Akiwa shuleni hapo alichukizwa pia na tabia ya wanafunzi kubishana juu ia matajiri waliongoza Tanzania na wengine walimtaja Mr.Carlos jambo lililomfanya asipende kukaa karibu na mabishano hayo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mafanikio yake kitaluuma yalionekana kutokana na juhudi zake na alifanikiwa kuongoza darasa lake mara kadhaa.Miaka mitatu baadaye akiwa kidato cha tatu alionekana akiwa mrefu,kifua kilicho tanuka na sura ya kuvutia.Mtu yeyote ambaye angemuona angegundua Kenny alikuwa mtu wa mazoezi, kutokana na muonekano wake wa kuvutia ndiyo uliosababisha atafutwe na wasichana wa shule tofauti mkoani Kilimanjaro, lakini alipuzia hisia zao na siku zote hakufikiria kitu kingine zaidi ya malipo ya kisasi. Kenny alifahamika vizuri shule tofauti mkoani Kilimanjaro kutokana na kipaji chake cha kuigiza kilichowavutia wanafunzi wa kike.Katika matamasha mengi ya mashule,watu walifurahishwa na jinsi alivyokuwa mcheshi katika kuigiza akiwa na kila sababu ya kuwa muigizaji.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog